Winamp Logo
Siha Njema Cover
Siha Njema Profile

Siha Njema

Swahili, Fitness / Keep-fit, 1 season, 84 episodes, 13 hours, 57 minutes
About
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episode Artwork

Simulizi kuhusu ugonjwa wa Endometriosis unaowasababishia wanawake maumivu

Ugonjwa wa Endometriosis hudhihirika msichana anapovunja ungo na huja na maumivu makali kabla ,wakati na hata baada ya hedhi Lilian Leley ameishi na maumivu hayo kwa zaidi ya miaka thelathini.Amefanya upasuaji mara mbili na anatazamiwa kwenda kwenye operesheni nyingine hivi karibuni katika kujaribu kutafuta tiba ya ugonjwa wa EndometriosisAnasimulia masaibu yake ,ambapo anasema ndani ya mwezi huenda ni mzimu tu kwa siku 10
7/24/202410 minutes, 16 seconds
Episode Artwork

Fahamu kuhusu ugonjwa wa Endometriosis na changamoto za afya zinazofungamana nao

Endometriosis hutokea wakati tishu kwenye ukuta  wa tumbo la  uzazi zinapopatikana katika maeneo mengine ya mwili ikiwemo mapafu ,utumbo na hata ubongo Endemotriosis huwa na dalili zinazofanana magonjwa mengine ya uzazi  na unaweza kubainika kupitia kipimo cha Laparoscopy ambapo tishu hizo zinachunguzwa moja kwa moja
7/16/202410 minutes, 23 seconds
Episode Artwork

Maandishi yenye tahadhari yatasaidia mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa

Bidhaa za vyakula au vinywaji zikiwa na machapisho ya kuonesha kuwa vina sukari nyingi ,chumvi nyingi  au mafuta mengi mnunuzi anakuwa na fursa ya kuchagua vema Watalaam wamesema lishe ni kiungo muhimu katika kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo yanazidi kuongezeka na kuwa mzigo kubwa kwa jamii na mifumo ya afya
7/10/202410 minutes, 22 seconds
Episode Artwork

Mashujaa wa kupambana na Vitiligo wana matumaini makubwa ya jamii kuwaelewa

Jamii nyingi bado hazielewi kuwa ugonjwa wa Vitiligo hauwezi kuambukizwa kwa kutangamana ,kugusana au hata kushiriki mlo
7/10/20249 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Dunia yaadhimisha siku ya ugonjwa wa ngozi - Vitiligo

Vitiligo ni hali ya ngozi ambapo madoa meupe au mabaka yanaonekana. Inaweza kuathiri mtu yeyote, ikiwa ni pamoja na watoto na vijana. Sio hatari, si kama saratani ya ngozi au maambukizi unayoweeza kupata na kwa hiyo huwezi kuipata kutoka kwa mtu mwingine. Watu wengi wenye vitiligo wana afya nzuri. Baada ya muda, mabaka zaidi yanaweza kuonekana kwenye sehemu tofauti za mwili, hata kwenye nywele au ndani ya kinywa na pua. Mara nyingi huanza katika maeneo yaliyopigwa na jua. Takriban 1% ya dunia ina vitiligo
6/29/202410 minutes, 33 seconds
Episode Artwork

Muguka inaweza kusababisha madhara ya afya mtu anapokuwa mraibu

Kumekuwa na mvutano kati ya serikali ,uongozi wa kaunti za Pwani ya Kenya ,kuhusu Muguka kupigwa marufuku kwa sababu za kiafya Wakulima ,wafanyabiashara  na wenyeji wa Embu wanaozalisha Muguka kwa kiasi kikubwa hata hivyo wanasema hawajapata madhara yoyoteHata hivyo watalaam wa afya wanaonya uraibu wa Muguka unaweza kudhuru afya
6/21/202410 minutes, 19 seconds
Episode Artwork

Sera kuhusu idadi ya watu inavyoathiri uchumi ,afya na hali ya maisha

Mataifa ya Afrika bado yanaendelea kushuhudia kasi ya ongezeko la watu ijapokuwa chumi za Afrika hazifanyi vizuri inavyotakikana Watalaam wanaonya iwapo idadi ya watu haitodhibitiwa ,kupangiwa huenda mataifa mengi yakalemewa na idadi ya watu wanaowategemea wengineAidha kuna hatari ya sera za serikali kushindwa kukidhi mahitaji ya raia wake ,idadi inapokuwa kubwa
6/11/20249 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

Juhudi za kuukabili ugonjwa wa Mycetoma kutumia dawa zilizofanyiwa utafiti Sudan

Mycetoma ni mojawapo ya magonjwa yaliyopuuzwa ingawa unaendelea kuwaathiri wengi haswa watu wanaokaa maeneo kavu na jamii zilizotengwa Mycetoma hujidhihirisha kama donda ambalo haliponi bali linaendelea kukua na kuchimba sehemu athirika katika mwili
6/8/202410 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Mataifa ya Afrika yashinikiza mwongozo wa kukabiliana na hali ya dharura

Mataifa wanachama wa shirika la afya duniani ,WHO yanayokongamano katika kongamano la afya ya 77 jijini Geneva yanataka kuwepo mwongozo wa afya kukabiliana na hali ya dharura baada ya janga la COVID 19  Mataifa haya yanasisitiza kuwepo usawa kwenye kuzalisha na matumizi ya sampuli za kutengeneza sampuli zinazochangiwa na nchi mbali mbaliAidha usawa kwenye ufadhili ,usambazaji wa chanjo mpya na chanjo zinazotumika wakati wa majanga Kongamano hilo pia linatazamiwa kuja na mwafaka kuhusu marekebisho kwenye sheria za afya za mwaka 2005
5/29/20249 minutes, 32 seconds
Episode Artwork

Matatizo ya afya ya akili yasipotatuliwa huwaathiri mustakabali wa watoto

Watoto na  vijana walioshuhudia dhulma , kupata kiwewe,mara nyingi wanajikuta hawaamini katika uhusiano ,huwa waathiriwa wa dhulma za kimapenzi
5/22/202410 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Changamoto za afya ya akili miongoni mwa watoto na vijana Afrika

Kumekuwa na ongezeko la idadi ya watoto na vijana wanaokabiliwa na changamoto za  afya  ya akili Kila mwezi Mei dunia huungana kufanya kampeni ya watu kuwa makini na afya zao za akili ili kuzuia changamoto zaidi za akili ambazo wakati mwingi huishia kwenye umauti na matatizo zaidi ya kiafyaWatalaam wa afya wanasema watoto na vijana pia nao hupatwa na changamoto hizi zinazohusishwa na afya ya akili ,matatizo hayo yakiwemo kiwewe na msongo wa mawazo.Daktari bingwa wa afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta kitengo cha watoto ,Dkt Josephine Omondi anasema mazingira yanayochochea hali hii ni mizozo ya kifamilia ,matumizi mabaya ya mitandao ,shinikizo kutoka mazingira ya shule na pia matatizo ya kiafya yanayohusishwa na miaka ya awali ya mtotoMshauri Nasaha Naomi Ngugi anasema ni wakati wazazi wakakumbatia ukweli kuwa watoto na vijana huhitaji washauri nasaha na matibabu mengine ya matatizo ya afya ya akili
5/14/202410 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Mimba za utotoni zaendelea kuongezeka ukanda wa Afrika Mashariki

Idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimbo za utotoni wapo katika nchi za Afrika kwa mujibu wa shirika la afya duniani pia UNFPA Sababu zinazochangia mimba za utotoni ni pamoja na umaskini ,dhulma za kimapenzi ,ngono biashara na tamaduni hasi
5/8/202410 minutes, 20 seconds
Episode Artwork

Methadone yatumika kuwasaidia waraibu wa dawa za kulevya kupambana na Ukimwi

Kenya imeanza kutumia Methadone kupambana na Ukimwi baada ya Tanzania
5/7/20248 minutes, 40 seconds
Episode Artwork

Ajali za barabara Afrika huchangiwa na utepetevu, kasi na msongo wa mawazo

Ajali za barabara huchangia vifo vingi vya watu walio katika umri kati ya miaka mitano hadi 29 kwa mujibu wa WHO Uchunguzi unaofanywa baada ya ajali huonesha madereva wengi hulaumi kufeli kwa breki ilhali wengi wana msongo wa mawazo ,imesema mamlaka ya usalama barabarani nchini Kenya ,National Transport and Safety Authority. Ongezeko la magari,mchipuko wa miundo mbinu bora na ongezeko la watu yanazidi kufanya uwezekano wa mtu kuhusika kwenye ajali  kuwa mkubwa.
4/23/202410 minutes, 25 seconds
Episode Artwork

Watu wengi wanajikuta na magonjwa ya figo na ini,watoto wengi Sudan wakiaga

Kuna ongezeko la magonjwa ya figo na ini kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO inabashiri kuwa ongezeko hilo litakuwa juu zaidi kufikia mwaka 2030 ,hali hii ikichangiwa na hali ya maisha haswa ya raia katika nchi zinazoendeleaUgonjwa wa ini maarufu Hepatitis pia ni tishio kubwa haswa kwa raia wa Afrika ambayo inachangia asilimia 63 ya visa vya HepatatisNchini Sudan watoto wengi haswa walio chini ya umri wa miaka mitano wanazidi kupoteza maisha kutokana na utapiamlo unaohusishwa na ukosefu msaada  wa kibinadaam wakati huu vita vikiendelea kurindima
4/17/202410 minutes, 9 seconds
Episode Artwork

Uhitaji wa huduma za dharura za afya washika kasi ukanda wa Afrika

Shirika la AMREF Flying doctors linaonya kuwa mlipuko wa magonjwa yasiyoambukizwa yanazidi kuongeza uhitaji huku wigo la kupanua biashara likitanuka pia
4/10/20249 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Wanawake waongoza juhudi za kampeni za Afya bora ,DRC ikizidisha mapambano ya Kipindu Pindu

Wawawake kutoka ukanda wa Afrika wanajumuika Dar Salaam  mwishoni mwa juma kupiga jeki kampeni za kuboresha afya Nchini DRC mikakati iliyoweka kudhibiti mlipuko wa Kipindu Pindu ulioripotiwa katika mataifa ya Afrika ya Kusini ,inaendelea kulipa na hata kuwa msaada kwa mataifa jirani kama vile Zambia
4/2/20249 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Mataifa ya Afrika yanayoendelea bado yanachangia mzigo mkubwa wa TB

Usalama mdogo nchini Sudan Kusini umesababisha wagonjwa wengi kuchelewa kubainishwa TB na kupata matibabu ya mapema Watalaam wa afya wanashauri ulimwengu kukumbatia teknolojia za kisasa kama vile Akili Mnemba kurahisisha ubainishaji na kuongeza usahihi wa vipimo
3/29/202410 minutes, 23 seconds
Episode Artwork

Mageuzi yanayoletwa na nishati bunifu kisiwa cha Ndeda magharibi mwa Kenya

3/20/202410 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Wanawake mbele kuinua sekta ya sayansi na utafiti nchini Kenya

Idadi ya wanawake wanaongoza katika sekta mbali mbali bado ni ndogo barani Afrika. Kauli mbinu mwaka huu wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake ni kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuongeza kasi ya maendeleo,tunaangazia wanawake wanasayansi na watafiti nchini Kenya ,wakijikita kwenye utafiti wa magonjwa yaliyotengwa
3/13/202410 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Jamii ya Kibera jijini Nairobi inavyopambana na mimba za utotoni

Mimba za utotoni ni kizingiti kikubwa kinachoathiri elimu ya wasichana barani Afrika
3/10/202410 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

UNITAID mbioni kurahisisha upatikanaji wa dawa nadra sokoni

UNITAID imekuwa ikishirikiana na mataifa kuleta dawa mpya na za bei nafuu Upatikanaji wa dawa zilizo za viwango vya juu na kwa bei nafuu bado ni changamoto kubwa kwa mataifa yanayoendelea.Matibabu ambayo bado ni mapya hukumbwa na vikwazo vingi kuingia soko la kimataifa na sasa UNITAID imekuwa mbioni kuziba pengo hilo
2/28/20249 minutes, 21 seconds
Episode Artwork

Ushirikiano kati ya shirika la Village Reach na wizara ya afya nchini Kenya na nchi za ukanda wa Afrika

Village Reach ambayo kwa tafsiri rahisi ni kufikia maeneo ya vijijini, imefungua ofisi za kikanda jijini Nairobi kujaribu kusaidia serikali kusimamia namba ya dharura,usafirishaji wa sampuli za Polio na kuboresha utendakazi wa wahudumu wa afya wanaofanya kazi katika jamii tofauti Baada ya kupata mafanikio makubwa katika nchi za Msumbiji, Malawi ,Village Reach inapanga kutumia mafunzo hayo kusaidia kuboresha huduma za afya katika mataifa ya Afrika.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,Village reach imeimarisha huduma za utoaji chanjo ,usafirishaji wa chanjo kutumia ndege zisizo na rubani katika maeneo yasiyo na miundo mbinu ikiwemo mkoa wa Equateur.Aidha shirika hilo linatoa huduma kwa ushirikiano na serikali katika mataifa mengine yenye mzozo kama vile Niger na Sudan Kusini.Afisa mkuu mtendaji Emily Bancroft amesisitiza mifumo ya afya inastahili kuwa thabiti ili kuwa na uwezo wa kustahimili majanga na hali za dharura kama ilivyoshuhudiwa wakati wa Uviko 19
2/6/202410 minutes, 7 seconds
Episode Artwork

Changamoto za afya ya akili katika mitaa ya mabanda nchini Kenya

Shirika la afya duniani limeorodhesha ongezeko la watu wanaokumbwa na changamoto za afya ya akili hususan tangu kuzuka janga la Corona,kupanda gharama ya maisha na mfumuko wa bei 
1/24/20249 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Mikakati kuboresha matibabu ya TB

Juhudi zinaendelea kuhakikisha dawa mwafaka ya TB miongoni mwa watoto zinaendelea Licha ya kuwa TB inaweza kuambukiza watu wa umri wowote ,watoto kwa miaka wamekuwa wakiachwa nyuma katika matibabu ya TB. Watoto kwa miaka walilazimika kutumia donge za watu wazima.
1/15/20248 minutes, 31 seconds
Episode Artwork

Muendelezo wa ugonjwa wa Kisukari nchini Kenya na Sudan Kusini

Nchi zinazoendelea zinashuhudia ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa ukiwemo Kisukari
1/5/20249 minutes, 43 seconds
Episode Artwork

Wadau wa afya wapaza sauti kuhusu ongezeko la magonjwa tengwa wakionya ni tishio katika mifumo ya afya

Wadau katika sekta ya afya wana wasi wasi kuhusu ongezeko la magonjwa yaliyotengwa ambayo mengi yao hayana tiba au matibabu yao hayapatikani kwa urahisi au ni bei juu Wawekezaji katika sekta ya uzalishaji dawa ,chanjo hawavutiwi kuzitengeneza dawa za magonjwa hayo. Magonjwa hayo ni kama vile ugonjwa wa malale,matende ,Chikukungunya  na Dengue.
12/22/202310 minutes, 20 seconds
Episode Artwork

Matumizi ya Akili mnemba au AI kuboresha huduma za Afya

Ulimwengu umeanza kukumbatia matumizi ya akili mnemba au AI kuboresha huduma muhimu licha ya kuwa bado kukamilika mchakato wa kudhibiti matumizi ya teknolojia hiyo. Katika sekta ya afya mfumo wa AI umeanza kutumika kwenye ubainishaji wa magonjwa na ufuatiliaji wa matibabu.
12/22/202310 minutes, 6 seconds
Episode Artwork

Ugonjwa wa Utindio wa Ubongo almaarufu Celebral Palsy

Ugonjwa unaofahamika kama Utindio wa ubongo au Cerebral Palsy kwa lugha ya kimombo ni ugonjwa unaoathiri ubongo, namara nyingi  unatokea kwa watoto na husababishwa wakati damu inapovuja kwenye ubongo au hakuna hewa yakutosha.Unaweza kutokea wakati Mtoto anapoanza kupoteza fahamu punde baada ya kuzaliwa au mwezi wa kwanza wa kuzaliwa.Vilevile Jeraha kwenye ubongo linaweza kusababisha matatizo ya kuongea na ugumu wa kufahamu mambo.Sikiliza makala haya kutambua zaidi kuhusu ugonjwa huu.
12/22/202310 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Afya ya umma barani Afrika

Kongamano la tatu la CPHIA kuhusu huduma za afya barani Afrika.
12/1/20239 minutes, 7 seconds
Episode Artwork

Mpango wa afya kwa wote barani Afrika

Mataifa mengi yana matamanio ya kuhakikisha raia wake wanapata huduma bora za afya kwa bei nafuu,safari hii ikiwa bado ina panda shuka kwa mataifa mengi. Huduma za afya barani Afrika  zina mfungamano na hali ya kisiasa,uchumi  na pia utawala bora.
11/21/202310 minutes, 19 seconds
Episode Artwork

Faida za mazoezi ya Yoga kwenye mwili wa mwanadamu

Yoga ni mazoezi ya mwili yanayoongeza nguvu kwa misuli na kunyoosha  mifupa lakini pia yoga inalenga kuunganisha mwili, ufahamu, na akili kwa pamoja. Hivyo ni tofauti kabisa na aina nyingine za mazoezi.Sikiliza makala haya kwa ufahamu zaidi.
11/16/202310 minutes
Episode Artwork

Ongezeko la visa vya mdomo Sungura

Watalaam wanahofu kuhusu ongezeko la watoto wanaozaliwa na mdomo sungura au Cleft Clip Licha ya kuwa utafiti haujabainisha moja kwa moja sababu ya mdomo sungura ,lishe,urithi na matumizi ya sigara zimetajwa kuchangia hali hii
11/3/20239 minutes, 46 seconds
Episode Artwork

Hofu kuhusu hatma ya mchakato wa amani DRC unaoratibiwa na AU

Umoja wa mataifa umeonya uwezekano wa kuibuka vita kati ya DRC na Rwanda Rwanda na DRC zimeendelea kulaumiana kuhusu hali mbaya ya usalama mashariki mwa DRC. Rwanda imeongeza usalama katika mipaka yake na DRC baada ya raia wake kujeruhiwa na risasi iliyotokea upande wa Congo.
10/25/202310 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Mpango wa afya kwa wote nchini Kenya ambapo wafanyikazi watachangia 2.75 ya mishahara

Kenya katika sherehe za hivi karibuni za mashujaa ,imezindua mpango wa afya kwa wote. Mpango huu wa afya unazingatia raia kupata huduma bora kuanzia vituo vya afya vya daraja la kwanza hadi hospitali kubwa bila malipo .
10/24/202310 minutes, 18 seconds
Episode Artwork

Ongezeko la akina baba wanaowalea watoto pekee yao

10/23/20239 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

Shirika la madaktari wasio na mpaka lataka wanawake waliodhulumiwa kingono kupata msaada zaidi ya matibabu

Wanawake wakimbizi jijini Goma waliokimbia vita wameathirika afya ya akili na mwili na wanahitaji msaada hata baada ya kupata matibabu.Wengi wamebakwa zaidi ya mara moja wakienda kutafuta chakula na mahitaji mengine
10/10/20239 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Wauguzi wanaowahudumia wagonjwa wa saratani walia kubeba mzigo mkubwa unaowaathiri hata afya zao

Idadi ya wagonjwa wanaougua saratani inazidi kupanda kila siku,katika mataifa ya ulimwengu,vile vile idadi ya vifo vinavyosababishwa na saratani Wauguzi wanaowahudumia wagonjwa hao hulazimika kutembea na mgonjwa ambaye mara nyingi huwa na maumivu makali , kudhurika wakati wa matibabu ,wengine kufariki na inapotokea ,muuguzi ndiye anayehitajiwa kuwashughulikia pia familia zao.
9/26/20239 minutes, 48 seconds
Episode Artwork

Wanawake wakimbizi eneo la Goma DRC wanakabiliwa na changamoto za kiafya na dhulma za kingono

Wanawake waliokimbia mapigano mashariki mwa DRC ,wamepitia dhulma za kijinsia zaidi ya mara moja ,hata baada ya kuwepo kwenye kambi za wakimbizi Shirika la madaktari wasio na mipaka ,MSF limesema kila siku ,kuna wanawake 70 wanaotibiwa katika vituo vyao kutokana na kukithiri dhulma za kingono.MSF huwapa huduma za dharura,kupanga uzazi na wengine wanalazimika kupewa huduma za kuavya mimba kwa njia salama.Hali ya kambi wanazokaa,inawaweka kwenye hatari ya kushambuliwa ,kubakwa huku wengine wakipitia dhulma hizo wanapokwenda nje ya kambi kutafuta mahitaji mengine ya kila siku.
9/19/202310 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Je matumizi ya sukari mbadala inafaa?

Mwezi Septemba dunia inapojiunga kuleta hamasa kuhusu afya ya akili,idadi ya vijana wanaojiua bado iko juu. Na watalaam vile vile wanaonya kuhusu sukari mbadala au artificial sweeteners ambazo japo zinadhaniwa kuwa salama ,zina madhara katika viungo vya mwili na utendakazi wa mwili
9/15/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Ongezeko kwa maambukizi ya HIV miongoni mwa vijana ni tishio kwa mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi

Ngono zembe miongoni mwa vijana inawaweka wengi kwenye hatari ya kupata HIV na saratani ya shingo ya uzazi
8/29/20239 minutes, 42 seconds
Episode Artwork

Soko huru ya sigara za kisasa ni tishio kubwa la afya

Kasi ya watumiaji wa sigara za kisasa kama vile Nicotine Pouches na Sigara ya Kielectroniki imezidi kupanda ,vile vile uraibu miongoni mwa vijana na wanafunzi Wanaotumia sigara za kisasa wanahoji kuwa hazina moshi au harufu mbaya ,hali ambayo watalaam wanasema inachangia uraibu wa haraka na madhara zaidi kwa viungo vya mwili
8/22/20239 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

Upandikizaji viungo vya mwili Afrika Mashariki

Kupandikiza au kuhamisha viungo vya mwili kama njia mojawapo ya matibabu inazidi kushika kasi .Mataifa mengi yanafanya upandikizaji wa figo ,moyo ,ini ,Cornea na sehemu za umme. Kuna hata hivyo changamoto katika hili,mataifa bado hayana sheria za kutosha kusimamia zoezi hili. Kwa sasa upandikizaji unafanyika kwa watu wanaohusiana huku kukiwa na hitaji kubwa ya viungo muhimu vya mwili.Hii ni kutokana na kuwepo wagonjwa wengi wanaopata viungo vyao muhimu vimefeli kutokana nao kuwa na magonjwa yasiyoambukizwa.
8/15/202310 minutes, 18 seconds
Episode Artwork

Chanjo ya Kipindu Pindu na changamoto za akina mama wanaonyonyesha

Juma la kwanza la Agosti ,ulimwengu huungana kupigia upatu juhudi za akina mama kuweza kuwanyonyesha wanao bila vikwazo katika miezi sita ya kwanza. Katika juhudi za kupambana na Kipindu Pindu ,Kenya inaendelea na kampeni ya kuchoma chanjo dhidi ya Kipindu Pindu chanjo ambayo imeshuhudia uhaba kutokana na uhitaji mkubwa katika mataifa mengi.
8/8/202310 minutes, 15 seconds
Episode Artwork

Mataifa ya Afrika yanavyopambana kukabili usugu wa vimelea,Antimicrobial Resistance

Tatizo la usugu wa vimelea ni changamoto kubwa katika sekta ya afya ,watalaam wakihitajika kutumia gharama kubwa kwenye matibabu
8/1/20239 minutes, 42 seconds
Episode Artwork

Mlipuko wa Magonjwa yanayohusishwa na wanyama

Mlipuko wa magonjwa yenye asili ya wanyama wa Pori na hata wale wa kufugwa nyumbani umeendelea kushuhudiwa ukanda wa Afrika Mashariki Magonjwa haya ni pamoja na Marburg ,Homa ya Mgunda , Ebola na Covid 19
7/13/20239 minutes, 31 seconds
Episode Artwork

Ushirikiano kati ya sekta binafsi na ya umma kuboresha huduma za afya

Mataifa mengi barani Afrika bado yana changamoto ya kuwahakikishia raia wao huduma za kisasa za afya na ambazo haziwagharimu zaidi Katika makala haya tunaangazia mjadala wa kushirikisha sekta binafsi kuboresha huduma za afya barani Afrika.Aidha tunaangazia mpango wa kupunguza idadi ya vifo vya watoto walio chini ya umri ya miaka mitano kaunti ya Kwale ,Pwani ya Kenya kwa kuorodhesha habari zao muhimu kwa mfumo wa kidijitali tangu wanapozaliwa
7/5/20239 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Ugonjwa wa Kipindu Pindu Homabay nchini Kenya

Mataifa mengi barani Afrika yameripoti mlipuko wa Kipindu Pindu Katika makala haya ,tunaangazia Kipindu Pindu katika kaunti ya Homabay ,magharibu mwa Kenya ,karibu na ziwa Victoria .Pia tutakufahamisha kuhusu juhudi za kupambana na ugonjwa huo
6/29/202310 minutes, 11 seconds
Episode Artwork

Ugonjwa wa Matende

Magonjwa yaliyotengwa kama Matende bado yanawapa changamoto nyingi raia wengi  Matende au Elephantiasis ni baadhi ya magonjwa yaliyotengwa au kusahaulika ijapokuwa madhara yake ni makubwa.Mara nyingi matibabu yake huwa gharama juu wakati kinga kupitia dawa za minyoo imeendelea kupuuzwa na raia wengi kutokana na dhana kuwa dawa zinazosambazwa bila malipo na serikali si vya viwango vya juu
6/22/20239 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Juhudi za kupunguza gharama katika matibabu ya macho

Raia wengi nchini Kenya wana uhitaji wa miwani kutokana na matatizo ya macho.Wengi wao hata hivyo hawapati miwani kutokana na gharama ya juu Katika makala haya tunaangazia mchango wa kampuni ya Mamy Eye Wear kupunguza gharama ya miwani huku ikizingatia ubora.
6/16/20239 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

Matumizi ya Dawa za Kulevya Sudan Kusini

Watu walioacha kutumia dawa za kulevya nchini Sudan wanasaidia juhudi za kupambana na dawa za kulevya
6/6/20239 minutes, 29 seconds
Episode Artwork

Mapambano kupunguza matumizi ya Tumbaku na mchango wa sekta binafsi katika afya

Mataifa ya ulimwengu yanapoadhimisha siku ya Tumbaku Mei 31,kuna hofu juhudi za kupunguza matumizi ya tumbaku zinaonekana kurudishwa nyuma na ukiukaji wa sheria za kupambana na matumizi ya tumbaku Sheria kuhusu ushuru unaotozwa kwenye bidhaa za tumbaku bado haifuatwi kikamilifu .Wafanyibiashara wanaouza sigara chini ya pakiti moja wanatuhumiwa vile vile kurudisha mapambano ya kupunguza matumizi ya tumbaku.Isitoshe kampuni zinazotengeneza bidhaa hizo zimekuja na bidhaa mpya ambazo zinawavutia watumizi wa umri mdogo na pia wanawake .Aidha kwenye makala haya tunakufahamisha kuhusu juhudi za sekta binafsi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuchangia kupunguza idadi ya raia wanaoumwa kwa kuwatuza na kuwasaidia kuepukana na magonjwa haswa yasiyoambukizwa.
5/31/202310 minutes, 7 seconds
Episode Artwork

Kuipa hedhi heshima kama haki ya msingi miongoni mwa wanawake

Umaskini  umechangia wasichana wengi kukosa Sodo  na kushindwa kwenda shule Ukosefu wa sodo ndio umeonekana kuchangia wasichana wengi nchini Kenya kutoudhuria shule hasa maeneo ya mashinani.Utamaduni pamoja na ufukara ndivyo vimeonekana kuchangia halii hii kwa asilimia kubwa. Utafiti uliofanywa na shirika la Borgen, asilimia 65 ya wasichana na wanawake nchini kenya hukumbwa na ukosefu wa sodo hivyo kuathiri masomo na shughuli zao za kila siku. Lakini hata hivyo katika kaunti ya kwale ,idadi ya wasichana imeanza kuongezeka shuleni baada ya jamii pamoja na mashirika mbalimbali kuanzisha mpango wa ugavi wa sodo kwa wasichana.
5/25/20239 minutes, 28 seconds
Episode Artwork

Nafasi ya wauguzi kwenye mkondo wa huduma za afya na huduma za afya kwa wanaoishi na ulemavu

Kila Mei kati ya tarehe 8- 14 dunia huwaenzi wauguzi ambao ni kiungo muhimu kwenye huduma za afya. Kwenye makala haya tunaangazia wauguzi na mchango wao kutoa huduma za afya .Tumezungumza na nesi Caroline Mwangi anayehudumu katika chumba cha dharura katika shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF,nchini Kenya. Tumezungumza pia na Faustin Chepchirchir kutoka shirika linalowashughulikia watu wanaoishi na ulemavu kuhusu namna ya kuboresha ubora wa huduma za afya kwa watu wa makundi tengwa
5/16/202310 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

Mchango wa Wakunga katika utoaji huduma za kimsingi kwenye jamii

Kila Mei tarehe tano ,ulimwengu huadhimisha siku ya kimataifa ya wakunga Jamii ya Wapemba wanaoishi kaunti ya Kwale ,Pwani ya Kenya kwa kuwa hawana uraia,imekuwa ikitegemea pakubwa huduma za mkunga.
5/9/202310 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

Mpango wa afya kwa wananchi wa Zanzibar

Zanzibar inaanza kutekeleza mpango wa mfuko wa bima wa afya kwa raia wote kupata huduma za afya bila malipo. Waziri wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui anasisitiza  ndio njia pekee itakayowawezesha Wananchi wote yakiwamo makundi yasiyokuwa na uwezo kufaidika na huduma za Afya kikamilifu.
5/2/202310 minutes, 1 second
Episode Artwork

Dunia yaadhimisha siku ya Malaria

Ulimwengu huadhimisha siku ya malaria kila tarehe 25 mwezi wa nne. Malaria ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaenezwa na mbu wa jenasi  anayefahamika kama Anopheles na kusababishwa na kidubini aina ya Plasmodium. Kulingana na shirika la afya duniani Nigeria inasajili visa hivyo  kwa asilimia 31.3, DRC asilimia 12.3,Tanzania kwa asilimia 4.1 na Niger kwa asilimia 3.9. Vilevile Kulingana na ripoti ya shirika la maendeleo ya Ufaransa nchini Kenya  AFD ni kwamba Kisumu inaongoza kwa visa vya malaria kwa hadi asilimia 40. Na Kwenye makala haya tunazungumzia ugonjwa huu na jinsi ya kupambana nao. Nimezungumza nae Peris Oloo  ambae anaugua malaria na anaelezea baadhi ya dalili alizokua nazo.kisha Daktari anaezungumzia Ugonjwa huu kwa kina na jinsi mtu anaeza uepuka.
4/26/20239 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Jinsi mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri afya na haki za akina mama

Mabadiliko ya tabia nchi yameendelea kufifiza usalama wa chakula chenye lishe,kupunguza uwezo wa akina mama wanaotegemea kilimo asili kulisha familia zao na kuongeza idadi ya magonjwa yasiyoambukizwa Kwenye makala haya tunaangazia kilimo cha wimbi ambacho japo ni cha asili,ni chakula chenye lishe na kinachohitajika kwa sasa kwa ajili ya wagonjwa wa kisukari.Kupungua kwa uzalishaji wa wimbi kutokana na ukame,gharama ya juu ya mbegu na mashamba yanayotumika kwa mara ya kwanza ,yamechangia akina mama wengi hawawezi kuwalisha familia zao kwa kuwa wimbi ni kipato cha wanawake,inatumika kuwalisha watoto na watu wenye umri uliokwenda wengi wao wakiwa wanauguza ugonjwa wa kisukari. Tunaangazia vile vile kilimo cha sasa cha wimbi ambacho wanawake katika kaunti ya Bomet ,kusini mwa bonde la ufa ,nchini Kenya wamebidi kukumbatia ili kuendelea na kilimo cha wimbi wakati huu ulimwengu unapokumbwa na athari haasi ya mabadiliko ya tabia nchi.
4/18/202310 minutes, 12 seconds
Episode Artwork

Afya ya kinywa na tabia za kuzingatia kuchochea afya ya kinywa

Afya ya kinywa ni muhumi ilivyo afya ya sehemu zingine za mwili. Katika makala haya ,tunakupa ufahamu zaidi kuhusu afya ya kinywa ;usafi wa meno,ulimi  na ufizi .Daktari David Amenya anaelezea namna ya kupiga mswaki,mswaki sahihi,matibabu ya meno miongoni mwa maswala mengine.
4/11/202310 minutes, 21 seconds
Episode Artwork

Mpango wa Car Free jijini Kigali unaolenga kuboresha afya na usafi wa jiji

Kila Jumapili ya kwanza ya kila mwezi na ya tatu wakazi wa Kigali hujumuika kufanya mazoezi ya pamoja Car Free jijini Kigali imezidi kupata umaarufu,raia wanajumuika kufanya mazoezi pamoja na kuja pamoja kama jamii,huku wakifurahia  mandhari ya mji huo ,usafi na mpangilio mzuri.Watalaam wa afya wanasema kuwa kuondoa pia magari barabarani husaidi kupunguza uchafuzi wa hewa kaa na kuwapa wananchi nafasi ya kuvuta hewa safi. Kwenye makala haya tunakupa mengi zaidi kuhusu mkakati wa Car Free.
4/5/202310 minutes, 12 seconds
Episode Artwork

Ugonjwa wa Marburg unavyosambaa Afrika na mapambano ya TB nchini Kenya

Mataifa zaidi barani Afrika yameripoti  virusi vya Marburg . Na kwenye mapambano ya TB nchini Kenya,ingawaje bado kuna idadi kubwa ya TB Sugu ,teknolojia mpya ya Gene expert iliyoboreshwa imeendelea kuchangia ubainishaji wa haraka Equitoria Guinea imeripoti vifo 8 vinavyohusishwa na ugonjwa wa Marburg,huku Tanzania ikiwa imeripoti vifo vya watu watano. Na kwenye mapambano ya TB nchini Kenya Michael Macharia mshauri wa kiufundi katika kanisa katoliki na pia Peter Muchui shujaa wa kupambana na TB wameeleza kuna hatua nyingi ambazo Kenya imepiga kuelekea mwaka wa 2030 ambapo mataifa yanatazamiwa yawe yameelekea kuushinda ugonjwa huo
3/28/202310 minutes, 22 seconds
Episode Artwork

Mapambano ya kumaliza kifua kifuu nchini Kenya kuelekea mwaka 2035

Kwa mujibu wa mpango kazi wa shirika la afya duniani,WHO,mataifa yanastahili kupunguza vifo vinavyosababishwa na TB kwa asilimia 90 na maambukizo mapya kwa asilimia 80. Kila mwake tarehe 24 mwezi Machi ,dunia huungana kuadhimisha siku ya TB , kaulimbiu ya siku ya kifua kikuu duniani mwaka huu. ikiwa  Ndiyo tunaweza kuwekeza zaidi kumaliza Kifua Kikuu nchini Kenya kufikia 2035 ikiwa tutashirikiana. Kukomesha Kifua Kikuu nchini Kenya si jukumu la Wizara ya Afya kupitia mpango wa kitaifa wa Kifua Kikuu pekee bali ni jukumu letu sote. Aidha katika makala haya ,utaskia utambulisho kuhusu usafi wa kinywa naye daktari David Amenya.
3/21/202310 minutes, 12 seconds
Episode Artwork

Kongamano la afya kujadili uthabiti wa mifumo ya afya na athari za mabadiliko ya tabia nchi Afrika

Kuna haja ya Afrika kuwa na mifumo thabit ya afya ,kuweka rasli mali zake pamoja na kuwa ajenda moja kuhusu afya ,wakati huu athari hasi ya mabadiliko ya tabia nchi zinapoendelea kukabili ulimwengu Viongozi wa mataifa ya Afrika pamoja na wadau kwenye sekta ya afya wamejadiliana jijini Kigali kwenye kongamano la AHAIC, kuhusu kutembea pamoja kuwa na ajenda inayofanana,mifumo inayostahimili majanga na jinsi ya kuoanisha swala la mabadiiko ya tabia nchi kwenye mifumo ya afya
3/14/202310 minutes, 14 seconds
Episode Artwork

Magonjwa yaliyotengwa ya Chikungunya na Homa ya Dengue bado changamoto

Magonjwa yaliyotengwa ingawaje hayajapewa kipau mbele bado ni changamoto kwa raia katika mataifa yanayoendelea Katika makala haya ,tunakufahamisha kuhusu ugonjwa wa Chikungunya na Homa ya Dengue,inayosababishwa na mbu anayependa mahali pana joto.Katika maeneo haya aina ya mbu anayebeba virusi vinavyosababisha magonjwa haya mawili yenye dalili za kufanana ,huzalia katika maeneo yenye maji maji na huambukiza hata mchana.Daktari Hussein Gure Bilal anasimamia kitengo cha magonjwa yaliyotengwa katika kaunti ya Mombasa
3/8/202310 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

Unene uliopitiliza na magonjwa yasiyoambukizwa

Shirika la afya duniani limeonya kuhusu kuongezeka kwa watu walio na uzito wa kupitiliza ,hali inayowaweka hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa Shirikisho lilaloangazia unene ulimwenguni ,limesema zaidi ya nusu ya watu ulimwengu watakuwa na uzito wa juu au unene wa kupitiliza kufikia mwaka 2035 ikiwa hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo hazitachukuliwa Mataifa yanayoendelea na maskini barani Afrika na Asia yanatazamiwa kushuhidia hali hii. Baadhi ya sababu zinazochangia hali hii ni ulaji na watu kushindwa kufanya mazoezi.Katika makala haya tunazungumza na watu wanaopambana kupunguza uzito,watalaam wa afya na pia wapishi kuelewa nini kinaweza kusaidia mtu kufanya chaguo zuri kuhusu chakula na mifumo ya maisha inayofanya mtu kuishi maisha yenye afya.
3/3/20239 minutes, 42 seconds
Episode Artwork

Wakaazi wa Mombasa washiriki matembezi ya masafa marefu kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa

Shirika la afya duniani limeonya kuhusu ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa haswa katika mataifa yanayoendelea Magonjwa yasiyoambukizwa ni changamoto kubwa kwa watu wengi kote ulimwenguni ,magonjwa haya yakichangiwa na maisha ya kisasa ambapo watu wengi hawazingatii vyakula vyenye lishe na mazoezi.Katika Makala haya tunakuletea namna moja ya kupambana na magonjwa haya ,mazoezi ya kutembea ambayo wakaazi wa Mombasa wamekumbatia.
2/21/202310 minutes, 19 seconds
Episode Artwork

Ongezeko la akina mama wanaochagua kujifungua kwa njia ya upasuaji nchini Kenya

 Idadi ya  Wanawake  nchini Kenya wanaojifungua hospitalini imeongezeka ingawaje idadi kubwa pia wanachagua njia ya upasuaji Licha ya gharama kubwa ya kujifungua kwa njia ya upasuaji,wanawake wengi nchini Kenya wanachagua njia hiyo na kupuzia hatari ambazo huwakumba wengi wanaotumia njia hiyo.
2/18/20239 minutes, 37 seconds
Episode Artwork

Vipimo vya DNA vinavyofanyika nyumbani

Utata kuhusu unasaba umekuwa ndiyo sababu ya watu wengi kutaka kufanya vipimo vya DNA ambavyo huwa ghali na kuhitaji umakini mkubwa. Ugunduzi wa vifaa vya kupimia  vipimo vya vinasaba au DNA nyumbani umeendelea kuibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maswala ya uhalisia wa vipimo hivyo na pia maadili ya kuzingatiwa katika vipimo hivyo.Daktari Yusuf Mahat anayehudumu katika hopsitali ya rufaa ya Nakura,nchini Kenya,anaeleza yote unayohitaji kufahamu kuhusu vipimo hivyo.
2/7/202310 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

Kushamiri kwa kipindu pindu katika mataifa ya Afrika na juhudi kuikabili

Mataifa ya Afrika yameendelea kuripoti uwepo wa  Kipindu Pindu nchi la Malawi ikiwa imeathirika zaidi. Barani Afrika ,mlipuko wa ugonjwa Kipindu Pindu umeendelea kuripotiwa .Taifa la Malawi ilibidi kufunga shule na kuomba msaada kutoka mataifa mengine kuikabili. Nchini DRC ,maambukizo mapya pia yamezifdi kupanda na wahudumu wa afya wako mbioni kutoa chanjo kwa raia katika maeneo yenye idadi kubwa ya maambukizo mapya.
2/3/202310 minutes, 10 seconds
Episode Artwork

HAMASISHO KUHUSU SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI ( CERVICAL CANCER)

Saratani ya shingo ya kizazi ni mojawapo ya aina ya saratani inayoongoza katika idadi ya vifo dunia ikifuatiwa na saratani ya matiti. Kwenye Makala ya wiki hii, mwandishi wetyu wa masuala ya afya Carol Korir, amezungumza na Dkt Yusuf Mahat, daktari nchini Kenya ilikufahamu zaidi kuhusu aina hii ya saratani.
1/24/20239 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Mzigo wa matumizi ya dawa za Kulevya nchini Kenya

Matumizi ya dawa za kulevya ,umeendelea kuwa mzigo katika mataifa mengi ,familia nyingi zikilazimika kuwapoteza jamaa zao ambao wangechangia ujenzi wa taifa Kwa mujibu wa shirika la afya duniani ,WHO ,kuna watu karibu milioni 40 ambao wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya na wanaohitaji msaada wa matibabu ya kitalaam kuwarejesha katika hali zao za kawaida. Kwenye makala haya tumezungumza na raia,watu waliotumia dawa za kulevya ,walio wahi kuuza na watalaam kuhusu swala zima la dawa za kulevya. Je ina manufaa yoyote?
1/20/20239 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Mashirika ya kiraia yanavyopambana na unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya HIV Kenya

Unyanyapaa na ukosefu wa usawa kwenye mikakati ya kupambana na HIV ni baadhi ya sababu zinazorudisha nyuma mapambana kushinda UKIMWI Katika mtaa wa Kibera ,jijini Nairobi Kenya ,mashirika ya kiraia yanawasaidia watu wanaoishi na virusi vya HIV kuishi maisha ya kawaida.Victor Moturi amezungumza na wakaazi wa Kibera wanaonufaika na mpango wa Mentor Mother
1/5/20239 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

MSF inatumia teknolojia ya Antibiogo kupambana na usugu wa vimelea

Shirika la afya duniani WHO limeeleza wasi wasi kuhusu ongezeko la usugu wa vimelea. Takwimu za WHO zinaeleza kuwa idadi ya kubwa ya dawa aina za antibiotics zinazotumika kwenye mataifa yanayoendelea,yanatumika vibaya na hii inatia wasi wasi ya kuongeza visa vya usugu wa vimelea vinavyosababisha magonjwa tofauti. Shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF limekuja na teknolojia mpya ya kukabili tatizo hili ,kutumia Antibiogo
12/26/20229 minutes, 20 seconds
Episode Artwork

WHO yasambaza chanjo ya Ebola Uganda ,utapiamlo ukiendelea kuwa Sugu Nigeria na nchi za Afrika

Shirika la afya duniania WHO limesambaza tayari dozi kadhaa za chanjo ya Ebola nchini Uganda. Na katika mataifa kadhaa ya Afrika yakiwemo Nigeria ,Kenya ,utapia mlo unaendelea kushuhudiwa. Katika Makala haya ,tumeangazia shughuli ya kuchoma chanjo ya Ebola nchini Uganda. Vile vile hali ya baa la njaa nchini Nigeria na mataifa ya Pembe ya Afrika  ,Afrika Mashariki ambapo hali hiyo imesababisha kuongezeka visa vya utapia mlo. Nchini Nigeria ,majimbo yanayokabiliwa na mashambulio ya makundi ya kijihadi ,yameathirika zaidi.
12/26/202210 minutes, 10 seconds
Episode Artwork

Waathiriwa wazungumzia unyanyapaa na ukosefu wa usawa

Shirika la umoja wa mataifa linaloratibu mikakati ya kupambana na Ukimwi ,UNAIDs limeonya kuhusu kutokuwa na usawa ulimwengu katika mapambano hayo Watu ambao wameishi na virusi vya HIV na kuongoza kampeni za kupigana na ugonjwa wa UKIMWI wamehofu kuwa bado unyanyapaa na ukosefu wa usawa ni tishio kubwa. Maureen Murenga ni mwanaharakati kutoka Kenya na Meja Rubaramira Rubanga anatokea Uganda
12/9/202210 minutes, 16 seconds
Episode Artwork

Vyakula vya kiasili kama njia ya kukabili njaa

Watu wengi wanakabiliwa na njaa barani Afrika Vyakula vya kiasili vimependekezwa kuwa njia mojawapo ya kupambana na njaa .Raia wanahimizwa kukuza na kukumbatia kando na vyakula walivyozoea kila siku.
12/5/20229 minutes, 25 seconds
Episode Artwork

Kuzalishwa kwa Vyakula vya GMO nchini Kenya,watalam wakinzana

Katika kujaribu kuimarisha usalama wa chakula nchini Kenya ,serikali iliondoa maarufuku ya uzalishaji na uagizaji wa vyakula vya GMO. Serikali ya Kenya miezi michache ,iliyopita iliidhinisha kuzalishwa na kuagizwa kwa vyakula vinavyozalisha kwa njia ya kisayansi ,GMO ,kuliziba pengo la uhaba wa chakula.Watalaam ,wasayansi wamekuwa wakilumbana kuhusu usalama wa vyakula hivyo na mahakama ya Kenya kwa sasa imeharamisha amri hiyo ya serikali.
12/5/202210 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Uviko 19 ulivyoathiri mapambano dhidi ya Ukimwi DRC

Uwekezaji kwenye mapambano dhidi ya Uviko 19 umefanya serikali kuweka pembeni mikakati ya kupigana na Ukimwi Katika maeneo kadhaa nchini DRC ,watalaam wameripoti ongezeko kubwa la maambukizo mapya ya virusi vya HIV na hata vifo tangu kuzuka kwa janga la Corona.
12/5/20229 minutes, 59 seconds
Episode Artwork

Dalili na utaratibu kuwasaidia wanaokabiliwa na matatizo ya afya ya akili

Katika makala  hayo ,tunatambua namna unaweza kumsaidia mapema yeyote anayesumbuka na afya ya akili Bara Afrika bado ina idadi kubwa ya watu wanaojitoa uhai au kusumbuliwa na matatizo ya akili. Ni muhimu basi kwa jamii kutambua baadhi ya viashiria vya mtu anayesumbuka na matatizo hayo na kuweza kumpa msaada mapema iwezekanavyo. Mshauri nasaha Naomi Ngugi anatupa mwanga nini cha kuangalia kuweza kutambua mtu huenda ana matatizo hayo ya akili.
11/11/202210 minutes, 6 seconds
Episode Artwork

Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwenye Mataifa ya Kusini mwa Afrika

Nchi kadhaa barani Afrika na Asia zimeripoti mlipuko wa kipindupindu mwaka 2021 na 2022, ambapo nchini Kenya takwimu zilionyesha katika mwezi Oktoba, kaunti 6 katii ya 47 zilikuwa katika hatari. 
11/9/20229 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Afya ya akili barani Afrika bado haizingatiwi

Kwenye makala haya ,tunazungumzia namna ya kujikinga na Ebola ,ugonjwa unaoendelea kuripotiwa nchini Uganda ,vile vile tunazungumzia afya ya akili ,wakati ulimwengu ukiwa umeadhimisha siku ya kimataifa ya afya ya akili ;jumatatu tarehe 10 mwezi wa Kumi.WHO ina was wasi idadi kubwa ya watu wanaojiua wanatokea Afrika
10/13/20229 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Hali ya Sekta ya Afya Afrika wakati wa magonjwa ya milipuko

Kwenye makala haya tunaangazia hali ya huduma za afya na hali ya wahudumu wa afya barani Afrika ,wakati huu ukanda huu ukiripoti kuongezeka kwa magonjwa ya milipuko.Shirika la afya duniani linasikitika kuwa wahudumu wa afya wanandelea kupoteza maisha wakati wanahudumia wagonjwa wakati wa magonjwa ya milipuko. Baada ya janga la Corona ,mataifa kadhaa ya Afrika yanashuhudia msambao wa ugonjwa wa Ebola
10/5/202210 minutes, 18 seconds
Episode Artwork

Mlipuko wa Ebola Sudan nchini Uganda

Tunazungumzia ugonjwa wa Ebola ambao unaendelea kuripotiwa nchini Uganda ukiwa ni mlipuko wa tano. Watu 24 wamepoteza maisha huku ugonjwa huu ukiendelea kusambaa. Aina hii ya Ebola Sudan japo haijaripotiwa kusababisha vifo vingi kwa haraka kama vile Ebola Zaire iliyokuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,bado haina chanjo. Mataifa majirani kama vile Rwanda ,Tanzania na Kenya kutokana na hali hii zimeanza kuweka mikakati ya kukabiliana na hali ya dharura 
9/29/20229 minutes, 24 seconds
Episode Artwork

Magari ya Tuk Tuk yanavyotumika Mombasa Kenya kuwaokoa akina mama

Idadi ya akina mama haswa waja wazito na watoto chini ya umri wa miaka mitatu wanaofariki ,bado iko juu barani Afrika.Hii ni kutokana na ukosefu wa huduma za afya au miundo mbinu ambazo wanawake wanaoweza kufikia kwa haraka.Jiji Mombasa ,Pwani ya Kenya wanaharakati wamekuja na mbinu ya Tuk Tuk ambazo zimekarabatiwa kuwa ambulensi kuwasaidia wanawake kufika hospitali kwa urahisi
9/23/20229 minutes, 52 seconds