Podcast namba moja Tanzania ambayo itakusaidia kuongeza thamani ya maisha yako kupitia mafunzo ya maendeleo binafsi, elimu ya fedha, elimu ya Mahusiano na elimu ya kujitambua
Maisha Ni Kuthubutu Podcast ipo kukupa maarifa yatakayo kusaidia wewe kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako
Podcast zinafanywa na Innocent Ngaoh
Instagram: @Lolo_Facts
Uchambuzi Wa Kitabu Cha WHO MOVED MY CHEESE? (Nani Kahamisha Jibini Yangu?)
Nani kahamisha jibini yangu? Ni kitabu ambacho kinakusaidia kukabaliana na mabadiliko ambayo hukutarajia wala kutegemea kwenye kazi na maisha.
Kitabu kipo kwa mfumo wa stori ambao inahusisha wahusika wanne ambao ni
1. Sniff
2. Scurry
3. Hem
4. Hew
Ni kitabu ambacho utajifunza namna ya kukabiliana na mabadiliko kwenye maisha.
Naamini kupitia uchambuzi wa kitabu hiki utafurahia Sana.
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
31-1-2024 • 27 minuten, 39 seconden
Uchambuzi Wa Kitabu Cha MONEY FORMULA (Kanuni Za Fedha)...!
Elimu ya fedha isiyofundishwa shuleni wala vyuo vikuu imepelekea kushindwa kupiga hatua kwenye eneo la fedha.
Kitabu cha MONEY FORMULA kinakupa mwongozo sahihi ni kwa namna gani unaweza kufanikiwa kifedha kupitia sheria, kanuni na mitazamo sahihi kuhusu fedha.
Hakikisha unafanyia kazi ambayo unajifunza.
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
24-1-2024 • 29 minuten, 45 seconden
Uchambuzi Wa Kitabu Cha THE RICHEST MAN FROM BABYLON (Tajiri Kutoka Babeli) Kwa Lugha Ya Kiswahili..
Unataka kufanikiwa kifedha na kuwa tajiri basi kitabu cha THE RICHEST MAN FROM BABYLON kitakupa mwongozo na sheria za fedha.
Uchambuzi wa sura 11 ambazo utapata kwenye episode hii.
Hakikisha unaandika pembeni ambayo utajifunza rafiki.
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
21-1-2024 • 46 minuten, 19 seconden
Uchambuzi Wa Kitabu Cha "BIRD BY BIRD"
Ni kitabu mahususi kimeandikwa na Anne Lemmot ambacho utajifunza mambo mengi kuhusu uandishi wa vitabu na kuishi maisha yenye uhuru ndani yake.
Hakikisha unaandika pembeni mambo ambayo utajifunza kupitia uchambuzi wa kitabu hiki kizuri cha BIRD BY BIRD yaani NDEGE KWA NDEGE.
Katika uchambuzi wa kitabu hiki utajifunza sura tano ambazo mwandishi ametushirikisha kuhusu uandishi wa vitabu na ndani ya sehemu hizo zimegwanyikwa part ndogo ndogo.
Ni kitabu kizuri kama unataka kuwa mwandishi mzuri wa Riwaya, Hadithi, Simulizi, Makala Na Vitabu Aina Yoyote basi uchambuzi ni mahususi kwako.
Kitabu cha BIRD BY BIRD ni kitabu kizuri basi unahitaji sana kusoma kitabu hiki.
Kurahisha nimekuandalia mambo yote muhimu kuhusu kitabu kwa lugha hadhimu ya Kiswahili.
Hakikisha una SUBSCRIBE podcast hii
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
11-1-2024 • 31 minuten, 51 seconden
Sababu 06 Za Kwanini Unaweza Kutimiza Malengo Yako Ya Mwaka 2024
Dakika 18 za kubadili kila kitu na uanze kuchukua hatua ili utimize malengo yako kwa kishindo.
Utajifunza mambo 06 ili ufanikishe mwaka 2024 kwa matokeo chanya na mafanikip makubwa
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
7-1-2024 • 18 minuten, 59 seconden
Aina Tano (05) Ya Marafiki Ambao Hupaswi Kuwapoteza...!
Hivi unajua kuna Marafiki ukiwa nao ni zaidi ya Baraka kubwa maishani pia kuna aina ya Marafiki ukiwa nao ni mwanzo wa kukaribisha majanga.
Unajua kwamba...
Wewe ni wastani wa Marafiki sita ambao unashinda nao muda mwingi.
Hata kama hupendi au hauna marafiki, lakini bado unahitaji watu si ndiyo?
Na watu hawa wakiwa na sifa fulani fulani ni Muhimu kuwatunza maana tupo zama tumezungukwa na Marafiki au watu ambao ni wanafiki sana...
...kuna aina tano za Marafiki ambao ukiwa nao ni zaidi ya Baraka kutoka wa Mungu maana ni Adimu zaidi ya Dhahabu kwenye machimbo ya Chunya pale Mbeya.
Ha!Ha!Ha! Unacheka au sio.
Hivi...
Ukiwa na rafiki ambaye anakuambia ukweli ambao unakujenga unajisikiaje? Jibu unalo.
Je, Ukiwa na rafiki ambaye anakupongeza unapofanya vizuri unajisikiaje? Jibu unalo.
Je, ukiwa na rafiki ambaye ni balozi wa kutangaza mazuri na kukunganisha kwenye Fursa na connection za faida?.
Majibu ya maswali umeshapata na unagundua unaweza kuwa unao au hauna. Sio tatizo kubwa.
Unashanga si ndiyo eeh...!
Ni hivi...
Haijalishi uko wapi na unafanya nini kama ni sehemu ambayo watu wapo basi unahitaji ukipata kati ya aina tano hizi za Marafiki basi usiwapoteze kabisa maana ni zaidi ya Tanzanite...
...pale machimbo ya Mererelani Arusha.
Unataka kuwajua aina hizi za marafiki.
Hata usiogope...
Ndiyo maana,
Nimekuandalia episode ya moto sana katika “Maisha Ni Kuthubutu Podcast” ujifunze zaidi kwa urahisi na kuelewa kwa kina.
Baada ya Kusikiliza pengine utajutia kwanini sikuiweka episode hii mwaka mmoja au miaka iliyopita! Muda sahihi ni sasa ndio sababu ya kusoma hapa.
Una sekunde 4 tu za kubofya link hapa chini Kusikiliza episode hii ili ujue aina 5 za Marafiki ambao ukiwa nao usiwapotezee.
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
7-3-2023 • 15 minuten, 51 seconden
Mambo Manne (04) Ya Kufanya Ili Kurudisha Hamasa Iliyopotea...!
Sikiliza episode hii ujue nini ufanye kurudisha hamasa iliyopotea na kuwa na morali ya kuendelea kupambania malengo, ndoto na maono yako.
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
7-4-2022 • 12 minuten, 1 seconde
Makosa Matano (05) Ambayo Unapaswa Kuepuka Ili Usipoteze Fedha Zako...!
Je umekuwa unapoteza fedha zako kirahisi? Umekuwa unataka kufanikiwa kwenye eneo la fedha lakini huoni hatua yoyote unapiga. Kupitia episode hii utaweza kujua makosa gani ambayo unapaswa kuepuka ili ufanikiwe kwenye eneo la fedha. Sikiliza episode hii kisha fanyia kazi ambayo utajifunza baada ya muda kupita utanipa ushuhuda kuwa hii episode imekupa matokeo chanya kwenye eneo la fedha
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
26-3-2022 • 14 minuten, 15 seconden
Siri Tatu (03) Za Kuzingatia Ili Uwe Mwekaji Mzuri Wa Akiba Ya Fedha Zako.
Kufanikiwa kwenye eneo la fedha inategemea sana na maarifa ambayo unayo juu ya fedha kwa maana hiyo ukiwa unataka kupiga hatua zaidi basi unapaswa kujenga tabia ya kuweka akiba ya fedha zako (Saving). Je unajua ufanye nini ili uweze kuweka akiba fedha zako? Basi Sikiliza episode hii upate kujua siri 3 ambazo zitakusaidia kujua namna gani uwe mwekaji mzuri wa akiba ya fedha zako
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
19-3-2022 • 8 minuten, 53 seconden
Sababu Saba (07) Za Kwanini Unapaswa Kujua Nguvu Ya Mabadiliko Kwenye Maisha Yako.
Je Unataka kubadili mfumo mzima wa maisha yako, mtazamo wako, aina ya marafiki, namna unavyofanya, mahusiano yako, biashara yako, Huduma yako n.k? Basi episode hii itakupa ufahamu wa nguvu wa mabadiliko kwenye maisha yako na kuweza kuchukua hatua Ili upate mabadiliko . Sikiliza mpaka mwisho upata kujua kwanini unaweza kupata mabadiliko kwenye eneo lolote ambalo upo
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
10-3-2022 • 16 minuten, 19 seconden
Maswali Matano (05) Ambayo Yatakusaidia Kugundua Kusudi La Kuzaliwa Kwako.
Je unataka kujua kwanini umezaliwa? Kabla ya kujua umezaliwa kufanya nini basi tambua kuwa wewe hujazaliwa kwa bahati mbaya, hujazaliwa kwa bahati nasibu, hujazaliwa kwa miujiza, hujazaliwa kwa kuwa wazazi wako walitaka mtoto. Lakini tambua kwamba wewe umezaliwa kwa kusudi hivyo haupo duniani kwa bahati mbaya. Ili maisha yako yawe yenye maana ni kujua kusudi la kuzaliwa kwako. Sikiliza Episode hii itakupa majibu ya KWANINI umezaliwa na hatimaye kuongeza thamani ya maisha yako kwa kuliishi kusudi lako
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
15-2-2022 • 17 minuten, 39 seconden
Hatua Saba (07) Za Kuzingatia Wakati Unapanga Malengo Yako.
Je unataka kutimiza malengo yako kwa asilimia ngapi? Unajua kwamba kutimiza malengo yako inategemea sana namna ya kupanga malengo yako kwa bahati mbaya changamoto kubwa watu wengi hawajui namna gani wanapanga malengo vizuri na kwa ufanisi. Sikiliza Podcast hii mpaka mwisho utaweza kujua hatua saba za kuzingatia wakati unapanga maalengo yako, Kutimiza malengo ipo ndani ya uwezo wako ni wewe kujua hatua saba za kuzingatia wakati unapanga malengo yako. Usisahau ku- Subscribe kwenye Apple Podcast na kuweka Nyota 🌟 5.
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
22-1-2022 • 11 minuten, 13 seconden
Gundua Maajabu Ya Kutumia Kioo Kubadili Maisha Yako.
Je unajua kioo kinaweza kubadili maisha yako? Kioo ni zaidi ya kujitazama kwa maana kwamba Kioo kina faida na matumizi mengi zaidi unavyojitazama. Sikiliza episode hii mpaka mwisho ujue maajabu ya kutumia kioo.
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
9-1-2022 • 13 minuten, 53 seconden
Jinsi Ya Kupanga Bajeti Ya Fedha Zako Kupitia Kanuni Ya 40/30/10/10/10.
Hii ni kwa watu wanaotaka kujua Kupanga bajeti ya fedha zao kwa usahihi lakini hawajaanza bado, Sikiliza mpaka mwisho utaweza kupanga bajeti ya fedha zako na Kanuni ya 40/30/10/10/10 ambayo ni rahisi sana. Kazi kwako kusikiliza madini haya kisha fanyia kazi ili mwaka 2022 uwe mwaka wa kufanikiwa wewe kwenye eneo la fedha
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
2-1-2022 • 10 minuten, 26 seconden
Makosa Matano (05) Ambayo Unafanya Na Kupelekea Kupoteza Fedha Zako.
Kufanikiwa kwenye eneo la fedha unahitaji sana kuwa na maarifa sahihi juu ya fedha, kupitia podcast hii kuwa na uhakika utaweza kusahihisha makosa haya ambayo hupelekea kupoteza fedha zako ikiwa tu utaweka utekelezaji kwenye maarifa haya kazi kupitia Podcast hii na kuweza kupiga hatua kwenye eneo la fedha
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message
28-11-2021 • 15 minuten, 4 seconden
Mambo Sita (06) Ya Kufanya Ili Uwe Msomaji Mzuri Wa Vitabu
Kusoma vitabu ni tabia, maarifa ni nguzo ya mafanikio kwenye maisha yako kama utafanyia kazi kwa maarifa ambayo unajifunza; maarifa mengi yapo kwenye vitabu kwa maana hiyo kupitia episode hii utaenda kuwa msomaji mzuri wa vitabu.
---
Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/maishanikuthubutu/message