Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina mada inayotupeleka nchini Kenya kuzunguza na uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mada tofauti ikiwemo uwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno HEKEMUA.Uchambuzi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) uliotolewa leo jijini New York, Marekani katika Siku ya Kimataifa ya Polio, unaonesha kwamba asilimia 85 ya watoto 541 waliokumbwa na polio duniani mwaka wa 2023 wanaishi katika nchi 31 zenye mifumo dhaifu, zinazokabiliwa na mizozo, halikadhalika zilizo hatarini.Umoja wa Mataifa ulijengwa na ulimwengu, kwa ajili ya ulimwengu, ndivyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, alivyouanza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku ya leo ya Umoja wa Mataifa.Na leo Oktoba 24 huko Kazan nchini Urusi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amehutubia mkutano wa viongozi wa kundi la BRICS yaani Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini akisisititiza amani duniani akizitaja Gaza, Lebanon, Ukraine na Sudan, akiwaambia wajumbe wa BRICS, “tunahitaji amani nchini Sudan, huku pande zote zikinyamazisha bunduki zao na kujitolea katika njia ya kuelekea amani endelevuKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno HEKEMUA! Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
24-10-2024 • 11 minuten, 22 seconden
Jifunze Kiswahili - maana ya neno HEKEMUA!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno HEKEMUA!
24-10-2024 • 0
23 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya Israeli kaskazini mwa Gaza unaoleta changamoto za kuendelea na chanjo ya polio, na virusi vya Marburg nchini Rwanda. Makala tunakupeleka nchini Uganda na mashinani nchini Lebanon, kulikoni?Mashambulizi makali ya anga kutoka kwa jeshi la Israel, idadi kubwa ya watu kutawanywa na ukosefu wa fursa ya kufika Gaza Kaskakzini vimelazimisha kuahirishwa kwa kameni ya chanjo kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani WHO, la kuhudumia watoto UNICEF na la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWAMkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali.Ndoa za utotoni,ubakaji na kutelekeza watoto, haya ndio matatizo yaliyokuwa yanaripotiwa mara nyingi zaidi kwa kuathiri watoto katika makazi ya wakimbizi katika wilaya Kyegegwa magharibi mwa Uganda. Hata hivyo, kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF na ufadhili kutoka wahisani wa Uingereza UKaid, maelfu ya wazazi katika makazi ya wakimbizi na jamii zinazohifadhi waakimbizi katika wilaya ya Kyegegwa wamepewa mafunzo juu ya malezi bora ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto, wanawake, na wasichana.Mashinani tunabisha hodi Lebanon, kumsikia Farah, Mkimbizi wa ndani anayepokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, baada ya kujifungua kwenye hema, akieleza alichokabiliana nacho.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
23-10-2024 • 10 minuten, 51 seconden
Mbinu bora za malezi zimebadilisha maisha katika Wilaya ya Kyegegwa - UNICEF Uganda
Ndoa za utotoni,ubakaji na kutelekeza watoto, haya ndio matatizo yaliyokuwa yanaripotiwa mara nyingi zaidi kwa kuathiri watoto katika makazi ya wakimbizi katika wilaya Kyegegwa magharibi mwa Uganda. Hata hivyo, kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF na ufadhili kutoka wahisani wa Uingereza UKaid, maelfu ya wazazi katika makazi ya wakimbizi na jamii zinazohifadhi waakimbizi katika wilaya ya Kyegegwa wamepewa mafunzo juu ya malezi bora ili kuondoa ukatili dhidi ya watoto, wanawake, na wasichana. Leo tuko katika wilaya ya Kyegegwa nchini Uganda ambapo, kwa msaada wa UNICEF, wafanyakazi wa kijamii, kamati za ulinzi na ustawi wa watoto, na kikosi cha polisi; wote wamepewa mafunzo mwafaka ili kuhakikisha ulinzi wa watoto unaofaa na wa kudumu, na tunakutana na Agnes Karungi mama mwenye umri wa miaka ishirini na mmoja wa wanufaika wa mradi wa malezi bora. Mbali na kukumbana na changamoto za kuwa mama kijana, mwanaye Agnes, ni mwenye ulemavu na zaidi ya hayo akatengwa na familia yake kwa kuzaa akiwa angali mwanafunzi.Cecily Kariuki anaeleza zaidi katika makala hii..
23-10-2024 • 3 minuten, 48 seconden
UN: Mashambulizi ya anga ya Israel yalazimisha kampeni ya chanjo kusitishwa Gaza Kaskazini
Mashambulizi makali ya anga kutoka kwa jeshi la Israel, idadi kubwa ya watu kutawanywa na ukosefu wa fursa ya kufika Gaza Kaskakzini vimelazimisha kuahirishwa kwa kameni ya chanjo kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Duniani WHO, la kuhudumia watoto UNICEF na la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA. Asante Anold, kampeni hiyo iliyoahirishwa ilitakiwa kuanza leo n ani duru ya mwisho ya chango ya kampeni iliyolenga kuwachanja watoto 119,279 kote Gaza Kaskazini kwa dozi ya pili ya chanjo ya polio aina ya nOPV2, lakini hali ya sasa imefanya iwe vigumu kwa familia kupeleka watoto wao kwenye vituo vya chanjo, na kwa wahudumu wa afya kuendesha huduma kwa usalama.Mashambulizi ya makombora yanayoendelea dhidi ya miundombinu ya kiraia yamepunguza maeneo yanayokubaliwa kwa usitishaji wa uhasama kwa mnajili ya masuala ya kibinadamu kuwa kwenye Jiji la Gaza pekee, ikilinganishwa na wakati wa awamu ya kwanza ya chanjo iliyofanyika tarehe 1-12 Septemba 2024.Hali hii inahatarisha kufikiwa kwa lengo la angalau asilimia 90 ya watoto kuchanjwa, jambo ambalo ni muhimu ili kukomesha usambaaji wa virusi vya polio na kulinda afya za watoto.WHO na UNICEF wamesema kuwa kucheleweshwa kwa chanjo ya polio kunaweza kuongeza hatari ya virusi kuenea zaidi Gaza na maeneo Jirani na kuchelewesha utoaji wa dozi ya pili ya chanjo ndani ya wiki sita kunapunguza uwezo wa chanjo hiyo kuimarisha kinga za watoto na kuzuia maambukizi.Tangu duru ya pili ilipoanza tarehe 14 Oktoba 2024, jumla ya watoto 442,855 wenye umri wa chini ya miaka kumi wamefanikiwa kuchanjwa katika maeneo ya kati na kusini mwa Gaza.UNICEF na WHO wanatoa wito kwa pande zote zinazohusika katika mzozo kutekeleza usitishaji mapigano wa kibinadamu na kuhakikisha kuwa raia, wahudumu wa afya, na miundombinu ya kiraia kama shule na hospitali inakingwa dhidi ya mashambulizi.Mashirika hayo yamesisitiza umuhimu wa kuanza tena kampeni ya chanjo mara moja ili kuzuia kupooza kwa watoto na kuimarisha kinga dhidi ya polio.Katika juhudi za kuhakikisha huduma bora, takribani watoto 357,802 pia walipatiwa virutubisho vya vitamini A kama sehemu ya juhudi za kuunganisha chanjo ya polio na huduma zingine muhimu za afya.Mashirika ya WHO na UNICEF ymesisitiza kuwa kusitisha vita na kuwezesha chanjo ni hatua muhimu ili kuzuia mlipuko wa polio kuendelea na kulinda afya ya watoto wote Gaza.
23-10-2024 • 2 minuten, 45 seconden
Dkt. Tedros: Heshima kwa wahudumu wa afya wa Rwanda wanavyopambana na Marburg
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani amewapongeza wahudumu wa afya wa nchini Rwanda kwa kazi kubwa wanaoyoifanya kukabiliana na ugonjwa wa Marburg. Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameeleza hisia zake hizo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika vituo mbalimbali vya afya katika mji Mkuu wa nchi hiyo, Kigali."Ninawapongeza wahudumu wa afya waliojitolea ambao wamejiweka hatarini kuokoa wenzao, na ambao wameendelea kufanya kazi licha ya hatari. Na ninaenzi wale ambao tumewapoteza."Pia Dkt. Tedros akaeleza kuwa yeye na wenzake wamefurahishwa na namna ya utoaji huduma ambayo haijawahi kutumiwa katika mlipuko ya magonjwa ya namna hii barani Afrika akitolea mfano wagonjwa wawili aliowashuhudia wakiendelea vizuri kwamba waliokolewa kwa kuwekewa mipira iliyopeleka hewa ndani ya mwili.“Tunaamini hii ni mara ya kwanza kwa wagonjwa wenye virusi vya Marburg barani Afrika kuingiziwa na kutolewa mpira wa hewa. Wagonjwa hawa wangefariki dunia katika milipuko ya hapo awali. Hii inaonesha kazi ambayo Rwanda imefanya kwa miaka mingi kuimarisha mfumo wake wa afya, kukuza uwezo wa huduma muhimu na msaada wa kuokoa maisha ambao unaweza kutumiwa katika huduma za kawaida za hospitali na katika dharura.”
23-10-2024 • 1 minuut, 22 seconden
Kuanza tena kwa shughuli za Redio RTNC kutawawezesha kupigana dhidi ya taarifa potofu na za uongo - MONUSCO
Umoja wa Mataifa unaendelea kuunga mkono serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC katika kukabili habari potofu na za uongo hususan huko mashariki mwa nchi ambako vikundi vilivyojihami vinaendelea kushambulia raia na kupambana na jeshi la serikali. Hivi karibuni Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, umeipatia kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini jengo na vifaa vyenye thamani ya takriban dola elfu hamsini za Kimarekani. Hatua hiyo iliwezesha RTNC kuanza tena matangazo yake. Mwandishi wetu wa DRC, George Musubao alifika kituoni hapo kuzungumza na wahusika na wanufaika.
22-10-2024 • 5 minuten, 26 seconden
22 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kufuatilia kazi za kituo cha Taifa cha Redio na Televisheni, RTNC huko Beni jimboni Kivu Kaskazini za kakabiliana na habari potofu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Cairo, Misri, imebainisha kwamba athari za vita zimerudisha nyuma maendeleo huko Gaza kwa takriban miaka 69. Ripoti hiyo iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP na Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi na Kijamii kwa Asia Magharibi imeonya kwamba bila kuondoa vikwazo vya kiuchumi na kuwekeza katika maendeleo, uchumi wa Palestina unaweza kushindwa kurejesha viwango vya kabla ya vita na kusonga mbele kwa kutegemea misaada ya kibinadamu pekee.Kiongozi wa timu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) ya kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Marburg Dkt. Janet Diaz ameeleza kwamba uongozi thabiti wa serikali ya Rwanda umewezesha kufanya uamuzi wa haraka na kuchukua hatua kuanzisha mwitikio wa sekta mbalimbali dhidi ya mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo wa Marburg nchini humo.Na uongozi wa Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon (UNIFIL) umeendelea kusisitiza kwamba pamoja na changamoto zilizopo, walinda amani wa UNIFIL wanaendelea kufanya kazi kwa karibu na jamii za kusini mwa Lebanon ili kuwezesha utoaji wa misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji. Hivi karibuni kumekuwa na mashambulizi dhidi ya walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa yanayotekelezwa na majeshi ya Israeli.Mashinani kupitia video ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura OCHA tunamuangazia mmoja wa watu waliokimbia makazi yao akiwa katika shule ya Al Rimal, akielezea changamoto wanazokutana nazo katika kukabiliana na hali ngumu inayowakabili raia wa Gaza.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
22-10-2024 • 9 minuten, 57 seconden
Nadipo: Asante WFP kwa mradi wa mizinga ya nyuki sasa familia yangu inatabasamu
Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Katika kaunti hii vumbi linalotimuka katika eneo tambarare lisilo na miti linakufanya kujiuliza je Nini kizuri kinaweza kufanyika hapa kwenye ukame uliotamalaki? Lakini cha kustaajabisha ni kwamba kwa kuwezeshwa mengi yanawezekana ikiwemo njia bora za kuhakikisha uhakika wa chakula na hata kubadili maisha ya watu kama anavyosema mkulima wa nyuki Nadipo Lotelei mnufaika wa mradi wa mizinga ya nyuki kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. “Hatua iliyochukuliwa na WFP kutupatia mizinga ya nyuki imekuja kama nyota ya jaha kwangu kwa sababu siwezi kutembea umbali mrefu kutokana na ajali niliyopata. Mradi huu umenisaidia sana mimi ili kuweza kusaidia watoto wangu na mke wangu. Mke wangu ameweza kuanzisha biashara ya duka kutokana na faida niliyopata ambayo sasa inatumika kama chnzo cha kipato cha mahitaji ya kaya yetu.”Nadipo ni miongoni mwa wafuga nyuki 1,900 katika kaunti ya Turkana ambao wamepewa mafunzo ya ufugaji nyuki na vifaa kupitia mradi wa WFP kwa ushirikiano na shirika binafsi la HIVE ambalo mwenyekiti mtendaji wake ni Christopher Nzuki. “Tunahusika katika ufungaji na usambazaji wa vifaa. Na wakati huohuo tunatoa mafunzo kwa wafugaji nyuki na kisha kuwapatia masoko. Tunachukua kila kitu wanachozalisha.”Ufugaji wa nyuki wa kisasa si kazi kubwa, na pia unatumia nafasi ndogo na maji kidogo. Nyuki huchavusha asilimia 80 ya miti ya maua ikiwemo mazao ya chakula. Huzalisha asali, nta, mafuta na sumu, bidhaa ambazo huuzwa kwa gharama kubwa sokoni. Kwa sasa WFP inasaidia karibu wafugaji wa nyuki 5,000 katika kaunti 9 nchini Kenya lakini lengo ni kuwafikia wengi zaidi na mradi huu kama anavyosema afisa wa WFP Timothy Koskei. “Dhamira yetu mwisho wa yote ni kuwafikia wastani wa wafuga nyuki 10,000 katika kaunti 9 na kuvuna takriban tani 600 za asali.” Kwa mujibu wa WFP nyuki wana uwezo mkubwa na wanaweza kutoa mavuno mengi ambayo ni neema kwa familia sisizojiweza katika maeneo haya kame. Mkurugenzi wa WFP nchini Kenya Lauren Landis anasema mradi umezaa matunda. “Hivi sasa tunasikia kutoka miongoni mwa wanaufaika ambao awali walikuwa wakipokea msaada wa chakula ,ambao sasa sio tu wanazalisha asali kwa ajili ya faida bali pia wanafikiria kuongeza ununuzi wa pembejeo zaidi kutoka kwa Hive. Hivyo tunachokishuhudia ni mchakato ulio wazi ambapo mtu anatoka kuwa mpokea msaada na kuwa mteja, kuwa mpokeaji wa faida na si mpokeaji wa msaada wa chakula.”Kwa mafanikio haya WFP inasema itaendelea kupanua wigo wa mradi huu ili kunufaisha familia nyingi zaidi.
21-10-2024 • 3 minuten, 20 seconden
Mlo shuleni ulibadilisha maisha yangu- Mkurugenzi wa WFP Somalia
Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia. "Mimi ni zao la mlo wa shule," hayo ni maneno ya El-Khidir Daloum ambaye ana shukrani tele kwa WFP kwa kuendesha programu ya ‘mlo shuleni’ iliyomfaidisha alipokuwa mwanafunzi. Hivi sasa, akiwa Mkurugenzi wa WFP nchini Somalia, Daloum ameweka dhamira ya kazi yake kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa wote. Je Daloum aliifahamu vipi programu ya mlo shuleni ya WFP kwa mara ya kwanza?“Tulipofika pale, tukakuta ni shule ya bweni, wakati huo wazazi wetu hawangeweza kugharamia shule hiyo. Kwa hivyo, shule ilifanya ushirikiano kati ya serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula Duniani (WFP). Na hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuonja dagaa wa Kijapani, maziwa ya unga kutoka Uholanzi, na jibini ya Denmark, yote yaliletwa kwetu kupitia mlo wa shule.”Je Daloum anadhani maisha yake yangekuwa vipi kama WFP isingetoa mlo shuleni?“Nikiwaza kuhusu kizazi changu, hasa wale waliokuwa katika shule za bweni, bila ushirikiano huo kati ya serikali ya nchi yangu na WFP, hatungeweza kumaliza elimu yetu. Ndio maana nakwambia kwamba mimi ni zao la mlo shuleni kutoka kwenye shule ya msingi kwenda katika shule ya kati na hatimaye sekondari, yote haya matatu yalifaulu kutokana na mlo shuleni.”
21-10-2024 • 1 minuut, 52 seconden
21 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa COP16 katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia na ufugaji nyuki Turakana nchini Kenya. Pia tunakupeleka nchini Somalia kufutilia programu wa WFP wa mlo shuleni na mashinani inatupeleka nchini Lebanon.Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili.Kila siku, mamilioni ya watoto kote ulimwenguni huenda shule wakiwa na njaa, wengi wao wakiteseka na utapiamlo sugu ambao huathiri ukuaji wa kiakili na utendaji wao katika masomo. Wanaobahatika huweza tu kumaliza masomo yao na kufanikiwa maishani kutokana na programu ya ‘mlo ya shuleni’ inayoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani (WFP). Mfano wa wanufaika hao ni El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa sasa wa WFP nchini Somalia.Makala inatupeleka Kaunti ya Turkana Kaskazini mwa Kenya moja ya maeneo kame ambako mradi wa ufugaji nyuki wa WFP umekuwa mkombozi kwa wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Waffiyah Diyah kutoka Lebanon ambaye ni muathirika wa vita vilivyolazimisha maelfu ya watu kufangasha viragoanaelezea hali ya familia yake baada ya kukimbia mashambulizi na kupoteza kila kitu, lakini sasa anapokea msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM).Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
21-10-2024 • 9 minuten, 58 seconden
COP16: Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baionuai waanza nchini Colombia
Mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa bayonuai (COP16) umeng’oa nanga leo katika mji wa Santiago de Cali au Cali huko nchini Colombia ambapo mataifa 196 yatajadili jinsi ya kusitisha na kubadili mwelekeo wa kudorora kwa ulimwengu wa asili. COP16 kwa siku 12, viongozi na wadau kutoka kote duniani wanatarajiwa kujadili namna ya wanadamu kuishi kwa amani na asili ya ulimwengu, kama wasemavyo nchi mwenyeji Colombia kwa lugha ya kihispanyola Paz con la Naturaleza yaani amani na asili.Washiriki, kwa kina watajadili utekelezaji wa mkakati wa Kimataifa wa Kunming-Montreal kuhusu bayoanuai, makubaliano ya kihistoria ya mwaka 2022 ya kusitisha na kubadili upotevu wa asili. Pia watachunguza jinsi ya kuelekeza mabilioni ya dola kwa nchi zinazoendelea ili kuhifadhi na kudhibiti bioanuai kwa uendelevu. Na watajadili sheria za msingi ambazo zinaweza kuhitaji kampuni za kibinafsi kufidia mataifa.Katika sherehe za ufunguzi wa mkutano huu hapo jana, kwa njia ya video, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye pia anategemewa kuhudhuria siku za mwishomwisho za mkutano huu, amewaeleza wajumbe akisema, “mkakati wa Kimataifa wa Bioanuwai unaahidi kurekebisha uhusiano na dunia na mifumo yake ya ikolojia. Lakini hatuko kwenye mstari. Jukumu lenu katika COP hii ni kubadilisha maneno kuwa vitendo.”
21-10-2024 • 1 minuut, 30 seconden
Nchi zote pamoja na mashirika ya kimataifa ikiwemo UN yanawajibika kukomesha ukaliwaji wa Palestina
Tume hiyo huru imeyasema hayo katika taarifa mpya ya msimamo wa kisheriia iliyotolewa mjini Geneva Uswis kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina ikiwemo Jerusalem Mashariki ambayo imeweka wazi maoni ya tume kuhusiana na wajibu wa serikali na jinsi Baraza Kuu na Baraza la Usalama linavyoweza kutambua na kutekeleza mbinu na hatua sahihi zinazohitajika kwa kazi hiyo hadi mwisho wa ukaliwaji huo, na kwa haraka iwezekanavyo.Tume ihiyo imebaini kwamba maoni ya ushauri ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusu matokeo ya Kisheria yanayotokana na sera na desturi za Israel katika eneo linalokaliwa la Palestina ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki ni wenye mamlaka na usio na utata kwa kusema kwamba kuendelea kuwepo kwa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu ni kinyume cha sheria na sheria ya kimataifa.Taarifa hiyo ikitolewa Geneva Gaza kwenyenyewe hali inaendelea kuwa tete, kwa mujibu wa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestinna UNRWA Phillipe Lazzarini, kwani shule nyingine ya UNRWA imeshambuliwa leo Jabalia Kaskazini mwa Gaza, watu kadhaa wameripotiwa kuuawa na miongoni mwao Watoto wengi waliokuwa wakipata hifadhi katika jengo hilo.Lazzarini amesema hili ni shambulio la tatu dhidi ya majengo ya UNRWA kwa wiki moja. Na pia wafanyakazi wa shirika hilo wanaendelea kuuawa sasa wameffikia 231 tangu kuanza kwa vita hii Oktoba mwaka jana.Naye msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF James Elder akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo amesema “Gaza ni mfano halisi wa ulimwengu wa kuzimu duniani kwa watoto milioni moja wa eneo hilo. Na hali inazidi kuwa mbaya, siku baada ya siku, tunapoona athari za kutisha za mashambulizi ya anga ya kila siku na operesheni za kijeshi za Israek kwa watoto wa Kipalestina.”Nalo shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA likiangazia Ukingo wa Magharibi limesema “Vikosi vya Israel vimekuwa vikitumia mbinu mbaya za vita katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na kuibua wasiwasi mkubwa juu ya matumizi ya nguvu kupita kiasi na kuongeza mahitaji ya kibinadamu ya watu.” Ameelezea wasiwasi kuhusu mashambulizi ya walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina na miti yao ya mizeituni wakati huu wa mavuno ya kila mwaka.
18-10-2024 • 2 minuten, 3 seconden
Mbegu za asili zinanisaidia kukabili mabadiliko ya tabianchi - Mkulima
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linapigia chepuo uwepo wa mifumo ya uzalishaji chakula inayoendana na kila eneo husika, mathalani kilimo kitumie mbegu za asili za eneo husika kama mbinu ya kukabili mabadiliko ya tabianchi. Kupata aina tofauti tofauti za mbegu za asili kwa eneo husika kunainua kipato cha wakazi wa vijijini na kuongeza mnepo majanga yanapotokea. Na hicho ndio anafanya mkulima kutoka Tanzania ambaye wakati wa maonesho ya siku ya chakula duniani huko mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa Tanzania alieleza kwa nini ameamua kuchukua hatua hiyo. Assumpta Massoi anasimulia zaidi.
18-10-2024 • 3 minuten, 40 seconden
UN Ripoti: Uwezekano wa kifo cha Dag Hammarskjöld kuwa ni hila unaongezeka kutokana na taarifa mpya
Ripoti nyingine mpya ya tathimini ya uchunguzi wa hali na mazingira ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1961 Dag Hammarskjöld imetolewa leo ikiwa na vipengele vinne vipya vikiongeza uwezekano kwamba kifo hicho cha ajali ya ndege kilikuwa ni hila. Asante Anold kwanza ikumbukwe kuwa hii sio ripoti ya kwanza na huenda isiwe ya mwisho ya kutathimini hali na mazingira yliyochangia ajali ya ndege iliyokatili maisha ya Dag Hammarskjöld tarehe 17 Septemba 1961 akiwa njia kuelekea Congo ambayo sasa ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Cngo DRC, kujadili usitishwaji wa uhasama ila ni ripoti ya karibuni zaidiRipoti inasema mwenyekiti wa jopo la tathimini ya uchunguzi jaji mkuu wa zamani wa Tanzania Mohamed Chande Othman amepokea taarifa mpya muhimu kutoka kwa nchi wanachama ambazo zinajumuisha maeneo haya Mosi: uingiliaji unaowezekana wa Nchi Wanachama wa mawasiliano husika.Pili: Uwezo wa wanajeshi wa Katanga, au wengine, wa kufanya shambulio linalowezekana kwenye ndege ya SE-BDY,Tatu: kuwepo kwa askari wa kigeni na wafanyakazi wa kijasusi katika eneo hilo la tukioNa nne: Taarifa zaidi mpya zinazohusiana na muktadha na matukio yanayozunguka kifo hicho mwaka 1961.Jaji Othman amemkabidi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ripoti hii ya tathimini ambaye naye ameiwasilisha kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.Na kufuatiia tathimini hii Guterres amesema anaizingatia ingawa kihistoria kumekuwa na nadharia nyingi zilizotolewa kama sababu inayowezekana ya ajali hiyo, na anazichukulia nadharia hizo nyingi kuwa zisizo na uthibitisho.Hata hivyo mwenyekiti wa jopo la tathimini anasema nadharia nyingine ambayo inabaki na inakubalika ni kwamba shambulio la nje au tishio lilikuwa sababu ya ajali.Pia amesema kuwa dhana mbadala zinazoonekana kuwepo ni kwamba ajali hiyo ilitokana na hujuma, au makosa ya kibinadamu yasiyokusudiwa.Katibu mkuu amekaribisha ushirikiano uliotolewa na baadhi ya nchi wanachama katika tathimini hiyo lakini bado jopo la tathimini linaaminikuna baadhi ya nchi wanachama wana taarifa muhimu ambazo hawajataka kuzitoa.
18-10-2024 • 2 minuten, 2 seconden
18 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia eneo linalokaliwa kwa mbavu la Kipalestina, na ndoto Mchezaji kijana wa soka zilizokatizwa na vita katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani Kenya, kulikoni?Tume Huru ya Kimataifa ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu eneo linalokaliwa la Palestina leo imesema mataifa yote na mashirika ya kimataifa, ikiwa ni amoja na Umoja wa Mataifa, wana wajibu chini ya sheria za kimataifa wa kukomesha uwepo haramu wa Israel katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, wakati mashambulizi Gaza yakishika kazi na kuongeza madhila kwa raia.Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo.Makala inatupeleka Tanzania hususan mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki ambako Assumpta Massoi amezungumza na mhifadhi wa mbegu za asili, mahojiano yaliyofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini humo. Mhifadhi mbegu anaanza kwa kujitambulisha.Na mashinani fursa ni yake Nosizi Reuben Dube ambaye kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), amefanikiwa kupata shahada ya chuo kikuu, akiwakilisha tumaini kwa jamii yake, ambayo imeishi Kenya kwa zaidi ya 50 bila uraia hadi walipotambuliwa hivi karibuni na serikali ya Kenya na kuwapatia vyeti vya uraiaMwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
18-10-2024 • 10 minuten, 38 seconden
Mohamed hajakata tamaa ya kuwa mwanasoka maarufu - Gaza
Katika ufukwe wa Al- Mawasi, magharibi mwa mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati, mchezaji mpira wa Klabu ya Soka ya Rafah Services anaendelea na mazoezi yake ili kuendeleza uthabiti wa mwili kama mchezaji wa soka wa kulipwa wa klabu hiyo muhimu wakati huu mashambulizi ya makombora yakiendelea kwenye eneo hilo. Jua linazama hapa kwenye ufukwe wa Al Mawasi, kwenye bahari ya Mediteranea, wengine wakiwa wanaogelea, na kwa mbali mahema ya waliosaka hifadhi baada ya kufurushwa kaskazini mwa Gaza, mmoja anaonesha mbwembwe za dana dana ya mpira, anajitambulisha."Naitwa Mohamed Abu Jalda, mchezaji wa Klabu ya Rafah Services katika daraja la kwanza. Nilikuwa na ari kubwa ya kuwa mchezaji mkubwa wa soka kama wengine walioko nje ya Ukanda wa Gaza, lakini kutokana na vita, tamaa yangu na maisha yangu yalicheleweshwa, sasa nina zaidi ya miaka 20, nikijaribu kuwa mchezaji wa soka, lakini siwezi kwa sababu naishi Gaza ambapo kuna mapigano ya mara kwa mara. Kila siku nahisi kama ninakufa; Mungu atujalie uvumilivu kuhimili maisha haya."Mohamed amekuwa akiwa na ndoto ya kucheza soka ya kulipwa tangu akiwa na umri wa miaka 10 na sasa ana umri wa miaka 20 anaona ndoto inayoyoma, lakini ana matumaini.."Wakati wowote nikipata muda na kutamani kucheza soka,ninakuja ufukweni, kwani ni sehemu pekee naweza kucheza kama mchezaji mwingine. Natumai Mungu atanijalia kufanikiwa kuwa mchezaji wa soka, na najivunia kuwa mpalestina kutoka Gaza. Natamani kucheza soka nje ya Gaza na timu ya taifa ya Palestina, kwa sababu ni haki yangu."
18-10-2024 • 1 minuut, 53 seconden
Tofauti ya maana ya maneno Ajali na Ajari, hasa pale yatakapotamkwa kwa kuchanganya herufi ‘R’ na ‘L’
Katika kujifunza lugha ya kiswahili, matamshi sahihi ya lugha husaidia kufikisha ujumbe sahihi. Kinyume cha hivyo ujumbe utakuwa sivyo ndivyo na ndio maana hii leo, mbobezi wa lugha ya Kiswahili, Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua tofauti ya maana ya maneno Ajali na Ajari, hasa pale yatakapotamkwa na mzungumzaji anayechanganya herufi ‘R’ na ‘L’
17-10-2024 • 1 minuut
17 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia juhudi za vijana hasa katika kuboresha mifumo ya elimu katika matumizi ya teknolojia ambapo Gloria Anderson, Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Shirika la TEDI anatufafanulia zaidi.Leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza umaskini duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema umaskini umesalia kuwa baa la dunia ukiathiri mamia ya mamilioni ya watu duniani kote.Huko MAshariki ya Kati, awamu ya pili ya utoaji wa chanjo dhidi ya polio imekamilika eneo la kati mwa Gaza, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema watoto 181,429 wamepatiwa. Wengine 148,064 wamepatiwa matone ya vitamini A. Ingawa hivyo vituo vinane vya afya vitasalia wazi ili kuendelea kutoa chanjo kwa familia zilishindwa kufikisha watoto wao katika siku tatu za chanjoMkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti amezuri Rwanda kujionea harakati za taifa hilo kukabili homa ya Marburg ambapo amepongeza serikali na wadau kwa ushirikiano kudhibiti mlipuko na kusema, tumeona idadi ya wagonjwa ikianza kupungua, halikadhalika idadi ya vifo baada ya wiki kadhaa za kazi ya kujituma.Katika kujifunza lugha ya kiswahili. matamshi sahihi ya lugha husaidia kufikisha ujumbe sahihi. Kinyume cha hivyo ujumbe utakuwa sivyo ndivyo na ndio maana hii leo, mbobezi wa lugha ya Kiswahili, Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua tofauti ya maana ya maneno Ajali na Ajari, hasa pale yatakapotamkwa na mzungumzaji anayechanganya herufi ‘R’ na ‘L’Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
17-10-2024 • 11 minuten, 14 seconden
Asante WFP sasa najua kuandika na kusoma jina langu – Mkimbizi DRC
Mbali na usaidizi mkubwa kwa watu waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro mashariki mwa DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linatoa msaada kupitia miradi iliyo ndani ya mfumo wa kuzuia na kupunguza hatari za unyanyasaji wa kijinsia unaohusishwa na uhakika wa kupata chakula. Takriban wanawake 40 waliokimbia makazi yao wanaoishi katika kambi ya Bulengo jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC wamenufaika na mafunzo ya kusoma na kuandika tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2024. Walengwa waliojifunza kusoma na kuandika wanashuhudia kwamba yamebadilisha maisha yao. Mwandishi wetu wa habari mashariki mwa DRC, George Musubao alisafiri kutoka Beni hadi Goma katika kambi ya Bulengo kuzungumza na mmoja wao.
16-10-2024 • 3 minuten, 34 seconden
Kambi ya huduma za macho ya UNICEF yawezesha watoto kuona vema
Nchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto. Mmoja wa wanufaika wa juhudi hii ni Candy, msichan wa mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino.Akiwa mwingi wa matumaini, Eric Odhiambo Okeyo, baba mzazi wa mtotohuyo alimpeleka kwenye kambi hiyo jijini Kisumu ambapo alifanyiwa uchunguzi na matibabu.Baada ya kufanyiwa uchunguzi, Candy alielekezwa kwa daktari wa macho ili abaini aina ya miwani ambayo ingemfaa.“Mtoto alipoanza shule niligundua kwamba mwendo wake katika masomo ulikuwa wa polepole sana na pia alikuwa analamika kwamba haoni anachoandika mwalimu. Hata akienda kucheza niliona kwamba alikuwa akifunga macho mara kadhaa. Ilikuwa inanikosesha amani kwa sababu nilihisi kuwa alikuwa akiteseka,” amesema Eric.Mpango huu wa kielelezo wa UNICEF na wadau wake unashughulikia changamoto zinazowazuia watoto wenye ulemavu na familia zao kupokea msaada muhimu wanaohitaji wakati wa majanga na dharura.Akiwa mwingi wa furaha, Eric anasema, “imechukua muda wa miaka sita ambapo nimekuwa nikizunguka tu kuhusu miwani. Mahali nilipoenda hapo awali, niliambiwa kulipia shilingi elfu arobaini ($313) lakini sikuweza kupata hiyo pesa. Nimefurahi kwamba leo nimepewa bila gharama yoyote.”Baada ya uchunguzi na mawaidha mbalimbali katika hii kambi, Eric na mwanaye Candy hawakuweza kuificha furaha yao kwa kupata suluhisho la tatizo ambalo limewaathiri kwa miaka sita.Hatimaye, Candy alipewa miwani yake maalum ili kumsaidia kuona vizuri zaidi.“Nimefurahia sana sina jukumu tena la kutafuta pesa za kununua miwani. Na nimefurahi pia mtoto wangu atakuwa na wakati rahisi. Amefurahia kabisa na anaipenda sana miwani yake. Amesema anajihisi vizuri. Kwa sababu ana miwani, natumaini anaweza kucheza bila shida yoyote, bila kujali kuhusu jua kwa sababu miwani inamkinga.”
16-10-2024 • 2 minuten, 1 seconde
16 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazi siku ya chakula duniani ikitupeleka jijini Roma Italia kufuatilia maadhimisho yake. Pia tunakupeleka nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani mashirika wanhaha kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto. Makala tunakwengda nchini DRC na mashinani Sierra Leone, kulikoni?Washiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Nchini Kenya, Idara ya Taifa ya Ulinzi wa Jamii kwa kushirikiana na Baraza la Kitaifa la Watu wenye ulemavu na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, wameendesha kambi ya kusaidia uoni kwa watu wenye changamoto ikiwemo Candy mwenye umri wa miaka 7 ambaye ana ualbino. Baba yake alifika kwenye kambi hiyo na anatusimulia kupitia video ya UNICEF Kenya.Makala inatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia harakati za shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP la kusaidia wanawake wakimbizi kuondokana na ujinga wa kutokujua kusoma na kuandika.Mashinani tunamsikia Mpishi Mkuu Fatmata Binta kutoka kabila la wafugaji wanaohamahama la fulani nchini Sierra Leone anaeleza jinsi ushirikiano wake na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, kuhusu ni kwa jinsi gani FAO umemwezesha kusambaza manufaa ya fonio, nafaka asili ya Afrika , inayoweza kuwa suluhisho la changamoto za ukosefu wa chakula na tabianchi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
16-10-2024 • 9 minuten, 54 seconden
Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya chakula duniani yaangazia haki ya chakula salama chenye lishe na cha bei nafuu
Washiriki wa Sherehe za kimataifa za mwaka huu wa 2024 za kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Chakula zilizofanyika leo katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) jijini Roma Italia wamesisitiza haja ya upatikanaji wa vyakula mbalimbali vya kutosha, vyenye lishe, bei nafuu na salama.Ni maadhimisho ambayo yamewaleta wadau wa kilimo na chakula kutoka kote duniani lakini yanakuja huku kukiwa na mvutano na mizozo ya kimataifa na majanga ya tabianchi ambayo ni miongoni mwa mambo yanayochangia changamoto ya mamia ya mamilioni ya watu duniani kote kukabiliwa na njaa na mabilioni ya watu kushindwa kumudu chakula bora, FAO inaeleza katika taarifa iliyochapishwa katika ukurasa wake wa wavuti.Katika hotuba yake ya ufunguzi Mkurugenzi Mkuu wa FAO, QU Dongyu, amesema mifumo ya kilimo cha chakula inabidi "kusaidia wakulima wadogo, wakulima wa ngazi ya familia na wafanyabiashara wadogo katika mnyororo wa thamani ambao katika nchi nyingi ni wa msingi katika kufanya vyakula vyenye lishe, vya aina mbalimbali vipatikane kwa wote, na kuhifadhi tamaduni za jadi za chakula.” Ujumbe huo wa mkuu wa FAO unafanana na ujumbe wa Papa Francis ambaye amesisitiza wafanya uamuzi wa kisiasa na kiuchumi katika ngazi ya kimataifa lazima wasikilize matakwa ya wale walio chini kabisa katika mnyororo wa chakula.Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia video amesema, "kuna kitu hakiko sawa katika ulimwengu ambao njaa na utapiamlo ni ukweli wa maisha kwa mabilioni ya watoto, wanawake na wanaume." Akasema ulimwengu usio na njaa unawezekana, lakini "mifumo ya chakula inahitaji mabadiliko makubwa," ili kuwa na ufanisi zaidi, ujumuishi, mnepo na endelevu.Gérardine Mukeshimana, Makamu wa Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) ametoa wito wa "uwekezaji wa haraka, wa pamoja na thabiti kwa wakulima maskini wa vijijini kutambua kwa ngazi ya chini kabisa haki yao ya msingi ya chakula chenye lishe." Akabainisha kuwa wakulima wadogo wanazalisha karibu nusu ya chakula cha dunia, ingawa pia wanakabiliwa na njaa na umaskini.Mfalme Letsie III wa Lesotho, ambaye ni Balozi Mwema Maalum wa FAO katika upande wa lishe anaeleza anavyoiunga mkono FAO kwa “kujaribu kuwa mtetezi mwaminifu na mwenye kujitolea katika masuala ya lishe, katika masuala ya uhakika wa chakula.” Anasema, “na mara kwa mara, mimi hutembelea sehemu nyingine za bara la Afrika nikivaa kofia yangu ya FAO, hasa kuhimiza serikali na viongozi kama bara kuwekeza zaidi katika masuala ya lishe na masuala ya uhakika wa chakula.”.
16-10-2024 • 1 minuut, 47 seconden
15 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani kesho ikiwa ni siku ya chakula duniani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatili juhudi za FAO za kuhakikisha haki ya chakula kwa maisha bora na mustakabali bora kwa wananchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Licha ya mashambulizi, awamu ya pili ya chanjo kwa watoto dhidi ya polio huko Gaza iliyoanza jana imeendelea leo Jumanne eneo la kati mwa Gaza na hadi sasa watoto wapatao Elfu 93 wenye umri wa chini ya miaka 10 wameshapatiwa dozi ya pili.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hii leo linatoa wito wa msaada wa dharura kuepusha janga la kibinamu eneo la kusini mwa Afrika kutokana na ukame uliochochewa na El- Niño.Na ubia mpya wa kutokomeza watu kukosa utaifa umezinduliwa huko Geneva, Uswisi ukilenga kutokomeza hadhi hiyo inayoathiri mamilioni ya watu duniani. Zaidi ya nchi 100, mashirika ya kiraia, taasisi zinazopigia chepuo kuondokana na hadhi hiyo, wanazuoni na wadau wengine wameanzisha ubia huo ikiwa ni kuendeleza kampeni ya muongo mmoja iliyopatiwa jina Mimi ni wa! Au I Belong.Mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya wanawake wa vijijini, ninampisha Motshekile Mlalazi, mkulima kutoka Gokwe, kaskazini mwa Zimbabwe, ambaye kupitia video ya FAO anatueleza kuhusu mbinu yake ya kilimo hai ya kuchanganya mazao aliyojifunza kizazi hadi kizazi ilivyochangia katika lishe bora, bayoanuwai ya kilimo, na pia kuongeza kipato.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
15-10-2024 • 10 minuten, 51 seconden
Wagonjwa majeruhi wa vita 16 wahamishwa kutoka hospitali ya Kamal Adwan kuwapeleka katika hospitali ya Al-Shifa
Operesheni ya vikosi vya jeshi la Israel inayoendeea Kaskazini mwa Gaza kwa njia ya anga na ardhini kukabiliana na wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas yamelifanya eneo hilo kukatwa na sehemu zingine za Gaza, kwa kiasi kikubwa raia wakikosa huduma za msingi kama chakula, elimu na matibabu. Hospitali karibu zote Gaza Kaskazini hazifanyi kazi na iliyosalia ni Kamal Adwan nayo ikitoa huduma kwa kiasi kidogo sana kutokana na ukosefu wa vifaa, wahudumu wa afya na mafuta. Majeruhi wa vita wamezidi uwezo wa hospitali hiyo ndio maana ikaamua kuomba msaada kutoka shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kuhamisha majeruhi hao kwenda hospitali Al-Shifa mjini Gaza. Katika makala hii Flora Nducha anamulika zoezi hilo la kuhamisha majeruhi.
14-10-2024 • 3 minuten, 28 seconden
UNICEF yatoa mafunzo ya kutengeneza sodo kwa kijana mkimbizi wa dani nchini Sudan
Sodo au taulo za kike, vile vile pedi, ni muhimu kwa wanawake na wasichana, lakini wengi hawawezi kuzipata wakati wa vita na ukimbizi. Leo tunakutana na Samer, mvulana huyu ambaye akiwa na umri wa miaka 16 tu, kwa msaada wa klabu ya usafi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, anatengeneza na kusambaza sodo kwa wanawake na wasichana katika maeneo ya wakimbizi wa ndani jimboni Atbara, nchini Sudan. Msaada wa kifedha kutoka Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF, vilabu vya usafi vya UNICEF, na Shirika la Marekani la misaada ya maendeleo USAID, vijana wakimbizi wa ndani wanawezeshwa kupata suluhisho kwa changamoto za usafi wanazokutana nazo, wakati wa vita na ukimbizi. Mmoja wa vijana hawa wakimbizi ni Samer mvulana mwenye umri wa miaka 16, ambaye amefundishwa kutengeneza sodo na sasa, anazisambaza bure kwa wanawake na wasichana wakimbizi wa ndani katika jimbo la Atbara, nchini Sudan.Nikataka kujua jinsi Samer anatengeneza sodo hizo…"Nashona kati ya vipande kumi na tano hadi ishirini kwa siku. Kwanza, nakata sponji au sifongo, kisha naweka ndani ya kitambaa. Naishona na kuongeza kifungo ili kuifunga vizuri."Kwa nini Samer, katika umri wa miaka 16, anatengeneza sodo"Hiki ndicho wasichana na akina mama wanachohitaji zaidi wakati wa ukimbizi, lakini hakipatikani. Ikiwa hawatumii sodo, huenda wasiweze kusafiri au kutembea kwa uhuru. Kwa hiyo, nazitengeneza na kuwapatia bure kwa ajili yao kutumia. Kwa sababu ya vita, watu hawana pesa za kununua pedi, kwa hiyo nazitengeneza na kuzisambaza. Sodo hizi zinaweza kufuliwa na kutumika tena. Pedi nyingi ni hutumiwa mara moja tu, na watu wanalazimika kununua mpya kila wakati."Je nini kilimpa Samer hamasa ya kutengeneza sodo, na anajisikia vipi anapoifanya kazi hii?"Nilipojiunga na warsha ya UNICEF, nilianza kusaidia familia yangu kwa kuwatengenezea sodo. Napokea vifaa kutoka kiwanda cha UNICEF. Nilipoanza kutengeneza sodo, nilihisi furaha kujua kuwa kuna watu wanaozihitaji. Baadhi yao, hawana pesa na wanakabiliwa na changamoto. Sijihisi aibu kwa kile ninachofanya, kwa sababu kutimiza mahitaji ya watu ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine chochote."
14-10-2024 • 2 minuten, 20 seconden
14 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya afya katika ukanda wa Gaza yakiwa ni pamoja na chanjo dhidi ya polio huku mashambulizi ya Israel yakiendelea, na kuwahamisha wagonjwa majeruhi. Pia tunaangazia mchango wa wakimbizi Sudan kwa jamii, na ndoa za utotoni Zambia.Mashambulizi yakiendelea kurindima kutoka pande hasimu, jeshi la Israeli na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na Hezbollah huko kusini mwa Lebanon, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na awamu ya pili ya chanjo dhidi ya Polio Ukanda wa Gaza, huku huko Lebanon ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ikisihi raia wasilengwe.Sodo au taulo za kike, vile vile pedi, ni muhimu kwa wanawake na wasichana, lakini wengi hawawezi kuzipata wakati wa vita na ukimbizi. Leo tunakutana na Samer, mvulana huyu ambaye akiwa na umri wa miaka 16 tu, kwa msaada wa klabu ya usafi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, anatengeneza na kusambaza sodo kwa wanawake na wasichana katika maeneo ya wakimbizi wa ndani jimboni Atbara, nchini Sudan.Makala inatupeleka Kaskazini mwa Gaza kwenye moja ya operesheni ngumu na hatari ya kuwahamisha wagonjwa majeruhi wa vita 16 katika hospitali ya Kamal Adwan kuwapeleka katika hospitali ya Al-Shifa mjini Gaza, wakati operesheni ya kijeshi ya Israel ikiendelea.tutaelekea Zambia kumsikia kiongozi wa jamii ya Chewa, Mashariki mwa Zambia anayeongoza mapambano dhidi ya ndoa za utotoni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
14-10-2024 • 10 minuten, 23 seconden
Awamu ya 2 ya chanjo dhidi ya Polio Gaza yaanza licha mashambulizi
Mashambulizi yakiendelea kurindima kutoka pande hasimu, jeshi la Israeli na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na Hezbollah huko kusini mwa Lebanon, mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na awamu ya pili ya chanjo dhidi ya Polio Ukanda wa Gaza, huku huko Lebanon ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ikisihi raia wasilengwe. Naanzia eneo la kati mwa ukanda wa Gaza ambako asubuhi ya leo Jumatatu awamu ya pili ya chanjo dhidi ya polio imeanza ikilenga watoto 591 700 wenye umri wa chini ya miaka 10, watakaopatiwa dozi ya pili ya chanjo hiyo kufuatia kuthibitishwa kwa polio Gaza mwezi Agosti mwaka huu.Chanjo inatolewa licha ya ripoti za makombora kurushwa kwenye shule moja iliyogeuzwa makazi ya wakimbizi huko Nuseirat na katika hospitali moja huko Deir Al-Balah ambako mahema kadhaa yaliteketezwa kwa moto wakati watu wamelala.Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, Louise Wateridge akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesema, “nimekuwa kwenye simu na mfanyakazi mwenzangu tangu saa 9 alfajiri ya leo. Alikuwa amejihifadhi kwenye hospitali ya Al Aqsa. Ni mmoja wa watu wengi ambao wamepoteza kila kitu. Hema lao limeteketezwa. Tumeona picha na video, inaonekana makazi ya familia nyingi yameteketezwa kwenye moto huu mkubwa, na yeye amenaswa kwenye zahma na mashambulizi. Inatia kiwewe hata kusikiliza hali anayokumbana nayo.”Picha za mnato pamoja na video kutoka UNRWA zinaonesha wafanyakazi wa uokoaji wakisaka manusura kwenye eneo la hospitali ya Al Aqsa, huku mahema yakiwa yanateketea na nondo zimesambaratika. Maiti walioteketezwa kwa moto walikuwa wamefunikwa kwa blankenti.Na nikigeukia Lebanon, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X, zamani Twitter inasema chuki kati ya Israeli na wanamgambo wa Hezbollah, inaendelea kusababisha vifo, majeruhi na ukimbizi.Mashambulizi yanayoripotiwa kulenga makazi ya watu ambako wakimbizi wamesaka hifadhi. Inataka pande kinzani ziheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu na kwamba raia na miundombinu ya kiraia isilengwe.Naye Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi akizungumza Geneva, Uswisi hii leo amesema kwa mara nyingine tena suala la kutofautisha kati ya raia na wapiganaji limekuwa halina maana, akimulika jinsi raia wanavyokimbia mashambulizi ya angani kutoka jeshi la Israeli huko Lebanon.
14-10-2024 • 3 minuten, 28 seconden
FAO yaleta nuru kwa wafugaji walioathiriwa na vita Gaza
Mwaka mmoja wa vita katika ukanda wa Gaza iliyochochewa na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israeli Oktoba 7, 2023 na kisha Israeli kujibu mashambulizi yanayoendelea hadi leo, umekuwa ukimulika zaidi madhara ya vifo na majeruhi. Lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekusogezea madhara ya vita katika kilimo na ufugaji na ndio makala yetu ya leo ikisimuliwa na Assumpta Massoi.
11-10-2024 • 3 minuten, 32 seconden
Guterres: Ni wakati muafaka sisi kuwasikiliza wasichana
Ikiwa le oni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akianza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia tarehe mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.“Wasichana wanachangia zaidi ya asilimia 70 ya maambukizi mapya ya Virusi Vya Ukimwi, VVU” anasema Guterres na kwamba wana uwezekano mara mbili zaidi wa wavulana kukosa elimu au mafunzo. Na ndoa za utotoni bado zimeenea, huku takriban msichana mmoja kati ya watano duniani akiolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18. Kotekote duniani, mafanikio yaliyopatikana kwa bidii ya usawa wa kijinsia yanafutwa na vita dhidi ya haki za kimsingi za wanawake na wasichana, na kuhatarisha maisha yao. kuzuia uchaguzi wao, na kuweka kikwazo cha mustakabali wa wasichana.Kwa kutumia kaulimbiu ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo ni ‘Dira ya Msichana’ kwa Zama Zijazo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anasema, wasichana tayari wana dira ya ulimwengu ambamo wanaweza kustawi. Wanafanya kazi kugeuza maono hayo kuwa vitendo, na kutaka sauti zao zisikike. Ni wakati muafaka sisi kusikiliza. Ni lazima tuwape wasichana nafasi kwenye meza, kupitia elimu, na kwa kuwapa rasilimali wanazohitaji na fursa za kushiriki na kuongoza.Ujasiri, matumaini na uamuzi wa wasichana ni nguvu ya kuzingatia. Ni wakati wa ulimwengu kuchukua hatua na kusaidia kubadilisha maono na matarajio yao kuwa ukweli.
11-10-2024 • 1 minuut, 45 seconden
11 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike na juhudi za Umoja wa Mataifa za kutokomeza ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na unaofanyika mtandaoni. Makala tunakupeleka katika ukanda wa Gaza, na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa kuwapa sikio watoto wa kike akisema uwezo wa wasichana zaidi ya bilioni 1.1 duniani hauna kikomo lakini tunapokaribia mwaka 2030, wa mwisho kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, ulimwengu unaendelea kuwaangusha wasichana.Nchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15.Makala tunakupeleka Gaza ambapo mwaka mmoja wa vita nchini Gaza iliyochochewa na mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israeli Oktoba 7, 2023 na kisha Israeli kujibu mashambulizi yanayoendelea hadi leo, umekuwa ukimulika zaidi madhara ya vifo na majeruhi. Lakini sasa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekusogezea madhara ya vita katika kilimo na ufugaji.Katika mashinani leo ikiwa ni Siku ya kimataifa ya Mtoto wa Kike tunaelekea nchini Tanzania kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo, kujifunza kutoka mtoto mmoja wa kike kuhusu haki za watoto.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
11-10-2024 • 9 minuten, 58 seconden
UNICEF nchini Ethiopia yarejesha matumaini kwa manusura wa ukatili wa kingono
Nchini Ethiopia hususan katika jimbo la Somali, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kusaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kuweza kujenga upya maisha yao wakati huu ambapo takwimu za shirika hilo zinaonesha kuwa zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 duniani kote wamekumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 15. Sauti hiyo ya Nasteyo Sahane Layle, Meneja wa kushughulikia visa vya ukatili wa kijinsia dhidi ya akina mama, watoto na wanawake hapa Gode, jimboni Somali mashariki mwa Ethiopia akisema kuwa kazi kubwa tunayoifanya ni visa vinavyohusu ukatili wa kingono.Ni katika video ya UNICEF iliyochapishwa kuonesha kiza kinachokumba watoto wa kike hususan leo ambayo ni siku ya kimataifa ya mtoto wa kike.Hapa Gode, UNICEF imeanzisha kituo hicho cha kutoa huduma zote na sasa kimekuwa ni kama eneo salama kwa manusura wa ukatili wa kingono.Anaonekana mmoja wa wasaka huduma kituoni hapa akifika tayari kupatiwa huduma, sura yake imefichwa ili kuficha utambulisho wako.Anapatiwa huduma ikiwemo kupimwa mapigo ya moyo na vipimo vingine na kisha kupatiwa dawa.Nasteyo anasema,“kinachotusikitisha zaidi ni watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 ambao walibakwa, na sasa mustakabali wao umeharibiwa.”Pamoja na Nasteyo, wahudumu wengine katika kituo hiki ni Nimo, Faduo, Ifrah na Hamdi, wote wanawake.Ni kutokana na huduma zao, manusura wanajiona wako salama kwani wanapatiwa huduma za kisaikolojia na nyingine muhimu wanazohitaji.Na kisha kupata tena uwezo wa kujiamini na kujenga upya maisha yao. TAGS: AfyaAdditional: AfyaNews: Ukatili wa Kingono, EthiopiaRegion: AfrikaUN/Partner: UNICEF
11-10-2024 • 1 minuut, 51 seconden
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa methali “Mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichika.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu hii leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichika.”
10-10-2024 • 1 minuut, 1 seconde
10 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika malengo ya maendeleo endelevu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwema za Lebanon, afya ya akili na ripoti ya UNICEF kuhusu ukatili wa kingono. Katika kujifunza Kiswahili tunakuletea uchambuzi wa methali.Nchini Lebanon ujumbe wa jeshi la Umoja wa Mataifa la mpito nchini humo, UNIFIL, unasema mapigano kati ya jeshi la Israeli, IDF, na wanamgambo wa Hezbollah kusini mwa Lebanon yamekuwa na madhara kwa ujumbe huo kwani makao yake makuu huko Naqourra na maeneo ya karibu yameshambuliwa mara kwa mara tangu kuanza kwa mapigano kati ya pande hizo mbili.Leo ni siku ya afya ya akili duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake amesisitiza udharura wa kupatia kipaumbele afya ya akili pahala pa kazi.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema zaidi ya wasichana na wanawake milioni 370 walioko hai hii leo, walikumbwa na ukatili wa kingono wakati wa utoto wao, yaani kabla ya kutimiza umri wa miaka 18.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu hii leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichika.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
10-10-2024 • 11 minuten, 20 seconden
Utoaji wa chanjo dhidi ya mpox nchini DRC
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imeanza chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya Nyani au MPOX mwishoni mwa wiki iliyopita. Hii ni hatua muhimu ya kuongeza juhudi zinazoendelea za kupambana na mlipuko wa ugonjwa huo ambao DRC inachangia asilimia 90 ya wagonjwa wote zaidi ya 18,000 duniani. Lengo sasa ni kuokoa maisha, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, kanda ya Afrika. Shuhuda wetu wakati wa kuanza kazi ya kutoa chanjo alikuwa mwandishi wetu wa Mashariki mwa DRC, George Musubao kutoka Goma, jimboni Kivu Kaskazini.
10-10-2024 • 3 minuten, 31 seconden
09 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani ikiwa ni siku ya posta duniani tunaangazia huduma za posta na juhudi za mashirika za kukabiliana na Mpox nchini DRC. Makala tunasalia huko huko DRC kufuatilia uzinduzi wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo huo, na mashinani tunakupeleka nchini Lebanon.Leo siku ya posta duniani huduma ambayo ilionekana kuwa itasambaratika kufuatia ujio wa maendeleo ya teknolojia ya intaneti lakini wenyewe wasimamizi wa huduma hii duniani wanasema licha ya mtikisiko sasa mambo yanashamiri, siri kubwa ikiwa ni ubia badala ya ushindani.Ukisikia makovu yasiyofutika ni ya simulizi hii utakayoisikia kuhusu familia moja huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupoteza watoto wanne kutokana na ugonjwa wa homa ya nyani au mpox huku mustakabali wao ukisalia mashakani kwani bado hawafahamu hali itakuwa vipi kwenye familia yao, baba na mama wakipambana na ugonjwa huo.Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo chanjo dhidi ya mpox imeanza.Na mashinani tutaelekea Lebabon ambapo, tutasikia simulizi ya Wahiba mwanamke mkimbizi kutoka Syria anayeishi Lebanon, ambaye sasa amelazimika kuikimbia Lebanon kufuatia mashambulizi nchini humo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
9-10-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Shirika la Umoja wa Mataifa la Posta lahimili changamoto kwa kugeuza changamoto kuwa fursa
Leo siku ya posta duniani huduma ambayo ilionekana kuwa itasambaratika kufuatia ujio wa maendeleo ya teknolojia ya intaneti lakini wenyewe wasimamizi wa huduma hii duniani wanasema licha ya mtikisiko sasa mambo yanashamiri, siri kubwa ikiwa ni ubia badala ya ushindani. Tunasherehekea miaka 150 ya shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU, tunatambua umuhimu wa moja ya mifano ya mapema zaidi ya ushirikiano wa kimataifa. Ni Masahiko Metoki, Mkurugenzi Mkuu wa UPU katika ujumbe wake wa siku hii adhimu akiongeza kuwa..“Kile kilichoanza na wanachama 22 sasa inajumuisha nchi 192, kikionesha uthabiti wa ushirikiano wa kimataifa.”Miaka 150 wamekumbana na changamoto, vita, majanga mabadiliko ya kasi ya teknolojia ya kidijitali. Lakini wanafanya nini?“Leo hii UPU inaongoza juhudi za kufanya huduma za posta kuwa za kisasa na bora. Inatoa fursa kwa nchi kushirikishana ufahamu, kusaka majawabu na kukabili changamoto za sasa. Moyo wetu wa ushirikiano ndio umetusaidia kugeuza vikwazo kuwa fursa na kufanya huduma za posta kuendana na dunia inayobadilika.”Na zaidi ya yote…“Awali tuliona ongezeko la mawasiliano ya kidijitali kuwa ni tishio kwani kiwango cha utumaji wa barua kwa njia ya posta kilipungua. Lakini sasa tunaona fursa za utajiri. Mtandao mkubwa wa UPU umesaidia kupanuka kwa huduma mbali mbali ikiwemo biashara mtandao, huduma za kifedha, kijamii na kidijitali, ikihakikisha ufikiaji wa kila mtu duniani hata wale walio ndani zaidi hawaachwi nyuma.”Kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, UPU imehimili changamoto kwa kuwa bunifu, jumuishi na kusongesha ushirikiano wa kimataifa.“Katika siku hii muhimu, hebu na tusherehekee na tupongeze kazi ya shirika la Posta duniani ya kuondoa umbali na kuunganisha dunia.”
9-10-2024 • 2 minuten, 10 seconden
Ugonjwa wa Mpox ‘umepoteza’ watoto wanne wa familia moja DRC
Ukisikia makovu yasiyofutika ni ya simulizi hii utakayoisikia kuhusu familia moja huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupoteza watoto wanne kutokana na ugonjwa wa homa ya nyani au mpox huku mustakabali wao ukisalia mashakani kwani bado hawafahamu hali itakuwa vipi kwenye familia yao, baba na mama wakipambana na ugonjwa huo. Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iliyochapishwa kwenye mtandao wa Instagram unatupeleka Mbandaka, mji ulioko jimboni Equateur, kaskazini-magharibi mwa DRC.Dkt. Douglas Noble Mkurugenzi Mshiriki, UNICEF ndiye mwenyeji wetu hapa kwani ametembelea kituo cha matibabu ya mpox hapa Mbandaka.“Tuko hapa Mbandaka, ambapo kuna idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wa mpox. Tumetembelea kituo cha matibabu, na ni huzuni kusikia hadithi ya familia moja yenye watoto sita, ambapo wanne walifariki dunia kwa mpox. Watoto wawili wako vizuri kwenye kituo cha watoto. Baba na mama bado wako kituo cha matibabu”"Ni kwa kuzingatia madhara ya ugonjwa wa mpox kwa watoto na jamii nchini DRC ndio maana Dkt. Noble anasema..“Simulizi kama hizi zinatufanya tutambue uzito wa ugonjwa huu kwa watoto na jinsi unavyoathiri jamii. Wito wetu ni kuwahamasisha watu na kujenga uwezo wao ili waweze kudhibiti hali hii.”Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC inatajwa kubeba asilimia 90 ya wagonjwa wote 18,815 walioripotiwa duniani kote.
9-10-2024 • 1 minuut, 48 seconden
08 OKTOBA 2024
Mnamo mwaka wa 2020, Umoja wa Mataifa ulipotimiza miaka 75 tangu kuanzishwa, pamoja na maadhimisho wakati huo ulimwengu ulianzisha mazungumzo ya kimataifa kuhusu matarajio na hofu kuhusu zama zijazo. Huo ndio ukawa mwanzo wa mchakato ambao hatimaye, miaka minne baadaye, hivi majuzi umefanyika Mkutano wa Zama Zijazo. Lakini kwa kuwa mikutano na mipango mingine ilishafanyika katika siku za nyuma, je huu nao unaweza kuwa ni mvinyo wa zamani katika chupa mpya kwa hiyo hautakuwa na mchango mkubwa chanya kwa dunia? Kuyajadili haya na mengine mara baada ya mkutano huo wa zama zijazo kukamilika jijini New York, Marekani, Anold Kayanda wa Idhaa hii aliketi na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Veronica Nduva aliyeshiriki mkutano huo.
8-10-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Wiki mbili za kusaka usalama DRC, mkimbizi asimulia madhila na atakacho.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imesalia katika mgogoro kwa miaka mingi, hali ambayo imewasababishia raia mateso ya hali ya juu zaidi yakiwemo mauaji, utekaji nyara, na kuteketezwa kwa nyumbaa zao. Mapigano hayo pia yamewafungisha viragozaidi ya watu milioni 6.4 nchini humo, na kulazimisha familia kutafuta usalama katika makazi ya muda yaliyojaa pomoni. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeonya kuwa mgogoro huu uliodumu kwa muda mrefu na ukiukwaji wa haki za binadamu ni mwiba kwa wakimbizi hawa wa ndani. Cicey Kariuki na taarifa zaidiRusayo ni eneo lililo na makazi ya muda ya wakimbizi mjini Goma katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Miongoni mwa wakimibizi wa ndani wanaishi kwenye makazi haya ni Sebororo, mwanamke mwenye miaka 38 akitembea na watoto wake.Sebororo pamoja na wananawe watano wanaishi kwenye makazi ya pamoja na familia nyingine 90 huku wakisubiri kutengewa nyumba katika eneo hilo. Mama huyu anaeleza jinsi alivyojikuta katika makazi ya wakimbizi. Anasema,“tulianza kukimbia kuktoka kule tarehe tano mwezi wa kumi, awali walikuwa wanakuja lakini hawakuua watu, lakini leo hii wanaua watoto,wanaume na wanawake, sisi yalitushinda maanake wengine walikuwa pia wanatekweteza mimea.”Sebororo na watoto wake watano walitembea kwa wiki mbili kutafuta usalama, baada ya wapiganaji kuvamia kijiji chao cha Kiseguru katika Mkoa wa Kivu Kaskazini. Katika nusu ya kwanza ya mwaka wa 2024 pekee, zaidi ya watu 940,000 walilazimika kukimbia kutokana na ukatili, uliofanywa na makundi mengi yenye silaha yasiyo ya kiserikali huku familia nyingi zikifurushwa mara kadhaa. Kwa sasa anachokitamani zaidi Sebroro ni amani. “Haja yetu sisi ni watusaidie kwa kusimamisha vita ili turejee kwetu kwa sababu watu wanaisha.”Anasema.Kufurika kwa watu katika makazi haya ya muda kumezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wahudumu wa kibinadamu kufuatia hatari ya kuenea kwa magonjwa, ikiwa ni pamoja na virusi vya homa ya nyani au mpox.Ruven Menikdiwela, Kamishna Msaidizi wa Operesheni wa UNHCR ambaye alitembelea eneo hilo na kukutana na familia mbalimbali za wakimbizi na kusikiliza wasiwasi wao, anasema, “leo asubuhi, nilizungumza na mwanamke huyu ambaye ana watoto wadogo watano. Alitembea kwa wiki mbili kufika katika eneo hili, bado anasubiri huduma, bado anasubiri watoto wake watibiwe, na bado anasubiri chakula. Ninatambua kwamba hii ni hali ya kawaida kwa watu wote wanaoishi katika eneo hili. Kila mmoja ana majanga yake binafsi, kwa hivyo hizi siyo tu takwimu, bali kuna hadithi za kibinafsi nyuma ya kila moja ya hizi takwimu na majanga ya kibinafsi na majanga yanayoendelea pia, kwa sababu hatuoni suluhisho lolote kwenye mustakabali.”Katika ziara yake kwenye makazi haya, Ruven Menikdiwela, pia alifanya vikao na wadau kadhaa akiwemo Waziri mkuu, mamlaka za mkoa na mashirika ya umoja wa Mataifa. Ujumbe wake ulikuwa wazi kwamba amani ndiyo suluhisho endelevu na dhabiti zaidi, na inahitajika kwa dharura. “Pande zote zinapaswa kukutana na kujadiliana kutoa fursa kwa amani, ili watu hawa wote, mamilioni ya watu waliolazimika kuhama, waweze kurudi nyumbani au kuunganishwa na jamii mahali walipo, na waweze kuishi kwa amani pamoja kama jamii moja.”
7-10-2024 • 2 minuten, 23 seconden
Tiba Salama Digital Health App shirika linalotumia teknolojia kutekeleza SDGs
Tiba Salama Digital Health App shirika la kijamii la lilalolenga kutumia teknolojia kutekeleza Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs katika kutoa huduma za afya kwa wanawake wajawazito, wanaolea na watoto.Lengo kuu ni kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa vifo vya wajawazito na watoto wadogo kwa kuoresha huduma za afya hususani kwa maeneo ya pembezoni yenye upatikanaji hafifu wa huduma za msingi za afya.Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza Simon Mashauri, Mkurugenzi na Mwazilishi wa shirika hilo lenye makao yake makuu mkoani Tanga, kaskazini mashariki mwa Tanzania.
7-10-2024 • 3 minuten, 31 seconden
Mwaka 1 wa vita Mashariki ya Kati: Ni wakati wa amani Gaza, asema Guterres
Leo ni mwaka mmoja tangu vita ianze huko Gaza, Mashariki ya Kati baada ya wanamgambo wa kipalestina, Hamas kushambulia Israeli na kuua waisraeli 1250 pamoja na wageni, kisha Israeli kujibu mashambulizi yaliyoripotiwa kuua hadi sasa zaidi ya wapalestina 41,000 ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pamoja na wakuu wa mashirika mbali mbali ya chombo hicho wametoa wito kutaka kukoma kwa vita hiyo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. Antonio Guterres huyu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake kwa njia ya video leo ikiwa in mwaka mmoja, anasema hii ni siku kwa jamii ya kimataifa kurejelea tena kwa sauti kubwa zaidi kulaani kwetu kwa vitendo vya kuchukiza vya Hamas ikiwemo utekaji nyara wa siku ile.Hamas waliteka nyara zaidi ya watu 250. Guterres amesema katika kipindi cha mwaka mmoja amezungumza na familia ambazo ndugu zao wanashikiliwa mateka hadi sasa. Amezungumzia pia machungu yaliyoibuka baada ya vita kuanza. Sasa anasema ni wakati wa kuachilia huru mateka. Wakati wa kunyamazisha bunduki. Wakati wa kukomesha machungu yaliyogubika ukanda huo. Wakati wa amani, sheria ya kimataifa na haki. Umoja wa Matiafa umejizatiti kufanikisha malengo hayo. Pisha nikupishe za manusura, magari ya wagonjwa na viwewe ni hali ya kawaida Gaza kwa mwaka mmoja sasa.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya ulimwenguni, WHO, pamoja na kusaidia waathiriwa wa vita, linashirikiana na mashirika ya kiraia kusaidia wale wanaosaidia manusura, mathalani madereva wa magari ya wagonjwa, wahudumu wa afya ambao waliathiriwa na kile walichokiona wakati wakisafirisha mahututi au kutambua maiti kwenye vifusi.Lile la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limemnukuu Abu Majdi mpalestina mwenye umri wa miaka 80 akisema baada ya mwaka mmoja wa ukimbizi, joto kali na baridi kali, hadi lini tutaendelea kuhimili ukimbizi huu? Hadi lini tutapata haki na maisha yetu?Naye Kaimu Mkuu wa Ofisi ya UN ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA Joyce Msuya anasema hakuna takwimu zinazoweza kueleza bayana madhila ya kimwili, kiakili na kijamii ya vita hiyo.
7-10-2024 • 2 minuten, 14 seconden
07 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani Flora Nducha anamulika mwaka mmoja tangu kuanza kwa vita mpya huko Gaza, ambapo viongozi wa Umoja wa Mataifa na mashirika wanatoa kauli zao. Leo ni mwaka mmoja tangu vita ianze huko Gaza, Mashariki ya Kati baada ya wanamgambo wa kipalestina, Hamas kushambulia Israeli na kuua waisraeli 1250 pamoja na wageni, kisha Israeli kujibu mashambulizi yaliyoripotiwa kuua hadi sasa zaidi ya wapalestina 41,000 ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pamoja na wakuu wa mashirika mbali mbali ya chombo hicho wametoa wito kutaka kukoma kwa vita hiyo.Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, imesalia katika mgogoro kwa miaka mingi, hali ambayo imewasababishia raia mateso ya hali ya juu zaidi yakiwemo mauaji, utekaji nyara, na kuteketezwa kwa nyumbaa zao. Mapigano hayo pia yamewafungisha viragozaidi ya watu milioni 6.4 nchini humo, na kulazimisha familia kutafuta usalama katika makazi ya muda yaliyojaa pomoni. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeonya kuwa mgogoro huu uliodumu kwa muda mrefu na ukiukwaji wa haki za binadamu ni mwiba kwa wakimbizi hawa wa ndani. Makala inaelekea nchini Tanzania kuangazia Tiba Salama Digital Health App, shirika la kijamii la lilalolenga kutumia teknolojia kutekeleza Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs katika kutoa huduma za afya kwa wanawake wajawazito, wanaolea na watoto. Mashinani ikiwa dunia Jumamosi iliyopita iliadhimisha siku ya mwalimu duniani, nafasi ni yake mshindi wa tuzo ya UNESCO-Hamdan kutoka Togo, Mwalimu Komlan Abalo Braly wa shule ya sekondari Tchitchao, akielezea juhudi za kuboresha ufundishaji katika shule hiyo.
7-10-2024 • 11 minuten, 33 seconden
Boti yazama Ziwa Kivu, UN yashikamana na waathiriwa
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini kwenye mji mkuu, Goma, Alhamisi ya Oktoba 3 iligubikwa na kiza nyakati za asubuhi baada ya boti kuzama kwenye Ziwa Kivu. Ilikuwa inasafiri kutoka Minova, jimboni Kivu Kusini. Zahma hii imesababisha vifo kwa mujibu wa vyombo vya habari huku Umoja wa Mataifa nao ukitoa kauli. Mwenyeji wetu huko Goma aliyeshuhudia tukio hilo ni George Musubao.
4-10-2024 • 3 minuten, 37 seconden
UNESCO: Tunapaswa kuthamini sauti za walimu kote duniani
Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu. Kama tunavyofahamu, siku yenyewe ya Kimataifa ya Walimu ni kesho Oktoba 5 kama ilivyo ada ya kila mwaka lakini katika makao makuu ya UNESCO hapa Paris Ufaransa, maadhimisho yamefanyika leo kuelekea mkesha wa siku hii muhimu kwa elimu ya ulimwengu.Miongoni mwa waliozungumza ni Mkurugenzi Msaidizi Mkuu wa Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Bi Stefania Giannini, ambaye ameitumia nafasi hii kusisitiza kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni 'Kutambua sauti za walimu.'Anasema, “walimu ni uti wa mgongo wa mifumo ya elimu na mawakala wakuu wa mabadiliko ya kubuni sera za elimu na kufanikisha SDGs. Tunapaswa kuthamini sauti za walimu; hili ndilo lengo kuu la Siku ya Kimataifa ya Walimu mwaka huu.”Kulingana na takwimu zilizotolewa na UNESCO, dunia inahitaji walimu wa ziada milioni 44 ili kufikia elimu ya msingi na sekondari kwa wote ifikapo mwaka 2030. Ingawa mahitaji ya walimu ni makubwa zaidi katika baadhi ya maeneo, uhaba wa walimu ni wa kimataifa.Walimu wanajiondoa kwenye taaluma hii kwa kiwango mara mbili zaidi ya miaka mitano iliyopita, hasa katika elimu ya sekondari. Hii inatokana na hali zao za kazi, zikiwemo mishahara midogo, mzigo mkubwa wa kazi, na ukosefu wa ushiriki katika maamuzi yanayohusu elimu. Akiiangizia changamoto hii, Mkurugenzi wa Kimataifa wa Elimu na Maendeleo ya Vijana katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Bi. Pia Britto, aliyejiunga katika hafla ya leo kwa njia ya video akiwa Pakistani amesema,"Leo nilikuwa na fursa nzuri ya kuzungumza na walimu wengi, ikiwa ni pamoja na mwalimu Tahseen Bashir hapa Islamabad, ambaye amenieleza baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na kufundisha madarasa mengi, uhaba wa vifaa vya kujifunzia, na changamoto za kutoweza kufundisha namna wanavyodhamiria. Lakini pia amenieleza jinsi alivyofurahi kuona wanafunzi wake wakifaulu. Wakati sauti ya mwalimu inaposikilizwa na wakati sauti za walimu zinapopewa kipaumbele, wanajiona kama wadau katika kuboresha elimu kwa wakati wote, na hatua hizo zinahitajika ili kuleta mabadiliko chanya hasa katika hali ngumu zaidi."Siku hii ya kimataifa ya walimu ni mahususi kwa ajili ya kutambua na kusherehekea mchango muhimu wa walimu ulimwenguni kote katika kutoa elimu bora na kujenga mustakabali wa jamii. Pia, ni fursa ya kuangazia changamoto wanazokabiliana nazo walimu.Kutoka hapa Paris Ufaransa, mimi ni Cecily Kariuki..
4-10-2024 • 2 minuten, 58 seconden
04 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Lebanon, na kesho ikiwa ni Siku ya walimu Dunia tunakupeleka Paris, Ufaranza kutsikia toka UNESCO. Makala tunafuatili ajali ya boti iliyozama katika ziwa Kivu nchini DRC na mashinani tunakupeleka Burundi, kulikoni? Mashirikika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya nchini Lebanon wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kushika kasi na kuwafungisha virago maelfu ya watu, wengi wakikimbia nchi jirani ya Syria ambako nako si shwari.Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walimu ililofanyika leo Oktoba 4 katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris, Ufaransa wamesisitiza wito wa kuthamini mawazo ya walimu katika kuboresha elimu ya ulimwengu.Makala inakupeleka huko Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako janga la kuzama kwa boti ya abiria na mizigo liligubika eneo hilo Alhamisi asubuhi za huko.Na mashinani kupitia video ya WHO Afrika, tunamsikia Dkt. Dieudonné Niyongere akizungumza kuhusu msaada muhimu wa washirika katika kuimarisha juhudi za kukabiliana na mlipuko wa Mpox nchini Burundi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
4-10-2024 • 11 minuten, 18 seconden
UN: Lebanon inakabiliwa na zahma kubwa wakati mashambulizi ya Israel yakiendelea
Mashirikika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya nchini Lebanon wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiendelea kushika kasi na kuwafungisha virago maelfu ya watu, wengi wakikimbia nchi jirani ya Syria ambako nako si shwari. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO linasema hali nchini Lebanon ni janga la kibinadamu watu wengi wamejeruhiwa , wengine kupoteza maisha na mfumo wa afya umelemewa.Kupitia ukurasa wake wa X Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema katika jitihada za kuwasaidia waathirika ndege ya kwanza ya msaada wa vifaa vya kitabibu vya upasuaji, dawa na vifaa tiba vingine imewasili mapema leo mjini Beiruti na vifaa hivyo vitatosha kuwatibu maelfu kwa maelfu ya watu na kuokoa maisha yao na ndege nyingine mbili zitawasili baadaye leo.Kwa upande wake Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema maelfu ya watu wanaendelea kukimbia mashambulizi ya makombora ya Israel na wengine wakivuka mpaka kwa miguu kuingia Syria kusaka uslama. Pamoja na kwamba linafanya kila liwezekanalo kuwasidia , limesema msaada zaidi unahitajika kukabiliana na wimbi la watu wanaoendelea kufurushwa.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva wao “ Wamelaani vikali mashambulizi yanayotekelezwa kwenda Israel na makundi yenye silaha yasiyo ya kiserikali yaliyopo Lebanon ambayo yamesababisha watu 63,000 kutawanywa nchini Israel. Wamesema wahusika lazima wawajibishwe na watu waliotawanywa wapewe msaada na ulinzi.”Hata hivyo wamesisitiza kwamba“ Israel haiwezi kutumia uhalifu huo kama sababu ya kuhalalisha uhalifu wao nchini Lebanon unaojumuisha vitendo vya machafuko yenye lengo la kuleta hofu miongoni mwa raia wanaowashambulia.”Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, chini ya muda wa mwezi mmoja idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Lebanon imeongezeka mara tatu na zaidi ya watu 1,600 wameuawa na wengine takriban 346,000 kujeruhiwa wakiwemo watoto 127.
4-10-2024 • 2 minuten, 1 seconde
Jifunze Kiswahili - Maana ya neno “NGEJA”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “NGEJA”
3-10-2024 • 1 minuut, 3 seconden
03 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kumulika ugonjwa wa homa ya nyani au mpox. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za machafuko Lebanon, Haiti na Sudan. Katika kujifunza Kiswahili Onni Sigalla anafafanua maana ya neno “NGEJA” Mashariki ya Kati, nchini Lebanon hali inaendelea kuwa tete amesema mratibu maalum wa Umoja wa mataifa nchini humo Jeanine Hennis Plasschaert. Kupiti ukurasa wake wa mtandao wa X amesema umekuwa usiku mwingine wa kutoka kulala mjini Beiruti milipuko ikighubika mji huo bila tahadhari, raia wakikumbwa na taharuki bila kujua mustakbali wao.Mtaalamu mhuru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Sudan Radhouane Nouicer, leo ametoa wito kwa jeshi la Sudan (SAF), Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na wanamgambo wenye silaha kuchukua hatua za haraka kuhakikisha ulinzi wa raia mjini Khartoum, huku kukiwa na ongezeko la uhasama na ripoti za kutatanisha za mauaji ya kiholela.Na zaidi ya watu laki 7, sasa ni wakimbizi wa ndani nchini Haiti huku zaidi ya nusu ya idadi hiyo ni watoto, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.Ripoti inasema kuna ongezeko la asilimia 22 la watu waliofurushwa makwao, ambapo machafuko ya magenge ya uhalifu yamewalazimisha watu 110,000 kuzikimbia nyumba zao katika miezi saba iliyopita pkee. IOM imesema ongezeko hilo linasisitiza haja ya msaada zaidi wa kibinadamu kwa ajili ya waathirika.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “NGEJA”?Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
3-10-2024 • 11 minuten, 16 seconden
Vivian Joseph: Taasisi ya Watoto Afrika ni fursa kwa kila mtoto kufikia uwezo wake
Moja ya malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu SDGs ani lengo namba 4 la kuhakikisha elimu bora kwa kila mtoto. Hata hivyo bado katika nchi nyingi hususan zinazoendelea watoto wengi hasa wenye ulemavu wanakosa fursa za kufikia uwezo wao kutokana na changamoto za kupata elimu iwe rasmi au isiyo rasmi na hivyo kusalia nyuma. Umoja wa Mataifa umekuwa ukizichagiza nchi na jamii kuchukua hatua ili kubadili mwelekeo huo. Nchini Tanzania kijana Vivian Joseph ni miongoni mwa walioitikia wito wa hatua na akaanzisha taasisi isiyo ya kiserikali ya Watoto Afrika Initiative nili kusaidia watoto wenye changamoto ikiwemo ulemavu waweze kupata fursa hiyo ya elimu. Katika makala hii amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa kuhusu taasisi hiyo akianza kwa kufafanua wanachokifanya.
2-10-2024 • 3 minuten, 27 seconden
Waandishi wa habari wana wajibu wa kusimamia utekelezaji wa SDGs - Hanna Dadzie
Umoja wa Mataifa kila uchao unapigia chepuo wadau mbali mbali wakiwemo waandishi wa habari kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs ili sio tu yaweze kufahamika bali pia wale wanaowajibika kuyatekeleza wafanye hivyo ili hatimaye maisha ya wananchi yawe bora na si bora maisha.Hivi karibuni mwandishi wa Radio Washirika KidsTime FM ya mkoani Morogoro nchini Tanzania alikuwa Cairo Misri kwenye mafunzo ya wanahabari ambapo alimuuliza Hanna Dadzie mwandishi wa habari kutoka Shirika la Utangazaji Ghana, GBC ni hatua gani anachukua kusongesha SDGs.“Naamini kama mwana habari wajibu wangu katika kuhamasisha malengo ya maendeleo endelevu, ni kutengeneza uelewa na kusimamia hasa mashirika au taasisi za serikali kuhakikisha kwamba watu wanapata elimu, na tunaposema elimu sio tu elimu ni elimu bora. Kama mwandishi wa habari napaswa kuhakikisha watu hawa wote wanapata elimu bora, kwa sababu sote tumezaliwa kuwa sawa.”Akamulika maeneo ya SDGs ambayo amejikita zaidi.“Naweza kusema nimefanya habari nyingi katika hayo, kuhamasisha SDGs hasa eneo la afya, watu hawana uhakika wa kupata matibabu bora ya afya, naweza kusema kama ukiwa na afya bora una uhai, kama mtu wa habari napaswa kufanya habari zinazohusiana na jamii, kutengeneza uelewa, kuwafanya viongozi wasimame katika nafasi zao, kuhakikisha tunakuwa sawa kwa sababu inatakiwa kuwe na usawa, moja ya lengo la SDGs linazungumzia usawa kwa wote, kwa hivyo, wote tunapaswa kuwa na sawa.”Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa hivi karibuni kuhusu utekelezaji wa SDGs inabainisha kuwa malengo hayo 17 yametekelezwa kwa asilimia 17 pekee ikiwa imeasalia 6 kufikia ukomo wake.
2-10-2024 • 1 minuut, 53 seconden
02 OCTOBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mokuu katika Siku ya Kimataifa ya Kutokuwa na Ghasia, na waandishi wa habari katika harakati za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu. Makala inatupeleka Tanzania kuangazia taasisi ya watoto Afrika Initiative, na mashinani inatupeleka Amhara, Ethiopia, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokuwa na Ghasia, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa amezitaka nchi kubadilisha kuwa uhalisia ahadi za kuleta amani duniani walizojiwekea katika Mkutano wa Zama zijazo uliokamilika hivi majuzi hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Umoja wa Mataifa kila uchao unapigia chepuo wadau mbali mbali wakiwemo waandishi wa habari kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs ili sio tu yaweze kufahamika bali pia wale wanaowajibika kuyatekeleza wafanye hivyo ili hatimaye maisha ya wananchi yawe bora na si bora maisha.Makala inatupeleka Tanzania kuangazia taasisi ya watoto Afrika Initiative, iliyoanzishwa ili kuwasaidia watoto hususani vijana balehe. Je, inawasaidia vipi? Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na mwanzilishi na mkurugenzi mtendajiwa taasisi hiyo Vivian Joseph ambaye anaanza kwa kufafanua kuhusu taasisi hiyo ya Watoto Afrika Initiative.Katikashinani fursa ni yake Teyban Mohammed kutoka Amhara, Ethiopia, mama aliyenufaika kwa vocha za milo mbalimbali yenye lishe bora kutoka kwa WFP, akieleza manufaa ya mradi huu kwa watoto pamoja na kina mama wajawazito na wanaonyonyesha?Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
2-10-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Guterres: Ili kutokuwa na ghasia duniani nchi zibadilishe ahadi kuwa uhalisia
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutotumia vurugu, Katibu Mkuu wa Umoja Mataifa António Guterres amezitaka nchi kubadilisha kuwa ukweli ahadi za kuleta amani duniani walizojiwekea katika Mkutano wa Zama zijazo uliokamilika hivi majuzi hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Ni kupitia kwenye ujumbe wake mahususi kwa ajili ya kuadhimisha Siku hii ya kimataifa ya kutotumia vurugu ambayo huadhimishwa kila tarehe pili ya mwezi Oktoba tarehe ya kuzaliwa Mahatma Gandhi, kiongozi wa vuguvugu la uhuru wa India na mwanzilishi wa falsafa na mkakati wa kutotumia vurugu kama njia ya kufanikisha mabadiliko katika jamii, Bwana Guterres amekumbushia namna ambavyo siku chache zilizopita katika Mkutano wa Zama Zijazo nchi zilikuja pamoja ili kuweka msingi wa umoja mpya wa ushirikiano wa kimataifa, ulio na nyenzo za kusaidia amani katika ulimwengu unaobadilika.Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa anataja kwamba moja ya ahadi walizojiwekea viongozi wa ulimwengu ni kuangalia upya sababu za msingi za migogoro kuanzia kwa ukosefu wa usawa hadi umaskini na mgawanyiko na kwa hivyo sasa “tunahitaji nchi kubadilisha ahadi hizo kuwa uhalisia.” Akasisitiza.Bwana Guterres anaeleza kwamba siku hii ya kimataifa ya kutotumia vurugu inathibitisha tena maadili ambayo Mahatma Gandhi alijitolea maisha yake yaani usawa, heshima, amani na haki.Gandhi aliamini kutotumia vurugu ndio nguvu kuu zaidi inayopatikana kwa wanadamu yenye nguvu zaidi kuliko silaha yoyote. Na hivyo Guterres akazitaka nchi kwa pamoja, zijenge taasisi za kuunga mkono dira hiyo adhimu.
2-10-2024 • 2 minuten, 12 seconden
Sehemu ya 2 ya mahojiano na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa - Viuavijiumbe maradhi/Tabianchi
Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79, umekunja jamvi jana Jumatatu ambapo viongozi wa Dunia walikusanyika hapa New York kwenye Umoja wa Mataifa na kujikita na mada kadha wa kadha, katika sehemu hii ya pili ya mahojiano na mmoja wa washiriki wa mjadala huo waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa -Majaliwa. Flora Nducha ameangazia mbili kati ya mada kuu 4 zilizopewa uzito, Ambayo ni usugu wa dawa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.
1-10-2024 • 6 minuten, 25 seconden
01 OKTOBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikiwa Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79, umekunja jamvi jana Jumatatu, tunaangazia sehemu ya pili ya mahojiano na mmoja wa washiriki wa mjadala huo waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na sauti za mashinani, kulikoni?Baada ya siku 6 za viongozi wa nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kutoa hotuba kuhusu masuala muhimu yanayogusa dunia hivi sasa, wakizingatia maudhui ya kutomwacha nyuma mtu yeyote, hatimaye Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umekunja jamvi Jumatatu ya Septemba 30 jijini New York, Marekani.Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limesema kufuatia tangazo la serikali ya Rwanda juu ya mlipuko wa ugonjwa wa homa ya virusi vya marburg tarehe 27 mwezi uliopita, hadi sasa watu 8 wamefariki dunia kati ya 26 waliothibitishwa kuugua ugonjwa huo, mara ya kwanza kuripotiwa Rwanda. Rwanda inashirikiana na wadau ikiwemo WHO kudhibiti kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo ambao hadi sasa hauna chanjo wala tiba. Asilimia 70 ya wagonjwa ni wahudumu wa afya kutoka vituo viwili vya afya kwenye mji mkuu Kigali.Na baada ya jeshi la Israeli hapo jana kujulisha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Mpito nchini Lebanon, UNIFIL juu ya nia yake ya kuanza mashambulizi ya ardhini dhidi ya wapiganaji wa Hezbollah nchini humo, hii leo ujumbe huo umesema licha ya hatari inayoendelea ya mashambulizi, walinda amani wamejipanga. UNIFIL imesema mara kwa mara wanabadili mwenendo na operesheni zao na tayari wana mipango ya kutekeleza iwapo itahitajika kufanya hivyo. IDF na Hezbollah wamekuwa wanashambuliana kusini mwa Lebanon.Mashinani leo ikiwa ni siku ya Kimataifa ya Wazee Duniani tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kusikia ujumbe kutoka kwa mmoja ya wazee, ana maoni gani?Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
1-10-2024 • 11 minuten
UNESCO na wadau wanajitahidi kuboresha elimu licha ya mashambulizi dhidi ya elimu katika migogoro.
Kama unavyojua, migogoro ya vita, majanga ya tabia nchi, dharura za afya ya umma, na mishtuko ya kiuchumi inaongezeka duniani kote kwa kasi, ugumu, na ukubwa. Mara nyingi dharura hizi hutokea kwa wakati mmoja, kwa mfano, wakati vita vinapoanza katika maeneo ambayo tayari yameathiriwa na majanga ya mabadiliko ya tabianchi. Hali hii inasababisha migogoro tata, iliyo changamana na ya muda mrefu, na athari zake kwenye elimu ni za kutisha. Nafikiri utakubaliana nami kuwa elimu ni mkombozi wa maisha na muhimu kwa kuendeleza maisha wakati wa dharura. Je UNESCO inatatua vipi changamoto hii? Cecili kariuki amezungumza na wataalamu wa elimu nchini Paris, Ufaranza.
30-9-2024 • 4 minuten, 27 seconden
Keita: Dhahabu na Koltani vyazidi kushamirisha mapigano Mashariki mwa DRC
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wameelezwa jinsi ushindani wa uchimbaji kupita kiasi na biashara ya maliasili huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC unavyozidi kuchochea mapigano kwenye eneo hilo, madini kama vile dhahabu na Koltani. Hayo yamo kwenye ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyowasilishwa mbele ya Baraza la Usalama na Mwakilishi wake Maalum nchini DR Congo, Bintou Keita, ikianzia tarehe 20 Juni hadi 19 mwezi huu wa Septemba.Bi. Keita amesema “jimboni Ituri, mapigano yaliyoshamiri hivi karibuni yamechochewa na vikundi vilivyojihami vikijaribu kudhibiti machimbo ya madini. Kwa kuwa faida imeongezeka kwa kupanua machimbo ya dhahabu, vikundi vilivyojihami vimegeuka kuwa wajasiriamali wa madini. Vikundi ya kijamii na jeshi la serikali lisilo na uwezo kifedha wakihaha kudhibiti makundi ambayo yameimarika kijeshi na kifedha.”Mwakikilishi huyo ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe waUmoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MMONUSCO, amesema jimboni Kivu Kaskazini, M23 inazidi kuimarisha udhibiti wake wa maeneo ya Masisi na Rutshuru jimboni Kivu Kaskazini, na hivyo wameweza kudhibiti kabisa uzalishaji wa madini ya Koltani.Ameongeza kuwa “biashara kutoka eneo la Rubaya linalokadiriwa kuchangia zaidi ya asilimia 15 ya uzalishaji wa madini ya Tantalum, imepatia M23 dola 300,000 kila mwezi. Hii inatia hofu na lazima ikomeshwe,.”Wajumbe pia walipata ripoti kutoka kwa Thérèse Nzale-Kove, mwanaharakati wa haki za wanawake kutoka Mfuko kwa Ajili ya Wanawake wa DRC au FFC.Bi. Nzale-Kove amesema kuondoka kwa MONUSCO jambo ambalo limesharidhiwa lazima kuzingatie changamoto za mifumo ya ulinzi wa haki za binadamu na ukosefu wa haki za kijamii na madhara yake.Ametaka kuzingatiwa kwa tathmini za kile walichojifunza baada ya MONUSCO kuondoka majimbo ya Tanganyika na Kivu Kusini.Kwa sasa MONUSCO imesalia jimbo la Kivu Kaskazini na inatakiwa iwe imeondoka kabisa DRC ifikapo mwisho wa mwaka huu.
30-9-2024 • 1 minuut, 36 seconden
30 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia amani na usalama nchini DRC, na suala la elimu katika malengo ya maendeleo endelevu tukimulika wanafunzi Kilifi nchini Kenya. Makala tunasalia na mada hiyo hiyo ya elimu na mashiani inamulika sheria za kibnadamu.Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo wameelezwa jinsi ushindani wa uchimbaji kupita kiasi na biashara ya maliasili huko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC unavyozidi kuchochea mapigano kwenye eneo hilo, madini kama vile dhahabu na Koltani.Maelfu ya watoto katika Kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya kwa miaka mitatu iliyopita wamelazimika kuacha shule kutokana na umasikini na ukame na mafuriko yaliyochangiwa na mabadiliko ya tabianchi. Lakini sasa wizara ya elimu ya Kenya kwa kushirikiana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wakfu wa Education Above all na wadau wengine juhudi zinafanyika kuwarejesha watoto shuleni.Makala leo inatupeleka Paris Ufaransa katika makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO kuzungmzia juhudi za shirika hili katika kuhakikisha kwamba wanafunzi walio katika maeneo ya migogoro wanaendelea na masomo yao na wenzao waliohamishwa wanapata ufikiaji wa elimu juu katika nchi zilizowapokea.Katika mashinani fursa ni yake Mirjana Spoljaric Egger, Rais wa Kamati ya Kimataifa ya chama cha Msalaba Mwekundu ICRC akitoa wito wa kutafakari machungu yanayowakumba waathirika wa mizozo wakati wa mazungumzo yake na waandishi wa habari kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
30-9-2024 • 12 minuten, 16 seconden
David Tumaini - Umasikini uliniachisha shule lakini asante mradi wa UNICEF sasa naendelea na ndoto yangu
Maelfu ya watoto katika Kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya kwa miaka mitatu iliyopita wamelazimika kuacha shule kutokana na umasikini na ukame na mafuriko yaliyochangiwa na mabadiliko ya tabianchi. Lakini sasa wizara ya elimu ya Kenya kwa kushirikiana na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, wakfu wa Education Above all na wadau wengine juhudi zinafanyika kuwarejesha watoto shuleni. “Niliacha shule darasa la nne ilikuwa mwaka 2022, kwasababu shuleni walikuwa wananirejesha nyumbani nikalete ada. Sasa nikifika nyumbani wazazi wanasema hawana”Huyo ni David Tumaini kijana mwenye umri wa miaka hivi sasa 16 mmoja wa wanafunzi waliolazimiika kukatiza masomo miaka miwili iliyopita katika shule ya msingi ya Soyosoyo kutokana na umasikini. Kwa miezi kadhaa alihaha kusaka njia ya kuendelea na masomo."Nilikaa nyumbani kwa muda wa miezi mitano, wakati wenzangu wanakwenda shule na ni siku za masomo na wewe uko nyumbani. Hii inakufanya ujihisi kama wewe si mtu muhimu.”Hisia kama hizo na mustakbali wa watoto hao ndio kilicholisukuma shirika la UNICEF kuanzisha mradi wa “Elimisha mtoto” likishirikisha wizara ya elimu ya kenya na wadau wengine ili kuhakikisha watoto kama David wanarejea shuleni. Elizabeth Waitha ni afisa elimu wa UNICEF.“Tuliweza kubaini Kaunti 16 ambazo zilikuwa na watoto zaidi ya 10,000 ambao wanaendi shuleni, na hii ilikuwa ni kwa shule za msingi tu. Na tukaangalia ni jinsi gani ya kuhakikisha mazingira bora ya kusoma kwa watoto waliosajiliwa kwenye mradi. Na tumeweza kuwasaidia zaidi ya wanafunzi milioni kwa vifaa vya shule na pia kwa waalimu vifaa vya kuandikia kama chaki, kalamu na vingine.”Na ndipo David akasikia kuhusu mradi huo,“Nilipata taarifa kutoka kwa walimu ya kwamba kuna mradi ambao unawasaidia watoto walioacha shule ili warehjee shuleni kuendelea na masomo. Sasa nilipokuja shuleni nikaambiwa wewe tutakusajili katika huu mradi wa msaada , ndipo nikaweza kurejea masomoni, hadi sasa nipo shuleni kwa sababu ya msaada huu. Vitu ambavyo nilipewa ni pamoja na mkoba wa madaftari, vitabu, kalamu na vifutio.”Hii imemrejeshea David matumaini ya ndoto yake“Mimi nikimaliza kusoma nataka kuwa Daktari ili kusaidia wagonjwa. Na katika kusaidia wagonjwa mshahara nitakaolipwa ntajisaidia mwenyewe na pia kusaidia familia yangu”Kupitia mradi huu mbali ya vifaa umewezesha zaidi ya watoto 256,000 kurejea shuleni na bado wanaendelea na masomo.
30-9-2024 • 2 minuten, 34 seconden
27 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea kipindi maalum. Leo mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa umeingia siku ya nne, miongoni mwa wahutubiaji ni Tanzania. Kabla ya kupanda katika mimbari ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili alipata fursa ya kuketi na mwakilishi wa taifa hilo katika mjadala huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kuzungumza naye masuala kadhaa ikiwemo mzigo wa madeni kwa nchi zinazoendelea na pia nafasi ya wanawake katika nyanja ya kimataifa. Lakini kwanza alitaka kufahamu Waziri Mkuu Majaliwa amekuja na ujumbe gani kutoka Tanzania kwenye mjadala huu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu nchini Lebanon, Imran Riza, akizungumza kutoka mji mkuu wa Lebanon, Beirut, kwa njia ya video amewaeleza waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi leo kwamba katika Lebanon kipaumbele kwa sasa ni kuhakikisha usitishaji mapigano wa haraka ili kukomesha mateso zaidi ya raia na uharibifu. Bwana Riza amesisitiza tena wito kwa jamii ya wahudumu wa kibinadamu kwa nchi zote kutumia ushawishi wao kusaidia katika kupunguza machafuko kwa dharura.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women inaangazia athari kubwa za janga la kibinadamu linaloongezeka kwa wanawake na wasichana wa Sudan, wakiwemo milioni 5.8 ambao ni wakimbizi wa ndani.Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi imetoa wito kwa mamlaka ya Haiti na jumuiya ya kimataifa kufanya zaidi kulinda watu na kuzuia mateso zaidi na kwamba hicho ndicho kinapaswa kuwa kipaumbele. Takwimu za hivi karibuni kutoka Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa takribani watu 3,661 wameuawa nchini Haiti tangu Januari mwaka huu.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
27-9-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Je wewe ni mmoja wa waathirika wa usugu wa viuavijiumbe maradhi, au Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa, UVIDA?
Leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kando ya mjadala mkuu wa UNGA79, viongozi wanakutana kwenye Mkutano wa Ngazi ya Juu ukimulika usugu wa viuavijiumbe maradhi, Antimicrobial Resistance, kwa kiswahili ikiitwa pia UVIDA, au Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa. Katika taarifa ya Pamoja iluyotolewa kwenye mkutno huo na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO, la mazingira UNEP, la chakula na kilimo FAO na shirika la afya ya Wanyama duniani WOAH, usugu wa viua vijiumbe maradhi unahusika moja kwa moja na vifo milioni 1.3 na kuchangia vingine milioni 5 kila mwaka.Unaweza kujiuliza ni nini na kwa nini ni muhimu wakutane? Bosco Cosmas, wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Profesa Mshiriki wa Vimelea Vya Magonjwa katika Chuo Kikuu cha Sayans iza Afya Bugando, mkoani Mwanza, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.
26-9-2024 • 6 minuten, 16 seconden
26 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika hospitali ya kanda Bugando, mkoani Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania kumulika chanzo na madhara ya usugu wa vimelea dhidi ya dawa au UVIDA. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na katika kujifunza Kiswahili tunabisha hodi nchini Zimbabwe, kulikoni?Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa leo kandoni mwa mjadala mkuu ulioingia siku ya tatu moja ya mada zinazopewa uzito ni usugu wa vijiuavijiumbe maradhi au Anti-Microbial Resistance (AMR). Katika taarifa ya Pamoja iluyotolewa kwenye mkutno huo na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO, la mazingira UNEP, la chakula na kilimo FAO na shirika la afya ya Wanyama duniani WOAH, usugu wa viua vijiumbe maradhi unahusika moja kwa moja na vifo milioni 1.3 na kuchangia vingine milioni 5 kila mwaka.Pia katika katika Mjadala Mkuu wa baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA79 miongoni mwa waliopanda katika mimbari leo kuhutubia ni Rais wa Jamhuri ya Kenya William Samoei Ruto ambaye amesema “Dunia iko katika wakati wa changamoto kubwa za kiusalama, ahati ya chata ya Umoja wa Mataifa kuokoa viizazi kutokana na vita iiko katika hatihati.” Aesema nadhariaya wao dhidi yetu ni chachu ya changamoto kubwa ikiwemo vita. Kuanzia Gaza, Darfur, Ukraine, Yemen, Mashariki mwa DRC , Sudan, Sahel na uhalifunchini Haiti,migogoro inasambaratisha maisha na uwezi wa watukuishi katika kiwangocha kihistoria.”Naye Rais wa Malawi Lazarus McCarthy Chakwera, amesema kila nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa inahusiana na nchi nyingine katika mambo matatu, ushirikiano migogoro na ushindani ulio na usawa, hivyo jinsi ya kushughulikia masuala hayo ndio itaamua mustakbali wa vizazi vvya kesho hasa ushirikiano unaofaidisha wote, ushindani ulio na usawa na utatuzi wa migogoro. Amesisitiza kuwa ushirikiano ni kitu cha muhimu sana na mfano mzuri ni nchi yake Malawi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili fursa ni yake Mary Chigumira kutoka Zimbabwe, mmoja wa waafrika aliyefika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa Jijini New York kwa ajili ya Mkutano wa Zama Zijazo uliokamilika hivi majuzi akieleza anavyotamani kujifunza zaidi lugha ya Kiswahili.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
26-9-2024 • 11 minuten, 32 seconden
Haya ndiyo tuliyowaeleza viongozi wa ulimwengu - Ibanomonde Ngema na Jerop Limo
Katika makala ya leo, Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na vijana wawili waliozaliwa tayari wakiwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na hivyo wameamua kujitolea kusukuma mapambano dhidi ya ugojwa huo hatari duniani. Katika mikutano inayoendelea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati huu wa Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA79 wasichana hawa wadogo wamepata fursa ya kushiriki katika mkutano wa ngazi ya juu uliondaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi UNAIDS.
25-9-2024 • 3 minuten, 35 seconden
Viongozi wajadili ongezeko la kina cha baharí; UNEP Tanzania yaonesha njia
Viongozi wa dunia wakiendelea kuhutubia kwenye Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa New York, Marekani, kandoni kunafanyika Mkutano wa Ngazi ya Juu ukimulika madhara ya ongezeko la kina baharí kutokana na kina cha baharí. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia viongozi wa dunia amewataka wachukue hatua za kijasiri kunusuru maisha na mbinu za kujipatia vipato kwa watu zaidi ya milioni 900 wanaoishi uwanda wa chini wa pwani ulio hatarini kuzama kutokana na kina cha baharí kuongezeka.Kwa Tanzania Umoja wa Mataifa umeanza kuchukua hatua kama unavyosikia kutoka kwa Clara Makenya, Mwakilishi wa shirika la UN la Mataifa la Mazingira, UNEP nchini humo huku tukipata ufafanuzi wa madhara ya ongezeko la kina cha baharí kwenye eneo lao kutoka kwa Segule Segule, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Maji Pangani
25-9-2024 • 1 minuut, 53 seconden
25 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa wanaharakati wa malengo ya maendeleo endelevu ambao wamekuja hapa makao makuu ya umoja wa mataifa kuwa sehemu ya utatuzi katika mijadala mikuu ya UNGA79. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakwenda DRC.Viongozi wa dunia wakiendelea kuhutubia kwenye Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hapa New York, Marekani, kandoni kunafanyika Mkutano wa Ngazi ya Juu ukimulika madhara ya ongezeko la kina baharí kutokana na kina cha baharí.Mjadala mkuu wa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 79 umeingia siku ya pili hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa nasi tunaendelea kuzungumza na washhiriki mbalimbali wakiwemo kutoka asasi za kiraia kusikia maoni yao kuhusu mkutano huu. Flora Nducha amebahatika kuongea na mmoja wao kutoka nchini Zimbabwe.Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na vijana wawili waliozaliwa tayari wakiwa na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi na hivyo wameamua kujitolea kusukuma mapambano dhidi ya ugojwa huo hatari duniani. Katika mikutano inayoendelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa wakati huu wa UNGA79 wasichana hawa wadogo wamepata fursa ya kushiriki katika mkutano wa ngazi ya juu uliondaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi UNAIDS.Na mashinani fursa ni yake mwananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC jimboni Kivu Kaskazini akiwasilisha ujumbe wake kwa viongozi wanaoshiriki mjadala Mkuu wa mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataiafa, UNGA79 hapa New York, Marekani.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
25-9-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Mwanaharakati Mary: Viongozi wa dunia wasiwape kisogo wanawake na wasicha wa vijijini
Mjadala mkuu wa wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 79 umeingia siku ya pili hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa nasi tunaendelea kuzungumza na washhiriki mbalimbali wakiwemo kutoka asasi za kiraia kusikia maoni yao kuhusu mkutano huu. Flora Nducha amebahatika kuongea na mmoja wao kutoka nchini Zimbabwe.Mary Chigumira ni mwanaharakati anayepiganiia haki za wanawake na wasichana nchini Zimbabwe kupitia shirikika lale la kiraia la “Unlimited hope alliance” au Muungano wa matumaini yasiokwisha ambao unawasaidia wasichana wenye changamto katika masuala ya elimu, huduma za maji , usafi na usafi wa mazingira au WASH na kuwawezesha kiuchumi.Amekuwa hapa Umoja wa Mataifa kuhuduria mkutano uliomalizika wiki hii wa Zama Zijazo na kabla hajarejea nyumbani ana ujumbe kwa viongozi wa dunia wanaokutana katika mjadala mkuu wa UNGA79 kuhusu mchango wao katika hataraki za kusaidia wanasichana na wanawake vijijini, nasema “Kwa viongozi tunawaomba wawe sehemu yetu, hatutaki kuwa katika safari hii pekeyetu, tunataka kuambatana nao. Endapo tutaambatana Pamoja nao tufafanikisha lengo letu.”Amesema hilo litawatia moyo hata wanawake na wasichana wanaopitia machungu na kukata tamaa, anawashauri akisema, “Kwa wanawake na wasichana ambao mnanisikiliza , asilani hamjachelewa, hata kama maisha yako yaliharibiwa, ulipata mtoto ukiwa na umri wa miaka 14, huo sio mwisho wa safari.”Akatoa mfano hai katika shirika lake, Mary anasema, “Tulikuwa na wasichana ambao walipata mimba wakiwa na umri wa miaka 14, lakini sasa wamerejea shuleni , hivyo hamjachelewa hata wale walio katika biashara ya ngono, mnaweza kubadili maisha yenu yaliyoharibika. Njooni kwetu mpate mafunzi ili muweze hata kuanzisha biashara zenu.”Mary anasema anaamini wakipigwa jeki basi shirika lao litaweza kusaidia wasichana wengi zaidi.
25-9-2024 • 1 minuut, 51 seconden
24 SEPTEMBA 2024
Jaridani tunakuletea mada kwa kina ikiwa hii leo Mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa mataifa UNGA79 umeng’oa nanga hii na tunakutana na mdau anayepigia chepuo malengo ya maendeleo endelevu hasa haki katika lengo namba 4 la Elimu Bora.Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA79 umeanza leo New York, Marekani ambapo Katibu Mkuu wa Antonio Guterres amesema anashawishika kwamba kuna kweli mbili chungu katika zahma zinazokumba dunia hivi sasa: Mosi-Hali ya dunia si endelevu na hatuwezi kuendelea kama ilivyo na pili; changamoto zilizozoko zinatatulika. Kinachohitajika ni kuweko kwa mfumo wa kimataifa wenye uwezo wa kutatua changamoto hizo.Rais Joe Biden wa Marekani ambaye amesema ni hotuba yake ya mwisho mbele ya Baraza hilo kama Rais wa Marekani na kwamba anatambua changamoto zinazokabili dunia ikiwemo vita, tabianchi na demokrasia. Lakini ana matumaini kuna suluhu kwa kuzingatia yote waliyofanya pamoja kwa miongo iliyopita.Huko Lebanon shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR linaomboleza vifo vya watumishi wake wawili waliouawa huko Bekaa Mashariki baada ya kombora lililorushwa na Israeli kuangukia makazi yao jana Septemba 23. UNHCR imerejelea wito wa Katibu Mkuu wa UN ya kwamba mashambulizi yakome.Na katika mashinani tunamsikia kijana mmoja aliyefika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria mkutano wa Zama Zijazo uliofunga pazia lake jana, ana wito wa kuwapa viongozi wa ulimwengu ambao wanashiriki katika Mjadala Mkuu wa Baraza la Umoja wa Mataifa ambao wenyewe umefungua pazialake leo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
24-9-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Vijana - Tumechoka na maneno ya viongozi sasa tunataka vitendo
Jana Jumapili ya Septemba 22 viongozi wa dunia walipitisha Mkataba wa Zama Zijazo. Mkataba huu unalenga kukabili changamoto za karne ya 21 kuanzia mizozo, mabadiliko ya tabianchi, haki za binadamu, hadi taarifa potofu na za uongo. Maeneo Matano makuu ni pamoja na maendeleo endelevu, amani na usalama duniani, sayansi na teknolojia, vijana na vizazi vijavyo na marekebisho ya usimamizi wa dunia, kipengele muhimu wakati huu ambapo taasisi za fedha za kimataifa na Umoja wa Mataifa wenyewe wameshindwa kuja na majawabu ya karne ya 21. Mkataba wa Kimataifa wa Kidijitali unaoelenga pamoja na mambo mengine usimamizi bora wa Akili Mnemba, pamoja na Azimio kwa ajili ya Vizazi Vijavyo linalotaka serikali za sasa kutilia maanani vizazi vijavyo zinapopitisha maamuzi yao ya leo, ni sehemu ya viambatanishi vya Mkataba huu wa Zama Zijazo. Assumpta Massoi ametaka kufahamu maoni ya vijana baada ya hatua hii, na ndio mada yetu kwa kina siku ya leo.
24-9-2024 • 7 minuten, 27 seconden
23 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kama nilivyokujulisha leo ambayo ni kipindi maalum kinachojumuisha hotuba za viongozi wa dunia na watetezi wa haki za binadamu ikiwa ni jana Jumapili Septemba 22 viongozi hao walipitisha Mkataba wa Zama Zijazo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Mkutano wa Zama Zijazo uliofanyika kwa siku nne tangu majuzi tarehe 20 ukianza na siku mbili za vijana kukutana na baadaye viongozi wakuu wa ulimwengu, unakunja jamvi hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kesho Septemba 24 unaanza Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukitajwa kuwa mkusanyiko mkubwa zaidi wa kidplomasia ulimwenguni unaofanyika kila mwaka. Kwa siku sita viongozi wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa watahutubia ulimwengu.Leo Jumatatu hali ya mvutano imezidi kutanda Mashariki ya Kati huku ripoti za mamia ya mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel dhidi ya Hezbollah yakilenga kusini mwa Lebanon na Gaza ikiwa ni pamoja na kambi ya wakimbizi, wameeleza wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa. Hatua hiyo inakuja wakati afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon Jeanine Hennis-Plasschaert aakianza ziara rasmi nchini Israel kukutana na maafisa wakuu wa serikali, baada ya kusisitiza kwamba "hakuna suluhu ya kijeshi ambayo itafanya pande zote mbili kuwa salama".Na Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Haki za Binadamu nchini Burundi Fortuné Gaetan Zongo, amehutubia mkutano wa 57 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi hii leo na kueleza kuwa hali ya kibinadamu katika taifa hilo la Maziwa Makuu bado inatia wasiwasi akitolea mfano tukio la mashinikizo kwa wapenzi waliokuwa wanaishi pamoja huko Ngozi, Kayanza na Kirundo mwezi Machi na Aprili mwaka huu.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
23-9-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Mataifa yahakikishe ulimwengu unakuwa mahali bora kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi - Jerop
Leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani vijana kutoka kila kona ya dunia wanakutana kuanza kujadili kuhusu mstakabali wao katika zama zijazo. Miongoni mwao ni Jerop Limo kutoka Kenya anayetumia uzoefu wake wa kuishi na Virusi Vya Ukimwi kwa miaka 24 ya umri wake kuhakikisha ulimwengu unakuwa mahali bora kwa watu ambao tayari wanaishi na virusi hivyo. Anold Kayanda amezungumza naye na hapa Jerop Limo anaanza kwa kueleza yale ambayo atawaeleza viongozi wa ulimwengu.
20-9-2024 • 2 minuten, 15 seconden
Viongozi wa kimataifa washikamane kuhakikisha ulimwengu wenye usawa wa kijinsia - Dorice Mkiva
Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ambako mkutano wa Zama Zijazo umen’goa nanga leo kwa siku mbili za kuchua hatua kabla ya kikao cha ngazi ya juu siku ya Jumapili na Jumatatu. Leo Vijana wanapata fursa ya kupaza sauti zao kuhusu dunia na mustakbali wautakao. Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na kijana mwenye ulemavu kutoka Tanzania ambaye ni mmoja wa wazungumzaji wa mkutao wa leo. Anaanza kwa kujitambulisha.
20-9-2024 • 3 minuten
20 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia uondoaji wa taka katika ukanda wa Gaza, na ujumbe wa vijana ambao watashiriki mijadala mikuu hapa makaomakuu ya Umoja wa Mataifa. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini, kulikoni?Hali inazidi kuwa si hali huko Ukanda wa Gaza kwani sasa raia wanakwepa sio tu mashambulizi na magonjwa bali pia nyoka, panya na wadudu ambao wanasambaa kutokana na mazingira machafu. Watu wanajihifadhi kwenye maeneo ya wazi bila mifumo ya majitaka au ya kuondoa maji ya mvua. Timu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina imefika kupuliza dawa ili kulinda wananchi hao.Leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani vijana kutoka kila kona ya dunia wanakutana kuanza kujadili kuhusu mstakabali wao katika zama zijazo. Miongoni mwao ni Jerop Limo kutoka Kenya anayetumia uzoefu wake wa kuishi na Virusi Vya Ukimwi kwa miaka 24 ya umri wake kuhakikisha ulimwengu unakuwa mahali bora kwa watu ambao tayari wanaishi na virusi hivyo.Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ambako mkutano wa Zama Zijazo umen’goa nanga leo kwa siku mbili za kuchua hatua kabla ya kikao cha ngazi ya juu siku ya Jumapili na Jumatatu. Leo Vijana wanapata fursa ya kupaza sauti zao kuhusu dunia na mustakbali wautakao.Na katika mashinani Balozi Mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Tendai Mtawarira, mwanamichezo nguli mstaafu wa mpira wa raga mzaliwa wa Zimbabwe lakini alichezea Afrika Kusini, akizungumzia alichokishuhudia katika safari yake ya kwanza nchini Sudan Kusini.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
20-9-2024 • 9 minuten, 58 seconden
UNRWA: Nyoka, panya na wadudu vyatishia wakazi wa Gaza
Hali inazidi kuwa si hali huko Ukanda wa Gaza kwani sasa raia wanakwepa sio tu mashambulizi na magonjwa bali pia nyoka, panya na wadudu ambao wanasambaa kutokana na mazingira machafu. Watu wanajihifadhi kwenye maeneo ya wazi bila mifumo ya majitaka au ya kuondoa maji ya mvua. Timu ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina imefika kupuliza dawa ili kulinda wananchi hao. Tuko Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza, video ya UNRWA inaonesha wafanyakazi wa shirika hilo wamefika kwenye makazi ya muda ya wakimbizi wa ndani. Katika eneo hili majitaka yamezingira makazi ya wakimbizi kwani hakuna mifumo ya kuyaondoa.Kando kidogo, mama anaonekana akimsafisha mwanae kwa kutumia maji yaliyohifadhiwa kwenye dumu.Mama huyu ambaye jina lake halikupatikana anasema, nilifurushwa kutoka jiji la Gaza hadi hapa Khan Younis. Tumefika kwenye eneo lililokuwa wazi, kwa hiyo uwepo wa panya na wadudu unahatarisha maisha ya watoto wangu. Nina hofu kubwa ya afya ya watoto wangu kutokana na wadudu na panya.Sasa anaonekana afisa mmoja wa UNRWA akiwa na wenzake wakipita hema kwa hema wakigawa dawa za kuua wadudu hao.Afisa huyu anasema wamewapatia ushauri na mwongozo wa jinsi ya kutumia dawa hizo.Halikadhalika wamepuliza dawa za kuulia wadudu na pia kuondoa taka zilizokuweko karibu na makazi ya wakimbizi hao wa ndani.UNRWA inasema viwango vya juu vya joto, na uweko wa makazi hayo kwenye eneo la wazi ni mazingira rafiki kwa panya, nyoka na wadudu wengine.Kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, tangu vita ianze Gaza, tarehe 7 Oktoba mwaka 2023, zaidi ya watu milioni 1.9 wamefurushwa makwao.
20-9-2024 • 1 minuut, 46 seconden
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa methali “Mke ni nguomgomba ni kupalilia”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Mke ni nguomgomba ni kupalilia.”
19-9-2024 • 1 minuut, 12 seconden
19 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tuankuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Sudan Kusini kufuatilia changamoto za kibinadamu na jinsi ambavyo mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyozitatua. Pi atunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo na ufafanuzi wa methali.Licha ya kuongezeka kwa majanga duniani, kuanzia umaskini hadi dharura ya tabianchi, Umoja wa Mataifa umesalia na azma yake ya kusongesha amani, maendeleo endelevu na kupunguza machungu yanayowapata binadamu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres katika ripoti yake ya mwaka ya utendaji wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo jijini New York, Marekani kabla ya kuanza kwa Mjadala Mkuu wa mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA79.Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ukimwi, UNAIDS hii leo limetoa ripoti yake huko Geneva, Uswisi ikionesha kuwa mzigo wa madeni unaokabili nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara unasababisha zibakie na fedha kidogo kugharimia huduma za afya, pamoja na huduma muhimu zaidi dhidi ya Virusi vya Ukimwi, VVU. Idadi kubwa ya watu wanaoishi na VVU duniani wako eneo hilo lakini mzigo wa madeni unarudisha nyuma maendeleo yaliyopatikana ya kutokomeza Ukimwi ifikapo 2030.Tukisalia na suala hilo hilo la UKIMWI, UNAIDS inasema vijana wawili wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na pia wana ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, Ibanomonde Ngema kutoka Afrika Kusini, na Jerop Limo kutoka Kenya, wako njiani kuja New York, Marekani kushiriki UNGA79 na Mkutano wa Zama Zijazo kwa lengo la kusihi viongozi wa dunia kushirikiana na vijana katika kutokomeza Ukimwi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Mke ni nguomgomba ni kupalilia.”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
19-9-2024 • 10 minuten, 55 seconden
Pamoja na kuahirisha uchaguzi tunachoimbea Sudan Kusini ni amani: FAO Meshack Malo
Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini Sudan Kusini limesema licha ya uchaguzi mkuu kuahirishwa nchini humo hadi 22 Desemba 2026 kitu kikubwa kwa taifa hilo changa zaidi barani Afrika ni amani. Akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili katika Makala hii Meshack Malo mwakilishi wa FAO Sudan Kusini amesema kuahirisha uchaguzi huo ambao awali ilikuwa ufanyike 22 Desemba mwaka huu 2024 ni uwamuzi wa Wasudan na wana sababu za msingi, hivyo jumuiya ya kimataifa itaendelea kushirikiana nao na kuliombea amani taifa hilo.
18-9-2024 • 3 minuten, 4 seconden
Mfuko wa Kimataifa yatoa karibia dola milioni 10 kukabiliana na mpox DRC
Kutokana na ombi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (the Global Fund) leo umetangaza kuchangia dola za Marekani milioni 9.5 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa mpox katika majimbo sita kati ya yale yenye viwango vya juu zaidi vya maambukizi nchini humo. Tangazo hilo lililotolewa leo Septemba 18 katika makao makuu ya Mfuko huo wa kimataifa unaofahamika kama The Global Fund, mjini Geneva, Uswisi imeeleza kuwa fedha hizo zinaelekezwa katika katika jimbo la Equateur, Ubangi Kusini, Sankuru, Tshopo, Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Kinshasa, jimbo lenye msongamano mkubwa wa watu milioni 17.
18-9-2024 • 1 minuut, 49 seconden
18 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia juhudi za Umoja wa Mataifa za kukabiliana na ugonjwa wa MPOX barani Afrika. Makala inatupeleka nchini Sudan Kusini kuangazia uhairishwaji wa uchaguzi na mashinani nchini Sudan ambapo vilabu vinatumiwa kuimarisha ulinzi wa wasichana.Kutokana na ombi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (the Global Fund) leo umetangaza kuchangia dola za Marekani milioni 9.5 kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa mpox katika majimbo sita kati ya yale yenye viwango vya juu zaidi vya maambukizi nchini humo.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Burundi linasema asilimia 33 ya wagonjwa wa homa ya nyani au mpox nchini humo ni watoto wa kwenda shule wenye umri wa kuanzia miaka 5 hadi 19, na hivyo kuwa changamoto mpya wakati familia zinajiandaa kwa mwaka mpya wa masomo.Makala leo inatupeleka Sudan Kusini ambako mwishoni mwa wiki serikali ilitangaza kuahirisha uchaguzi mkuu ambao ulikuwa ufanyike 22 Desemba mwaka huu 2024.Mashinani tuko katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam nchini Sudan ambako shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi (UNFPA) linatumia vilabu kufanikisha ulinzi wa wasichana walio hatarini. Sasa Ikhlas Mousa Andulkareem ambaye ni mfanyakazi wa kijamii katika shirika lisilo la kiserikali la Nada ALAzhar, linalopata usaidizi kutoka UNFPA anatueleza jinsi eneo salama kwa wanawake na wasichana litawanufaisha waathiriwa kwenye kambi hii ya Zamzam.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
18-9-2024 • 9 minuten, 58 seconden
UNICEF Burundi: Asilimia 33 ya wagonjwa wa mpox wana umri wa kati ya miaka 5-19
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Burundi linasema asilimia 33 ya wagonjwa wa homa ya nyani au mpox nchini humo ni watoto wa kwenda shule wenye umri wa kuanzia miaka 5 hadi 19, na hivyo kuwa changamoto mpya wakati familia zinajiandaa kwa mwaka mpya wa masomo.Mwakilishi wa UNICEF nchini Burundi France Bégin amesema ongezeko la maambulizi ya mpox miongoni mwa watoto nchini Burundi wakiwemo wenye umri wa chini ya miaka mitano linatia wasiwasi mkubwa na kuwalinda ndio kipaumbele chetu.“Halikadhalika, kuhakikisha watoto wote wanaweza kurejea shule salama licha ya mlipuko huu ni jambo muhimu. Timu yetu inashirikiana na Wizara ya Elimu kutekeleza mikakati ya afya shuleni, kulinda wanafunzi na kuepusha kuvurugwa zaidi kwa fursa za wanafunzi kusoma,” amesema Bi. Bégin .Tangu kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza wa mpox nchini Burundi tarehe 25 mwezi Julai mwaka huu, taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika limethibitisha kuweko kwa wagonjwa 564 , ambapo asilimia 62.9 wana umri wa chini ya miaka 19. Halikadhalika kuna washukiwa 1,576 wa ugonjwa huo ambao tayari shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limeidhinisha chanjo yake.UNICEF inasema kumekuwa na matukio 1,774 ya maonyo ya uwepo wa ugonjwa huo katika wilaya zote 34 za wilaya kiafya za Burundi kati ya 49 nchini kote, ambako wilaya 3 katika mji mkuu Bujumbura ndio kitovu cha mlipuko.Watoto na jamii zilizoko hatarini zaidi wamekuwa waathiriwa zaidi wa mpox katika nchi za kusini na mashariki mwa Afrika.Zaidi ya watoto milioni 3 nchini Burundi wakitarajiwa kurejea shuleni katika mwaka mpya ulioanza tarehe 16 mwezi huu wa Septemba, UNICEF na serikali wanaongeza jitihada ili waweze kurejea salama shuleni.Mathalani UNICEF inasaidia harakati za kubaini wagonjwa, kupatia mafunzo wahudumu wa afya, kuelimisha jamii na kupatia majawabu hofu zao, kuimarisha huduma za kujifasi na kusambaza vifaa muhimu.Ili kufanikisha hilo, UNICEF inatoa wito wa ombi la dola milioni 58.8 kukabili janga la mpox barani Afrika ikiwemo Burundi ambako watoto ndio wameathirika zaidi.UNICEF pia inasaidia kukabiliana na unyanyapaa kwa waliopona na kusaidia familia kwenye vituo walikotengwa kupata huduma.
18-9-2024 • 1 minuut, 53 seconden
17 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Nairobi Kenya ambako tutamsikiamwanamuziki nyota, mjasiriamali na mwanaharakati wa haki za wanawake Lizi Ogumbo. Pia tunakuletea habari kwa ufufpi na mashinani.Vurugu dhidi ya wapinzani wa serikali nchini Venezuela zimefurutu ada, imesema tume huru ya uchunguzi ikitaja kukamatwa, ukatili wa kingono na utesaji kama mbinu zitumiwazo na serikali ya Rais Nicolas Maduro ili aendelee kuweko madarani.Mwaka 2024 ukiripotiwa kuwa na idadi kubwa ya chaguzi kwenye nchi zaidi ya 60 ambako zaidi ya watu bilioni 1 watapiga kura kuchagua viongozi wao wa umma, wataalamu wa Umoja wa Mataia wanaelezea hofu yao juu ya kitendo cha watu kutoweshwa katika kipindi hicho ili kunyamazisha demokrasia, kitendo ambacho wamesema kinabinya uhuru wa kupiga kura.Na hii leo matokeo ya utafiti uliofanywa na Umoja wa Mataifa yameonesha kuwa licha ya majanga yanayoendelea kukumba dunia, nchi wanachama zimeendelea kujizatiti kuanzisha huduma za serikali mtandao ili wananchi waweze kupata huduma mbali mbali kidijitali, ambapo ripoti inazitaja Denmark, Estonia na Singapore kushika nafasi ya juu kati ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa, kwa mawanda na ubora wa huduma za serikali mtandaoni.Katika mashinani Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP nchini Bangladesh Stefan Liller anatueleza kiwango cha athari za mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
17-9-2024 • 9 minuten, 54 seconden
WFP Bigenimana: Nilichokishuhudia Maiduguri Nigeria ni zahma kubwa
Wahudumu wa kibinadamu wanahaha hivi sasa kufikisha msaada Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kwenye jimbo wa Borno mjini Maiduguri ambako maelfu ya watu wametawanywa baada ya bwawa la Alau kufurika na kupasua kingo zake usiku wa manane wiki iliyopita kutokana na mvua kubwa. Shirika la Umoja wa Matifa la mpango wa chakula duniani WFP ni mdau mkubwa katika kufikisha misaada hiyo na mkuu wa ofisi yake ya Maiduguri Emmanuel Bigenimana anaeleza alichokishuhudia katika Makala hii inayoletwa kwako na Flora Nducha.
16-9-2024 • 3 minuten, 4 seconden
Guterres: Katika Siku hii ya Ozoni, tujitolee kuweka amani kati yetu na sayari yetu
Pamoja na chapisho lililotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa (WMO) kuangazia ushahidi unaoongezeka kwamba tabaka la ozoni kwa hakika liko mbioni kurejea katika hali nzuri, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake maalumu kwa ajili ya siku ya leo ya Kimataifa ya Uhifadhi wa Tabaka la Ozoni amesisitiza mataifa yote ulimwenguni kuidhinisha na kutekeleza maazimio ya maboresho ya Itifaki ya Montreal yaliyozaa Marekebisho ya Kigali kwa lengo la kupunguza gesi chafuzi zenye nguvu zinazoongeza joto duniani. Katika ujumbe huo, Bwana Guterres ameeleza kwamba Marekebisho ya Kigali ya Itifaki ya Montreal ambayo yanalenga katika kupunguza hydrofluorocarbons (HFCs) ambazo ni gesi zinazoongeza joto duniani yanaweza kuchangia katika kuendeleza juhudi za kukabiliana na tabianchi, kulinda watu na sayari. “Na hilo linahitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwani rekodi za joto zinaendelea kuongezeka.” Akasisitiza.Itifaki ya Montreal ilikubaliwa mnamo mwaka 1987 huko nchini Canada na kuanza kutumika mwaka 1989. Maboresho yake yalifanyika mwaka 2016 mjini Kigali Rwanda na marekebisho hayo ya Kigali yakawa sehemu ya Itifaki ya Montreal kuanzia mwaka 2017. Hadi kufikia Aprili mwaka huu 2024 ni nchi 158 pekee zimeidhinisha marekebisho hayo.Guterres anaendelea kueleza kwamba, “iwapo yataidhinishwa kikamilifu na kutekelezwa, Marekebisho ya Kigali ya Itifaki ya Montreal yanaweza kusaidia kuepuka ongezeko la hadi nyuzi joto 0.5 za Selsiasi duniani kufikia mwisho wa karne hii.”Anasema “wakati ambapo ushirikiano kimataifa uko chini ya shinikizo kubwa, Itifaki ya Montreal ya kusaidia kulinda tabaka la ozoni inajitokeza kama ishara yenye nguvu ya matumaini. Ni ukumbusho kwamba nchi zinapoonesha azimio la kisiasa kwa manufaa ya wote, mabadiliko yanawezekana.”Ushahidi wa mafaniko ya Itifaki ya Montreal pia uko katika ujumbe wa Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Inger Andersen alioutoa leo kwa njia ya video akisema,“hatua zilizochukuliwa chini ya Itifaki hii ya Montreal ziliondoa gesi zilizokuwa zinatumika viwandani, gesi ambazo zilikuwa zilizoharibu tabaka la ozoni na ziliongeza joto duniani.”
16-9-2024 • 1 minuut, 57 seconden
16 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN wa Tabaka la Ozoni, na mssada wa kibinadamu kwa wenyeji wa kisiwa kidogo cha Carriacou, Grenada waliokumbwa na kimbunga Beryl. Makal tunakupeleka nchini Nigeria na mashinani nchini Sudan.Pamoja na chapisho lililotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa (WMO) kuangazia ushahidi unaoongezeka kwamba tabaka la ozoni kwa hakika liko mbioni kurejea katika hali nzuri, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake maalumu kwa ajili ya siku ya leo ya Kimataifa ya Uhifadhi wa Tabaka la Ozoni amesisitiza mataifa yote ulimwenguni kuidhinisha na kutekeleza maazimio ya maboresho ya Itifaki ya Montreal yaliyozaa Marekebisho ya Kigali kwa lengo la kupunguza gesi chafuzi zenye nguvu zinazoongeza joto duniani.Kimbunga Beryl, kilichopiga tarehe 1 Julai 2024, kimewaacha wakazi wa kisiwa kidogo cha Carriacou, Grenada, na athari kubwa . Kufuatia changamoto zinazowakabili wasamaria kutoka maeneo mbalimbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) wamewasaidia kurejesha matumaini kama anavyosimulia Anthony St. Hilaire manusura wa kimbunga hicho.Makala inatupeleka Maiduguri Nigeria ambako mafuriko yanayoshuhudiwa baada ya bwawa la Alau kupasua kingo zake kutokana na mvua kubwa hayajawahi kuonekana katika miaka ya karibuni. Shirika la Umoja wa Matifa la mpango wa chakula duniani WFP ni mdau Mkubwa katika kufikisha misaada kwa waathirika na mkuu wa ofisi yake ya Maiduguri Emmanuel Bigenimana anaeleza alichokishuhudia.Na katika mashinani Aziza, mama wa watoto wanne kutoka Sudan ambaye alikuwa mhudumu wa kibinadamu na sasa amejikuta mkimbizi nchini Uganda baada ya kukimbia nyumbani kwao Sudan kufuatia mapigano yaliyoanza Aprili 2023. Nyumba yao iliporwa kila kitu na sasa akiwa ukimbizi anasimulia maisha yalivyo tangu ahamishwe na kuwa mkimbizi huku akinufaika na msaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
16-9-2024 • 9 minuten, 56 seconden
Baada ya kimbunga Beryl Wasamaria na IOM waishika mkono jamii ya Carriacou
Kimbunga Beryl, kilichopiga tarehe 1 Julai 2024, kimewaacha wakazi wa kisiwa kidogo cha Carriacou, Grenada, na athari kubwa . Kufuatia changamoto zinazowakabili wasamaria kutoka maeneo mbalimbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) wamewasaidia kurejesha matumaini kama anavyosimulia Anthony St. Hilaire manusura wa kimbunga hicho. Anthony aliyekumbwa na hofu kubwa wakati mawimbi makali ya bahari na upepo wa kimbunga Beryl vilipoanza kusambaratisha nyumba yake anasema hakika hali ilikuwa si hali, kwani akijua fika kulikuwa na hatari ya kupoteza maisha ."Awali, upepo ulianza kuvuma kwa nguvu, tukafunga kila kitu. Kisha kina cha bahari kilianza kupandana mawimbi kugonga madirisha na mlango. Ilibidi tufungue mlango ili kupunguza kasi ya upepo na maji."Anthony anaendelea kueleza jinsi alivyorejea nyumbani baada ya kimbunga, na akakuta kila kitu kimekwenda na maji"Haikuwa rahisi. Rafiki yangu mmoja alinipigia simu na kuniambia kuwa kila kitu kimesafishwa. Nilipofika, karibu nilie. Akaniambia usijali, haya ni mambo ya kidunia. Tumebakiwa na jambo kubwa zaidi ambalo ni uhai."Pamoja na maafa hayo na athari zake IOM ikishirikiana na wadau wengine wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha familia zenye uhitaji mkubwa hazikati tamaa , zinakuwa na matumaini na kuapata misaada haraka iwezekanavyo.
16-9-2024 • 1 minuut, 45 seconden
Walinda amani wa Tanzania wang'ara katika ulinzi wa amani nchini Afrika ya Kati, CAR
Umoja wa Mataifa umewatunuku nishani Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kikosi cha 7 kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR chini ya mwamvuli wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSCA) kimetunukiwa nishani za Umoja wa Mataifa mnamo tarehe10 Septemba 2024. Afisa Habari wa kikosi hicho, Kapteni Emanuel Ngonela alikuwa shuhuda na ametuandalia makala hii.
13-9-2024 • 2 minuten, 33 seconden
UN: Watoto zaidi ya 560,000 wamepata chango ya polio katika duru ya kwanza ya kampeni ya chanjo Gaza
Zaidi ya watoto 560,000 wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya polio aina ya pili (cVDPV2) kwenye Ukanda wa Gaza katika duru ya kwanza ya kampeni kubwa ya chanjo iliyomalizima jana yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa.Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, watoto waliopokea chanjo hiyo kupitia kampeni ya dharura ya chanjo Gaza ni wale wenye umri wa chini ya miaka 10.Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X zamani Twitter Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Adhanon Ghebreyesus amesema “Tunafurahia timu zote za wahudumu wa afya, zilizoendesha operesheni hii ngumu. Tunashukuru sana kwa familia kwa imani na ushirikiano wao. Haya ni mafanikio makubwa huku kukiwa na hali mbaya ya kila siku ya maisha katika Ukanda wa Gaza. Hebu fikiria nini kingeweza kufikiwa endapo kungekuwa na ushitishwaji mapigano.”Awamu ya kwanza ya chango ilianza Septemba Mosi na lengo lilikuwa ni katika kila duru kuchanja zaidi ya watoto 640 000 wa umri wa chini ya miaka 10.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema maelfu kwa maelfu ya watoto wmechanjwa na kukamilika kwa awamu hiyo ya kwanza ya chanjo ni mafanikio makubwa kwa shirika hilo na wadau wote walioshiriki kwani wamefikia lengo kwa asilimia 90 ingawa sasa changamoto ni kutoa dozi ya pili ya chanjo hiyo katika awamu ya pili ya kampeni inayotarajiwa katika wiki zijazo.Dozi za chanjo ya polio zaidi ya milioni 1.6 ziliwasili Gaza ili kukamilisha awamu zote mbili za chanjo inayohusisha wahudumu wa afya zaidi ya 2700.
13-9-2024 • 1 minuut, 41 seconden
13 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia chanjo za polio katika ukanda wa Gaza, na kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda. Makala inatupeleka nchini CAR na mashinani tutaelekea Gambella, Ethiopia, kulikoni?Zaidi ya watoto 560,000 wamepokea chanjo dhidi ya virusi vya polio aina ya pili (cVDPV2) kwenye Ukanda wa Gaza katika duru ya kwanza ya kampeni kubwa ya chanjo iliyomalizima jana yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa.Mnara wa kudumu wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda umesimikwa kwenye bustani ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kuhakikisha kilichotokea hakitosahaulika na asilani kisitokee tena.Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako Umoja wa Mataifa umewatunuku nishani Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kikosi cha 7 kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya mwamvuli wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo CAR (MINUSCA).Na katika mashinani tutaelekea Gambella, Ethiopia ambapo kupitia video ya UNICEF, tunakutanisha na Ariet, mtoto wa umri wamiaka 10 aliyekumbwa na utekaji baada ya kijiji chake kuvamiwa. Ariet anaeleza jinsi alivyofurahi baada ya kupata msaada wa UNICEF, ili kurejea kwenye maisha ya kawaida.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
13-9-2024 • 9 minuten, 40 seconden
Mnara wa kudumu kukumbuka mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda umewekwa katika makao makuu ya UN
Mnara wa kudumu wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda umesimikwa kwenye bustani ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kuhakikisha kilichotokea hakitosahaulika na asilani kisitokee tena. Hapa katika bustani ya Umoja wa Mataifa mnara huo uliopewa jina “Kumbukumbu ya Mshumaa wa matumaini au Mshumaa wa mautumaini wa Kwibuka” unaonekana bayana hata ukiwa mbali. Na umetengenezwa mithili ya mshumaa Mkubwa uwakao ikiwa ni zawadi maalum kutoka Jamhuri ya Rwanda kwa Umoja wa Mataifa na umesimikwa hapa rasimi jana Alhamisi.Una kitako cha rangi neyusi na maadhindi ya rangi ya dhahabu ukiwa ni mfano wa mshumaa uwkao wa rangi ya kijivu ukiwa umeandikwa maneno ya kiingereza yakimaanisha “Mauji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda, kumbuka-ungana-upya na Kwibuka mshumaa wa matumaini”Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mnara huu ni ishara ya mnepo na ujasiri wa watu wa Rwanda tangu mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi na wengine wenye msimamo wa wastani ambapo zaidi ya watu milioni 1 waliuawa kufuatia miaka mingi ya taarifa potofu, za uongo, na kauli za chuki zilizochochea mivutano ya kijamii.Wakati wakisimika mnara huo msaididizi wa Katibu Mkuu wa idara ya mawasiiano ya kimataifa Melissa Flemming alifunguka akisema "Mshumaa wa matumaini wa Kwibuka utawaka milele kama kumbusho kwa jumuiya ya kimataifa na wageni wote wanaokuja hapa kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu haja ya kuzungumza wazi na kusema Hapana kwa chuki.”Mnara huo umesimikwa wakati Umoja wa Mataifa ukijiandaa na mkutano wa zama zijazo utakaoanza mwisho wa wiki ijayo ukifuatiwa na mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kikao cha 79.
13-9-2024 • 2 minuten, 13 seconden
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno “KILIWAZO”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KILIWAZO”.
12-9-2024 • 0
12 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania, kulikofanyika mashauriano kuhusu mkutano wa zama zijazo, ambapo baadhi ya washiriki wameeleza walichojadili na walichopendekeza. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na maana ya neno “KILIWAZO”.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X amelaani vikali tukio la jana huko Gaza ambapo vikosi vya anga vya Israel vilishambulia makazi ya wakimbizi wa ndani wapatao 12, 000. Katika shambulio hilo wafanyakazi 6 wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA walifariki dunia na kufanya tukio hilo kuwa lenye vifo vingi zaidi vya wafanyakazi wa UNRWA katika tukio moja.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na wadau wake, jana Septemba 11 huko Gaza wamefanikiwa kuhamisha wagonjwa 97 na watu wengine 155 wenye majeraha makubwa zaidi. Katika unaotajwa kuwa uhamishaji mkubwa wa wagonjwa tangu ule wa Oktoba 2023 wagonjwa walisafirishwa kupitia Kerem Shalom hadi Uwanja wa Ndege wa Ramon nchini Israel kwa safari ya kuelekea Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.Tukisalia huko Gaza, takribani robo moja au watu elfu ishirini na mbili na mia tano ya wale waliojeruhiwa huko Gaza kufikia Julai 23 wanakadiriwa kuwa na majeraha ambayo yatabadilisha kabisa maisha yao na kwa hivyo wanahitaji huduma za uangalizi sasa na hata kwa miaka ijayo. Hiyo ni kwa mujibu wa uchambuzi uliotolewa leo na WHO.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KILIWAZO”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
12-9-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Mradi wa KiTiKi wainua wakulima wadogo na wakimbizi nchini Tanzania
KiTiKi yaani Kilimo Tija Kigoma ni mradi wa kuimarisha mnyororo wa thamani ya kilimo cha wakulima wadogo, usawa wa jinsia na amani katika mkoa wa Kioma unaohifadhi wakimbizi zaidi kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Serikali na watu wa Jamhuri ya Korea wamechangia Dola za Marekani milioni 6 kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ili kuimarisha kilimo cha wakulima wadogo na kuimarisha uhakikika wa chakula na lishe miongoni mwa wakimbizi na jamii zinazowahifadhi mjini Kigoma kwa miaka minne tangu mwishoni mwa mwaka juzi 2022. Anold Kayanda kupitia video ya WFP Tanzania anatupeleka mkoani Kigoma kaskazini magharibi mwa Tanzania kusikia manufaa ya mradi wa Kilimo.
11-9-2024 • 2 minuten, 28 seconden
MONUSCO yafanikisha kufufuliwa kwa kituo cha Redio na TV cha taifa RTNC mjini Beni
Wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wana furaha tele baada ya kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC. Kupitia msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wakazi hao sasa wanaweza kusikiliza na kutazama vipindi vyao wanavyovipenda, waandishi wa habari nao, hawafanyi tena kazi chini ya mti. Kupitia video ya Monusco iliyochapishwa mtandao wa X, John Matemuli, mwandishi wa habari wa kituo hicho cha Redio na Televisheni Beni, kilichositisha matangazo kwa karibu miaka mitano, anafafanua jinsi mambo yalivyokuwa kabla ya kujengwa upya kwa kituo hicho.“Miaka mitano bila Radio na Televisheni ya kitaifa ya Kongo (RTNC) mjini Beni ilikuwa ya machafuko sana. Kulikuwa na wakati ambapo tulikuwa tukifanya kazi hata kutoka juu ya mti, unaweza kuamini! Tulihisi kwamba kulikuwa na hitaji, wananchi na hata baadhi ya viongozi walihisi vivyo hivyo.”Ezechiel Kambale, mkazi wa Beni naye pia anaeleza furaha yake.“Ulipita muda mrefu tangu redio hii kuwa hewani. Lakini sasa nashukuru kwamba wamerudi. Kuna tofauti kubwa ikilinganishwa na zamani, kwa sababu leo, hata kama niko mbali na mji, bado nayapata mawimbi ya redio kana kwamba nipo hapa mjini.”Tulimrudia John na kumuuliza kilichokuwa tofauti kuhusu kituo hicho hasa kabla ya msaada wa MONUSCO.“Kazi ilofanywa hapa imewaridhisha wananchi. Leo, tuna ofisi za usimamizi. Tuna studio za kisasa za televisheni. Tuna studio ya redio kwa ajili ya kutengeneza vipindi vyetu. Tuna chumba cha habari kilicho na vifaa vya kutosha. Tulikumbana na matatizo ambayo yalihitaji msaada katika ngazi zote, lakini MONUSCO ilitupatia vifaa, ambavyo sasa vinaturuhusu kufanya kazi katika hali bora.”
11-9-2024 • 1 minuut, 55 seconden
11 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa wa homa ya nyani au mpox barani Afrika na kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC huko Beni nchini DRC. Makala tanakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Ugonjwa wa homa ya nyani au mpox ukisalia kuwa dharura ya afya ya umma duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasaka zaidi ya dola milioni 21 zitakazotumika hadi mwishoni mwa mwaka huu kuongeza harakati dhidi ya ugonjwa huo miongoni mwa wakimbizi katika nchi zilizokumbwa na dharura ya ugonjwa huo, hususan Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Wakazi wa mji wa Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wana furaha tele baada ya kufufuliwa kwa kituo chao cha Redio na Televisheni ya Taifa, RTNC. Kupitia msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, wakazi hao sasa wanaweza kusikiliza na kutazama vipindi vyao wanavyovipenda, waandishi wa habari nao, hawafanyi tena kazi chini ya mti.Makala inatupeleka mkoani Kigoma kaskazini magharibi mwa Tanzania kusikia manufaa ya mradi wa Kilimo Tija Kigoma (KiTiKi) unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa ufadhili wa Watu wa Jamhuri ya Korea.Na mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani kanda ya Afrika, tunamsikia Shane Prigge mkuu wa mnyororo wa usambazaji, WFP Kenya akieleza jinsi UNHAS ambalo ni shirika la ndege la Umoja wa Mataifa la huduma za kibinadamu linavyowezesha mashirika ya kibinadamu kufanya kazi zao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
11-9-2024 • 9 minuten, 59 seconden
UNHCR yatoa ombi la dharura la dola milioni 21.4 kukabili mpox miongoni mwa wakimbizi barani Afrika
Ugonjwa wa homa ya nyani au mpox ukisalia kuwa dharura ya afya ya umma duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasaka zaidi ya dola milioni 21 zitakazotumika hadi mwishoni mwa mwaka huu kuongeza harakati dhidi ya ugonjwa huo miongoni mwa wakimbizi katika nchi zilizokumbwa na dharura ya ugonjwa huo, hususan Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Assumpta Massoi anafafanua zaidi.UNHCR imetangaza ombi hilo leo la dola milioni 21.4, fedha zinazolenga kusaidia watu milioni 9.9 waliolazimika kukimbia makwao kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo vita. Watu hao wako kwenye nchi 35 barani Afrika.Hatua hii ya UNHCR inakuja baada ya wagonjwa 88 wa mpox kuwa ni wakimbizi na kati yao hao 68 wako DR Congo, taifa ambalo limeripoti idadi kubwa zaidi ya wagonjwa wa mpox duniani. Wagonjwa pia wameripotiwa Jamhuri ya Congo au Congo-Brazaville na vile vile Rwanda.Taarifa ya UNHCR kutoka Geneva, USwisi inasema, ingawa mpox ni ugonjwa wa muda mrefu barani Afrika, ongezeko la wagojwa hasa wenye mnyumbuliko mpya wa mpox yaani Clade 1b umefanya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO kutangaza tarehe 14 mwezi Agosti kuwa mpox ni dharura ya afya ya umma duniani. Na tangu wakati huo watu 20,000 barani Afrika wameshukiwa kuwa na ugonjwa huo.Allen Maina, Mkuu wa Afya ya Umma UNHCR anasema kwa mazingira ya sasa walio hatarini kuambukizwa zaidi ni wakimbizi wanaoishi kwenye mazingira magumu bila maji, wala sabuni na lishe bora.Sasa wanahitaji kusaidia serikali na wadau katika hatua dhidi ya mpox kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma. Hivyo fedha zitaimarisha mifumo ya afya, maji na huduma za kujisafi na kuhakikisha wakimbizi wanajengewa mnepo sasa na siku za usoni.UNHCR inatoa wito kwa wahisani kuonesha ukarimu wao kwa kuwa fedha hizo zitawezesha ujumuishaji wa wakimbizi kwenye mipango ya serikali katika nchi husika ya kujiandaa na kujikinga dhidi ya mpox kwa mujibu wa Mpango wa Afrika dhidi ya mpox ulioandaliwa na kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, CDC na WHO.
11-9-2024 • 2 minuten, 7 seconden
10 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Mwanza kaskazini Magharibi mwa Tanzania kupata ufafanuzi wa athari za moshi wa kuni kwa binadamu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na sauti kutoka mashinani.Miaka 63 tangu kifo cha ajali ya ndege cha Katibu Mkuu wa pili wa Umoja wa Mataifa Dag Hammarskjöld huko Ndola Zambia, bado majibu hayajapatikana ya nini kilisababisha ajali hiyo wakati akielekea kusaka amani kwa iliyokuwa Congo, sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limesema kampeni ya chanjo eneo la kaskazini mwa Gaza imeendelea leo jumanne licha ya tukio la jana la jeshi la Israeli kuzuia kwa saa nane msafara wa wafanyakazi waliokuwa wanasafiri kwenda kutoa huduma hiyo.Na leo septemba 10, mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA78 unakunja jamvi baada ya mwaka mzima wa mikutano na mijadala, na hivyo kuashiria kuanza kwa mkutano wa 79 au UNGA79 ambapo kuanzia tarehe 22 vitaanza vikao vya ngazi ya juu na Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu. Rais anayemaliza muda wake ni Balozi Dennis Francis kutoka Trinidad na Tobago na anayempatia kijiti ni Philemon Yang kutoka Cameroon.Katika mashinani, tunamulika mwaka mmoja tangu kimbunga Daniel kipige mji wa Dema mashariki mwa Libya na vitongoji vyake na kuleta mvua kubwa iliyosababisha mafuriko yaliyoua zaidi ya watu 5,000, na kuacha makovu hadi sasa. Maelezo ya Hawa Bu Zqeeba aliyempoteza baba yake katika mafuriko hayo yanakupatia taswira halisi ya makovu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
10-9-2024 • 9 minuten, 58 seconden
ECW yarejesha matumaini kwa msichana Fatima wa Nigeria
Alipokuwa na umri wa miaka 10 mnamo mwaka 2015, Fatima na familia yake walilazimika kutoroka nyumbani kwao Konduga, ili kuepuka mashambulizi kutoka kwa makundi yenye silaha. Konduga iko kilomita 25 kusini mashariki mwa mji wa Maiduguri, kaskazini mashariki mwa Nigeria.Familia ya Fatima haikuwa na namna ya kumuandikisha katika shule yoyote rasmi. Alitumia muda wake mwingi kuuza chakula.Shukrani kwa usaidizi wa mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri yaani Education Cannot Wait (ECW) na wadau wake wa kimkakati, Fatima sasa amesajiliwa katika mpango mesto unaolenga kuwapa elimu wasichana walio nje ya shule.Msichana huyu ni mmoja wa walengwa 250 wa programu ya miezi mitano ya kusoma, kuandika na kuhesabu, ambayo imemwezesha kusoma kwa lugha ya Kihausa na hata kuandika jina lake kama anavyoeleza."Niliingia katika shule ya ufundi baada ya kusikia kuihusu wakati nilipokuwa nimeenda kuuza chakua. Mara moja nilihifadhi kile nilichoenda kuuza kisha nikajiandikisha jina langu. Wale ambao tulikuwa hatuendi shule tulitambuliwa na kuchaguliwa. Tulifundishwa jinsi ya kusoma na kuandika. Kabla hapo nilikuwa siwezi hata kuandika jina langu.”Sehemu ya pili ya programu hii mseto ilihusisha kipengele cha ufundi ambapo wasichana wanaoishi katika mazingira hatarishi hupata mafunzo ya ufundi kwa muda wa miezi mitatu. Mpango unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, Norwegian Refugee Council (NRC) na Save the Children."Pia, sasa ninajua namba, na ninaweza kupima watu ninaposhona." Anasema Fatima ambaye katika kipengengele cha ufundi yeye amechagua ushoni wa nguo.Mpango huu tayari umewanufaisha wasichana balehe 600 tangu kuanzishwa kwake, na kuwapa vifaa vya kuanzia na ujuzi wa kujitegemea. Fatima naye ana matumaini.“Nataka kujifunza stadi hii ili niwahishimishe wazazi wangu na wawe na furaha. Nikimaliza kujifunza nataka kuwa mtu wa kuwashonea ndugu zangu nguo.”Kama ambavyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anatoa wito kwa nchi zote kuwekeza katika elimu na kufanya juhudi za kila namna kulinda elimu na maeneo ya kusomea, kulinda wanafunzi na walimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Education Cannot Wait (ECW) Yasmine Sherif, anaeleza namna ambavyo mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri umejizatiti kuendelea kuiunga mkono elimu kote duniani wakati huo akitoa wito kwa kila anayeweza kuwaongezea nguvu afanye hivyo."Kuna ustahimilivu na watoto hawa wamepitia kiwewe na mambo mengi. Ni lazima tuwepo kwa ajili yao, na tunaweza kuona matokeo. Tunatazamia kuufanya tena mpango huu mwaka katika mwaka huu, tunatarajia kufanya hivyo kwa takribani dola milioni 15, kama sio zaidi. Ikiwa nyinyi nyote mtakuja na kutusaidia kuongeza."
9-9-2024 • 3 minuten, 12 seconden
09 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia suala la elimu katika maeneo ya migogoro, na msaada wa kibinadamu huko Upper Nile nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Nigeria na mashinani nchini Afghanistan, kulikoni??Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda elimu isishambuliwe wakati wa mizozo kutokana na umuhimu wake kwa watoto na jamii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema miaka ya karibuni imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya wanafunzi, walimu na shule duniani kote. Hivyo ndivyo alivyoanza ujumbe wake wa siku hii.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano.Makala inatupeleka Maiduguri nchini Nigeria kusikia namna mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri yaani Education Cannot Wait (ECW) kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) na wadau wengine wanarejesha matumaini kwa waliokosa elimu rasmi hasa kutokana na hali mbayá ya usalama katika maeneo yao.Na katika mashinani, fursa ni yake Faeza, mfanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza biskuti nchini Afghanistan, mradi unaowezeshwa na shirika la WFP akitueleza manufaa ya mradi huo kwa jamii iliyoathirika na vita hasa wanawake na watoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
9-9-2024 • 9 minuten, 58 seconden
UNMISS: Wananchi wa kaunti ya Nasir watakiwa kuepuka mapigano ili wapelekewe maendeleo
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umewaeleza wananchi wa Kaunti ya Nasir au Keich Kon iliyoko jimboni Upper Nile nchini Sudan Kusini kuwa ili waweze kurejeshewa huduma za misaada ya kibinadamu ni vyema wakafikia makubaliano ya kusitisha mapigano. UNMISS pamoja na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu walifikia uamuzi wa kusitisha huduma zao katika kaunti ya Nasir kutokana nae eneo hilo kutofikika na pia ukosefu wa usalama uliosababishwa na mapigano ya mara kwa mara baina ya wanajamii wa kuanti hiyo, na pia mapigano na kaunti za jirani.Hata hivyo mwanzoni mwa mwezi huu wa Septemba kilifanyika kikao kilichowaleta pamoja wadau na wananchi baada ya kupatikana uongozi mpya wa kaunti hiyo ambapo katika kikao hicho, wadau wa misaada ya kibinadamu ikiwemo Umoja wa Mataifa waliombwa kurejesha operesheni zao hususan UNMISS, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) na wadau wa Sekta ya afya.Paul Ebikwo ni afisa wa masuala ya kiraia wa UNMISS na akawaeleza anaelewa wasiwasi wao.“Wasiwasi wenu ni wa halali, ni wa kweli, tunaelewa. Lakini mkiongeza mizozo ndani yake, mnafanya mambo kuwa mabaya zaidi, kwa hivyo hebu tufanye maamuzi ya kuachana, na kuweka kando migogoro na sote tufikirie jinsi ya kutatua maswala haya.”Bwana Ebikwo aliongeza kuwa suluhu zote za kuzuia ghasia lazima ziongozwe na wanajamii wenyewe huku akitoa wito kwa makundi ya vijana wanaotumia silaha kujiepusha na mapigano na kutafuta amani.Majadiliano yalihitimishwa kwa wote kukubaliana kuwa na dhamira ya pamoja ya kutafuta njia za kuleta jamii hususani vijana pamoja kwa ajili ya upatanisho na ujenzi wa amani ili kusaidia kurejesha utulivu na kuwezesha jamii katika kaunti ya Nasir kupata ahueni na maendeleo baada ya kuteseka kwa muda mrefu.
9-9-2024 • 1 minuut, 56 seconden
Guterres: Vita huharibu miili, akili na fikra za vijana na watoto
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kulinda elimu isishambuliwe wakati wa mizozo kutokana na umuhimu wake kwa watoto na jamii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema miaka ya karibuni imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya wanafunzi, walimu na shule duniani kote. Hivyo ndivyo alivyoanza ujumbe wake wa siku hii. Katibu Mkuu anasema kuanzia Gaza hadi Sudan, Myanmar, Ukraine, Colombia hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kwingineko, vita inasababisha ukatili kwa binadamu, lakini kwa watoto na vijana waliokutwa katikati ya jinamizi la vita, gharama haiwezi kukokotolewa.Anasema ndio maana siku hii inatukumbusha jinsi vita inaharibu miili, akili na fikra za watoto na vijana. Kuanzia majeraha hadi vifo, kutekwa nyara, kulazimika kukimbia, ukatili wa kingono, kutumikishwa vijana na kupoteza fursa. Hatari ni kubwa sana.Anakumbusha kuwa elimu sio tu haki ya msingi ya binadamu, bali ni muhimu kwa ajili ya kutimiza haki nyingine zote za binadamu.Ni kwa mantiki hiyo anataka nchi ziwekeze kwenye elimu na zifanye juhudi zote kuhakikisha wakati wa mizozo elimu na maeneo ya kujifunza yanalindwa, zilinde wanafunzi na walimu na ziwawajibishe wale wote wanaoshambulia shule.Ametumia pia ujumbe huo kuzitaka nchi ziridhie na zitekeleze Azimio la Shule Salama, ziunge mkono Ubia wa Kimataifa wa Kuepusha Mashambulizi dhidi ya Shule na zishikamane na juhudi zote za kuhakikisha watoto na vijana wanaendelea kujifunza iwe wakati wa majanga au wakati majanga yanapokoma.Ametamatisha akisema hebu na tulishe elimu isishambuliwe, tulinde haki ya msingi ya elimu ambayo ni haki ya kila mtoto, kila mtu kokote kule.
9-9-2024 • 1 minuut, 47 seconden
Operesheni dhidi ya makundi yenye silaha likiwemo la CODECO nchini DRC - Brigedia Jenerali Alfred Matambo
Mkuu wa kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC-MONUSCO anayemaliza muda wake mwezi huu baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja Brigedia Jenerali Alfred Matambo akizungumza na George Musubao, Mwandishi wetu wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anaeleza matokeo ya moja ya operesheni kubwa za kijeshi 15 walizotekeleza dhidi ya makundi yenye silaha likiwemo la CODECO na kazi za ujumbe huo nchini DRC.
6-9-2024 • 4 minuten, 33 seconden
Wachunguzi wa haki za binadamu wataka kuongezwa kwa vikwazo vya silaha Sudan - UN
Ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ukweli nchini Sudan, leo Septemba 6 jijini Geneva, Uswisi, wametoa wito wa kuwekwa vikwazo vya silaha kote nchini Sudan kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kikatili kama vile mashambulizi ya kutisha ya kingono. Ni mbobevu wa sheria duniani, Mohamed Chande Othman, Mwenyekiti wa Ujumbe huo Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa Mataifa wa kutafuta ukweli kuhusu yanayoendelea Sudan akiwaeleza waaandishi wa habari leo kwamba, "tangu katikati ya Aprili mwaka 2023, mzozo wa Sudan umeenea hadi majimbo 14 kati ya 18 na kuathiri nchi nzima na ukanda huo, na kuwafanya Wasudan milioni nane kuwa wakimbizi wa ndani kutokana na mzozo huo, na milioni mbili - zaidi ya milioni mbili – kulazimishwa kukimbilia nchi jirani.”Katika ripoti yao hii ya kwanza tangu Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa lilipounda jopo hilo mwaka jana 2023, wajumbe hawa wamesisitiza kwamba pande zote mbili zinazohasimiana yaani wanajeshi wa Jeshi la Sudan (SAF) na Vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF), pamoja na washirika wao, wanahusika na mashambulizi makubwa, ya kiholela na ya moja kwa moja yaliyohusisha mashambulizi ya anga na makombora dhidi ya raia, shule, hospitali, mitandao ya mawasiliano na miundombinu mingine muhimu ya maji na umeme ikionesha kutozingatia kabisa ulinzi wa wasio wapiganaji.Joy Ngozi Ezeilo, mmoja wa wajumbe wa jopo hilo la wataalamu huru anaeleza kwamba, waathirika walisimulia kushambuliwa wakiwa kwenye nyumba zao na kutishiwa kifo au kuumizwa kwa ndugu au watoto wao kabla ya kubakwa na zaidi ya mtu mmoja.”Wachunguzi hao licha ya kupendekeza uwekaji zaidi wa vikwazo vya silaha kwa Sudan, pia wamehimiza kuanzishwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani na ama kiwe chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa au mamlaka nyingine ya kikanda.
6-9-2024 • 1 minuut, 54 seconden
06 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya kutisha ya kingono nchini Sudan, na mafunzo ya kidijitali. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Ujumbe Huru wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ukweli nchini Sudan, leo Septemba 6 jijini Geneva, Uswisi, wametoa wito wa kuwekwa vikwazo vya silaha kote nchini Sudan kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kikatili kama vile mashambulizi ya kutisha ya kingono.Uhusiano kati ya teknolojia, elimu, na mabadiliko ya tabianchi ni upi? Hili ndilo limekuwa swala kuu katika mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) uliopewa jina la Wiki ya Kujifunza kwa Kidijitali au Digital Learning Week uliokamilika jana Alhamisi huko Paris Ufaransa. Mkutano huu uliangazia maswala nyeti ya mchango wa teknolojia katika elimu inayolenga maendeleo.Makala tunaelekea DRC ambako George Musubao, Mwandishi wetu wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akizungumza na Mkuu wa kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC-MONUSCO anayemaliza muda wake mwezi huu baada ya kuhudumu kwa mwaka mmoja Brigedia Jenerali Alfred Matambo. Brigedia Jenerali Matambo anaanza kwa kuzungumzia matokeo ya moja ya operesheni kubwa za kijeshi 15 walizotekeleza dhidi ya makundi yenye silaha likiwemo la CODECO.Na katika mashinani, Daktari Erick Mashimango aliyeko nchini DRC anatueleza kuwa kuenea kwa ugonjwa wa mpox kwa kasi nchini humo ambako kumegharimu maisha ya ziadi ya watu 600 kumewafanya wananchi kuwa tayari kupokea chanjo.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
6-9-2024 • 10 minuten
UNESCO: Je AI ina nafasi gani katika kudhibiti habari potofu na za uongo?
Huko Paris, Ufaransa kumekamilika mkutano wa wiki moja ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ukipatiwa jina Wiki ya Kujifunza Masuala ya Kidijitali au Digital Learning Week ambapo hoja ya Akili Mnemba kudhibiti habari potofu na za uongo imepatiwa kipaumbele.Mkutano huo ulimulika mchango wa teknolojia ya kidijitali katika elimu inayolenga maendeleo badala ya kuyadumaza. Mathalani ni kwa jinsi gani mifumo ya kidijitali inaweza kukabiliana na taarifa potofu kuhusu mabadiliko ya tabianchi.Simon Wanda, Afisa Programu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni amefafanua nafasi ya teknolojia kwenye kukabili taarifa hizo.“Mifumo hii inaweza kuchambua na kutathmini yale yanayowekwa kwenye matandao na kutambua taarifa za uongo au za kupotosha.”Mmoja wa washiriki wa mkutano huo ni Doris Mwikali, Mwanasheria na mtetezi wa elimu kutoka Kenya. Tukamuuliza maoni yake kuhusu nafasi ya teknolojia za kidijitali kwa vijana."Ninafahamu kwamba kuna mazungumzo yanaendelea kuhusu jinsi kampuni za mitandao ya kijamii zinavyopambana na habari potofu na za uongo. Lakini nadhani kuna zana mpya za akili mnemba zinazotumika na baadhi ya kampuni, kuhakiki taarifa kwenye mitandao ya kijamii. Ingawa haitakuwa na mchango mkubwa ikilinganishwa na kampuni za mitandao ya kijamii kuchukua jukumu la kudhibiti habari potofu kwenye majukwaa yao, Bado kuna jukumu kubwa kwa akili mnemba katika uhakiki wa taarifa kwenye mitandao ya kijamii, na hiyo imefanywa na mashirika mengi yasiyo ya kiserikali."Nikarejea kwa Bwana Wanda na kumuuliza maoni yake kuhusu maendeleo ya akili mnemba au AI na ujumuishaji wa sauti kutoka pande zote wakati wa kusongesha AI.“Zipo jamii nyingi zetu za kiafrika kama wamaasai wa Kenya na Tanzania, ambao kwa muda mrefu wamekuwa na elimu ya asili kuhusu kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambayo ni elimu inayofaa kutopuuzwa katika makuzi haya ya teknolojia. Hivyo, hili ni suala la kuhoji sana hasa tunapozingatia kwamba maendeleo katika teknolojia yasiegemee eneo moja la elimu tu, ambayo ni elimu ya magharibi, na kupuuza elimu ya kiasili, ambayo ni tunu.”
6-9-2024 • 2 minuten, 9 seconden
Ufafanuzi wa methali "Jawabu la kesho andaa leo"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, Mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anafafanua methali “Jawabu la kesho andaa leo.”
5-9-2024 • 0
05 SEPTEMBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha nchini Bahrain kufuatilia harakati za vijana za kufanikisha haki za watoto waliozaliwa na usonji au Down Syndrome. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na uchambuzi wa methali “Jawabu la kesho andaa leo.”Awamu ya kwanza ya kampeni ya utoaji chanjo ya polio kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 10 imehamia hii leo eneo la kusini mwa ukanda huo hususan Khan Younis na itakamilika Jumapili hii. Mama mmoja aliyepeleka mtoto wake leo amesema aliposikia tu chanjo inatolewa dhidi ya polio alikimbilia kituo cha jirani cha tiba ili ampatie chanjo kwani anahofia itasambaa kutokana na mazingira machafu ya majitakama wanamoishi. Awamu hii itamalizika Jumapili. Awamu ya Pili itaanza baada ya wiki nne.Nchini China Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anahudhuria mkutano wa China na nchi za Afrika, leo amehutubia mkutano huo na kueleza masuala kadhaa yakusaidia kusongeza nchi za Afrika ikiwemo haja ya kutatua changamoto ya nchi za Afrika kuwa na madeni makubwa na kushindwa kuwekeza katika miradi ya maendeleo, ushirikiano wa kusini -kusini na hitaji la Afrika kuwa na uwakilishi wakudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Na leo ni siku ya Kimataifa ya ukarimu duniani, mfano mmoja tu wa ukarimu unaoendelea sasa duniani ni ule shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA wanaopokea kutoka kila kona ya dunia kuanzia kwa watu maarufu, asasi za kiraia, mpaka watu binafasi, wote lengo likiwa ni kuwawezesha UNRWA kuhudumia wapalestina milioni mbili walio katikati ya mzozo huko Gaza.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, Mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anafafanua methali “Jawabu la kesho andaa leo.”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
5-9-2024 • 9 minuten, 58 seconden
WHO na Zanzibar zashirikiana kutokomeza ugonjwa wa matende
Huko Zanzibar Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO kanda ya AFrika, linashirikiana na serikali kukabili ugonjwa wa matende ambao ni miongoni mwa magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa au NTDs. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.(Taarifa ya Bosco Cosmas)Video ya WHO kanda ya Afrika inatupeleka Zanzibar, Tanzania nyumbani kwa Hamis Njani akitembea kwa shida, miguu imevimba. Alipata ugonjwa wa matende akiwa na umri wa miaka 18 lakini sasa WHO imempatia matumaini.(Sauti ya Hamis Njani)“Inaweza kukupata homa siku mbili kwa wiki, kwa hiyo nikashindwa kwenda shuleni. Wakati mwingine nashindwa kuhudhuria shule kwa miezi hata mitatu. Ninapokwenda kule hospitali, ninapata huduma na mafunzo ya jinsi ya kuishi na haya maradhi kama vile kusafisha, kutumia dawa na mengine yote.”Ugonjwa huu huenezwa na mbu. Husababisha miguu au korodani kujaa maji .Tangu mwaka 2010 Zanzibar imeendesha kampeni 20 za mgao wa dawa na WHO imetoa dawa kutibu watu milioni 1.5 kila mwaka. Asha Makame ni Mgawaji wa dawa kwenye jamii.(Sauti ya Asha Makame)“Mwanzo ulikuwa mgumu kwa sababu watu walikuwa hawaelewi. Kwa sasa hivi mwitikio ni mzuri kwa sababu kile kitu watu wamekitumia na wanajua faida yake.WHO imefundisha pia madaktari katika kila hospitali ya wilaya kufanya upasuaji wa kisasa wa mabusha kwa wagonjwa 500. Dkt. Shali Ahmed ni Meneja Mradi wa NTDs, Wizara ya Afya, Zanzibar.(Sauti ya Dkt. Shali Ahmed - Meneja wa mradi)“Ninaamini kufikia mwaka 2030, hata kabla ya hapo tutakuwa tumekomesha ugonjwa wa matende. Kwa hiyo tunawashukuru sana WHO kwa ushirikiano tunaoupata kwa kupata dawa, mara nyingi tunapata dawa kwa wakati na za kutosha kwa ajili ya nchi nzima.”
4-9-2024 • 1 minuut, 52 seconden
Kemia na ujasiriamali vinavyoambatana katika Chuo Kikuu cha Kenyatta
Je umeshawahi kujiuliza ni kwa vipi wataalamu wa kemia wanahusiana na ujasiriamali? Kama ndivyo, basi vivyo hivyo kwa Assumpta Massoi akiwa Manama, nchini Bahrain akishiriki Jukwaa la Nne la Uwekezaji kwa Wajasiriamali, WEIF2024 lililoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO, Ofisi ya Uendelezaji wa Biashara, ITPO nchini humo, alikutana na Profesa Ruth Wanjau, Mtafiti na Mshauri wa Masuala ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati katika Chuo Kikuu cha Kenyatta nchini Kenya. Alimuuliza maswali kadhaa ikiwemo ushiriki wake kwenye jukwaa hilo na nini anafanya kusongesha ujasiriamali.
4-9-2024 • 4 minuten, 39 seconden
Afrika yakutana kujadili ukuaji endelevu wa miji kwa mabadiliko ya Afrika
Mkutano wa siku tatu unaolenga kuendeleza bara la Afrika kupitia ukuaji endelevu wa miji umeanza leo jijini Addis Ababa, Ethiopia kwa ushirikiano wa Muungano wa Afrika, shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani, UN Habitat na Serikali ya Ethiopia. Anold Kayanda ameifuatilia siku ya kwanza ya mkutano huu wa siku tatu na hii ni taarifa yake.(Taarifa ya Anold)Ni mkutano ambao unawapa jukwaa wadau wakuu kutoka kote barani Afrika kuendeleza malengo ya Ajenda ya mwaka 2063 inayosema Afrika Tunayoitaka.Jukwaa hili litachunguza jukumu muhimu la ukuaji wa miji katika kufikia malengo ya Ajenda 2063 na kuunda mustakabali wa miji ya Afrika kwa kuweka mikakati ya kujenga miji ambayo ni endelevu kwa mazingira, inayojumuisha jamii, na inayostahimili uchumi.(Nats)Huyo ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kikanda na Biashara cha Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa ajili ya Afrika (ECA), Dkt. Stephen Karingi akihutubia mkutano huo anaeleza kuwa ukuaji wa miji wa haraka barani Afrika umekuja na changamoto kama miundombinu duni, kukosekana kwa usawa wa kijamaa na kiuchumi na changamoto za tabianchi na akatumia nafasi hiyo kutoa ahadi kuwa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Uchumi kwa ajili ya Afrika (ECA) iko tayari kushirika katika kuzitatua changamoto hizo kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka Sera fanisi za Uchumi mkuu na ufadhili kwa ajili ya maendeleo.Mkutano huu utahusisha shughuli mbalimbali ikiwemo mijadala, matukio ya kandoni mwa mkutano na maonesho.Tags: UN-Habitat, Afrika, Africa Urban Forum, Ajenda 2063
4-9-2024 • 1 minuut, 32 seconden
4 SEPTEMBA 2024
Ungana na Leah Mushi anayekutea jarida la Umoja wa Mataifa hii leo likiangazia juhudi za Afrika katika kujenga miji endelevu, mapambano ya kutokomeza magonjwa ya kitropiki yasiyopewa kipaumbele, matumizi ya sayansi katika nyanja mbalimbali za maisha na mashinani utasikia juhudi za kuhakikisha mipaka ya nchi inaendelea kuwa wazi hata wakati wa majanga ya asili na migogoro.
4-9-2024 • 10 minuten
03 SEPTEMBA 2024
Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo mwenyeji wako Anold Kayanda anakuletea mada kwa kina inayoangazia nafasi ya vijana katika uongozi. pia utasikia muhtasari wa habari na mashinani inayoangazia kampeni ya utoaji chanjo ya polio huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati.
3-9-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Tumefika Sudan kujionea hali halisi- Bi. Amina
Sudan, kila uchao ripoti za majanga, mapigano na ukosefu wa huduma za msingi vinaripotiwa wakati huu ambapo mzozo ulioanza mwezi Aprili mwaka jana hadi leo hii, umezidi kutia moto kwenye mafuta na kuyoyomesha matumaini ya kufikia sitisho la mapigano kati ya jeshi la serikali na lile la usaidizi wa haraka, RSF.Umoja wa Mataifa ukaamua kufika mji wa Port Sudan nchini Sudan kujionea hali halisi ya kinachoendelea hasa kwa kuzingatia ufunguzi wa eneo la mpakani wiki iliyopita na hiyo ndio makala yetu leo ikiletwa kwako na Evarist Mapesa.
30-8-2024 • 3 minuten, 36 seconden
JIFUNZE KISWAHILI: TAFSIRI YA NENO LINK
Maendeleo ya teknolojia hasa kwenye mitandao ya kijamii yamesababisha kushamiri kwa matumizi ya neno la kiingereza link. Baadhi ya watu wanalitohoa lakini Idhaa ya Umoja wa Mataifa imemuuliza Mhadhiri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania, BAKITA ni nini tafsiri sahihi ya neno link kwa lugha ya kiswahili.
30-8-2024 • 0
Mradi wa WFP wawezesha vijana Tanzania kuvuna mazao mwaka mzima
Mradi wa Vijana Kilimo Biashara (VKB) unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) nchini Tanzania unawapatia vijana wakulima wadogo ujuzi na rasilimali zinazohitajika ili kuboresha uzalishaji wa chakula na kujenga uchumi endelevu wakati huu ambao madhara ya El niño [EL NINYO] yanayosabisha ukame na mafuriko yamekuwa dhahiri. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.Hali ya El Nino huwa changamoto kwa wakulima kwani hawana uhakika wa mavuno ya kile walichopanda. Hali ni tofauti kwa mkulima kijana Coletha Kiwenge anayeendesha kilimo biashara kupitia mradi huo wa WFP wa Vijana Kilimo Biashara (VKB) nchini Tanzania. Yeye amefanikiwa kuvuna mazao mwaka mzima, licha ya changamoto za hali ya hewa zinazotokana na El Niño.“Pamoja na mradi huu wa Vijana Kilimo Biashara, unaofadhiliwa na Shirika la mpango wa chakula duniani na mtekelezaji ‘Farm Afrika’, tumejifunza yafuatayo: - Moja, matumizi ya mbegu bora, na kwa msimu huu tumetumia mbegu bora au mbegu chotara za alizeti Pamoja na mtama Pamoja na kufadhiliwa hizo mbegu ambazo zina mazao mengi.”Kutokana na madhara ya hali ya hewa na tabianchi, WFP imeelekeza nguvu katika kilimo cha umwagiliaji kwa wakulima hao.“Lakini pia tumechimbiwa kisima na Shirika la Mpango wa chakula duniani WFP, kisima hiko ni lengo na madhumuni kwaajili ya kilimo cha bustani, na kwasasa kwenye bustani yetu tumeanza na nyanya na ziko shambani. Lakini kwenye kikundi cha KAPATA, tunaendelea na upando mbalimbali.”
30-8-2024 • 1 minuut, 50 seconden
MONUSCO yachukua hatua kudhibiti waasi wa CODECO huko Ituri, DRC
Afya ya mlinda amani wa Umoja wa Mataifa aliyejeruhiwa katika shambulizi lilitekelezwa na kundi la waasi, CODECO juzi Agosti 28 huko Bali, kaskazini mashariki mwa Djugu jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inaendelea vizuri. Anold Kayanda na maelezo zaidi. Stéphane Dujarric, Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amewaeleza waandishi wa habari jana Agosti 29 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kuhusu tukio hilo la kushambuliwa kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa wakiwa katika shughuli zao za kuwahakikishia usalama raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.“Walinda amani walizuia shambulio hilo, na kuwalazimisha wanamgambo kuondoka. Hata hivyo, tunasikitika kuripoti kwamba mlinda amani mmoja alijeruhiwa.” Anaeleza Dujarric lakini akiwaondolea wasiwasi waandishi waliokuwa wakimsikiliza kwamba mlinda amani huyo aliyejeruhiwa sasa yuko katika hali nzuri.Licha ya kushambuliwa, walinda amani wanaohudumu nchini DRC katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO wameendelea na shughuli za ulinzi si tu kaskazini mashariki mwa Djugu, bali pia kusini mashariki mwa eneo hilo jimboni Ituri ambako CODECO wameweka kambi katika maeneo mawili. Msemaji wa Katibu Mkuu anaeleza kwamba walinda amani walifanikiwa kusaidia raia wa kawaida kuweza kutoka eneo moja kwenda jingine.Mashambulizi haya yanatokea ikiwa imesalia miezi michache kufika Desemba 31 mwaka huu ambayo ni tarehe iliyoridhiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba uwe mwisho wa MONUSCO kutokana na ombi la serikali ya DRC lilioomba MONUSCO iondoke katika nchi hiyo iliyogubikwa na vita kwa miaka mingi.
30-8-2024 • 1 minuut, 47 seconden
30 AGOSTI 2024
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Cecily Kariuki akikupatia yaliyojiri kutoka huko Paris, Ufaransa. Anamulika usalama wa walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko DRC; Mradi wa WFP Tanzania kwa vijana wakulima; makala ni ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa UN Sudan na mashinani ni afya Tanzania.Afya ya mlinda amani wa Umoja wa Mataifa aliyejeruhiwa katika shambulizi lilitekelezwa na kundi la waasi, CODECO juzi Agosti 28 huko Bali, kaskazini mashariki mwa Djugu jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inaendelea vizuri, amesema msemaji wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Taarifa ya Anold Kayanda inaeleza zaidi.Mradi wa Vijana Kilimo Biashara (VKB), unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) nchini Tanzania, unawapatia vijana wakulima wadogo ujuzi na rasilimali zinazohitajika, ili kuboresha uzalishaji wa chakula na kujenga uchumi endelevu wakati huu ambao madhara ya El niño [EL NINYO] yanayosabisha ukame na mafuriko yamekuwa dhahiri. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.Makala, Evarist Mapesa anatupeleka Sudan kusikia ziara ya ujumbe mzito wa Umoja wa Mataifa nchini humo ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina J. Mohammed. Mashinani, tunakwenda nchini Tanzania ambako nampisha Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi, akihimiza wananchi wa taifa hilo la Afrika Mashariki kusaka huduma dhidi ya ugonjwa huo.
30-8-2024 • 9 minuten, 56 seconden
29 AGOSTI 2024
Yaliyomo kwenye Jarida la Habari za UN hii leo ni pamoja na ziara ya Katibu Mkuu wa UN huko Timor-Leste; maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kupinga majaribio ya nyuklia na kauli ya Mkurugenzi Mteule wa WHO kanda ya Afrika, Dkt. Faustine Ndugulile baada ya kuteuliwa. Mada kwa kina ni Morogoro Tanzania. Na pia kuna kujifunza lugha ya kiswahili. Karibu na mwenyeji wako ni Anold Kayanda.Nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro, ulioko mashariki mwa nchi hiyo, wakulima 50 kutoka skimu za umwagiliaji za Ifakara Dakawa mkoani humo na Mbarali mkoa wa Mbeya, kusini magharibi mwa Tanzania wamepatiwa ujuzi wa kutumia zana bora za kisasa za Kilimo cha mpunga ikiwemo zana za kusawazisha mashamba, kupanda mbegu na kuvuna. Lengo ni kuongeza thamani katika uzalishaji wa zao la mpunga. Mafunzo yaliyotolewa na Taasisis ya Utafiti wa Kilimo TARI kwa usimamizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO huku zana zikiwezeshwa na shirika la Korea Kusini la ushirikiano wa maendeleo, KOICA. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time FM mkoani Morogoro alifika kwenye skimu hiyo kuzungumza na wakulima walionufaika. Je wajua neno la kiingereza LINK tafsiri yake ni ipi kwa lugha ya Kiswahili? Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania anafafanua.
29-8-2024 • 11 minuten, 1 seconde
Monusco yafadhili ujenzi wa zahanati katika gereza kuu la Beni,DRC
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, umeboresha huduma za afya kwenye Gereza Kuu la Beni, jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika kwa kujenga zahanati iliyoboresha sit u mazingira ya kazi kwa wahudumu wa afya bali pia huduma za matibabu kwa wafungwa. Cecily Kariuki anasimulia zaidi(Taarifa ya Cecily Kariuki)Video ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, zamani Twitter inaonesha jengo la zahanati hiyo likiwa la rangi nyeupe na buluu, wahudumu wa afya wakiwa na makoti meupe, masafi kabisa, halikadhalika mazingira ya kituo hiki.Miongoni mwao ni Dkt. Michel Muhindo ambaye hawezi kuficha furaha yake.(Dkt Michel Muhindo)- Bosco“Msaada huu wa zahanati ni ahueni kubwa kwetu sisi tunaofanya kazi hapa, na hata kwa wafungwa, kwa sababu wanapatiwa huduma nzuri ya uchunguzi, na tunafanikiwa kutoa majibu mazuri na tunawatibu ipasavyo. Tunakadiria kwamba kweli ilikuwa inahitajika.”Je, hali ilikuwa vipi kabla ya maboresho haya?(Dkt Michel Muhindo)- Bosco“Kabla ya kupata huduma hii ya matibabu, yaani zahanati hii, kulikuwa tu na vyumba ambavyo tulikuwa tunawaweka wagonjwa kwa ajili ya uchunguzi. Lakini hakukuwa na maabara, wala ofisi nzuri za ushauri. Tulikuwa na wakati mgumu sana, kulikuwa na kelele. Ilibidi kuwa makini sana ili kuweza kusikiliza wafungwa wagonjwa.”Sasa wafungwa wanapata huduma kwa nafasi kabisa..(Dkt Michel Muhindo)- Bosco“Hii inapunguza muda wa huduma kwa wafungwa katika zahanati hii. Sasa kuna maeneo maalumu yaliobainishwa vizuri. Tunaweza kusema: hiyo ni maabara, hicho ni chumba cha uchunguzi wa wagonjwa, hicho ni chumba cha daktari, kwa wauguzi, pamoja na mapokezi ambapo tunaweza kuwakaribisha wafungwa wanaokuja kwa ushauri wa matibabu.”
28-8-2024 • 1 minuut, 56 seconden
Kila mmoja achukue hatua kuondokana na vikwazo vya ujumuishaji watu wenye ulemavu - Guterres
Kila mmoja achukue hatua kuondokana na vikwazo vya ujumuishaji watu wenye ulemavu - GuterresUmoja wa Mataifa uko tayari kufanya kazi na Kamati ya Kimataifa ya Michezo ya Olimpiki ya Watu wenye Ulemavu (Paralympic) ili kufikia maono ya jamii shirikishi, jumuishi na endelevu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito michuano ya Paralympic iking’oa leo jijini Paris, Ufaransa. Anold Kayanda na maelezo zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Bwana Guterres aliyeko ziarani nchini Timor Leste, barani Asia, ametuma ujumbe kwa Mkutano wa Kimataifa wa Ujumuishaji watu wenye Ulemavu unaofanyika katika makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris Ufaransa ambako michezo ya Olimpiki ya watu wenye ulemavu, Paralimpiki 2024 imeanza kutimua vumbi leo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaamini Michezo ya Olimpiki ya Watu wenye Ulemavu inahimiza kila mtu, kuanzia kwa serikali, mamlaka za mitaa na watoa uamuzi kila mahali, kuchukua hatua ili kuondokana na vikwazo vya ushirikishwaji kamili na wa maana wa watu wenye ulemavu na Umoja wa Mataifa unaahidi kushiriki kikamilifu kutimiza lengo hilo.Aidha katika mkutano huu wa ngazi za juu, UNESCO imeitumia nafasi hiyo kuzindua Kijitabu na mfululizo wa video za mafunzo kuhusu Usawa wa Ulemavu katika Vyombo vya Habari. Kitabu hicho cha mwongozo kina masomo yanayolenga kuwapa wataalamu wa vyombo vya habari maarifa na zana wanazohitaji ili kuhakikisha mashirika yao yanakuwa jumuishi kwa kuwazingatia watu wenye ulemavu.Moja ya vivutio vikubwa katika paralimpiki za mwaka huu zitakazofanyika hadi tarehe 8 ya mwezi ujao Septemba ni timu ya wakimbizi wanane waliopelekwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
28-8-2024 • 1 minuut, 33 seconden
28 AGOSTI 2024
Karibu kusikiliza jarida linaloletwa kwako hii leo na Leah Mushi ambapo miongoni mwa utakayo yasikia ni wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu michuano ya watu wenye ulemavu. Kutoka barani Afrika hii leo utasikia MONUSCO na msaada wao kwa jamii huko Mashariki ya Kati nchini DRC. Makala yetu hii leo inatoka Gaza, utamsikia mzazi wa mtoto aliyeugua Polio na mashinani itatoka nchini Tanzania.
28-8-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Natamani mwanangu arejee hali ya kawaida na atembee- Niveen
Mgonjwa wa kwanza wa polio kubainika Gaza huko Mashariki ya Kati baada ya miaka 25 ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi 10. Mtoto huyo na mama yake pamoja na familia nzima wamekuwa wakihamahama na hivyo akakosa chanjo dhidi ya polio. Amri za Israeli za kutaka wapalestina wahame mara kwa mara sasa zinaleta madhara kwa asilimia 90 ya wakazi wa Gaza. Mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la Afya, WHO, la kuhudumia watoto, UNICEF na la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA wamejipanga kupatia chanjo watoto 640,000 huko Gaza wiki chache zijazo. Lakini mipango hiyo ikiendelea, Assumpta Massoi kupitia mahojiano yaliyofanywa na Ziad Tarib wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa huko Ukanda wa Gaza, anakuletea makala inayojikita kwenye simulizi ya mama wa mtoto aliyepooza, changamoto na ndoto zake.
28-8-2024 • 3 minuten, 51 seconden
27 AGOSTI 2024
Kati Jarida la Habari za UN hii leo: Juhudi za WHO kudhibiti Mpox kwa wakimbizi wa ndani mshariki mwa DRC. WHO inasema kugundulika kwa maambukizi ya mpox katika kambi ya wakimbizi wa ndani karibu na Goma kunatia wasiwasi kwani msongamano mkubwa wa watu unaweza kusababisha kuenea zaidi kwa ugonjwa, na mienendo ya watu inaweza kutatiza juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo ndio maana shirika hilo kwa kushirikiana na wadau linachukua kila hatua inayowezekana ili kuudhibiti ugonjwa. Kutoka DRC, George Musubao anaeleza zaidi kupitia video iliyoandaliwa na WHO siku chache zilizopita katika Hospitali Kuu ya Nyiragongo, Kivu kaskazini.Leo mashinani tunakwenda kambi ya wakimbizi ya Nduta mkoani Kigoma nchini Tanzania. Karibu!
27-8-2024 • 11 minuten, 8 seconden
Msaada wa fedha kutoka mashirika ya UN wamwezesha mkimbizi wa Sudan kujiwezesha kiuchumi
Limiya Daud mwenye umri wa miaka 30 ni mmoja wa wakimbizi wa Sudan aliyekimbilia nchini Sudan Kusini kusaka hifadhi baada ya machafuko kuibuka nchini mwake. Kutokana na wingi wa wakimbizi wanaoingia katika nchi zilizo jirani na Sudan baadhi yao wamekuwa wakihamishwa na kupelekwa katika kambi za wakimbizi ambazo zilishaanzishwa hapo awali ili waweze kupata huduma zote muhimu.Tuungane na Evarist Mapesa akituletea simulizi ya Limiya Daud na watoto wake ambao baada ya kukimbilia nchini Sudan Kusini kusaka hifadhi alihamishiwa katika kambi ya Maban iliyoko huko Renk na msaada wa fedha alioupata kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa umemuwezesha kufungua genge.
26-8-2024 • 3 minuten, 9 seconden
UNHCR na KOICA waleta matumaini kwa wakimbizi wanaorejea nyumbani Burundi
Kwa wakimbizi, kurudi nyumbani ni jambo moja na kuanza upya ni jambo lingine. Wengi wao hawana chaguo lingine isipokuwa kuanza maisha yao upya. Mkoani Makamba, nchini Burundi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) wanawawezesha wakimbizi kujenga upya na kuanza maisha yenye tija. Mmoja wa wakimbizi hao ni KABURA Emelyne, ambaye sasa anamiliki nyumba na ni mfanyabiashara. Bosco Cosmas anatupa habari kamili…Tangu mwaka 2017, takriban wakimbizi 250,000 wa Burundi wamepewa msaada wa kurejea nyumbani kutoka nchi jirani ya Tanzania. Wengi kama Emelyne hawakuwa na chaguo jingine ila kuanza maisha upya. Lakini kwa ufadhili wa (UNHCR) kwa ushirikiano na (KOICA) sasa wanaishi kwa tija.Emelyne anasema, “nilifurahi sana kuvuka mpaka wa Manyovu na kurejea nchini mwangu Burundi. Ninapoona maendeleo mapya na miji inayostawi, najihisi nimeridhika. Nilikimbilia Tanzania mwaka 2015 na nikarejea mwaka 2021.”Sasa Emelyne ameanza kujishughulisha na kilimo na kuuza mihogo, kutengeneza mafuta ya mawese, na kufuga sungura kwa ajili ya nyama na mbolea. “Najisikia furaha ninapowalisha sungura wangu kwa sababu wananiwezesha kupata mbolea. Nashukuru kwamba kupitia mauzo ya sungura nilikodi kipande cha ardhi kwa ajili ya kulima na nikapata fedha za kuanzisha biashara yangu ya mihogo na mafuta ya mawese.”Msaada kutoka Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) unawawezesha waliorejea kujenga upya na kuanza maisha mapya. Kwa mujibu wa Emelyne, "UNHCR walitukaribisha na kutusaidia. Kwa msaada wa kifedha tuliopewa, tulinunua ardhi hii, tukatengeneza matofali na kujenga kuta za nyumba yetu. Kisha tukapokea mabati, nguzo, madirisha, na milango ili kukamilisha nyumba. Kama ningalikuwa bado kwenye kambi, nisingeweza kupiga hatua kubwa kiasi hiki.”
26-8-2024 • 1 minuut, 56 seconden
Dozi za chanjo dhidi ya polio zapelekwa Gaza - UNICEF
Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linapeleka Gaza huko Mashairki ya Kati dozi milioni 1.2 za chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio aina ya 2, wakati huu ambapo ugonjwa huo hatari umethibitishwa kuweko eneo hilo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, UNICEF inasema dozi hizo milioni 1.2 za chanjo dhidi ya polio zitatumiwa kwa watoto zaidi ya 640,000.Chanjo hizo zinapelekwa wakati wiki iliyopita shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO lilithibitisha kuwa mtoto mmoja mwenye umri wa miezi 10 huko Deir al-Balah aliugua polio hiyo aina ya 2 na amepooza sehemu ya chini ya mguu wake. Ingawa hivyo hivi sasa hali yake inaendelea vizuri.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, nalo kupitia mtandao wa X linasema kwa kuzingatia hatari kubwa ya kusambaa kwa ugonjwa huo hatari huko Gaza kutokana na ukosefu wa huduma za kujisafi na maji safi, kwa kushirikiana na UNICEF na WHO siku zijazo watazindua kampeni ya chanjo dhidi ya polio kwa watoto zaidi ya laki sita wenye umri wa chini ya miaka 10.Kwa mujibu wa UNRWA, operesheni za jeshi la Israeli huko Deir Al Balah zimeharibu miundombini ya maji na kwamba ni visima vya maji 3 tu kati ya 18 ndio vinafanya kazi na kwa mantiki hiyo uhaba wa maji ni asilimia 85.
26-8-2024 • 1 minuut, 22 seconden
26 AGOSTI 2024
Hii leo jaridani tunamulika kupelekwa kwa chanjo dhidi ya polio huko Gaza; mkimbizi wa Burundi aliyerejea nyumbani kutoka Tanzania ainuliwa kiuchumi; makala ni mkimbizi wa Sudan aliyeko ugenini naye awezeshwa kijasiriamali na mashinani tunabisha hodi nchini Rwanda kumulika usawa wa kijinsia kwenye michezo.Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linapeleka Gaza huko Mashairki ya Kati dozi milioni 1.2 za chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio aina ya 2, wakati huu ambapo ugonjwa huo hatari umethibitishwa kuweko eneo hilo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Kwa wakimbizi, kurejea nyumbani ni jambo moja na kuanza upya ni jambo lingine. Wengi wao hawana chaguo lingine isipokuwa kuanza maisha yao upya. Mkoani Makamba, nchini Burundi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) wanawawezesha waliorejea nyumbani kujijenga upya na kwa tija. Miongoni mwao ni Emelyne Kabura kama anavyosimulia Bosco CosmasKatika makala Evarist Mapesa anatuletea simulizi ya mkimbizi wa Sudan ambaye sasa anaishi Sudan Kusini. Baada ya kupitia madhila lukuki amewezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na sasa anajishughulisha na ujasiriamali.Na sasa ni mashinani Christelle Umuhoza, Mkurugenzi wa Programu wa Rwanda katika shirika la Shooting Touch, kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO nchini humo, anaeleza umuhimu wa michezo katika kuondoa vikwazo vya kijinsia.
26-8-2024 • 9 minuten, 43 seconden
Uhalifu kote duniani unaleta madhila yaleyale kwa wanadamu – Maonesho ya picha za ICC
Ikiwa leo ni siku ya mwisho ya maonesho ya picha yaliyoandaliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Anold Kayanda anatupitisha katika picha hizo zinazoonesha athari mbalimbali kwa wanadamu kutokana na uhalifu unaotekelezwa katika maeneo mbalimbali duniani.Maonyesho haya yanachunguza uhusiano wa pamoja unaooneshwa katika simulizi za watu kutoka hali zote ambapo ICC imeanzisha uchunguzi. Maonesho haya pia yanaangazia baadhi ya wapokeaji wa kwanza wa maagizo ya malipo ya ICC.Ingawa simulizi hizi zinatoka katika mabara manne, zina ufanano mwingi. Watu wanapoteza nyumba, ardhi na familia zao. Pia zinaonesha jinsi jamii ni muhimu katika kujenga upya maisha. Kwako Anold
23-8-2024 • 3 minuten, 55 seconden
Msumbiji yazindua mpango wa kutoa mapema maonyo ya majanga kwa wote EW4ALL
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, amezindua mpango wa kitaifa wa kuhakikisha kila mtu anapata Maonyo ya Mapema kuhusu hali ya hewa, EW4All ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027 huku akitangaza uwekezaji mpya muhimu ili kuboresha uchunguzi wa kimsingi wa hali ya hewa, uzinduzi uliofanyika katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.Mpango huo unajumuisha mnyororo mzima wa thamani kwenye utabiri wa hali ya hewa, kuanzia kukusanya takwimu za hali ya hewa, tabianchi, kuimarisha utabiri wa hali ya hewa, na mfumo wa utoaji wa maonyo hadi kutoa taarifa kuhusu mipango bora ya kuhimili tabianchi.(Sauti ya Filipe Jacino Nyusi - Rais wa Msumbiji) Bosco“Msumbiji ni nchi ambayo inakabiliwa na tishio la kudumu la majanga, hasa yale yanayosababishwa na majanga ya kiasili ya kupitiliza, huku mafuriko, vimbunga na ukame vikiwa vya mara kwa mara. Matukio haya mabaya yanapotokea, yanaacha mwenendo wa uharibifu ya vifo vya binadamu na uharibifu wa mali, na mazingira na madhara makubwa kwa jamii na uchumi wetu. »Mpango huu wa kutoa onyo la mapema kabla majanga hayajatokea umechagizwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, na sasa unajumuishwa kwenye sera za Msumbiji. Rais Nyusi akaelezea umuhimu wake.(Sauti ya Filipe Jacino Nyusi - Rais wa Msumbiji) - Bosco“Mengi yanaweza kufanywa ili kupunguza kupoteza maisha ya binadamu na madhara makubwa zaidi. Onyo la mapema hutusaidia kufanya hivyo, ili kujilinda. Kama ninavyosema, mojawapo ya majibu bora zaidi yanatokana na kuboresha uwezo wetu wa kuzuia na kutayarisha, uwezo wa kuzuia, hatari ya maafa, hasa hatua za tahadhari za mapema."Uwekezaji unaotajwa ni ujenzi wa vituo vipya 6 vya ardhini vya hali ya hewa na uboreshaji wa vingine 15 pamoja na kuanzisha vinne vipya vya angani.
23-8-2024 • 1 minuut, 59 seconden
Polio yathibitishwa Gaza, WHO yasema ni mtoto mwenye umri wa miezi 10
Vuta nikuvute ikiendelea Gaza kuhusu ufikishaji, usambazaji na utoaji wa chanjo dhidi ya polio wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima kutoka jeshi la Israeli, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO, limethibitisha kubainika kwa mgonjwa mmoja wa polio, ikiwa ni miaka 25 tangu ugonjwa huo utokomezwe eneo hilo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Ni kwamba tarehe 20 mwezi uliopita wa Julai, mtoto huyo mwenye umri wa miezi 10 alilazwa katika hospitali ya Al-Aqsa akiwa ana homa kali, anatapika, anahara huku akiwa hana nguvu mwilini, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA katika ripoti yake ya 130 kutolewa tangu vita ianze huko Gaza, ikimulika Gaza, Ukingo wa Magharibi na Yerusalem Mashariki.Tarehe 22 Wizara ya Afya kwenye eneo linalokaliwa la Palestina likathibitisha ugonjwa wa polio virusi namba 2 kwa mtoto huyo ambaye hakuwa amepatiwa chanjo kutoka Deir al-Balah huko Gaza. Siku tatu baadaye yaani tarehe 25 Julai mtoto huyo akapooza sehemu ya chini ya mguu wake. Hivi sasa anaendelea na matibabu na hali yake ni nzuri.Uchunguzi uliofanywa na Kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia magonjwa, CDC ukaunganisha virusi hivyo na aina ya ile iliyobainika kwenye mazingira huko Gaza mwezi Juni mwaka huu.Sasa WHO imethibitisha kuwa ni polio ambapo Mkurugenzi Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini kupitia mtandao wa X amesema “inasikitisha sana kwamba mtoto huyo amepooza kutokana na Polio. Polio haitotofautisha kati ya watoto wa Palestina na Israeli. Kuchelewecha sitisho la mapigano kwa misingi ya kiutu kutaongeza hatari ya ugonjwa huo kusambaa zaidi kwa watoto.”Awamu mbili za utoaji chanjo zimepangwa kuanza wiki zijazo na UNRWA imesema wataalamu wake wa afya na kupitia kliniki zake tembezi watasaidia usambazaji kwa ushirikiano na WHO na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.
23-8-2024 • 2 minuten, 2 seconden
23 AGOSTI 2024
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akimulika ripoti ya kuthibitishwa kwa mgonjwa wa polio huko Gaza; Tukio la uzinduzi wa mpango wa utoaji taarifa mapema kuhusu majanga; Makala ikimulika kazi za Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC na mashinani ikienda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mhudumu wa afya anayefanikisha kazi za uteguaji wa mabomu yaliyotegwa ardhini.Vuta nikuvute ikiendelea Gaza kuhusu ufikishaji, usambazaji na utoaji wa chanjo dhidi ya polio wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima kutoka jeshi la Israeli, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO, limethibitisha kubainika kwa mgonjwa mmoja wa polio, ikiwa ni miaka 25 tangu ugonjwa huo utokomezwe eneo hilo. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, amezindua mpango wa kitaifa wa kuhakikisha kila mtu anapata Maonyo ya Mapema kuhusu hali ya hewa, EW4All ifikapo mwishoni mwa mwaka 2027 huku akitangaza uwekezaji mpya muhimu ili kuboresha uchunguzi wa kimsingi wa hali ya hewa, uzinduzi uliofanyika katika mji mkuu wa Msumbiji, Maputo.Makala inasalia makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ikiwa leo ni siku ya mwisho ya maonesho ya picha yaliyoandaliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Anold Kayanda anatupitisha katika picha hizo zinazoonesha athari mbalimbali kwa wanadamu kutokana na uhalifu unaotekelezwa katika maeneo mbalimbali duniani. Kwako AnoldMashinani: Fursa ni ya Chantal Zingapako, muuguzi anayejitolea kusaidia timu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, ya kutegua mabomu ya ardhini.
23-8-2024 • 10 minuten, 19 seconden
Chiriku hana hisani
Wiki hii katika kujifunza Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka nchini Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Chiriku hana hisani.”
22-8-2024 • 1 minuut, 11 seconden
22 AGOSTI 2024
Karibu kusikiliza jarida ambapo hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathiriwa wa vitendo vya ghasia kwa misingi ya dini na imani, msomaji wako wa jarida ni ANOLD KAYANDA na jaridani anakuletea mada kwa kina ambayo inamulika wanawake wa kimasai na biashara ya bidhaa zitokanazo na shubiri nchini Kenya. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na kujifunza kiswahili hii leo mtaalamu wetu Dkt.Josephat Gitonga atafafanua maana ya methali “Chiriku hana hisani.”
22-8-2024 • 11 minuten, 28 seconden
Madhila ya ugaidi mpaka lini?
Tarehe 21 ya mwezi Agosti kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi Wathirika wa Ugaidi, Anold Kayanda anatupitisha katika moja ya shoroba za ndani ya makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambako zimewekwa picha za baadhi ya manusura na waathirika wa ugaidi zikiwa na maelezo ya kile kinachowafanya kusonga mbele.
21-8-2024 • 3 minuten, 38 seconden
Haiti: UNICEF imeanzisha kituo cha watoto kujifunza na kufurahi
Idadi ya watoto wanaoshindwa kupata huduma za msingi ikiwemo maeneo rafiki ya kucheza ikizidi kuongeza nchini Haiti kutokana na magenge ya uhalifu kuendesha ghasia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaendelea kufungua vituo rafiki kwa watoto ili waweze kujifunza na kucheza badala ya kukumbwa na msongo kama anavyosimulia Bosco Cosmas. (Taarifa ya Bosco Cosmas)Nats..Tuko mkoa wa Artibonite, ulioko kaskazini mwa mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince. Video ya UNICEF imeanzia ndani ya nyumba ya banda la bati, makazi ya Roseline mama mzazi wa Alicha, mtoto mwenye umri wa miaka 7, wanaonekana wakichambua mboga. Roseline anasema,(Sauti ya Roseline – Mama yake Alicha) Asha “Ni mimi ninampatia chakula Alicha, kila kitu anachokitaka, mimi ndiye ninayewajibika. Baba yake alimuacha tangu alipoanza kujifunza kuketi.” Familia nyingi Haiti, ikiwemo ya Alicha zinahaha kukimu mahitaji ya watoto huku zikitakiwa kuwapatia malezi ili wakue. Shule zimefungwa kutokana na ghasia za magenge. Na ndio maana UNICEF ikaanzisha maeneo rafiki kwa watoto. (Sauti ya Roseline – Mama yake Alicha) Asha “Nimefahamu kuhusu klabu hiki cha watoto kutoka kwa kiongozi wa kuchaguliwa wa eneo hili. Alinieleza kuna sehemu rafiki kwa watoto, na Alicha alipoiona na kuona watoto wanacheza alikuja kuniambia mama sitaki kukaa tena kwa bibi, kwa sababu nimeipenda ile klabu ya watoto na ninataka kwenda”. Alicha akiwa kwenye kituo hicho akiwa anacheza na wenzake na mwalimu akiwaelekeza anasema, “ninaipenda hii sehemu kwa sababu wananifundisha vizuri, wananionesha michezo, wananionesha jinsi ya kuruka Kamba. Ninawapenda mwalimu na ninapenda kila kitu katika sehemu hii.” Video inatamatika kwa Roseline kueleza kuwa anapenda kituo hicho kwani kinawasaidia watoto, na yeye kama mzazi anaipenda kwa ajili yao.
21-8-2024 • 2 minuten
Guterres: Tujifunze kutoka kwa waathirika wa ugaidi
Wakati dunia hii leo inawakumbuka na kutoa heshima kwa waathirika na manusura wote wa ugaidi duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema huu ni wakati muhimu wa kuwasilikiza waathirika hao na kujifunza kutoka kwao.Katika ujumbe wake wa siku hii alioutoa kwa njia ya video Guterres amesema vitendo vya ugaidi vinaleta huzuni isiyoelezeka, na familia na jamii zinazokumbwa na vitendo hivyo husambaratishwa milele huku makovu yanayoonekana na yasiyo onekana hayawezi kupona kikamilifu.Cue Guterres – Evarist“Tunatoa heshima zetu kwa waathirika na manusura wote, ikiwemo wale waliochagua kutushirikisha simulizi zao kuhusu uvumilivu na msamaha huku tukitafakari juu ya kiwewe walichopitia ili kuelimisha wengine kuhusu vitendo vyao vya ujasiri mkubwa. Siku hii inatuhimiza sote tusikilize na kujifunza na ukumbusho kuwa lazima wote tutafute nuru ya matumaini. Kwa pamoja, tunaweza kupaza sauti za waathiriwa na manusura wote. Kwa pamoja, tunaweza kusaidia kuelimisha vizazi vya sasa na vijavyo na kwa pamoja, tunaweza kujenga jamii zenye amani na uthabiti zaidi kwa wote.”Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka waathirika wa ugaidi mwaka huu inasema “Sauti za amani: Wahanga wa ugaidi kama watetezi wa amani na waelimishaji.”Katibu Mkuu Guterres pia amesifu subira za waathirika wa ugaidi kwa kueleza licha ya kupitia mateso na maafa lakini dunia imeshuhudia mifano yao ya ustahimilivu na nguvu ya ubinadamu wetu wa pamoja.
21-8-2024 • 1 minuut, 28 seconden
21 AGOSTI 2024
Hii leo ikiwa ni siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi Wathirika wa Ugaidi msomaji wako Leah Mushi anakuletea ujumbe uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu haja ya kuwasikiliza na kujifunza kutoka kwa waaathirika wa ugaidi, pia utapata simulizi ya maonesho ya picha za wahanga wa ugaidi zilizowekwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani na utasikia wito wa mmoja wa watu waliowahi kutekwa na magaidi kwa miaka 8 na kisha kuokolewa. Mbali na masuala ya ugaidi utasikia jinsi watoto walioko Haiti wanavyosaidiwa kutopata msongo wa mawazo kutokana na changamoto za usalama wanazo kabiliana nazo.
21-8-2024 • 9 minuten, 59 seconden
20 AGOSTI 2024
Karibu kusikiliza jarida linalo letwa kwako na Anold Kayanda ambapo hii leo anakuletea mada kwa kina ambayo inamulika wahudumu wa kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususan kile kinachosababisha waendelee kutekeleza jukumu hilo licha ya changamoto za kiusalama wanazopitia. Pia utasikia muhtasari wa habari ukiletwa kwako na Leah Mushi ambapo ameangazia suala la nishati ya mafuta huko Gaza, ugonjwa wa Mpox huko barani ulaya, na maadhimisho ya siku ya mbu duniani yanayolenga kuelimisha jamii jinsi ya kupambana na mdudu huyo hatari.
20-8-2024 • 9 minuten, 56 seconden
IOM kupitia mradi wa COMPASS warejesha ndoto ya maisha bora kwa Burte nchini Ethiopia
Changamoto za maisha ikiwemo sintofahamu ya nini utakula husababisha binadamu kufikiria kuhamia maeneo mengine ili pengine aweze kujipatia riziki. Ingawa hivyo si kila ahamie eneo lingine anapata kile alichotarajia. Hii imemkuta msichana Burte Kase wa nchini Ethiopia ambaye matarajio ya kuboresha maisha yake kwa kukimbilia Saudi Arabia. Machungu yaliremjesha nyumbani na ndoto zake zikatimizwa nyumbani Ethiopia kwa kupitia mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM. Je ni nini walifanya? Evarist Mapesa anakujulisha kupitia makala hii.
19-8-2024 • 3 minuten, 29 seconden
Watoto Sudan wako taabani, vita ikome - UNICEF
Mgogoro unaoendelea Sudan unazidisha hali mbaya ya maisha na mustakabali wa haki za kibinadamu hasa kwa watoto ambao wanakumbana na mateso makubwa ikiwemo njaa, ukatili na vitisho. UNICEF kupitia msemaji wake James Elder imetembelea katika moja ya kambi za kuhifadhi wakimbizi na kushuhudia kinachoendelea kama anavyosimulia Bosco Cosmas.Amesema "matukio kote Sudan yanashangaza, ninamaanisha miezi 16 ya watoto wanaoshambuliwa. Sijui kama unaweza kusikia sasa nyuma yangu, milio ya risasi. Hakika, watoto ni wengi hapa. Hivi ndivyo tunavyoshuhudia kila siku, watoto wakishambuliwa. Hawa ni mamilioni ya watoto wanaolazimika kukimbia makwao. Tunaiona hali hii kila mahali."Nini sasa kifanyike, ili kuweka hali ya watoto nchini Sudan katika usalama? Elder anasema "endapo pande zinazopigana na jumuiya ya kimataifa wangezingatia watoto wa Sudan, naweza kukuambia kile ambacho tusingekuwa tunakiona hivi sasa. Tusingekuwa baa la njaa. Tusingeona mamilioni ya watu ambao wamelazimika kukimbia nyumba zao, kazi zao, kuungana na familia zao,kila kitu kwa sababu ya mapigano haya makubwa yanayoendelea. Hatungekuwa tunashuhudia vikifo, majeraha, kiwewe, na unyanyasaji wa kijinsia.”Amesisistiza kuwa "kama sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu zitazingatiwa, watoto wa Sudan watanufaika zaidi na kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu na maisha bora."
19-8-2024 • 1 minuut, 49 seconden
Mwaka 2023 ulikuwa hatari zaidi kwa wahudumu wa kibinadamu- Guterres
Kokote kwenye machungu ya binadamu wafanyakazi wa kiutu wanahaha kupunguza machungu na maumivu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya wahuduku wa kibinadamu.Kupitia ujumbe kwa njia ya video, Guterres amesema oOperesheni za kiutu zinazoratibiwa na Umoja wa Mataifa husambaza misaada ya kuokoa maisha kwa zaidi ya watu milioni 140 kila mwaka.Amesema wafanyakazi wa misaada, wengi wao wa kitaifa huhudumu ndani ya jamii zao, wakivumilia licha ya vitendo vya ukatili. Wanaendeleza jitihada zao kukabili vikwazo vyote ili kusaidia wananchi wenye uhitaji- katika mazingira ya ukata mkubwa.Katika Siku hii ya Usaidizi wa kibinadamu kwa mara nyingine tena tunapongeza ujasiri wao, na kujizatiti kwao, na huduma yao kwa ubinadamu. Na tunatambua kuwa kuwaenzi wahudumu wa kibinadamu haitoshi. Mwaka 2023 ulikuwa wa hatari zaidi kwa wahudumu wa kibinadamu.Huko Gaza, Sudan na maeneo mengine mengi, wafanyakazi wa kibinadamu wanashambuliwa na kuuawa, wanajeruhiwa na wanatekwa nyara sambamba na raia wanaowaunga mkono. Kampeni zenye habari potofu zinasambaza uongo unaogharimu maisha.Kwa kutambua wahalifu wengi wanakwepa sheria, Guterres amesema, “tunataka serikali zishinikize pande zote kwenye mzozo zilinde raia. Tunataka kutokomezwa kwa usafirishaji silaha kwa majeshi na vikundi vinavyokiuka sheria ya kimataifa. Tunadai kutokomezwa kwa ukwepaji sheria ili wahalifu wafikishwe mbele ya sheria. Kushereheka watoa huduma za kiutu haitoshi Sote tuongeze bidii kulinda na kuhifadhi utu wetu wa pamoja.”Siku ya wahudumu wa kibinadamu ilipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2009 kufuatia mashambulizi kwenye ofisi za makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko Baghdad Iraq tarehe 19 Agosti 2003 yaliyosababisha vifo vya wahudumu 22 wa kibinadamu akiwemo Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Sergio Vieira de Mello.***
19-8-2024 • 2 minuten, 7 seconden
JIFUNZE KISWAHILI: NENO - NGAWIRA
Hii leo katika kujifunza lugha ya Kiswahli, Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi katika Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, anafafanua maana ya neno 'Ngawira" ambalo limekuwa linatumika ndivyo sivyo.
19-8-2024 • 0
19 AGOSTI 2024
Hii leo siku ya wahudumu wa kibinadamu ikitambulika pia siku ya usaidizi wa kiutu tunamulika ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN akitaka wahudumu hao wasilengwe; tunakwenda pia Sudan, kisha Ethiopia na tunamalizia na mashinani, na mwenyeji wako ni Flora Nducha.Kokote kwenye machungu ya binadamu wafanyakazi wa kiutu wanahaha kupunguza machungu na maumivu, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya wahudumu wa kibinadamu.Tukiwa bado na siku hii ya wahudumu wa kibinadamu duniani, tunaelekea nchini Sudan kuambatana na muhudumu wa kibinadamu James Elder ambaye ni msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF akisimulia alichokishuhudia nchini humo na nini kifanyike ili kulinusuru taifa hilo na hasa mustakabali wa watoto kupitia taarifa ya Bosco Cosmas.Katika makala Evarist Mapesa anatupelea Ethiopia kutukutanisha na mnufaika wa mradi wa shirika la Umoja wa MAtaifa la Uhamiaji, IOM wa kusaidia wahamiaji kurejea nyumbani kwao salama na hatimaye kujumuika katika jamii kupitia majawabu endelevu, COMPASS. Mashinani leo fursa ni yake Amal Shammala, dereva mwanamke wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Chakula Duniani WFP, anayegawa msaada wa kibinadamu kwa familia zilizoathirika na vita Gaza."
19-8-2024 • 10 minuten, 42 seconden
Ni muhimu serikali kushikana na vijana kusongesha SDGs: Vivian Joseph
Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia upatu vijana kujitokeza na kushiriki katika kusongesha ajenda ya maendeleo endelevu SDGs sasa ikiwa imesalia chini ya miaka 6 kabla ya kufikia ukomo mwaka 2030. Vijana katika sehemu mbalimbali duniani wanakumbatia wito huo kwa kushiriki kwenye miradi mbalimbali. Leo Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na Vivian Joseph kijana afisa tabibu wa kitengo cha afya katika jukwaa la vijana la jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC aliyehudhuria jukwaa la vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Uchumi na Kijamii, ECOSOC, lililofanyika hapa Umoja wa Mataifa mwezi Aprili akitaka kujua mchango wa vijana wa SADC katika kusongesha malengo hayo ya SDGs hasa lengo namba 3 la afya bora na ustawi. Vivian ananza kwa kufafanua majukumu yake na kazi za jukwaa hilo
16-8-2024 • 4 minuten, 36 seconden
Sweden yathibitisha mgonjwa wa mpox; WHO yataka ushirikiano kudhibiti
Homa ya nyani au mpox aina ya Clade 1B imevuka barani Afrika na kuingia Ulaya hususan Sweden, ikiwa ni nchi ya kwanza nje ya bara hilo kuthibitisha kuwa na ugonjwa huo ambao tayari WHO imetangaza kuwa ni dharura ya afya ya umma duniani. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO kanda ya Ulaya. Bosco Cosmas na maelezo zaidi. Juzi Jumatano WHO ilitangaza kuwa mpox ni dharura ya afya umma duniani baada ya kasi kubwa ya kusambaa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa Clade 1B ambavyo ni virusi vipya vya mpox na hatari zaidi, ikilinganishwa na vile vya awali vya mwaka 2022.Hans Kluge ambaye ni Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Ulaya, amenukuu mamlaka za afya nchini Sweden zikisema kuwa mgonjwa huyo alisafiri maeneo ya Afrika yanayokabiliwa na mlipuko wa mpox, ingawa hakutaja eneo husika.Kluge amesema walishaeleza awali kuwa haitochukua muda mrefu kwa virusi hivyo vipya vya mpox kusambaa maeneo mengine nje ya Afrika kwa kuzingatia muunganiko wa dunia.Kwa sasa mgonjwa anatibiwa dalili za ugonjwa huo, sambamba na kumtenga na kufuatilia waambata wake.Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, amesema kubainika kwa mgonjwa Sweden kunasisitiza umuhimu wa nchi zenye maambukizi kushirikiana kukabili virusi hivyo.Ametaka nchi ziimarishe ufuatiliaji, zibadilishane takwimu na kufanya kazi pamoja kuelewa njia za maambukizi, kushirikishana chanjo na kujifunza kutokana na masomo ya awali wakati mpox ilipotangazwa kuwa dharura ya afya ya umma duniani.Barani Afrika, mlipuko wa mpox umethibitishwa DRC na Burundi, huku Kenya, Uganda na Côte d'Ivoire zikiwa na wagonjwa tu wa hapa na pale.
16-8-2024 • 1 minuut, 33 seconden
UNICEF yaimarisha huduma za afya kwa zahanati 10 mikoa ya Songwe na Mbeya nchini Tanzania
Nchini Tanzania hususan wilaya ya Mbozi mkoani Songwe changamoto za huduma za afya kwenye zahanati ya Nansama zimesalia historia baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kupitia ufadhili wa Korea ya Kusini kuboresha huduma za usafi na kujisafi kwenye zahanati 10 za mikoa ya Mbeya na Songwe. Kutoka Tanzania Evarist Mapesa anatupasha zaidi.Kile kipindi cha nyuma, hapa tulikuwa na kitanda kimoja tu cha kuzalia na maji hayakuweko. Wajawazito walikuwa ni wengi, na hatukujua tuzalie wapi na tufanyeje.Ni kauli ya Sabrina Kibona, mkazi wa wilaya ya Mbozi mkoa wa Songwe, kusini-magharibi mwa Tanzania akikumbuka hali ilivyokuwa awali katika zahanati ya Nansama.Mazingira hayo hatarishi ya kiafya yanaelezewa pia na Hidaya Mwalusapo, muuguzi katika zahanati hii ambaye anasema “zahanati hii inahudumia vijiji viwili. Kipindi kabla miundombinu haijaboreshwa, wagonjwa wengi walikuwa wanapitiliza na kwenda kituo cha afya cha Isansa, kutokana na miundombinu iliyokuweko.”Mama akijifungua kondo lilitupwa chooniAnasema enzi hizo mama akijifungua, kondo linatupwa chooni kwa sababu hatukuwa na eneo la kuteketezea taka za hospitali.Kilio chao kikafika UNICEF na mambo yakabadilika. Remijus Sungu, Afisa wa huduma za usafi na kujisafi, au WASH katika UNICEF nchini Tanzania anasema, “UNICEF kwa ufadhili wa serikali ya Korea Kusini walifadhili kitengo cha usafi ,maji na mazingira, WASH, kuimarisha huduma za maji na udhibiti wa maambukizi au IPC katika zahanati 10.”UNICEF imewezesha ujenzi wa eneo la kutupa taka za hospitaliBwana Sungu anasema, katika vituo vyote 10 “tulitekeleza mradi kamilifu wa WASH, kwa maana ya kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama, udhibiti na uteketezaji sahihi wa taka zinazozalishwa maeneo ya hospitali, na pia kuzuia maambukizi yatokanayo na huduma za afya, na pia kuhakikisha mama na mtoto wanakuwa salama wanapokuja kupata huduma kwetu.”Kwa mujibu wa muuguzi Hidaya, chumba cha mama na mtoto kimekarabatiwa, kuna matenki ya kutosha ya kuhifadhi maji, halikadhalika eneo la kufulia nguo chafu. Tumejengewa vyoo bora. Na kwa mwezi mzima idadi ya wajawazito wanaojifungua imeongezeka.Na kwa Sabrina, anashukuru maboresho kwani anasema zamani hapakuwa hivi, sasa hivi pamekuwa pazuri kabisa, tumefurahi.
16-8-2024 • 2 minuten, 5 seconden
16 AGOSTI 2024
Hii leo katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anamulika masuala ya afya, hususan mpox kuthibitika Sweden; huduma za afya ya mama na mtoto huko mkoani Songwe, Tanzania. Makala ni vijana wa SADC na kusongesha SDGs, na mashinani ni mwanamke aliyenusurika kutumikishwa kwenye biashara ya ngono huko Dubai, Falme za kiarabu. Karibu!Homa ya nyani au mpox aina ya Clade 1B imevuka barani Afrika na kuingia Ulaya hususan Sweden, ikiwa ni nchi ya kwanza nje ya bara hilo kuthibitisha kuwa na ugonjwa huo ambao tayari WHO imetangaza kuwa ni dharura ya afya ya umma duniani. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO kanda ya Ulaya. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.Nchini Tanzania hususan wilaya ya Mbozi mkoani Songwe changamoto za huduma za afya kwenye zahanati ya Nansama zimesalia historia baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kupitia ufadhili wa Korea ya Kusini kuboresha huduma za usafi na kujisafi kwenye zahanati 10 za mikoa ya Mbeya na Songwe. Kutoka Tanzania Evarist Mapesa anatupasha zaidi.Makala leo Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na Vivian Joseph afisa tabibu wa kitengo cha afya katika jukwaa la vijana la jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC aliyekuweko hapa Umoja wa Mataifa mwezi Aprili kwa vikao vya UN akitaka kujua mchango wa vijana wa SADC katika kusongesha ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu SDGs hasa lengo namba 3 la afya bora na ustawi. Vivian ananza kwa kufafanua majukumu yake na kinachofanywa na jukwaa hilo.Mashinani: Tunakukutanisha na Aaliya, mwanamke kutoka Nigeria ambaye alikwenda Dubai, Falme za kiarabu na kunusurika kutumbukia kwenye biashara haramu ya ngono na sasa amenzisha biashara kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji (IOM).
16-8-2024 • 9 minuten, 59 seconden
15 AGOSTI 2024
KatikaJ arida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, (WHO) jana Jumatano limetangaza mpox kuwa ni dharura ya afya ya umma kimataifa, hivyo sasa fahamu mambo matano muhimu kuhusu mpox. -Dkt. Abdou Salam Gueye, Mkurugenzi wa Dharura, WHO Kanda ya AFrika anasema kuna sababu ya kuamini kwamba nchini Congo DRC na Burundi kuna maambukizi ya mpox miongoni mwa jamii-Mada kwa kina leo inajikita na vijana na uongozi ambapo kijana Joram Nkumbi kutoka Tanzania anabonga bongo na Assumpta Massoi-Na ni Alhamisi ya kujifunza Kiswahili tuko Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania BAKITA kupata ufafanuzi wa neno "NGAWIRA"
15-8-2024 • 10 minuten
Vijana wasisitiziana umuhimu wa kutumia kwa usahihi vifaa vya kidijitali
Jumatatu ilikuwa ni maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vijana iliobeba maudhui ya fursa za kidijitali kwa vijana kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu. Nchini Tanzania, vijana walipata fursa ya kujifunza kuhusu mbinu mbalimbali za kujikwamua katika maisha na tutawaskia vijana wawili wakitueleza kakitoa maoni yao kuhusu mchango wa teknolojia katika maisha ya vijana. Cecily Kariuki anaelezea yaliyojiri katika makala hii iliyofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na AFya ya Uzazi, UNFPA nchini Tanzania.
14-8-2024 • 3 minuten, 31 seconden
Kanuni zaendelezwa kwa mwaka mmoja zaidi ili kuepusha kusambaa kwa Mpox
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO leo limeongeza mwaka mwingine wa utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya kimataifa ya kanuni za afya IHR kuhusu ugonjwa wa homa ya nyani au mpox ili kuzisaidia nchi zinazokabiliwa na mlipuko wa ugonjwa huo hivi sasa barani Afrika kuudhibiti. Flora Nducha na taarifa zaidi.Mapendekezo hayo yametolewa mjini Geneva Uswisi wakati wa kikao cha dharura cha makati ya kimataifa ya kanuni za afya ambacho kilitarajiwa kutangaza endapo mlipuko wa mpox ni dharura ya kimataifa ya afya ya umma ama la. Ingawa haikutangazwa hivyo mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ugonjwa huo bad oni tishio hivi sasa ukisambaa katika nchi tano za kanda ya Afrika ya WHO ambazo ni Jamhur ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambako uliripootiwa zaidi ya muongo mmoja uliopita jumla ya wagonjwa 14,000 wamethibitishwa na vifo 524.Lakini sasa ugonjwa unasambaa katikammataifa ya Uganda, Rwanda , Kenya na Burundi ambako wagonjwa 90 wameripotiwa.Amesema Nilipotangaza mwisho wa mlipukouliopita wa mpox mwaka jana, nilitoa mapendekezo ya kudumu chini ya IHR, ambayo muda wake unakaribia kuisha wiki ijayo. Nimeamua kuwaongezea mwaka mwingine ili kusaidia nchi kukabiliana na hatari ya muda mrefu ya mpox.Ikiwa ningeamua, kwa ushauri wenu kwamba hali ya sasa inawakilisha dharura ya kimataifa ya afya ya umma, ningetoa mapendekezo ya muda kwa mujibu wa Iushauri wa kamati.Hata hivyo amesema kibaya zaidi katika mlipuko wa sasa “Hatukabiliwi na mlipuko wa aina moja, tunakubwa na milipukoya aina tofauti katika nchi tofauti zenye njia tofauti za maambukizi na viwango tofauti vya hatari.”Amesisitiza kwamba ili Kukomesha milipuko hii kutahitaji hatua zilizoboreshwa na za kina, pamoja na kuizijumuisha jamii katika mapambano hayo.Amesema WHO inashirikiana na serikali za nchi zilizoathiriwa, kituco cha kudhibiti magonjwa cha Afrika CDC, mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs, asasi za kiraia na washirika wengine kuelewa na kushughulikia vichochezi vya milipuko hii.Pia Dkt. Tedros amesema WHO imeandaa mpango wa kikanda wa kukabiliana milipuko hiyo mbao unahitaji dola milioni 15 za awali ili kusaidia shughuli za ufuatiliaji, maandalizi na hatua.Ili kufadhili hatua hizo mesema “Tumetoa dola milioni 1.45 kutoka kwa hazina ya dharura ya WHO na tunapanga kutoa zaidi katika siku zijazo. Pia tunatoa wito kwa wafadhili kufadhili mpango uliosalia wa hatua.”
14-8-2024 • 2 minuten, 45 seconden
Haiti: Baada ya uchungu wa muda mrefu nashukuru nimejifungua salama, asante UNFPA
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu Haiti imekumbwa na vurugu kubwa kutoka magenge ya uhalifu na kusababisha kuzorota kwa huduma nyingi ikiwemo huduma ya afya kwa wajawazito. Ingawa hivyo, shirika la Umoja wa Mataifa ya afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA nchini Haiti linaendelea kuleta tabasamu usoni mwa wajawazito.,Video ya UNFPA inaanzia ndani ya hospitali ya Eliaza Germain ikimuonesha Jolanda akiwa kitandani na kando yake ni mtoto wake wa kiume aliyejifungua.Jolanda anasema, “huyu ni mtoto wangu wa kwanza, ana umri wa siku mbili. Niliingia chumba cha kujifungulia saa 12 asubuhi na daktari alifanya kila liwezekanalo kunisaidia kujifungua lakini kwa bahati mbaya haikwenda kama ilivyopangwa ndipo walinipeleka chumba cha upasuaji na kila kitu kikaenda sawa, mtoto wangu yuko salama kabisa.”Hata kabla ya ghasia za magenge ya uhalifu, kujifungua ilikuwa ni hatari kwani Haiti ina idadi kubwa ya zaidi ya vifo vya wazazi kwa ukanda wa nchi za magharibi. Usaidizi wa vifaa umekuwa nuru kwa wajawazito kama Jolanda na mtoto wake yu na afya njema.Akiwa amembeba mwanae, Jolanda anasema baada ya kujifungua, nilikuwa na furaha sana kwasababu huyu ndiye mtoto wangu wa kwanza. Ingawa sikuwa katika hali nzuri, kwa sababu nilijifungua kwa upasuaji. Sikuwa ninajisikia vizuri, lakini niña furaha kuwa na mtoto wangu wa kwanza.Kwa kushirikiana na wadau, UNFPA inasambaza vifaa vya matibabu kama vile dawa za kuzuia wanawake kuvuja damu baada ya kujifungua. Mwezi Juni pekee takribani wajawazito 260 walisaidiwa kwenye vituo 13 vinavyosaidiwa na UNFPA
14-8-2024 • 1 minuut, 54 seconden
14 AGOSTI 2024
Hii leo jaridani mwenyeji wako Assumpta Massoi anakupatia taarifa kuhusu mapendekezo ya kudhibiti Mpox; Harakati za UNFPA Haiti kunusuru wajawazito na watoto wachanga; vijana na kile walichoondoka nacho baada ya maadhimisho ya siku ya vijana nchini Tanzania; Mashinani ni mabadiliko chanya kwa mkulima wa kakao baada ya mafunzo kutoka ILO.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO leo limeongeza mwaka mmoja zaidi wa uzingatiaji na utekelezaji wa mapendekezo ya Kamati ya kimataifa ya kanuni za afya IHR kuhusu ugonjwa wa homa ya nyani au mpox ili kuzisaidia nchi zinazokabiliwa na mlipuko wa ugonjwa huo hivi sasa barani Afrika kuudhibiti. Flora Nducha na taarifa kamili.Tangu mwanzoni mwa mwaka huu Haiti imekumbwa na vurugu kubwa kutoka magenge ya uhalifu na kusababisha kuzorota kwa huduma nyingi ikiwemo huduma ya afya kwa wajawazito. Ingawa hivyo, shirika la Umoja wa Mataifa ya afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA linaendelea kuleta tabasamu usoni mwa wajawazito kama anavyosimulia Bosco Cosmas akimmulika Jolanda Dimanche, mama mkimbizi wa ndani nchini Haiti.Makala nampisha Cecily Kariuki ambaye amefuatilia vijana wa kitanzania walioshiriki wiki ya vijana huko Dodoma Tanzania kumulika yale waliyoondoka nayo. Kwako Cecily!! Kilimo cha mazoea cha toka enzi za mababu na mababu kimekuwa kikimuumiza mgongo na viungo vingine mkulima Yabao Oumarou nchini Cameroon bila kusahau kutumikisha watoto wake. Sasa shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO liliwapatia mafunzo ambayo matokeo yake ndio anaelezea Yabao.
14-8-2024 • 9 minuten, 58 seconden
13 AGOSTI 2024
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Sudan shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema ukatili unaoendelea dhidi ya watoto unakatisha ndoto zao , ikiwemo ubakaji na mauaji-Kikao cha kujadili iwapo mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nyani au Mpox ni dharura ya afya ya umma kimataifa kikitarajiwa kufanyika kesho, hii leo WHO inasema katika wiki za karibuni kumekuweko na ongezeko la kipekee la idadi ya nchi ukanda wa Afrika zinazoripoti wagonjwa na milipuko. Miongoni mwao ni Burundi, Kenya, Rwanda na Uganda-kuna ushahidi wa kutosha ya kwamba uhalifu wa kikatili wa kivita dhidi ya binadamu uliotekelezwa na jeshi la Myanmar ulisambaa kwa kiasi kikubwa nchini kote, imesema ripoti ya uchunguzi ya jopo huru lililoundwa na Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu kuchunguza matukio ya kipindi cha Julai mosi 2023 hadi Juni 30 wakati upinzani dhidi ya utawala wa kijeshi Myanmar uliposhamiri.-Mada kwa kina inatupeleka DRC kuangazia vijana na masuala ya kidijitali hususan changamoto wanazokumbana nazo kutokana na mzozo unaoendelea-Na mashinani tunabisha hodi Tanzania kwa kijana Emmanuel Cosmas akitujuza vijana walivyonufaika na kongamano la kitaifa la siku ya kimataifa ya vijana lililofanyika mjini Dodoma.
Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi COP29 utafanyika Baku nchini Azerbaijan kuanzia tarehe 11 hadi 22 mwezi Novemba mwaka huu wa 2024. Lengo ni kutathmini yale yaliyopitishwa mwaka jana kwenye COP28 huko Dubai, Falme za kiarabu ikiwemo hoja ya elimu ya mabadiliko ya tabianchi kwenye shule. Sasa kuelekea Baku, mwezi Novemba, mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la Elimu, Sayansi na Utamaduni yamechukua hatua kuhakikisha walimu na waelimishaji vijana wanapatiwa ufahamu wa nini wanapaswa kufundisha ili hatimaye wanafunzi wawe kichocheo cha kufanikisha hatua kwa tabianchi. Azerbaijan ambayo ndio mwenyeji wa COP29, iliitisha mkutano wa mafunzo kwa walimu vijana kuelekea kilele chenyewe mwezi Novemba. Evarist Mapesa kupitia makala hii iliyofanikishwa na Cecily Kariuki anatupitisha tufahamu kile kilichofanyika. Kwako Evarist.
12-8-2024 • 4 minuten, 5 seconden
Maonesho siku ya vijana yatoa fursa vijana kuonesha stadi za kidijitali
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya vijana mwaka huu ikibeba maudhui ya fursa za kidijitali kwa vijana kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu tunakwenda Tanzaniaambako tamasha la sikutatu linafanyika kuwatanabaisha vijana kuhusu dira ya kitaifa ya mwaka 2050 iliyodhamiria kutomwacha kijana nyuma nyuma. Vijana 3000 kutoka maeneo mbalimbali ya taifa hilo wamekusanyika makao makuu ya nchi hiyo Dodoma kusherehekea siku hii na kujadili masuala muhimu yanayowahusu. Ni yapi hayo? Afisa Mwandamizi Uwezeshaji wa Vijana katika shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA amba ni wadau wakubwa katika ajenda hiyo anaeleza kuwa " Kuanzia tarehe 10kumekuwa na mijadala mbalimbali ambayo imekuwa ikiendeshwa na wadau ikiangazia dira ya taifa ya mwaka 2050 lakini vilevile inaangazia masuala ya kidijitali ambayo ndio kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya mwaka huu."Ameongeza kuwa "tamasha hilo pia limeaangazia sera ya vija ya mwaka 2024 ambayo imeweza kuhuishwa. Mbali ya hayo kumekuwa na maonesho ya vijana kupitia mabanda mbalimbbali ambayo yameweka rasmi ili kutoa fursa kwa vijana kuweza kuonesha shughuli zao za kitaalamu, kuweza kuonesha ubunifu lakini vilevile kutoa somo kwa vijana wengine waweze kujifunza kwa kutembelea sehemu maalum mfano mashuleni, katika makundi mbalimbali ya vijana katika jamii na kuweza kutoa elimu mbalimbali kuhusu masuala ya vijana."Na kuhusu mchango wa Umoja wa Mataifa Bi. Hassan amesema "Kwa hiyo kama mashirika ya Umoja wa Mataifa tumekuwa na mchango wa moja kwa moja ili kuhakikisha kwamba Tanzania inapata sera mpya ya maendeleo ya vijana."Na miongoni mwa vijana hao 3000 walioshiriki ni Getrude Clement kutoka jopo la vijana washauri wa UNFPA anasema "Kipekee kabisa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana yamekuwa na utofauti mkubwa kutokana na kwamba tunazungumzia mambo ya kidijitali na kwa namna moja au nyingine nimeona vijana ambavyo wamejitokeza kutoa maoni yao kuhususiana na mambo ya kidijitali inaonyesha kwamba Tanzania vijana wanaelewa mambo ya kidijitali, wanaelewa mambo ya teknolojia na wanayafuatilia."
12-8-2024 • 1 minuut, 58 seconden
Hofu yatanda kutokana na ongezeko la vijana wasio na ajira, elimu au mafunzo- ILO
Hofu yatanda idadi ya vijana wasio kwenye ajira, elimu au mafunzo- ILORipoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu mwelekeo wa Ajira kwa vijana, GET for Youth, inaonesha fursa za ajira kwa vijana kwa miaka minne iliyopita ziliimarika na zinatarajiwa kuimarika kwa miaka miwili ijayo, ingawa inaonya kuwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 24 hawako kwenye ajira, elimu au mafunzo au NEET. Flora Nducha amefuatilia ripoti hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo.(Taarifa ya Flora Nducha)Hakika Assumpta! Ripoti inaanza kwa kutia matumaini hayo kwamba soko la ajira linaimarika lakini kuna dosari hiyo ya NEET yaani vijana wasio kwenye ajira, elimu au mafunzo kama alivyosema Gilbert Houngbo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO akizungumza na waandishi wa habari huko Geneva Uswisi, wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo ya 20 kutolewa.Anasema “duniani, kiwango cha NEET kiko asilimia 20.4, na NEET kwa wanawake ni asilimia 28.1 ambacho ni maradufu ya kiwango cha vijana wa kiume. Ni kwamba watu wawili kati ya watatu kwenye NEET ni wanawake.”Jambo lingine linalotia hofu ILO ambayo ndio mwandishi wa ripoti hiyo ni kwamba kuna maendeleo kidogo katika kupunguza mzigo wa vijana walio kwenye NEET duniani kote kwani kijana 1 kati ya watatu anaishi kwenye nchi ambako hakuna mwelekeo wa kupunguza kiwango hicho cha vijana wasio na ajira, elimu au mafunzoni. Ametaja nchi za uarabuni, Kaskazini mwa Afrika na Kusini mwa Asia.Bwana Houngbo anasema pia ukosefu wa kuanzishwa kwa fursa za kazi za kidijitali na hali ya ajira ya uhakika ni finyu kwani ni kijana 1 kati ya 4 katika nchi za kipato cha chini ana ajira ya uhakika ikilinganishwa na robo tatu ya wenzao katika nchi za kipato cha juu.Na piatheluthi mbili ya vijana wa nchi za kipato cha chini na kati hawana elimu ya kinachotakiwa kwenye soko la ajira. Ni kwa sababu elimu waliyo nayo ni tofauti na ajira yao.Vijana wana hofu kuwa watakuwa na maisha dhalili kuliko wazazi wao hivyo ripoti inapendekeza wasikilizwe na wapatie msaada thabiti na wa kitaasisi ili mustakabali wao uwe bora.
12-8-2024 • 2 minuten, 20 seconden
12 AGOSTI 2024
Leo ni siku ya vijana duniani na jarida kwa kiasi kikubwa linaangazia mustakabali wa vijana na ajira duniani, na huko Tanzania vijana na masuala ya kidijiltali, makala ni walimu vijana na mabadiliko ya tabianchi huko Baku, na mashinani ni harakati dhidi ya polio nchini DRC. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu mwelekeo wa Ajira kwa vijana, GET for Youth mwaka 2024, inaonesha fursa za ajira kwa vijana kwa miaka minne iliyopita ziliimarika na zinatarajiwa kuimarika kwa miaka miwili ijayo, ingawa inaonya kuwa vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 na 24 hawako kwenye ajira, elimu au mafunzo kwa kifupi NEET. Flora Nducha amefuatilia ripoti hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo.Tukiendelea na masuala ya vijana katika siku ya vijana hii leo maudhui yakiwa fursa za kidijitali kwa vijana kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu tunakwenda Tanzania ambako tamasha la siku tatu linafanyika kuwatanabaisha vijana kuhusu dira ya Taifa ya mwaka 2050 iliyodhamiria kutomwacha kijana nyuma. Kwenye makala, Evarist Mapesa anatupeleka Baku, mji mkuu wa Azerbaijan kuangazia mkutano wa 29 ulioleta pamoja walimu vijana ikiwa ni harakati za kufanikisha hatua kwa tabianchi kuelekea kilele cha COP29 mwezi Novemba mwaka huu nchini humoLokua Kanza, Balozi Mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na ushauri wa kukinga watoto dhidi ya polio.Karibu!
12-8-2024 • 9 minuten, 55 seconden
Je wajua magunzi ya msonobari ni lulu iliyofichika?
Mbegu za misonobori ni maarufu sana kwenye mapishi, lakini magunzi yake hugeuka adha kwa mazingira. Nchini Tunisia mhitimu wa Chuo Kikuu baada ya kukosa ajira alipata wazo la kutumia taka hizo kuzalisha mboji ambayo sio tu inamwongezea kipato bali pia inalinda mazingira kwa kuondoa taka na pia kuepusha wakulima kutegemea mbolea za viwandani pekee ambazo huchafua vyanzo vya maji ardhini. Wazo lake lilipata msukumo wa kiufadhili kutoka Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD na serikali ya Tunisia na tangu aanze biashara hiyo mwezi Januari mwaka huu ameshauza tani 40 na soko linazidi kupanuka. Je ni nini hasa kinafanyika? Fuatana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.
9-8-2024 • 3 minuten, 59 seconden
Maziwa ya mama ni muhimu kwa mustakbali wa mtoto
9-8-2024 • 1 minuut, 54 seconden
Watu wa asili wana haki ya kulinda utamaduni wao: Guterres
9-8-2024 • 1 minuut, 56 seconden
09 Agosti 2024
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Flora Nducha akimulika watu wa jamii ya asili, mtoto kunyonyeshwa maziwa ya mama, matumizi ya magunzi ya msonobari kutengeneza mboji salama na mashinani ni ujumbe wa mshairi mashuhuri duniani kutoka nchini Marekani.Kulinda haki za watu wa jamii ya asili za kujitenga kwa ridhaa na kuishi maeneo yao asilindio ujumbe wa mwaka huu wa siku ya kimataifa ya watu wa jamii ya asili dunia, ujumbe ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni sahihi na kila mtu anapaswa kuuzingatia.Afisa wa UNICEF nchini Tanzania akionesha kivitendo kile wanachohamasisha kwa akina mama yaani kunyonyesha watoto wao maziwa ya mama pindi wanapojifungua.Katika makala, Assumpta Massoi anamulika ni kwa vipi magunzi ya mbegu za msonobari yamegeuka lulu huko Tunisia na kuwa chanzo cha kipato kwa mhitimu wa Chuo Kikuu aliyekaa miaka 6 bila ajira.Ujumbe wa mshairi Amanda Gorman kuhusu vita inayoendelea huko Gaza na madhara yake kwa watoto.
9-8-2024 • 10 minuten, 46 seconden
Usitishaji uhasama ni lazima Gaza kutokana na ongezeko la hali za dharura
7-8-2024 • 1 minuut, 33 seconden
Maji ni changamoto kubwa kwa wakazi wa Gaza: UNICEF
7-8-2024 • 1 minuut, 50 seconden
07 AGOSTI 2024
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani, WHO na lile la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA, yamezungumzia umuhimu wa sitisho la mapigano huko Gaza ili kufanikisha utoaji wa chanjo kwa watoto dhidi ya magonjwa hatarishi kama vile polio-Maji safi na salama imekuwa ni mtihani mkubwa Gaza na kutishia milipuko ya magonjwa limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF huku likifanya kila jitihada kusaidia waathirika-Makala leo inammulika kijana Willy Ng'ang'a kutoka Kenya anayetumia sayansi kutatua changamoto za mazingira katika jamii kwa kutumia dungusikakati kusafisha maji-Na mashinani tunaelekea Jijini Dhaka, Bangladesh kusikia ushauri wake Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bi Gwyn Lewis kwa wananchi Bangladesh kuhusu jinsi ya kulijenga upya taifa lao.
7-8-2024 • 9 minuten, 59 seconden
06 AGOSTI 2024
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Baada ya wiki kadhaa za maandamano makubwa na machafuko yaliyosababisha vifo vya zaidi ya vijana na raia 300 #Bangladesh sasa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Gwyn Lewis, amesema kufikia leo utulivu kiasi umerejea nchini Bangladesh -Nchini Uingereza ambako maandamano yaliyochochewa na taarifa potofu na za uongo yanazidi kusambaa Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi amesema ghasia hizo ikiwemo dhidi ya wasaka hifadhi zinashtusha na kila mtu bila utofauti wowote ana haki ya kujihisi salama kwenye jamii zao na kuishi huru bila hofu-Leo ikiwa ni miaka 79 tangu MArekani iangushe bomu la atomiki la nyuklia huko Hiroshima nchini Japani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ni ajabu kuwa silaha hizo na tishio lake la kuzitumia bado havijaondolewa kwenye matumizi. -Mada kwa kina leo inamulika juhudi za Tanzania katika kutumia sayansi na teknolojia kusongesha lengo namba 16 la maendeleo endelevu linalohusu masuala ya sheria na haki.-Na mashinani tunabisha hodi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR katikashule ya Bombouthi ambayo inalishukuru shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa juhudi za kurejesha elimu
6-8-2024 • 10 minuten, 27 seconden
GAZA: Kutoka Gaza hadi Abu Dhabi kupata matibabu sahihi
Tangu kuanza kwa mzozo huko Ukanda wa Gaza mwezi Oktoba mwaka jana 2023 baina ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas mzozo ambao umesababisha vifo vingi, majeruhi, watu kupoteza kila kitu na wengine kutekwa, wiki iliyopita Ukanda huo umeshuhudia uhamisho mkubwa zaidi wa wagonjwa ambao wamepelekwa kupatiwa matibabu nje ya nchi.Jumla ya wagonjwa na majeruhi walio mahututi 85 wamefanikiwa kuondolewa kutoka Ukanda wa Gaza kwenda Abu Dhambi katika Falme za kiarabu katika operesheni iliyotajwa kuwa “ngumu sana” iliyotekelezwa kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO wakishirikiana na serikali ya Falme za kiarabu UAE pamoja na wadau wengine. Leah Mushi anatujuza zaidi katika makala haya.
5-8-2024 • 4 minuten, 32 seconden
Hofu yatanda mzozo Mashariki ya Kati kusambaa zaidi
Kamishina Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za binadamu Volker Türk leo ameonya juu ya ongezeko la hatari ya kusambaa kwa mzozo Mashariki ya Kati na kuzitaka pande zote husika kutoa kipaumbele cha kuwalinda raia. Flora Nducha na taarifa zaidiAsante Assumpta. Katika taarifa yake fupi iliyotolewa mjini Geneva Uswis Kamishina Mkuu Türk amesema “Nina wasiwasi mkubwa juu ya hatari inayoongezeka ya mzozo mkubwa zaidi Mashariki ya Kati na ninazisihi pande zote husika katika mzozo huu, pamoja na nchi zenye ushawishi, kuchukua hatua za haraka ili kudhibiti hali hii ambayo imekuwa ni ya hatari sana.”Amesisitiza kuwa kwa hali yoyote ile “Haki za binadamu na hasa ulinzi wa raia lazima iwe kipaumbele cha kwanza.”Kamishina Mkuu huyo wa Haki za binadamu amesema tayari, katika kipindi cha miezi 10 iliyopita ya mzozo huo, raia wengi wao wakiwa wanawake na watoto wamevumilia madhila na mateso yasiyoweza kuvumilika kutokana na mabomu na mtutu wa bunduki unaorindima kila uchao.Hivyo amesema “Kila kitu, na ninamaanisha kila kitu, lazima kifanyike ili kuepusha hali hii kusambaa zaidi na kutumbukia kwenye shimo ambalo litakuwa na matokeo mabaya zaidi kwa raia.”Tangu mzozo huo kuanza Oktoba 7 mwaka jana shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema zaidi ya watu 38,000 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 88,000 kujeruhiwa huku mateka zaidi ya 110 bado wanashikiliwa.
5-8-2024 • 1 minuut, 35 seconden
05 AGOSTI 2024
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea-Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameonya juu ya ongezeko la hatari ya kusambaa kwa mzozo Mashariki ya Kati na kuzitaka pande zote husika kutoa kipaumbele cha kuwalinda raia-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania limetumia ukurasa wake wa X, kuelezea mambo muhimu matatu ya manufaa ya maziwa ya mama kwa mtoto. -Makala yetu leo inatupeleka Gaza ambako shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO limesema wagonjwa 85 kutoka Gaza wamesafirishwa kwenda kupata matibabu huko Abu Dhabi katika Falme za kiarabu.-Na mashinani mwanaharakati Plamedie Ndaya kutoka Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, anawashauri wanawake wa Afrika kupigania kutambuliwa kwa haki zao.
5-8-2024 • 9 minuten, 53 seconden
Utipatipwa waongezeka miongoni mwa watoto barani Afrika
Utipwatipwa ni tatizo la afya la kimataifa na linalokua kwa kasi sana barani Afrika. Kati ya mwaka 2000 na 2016, idadi ya watu wazima wenye utipwatipwa au uzito wa kupindukia barani Afrika ilikaribia kuongezeka maradufu, na mwenendo huo huo sasa unaonekana kwa watoto. Cecily Kariuki wa Idhaa hii kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO amefuatilia kile ambacho mashirika ya Umoja wa MAtaifa na wadau wanafanya ili kukabiliana na changamoto hiyo ya kiafya duniani. Kwako Cecily!
2-8-2024 • 3 minuten, 28 seconden
Utapiamlo una waathiri watoto wa Sudan
Njaa na utapiamlo unaenea kwa viwango vya kutisha nchini Sudan huku takribani watoto milioni 3.6 wakikakabiliwa na utapiamlo. Wataalamu wa lishe huko Darfur Kaskazini wanaendelea kusaidia familia kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na wadau wake. Hata hivyo suluhisho la uhakika ni usitishaji wa mapigano ili kuweza kuruhusu misaada ya kibinadamu kufikia wote wenye uhitaji. Taarifa ya Bosco CosmasHali ya lishe kwa watoto ni ngumu sana katika maeneo mengi ya Darfur Kaskazini nchini Sudan kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo pamoja na hali mbaya ya kiuchumi jambo linalowaweka watoto mtegoni, kupata magonjwa ya lishe ikiwemo utapiamlo. UNICEF na wadau wengine wa afya, wanafanya kazi kuhakikisha watoto wanapata tiba stahiki.Halima ni mtaalamu wa lishe huko kitongoji cha Tawila, Darfur kaskazini anasimulia hali ilivyoHALIMA – Sabrina“Nimefanya kazi katika masuala ya lishe tangu mwaka 2017. Watoto wanasumbuliwa sana na utapiamlo. Hakuna chakula cha kutosha kutokana na ugumu wa maisha wanaopitia familia nyingi za Darfur, familia hazina pesa ya kutosha kununua aina mbalimbali za vyakula, kwahiyo mtoto anaweza aina moja tu ya kwa mwezi mzima kama vile, uji. Hakuna matunda wala mboga mboga ama kitu chochote jambo linalosababisha utapiamlo.”Mbali na changamoto wazipatazo watoto, Halima anaeleza magumu anayopitia katika utendaji kazi wake.HALIMA – Sabrina“Ninafanya hii kazi ya kusaidia maisha ya Watoto, tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba hatujapokea mshahara wetu, hapa tupo wanne tu na tunafanya kazi usiku na mchana. Tunawapatia maziwa yenye virutubisho na pia matibabu kwa watoto wanaoharisha na kutapika na matibabu mengine ya kila siku. Hatuna vikonge wala majagi ya kutosha, tunatumia majagi ya kutengenezea maziwa, inaumiza sana kutokuwa na vitendea kazi hivi, iwapo hakutakuwa na chakula cha tiba wala maziwa ya tiba kwa ajili ya kuwapa hawa watoto itakuwa vigumu sana kuwapatia matibabu watoto hawa. Tunawafundisha wazazi hatua za kuchukua wawapo majumbani mwao na pia tunawafundisha kuhusu usafi na lishe. Tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha tunawapatia dawa na kuokoa maisha ya watoto huku tukiwa na matumaini kuwa watakuwa na afya njema na kupona utapiamlo”UNICEF Pamoja na wadau wengine wa afya wanaendelea kusambaza misaada ya lishe kwa watoto wenye utapiamlo hata katika maeneo ya vita ili kuendelea kuokoa maisha ya watoto hao ambao wapo hatarini zaidi. Misaada hiyo inawanufaisha zaidi ya watoto 240,000 wenye utapiamlo, katika mji wa Darfur.
2-8-2024 • 1 minuut, 58 seconden
Joto laua watu 175,000 barani Ulaya kila mwaka, na idadi yaweza kuongezeka - WHO
Viwango vya joto barani Ulaya vinaongezeka maradufu hivi sasa na kuwa vya juu wakati huu ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO linasema watu 175,000 wanakufa kila mwaka barani humo kutokana na joto kali na idadi hiyo inaweza kuongezeka. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Kote barani Ulaya, zaidi ya nchi 50 zinagharimika zaidi, amesema Mkurugenzi wa WHO kanda ya Ulaya Dkt.t Hans Kluge, siku chache tu tangu dunia ivunje rekodi ya joto na kufikia nyuzijoto 17.16 katika kipimo cha Selsiyasi, huku mawimbi ya joto ya kiangazi yakivuma kote, katika ukanda wa kaskazini mwa dunia.Akifafanua madhara ya hali hiyo, Robb Butler ambaye ni Mkurugenzi wa WHO akihusika na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Mazingira na Afya amesema,“katika bara la Ulaya joto kali ni sababu kuu ya vifo vinavyochochewa na tabianchi. Viwango vya juu vya joto kama tunavyovipata hivi sasa vinaongeza magonjwa makali kama vile moyo, mfumo wa kupumua, ubongo, afya ya akili, pamoja na kisukari. Joto kali pia ni tatizo kubwa pia kwa wazee hasa wanaoishi peke yao, na linaweza kuwa mzigo wa ziada kwa wajawazito.”Anasema tayari nchi 20 barani Ulaya zina mipango ya utekelezaji kuhusu afya na joto ili kuhakikisha jamii ziwe na mnepo sasa na siku za usoni dhidi ya joto kali.Sasa hapo ulipo unaweza kufanya nini kujinasua na joto? WHO inasema, epuka kuwa nje wakati wa jua kali, weka nyumba katika hali ya ubaridi, kunywa maji ya kutosha na vaa nguo nyepesi na pia jijali wewe na wengine bila kusahau wazee.
2-8-2024 • 1 minuut, 45 seconden
02 AGOSTI 2024
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Leah Mushi anakuletea -Joto laua watu 175,000 barani Ulaya kila mwaka, na idadi yaweza kuongezeka limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO-Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, watoto milioni 3.6 wanakabiliwa na utapiamlo mkali nchini Sudan-Katika makala Afrika ina asilimia 28 ya watoto wenye utipwatipwa duniani walio na umri wa chini ya miaka 5. Sasa mashirika ya Umoja wa Mataifa ya WHO, UNICEF, na Muungano wa Afrika wanapambana na tatizo hilo la kimataifa-Na katika mashinani shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema limeongeza hatua za dharura za kusaidia wananchi waliokumbwa na baa la njaa Darfur Sudan
2-8-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Neno Kangaya
Katika kujifunza Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “KANGAYA”
1-8-2024 • 1 minuut, 7 seconden
1 Agosti 2024
Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa ambalo leo linaletwa kwako na Flora Nducha ambalo kwanza linaanza na muhtasari wa habari unaoangazia njaa nchini Sudan, kuanza kwa wiki ya unyonyeshaji duniani na watoto wa Gaza kuanza kufundishwa kwa njia mbadala ambayo sio madarasani. Kisha utasikiliza mada kwa kina kutoka Bahrain inayoangazia uchumi wa rangi ya chungwa, ukijulikana pia kama uchumi utokanao na ubunifu, na mwisho utajifunza kiswahili hii leo utapata maana ya neno Kangaya.
1-8-2024 • 10 minuten
Wanangu wanakula na kuvaa sababu ya mradi wa UNHCR wa ufugaji wa inzi: Mkimbizi Francine
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Zimbabwe kwa ufadhili wa Benki ya Dunia limeanzisha mradi wa kuwasaidia wakimbizi wakulima na wafugaji katika kambi ya wakimbizi ya Tongogara nchini humo. Mradi huo wa majaribio ni wa ufugaji wa inzi kwa ajili ya kutengeneza chakula cha mifugo kama kuku. Wanufaika wakubwa ni wakimbizi wa kambini hapo. Je wananufaika vipi? Ambatana na Flora Nducha akimmulika mmoja wa wanufaika hao mkimbizi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, katika makala hii
31-7-2024 • 3 minuten, 13 seconden
UNAIDS yatoa mafunzo ya kujikinga na UKIMWI kwa vijana nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI UNAIDS nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR linahamasisha jamii kupamba na na UKIMWI kwa kutoa elimu ya ngono salama kwa vijana. (Taarifa ya Cecily Kariuki)Takwimu za UNAIDS zinaonesha watu milioni 30.7 wanaoishi na Virusi vya UKIMWI - VVU sasa wanapata matibabu. Hii ni hatua kubwa katika afya ya umma ambayo pia imepunguza takriban nusu ya vifo vinavyohusiana na UKIMWI tangu mwaka 2010, kutoka zaidi ya milioni moja hadi 630,000 mwaka 2023. Hata hivyo vifo hivyo ni vingi ikilinganishwa na lengo la kuwa na vifo 250,000 ifikapo mwaka 2025.UNAIDS wanasema mwaka 2023 kulikuwa na wastani wa maambukizi mapya ya VVU milioni 1.3 na takriban nusu ya walioambukizwa wanaishi mashariki na kusini mwa Afrika (35%) huku magharibi na Afrika ya kati wakiwa na maambukizi kwa asilimia 15%.Ni kutokana na takwimu hizi ndio maana Mkurugenzi wa UNAIDS, nchini CAR Chris Fontaine akaona haja ya kutoa elimu kwa vijana.Chris Fontaine – Bosco“Vita na umaskini vimesababisha vifo vingi vya mapema nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, na matokeo yake, ni kuwa asilimia 78 ya idadi ya watu, ni chini ya umri wa miaka 35. Vijana hawa wanakabiliana na changamoto kubwa kupata elimu bora; kwa mfano, ni watu 4 kati ya 10 tu wa Kati ya Afrika ambao wanaweza kusoma na kuandika Ukosefu wa usawa wa kijinsia na ukatili wa kijinsia umewaacha wanawake katika hali hatarishi zaidi kwa VVU.”Miongoni mwa waliopatiwa mafunzo katika Kituo cha Elimu kwa Afya ya Jinsia kwa Vijana, CISJEU ni Gniwali Ndangou.Gniwali Ndangou - Sabrina“Mimi ni yatima, ni mimi pekee kati ya ndugu zangu watatu ambaye ninapata matibabu kila siku na ninakunywa dawa bila kuacha. Ninaishi na VVU tangu nilipozaliwa. Zaidi ya mara moja, nilijaribu kujiua kwa kunywa vidonge.”Gniwali Ndangou ambaye sasa ni mwalimu rika wa CISJEU amekuwa mstari wa mbele katika juhudi za kupambana na UKIMWI.
31-7-2024 • 1 minuut, 38 seconden
Maelfu ya wapalestina washikiliwa na mamlaka za Israeli bila kujulikana waliko
Hii leo ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, imechapisha ripoti kuhusu mamlaka za Israeli kukamata wapalestina kiholela na kwa muda mrefu tangu mwezi Oktoba mwaka jana akiwemo mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 80 mwenye ugonjwa wa kusahau. Assumpta Massoi amepitia ripoti hiyo na kuandaa taarifa ifuatayo. (Taarifa ya Assumpta Massoi)Ripoti ni ya kurasa 23 ikiweka bayana machungu wanayopitia wale wanaoshikiliwa na Israeli, halikadhalika ikinyooshea mkono vikundi vilivyojihami vya kipalestina, ikiwemo Hamas ambao wanashikilia mateka wa Israeli tangu vita ianze Oktoba 7 mwaka jana.Wapalestina walikamatwa wakati wamesaka hifadhi kwenye shule, hospitail, nyumbani au kwenye vituo vya ukaguzi wakati idadi kubwa ya wapalestina walikuwa wanahama kutoka kaskazini mwa Gaza kuelekea kusini.Miongoni mwao ni mwanamke huyo wa umri wa zaidi ya miaka 80 pamoja na wasichana, wavulana, na wanaume wasiohusiana na vikundi vilivyojihami.Jeremy Laurence, Msemaji wa Ofisi hiyo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu anasema, ripoti inajumuisha madai ya kuteswa na kutendewa vibaya na aina nyingine za ukatili. Mahabusu wanashikiliwa kwenye maeneo kama vizimba, wanavuliwa nguo zote na kuachwa na nguo ya ndani pekee kwa muda mrefu, mbwa wakiachiliwa wawang’ate, wananing’inizwa kwenye dari na pia kuna ripoti za ukatili wa kijinsia na kingono wanapokuwa wanashikiliwa.”Mamlaka za Palestina kwa upande wake zimeripotiwa kukamata kiholela watu huko Ukingo wa Magharibi ili kuzuia kukosolewa na upinzani wa kisiasa.Bwana Laurence anasema sheria ya kimataifa inataka wale wanaoshikiliwa watendewe kiutu na kibinadamu na inakataza mateso au aina nyingine ya ukatili.Hivyo anasema, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu. Volker Türk, anasisitiza wito wake wa kuachiliwa mara moja kwa mateka wote wanaoshikiliwa Gaza. Wapalestina wote wanaoshikiliwa kiholela na Israeli lazima waachiliwe huru.Kamishna Mkuu Türk ametaka pia uchunguzi wa haraka, huru na wa kina wa matukio yote yaliyosababisha ukiukwaji wa sheria ya kimataifa, na kuhakikisha wahusika wanawajibishwa na kwamba manusura na familia zao wapatiwe haki yao ya fidia. TAGS: Haki za binadamuAdditional: Amani na UsalamaNews: Gaza, Palestina, IsraeliRegion: Mashariki ya KatiUN/Partner: OHCHR
31-7-2024 • 1 minuut, 57 seconden
31 Julai 2024
Hii leo katika jarida la Umoja wa Mataifa Leah Mushi anakuletea taarifa mbalimbali ikiwemo ripoti kuhusu mamlaka za Israeli kukamata wapalestina kiholela na kwa muda mrefu tangu mwezi Oktoba mwaka jana, juhudi za UNAIDS kuelimisha vijana nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR jinsi ya kujikinga na UKIMWI. Makala utasikia kuhusu ufugaji nzi weusi kwa ajili ya chakula cha mifugo na mashinani utasikia jinsi UNICEF inavyosaidia jamii huku Timbuktu nchini Mali kupambana na utapiamlo hususan kwa watoto.
31-7-2024 • 9 minuten, 54 seconden
30 JULAI 2024
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Fora Nducha anakuletea-Gaza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA linasema watoto wengi wako hatarini kuambukizwa ugonjwa wa homa ya ini aina ya A -Venezuela ambako kulifanyika uchaguzi wa Rais Jumapili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amepongeza azma ya wananchi kwa kuelezea utashi wao kwa amani kupitia sanduku la kupigia kura-Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO inasema msichana barubaru 1 kati ya 6 waliokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi mwaka jana, alikumbwa na ukatili wa kimwili au kingono kutoka kwa mpenzi wake-Katika mada kwa kina tuko Jamhuriya Kidemkrasia ya Congo DRC ambako shirikala mpango wa chakula duniani WFP laleta nuru kwa wakimbizi wa ndani Magina-Na mashinani katika kuadhimisha siku ya kupinga usafirishaji haramu wa binadamu duniani utapata ujumbe kutoka kwa IOM Khazakstan kuhusu jinsi ya kuzuia usafirishaji haramu wa watoto kupitia mtandao
30-7-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Mkimbizi Sudan Kusini atumia stadi za ujasiriamali kuhudumia familia yake
Zaidi ya watu 1,000 wanaokimbia vita nchini Sudan wanavuka mpaka na kuingia nchini Sudan Kusini kila siku, na hivyo kuvipatia shinikizo vituo vya mpito vilivyoko mji wa mpakani wa Renk nchini Sudan Kusini. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linasema idadi kubwa ni wakimbizi wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani ambao wamekuwa wakiishi Sudan tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwao Sudan Kusini. Miongoni mwao ni Juma Peter Gai ambaye yeye na familia yake sasa wameamua kusalia Renk. Mapito na changamoto zao ndio msingi wa makala hii inayowasilishwa kwako na Assumpta Massoi.
29-7-2024 • 3 minuten, 51 seconden
WFP yasaidia wakulima nchini Kenya kuchangamkia kilimo biashara
Jitihada za kujikomboa na janga la njaa bado zinaendela nchini Kenya, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kupitia kituo cha huduma kwa wakulima likiwapa wakulima elimu ya namna sahihi ya kuongeza uzalishaji licha ya changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo na hasa kwa kukumbatia kilimo biashara.(Taarifa ya Bosco Cosmas)Kilimo ni uti wa mgongo kwa jamii nyingi sana za Afrika, ndivyo ilivyo katika nchi ya Kenya ambapo wakulima wamekuwa wakipitia changamoto kubwa ya uzalishaji kutokana na majanga ya asili yanayoendelea nchini humo ikiwemo mafuriko.Shirika la WFP kupitia mpango wake wa huduma kwa wakulima, limeweza kumsaidia mkulima Farah ambaye hapo awali alikumbana na uzalishaji hafifu kwaajili ya matumizi ya chakula na sasa amehimizwa kwenda mbali zaidi ya mlo wa kila siku kwa kuingia katika kilimo biashara.Uelewa wa kilimo biashara si mkubwa lakini Farah, anasimama kidete huku akionesha nita yake ya kuondoa njaa.(CUT, FARAH )“Lengo langu ni kuboresha uhakika wa chakula katika nyumba yangu, cha pili ni kuingia kwenye biashara, cha tatu kuondoa njaa nchini Kenya.”WFP kupitia mradi wake, imeweza kubadili fikra za Farah kuhusu kilimo(CUT, FARAH )“Tangu nilipozaliwa, nilikuta baba yangu akifanya shughuli za kilimo lakini sio cha kisasa, lakini mwaka jana baada ya WFP kutambulisha mpango mpya wa huduma kwa wakulima imesaidia kutuinua. Tulikuwa hatufanyi kilimo kama biashara kwa sababu tulikuta baba zetu wanafanya hivyo.”Katika mradi huo WFP inafanya kazi kwa kushirikiana na wadau wa kilimo ili kuimarisha uhakika na uzalishaji wa mazao kwa ajili ya lishe bora na kusaidia wakulima sio tu kuweka mlo mezani bali kilimo pia kuwaingizia fedha kwa kukigeuza kuwa kuwa biashara.
29-7-2024 • 2 minuten, 3 seconden
Watu 97 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa katika mashambulizi Al- Fasher Sudan, UN yalaani vikali
Takriban raia 97 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kwenye mashambulizi katika hospitali, maeneo ya makazi na soko la mifugo kwenye Jiji la Al Fasher katika Jimbo la Darfur Kaskazini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Clementine Nkweta-Salami. Flora Nducha na taarifa zaidi(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Asante Leah katika taarifa hiyo aliyoitoa mjini Port Sudan Nkweta- Salami amelaani vikali muaji hayo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki . Amesema "Nimehuzunishwa sana na mashambulizi haya ya kutisha dhidi ya raia na miundombinu ya kiraia kama vile hospitali, nyumba na masoko. Miundombinu ya kiraia haipaswi kamwe kulengwa na inalindwa chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu. Umoja wa Mataifa nchini Sudan unalaani vikali mashambulizi haya ya kiholela na tunatuma rambirambi zetu kwa familia zilizopoteza wapendwa wao.”Ameongeza kuwa mashambulizi hayo ya Al Fasher yamewashtukiza watu kwani mji ulikuwa umetulia kwa karibu wimbi mbili hali iliyoruhusu masoko kufunguliwa na familia nyingi kuendelea na maisha.Kurejea kwa hali ya kuweza kutafuta riziki kwa watu na shughuli nyingine za kiuchumi, ufikishaji wa msaada wa kibinadamu usiozuiliwa na ongezeko la ufadhili wa kibinadamu ni muhimu kwa Sudan ili kuepusha tishio linalokuja la njaa. Amesema Nkweta- Salami.Ameendelea kusema kuwa nchi hiyo inakabiliwa na viwango vibaya zaidi vya uhaba wa chakula katika historia yake, huku zaidi ya nusu ya wakazi wake sawa na watu milioni 25.6 wakiwa na njaa kali, wengine milioni 8.5 wanakabiliwa na viwango vya dharura vya njaa na wakati zaidi ya watu 755,000 wako katika hali ya janga katika majimbo ya Darfur, Kordofan Kusini na Kaskazini, Blue Nile, Al Jazirah, na Khartoum.Tangu kuzuka kwa mzozo mpya Aprili mwaka jana zaidi ya watu 18,800 wameuawa, zaidi ya 33,000 kujeruhiwa na watu zaidi ya milioni 10 wamezikimbia nyumba zao na miongini mwao zaidi milioni 5 wakivuka mpka na Kwenda kusaka usalama nchi za jirani.Nkweta-Salami ametoa wito kwa pande zote katika mzozo huo kukomesha mapigano mara moja na kuwalinda raia kwa gharama yoyote.
29-7-2024 • 1 minuut, 58 seconden
29 JULAI 2024
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akiangazia shambulio huko Sudan, kilimo biashara nchini Kenya. Makala inakupeleka Sudan Kusini harakati za mkimbizi aliyefurushwa mara mbili na sasa amerejea nyumbani na mashinani ni huko Paris Ufaransa kunakofanyika michezo ya olimpiki ya majira ya joto.Takriban raia 97 wameripotiwa kuuawa au kujeruhiwa kwenye mashambulizi katika hospitali, maeneo ya makazi na soko la mifugo kwenye Jiji la Al Fasher katika Jimbo la Darfur Kaskazini, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Clementine Nkweta-Salami. Flora Nducha na taarifa zaidiJitihada za kujikomboa na janga la njaa bado zinaendela nchini Kenya, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kupitia kituo cha huduma kwa wakulima likiwapa wakulima elimu ya namna sahihi ya kuongeza uzalishaji licha ya changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo na hasa kwa kukumbatia kilimo biashara.Makala: Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR anakupeleka nchini Sudan Kusini kusikia mkimbizi aliyelazimika kurejea nyumbani baada ya vita kuzuka nchini Sudan mwezi Aprili mwaka jana wa 2023.Mashinani: Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake (UN Women) Sima Bahous, akitoa kauli yake kuhusu kuwatambua na kuwapa fursa sawa wanariadha wa kike. Karibu!
29-7-2024 • 10 minuten
Perina Nakang alenga kushinda Olimpiki kuinua timu na familia yake
Perina Nakang, ni mmoja wa wanariadha 37 wanaounda timu thabiti ya wakimbizi kwenye michezo ya Olimpiki iliyoanza leo Julai 26 huko Paris, Ufaransa. Familia yake ilikimbia Sudan Kusini kwa sababu ya vita yeye akiwa na umri wa miaka 7 na kufika kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Sasa ana umri wa miaka 21, akikimbia mbio za mita 800 ambapo katika mazoezi alimaliza kwa muda wa dakika 2 na sekunde 12 na lengo lake ni kufikia muda wa dakika 2 na sekunde 10. Assumpta Massoi katika makala hii iliyoandaliwa na UNHCR anamulika safari yake ya mazoezi na ndoto yake Perina.
26-7-2024 • 3 minuten, 41 seconden
Guterres: Pongezi IOC kwa kuendelea kujumuisha wanariadha wakimbizi kwenye Olimpiki
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko Paris Ufaransa kuhudhuria ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto mwaka 2024 amezungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach na kuipongeza kamati hiyo kwa kuendelea kuwajumuisha wakimbizi wanamichezo. Flora Nducha amefuatilia hotuba hiyo na kuandaa ripoti ifuatayo.Hakika Leah! Hotuba ya Katibu Mkuu imeoanisha michezo ya Olimpiki na amani na jinsi ilivyoweza kuwapatia fursa wanamichezo waliofurushwa makwao kutokana na vita kuweza kuonesha vipaji vyao kwenye michezo hiyo.Guterres amesema napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa kile ambacho Kamati hii ya Olimpiki imefanya kwa kuruhusu timu ya wakimbizi kushindana kwa mara nyingine tena kwenye michezo ya Olimpiki.Amesema yeye alikuwa Kamishna Mkuu wa wakimbizi kwa miaka 10 na ni muhimu sana kutomwacha mtu yeyote nyuma, na zaidi kutowaacha nyuma wale waliolazimika kukimbia, kuacha nchi zao na wana haki sawa ya kushiriki michezo kama raia wengine wa dunia.Amezungumzia pia umuhimu wa nchi zilizo kwenye mizozo kuzingatia sitisho la kwanza kabisa la mapigano wakati wa michezo ya Olimpiki karne ya 8 huko Ugiriki ili kuepusha mashambulizi wakati wa michezo.Guterres amesema tunaishi katika dunia iliyogawanyika, ambako mizozo inaendelea kwa kiasi kikubwa kuanzia Ukraine hadi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Hivyo amesema katika zama kama hizo, ni muhimu kusema kuzingatia sitisho hilo la mapigano la kwanza duniani.Amesisitiza kuwa michezo ya Olimpiki inapoanza ni wakati wa kukumbusha dunia kuzingatia sitisho hilo la mapgano ili kuifanya dunia itambua umuhimu wa kunyamazisha silaha.Katibu Mkuu ametaka nchi zote duniani zishikamane pamoja kama ilivyo kwa wanamichezo wa Olimpiki ambao wanacheza bila kujali tofauti zao.Michezo ya olimpiki ya majira ya joto inaanza Julai 26 hadi tarehe 11 Agosti, ikifuatiwa na ile ya watu wenye ulemavu itakayoanza tarehe 28 Agosti hadi tarehe 8 Septemba nchini Ufaransa
26-7-2024 • 1 minuut, 50 seconden
26 Julai 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ufunguzi wa michezo ya Olimpiki na Jitihada za pamoja za kukabiliana na changamoto za afya ya umma barani Afrika. Makala tutasalia nchini Paris katika michezo ya Olimpiki na mashinani tunasikia mafunzo kushusu ulemavu wa kutosikia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko Paris Ufaransa kuhudhuria ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto mwaka 2024 amezungumza katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach na kuipongeza kamati hiyo kwa kuendelea kuwajumuisha wakimbizi wanamichezo.Jitihada za pamoja za kukabiliana na changamoto za afya ya umma zinazidi kuboresha upatikanaji na utoaji wa huduma za afya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kanda ya Afrika kwa kushirikiana na nchi wanachama na washirika wake linaendelea kutimiza ajenda yake ya mabadiliko ili kuimarisha mifumo ya afya na kuongeza misaada kwa nchi katika ukanda wa Afrika.Makala inamulika mmoja wa wanariadha wanaowakilisha timu ya wakimbizi kwenye michezo ya olimpiki iliyoanza leo Paris, Ufaransa. Safari yake na matumaini yake akilenga kukimbia mbio za mita 800 kwa dakika 2 na sekunde 10 badala ya dakika 2 na sekunde 12.Na mashinani Dkt. Kaitesi Batamuliza Mukara, Mshauri wa masuala ya masikio, kusikia na uangalizi wa macho kutoka Ofisi ya kikanda barani Afrika ya Shirika la Afya Duniani, WHO akieleza juhudi za shirika hilo za kusaidia watu wenye changamoto ya kusikia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
26-7-2024 • 10 minuten
WHO yafanikiwa kuboresha afya ya umma barani Afrika
Jitihada za pamoja za kukabiliana na changamoto za afya ya umma zinazidi kuboresha upatikanaji na utoaji wa huduma za afya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO kanda ya Afrika kwa kushirikiana na nchi wanachama na washirika wake linaendelea kutimiza ajenda yake ya mabadiliko ili kuimarisha mifumo ya afya na kuongeza misaada kwa nchi katika ukanda wa Afrika.Miaka kumi iliyopita, mlipuko wa Ebola ulifichua udhaifu katika mifumo ya afya barani Afrika, kutoka maandalizi na mwitikio wa dharura hadi kudumisha huduma za kawaida za afya.Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti anasema sasa wanajivunia mafanikio makubwa yaliyoifikiwa katika kuboresha sekta ya afya kwa umma barani Afrika.“Tunakuwa WHO ambayo wadau wengi wanataka iwe. Kwa kutumia vyema rasilimali na utaalamu wetu, tunatengeneza mabadiliko endelevu na chanya, kuongeza matokeo na kuzidisha uaminifu kama mshirika wa thamani.”WHO Afrika, imetoa mifano kadhaa kati ya mafanikio mengi yaliyofikiwa, madhalani muda wa kudhibiti magonjwa ya milipuko umepungua kwa kiwango kikubwa, kutoka siku 418 mwaka 2016, hadi siku 40 kufikia mwaka 2020.Mapambano dhidi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele ya kitropiki pia yanaongezeka kasi. Nchi 19 za Afrika zimeondoa angalau ugonjwa mmoja wa kitropiki usiopewa kipaumbele.Dkt Daniel Kyabanyize ambaye ni mkurugenzi wa afya kwa umma nchini Uganda anatoa ushuhuda wa mafanikio ya ushirikiano na WHO Afrika.“Katika tukio la hivi karibuni, tulikuwa na mlipuko mkubwa wa Ebola nchini Uganda ambao ulianzia katikati ya nchi na tuliweza kushughulikia na kumaliza janga hilo bila ya kuenea katika nchi zilizo jirani yetu.”Msaada wa WHO katika ukanda wa Afrika’ tayari umeimarisha maisha ya watu wengi. Kwa ushirikiano thabiti kutoka kwa nchi wanachama na washirika, ukanda wa Afrika utaendelea kupata mafanikio makubwa zaidi ya afya ya umma.Jitihada nyingine ni katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga na mkuu wa mkoa wa Kabadjougou, nchini Côte d'Ivoire Rene Famy amezipokea kwa shukrani kubwa, “Nina furaha kwamba Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni limekubali kutuunga mkono katika mapambano dhidi ya vifo vya akina mama wakati wa kujifungua.”Wafanyakazi waliopata mafunzo mazuri ni muhimu kwa huduma za afya na WHO Afrika inaweka juhudi za kuimarisha ujuzi wa wafanyakazi wa afya katika ukanda huo kwa kusaidia katika mafunzo.Profesa Marycelin Baba, Mkurugenzi wa Maabara ya Kitaifa ya Polio Maiduguri, nchini Nigeria anasema kuwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi huchangia moja kwa moja katika maendeleo ya nchi. “Wanafunzi wengi wamepata ujuzi na maarifa. Wanafunzi wa tiba na wanafunzi wa taaluma za huduma za dharura wote wamefaidika. Hiyo ni maendeleo ya binadamu, ambayo hayawezi kamwe kupuuzwa. Kwa sababu kinachofanya nchi iwe na maendeleo ni binadamu.” ParaphraseMsaada wa WHO katika ukanda wa Afrika tayari umeimarisha maisha ya watu wengi. Kwa ushirikiano thabiti kutoka kwa nchi wanachama na washirika, ukanda wa Afrika utaendelea kupata mafanikio makubwa zaidi ya afya ya umma.
26-7-2024 • 2 minuten, 1 seconde
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa methali “Lakupita lapishwa.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, Mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Lakupita lapishwa.”
25-7-2024 • 1 minuut, 7 seconden
25 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya kimataifa ya kuzuia watu kuzama majini na tunakupeleka nchini Tanzania kufuatilia suala hili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Ethiopia, Bangladesh kusini mwa Afrika. Pia tunakuletea ufafanuzi wa msemo “Lakupita lapishwa.”Idadi ya watu Ethiopia waliokufa baada ya matukio matatu ya maporomoko ya udongo kusini mwa Ethiopia yaliyochochewa na mvua kubwa imeongezeka na kufikia 257 jana Jumatano huku idadi ikitarajiwa kufikia 500, na kwamba watu zaidi ya 15,000 wanatakiwa kuhamishwa. Imesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA.Maandamano ya kupinga serikali yakiendelea nchini Bangladesh ambako zaidi ya watu 160 wakiwemo polisi wameripotiwa kuuawa, wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu wameitaka serikali ya Bangladesh iache mara moja msako dhidi ya waandamanaji na wapinzaji wa kisiasa, irejeshe mtandao wa intaneti na iwajibike na ukiukwaji wa haki za binadamu.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema ukame mkali unaokumba eneo la kusini mwa Afrika unatishia mamia ya maelfu ya watoto kwenye nchi sita zilizoathiriwa vibaya zaidi na ukame kukabiliwa na utapiamlo uliokithiri. Nchi hizo ambazo zimetangaza janga la uhaba wa chakula kitaifa kutokana na ukame ni Lesotho, Botswana, Malawi, Namibia, Zambia na Zimbabwe.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, Mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Lakupita lapishwa.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
25-7-2024 • 9 minuten, 56 seconden
Viazi lishe vimetukomboa na mafunzo ya FAO yametuimarisha
Nchini Tanzania, hususan mkoa wa Singida ulioko katikati kwa taifa hilo la Afrika Mashariki, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO linaendelea na harakati zake za kuhakikisha taifa hilo la Afrika Mashariki linafanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, likiwemo lile la kwanza la kutokomeza njaa na la pili la kutokomeza umaskini yanafikiwa. Miongoni mwa harakati za karibuni ni mradi wa pamoja wa kuongeza kasi ya uwezeshaji wanawake kiuchumi vijijini unaotekelezwa wilaya ya Ikungi, mkoani humo ambapo wanaume wanashirikiana pia na wake zao kwenye shughuli za kilimo shambani. Makala ya leo imemmulika mmoja wa wanaume hao akiwa shambani mwake, huku Afisa ugani wilayani Ikungi akifafanua utekelezaji wa mradi huo.
24-7-2024 • 3 minuten, 47 seconden
Madaraja yaliyojengwa na UNMISS yaondolea adha wananchi nchini Sudan Kusini
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umefadhili ujenzi wa madaraja matatu huko Yubu, Turbiwa na Bundri kwenye kaunti ya Tambura jimboni Equitoria Magharibi. Lengo la ujenzi huo kupitia miradi ya matokeo ya haraka au QIPs, ni kurahisisha kurudi nyumbani kwa hiari kwa wakimbizi waliofurushwa makwao.Madaraja hayo matatu yanalenga kuwaunganisha watu, kuimarisha mshikamano wa kijamii, na kuboresha upatikanaji wa huduma za afya, shule, na masoko halikadhalika utekelezaji wa jukumu la ulinzi wa raia.Benina Mbiko, mama wa watoto watano, anaamini kwamba daraja hilo litaongeza biashara na hivyo kuinua uchumi na zaidi ya yote..."Kwetu sisi tulio kijijini, huwa ni vigumu kuja mjini wakati wa msimu wa mvua kwa sababu maji yanapokuwa mengi, hatuwezi kuvuka mto. Daraja hili ni zuri sana, asante kwa wale waliojitokeza kutujengea." Kwa wengi, miundombinu mipya inayonufaisha jamii nzima ni ishara ya maendeleo yanayokuwa kama anavyoeleza Chifu Mkuu wa Kijiji cha Tambura, Mboribamo Renzi.Anasema daraja hili litasaidia jamii kwa jumla katika nyanja za kilimo, kusafirisha bidhaa zao hadi sokoni, kurahisisha usafiri wa wagonjwa kutoka vijijini hadi mjini, kuimarisha usalama; na haya yote ni sehemu ya maendeleo.”Kwa upande wake, Mwakilishi wa UNMISS, Anthony Moudie, alisisitiza athari chanya za mradi kama huu akisema..‘‘Daraja hili litasaidia au kurahisisha ulinzi wa raia wa pande zote mbili. Litasaidia serikali kupeleka vyombo vya usalama kuhakikisha kuwa raia wanakuwa salama. Pia, daraja hili litafanikisha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa pande zote mbili.’’UNMISS imesema itaendelea kufadhili baadhi ya miradi midogo inayodhaniwa kuwa na uwezo wa kuboresha kwa kiasi kikubwa maisha ya jamii za maeneo ambako miradi hiyo inatekelezwa.
24-7-2024 • 2 minuten, 4 seconden
24 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti mpya ya Hali ya Uhakika wa Chakula na Lishe Duniani SOFI, na miundombinu yanayofadhiliwa na UNMISS nchini Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Chad, kulikoni?Takriban watu milioni 733 walikabiliwa na njaa mwaka 2023, hii ikiwa ni sawa na mtu 1 kati ya 11 duniani na mtu mmoja kati ya watano barani Afrika, kulingana na ripoti mpya ya Hali ya Uhakika wa Chakula na Lishe Duniani SOFI, iliyochapishwa leo na mashirika matano ya Umoja wa Mataifa.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umefadhili ujenzi wa madaraja matatu huko Yubu, Turbiwa na Bundri kwenye kaunti ya Tambura jimboni Equitoria Magharibi. Lengo la ujenzi huo kupitia miradi ya matokeo ya haraka au QIPs, ni kurahisisha kurudi nyumbani kwa hiari kwa wakimbizi waliofurushwa makwao.Makala inatupeleka mkoa wa Singida ulioko katikati mwa Tanzania kumsikia mnufaika wa mafunzo kilimo cha viazi lishe yaliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO nchini humo. Mnufaika huyo ambaye atajitaja jina lake, anazungumza akiwa katikati ya shamba lake la matuta ya viazi lishe.Na katika mashinani ikiwa tangu mwezi Aprili mwaka jana wa 2023, zaidi ya watu takribani laki 5 wakiwemo watoto zaidi ya laki 3 wamekimbia Sudan na kuvuka mpaka na kuingia Chad, mmoja wao ni Roumaiza, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 ambaye anaeleza matumaini anayoyapata sasa katika kambi ya wakimbizi nchini Chad ambayo inahudumiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) pamoja na wadau wengine.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
24-7-2024 • 9 minuten, 58 seconden
UN Ripoti SOFI: Watu takriban milioni 733 walikabiliwa na njaa 2023
Takriban watu milioni 733 walikabiliwa na njaa mwaka 2023, hii ikiwa ni sawa na mtu 1 kati ya 11 duniani na mtu mmoja kati ya watano barani Afrika, kulingana na ripoti mpya ya Hali ya Uhakika wa Chakula na Lishe Duniani SOFI, iliyochapishwa leo na mashirika matano ya Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo ya kila mwaka iliyozinduliwa nchini Brazili katika mkutano wa mawaziri wa nchi 20 zenye kipato cha juu duniani au G-20 imeonya kwamba dunia iko mbali sana kufikia lengo la 2 la Maendeleo Endelevu, la kutokomeza njaa, ifikapo mwaka 2030.Pia inafichua kwamba dunia imerudi nyuma miaka 15, huku viwango vya utapiamlo vikilinganishwa na vile vya mwaka 2008-2009.Ripoti inasema licha ya maendeleo kiasi yaliyopigwa katika maeneo maalum kama vile kudumaa na kunyonyesha mtoto maziwa ya mama pekee, viwango vya njaa duniani vimedorora kwa miaka mitatu mfululizo, na mwaka 2023, kulikuwa na watu milioni 152 zaidi wenye utapiamlo kuliko mwaka 2019.Kwa mmujibu wa mashirika matano ya Umoja wa Mataifa yaliyoandaa ripoti hiyo lile la chakula na kilimo FAO, la mpangowa chakula duniani WFP, la ufadhili wa maendeleo ya kilimo IFAD, la kuhudumia watoto UNICEF na la afya duniani WHObara linaloongoza kwa ongezeko la watu wenye njaa ni Afrika kwa asilimia 20.4, Asia asilimia 8.1 na Amerika ya Kusini asilimia 6.2.Ripoti hiyo imegawanyika katika sehemu tatu: Mosi viasharia vya njaa ambapo inasema upatikanaji wa chakula unaendelea kuwa mtihani kwa mamilioni ya watu, ukosefu wa fursa za kiuchumi za kupata mlo kamili ni changmoto kubwa ,watoto kuzaliwa na uzito mdogo na kudumaa ni matatizo sugu na katika muongo uliopita kumekuwa na ongezeko kubwa la utipwatipwa.Pili imetaja sababu za ongezeko la njaa kuwa ni mfumuko wa bei, vita na mabadiliko ya tabianchi.Na tatu nini kifanyike: Ripoti inapendekeza uwekezaji ili kufadhili kukomesha njaa, uhaba wa chakula na aina zote za utapiamlo.Na imeonya kwamba ikiwa hali ya sasa itaendelea, takriban watu milioni 582 watakuwa na utapiamlo sugu ifikapo 2030, nusu yao wakiwa barani Afrika.
24-7-2024 • 1 minuut, 56 seconden
23 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika maoni ya vijana kuhusu SDGs, mmoja wao ni Monicah Malith Mkimbizi nchini Kenya kutoka Sudan Kusini akieleza alichotoka nacho kwenye mkutano wa HLPF. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu imelaani ukimbizi wa mara kwa mara utokanao na amri za kuhama zinazotolewa na jeshi la Israeli dhidi ya raia huko kaskazini mwa Khan Younis, Ukanda wa Gaza.Barani Afrika, mashambulizi mapya yanayofanywa na vikundi vilivyojihami dhidi ya raia huko mashariki mwa Burkina Faso yamelazimu maelfu ya watu hao kukimbilia nchi jirani ya Niger ili kusaka usalama, wakati huu ambapo hali ya dharura inazidi kushamiri kwenye taifa hilo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.Na hatimaye michezo ya olimpiki ya majira ya joto mwaka 2024 inaanza Ijumaa hii huko Paris, UFaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma ujumbe wake.Mashinani ikiwa jana Julai 22 Ripoti mpya kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi ilitolewa, hivyonampa fursa Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS Winnie Byanyima akitahadhrisha kuhusu kuongeza kasi ya vita dhidi ya ukimwi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
23-7-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Wafugaji Samburu: Ngamia sio tu wamenusuru familia zetu, pia wametufungulia ukurasa mpya
Kauti ya Samburu Kaskazini mwa Keny ni miongoni mwa maeneo mengi yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Jamii ya Wasamburu kwa kawaida ni wafugaji, baada ya ukame kukatili maisha ya mifugo yao haswa ng’ombe na mbuzi wakazi wengi walipoteza matumaini hadi pale FAO ilipowaletea mradi wa ufugaji wa ngamia kama mbadala wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Nankaya Lepitiling, mwanachama wa kikundi cha wanawake cha Salato Samburu ambaye ameona faida ya ufugaji wa ngamia kupitia mradi wa FAO, anasema “Tumewaonna ngamia kwa mda mrefu kwenye kikundi chetu, na mimi niimeshakuwa kiongozi wa kikundi cha Salato, tulipewa ngamia wa mradi, wanafika karibu ngamia 30 hivi”Ntomuan Selaina naye ni mnufaifa wa mradi huo..“Wametusaidia sana kwa chakula cha watoto, hakuna shida hata kidogo, hata chai wengine wanakunywa ya siturungi nami nakunywa ya maziwa , nawapatia pia watu wengine na sasa kuna huyu mtoto amekuja hapa kwa sababu mama yake hana maziwa tunampatia ya ngamia wngu.”Kwamujibu wa FAO ukame ulichochea ongezeko la utapiamlo na magonjwa mengine ya ukosefu wa lishe bora hususan miongoni mwa watoto ndio FAO ikachukua hatua kwa kuanza kugawa ngamia kupitia mradi wa ubunifu wa PEAR ambao pia unawapa wafugaji mafunzo . Timothy Lesingran ni mtaalam wa wanyama katika mradi huo wa PEAR“Tunatoa mafunzo kwa wanawake na tumewafunza wanawake wengi tuu katika ngazi mbalimbali na wengi wamefurahia sana kufanyakazi nasi.”Pia mradi huu umewapa wanawake hawa wafugaji fursa nyingine kama wanavyosema Ntomuan na Nangaya,“Hata vikapu tunavyotumia kukamua maziwa tunavishona wenyewe na tunaviuza pesa tunayopata tunanunua chakula cha kutulisha sisi na watoto wetu. Na tangu tulipopata ngamia tena tukenda kujenga mahali pengine duka la maziwa sasa tunakamua maziwa , tunayaweka kwenye mashine, tunachuja mafuta , tunauza maziwa freshi na mazia lala, na tunatengeneza peremende ya jibini ya maziwa ya ngamia”Mradi huu wa FAO umewalenga zaidi wanawake na familia zinazogawiwa ngamia zimewajibika kutia saini mkabata unaosema ngamia waliyepokea ni wa mama wa familia hiyo, lakini faida kubwa imekuwa kwa familia nzima na hasa watoto kama Juma Lesaina mtoto wa Ntomuan, anasema mama (PARAPHRASE)“Alininunulia sare za shule kutokna na maziwa aliyopata ya ngamia na ndipo nilipoweza kujiunga na shule kwa msaada wa ngamia, na nimesomea uhandisi wa masualaya umeme , hivyo nimefika hapa nimatokeo ya ngamia na watu waliona ngamia maisha yao yamebadilika.”FAO sasa imepanua wigo wa mradi huo katika kaunti zingine za jirani ikiwemo Isiolo na lengo ni kuzifikia kaunti nyingi zaidi za wafugaji.
22-7-2024 • 3 minuten, 9 seconden
WFP: Sera rafiki zinawainua kiuchumi wakimbizi nchini Uganda
Je wafahamu kuwa Uganda ndio nchi inayohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika? Na sera rafiki za maendeleo za nchi hiyo zinawapa wakimbizi fursa ya kuzalisha chakula chao wenyewe.Mmoja wa wanaofaidi sera hizo ni Jeniffer mkimbizi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC ambaye anaeleza ni muhimu kwa wakimbizi kuzalisha chakula chao wenyewe.“Niliondoka DR Congo sababu ya vita. Ninapokea Msaada wa chakula kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP lakini ukweli ni kuwa chakula hicho hakitoshi ndio maana nikahamia kwenye kilimo.”Wakimbizi milioni 1.6 wanapatiwa hifadhi nchini Uganda, idadi hii ni mara nne zaidi ya idadi ilivyokuwa muongo mmoja uliopita. Wakimbizi wanapatiwa fursa ya kumiliki ardhi na kuyafikia masoko na hii inawapa fursa ya kuzalisha chakula chao wenyewe“Nilikuwa mkulima nilipokuwa nchini kwangu na hapa niliungana na wananchi wa hapa pamoja na wakimbiziwengine na tukaanza kilimo cha mbogamboga. Tunashirikiana na wazawa na sote tunafundishana, tunalima nyanya, kabichi, maharage na matikiti maji. Mwezi uliopita niluza mazao yang una kupata dola 140, nilitumia fedha hizo kununua chakula na kukodisha ardhi zaidi ya kilimo.”WFP inafanya kazi na wakimbizi na jamii zinazowakaribisha kujenga jamii zenye ustahimilivu.
22-7-2024 • 1 minuut, 33 seconden
22 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya juhudi za kutokomeza ukimwi, na miradi ya WFP kwa wakimbizi nchini Uganda. Makala tunamulika faida ngamia kkwa wafugaji nchini Kenya, na mashinani tunaangazia ziara za Fillipo Grandi nchini Ukraine.Ripoti mpya iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS na muungano wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi unaojumuisha mashirika mbalimbali, inaonyesha kwamba dunia iko katika wakati muhimu wa kubaini endapo viongozi wa dunia watatimiza ahadi zao za kumaliza janga la ukimwi kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030.Je wafahamu kuwa Uganda ndio nchi inayohifadhi idadi kubwa ya wakimbizi barani Afrika? Na sera rafiki za maendeleo za nchi hiyo zinawapa wakimbizi fursa ya kuzalisha chakula chao wenyewe. Mmoja wa wanaofaidi sera hizo ni Jeniffer mkimbizi kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC ambaye anaeleza ni muhimu kwa wakimbizi kuzalisha chakula chao wenyewe.Makala tunakwenda kauti ya Samburu Kaskazini mwa Kenya ambayo ni miongoni mwa maeneo mengi yaliyoathirika na ukame kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Jamii ya Wasamburu kwa kawaida ni wafugaji, baada ya ukame kukatili maisha ya mifugo yao haswa ng’ombe na mbuzi wakazi wengi walipoteza matumaini hadi pale FAO ilipowaletea mradi wa ufugaji wa ngamia kama mbadala wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.Na mashinani tunamsikia Fillipo Grandi, Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambaye amehitimisha ziara yake mwishoni mwa wiki nchini Ukraine kushuhudia matokeo ya mlipuko wa hivi karibuni wa hospital ya Okhmatdyt.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
22-7-2024 • 9 minuten, 52 seconden
Tanzania, Kenya na Uganda zasonga mbele kuzuia maambukizi ya UKIMWI kwa watoto- UNAIDS
Ripoti mpya iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na ukimwi UNAIDS na muungano wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi unaojumuisha mashirika mbalimbali, inaonyesha kwamba dunia iko katika wakati muhimu wa kubaini endapo viongozi wa dunia watatimiza ahadi zao za kumaliza janga la ukimwi kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030. Ripoti hiyo, iliyotolewa mjini Geneva na Munich inasisitiza uharaka wa kuchukua hatua kwani ukimwi uko njiapanda na inatanabaiisha, takwimu mpya na tafiti zinazoonyesha kwamba maamuzi na uchaguzi wa sera vinahitajika sasa.Inasema utoaji wa haraka wa huduma za VVU pekee ndio utakaotimiza ahadi ya kukomesha UKIMWI kwa watoto ifikapo 2030.Ripoti hiyo”Kubadili maono kuwa hali halisi” inaonyesha kwamba janga la Ukimwi linaweza kumalizika ifikapo 2030, endapo viongozi wa dunia wataongeza rasilimali na kulinda haki za binadamu hivi sasa.Kwani inaonyesha kuwa programu maalum zinazolenga maambukizi ya VVU zimesaidia kuepusha maambukizi milioni 4 miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 0-14 tangu mwaka 2000.Ulimwenguni kote, maambukizi mapya ya VVU miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka 0-14 yamepungua kwa asilimia 38 tangu mwaka 2015 na vifo vimepungua kwa asilimia 43.Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima amesema"Ninapongeza maendeleo ambayo mataifa mengi yanapata katika kusambaza huduma za VVU ili kuwapa afya bora wanawake vijana na kuwalinda watoto wachanga na watoto wengine dhidi ya VVU. Kwa dawa na sayansi zilizopo leo, tunaweza kuhakikisha kuwa watoto wote wanazaliwa na kuishi bila VVU, na kwamba watoto wote wanaoishi na VVU wanapata huduma na kusalia kwenye matibabu. Huduma za matibabu na kinga lazima ziongezeke mara moja ili kuhakikisha kuwa zinawafikia watoto wote kila mahali. “Ameongeza kuwa Hatuwezi kupumzika kwani kifo cha mtoto yeyote kutokana na sababu zinazohusiana na UKIMWI sio tu janga, lakini pia hasira. Ninakotoka, watoto wote ni watoto wetu. Ulimwengu unaweza na lazima utimize ahadi yake ya kukomesha UKIMWI kwa watoto ifikapo 2030.”Miongoni mwa nchi 12 za muungano wa kimataifa wa kutokomeza ukimwi, kadhaa zimefanikisha upatikanaji wa matibabu ya kudumu ya dawa za kuongeza mud awa kuishi miongoni mwa wanawake wajawazito na wanaonyonyesha wanaoishi na VVU, huku Uganda ikikaribia asilimia 100, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 98, na Afrika Kusini kwa asilimia 97, Msumbiji imefikia asilimia 90, Zambia asilimia 90, Angola na Kenya kwa asilimia 89, Zimbabwe kwa asilimia 88, na Cote d'Ivoire kwa asilimia 84.
22-7-2024 • 1 minuut, 59 seconden
WHO: Polio mwiba mpya kwa watu wa Gaza, wahudumu wa kibinadamu wanaonya
Wananchi wa Gaza wakikabiliwa na machungu ya kila namna, kugunduliwa kwa tishio la ugonjwa wa polio unaoambukiza sana unaohusishwa na hali mbaya ya usafi iliyosababishwa na mzozo unaoendelea kumekuwa kama chumvi kwenye kidonda.Katika taarifa aliyoitoa Christian Lindmeier, msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi leo amesema virusi vya polio (VDPV2) vimepatikana katika maeneo sita katika sampuli za maji taka zilizokusanywa tarehe 23 mwezi Juni kutoka katika maeneo ya Khan Younis na Deir al Balah huko Ukanda wa Gaza."Ni muhimu kutambua virusi vimetengwa kutoka kwenye mazingira kwa wakati huu tu; hakuna tukio lolote lililogunduliwa la kupooza linalohusiana na haya," amewaambia waandishi wa habari.Kama sehemu ya juhudi za kukabiliana na hali hiyo, WHO katika eneo linalokaliwa la Palestina tayari inafanya kazi na mamlaka ya afya ya eneo hilo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) na washirika wanatathimini ni kwa ukubwa kiasi gani virusi hivyo vya polio vimeenea.“Kazi hii itaamua hatua zinazohitajika kukomesha kuenea zaidi, "ikiwa ni pamoja na kampeni za chanjo za haraka", msemaji wa WHO ameeleza.Virusi vya polio mwitu vilitokomezwa zaidi ya miaka 25 iliyopita katika Gaza kutokana na kampeni ya kina ya chanjo. WHO inasema chanjo kabla ya vita ilikuwa asilimia 95 mwaka 2022.Lakini zaidi ya miezi tisa ya vita, kuhama mara kwa mara kwa watu wengi na "kuharibika kwa mfumo wa afya, ukosefu wa usalama, viuzuizi, uhamisho wa mara kwa mara wa watu, uhaba wa vifaa vya matibabu, uduni wa ubora wa maji na vyoo dhaifu" vimeunda "mazingira bora” kwa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kuenea na polio ni moja kati ya hayo amebainisha Christian Lindmeier wa WHO.Leo huko Gaza, ni hospitali 16 tu kati ya 36 ambazo zinafanya kazi kwa kiasi, na 45 kati ya vituo 105 vya huduma ya afya ya msingi ndivyo vinafanya kazi, kulingana na afisa huyo wa WHO, ambaye amesisitiza kuwa ni usitishaji wa mapigano tu ndio utakaoruhusu kuongezeka kwa kasi kwa shughuli za chanjo "kushughulikia mapungufu yaliyotokana na vita vinavyoendelea".
19-7-2024 • 1 minuut, 45 seconden
Monicah Malith: Hizi ndizo sababu zimenifanya kusomea sheria katika Chuo Kikuu cha Nairobi
Katika makala hii Anold Kayanda Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Monicah Malith mmoja wa vijana waliofika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria Jukwaa la Kisiasa la Ngazi za Juu la Umoja wa Mataifa (HLPF) mwaka 2024. Monicah Malith aliikimbia nchi yake Sudan Kusini na kuingia Kenya. Kupitia makala hii anaeleza kwa nini aliamua kuisoma kozi anayoisoma sasa katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwani ana matumaini kozi hiyo itasaidia kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.
19-7-2024 • 2 minuten, 51 seconden
19 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia tishio la polio Gaza, na kauli za chuki zinazoweza kusababisha mauaji ya kimbari na ukosefu wa amani. Makala tunaangazia vijana kutoka Uganda katika mkutano wa HLPF hapa makao makuu, na mashinani tunakupeleka nchini Somalia, kulikoni?Wananchi wa Gaza wakikabiliwa na machungu ya kila namna, kugunduliwa kwa tishio la ugonjwa wa polio unaoambukiza sana unaohusishwa na hali mbaya ya usafi iliyosababishwa na mzozo unaoendelea kumekuwa kama kuongeza chumvi kwenye kidonda.Alice Wairimu Nderitu mashauri maalum wa Umoja wa Mataifa katika kuzuia auaji ya kimbari akizungumza na UN New Kiswahili hivi karibuni na huku akitoa raia kuhusu mauaji hayo na kutaka kila mtu kumakinika na kuchukua hatua.Katika makala Anold Kayanda anazungumza na Monicah Malith mmoja wa vijana waliofika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuhudhuria Jukwaa la Kisiasa la Ngazi za Juu la Umoja wa Mataifa (HLPF) mwaka 2024. Monicah Malith aliikimbia nchi yake Sudan Kusini na kuingia Kenya. Kupitia makala hii anaeleza kwa nini aliamua kuisoma kozi anayoisoma sasa katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwani ana matumaini kozi hiyo itasaidia kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs.Na mashinani Fosiya Ibarahim Botan mkulima katika kijiji cha Erigavo nchini Somalia akitueleza jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, linasaidia wakulima kujikimu kimaisha kupitia msaada wa fedha taslimu, elimu na uundaji wa vyama vya mikopo vya akiba vya vijiji.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
19-7-2024 • 9 minuten, 57 seconden
Alice Nderitu: Kauli za chuki na mauaji ya kimbari ni lila na fila havitengamani
Alice Wairimu Nderitu mashauri maalum wa Umoja wa Mataifa katika kuzuia auaji ya kimbari akizungumza na UN New Kiswahili hivi karibuni na huku akitoa raia kuhusu mauaji hayo na kutaka kila mtu kumakinika na kuchukua hatua.“Ningependa watu wajue kwamba mauaji ya kimbari huwa hayafanyiki bila mpango. Na wenye kupanga huwa wanajua wale watu wanaopanga kuwaangamiza ni lazima kwanza wawatoe utu , wawaonyeshe kwamba wao sio binadamu. Na ndio maana huwa wanaitwa mende kama walivyokuwa wakiwaita Watutsi, au chawa kama walivyowaita watu wa Rohingya au watu wachafu kama walivyokuwa wanawaita watu wa Yazid huko Iraq. Na kila mtu akisikia watu wanaitwa haya majina ya wanyaka inafaa wajue mpango unaweza kuwepo, na huo mpango unaweza kuwa ni wa mauaji ya kimbari.”Akaenda mbali zaidi na kusisitiza kuwa,“Kwa hivyo kila mtu achukulie kauli za chuki kwa uzito mkubwa. Kama tungependa kuishi kama watu walio na utu na tungependa kurejesha utu duniani , tuendelee kuwasaka walio na utu ndio tuweze kuwachukulia hatua wale wanaotoa kauli za chuki, kuzungumza nao na kuwafunza watoto na kufunza watu wengi kwenye hii dunia maana ya kauli za chuki sababu nisingependa watu wasahau ya kwamba hakuna mauaji ya kimbari yalishafanyika bila kauli za chuki. Hatungependa yale yaliyofanyika Rwanda yatokee tena. Hivyo kama hatutaki yafanyike tena tukumbuke kwamba kauali za chuki zinatuelekeza sote kwenye mauaji ya kimbari.
19-7-2024 • 1 minuut, 54 seconden
18 JULAI 2024
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -WFP limeonya kwamba amri ya hivi karibuni kabisa ya Jeshi la Israel ya watu kuondoka Gaza imesababisha idadi kubwa zaidi ya watu kutawanywa tangu mwezi Oktoba mwaka jana.-Leo ni siku ya kimtaifa ya Nelson Mandel mwaka huu ikibeba maudhui “Bado ni jukumu letu kutokomeza njaa na pengo la usawa” -Hatua za haraka zinahitajika kuhakikisha haki za binadamu katika vituo vya rumande nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kuleta Utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA. -Mada yetu kwa kina leo inaangazia siku ya Mandela na jinsi watu wanavyomfahamu na kuenzi mchango wake-Na matika jifunze Kiswahili tunakupeleka Baraza la Kiswahili Zanzibar BAKIZA nchini Tanzania kupata ufafanuzi waneno HAZAMA
18-7-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Edem Wosornu: Watu wa Haiti wanaomba mambo matatu
Wakati wa ziara ya siku nne nchini Haiti hivi karibuni, Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utetezi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Dharura (OCHA), Edem Wosornu ametembelea maeneo kadhaa ya miradi ya misaada ya kibinadamu na kukutana na jamii zilizoathirika, mamlaka za Haiti, pamoja na washirika wa kitaifa, kimataifa na wa ndani, kujadili janga la kibinadamu nchini humo pamoja na mikakati zaidi ya misaada ya dharura.Akieleza hali aliyoikuta Bi Wosornu anasema, “Watu wa Haiti wanaomba mambo matatu. Wanaomba amani, wanaomba ghasia za magenge zikome, wanaomba kurejeshewa nchi yao.”Ziara hiyo inakuja wakati ambapo Haiti inakabiliwa na mgogoro ambao umezidi kuwa mbaya zaidi tangu Machi mwaka huu kukiwa na vurugu mpya katika mji mkuu, Port-au-Prince. Kwa mujibu wa OCHA, zaidi ya watu 578,000 kwa sasa wamekimbia makazi yao nchini Haiti, na zaidi ya shule 900 zimefungwa tangu Januari mwaka huu yaani zaidi ya nusu mwaka.Anaeleza alichozungumza na watoto akisema,"Watoto nilioshirikiana nao huko Gonaives, huko Les Cayes lakini pia huko Port-au-Prince, wanaomba kuweza kurejea shuleni. Watoto niliokutana nao wanataka kuwa madaktari, wanataka kuwa wanasheria, wanataka kuwa walimu, wanataka kuwa wauguzi. Watu wa Haiti wamechoshwa na ghasia. Watu wa Haiti wanataka kurejea katika maisha yao.”Emile Macier, mkuu wa shule ya Joseph Bernard des Frères ya mjini Port-au-Prince kwa masikitiko anaeleza,“Maelfu ya wanafunzi wananyimwa masomo. Nani anajua, labda magenge yamewachukua. Nia yangu kubwa ni kwamba tutafute sehemu nyingine ya kuwahifadhi waliofurushwa ili shule ifanye kazi. Hatuwezi kufunga shule. Je, itakuwaje kwa watoto? Huwezi kujua magenge yamewawajiri wangapi? Huweze kujua wasichana wangapi walibakwa na kupata mimba. Hatujui.”Kwa upande wa afya nako hali ni tete kama alivyojionea Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utetezi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Dharura (OCHA), Edem Wosornu,“Tunatakiwa kuhakikisha kuwa vituo vya afya vya nchi hii vina uwezo wa kuwasaidia wananchi. Tunahitaji kuhakikisha kuwa miundombinu ya elimu ina uwezo wa kusaidia watu. Suluhu za muda mrefu zinahitajika za haraka na za muda mfupi.Bi Wosornu anaeleza kwamba, Bi Wosornu anaeleza kwamba, "Watu milioni 1.6 kati ya watu milioni 5 ambao wana uhaba wa chakula katika nchi hii wanahitaji sana usaidizi. Nchi inayozalisha maembe na ndizi na viazi vikuu na ndizi na nchi ambayo ina udongo halisi, wenye rutuba na wenye rutuba haipaswi kuwa na uhaba wa chakula. Vurugu lazima zikome ili kuruhusu watu kurudi kwenye mashamba yao, ili waweze kuishi maisha yao.Ni nini kifanyike? Wosornu anaeleza,"Wadau wa misaada ya kibinadamu ni sehemu ya suluhisho, lakini pia tunahitaji washirika wa maendeleo kwa mbinu za muda mrefu. Tunahitaji suluhu za pamoja, sio tu kutoka kwa sehemu moja ya mwavuli wa usaidizi, lakini kutoka kwa nyanja zote tofauti za mambo.”
17-7-2024 • 3 minuten, 7 seconden
UN: Hali inaendelea kuwa kizungumkuti Gaza mashambulizi yakishika kasi
Hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya Gaza huku leo mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yakiripoti kuendelea kwa mashambulizi yanayokatili maisha ya watu na kuathiri miundombinu ya raia kuanzia kwenye shule hadi vituo vya afya huku maelfu ya watu wakiendelea kukabiliwa na ukosefu wa huduma za msingi ikiwemo afya, makazi, maji na chakula kadri vita vinavyoendelea. Asante Leah nikianza na shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO ambalo leo limeendelea kusihi pande zinazozozana kwenye Ukanda wa Gaza kuheshimu sheria za kimataifa na kulinda vituo vya afya na wahudumu wa afya linasema tangu Oktoba 7 mwaka jana mzozo huu mpya ulipozuka limeorodhesha mashambulizi zaidi ya 1000 kwenye vituo vya afya katika eneo hilo linalokaliwa la Palestina.Hivyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X limesema “Tunatoa ombi la ulinzi wa wahudumu wa afya na vituo vya afya kwa ajili ya fursa za kuweza kutoa msaada wa kibinadamu na mapigano lazima yakome mara moja.”Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA likiunga mkono usitishwaji wa mapigano mara moja kwa minajili ya kibinadamu limesema Watoto wa Ukanda wa Gaza wameporwa utoto wao na mustakbali wao, elimu imegeuka ndoto na madhila ya kiafya ni tishio lingine.Philippe Lazzarini Kamishina Mkuu wa UNRWA ameandika kwenye ukurasa wake wa X kwamba “Karibu kila siku kuna mashambulizi dhidi ya vituo vya elimu. Takribani shule 8 zimeshambuliwa katika siku 10 zilizopita zikiwemo shule 6 za UNRWA. Vita vimewapora wasichana na wavulana wa Gaza utoto wao na elimu yao.”Ameongeza kuwa changamoto za afya ni mtihani mwingine unaotishia mustakbali wa watoto wa Gaza akimtolea mfano mvulana wa umri wa miaka minne akisema “ Mvulana huyu anaugua magonjwa ya ngozi kutokana na hali mbaya ya familia yake, wakilala katika mahema yaliyoezekwa kwa karatasi za plastiki bila kupata vifaa vya usafi au maji safi ya kutosha hii ni hatari kubwa. Timu zetu za UNRWA zinatoa dawa, lakini bila ya hali kuboreka, maambukizi ya magonjwa yanarudi tena”.Amesisitiza kwamba ili madhila yote haya yaishe ni lazima vita vikome mara moja.
17-7-2024 • 1 minuut, 57 seconden
17 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na huduma za afya kwa watoto na wanawake nchini Afghanistan. Makala inatupeleka nchini Haiti na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Hali ya kibinadamu inaendelea kuwa mbaya Gaza huku leo mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yakiripoti kuendelea kwa mashambulizi yanayokatili maisha ya watu na kuathiri miundombinu ya raia kuanzia kwenye shule hadi vituo vya afya huku maelfu ya watu wakiendelea kukabiliwa na ukosefu wa huduma za msingi ikiwemo afya, makazi, maji na chakula kadri vita vinavyoendelea.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF nchini Afghanistan limeweka programu maalum ya mama na watoto inayotolewa na waajiriwa wanawake ambao huwafanyia uchunguzi na kuwatibu watoto wenye utapiamlo na pia kuwafundisha wakina mama namna ya kuandaa chakula chenye lishe bora kwa watoto waoMakala inaangazia ziara ya siku nne nchini Haiti aliyoifanya hivi karibuni Mkurugenzi wa Uendeshaji na Utetezi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Dharura (OCHA), Edem Wosornu.Mashinani Inatupeleka katika kaunri ya Marsabit nchini Kenya kusikia ujumbe wa Amina Godana ambaye ni Msaidizi wa chifu, na Halima Somo, Mwanachama wa kikundi cha raia wanaohakikisha uwepo wa amani na utangamano wakieleza ni kwa jinsi gani Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limeziwezesha jamii za kijiji chao kuondokana na usafirishaji haramu wa binadamu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
17-7-2024 • 9 minuten, 59 seconden
UNICEF nchini Afghanistan inatoa huduma za lishe bora kwa wanawake na watoto
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF nchini Afghanistan limeweka programu maalum ya mama na watoto inayotolewa na waajiriwa wanawake ambao huwafanyia uchunguzi na kuwatibu watoto wenye utapiamlo na pia kuwafundisha wakina mama namna ya kuandaa chakula chenye lishe bora kwa watoto wao.Video ya UNICEF inaanza kwa kuwaonesha wanawake watatu kila mmoja akiwa amembeba mtoto wakielekea katika kituo cha afya kinachotoa virutubisho vya lishe kila siku. Mmoja wa wanawake hao ni Khatira Salemii. Anasema, “katika kituo hichi, wamempa mwanangu chakula cha lishe, baada ya kuhuduhuria kwa takriban mara tano au sita walimpima uzito na urefu wake na nilishukuru waliponiambia ni sasa mtoto wangu mwenye afya tena”.Mjini Kabul, vituo vya afya mara nyingi huwa na msongamano mkubwa wa watu au wafanyakazi wachache hivyo UNICEF hili kushughulikia tatizo hilo ilianzisha vituo 50 vinavyotoa lishe katika vitongoji vyenye watu wengi.Wote wanaotoa huduma vituoni hapo ni wanawake na mmoja wao ni Sodaba Osman.“Tunatoa chakula cha matibabu kilicho tayari kutumika kwa watoto wenye utapiamlo, inafurahisha sana kwamba ninafanya kazi ya kuponya watoto, pia tunawashauri wajawazito na wakina mama wanaonyonyesha. Nawafundisha kuwa wakiwa nyumbani wanapaswa kula vyakula vyenye afya, mboga mboga na vyakula vingine ambavyo ni vyema kwao na vinajumuisha vitamini nyingi, hilo linanifurahisha sana”Kwa mwaka huu UNICEF inalenga kuwafanyia uchunguzi watoto milioni 1.2 wenye utapiamlo, kutibu watoto 90,000 wenye utapiamlo mkali na kufikia akina mama 347,000 wanaonyonyesha nakuhakikisha wanapata lishe bora.
17-7-2024 • 1 minuut, 56 seconden
Mataifa yanapaswa kushikamana kusongesha agenda 2030 ya SDGs: Mweli
Jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa HLPF, kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs linaelekea ukingoni hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa likitarajiwa kukunja jamvi hapo kesho Julai 17. Wawakilishi mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wamekuwa hapa kwa takriban wiki mbili kujadili jinsi ya kusongesha malengo hayo endelevu. Miongoni mwao ni Gerald Geofrey Mweli, Katibu Mkuu kutoka wizara ya kilimo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amemweleza Flora Nducha wa idhaa hii kuhusu ushiriki wake katika jukwaa hili.
16-7-2024 • 8 minuten, 22 seconden
16 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kutoka hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo Gerald Geofrey Mweli, Katibu Mkuu kutoka wizara ya kilimo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuotoa mkutano wa HLPF amezungumza na Flora Nducha. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Muda unazidi kuyoyoma kwa raia wanaokabiliwa na njaa nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wameonya leo wakati mazungumzo yanayohusisha pande zinazozozana nchini humo yakiendelea mjini Geneva wiki hii.Dharura ya kibinadamu nchini Haiti inahitaji uangalizi wa haraka, Wawakilishi kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), na Idara ya Ulinzi wa Raia na Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Ulaya (ECHO) wamesema walipokamilisha ziara ya siku nne nchini humo.Na Cote d'Ivoire ikiwa inakabiliwa na kuongezeka kwa matatizo ya maji na athari za mabadiliko ya tabianchi kwenye rasilimali za maji inazopakana na majirani zake, nchi hiyo sasa imejiunga na Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa wa kuboresha usimamizi wa pamoja wa maji katika mipaka.Mashinani ikiwa hivi karibuni dunia imetoka kuadhimisha siku ya idadi ya watu duniani shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi UNFPA likisihi mataifa yote duniani kuelimisha uma kuhusu mchango wa sensa katika malengo ya maendeleo endelevu, nampisha kijana kutoka Mwanza, nchini Tanzania akieleza umuhimu wa sensa katika utendaji wa serikali.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
16-7-2024 • 9 minuten, 59 seconden
FAO: Mradi wa maendeleo ya mifumo ya chakula kutekelezwa Zanzibar
Uwepo wa athari za mabadiliko ya tabianchi yanayosababishwa na shughuli kibinadamu umeendelea kupata ufumbuzi ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), nchini Tanzania limeratibu kikao kazi cha maandalizi ya kutengeneza Mradi wa maendeleo ya mifumo ya chakula katika nyanda za juu kusini maeneo ya Bonde la Usangu pamoja na visiwani Zanzibar, Mradi ambao tayari umetengewa Dola za kimarekani Milioni 8.4 kwa ufadhili wa Mfuko wa mazingira wa Dunia (GEF – 8). Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time kutoka Mkoa wa Morogoro amefuatilia Kikao kazi hicho na kuandaa makala hii.
15-7-2024 • 4 minuten, 52 seconden
UNMISS wapatia mafunzo ya ulinzi wa amani polisi wa Sudan Kusini
Maafisa wa polisi wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wametoa mafunzo kwa askari polisi wa nchi hiyo ili waweze kuimarisha ulinzi na usalama wakati huo huo wakiheshimu haki za binadamu. TNchi ya Sudan Kusini inakabiliwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei huku ajira nazo zikiwa ngumu kupatikana hali hizi mbaya zimechocheea uhalifu. Jeshi la polisi limejikuta kwenye shinikizo kubwa la kushughulikia changamoto hizo wakati wakiwa na rasilimali chache wakati huo huo wakienda miezi kadhaa bila ya kulipwa mishahara.Pamoja na changamoto hizo bado wanawajibu wa kulinda raia na mali zao ndio maana polisi wa UNMISS wakaandaaa mafunzo ya vitendo katika makao makuu ya nchi hiyo jijini Juba yakihusu matumizi sahihi ya nguvu wanapokamata wahalifu, namna ya kuwasaka watuhumiwa kwa usalama, ulinzi usio na silaha, huduma ya kwanza, ulinzi wa viongozi na watu mashuhuri, usalama wa misafara ya magari, doria ndani ya jamii na kufanya uchunguzi.Sophia Ennim ni Afisa Polisi wa Umoja wa Mataifa chini ya UNMISS na anasema mafunzo hayo yatasaidia sio tu kupambana na wahalifu bali pia wakati wa uchaguzi wa kwanza ya nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu“Tunataka kubadilishana nao uzoefu na tena, tunajua wanajitayarisha kuelekea uchaguzi na tunafikiri wakati huu ndio bora kwao kujikumbusha upya mbinu zao za kipolisi.”Samuel Nai, ni mmoja wa maafisa wa Polisi wa Sudan Kusini aliyehitimu mafunzo hayo.“Kazi hii ya upolisi inachosha sana, inachangamoto sana, lakini uzoefu tulioupata hapa utatusaidia kufanya vyema zaidi katika siku zijazo. Haya ndiyo mabadiliko tunayotaka kutoka kwa polisi.”Mbali na kushukuru kwa mafunzo hayo Afisa wa polisi wa Suda Kusini Lilian Poni ambaye anatumikia polisi kwa miaka 19 ametoa wito kwa wanawake zaidi kupata fursa sawa ili kukuza zaidi taaluma zao.“Nikiwa nimekaa hapa, naona wanaume ni wengi wanawake ni wachache. Kwa hivyo angalau wanapaswa kuweka usawa wa kijinsia, ikiwa wanaume ni 10, wanawake wanapaswa kuwa 10 pia.”Mafunzo haya kwa jeshi la polisi yanafuatia kikao cha usimamizi wa utulivu wa umma ambacho kiliomba askari wapatiwe mafunzo ili kusaidia kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo unafanyika kwa njia huru, ya haki, ya kuaminika na ya amani.UNMISS wameeleza kuwa pamoja na changamoto za ulinzi na usalama na taifa hilo kujiandaaa na uchaguzi lakini mafunzo yanayoendeshwa nao yana lengo kuu la kujenga uwezo wa maafisa wa polisi wa Sudan Kusini kukidhi mahitaji ya jamii zao.
15-7-2024 • 2 minuten
15 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya harakati za chanjo kwa watoto na ulinzi wa amani na usalama inaozingatia haki za binadamu nchini Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Rwanda, kulikoni?Viwango vya chanjo za utotoni ulimwenguni kote vilikwama mwaka 2023 na kuacha watoto milioni 2.7 bila chanjo au kupata kiwango kisichotosheleza cha chanjo ikilinganishwa na viwango vya kabla ya janga la COVID-19 mwaka 2019, kwa mujibu wa takwimu za ripoti mpya zilizochapishwa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEFMaafisa wa polisi wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wametoa mafunzo kwa askari polisi wa nchi hiyo ili waweze kuimarisha ulinzi na usalama wakati huo huo wakiheshimu haki za binadamu.Katika makala Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Tanzania limefanya kikao kazi cha maandalizi ya kutengeneza Mradi wa maendeleo ya mifumo ya chakula katika nyanda za juu kusini maeneo ya Bonde la Usangu pamoja na visiwani Zanzibar.Na mashinani Prince ISHIMWE mwanafunzi wa Shule ya ufundi ya Forever TSS nchini Rwanda anatueleza jinsi uunganishwaji wa intaneti shuleni unamsaidia kuwasiliana na kushirikiana na wanafunzi wenzake katika kujifunza na kuafanya utafiti mtandaoni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
15-7-2024 • 12 minuten, 34 seconden
WHO/UNICEF: Watoto 3 kati ya 4 wanaishi katika nchi ambako upatikanaji wa chanjo ni mdogo na kusababisha milipuko ya magonjwa
Viwango vya chanjo za utotoni ulimwenguni kote vilikwama mwaka 2023 na kuacha watoto milioni 2.7 bila chanjo au kupata kiwango kisichotosheleza cha chanjo ikilinganishwa na viwango vya kabla ya janga la COVID-19 mwaka 2019, kwa mujibu wa takwimu za ripoti mpya zilizochapishwa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF. Makadirio ya hivi karibuni ya WHO na UNICEF ya utoaji wa chanjo kitaifa (WUENIC) ambayo hutoa kiwango kikubwa zaidi cha takwimu duniani kuhusu mwelekeo wa chanjo dhidi ya magonjwa 14 yanasisitiza haja ya jitihada zinazoendelea za kujikwamua, kurejesha na kuimarisha mifumo ya chanjo. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell amesema "Mienendo ya hivi karibuni inaonyesha kwamba nchi nyingi zinaendelea kukosa chanjo kwa watoto wengi. Kuziba pengo la chanjo kunahitaji juhudi za kimataifa, serikali, washirika, na viongozi wa eneo hilo kuwekeza katika huduma za afya ya msingi na wahudumu wa jamii ili kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo, na kwamba huduma ya afya kwa ujumla inaimarishwa."Takwimu hizo zinaonyesha kwamba umla ya watoto milioni 14.5 duniani kote walikosa chanjo mwaka 2023 ikiwa ni Pamoja nay a ugonjwa wa surua na “Zaidi ya nusu ya watoto ambao hawajachanjwa wanaishi katika nchi 31 zenye mazingira magumu, zilizoathiriwa na migogoro na mazingira hatarishi, ambapo watoto wako katika hatari ya kupata magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa sababu ya changamoto na ukosefu wa usalama, lishe na huduma za afya.”Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema "Milipuko ya surua ni tahadhari ya hatari katika mgodi wa makaa ya mawe, ikifichua na kutumia mapengo katika chanjo na kuathiri walio hatarini zaidi kwanza. Hili ni tatizo linaloweza kutatuliwa. Chanjo ya surua ni nafuu na inaweza kutolewa hata katika maeneo magumu zaidi. WHO imejitolea kufanya kazi na washirika wetu wote kusaidia nchi kuziba mapengo haya na kuwalinda watoto walio katika hatari zaidi haraka iwezekanavyo.”Pamoja na changamoto takwimu hizo zinasema kuna matumaini hasa katika utoaji wa chanjo dhidi ya visusi vya papilloma vinavyosababisha saratani ya shingo ya kizazi ambapo kwa msaada wa muungano wa chanjo duniani GAVI wasichana wengi wamefanikiwa kupata chanjo hiyo katika nchi 57 hasa Bangladesh, Indonesia na Nigeria.Hata hivyo, GAVI inasema chanjo ya chanjo ya HPV iko chini ya lengo la asilimia 90 la kuondoa saratani ya mlango wa kizazi kama tatizo la afya ya umma, na inafikia asilimia 56 tu ya wasichana katika nchi zenye kipato cha juu na 23% katika nchi za kipato cha chini na cha kati.
15-7-2024 • 3 minuten, 4 seconden
Mdau wa biashara na Uchumi Tanzania waeleza faida za kuhesabiwa
Ikiwa ni jana tu Julai 11, ambapo dunia iliadhimisha Siku ya Idadi ya watu duniani ikiwa na mahudhui ya kuangazia umuhimu wa kukusanya takwimu jumuishi kwa kuhesabu kila mtu, kila mahali na jinsi alivyo. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi UNFPA limesisitiza haja ya Sensa ili kuhakikisha usawa na jamii jumuishi duniani.Nchini Tanzania, kama ilivyo katika nchi nyingi za Afrika, suala hili la sensa limebeba mustakabali mkubwa kwa wananchi wa Taifa hilo. Ni kwa vipi? Tuungane na Bosco Cosmas katika Makala hii.
12-7-2024 • 2 minuten, 53 seconden
12 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia janga la kiafya na misaada ya kibinadamu nchini DRC, na mchakato wa uchaguzi mkuu nchini Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani inaturejesha nchini DRC, kulikoni?Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC iko katikati ya janga la kiafya linaloongezeka limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani (WHO) na kusisitiza kwamba magonjwa ya milipuko yamezorotesha sana hali nchini humo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na kuchochewa na ghasia na mafuriko.Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wake wa kwanza mwaka huu mwezi Desemba, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umeendesha kongamano la siku tatu la vyama vya siasa katika mji wa Rumbek ili kujadili masuala ambayo ni muhimu katika maandalizi ya uchaguzi huo.Katika makala Bosco Cosmas anatukutanisha na Katibu tawala katika kitivo cha Biashara na Uchumi kutoka chuo kikuu cha Mt. Agustino akieleza kuhusu jinsi kujua idadi ya watu kunavyoleta manufaa katika kuhakikisha maendeleo endelevu kwa jamii.Katika mashinani Deborah Dhra ambaye ni mama wa watoto wawili akitueleza jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Usaidizi wa Dharura, CERF linaboresha afya ya jamii zilizoathiriwa na migogoro kwa kuweka matanki na mabomba ya maji safi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
12-7-2024 • 10 minuten, 1 seconde
WHO inasema janga la kiafya linashika kasi Congo DRC
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC iko katikati ya janga la kiafya linaloongezeka limeonya leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO na kusisitiza kwamba magonjwa ya milipuko yamezorotesha sana hali nchini humo katika miezi ya hivi karibuni kutokana na ghasia na mafuriko. Kulingana na WHO, DRC imekabiliwa na ongezeko la migogoro na ghasia, na kusababisha watu wengi kukimbia makazi yao, magonjwa kuenea, unyanyasaji wa kijinsia, na kiwewe kikubwa cha akili, haswa mashariki mwa nchi hiyo.Dkt. Adelheid Marschang, Afisa wa Dharura wa WHO, ameuambia mkutano wa waandishi wa habari wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva kwamba"Kutokana na hali hiyo, watu wanakabiliwa na milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu, surua, uti wa mgongo, ndui na tauni, yote yakichangiwa na mafuriko makubwa na maporomoko ya ardhi yanayoathiri sehemu kadhaa za nchi hiyo."Tangu mwanzoni mwa mwaka, WHO inasema zaidi ya visa 20,000 vya kipindupindu vimerekodiwa, viki katika eneo la Kivu Kaskazini.Pia kumekuwa na zaidi ya wagonjwa 65,000 wa surau na vifo 1,523, huku idadi halisi ikiwezekana kuwa kubwa zaidi kutokana na kutofuatilia na kuripoti magonjwa kwa kiasi cha kutosha. Wakati huo huo, kumekuwa na kesi 3,073 za homa ya uti wa mgongo ikiwa ni pamoja na vifo 251vilivyoripotiwa katika katika nchi hii ya Maziwa Makuu.WHO pia imekuwa na wasiwasi juu ya lahaja ya mpox katika miezi ya hivi karibuni ambapo zaidi ya kesi 11,000 zikijumuisha vifo 445 zimerekodiwa, na kukiwa na kiwango cha juu cha vifo vya zaidi ya asilimia 4. Watoto wameelezwa kuathiriwa zaidi na janga hili, na viwango vya juu zaidi vya vifo.Migogoro ya silaha na watu kuhama makazi yao vimetajwa kuwa ni vichocheo vikuu vya uhaba wa chakula.WHO inasema takriban asilimia 40 ya watu ambayo ni sawa na watu milioni 40 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula nchini DRC na, watu milioni 16 kati yao wako katika hatari ya kutokuwa na uhakika wa chakula. Jumla ya watu milioni 25 nchini humo wanategemea msaada wa kibinadamu kuweza kuishi na kuifanya DRC kuwa sasa ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu duniani.
12-7-2024 • 2 minuten, 29 seconden
UNMISS yafanya kongamano na vyama vya siasa jimboni Rumbek: Uchaguzi Mkuu Sudan Kusini
Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kwa uchaguzi mkuu wake wa kwanza mwaka huu mwezi Desemba, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umeendesha kongamano la siku tatu la vyama vya siasa katika mji wa Rumbek ili kujadili masuala ambayo ni muhimu katika maandalizi ya uchaguzi huo. Mchakato wa uchaguzi nchini Sudani Kusini unafungamana na utekelezaji wa masharti ya mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2018 ambao unataka hatua za amani kuchukuliwa si tu katika ngazi ya kitaifa bali majimboni na maeneo yote ya utawala.Lakini hivi karibuni kumezuka zahma huko katika mji wa Rumbek jimboni Lakes ambako jamii zimejikuta kwenye vurugu za jumuiya mara kwa mara. Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana viongozi wa mamlaka za mitaa wakaomba Umoja wa Mataifa kuja kusaidia kuleta amani na umoja kati ya vyama vya siasa vya serikali, vikosi vya usalama na mashirika ya kiraia.Christopher Muchiri Murenga, ni Mkuu wa Ofisi ya Rumber wa UNMISS, anasema "Sehemu ya kazi yetu muhimu ni kuunga mkono na kusaidia kujenga uaminifu na imani kati ya vyama vya siasa. Wote wamekaa pamoja na kujadili kufungua nafasi ya kiraia na kisiasa katika Jimbo la Lakes, na jambo moja lililotajwa zaidi na watu ni kwamba kongamano hili lisiwe katika manispaa ya Rumbek pekee.”UNMISS na washirika wa kikanda wanatumaini kuwa kongamano hili na matukio mengine kama haya yatakayo fuata nchini kote yatatengeneza jukwaa la mazungumzo ya wazi na jumuishi kati ya vyama vya siasa na wapiga kura wao kama anavyodhibitisha Waziri wa serikali za mitaa na utekelezaji wa sheria katika jimbo hilo la Lakes bwana Chol Kodowel.“Tuna jukumu la kuleta utulivu katika jumuiya yetu ili upigaji kura ufanyike katika mazingira ya amani na hilo ni jukumu si kwa serikali ya mtaa peke yake, au jimboni, bali ni jukumu letu sote kama jamii pamoja na wadau wetu.”Katika ngazi ya kitaifa, vyama vya siasa kwa sasa vinafanya kazi kwa karibu na vikundi mbalimbali ili kuwaleta katika mkondo mkuu wa mchakato wa amani na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa amani, wakidemokrasia na wa kuaminika.
12-7-2024 • 1 minuut, 59 seconden
11 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika yanayojiri katika Jukwaa la kisiasa la ngazi ya juu la Umoja wa Mataifa HLPF kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs, ambapo Anold Kayanda alizungumza na Katibu Mkuu Mhandisi Cyprian John Luhemeja wa Ofisi ya Makamu wa Rais wa Tanzania. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zifuatazo..Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya idadi ya watu duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kwa siku hii amehimiza umuhimu wa kuwekeza katika ukusanyaji wa taarifa za watu ili kuweza kufahamu matatizo, kuchambua aina ya suluhu zitakazofaa wakati wa kushughulikia matatizo hayo na kuleta maendeleo kwa haraka.Kwa mara ya kwanza hii leo dunia inaadhimisha siku ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1995 ya Srebrenica ambapo zaidi ya Waislamu 8,000 wa Bosnia waliuawa kikatili, na mabaki yao kuzikwa katika makaburi ya pamoja. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitoa ujumbe wa siku hii ametahadharisha dhidi ya ukanaji wa maujaji hayo na upotoshaji wa ukweli na kutoa wito wa kuendeleza juhudi za kutambua kila mwathirika.Na tuhitimishie huko mashariki ya kati ambapo Ofisi ya kuratibu wa misaada ya Umoja wa Mataifa OCHA imetoa takwimu za athari za mzozo huko Ukanda wa Magharibi na kueleza kuwa tangu vita kuanza kati ya Israel na Palestina mwezi Oktoba mwaka jana, zaidi ya wapalestina 550 wameuawa, zaidi ya mashambulizi elfu moja ya walowezi dhidi ya wapalestina yamerekodiwa, na takriban watu 1,400, wakiwemo watoto 660, wameyakimbia makazi yao kutokana na ghasia za walowezi na vizuizi.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili le tunakuletea ujumbe wa Balozi wa Burundi akieleza kuhusu anayofikiri itakuwa mikakati mizuri ya kukisongesha Kiswahili duniani hasa kwa kutumia balozi za kiafrika kote duniani na baadaye kuweka msukumo zaidi ndani ya UN.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
11-7-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Sekta ya uvuvi: Wananchi Terekeka Sudan Kusini wanufaika na mradi wa FAO
Wananchi katika Kaunti ya Terekeka nchini Sudan Kusini wameeleza kufurahishwa na mafanikio wanayoyapata kutokana na mradi wa miaka mitano wa kuboresha mnepo wa Jamii za Wavuvi (FICREP). Cecily Kariuki na maelezo zaidi.Huyo ni Stelle Clement, mjasiriamali wa mghahawa katika jamii ya Terekeka, Equatoria ya Kati nchini Sudan Kusini. Anasema, “faida ninayopata kutokana na biashara yangu ni tegemeo la familia yangu. Inaniwezesha kuwaandalia watoto wangu mahitaji, kuweka chakula mezani, na kuhakikisha wanapata matibabu yanapohitajika.”Stelle Clement ni mmoja wa wanufaika wa mradi huu wa uvuvi ambao umeiinua sana jamii ya hapa kupitia ufadhili wa dola za Kimarekani milioni tano kutoka Ufalme wa Uholanzi ikiwa ni moja ya njia za kushughulikia baadhi ya changamoto kuu za janga la tabianchi.Samaki ndiyo bidhaa pekee ya kilimo ambayo inasafirishwa mara kwa mara kutoka Sudan Kusini kwenda nje ya nchi, na inazalisha takribani dola milioni 30 kwa mwaka.Miongoni mwa malengo mengine, mradi umeunda vikundi 20 vya wavuvi na, kwa mara ya kwanza, mradi umeanzisha kituo bora cha kuunda mitumbwi kwa ajili ya vijana.Yametolewa mafunzo kwa watengeneza mitumbwi 40 chipukizi ili kuunda mitumbwi ya kienyeji lakini sasa kwa kutumia gundi imara zaidi ili kuiewezesha mitumbwi hii kudumu kwa muda mrefu na pia kukarabatiwa kirahisi.Demissie Redeat Habteselassie, Afisa Uvuvi wa FAO nchini Sudan Kusini anaeleza zaidi akisema, “Tumeboresha tanuri za kukaushia samaki, tumeboresha chanja za kukaushia samaki, na hii imesaidia jamii za wavuvi kupata mapato zaidi, kupunguza hasara zao na kuongeza mapato yao kupitia bidhaa za samaki zilizoongezwa thamani. Na hapa, kwa kawaida, jamii za wavuvi zinategemea zaidi samaki na uwezo wao wa kuzalisha na kuongeza faida yao ni muhimu sana. Kwa hiyo, hilo ndilo mradi wetu kimsingi unafanyia kazi.”Uchumi wa Sudan Kusini unategemea zaidi mafuta, yakichangia takriban asilimia 95 ya mauzo ya nje na ni kichocheo kikuu cha mapato ya serikali.Hata hivyo, nchi inakabiliwa na ukuaji tete wa uchumi huku mfumuko wa bei ukisukuma takriban watu milioni 1.6, au takriban asilimia 12 ya watu wote, kuwa hatarini na hivyo njia mbadala za kujipatia kipato ni muhimu.
10-7-2024 • 1 minuut, 55 seconden
WHO na wadau wake Tanzania yasaidia kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua
Hakuna mwanamke anayepaswa kufa wakati wa kujifungua, ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa la afya Ulimwenguni WHO nchini Tanzania baada ya kushuhudia ongezeko la vifo vya wajawazito kutokana na wajawazito kupata ugumu kuvifikia vituo vya afya ilitafuta fedha ya kusaidia kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo miundombinu na kuongeza maarifa kwa wataalamu wa afya.Hatimaye WHO Tanzania wakafanikiwa kupata fedha kutoka Ubalozi wa Norway nchini Tanzania na kuzielekeza katika kutatua changamoto mbalimbali na sasa vifo vya uzazi vimepungua katika kanda ukanda huo. Ni kwa vipi basi ? Tuungane na Leah Mushi katika makala haya.
10-7-2024 • 3 minuten, 19 seconden
10 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya Uchumi wa kidijitali 2024, na uvuvi nchini Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Tanzania kumulika afya kwa wajawazito na mashinani nchini Kenya kusikia simulizi ya mwathirika ya mafuriko.Ripoti mpya iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo UNCTAD kuhusu “Uchumi wa kidijitali 2024” imeweka bayana kuhusu athari za kimazingira za sekta ya kimataifa ya kidijitali na mzigo mkubwa wa athari hizo unaobebwa na nchi zinazoendelea.Wananchi katika Kaunti ya Terekeka nchini Sudan Kusini wameeleza kufurahishwa na mafanikio wanayoyapata kutokana na mradi wa miaka mitano wa kuboresha mnepo wa Jamii za Wavuvi (FICREP).Na kikao cha 56 cha kawaida cha Baraza la Haki za Binadamu kikiendelea huko Geneva Uswisi Katika kikao hicho Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameitaka jumuiya ya kimataifa kufikiria upya kuhusu kusitisha makubaliano yake na nchi za Kaskazini mwa Afrika kuhusu watafuta hifadhi.Katika tutakupeleka katika mitaa ya Mathare iliyoko Nairobi nchini Kenya kusikia simulizi ya mwathirika wa mafuriko.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
10-7-2024 • 9 minuten, 57 seconden
UNCTAD: Uchumi wa kidijitali ni lulu lakini pia unaathari za kimazingira hasa kwa nchi zinazoendelea
Ripoti mpya iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo UNCTAD kuhusu “Uchumi wa kidijitali 2024” imeweka bayana kuhusu athari za kimazingira za sekta ya kimataifa ya kidijitali na mzigo mkubwa wa athari hizo unaobebwa na nchi zinazoendelea. Flora Nducha ameisoma ripoti hiyo na anafafanua zaidiRipoti hiyo iliyozinduliwa mjini Geneva Uswisi imetanabaisha kwamba kuanzia kwa uchimbaji wa malighafi na matumizi ya teknolojia za kidijiti hadi uzalishaji taka, inachunguza asili na ukubwa wa athari za kimazingira za sekta hii.Kinachoonekana karika ripotihiyo ni kwamba nchi zinazoendelea zinateseka kupita kiasi kutokana na athari mbaya za mazingira za uwepo na ukuaji wa sekta ya kidijitali, huku zikikosa fursa za maendeleo ya kiuchumi kutokana na pengo kubwa la kidijitali.”Ripoti hii ya kina inaangazia kwamba ingawa uboreshaji wa kidijitali huchochea ukuaji wa uchumi duniani na kutoa fursa za kipekee kwa nchi zinazoendelea, athari zake za kimazingira zinazidi kuwa kubwa na mbaya.Iesisitiza kuwa Nchi zinazoendelea zimesalia kuathiriwa kwa njia isiyo sawa kiuchumi na ikolojia kutokana na pengo liliopo la kidijitali na maendeleo lakini zina uwezo wa kutumia fursa ya mabadiliko haya ya kidijitali ili kukuza maendeleo.Katibu Mkuu wa UNCTAT Rebeca Grynspan, amesema “Kuhusu athari za Uchumi wa kidijitali ni lazima tujumuishe masuala ya mmazingira katika sera za kidijitali. Tukumbtie Uchumi wa mzunguko, tutoe kipaumbele katika ujerejelezaji wa bidhaa, utumiaji tena wa bidhaa za kidijitali, kutekeleza mikakati ya matumizi ikiwemo mufa wa matumizi ya vifaa vya kielektroniki tunavyotumia.”Amesisisitiza kuwa “Kuna haja ya kuwa na mtazamo wenye uwiano, ni lazima tukumbatie nguvu ya kidijitli ili kusongesha ujumuishaji na maendeleo endelevu huku tukikabiliana na athari za kimazingira za sekta hiyo hasa kwa kubadili mwelekeo na kuwa na Uchumi wa kidijitali wa mzunguko ukijumuisha uwajibikaji wa matumizi na uzalishhaji, matumizi ya nishati jadidifu na udhibiti wa taka za kielektroniki kwani athari za kimazingiza zinaweza kudhibitiwa.”Ripoti hiyo pia inasisitiza haja kubwa ya kushughulikia gharama za kimazingira za mabadiliko ya haraka ya kidijitali.Wasiwasi mkubwa ni pamoja na kupungua kwa malighafi za teknolojia ya kidijitali na matumizi madogo ya hewa ukaa, kuongezeka kwa matumizi ya maji na nishati na suala linalokua la taka zinaohusiana na masuala ya kidijitali.Kadiri uboreshaji wa kidijitali unavyoendelea kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, kuelewa uhusiano wake na uendelevu wa mazingira kunazidi kuwa muhimuUNCTAD inatoa wito wa kuwepo kwa sera za kimataifa zinazohusisha wadau wote kuwezesha uchumi wa kidijitali wa mzunguko zaidi na kupunguza athari za kimazingira kutokana na mfumo wa kidijitali, huku zikihakikisha matokeo ya maendeleo jumuishi.
10-7-2024 • 1 minuut, 53 seconden
Nafasi ya elimu ya sanaa katika kueneza na kukuza lugha ya kiswahili
Hivi karibuni dunia imeadhimisha siku ya Kiswahili duniani ikiwa ni maadhimisho ya tatu, lakini ya kwanza tangu Umoja wa Mataifa utambue Julai 7 kuwa siku ya lugha ya Kiswahili duniani. Kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa maadhimisho yalifanyika Julai 3 maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa katika kueneza na kukuza lugha ya kiswahili. Anold kayanda anakuletea kwa muhtasari yaliyojiri.
9-7-2024 • 5 minuten, 23 seconden
09 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia ujumbwa wa viongozi katika maadhimisho ya hivi karibuni ya siku ya Kiswahili duniani. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Gaza, Libya na Kusini mwa Afrika. Mashinani inayotupeleka nchini Sudan.Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa hii leo wamesema ni dhahiri shahiri kuwa baa la njaa imeenea katika ukanda mzima wa Gaza kufuatia vifo vya hivi karibuni vya watoto wa kipalestina kutokana na njaa na utapiamlo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP limesema takriban dola milioni 409 zinahitaji mara moja ili kusaidia zaidi ya wananchi milioni 4.8 katika nchi za Malawi, Zambia na Zimbabwe.Na kikao cha 56 cha kawaida cha Baraza la Haki za Binadamu kikiendelea huko Geneva Uswisi Katika kikao hicho Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameitaka jumuiya ya kimataifa kufikiria upya kuhusu kusitisha makubaliano yake na nchi za Kaskazini mwa Afrika kuhusu watafuta hifadhi.Katika mashinani Alfatih Awad Alkheder, Mfanya biashara mwenye watoto 6 ambaye pia ni mkimbizi wa ndani kutoka Port Sudan na katika video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP anasimulia kilichomkumba yeye na familia.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
9-7-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Mafunzo ya FAO/ILO yataniwezesha kupanga bei sahihi ya mazao- mnufaika wa mafunzo
Elimu ya Biashara imekuwa na faida kubwa kwa wajasiriamali wadogo wanaojishughulisha na kilimo, ikiwemo wakulima wadogo wadogo, vijana, wanawake, na wasimamizi wa mashamba ya uzalishaji mbegu mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Kwa kutambua hilo, washiriki kutoka wilaya za mkoa huo chini ya Mradi wa Pamoja Kigoma (KJP) awamu ya Pili) wakiwemo Vijana, wanawake, wasimamizi wa mashamba toka gereza la Ilagala huko Uvinza na kambi ya jeshi la kujenga Taifa kikosi cha 824 Kanembwa huko Kakonko walipata fursa ya kupata mafunzo ya kuendesha miradi kibiashara yaliyofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kupitia KJP. Je nini ambacho washiriki waliondoka nacho? Assumpta Massoi wa Idhaa hii anakufafanulia zaidi kwenye makala hii.
8-7-2024 • 4 minuten, 8 seconden
Ukraine yakumbwa na wimbi jipya la mashambulizi ya makombora ya Urusi
Nchini Ukraine Jumatatu ya leo Julai 8 imeanza na wimbi jingine la mashambulizi makubwa ya kijeshi yaliyotekelezwa na Urusi na kuua makumi ya watu, hospitali ya watoto ikiwa ni miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa. Flora Nducha ameifuatilia taarifa hiyo. Mashambulizi haya ya leo yaliyotokea wakati watu waliopokuwa ndio kwanza wanaianza siku, yameilenga miji kadhaa ya Ukraine ikiwemo mji mkuu, Kyiv na mji mingine kama Kryvyi Rih na Pokrovsk.Akilaani mashambulizi hayo, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine ambaye pia ni mratibu mkuu wa misaada ya kibinadamu nchini humo, Denise Brown, amesema, "ni jambo lisilokubalika kuona kwamba watoto wanauawa na kujeruhiwa katika vita hii. Chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu, hospitali zina ulinzi maalum. Raia lazima walindwe."Mbali na Hospitali ya Watoto ya Ohmatdyt huko Kyiv, miundombinu mingine ya umma pia imeharibiwa, pamoja na majengo ya biashara na makazi katika miji ikiwa ni pamoja na Dnipro, Kramatorsk, Kryviy Rih, Kyi na Pokrovsk.Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, takriban watu 20 wameuawa katika mashambulizi haya ya leo Julai 8.Rais Volodymyr Zelenskiy wa Ukraine amesema zaidi ya makombora 40 yamerushwa.
8-7-2024 • 1 minuut, 22 seconden
08 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi makubwa ya kijeshi nchini Ukraine yaliyotekelezwa na Urusi, na miradi ya maji nchini Sudan Kusini. Makala inamulika biashara kwa wakulima, vijana na wanawake, na mashinani inatupeleka nchini Ethiopia, kulikoni?Nchini Ukraine Jumatatu ya leo Julai 8 imeanza na wimbi jingine la mashambulizi makubwa ya kijeshi yaliyotekelezwa na Urusi na kuua makumi ya watu, hospitali ya watoto ikiwa ni miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa.Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Beth Bechdol amefanya ziara ya siku sita nchini Sudan Kusini na kuzindua miradi inayo saidia ukuaji wa kiuchumi huku ikipunguza migogoro na kuongeza uwezo wa wanachi kwenye kilimo.Katikamakala Assumpta Massoi akimulika mafunzo yaliyotolewa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na wadau ili kuimarisha biashara kwa wakulima, vijana, wanawake na wasimamisi wa mashamba ya kuzalisha mbegu mkoani Kigoma, kaskazini magharibi mwa Tanzania.Mashinani tutakupeleka Tigray nchini Ethiopia katika shule ya msingi ya Siye kusikia jinsi Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ushirikiana na Muungano wa Ulaya lilivyoongeza kiwango cha uandikishaji na uhifadhi wa wanafunzi shuleni kupitia ukarabati wa madarasa na mpango wa mlo shuleni lakini kwanza ni makala.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
8-7-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Miradi ya maji yasaidia kupunguza migogo ya wafugaji nchini Sudan Kusini - FAO
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Beth Bechdol amefanya ziara ya siku sita nchini Sudan Kusini na kuzindua miradi inayo saidia ukuaji wa kiuchumi huku ikipunguza migogoro na kuongeza uwezo wa wanachi kwenye kilimo.Akiwa ameambatana na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika Rukia Abdullahi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Sudan Kusini Onyoti Adigo na viongozi wengine wa ngazi za juu wa FAO, wametembekea maeneo mbalimbali ikiwemo mji wa Kapoeta ulioko jimboni Equatorial Mashariki unaokabiliwa na ukame ambapo mifugo ndio chanzo kikuu cha chakula na lishe na tegemeo la kuwaingizia kipato wananchi.Ziara ya Bi. Bechdol inakuwa wakati huu kukiwa na wasiwasi wa kuzorota kwa hali ya uhakika wa upatikanaji wa chakula kutokana na mafuriko yanayotarajiwa kuathiri nchi hiyo mwezi Septemba. Lakini kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika jumla ya dola milioni 44 zimewekezwa kwenye miundombinu ya uvunaji wa maji inayozingatia mabadiliko ya tabianchi (wananchi wa Kapoet wakiita Haffirs).Mradi huu umesaidia kupunguza migogoro na mivutano baina ya kaya za wafugaji iliyokuwa ikisababishwa na uhaba wa maji pamoja na kupunguza tabia za wafugaji kuhama hama kwani sasa zaidi ya kaya 13,000 zinanufaika kwa upatikanaji wa maji.Akiwa katika jijiji cha Riwoto huko Kapoeta Kaskazini Bi. Bechdol alizindua visima cha maji na kueleza kuwa, “Huu ni mfano kamili wa jinsi tunavyoshirikiana na serikali ya Sudan Kusini na washirika muhimu wa rasilimali kama Benki ya Maendeleo ya Afrika, na kuleta uwezo kamili wa uongozi wa FAO kwa watu wa Sudan Kusini.”Bi. Marta Nakwee mkulima kutoka Riwoto anashukuru kwa mradi huo kwani umebadilisha maisha yao.“Hapo awali nilikuwa naenda mbali sana kuteka maji ilikuwa ikinichukua sehemu kubwa ya siku yangu. Nililazimika kuwaacha watoto wangu wakiwa na njaa siku nzima na maranyingine waliugua lakini kwa sasa sina tatizo hilo tena.”Mbali na miradi ya maji FAO na washirika wake kujenga uwezo wa kustahimili hali ya maisha kwa kusaidia wananchi kuzalisha mbegu zao wenyewe kwa ajili ya kilimo, kujenga miundombinu, kuboresha upatikanaji wa maji safi na salama, kutoa chakula chenye lishe bora kwa watoto mashuleni na kupunguza utegemezi wa misaada ya kibinadamu.
8-7-2024 • 1 minuut, 52 seconden
DRC ni zaidi ya muziki, tutatumia Kiswahili kueneza utamaduni wetu - Balozi Ngay
Kufuatia lugha ya Kiswahili kutambuliwa na Umoja wa Mataifa na kutengenewa siku maalum, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC sasa imesema itajengea uwezo wasanii wake wanaoimba kwa lugha ya Kiswahili kama njia mojawapo ya kusambaza utamaduni wa taifa hilo.Mwakilishi wa Kudumu wa DRC kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zénon Mukongo Ngay amesema hayo katika ujumbe wake kupitia Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.Ikumbukwe kuwa tarehe 1 Julai mwaka huu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kutangaza tarehe 7 Julai kuanzia mwaka huu kuwa siku ya Kiswahili dunia na kutaka nchi wanachama na wadau pamoja na mashirika kuchukua hatua kusongesha lugha hiyo ya 10 kwa kuwa na wazungumzaji wengi zaidi duniani, kwa mujibu wa UNESCO.Balozi Ngay kwenye ujumbe wake amesema DRC imefurahishwa na kitendo cha Kiswahili kutambulika katika kiwango cha kimataifa.DRC ni zaidi ya muziki, tutatumia kiswahili kueneza utamaduni wetu“Siku ya Julai 7 itabakia katika kumbukumbu. Kiswahili ni lugha itakayokuwa chombo cha biashara duniani kote, ni jambo la kujivunia,” amesema Balozi Ngay.Ametanabaisha kuwa DRC ni mashuhuri si katika muziki peke yake, akisema utamaduni wa DRC ni mkubwa, muziki ni kipengele kimoja tu cha utamaduni wetu.Amesema idadi kubwa ya wakongomani wanaoimba kwa lugha ya kiswahili wameingia kwenye injili na nyimbo zao nyingi zinatambulika kwenye sehemu ya eneo la Mashariki mwa Afrika.Tutahimiza matumizi ya Kiswahili kweney muziki wa kijamiiKwa kuzingatia uzito wa sasa wa Kiswahili, DRC pia itahimiza matumizi ya lugha hiyo katika kile kinachoitwa muziki wa kijamii.Balozi Ngay amesema watakachofanya wao sasa ni kukuza wasanii wanaoweza kuimba kwa lugha ya Kiswahili.Tarehe 1 Julai mwaka huu wa 2024 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha Azimio (A/78/L.83) la kutambua Julai 7 kuwa Siku ya Kimataifa ya Kiswahili.Awali siku hii ilikuwa inatambuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kupitia azimio lililopitishwa mwezi Novemba mwaka 2021.
5-7-2024 • 2 minuten, 2 seconden
Machungu yakumbayo wahamiaji na wakimbizi njia za ardhini ni makubwa kuliko baharini Mediteranea
Ripoti mpya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yabaini kuwa wahamiaji na wakimbizi wanaotaka kuelekea Ulaya kusaka maisha bora kupitia njia za ardhini Afrika, wanakumbwa na ukatili sio tu wanapokuwa baharini, bali pia ardhini wanapokatiza nchi zingine kuelekea fukwe za bahari ya Mediteranea. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.Ikipatiwa jina Katika safari hii hakuna anayejali unaishi au unakufa, ripoti imeandaliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na la wahamiaji, IOM kwa ushirikiano na lile la Kimataifa la Wahamiaji Mseto (MMC).Ripoti inasema wakimbizi na wahamiaji wanazidi kupita maeneo ya ardhini ambako makundi ya waasi, wanamgambo na wahalifu wengine wanafanya kazi, na ambapo biashara haramu ya binadamu, utekaji nyara kwa ajili ya kikombozi, utumikishwaji kwenye kazi na ukatili wa kingono umeenea.Hayo yanatokea wakati inakadiriwa kuwa watu wengi huvuka zaidi kulekea Ulaya kupitia jangwa la Sahara kuliko bahari ya Mediterania huku vifo vya wakimbizi na wahamiaji jangwani vikidhaniwa kuwa ni maradufu zaidi ya vile vinavyotokea kwa wanaovuka kupitia bahari ya Mediterania huku ikionya juu ya ongezeko kubwa la watu wanaojaribu kuvuka eneo hilo hatari.Licha ya ahadi zinazofanywa na Jumuiya ya Kimataifa kuokoa maisha na kushughulikia udhaifu unaondelea, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, mashirika hayo matatu yanaonya kwamba hatua za sasa za Kimataifa hazitoshi kutokana na mapungufu makubwa kwenye ulinzi katika njia ya kati ya Mediterania.Yanachotaka sasa mashirika hayo ni ulinzi mahsusi kulingana na njia wanazotumia wakimbizi na wahamiaji ili kuokoa maisha, kupunguza machungu na kung’oa mzizi wa kile kinachosababisha watu kukimbia nchi zao kwa kusaka mbinu bora za ujenzi wa amani.
5-7-2024 • 1 minuut, 45 seconden
05 JULAI 2024
Hii leo kwenye jarida mwenyeji wako ni Assumpta Massoi akimulika shamrashamra za Kiswahili, wakimbizi na wahamiaji na mateso njiani Afrika, mafunzo kwa wataalamu wa mifugo Tanzania na harakati za OCHA Sudan kusaidia wahitaji.Wadau wa Kiswahili duniani kote wakiendelea na shamrashamra baada ya Umoja wa Mataifa kutambua lugha hiyo kuwa ya kimataifa na hadi kutengewa tarehe 7 Julai kuwa siku maalum kusherehehea siku hiyo, Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Zénon Mukongo Ngay naye ametoa ujumbe wake.Ripoti mpya ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yabaini kuwa wahamiaji na wakimbizi wanaotaka kuelekea Ulaya kusaka maisha bora kupitia njia za ardhini Afrika, wanakumbwa na ukatili sio tu wanapokuwa baharini, bali pia ardhini wanapokatiza nchi zingine kuelekea fukwe za bahari ya Mediteranea. Bosco Cosmas na maelezo zaidi.Makala inatupeleka nchini Tanzania ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili ya Shirika la Marekani la misaada ya maendeleo (USAID), limehitimisha awamu ya nne ya mafunzo kwa maafisa mifugo 30 wa serikali ya Tanzania, yatakayowawezesha kutambua na kutibu magonjwa ya mifugo ili kuboresha ufugaji wenye tija na kulinda soko la Mifugo kimataifa. Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM ya Morogoro, amehudhuria shughuli ya uhitimishaji wa mafunzo hayo na kuandaa makala inayoanza na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tanzania, Profesa Riziki Shemdoe.Mashinani Clementine Nkweta-Salami ambaye ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa kwa Misaada ya kibinadamu nchini Sudan akitueleza jinsi changamoto ya usalama wa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu inavyokwamisha ufikishaji wa misaada kwa wahitaji.
5-7-2024 • 9 minuten, 49 seconden
FAO Tanzania na USAID wafanikisha mafunzo kwa Maafisa Mifugo Tanzania
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili ya Shirika la Marekani la misaada ya maendeleo (USAID), limehitimisha awamu ya nne ya mafunzo kwa Maafisa Mifugo 30 wa serikali ya Tanzania, yatakayowawezesha kutambua na kutibu magonjwa ya mifugo ili kuboresha ufugaji wenye tija na kulinda soko la Mifugo kimataifa. Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM ya Morogoro, amehudhuria shughuli ya uhitimishaji wa mafunzo hayo na kuandaa makala inayoanza na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Tanzania, Profesa Riziki Shemdoe.
5-7-2024 • 3 minuten, 15 seconden
03 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia tunaangazia maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa. Makala tunatupeleka nchini Ghana kumulika umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili, na mashinani tunakupeleka nchini China kusikia ujumbe wa mdau kuhusu lugha y aKiswahili.Hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Maadhimisho haya yanafanyika tarehe 3 kwa kuwa siku yenyewe ya Kiswahili duniani yaani tarehe 7 Julai itaangukia siku ya Jumapili na Anold Kayanda anafuatilia kwenye maadhimisho hayo.Tukiendlea na maadhimisho ya Siku ya Kiswahili duniani mwenzetu Assumpta Massoi naye anafuatilia maadhimisho hayo na ametuandalia taarifa pamoja na mazungumzo yake na aliyehudhuria maadhimisho hayo.Katika makala Bosco Cosmas anatupeleka nchini Ghana kumulika umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili.Na katika mashinani Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili inaadhimishwa Jumapili Julai 7, Masika Yang, Mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) anatoa ujumbe kuhusu lugha ya Kiswahili.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
3-7-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili nchini Ghana
Hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika maadhimisho ya tatu ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani maudhui yakiwa nafasi ya elimu ya sanaa katika kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili.Maadhimisho haya yanafanyika tarehe 3 kwa kuwa siku yenyewe ya Kiswahili duniani yaani tarehe 7 Julai itaangukia siku ya Jumapili. Katika makala hii Bosco Cosmas anatupeleka nchini Ghana kumulika umahiri wa wanafunzi wa Kiswahili.
3-7-2024 • 3 minuten, 27 seconden
02 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia tukio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jana Julai Mosi la kuidhinisha tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani kama zifutazo…Huko Gaza shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA linasema wiki chache tu baada ya jeshi la Israeli kulazimisha watu kurejea mji wa Khan Younis ulioharibiwa, leo hii mamlaka za Israeli zimetoa amri mpya ya kuhama kutoka eneo hilo licha ya kwamba hakuna pahala paliko salama Ukanda wa Gaza. Watu 250,000 watalazimika kuhama tena.Nchini Sudan vita ikiendelea kurindima, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeziongeza Libya na Uganda kama nchi zinazopokea wakimbizi kutoka Sudan na hivyo kufanya nchi zinazowapokea kufikia saba zikiwemo Libya, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sudan Kusini, Chad na Ethiopia, na sasa linahitaji fedha dola bilioni 1.5 badala ya dola bilioni 1.4 iliyotangazwa awali.Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Bruno Lemarquis, amelaani vikali shambulio la tarehe 30 Juni mwaka huu dhidi ya msafara wa shehena za misaada ya kiutu huko Butembo jimboni Kivu Kaskazini, shambulio lililosababisha vifo vya wahudumu wawili wa misaada ya kibinadamu. Bwana Lemarquis ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki za watumishi hao.Na katika mashinani tutamsikia Estelle Zadra wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni (UNESCO) akieleza mikakati yao katika kukuza lugha ya Kiswahili duniani.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
2-7-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Hizi ndizo shughuli zetu CIMIC ya TANBAT 7 - Kapteni John Zablon Mashamy
Kutokana na hali tete ya usalama nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Umoja wa Mataifa kwa miaka mingi umekuwa ukifanya juhudi za kuleta amani na kuilinda kwa kutuma ujumbe wake, MINUSCA ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa huchangia vikosi mbalimbali. Kikosi cha 7 kutoka Tanzania, TANBAT 7 ni miongoni mwa walinda amani waliko huko, hususani wakihudumu katika eneo la Berbérati, magharibi mwa nchi.Kupitia makala hii, Afisa uhusiano wa TABAT 7, Kapteni John Zablon Mshamy anaeleza shughuli zinazofanywa na kitengo cha uhusiano, CIMIC anachokiongoza.
1-7-2024 • 3 minuten, 18 seconden
Watu wasiojulikana wapora shehena ya msaada wa chakula nchini Sudan
Huko nchini Sudan, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP linasema msafara wake uliokuwa umesheheni misaada ya vyakula umeshambuliwa hii leo na watu wasiojulikana. Kupitia ukurasa wake wa X, zamani Twitter, WFP imesema watu wasiojulikana waliokuwa na silaha walishambulia malori matatu yaliyokuwa na msaada huo wa chakula ukilekea jimbo la kati la Darfur.WFP inasema shehena hiyo iliyoibwa ililenga maelfu ya watu wenye uhitaji.Hivyo shirika hilo limesihi mamlaka husika kwenye eneo hilo ihakikishe waliofanya kitendo hicho wanawajibishwa.Kufuatia kitendo hicho, Clementine Nkweta-Salami ambaye ni Mratibu Mkazi wa Misaada ya kibinadamu Sudan, ametumia ukurasa wake wa X kueleza kuwa kuporwa kwa shehena hizo kunamaanisha chakula kinachohitajika hakitafikia walengwa.Amesema uporaji umefanyika wakati wanakimbizana na muda kuepusha baa la njaa Sudan na kwamba kuwaibia walengwa chakula ni jambo la kusikitisha.
1-7-2024 • 0
01 JULAI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini Sudan, na uhamasishaji wa wakulima nchini Zambia kuachana na kilimo cha tumbaku na badala yake kulima mazao mbadala. Makala inatupeleka nchini CAR na mashinani nchini Ghana, kulikoni?Huko nchini Sudan, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP linasema msafara wake uliokuwa umesheheni misaada ya vyakula umeshambuliwa hii leo na watu wasiojulikana.Nchini Zambia, mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, Kanda ya Afrika wa kuhamasisha wakulima kuachana na kilimo cha tumbaku na badala yake kulima mazao mbadala umeanza kuzaa matunda kama anavyoelezea mmoja wa wakulima walioitikia wito huo.Makala inakupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kumsikiliza Afisa Uhusiano wa Kikosi cha 7 kutoka Tanzania kinacholinda amani chini ya Ujumbe wa kulinda amani nchini CAR, MINUSCA, Kapteni John Zablon Mshamy akieleza shughuli za kitengo cha kijeshi kinachofahamika kama CIMIC katika shughuli za ulinzi wa amani.Mashinani ikiwa hivi karibuni dunia itasheherekea siku ya Kiswahili Duniani ambayo bila shaka ni bidhaa ya kimataifa, tunakuletea ujumbe wa Dkt. Felix Sosoo, Mhadhiri wa lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Ghana akitoa maoni yake kuhusu wanaobeza lugha ya Kiswahili.”Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
1-7-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Mkulima Zambia: Tumegeukia mazao ya chakula kulinda afya badala ya tumbaku
Nchini Zambia, mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, Kanda ya Afrika wa kuhamasisha wakulima kuachana na kilimo cha tumbaku na badala yake kulima mazao mbadala umeanza kuzaa matunda kama anavyoelezea mmoja wa wakulima walioitikia wito huo.Tuko wilaya ya Chipangali nchini Zambia ambako video ya WHO kanda ya Afrika inaanzia katikati ya shamba lililostawi la mahindi na mtu mmoja akitembea katikati na kisha anajitokeza akiwa na tabasamu! Huyu ni Titus Mwanza, mkulima wa zamani wa tumbaku ambaye amekipa kisogo kilimo hicho na kugeukia mazao mengine. Kulikoni?“Niliacha kulima tumbaku miaka minne iliyopita Kilichonifanya niache kulima zao hili ni matatizo yaliyokuweko kwenye familia yangu, na faida haikuwa nzuri. Vile vile ugonjwa wa saratani au kansa unaohusishwa na zao hili. Wale wanaovuta wanapata aina mbali mbali za magonjwa.”Uelewa huu unafuatia ziara ya mwishoni mwa mwaka 2022, ambapo Bwana Mwanza na wakulima wenzake wawili kutoka Zambia walishiriki ziara ya mafunzo nchini Kenya ambako mashamba ya kwanza kabisa yasiyo na tumbaku yalianzishwa mwaka 2021. Katika mashamba hayo wakulima 6,000 wa tumbaku tayari wameacha kulima zao hili na wanalima mazao mbadala.Baada ya kurejea Zambia anasema,“Niliacha kilimo cha tumbaku na kuanza kulima mazao mengine. Mazao kama maharage ya soya, alizeti, karanga na maharage. Hayo ndio mazao ninayolima kwa sasa.”Bwana Mwanza amekuwa mkulima kiongozi akifundisha wenzake kilimo mbadala na tayari amefundisha wakulima 50.“Kinachotuhamasisha ni kwamba tunalima kile ambacho baadaye tunakula. Tunalima mahindi, kisha tunakula. Tunalima mbaazi, kisha tunakula. Tunatengeneza maziwa kutokana na maharage ya soya. Vile vile tunatumia maharage ya soya kutengeneza soseji. Ni kitu ambacho tunalima na kisha tunakula. Ni chakula chenyewe. Tumbaku sio chakula, tumbaku ni dawa.”Video inatamatika huku Bwana Mwanza akiwa kwenye shamba lake la mahindi lililostawi vizuri, mahindi yamekomaa na tabasamu kamili usoni mwake.
1-7-2024 • 2 minuten, 7 seconden
Manusura wa mafuriko yaliyokumba taifa la Tanzania washukuru UNICEF
Makala hii inatupeleka nchini Tanzania ambapo Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania anamulika usaidizi wa shirika hilo kwa manusura wa mafuriko yaliyokumba taifa hilo la Afrika Mashariki.
28-6-2024 • 3 minuten, 33 seconden
28 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya mwaka 2024 ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs, na juhudi za mashirika ya Umoja wa Mataifa za kuwawezesha wakulima nchini Somalia. Makala tunakupeleka nchini Tanzania, na mashinani ujumbe ubunifu na vijana barani Afrika.Bila uwekezaji mkubwa na kuongeza hatua, kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kutasalia kuwa mgumu, imeonya Ripoti ya mwaka huu 2024 kuhusu mwenendo wa utekelezaji wa malengo hayo ikiwa imesalia miaka sita pekee kufikia muda ambao ulimwengu ulijiwekea kuwa umeyatimiza malengo yote 17.Huku takriban watu milioni 7 nchini Somalia wakihitaji msaada wa kuokoa maisha mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linahimiza jumuiya ya kimataifa kuendelea kuunga mkono Wasomali wanaokabiliwa na athari za njaa,mabadiliko ya tabianchi, migogoro na kufurushwa makwao.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Tanzania anamulika usaidizi wa shirika hilo kwa manusura wa mafuriko yaliyokumba taifa hilo la Afrika Mashariki.Mashinani tutasikia jinsi shirika la umoja wa mataifa la Afya ulimwenguni, WHO linakuza ubunifu miongoni mwa wanasayansi vijana wa afya barani Afrika ili kuboresha ufanisi, ubora wa huduma za afya na maendeleo katika matibabu na tiba.”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
28-6-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa yaonya kuwa dunia inashindwa kutimiza SDGs
Bila uwekezaji mkubwa na kuongeza hatua, kufikiwa kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs kutasalia kuwa mgumu, imeonya Ripoti ya mwaka huu 2024 kuhusu mwenendo wa utekelezaji wa malengo hayo ikiwa imesalia miaka sita pekee kufikia muda ambao ulimwengu ulijiwekea kuwa umeyatimiza malengo yote 17.Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa iliyowekwa wazi leo Juni 28 inafichua kuwa ni asilimia 17 tu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ndio yako katika mwenendo mzuri, huku karibu nusu ikionesha maendeleo madogo au ya wastani, na zaidi ya theluthi moja yamekwama au kurudi nyuma. Athari zinazoendelea za janga la COVID-19, mizozo inayoongezeka, mivutano ya kijiografia na kuongezeka kwa machafuko ya tabianchi kumezuia maendeleo kwa kiasi kikubwa.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo asubuhi ya leo kwa saa za New York, Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anasema,"kushindwa kwetu kupata amani, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, na kuongeza fedha za kimataifa kunadhoofisha maendeleo. Ni lazima tuharakishe hatua kwa ajili ya Malengo ya Maendeleo Endelevu na hatuna muda wa kupoteza."Kulingana na ripoti hiyo, watu zaidi ya milioni 23 walisukumwa katika ufukara na zaidi ya watu milioni 100 zaidi walikuwa wakikabiliwa na njaa mwaka wa 2022 ikilinganishwa na mwaka 2019. Idadi ya vifo vya raia katika vita vya kijeshi iliongezeka mwaka jana 2023. Mwaka huo pia ulikuwa wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa huku halijoto duniani ikikaribia kiwango cha juu cha nyuzijoto 1.5 za Selsiasi.
28-6-2024 • 1 minuut, 37 seconden
FAO yafanikisha miradi ya kusaidia jamii nchini Somalia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Huku takriban watu milioni 7 nchini Somalia wakihitaji msaada wa kuokoa maisha mwaka huu, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linahimiza jumuiya ya kimataifa kuendelea kuunga mkono Wasomali wanaokabiliwa na athari za njaa,mabadiliko ya tabianchi, migogoro na kufurushwa makwao. FAO sio kwamba wao wanahimiza wengine kusaidia wasomali, bali wao pia na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa wanatekeleza miradi mbalimbali yakuwasaidia wananchi wa Somalia hususan katika kuhakikisha wana uhakika wa kujipatia chakula na kupunguza athari za vichocheo muhimu vya uhaba wa chakula ambavyo ni kama vile mafuriko, ukame, bei juu za chakula pamoja na migogoro.Programu zinazotekelezwa ni pamoja na kuboresha kinga na kujiandaa kwa majanga ya chakula katika jamii za vijijini, kuimarisha uzalishaji wa mifugo, na kutoa mafunzo kwa wakulima kuhusu kilimo kinachozingatia hali ya hewa.Bi. Edeba Ali Hassan (33), ni mkulima aliyelazimika kukimbia huko Bakool kutokana na machafuko na kuhamia Dolow, ni mnufaika wa programu iitwayo Mpango wa Hatua za Pamoja za Ustahimilivu – JOSP unaotekelezwa na FAO kwa ushirikiano na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Mpango wa Chakula Duniani (WFP).Bi. Edeba anasema programu hiyo imempatia fedha taslimu, pembejeo za kilimo kwa misimu miwili, amepewa shamba pamoja na mfumo wa umwagiliaji unaotumia nishati ya jua.“Nina watoto 10, na siwezi kuwahudumia kwa sababu hakuna kazi isipokuwa kilimo, ndiyo maana nilijiunga na Mpango wa Pamoja wa Ustahimilivu.”Alexander Jones, Mkurugenzi, Idara ya Uhamasishaji Rasilimali wa FAO anasema programu wanazozitekeleza nchini Somalia zinalenga zaidi kusaidia watu katika kupata uhakika wa chakula katika maeneo ambayo mara kwa mara yanaathiriwa na ukame na mafuriko.“Mradi wa JOSP unasaidia kukarabati eneo kubwa lenye takriban wanufaika milioni 1.5 kupitia usimamizi wa maji, kupitia programu za kijamii za maji, kwa ajili ya maeneo yanayoathirika na mafuriko na ukame.”Mpango huu mkubwa wa kuleta mabadiliko nchini Somalia unatekelezwa kwa ufadhili kutoka kwa Ubalozi wa Uingereza mjini Mogadishu, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kujenga Amani (UNPBF), pamoja na michango inayotarajiwa kutoka kwa shirika la Marekani la misaada ya maendeleo USAID na Mfuko wa Pamoja wa Somalia (SJF).
28-6-2024 • 1 minuut, 55 seconden
Methali: “Chombo cha kuzama hakina usukani.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Chombo cha kuzama hakina usukani.”
27-6-2024 • 1 minuut, 8 seconden
27 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikiangaazia hafla maalum ya UNICEF na wadau wake pamoja na wasanii iliyofanyika Nairobi Kenya, mada ikiwa “Ungana na watoto wa Sudan”. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za maandamano Kenya, Janga la njaa Sudan, na MSMEs. Katika kujifunza kiswahili tunakuletea uchambuzi wa methali.Kufuatia madhila yaliyotokana na maandamano makubwa nchini Kenya dhidi ya mswada wa fedha, leo Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR imeeleza kwamba Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk amesikitishwa na vifo na kujeruhiwa kwa watu.Zaidi ya Wasudan milioni 25 yaani zaidi ya nusu ya idadi ya watu wote nchini humo wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa ya viwango vya Uhakika wa Chakula (IPC) kutokana na tathimini iliyofanywa kati ya mwishoni mwa mwezi Aprili na mapema mwezi huu wa Juni.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya biashara ndogo sana, ndogo na za ukubwa wa kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii amesisitiza jukumu muhimu la wajasiriamali hao katika uchumi wa kimataifa, ikiangaziwa michango yao katika uundaji wa nafasi za kazi, ukuaji wa uchumi, na uwezeshaji wa makundi mbalimbali yaliyotengwa.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Chombo cha kuzama hakina usukani.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
27-6-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Ulevi na matumizi ya dawa za kulevya inaathiri afya, pata usaidizi uondokane nazo
Ripoti iliyotolewa jana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO imesema mamilioni ya vifo vinachangiwa na unywaji pombe na matumizi ya dawa za kulevya na imetoa wito wa haraka wa kutekeleza lengo namba 3.5 la Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG la kupunguza matumizi ya pombe na dawa za kulevya na kuboresha upatikanaji wa matibabu bora kwa matatizo ya matumizi ya dawa. Halikadhalika leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya kutokomeza matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na ulanguzi wa madawa hizo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa na Uhalifu (UNODC) wamechapisha ripoti yao inayosisitiza haki ya afya kwa wote ikiomba Umoja wa Mataifa kuongza kasi katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa. Kevin Keitany wa redio Washirika wetu Domus FM anatupeleka nchini Kenya kufuatilia juhudi za mashirika ya kiraia na serikali hasa katika huduma za afya kwa waathirika wa madawa ya kulevya na pombe.
26-6-2024 • 4 minuten, 30 seconden
26 JUNI 2024
Hii leo jaridani Tunafuatilia machafuko yaliyotokana na maandamano yaliyoanza nchini Kenya, na ripoti ya utumiaji wa dawa za kulevya. Makala tunarejea nchini Kenya kufuatilia matibabu ya waathirika wa dawa za kulevya na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni?Viongozi wa Umoja wa Mataifa wamekazia wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres kwa mamlaka za Kenya kufuatia machafuko yaliyotokana na maandamano yaliyoanza nchini humo Juni 18 kupingwa muswada wa fedha wa mwaka 2024.Kuibuka kwa dawa mpya za kulevya za kutengenezwa na rekodi ya usambazaji na mahitaji ya dawa zingine kumeongeza athari za dawa hizo ulimwenguni, na kusababisha kuongezeka kwa shida za utumiaji wa dawa za kulevya na madhara kwa mazingira, imesema leo Ripoti ya Dunia ya Dawa ya 2024 iliyozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa ya kukabili dawa za kulevya na uhalifu, UNODC.Katika makala leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya kutokomeza matumizi mabaya ya madawa ya kulevya na ulanguzi wa madawa hizo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa na Uhalifu (UNODC) wamechapisha ripoti yao inayosisitiza haki ya afya kwa wote ikiomba Umoja wa Mataifa kuongza kasi katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa. Kevin Keitany wa redio Washirika wetu Domus FM anatupeleka nchini Kenya kufuatilia juhudi za mashirika ya kiraia na serikali hasa katika huduma za afya kwa waathirika wa madawa ya kulevya na pombe.Mashinani tunaelekea nchini Sudan kusikia simulizi ya mwathirika wa vita inayoendelea nchini humo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
26-6-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Viongozi wa UN wasihi haki ya watu kuandamana Kenya iheshimiwe - Kenya
Viongozi wa Umoja wa Mataifa wamekazia wito uliotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Antonio Guterres kwa mamlaka za Kenya kufuatia machafuko yaliyotokana na maandamano yaliyoanza nchini humo Juni 18 kupingwa muswada wa fedha wa mwaka 2024. Maandamano yalianza Juni 18, yakiongozwa na vijana wakitaka muswada huo wa fedha ukataliwe wakidai yaliyomo yatasababisha maisha kuwa magumu zaidi.Mathalani ongezeko la kodi kwenye bidhaa muhimu kama vile mkate na taulo za kike, mapendekezo ambayo baadaye yaliondolewa kwenye rasimu na Bunge.Wabunge waliupitisha muswada huo jana Jumanne kitendo kilichochochea maandamano zaidi katika kaunti mbali mbali za Kenya na ambapo vyombo vya habari vinaripoti vifo zaidi ya watu 18, na wengine wamejeruhiwa.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia msemaji wake alisema..“Ni muhimu sana haki za watu kuandamana kwa amani zizingatiwe. Kama tusemavyo duniani kote. Ni muhimu pia mamlaka zihakikishe kuwa haki hizo zinalindwa, na matukio ya vifo mikononi mwa vikosi vya usalama yachunguzwe. Watu wawajibishwe, polisi wa Kenya, mamlaka na jeshi wajizuie, na kwa waandamanaji waandamane kwa amani. »Inger Anderesen ambaye ni Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP pamoja na kuunga mkono kauli ya Katibu Mkuu amesihi mamlaka za Kenya kuhakikisha maandamano ya amani yanaweza kufanyika nchini Kenya.Bi. Andersen amesikitishwa pia na ripoti za vifo na majeruhi na kutuma salamu za rambirambi kwa familia ambazo zimepoteza wapendwa wao.Naye Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya, Stephen Jackson yeye ametumia ukurasa wake wa X kuchapisha ujumbe wa Katibu Mkuu Guterres.Wakati huo huo, Rais wa Kenya William Rutto amehutubia taifa kwa mara ya pili ndani ya chini ya saa 24 na kusema pamoja na kwamba bunge limepitisha na mabadiliko, na wananchi wamezungumza kupitia maandamano kuukataa, ameamua kutotia saini muswada huo na hivyo utaondolewa bungeni na amekubaliana na wabunge kuwa ni uamuzi wao wa pamoja.
26-6-2024 • 1 minuut, 46 seconden
Utumiaji wa dawa za kulevya umeongezeka 2024 - Ripoti ya dawa za kulevya
Kuibuka kwa dawa mpya za kulevya za kutengenezwa na rekodi ya usambazaji na mahitaji ya dawa zingine kumeongeza athari za dawa hizo ulimwenguni, na kusababisha kuongezeka kwa shida za utumiaji wa dawa za kulevya na madhara kwa mazingira, imesema leo Ripoti ya Dunia ya Dawa ya 2024 iliyozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa ya kukabili dawa za kulevya na uhalifu, UNODC . Kwa mujibu wa ripoti hiyo idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya ulimwenguni imeongezeka na kufikia watu milioni 292 mwaka 2022 ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 katika kipindi cha miaka 10.Akizindua ripoti hiyo jijini Vienna Austria Mkurugenzi Mkuu wa UNODC Ghada Waly ameeleza kuwa uzalishaji wa dawa za kulevya na matumizi yake unazidisha ukosefu wa utulivu na usawa wakati huo huo ukisababisha madhara makubwa kwa afya, usalama na ustawi wa watu.“Tunahitaji kutoa matibabu yaliyofanyiwa uchunguzi na kuwa na Ushahidi wa kuweza kusaidia wale walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya huku tukilenga soko haramu la dawa za kulevya na kuwekeza zaidi katika kuzuia matumizi ya dawa hizo.” Amesema Bi. Waly.Matumizi ya bangi yamesalia kutumika zaidi duniani kote ambapo kuna watumiaji watumiaji milioni 228.Ripoti hiyo pia imesema uzalishaji wa cocaine umeweka rekodi mpya ya juu ya uzalishaji wa tani 2,757 mwaka2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 zaidi tangu mwaka 2021.Ingawa wastani wa watu milioni 64 duniani kote wanakabiliwa na matatizo yatokanayo na matumizi ya madawa ya kulevya, ni mtu mmoja tu kati ya 11 anayetibiwa.Wanawake wanapata huduma ndogo zaidi za matibabu ikilinganishwa na wanaume.Ripoti hiyo imeeleza jinsi haki ya afya ni haki ya binadamu inayotambulika kimataifa ambayo ni ya binadamu wote, hivyo kutaka wale wote wanaotumia dawa za kulevya kupata haki yao ya matibabu hatakama wameshikiliwa na vyombo vya dola.Kusoma ripoti kamili bofya hapa.
26-6-2024 • 1 minuut, 54 seconden
FAO yaimarisha Afya ya Mifugo Kupitia mradi wa ISAVET nchini Tanzania
Nchini Tanzania, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linaendesha programu ya mafunzo yanayolenga kuboresha ujuzi wa wataalamu wa mifugo katika kudhibiti magonjwa ya wanyama na kuimarisha afya ya mifugo ili kuihakikishia jamii uhakika wa chakula na chakula salama. John Kabambala wa redio washirika wetu KidsTime ya mkoani Morogoro Tanzania amezungumza na wadau kandoni mwa mafunzo hayo.
25-6-2024 • 5 minuten, 8 seconden
25 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulikaza juhudi za kuimarisha afya ya mifugo ili kuihakikishia jamii uhakika wa chakula na chakula salama. Pia tunakuletea muhutasari wa habari zikiwemo za Gaza, mabaharia, na ripoti ya ya matumizi ya pombe. Mashinani tunasalia na siku ya mabaharia duniani. Katika Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati tathmini mpya iliyofanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula Duniani WFP imethibitisha wasiwasi wa kuendelea kuwepo kwa viwango vya njaa ambapo asilimia 96 ya wananchi wanakabiliwa na uhaba wa chakula.Leo ni siku ya mabaharia duniani ikibeba maudhui ya kuangalia usalama wao kazini. Katika ujumbe wake kwa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kukomeshwa kwa vitendo vya kiharamia vya meli kutekwa nyara na kueleza kuwa mabaharia hawapaswi kuwa waathiriwa wa migogoro ya kijiografia na kisiasa.Na ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO imeonesha vifo milioni 2.6 kwa mwaka vinachangiwa na unywaji pombe hii ikiwa ni sawa na asilimia 4.7 ya vifo vyote duniani, na vifo laki sita kwa matumizi ya dawa za kulevya.Mashinani leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mabaharia, na kupitia ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya baharí, IMO Arsenio Dominguez anawatakia kila la heri mabaharia wote akiwaalika katika meza ya kubonga bongo kuhusu masuala ya usalama wa baharini.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
25-6-2024 • 9 minuten, 53 seconden
India: Majiko yaliyoboreshwa yaondolea adha wanawake kuvaa miwani wakipika
Katikati ya bonde la mto Ganges kaskazini mwa India, ndiko liko jimbo la Bihar ambalo sasa linahaha kutokana na uchafuzi wa hewa, kwani moshi utokao kwenye majiko ya kuni na samadi ya ng’ombe yanasababisha kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa hewa. Licha ya maendeleo makubwa ya kutumia gesi kama chanzo cha nishati, halikadhalika nishati itokanayo na samadi, bado familia au kaya maskini zinashindwa kumudu vyanzo hivyo na kujikuta vikutumia kuni au samadi ya ng’ombe kupikia, ambavyo huchafua hewa. Sasa Benki ya Dunia imewezesha kuundwa kwa vikundi vya kujiwezesha au SHGs ambapo wanawake wanapatiwa elimu ya masuala mbali mbali ikiwemo nishati salama na hivyo kuboresha afya zao. Assumpta Massoi kupitia video ya Benki ya Dunia amefuatilia mradi huo na kuandaa makala hii.
24-6-2024 • 2 minuten, 44 seconden
UNMISS ziarani Nadiangere na uzinduzi wa shule ya msingi
Ikiwa ni moja ya majukumu yake, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wakishirikiana na mamlaka za mitaa za nchi hiyo umefanya ziara maalum katika Kijiji cha Nadiangere na kusikiliza kero za wananchi pamoja kuzindua shule mpya ya msingi. Ndege ya UNMISS ikiwa na timu ya walinda amani na wawakilishi kutoka serikali za mitaa inafika kijiji cha Nadiangere kilichoko katika jimbo la Equatorial Magharibi na kulakiwa kwa shamsham na wananchi wa kijiji hicho wakiamini msemo wa Kiswahili usemao “Mgeni njoo mwenyeji apone.” Katika mkutano wa pamoja, wananchi hao walieleza changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo ukosefu wa huduma za kimsingi kama viles hule, huduma za afya pamoja na usalama. Wananchi hao wakaeleza uhaba huu umechangiwa na kuwasili kwa wakimbizi wa ndano wanaokimbia kuzuka kwa vurugu za wenyewe kwa wenyewe hivi karibuni huko karibu na eneo la Tambura. Severina Angelo mwenye umri wa miaka 21, mama wa watoto wawili akapaza sauti.“Tumechoka sana, tunahitaji amani, tumeshateseka sana. Tunahitaji shule, tunahitaji hospitali na vitu vingine vingi ambavyo tunakosa.”Jane Lanyero Kony, Ni Mkuu wa Ofisi ya UNMISS kwa jiji la Yambio na anawaeleza wanakijiji hao kuwa “Subira yavuta heri.”“Unajua sisi tuko hapa kusikiliza changamoto zenu ni zipi na kisha tunaporudi ofisini tunaenda kuangalia ni kwa kiwango gani tunaweza kuhamasisha upatikanaji wake miongoni mwa jumuiya ya Umoja wa Mataifa. Kama UNMISS, tunaendelea kufanya kile ambacho ni mamlaka yetu, ambacho ni, ulinzi wa raia. Tunaendelea kufanya kazi na serikali, ili kukamilisha juhudi zao za kulinda kila raia nchini Sudan Kusini.”Mbali na kuwasikilisha wananchi pia wamezindua shule ya msingi iliyojengwa kwa ufadhili wa UNMISS katika eneo hilo. Shule hiyo ina vyumba vitatu vya madarasa, ofisi ya walimu, na inatoa mazingira bora ya kujifunzia kwa zaidi ya wasichana na wavulana 300.
24-6-2024 • 1 minuut, 47 seconden
24 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu Gaza hasa kwa watoto, na ziara maalum ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS. Makala inatupeleka nchini India na mashinani nchini Uganda, kulikoni? Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, Philippe Lazzarini, hii leo Juni 24 ametahadharisha vikali kwamba UNRWA itaporomoka kama ufadhili hautapatikana haraka, na "kizazi kizima" cha watoto wako katika hatari ya kuangukia kwenye "umaskini, chuki na migogoro ya baadaye”. Ikiwa ni moja ya majukumu yake, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS wakishirikiana na mamlaka za mitaa za nchi hiyo umefanya ziara maalum katika Kijiji cha Nadiangere na kusikiliza kero za wananchi pamoja kuzindua shule mpya ya msingi..Katika makala Assumpta Massoi anatupeleka India kumulika jinsi mradi wa Benki ya DUnia umeondolea kaya adha ya changamoto za kiafya na kiuchumi zitokanazo na matumizi ya kuni na samadi ya ng'ombe kwenye kupikia.Na mashinani tunaelekea nchini Uganda kusikia ujumbe wa kiongozi wa jamii ambaye ni mkimbizi kutoka Sudan Kusini.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
24-6-2024 • 9 minuten, 52 seconden
‘Kizazi kizima’ kinaweza kupotea Palestina, Mkuu wa UNRWA aonya
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, Philippe Lazzarini, hii leo Juni 24 ametahadharisha vikali kwamba UNRWA itaporomoka kama ufadhili hautapatikana haraka, na "kizazi kizima" cha watoto wako katika hatari ya kuangukia kwenye "umaskini, chuki na migogoro ya baadaye”. Katika ombi la uungwaji mkono wa kisiasa na kifedha kutoka kwa Mataifa Wanachama wa Umoja wa Mataifa alilolitoa mbele ya Kamisheni ya Ushauri ya UNRWA mjini Geneva, Uswisi, Philippe Lazzarini amesisitiza kwamba shirika hilo linajikongoja chini ya uzito wa mashambulizi yasiyokoma huko Gaza baada ya karibu miezi tisa ya mashambulizi makali ya Israel.Mbali na wafanyakazi 193 wa UNRWA waliouawa tangu mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas na utekaji nyara kuzusha vita, Bwana Lazzarini ameeleza kwa kina ukubwa wa uharibifu huo katika majengo ya Umoja wa Mataifa akisema sasa shinikizo kwa shirika hilo ni kubwa zaidi.Amesema zaidi ya miundombinu 180 imevunjwa au kuharibiwa tangu Oktoba 7 na takribani watu 500 wameuawa wakitafuta ulinzi chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa."Majengo yetu yametumiwa kwa madhumuni ya kijeshi na Israel, Hamas na makundi mengine yenye silaha ya Palestina," mkuu huyo wa UNRWA amewaeleza wajumbe akiongeza kuwa, misafara ya UNRWA imeshambuliwa na hivyo nafasi ya uutendaji kazi inapungua.Akiangazia jinsi Gaza ilivyo sasa, Lazzarini amesema ni kuzimu kwa zaidi ya watu milioni mbili huko, akibainisha kuwa watoto wanaendelea kufa kwa utapiamlo na upungufu wa maji mwilini, "huku chakula na maji safi vikisubiri kwenye malori" nje ya eneo hilo.
24-6-2024 • 1 minuut, 47 seconden
UN Women: Wanawake Gaza hawataki kufa au kuzika wapendwa wao
Baada ya ziara ya wiki moja huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, Maryse Guimond ambaye ni Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli,Israeli amesema kilicho alichoshuhudia hakina maelezo ya kutosha.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kutokea mjini Yerusalemu, Bi. Guimond amesema unapoingia tu kwenye kivuko cha Shalom na lango linafungwa, unahisi umefungiwa kwenye dunia ya uharibifu. Kuanzia shule, hospitali, makazi yaliyolundikana watu na uhaba wa vitu, watu wakihaha kusaka usalama, wanawake wakimuuliza vita itakoma lini? Na zaidi ya yote. “Wakazi wa Gaza wanataka hii vita ikome. Kila siku ambayo mzozo huu unaendelea, inazidi kuleta uharibifu na mauaji. Lazima hii ikome. Wavulana na wasichana walikuwa wananiuliza ni lini vita hii itaisha? Nami sikuwa na jibu la kuwapatia.” Akaendelea kusema.. “Gaza ni zaidi ya simulizi zaidi ya milioni mbili za kupoteza. Kila mwanamke niliyekutana naye ana simulizi ya kupoteza mtu. Zaidi ya wanawake 10,000 wamepoteza wapendwa wao. Zaidi ya familia 6,000 zimepoteza mama zao. Wanawake na wasichana milioni 1 wamepoteza utu wao, makazi yao, familia zao na kumbukumbu zao.” Bi. Guimond akasema kwa sasa.."Swali si kwamba ni nini wanawake wanahitaji: Swali linapaswa kuwa ni nini wanawake hawahitaji. Wanawake hawataki kufa, hawataki kuzika wapendwa wao, hawataki kubakia wenyewe kupata machungu.”
21-6-2024 • 2 minuten, 14 seconden
UNHCR: Utoaji wa vitambulisho kwa wakimbizi nchini Ethiopia waboresha maisha yao
Wakati dunia hapo jana Juni 20 ikiwa imeadhimisha siku ya wakimbizi duniani na wito kutolewa kila kona wa kuhakikisha wakimbizi wanajumuishwa katika masuala yote ya kuweza kuwasaidia kustawi katika nchi wanayopatiwa hifadhi hii leo tunaelekea nchini Ethiopia kujionea namna mradi wa kutoa vitambulisho vya kitaifa ambao unajumuisha wakimbizi na wasaka hifadhi ulivyobadiliasha maisha ya wakimbizi. Makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR inathibitisha namna mradi huo wa vitambulisho vya kitaifa uliofadhiliwa na Benki ya Dunia umeleta matumaini pamoja na upatikanaji wa ajira kwa wakimbizi na hivyo kuwaondoa katika kundi la watu tegemezi kwani sasa wanaweza kufanya shughuli za kuwaingizia kipato. Leah Mushi anatujuza zaidi.
21-6-2024 • 3 minuten, 8 seconden
Jengo la uchunguzi wa magonjwa ya mlipuko mpakani Mutukula lakabidhiwa kwa serikali ya Tanzania
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni (WHO) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), hivi karibuni limekabidhi kwa Wizara ya Afya nchini humo jengo maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wanaohisiwa kuwa na magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza wanapopita katika mpaka wa Mutukula unaounganisha Tanzania na Uganda kaskazini. Hatua hii ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mapema dhidi ya milipuko ya magonjwa imekuja ukiwa umetimia mwaka mmoja kamili tangu mlipuko wa ugonjwa wa Homa ya virusi vya Marburg ulipotangazwa kuisha kabisa nchini Tanzania baada ya kuwa umetokea mwanzoni mwa mwaka jana 2023 katika mkoa wa Kagera kaskazini magharibi mwa nchi.Dkt. Janeth Masuma, Afisa wa Kitengo cha WHO Tanzania cha kuzuia na kudhibiti maambukizi anasema, “kwa hiyo kwa kuwa na mafanikio haya makubwa ya jengo la utambuzi wa wagonjwa katika mpaka wa Mutukula kutasaidia uchunguzi wa haraka na kuwatenganisha wote wanaohisiwa kuwa na maambukizi ili kuhakikisha mipaka yote imelindwa, kulinda nchi nyingine na kuhakikisha kwamba hakuna wasafiri wowote watapeleka ugonjwa nje ya Tanzania kwa mujibu wa mapendekezo na wajibu wa afya kimataifa.”Salum Rajab Kimbau, Mratibu wa Chanjo wa Mkoa wa Kagera anaeleza ilivyo faida kubwa kuwa na jengo la namna hii mpakani akisema, “huu mradi kiujumla una faida kwenye mkoa. Tumeupokea na kufurahi na pia furaha hii iko upande wa halmashauri ya mkoa n anchi kwa ujumla. Mradi una sehemu mbili za matibabu na kinga. Awali tulikuwa tunatumia hema moja ambalo lilikuwa linakusanya wahisiwa wote wa kike na wa kiume lakini hata mazingira yenyewe siyo rafiki kwa maana ya joto kali lakini pia akiingia mgonjwa badala ya kupona kwa haraka au badala ya kukaa kustahimili vizuri inakuwa kazi.”Kituo hiki ni moja ya afua nyingi zinazoendelea ili kuhakikisha uimarishaji wa mifumo ya afya nchini Tanzania ili kuongeza kasi ya ajenda ya afya kwa wote.
21-6-2024 • 1 minuut, 53 seconden
21 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake huko Gaza, na masuala ya afya nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Ethiopia na mashinani tunasalia nchini Tanzania, kulikoni? Baada ya ziara ya wiki moja huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati, Maryse Guimond ambaye ni Mwakilishi Maalum wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli,Israeli amesema kilicho alichoshuhudia hakina maelezo ya kutosha. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni (WHO) nchini Tanzania kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), hivi karibuni limekabidhi kwa Wizara ya Afya nchini humo jengo maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wanaohisiwa kuwa na magonjwa ya mlipuko ya kuambukiza wanapopita katika mpaka wa Mutukula unaounganisha Tanzania na Uganda kaskazini.Makala inatupeleka nchini Ethiopia ambako nchi hiyo kwasasa inatekeleza mpango wa kihistoria wa utoaji wa vitambulisho vya kitaifa unaojumuisha wakimbizi na wasaka hifadhi.Na mashinani tutakepeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe wa watoto kuhusu elimu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
21-6-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Methali: “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”
20-6-2024 • 1 minuut, 6 seconden
20 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Japan kufuatilia harakati za kusongesha teknolojia rafiki na nafuu ili dunia iwe mahali salama kwa miti na binadamu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo, na uchambuzi wa methali.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi, Umoja wa Mataifa umeitumia siku hii kutoa wito wa mshikamano na wakimbizi kote duniani. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema, "wanapopewa fursa, wakimbizi hutoa mchango mkubwa kwa jamii zinazowahifadhi."Mashambulizi ya Israel kwa kutumia mabomu kutoka angani, nchi kavu na baharini yanaendelea kuripotiwa katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza, na kusababisha vifo zaidi vya raia, kuhama makazi yao, na uharibifu wa nyumba na miundombinu mingine ya raia, imeeleza ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limeipongeza Chad kwa kufanikiwa kuutokomeza ugonjwa wa malale. Chad ni nchi ya kwanza kwa mwaka huu kutambuliwa kwa kutokomeza ugonjwa huo ulio katika kundi la magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika (NTDs) na inakuwa nchi ya 51 kufikia lengo kama hilo ulimwenguni. Ugonjwa huu husambaa kutokana na binadamu kung’atwa na mdudu Mbung’o mwenye maambukizi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Heri kufa macho kuliko kufa moyo.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
20-6-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Rais wa Baraza Kuu: Redio Miraya ninakutakieni heri ya miaka mingine 18 ya utendaji
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis mwishoni mwa wiki Juni 16 ametumia sehemu ya muda wa ziara yake nchini Sudan Kusini kukitembelea kituo cha redio Miraya kinachoendeshwa chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS huku mwisho wa mwezi huu wa Juni redio hiyo ikitimiza miaka 18 tangu kuanzishwa kikisalia kuwa chombo muhimu kwa amani na ustawi wa watu wa Sudan Kusini. Pia akiwa kituoni hapo akaitumia nafasi hiyo kuongelea masuala mengine muhimu ya kijamii ikiwemo elimu. Anold Kayanda ameandaa makala hii kutokana na video iliyoratibiwa na UNMISS.
19-6-2024 • 3 minuten, 31 seconden
Hongera Tanzania kwa kuanzisha kituo cha operesheni na mawasiliano ya dharura - UNDRR
Nchi ya Tanzania imepongezwa kwa kuzindua kituo cha kutoa taarifa na maonyo ya mapema kuhusu dharura hivyo kuwezesha wadau mbalimbali kuchukua hatua stahiki kabla ya majanga kutokea. Akihudhuria uzinduzi rasmi wa kituo hicho cha kwanza nchini Tanzania cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura (EOCC) ambacho kimeanzishwa chini ya Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Tahadhari za Mapema na Mfumo wa kuchukua Hatu za Mapema wa Umoja wa Afrika AMHEWAS, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Kupunguza Hatari za Maafa Kamal Kishore, amelipongeza taifa hilo na kusema uzinduzi huo unaashiria hatua kubwa katika safari ya nchi kuelekea kujenga ustahimilivu wa majanga.“Leo tumezindua chumba cha hali ya hewa Dodoma Tanzania, Hii ni hatua muhimu, matokeo, matokeo ya muunganiko wa taasisi mbalimbali zinazoshirikiana katika kituo hiki yatasaidia kuwezesha jamii kuchukua hatua stahiiki na kulinda maisha na mali za wananchi.” Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu Dkt Jim. J. Yonazi amesema kituo hicho kilicho chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, na kitafanya kazi kuchanganya takwimu wanazo kusanya wakati halisi kuhusu hatari zinazojitokeza pamoja na takwimu kuhusu majanga yaliyopita ili kutoa utabiri na taarifa kwa wakati.“Tumezindua chumba hiki na kinakwenda kwa kweli kusaidia Tanzania kutabiri taarifa za aina mbalimbali za maafa yakiwemo mafuriko, ukame nakadhalika. Na hili ni muhimu sana kwetu kuweza kupanga mikakati, jinsi gani tunaweza kuzuia, lakini tena ikitokea, jinsi ya kujidhatiti baada ya majanga, na tena jinsi ya kutoa taarifa zaidi kwa wadau wetu jinsi ya kurejesha maisha katika hali yake ya awali.”Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza hatari za majanga UNDRR nchi zilizo na mifumo ya kutoa tahadhari za mapema kuhusu hatari mbalimbali zina viwango vya vifo vya maafa ambavyo ni mara sita chini ya nchi zisizo na mifumo au mifumo dhaifu. Zaidi ya hayo, utoaji wa onyo mapema kwa saa 24 tu una uwezo wa kupunguza uharibifu unaofuata kwa asilimia 30. Licha ya manufaa haya, ni asilimia 45 pekee ya nchi barani Afrika zimeripoti kuwepo kwa mifumo hiyo, kulingana na ripoti ya UNDRR ya mwaka 2023 kuhusu Hali ya Ulimwenguni ya Mifumo ya Mapema ya Utoaji Tahadhari za Hatari Mbalimbali.
19-6-2024 • 1 minuut, 48 seconden
Watu milioni 8.1 duniani walikufa kutokana na uchafuzi wa hewa mwaka 2021
Ripoti mpya ya kina inayoonesha athari hasi ya hewa chafuzi kwenye afya imetolewa leo nchini Marekani huku ikiweka bayana kuwa uchafuzi wa hewa umeibuka na kushika nafasi ya pili duniani kama kihatarishi kinachoweza kusababisha kifo, kuliko hata uvutaji tumbaku na ukosefu wa lishe bora. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Ikipatiwa jina Hali ya Hewa Duniani au SoGA ripoti imetolewa katika majimbo ya Massachussets na New York nchini Marekani na taasisi ya Health Effects au HEI kwa ushirikiano kwa mara ya kwanza na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.SoGA inasema mwaka 2021 watu zaidi ya milion 8 walikufa kwa sababu ya kuvuta hewa chafuzi kama vile itokayo kwenye moshi wa jiko ndani ya nyumba lisilotumia nishati safi kama vile kuni, au uchimbaji wa mafuta kisukuku na vile vile hewa chafuzi kutoka kwenye magari.Hewa chafu imekuwa tishio zaidi kwa uhai wa mtoto kuliko hata tumbaku na lishe duni, kwani watoto zaidi ya 700,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano walikufa kwa kuvuta hewa chafu na wengi wao barani Afrika na Asia.Utafiti huo wa uwepo wa hewa chafuzi ulifanyika katika nyumba zaidi ya 200 duniani kote na kuchambua uwepo wa hewa chafuzi kama vile chembechembe ndogo au PM2.5 ambazo si rahisi kuzibaini kwa macho.Ripoti inabainisha kuwa chembe chembe hizo huweza kuingia moja kwa moja kwenye mfumo wa damu na kwenye mapafu na kusababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile kisukari, moyo, kiharusi na saratani.Asilimia 90 ya vifo vyote zaidi ya milioni 8 duniani vimesababisha na uvutaji wa aina hii ya chembe chembe za hewa.Akizungumzia ripoti hiyo Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Kitty Van Der Heijden amesema ni vema serikali na sekta ya biashara wazingatie takwimu hizo na wazitumie vema ili kupunga uchafuzi wa hewa na kulinda watoto na dunia nzima.Licha ya takwimu zenye kiza, SoGa inasema kuna nuru ya matumaini kwani hatua zimeanza kuchukuliwa kuboresha hewa kupitia kupanua huduma za nishati safi na salama ya kupikia, kuboresha huduma za afya na lishe bora na kuongezeka kwa uelewa kuhusu uchafuzi wa hewa majumbani bila kusahau matumizi ya magari ya umeme.
19-6-2024 • 2 minuten, 7 seconden
19 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya kina ya athari ya hewa chafuzi, na uzinduzi wa kituo cha kutoa taarifa na maonyo ya mapema kuhusu dharura nchini Tanzania. Makala inafuatilia ziara za Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Dennis Francis nchini Sudan Kusini na mashinani inatupeleka nchini Kenya kumsikia mwanafunzi mwanaharakti wa mazingira.Ripoti mpya ya kina inayoonesha athari hasi ya hewa chafuzi kwenye afya imetolewa leo nchini Marekani huku ikiweka bayana kuwa uchafuzi wa hewa umeibuka na kushika nafasi ya pili duniani kama kihatarishi kinachoweza kusababisha kifo, kuliko hata uvutaji tumbaku na ukosefu wa lishe bora. Nchi ya Tanzania imepongezwa kwa kuzindua kituo cha kutoa taarifa na maonyo ya mapema kuhusu dharura hivyo kuwezesha wadau mbalimbali kuchukua hatua stahiki kabla ya majanga kutokea.Makala inatupeleka nchini Sudan Kusini ambako Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Dennis Francis mwishoni mwa wiki ametumia sehemu ya muda wa ziara yake nchini Sudan Kusini kuitembelea redio Miraya ambayo mwisho wa mwezi huu wa Juni inatimiza miaka 18 tangu kuanzishwa na ikisalia kuwa chombo muhimu kwa amani na ustawi wa watu wa Sudan Kusini. Anold Kayanda ameandaa makala hii kutokana na video iliyoratibiwa na UNMISS.Na mashinani tutaelekea katika kaunti ya Kitui nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu utunzaji wa mazingira.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
19-6-2024 • 11 minuten, 3 seconden
Kauli za chuki zinasababisha mauaji ya kimbari - Alice Wairimu Nderitu
Leo siku ya kimataifa ya kupinga kauli za chuki ikiadhimishwa ambayo mwaka huu imebeba maudhui “Nguvu ya Vijana ya Kupinga na Kushughulikia Kauli za Chuki”, Dunia bado iko katika kumbukumbu za maombolezo ya siku 100 za mauaji ya Kimbari ya Rwanda yaliyofanyika miaka 30 iliyopita, ambapo kauli za chuki zimeelezwa kuwa moja ya chachu kubwa ya mauaji hayo. Flora Nducha wa Idhaa hii ameketi na Alice Wairimu Nderitu mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbali kujadili kuhusu mchango wa kauli za chuki katika zahma duniani, jukumu la vijana na nini kifanye kuzitokomeza. Na Bi. Nderitu anaanza kwa kufafanua je dunia inaelewa kuhusu mchango wa kauli hizo za chuki katika mauaji ya kimbari.
18-6-2024 • 7 minuten, 53 seconden
18 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikimulika nguvu ya Vijana ya Kupinga na Kushughulikia Kauli za Chuki. Pia tunakuletea muhtasari wa habari, na mashinani inayoangazia michango mikubwa ya kiuchumi ya utumaji fedha kutoka ughaibuni.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk hii leo katika Taarifa yake kupitia katika kikao cha 56 cha Baraza la Haki za Kibinadamu kilichoanza leo Juni 18 mjini Geneva, Uswisi, ameelezea wasiwasi wake juu ya athari mbaya za migogoro ya kimataifa inayoendelea kwa raia, akibainisha ongezeko la asilimia 72 la vifo vya raia kwa mwaka jana 2023. Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kupinga Kauli za Chuki, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameyaeleza mataifa ulimweguni kote kwamba yana wajibu chini ya sheria ya kimataifa kuzuia na kupambana na uchochezi wa chuki na badala yake kuhamasisha kutambua tofauti, kukuza maelewano na mshikamano.Utafiti mkubwa kuhusu mitazamo ya watu kwa wakimbizi kote Kaskazini na Kusini mwa Ulimwengu unaonesha kwamba ingawa uungaji mkono wa upokeaji wakimbizi umepungua katika baadhi ya nchi hasa baada ya uvamizi wa Urusi kwa Ukraine lakini robo tatu ya watu wazima ulimwenguni wanaendelea kuamini kwamba watu wanaokimbia vita au mateso wanapaswa kutafuta usalama katika nchi nyingine.Na mashinani mashinani, hivi majuzi katika siku ya kimataifa ya utumaji fedha kutoka ughaibuni, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD ulisisitiza nafasi ya fedha hizo katika kuokoa maisha kwa mamia ya mamilioni ya watu, nusu yao walioko maeneo ya vijijini, kauli ambayo inapata pongezi na shukrani kutoka kwa Dkt. Shea Mochodo, Mkuu wa Muungano wa raia wa Kenya wanaoishi ughaibuni.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
18-6-2024 • 12 minuten, 39 seconden
UNICEF inasisitiza umuhimu wa kucheza katika ukuaji wa watoto
Shirika la Umoja wa Mataifa shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF inasisitiza mchango muhimu wa kucheza katika ukuaji wa watoto na afya yao ya akili. Makala hii inatupeleka Nairobi Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya aliyekuwa shuhuda wa maadhimisho ya kwanza ya siku ya kucheza duniani yaliyofayika wiki hii katika moja ya shule ya msingi inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini humo katika kampeni maalum ya kudumisha michezo kwa watoto hasa mashuleni.
14-6-2024 • 4 minuten
Dkt. Moeti: Shukrani kwa kila mmoja achangiaye damu Afrika
Ikiwa leo ni siku ya uchangiaji damu duniani, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti ametoa shukrani kwa kila mtu anayejitoa kuchangia damu barani Afrika, akisema kila mchango wa damu ni nguzo ya matumaini kwa uhai wa binadamu mwingine aliye kwenye uhitaji lakini hasama zaidi inahitajika.Amesema Dkt. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi huyu wa WHO kanda ya Afrika katika ukurasa wake wa X, kwenye ujumbe wake wa siku ya leo ya uchangiaji damu duniani, maudhui yakiwa Miaka 20 ya kuchangia: Asanteni Wachangiaji wa damu.Anashukuru wachangiaji wote wa damu barani Afrika. Akisema wanaokoa maisha. Na zaidi ya yote anapenda kuwahamasisha wawe wachangiaji wa damu mara kwa mara.“Nimekutana na mabingwa kadhaa ambao wamekuwa wakichangia damu kwa muongo mmoja au zaidi. Hili ni jambo ambalo tunafanya mara moja kwa mwaka pindi tunaposherehekea siku hii kama leo, lakini kwa kawaida mara tatu au mara nne kwa mwaka.”Lakini ni nini kinahitajika?“Tunahitaji kuhamasisha watu kujitolea zaidi kuchangia damu barani Afrika. Hali inazidi kuimarika lakini bado safari ni ndefu.”Kulikoni safari ni ndefu?Kwa sababu tunahitaji kuongeza maradufu uchangiaji wa damu angalau Afrika. Kwa sasa kiwango chetu ni Uniti 5 za damu kwa watu 100. Tunahitaji angalau uniti 10 kwa watu 1000. Kwa hiyo jitokezeni mara kwa mara.”Akaelekeza wito kwa kundi mahsusi..“Njooni kila mwaka. Hebu tuwahusishe vijana na tuweze kuimarisha hali ya afya kwa wakazi wa Afrika.”WHO inasema damu salama inaokoa maisha na uchangiaji wa damu mara kwa mara kutoka kwa watu wenye afya kunahitajika ili kuhakikisha damu inapatikana wakati wowote pale inapohitajika.
14-6-2024 • 1 minuut, 57 seconden
14 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Utoaji Damu Duniani na umuhimu wake, na wakimbizi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Ufilipino, kulikoni?Ikiwa leo ni siku ya uchangiaji damu duniani, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Kanda ya Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti ametoa shukrani kwa kila mtu anayejitoa kuchangia damu barani Afrika, akisema kila mchango wa damu ni nguzo ya matumaini kwa uhai wa binadamu mwingine aliye kwenye uhitaji lakini hasama zaidi inahitajika. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa Kikosi cha saba kutoka Tanzania, TANBAT 7 wamefanikisha kuwarejesha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR zaidi ya wakimbizi mia tatu na hamsini waliokuwa katika kambi ya Batuli Mashariki mwa Cameroon.Makala inatupeleka Nairobi Kenya kwa mwandishi wetu Thelma Mwadzaya aliyekuwa shuhuda wa maadhimisho ya kwanza ya siku ya kucheza duniani yaliyofayika wiki hii katika moja ya shule ya msingi inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini humo katika kampeni maalum ya kudumisha michezo kwa watoto hasa mashuleni.Mashinani tunasalia kwa hii ya Utoaji Damu Duniani, na tutaelekea jijini manila ufilipino amabapo wafanya kazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani wanaongoza mstari wa mbele kwa kutoa damu wakitueleza umuhimu shughuli hii”Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
14-6-2024 • 10 minuten, 47 seconden
TANBAT 7 yashirikishwa na UNHCR kuwarejesha makwao wakimbizi wa CAR
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa Kikosi cha saba kutoka Tanzania, TANBAT 7 wamefanikisha kuwarejesha nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR zaidi ya wakimbizi mia tatu na hamsini waliokuwa katika kambi ya Batuli Mashariki mwa Cameroon. Shughuli ya makabidhiano ya wakimbizi kutoka upande mmoja kwenda mwingine yamefanyika katika Wilaya ya Gamboula iliyoko mpakani mwa nchi hizo mbili mkoani Mambéré-Kadéï magharibi mwa CAR na yameshuhudiwa na wawakilishi wa masharika mbalimbali ya Umoja wa mataifa, vikosi vinavyohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini CAR, MINUSCA wakiwemo TANBAT 7 pamoja na majeshi ya Cameroon na CAR.Kwa niaba ya ujumbe wa UNHCR kutoka kambi ya Batuli ya nchini Cameroon Mkuu wa kitengo cha Usalama wa wakimbizi wa Kambi hiyo Samwel Forterbel amesema kundi hili ni la wakimbizi ni wale walioamua kurudi nyumbani kwao kwa hiari yao wenyewe "baada ya hali ya Usalama kuimalika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati na tukio hili lina maana kwamba wakivuka mpaka sio wakimbizi tena na hayo ni mafanikio makubwa."Kwa upande wa Mkuu wa Msafara huo kutoka kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha 7 kutoka Tanzania TANBAT 7, Kapteni Cosmas Mnyasenga amesema wamekamilisha kuwasafirisha salama waliokuwa wakimbizi hao na kuwafikisha salama nchini mwao, "katika makazi ya muda mjini Berberati." Mwaka 2013 nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ilikumbwa na mya ndani ambapo makundi ya 3R, Anti Balaka na Seleka yalihitirafiana na kusababisha watu zaidi ya laki nne kuikimbia nchi hiyo na kwenda kuishi uhamishoni katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Chad na Cameroon na sasa baadhi wameanza kurejea nchini mwao na kuanza kulijenga taifa lao mara baada ya amani kuendelea kuimarika siku baada ya siku.
14-6-2024 • 1 minuut, 55 seconden
Jifunze Kiswahili: Pata ufafanuzi wa neno "Kotokoto"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo furs ani yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno“KOTOKOTO.”
13-6-2024 • 0
13 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uvuvi endelevu kwa kutumia kanuni za uvuvi na tunafuatilia mtazamo wa wakazi wa eneo la ziwa Taganyika kuhusu kufungwa zia hilo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za watoto katika migogoro, Ualbino na COSP17. Katika kujifunza Kiswahili tunakuletea ufafanuzi wa neno “Kotokoto.”Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo kuhusu viwango vya ukatili dhidi ya watoto kwenye maeneo ya mizozo yenye matumizi ya silaha inaonesha kuwa mwaka 2023 kulikuwa na ukatili wa kupindukia. Ripoti hiyo inayotolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kila mwaka inasema “Mwaka wa 2023 watoto waliandikishwa na kutumika vitani ikiwa ni pamoja na kwenye mstari wa mbele, kushambuliwa majumbani mwao, kutekwa nyara wakielekea shuleni, shule zao zikitumiwa kijeshi, madaktari wao wakilengwa, na orodha ya kutisha inaendelea. Ikiwa leo ni Siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino, Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu kufurahia haki za binadamu kwa watu wenye ualbino, Muluka-Anne Miti-Drummond amepongeza maendeleo ya pamoja yaliyopatikana katika kufuatilia haki za binadamu kwa watu wenye ualbino, tangu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipotambua rasmi tarehe 13 Juni kuwa Siku ya kimataifa ya kuelimisha jamii kuhusu watu wenye ualbino miaka kumi iliyopita. Hata hivyo, amesema wanatambua kwamba safari ya kuelekea katika ulimwengu wa haki sawa kwa watu wenye ualbino bado inakumbwa na changamoto na ugumu mkubwa.Na leo ndio ndio tamati ya Mkutano wa 17 wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu, COSP17 uliodumu kwa siku tatu katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Sarah Muthoni Kamau, Mwenyekiti wa Jukwaa la Watu wenye ulemavu la Jumuiya ya Madola ni mmoja wa waliohudhuria mkutano huu uliodumu kwa siku tatu.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo furs ani yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno“KOTOKOTO”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
13-6-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Nilikuwa mwathirika wa ajira ya watoto lakini sasa nafanya kazi ya kuizuia
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupinga ajira kwa watoto ambayo mwaka huu imebeba maudhui “Hebu tutekeleze ahadi zetu kukomesha ajira ya watoto” tunaelekea nchini Argentina kukutana na muathirika wa ajira ya watoto ambaye sasa ameamua kulivalia njuga suala hilo na anafanya juu chini kuitokomeza ajira kwa watoto ambayo imekita mizizi nchinihumo kwa miaka nenda miaka rudi. Kwa mujibu wa shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO ajira kwa watoto ni ukiukwaji mkubwa wa haki zao n ani uhalifu unaokwenda kinyume na sheria na mikataba ya kimataifa ya kazi lakini pia ni kosa la jinai. Flora Nducha anafafanua zaidi katika makala hii.
12-6-2024 • 3 minuten, 4 seconden
Wapiganaji walitupokonya vitu vyetu: Simulizi kutoka Sudan
Nchi ya Sudan inakabiliwa na hatari inayoongezeka ya njaa inayosababishwa na migogoro ambayo itakuwa na matokeo mabaya ikiwa ni pamoja na watu kupoteza maisha, haswa kwa watoto wadogo. Hata pale wananchi wanapojaribu kukimbia vita ili kwenda kusaka msaada maeneo mengine wanakumbana na changamoto lukuki ikiwemo kuporwa mizigo yao na makundi ya wapiganaji. Leah Mushi na maelezo zaidi.Kiujumla hali ni mbaya nchini Sudan kutokana na mapigano yanayoendelea baina ya makundi mawili ambayo ni vikosi vya kijeshi vya serikali na vikosi vya msaada wa haraka. Wananchi maisha yao yamebadilika kabisa maana sasa hawawezi kuendelea na shughuli zao za kawaida kama vile kilimo. Mmoja wa waathirika wa vita nchini Sudan ni Bi. Thuraya mwenye umri wa miaka 37 aliyekimbia eneo la El Fasher Kaskazini mwa Darfur na watoto wake kwenda kusaka hifadhi katika kambi ya wakimbizi ya Zamzam anasema maisha yamekuwa magumu hawana hata chakula cha kuwapikia watoto. “Tumekuja kutokea Tawila, tulilazimika kuondoka usiku, hatukuweza kuondoka mchana sababu tulikuwa tunaogopa mapigano na silaha nzito. Walitukagua na kututishia, mnaenda wapi? mmebeba nini kwenye mabegi yenu?. Walichukua vitu vyetu na kutuacha na vitu vichache, na hela kidogo tulizokuwa nazo tuliweza kufika katika kambi hii ya wakimbizi.”Masikini Bi.Thuraya anatamani maisha yake kabla ya vita. “Kabla ya vita maisha yetu yalikuwa ya furaha, tulikuwa tunaenda shambani, hatukuwa tunanunua mkate wala chochote sokoni. Tulikuwa tukienda huko tunanunua nguo. Tulikula nyama kutoka kwenye mifugo yetu majumbani lakini wameiiba yote. Tulivyofika hapa kambini walitupa vitu vichache lakini vimeisha vyote. …… Ujumbe wangu kwa dunia ni watusaidie tupate amani. Hilo ndilo jambo letu Pekee.”Uchambuzi wa hivi karibuni uliofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, ikijumuisha lile la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Mpango wa Chakula (WFP) na la Afya Duniani (WHO) unaonesha kwamba uhasama unaoendelea unazidisha visababishi vya utapiamlo kwa watoto.
12-6-2024 • 1 minuut, 55 seconden
Ripoti yaweka wazi Israeli na Hamas wanahusika na uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.
12-6-2024 • 2 minuten, 35 seconden
12 JUNI 2024
Ripoti yaweka wazi Israeli na Hamas wanahusika na uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu.Simulizi kutoka Sudan: Wapiganaji walitupokonya vitu vyetu.Nilikuwa mwathirika wa ajira ya watoto lakini sasa nafanya kazi ya kuizuia.Mashinani: Kutokana na kuzuka upya kwa mizozo katika jimbo la Equotoria Magharibi, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umeimarisha uwepo wa askari wake wa kulinda amani ili kuwalinda na kuwapatia msaada wa kibinadamu mamia ya watu katika kambi za wakimbizi wa ndani za eneo la Tambura.
12-6-2024 • 10 minuten
MONUSCO yatoa mafunzo ya mbinu za kuondokana na habari potofu na za uongo DR Congo
Umoja wa Mataifa kila uchao hivi sasa unapigia chepuo kampeni za kutokomeza habari potofu na za uongo kwani zimethibitika kuwa na madhara makubwa kwa jamii. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, habari hizo zimewahi kusababisha madhara ikiwemo vifo. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umeamua kuchukua hatua kwa kuendesha mfululizo wa mafunzo wa mbinu za kuondokana na habari hizo potofu na za uongo kama alivyotangaza Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita ambaye pia ndie mkuu wa MONUSCO. Alitangaza hayo mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwaka jana wa 2023 na sasa hatua zimechukuliwa na matunda yanaanza kuonekana. Mwandishi wetu wa habari huko Beni, jimboni kivu kaskazini, mashariki mwa DRC, George Musubao amevinjari kufahamu madhara ya habari hizo na hatua zinazochukuliwa.
11-6-2024 • 6 minuten
11 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika kampeni za kutokomeza habari potofu na za uongo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambazo zimewahi kusababisha madhara ikiwemo vifo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Gaza, vifo vya wahamiaji na mkutano wa COSP17. Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Huko Bahari ya Chumvi Jordan kwenye mkutano wa ngazi ya juu kwa ajili ya hatua za haraka za kibinadamu Gaza, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ametoa wito wa msaada wa haraka wa kibinadamu kwa ajili ya Gaza akianinisha hali mbaya inayoendelea ikiwemo kutawanywa kwa watu milioni 1.7, kusambaratishwa kwa hospitali, ukosefu Mkubwa wa vifaa tiba muhimu, maji safi na chakula. Takriban wahamiaji 49 wamepoteza maisha na wengine 140 kutojulikana waliko baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama Pwani ya Yemen kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. Boti hiyo iliyozama jana karibu na kituo cha Alghareef jimbo la Shabwah ilikuwa imebeba jumla ya wahamiaji 260 na miongoni wa waliopoteza maisha 31 ni wanawake na watoto.Na mkutano wa 17 wa mkataba wa watu wenye ulemavu COSP17 ambao maudhui yake makuu ni kutafakari ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu katika mazingira ya sasa, umefungua pazia leo hapa kwenye Mkao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani. Flora Nducha yuko ndani ya ukumbi wa Baraza Kuu kunakofanyika mkutano huo.Mashinani leo ikiwa ni siku ya michezo, tunakwenda Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania kupata maoni ya wazazi na watoto kuhusu umuhimu wa kucheza.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
11-6-2024 • 11 minuten, 48 seconden
WHO yatahadharisha kuhusu kushambuliwa kwa hospitali muhimu Al Faher Sudan
Shambulio kubwa lililofanywa na wanamgambo wa Rapid Support Forces, au RSF mwishoni mwa wiki katika mji wa Al Fasher kaskazini mwa Sudan limelazimisha kufungwa kwa hospitali kuu inayotegewa katika eneo hilo na hivyo kusababisha kupungua upatikanaji wa huduma za kuokoa maisha, limeripoti leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO. Kwa mujibu wa taarifa za WHO, Wizara ya Afya ya Sudan na shirika lisilo la kiserikali la Madaktari wasio na mipaka Médecins Sans Frontières (MSF) walilazimika kuifunga hospitali hiyo kubwa pekee inayotoa huduma za upasuaji katika El Fasher nzima baada ya wanamgambo hao wa Rapid Support Forces (RSF) kuingia ndani ya hospitali na kufyatua risasi kisha wakaiba vifaa tiba na gari la wagonjwa. WHO Sudan imeeleza kusikitishwa na shambulio hilo na wamesema, "Kufungwa kwa hospitali hiyo kufuatia shambulio hilo kumeziongezea hospitali nyingine mbili mzigo zaidi ya uwezo wake.”Pia WHO imelaani "shambulio lingine" kwenye kituo cha afya huko Wad Al-Nura katika jimbo la Al-Jazirah kusini mwa Khartoum, ambalo lilisababisha kifo cha muuguzi ambaye alikuwa zamu akihudumia wagonjwa wakati huo.“WHO inalaani vikali mashambulizi dhidi ya huduma za afya.” WHO Sudan imeeleza kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X. “Wahudumu wa afya na wagonjwa hawapaswi kuhatarisha maisha yao ili kutoa na kupata huduma za afya.” Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesisitiza ikiwa ni siku chache pia baada ya shambulio katika moja ya vijiji nalo likiripotiwa kutekelezwa na wanamgambo wa RSF wakitumia mizinga mikubwa kushambulia kijiji na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100.
10-6-2024 • 1 minuut, 37 seconden
Hatutaki kuona umwagaji damu upande wowote – Mkazi Gaza
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Mamlaka ya Palestina, mashambulio yaliyofanywa na Israeli tarehe 8 mwezi Juni kwenye eneo la kati la Deir El Balah huko Ukanda wa Gaza yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 270 na wengine zaidi ya 700 walijeruhiwa wengine wako mahututi. Shule ilishambuliwa kwenye eneo hilo hilo siku mbili kabla ya shambulio hilo la tarehe 8 na kusababisha vifo vya watu 40, wakiwemo watoto 14 na wanawake 9. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura ilifika Deir El Balah na kuzungumza na mmoja wa wakazi anayesimulia kilichotokea na wito wake, na hicho ndio msingi wa makala hii inayosimuliwa na Assumpta Massoi.
10-6-2024 • 3 minuten, 19 seconden
10 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya nchini Sudan huku mgogoro ukiendelea, na ndoa za utotoni nchini Uganda. Makala inatupeleka katika eneo la Deir El – Balah Gaza kusikia simulizi za waathirika wa vita, na mashinani tunakwenda Geneva, Uswisi kumsikia Deogratius Ndejembi kwe nye mkutano wa ILO.Shambulio kubwa lililofanywa na wanamgambo wa Rapid Support Forces, au RSF mwishoni mwa wiki katika mji wa Al Fasher kaskazini mwa Sudan limelazimisha kufungwa kwa hospitali kuu inayotegewa katika eneo hilo na hivyo kusababisha kupungua upatikanaji wa huduma za kuokoa maisha, limeripoti leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO. Mradi wa Wasichana kuwawezesha wasichana wenzao GEG, ni mradi wa kwanza nchini Uganda wa ulinzi wa kijamii unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa ushirikiano wa mamlaka ya mji mkuu wa Kampala kupitia ufadhili uliotolewa na serikali ya Ubelgiji ukiwalenga watoto wa kike na mustakbali wao.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA anatupeleka Gaza hususan eneo la Deir El – Balah ambako mashambulizi ya Israeli wiki iliyopita yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 300 na wengine wapatao 700 walijeruhiwa wakiwemo watoto.Mashinani tunakwenda Geneva, Uswisi kumsikia Deogratius Ndejembi, Wazir wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu akizungumzia ushiriki wa Tanzania kwenye mkutano wa 12 wa shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
10-6-2024 • 11 minuten, 17 seconden
Zainab: Mradi wa UNICEF wa GEG umeokoa mustakbali wangu
Mradi wa Wasichana kuwawezesha wasichana wenzao GEG, ni mradi wa kwanza nchini Uganda wa ulinzi wa kijamii unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa ushirikiano wa mamlaka ya mji mkuu wa Kampala kupitia ufadhili uliotolewa na serikali ya Ubelgiji ukiwalenga watoto wa kike na mustakbali wao. Mradi huo wa GEG unatekelezwa katika wilaya zote tano za Kampala na unahakikisha wasicha barubaru walio shuleni na nje ya shule wanakuwa na mabadiliko bora kutoka utotoni kuingia ukubwani kwa kupokea elimu, ushauri na mafunzo ambayo yanawajengea uwezo wa kufikia malengo yao. Wengi walio katika mradi huu wamepitia changamoto lukuki na mfano halisi ni Zainab mwenye umri wa miaka 18 mwanafunzi wa shule ya msingi Kampala“Siku moja nyanya yangu alipokea simu kutoka kijijini wakimwambia nahitajika kijijini. Na nilipowasili huko nilikuwa viroba vya sukari, mchele na kadhalika na nikamuuliza msichana niliyemkuta pale hivi vitu ni vya nani? Kisha akaniambia haujui kwamba unaolewa? Nilikuwa na umri wa miaka 16 tu na walikuwa wananiambia mi ni mkubwa”Familia ya Zainab ilipanga na kumuandalia ndoa bila ridhaa yake na baada ya kupokea mahari alilazimishwa kwenda kuishi na bwana na mambo yalikuwa mabaya anasema ZainabMwanaume huyo alitaka kulala nami kwa nguvu, alitaka kunibaka. Nilimwambia hapana nataka kurejea shuleni. Nilikuwa nalia kila siku , sikujua cha kufanya nilichanganyikiwa. Na hapo nikamkumbuka mshauri wangu aliniambia wakati wowote ukipata tatizo nipigie nitakusaidia. Basi nikampigia naye akampigia baba yangu sijui walichozungumza lakini baada ya siku moja, nilirejea Kampala nikarejea shuleni.”Mshauri huyo ni kutoka mradi wa UNICEF wa GEG aliokoa Maisha ya Zainab ambaye baada ya kunusika ndoa ya utotoni na kubakwa ana matumaini ya muskabali wake“Sasa niña furaha sana kwani nimekuwa shuleni na bado naendelea na shule. Nimemaliza darasa la saba, naenda sekondari na nitafaulu. Nataka kuwa mwanasheria niweze kupigania haki za watoto ili kusiwe na mtoto yoyote atakayelazimishwa kufanya asichotaka.”Mradi wa GEG umegawanyika katika sehemu kuu tatu, mosi kuwawezesha wasichana kupitia mtandao wa washauri rika, pili kuwashirikisha wasichana kupitia elimu, mafunzo na kuwaelekeza kwa kupata msaada wa huduma na tatu kuwawezesha wasichana kutafuta fursa bora za maisha yao ya baadaye kupitia msaada mdogo wa fecha wanaopokea.
10-6-2024 • 2 minuten, 52 seconden
Mfumo wa kutoa tahadhari mapema warejesha imani kwa wakazi wa Ituri, DRC
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan mashariki mwa taifa hilo la Maziwa Makuu, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umeanzisha mfumo wa kutoa tahadhari mapema kuhusu mashambulizi dhidi ya raia yanayoendeshwa na waasi kwenye mji wa Bunia jimboni Ituri. Mfumo huu unaweza jamii, jeshi la serikali na MONUSCO kubadilishana taarifa na hivyo wananchi wanakuwa na hakikisho la usalama wao kwani pindi taarifa inapotolewa, hatua sahihi zinachukuliwa kama anavyosimulia Assumpta Masso kwenye makala hii iliyofanikishwa na MONUSCO.
7-6-2024 • 3 minuten, 39 seconden
WHO: Takribani watu milioni 1.6 huugua kila siku kutokana na chakula kisicho salama
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti kwamba kila siku, takribani watu milioni 1.6 kote duniani huugua kwa kula chakula kisicho salama na karibu asilimia 40 ya mzigo huo ukibebwa na watoto wadogo, chini ya umri wa miaka mitano. Hii leo kupitia mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari jijini Geneva, Uswisi uliowahusisha Dkt. Francesco Branca, Mkurugenzi wa Idara ya Lishe na Usalama wa Chakula wa WHO na Markus Lipp, Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Chakula wa FAO imeelezwa kuwa madhara yatokanayo na chakula kisicho salama hayaangalii mipaka na yametapakaa katika nchi nyingi duniani. Dkt. Francesco Branca aliyekuwa katika ukumbi huo wa mikutano ametoa taarifa kwamba "kutokana na kuugua kwa takribani watu milioni 1.6 kila siku kunakosababishwa na vyakula visivyo salama, watu 420,000 hufariki dunia kutokana na sababu hiyo."Mwaka huu, kaulimbiu ya kampeni ya Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, ni Jiandae kwa Yasiyotarajiwa, ambayo sio tu inasisitiza umuhimu wa kuwa tayari kudhibiti matukio ya usalama wa chakula ili yasiwe ya dharura, lakini pia umuhimu wa kuchukua muda kupanga, kuandaa na kuwa tayari kuchukua hatua katika mazingira ya dharura.Kwa upande wake Markus Lipp, Afisa Mwandamizi wa Usalama wa Chakula katika Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), kwa njia ya video akizungumza kutoka Roma, Italia ameeleza namna FAO inavyohusisha chakula salama na utimizaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu…anasema, “Chakula kinapozalishwa na kuuzwa katika mfumo wa kilimo salama na endelevu, kinachangia maisha yenye afya na kuboresha uendelevu kwa kuwezesha upatikanaji wa soko na tija, ambavyo vinasukuma maendeleo ya kiuchumi na kupunguza umaskini, hasa katika maeneo ya vijijini.”
7-6-2024 • 1 minuut, 51 seconden
07 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia usalama wa chakula, na ripoti ya ILO kuhusu suala la ajira Gaza wakati huu wa machafuko. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Chakula, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO limeripoti kwamba kila siku, takribani watu milioni 1.6 kote duniani huugua kwa kula chakula kisicho salama na karibu asilimia 40 ya mzigo huo ukibebwa na watoto wadogo, chini ya umri wa miaka mitano. Tukimulika suala la ajira Gaza ambapo ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaweka bayana ni kwa vipi vita iliyoanza tarehe 7 Oktoba mwaka jana wa 2023 inasukuma kiwango cha ukosefu wa ajira kufikia takribani asilimia 80 huku pato la ndani la ukanda huo wa Gaza likipungua kwa asilimia 83.5..Katika makala Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa anatupeleka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mashambulizi ya mara kwa mara kutoka makundi ya waasi waliojihami dhidi ya raia, yamesababisha Umoja wa Mataifa na kuja na mfumo wa kutoa tahadhari mapema ili kuimarisha ulinzi wa wa raia.Mashinani leo ikikiwa ni siku ya usalama wa chakula duniani tunakwenda nchini Sudan kumulika masuala ya lishe.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
7-6-2024 • 10 minuten, 30 seconden
Vita katika ukanda wa Gaza yasababisha ukosefu wa ajira kufikia asilimia 80 – ILO
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaweka bayana ni kwa vipi vita iliyoanza tarehe 7 Oktoba mwaka jana wa 2023 inasukuma kiwango cha ukosefu wa ajira kufikia takribani asilimia 80 huku pato la ndani la ukanda wa Gaza likipungua kwa asilimia 83.5. Takwimu hizo zinamaanisha kuwa kati ya kila watu 10 Ukanda wa Gaza wenye uwezo wa kufanya kazi, ni watu wawili tu wenye ajira, imesema ripoti hiyo iliyoandaliwa na ILO kwa ushirikiano na Ofisi Kuu ya Takwimu ya Palestina kuonesha ni kwa vipi vita imeathiri soko la ajira na njia za kujipatia kipato kwenye eneo hilo la Palestina linalokaliwa na Israeli.Ripoti inasema miezi minane ya vita imesababisha watu kupoteza kwa kiwango kikubwa ajira na mbinu zao za kujipatia kipato Gaza.Ukingo wa Magharibi nako vita hiyo imeathiri vibaya kwani ukosefu wa ajira umefikia asilimia 32.Ripoti inaonya kuwa takwimu hazijumuishi wale waliolazimika kuacha kazi kwa sababu ya vita, na kwamba idadi halisi ya waliolazimika kuacha kazi ni kubwa kuliko kinachodokezwa kwenye ripoti.Biashara zikiwa zimefungwa, kipato cha kaya nacho kimepungua kwa asilimia 87 na zinatuma watoto wao kufanya kazi ili kupata kipato.Mkurugenzi wa ILO Kanda ya nchi za kiarabu Ruba Jadarat anasema vita Gaza imesababisha vifo, hali ngumu ya kibinadamu ikiambatana na kusambaratika kwa hali ya kiuchumi na kujipatia kipato Gaza na Ukingo wa Magharibi. Hivyo kurejesha mbinu za watu kujipatia kipato na kuweka fursa za ajira zenye hadhi ni muhimu ili wapalestina waweze kukwamuka kutoka kwenye vitisho na ukatili ambao vita imewatumbukiza.Amesema kukwamuka huko kuende sambamba na harakati za sasa za usaidizi wa kibinadamu na kwamba ILO na wadau wake wanatekeleza kupitia Mpango wa Hatua wa Dharura kwa Palestina.
7-6-2024 • 2 minuten, 6 seconden
Jifunze Kiswahili - Pata ufafanuzi wa neno "Nyendea"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua matumizi ya neno “NYENDEA”
6-6-2024 • 0
06 JUNI 2024
Katika Jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Gaza Nuiserat Israel imeshambulia shule moja iliyokuwa inahifadhi wakimbizi 6,000 wa kipalestina na kuua watu 35, na wengine wengi wamejeruhiwa,-Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa leo kumefanyika tukio la kukumbuka wafanyakazi 188 wa chombo hicho waliouawa mwaka 2023 pekee wakiwemo 135 watumishi wa UNRWA waliouawa ukanda wa Gaza-Duniani kote mtoto mmoja kati ya wanne anaishi katika mazingira ya umaskini wa chakula akila aina moja au mbili tu ya mlo kutokana na vita, mizozo, janga la tabianchi na ukosefu wa uwiano, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. -Katika mada kwa kina utamsikia Erick Mukiza mmoja wa wanasheria waliothibitishwa kuwa wapatanishi au wasuluhishi wa migogoro nje ya mahakama nchini Tanzania na mipango yake ya kujumuisha wenye ulemavu ili wanufaike na mpango huo wa serikali ya Tanzania.-Na katika jifinze Kiswahili Onni Sigalla anafafanua maana ya neno Nyendea
6-6-2024 • 9 minuten, 58 seconden
UN: Kila mtu ana wajibu wa kuhusika na urejeshaji wa ubora wa ardhi
Leo ni siku ya mazingira duniani na Umoja wa Mataifa unaisa dunia kuchukua hatua sasa kurejesha Uhai wa ardhi iliyoharibiwa na kujenga mnepo dhidi ya kuongezeka kwa hali ya jangwa na ukame na hiyo ndio kaulimbiu ya siku ya mwaka huu. Akisisitiza maudhui hayo Inger Andersen Mkurugenzi mtendaji wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP amemtaka kila mtu kujiunga na harakati za kimataifa za kurejesha ardhi yenye afya na kujenga mnepo wa majanga mengine kama vile ukame na hali ya jangwa. Flora Nducha anatupasha zaidi katika makala hii..
5-6-2024 • 4 minuten, 42 seconden
Lengo la kudhibiti ongezeko la joto duniani kwenye nyuzijoto 1.5 linaning’inia - Katibu Mkuu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres asubuhi ya leo saa za New York, Marekani kupitia Hotuba Maalumu kuhusu Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ametahadharisha kuhusu hatari ya wazi ya uwezekano wa ongezeko la joto juu ya nyuzijoto 1.5 za selsiasi linaloukabili ulimwengu ikiwa uzalishalishaji wa hewa chafuzi utaendelea kwa viwango vya sasa. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Ni hotuba ambayo imepewa jina “Wakati wa Ukweli”…Hotuba ambayo Katibu Mkuu wa Guterres ameitumia kuuleza ulimwengu ukweli kuwa utafiti wa kitaalamu unaonesha kuwa ni tani bilioni 200 tu za hewa ukaa ambazo dunia inaweza kuzihimili kabla ya kuvuka nyuzijoto 1.5 za Selsiasi juu ya viwango vya kabla ya viwanda jambo ambalo ni hatari kubwa kwa ulimwengu.Ikumbukwe kuwa chini ya Mkataba wa Paris mnamo mwaka 2015, nchi zilikubaliana kupunguza kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa hewa chafuzi duniani ili kuwezesha ongezeko la muda mrefu la wastani wa joto la uso wa dunia kuwekwa chini ya nyuzijoto 2 za selsiasi juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda na kuendeleza juhudi za kulipunguza joto hadi nyuzijoto 1.5 za selsiasi kisha kuhakikisha halizidi hapo.Lakini kiongozi huyu wa Umoja wa Mataifa anaeleza kwamba kwa kasi ya sasa ya uzalishaji hewa chafuzi kwa kiasi cha tani bilioni 40 kwa mwaka ni wazi uwezo wa dunia kuendelea kudhibiti joto lisipande utaisha mapema. “Sote tunaweza kufanya hisabati. Kwa kiwango hiki, uwezo wote wa dunia kuhimili hewa ukaa utaondolewa kabla ya mwaka 2030. Ukweli ni kwamba uzalishaji wa hewa chafuzi duniani unahitaji kushuka kwa asilimia tisa kila mwaka hadi mwaka 2030 ili kuweka hai kikomo cha ongezeko la nyuzi joto 1.5. Lakini zinaelekea kubaya. Mwaka jana zilipanda kwa asilimia moja. Ukweli ni kwamba tayari tunakabiliwa na mashambulizi katika eneo la nyuzijoto 1.5 za Selsiasi.” Amesema Guterres.Guterres ameeleza kwamba hakuna nchi inayoweza peke yake kutatua janga la tabianchi akisema, “Huu ni wakati wa kila mtu kushiriki. Umoja wa Mataifa unajitolea kufanya kazi ili kujenga uaminifu, kutafuta ufumbuzi, na kuhamasisha ushirikiano ambao ulimwengu wetu unahitaji sana.”Na kwa vijana, kwa mashirika ya kiraia, kwa miji, mikoa, biashara na wengine ambao wamekuwa wakiongoza hatua kuelekea ulimwengu salama na safi, Katibu Mkuu amesema, Asante.
5-6-2024 • 2 minuten, 7 seconden
05 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya mazingira duniani, na msaada wa kibinadamu nchini Haiti. Makala tunamulika hatua za kurejesha afya ya ardhi iliyoharibiwa na mashinani tunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe wa Martin Griffiths anayestaafu mwishoni mwa Juni. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres asubuhi ya leo saa za New York, Marekani kupitia Hotuba Maalumu kuhusu Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ametahadharisha kuhusu hatari ya wazi ya uwezekano wa ongezeko la joto juu ya nyuzijoto 1.5 za selsiasi linaloukabili ulimwengu ikiwa uzalishalishaji wa hewa chafuzi utaendelea kwa viwango vya sasa. Licha ya machafuko na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha huko nchini Haiti, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani limeendelea kuimarisha operesheni zake katika mji mkuu wa Port-au-Prince na kusaidia jamii zilizoathiriwa na ghasia ambapo kwa mwezi Mei shirika hilo limeweza kuwafikia zaidi ya watu 93,000.Katika makala ikiwa leo ni siku ya mazingira duniani Umoja wa Mataifa unaisa dunia kuchukua hatua sasa kurejesha afya ya ardhi iliyoharibiwa na kujenga mnepo dhidi ya kuongezeka kwa hali ya jangwa na ukame. Na hiyo ndio kaulimbiu ya siku ya mwaka.Mashinani tunasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York kusikiliza ujumbe, wa Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Kibinadamu na Misaada ya Dharura Martin Griffiths anayestaafu wadhifa huo mwishoni mwa Juni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
5-6-2024 • 10 minuten, 55 seconden
WFP yafanikiwa kufikisha Msaada wa chakula nchini Haiti licha ya hali tete ya usalama
Licha ya machafuko na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha huko nchini Haiti, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani limeendelea kuimarisha operesheni zake katika mji mkuu wa Port-au-Prince na kusaidia jamii zilizoathiriwa na ghasia ambapo kwa mwezi Mei shirika hilo limeweza kuwafikia zaidi ya watu 93,000. Kwa mujibu wa tathmini ya viwango vya njaa iliyofanyika mwezi Machi mwaka huu nchini Haiti, takriban watu milioni 5 ambao ni sawa na nusu na idadi ya watu wote wa taifa hilo, wanakabiliwa na ukosefu wa uhakika wa chakula ikiwemo watu milioni 1.64 ambao wametajwa kuwa hatua moja tu kabla ya kufikia baa la njaa yani IPC4. Maisha ya wanajamii yamebadilika sana, wale waliokuwa wanaweza kujikimu sasa wamegeuka ombaomba kama anavyoeleza bibi Heugenie Pierre Charles, mwenye umri wa miaka 70 mkazi wa Port- au – Prince. “Kuna wakati mwingine nakuwa na njaa sana. Nawaomba watu wanaokula wanigawie kidogo wanachokula. Lakini wananidhalilisha. Huko nyuma sikuwahi kuwa naomba, nilikuwa naweza kuendesha biashara zangu. Inaniuma sana. Nilikuwa na kazi yangu, lakini magenge ya wenye silaha yamesababisha nifunge. Na sasa naishi katika hali ambayo inanifanya nalia. Nipo hapa katika kambi ya wakimbizi wa ndani. Nilikuwa nimebakiwa na birika tu. Kwa bahati mbaya imeibiwa. Sasa sina kitu chochote. Nilikuwa natumia birika yangu kuchemsha chai na chakula.”WFP kwa kutambua madhila yanayowakumba wananchi mwezi Mei ilifanikiwa kuingiza shehena ya chakula nchini Haiti na miongoni mwa walionufaika ni zaidi ya wananchi 93,000 walioko Cité Soleil, mojawapo ya vitongoji vilivyo vigumu kufikika kutokana na usalama, walifanikiwa kufikishwa msaada wa chakula kwani wananchi hao wako hatarini zaidi kukumbwa na njaa.Mwakilishi wa WFP nchini Haiti Jean-Martin Bauer anasema ndege ya shirika hilo iliyotua Port au Prince mwezi Mei imekuwa mkombozi. “Barabara za kuingia na kutoka katika mji wa wa Port-au-Prince zinashikiliwa na makundi yenye silaha. Bandari ilifungwa muda mrefu uliopita Kwani iliporwa, na uwanja wa ndege nao ukafungwa, kwa ufupi Port au Prince kwa miezi michache imekuwa kama kisiwa. Kwa hivyo ni muhimu sana kwa WFP na wasaidizi wengine wa kibinadamu kuweza kuleta misaada mjini hapa na, kuendesha programu muhimu. Kwa hivyo huduma muhimu ambazo watu wanategemea, iwe huduma ya afya, maji na usafi wa mazingira, chakula, zinahitaji usafirishaji wa bure wa bidhaa na watu, na hivi sasa hatujapata hiyo. Kwa hivyo tunachofanya na safari hii ya ndege ni kufungua tena mlango huo na kuhakikisha kuwa mahitaji muhimu yanaingia ili kuruhusu huduma hizi muhimu kufanya kazi.”Mbali na kusambaza misaada mbalimbali ya chakula kwa mwaka huu WFP imesaidia zaidi ya watu 108,000 waliokimbia makazi yao kwa kuwapatia chakula cha moto. Pia wanatoa Msaada wa kuwapatia fedha taslimu na mwitikio huu wa kibinadamu pia unajumuisha nyongeza ya lishe kwa kaya zilizo na wajawazito au watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
5-6-2024 • 3 minuten, 23 seconden
04 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako UNICEF na wadau wake imefanikisha utengenezaji wa sodo za kufuliwa. Piatunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Gaza, wahamiaji kutoka bara la Afrika na watoto katika migogoro. Mashinani inatupeleka nchini DR Congo, kulikoni?Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura (OCHA) imeripoti ubomoaji wa makazi leo kwenye eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu katika miji ya Shuqba, Al Jwaya na Mantiqat Shi'b al Butum, katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) imeangazia hatari zinazowakabili wakimbizi na wahamiaji wanapokuwa njiani kutoka Afrika kwenda Ulaya. UNHCR imeweka wazi kuwa wengi wao hufariki dunia wakivuka jangwa au karibu na mipaka, hufanyiwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Shirika hilo limetoa wito kwa wafadhili kuangazia usaidizi na watu kuelezwa njia mbadala halali za kuhama nchi.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya kukumbuka watoto walio kwenye maeneo yenye mizozo ikihusisha ukatili na unyanyasaji, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Denise Brown ameitaka Jumuiya ya Kimataifa kukataa kuhalalisha vita na athari zake kwa watoto. Akitathimini hali ya watoto nchini Ukraine kutokana na uvamizi wa Urusi amesema zaidi ya watoto 600 wameshauawa na 1,420 wamejeruhiwa tangu Februari mwaka 2022.Katika mashinani na ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka watoto wasio na hatia waathiriwa wa uvamizi na ukatili tunaelekea nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC kusikia simulizi ya msichana ambaye alitumikishwa na makamanda wa kundi la waasi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
4-6-2024 • 13 minuten, 17 seconden
Watumiaji wa baiskeli wasema manufaa ni zaidi ya afya
Baiskeli! Umoja wa Mataifa uliitambua rasmi umuhimu wake tarehe 13 mwezi Machi mwaka 2022 kwa kupitisha azimio la kutambua tarehe 3 mwezi Juni kila mwaka kuwa siku ya baiskeli duniani. Umuhimu wake kama chombo cha usafiri chenye gharama nafuu, hakichafui mazingira na zaidi ya yote afya kwa watumiaji kwani ni mazoezi. Huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya, taifa lililo Afrika Mashariki, utamaduni wa kutumia baiskeli kama njia ya usafiri unazidi kushamiri na miongoni mwa watumiaji hao wanaelezea kwenye makala hii msingi wa matumizi, changamoto na nini kifanyike ili matumizi ya baiskeli yawe salama.
3-6-2024 • 3 minuten, 33 seconden
UNRWA: Gaza hali si hali tena huku watu milioni 1 wakikimbia Rafah
Watu milioni moja sasa wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ka mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huku kukiwa na ripoti mpya za mashambulizi ya usiku kuamkia leo katika maeneo ya kusini, kati na kaskazini yanayofanywa na vikosi vya Israel. Katika tarifa yake iliyotolewa leo kupitia mtandao wa kijamii wa X UNRWA imesema mji wa Rafah kwenye mpaka wa kusini wa Gaza na Misri ulikuwa nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja waliokimbia makazi yao kwa karibu miezi minane ya mashambulizi ya kila siku ya jeshi la Israel, kujibu shambulio la kigaidi lililoongozwa na Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana."Maelfu ya familia sasa wanaishi katika vituo vilivyoharibiwa na kusambaratishwa huko Khan Younis ambapo UNRWA inaendelea kutoa huduma muhimu, licha ya changamoto zinazoongezeka. Masharti hayaelezeki,” Haya yanajiri siku tatu tangu Rais wa Marekani Joe Biden kuzindua pendekezo la usitishaji mapigano kwa kuzingatia usitishaji wa hatua kwa hatua kwa vita hiyo, pendekezo likiripotiwa kujumuisha kuondolewa kwa majeshi ya Israel kutoka maeneo wyalikorundikana, kuachiliwa kwa mateka wa Israel na wafungwa wa Kipalestina, pamoja na mpango wa ujenzi mpya wa Gaza.Kulingana na UNRWA, maelfu ya familia zimelazimika kutafuta makazi katika majengo yaliyoharibiwa vibaya huko Khan Younis jiji ambalo liko kaskazini mwa Rafah, na linakadiriwa kuwa na watu wapatao milioni 1.7. Imeripotiwa kwamba makao yote 36 ya UNRWA huko Rafah sasa yamesalia matupu.Shirika hilo limeongeza kuwa Takriban wanawake na wasichana 690,000 wanaaminika kukosa vifaa vya msingi vya usafi wakati wa hedhi, faragha na maji ya kunywa.Ikiangazia mapambano ya kila siku yanayowakabili watu walio hatarini sana huko Gaza, UNRWA imelinukuu Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya uzazi UNFPA ambalo linakadiria kwamba karibu wanawake 18,500 wajawazito wamelazimika kukimbia Rafah. "Takriban 10,000 zaidi wamesalia huko katika hali mbaya na upatikanaji wa huduma za afya na vifaa vya uzazi ni mdogo. Afya ya mama na mtoto iko hatarini.”Likirejea wasiwasi huo mkubwa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP kupitia Matthew Hollingworth, Mkurugenzi wa WFP katika eneo linalokaliwa la Palestina lisema sasa hakuna "kikubwa tunachoweza kuwafanyia watu ambao bado wako Rafah, ambako barabara si salama, hazifikiki vizuri, na washirika wetu wengi na mashirika mengine ya kibinadamu yametawanywa”.Ameonya kwamba hofu ya afya ya umma sasa imevuka viwango vya janga, wakati sauti, harufu, na maisha ya kila siku, ni ya kutisha na ya kuzimu. Watu "wamekimbilia maeneo ambayo maji safi, vifaa vya matibabu na usaidizi havitoshi, usambazaji wa chakula ni mdogo, na mawasiliano ya simu yamesitishwa."
3-6-2024 • 1 minuut, 58 seconden
03 JUNI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na afya ya uzazi nchini Randa. Mashinani tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Watu milioni moja sasa wamefungasha virago na kuukimbia mji wa Rafah kusini mwa Gaza, ka mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huku kukiwa na ripoti mpya za mashambulizi ya usiku kuamkia leo katika maeneo ya kusini, kati na kaskazini yanayofanywa na vikosi vya Israel. Nchini Rwanda, hivi karibuni Wizara ya Afya ya nchi hiyo, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), imeanza usambazaji wa Vidonge vyenye virutubisho vingi vya lishe (MMS) ili kuboresha lishe ya wajawazito kama njia ya kupunguza kasi ya udumavu kwa watoto.Katika makala Umoja wa Mataifa uliitambua rasmi umuhimu wa baiskeli tarehe 13 mwezi Machi mwaka 2022 kwa kupitisha azimio la kutambua tarehe 3 mwezi Juni kila mwaka kuwa siku ya baiskeli duniani. Umuhimu wake kama chombo cha usafiri chenye gharama nafuu, hakichafui mazingira na zaidi ya yote afya kwa watumiaji kwani ni mazoezi.Na mashinani tutaelekea Mwanza nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu mikakati ya kudhibiti uhalifu katika mipaka Afrika mashariki.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
3-6-2024 • 9 minuten, 57 seconden
UNICEF yafanikisha mradi wa Lishe Bora kwa Wanawake Wajawazito nchini Rwanda
Nchini Rwanda, hivi karibuni Wizara ya Afya ya nchi hiyo, kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), imeanza usambazaji wa Vidonge vyenye virutubisho vingi vya lishe (MMS) ili kuboresha lishe ya wajawazito kama njia ya kupunguza kasi ya udumavu kwa watoto. Nshimiyimana Clementine, ni Mkuu wa Kituo cha Afya cha Kabaya, Wilayani Ngororero katika Jimbo la Magharibi nchini Rwanda anasema, “Wajawazito wanapata taarifa kutoka kwa Wahudumu Afya Jamii ambao wanawaelekeza kwenda kwenye vituo vya afya kwa ajili ya vipimo muhimu na kupata vidonge vya lishe.”“Tunawashauri kumeza kidonge kimoja kila siku angalau kwa miezi sita. Na sasa kwa kuwa tumeanza kusambaza vidonge lishe hivi tunaamini vitakuwa na manufaa kwa kuzingatia lishe zilizomo. Wajawazito hawatakosa virutubisho kutoka kwenye matunda na mbogamboga kwa kuwa hivi vidonge vinavyo. Japo bado tunawahimiza wajawazito kula matunda na mbogamboga, lakini wale wasiomudu hawataathirika na upungufu wa virutubisho. ”Umugwaneza Yvette ni mmoja wa wajawazito wanufaika wa programu hii iliyowezeshwa kwa ukarimu wa KIRK Humanitarian shirika lisilo la kiserikali linalojitolea kuhakikisha Virutubisho lishe kupitia Umoja wa Mataifa vinawafikia wajawazito kokote waliko duniani.“Wakati usambazaji wa vidonge vya MMS ulipoanza, nilikuwa miongoni mwa watu wa mwanzo kupokea. Mwili wangu umevipokea vizuri. Sijapata changamoto yoyote. Ninameza mara kwa mara na ninajisikia mwenye afya.”
3-6-2024 • 1 minuut, 56 seconden
Akili Mnemba inarahisisha mambo lakini inahitaji usimamizi - Profesa Pillay
Kila uchao, mikutano ifanyika kona mbali mbali za dunia kubonga bongo ni kwa vipi akili mnemba inaweza kutumika kwa manufaa ya binadamu na si vinginevyo kwani Umoja wa Mataifa unataka nyenzo hiyo iwe ya manufaa hasa katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu. Huko Geneva, Uswisi kumetamatika mkutano wa kujadili ni kwa vipi akili mnemba italeta manufaa. Suala hilo hilo pia lilikuwa miongoni mwa mijadala ya jukwaa la 4 la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali huko Manama, Bahrain ambapo mmoja wa wanajopo alikuwa Profesa Dokta Selvaraj Oyyan Pillay kutoka Malaysia ambaye katika makala hii Assumpta Massoi alizungumza naye na kuumuliza iwapo ana shaka na shuku kuhusu mustakabali wa akili mnemba na nini kifanyika.
31-5-2024 • 3 minuten, 2 seconden
UNICEF inawasaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kutosikia kujifunza kidijitali nchini Kenya
Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.Mmoja wa walimu walionufaika na mafunzo hayo ni Terika Gevera, Mwalimu katika Shule ya Viziwi ya Maseno katika Kaunti ya Kisumu."Wanafunzi wetu mara nyingi hupata ujifunzaji wao kupitia hisia ya kuona, kwa sababu usikivu wao hauwafai sana. Kwa hivyo, UNICEF kuunganisha shule kwenye intaneti kumesaidia sana hasa katika kuboresha ufundishaji wetu. Watoto wetu wanaweza kujifunza na hasa kujifunza kupitia njia ya kuona wanaweza kupata maarifa kwa njia bora zaidi.”Mwalimu Terika Gevera anafafanua zaidi akisema,"Intaneti ni sehemu muhimu sana katika kujifunza. Tuliamunganishwa katika nyenzo za E-Kitabu. E-Kitabu wamejaribu kuandika hadithi zao kwa lugha ya ishara, hivyo wanafunzi hutazama picha, huangalia ishara na mwisho wa kila hadithi, wanafunzi huulizwa maswali kuhusu hadithi ambayo imesimuliwa kwa ishara. Kupitia hilo wanafunzi wamefahamu kuwa wanaweza kusoma hadithi, kuelewa na kujibu maswali.”
31-5-2024 • 1 minuut, 37 seconden
31 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Burkina Fasso na mradi unofahamika kama GIGA unaosaidia kufanikisha masomo ya kidijitali kwa wanafunzi nchini Kenya. Makala inamulika usimamizi wa Akili Mnemba na mashinani inatupeleka Garissa nchini Kenya, kulikoni?Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai ya kuwajibika na mauaji hayo kutoka pande zote, makundi yenye silaha na serikali. Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi unofahamika kama GIGA, kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu, wameunganisha wanafunzi zaidi ya 257,000 kwenye mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanafunzi 7,690 wenye mahitaji maalum, na pia mafunzo ya kidijitali kwa maelfu ya walimu.Makala inaturejesha Bahrain kufuatilia usimamizi wa Akili Mnemba wakati huu ambapo huko Geneva, wabobezi wa Akili Mnemba na wawakilishi kutoka sekta ya umma na binafsi wakibonga bongo kuhusu matumizi sahihi ya teknolojia hiyo, Assumpta Massoi amezungumza na mwanazuoni kutoka Malaysia kandoni mwa jukwaa la Umoja wa Mataifa la Uwekezaji kwa wajasiriamali lililomalizika hivi karibuni huko Manama.Na katika mashinani tutasalia nchini Kenya kaunti ya Garissa ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM linaendelea kutoa msaada kwa maelfu ya watu waliopoteza makazi yao kutokana na mafuriko yanayoendelea.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
31-5-2024 • 9 minuten, 51 seconden
Volker Türk: Mauaji ya raia Burkina Faso yamefurutu ada lazima yakome
Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameelezea wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la hivi karibuni la mauaji ya raia nchini Burkina Faso, huku kukiwa na madai pande zote, makundi yenye silaha na serikali kuhusika na mauaji hayo. Kwa mujibu wa tarifa ya ofisi ya Kamishina Mkuu wa haki za binadamu OHCHR kati ya Novemba 2023 na Aprili mwaka huu 2024 imepokea madai ya ukiukwaji wa haki na ukatili unaokiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu ukiwaathiri takriban watu 2732 hili likiwa ni ongezeko la asilimia 71 ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu ukilinganisha na miezi sita iliyopita.Taarifa inasema watu 1794 ay asilimia 65 miongoni mwa watu hao ni waathirika wa mauaji ya kinyume cha sheria.Ofisi hiyo ya haki za binadamu imesema Makundi yenye silaha, kama vile Jamāʿat nuṣrat al-islām wal-muslimīn, Kundi kubwa la Kiislamu katika Jangwa la Sahara na makundi mengine yanayofanana na hayo, yamezidisha mashambulizi yao dhidi ya raia, ikiwa ni pamoja na dhidi ya wakimbizi wa ndani. Kwa mujibu wa Bwana Türk "Wakati makundi yenye silaha yanadaiwa kuhusika na idadi kubwa ya matukio na waathirika, na yanapaswa kuwajibika, pia ninasikitishwa sana kwamba vikosi vya usalama na ulinzi na wasaidizi wao ambao ni watu waliojitolea kwa ulinzi wan chi yao wanadaiwa kutekeleza mauaji ya kiholela, ikiwa ni pamoja na kunyongwa,”Awali mkuu huyo wa haki za binadamu alizungumzia masuala haya na Kapteni Ibrahim Traoré, Rais wa Burkina Faso, wakati wa ziara yake nchini humo Machi mwaka huu.Türk ameongeza kuwa "Ninatambua kikamilifu vitisho tata vya usalama ambavyo Burkina Faso inakabiliana nayo. Jawabu dhidi ya vitisho hivi litafaulu tu ikiwa sheria za kimataifa zitaheshimiwa kikamilifu kote nchini. Kwa hivyo narudia wito wangu kwa mamlaka nchini Burkina Faso kuchukua hatua zote zinazowezekana ili kuhakikisha ulinzi wa raia,” Kamishna Mkuu ametoa wito kwa Serikali ya Burkina Faso kuunga mkono uchunguzi wa kina, huru na wa uwazi kuhusu tuhuma zote za ukiukaji wa haki na ukiukwaji wa sheria za kimataifa, na kuhakikisha kuwa wahalifu wanafikishwa mahakamani, katika kesi zinazokidhi viwango vya kimataifa, ili kuhakikisha haki ya kweli kwa waathirika na fidia.Amesisitiza kwamba ni “Lazima kuweka na haki na uwajibikaji endapo mamlaka inataka kweli kuihakikishia jamii inarejesha mshikamano wa kijamii na kujenga upya uaminifu kati ya raia na vikosi vya usalama."
31-5-2024 • 1 minuut, 53 seconden
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno "Kibuhuti"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIBUHUTI”
30-5-2024 • 0
30 MEI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika ni kwa vipi wabunifu wanaweza kumiliki kazi zao na zikasongesha SDGs ikiwemo kutokomeza umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za Sudan, Gaza na jukwaa la Kimataifa la “AI for Good”, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki.Mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa leo yametoa onyo kali kwamba dalili zote zinaonesha kuzorota kwa kiasi kikubwa kwa hali ya lishe kwa watoto na wanawake katika nchi ya Sudan inayokumbwa na vita. Uchambuzi wa hivi karibuni uliofanywa na Mashirika hayo matatu la Kuhudumia Watoto (UNICEF), la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na la afya ulimwenguni (WHO) unaonesha kwamba uhasama unaoendelea unazidisha visababishi vya utapiamlo kwa watoto. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kutoa wito wa usitishaji mapigano katika Ukanda wa Gaza kwasababu hali inazidi kuwa tete kila uchao. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema hakuna mengi ambayo linaweza kufanya kwa sasa huko Rafah kwani akiba ya chakula ni ndogo na kuna vikwazo vingi kuwafikia watu.Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa wa Akili Mnemba umeanza leo Mei 30 mjini Geneva, Uswisi kujadili matumizi bora ya Akili Mnemba (AI) ili kuharakisha kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa na unaunganisha wabunifu wa Akili Mnemba na watoa uamuzi wa sekta ya umma na binafsi ili kusaidia kuongeza ufumbuzi unaotokana na akili Mnemba kote duniani.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIBUHUTI”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
30-5-2024 • 11 minuten
Nilikuwa na ujauzito wa miezi tisa nyumba yangu ilipopigwa bomu - Simulizi ya mkimbizi Sudan
Makala hii inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika. Sara alikuwa na ujauzito wa miezi 9 wakati bomu lilipopiga nyumba yake na kumlazimu kukimbia na hatimaye kujifungua mtoto wake peke yake bila uangalizi wowote wa kitabibu. Familia nyingi nchini Sudan zimesambaratishwa na mzozo unaoendelea. Selina Jerobon ndiye msimulizi wetu..
29-5-2024 • 2 minuten
29 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa. Makala inatupeleka nchini Sudan kusikia simulizi ya mmoja wa wakimbizi na mashinani tunakupelekea nchini Ethiopia kusiki jinsi ambavyo wasichana wanavyosaidiwa kubaki shule.Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee wa kimataifa. Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.Makala inatupeleka nchini Sudan kuangazia maisha ya Sara, mmoja wa wakimbizi wa ndani katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.Na mashinani tutaelekea Gambella nchini Ethiopia kusikia ni kwa jinsi gani shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linahakikisha kuwa wasichana hawakosi masomo yao kwa kukosa sodo au taulo za kike wakati wa hedhi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
29-5-2024 • 9 minuten, 43 seconden
Ulinzi wa amani wa UN ni ushirikiano wa kipekee wa kimataifa
Leo ni siku ya kimataifa ya walindaamani wa Umoja wa Mataifa mwaka huu ikibeba maudhui “Kuwa tayari kwa ajili ya ujenzi wa mustakbali bora kwa pamoja”. Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa ulinzi wa amani unasialia kuwa ushirikiano wa kipekee wa kimataifa. Katika ujumbe wake kwa siku hii Antonio Guterres amesema "Leo tunawaenzi walinda amani zaidi ya 76,000 wa Umoja wa Mataifa ambao wanadumisha lengo bora zaidi la ubinadamu, amani. Siku baada ya siku, wakihatarisha Maisha yao, wanawake na wanaume hawa wanafanya kazi kwa ujasiri katika baadhi ya maeneo hatari na yasiyo na utulivu duniani ili kulinda raia, kudumisha haki za binadamu, kumsaidia masuala ya uchaguzi na kuimarisha taasisi. Zaidi ya walinda amani 4,300 wamelipa gharama ya Maisha yao wakati wakihudumu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa. Hatutawasahau kamwe.”Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa maudhui ya siku ya mwaka huu yanaashiria kwamba wakati ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa umethibitika kuwa sehemu ya suluhu kwa zaidi ya miaka 75 ukizisaidia nchi mwenyeji kuvuka mapito kutoka kwenye migogoro hadi amani muhtasari wa Sera wa Katibu Mkuu wa Ajenda mpya ya amani unaweka njia ya operesheni za kimataifa za amani na usalama mbele ili kusalia kuwa zana zinazofaa kushughulikia vita na migogoro ijayo.Naye mkuu wa operesheni za Umoja wa Mataifa za ulinzi wa amani Jean-Pierre Lacroix,akiongeza sauti yake katika siku hii amesema "Ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa unasalia kuwa ushirikiano wa kipekee wa kimataifa, huku walinda amani kutoka zaidi ya nchi 120 wakifanya mabadiliko yenye tija kila siku kwa mamilioni ya watu katika baadhi ya maeneo magumu zaidi duniani. Tunapokabiliana na changamoto za kesho, ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa unaendelea kubadilika, na kuhimiza ushirikiano kuwa mahiri, msikivu na unaofaa kwa madhumuni yaliyokusudiwa, kukuza utulivu, kulinda walio hatarini na kusaidia kujenga amani ya kudumu."Siku ya Kimataifa ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa inaadhimishwa kila mwaka Mei 29 na ilianzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2002 ili kuwaenzi wanaume na wanawake wote katika operesheni za ulinzi wa amani na kuenzi kumbukumbu ya wale wote waliopoteza Maisha yao kwa lengo la kuleta amani.
29-5-2024 • 2 minuten, 35 seconden
Jenerali Birame Diop: Ulinzi wa amani uwe na mkakati wa kudhibiti habari potofu na za uongo
Mshauri wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kijeshi, Jenerali Birame Diop amesema kadri binadamu wataendelea kuweko duniani mizozo na majanga yataendelea kuweko na hivyo kinachohitajika ni mfumo wa kupunguza uweko na utatuzi wa majanga hayo.Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha siku ya walinda amani duniani, Jenerali Diop ambaye anatamatisha jukumu lake anasema angalau kwa sasa kuna jawabu la ulinzi wa amani ambalo licha ya changamoto zake linaleta nuru.“Na ulinzi wa amani umethibitisha kuwa unaweza kutatua baadhi ya mizozo. Ninaweza kukupatia mfano wa Timor-Letse [TIMORLETSI]. Ninaweza kukupa mifano ya Côte d'Ivoire, ya Sierra Leone, ya Liberia, ambako ulinzi wa amani umesaidia kurejesha amani na utulivu. Na sasa nchi hizi hata zinashiriki kwenye ulinzi wa amani.”Ingawa ulinzi wa amani unazaa matunda, kwa Jenerali Diop ambaye anatoka Senegal, jambo muhimu ni kuzidi kuboresha huduma hiyo kwani itaendelea kuwa muhimu huku Umoja wa Mataifa ukihakikisha ujumbe wa ulinzi wa amani unapatiwa mamlaka na majukumu sahihi ili kukidhi mantiki ya uwepo wake. Na zaidi ya yote.“Tunatakiwa pia leo hii kuambatanisha ujumbe wa ulinzi wa amani na mfumo wa kimkakati wa mawasiliano ili kuzuia habari potofu na habari za uongo zinazoharibu kila kitu tunachofanya. Ulinzi wa amani hautafanikiwa iwapo nchi mwenyeji haiungi mkono ujumbe wa ulinzi wa amani.”
29-5-2024 • 1 minuut, 33 seconden
28 MEI 2024
Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea-Watu zaidi ya 2000 wahofiwa kufunikwa na maporomoko ya udongo Papua New Guinea , Umoja wa Mataifa wasaidia-Ripoti ya UNRWA inasema wakimbizi wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza wanakabiliwa na dharura ya kiafya isiyokuwa na mfano wake iliyosababishwa na vita mbaya zaidi katika historia ya Gaza- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameuambia Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea (SIDS4) Antigua na Barbuda kwamba ulimwengu unahitaji kuchukua hatua ili kusaidia vyema na kuhamasisha ufadhili kwa Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea (SIDS) -Katika kuelekea siku ya walindamani hapo kesho leo kikosi cha Tanzania TANZBAT11 nchini DRC chashikamana na wananchi katika miradi mbalimbali-Na mashinani utamsikia mlindamani kutoka Italia anayehudumu katika mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL
28-5-2024 • 10 minuten, 34 seconden
Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ yaamua juu ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu Gaza
Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo.Leo Kwa kura 13 dhidi ya 2 mahaka ya ICJ imeamua kwamba:1. Inathibitisha tena hatua za muda zilizoainishwa katika Maagizo yake ya tarehe 26 Januari 202 na 28 Machi 2024, ambayo yanapaswa kutekelezwa mara moja na kwa ufanisi2. Imeainisha hatua zifuatazo za muda kwamba : Taifa la Israeli, kwa kuzingatia wajibu wake chini ya Mkataba juu ya Kuzuia na Adhabu ya Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari, na kwa kuzingatia hali mbaya ya maisha inayowakabili raia katika Jimbo la RafahIsitishe mara moja mashambulizi yake ya kijeshi, na hatua nyingine yoyote katika jimbo la Rafah ambayo yanaweza kusababishia kundi la Wapalestina Gaza hali hiyo ya maisha inayoweza kuleta uharibifu wa kimwili kwa ujumla au sehemu;Iendeleel kukiacha wazi kivuko cha Rafah kwa utoaji usiozuiliwa kwa kiwango cha haraka cha huduma za msingi zinahitajika na msaada wa kibinadamu;Kuchukua hatua madhubuti ili kuhakikisha ufikiaji usiozuiliwa wa Ukanda wa Gaza kwa tume yoyote ya uchunguzi, ujumbe wa kutafuta ukweli au chombo kingine cha uchunguzi kilichoagizwa na vyombo vyenye uwezo wa Umoja wa Mataifa kuchunguza tuhuma za mauaji ya kimbari;3. Mahakama imeamua kwamba Israeli itawasilisha ripoti kwa Mahakama juu ya hatua zote kuchukuliwa ili kutekeleza agizo hili, ndani ya mwezi mmoja kuanzia tarehe ya agizo hili.
24-5-2024 • 1 minuut, 54 seconden
WHO: COVID-19 imerudisha nyuma muongo wa maendeleo ya umri wa watu kuishi
Ripoti mpya ya Takwimu za Afya Ulimwenguni iliyotolewa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, inaonyesha kuwa janga la COVID-19 limebadilisha mwelekeo wa kuongezeka kwa umri wa watu kuishi wakati wa kuzaliwa na matarajio ya maisha yenye afya wakati wa kuzaliwa HALE.Ripoti hiyo ya takwimu za afya ulimwenguni hutolewa kila mwaka na WHO ikijumuisha viashirikia vya afy na vinavyohusiana na imekuwa ikitolewa tangu mwaka 2005.Ripoti yam waka huu kwa mujibu wa WHO imetathimini Zaidi ya viashiria 50 vinavyohusiana na afya kuanzia malengo ya maendeleo endelevu SDGs na mikakati kazi 13 ya WHO au GPW13.Ripoti inasema Janga la COVID-19 limefuta karibu muongo mmoja wa maendeleo katika kuboresha umri wa watu kuishi ndani ya miaka miwili tu. Kati ya 2019 na 2021, umri wa kuishi duniani ulipungua kwa mwaka 1.8 hadi miaka 71.4 ukirejea nyuma hadi kiwango cha mwaka 2012.”Pia ripoti imeongeza kuwa umri wa kuishi kwa afya duniani ulipungua kwa miaka 1.5 hadi miaka 61.9 mwaka 2021 ukiwa umerudi nyuma kwenye kiwango cha mwaka 2012. Ripoti hiyo ya 2024 pia imeainisha ni jinsi gani athari hizo zimehisiwa tofauti na hazilingani kote duniani.Maeneo ya WHO yaliyoathirika Zaidi ripoti inasema ni Ukanda wa Amerika na Kusini-Mashariki mwa Asia, ambako umri wa kuishi ukishuka kwa takriban miaka 3 na matarajio ya maisha yenye afya yakishuka kwa miaka 2.5 kati ya mwaka 2019 na 2021.Kinyume chake, Kanda za Pasifiki Magharibi zimeathiriwa kidogo wakati wa miaka miwili ya kwanza ya janga hla COVID-19 na kupata hasara ya chini ya miaka 0.1 katika umri wa kuishi na miaka 0.2 katika matarajio ya maisha yenye afya.
24-5-2024 • 2 minuten, 25 seconden
Wanajeshi walinda amani wa UN wana majukumu mengine muhimu zaidi ya bunduki: TANBAT 7
Zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na kuwatia moyo na leo tunaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasikia baadhi yao kutoka katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA)
24-5-2024 • 3 minuten, 15 seconden
FAO na wadau wawakutanisha wadau wa kilimo na chakula Tanzania
Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021. Hamad Rashid wa Redio washirika wetu Mviwata FM ya Mkoani Morogoro amehudhuria Kikao hicho na kuandaa taaarifa hii.
24-5-2024 • 3 minuten, 50 seconden
24 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia maamuzi ya ICJ ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel, na mifumo ya chakula nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na mashinani nchini Kenya, kulikoni? Mahakama ya kimataifa ya haki ICJ leo imetoa maamuzi ya kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel kuhusu utekelezaji wa Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari katika Ukanda wa Gaza Flora amefuatilia uamuzi huo. Nchini Tanzania, kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na wadau wake kama Kitovu cha Kuratibu Mifumo ya Chakula cha Umoja wa Mataifa, Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Kilimo na Lishe, wakulima, sekta binafsi, na watafiti na Taasisi za kitaaluma wamekutana mjini Morogoro ili kupitia na kuboresha vipaumbele na ramani ya mifumo ya chakula iliyoanzishwa mwaka 2021.Katika makaala zikiwa zimesalia siku chache kufika Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila Mei 29, tunaangazia shughuli zao na kuwatia moyo na leo tunaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kuwasikia baadhi yao kutoka katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR (MINUSCA).Na mashina Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM inaendelea kutoa vifaa muhimu vya nyumbani na usafi pamoja na usaidizi wa pesa kwa maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kutokana na mafuriko yanayoendelea nchini Kenya, Mahmood Abdirahman, kuongozi wa jamii katika kaunti ya Garissa anasimulia changamoto zilizowakumba jamii hizo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
24-5-2024 • 10 minuten
Jifunze Kiswahili: Pata ufafanuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Kanga hazai ugenini.”
23-5-2024 • 1 minuut, 23 seconden
23 MEI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada ka kina inayotupeleka huko wilaya ya Abyei iliyoko kati ya mpaka wa Sudan Kusini na Sudan lilifanyika shambulizi la kuvizia wakati gari la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likisafirisha raia waliojeruhiwa, ambalo lilisababisha kifo cha mlinda amani. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.” Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza ugonjwa wa Fistula ambalo ni tundu kati ya njia ya uzazi na kibofu cha mkojo, inayosababishwa mara nyingi na uchungu wa muda mrefu wakati wa kuelekea kujifungua, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na masuala ya kijinsia UNFPA Natalia Kanem amesema Fistula ya uzazi ni matokeo ya kusikitisha ya kushindwa kulinda haki za uzazi za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu zaidi na ni lazima itokomezwe kwa watu wote. Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Palestina Matthew Hollingworth ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba maelfu ya familia zinazokimbia Rafah zinajikuta zikiwa na uhaba wa chakula na maji safi.Mvua nyingi zaidi kuliko kawaida inatabiriwa katika maeneo mengi ya Pembe ya Afrika kuanzia mwezi Juni hadi Septemba mwaka huu. Maeneo yatakayotarajiwa kuwa na hali hiyo ni Djibouti, Eritrea, kaskazini na katikati mwa Ethiopia, magharibi na pwani ya Kenya, sehemu kubwa ya Uganda, Sudan Kusini, na Sudan.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Kanga hazai ugenini.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
23-5-2024 • 10 minuten, 36 seconden
Waathirika Garisa Kenya washukuru UNICEF kwa msaada wa fedha baada ya mafuriko
Kenya inashuhudia kiwango kikubwa cha mvua zaidi ya kile cha kawaida ambacho kimesababisha mafuriko makubwa,maporomoko ya udongo na maelfu ya watu kutawanywa hivi karibuni. Miongoni mwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni Kaunti ya Garisa , ambako hivi sasa asante kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake kama shirika la Norway kwa ajili ya ushirikiano wa maendeleo NORAD, Mamlaka ya Kitaifa ya kudhibiti Ukame Kenya NDMA, na serikali ya Kaunti ya Garasa kwani kaya zilizoathirika na mafuriko zinapokea msaada wa fedha taslim kupitia M-pesa na vocha za kielektroniki ili kujikimu kimaisha. Flora Nducha anafafanua zaidi katika makala hii
22-5-2024 • 3 minuten, 11 seconden
UNICEF: Vurugu zinatikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka
Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini Port-Au-Prince imeeleza kwamba vurugu zimeutikisa mfumo wa afya wa Haiti unaoporomoka kutokana na kwamba makundi yenye silaha yamenyonga minyororo ya usambazaji, na kuweka mamilioni ya watoto katika hatari ya magonjwa na utapiamlo.Kila hospitali nchini Haiti imeripoti ugumu wa kupata na kutunza vifaa muhimu vya matibabu, kwani safari za ndege za kimataifa na za ndani za mizigo kutoka na kwenda katika viwanja vya ndege vya Port-Au-Prince zilirejea kufanya kazi hivi majuzi tu, zikiwa na uwezo mdogo na mrundikano mkubwa, kama ilivyokuwa kwa bandari kuu ambayo hapo awali ilikuwa mikononi mwa makundi yenye silaha."Mfumo wa afya wa Haiti uko karibu kuporomoka," Bruno Maes, Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti amesema akiongeza kwamba, "Mchanganyiko wa vurugu, ufurushaji wa watu wengi, milipuko hatari, na kuongezeka kwa utapiamlo kumeupinda mfumo wa afya wa Haiti, lakini kunyongwa kwa minyororo ya usambazaji kunaweza kuwa ndio kunauvunja."Makontena yaliyojazwa vifaa muhimu yamezuiliwa, au kuporwa, kama ilivyokuwa kwa maghala na maduka mengi ya dawa. Wakati huo huo, mamia ya makontena yaliyosheheni vifaa vya kibinadamu yamekwama huko Port-Au-Prince ikiwa ni pamoja na kontena za UNICEF zilizo na vifaa vya watoto wachanga, wajawazito na vya matibabu.Port-Au-Prince, kitovu kikuu cha Haiti, kwa kawaida hupokea na kutuma mizigo ya uagizaji wa vifaa tiba vya Haiti. Sasa jiji hilo limelemazwa na vurugu, na wakazi wake zaidi ya 160,000 wameyakimbia makazi yao, jiji hilo haliwezi kutosheleza mahitaji ya watu ambao kwa wakati mmoja wanapambana na majeraha ya kimwili na hatari ya magonjwa, inafafanua taarifa ya UNICEF.Mawimbi ya familia zilizofurushwa zinazotafuta usalama, hasa katika sehemu ya kusini mwa nchi, yanaleta shinikizo la ziada kwa huduma za afya za wanakokimbilia, ambazo hata kabla ya kuongezeka kwa mzozo hazikuweza kuhimili mahitaji. Uhaba wa wafanyakazi umeenea, na takriban asilimia 40 ya wafanyakazi wote wa matibabu wameondoka nchini Haiti kutokana na viwango vya juu vya ukosefu wa usalama.Kati ya Oktoba 2022 na Aprili 2024, Haiti iliripoti jumla ya visa 82,000 vinavyoshukiwa kuwa na kipindupindu. Takriban watu milioni 4.4 nchini Haiti wanahitaji msaada wa haraka wa chakula, na watu milioni 1.6 wanakabiliwa na viwango vya dharura vya uhaba wa chakula, jambo ambalo linaongeza hatari ya kupata tatizo la uzito mdogo kwa watoto na utapiamlo. Kuwasili kwa msimu wa mvua kunatazamiwa kuzidisha hali kuwa mbaya zaidi, hivyo kusababisha ongezeko la visa vya magonjwa yatokanayo na maji pamoja na magonjwa yanayoenezwa na mbu, kama vile malaria.Ili kukabiliana na hali hiyo, UNICEF na wadau wanatafuta njia mbadala za kuagiza na kusambaza mizigo. Kupitia njia za pili za uingizaji na utoaji, pamoja na Wizara ya Afya, wafadhili wa kimataifa na washirika, UNICEF imeweza kuendelea kupeleka chanjo, dawa na vifaa vya matibabu kwa watoto nchini Haiti ambao wanahitaji zaidi.Tarehe 18, 20 na 21 Mei 2024, UNICEF iliwezesha kuwasilisha tani 38 za vifaa vya kuokoa maisha, ikiwa ni pamoja na vifaa vya afya na kipindupindu, na bidhaa nyingine muhimu za matibabu nchini Haiti kupitia njia ya anga kwa kuungwa mkono na Muungano wa Ulaya na WFP kutoka Panama hadi mji mkuu wa Haiti, ambapo UNICEF na Umoja wa Mataifa wameanzisha kituo kipya cha kufanya kazi. Lakini msaada zaidi unahitajika."Hatuwezi kuruhusu vifaa muhimu ambavyo vinaweza kuokoa maisha ya watoto kubaki vikiwa vimezuiliwa kwenye maghala na makontena. Lazima viwasilishwe sasa,” amesisitiza Maes, Mwakilishi wa UNICEF nchini Haiti.
22-5-2024 • 1 minuut, 34 seconden
22 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya kwa watoto nchini Haiti na simulizi afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO kuhusu yanayoenndelea Gaza. Makala tnakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni? Ghasia zikiwa zinaongezeka katika mji mkuu wa Haiti, Port-Au-Prince, hospitali sita kati ya kumi nchini humo ziko katika hali mbaya ya utoaji huduma limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF. Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”Makala inatupeleka Kaunti ya Garisa nchini Kenya ambako waathirika wa mafuriko na maporomoko ya udongo ya hivi karibuni walio katika makambi za muda za wakimbizi wa ndani wanapokea msaada wa fecha na vocha kutoka kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake ikiwaweze kujikimu.Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
22-5-2024 • 10 minuten, 29 seconden
Niliyoshuhudia Gaza yanatisha na kusikitisha - Nika Alexander
Afisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO aliyerejea hivi karibuni kutoka Ukanda wa Gaza amesimulia yale aliyoshuhudia akiwa huko huku huku akisisitiza kuwa "hakuna mahali salama" katika Ukanda huo na aliyoshuhudia ni “yakusitikisha na ya kutisha.”Ni Nika Alexander kiongozi wa timu ya mawasiliano ya dharura kutoka WHO akieleza tofauti ya kwanza anayoona sasa akiwa amerejea kutoka Gaza ambapo wakati angali kule siku baada ya siku wakisikia mlio wa ndege basi bomu linaweza kuanguka dakika yoyote, wakati sasa ukiwa sehemu ambayo si ya vita akisikia mlio wa ndege pengine ni watu wanaendea likizo ni kama watu wa Gaza wanaishi kinyume na ulimwengu. Akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya kurejea Gaza Bi.Nika anasimulia hali ya kule. “Nilichoondoka nacho ni mawazo ya jinsi hali ilivyo mbaya kwa watu wa Gaza, jinsi hali ilivyo ngumu kwa watu wanaojaribu kuwasaidia watu wa Gaza na jinsi kulivyo hatari.” Amesema hospitali zinazofanya kazi ni chache na hazifanyi kazi kamili.“Kimsingi, kote Gaza, ni theluthi moja ya hospitali ndio zinafanya kazi. Kwa hivyo takriban hospitali 12 kati ya 36 bado zinaweza kufanya kazi kwa namna fulani. Hawawezi kutoa huduma kamili. Baadhi yao wanafanya kama sehemu ya kutoa huduma ya kwanza na kusaidia wenye kiwewe, ambapo wanajaribu tu kutibu wake wanakuwa wanavuja damu na vyovyote vile wawezavyo ilimradi watu wasife kutokana na majeraha.”Afisa huyu wa mawasiliano ya dharura anasema pamoja na yote hayo lakini lipo lililompa matumaini licha ya kutokuwepo kwa eneo lolote salama katika Ukanda wa Gaza. “Kilichonivutia sana ni kwa jinsi kila mtu anavyofanya kazi kwa bidii licha ya hali mbaya ambapo kila kelele inaweza kuwa ni mlipuko karibu yako, au unaweza kuwa unakulipukia wewe. Nilipoondoka Rafah wiki moja iliyopita, tulikuwa wafanyakazi 19 wanaondoka na wengine 20 wa Umoja wa Mataifa wanaingia Rafah. Ninawaona wenzangu hao kuwa wajasiri sana, na sio kwamba wanakuja kujifanyia kazi wenyewe bali wanakuja kushirikiana na wafanyakazi wa Gaza wa sekta ya afya.”
22-5-2024 • 2 minuten, 52 seconden
21 MEI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kufuatilia mradi wa mradi wa Cookfund, Elisabeth Ngoye amezungumza na Laurien Kiiza wa UNIC Dar es Salaam. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za afya, Gaza na Ukraine. Mashinani inatupeleka nchini Kenya, kulikoni? Ripoti mpya iliyotolewa leo Mei 21 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO inaashiria ongezeko kubwa la magonjwa ya zinaa duniani, huku kukiwa bado na changamoto za Virusi Vya Ukimwi na homa ya ini. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X ameeleza wasiwasi mkubwa walio nao juu ya usalama wa wagonjwa na wafanyakazi waliokwama katika hospitali ya Al-Awda kaskazini mwa Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini Ukraine, limeeleza kuhusu wasiwasi mkubwa kutokana na hali inayozidi kuwa mbaya na kusababisha ongezeko la mahitaji ya kibinadamu kwa Waukraine na kulazimishwa kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi mapya ya ardhini ya Jeshi la Urusi katika eneo la kaskazini-mashariki la Kharkiv.Na katika mashinani leo tunakupeleka katika eneo Bunge la Ngong lililoko katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa utunzaji wa chemichemi ya maji.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
21-5-2024 • 10 minuten, 52 seconden
Ninajisikia fahari sana kutatua changamoto za wanawake na watoto wa CAR - Meja Lilian Laizer
Makala hii inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo. Meja Lilian Laizer anashughulika na masuala ya jinsia na watoto katika kikosi na jamii ya wenyeji. Msimulizi ni Anold Kayanda
20-5-2024 • 3 minuten, 25 seconden
Baadhi ya wapalestina warejea kwenye nyumba zao zilizoathiriwa na mabomu baada ya kulazimishwa kuondoka Rafah
Kuongezeka kwa shughuli za kijeshi huko Rafah, kusini mwa Gaza, kumesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao, na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa maelfu ya familia ambazo tayari zimelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP lina wasiwasi mkubwa kwamba hali hii ya kuhama hama inaweza kusababisha janga la kibinadamu, nakupelekea kusimama kwa shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu.Baada ya kufika nyumbani kwake, Ibrahim Kamal Ibrahim Amtair anamuonesha mtoto wake mdogo wa kike box lililojaa bidhaa mbalimbali za msaada aliopokea kutoka WFP. Ibrahim ni mmoja wa watu waliokimbia makazi yao Khan Younis na kukimbilia Rafah baada ya amri ya Jeshi la Israel lakini baada ya Israel wiki iliyopita kutoa tena amri ya kuwataka kuondoka Rafah ameona hana tena pa kukimbilia na kuamua kurejea katika nyumba yake. Amekuta nyumba yake imeathirika vibaya na mabomu pamoja na risasi, baadhi ya maeneo hakuna madirisha wala milango huku kukiwa na matundu ambayo ameyafunika kwa mabox na anasema mpango wake ni kukarabati matundu hayo ili watoto wake wasijeumia. “Hawakusema kuwa eneo hili liko salama, lakini tumerudi kwa sababu hatuna mahali pa kwenda, na hatukuwa sawa katika maeneo tuliyokuwepo. Hakuna anayejisikia raha isipokuwa akiwa nyumbani kwake, hata kama nyumba ikiwa imeharibiwa.”Mbali na chakula cha msaada pamoja na vifurushi vya msaada wanavyo patiwa wananchi wa Palestina ambavyo vina vyakula kama vile makopo ya maharage, mbaazi na nyama ya kopo, Mkurugenzi wa WFP huko Palestina, Matthew Hollingworth anasema hifadhi iliyopo sasa ya chakula na mafuta itaisha baada ya siku chache.“Hatujaweza kufikia ghala letu huko Rafah kwa zaidi ya wiki moja sasa. Tuna chakula kidogo na mafuta yanayokuja kupitia vivuko vya mpaka kusini na tunajitahidi kila wakati lakini tunashindwa kwa sasa kuleta kiasi cha kutosha cha chakula. Tunajua, tunahitaji njia za ziada za kuingilia na kila njia ya kuingilia ni mshipa wa kusukuma damu kuingia Gaza. Kwahiyo, tutafanya kazi kwa bidii ili kuendelea kupata njia mpya za kuingia na kupata usaidizi zaidi, kwa wingi na mara kwa mara ili kusaidia kukomesha njaa ambayo inajongea.”Pamoja na changamoto nyingi, WFP inaendelea kusalia Gaza na kushirikiana na wadau wengine katika kutoa msaada kwa wapalestina.
20-5-2024 • 2 minuten, 32 seconden
20 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya sheria na uhalifu na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini CAR kufatilia kazi za walinda amani na mashinani tunakuletea ukumbe kuhusu ufugaji nyuki na thamana yao. Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Karim Khan ametangaza leo Mei 20 maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Israel kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Gaza. Kuongezeka kwa shughuli za kijeshi huko Rafah, kusini mwa Gaza, kumesababisha mamia kwa maelfu ya watu kuyahama makazi yao, na kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa maelfu ya familia ambazo tayari zimelazimika kuyahama makazi yao mara kadhaa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP lina wasiwasi mkubwa kwamba hali hii ya kuhama hama inaweza kusababisha janga la kibinadamu, nakupelekea kusimama kwa shughuli za kutoa misaada ya kibinadamu.Makala inamwangazia Meja Lilian Laizer, Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu katika Kikosi cha 7 cha ulinzi wa amani kutoka Tanzania TANBAT 7 kinachohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR chini ya MINUSCA ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo. Meja Lilian Laizer anashughulika na masuala ya jinsia na watoto.Na katika mashinani leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Nyuki tutasikia uhusiano kati ya nyuki na jamii za watu wa asili.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
20-5-2024 • 11 minuten, 20 seconden
ICC yawasilisha ombi kwa Baraza la Usalama la hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Netanyahu wa Israel
Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, Karim Khan ametangaza leo Mei 20 maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na Israel kwa madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo la Gaza. Ni Karim Khan, Mwendesha Mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu mapema leo alipotangaza kwamba anawasilisha maombi ya hati za kukamatwa viongozi wa Hamas na wa Israel kwa majaji wa mahakama hiyo ambao ndio watakaotoa uamuzi wa kutolewa kibali cha kukamatwa.Bwana Khan amesema kuna sababu za msingi za kuamini kwamba Yahya Sinwar wa Hamas, Mohammed Diab Ibrahim Al-Masri (Deif) na Ismail Haniyeh "wanawajibikia kijinai" kwa mauaji, kuangamiza na kuchukua watu mateka miongoni mwa uhalifu mwingine mwingi tangu mzozo wa Gaza ulipozuka kufuatia mashambulizi yaliyoongozwa na Hamas kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba mwaka jana 2023.“Pia kuna misingi ya kuridhisha ya kuamini kwamba Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Yoav Gallant, Waziri wa Ulinzi wa Israel, wanahusika na uhalifu mwingine na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa katika eneo la Palestina” Amesema Mwendesha Mashitaka wa ICC.Ametaja miongoni mwa vitendo vya uhalifu wa kivita vilivyotekelezwa kuwa ni pamoja na kutumia njaa dhidi ya raia kama mbinu ya vita na pia kuelekeza kwa makusudi mashambulizi dhidi ya raia.Ingawa ICC si shirika la Umoja wa Mataifa, ina makubaliano ya ushirikiano na Umoja wa Mataifa. Na kunapotokea suala ambalo haliko ndani ya mamlaka ya Mahakama, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaweza kulipeleka suala hilo kwa ICC, na kuipa mamlaka ya kulishughulikia.Tutaendelea kukupa taarifa kwa kina kuhusu hatua hii ya ICC ingawa pia kwa sasa unaweza kujisomea zaidi katika wavuti wetu news.un.org/sw
20-5-2024 • 2 minuten, 13 seconden
Orodha mpya ya bakteria sugu dhidi ya dawa yatolewa na WHO
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa. Katika taarifa iliyotolewa leo, WHO inafafanua kuwa usugu wa vijiumbemaradhi dhidi ya dawa hutokea pale ambapo bakteria, virusi, fangasi, na vimelea vingine vya magonjwa haviitikii tena dawa, hivyo kuongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa, watu kuugua na hata vifo.WHO inaeleza kwamba kwa sehemu kubwa hali hii ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa inasababishwa na matumizi mabaya ya dawa za viuavijumbe maradhi.Utafiti huu mpya uliotolewa leo unajumuisha uthibitisho mpya na maarifa ya kitaalamu ili kuongoza utafiti na maendeleo kwa ajili ya viuavijiumbemardahi yaani Antibiotics mpya na kuhamasisha uratibu wa kimataifa ili kukuza uvumbuzi.Baadhi ya bakteria sugu zilizotajwa ni Neisseria gonorrhoeae inayosababisha na Mycobacterium tuberculosis inayosababisha ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB).Orodha kama hii ya vijiumbemaradhi hatari kwa afya ya binadamu ambavyo vimejenga usugu dhidi ya dawa, ilitolewa na WHO miaka 7 iliyopita.Kusoma zaidi kuhusu ripoti hii mpya bofya hapa
17-5-2024 • 1 minuut, 31 seconden
Uchumi wa dunia umeboreka kidogo ingawa Afrika bado kuna changamoto - Nelly Muriuki
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya katikati ya mwaka ya hali na mtazamo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024 iliyotolewa leo inaonyesha matarajio ya kiuchumi duniani yameboreka tangu utabiri uliotolewa Januari 2024, lakini mtazamo ni wa matumaini yanayohitaji tahadhari. Je, Afrika hali iko vipi? Flora Nducha amezungumza na Nelly Rita Muriuki mchumi kutoka Idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA ambao ndio wamezindua ripoti hiyo.
17-5-2024 • 6 minuten, 52 seconden
17 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics, na hali ya kibinadamu nchini Ukraine. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunaelekea nchini Afghanistan, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) leo limetoa Orodha mpya ya inayojumuisha familia 15 za bakteria zenye usugu dhidi ya viuavijiumbe maradhi au antibiotics. Orodha hiyo inatoa mwongozo kuhusu maendeleo ya matibabu mapya na ya lazima ili kukomesha kuenea kwa usugu dhidi ya dawa. Mashirika ya kibinadamu yanafanya kazi bila kuchoka kusaidia kuwaondoka raia katika eneo la Kharkiv ambalo siku za hivi karibuni limeshuhudia kuzorota kwa hali ya usalama na kutanda kwa wimbi la mapigano ambayo yamesababisha vifo vya raia na majeruhi ikiwa ni pamoja na watoto.Makala inaturejesha hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulikozinduliwa ripoti ya nusu mwaka ya mtazamo wa ukuaji na matarajio ya uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024. Je Afrika hali iko vipi? Flora Nducha amezungumza na Nelly Rita Muriuki mchumi kutoka Idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa DESA ambao ndio wamezindua ripoti hiyo.Na katika tunamsikia mama yake Hasenat, mtoto mwenye umri wa miezi saba anayeugua utapiamlo akisimulia jinsi mwanaye anaendelea kupata nafuu baada ya kula chakula cha tiba kiitwacho RUFT ambacho ni uji wenye virutubisho vya vitamini na madini kinachosambazwa na Shirikika la Umoja wa Mataifa ya kuhudumia Watoto, UNICEF.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
17-5-2024 • 10 minuten
Mashirika ya kibinadamu yanahaha kuondoa watu huko Kharkiv Ukraine
Mashirika ya kibinadamu yanafanya kazi bila kuchoka kusaidia kuwaondoka raia katika eneo la Kharkiv ambalo siku za hivi karibuni limeshuhudia kuzorota kwa hali ya usalama na kutanda kwa wimbi la mapigano ambayo yamesababisha vifo vya raia na majeruhi ikiwa ni pamoja na watoto. Video ya ofisi kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura ya Umoja wa Mataifa, OCHAinaanza kwa kuonesha watu wakishuka katika bus, hawa ni raia walioondolewa huko Kharkiv ambako mapigano kati ya Ukraine na Urusi yanaendelea. Uokoaji unaendelea kupitia mabasi yanayoratibiwa na mashirika ya misaada ya kibinadamu, watu binafsi wanaojitolea na serikali za mitaa. Kwa mujibu wa OCHA kati ya tarehe 10 na 15 Mei, karibu watu 2,400 wamefanikiwa kuhamishwa na kuletwa kwenye kituo cha muda ambapo wanapokea usaidizi. Mmoja wa watu hao ni Bibi huyu aitwaye Valentyna anayetujuza hali ilivyokuwa huko alipotoka "Sisi kwetu ni Okhrimivka. Tunaishi pamoja na binti yangu ambaye ni mlemavu. Kijiji chetu kilipigwa na makombora. Kila kitu kimeharibiwa. Ni nyumba 35 tu zimesalia. Wakati wa milipuko ya mabomu tulikuwa tukijificha ghorofa ya chini.”Dmytro Filipskyi kutoka OCHA anasema zaidi ya watu 1,700 wameandikishwa kituoni hapo na wamepatiwa msaada. “Katika eneo hili utaona mashirika yasiyo ya kiserikali na ya misaada ya kibinadamu, mashirika ya Umoja wa Mataifa na ya kimataifa yakitoa msaada wa vifaa vya usafi na kujisafi, chakula, fedha, msaada wa kisaikolojia, ulinzi kwa watoto na makundi mengine yote. Mashirika yote yanahusika katika mchakato huu.” Mashirika ya kibinadamu yalikusanya rasilimali kwa haraka ili kutoa usaidizi wa dharura kwa watu wanaokimbia kusaka usalama. Wamekuwa wakifanya kazi katika kituo hicho ambacho ndio nimekuwa kitovu cha kupokea watu wote wanaokimbia machafuko katika Jiji la Kharkiv na kuratibu usambazaji wa misaada ya kibinadamu tangu kuongezeka kwa mapigano tarehe 10 mwezi huu wa Mei.
17-5-2024 • 2 minuten, 17 seconden
Jifunze Kiswahili: Pata uchambuzi wa neno “HIZAYA.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “HIZAYA.”
16-5-2024 • 0
16 MEI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Bahrain kwenye mji mkuu Manama, ambako wajasiriamali wamekusanyika kwa lengo la kutumia ugunduzi na ujasirimali kusongesha SDGs. Pia tunakuletea muhtasariwa habari kutoka ICJ, WHO na huko huko Bahrain, pamoja na uchambuzi wa neno “HIZAYA.”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerejea wito wake wa kutaka usitishwaji wa mashambulizi huko Rafah kwani wananchi wanazidi kuteseka kutokana na kulazimika kuhama kila wakati huku wakikosa huduma muhimu za kijamii ikiwemo msaada wa chakula na matibabu. Hii leo Mahakama ya Haki ICJ inasikiliza ombi kutoka taifa la Afrika Kusini ambalo linaiomba mahakama hiyo kuliwekea vikwazo zaidi jeshi la Israel ambalo linafanya mashambulizi ya anga na ardhini huko Ukanda wa Gaza mashambulizi ambayo yamegharibu maelfu ya maisha ya watu.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO hii leo limetoa muhtasari wa ugonjwa wa kipindupindu ulimwenguni ambao mpaka sasa umetajwa kuenea katika mataifa 24 katika kanda tano za shirika hilo huku Afrika ikirekodi idadi kubwa ya wagonjwa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “HIZAYA.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
16-5-2024 • 11 minuten, 26 seconden
Mafunzo ya UNIDO yameboresha bidhaa zetu sasa tunahitaji masoko ya uhakika
Huko Manama mji mkuu wa Bahrain huko Asia ya Magharibi kunafanyika mkutano wa tano wa Jukwaa la Uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024. Zaidi ya washiriki 1000 ni wajasiriamali kutoka Afrika wakisaka kujenga mitandao na ubia ili kusaka masoko ya uhakika ya bidhaa zao na hatimaye kuondokana na umaskini, moja ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa. Mkutano umeandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya Viwanda, UNIDO ofisi ya ugunduzi wa teknolojia, ITPO nchini Bahrain. Assumpta Massoi aliyeko Manama anazungumza na mjasiriamali kutoka Kenya, Edith Lewela, Mwenyekiti wa kundi la wanawake wajasiriamali wa Taita-Taveta na pia mnufaika wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na UNIDO mwaka 2009. Bi. Lewela anaanza kuelezea manufaa ya mafunzo hayo ambayo anapatia pia wenzake.
15-5-2024 • 3 minuten, 54 seconden
Ziara za Catriona Laing za kuwaaga viongozi Somaliland
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing ameendelea na ziara yake ya kuwaaga viongozi wa eneo hilo na sasa ametembelea Somaliland. Juzi Mei 12, Catriona Laing alikuwa Dusmareb, mji mkuu wa jimbo la Galmudug katikati mwa Somalia ambako alipongeza juhudi za kupambana na ukeketaji. Kisha jana Mei 14 akatua Hargeisa mji mkuu wa Somaliland ambako amekutana na uongozi na kujadili msaada wa Umoja wa Mataifa kwa maendeleo na juhudi za kibinadamu. Miongoni mwa aliokutana nao ni Rais Muse Bihi na wajumbe wa baraza lake la mawaziri na washauri."Tumekuwa na mjadala mzuri sana, na Rais amezungumza nami kuhusu mpango wa maendeleo, ambao unaweka maono yake ya muda mrefu ya kiuchumi kuhusu faida za 'uchumi wa buluu,' kuhusu madini, na kufikiria juu ya mabadiliko ya biashara ya mifugo kama tunajiandaa dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kwa watu wenye maisha ya kuhamahama. Tumezungumza kuhusu jukumu la Umoja wa Mataifa katika kuunga mkono kufanikisha dira ya kiuchumi na kazi nyingine zote tunazofanya kuhusu maendeleo ya kijamii, afya, elimu, kibinadamu na katika maeneo mengine.Hali katika eneo la Laascaanood-Sool -ambako migogoro ilipamba moto mwaka jana, na kusababisha kupoteza maisha na maelfu ya watu kuyahama makazi yao pia ilijadiliwa kama anavyoeleza Bi Liang kwamba, "Kumekuwa na changamoto huko nyuma na sote tulifurahi kuona kwamba mambo yametulia, na Rais amenihakikishia kuwa ni lengo lake kwamba mambo yabaki shwari. Umoja wa Mataifa utafanya sehemu yake katika kutoa msaada wa kibinadamu na kutegua mabomu kwa manufaa ya watu katika eneo hilo.”Mwakilishi huyo Maalum wa Umoja wa Mataifa pia alichukua fursa hiyo kumtambulisha rasmi mkuu mpya wa ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Hargeisa, Nikolai Rogosaroff, ambaye alichukua wadhifa wake Machi mwaka huu. Alielezea uwepo wake hapo kama ishara ya kujitolea kwa Umoja wa Mataifa kusaidia maendeleo ya ndani na juhudi za kibinadamu. Hivi sasa, zaidi ya mashirika kumi na mbili ya Umoja wa Mataifa, fedha na program yanafanya kazi Somaliland.Bi. Laing atakamilisha kazi yake baadaye mwezi huu wa Mei.
15-5-2024 • 1 minuut, 50 seconden
15 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko Gaza, na ziara za Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing. Makala tunakupeleka mjini Manama huko Bahrain na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kuonya kuhusu hali mbayá ya Rafah Gaza ambako mashambulizi ya Israel yanaendelea kukatili Maisha ya watu na kulazimisha maelfu kufungasha vitago tena kwenda kusaka usalama. Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Catriona Laing ameendelea na ziara yake ya kuwaaga viongozi wa eneo hilo na sasa ametembelea Somaliland.Makala tunakwenda Manama mji mkuu wa Bahrain huko Asia ya Magharibi kunakofanyika mkutano wa tano wa Jukwaa la Uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 ambapo Assumpta Massoi amezungumza na mjasiriamali kutoka Kenya, Edith Lewela, Mwenyekiti wa kundi la wanawake wajasiriamali wa Taita-Taveta. Yeye ni mnufaika wa mafunzo ya ujasiriamali yaliyotolewa na UNIDO mwaka 2009, sasa anafundisha wenzake.Mashinani tutaelekea katika mitaa ya mabanda ya Nairobi nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani Umoja wa Mataifa unatumia michakato ya kiteknolojia ya kompyuta kutoa msaada wa chakula kwa wakati.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
15-5-2024 • 10 minuten, 43 seconden
UN: Hali Rafah ni mbayá mashambulizi yanakatili maisha na kufurusha watu kwa maelfu
Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kuonya kuhusu hali mbayá ya Rafah Gaza ambako mashambulizi ya Israel yanaendelea kukatili maisha ya watu na kulazimisha maelfu kufungasha vitago tena kwenda kusaka usalama. Kwa mujibu wa tarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA kuendelea kwa mashambulizi ya wanajeshi wa Israel, kwenye Ukanda wa Gaza kwa njia ya angani, ardhini na baharini kunazidisha vifo vya raia, kulazimika wengi kukimbia na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya makazi na miundombinu mingine muhimu ya raia. Shirika hilo limeongeza kuwa na mashambulizi ya ardhini ya Israeli yanaendelea kupanua wigo, haswa katika maeneo ya kusini mwa mji wa Gaza na Mashariki mwa Rafah, hususan karibu na Kerem Shalom na vivuko vya Rafah.Kana kwamba hayo hayatoshi Philippe Lazzarini ambaye ni Kamishina Mkuu wa UNRWA amesema kumekuwa na jaribio lingine la uchomaji moto la watoto na vijana wa Israel kwenye majengo ya UNRWA huko Jerusalem jana usiku. Akiweka video fupi inayoonyesha moto ukiwaka nje ya majengo ya ofisi hizo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X Lazzarini amesema imetosha na mashambulizi hayo lazima yakome.Likimulika zaidi watoto shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema Kuongezeka kwa uhasama huko Rafah na kote katika Ukanda wa Gaza kumeongeza mateso ya mamia ya maelfu ya watoto, ambao wamevumilia jinamizi lisiloisha kwa siku 218 zilizopita.Shirika hilo limerejea wito wake wa kukomeshwa mara moja uhasama ili kuokoa maisha ya raia wasio na hatia wakiwemo malaki ya watoto.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema linaendelea kujitahidi kusambaza msaada wa chakula licha ya changamoto kubwa za kiusalama na miundombinu. Shirika hilo linasema mamia ya familia zinalazimika kushinda njaa ili chakula kidogo kinachopatikana ziweze kulisha watoto wao. Miongoni mwa chakula kinachotolewa ni lishe ambayo iko tayari kuliwa hususan kwa watoto.
15-5-2024 • 1 minuut, 41 seconden
14 MEI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika ugunduzi na ukuaji uchumi. Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO ni sehemu ya wawezeshaji wa jukwaa la WEIF 2024 na mwakilishi wake amezungumza na mwenyeji wetu huko Manama Bahrain Assumpta Massoi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Huko Gaza Wapalestina zaidi waliouawa kutokana na mashambulizi ya kijeshi ya Israel wakiendelea kutambuliwa na mamlaka ya afya ya eneo hilo, wasaidizi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza tena kwamba kwa hakika katika ya watu 35 ambao wameshauawa, idadi kubwa ya wanawake na watoto. Kufuatia tathmini za kina nchini Malawi na Msumbiji, Timu huru ya Tathmini ya Kukabiliana na Mlipuko wa Polio (OBRA) leo Mei 14 imependekeza kufikia ukomo wa mlipuko wa virusi vya polio aina ya 1 (WPV1) nchini Malawi na Msumbiji, kuashiria hatua muhimu katika mapambano dhidi ya polio katika eneo la Afrika. Kisa cha mwisho cha WPV1 katika Kanda ya Afrika, kilichohusishwa na aina hiyo ya polio kiliripotiwa katika Jimbo la Tete la Msumbiji mnamo Agosti 2022. Jumla ya wagonjwa tisa waligunduliwa nchini Msumbiji na nchi jirani ya Malawi, ambapo mlipuko huo ulitangazwa Februari 2022.Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa njia ya video leo amewaeleza viongozi wa kimataifa jijini Paris Ufaransa kwamba “Tunahitaji hatua ya haraka ili kumpa kila mtu, kila mahali ufikiaji wa nishati safi ya kupikia.” Guterres amewasisitiza viongozi hao wanaoshiriki Mkutano kuhusu nishati safi ya kufikia barani Afrika kwamba, “Tunacho kichocheo cha mafanikio: Ramani yetu ya Kimataifa ya Ubadilikaji ulio wa haki na jumuishi kuelekea nishati safi ya kupikia.”Mashinani tutaelekea nchini Somalia kufuatilia ziara za Bi. Catriona Laing, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia za kuwaaga viongozi nchini humo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
14-5-2024 • 11 minuten, 35 seconden
Uwekezaji kwa wajasiriamali duniani kumulikwa Manama, Bahrain
Jukwaa la 5 la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali, WEIF 2024 linaanza kesho kwenye mji mkuu wa Bahrain, Manama ukileta pamoja washiriki zaidi ya 1000, wakiwemo wajasiriamali kutoka pembe zote za dunia. Jukwaa hili linafanyika kwa siku tatu na na maudhui ni kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwa kuendeleza uvumbuzi na ukuaji wa kiuchumi. Jukwaa hili linalenga basi kupatia majawabu changamoto za dunia ikiwemo umaskini, ukosefu wa usawa, mabadiliko ya tabianchi, amani, haki kwa muktadha wa SDGs. Dkt. Hashim Hussein, ni mtaalamu wa kuendeleza uwekezaji katika shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda, UNIDO anaeleza ni nini hasa wanatarajia kutoka jukwaa hili alipopata fursa kuzungumza na Assumpta ambaye tayari yuko Manama kutujuza kitakachojiri.
13-5-2024 • 4 minuten, 28 seconden
Mashirika ya UN yaonya kuwa maelfu ya maisha ya watu El Fasher Sudan yako hatarini
Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini El Fasher Sudan, kufuatia mashambulizi makali yanayoendelea ambapo moja ya hospitali Darfur Kaskazini imeshambuliwa na kukatili maisha ya watu wawili lakini pia kuchochea hofu ya kurejea kwa baa la njaa. Kwa mujibu wa Mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths, “Shambulio hilo limeharibu paa la hospitali katika kituo cha huduma za dharura kwenye Hospitali ya Sourthen katika mji wa El Fasher ambayo ndio hospitali pekee inayofanyakazi kwas asa katika jimbo la Darfur Kaskazini na ambako vifaa vya matibabu na dawa sasa karibu vinakwisha.” Amesema takriban watu 800,000 wanaishi katika mji wa El Fasher na maelfu ya maisha yao yako hatarini huku taifa zima la Sudan likiwa katika hali mbaya.Shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limesema makumi ya raia waliuawa mwishoni mwa wiki katika mapigano mapya makubwa yaliyozuka Ijumaa kati ya vikosi vya serikali ya Sudan SAF na vikosi vya msaada wa haraka RSF katika eneo la Darfur Kaskazini ambalo ndilo lililosalia chini ya udhibiti wa serikali.Shirika hilo linasema hivi sasa karibu watu milioni 25 nchini Sudan wanahitaji msaada wa kibinadamu na watu milioni 17.7 miongoni mwao wanakabiliwa na hali mbaya ya kutokuwa na uhakika wa chakula na kuna hofu kubwa ya kurejea kwa baa la njaa Darfur.Nayo mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la luhudumia wakimbizi UNHCR na la uhamiaji IOM yamesema takriban watu 570,000 wametawanywa katika jimbo la Darfur Kaskazini katika miezi 13 iliyopita, wengine milioni 6.7 nchini Sudan ni wakimbizi wa ndani huku milioni 1.8 wamekimbilia katika nchi za jirani.
13-5-2024 • 1 minuut, 50 seconden
13 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi makali yanayoendelea nchini Sudan, na huduma za afya uzazi Kalobeyei nchini Kenya. Makala inatupeleka Bahrain ambako Jukwaa la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali WEIF 2024 linaanza Manama hapo kesho Jumanne, na mashinani tunasikiliza simulizi ya mkimbizi wa ndani nchini DRC.Mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kwamba maisha ya maelfu ya watu yako hatarini El Fasher Sudan, kufuatia mashambulizi makali yanayoendelea ambapo moja ya hospitali Darfur Kaskazini imeshambuliwa na kukatili maisha ya watu wawili lakini pia kuchochea hofu ya kurejea kwa baa la njaa. Turkana nchini Kenya katika eneo la Kalobeyei ni makazi ya wakimbizi pamoja na jamii za wenyeji na huko Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatuunganisha na mkunga Jane Rose anaeleza namna anavyohakikisha anatoa huduma bora kwa wajawazito na watoto.Makala inatupeleka Bahrain huko Jukwaa la kimataifa la uwekezaji kwa wajasiriamali WEIF 2024 linaanza kesho Jumanne Kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Manama likiwaleta pamoja washirika mbalimbali wakiwemo viongozi katika sekta ya biashara duniani na wajasiriamali. Jukwaa hili linafanyika kwa siku tatu na mwenzetu Assumpta tayari yuko Manama kutujuza kitakachojiri.Na mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kusikia simulizi ya mkimbizi wa ndani.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
13-5-2024 • 11 minuten, 22 seconden
Kalobeyei: Wakunga wafurahia kutoa huduma kwa wajawazito na watoto wachanga
Turkana nchini Kenya katika eneo la Kalobeyei ni makazi ya wakimbizi pamoja na jamii za wenyeji na huko Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatuunganisha na mkunga Jane Rose anaeleza namna anavyohakikisha anatoa huduma bora kwa wajawazito na watoto. Anasema anaitwa Jane Rose Akwam, ni mkunga anayehudumia wajawazito pamoja na watoto wachanga, huduma ambayo inatolewa bure katika katika eneo hili la Kalobeyei. “Katika hospitali hii tunafanya kazi na jamii za wenyeji na wakimbizi, wanapokuja najitambulisha na kuwaeleza kazi yangu katika idara hii na pia nawaelezea kile ninachokuelezea ni kile ambacho hata mimi nilipitia.”Wakati ulimwengu ulisherehekea siku ya wauguzi hapo na siku ya wakina mama hapo jana Mei 12, Rose anaeleza kile kinachompa furaha zaidi katika kazi yake hii ya ukunga.“Ni furaha yangu ninapomuona mjamzito anapokuja kwa ajili ya kujifungua na mwisho wa siku anajifungua mtoto mwenye afya njema. Huduma hapa hutolewa bure ukitoa hata sumni bado itakurudia mwenyewe. Ni kama ninapotoa huduma kwa hawa wakina mama vyema najua zawadi yangu ipo pale.”
13-5-2024 • 1 minuut, 26 seconden
Ally Mwamzola: Vijana tushiriki kuanzia kuandaa hadi kutekeleza ‘Mkataba wa siku zijazo’
Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitamatika leo, miongoni mwa waliohudhuria ni Ally Mwamzola kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA Tanzania). Yeye akiwa anapeperusha bendera ya vijana kwa kuzingatia kuwa pia ni Mratibu wa Mradi wa Ujumbe wa Vijana wa Afrika kwenda Umoja wa Mataifa anayataja mambo matatu ambayo katika mkutano huu vijana walikuwa wanayalenga zaidi. Amezungumza na Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa, UNIS nchini Kenya na anaanza kwa kumweleza waliyowasilisha.
10-5-2024 • 3 minuten, 6 seconden
Peter Njenga: Mchezo wa riadha watumika kukaribisha wageni wa mkutano Kenya
Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.Bwana Njenga akaoanisha michezo na amani.
10-5-2024 • 1 minuut, 24 seconden
10 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) unaofunga pazia leo, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa hotuba yake kwa waandishi wa habari, na tutasikia ujumbe wa washiriki wengine. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa. Siku ya kwanza ya mkutano huo wa Umoja wa Mataifa wa mashirika ya kiraia, UNCSC ilitanguliwa na mbio za kukaribisha wageni kwenye jiji la Nairobi, nchini Kenya ambapo Peter Njenga anayehusika na michezo ya riadha katika Kaunti ya Nairobi anaelezea umuhimu wa mbio hizo walizoandaa kwa ushirikiano na waandaji wa mkutano huo.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia (UNCSC) ukitamatika leo, miongoni mwa waliohudhuria ni Ally Mwamzola kutoka Asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania (UNA Tanzania). Amezungumza na Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha mawasiliano cha Umoja wa Mataifa, UNIS nchini Kenya na anaanza kwa kumweleza waliyowasilisha.Na katika mashinani tunasalia mjini Nairobi katika mkutano wa asasi za kiraia kusikia ujumbe kuhusu janga la mafuriko yanayoendelea nchini Kenya.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
10-5-2024 • 9 minuten, 43 seconden
Guterres: Afrika inaweza kuwa jabalí la nishati jadidifu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Nairobi Kenya kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mashirika yasiyo ya kiserikali, UNCSC amezungumza na waandishi wa habari ambapo pamoja na mambo mengine amesema wakati huu ambapo bara la Afrika linakabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, bara hilo linaweza kuwa jabalí wa uzalishaji nishati jadidifu duniani iwapo litawezeshwa. Katibu Mkuu Guterres [GUTERESH] amesema dunia inakabiliwa na majanga lukuki, lakini Afrika ndio inaathiriwa vibaya kwa kiasi kikubwa.Bara la Afrika linatikiswa na hali mbayá ya hewa kupindukia, ikichochewa na janga la tabianchi ambalo halijasababishwa na bara hili. Kuanzia mafuriko makubwa mashariki hadi ukame mkali kusini.Afrika inaweza kuwa jabali la nishati jadidifu, amesema Guterres, kwani ina hifadhi ya asilimia 30 ya madini muhimu kwa ajili ya nishati jadidifu, na asilimia 60 ya rasilimali ya sola au nishati ya jua. Lakini katika miongo ya karibuni, imepokea asilimia mbili tu ya uwekezaji kwenye nishati jadidifu.Amesema jopo la mpito muhimu wa madini husika kwenye nishati litaanda kanuni za hiari ili nchi zinazoendelea zinufaike na rasilimali hizo.Ametoa wito kwa nchi zilizoendelea kutimiza ahadi zao wa ufadhili wa tabianchi ikiwemo kusaidia nchi kujiandaa kwa madhara makubwa ya tabianchi, na serikali za Afrika ziunge mkono juhudi za kuondokana na mafuta kisukuku.Ametumia pia hotuba yake kupongeza Kenya kwa kukubali kuongoza juhudi za kimataifa za kukabili ghasia nchini Haiti, wakati huu ambapo taifa hilo linakumbana na madhara ya mafuriko yaliyosababisha vifo, ukimbizi na uharibifu wa mali.
10-5-2024 • 9 minuten, 43 seconden
Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuinua uchumi na kusongesha agenda ya SDGs - Zahra Salehe
Mnamo tarehe Mosi Januari mwaka 2016, Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yalianza kufanyiwa kazi rasmi. Tangu wakati huo watu ulimwenguni kote kwa ngazi tofautifauti wamekuwa wakihaha kuhakikisha kufikia mwaka 2030 malengo hayo yanafikiwa. Na kila mara Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani yamekuwa uwanja wa wazi kwa wadau kutoka kila pembe ya dunia kuja katika mikutano mbalimbali na kubadilishana uzoefu. Mfano ni Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ulifanyika hivi karibuni na mmoja wa waliohudhuria ni Zahra Salehe, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji, ICCAO Tanzania ambaye katika mahojiano haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii tunapata kufahamu baadhi ya malengo yanavyotekelezwa na shirika lake nchini Tanzania.
9-5-2024 • 5 minuten, 17 seconden
Jifunze Kiswahili: Tofauti ya “Adili na Idili.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adili na Idili.”
9-5-2024 • 0
09 MEI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika kazi za Zahra Salehe na timu yake ya ICCAO nchini Tanzania katika kusongesha Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kuhusu Gaza na asasi za kiraia Nairobi Kenya, pamoja na uchambuzi wa neno la wiki. Leo mkutano wa Umoja wa Mataifa wa asasi za kiraia umeng’oa nanga mjini Nairobi Kenya ukiwaleta pamoja washiriki takriban 1500 kutoka kila kona ya dunia wakifanya majadiliano ya awali na kutoa takwimu kuelekea mkutano wa wakati ujao utakaofanyika New York Marekani mwezi Sepemba mwaka huu. Umoja wa Mataifa Kenya ndio mwenyeji wa mkutano huo ambapo Mratibu Mkazi wa Umoja huo nchini humo Dkt. Stephen Jackson amesema taifa hilo la Afrika Mashariki limekuwa mstari wa mbele kwenye kusongesha ushirikiano wa kimataifa tangu uhuru wake.Huko Gaza takriban watu 80,000 wamekimbia Rafah tangu Jumatatu wiki hii wakati mashambulizi ya Israel yakishika kasi usiku kucha kuamkia leo ndani na katika viunga vya vya mji huo a Kusini mwa Gaza kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Na kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adili na Idili.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
9-5-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Hatuna uhakika wa kuitimiza SDG5 kwa 100% lakini tunaweza kufikia hata 90% - Abeida Rashid Abdallah
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nchini Tanzania, Abeida Rashid Abdallah hivi karibuni akiwa katika safari ya kikazi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kushiriki vikao vya mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 anajibu swali aliloulizwa na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kwamba Je, Lengo namba 5 la Maendeleo Endelevu linalohamasisha usawa wa kijinsia litafikiwa huko Zanzibar kufikia mwaka 2030?
8-5-2024 • 3 minuten, 28 seconden
Mafuriko katika Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki yaathiri watu 637,000
Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao. Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limetoa takwimu hizo likinukuu ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, huku ikisema kuwa idadi inazidi kuongezeka kila uchao.IOM kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Geneva, Uswisi na Nairobi, Kenya inasema mvua hizo za masika zimesababisha mafuriko makubwa, maporomoko ya udongo na kuharibu miundombinu muihmu kama vile barabara, madaraja na mabwawa ya maji.Mkurugenzi wa IOM Kanda ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika Rana Jaber anasema mafuriko hayo ya kipekee na yaliyosababisha uharibifu yameibua ukweli mchungu wa mabadiliko ya tabianchi, kwa kusababisha vifo na kufurusha watu makwao, watu ambao sasa wanakabiliwa na kazi kubwa ya kujijenga upya huku hali zao zikizidi kuwa taabani.Ni kwa mantiki hiyo anaesema katika nyakati hizi muhimu, wito wa IOM unasalia kuchukuliwa kwa hatua endelevu na za dharura za kutatua ukimbizi wa binadamu unaochochewa na mabadiliko ya tabianchi.Pamoja na kushirikiana na serikali na wadau kusambaza misaada ya hali na mali ya kuokoa maisha ikiwemo fedha taslimu kwa walioathiriwa huko Burundi, Kenya, Somalia, Ethiopia na Tanzania, IOM inasema mjadala ujao huko Ujerumani kuhusu Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya tabianchi, UNFCCC ni dhahiri shairi kuwa mazungumzo kuhusu tabianchi lazima yazingatie ukimbizi utokanao na janga hilo.Afrika inaathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi licha ya kuchangia asilimia 4 pekee ya hewa chafuzi duniani.
8-5-2024 • 1 minuut, 54 seconden
08 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, na wakimbizi wanaorejea nchini Sudan Kusini kutoka Sudan. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini DRC, kulikoni?Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini Sudan kusini kwa kushirikiana na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wanafanya kazi usiku na mchana kusaidia wakimbizi walioko Sudan wanaotaka kurejea nyumbani nchini Sudan Kusini na kuwaunganisha tena na familia zao.Katika makala Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nchini Tanzania, Abeida Rashid Abdallah hivi karibuni akiwa katika safari ya kikazi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kushiriki vikao vya mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, alipata nafasi kuzungungumza na Anold Kayanda.Na mashinani inatupeleka katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri wa Kidemkrasia ya Congo DRC, ambako mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa siku kadhaa sasa zimesababisha maafa, ikiwemo maelfu ya familia kuathirika. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
8-5-2024 • 10 minuten, 38 seconden
Wahamiaji waliorejeshwa Sudan Kusini kutoka Sudan wanasema asante IOM
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini Sudan kusini kwa kushirikiana na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wanafanya kazi usiku na mchana kusaidia wakimbizi walioko Sudan wanaotaka kurejea nyumbani nchini Sudan Kusini na kuwaunganisha tena na familia zao. Waswahili husema “Mkataa kwao mtumwa” na hili ndio hasa alilowaza Bi. Lydia John Wol Mabior ambaye alikuwa ukimbizini nchini Sudan lakini huko nako vita ilipoanza akakumbuka usemi “Nyumbani ni nyumbani hata kama vichakani” kwani ilikuwa si hali. Anasema, “Nilipokuwa Khartoum sikulala usiku wala mchana, niliona ni bora nije kuteseka Sudan Kusini. Na leo nina furaha sana kwasababu nimefika nchini kwangu”Lidya ya familia yake miaka kadhaa iliyopita aliikimbia nchini yake ya Sudan Kusini pale vita vilipozuka. Na shukran ziliendee shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM ambalo limefanikisha kumrejesha nchini mwake.“Niliambiwa kuna shirikia lakutusaidia kufika Sudan Kusini, na tangu tumefika hapa eneo la Renk, tumepewa msaada wa kifedha tunamshukuru Mungu. Baada ya kusafiri kwa boti kutokea Malakal tulipewa msaada na IOM na sasa tunachotaka ni kusaidiwa Kwenda nyumbani kwetu huko Wau kwa msaada wa IOM.”Lydia ametoa shukran zake za dhati kwa shirika la IOM na wadau wake kwa msaada wote waliowapatia katika kusaidia kuwaunganisha tena na familia zao.
8-5-2024 • 1 minuut, 32 seconden
07 MEI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya ambako Umoja wa mataifa uko mstari wa mbele kuwapa msaada wakenya wanaotatizika kutokana na mafuriko. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kuhusu Gaza, Uhamiaji na misitu. Mashinani inatupeleka nchi Haiti, kulikoni? Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerejea kusisitiza wito wake wa kusitishwa mapigano, kuachiliwa kwa mateka wote na kuepusha zahma kubwa ya kibinadamu kwa watu wa Gaza. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani amesema “Tuko katika wakati maamuzi kwa ajili ya watu wa Palestina na Israeli na kwa hatima ya Ukanda mzima.Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM leo limezindua Ripoti ya Dunia ya Uhamiaji 2024, ambayo inaonyesha mabadiliko makubwa katika mifumo ya uhamiaji duniani, ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao na pia ongezeko la fedha zinazotumwa kimataifa. Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope amezindua rasmi ripoti hiyo nchini Bangladesh, nchi ambayo iko mstari wa mbele katika changamoto za uhamiaji na kusema "Ripoti ya Uhamiaji Duniani ya 2024 inasaidia kuondoa utata wa uhamaji wa binadamu kupitia takwimu na uchambuzi unaozingatia ushahidi." Kati ya mwaka 2,000 na 2022 ongezeko la utumaji fedha nyumbani kimataifa kwa mujibu wa Ripoti lilikuwa ni zaidi ya asilimia 650 na kufikia dola bilioni 831 bilioni.Na jukwaa la Umoja wa Mataifa kuhusu misitu kikao cha 19 kinaendelea hapa kwenye makao makuu wa Umoja wa Mayita New York Marekani kikimulika mada mbalimbali ikiwemo jukumu la sheria katika afya ya misitu. Akizungumzia hilo Patricia Kameri-Mbote mkurugenzi wa idara ya sheria katika shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP amesema “Misitiu ni muhimu sana katika kushughulikia majanga matatu makubwa yanayoikabili Dunia ambayo ni uchafuzi wa hewa, opotevu wa bayoanuwai na mabadiliko ya tabianchi.” Na kwamba afya ya misitu ni nguzo ya kuhakikisha afya ya sayari dunia na kwa mantiki hivyo sheria za kulindwa kwa misitu zina wajibu muhimu sana na sio chaguo bali ni lazima.Na mashinani huku kukiwa na ghasia zinazoendelea nchini Haiti, Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limepanua kwa haraka msaada wake wa chakula, na kufikia zaidi ya watu nusu milioni tangu kuanza kwa mzozo, ikiwa ni pamoja na watoto wa shule, Evenie Joseph, mama mjasiriamali anasema mpango wa mlo shuleni umeleta manufaa kwa watoto wanaokimbia ghasia hizo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
7-5-2024 • 12 minuten, 13 seconden
UNHCR inawasaidia wakimbizi dhidi ya mafuriko Afrika Mashariki
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linapambana kuhakikisha linawasaidia wakimbizi katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Afrika Mashariki dhidi ya madhila yanayosababishwa na mafuriko makubwa kutoka na mvua za El Niño zinazoendelea. Makala hii ambayo video zake zimekusanywa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR inaanzia Bujumbura Burundi kisha inakupeleka Kenya katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab, kama inavyosimuliwa na Evarist Mapesa.
6-5-2024 • 3 minuten, 13 seconden
UNICEF: Watoto walioko Rafah wasihamishwe kwani tayari wako taabani
Janga la kibinadamu likizidi kushamiri kila uchao huko Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaonya kuwa kuzingirwa kijeshi kwa eneo hilo sambamba na operesheni za ardhini za kijeshi huko Rafah kutasababisha janga kubwa kwa watoto 600,000 waliosaka hifadhi kwenye eneo hilo. Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini New York, Marekani inakumbusha kuwa amri ya kuhamia Rafah, kusini mwa Gaza iliyotolewa mwezi Oktoba mwaka jana na Israel imefanya eneo hilo sasa kuhifadhi watu wapatao milioi 1.2, nusu yao wakiwa ni watoto wakiishi kwenye mahema au nyumba zisizo kamilifu.Kwa kuzingatia mlundikano wa watoto, wakiwemo wengi walio hatarini wakihaha kuishi, pamoja na ukubwa wa ghasia zinazoendelea na njia za kutumia kukimbia zikiwa na vilipuzi au hakuna njia kabisa , UNICEF inaonya madhila zaidi kwa watoto na operesheni za kijeshi vitaongeza vifo zaidi vya raia na miundombinu ya huduma za msingi iliyosalia kusambaratishwa.Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell amesema zaidi ya siku 200 za vita zimekuwa ‘mwiba’ kwa watoto na Rafah hivi sasa ni mji wa watoto wasio na pahala salama pa kukimbilia Gaza. Iwapo operesheni kubwa za kijeshi zikianza, watoto sio tu watakuwa hatarini na ghasia, bali pia vurugu na kiwewe wakati ambapo hali zao kimwili na kiakili zimeshadhoofishwa.Hivyo UNICEF inasisitiza wito wa Kamati ya Mashirika ya UN kwa Israel ya kuzingatia wajibu wake kwa mujibu wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu na haki za binadamu ya kupatia chakula na matibabu watoto na kuwezesha operesheni za kugawa misaada na kwa viongozi wa dunia kuzuia janga zaidi kwa watoto Gaza sambamba na sitisho la mapigano.
6-5-2024 • 1 minuut, 39 seconden
06 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama huko Rafah kusini mwa ukanda wa Gaza, na mafuriko nchini Kenya huku mashirika wakihaha kusaidia waathirika. Makala tunasalia na mada hiyo ya mafuriko Afrika mashariki na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni? Janga la kibinadamu likizidi kushamiri kila uchao huko Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaonya kuwa kuzingirwa kijeshi kwa eneo hilo sambamba na operesheni za ardhini za kijeshi huko Rafah kutasababisha janga kubwa kwa watoto 600,000 waliosaka hifadhi kwenye eneo hilo..Wingu kubwa la mvua likiwa limetanda kwenye mji wa Garsen, ulioko kaunti ya Mto Tana nchini Kenya, Eva Ghamaharo, mama wa watoto watatu anarejea nyumbani akitembea na watoto wake wawili mapacha wenye umri wa miaka mitatu baada ya kununua matumizi ya nyumbani kutoka kioski cha jirani. Watoto hawa wawili mapacha wa kike ni Grace na Jane na wanaonekana na furaha kwani angalau leo mama yao ameweza kuwanunulia kila mmoja pakiti ya maziwa na wanakunywa kwa furaha..Makala inaangazia madhila ya mafuriko kwa wakimbizi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katuka ukanda wa Afrika Mashariki.Na mashinani tutaelekea Darfur nchini Sudan kusikia ni kwa jinsi gani Umoja wa Mataifa umerejesha matumaini kwa waathirika wa vita.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
6-5-2024 • 9 minuten, 59 seconden
Mafuriko Kenya: UNICEF yapatia wakazi wa Kaunti ya Mto Tana fedha za kujikimu
Mvua za El-nino zikiendelea kutikisa ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo taifa la Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo kwa ufadhili wa serikali ya Uingereza limepatia msaada wa hali na mali wakazi wa kaunti ya mto Tana walioathiriwa na mafuriko hayo. Cecily Kariuki na taarifa zaidi.Video ya UNICEF Kenya inaanza ikimuonesha mkazi huyu wa hapa mji wa Garseni katika kaunti ya mto Tana akiwa amebeba kikapu huku akiwa na watoto wake wawili wakirejea nyumbani.Huyu si mwingine bali Eva Ghahamaro akisimulia yaliyowasibu na msaada ulivyowafikia. Anasema, “Maisha yalikuwa magumu kwa sababu mafuriko yaliharibu nyumba na mashamba. Vyakula vilisombwa. Watu wengi waliteseka sana. Maafisa wa kaunti waliona tunateseka, walitembea nyumba kwa nyumba wakisajili majina watu wenye watoto na wajauzito. Nilikuwa nikipata shilingi 2,750.”Shilingi 2750 ni sawa na dola 20 za kimarekani, na wanapatiwa kila mwezi. Rachael Wamoto ni afisa kutoka UNICEF Kenya na anafafanua kuhusu usaidizi huo ambao haukulenga tu waathiriwa wa mafuriko bali pia kaya zenye watoto walio na utapiamlo.“Kwa programu hii tuko katika kaunti sita. Kwa kaunti ya Mto Tana tumeweza kufikia kaya 1,800 (Elfu Moja Mia Nane) katika miji ya Galole na Garsen. Vikundi kazi vya Kaunti ndio vilihusika kwenye kuchagua kaya zenye uhitaji. Hivyo tuliweza kutambua watu walioathiriwa na mafuriko na waliokimbia makwao. Tunashirikiana na serikali na mamlaka ya taifa ya udhibiti wa ukame. Tuliweza kutumia orodha yao na hivyo kufikia haraka wahitaji.”Msaada wa fedha taslimu uliofadhiliwa na serikali ya Uingereza, umekuwa na manufaa kwa Eva. Akisema twins, anamaanisha watoto mapacha.“Nilitumia hizo fedha kununulia wanangu chakula, uji, mkaa na pia mahindi na mchele kwa familia yangu. Halikadhalika, watoto wangu hawa mapacha niliwaandikisha shule nikawanunulia sare na mabegi ya shule. Nimeshukuru sana UNICEF kwa msaada wao kwa sababu mmetusaidia.
6-5-2024 • 2 minuten, 6 seconden
Wanahabari waweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira
Leo ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira.
3-5-2024 • 3 minuten, 13 seconden
Umoja wa Mataifa umeanza kufikisha misaada kwa wakimbizi ili kujiandaa na mafuriko
Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi.Katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Matal Amin iliyoko Baidoa nchini Somalia zaidi ya wananchi 1500 wanahaha huku na kule kurekebisha maturubai yao ambayo hasa ndio makazi yao ikiwa ni maandalizi ya mvua kubwa zinazotarajiwa kuanza muda wowote. Hali ni hivyo hivyo pia katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Rama cade kama anavyotueleza Kiongozi wa kambi hiyo Abdulkadir Adinur Aden anasema “Tunajiandaa na msimu wa mvua ili kupunguza athari za mafuriko, tunatumia maturubai ya plastiki kufunika makazi yetu na pia tunatumia viroba vilivyojazwa michanga ili kuzuia mnomonyoko mafuriko yatakapo tukumba.”Wadau mbalimbali wa misaada ya kibinadamu ikiwemo OCHA wamepeleka katika kambi hizo misaada kama vile chakula na lishe, viroba vilivyojazwa michanga, maji safi na salama pamoja na dawa mbalimbali ikiwemo za kipindupindu hata hivyo mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa OCHA nchini Somalia Erich Ogoso anasema mengi ya makazi hayataweza kuhimili mvua kubwa na hivyo yataharibiwa.“Wananchi wanaoishi katika kambi hii ya Matal Amin walifika hapa mwaka 2017 wakitokea katika mkoa wa Bay ambako walikimbia ukame, mzozo, na mambo mengine. Wamekuwa wakiishi hapa tangu kipindi hicho, mafuriko yanapokuja wamekuwa wakiondoka eneo hili na kukikauka wanarejea na sasa wanajiandaa tena na mafuriko na kuna uwezekano wakutakiwa kuondoka eneo hili.” OCHA wanasema taarifa walizopokea kutoka kwa wadau wao walioko mashinani mpaka kufikia tarehe 28 mwezi Aprili mwaka huu, mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Somalia zimewaathiri zaidi ya watu 124,155 na kuwaacha zaidi ya 5,130 bila makazi huku vifo vya watoto saba vikiripotiwa.
3-5-2024 • 2 minuten, 17 seconden
03 MEI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira. Pia tunakupeleka nchini Somalia na Jamhuri ya Kidemcrasia ya Congo, kulikoni? Hii leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari maudhui yakiwa Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kwa kushirikiana na shirikisho la waandishi wa habari duniani, IFJ wametoa ripoti yao ikionesha kuwa ni katika kipindi cha miaka 15 iliyopita waandishi wa habari 44 waliuawa wakiwa wanachunguza masuala ya mazingira. Kampeni ya siku hii ni kwamba kila habari kuhusu mazingira lazima isimuliwe hivyo waandishi wa habari walindwe.Tukiwa katika msimu wa mvua kwa nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, tuelekee nchini Somalia, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura, OCHA limesema wao na wadau wao wamejiandaa kufikisha mahitaji kwa watu 770,000 katika wilaya 22 za nchi hiyo ambao wanatarajiwa kuathirika na mvua za msimu huku wakieleza kuwa wakimbizi wa ndani wanatarajiwa kuaahirika ziadi.Katika makala tukisalia na siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa ni Uandishi wa Habari wakati huu wa janga la mazingira, namkaribisha Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akimulika sakata la vifo vya waandishi wa habari wanaoweka maisha yao rehani kuripoti masuala ya mazingira.Na mashinani tutaeleke nchini Jamhuri ya Kidemcrasia ya Congo kufuatili jinsi ambavyo mashirika wanavyohaha kusaidia waathirika wa miozo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu
3-5-2024 • 11 minuten, 11 seconden
UN: Wanahabari wana jukumu muhimu la kuelimisha juu ya mabadiliko ya tabianchi
Leo ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani mwaka huu ikibeba maudhui “Vyombo vya Habari kwa ajili ya Sayari: Uandishi wa habari katika kukabiliana na mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi” kwani Umoja wa Mataifa unasema mchango wa wanahabari na vyombo vya habari ni kiini katika kuhabarisha na kuelimisha umma kuhusu changamoto hiyo ya tabianchi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akisistiza kuhusu maudhui ya maadhimisho ya mwaka huu katika ujumbe wake amesema dunia hivi sasa inapitia dhadhura ya mazingira ambayo haijawahi kushuhudiwa na inatishia kizazi hiki na vijavyo hivyo watu wanahitaji kujua kuhusu janga hili akiongeza kuwa “Waandishi wa habari na wafanyakzi wa vyombo vya habari wana jukumu muhimu la kuwahabarisha na kuwaelimisha. Vyombo vya habari vya kijamii, kitaifa na kimataifa vinaweza kutangaza habari kuhusu janga la mabadiliko ya tabianchi, kupotza kwa bayoanuwai na haki ya mazingira.”Zaidi ya hapo amesema wanatoa ushahidi kuhusu uharibifu wa mazingira ambao unaweza kusaidia kuwawajibisha wahusika na ndio maana haishangazi kwamba baadhi ya watu wenye nguvu, makampuni na taasisi wanafanya kila wawezalo kuwazuia waandishi wa habari za mazingira kufanya kazi yao.Guterres ameonya kwamba hivi sasa “Uhuru wa vyombo vya habari umebinywa. Na uandishi wa habari za mazingira ni taaluma inayozidi kuwa hatari. Makumi ya waandishi wa habari wanaoripoti uchimbaji haramu wa madini, ukataji miti, ujangili na masuala mengine ya mazingira wameuawa katika miongo ya hivi karibuni nakatika idadi kubwa ya kesi zao, hakuna mtu ambaye amewajibishwa.”Akiunga mkono kauli hiyo mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO Audrey Azoulay amesema “Wakati ubinadamu unakabiliana na hatari hii iliyopo, lazima tukumbuke, katika Siku hii ya Dunia, kwamba changamoto ya mabadiliko ya tabianchi pia ni changamoto ya uandishi wa habari na wanahabari. Hakuna hatua madhubuti ya hali ya hewa inayowezekana kufikiwa bila fursa huru ya kupata habari za kisayansi na za kuaminika. Ndiyo maana maudhui ya mwaka huu yanaangazia uhusiano muhimu kati ya kulinda uhuru wa kujieleza ambayo ni manufaa ya umma duniani na kulinda sayari yetu.”Kwa mujibu wa ripoti ya UNESCO ya hivi karibuni kabisa katika miaka 15 iliyopita kumekuwa na mashambulizi 750 dhidi ya wanahabari na vyombo vya habari vinavyoripoti masuala ya mazingira na mashambulizi hayo yanaongezeka.Na zaidi ya hayo “Asilimia 70 ya waandishi wa habari za mazingira wamekuwa waathiriwa wa mashambulizi, vitisho au shinikizo kwa sababu ya kazi yao, na waandishi wa habari za mazingira 44 wameuawa katika miaka hiyo 15 iliyopita. Hivyo Bi. Azoulay amesisitiza kuwa “Upatikanaji wa habari za kuaminika ni muhimu zaidi katika mwaka huu wa chaguzi kuu ambapo wananchi wapatao bilioni 2.6 kutoka mataifa mbalimbali wanatarajiwa kushiriki haki yao ya msingi ya kupiga kura.”Hivyo Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba “Bila ukweli, hatuwezi kupigana na habari potofu na za uongo. Bila uwajibikaji, hatutakuwa na sera madhubuti na bila uhuru wa vyombo vya habari, hatutakuwa na uhuru wowote hivyo uhuru wa vyombo vya habari sio chaguo, bali ni lazima.”Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu ametoa wito kwa serikali, sekta binafsi na mashirika ya kiraia kuungana na Umoja wa Mataifa katika kuthibitisha dhamira ya kulinda uhuru wa vyombo vya habari na haki za wanahabari na wanataaluma wa vyombo vya habari duniani kote.
3-5-2024 • 2 minuten, 23 seconden
Jifunze Kiswahili: Totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno "ELEKEZA NA ELEZA."
2-5-2024 • 0
02 MEI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uhuru wa vyombo vya habari ikijikita kwenye umuhimu wa uandishi wa habari na uhuru wa kujieleza katika muktadha wa kukabiliana na janga la tabianchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno la wiki.Nchini Kenya mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha yameathiri maelfu ya watu yakisababisha vifo na kuwaacha wengi bila makazi. Umoja wa Mataifa unaendelea kushirikiana na serikali na wadau kuwasaidia waathirikaRipoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na Tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kiuchumi na kijamii kwa nchi za Asia Magharibi ESCWA inasema vita inayoendelea Gaza imesababisha athari mbaya za kiuchumi na maendeleo ya binadamu katika eneo zima la Palestina.Niger mwaka huu inakabiliwa na ongezeko la asilimia 50 la wagonjwa wa uti wa mgongo au meningitis ikilinganishwa na mwaka jana, limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Katika taarifa yake iliyotolea leo mjini Namey WHO inasema katika wiki ya 16 ya mwaka huu jumla ya wagonjwa 2012 wameripotiwa na vifo 123 na ongezeko hili na wagonjwa na vifo linatia wasiwasi mkubwa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua totauti ya matumizi ya maneno ELEKEZA NA ELEZA!Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
2-5-2024 • 11 minuten, 16 seconden
Mabadiliko ya tabianchi yamefanya urembo wa Kimaasai Kenya kuwa mbadala wa kujikimu kimaisha: Samante Anne
Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa jamii nyingi yakizilazimu kubadili mfumo wao wa Maisha ili kukabiliana na athari zake kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Miongoni mwa jamii zilizoathirika na janga hilo ni za watu wa asili wakiwemo Wamaasai kutoka Kenya na hususan wanawake. Je wanahimili vipi athari hizo? Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wanawake wa jamii hizo za Wamaasai aliyekuwa New York hivi karibuni kushiriki jukwaa la watu wa jamii za asili Bi. Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO).
1-5-2024 • 2 minuten, 49 seconden
UN: Wananchi wa Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano
Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP ambapo kupitia mkurugenzi wake wa eneo linalokaliwa la Palestina Matthew Hollingworth, limesema "Theluthi moja ya familia zote zinazoishi hapa zina watoto wa umri wa chini ya miaka mitano, hao ni watoto wengi sana” Akizungumza kutoka shule ya Deir Al Balah, inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA amesema watoto hawa wana mahitaji mengi “Wanachohitaji ni shule, maji safi na salama, utulivu zaidi, na pia wanahitaji kurejea kwa maisha ya kawaida, "Likiunga mkono wasiwasi huo shirika la UNRWA limegusia mashambulizi yanayoendelea likisema“kumekuwa na zaidi ya mashambulizi 360 kwenye vituo vyake tangu kuanza kwa vita. Mbali na makumi ya maelfu ya waathiriwa, miundombinu muhimu imeathiriwa pia, pamoja na kisima cha maji cha shirika hilo kilichoko katika jiji la Khan Younis.”Na ili kukarabati chanzo hicho cha maji UNRWA inasema kunahitajika kuondoa tani za uchafu ikiwemo vilipuzi na vifaa vingie vya mabaki ya virta kama vilivyobainiwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya msaada wa kutegua mabomu UNMAS nav yote vinahitaji kuondolewa kwa usalama kipande kwa kipande,."Na wizara ya afya ya Gaza imeonya kwamba endapo hakutopatikana usitishwaji mapigano basi Maisha ya watu yataendelea kukatiliwa zaidi na hali itakuwa janga kubwa la kibinadamu kwani hadi sasa takriban watu 34,568 wameuawa na 77,765 wamejeruhiwa tangu Oktoba 7 mwaka jana.
1-5-2024 • 1 minuut, 57 seconden
01 MEI 2024
Hii leo jaridani inaangazia hali ya kibinadamu Rafah ambapo wakimbizi wa ndani Gaza wako katika jakamoyo wakisubiri taarifa kuhusu wito wa kusitisha mapigano. Pia inamulika udhibiti wa taka za plastiki kambini Kakuma. Makala inaangazia jamii ya watu wa asili na mashinani inatupeleka nchini DRC, kulikoni?Wakati kukiwa na ongezeko la wito wa kimataifa kwa Israel kujizuia na mashambulizi zaidi Gaza na ripoti za leo za mashambulizi mengine mabaya zaidi ya usiku kucha, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuhusu athari mbaya zinazoendelea za vita hiyo na haja ya kuhakikisha njia za kuaminika za usambazaji wa misaada kwa watu wanaohitaji kwa udi na uvumba zinapatikana.Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaskazini magharibi mwa Kenya, ambapo mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amegeuza taka ngumu kuwa lulu na hivyo sio tu kuweka usafi kwenye makazi ya kambini, bali pia kuinua kipato chake na cha jamii inayomzunguka.Makala inaangazia changamoto za mabadiliko ya tabianchi zilizowalazimisha wanawake wa jamii ya Kimaasai nchini Kenya kutafuta njia mbadala ya kukabiliana na athari hizo ili kujikimu kimaisha.Na katika mashinani inayotupeleka katika kambi ya wakimbizi wa ndani huko Goma Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambapo vurugu za kutumia silaha zinaendelea kusababisha raia kupoteza maisha yao. Katika video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi DRC, wanawake wanaomba amani irejee.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
1-5-2024 • 9 minuten, 59 seconden
UNHCR: Taka ngumu Kakuma zageuka lulu, wakimbizi vipato vyaongezeka
Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko kaskazini magharibi mwa Kenya, mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amegeuza taka ngumu kuwa lulu na hivyo sio tu kuweka usafi kwenye makazi ya kambini, bali pia kuinua kipato chake na cha jamii inayomzunguka.Ninapoona plastiki naona fursa za ajira! Ni kauli hiyo ya Raphael Bassemi, mkimbizi kutoka DRC akiwa hapa kambini Kakuma akizungumza huku wanawake na wanaume waliovalia maovaroli na glovu na barakoa wakiokota taka. Anasema anafurahi anapoona jamii inashiriki na zaidi ya yote wanawake wasiokuwa na ajira sasa wameajiriwa, "Nilipoanza nilijikita tu kwenye plastiki, lakini ilibainika kuwa kuna takangumu nyingi za kudhibitiwa. Sasa ninajishughulisha na aina zote za taka.”Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linaonesha taka mbalimbali zikiwemo mifupa ya mafuvu ya ng’ombe, vyuma, seng’eng’e na kadhalika. Sasa amesharejeleza tani zipatazo 100 za takangumu."Tunatengeneza rula kwa ajili ya wanafunzi, vibanio vya kuanikia nguo, sahani za kulia chakula na vikombe vya chai na kahawa. »Raphael na wenzake wakiwa kwenye kiwanda hiki alichoanzisha wanapata ugeni ukiongozwa na Dominique Hyde kutoka UNCHR. Baada ya ziara, Bi. Hyde anasema, "Kilichotuvutia ni jinsi wanaweka mawazo yao kwenye hii biashara ili istawi, na pia kushirikisha jamii ipate ajira na hatimaye kipato walipie elimu na umeme. Kama sisi sote tunahitaji kazi, wao wanahitaji kazi, na wao wameanzisha hii ajira wenyewe. »Sasa Raphael anasema jamii ina furaha naye ana furaha na zaidi ya yote."Ninapoona wanawake ninaofanya nao kazi wana furaha, nami nina furaha na ninatamani kuchukua hatua zaidi."
1-5-2024 • 1 minuut, 42 seconden
Mama akivaa kofia yake tunaweza kurejesha amani kuanzia katika familia hadi kimataifa: Adam Ole Mareka
Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII limekunja jamvi mwishoni mwa wiki hapa Umoja wa Mataifa baada ya wiki mbiliza kujadili masuala mbalimbali ikiwemo mchango wa jamii hizo katika kudumisha amani Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania alikuwa miongoni mwa washiriki ambao walikuja katika jukwaaa hilo na azimio maalum linalohimiza mama kuvaa kofia yake ili kusaidia kutatua migogoro kuanzia ngazi ya familia, jamii hadi kimataifa. Amezungumza na Flora Nducha wa idhaa hii ya Kiswahili akianza kwa kufafanua kuhusu azimio hilo
30-4-2024 • 8 minuten, 38 seconden
30 APRIL 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, Adam Kulet Ole Mwarabu Ole Mareka kutoka jamii ya Wamaasai wa Parakuyo iliyoko mjini Morogoro nchini Tanzania anazungumza na Flora Nducha. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Kamishina Mkuu wa sririka la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA leo amesema watu waliokamatwa wakati wa vita inayoendelea Gaza wamenyanyaswa, kuteswa na kufanyiwa vitendo visivyo vya kibinadamu. Katika taarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi Phippe Lazzarini amesema “Watu tuliozungumza nao wametueleza kwamba walipokamatwa kila mara walikuwa wakikusanywa Pamoja, kuvuliwa nguo na kubaki na chupi na kisha kupakiwa katika malori. Watu hawa wametendewa vitendo vya kikatili visivyo vya kibinadamu ikiwemo kuzamishwa kwenye maji na kuumwa na mbwa.”Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ndio nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu duniani kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada wa kibinadamu na masuala ya dharura OCHA. Katika ukurasa wake wa X hii leo shirika hilo limesema jimboni Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini pekee watu milioni 5.4 hawana uhakika wa chakula, milioni n6.4 ni wakim bizi wa ndani na wagonjwa wa kipindupindu kwa mwaka huu pekee wamefikia 8,200. OCHA imeongeza kuwa sasa dola bilioni 1.48 zinahitajika ili kutoa msaada wa kuokoa Maisha kwa watu zaidi ya milioni 4. Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk amesema anatatizwa na mlolongo wa hatua nzito zinazochukuliwa kutawanya na kusambaratisha maandamano katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani.Kupitia tarifa yake iliyotolewa leo mjini Geneva Bwana Türk amesisitiza kuwa "Uhuru wa kujieleza na haki ya kukusanyika kwa amani ni jambo la msingi kwa jamii hasa wakati kuna kutokubaliana vikali juu ya masuala makubwa, kama vile ilivyo sasa ikihusiana na mzozo unaoendelea katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel,"Na katika mashinani shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linashirikisha wadau mbalimbali katika harakati za kutunza mazingira kupitia upandaji miti na kupitia video iliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus FM nampisha mwanaharakati wa mazingira ambaye alitembelea eneo Bunge la Ngong katika kaunti ya Kajiado jijini Nairobi ili kushirikiana na wanafunzi katika kutimiza wito wa UNEP wa upanzi wa miti.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
30-4-2024 • 12 minuten, 36 seconden
Wanawake Tanzania wainua wanawake wenzao katika ujasiriamali kupitia mradi wa CookFund
Nchini Tanzania mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.
29-4-2024 • 3 minuten, 37 seconden
29 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mzozo na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na msaada wa kibinadamu nchini Ethiopia. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Somalia, kulikoni? Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia pia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni.Nchini Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi. Makala inakwenda nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.Mashinani ikiwa ni wiki ya chanjo, kniniki tembezi inayofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imekuwa uti wa mgongo wa mfumo wa afya nchini Somalia na tunakutana na Jamila Moham, Mhudumu wa afya ya jamii katika kijiji cha Dhusamareeb.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
29-4-2024 • 11 minuten, 8 seconden
UNRWA: Watoto 17,000 wametenganishwa na wazazi au familia zao Gaza
Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni. Kwa mujibu wa tarifa fupi ya UNRWA iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa X, shirika hilo linasema maisha ya watoto Gaza yamekuwa jinamizi na takriban 17,000 wako peke yao hawana wazazi au walezi ama wametenganishwa na familia zao.Pia imesema watoto hao wahaudhurii masomo kutokana na vita inayoendelea kwani zaidi ya asilimia 70 ya nyumba zimesambaratishwa au kubomolewa na watoto wengi wamepoteza nyumba zao.UNRWA imeongeza kuwa shule sasa zimelazimika kuwa mkazi ya manusura wa vita hivyo na sio mahala pa elimu tena na kufanya mustakbali wa watoto hao kuwa njiapanda na unahitaji kulindwa.Kutokana na hali mbayá ya hewa na ongezeko la joto UNRWA inasema watu wengi wanhaha hata kupata mahitaji muhimu kama maji ya kunywa ambapo wakimbizi wa ndani wanapokea chini ya lita moja ya maji kwa mtu kwa ajili ya kunywa, kufua na kuonga ikiwa ni tofauto kubwa na lita 151 ambacho ni kiwango cha chini wanachostahili kupata.Na jana Jumapili UNRWA na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya msaada w uteguzi wa mabomu UNMAS walianza operesheni muhimu ya kutathimini uharibifu katika vituo vya UNRWA kuweka alama kwa makombora yoyote na vifaa vyovyote ambavyo hvijalipuka.Mitambo 165 ya UNRWA huko Ukanda wa Gaza imeathiriwa wakati wa vita hii inayoendelea. Na UNMAS inasema ili kuifanya Gaza kuwa salama dhidi ya vifaa vya milipuko ambayo haijalipuka inaweza kuchukua miaka 14.
29-4-2024 • 1 minuut, 59 seconden
Wananchi nchini Ethiopia wapongeza mfumo mpya wa kutambua wenye uhitaji
Nchini Ethiopia Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi Ethiopia ni moja ya nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za mizozo mingi inayoingiliana kama vile ukame, mafuriko pamoja na mizozo. Ili kukabiliana na mahitaji yanayokua WFP na wadau wake wameamua kuanzisha mfumo mpya wa kutambua familia zenye uhitaji zaidi miongoni mwa wanajamii. Mbinu hii inayoendeshwa na wana jumuiya wenyewe inaweka kiwango kipya cha usaidizi wa kibinadamu nchini humo, kama anavyoeleza Mola Suleiman ambaye ni Mshiriki wa Msaada wa WFP anasema, "Wanaotambua wenye uhitaji zaidi sio viongozi, bali watu wasioegemea upande wowote waliochaguliwa na jamii. Tunaweza kwenda kwenye madawati ya usaidizi yaliyoanzishwa huko wilayani Kebeles na viunga vyake na kupeleka malalamiko yetu. Kwa kufuata utaratibu wa uwazi, tunakagua na kuthibitisha wale waliochaguliwa na jumuiya pana, kwakweli huu mfumo ni bora kuliko ule wa awali”Selam Ambachew ni mwanakamati aliyechaguliwa na jamii."Kama jumuiya, tulichagua kamati, kisha kamati ikaanza tathmini yake, tunapokea orodha ya watu wote wanaoishi katika eneo hili, na tunachunguza orodha ili kuona ni nani anayefaa kwa vigezo vya usaidizi katika jamii"Tadel Gebeyehu ni mmoja wa wananchi walionufaika na mfumo huu mpya wa jamii yenyewe kuchagua wenye uhitaji zaidi wa Msaada wa kibinadamu, anasema "Tulipewa kadi za mgao na lazima tuzioneshe tunapokwenda kupokea chakula. Kadi hizi za mgawo ni muhimu kwa sababu zinazuia watu masikini kunyanyaswa"Ama hakika mwitikio wa kibinadamu nchini Ethiopia unazingatia uwazi, unaendeshwa kwa kuzingatia takwimu na kufikia wale wenye uhitaji zaidi, na hili linathibitishwa Haftom Gebretsadik mmoja wa wagawaji wa msaada.“Mchakato wa kugawa Msaada ni mzuri sana, kila nyanja ni nzuri sana, kinachofanya uwe ya kipekee ni heshima ya utu na ubinadamu. Mfumo ni wa uwazi, hakuna mkanganyiko wala wizi, kwa ujumla mchakato huo ni wa kupongezwa”.
29-4-2024 • 2 minuten, 28 seconden
Mabadiliko ya tabianchi yanachangia katika migogoro katika jamii za asili - Alois Porokwa
Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII uliodumu kwa wiki mbili hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umefikia tamati leo Aprili 26. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa ni mabadiliko ya tabianchi na mazingira, likiwa ni suala ambalo pia miezi miwili iliyopita lilipewa kipaumbele cha juu wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 jijini Nairobi, Kenya. Wakati huo Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS, Stella Vuzo alipata fursa ya kuzungumza na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai wa Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi hususani kwa jamii ambazo bado zinaishi katika mifumo ya asili.
26-4-2024 • 4 minuten, 3 seconden
Raia Sudan wakumbwa na kihoro kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF
Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.
26-4-2024 • 2 minuten, 11 seconden
26 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mzozo nchini Sudan, na jinsi amabvyo mzozo huo unavyathiri wanawake. Makala tunaangazia changamoto ya mabadiliko ya tabianchi kwa jamii za watu wa asili na mashinani usafi wa mazingira katika makazi yasiyo rasmi nchini Kenya. Huko nchini Sudan jimboni Darfur Kaskazini, hususan mjini El-Fasher na viunga vyake mapigano kati ya jeshi la serikali SAF na wanamgambo wa RSF yanazidi kuwa na madhara kwa rai ana kumtia hofu kubwa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk. Katika kufahamu hali iko vipi, Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Seif Magango msemaji wa ofisi ya Kamishna Türk kutoka Nairobi, Kenya na anaanza kwa kueleza nini hasa kinamtia hofu Kamishna huyo.Na tukisalia nchini Sudan, mwaka mmoja wa mzozo umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi. Fatima ambaye alibakwa na kupata ujauzito. Katika makala Stella Vuzo alipata fursa ya kuzungumza na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai wa Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi hususani kwa jamii ambazo bado zinaishi katika mifumo ya asili.Mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani mashirika wanahaha kushughulikia changamoto za usafi wa mazingira katika makazi yasiyo rasmi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
26-4-2024 • 12 minuten, 8 seconden
Simulizi ya mwanamke aliyebakwa na kupata ujauzito wakati wa mzozo Sudan
Mwaka mmoja wa mzozo nchini Sudan umewafanya wananchi wengi kukimbia maeneo waliyokuwa wakiishi kusaka hifadhi pamoja na kukimbilia nje ya nchi. Pamoja ya kukimbia vita lakini pia wanasalia na majeraha ndani ya mioyo yao kutokana na masahibu waliyopitia. Mmoja wao ni Bi. Fatima ambaye alibakwa na kupata ujauzito. Fatima sio jina lake halisi, tunalitumia hili ili kuficha utambulisho wake na hapa anaanza kueleza yale yaliyomsibu akiwa mikononi mwa wanamgambo wenye silaha.“Nilibakwa mara tatu. Aliniambia lala chini, usipotaka kulala chini naweza kukuuwa. Sijui sasa kama ni huyo mwanaume aliniingilia mara tatu au kulikuwa na wengine.” Akiwa na kiwewe na aliyekata tamaa, Fatima akaukimbia mji wake wa Khartoum akiwa na watoto wake kwenda kusini mashariki mwa Sudan, kusaka hifadhi na alipofika huko, anasema “Nilikwenda kuripoti tukio hilo katika kliniki na kusaka msaada ili waweze kunifanyia uchunguzi wa jumla. Nikaenda hospitalini na kila kitu kilikuwa sawa. Baada ya miezi miwili nilienda tena kliniki na wafagundua kuwa nina ujauzito.”Pole sana Fatima, sasa ni nini unachohitaji wakati huu nchi yako bado ingali vitani? “Tunahitaji amani kwa ajili yetu, ili tuweze kurudi na kuishi nchini Sudan.”Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kama vile UN WOMEN, OCHA, UNHCR na hata Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukatili wa Kingono kwenye mizozo wamekuwa wakipazia unyanyasaji wa kijinsia nchini Sudan huku wakieleza wasiwasi wao mkubwa kuwa ukubwa halisi wa mgogoro bado haujajulikana na kumekuwa na viwango vidogo vya kuripoti matukio ya kikatili kwani baadhi ya wanawake na wasichana wanaogopa unyanyapaa na kutokuwa na imani na taasisi za kitaifa.
26-4-2024 • 2 minuten, 2 seconden
Jamii za watu wa asili wanaathiriwa pakubwa na mabadiliko ya tabianchi - Samante Anne
Hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Mkutano wa 23 wa Jukwaa la Kudumu kuhusu Masuala ya Watu wa Asili, UNPFII ukielekea ukingoni huku mambo kadha yakiwa yamejadiliwa kwa wiki mbili na miongoni mwa mambo hayo ni suala la mabadiliko ya tabianchi na mazingira, nilipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO) akieleza namna mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri jamii za watu wa asili nchini mwake.
25-4-2024 • 4 minuten, 44 seconden
Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”
25-4-2024 • 1 minuut
25 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO) anaeleza namna mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri jamii za watu wa asili nchini mwake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki. Leo ni siku ya Malaria duniani ambapo mwaka huu inahamasisha kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa huu ili kuwa na ulimwengu wenye usawa zaidi kwani imebainika kuwa watu wanaoishi katika mazingira magumu ndio wanaoathirika zaidi.Leo pia ni siku ya kimataifa ya wasichana katika tehama na mwaka huu inasherehekea uongozi ikisisitiza hitaji muhimu la kuwa na mifano thabiti ya wanawake viongozi katika taaluma ya sayansi, teknolojia, uhandishi na hisabati -STEM kwani hali ilivyo sasa kuna wanawake viongozi wachache katika maeneo hayo. Na tukisalia na masuala ya wasichana katika tehama Shirika la Umoja Wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limetoa ripoti inayoonya kuwa pamoja na faida za kufundisha na kujifunza kidigitali maendeleo hayo ya kidigitali yanaweza kuwaathiri wasichana kwa kuingilia faragha zao, kuvuruga masomo yao na unyanyasaji mtandaoni.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
25-4-2024 • 10 minuten, 20 seconden
Watoa chanjo wavuka mabonde na mito kufikisha chanjo kwa walengwa Tanzania
Wiki ya kimataifa ya chanjo ikifungua pazia, nchini Tanzania wahudumu wa afya kama Prisca Mkungwa wanajitoa kwa kadri ya uwezo wao kuhakikisha huduma za chanjo zinafikia walengwa wote hata wale walioko maeneo ya mbali. Mathalani huko wilayani Chunya, mkoani Mbeya, kusini magharibi mwa taifa hilo ambako kupitia ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, chanjo dhidi ya surua inatolewa kwa watoto. Prisca na wenzake kutokana na kupenda kazi yao wanafanya kila njia iwe ni kutumia usafiri wa bodaboda au hata kuvuka mito na mabonde kwa miguu kuhakikisha chanjo zinafika. Kufahamu kwa kina ungana na Assumpta Massoi katika makala hii iliyoandaliwa na UNICEF Tanzania.
24-4-2024 • 3 minuten, 32 seconden
Wiki ya Chanjo Duniani yaanza leo 24 hadi 30 Aprili
Leo ni siku ya kwanza ya siku saba za Wiki ya Chanjo Duniani.(Taarifa ya Anold Kayanda)Wiki ya Chanjo Duniani ambayo huadhimishwa katika kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, inalenga kuangazia hatua za pamoja zinazohitajika na kuhimiza matumizi ya chanjo kuwalinda watu wa rika zote duniani dhidi ya magonjwa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO linashirikiana na nchi kote ulimwenguni kuhamasisha ufahamu wa thamani ya chanjo na uchanjaji na kuhakikisha kuwa serikali zinapata mwongozo unaohitajika na usaidizi wa kiufundi ili kutekeleza programu za uchanjaji zenye ubora wa hali ya juu.Lengo kuu la Wiki ya Chanjo Duniani ni kwa watu zaidi na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayoweza kuzuilika.WHO inasema chanjo zimesaidia sana ikitolea mfano namna ulimwengu umeweza kutokomeza ugonjwa wa ndui ambapo mtu wa mwisho kuugua ugonjwa huo ni miaka 47 iliyopita.Mwaka huu Wiki ya Chanjo Duniani inaadhimisha miaka 50 ya EPI ambao ni mpango ambao WHO iliuanzisha mwaka 1974 kwa lengo la kufanya chanjo zipatikane kwa watoto wote duniani.WHO inatoa wito kwa nchi kote duniani kuongeza uwekezaji katika mipango ya chanjo ili kulinda vizazi vijavyo.Tags: Siku za UN, WHO, Chanjo, EPI, Wiki ya Chanjo Duniani
24-4-2024 • 1 minuut, 17 seconden
Mtu 1 kati ya 5 katika nchi 59 duniani anahitaji hatua za haraka kuepushwa na baa la njaa: FAO
Ripoti mpya ya kimataifa iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO kuhusu mgogoro wa chakula duniani inasema karibu watu milioni 282 walio katika nchi 59 walikabiliwa na viwango vya juu vya njaa mwaka 2023. (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Asante Leah. Kwa hakika ripoti hiyo ya “Mgogoro wa kimataifa wa chakula” GRFC inasema kiwango cha watu wenye njaa duniani kiliongezeka kwa watu milioni 24 kutoka mwaka 2022 hadi 2023 na ni asilimia 21.5 ya watu waliofanyiwa tahimini na hicho ni kiwango kikubwa sana ukilinganisha na ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19 limesema shirika la FAO likiongeza kuwa idadi ya walio na njaa duniani inaendelea kuongezeka.Ripoti imetaja sababu kuu tatu ambazo zinachangia kwa kiasi kikubwa janga la njaa duniani ambazo ni mosi migogoro na vita ambapo inasema inaathiri katika nchi 20 zilizo na jumla ya watu milioni 135 wanaokabiliwa na njaa zikiwemo Sudan, Yemen na Palestina katika Ukanda wa Gaza.Pili ni matukio mabaya ya hali ya hewa yaliyochangiwa na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa chanzo cha njaa katika nchi 18 na kuathiri kwa njaa zaidi ya watu milioni 77.Na tatu mdororo wa kiuchumi uliokuwa chachu ya njaa katika nchi 21 na kuathiri jumlaya watu milioni 75.FAO imesema kwa miaka minne mfululizo takriban asilimia 22 ya watu waliofanyiwa tathimini duniani wamekuwa wakikabiliwa na kutakuwa na uhakika wa chakula. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “Mgogoro huu unahitaji hatua za haraka. Kutumia takwimu zilizoainishwa katika ripoti hii ili kufanyia marekebisho mifumo ya chakula na kushughulikia mizizi ya kutakuwa na uhakika wa chakula itakuwa muhimu sana”Kwa mujibu wa ripoti waathirika wakubwa ni watoto, wanawake na watu wenye ulemavu.Mtandao wa kimataifa dhidi ya mgogoro wa chakula imetoa wito wa haraka wa kubadili mtazamo ili ujumuishe amani, hatua za kuzuia na za maendeleo sambaba na juhudi za dharura kuvunja mzunguko wa janga la njaa ambalo linasalia katika viwango vya juu
24-4-2024 • 2 minuten, 23 seconden
24 APRILI 2024
Karibu kusikiliza jarida hii leo linaangazia masuala mbalimbali ikiwemo ripotoi ya mgogoro wa chakula duniani, kuanza kwa wiki ya chanjo na utoaji chanjo kwa watoto mashinani.
24-4-2024 • 10 minuten
23 APRILI 2024
Hii leo jaridani utasikia kuhusu ushirikishwaji wa vijana katika vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa Maendeleo UNDP.Pia utasikia muhtasari wa habari kuhusu wasaka hifadhi huko nchini Uingereza kuhamishiwa Rwanda, Makaburi ya halaiki huko Gaza na kuongezeka kwa mlipuko wa ugonjwa wakipindi pindu duniani.Kwa upande wa mashinani hii leo utasikia kuhusu harakati za mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali katika kuhakikisha usalama wa mipaka.
23-4-2024 • 10 minuten, 49 seconden
Rein Paulsen: Wakati wa kuchukua hatua kuepusha baa la njaa Sudan ni sasa
Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni sasa. Sabrina Moshi anasimulia.
22-4-2024 • 3 minuten, 27 seconden
DRC: WFP waomba msaada wa $Mil 425 kusaidia wakimbizi wa ndani
Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao. Mratibu wa masuala ya dharura wa WFP huko mashariki mwa DRC Bi. Cynthia Jones amesema hapo awali walipata bahati ya kuanzisha mpango ambapo walikuwa wanaweza ama kuwapatia wakimbizi wa ndani chakula au kuwapatia fedha taslimu na hiyo iliwaruhusu kutoa aina thabiti zaidi ya usaidizi lakini kwa sasa hali ilivyo watalazimika kufanya maamuzi magumu. “Sasa hivi tulikuwa katika hali ambayo tunajitahidi kufikia watu milioni 1.2 na sasa tuna wakimbizi wengine milioni 1.2 wameongezeka. Na kwa hivyo itamaanisha tunapaswa kufanya maamuzi magumu juu ya jinsi tunavyotanguliza nani atakula na nani asile. Tunajaribu kuchukua rasilimali tulizo nazo na kuzitumia vyema na kuzisambaza, lakini sio jambo la maana kwani kitendo hicho ni kusema tuna sawazisha hali mbaya zaidi ya Kivu Kaskazini ni kwamba tunapaswa kupungua, inaweza kuwa ituri au Kivu Kusini. Hayo pia ni maamuzi magumu kwa sababu kuna watu wengi ambao hawana uhakika wa chakula katika maeneo hayo pia.”Bi.Jones amesema pamoja na kuwa na fahari na kazi kubwa waliyoifanya ya kusaidia wakimbizi wengi hapo awali, mtiririko mkubwa wa wakimbizi wanaowasili kusaka hifadhi katika makambi katika miezi ya hivi karibuni umefanya kazi yao kuwa ngumu zaidi.
22-4-2024 • 1 minuut, 49 seconden
22 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya hali ya joto dunianina madhara yake kwa afya na wafanyakazi, Naomi la ufadhili kwa ajili ya wakimbizi wa ndani DR Congo. Makala tunakupeleka nchini Sudan na mashinani nchini Sudan Kusini, kulikoni? Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi.Wakati Mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemorkasia Kongo DRC ikiripoti kuwa na zaidi ya wakimbizi wa ndani 738,000 kwa kipindi cha mwaka huu wa 2024 pekee kutokana na kuongezeka kwa machafuko, Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limeeleza kuwa na uhitaji wa haraka wa dola milioni 425 ili waweze kuwasaidia wakimbizi hao wanaoongezeka kila uchao. Katika mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, afisa mwandamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) anayehusika na masuala ya dharura na mnepo, Rein Paulsen ametahadharisha kuwa hatari ya kutokea baa la njaa nchini Sudan ni halisi na kwa hivyo wakati wa kuchukua hatua ni sasa.Na mashinani tutapeleka Tambunra nchini Sudan Kusini kumsikia mkimbizi wa ndani akisihi kurejea kwa amani illi aweze kurudia nyumbani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
22-4-2024 • 12 minuten
ILO: Joto la kupindukia linaathiri asilimia 70 yawafanyakazi kote duniani
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa duniani ILO, inasema zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wote duniani wanakabiliwa na uwezekano wa hatari za kiafya kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Asante Anold, akizungumza na waandishi wa habari hii leo mjini Geneva Uswis wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo Manal Azzi, afisa wa masuala ya usalama kazini na afya wa shirika la ILO amesema takwimu hizi za kustaajabisha zinasisitiza haja kubwa ya kurekebisha hatua zilizopo za usalama na afya kazini ili kushughulikia ipasavyo vitisho vinayojitokeza kutokana na hatari zinazohusiana na changamoto za hali ya hewa.Ameongeza kuwa “Zaidi ya asilimia 70 ya wafanyakazi wetu wanakabiliwa na joto jingi, angalau joto la kupindukia, katika wakati mmoja wa maisha yao ya kazi. Hiyo ni jumla ya wafanyakazi bilioni 2.4 duniani kote, kati ya wafanyakazi wa kimataifa wa bilioni 3.4.”Ripoti hiyo iliyopewa jina “Kuhakikisha usalama na afya kazini katika mazingira yanayobadilika” inaeleza kwamba mabadiliko ya tabianchi tayari yameleta athari kubwa kwa usalama na afya ya wafanyakazi katika kanda zote duniani.Kwa mujibu wa ILO waafanyakazi, hasa wale walio katika maeneo yenye umaskini zaidi duniani, wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kukabiliwa na hatari za mabadiliko ya tabianchi kama vile joto kali, ukame wa muda mrefu, moto mkubwa wa nyika, na vimbunga vikali.Bi. Azzi amesema "Wafanyakazi zaidi ya milioni 22 wanaugua magonjwa na majeraha yanayohusiana na joto kali na haya yanaweza kutoka na sababu mbalimbali ikiwemo ajali katika usafiri, katika ajali za barabarani kutokana na usingizi kwa kutolala vizuri usiku kwa sababu kulikuwa na joto kupita kiasi, hadi ajali za ujenzi, majeraha, kuteleza na kuanguka. kunkohusiana na ongezeko la joto kali."Ripoti hiyo inabainisha kuwa baadhi ya athari za kiafya kwa wafanyakazi zilizohusishwa na mabadiliko ya tabianchi, ni pamoja na saratani, ugonjwa wa moyo na mishipa, magonjwa ya kupumua, figo kuharibika na hali ya afya ya akili. Pia kuongezeka kwa joto na unyevu wa hali ya juu, dawa nyingi za wadudu hutumiwa katika sekta ya kilimo na kufanya wafanyikazi milioni 870 katika kilimo kuwa na uwezekano wa kuathiriwa na viuatilifu, huku kukiwa na zaidi ya vifo 300,000 vinavyohusishwa na sumu ya dawa hizo kila mwaka.Bi Azzi amesisitiza kuwa mambo haya yote yanaingiliana na kwamba zana zinazofaa zinapaswa kuwepo ili kupima athari na kuwa na uwezo wa kufanyia kazi mapendekezo.Mkutano mkuu umepangwa kufanyika 2025 na ILO kwa kushirikisha wawakilishi wa serikali, waajiri na wafanyakazi ili kutoa mwongozo wa sera kuhusu hatari za mabadiliko ya tabianchi katika masuala ya kazi.
22-4-2024 • 2 minuten, 58 seconden
Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT
Lugha ni miongoni mwa njia za kimsingi za kujenga utangamano duniani. Umoja wa Mataifa unatambua kuwa lugha ni chombo cha kusongesha tamaduni na miongoni mwa lugha zilizotengewa siku mahsusi kusherehekewa ni kichina ambacho shamrashamra zake ni tarehe20 mwezi Aprili ya kila mwaka.Lugha hii imesambaa duniani ikiwemo Tanzania ambako hii leo Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM ya mkoani Mwanza kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki amefuatilia mafunzo yake kwenye Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino.
20-4-2024 • 5 minuten, 18 seconden
Joram Nkumbi na Vivian Joseph: Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza toka kwa wenzetu
19-4-2024 • 3 minuten, 19 seconden
Francesco La Camera: Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kuhamia haraka katika nishati jadidifu
19-4-2024 • 2 minuten, 27 seconden
19 APRILI 2024
Ushirikiano wa kimataifa utasaidia kufanikisha kuhamia katika nishati jadidifu - Francesco La Camera.Vijana wa Afrika lazima tuchangamkie fursa na kujifunza: Joram Nkumbi na Vivian Joseph.Lugha ya kichina imepanua fursa za ajira kwa wanafunzi wa SAUT – Tanzania.Mashinani ni nchini Kenya kusikia jinsi ambavyo mafunzo ya ukulima endelevu na mikopo ya fedha katika mzunguko wa kijamii (Merry-go) inavyowasaidia wakulima kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
19-4-2024 • 14 minuten, 40 seconden
Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhiri na hadhiri.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na hadhiri.”
18-4-2024 • 1 minuut, 11 seconden
18 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina amabyo hivi karibuni tulizungumza na Peter Mmbando kutoka Tanzania akifafanua nini wanafanya ili kuimarisha matumizi endelevu ya teknolojia ya kidijitali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhiri; na hadhiri."Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea hofu yao juu mwenendo wa mashambulizi dhidi ya shule, vyuo vikuu, waalimu na wanafunzi kwenye Ukanda wa Gaza hali ambayo wamesema ni ishara ya mpango wa uharibifu mkubwa wa mfumo wa elimu wa Palestina.Muungano wa chanjo duniani GAVI na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wamekaribisha taarifa kwamba chanjo mpya ya matone ya kipindupindu Euvichol-S, sasa imepokelewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na inaweza kupatikana katika nchi mbalimbali duniani. Kupitishwa kwa chanjo hiyo mpya kutasaidia kuongeza usambazaji wake kwa takriban dozi milioni 50 mwaka huu ikilinganishwa na dozi milioni 38 zilizosambazwa mwaka 2023. Mkutano wa Wiki ya Uendelevu ya Umoja wa Mataifa unaendelea hapa Makao Makuu New York Marekani, leo ukijikita na mada ya miundombinu endelevu na inayoaminika ambayo Umoja wa Mataifa unasema itazisaidia nchi kuelekea kwenye maendeleo yenye miumbombinu bora, isiyo ya hatari na itakayoongeza kasi ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDGs.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhiri; na hadhiri.”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
18-4-2024 • 11 minuten, 34 seconden
Vijana wakiwezeshwa wanaweza kuvumbua teknolojia ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu
Hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Hafla hii pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania. Wameketi na Flora Nducha na kumweleza walichoambulia hadi sasa katika jukwaa hilo litakalokunja jamvi kesho..
17-4-2024 • 8 minuten, 35 seconden
Mapigano na mizozo DR Congo yanyima wananchi manufaa ya utajiri wa nchi yao - Türk
Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Video ya Umoja wa Mataifa inaanzia Kinshasa mji mkuu wa DRC ambako Bwana Türk na aafisa mmoja wa Umoja wa Mataifa wanatazama ramani ya taifa hilo lililoko Maziwa Makuu na kisha anasema ni moja ya nchi tajiri zaidi duniani, lakini tunaona ni kwa vipi utajiri huu kwa bahati mbayá hauko kunufaisha wananchi kwa sababu ya mapigano.Na kisha anaelezea mipango ya ziara yake ya kutathmini hali ya haki za binadamu akisemakwanza ni kukutana na watu waliofurushwa makwao kutokana na ghasia na vile vile kuonana na mamlaka husika na mashirika ya kiraia.Baada ya hapo safari inaanza akiambatana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Bintou Keita, mwelekeo ni Mashariki mwa nchi jimboni Ituri. Taswira ya angani kutoka ndege hii ya Umoja wa Mataifa na kisha wanawasili. Mapokezi hapa Bunia, kutoka kwa wenyeji wao.Moja kwa moja msafara wao wa magari unafika kwenye kambi ya wakimbizi nje kidogo ya mji wa Bunia na wanaingia ndani ambako wanawake, wanaume na watoto, wazee na vijana, nyuso zao zinaonesha matuamini kwani wahenga walinena mgeni njoo mwenyeji apone.Mkalimani akamweleza Turk kuwa wanachosema maeneo yao yametawaliwa na waasi na hawawezi kurejea makwao.Na ndipo Kamishna huyu Mkuu wa Haki za Binadamu baada ya kuwasikiliza wakimbizi na kuzungumza nao akatoka nje na kusema, “Nimekutana na kundi la watu ambao wamefurushwa makwao kutokana na mauaji ya kikatili na ya kutisha yaliyotekelezwa kwenye makazi yao. Na wamekuweko hapa kwa miaka minne sasa. Tamanio lao kubwa kabisa ni kuweza kurejea makwao.”Kwa sasa kuna takribani watu milioni 1.8 waliofurushwa makwao jimboni Ituri kati ya wakimbizi wote wa ndani milioni 7.2 nchini kote DRC.Kesho Bwana Turk atakuwa na mazungumzo na Rais President Félix Tshisekedi na maafisa wengine wa serikali, Umoja wa Mataifa, wanadiplomasia na vyama vya siasa pamoja na watetezi wa haki za binadamu na kisha atazungumza na waandishi wa habari.
17-4-2024 • 2 minuten, 31 seconden
17 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ghasia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na jitihada za Umoja wa Mataifa za kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunaelekea nchini Madagascar, kulikoni?Kaminshna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ambaye yuko katika ziara rasmi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC amestaajabu ni kwa vipi utajiri wa maliasili uliosheheni kwenye taifa hilo umeleta manufaa kidogo kwa wananchi wako kutokana na ghasia na mapgano.Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo. Makala inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunakofanyika jukwaa la vijana la Baraza la kiuchumi na kijamii ECCOSOC ambalo linatoa ukumbi wa kimataifa wa mazungumzo kati ya nchi wanachama na viongozi vijana kutoka kote ulimwenguni kujadili suluhu za changamoto zinazoathiri ustawi wa vijana. Pia hutumika kama nafasi ya kipekee kwa vijana kushiriki maono na hatua zao ili kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya 2030 na SDGs ikiwemo masuala ya uvumbuzi na teknolojia. Miongoni mwa wanaohuduria jukwaa hilo kutoka Tanzania ni Vivian Joseph Afisa tabibu na mkuu wa wa kitengo cha afya akiwasilisha vijana katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na Joramu Nkumbi mkurugenzi mtendaji wa jukkwaa la Afrika la viongozi vijana kwa upande wa Tanzania.Na mashinani tutakupeleka nchini Madagascar kusikia ujumbe kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, lakini kwanza ni makala.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
17-4-2024 • 13 minuten, 1 seconde
Mkutano wa ufadhili wapata msaada wa fedha wa dola milioni 610 kwa ajili ya Ethiopia
Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Kutoa ahadi kwa ajili ya ufadhili wa kukwamua hali ya Kibinadamu nchini Ethiopia uliokamilika jana mjini Geneva, Uswisi umetangaza kwamba wafadhili 20 wametangaza msaada wa kifedha wa Dola za Marekani milioni 610 angalau kuhakikisha misaada kwa miezi michache ijayo.Mkutano huo uliolenga kukusanya dola bilioni 1 za kimarekani kwa ajili ya miezi mitano ijayo, ulikuwa umeandaliwa kwa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Serikali ya Ethiopia na Uingereza, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa masuala ya kibinadamu. Mara tu baada ya mkutano huo Naibu Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura OCHA, Joyce Msuya, aliwashukuru wafadhili hao na kusema kuwa huo ni mwanzo tu na matumaini ni kuendelea na kuongeza msaada kwa mwaka mzima.Dharura ya kibinadamu nchini Ethiopia imekuwa ikiongezeka kupitia mizunguko ya ukame na mafuriko, na migogoro. Ukosefu wa uhakika wa chakula na utapiamlo unatarajiwa kufikia kiwango cha juu kwa watu milioni 10.8 wakati wa msimu wa muwambo kati ya mwezi Julai na Septemba.Viwango vya utapiamlo katika sehemu za Afar, Amhara, Tigray na mikoa mingine vinatia wasiwasi mkubwa na vinaendelea kuwa vibaya zaidi. Wakati huo huo, migogoro katika Tigray na mikoa mingine imeharibu maelfu ya shule, vituo vya afya, mifumo ya maji na miundombinu mingine ya jamii.Mama huyu ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama ni wa eneo la Afar, mashariki mwa Ethiopia ambako pia kumeathiriwa na mafuriko anapaza sauti akisema, “Ninataka kulea na kusomesha watoto wangu vizuri. Nawatakia watoto wangu mema.”Umoja wa Mataifa na wadau wa kibinadamu wanaunga mkono mwitikio wa kitaifa wa kuongeza msaada wa kuokoa maisha kwa watu milioni 15.5, na msaada wa chakula kwa watu milioni 10.4 nchini humo Ethiopia. Kwa mwaka mzima, ili mpango huo ufanikiwe unahitaji dola za Marekani bilioni 3.24.
17-4-2024 • 1 minuut, 56 seconden
16 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tanzania, Abeida Rashid Abdallah anafafanua kwa nini Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Zanzibar ni chanda na pete. Pia tunakuletea muhtasari ya habari na mashinani kama zifuatazo.Leo mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kuonya juu ya vita inayoendelea kukatili maisha ya watu Gaza, na kusambaratisha miundombinu yakitaja kuwa wanawake karibu 10,000 wamepoteza Maisha tangu vita kuanza miezi sita iliyopita huku mtoto mmoja anajeruhiwa au kuuawa kila dakika 10.Jukwaa la vijana la Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limeng’oa nanga hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Matrekani likiwaleta maelfu ya vijana kutoka kila kona ya Dunia. Joramu Nkumbi ni miongoni mwa washiriki wa jukwaa hilo kutoka Tanzania na anafafanua wanachokijadili mwaka huu. Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kwa shirikiana na mashirika mengine 48 ya kibinadamu, ya maendeleo na serikali wametoa ombi la haraka la dola milioni 112 ili kuwasaidia zaidi ya wahamiaji milioni 2.1 na jamii zinazowahifadhi. Kwa mujibu wa IOM wahamiaji na jamii hizo ni katika njia za uhamiaji za Mashariki na Kusini zkijumuisha Djibouti, Ethiopia, Somalia, Yemen, Kenya na Tanzania.Na mashinani leo tunakwenda mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC hususan jimboni Ituri ambako huko ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umechukua hatua kukabili mashambulizi kutoka waasi, mashambulizi ambayo kila uchao yanazidi kufurusha raia. Mzungumzaji wetu ni Luteni Kanali Mensah Kedagni, msemaji wa kijeshi wa MONUSCO.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
16-4-2024 • 12 minuten, 9 seconden
Ni dhana potofu kudai Wamaasai wanaua Simba ili kupata mke - Alois Porokwa
Katika harakati za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, kuna wakati jamii ambazo bado zinaishi kiasili zimekuwa zikilaumiwa kwamba zinachangia kuharibu mazingira kutokana na wao kuishi katika mazingira fulani; mathalani misitu na mbuga jambo ambalo linakanushwa na jamii hizo wakidai kwamba kimsingi wao ndio watunzaji wazuri wa mazingira kwani wanayategemea moja kwa moja kwa mustakabali wa maisha yao ya kila siku na siku zijazo. Hivi karibuni wakati wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika jijini Nairobi, Kenya, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, Stella Vuzo alimhoji Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania. Ni katika mazungumzo hayo ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.
15-4-2024 • 3 minuten, 3 seconden
Jukwaa la Jamii za watu wa asili lafungua pazia katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa
Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali. Hiki ni kikao cha 23 cha jukwaa hili la kudumu la watu wa jamii za asili ambao leo mkutano wa kwanza umefunguliwa rasmi ukihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Balozi Dennis Francis. Majadiliano ya wiki mbili za mkutano huu yataongozwa na dhima ya kuangazia haki za watu wa asili kujitawala pamoja na sauti za vijana wa jamii ya asili. Sehemu muhimu ya majadiliano haya inalenga kuhakikisha watu wa jamii za asili wanapata haki ya kujiamulia na kupata ufadhili utakao wawezesha kudai haki zao vyema, kuendeleza maendeleo yao ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni na kufadhili miundo ya utawala wao, kama ilivyoainishwa katika Azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Watu wa Kiasili.Mwenyekiti wa Jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusuu watu wa asili Bi. Hindou Oumarou Ibrahim akizungumza katika jukwaa hilo amesema “Kuondolewa vikwazo kwenye upatikanaji wa fedha ni muhimu ili kuhakikisha watu wa asili wanatekeleza kwa vitendo mipango yao na kuwa na njia ya kudumisha kujitawala,” Kwa upande wake Bwana Li Junhua, ambaye ni msaidizi waKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kiuchumi na kijamii (DESA) amesema “unahitaji ufadhili wa muda mrefu, unaotabirika, na wa moja kwa moja kwa Watu wa Asili, ikijumuisha kupitia mifumo ya ufadhili ya umma, ya kibinafsi, na inayoongozwa na Wenyeji ambayo inashirikisha kikamilifu Wanawake na vijana wa kiasili.”Unaweza kufuatilia moja kwa moja matangazo ya jukwaa hili yanayorushwa mubashara na Umoja wa Mataifa kupitia wavuti wake wa UN Web TV,matangazo yanarushwa kwa lugha rasmi sita za umoja wa Mataifa ambazo ni Kingereza, Kifaransa, Kiarabu, Kichina, Kispanishi na Kirusi.
15-4-2024 • 1 minuut, 53 seconden
15 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia utekwaji nyara wa watoto wa kike 275 huko Chibok nchini Nigeria, na uwezeshaji kiuchumi wa watu wa asili. Makala inamulika masuala ya mazingira ikiangazia watut wa asili na mchango wao, na mashinani tunakupeleka nchini Chad kusikia simuliza ya mkimbizi kutoka Sudan. Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi.Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York Marekani, Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili limeanza rasmi na litadumu kwa muda wa wiki mbili likiwaleta pamoja zaidi ya washiriki 2000 wa jamii za asili kutoka kila pembe ya dunia kujadili masuala mbalimbali. Makala Stella Vuzo, Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Kenya, anatuletea mazungumzo kati yake na Alois Porokwa, Mkurugenzi wa shirika la NALEPPO kutoka jamii ya Wamaasai aliyesafiri kutoka Kijiji cha Emboreet, Wilaya ya Simajiro, Mkoa wa Manyara, Tanzania kuhudhuria wa Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 uliofanyika mwezi uliopita jijini Nairobi, Kenya. Kwa kuwa jamii zinazoishi kiasili wakati mwingine zimekuwa zikilaumiwa kuwa zinachangia katika uharibifu wa mazingira ndipo Stella Vuzo akakumbuka kumuuliza Alois Porokwa swali hili ambalo ni dhana inayohusisha jamii ya Wamaasai kuua wanyama.Na mashinani tunamulika vita nchini Sudan ambayo inaendelea kuwalazimisha mamilioni ya watu kukimbia kuokoa maisha yao. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, mkimbizi ambaye alikimbia machafuko nchini humo kuelekea Chad anasimulia changamoto alizozipitia.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
15-4-2024 • 11 minuten, 5 seconden
UNICEF: Miaka 10 ya watoto kutekwa Chibok, bado hakuna mifumo ya ulinzi
Nigeria inapotimiza miaka 10 tangu tukio la utekwaji nyara la watoto wa kike 275 huko Chibok, kaskazini magharibi mwa taifa hilo, hadi sasa bado watoto 90 wamesalia mateka na nchi hiyo inasalia na kumbukumbu ya tukio linguine la wanafunzi wa shule kutekwa nyara jimboni Kaduna mwezi Machi mwaka huu, hali inayosababisha Umoja wa Mataifa kutoa wito mahsusi. Ilikuwa usiku wa tarehe 15, Jumatatu ndipo watoto hao wa kike wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 17 walitekwa na kundi la Boko Haram huko jimboni Borno, na ndio maana kwa mazingira yalivyo sasa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema safari bado ni ndefu kwa watoto nchini Nigeria kutimiza ndoto yao ya kusoma kwenye mazingira yaliyo salama, kwani ni asilimia 37 tu ya shule kwenye majimbo 10 yaliyo kwenye mazingira hatarishi ndio zina mifumo ya kubaini mapema vitisho kama vile shule kushambuliwa. Ripoti ya UNICEF iliyotolewa leo Abuja, miji Mkuu wa Nigeira ikipatiwa jina Viwango vya Chini Vya Usalama Shuleni au MSSS kwa lugha ya kiingereza, inaonesha ukweli mchungu wa kufanikisha safari hiyo kwa mtoto nchini Nigeria kuweko shuleni bila uoga. Mwakilishi wa UNICEF nchini humo Cristian Munduate amesema tukio la kutekwa nyara wasichana wa Chibok ni kengela ya kutuamsha juu ya hatari kubwa watoto wetu wanakabiliwa nayo wanaposaka elimu. Anasema leo tunapotafakari janga hili na mengine ya hivi karibuni ni dhahiri kuwa juhudi zetu za kulinda mustakabali wa watoto wetu lazima ziimarishwe. Mwakilishi huyo anasema kwa kuzingatia takwimu zilizotolewa na ambazo zinatia hofu kubwa, ni lazima kupata majawabu ya sio tu dalili bali pia chanzo cha janga hilo la utekaji nyara watoto. Bi. Munduate amekumbusha kuwa elimu ni haki ya msingi na ni njia muhimu ya kuelekea kuondokana na umaskini. Lakini kwa watoto wengi nchini Nigeria inasalia kuwa ndoto isiyotimizika. Ripoti ilimulika maeneo 6 ikiwemo mifumo thabiti ya shule, ukatili dhidi ya watoto, majanga ya asili,mizozo ya kila siku na miunmdombinu ya shule na kubaini utofauti mkubwa wa vigezo hivyo katika majimbo yote 36. Jimbo la Borno liko thabiti kwani limekidhi viwango kwa asilimia 70 ilhali majimbo ya Kaduna na Sokoto bado yako nyuma. Uchambuzi huu unakuja wakati kuna ripoti za ongezeko la ghasia dhidi ya shule ambapo katika miaka 10 iliyopita, matukio ya mashambulizi yamesababisha watoto zaidi ya 1,680 kutekwa nyara wakiwa shuleni au kwinigneko. UNICEF inataka Nigeria pamoja na mambo mengine ihakikishe shule kwenye majimbo yote zina rasilimali za kutekeleza MSSS. Pia itatue pengo la uwiano wa usawa katika hatua za kuimarisha usalama shuleni. Nigeria pia iimarishe usimamizi wa sheria na mikakati ya usalama ya kulinda taasisi za elimu na jamii dhidi ya utekwaji. Kwa sasa UNICEF inashirikiana na serikali kuhakikisha kila mtoto anakuwa na mazingira salama ya kusomea. Soma ripoti nzima hapa.
15-4-2024 • 2 minuten, 58 seconden
Guterres/Kwibuka 30: Vijana kemeeni kauli za chuki kokote muisikiapo na muionapo
Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda au KWIBUKA30, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametumia hotuba yake pamoja na mambo mengine kuwasihi vijana kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kukemea chuki kokote wanapoisikia au kuiona. Tukio lilianza kwa ukumbi kuwa giza na video ya dakika tano ikachezwa kueleza kuwa watu wengi wanaijua Rwanda kuanzia 1994, lakini ilikuweko hata kabla ya ukoloni, na kwamba wakoloni ndio waligawa watu kwa misingi ya makundi licha ya kwamba lugha yao ilikuwa moja. Manusura na watekelezaji wa mauaji walizungumza pia kwenye video hiyo!Video ikafuatiwa na kuwasha mishumaa kukumbuka waliouawa na kisha hotuba ambapo Katibu Mkuu Guterres akawa ana ujumbe mahsusi kwa vijana wa Rwanda walioshiriki kimtandao na pia ukumbini.Anasema rafiki zangu, katu hatutasahau vitisho vya siku 100. Lakini tunahitaji msaada wenu. Tunahitaij sauti na uchechemuzi wenu kusongesha kumbukizi za wale waliouawa. Na kukemea chuki kokote muisikiako au muionapo. Mijini kwenu, vitongojini, shuleni, mtandaoni, popote pale na kila mahali.Akaendelea kusema kuwa hebu na tuondoe chuki na ukosefu wa stahmala kokote tuvionapo. Kumbukumbu za waliouawa zichochee vitendo vyetu, na azma yetu ya kuhakikisha dunia bora na salama kwa watu wote. Guterres amesema Umoja wa Mataifa kila wakati utashikamana na vijana katika juhudi hizo muhimu. Mauaji ya kimbari Rwanda ya mwaka 1994 yalifanyika kwa siku 100 kuanzia tarehe 7 Aprili na zaidi ya watu milioni moja waliuawa, wengi wao Watutsi, halikadhalika wahutu wenye msimamo wa kati na watu wengine waliokuwa wanapinga mauaji hayo. Katibu Mkuu amesema siku hizo 100 ziliakisi ubaya zaidi wa ubinadamu. Lakini kipindi baada ya mauaji kilidhihirisha ubora wa roho ya ubinadamu: mnepo, maridhiano, ujasiri na nguvu. Amesema simulizi za manusura ni ushahidi wa nguvu ya matumaini na msamaha ambapo amemtaja manusura Laurence Niyonangira ambaye alipoteza jamaa zake 37 wakati wa mauaji hayo. “Alichagua kusamehe mmoja wa wahusika wa mauaji ya familia yake baada ya mhusika kuungama na kutumikia muda jela kwa makosa aliyotenda. Kama manusura, Laurence alisema ‘tunaweza kuponya vidonda kwa kushirikiana wale waliovisababisha.” Amesema Guterres. Hivyo Katibu Mkuu amesema mwaka huu ambapo kumbukizi inajikita kwenye mzizi wa mauaji ya kimbari ambao ni chuki, ambayo sasa inakolezwa na mitandao ya kijamii, “ni lazima tushikamane pamoja na kurejelea shinikizo la dunia la kuridhia na kutekeleza kikamilifu Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya kimbari, huku tukiimarisha mifumo ya kuzuia, kuelimisha vizazi vipya kuhusu mauaji ya kimbari yaliyopita na kukabili taarifa potofu na za uongo ambazo huchochea kauli za chuki na nia na vitendo ya mauaji ya kimbari.”
12-4-2024 • 3 minuten, 37 seconden
Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 watoa matibabu kwa raia nchini DRC
Kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO wametekeleza wajibu wao wa kulinda raia kwa kuwapatia huduma ya matibabu kwenye Kijiji cha Matembo kilichoko mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini. Shuhuda wetu ni Kapteni Fadhila Nayopa, Afisa habari wa kikosi hicho.
12-4-2024 • 3 minuten, 38 seconden
12 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia kumbukizi wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, na wakimbizi wa Sudan wanaovuka mpaka kuelekea nchini Sudan Kusini. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu limekuwa na tukio maalum la kumbukizi ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda au KWIBUKA30, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres ametumia hotuba yake pamoja na mambo mengine kuwasihi vijana kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kukemea chuki kokote wanapoisikia au kuiona.Tarehe 15 April wiki ijayo siku ya jumatatu nchi ya Sudan itatimiza mwaka mmoja rasmi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF). Vita hiyo imesababisha maelfu ya watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kusaka hifadhi nchi Jirani. Mashirika ya misaada ya kibinadamu nayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wenye uhitaji japo yanakabiliwa na ufinyu wa bajeti. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako kikosi cha 11 cha walinda amani kutoka Tanzania, TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wametekeleza wajibu wao wa kulinda raia kwa kuwapatia huduma ya matibabu kwenye Kijiji cha Matembo kilichoko mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini.Na mashinani tunakuletea ujumbe wa Marthe Nyangoma, mtumishi wa umma kutoka eneo la Irumu, huko Ituri nchini DRC, ambaye kwa uwezeshaji wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa MONUSCO, anahamasisha jamii dhidi ya taarifa potofu na kauli za chuki akisistiza kuwa kabla ya kuwasilisha taarifa, lazima zidhibitishwe ili kuepusha mgawanyiko.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
12-4-2024 • 13 minuten, 28 seconden
Wakimbizi kutoka Sudan wanoingia Sudan Kusini wanaendelea kuongezeka
Tarehe 15 April wiki ijayo siku ya jumatatu nchi ya Sudan itatimiza mwaka mmoja rasmi tangu kuanza kwa mzozo kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) na Vikosi vya jeshi la Sudan (SAF). Vita hiyo imesababisha maelfu ya watu kuwa wakimbizi wa ndani na wengine kusaka hifadhi nchi Jirani. Mashirika ya misaada ya kibinadamu nayo yamekuwa mstari wa mbele kusaidia wananchi wenye uhitaji japo yanakabiliwa na ufinyu wa bajeti.Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP inaanza kwa kuonesha wananchi wakiwa na vifurushi mikononi, wengine wakiwa wamepanda usafiri unaosukumwa na ngombe na wengine mabasi wakiingia katika mpaka wa Joda nchini Sudan kusini wakitokea nchini Sudan.“Tumesafiri kwakutumia basi na imetuchukua siku mbili kufika hapa”, ndivyo anavyosema Hamida Ibrahim mkimbizi kutoka Sudan. Anaendelea kwa kueleza kile wanachohitaji kwa sasa. “Tunahitaji chakula. Huo ndio msaada wa haraka tunaohitaji ili tuweze kuishi. Kwa sababu tupo na watoto na hawana uwoga wanachojua wanakuja hapa kufata usalama” Kiongozi wa WFP katika eneo hili Leonidace Rugemalila anasema mzozo huu wa Sudan umemuathiri kila mtu.“Katika kipindi cha miezi mitatu idadi ya watu wanaovuka mpaka huu kila siku imeongezeka kutoka watu 1,500 mpaka takriban watu 2,500.”Naye Mkuu wa lishe Aachal Chand anasema wengi wa waaathirika wa mzozo nchini Sudan ni wanawake na watoto, na walioathirika zaidi ni wajawazito, wanawake wanaonyonyesha na watoto wenye umri chini ya miaka mitano. “Wanapovuka mpaka, mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka mitano anapatiwa biskuti za lishe kama chakula cha haraka chakumpa lishe. Kwa watoto chini ya miaka mitano tunawapa chakula maalum cha lishe. Kuanzia saa mbili asubuhi mpaka wakati huu saa 10 jioni wameshatoa lishe kwa takriban watoto 400 ambao wamepokea matibabu ya utapiamlo au huduma za matibabu.”Chand ameeleza kuwa WFP na wadau wake wanaendelea kutoa msaada hata hivyo wanakabiliwa na ufinyu wa bajeti.“Watu wanahitaji msaada wa afya na lishe, watu wanahitaji usaidizi katika kupata uhakika wa chakula, watu wanahitaji msaada wa kuweza kuwasaidia kufika katika maeneo wanayotaka kuelekea.Sudan na athari zake kwa nchini ya Sudan Kusini zinasahaulika na tunatakiwa kuhakikisha hatusahau mzozo huu kwasababu hawa ni watu na wanapata athari halisi katika maisha yao.”
12-4-2024 • 2 minuten, 42 seconden
11 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Alice Nderitu, Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa katika kuzuia mauaji ya kimbari akiwa Kigali hivi majuzi kwenye kumbukizi anamulika nini kifanyike kuhakikisha kitendo kama hicho kinasalia historia. Pia tunakuletea muhtasari wa habari za Gaza, Sudan, Uganda na uchambuzi wa neno “PAMBAJIO”.Wakati mgogoro nchini Sudan ukiingia katika mwaka wake wa pili, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kutafuta Ukweli nchini Sudan umezitaka pande zinazokinzana zisitishe mapigano, zilinde raia na kuruhusu mtiririko wa misaada. Taarifa iliyochapishwa leo na OHCHR imemnukuu Mwenyekiti wa ujumbe huo, Mohamed Chande Othman akisema, "Pande zinazopigana Sudan zina wajibu wa kisheria kuwalinda raia, lakini zimeonesha kutojali kufanya hivyo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetangaza kwamba moja ya magari yake jana yakisubiri kuingia kaskazini mwa Gaza lilishambuliwa kwa risasi za moto. Pia UNICEF imechapisha katika ukurasa wake wa mtandao wa X video ya Msemaji wa shirika hilo, Tess Ingram akiwa katika hospitali ya Deir Al Balah, akizungumza kuhusu mtoto Omar mwenye umri wa miaka saba ambaye amelazwa hapo akisumbuliwa na utapiamlo baada ya kula nyasi kwa wiki kadhaa zilizopita. Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limezindua mradi wa thamani ya euro milioni 15 sawa na dola milioni 16.29 unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya (EU) ili kusaidia sekta ya misitu ya Uganda kuchangia kwa uendelevu zaidi kwa uchumi na mazingira. Mpango wa miaka mitano wa Minyororo ya Thamani Endelevu ya malighafi za miti nchini Uganda, unalenga kuhakikisha upatikanaji endelevu wa malighafi halali za miti kutoka katika misitu iliyopandwa, kuongeza uwezo wa usindikaji na mahitaji ya soko ya bidhaa za mbao na kuboresha uwepo na upatikanaji wa ufadhili nafuu.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “PAMBAJIO”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
11-4-2024 • 11 minuten, 7 seconden
Jifunze Kiswahili: Pata uchambuzi wa neno “PAMBAJIO”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “PAMBAJIO”.
11-4-2024 • 1 minuut, 6 seconden
Alice Nderitu: Dunia bado haijajifunza lolote kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi
Miaka 30 iliyopita mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda yaliyoishangaza, dunia yalitokea kuanzia Aprili 7 mwaka 1994 na kudumu kwa siku 100 zilioghubikwa na ukatili wa hali ya juu na mamilioni ya watu kufurushwa makwao. Tangu wakati huo Umoja wa Mataifa umekuwa mstari wa mbele kuchukua hatua kuhakikisha asilani jinamizi hilo halitokei tena popote pale duniani. Manusura wa mauaji hayo wanasemaje kuhusu kumbukumbu hii? Na je dunia imejifunza nini kutokana na mauaji hayo ya Rwanda taifa ambalo limeshafungua ukurasa mpya na kuyapa kisogo? Twende mjini Kigali ambako kumbukumbu kubwa imefanyika mwishoni mwa wiki na itaendelea kwa siku 100, shuhuda wetu ni Eugene Uwimana afisa mawasiliano wa ofisi ya mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda.
9-4-2024 • 6 minuten, 8 seconden
09 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka mjini Kigali ambako kumbukumbu ya mauaji ya kimbari imefanyika mwishoni mwa wiki na itaendelea kwa siku 100. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini.Baada ya huduma ya ulinzi wa amani kwa zaidi ya miaka 20 huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, walinda amani kutoka China, hii leo wameondoka kutoka kambi yao iliyoko nje kidogo ya mji mkuu wa jimbo la Kivu Kusini, Bukavu ambako walishiriki kwa kiasi kikubwa katika ujenzi wa miundombinu.Msemaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Olga Sarrado Mur katika mkutano na waandishi wa habari leo mjini Geneva, Uswisi ameeleza kwamba vita nchini Sudan ikikaribia kutimiza mwaka mmoja kamili na ikiendelea kupamba moto, idadi ya Wasudan waliolazimika kukimbia sasa imepita watu milioni 8.5, huku milioni 1.8 kati yao wakiwa wamevuka mipaka ya nchi. Na kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa leo, idadi ya watu wanaofariki dunia kutokana na virusi vya homa ya ini inaongezeka. Ugonjwa huo ni wa pili kwa kusababisha vifo vya watu milioni 1.3 kwa mwaka, sawa na ugonjwa wa kifua kikuu, ambao ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababisha vifo vingi zaidi kwa sasa. Hata hivyo WHO inasema lengo la kutokomeza Homa ya ini ifikapo 2030 bado linapaswa kufikiwa.Na katika mashinani tutaelekea nchini Sudan Kusini kusikia ujumbe kuhusu hatari vilipuzi na mabomu ya kutegwa ardhini, salia hapo tafadhali.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
9-4-2024 • 10 minuten, 42 seconden
Mariam Suleiman: Wanawake tuna ujuzi, tuna uweo na tunaweza
Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Kutana na Mariam Suleiman ambaye kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR anasema vita ilimfungisha virago Congo DRC hadi hapa kambini Kakuma, ingawa ilimvurugia amani yake haikumkatishia ndoto zake za kuendelea na ufundi wa kuchomelea vyuma na pia kuwa mkufunzi wa kazi hiyo.“Katika kuchomelea vyuma ninafurahia sana kufanyakazi kazi hiyo ninapokwenda kazini na kujikuta ni mwanamke peke yangu uwanjani na hivyo ninajivunia sana kwa sababu sio kazi rahisi kwenda hapo ukiwa mwanamke peke yako katikati ya wanaume 15. Hivyo ninajivunia sana kuwa mchomelea vyuma na mkufunzi wa kuchomelea na kutengeneza vyuma”Kwa Mariam matunda ya kazi yake yako dhahiri.“Moja ya kazi zangu zinazovutia ambazo nimefanya ni lango kuu la kliniki 4”Pamoja na mafanikio hayo Marian anatamani kusoma zaidi kuongeza ujuzi.“Nilisoma hadi daraja la sita hiyo ni ngazi ya Diploma. Natamani kuchimba ndani zaidi ya hii tasnia ya kuchomelea vyuma lakini hapa Kenya hatuna hiyo kozi. Ipo katika taasisi ya uchomeleaji vyuma ya Afrika Kusini. Ningependa kwenda huko na kusoma uchomeleaji vyuma chini ya maji.”Na kwa kuwa yeye ameweza anaamini hakuna kinachomshinda mwanamke kwani“Wanawake tuna uwezo, wanawake tuna ujuzi, wanawake tunaweza kufanyakazi zinazofanywa na wanaume, wanawake tunaweza kufurahia kazi zetu, wanawake hebu tusimame kidete tunaweza”
8-4-2024 • 2 minuten, 7 seconden
Raia nchini DRC wasimulia jinsi wanavyonufaika na miradi iliyofanikishwa na MONUSCO
Kadri siku za MONUSCO kuondoka nchini DRC zinavyokaribia, vivyo hivyo wananchi wanufaika wa miradi iliyofanikishwa na ujumbe huo wanazidi kujitokeza kuelezea hisia zao, kwani ujumbe huo unatakiwa uwe umeondoka nchini humo mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.Miongoni mwa wanufaika ni shule ya msingi Lubumba hapa Kamanyola na Mwalimu Mkuu Texas Chekabiri anaelezea hali ilivyokuwa. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuelezea zaidi katika makala hii.
8-4-2024 • 3 minuten, 4 seconden
08 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ombi la Palestina kujiunga rasmi kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa, na uwezeshaji wa wanake ambapo tunatembelea mkimbizi katika kambi ya Kakuma nchini Kenya. Makalatunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Tanzania.Huko Gaza, watoa misaada ya kibinadamu wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mipango ya Israel kuvamia eneo la Rafah hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Palestina imeanza mchakato wa kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwani hivi sasa ujumbe wake ni uangalizi usioipatia hadhi ya kupiga kura. Mchakato huo unaanzia ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Mwanamke akiwezeshwa anaweza, huo ndio umekuwa usemi wa Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo wanawake kujumishwa katika kila Nyanja ya Maisha ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuchangia katika maendeleo ya jamii. Usemi huo unaungwa mkono na mwanamke mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambaye sasa anaishi Kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Katika makala makala ambapo Assumpta Massoi anatupeleka jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia manufaa ya uwepo wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO ambao sasa unafunga virago baada ya kuhudumu kwa miaka 22.Na katika mashinani tutakuwa Tanzania kuangalia endapo lengo la ujumuishwaji wanawake katika huduma za kifedha litatimia ifikapo mwaka 2030.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
8-4-2024 • 11 minuten, 27 seconden
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili ombi la Palestina kuwa mwanachama
Huko Gaza, watoa misaada ya kibinadamu wakiwa na wasiwasi mkubwa juu ya mipango ya Israel kuvamia eneo la Rafah hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Palestina imeanza mchakato wa kuwa mwanachama rasmi wa Umoja wa Mataifa kwani hivi sasa ujumbe wake ni uangalizi usioipatia hadhi ya kupiga kura. Mchakato huo unaanzia ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Ratiba ya mikutano hii leo hapa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa Baraza la Usalama lenye wajumbe 15 kuanzia saa nne kamili asubuhi mpaka saa sita kamili mchana kwa saa za New York Marekani, litakutana kwanza katika kikao cha faragha na kisha kikao kitafunguliwa kwa umma kusikiliza wanapojadili ombi la Palestina kuwa mwanachama wa Umoja wa Mataifa.Palestina imekuwa ikishiriki katika masuala mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa lakini kwa ngazi ya muangalizi na sasa uongozi wa Palestina inataka hadhi hiyo kubadilishwa na kuwa mwanachama kama wanachama wengine 193 wa Umoja wa Mataifa.Wajumbe katika baraza hilo la UN katika mazungumzo yao watazingatia ombi la Wapalestina la mwaka 2011 baada ya ombi lililowasilishwa kwa njia ya maandishi wiki iliyopita na Bwana Riyad Mansour, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mamlaka ya Palestina ambaye pia ni Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa.Wakati tukisubiri kusikia nini kitajadiliwa na Baraza hilo, huko Ukanda wa Gaza hali bado si hali kwani watoa misada ya kibinadamu wana wasiwasi mkubwa juu ya uvamizi unaopangwa kufanywa na Israel katika eneo la Rafah ambalo limefurika wapalestina waliokimbia kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo kusini, kati na kaskazini mwa Gaza kufuatia mapigano yanayoendelea baina ya wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na wanajeshi wa Israel.Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Misaada ya Kibinadamu katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Jamie McGoldrick, akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa hapo jana alisema kuwa “Mpango unaendelea wa uvamizi wa Rafah, ambao unaweza kusababisha hadi watu 800,000, kuyakimbia makazi yao…. Tulipata tabu sana kuleta mahitaji muhimu hapa kama vitu ambavyo si vyakula, malazi, nyenzo mbalimbali na maji…. Hatuna tena uwezo na rasilimali kwa sasa. Na tunatatizika sana kujiandaa.”Ili kuongeza kiwango cha usaidizi wa kibinadamu kufika eneo hilo, Umoja wa Mataifa unaunga mkono wito wa bandari ya Ashdod ya Israel kufunguliwa tena hulo kaskazini mwa Gaza, ili misaada zaidi ipatikane kupitia nchi ya Jordan.
8-4-2024 • 2 minuten, 24 seconden
UNICEF na jitihada za kuimarisha huduma za Afya ya Akili kwa vijana nchini Rwanda
Makala hii inaeleza safari ya matumaini na uthabiti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNICEF Rwanda linaposhirikiana na Rwanda Biomedical Center (shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya) kuleta mapinduzi katika huduma za afya ya akili kwa vijana. Katika mpango huu wa kutia moyo, UNICEF inavunja vizuizi na kukuza ujasiri kwa kutoa usaidizi muhimu kama vile nasaha shuleni
5-4-2024 • 2 minuten, 54 seconden
Mlo shuleni wawawezesha wasichana kuepuka ndoa za utotoni Sudan Kusini
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP nchini Sudan Kusini kupitia programu yake ya chakula shuleni imefanikiwa kuwasaidi wasichana wengi kuepukana na ndoa za utotoni. Sudan Kusini ni moja kati ya mataifa yenye viwango vya chini vya watu wanaojua kusoma na kuandika hususani kwa wasichana. Jamii katika taifa hilo la afrika ya mashariki huwaoza mabinti ikiwa ni njia moja wapo ya familia kujipatia mali na hivyo mtoto wa kike hujikuta akikosa haki yake ya msingi ya kupata elimu.Huko Kapoeta Mashariki katika jimbo la Equatoria mashariki, shule moja ya msingi ambayo hatutaitaja jina imekuwa kimbilio la wasichana walio katka hatari ya kuolewa katika umri mdogo, mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo ni Grace mwenye umri wa miaka 16 anasema shule hiyo imekuwa nikama peponi.“Nilipokuwa kijijini, wakati baba yangu alikuwa hai, maisha yalikuwa sawa na nilifurahia kila kitu maishani. Lakini mara baada ya baba yangu kufariki, hapo ndipo maisha yangu yakawa magumu, kaka yangu alitaka niolewe katika umri mdogo, na hapo ndipo maisha yakawa magumu”.Grace anasema anachosikita ni kuwa watoto wa kike hawaheshimiki.“Kwa sababu mimi ni mtoto wa kike maisha ya kijijini sio mazuri, tunatazamwa kama chanzo cha utajiri, na sisi ndio tunalazimika kufanya kazi za mashambani, kitu chochote kinachohusiana na shule hakithaminiwi, na hawataki hata kujua ni nini. Wao wanaona kama kitu kisicho na maana, hawajui chochote kuhusu elimu, na hawako tayari kwa hilo”.Hellen Locham ni mwalimu wa shule anayosoma Grace na anasema wamekuwa wakihamasisha jamii kuhusu umuhimu wa shule kwa wasichana.“Hawa wasichana wanaitwa "washindi" kwa sababu wasichana hawa wanalazimishwa kuolewa wakiwa na umri wa miaka 9, na wengine huposwa wangali wadogo, na walifanikiwa kukimbia vijijini, wakiteseka njiani na wamefanikiwa kuja shuleni”. Tumekuwa tukiwaambia watu ikiwa unapata msichana ambaye anapitia changamoto, msichana ambaye amelazimishwa kuolewa, wanaweza kupata elimu wanayotaka".Mwalimu Hellen Locham anasema mbali na shule kupokea wasichana lakini wanalishukuru zaidi shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani kwa kuwawezesha kupata chakula shuleni. Chakula kuwa shuleni ni muhimu sana, ikiwa hakuna chakula na haujala kitu huwezi kuwa katika nafasi ya kuwa darasani, huwezi kufanya chochote, WFP imesaidia sana shule hii, wakati wa likizo hali inekuwa ngumu kwa wasichana hawa kuwa shuleni ikiwa hakuna chakula. Wengi wao wangaliweza kukimbia, wangaliweza kurudi makwao, wangesema bora niende kuteseka kuliko kufa hapa kwa njaa.WFP inaendelea kusaidia wasichana walio hatarini zaidi kwa kuwaatia msaada wa chakula shuleni wakati wa likizo.
5-4-2024 • 3 minuten, 2 seconden
05 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia vita katika Ukanda wa Gaza ukielekea miezi siti hapo kesho, na programu ya mlo shuleni nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na mashinani nchini DRC, kulikoni?”.Kesho kutwa jumapili ikiwa ndio itatimu miezi sita ya mzozo wa Gaza, huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani akirejelea wito wake wa sitisho la mapigano kwa misinigi ya kiutu, kuachiliwa kwa mateka wote bila masharti, ulinzi wa raia na misaada ya kiutu ifikie walengwa bila vikwazo vyovyote huku akikgusia pia Israeli kutumia akili mnemba kwenye operesheni zake.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP nchini Sudan Kusini kupitia programu yake ya chakula shuleni imefanikiwa kuwasaidi wasichana wengi kuepukana na ndoa za utotoni. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka nchini Rwanda kusikia programu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Rwanda kudhibiti tatizo la changamoto ya afya ya akili kwa vijana balehe.Na katika mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC kusikia simulizi ya mkimbizi wa ndani”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
5-4-2024 • 11 minuten, 58 seconden
Kuelekea miezi 6 ya mzozo wa Gaza, Guterres apinga matumizi ya akili mnemba kusaka wahalifu
Kesho kutwa jumapili ikiwa ndio itatimu miezi sita ya mzozo wa Gaza, huko Mashariki ya Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani akirejelea wito wake wa sitisho la mapigano kwa misinigi ya kiutu, kuachiliwa kwa mateka wote bila masharti, ulinzi wa raia na misaada ya kiutu ifikie walengwa bila vikwazo vyovyote huku akikgusia pia Israeli kutumia akili mnemba kwenye operesheni zake. Guterres akianza hotuba yake kwa kuelezea kuwa Jumapili hii inatimu miezi sita tangu mashambulizi hayo na kuelezea kuwa tarehe 7 Oktoba ni siku ya machungu kwa Israel na dunia, kwani Umoja wa Mataifa na yeye binafsi wanaomboleza vifo vya waisrael 1,200 waliouawa hadi sasa. Hakuna kinachohalalisha mashambulizi yale ya Hamas, amesema Guterres akisema pia katika kipindi cha miezi sita pia wapalestina zaidi ya 32,000 wameuawa na wengine zaid iya 75,000 wamejeruhiwa. Maisha ya watu yametwamishwa na heshima ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu imesambaratishwa.Akarejelea ziara yake ya hivi karibuni kwenye kivuko cha Rafah ambako anasema nilikutana na wasaidizi wa kiutu wabobezi walionieleza wazi kuwa janga hili na machungu ya Gaza si ya kawaida na hawajawahi kushuhudia kokote.Na zaidi ya yote anasema aliona misururu mirefu ya malori yenye shehena za misaada yakiwa yamezuiwa kuingia Gaza.Anasema pindi milango ya misaada inapofungwa, milango ya njaa inafunguliwa. Zaidi ya watu milioni moja wanakabiliwa na njaa. Watoto hivi sasa wanakuga kwa njaa na kukosa maji. Hakuna kinachohalalisha adhabu hii ya jumla kwa wananchi wa Palestina.Ameelezea pia kuchukizwa na kitendo cha Israel kutumia Akili Mnemba kusaka wahalifu Gaza tena kwenye maeneo yenye watu wengi.Akili Mnemba inapaswa kutumika kwa manufaa na sio kuchangia kwenye kusongesha vita.Amekumbusha kuwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kiraia na waandishi wa habari nao wameuawa kwenye mzozo huo. Na zaidi ya yote.Vita dhidi ya habari imeongeza machungu.. kuficha ukweli na kurushiana lawama. Kuwanyima waandishi wa habari wa kimataifa kibali cha kuingia Gaza kunaruhusu kusambaa kwa habari potofu na za uongo.Ametamatisha hotuba yake ya dakika 7 kwa kutaka pia uchunguzi huru wa kilichotokea Gaza, utekelezaji wa kikamilifu wa azimio la wiki iliyopita la Baraza la Usalama la kutaka sitisho la mapigano na misaada ifikie walengwa kwani baa la njaa linajongea Gaza.
5-4-2024 • 2 minuten, 40 seconden
Ujumuishwaji wa wanawake katika huduma za kifedha ni muhimu - Nangi Massawe, Benki Kuu Tanzania
Lengo namba 5 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa au SDG5 linahimiza kila nchi kuhakikisha wanawake wanawezeshwa na kujumuishwa katika kila nyanja ya Maisha ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 hawasalii nyuma katika maendeleo.Moja ya masuala yanayotiliwa msukumo zaidi hivi sasa ni ujumuishwaji wa wanwake katika masuala ya huduma za kifedha n anchi nyingi zimeanza kuchukua hatua ikiwemo Tanzania. Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na Nangi Moses Massawe kutoka Benki Kuu ya Tanzania ambaye ni meneja wa kitengo cha huduma jumuishi za kifedha.
4-4-2024 • 10 minuten, 23 seconden
Jifunze Kiswahili: Tofauti ya maneno “Adhuhuri na Alasiri.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhuhuri na Alasiri.”
4-4-2024 • 1 minuut, 11 seconden
04 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia ujumuishwaji wa wanawake katika masuala ya kifedha kwa lengo la kutimiza lengo la Umoja wa Mataifa la usawa wa kijinsia katika Nyanja zote. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na katika kujifunza kiswahili tunakuletea ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhuhuri na Alasiri”.Leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na msaada wa kuchukua hatua dhidi ya mabomu hayo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mabomu, vilipuzi na vifaa vingine vya mlipuko vinaendelea kuua na kujeruhi watu katika maeneo mengi yenye changamoto kubwa za migogoro duniani na matokeo yake vifaa hivyo vya mlipuko, kwa wastani hukatili maisha ya mtu mmoja kila saa, na waathirika wakubwa wakiwa ni watoto.Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Jamie McGoldrick anaelekea Gaza leo. Umoja wa Mataifa unaeleza kuwa mapigano makali kati ya wanajeshi wa Israel na makundi yenye silaha ya Palestina yanaendelea kuripotiwa katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza. Mfumo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) wa Ufuatiliaji kuhusu Mashambulizi dhidi ya Huduma za Afya (SSA) wameeleza kuwa inatia wasiwasi kwamba nchini Ukraine wahudumu wa afya katika gari za wagonjwa na wafanyakazi wengine wanaotoa huduma za usafiri wa afya wanakabiliwa na hatari ya kujeruhiwa na kifo mara 3 zaidi ya ile ya wafanyakazi wengine wa huduma za afya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhuhuri na Alasiri.”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
4-4-2024 • 11 minuten, 7 seconden
UNCTAD, UNECA, Kenya kuunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia upatu lengo namba tano la Malengo Endelevu ya Umoja huo linalohimiza usawa kwa wote katika nyanja zote ifikapo mwaka 2030. Hata hivyo ili kuelewa jinsi biashara inavyoathiri wanaume na wanawake ni muhimu kuunda sera za biashara zinazojumuisha zaidi na zenye usawa ambazo zinakuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wote,hii inahitaji takwimu nzuri za kitaifa kuhusu jinsia katika biashara.Kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD na Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kiuchumi ya Afrika UNECA, Kenya inaunda viashirio vipya vya kupima usawa wa kijinsia katika sekta ya biashara. Evarist Mapesa amefuatilia taarifa hiyo kwa kina na kutuandalia makala hii.
3-4-2024 • 3 minuten, 8 seconden
Mbinu za medani tulizopatiwa ni za kimataifa- Afisa FARDC
Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali. Je, FARDC linajengewa uwezo gani? Assumpta Massoi anafafanua zaidi.Hapa si uwanja wa vita bali ni uwanja wa mazoezi! Wanajeshi 30 wa FARDC au jeshi la serikali nchini DRC wakiwa kwenye mafunzo ya kulenga shabaha. Mbele kuna karatasi lililochorwa binadamu na sasa wanatakiwa kulenga maeneo mbali mbali ya mwili yaliyowekwa alama.Ni mbinu wanazopatiwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Brazil, hapa Beni jimboni Kivu Kaskazini ili waweze kukabiliana na waasi kwenye maeneo misituni. Kapteni Rombaut Mukoka ni Afisa wa jeshi la FARDC na anasema, “Mafunzo haya ni muhimu sana. Yanapaswa kuendelea ili hatimaye wanajeshi wetu waweze kunufaika. Hizi mbinu walizojifunza ni mpya sana kwetu na zinatambulika katika medani za kimataifa.”Mafunzo ya kulenga shabaha yanaendelea na kisha mkufunzi kutoka Brazil anajongea kwenye picha ile akiwa na mmoja wa wanafunzi ili kuonesha ni wapi haswa wanapaswa kulenga.Jenerali Luciano Alfred Matamba ni Mkuu wa kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha MONUSCO mjini Beni na anafafanua lengo la mafunzo hayo yaliyofanyika kwa wiki tatu.“Lengo la mafunzo haya ni kuwapatia mbinu na ufundi za kuendesha operesheni msituni. Kama unavyofahamu hapa Kivu Kaskazini tuko kwenye eneo la operesheni ambalo kwa kiasi kikubwa ni pori na mashambulizi yanayofanywa na waasi wa ADF yanahitaji mbinu mtu kuwa na hizo mbinu za kupigana msituni. FARDC [EF EI AR DE SE] ni wadau wetu ambao tunapaswa kushirikiana nao kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa namba 2717 [Mbili Saba Moja Saba]. Ni pale tu ambapo tutajifunza pamoja na kuwa na mbinu sawa ndio tutaweza kutatua matatizo yaliyoko hapa.”
3-4-2024 • 2 minuten, 12 seconden
03 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo kwa mara nyingine yameonya kwamba bila dalili zozote za usitishaji mapigano Gaza hali ya kibinadamu inaendelea kuwa janga huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kukatili maisha, kufurusha watu na kusababisha uharibifu usioelezeka na njaa nayo ikiongeza hofu ya hatma ya watu wa eneo hilo.Siku zikizidi kuhesabiwa kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, kuondoka nchini humo, ujumbe huo unaendelea kutekeleza wajibu wake wa kujengea uwezo jeshi la serikali, FARDC kuweza kukabili vikundi vilivyojihami ambavyo vinatajwa kuhusika na asilimia 65 ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo mwezi Februari mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na serikali. Makala inatupeleka nchini kenya ambako serikali ya nchi hiyo kwa kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa wanaunda viashiria vipya ya kupima usawa wa kijinsia katika biashara.Na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu jinsi ambavyo miradi ya maji mkoani Kigoma inavyowasaidia wanfunzi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
3-4-2024 • 11 minuten, 24 seconden
UN - Bila usitishaji mapigano hali ya kibinadamu inaendelea kuwa tete Gaza
Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo kwa mara nyingine yameonya kwamba bila dalili zozote za usitishaji mapigano Gaza hali ya kibinadamu inaendelea kuwa janga huku mashambulizi ya Israel yakiendelea kukatili maisha, kufurusha watu na kusababisha uharibifu usioelezeka na njaa nayo ikiongeza hofu ya hatma ya watu wa eneo hilo. Asante Anold kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA usiku wa kuamkia leo makombora ya Israel yameendelea kuvurumishwa kuelekea Gaza Kaskazini, Khan Younis na Rafah ambako takriban Wapalestina milioni 1.2 sasa wanaishi katika makazi rasmi na yasiyo rasmi na hivyo kuwaongezea hofu ya mustakbali wa maisha yao.Pia shirika hilo linasema fursa ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wenye uhitaji mkubwa bado ni mtihani hasa kutokana na mamlaka ya Israel kuendelea kulinyima vibali shirika la UNRWA kufikisha msaada muhimu wa chakula na mahitaji mengine hasa Gaza Kaskazini.Hatua hiyo kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA imezidisha njaa kwa watu ambao tayari wako taaban na mapigano yanayoendelea. Tangu Machi mosi OCHA inasema Israel imekataa kuruhusu asilimia 30 ya operesheni za kibinadamu Gaza Kaskazini na kuathiri kwa kiasi kikubwa operesheni za UNRWA.Watoto 27 wameripotiwa kufa njaa kutokana na utapiamlo hadi sasa huku shirika la Kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF likionya kwamba Maisha ya maelfu wengine yako hatarini ukizingatia ukweli kwamba tangu Oktoba 7 mwaka jana watoto zaidi ya 13,000 wameuawa kutokana na vita inayoendelea lakini njaa nayo ni tishio kubwa.Kuhusu uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na vita inayoendelea ripoti ya pamoja ya tathimini ya Umoja wa Mataifa na Benk ya Dunia iliyotolewa leo inasema uharibifu huo unakadiriwa kuwa takriban dola bilioni 18.5 ambao ni sawa na asilimia 97 ya pato la taifa la Ukingo wa Magharibi na Gaza kwa mwaka 2022.Na hapa Makao Makuu leo Umoja wa mataifa umepokea barua rasmi kutoka kwa mamlaka ya Palestina ikiomba kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa badala ya nafasi ya uangalizi iliyonayo sasa.
3-4-2024 • 2 minuten, 31 seconden
Bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kote duniani - Paulina Ngurumwa
Kinara wa elimu nchini Tanzania Paulina Ngurumwa anasema bado kazi ipo kupigania haki za mwanamke kwa hiyo harakati hizo hazitakiwi kupoa. Paulina Ngurumwa ni mwanaharakati wa haki za kijamii kupitia shirika la KINNAPA Development Programme. KINNAPA Development Programme ni shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara, kaskazini mwa Tanzania likiwa ni chombo cha kutatua matatizo yao hasa ya ardhi. Shirika hili lilianzishwa mwaka 1992 na kwa miaka hiyo yote linajivunia kuendelea kufanikisha malengo yake na sasa hata limepanua mawanda ya huduma zake kama anavyoeleza mmoja wa viongozi Paulina Nguruma, katika mahojiano aliyoyafanya na Anold Kayanda wa Idhaa hii hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa.
2-4-2024 • 5 minuten, 51 seconden
02 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika harakati za kuwainua wanawake na wasichana nchini Tanzania Tanzania, ambapo Paulina Ngurumwa kutoka KINNAPA Development Programme, shirika lisilo la kiserikali lililoanzishwa na wanajamii ya Wilaya ya Kiteto, Mkoani Manyara anazungumza na Anold Kayanda wa idhaa hii. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Leo maafisa wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wamelaani vikali mauaji ya wafanyakazi wa misaada 7 wa shirika lisilo la kiselikali au NGO la World Central Kitchen yaliyofanywa na jeshi la Israel, maafisa hao wakirejea kueleza hofu yao kwamba hakuna mahali palipo salia kuwa salama Gaza.Tume ya pamoja ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya UNJHRO imesema kumekuwa na ongezeko la asilimia 14 ya visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini DRC. Leo ni siku ya kimataifa ya kuelimishana kuhusu usonji maudhui yakiwa kutoka kuishi kuelekea kwenye ustawi, kwa watu wenye usonji au kwa kiingereza Autism, ambapo kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, usonji hukumba mtoto mmoja kati ya kila watoto 160 duniani.Na mashinani tunaelekea Gaza kuona ni kwa jinsi gani mashambulizi ya Israel ya hivi majuzi yameathiri huduma za afya katika hospitali ya Al-Shifa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
2-4-2024 • 11 minuten, 38 seconden
Mradi wa maji warejesha matumaini kwa familia Wajir
Maji ni uhai, ni kauli mbiu ya miaka nenda rudi, lakini imesalia ndoto kwa wengi duniani hasa wakati huu mabadiliko ya tabianchi yanachochea ukame unaovuruga maisha ya binadamu, wanyama na mimea. Nchini Kenya katika kaunti ya Wajir, iliyoko kaskazini-mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, uhaba wa maji ulisababisha familia kupoteza mifugo yao, mazao kukauka na ustawi wa jamii kutoweka. Lakini shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, kwa kushirikiana na serikali ya Kaunti walianzisha mradi wa ujenzi wa kuchimba visima wa Giriftu kwa ili jamii iwe na uhakika wa kupata maji wakati wowote. Mradi umezaa matunda na ndio msingi wa makala yetu ya leo inayoletwa na Assumpta Massoi.
1-4-2024 • 4 minuten, 24 seconden
Griffiths: Jaribio la kuitenga UNRWA lazima likome
Mratibu Mkuu wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za Kibinadamu Gaza hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome. Bwana Griffiths ametoa kauli hiyo leo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X zamani Twitter akisistiza kuwa juhudi zozote za kusambaza misaada ya kibindamu kwenye Ukanda wa Gaza bila kupitia shirika la UNRWA haziwezi kufanikiwa na watu zaidi ya milioni 2 wanaitegemea UNRWA ili kuendelea kuishi. Ameendelea kusema kwamba hadi sasa hakuna shirika lingine lolote lenye uwezo wa kufika kila kona ya Gaza, uzowefu na imani ya jamii ya kutekeleza majukumu yake kama lilivyo shirika la UNRWA.Wakati huohuo shirika la UNRWA limeonya kwamba mashambulizi ya Israel yameendelea tena usiku wa kuamkia leo huko Gaza Kaskazini Khan Younis na Rafah ambako watu milioni 1.2 wanapata hifadhi na kusababisha vifo zaidi.Huku lile la afya la Umoja wa Mataifa WHO likisema wakati timu yake ikiwa katika operesheni ya kibinadamu katika hospital ya Al-Aqsa jana Jumapili maeneo ya hospital yalipigwa na shambulio la anga lililokatili maiasha ya watu 4 na kujeruhi wengine 17.Nalo shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linajitahidi kwa kila hali kutoa msaada wa chakula unaohitajika sana kwa watu milioni 1.45 Gaza lakini msaada huo hautoshi na bila usitishaji vita hawawezi kumfikia kila mtu na hivyo kufanya Maisha ya watu wengi kusalia hatarini.
1-4-2024 • 1 minuut, 49 seconden
01 APRILI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu Gaza, na jitihada za kukabili habari potofu nchini DR Congo. Makala tunaku[eleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Mratibu Mkuu wa Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths amesema shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ni uti wa mgongo wa operesheni za Kibinadamu Gaza hivyo jaribio la kulitenga shirika hilo lazima likome.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kituo kilichojengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kimesaidia vijana kukabiliana na habari potofu na za uongo ambazo huchochea ukosefu wa amani kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika. Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Kenya, anakupeleka kaunti ya Wajir kuona jinsi mradi wa maji ulivyoleta matumaini kwa familia na jamii.Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu afya kwa watoto.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
1-4-2024 • 11 minuten, 10 seconden
Kituo cha amani DR Congo chakabili habari potofu na za uongo
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kituo kilichojengwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO kimesaidia vijana kukabiliana na habari potofu na za uongo ambazo huchochea ukosefu wa amani kwenye taifa hilo la Maziwa Makuu barani Afrika. Jean Claude Batumike, ambaye ni Mkuu wa kituo cha vijana cha Amani, kilichoko eneo la Kamanyola huko jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akizungumza kupitia video ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye mtandao wa Instagram anasema kituo hicho kilipojengwa watu walijihisi wako na amani zaidi.Anasema kituo cha amani kilijengwa kwa ajili ya amani ili kuondoa migogoro kwa vijana na jamii kwa ujumla. Kituo kina kompyuta, mtandao wa intaneti wakati wote na skrini kubwa ambapo katika video hiyo wanaonekana vijana wakipita hapa na pale huku wakipatiwa maelezo na Bwana Batumike.Akilinganisha hali kabla na baada ya kujengwa kwa kituo hicho, Bwana Batumike anasema, “mara nyingi wakati tulikuwa na mizozo hapa kwenye eneo letu, hakukuweko na mahali ambapo watu wanaweza kwenda na kutatua mizozo, lakini tangu wamejenga hiki kituo cha Amani, kushikakuweko na mzozo wa vijana au jamii, wanakimbilia kituo cha Amani, wanakaa pamoja na kutatua mizozo na hatimaye mambo yanakuwa mazuri zaidi.”Bwana Batumike akaelezea kuwa kituo cha Amani kinasaidia kukabili habari za uongo na potofu kwa kuwa kituo kina mtandao wa uhakika wa intaneti, kompyuta na skrini na wanaweza kupata habar iza ukweli.“Mara nyingi vijana wanapokuwa na habari za wasiwasi ambazo hawana uhakika nazo ni rahisi kufika kituo cha Amani, wanajiunganisha kwenye intaneti, wanarambaza na kusogoa na wengine kwa mtandao na kupata habari za ukweli. Na katika sehemu yenye mzozo, unahitaji kupata habari za uhakika,” anasema Bwana Batumike.
1-4-2024 • 2 minuten, 3 seconden
Kituo cha malezi ya watoto nchini Kenya chatekeleza azma ya Umoja wa Mataifa
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ulifunga pazia hivi majuzi jijini New York Marekani ukipigia chepuo uwekezaji kwa wanawake na wasichana, na leo tunabisha hodi nchini Kenya wasichana waliokumbwa na ujauzito utotoni na kukatishwa ndoto za kuendelea na masomo au kupata ajira wamepata jawabu la changamoto wanazokumbana nazo pindi wakijifungua watoto wao. Changamoto kama vile mahali pa kumwacha mtoto kwa malezi ili aweze kuendelea na shule au kupata ajira. Umoja wa Mataifa unasema kila mtu ana haki ya elimu hata kama amepata changamoto gani maishani. Na ndipo ushirikiano kati ya mashirika ya kiraia lile la “Work for life”, pamoja na lile la “A Pack a Month”, linalohusika na utoaji wa misaada mbali mbali ikiwemo taulo za kike kwa wazazi wenye mahitaji na wasichana wanaokwenda shule walizindua kituo cha malezi ya watoto wachanga nyakati za mchana katika mitaa ya Kibera jijini Nairobi, Kenya. Mradi unaungwa mkono na wadau kadhaa ikiwemo serikali ya Kenya. Selina Jerobon ni msimulizi wetu kupitia mada hii iliyofanikishwa na Redio washirika DOMUS ya huko Kenya.
28-3-2024 • 7 minuten, 35 seconden
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno “UDENDA”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “UDENDA”.
28-3-2024 • 1 minuut
28 MACHI 2024
Hii leo jaridani tnakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kufuatilia jitihada za mashirika za kuhahikisha watoto waathrika wa mimba za utotoni wameweza kurejea shule. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Gaza, Haiti na wakimbizi wakimbizi wa Sudan Kusini. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunapata maana ya neno “UDENDA.” Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina (UNRWA) leo Machi 28 limetahadharisha kuhusu ujio wa baa la njaa katika Ukanda wa Gaza. UNRWA imesema yenyewe ni uti wa mgongo wa misaada ya kibinadamu Gaza lakini bado misafara yao ya chakula imezuiwa kufika kaskazini, ambako baa la njaa linajongea. Wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limesema kati ya hospitali 36 katika Ukanda wa Gaza, ni 10 tu ambazo zimesalia zikifanya kazi japo nazo kwa kiasi kidogo.Ripoti ya Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo inataka hatua za haraka na za ujasiri ili kukabiliana na hali ya "janga" nchini Haiti. Ripoti imeeleza kuwa magenge yanaendelea kutumia unyanyasaji wa kingono kuwatendea unyama, kuwaadhibu na kuwadhibiti watu. Wanawake wamebakwa hata baada ya kushuhudia waume zao wakiuawa mbele yao. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), pamoja na wadau wake 123, Alhamis ya leo limetangaza kuwa linatafuta dola bilioni 1.4 mwaka huu ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi milioni 2.3 wa Sudan Kusini wanaoishi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ethiopia, Kenya, Sudan na Uganda. Janga la wakimbizi wa Sudan Kusini linasalia kuwa ndilo kubwa zaidi barani Afrika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “UDENDA”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
28-3-2024 • 11 minuten, 29 seconden
Simulizi za raia wanaokimbia mashambulizi kaskazini mwa Msumbiji
Mgogoro ambao hauripotiwi sana kaskazini mwa Msumbiji umesababisha mamia kwa maelfu ya familia kuwa wakimbizi, ambao wanaendelea kutatizika kutafuta chakula, malazi na usalama. Anold Kayanda anasimulia zaidi katika makala hii.
27-3-2024 • 3 minuten, 13 seconden
Innoss B kushirikiana na WFP kusongesha lishe na elimu DRC
Mwanamuziki Innocent Balume, al maaruf Innoss’B ametangazwa kuwa muungaji mkono wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP katika kusongesha milo yenye afya na lishe bora nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Nimeshuhudia njaa mara nyingi sana wakati wa utoto wangu, kabla ya kwenda shule tulikuwa na njaa na kabla ya kulala tulikuwa na njaa, ndivyo asemavyo mwanamuziki Innocent Balume, al maaruf Innoss’B ambaye ametangazwa kuwa muungaji mkono wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP katika kusongesha milo yenye afya na lishe bora nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Taarifa ya WFP iliyotolewa Kinshasa, mji mkuu wa DRC imemnukuu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Cindy McCain akisema “ninafurahia sana kumkaribisha kwenye timu yetu ya WFP, tukiwa na Innos tutaweza kuwa na athari chanya kwenye vita dhidi ya njaa na utapiamlo DRC.” Innos amenukuliwa akisema njaa ilikuwa sehemu ya maisha yake wakati akiwa mtoto na kwamba “kila siku unalazimika kufirikia leo nitakula vipi? Nitapataje chakula hii leo? Hakukuwa na matumaini.” Sasa mwanamuziki huyu aliyejipatia umaarufu sio tu nchini mwake bali pia Afrika na dunia nzima kutokana na mitindo yake ya AfroBeat na Rumba amepatiwa jukumu na WFP kutumia muziki wake kuelimisha jamii umuhimu wa lishe bora na elimu nchini mwake DRC. Innos ambaye ni mzaliwa wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC, anasema njaa ilikuwa kichocheo cha muziki na hivyo aliona ana deni kwa jamii yake ya kusaidia kuongeza uelewa na hamasa kuhusu tatizo hilo. Kupitia video ya WFP Innoss’B akiwa kwenye moja ya mashamba ya mboga za majani nchini DRC, akiambatana na wanawake na kwingine akiwa na wanafunzi anasema, “leo nina furaha kwa sababu kwa mara moja nina fursa ya kuwa karibu na jambo ambalo linanigusa mno. Kuhakikisha kila mtu ana afya njema . Kuhakikisha kila mtu ana nguvu, kuhakikisha kila mtu anaweza kupata chakula. Ujumbe huo utasikika . Hivyo niña furaha sana, hii itakuwa ni safari nzuri. Nina furaha.” Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, ambaye kwa mara ya kwanza alikutana na Innoss’B mjini Goma, miaka 14 iliyopita, wakati huo Innoss akiwa na umri wa miaka 13, amesema amekuwa anajivunia sana kuona kila kitu alichofanikiwa kama msanii na msongeshaji wa utu wa kibinadamu.Amesema kujituma kwake katika kujenga mustakabali bora kwa wananchi wa DRC ni hamasa ya dhati. Innos anasema anaamini kwenye nguvu ya muziki na utamaduni katika kuleta mabadiliko chanya. Kushirikiana na WFP kunaniruhusu kuchangia katika kutatua masuala nyeti ya lishe na elimu nchini mwangu. Kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko yenye maana kwa maisha ya vijana.”Peter Musoko ambaye ni Mwakilishi Mkazi wa WFP nchini DRC anasema wanafuraha kubwa kushirikiana na Innos’B na kutumia nguvu ya muziki kusongesha ustawi wa DRC na wananchi wake. “Kwa kuunganisha nguvu, tunaweza kuchochea hatua chanya na kutatua changamoto kubwa ya utapiamlo na ukosefu wa uhakika wa chakula.”Wakati huu ambapo WFP inaendelea na jitihada za kuimarisha uhakika wa kupata chakula DRC, ushirikiano na Innoss’B unaongeza sauti muhimu katika kampeni hiyo.Hata hivyo WFP inasema ukata ni tatizo kwa sasa kwani bajeti yake kwa DRC ina pengo la dola milioni 548.5, fedha ambazo zinahitajika kwa kipindi cha miezi sita ijayo kuweza kukidhi mahitaji ya kiutu yanayoongezeka kila uchao.
27-3-2024 • 2 minuten, 6 seconden
27 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia jitihada za kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia, na mchango wa wasanii katika msaada wa kibinandamu nchini DRC. Makala tunamulika mgogoro ambao hauripotiwi sana kaskazini mwa Msumbiji na mashinani tunasalia nchini DRC, kulikoni?Juhudi na ushirikiano wa pamoja wa wahudumu wa afya, vituo na Jamii, vimefanikisha kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia kwa mujibu wa Shirika Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO nchini Zambia, ambalo limeeleza kwamba ugunduzi wa mapema na matibabu husaidia kukabiliana na ugonjwa huo na kupunguza idadi ya vifo.Mwanamuziki Innocent Balume, al maaruf Innoss’B ametangazwa kuwa muungaji mkono wa ngazi ya juu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP katika kusongesha milo yenye afya na lishe bora nchini mwake Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala tunaangazia mgogoro ambao hauripotiwi sana kaskazini mwa Msumbiji umesababisha mamia kwa maelfu ya familia kuwa wakimbizi, ambao wanaendelea kutatizika kutafuta chakula, malazi na usalama.Na mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC kusikia ujumbe wa mlinda amani wa kuhusu elimu kwa wasichana.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
27-3-2024 • 11 minuten, 8 seconden
WHO Zambia yashirikiana na Serikali kutokomeza Kipindupindu
Juhudi na ushirikiano wa pamoja wa wahudumu wa afya, vituo na Jamii, vimefanikisha kukomesha mlipuko wa kipindupindu uliozuka nchini Zambia kwa mujibu wa Shirika Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO nchini Zambia, ambalo limeeleza kwamba ugunduzi wa mapema na matibabu husaidia kukabiliana na ugonjwa huo na kupunguza idadi ya vifo. Jioni moja Philta Samazimva alilalamika ghafla tumbo kuuma, baada ya kuharisha sana, mama yake mzazi Hildar Samazimba alimpeleka kliniki.Baadhi ya watu hapa walisema usiende hospitali mtoto atapona, hakuna kitu watakachompatia mtoto na atakufa. Lakini nilipoona jinsi mtoto wangu alivyokuwa anaonekana, nilisema wacha niwahi kliniki.Philta alipelekwa kwenye kituo cha matibabu cha Heroes Cholera, ambapo alipata ahueni baada ya matibabu. Dr Mavis Chisala, Ni Daktari wa magonjwa ya watoto katika kituo cha kutibu kipindupindu cha Mashujaa. "Tumekuwa tukihakikisha tunamfuatilia mgonjwa wetu, kwa sababu kwa watoto wanaimarika haraka sana unapochukua hatua sahihi kwa wakati muafaka.Kiwango cha vifo vya wagonjwa wa kipindupindu katika vituo vya afya ni asilimia 1.3, ikilinganishwa na asilimia 3.3 kwa ujumla, kutokana na kazi inayofanywa na matabibu hao kwa ushirikiano na WHO ambao umerejesha matumaini kwa Samazimba “ kikubwa tulifanya kazi kwa ushirikiano, ninawashukuru Wauguzi, matabibu kwa kazi waliyoifanya, kwasababu sikujua kama mtoto wangu ataponaWHO imeisaidia wizara ya afya nchini Zambia kurekebisha miongozo ya huduma za kliniki na kununua vifaa tiba na vifaa vingine kwa ajili ya kukabiliana na mlipuko wa kipindupindu. Dkt. Kalima Nawa, kiongozi mkuu wa kituo cha matibabu cha mashujaa wa kipindupindu anasema Hold under……03 sec “tunatarajia kuendelea kufanya kazi na WHO katika mlipuko huu, na pia kupanga kwa ajili ya milipuko ya baadaye na kutusaidia kujiandaa kwa hayo”.Kipindupindu kinatibika kwa urahisi iwapo kitagunduliwa kwa wakati.
27-3-2024 • 2 minuten, 9 seconden
26 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DR Congo ambako Umoja wa Mataifa unasema wananchi milioni 23.4 wanakabiliwa na njaa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu SEA, machafuko DRC na vifo vya wahamiaji. Mashinani inamulika miradi ya maji nchini Tanzania. Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Hatua Maalum za Ulinzi dhidi ya Unyonyaji na Unyanyasaji wa Kingono imewekwa wazi hii leo.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR) limetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kutokana na ongezeko la hatari kwa watu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Na wakati mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) unaohusu Wahamiaji Wasiofahamika waliko ukitimiza miaka kumi, ripoti mpya ya shirika hilo iliyopewa jina ‘Muongo mmoja wa kukusanya taarifa za vifo vya wahamiaji’ inaonesha mienendo ya kutisha ya vifo na kupotea kwa wahamiaji katika muongo mmoja uliopita na kwamba mtu mmoja kati ya watatu hufariki duniani katika harakati za kukimbia migogoro katika nchi yake.Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Mhandisi Denis Arbogast, Msimamizi wa mradi wa maji Kasulu mkoani Kigoma nchini Tanzania, mradi inayofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
26-3-2024 • 10 minuten, 35 seconden
Nyumba salama kwa waathirika wa unyanyasaji wa kingono Sudan Kusini
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wadau wake wamefungua nyumba salama huko Andari Magharibi katika jimbo la Equatoria kwa ajili ya kusaidia manusura wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro nchini humo. Leah Mushi na maelezo zaidi.Kwa mujibu wa Mkuu wa zamani wa UNMISS ofisi ya Yambio, Christopher Muchiri Murenga, mradi huu ulioanzishwa na kitengo cha ushauri cha ulinzi wa wanawake cha UNMISS na umefadhiliwa na Muungano wa Ulaya pamoja na Shirika la Rural Action Aid lengo likiwa ni kuwasaidia waathirika wa unyanyasji wa kijinsia unaohusiana na migogoro.Bwana Murenga anasema,“kama sehemu ya kutafuta amani ya kudumu na jumuishi nchini Sudan Kusini, imebidi tuwalete manusura pamoja ili waweze kuponya majeraha yao. Kisha watakuwa wanajamii wenye tija, wakichangia ustawi wa kijamii na kiuchumi wa serikali.”Kituo hiki kinatoa ushauri nasaha, kuponya watu wenye kiwewe pamoja na mafunzo ya stadi za maisha na kinalenga kusaidia manusura 195. Mmoja wa wanufaika ni Azande ambaye katika video ya UNMISS amefichwa sura yake wakati akieleza masahibu aliyopitia akisema, “tulipotoka porini nilikuwa na kiwewe, walitupa ushauri nasaha na mawazo yote mabaya yaliyokuwa akilini mwangu yaliondoka na sasa niko thabiti zaidi. Mimi ni miongoni mwa wale ambao sasa wanajifunza ushonaji. Wakati nipo msituni nilijifungua mtoto wa kike sasa ana umri wa miaka 6. Ana matatizo ya tumbo kwa sababu wakati mjamzito nilikuwa nakula vitu vya hatari ndio maana sasa naomba msaada wa dawa kwa ajili yake.”Kiongozi wa kikundi cha wanawake katika eneo la Ezo Henrica Elias anasema nyumba hii itasaidia wasichana na wanawake wengi sana kwa kuwa, “kituo hiki ni kama ndoto inayotimia, imetuletea furaha ambayo hatuwezi kuieleza. Yaliyotusibu sisi wanawake na wasichana wakati wa mzozo ni yakutisha. Mambo mengi mabaya yalitendeka katika vijiji vyetu, ambapo wasichana wadogo na wavulana pia walitekwa nyara.”Migogoro nchini Sudan Kusini imesababisha tajriba ya kuhuzunisha kwa vijana wengi wa kike na wa kiume, hasa wale ambao walilazimika kujiunga na makundi yenye silaha nchini humo.
25-3-2024 • 1 minuut, 55 seconden
Guterres: Tekelezeni kikamilifu mkataba wa mwaka 1994 wa kuwalinda wafanyakazi wa UN
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Walio vizuizini na wasiofahamika waliko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa ulimwengu kuenzi ujasiri na kujitolea kwa wafanyakazi wanaotoa huduma za kibinadamu kila mahali kokote waliko kwa kuahidi kuwalinda na kuwaunga mkono wanaposaidia kujenga dunia yenye amani zaidi na ya utu kwa ajili ya watu wote. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Siku hii ya Kimataifa ya Mshikamano na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Walio vizuizini na wasiofahamika waliko huadhimishwa kila mwaka Machi 25 katika kumbukumbu ya kutekwa nyara kwa Alec Collett, mwandishi wa habari wa zamani ambaye alikuwa akifanya kazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) wakati alipotekwa nyara na mtu aliyekuwa na silaha mwaka wa 1985 na baadaye mwili wake kupatikana katika Bonde la Bekaa nchini Lebanon mwaka wa 2009 yaani miaka 24 baadaye.Maadhimisho ya siku hii, katika miaka ya hivi karibuni yamekuwa hata ana umuhimu mkubwa zaidi kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya Umoja wa Mataifa.Katibu Mkuu Guterres kupitia ujumbe wake kwa maadhimisho ya mwaka huu anatoa takwimu za hivi karibuni akieleza kwamba tangu mwaka juzi 2022, wafanyakazi 381 wa Umoja wa Mataifa wamewekwa kizuizini ikiwa ni pamoja na wafanyakazi 7 mnamo mwezi Januari na Februari mwaka huu 2024. Kwa jumla, wafanyakazi 27 wa Umoja wa Mataifa bado wako kizuizini.Bwana Guterres anasema leo ni ukumbusho mzito wa hatari kubwa zinazowakabili wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanapofanya kazi yao muhimu chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa na kwamba, "Mioyo yetu iko pamoja na familia zao na wafanyakazi wenzao”, na kwamba hatakataa tamaa kutaka waachiliwe na kurudi salama."Kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa anazisihi nchi zote kutekeleza kikamilifu Mkataba wa mwaka 1994 wa Usalama wa Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Washirika wao, na pia Itifaki ya Hiari ya mwaka 2005 ya Mkataba huo.
25-3-2024 • 1 minuut, 45 seconden
25 MACHI 2024
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akianzia na siku ya kimataifa ya kukumbuka watumishi wa UN wanaoshikiliwa vizuizini na wasiofahamika waliko, kisha anakwenda Sudan Kusini na harakati za kusaidia manusura wa ukatili wa kingono. Makala ni harakati za kumkomboa mwanamke na mashinani arejea Sudan Kusini.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa Walio vizuizini na wasiofahamika waliko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa ulimwengu kuenzi ujasiri na kujitolea kwa wafanyakazi wanaotoa huduma za kibinadamu kila mahali kokote waliko kwa kuahidi kuwalinda na kuwaunga mkono wanaposaidia kujenga dunia yenye amani zaidi na ya utu kwa ajili ya watu wote. Assumpta Massoi anaeleza zaidi.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wadau wake wamefungua nyumba salama huko Andari Magharibi katika jimbo la Equatoria kwa ajili ya kusaidia manusura wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro nchini humo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.Makala leo inatupeleka Nairobi Kenya ambako mkutano wa maandalizi wa asasi za kiraia umekunja jamvi hivi karibuni na Stella Vuzo wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya UNIS Nairobi alizungumza na Carole Osero-Ageng'o Mwenyekiti mwenza wa mkutano huo. Anazungumzia harakati za kumkomboa mwanamke.Mashinani ni mlinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini kutoka taifa la Bhutan.
25-3-2024 • 11 minuten, 42 seconden
Maji yanaweza kuleta amani au kuchochea migogoro
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Maji, Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM ya nchini Kenya amezungumza na baadhi ya wakazi wa Kaunti ya Kajiado nchini humo kuhusu umuhimu wa uwepo wa maeneo mengi ya kupata maji katika jamii. Dhima ya Siku ya Kimataifa ya Maji ya mwaka huu wa 2024 ni "Maji kwa ajili ya amani" ikieleza kuwa kunapokuwa na ushirikiano katika suala la maji inaleta athari chanya kukuza maelewano, kuhamasisha ustawi na kujenga uwezo wa kukabiliana na changamoto za pamoja.
22-3-2024 • 3 minuten, 15 seconden
22 MACHI 2024
Hii leo jaridani ikiwa ni Siku ya maji duniani, tunaangazia utunzaji wa vyanzo vya maji. Pia tunamulika mkutano wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW68 ambao umekunja jamvi hii leo. Makala tuankupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania kufuatilia jinsi ambayo miradi ya maji inavyoleta manufaa kwa jamii.Leo ni siku ya maji duniani chini ya kauli mbiu Maji kwa amani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kwa siku hii amehimiza nchi kuhakikisha zinashirikiana na kuwa na makubaliano ya kutumia vyanzo vya maji.Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW68 umekunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataia jijini New York, Marekani na miongoni mwa washiriki ni Matika Maiseli, Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka Mamlaka ya Afya na Mimea na Viuatilifu, TPHPA iliyo chini ya Wizara ya Kilimo nchini Tanzania. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ubaguzi wa rangi ni jinamizi linaloathiri nchi na jamii kote duniani chimbuko lake likitokana na sera za ukoloni na utumwa. Kupitia ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi hii leo inayojikita na mada ya watu wenye asili ya Afrika katika kutambuliwa kwao, kupewa haki na maendeleo, ametaka kutokomezwa kwa jinamizi hilo kwani linapokonya fursa, kunyima utu, kukiuka haki, kupora maisha na pia kuyaharibu.Katika mashinani tutakupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu jinsi ambavyo miradi ya maji imeleta nafuu kwa jamii.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
22-3-2024 • 11 minuten
Tunawezesha wakulima wanawake Tanzania ili wapate masoko ndani na nje ya nchi - CSW68
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW68 umekunja jamvi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataia jijini New York, Marekani na miongoni mwa washiriki ni Matika Maiseli, Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala kutoka Mamlaka ya Afya na Mimea na Viuatilifu, TPHPA iliyo chini ya Wizara ya Kilimo nchini Tanzania.Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa amezungumza naye kufahamu ni nini anaondoka nacho kutoka mkutano huu uliolenga kusongesha usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake na kutokomeza umaskini.
22-3-2024 • 3 minuten, 9 seconden
Umoja wa Mataifa yataka nchi kuwa na makubaliano ya ushirikiano wa matumizi ya vyanzo vya maji
Leo ni siku ya maji duniani chini ya kauli mbiu Maji kwa amani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kwa siku hii amehimiza nchi kuhakikisha zinashirikiana na kuwa na makubaliano ya kutumia vyanzo vya maji. Katika ujumbe wake huo Guterres ameeleza kuwa mpaka sasa ulimwenguni “Nchi 153 zinashirikiana vyanzo vya maji lakini ni nchi 24 pekee zenye makubaliano kwa vyanzo vyao vyote vya maji wanavyoshirikiana.” Amesema hali haipaswi kuwa hivyo na nchi zinatakiwa “kutekeleza Mkataba wa Maji wa Umoja wa Mataifa ambao lengo lake ni kuhamasisha usimamizi wa rasilimali za maji za pamoja kwa njia endelevu.”Hii leo kukiwa na mikutano mbalimbali pamoja na ripoti za mashirika ya Umoja wa Mataifa, kimataifa, kitaifa na asasi za kiraia zinazoelezea matumizi ya maji pamoja na changamoto zake ulimwenguni, Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ametaka watu wote kutambua kwamba kushirikiana katika kulinda vyanzo vya maji kunaweza kuimarisha na kudumisha amani. Kama Kauli mbiu ya mwaka huu inavyosema “Maji kwa amani” Guterres amesema “Hatua zinachokuliwa kwa ajili ya maji ni hatua kwa ajili ya amani na hii inahitajika zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Usimamizi wa maji unaweza kuimarisha ushirikiano wa kimataifa na uhusiano kati ya jamii, na kujenga uwezo wa kukabiliana na majanga yaletwayo na mabadiliko ya tabianchi. Unaweza pia kuendeleza maendeleo kuelekea Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs ambayo ni msingi wa jamii zenye amani, ikiwa ni pamoja na kuboresha afya, kupunguza umaskini na ukosefu wa usawa, na kuimarisha usalama wa chakula na maji.Amehitimisha kwa kutoa wito kwa jamii yote kujitolea kufanya kazi pamoja, kufanya maji kuwa nguvu ya ushirikiano, maelewano na utulivu, na hivyo kusaidia kuunda ulimwengu wa amani na ustawi kwa wote.
22-3-2024 • 1 minuut, 57 seconden
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno "Panda"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Nicholus Makanji mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya akitufafanulia maana ya neno “PANDA”
21-3-2024 • 1 minuut, 10 seconden
21 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika changamoto zitokanazo na matumizi ya mtandao na utasikiliza mahojiano ya Peter Mmbando, Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Digital Agenda For Tanzania Initiative. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Gaza, afya na ubaguzi. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili utapata ufafanuzi wa neno “Panda”Wakati hali ya kibinadamu ikiendelea kuwa mbayá Gaza mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la afya duniani WHO yamerejea wito wa kutaka kusitishwa mapigano mara moja na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inaingia Gaza ambako maisha ya zaidi ya watu milioni 1 yako hatarini kwa njaa..Leo ni siku ya kimataifa ya ugonjwa unaoathiri uwezo wa mtu kujifunza au downsyndrome mwaka huu ikibeba maudhui ya kutokomeza unyanyapaa yakimchagiza kila mtukuwajumuisha watu wenye downsyndrome kwenye nyanja zote za maisha na kutowabagua. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ubaguzi wa rangi ni jinamizi linaloathiri nchi na jamii kote duniani chimbuko lake likitokana na sera za ukoloni na utumwa. Kupitia ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kutokomeza ubaguzi wa rangi hii leo inayojikita na mada ya watu wenye asili ya Afrika katika kutambuliwa kwao, kupewa haki na maendeleo, ametaka kutokomezwa kwa jinamizi hilo kwani linapokonya fursa, kunyima utu, kukiuka haki, kupora maisha na pia kuyaharibu.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Nicholus Makanji mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya akitufafanulia maana ya neno “PANDA”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
21-3-2024 • 12 minuten, 57 seconden
Watoto Gaza waamua vita isiwe sababu ya kunyong’onyea wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani
Huko Ukanda wa Gaza, vita inayoendelea tangu Oktoba 7 mwaka 2023 baada ya Hamas kurusha makombora Israel na kisha Israel kuamua kujibu mashambulizi licha ya kusababisha vifo vya watu 31,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto, watoto waliosalia wameona mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani usipite hivi hivi. Wakiwa katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Deir El Balah katikati mwa Gaza, watoto hao wameona furaha ni bora kuliko machungu ya njaa, ukimbizi, ukosefu wa huduma muhimu za kijamii unaowakabili. Mwandishi wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa huko Gaza, Ziad Talib amefika hapo ili kufahamu hasa msingi wa hatua ya watoto hao na ndio makala ya leo inayosimuliwa na Assumpta Massoi.
20-3-2024 • 4 minuten, 35 seconden
WHO: Madaktari Gaza wanafanyakazi kutwa kucha kuokoa maisha bila kutia chochote tumboni
Wahudumu wa afya Gaza wanafanya kazi mchana kutwa na usiku kucha wakihaha kuokoa Maisha ya wagonjwa na majeruhi katika hospitali chache zilizosalia zikifanyakazi bila kutia chochote tumboni kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. WHO inasema wafanyakazi hao wanaolazimika kufanyakazi saa 24 kuokoa maisha ya watu kama ambavyo wanakosa vifaa muhimu na vitendeakazi vingine vivyo hivyo wanakosa chakula cha kutosha kama ilivyo kwa maelfu mengine ya raia wa Gaza.Timu ya WHO iliyozuru Hospitali ya Al-Aqsa katikati mwa Ukanda wa Gaza ili kupeleka vifaa muhimu imezungumza na wafanyakazi kuhusu hali zao, ikiwa ni pamoja na hali yao ya lishe.Bashar Abdelkader, ambaye ni daktari wa kujitolea katika hospitali hiyo, amesema madaktari wanapewa chakula lakini wanakosa viambato muhimu vya lishe, hasa mchele na mboga nichache. Ameongeza kuwa mlo mmoja unaweza kugawiwa kwa watu wawili na zaidi ya yote,chakula haitoshi kwa daktari wa zamu wanofanyakazi kwa saa 24 hospitalini hapo.Tahani al-Samra, ambaye pia ni daktari wa kujitolea katika hospitali ya al-Aqsa amesema "Tunakabiliwa na utapiamlo na ukosefu wa nyenzo tunazohitaji. Kwa sasa hakuna mboga za asili za majani, matunda au virutubisho vingine muhimu. Tunategemea vyakula vya makopo, ambavo bei yake inapanda kwa kasi."WHO na washirika wake wanafanya operesheni ya hatari kubwa wakihaha kupeleka dawa, mafuta na chakula kwa wahudumu wa afya na wagonjwa. Lakini maombi ya ufikishaji wa bidhaa mara nyingi hukataliwa au kutatizwa. Uharibifu wa barabara na mapigano yanayoendelea, ikiwa ni pamoja na ndani na karibu na hospitali, pia yanatatiza utoaji wa misaada.WHO imeonya kwamba bila kuwepo hatua kubwa na za haraka za utoaji wa chakula, maji na vifaa vya msingi, hali ya Gaza, ambako njaa inaathiri karibu watu wote, karibu familia zote zinalazimika kuruka mlo kila siku na watu wazima wanapunguza kiwango cha ulaji wao wa kula.Nusu ya watu wote ambao ni watu milioni 1.1 huko Gaza, wamechoka kabisa na hakuna usambazaji wa chakula na uwezo wao wa kukabiliana na njaa mbaya ni mdogo. Umoja wa Mataifa unasema “Hii ndiyo idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika orodha ya watu wanaokabiliwa na njaa kali Gaza.”
20-3-2024 • 2 minuten, 32 seconden
20 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya huduma za afya katika ukanda wa Gaza, na harakati za chanjo kwa watoto nchini Yemen. Makala tunasalia huko huko Gaza na mashinani inatupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu siku ya furaha duniani.Wahudumu wa afya Gaza wanafanya kazi mchana kutwa na usiku kucha wakihaha kuokoa Maisha ya wagonjwa na majeruhi katika hospitali chache zilizosalia zikifanyakazi bila kutia chochote tumboni kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO.Katika kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote zinazohitajika, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Yemen limekuja na mbinu ya kutumia watoto kuhamasisha jamii kupeleka watoto kupata chanjo. Makala inatupeleka Gaza huko Mashariki ya Kati kupata taswira tofauti na ile ambayo imezoeleka kwa takribani miezi sita sasa. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi katika makala hii iliyoandaliwa na Ziad Talib, mwandishi wa Habari wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa huko Gaza.Katika mashinani ikiwa leo ni siku ya furaha duniani Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM ya mkoani mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania ameuliza wananchi furaha ina maana gani kwao.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
20-3-2024 • 11 minuten, 52 seconden
UNICEF yatumia watoto kuhamasisha jamii kupata chanjo nchini Yemen
Katika kuhakikisha watoto wanapata chanjo zote zinazohitajika, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Yemen limekuja na mbinu ya kutumia watoto kuhamasisha jamii kupeleka watoto kupata chanjo. Mtoto Leen mwenye umri wa miaka 10 kutoka nchini Yemen, anasema kupitia mpango wa ufadhili wa mtoto, programu inayotumia watoto kwenda kuhamasisha jamii kupata chanjo ili wawe na afya bora amefanikisha watoto 150 kupata chanjo katika jamii yake. Akieleza hasa jumuku lake Leen anasema ‘Nawasisitiza walezi, umuhimu wa kupata chanjo na pia nacheza na watoto pale wanapokuwa wanachomwa sindano za chanjo ili kuwafanya wajisikie vizuri”Katika kipindi cha miaka mwili UNICEF imefanikiwa kuwapatia mafunzo watoto 1000 ambao kwa pamoja wamefanikiwa kushawishi watoto 33,000 kupatiwa chanjo. Watoto hao kama Leen huambatana na mtu mzima ambaye ni muhamasishaji wa jamii kwenda kuhamasisha familia kuhusu chanjo za kawaida ambazo watoto wanapaswa kupata. Mmoja wa waliohamasishwa na mtoto Leen ni Somaia Mohammed, mama wa watoto watatu.“Nilikuwa najizuia kwenda kuwapatia chanjo watoto wangu, hata hivyo baada ya Leen kunitembelea nyumbani kwangu baada ya mtoto wangu kuugua surau na kunielezea kama ningekuwa nimewapatia chanjo watoto wangu wasingeugua kiasi hicho nilihamasika na ushauri wao na kutembelea kituo cha afya kuwapatia chanjo watoto wangu.” Na mtoto Leen anafurahi kuona jirani yake Somaia na watoto wake watatu wamepata chanjo baada ya kumtembelea mara kadhaa.Anasema kati ya mambo aliyokuwa akimwambie wakati akienda kumhamasisha alikuwa akisema “Angalia nilivyo na afya bora na nilivyo na nguvu naweza kwenda shuleni sababu nimepata chanjo zote zinazohitajika”
20-3-2024 • 2 minuten, 6 seconden
19 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo kandoni mwa mkutano wa leo tunazungumza na Nasra Kibukila ambaye kwa ufadhili wa Mfuko wa Malala (Malala Fund), amewakilisha Shirika la Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MeT). Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani kama zifuatazo. Mashirika Umoja wa Mataifa yanayotoa msaada wa kibinadamu huko Gaza hii leo yamesisitiza azma yao ya kusaidia wakazi wa eneo hilo ambako watoto walio hatarini kufa kutokana na njaa kali iliyosababishwa na miezi mitano ya mashambulizi ya Israel na kushindwa kufikishiwa misaada inazidi kuongezeka.Mwaka 2023 ulikuwa mwaka wenye joto zaidi duniani katika rekodi zote zilizowahi kunukuliwa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani, WMO katika ripoti yake iliyotolewa hii leo huko Geneva, Uswisi, rekodi za viwango vya joto ardhini, baharini zikivunjwa, barafu na theluji ncha ya kusini zaidi mwa dunia navyo vikiyeyuka. Na ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO inaonesha kitendo cha sekta binafsi kutumikisha watu huzalishafaida isiyo halali yad ola bilioni 236 kwa mwaka ikiwa ni ongezeko la asilimia 37 tangu mwaka 2014.Katika mashinani tutaelekea katika ukanda wa Gaza ambapo kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, katika mwezi mmoja utapiamlo uliokithiri umeongezeka maradufu kaskazini mwa ukanda huo..Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
19-3-2024 • 9 minuten, 59 seconden
LANDESA yaelezea ni vipi ushiriki wao CSW68 unaleta nuru kwa wanawake Tanzania
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ukiendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeendelea kuzungumza na washiriki ili kufahamu yale wanayofanya kutekeleza maudhui ya kipaumbele ya mwaka huu ya kumwezesha mwanamke na mtoto wa kike ili hatimaye kupunguza umaskini na kuimarisha usawa wa kijinsia. Shirika la kiraia la kutetea haki ya ardhi kwa wanawake, LENDESA tawi la Tanzania linaloungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia masuala ya wanawake ni miongoni mwa washiriki ambapo Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Khadija Mrisho, anayeongoza kampeni ya kimataifa ya Linda Ardhi ya Mwanamke au Stand For Her Land. Khadija anaanza na kile kilichowaleta.
18-3-2024 • 5 minuten, 18 seconden
FAO: Baa la njaa lanyemelea Gaza
Hali ya uhakika wa kupata chakula huko Gaza, ni tete na baa la njaa linanyemelea kwenye majimbo ya kaskazini mwa eneo hilo imesema ripoti mpya ya hali ya chakula Gaza iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, likisema jawabu la kuondokana na hali hiyo ni amani. Rein Paulsen, Mkurugenzi wa Ofisi ya Masuala ya Dharura na Mnepo FAO akizungumza hii leo huko Roma, Italia wakati wa kutolewa kwa ripoti hiyo ya uchambuzi wa viwango vya uhakika wa kupata chakula au IPC kwa Ukanda wa Gaza, anasema takwimu zinajenga taswira ya hali ya kutia wasiwasi mkubwa. Na pindi tunapofikiria kuhusu Gaza Kaskazini, ambako hali ni mbaya zaidi, uchambuzi wa sasa unatuonesha kuwa njaa ni dhahiri katika kipindi cha kuanzia sasa na Mei 2024.Hii ina maana tunapotazama mwelekeo wa takwimu za hali ya upatikanaji chakula na lishe tunaona hali ya kutisha. Kusini, hali nayo imezidi kuwa mbaya na huko tunashikilia makadirio yetu ya uwezekano wa baa la njaa.”Ripoti inaonesha kuwa mwendelezo wa uhasama umesambaratisha sekta ya kilimo, ambayo familia za Gaza inategemea kwa ajili ya kujipatia kipato.“Watu wote kwenye ukanda wa Gaza wanakabiliwa na viwango vya juu vya ukosefu mkubwa wa chakula ukiwekwa katika kiwango cha 3, na 4. Hii inaamanisha nusu ya idadi ya watu wote wa eneo hilo, takribani milioni 1.1 wanaweza kukabiliwa na janga kubwa la ukosefu wa uhakika wa chakula la kiwango cha 5.”Hivyo amesema usaidizi wa haraka unahitajika kurejesha uzalishaji wa chakula na kwa mujibu wa ripoti“Inatueleza kuwa baadhi ya mifugo iko hai, na inaweza kusaidiwa na ndio maana FAO inajikita kusaidia mahitaji ya kujipatia kipato Ukanda wa Gaza. Kwa sasa tumepata kibali cha kupeleka tani 1500 za ujazo za chakula cha mifugo.”Amesema uhai wa mifugo utakuwa hakikisho la upatikanaji wa maziwa kwa familia, maziwa ambayo yatakuwa ni lishe bora kwa watoto na hivyo kukabili utapimlo uliokithiri miongoni mwa watoto.Akatamatisha akisema, “uhakika wa kupata chakula utawezekana kukiweko na amani. Na haki ya kupata chakula ni haki ya msingi. Hili linapaswa kuzingatiwa na wadau wote.”
18-3-2024 • 2 minuten, 7 seconden
18 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia baa la njaa unalowakumba waPalestina katika ukanda wa Gaza, na kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi ya Sudan Kusini. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni? Hali ya uhakika wa kupata chakula huko Gaza, ni tete na baa la njaa linanyemelea kwenye majimbo ya kaskazini mwa eneo hilo imesema ripoti mpya ya hali ya chakula Gaza iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, likisema jawabu la kuondokana na hali hiyo ni amani.Timu kutoka Kurugenzi ya Haki na Sheria ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) mwishoni mwa wiki kwa usaidizi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), imehitimisha tathmini yake katika Kaunti ya Maridi jimboni Equatorial Magharibi kutathmini kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi hiyo. Assumpta Massoi wa Idhaa hii akizungumza na Khadija Mrisho, Afisa kutoka shirika la kiraia la kutetea haki ardhi kwa mwanamke LANDESA tawi la Tanzania yeye akiwa kiongozi wa kampeni ya kimataifa ya Linda Ardhi ya Mwanamke. Akiwa hapa New York, Marekani akishiriki mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, anaelezea kile walichojifunza. Lakini anaanza na kile kilichowaleta.Katika mashinani tutaelekea Ngong nchini Kenya kusikia ujumbe unaotia moyo wasichana waathirika wa mimba za utotoni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
18-3-2024 • 11 minuten, 32 seconden
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wasaidia jeshi la Sudan Kusini kutathmini kesi dhidi ya askari
Timu kutoka Kurugenzi ya Haki Sheria ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Sudan Kusini (SSPDF) mwishoni mwa wiki kwa usaidizi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), imehitimisha tathmini yake katika Kaunti ya Maridi jimboni Equatorial Magharibi kutathmini kesi zinazohusisha wanajeshi wa nchi hiyo.Tathimini itawezesha kufunguliwa mashtaka kwa askari wa jeshi ambao wanashukiwa kufanya uhalifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia.Mama Sarah Bennert, mwanaharakati na mwakilishi wa wanawake anasema hatua hii inawakilisha ishara ya haki na uwajibikaji."Tuna masuala mengi yanayotukabili hapa kama wanawake. Wakati mwingine unaripoti kesi na haki imechelewa na unabaki kukata tamaa na bila msaada wowote. Sasa, kwa uwepo wa timu ya tathmini hapa chini tunatumai kesi hizo zote walizozizingatia zitasikilizwa kwa sababu baadhi yetu ambao bado tuna kesi tuna kiwewe."Idrissa Sylvaine ni Mshauri wa haki sheria wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) anasema,“Tathmini hiyo itasaidia kukuza utawala wa sheria, kuleta haki kwa waathiriwa na kuwawajibisha askari wa SSPDF. Tathmini hiyo pia itachangia katika mchakato wa amani nchini Sudan Kusini.”
18-3-2024 • 1 minuut, 24 seconden
Ushirkiano wa dhati waliotuonesha ulifanya wananchi waachane na mpango wa kuwapiga mawe MONUSCO- Chifu Makofi
Hii leo huko jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kikosi cha 10 cha Tanzania (TANZBATT-10) kilichoko kwenye brigedi ya mapigano (FIB) ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO imekabidhi majukumu kwa kikosi cha 11, TANZBATT-11, katika hafla iliyofanyika eneo la Beni-Mavivi. Msimulizi wetu ni Kapteni Abubakari Muna, Afisa Habari wa TANZBATT-10.Mkuu wa TANZBATT-10 Luteni Kanali John Peter Kalabaka amekabidhi bendera ya Tanzania kwa Kamanda wa TANZBATT-11 Luteni Kanali Vedasto Ernest Kikoti ikiwa ni ishara ya kuanza majukumu ya ulinzi wa amani, katika tukio ambalo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Kamanda wa FIB-MONUSCO Kanali Alex Tamson Malenda.Akizungumza kwenye hafla hiyo Luteni Kanali Kalabaka amesema kwenye upande wa operesheni wameweza kukabili na kupunguza mashambulizi yanayofanywa na vikundi vilivyojihami kwenye eneo la ulinzi la TANZBATT-10 halikadhalika kuepusha mauaji ya raia wasio na hatia na pia kuepusha vitendo vya ubakaji.“Kijamii tumeweza kushirikiana na jamii ya hapa Beni-Mavivi na pia kuwapatia misaada mbali mbali ya kijamii,” amesema Mkuu huyo wa TANZBATT-10.Luteni Kanali Vedasto Ernest Kikoti ambaye amepokea jukumu la ulinzi akaeleza bayana kuwa watatekeleza majukumu yao vyema kwa kuzingatia taratibu za Umoja wa Mataifa na kwamba watakuwa tayari kuendelea kushirikiana na raia. “Tunaomba wananchi wakubali na waelewe dhamira hiyo, waukubali Umoja wa Mataifa ili kuupa nafasi uweze kutekeleza wajibu wake wa kulinda wananchi wa DRC,” ameeleza Luteni Kanali Kikoti.Makofi Bukuka Gervain ambaye ni Chifu wa eneo hilo akashukuru TANZBATT-10 kwa ushirikiano walioonesha wakati wote wa kipind ichao cha ulinzi wa amani Beni-Mavivi na kueleza kuwa Kamanda wa Kikosi hicho alikuwa yuko karibu sana na wanajamii akitolea mfano wakati wa michezo ikiwemo mpira wa miguu.“Ushirikiano wao na sisi umewezesha raia kufungua nyoyo zao na kuondokana na fikra zao za kupiga mawe MONUSCO barabarani. Sasa barabara zilibaki wazi na MONUSCO wakafanya kazi yao vema,” amesema Chifu MakofiMeja Fatuma Haruna Makula, wa TANZBATT-11 ameahidi kuendeleza uhusiano mzuri kati ya wanajeshi wanawake kutoka Tanzania na wanawake wa Beni-Mavivi akisema, “wanawake maafisa na askari tuliokuja hapa wote tumepita mafunzo mbali mbali kuhusu suala zima la ulinzi wa amani. Tutahakikisha wanashiriki vema shughuli za ulinzi wa mani kwa mujibu wa taratibu za Umoja wa Mataifa chini ya MONUSCO.” Imeandaliwa na Luteni Abubakari Muna, Afisa Habari, TANZBATT-10 TAGS: Amani na UsalamaNews: TANZBATT 10, TANZBATT-11REgion.: AfrikaFocus: DRCUN/Partner: MONUSCO
15-3-2024 • 3 minuten, 28 seconden
Wasichana ni majaji watarajiwa, wafuate ndoto zao katika masomo ya Uanasheria - Hakimu Pamela Achieng
Maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Majaji Wanawake duniani yalifanyika tarehe 10 Machi 2022, ikiangazia Haki katika Mtazamo wa Kijinsia. Umoja wa Mataifa umeendelea kuadhimisha siku hii kama sehemu ya juhudi za kimataifa za kuhakikisha usawa wa kijinsia na kushughulikia masuala ya uadilifu wa mahakama yanayohusiana na jinsia. Huku mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68 ukiendelea hapa jijini New York Marekani, nchini Kenya Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kupitia video iliyoandaliwa na washirika wetu Redio Domus amekutana na Pamela Achieng, Hakimu katika mahakama ya Ngong iliyo katika Kaunti ya Kajiado ambaye anaanza kwa kuelezea ni kwa nini kama mwanamke aliamua kuingia katika tasnia hii.
15-3-2024 • 6 minuten, 16 seconden
15 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa ulinzi wa amani DRC, MONUSCO, na yaliyojiri katika mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Hii leo huko jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kikosi cha 10 cha Tanzania (TANZBATT-10) kilichoko kwenye brigedi ya mapigano (FIB) ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO imekabidhi majukumu kwa kikosi cha 11, TANZBATT-11, katika hafla iliyofanyika eneo la Beni-Mavivi. Msimulizi wetu ni Kapteni Abubakari Muna, Afisa Habari wa TANZBATT-10.Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ukiwa umeingia siku yake ya 5 leo, Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikizungumza na washiriki kutoka mataifa mbalimbali. Leo ni baadhi ya washiriki kutoka Tanzania, vinara wa elimu wanaofadhiliwa na Mfuko wa Malala. Katika makala ambapo hivi majuzi kuliadhimishwa Siku ya Majaji Wanawake Duniani ambayo Umoja wa Mataifa umeendelea kuiadhimisha kila mwaka tarehe 10 Mwezi wa Machi kama sehemu ya juhudi za kimataifa za kuhakikisha usawa wa kijinsia na kushughulikia masuala ya uadilifu wa mahakama yanayohusiana na jinsia na tunakupeleka nchini Kenya kusikia ujumbe wa Hakimu Pamela Achieng.Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akisimulia jinsi alivyotekwa na makundi yaliyojihami ya waasi lakini hatimaye sasa amenasuliwa na amerejea kwenye jamii kwa msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
15-3-2024 • 12 minuten, 5 seconden
CSW68: Vinara wa elimu kutoka Tanzania wajizatiti kuhakikisha sauti za wasichana zinasikika
Mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani, CSW68 ukiwa umeingia siku yake ya 5 leo, Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imekuwa ikizungumza na washiriki kutoka mataifa mbalimbali. Leo ni baadhi ya washiriki kutoka Tanzania, vinara wa elimu wanaofadhiliwa na Mfuko wa Malala.Zahra Salehe Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linaloitwa ICCAO anaeleza ujumbe mkubwa waliokuja nao.“Tumeletwa hapa kwa ajenda moja ya elimu na ujumbe mkubwa tuliokuja nao ni wa kuhakikisha sauti za wasichana na wanawake vijana zinasikika kwenye majukwaa makubwa kama haya CSW68 na sisi ajenda kubwa ambayo tunaiona kwas asa ni ‘reentry’ ambayo ni ruhusa ya msichana kurudi shule baada kupitia changamoto kubwa. Tisimuache mtu nyuma kwa sababu ya sababu mbalimbali ambazo zote zimeletwa na kutokuwa na usawa wa kijinsia. Wanaendelea na wanaendelea kutimiza ndoto zao.”Paulina Ngurumwa kutoka taasisi ya KINNAPA anakubaliana na anachosema kinara wa elimu mwenzake na anasema wanapambana na vikwazo dhidi ya elimu ya wanawake ingawa bado kuna ugumu“Hatuna mabweni, hatuna mahali pa kuwaweka kwa hiyo tunajikuta kuna mzigo mwingi. Kwa hiyo wito wetu wadau kwa ngazi ya ulimwengu, kwa ngazi ya mataifa, kwa ngazi ya taifa letu la Tanzania tushikamane tuone ni namna gani tunaweza kutafuta hata namna gani tuwapatie hawa watoto mabweni ambayo wanaweza wakasomea na wakakaa pale wakawa katika mazingira salama ili waeze kutimiza ndoto zao.”Kutokana na changamoto kama hizo Nasra Kibukila kutoka shirika la TEN/MeT anapigia chepuo Bajeti ya nchi inayozingatia jinsia“Kwa sasa hivi Tanzania tumeshaanza mchakato wa kutengeneza bajeti ya mwaka 2024-2025 na kwas asa hivi iko kwenye ngazi ya wabunge. Tutakapotoka hapa, tutakayojifunza hapa tukirudi nyumbani tunaenda kuwa na mkutano pamoja na wabunge kuweza kuwaelezea yapi tumejifunza kwa jinsi gani kuwa na majeti yenye mrengo wa kijinsia na wao waweze kutusaidia kuhakikisha kuwa pale tutapakuwa na bajeti ya 2024-25inakuwa iko kwenye mrengo wa kijinsia kuweza kuhakikisha kuwa makundi yote maalumu yanakuwa yana bajeti yao kuwawezesha.”
15-3-2024 • 2 minuten, 9 seconden
Je wafahamu maana ya neno "Kupwemka?"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua maana ya neno “KUPWEMKA”.
14-3-2024 • 1 minuut, 12 seconden
14 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ambapo Jumuiya ya Madola anaelezea kinagaubaga mambo ambayo wanapenda kuona yanatekelezwa ili maudhui ya mwaka huu ya CSW68 ya kuwezesha wanawake kiuchumi na hatimaye kutokomeza umaskini yanafanikiwa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Haiti, Gaza na dawa za kulevya. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakuletea uchambuzi wa neno “KUPWEMKA”Baada ya Kenya kutangaza kusitisha mpango wake wa kupeleka askari wa kuleta utulivu nchini Haiti hadi pale hali ya kisiasa itakapotengamaa, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kusaidiana katika kuunda operesheni ya usaidizi kwa watu wa Haiti haraka iwezekanavyo.Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu dawa za kulevya (CND), imeanza mkutano wake hii leo huko Vienna Austria kukagua maendeleo yaliyopatikana katika kushughulikia tatizo la dawa za kulevya duniani na jinsi ya kuhakikisha utekelezaji wa ahadi za kimataifa. Na kukiwa na ripoti za kwamba leo Wapalestina 6 wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine 83 wakijeruhiwa wakati wakisubiri malori ya misaada huko Gaza, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Martin Griffiths kupitia ukurasa wa mtandao wa X ametoa wito wa kulindwa kwa operesheni za misaada ya kibinadamu inayohitajika sana Gaza.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua maana ya neno “KUPWEMKA”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
14-3-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Kauli ya ‘usifanye hiki usifanye kile’ inadidimiza ndoto za wasichana – Frida Amani
Makala hii inakupeleka Nairobi, Kenya ambako Priscilla Lecomte wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Mratibu wa hatua dhidi ya majanga ya tabianchi na El Niño anazungumza na Mwanamuziki Frida Amani wa Tanzania. Frida Amani anatoa wito kwa watoto wa kike duniani kutokatishwa tamaa kwa kuambiwa “usifanye shughuli fulani kwa kuwa ni ya kiume” kwani kama yeye angekata tamaa asingeweza kuwa msanii wa Hip Hop ambayo imemfikisha katika majukwaa ya kimataifa kiasi cha kuandaa wimbo wa kuhamasisha ushirikiano wa kimataifa katika kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, wimbo ambao umeungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Duniani (UNEP). Hapa Frida anaanza kwa kueleza kwa nini wimbo alioshirikiana na msanii Dex Mc Bean wa Marekani waliamua kuupa jina Twende na Mpango.
13-3-2024 • 3 minuten, 8 seconden
Kauli ya ‘usifanye hiki usifanye kile’ inadidimiza ndoto za wasichana – Frida Amani
Makala hii inakupeleka Nairobi, Kenya ambako Priscilla Lecomte wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Mratibu wa hatua dhidi ya majanga ya tabianchi na El Niño anazungumza na Mwanamuziki Frida Amani wa Tanzania. Frida Amani anatoa wito kwa watoto wa kike duniani kutokatishwa tamaa kwa kuambiwa “usifanye shughuli fulani kwa kuwa ni ya kiume” kwani kama yeye angekata tamaa asingeweza kuwa msanii wa Hip Hop ambayo imemfikisha katika majukwaa ya kimataifa kiasi cha kuandaa wimbo wa kuhamasisha ushirikiano wa kimataifa katika kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, wimbo ambao umeungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Duniani (UNEP). Hapa Frida anaanza kwa kueleza kwa nini wimbo alioshirikiana na msanii Dex Mc Bean wa Marekani waliamua kuupa jina Twende na Mpango.
13-3-2024 • 3 minuten, 8 seconden
Watoto waliouawa Gaza ni wengi kuliko miaka 4 ya vita duniani
Wakati kukiwa na ripoti za mashambulizi kwa njia ya anga yanayotekelezwa na Israel huko Gaza usiku wa kuamkia leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limesema idadi ya watoto waliouawa katika miezi ya hivi karibuni ni kubwa kuliko miaka minne ya mizozo duniani. Phillipe Lazzarini ambaye ni Mkuu wa shirika hilo la msaada kwa wakimbizi wa kipalestina hii leo kupitia mtandao wake wa X zamani Twitter ameandika ujumbe alioambatanisha na mchoro unaoonesha mambo mamwili kushoto kwenye rangi ya buluu idadi ya watoto waliouawa kutokana na vita tangu mwaka 2019 mpaka 2022 ambao ni 12, 193 na kulia ni idadi ya watoto waliouawa Gaza tangu mwezi Oktoba mwaka jana 2023 mpaka mwezi Februari 2024 ambao ni zaidi ya 12,300. Na ndipo akaandika ujumbe kuwa “Vita hii ni vita dhidi ya watoto. Ni vita dhidi ya utoto wao na mustakabali wao.”Mkuu huyo wa UNRWA akaendelea na ujumbe wake na kusema kuwa “Sitisheni mapigano sasa kwa ajili ya watoto wa Gaza“.Kwa mujibu wa takwimu kutoka mamlaka za afya huko Gaza, mpaka sasa zaidi ya wapalestina 31,184 wameuawa na wengine 72,889 kujeruhiwa. Mpaka kufikia tarehe 12 ya mwezi huu wa Machi, wanajeshi 247 wa Israel wameripotiwa kuuawa na wengine 1,475 kujeruhiwa tangu kuanza kwa operesheni za ardhini kwa mujibu wa takwimu za jeshi la Israel. Sio mashambulizi tu ya mabomu yanayo gharimu maisha ya watoto na wakazi wa Gaza, janga la njaa nalo pia lipo hatihati kukumba wananchi hao ambao a misaada ya kibiandamu kuwafikia imekuwa changamoto kubwa. Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kibinadamu yamekuwa yakirejea kutoa maonyo kuhusu hali mbaya ya Gaza ambapo mtu mmoja kati ya wanne anakaribia kukumbwa na njaa. Mpaka sasa takriban watu 25 wamekufa kutokana na utapiamlo mkali na upungufu wa maji mwilini kaskazini mwa Gaza kulingana na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada, OCHA, 21 kati yao wakiripotiwa kuwa watoto.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limeonya kuwa vijana ni miongoni mwa wale ambao hawawezi kustahimili njaa na magonjwa, huku vijana milioni moja wakiwa tayari wameondolewa makwao kutokana na vita, na watoto 17,000 wasio na wasindikizaji au waliotenganishwa nao sawa na 1% ya watu milioni 1.7 ya wananchi wa Gaza wamelazimika kuyakimbia makazi yao.Juhudi za ushirikiano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kusaidia kupunguza hali hiyo ya kukatisha tamaa zinaendelea na hapo jana Shirika lake la Mpango wa Chakula Duniani WFP lilifanikiwa kufikisha Msaada mjini Gaza ambapo hawakuwahi kufika tangu tarehe 20 Februari.Shirika jingine la UN lile la Afya WHO na wadau wake nao walifanikiwa kufikia hospital mbili zilizoko Gaza Kaskazini Al Shifa na Al Helo una kufikisha misaada ya vifaa tiba pamoja na mafuta ya kuendeshea mitambo ya hospitali. Hata hivyo mkuu wa shirika hilo la WHO Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus kupitia mtandao wa X alisema kuwa Hospitali ya Al Shifa ilikuwa na inafanya kazi sehemu ndogo tu na inahitaji haraka wafanyakazi maalum wa afya.Mahitaji yanasalia kuwa makubwa na ya haraka katika hospitali ya Al Helou, Dkt. Tedros aliongeza, huku huduma zikiwa chache katika idara zote, pamoja na uhaba wa mafuta, chakula, vifaa vya upasuaji na wafanyikazi wa matibabu.
13-3-2024 • 2 minuten, 48 seconden
Watoto waliouawa Gaza ni wengi kuliko miaka 4 ya vita duniani
Wakati kukiwa na ripoti za mashambulizi kwa njia ya anga yanayotekelezwa na Israel huko Gaza usiku wa kuamkia leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limesema idadi ya watoto waliouawa katika miezi ya hivi karibuni ni kubwa kuliko miaka minne ya mizozo duniani. Phillipe Lazzarini ambaye ni Mkuu wa shirika hilo la msaada kwa wakimbizi wa kipalestina hii leo kupitia mtandao wake wa X zamani Twitter ameandika ujumbe alioambatanisha na mchoro unaoonesha mambo mamwili kushoto kwenye rangi ya buluu idadi ya watoto waliouawa kutokana na vita tangu mwaka 2019 mpaka 2022 ambao ni 12, 193 na kulia ni idadi ya watoto waliouawa Gaza tangu mwezi Oktoba mwaka jana 2023 mpaka mwezi Februari 2024 ambao ni zaidi ya 12,300. Na ndipo akaandika ujumbe kuwa “Vita hii ni vita dhidi ya watoto. Ni vita dhidi ya utoto wao na mustakabali wao.”Mkuu huyo wa UNRWA akaendelea na ujumbe wake na kusema kuwa “Sitisheni mapigano sasa kwa ajili ya watoto wa Gaza“.Kwa mujibu wa takwimu kutoka mamlaka za afya huko Gaza, mpaka sasa zaidi ya wapalestina 31,184 wameuawa na wengine 72,889 kujeruhiwa. Mpaka kufikia tarehe 12 ya mwezi huu wa Machi, wanajeshi 247 wa Israel wameripotiwa kuuawa na wengine 1,475 kujeruhiwa tangu kuanza kwa operesheni za ardhini kwa mujibu wa takwimu za jeshi la Israel. Sio mashambulizi tu ya mabomu yanayo gharimu maisha ya watoto na wakazi wa Gaza, janga la njaa nalo pia lipo hatihati kukumba wananchi hao ambao a misaada ya kibiandamu kuwafikia imekuwa changamoto kubwa. Mashirika ya Umoja wa Mataifa ya kibinadamu yamekuwa yakirejea kutoa maonyo kuhusu hali mbaya ya Gaza ambapo mtu mmoja kati ya wanne anakaribia kukumbwa na njaa. Mpaka sasa takriban watu 25 wamekufa kutokana na utapiamlo mkali na upungufu wa maji mwilini kaskazini mwa Gaza kulingana na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada, OCHA, 21 kati yao wakiripotiwa kuwa watoto.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limeonya kuwa vijana ni miongoni mwa wale ambao hawawezi kustahimili njaa na magonjwa, huku vijana milioni moja wakiwa tayari wameondolewa makwao kutokana na vita, na watoto 17,000 wasio na wasindikizaji au waliotenganishwa nao sawa na 1% ya watu milioni 1.7 ya wananchi wa Gaza wamelazimika kuyakimbia makazi yao.Juhudi za ushirikiano wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa kusaidia kupunguza hali hiyo ya kukatisha tamaa zinaendelea na hapo jana Shirika lake la Mpango wa Chakula Duniani WFP lilifanikiwa kufikisha Msaada mjini Gaza ambapo hawakuwahi kufika tangu tarehe 20 Februari.Shirika jingine la UN lile la Afya WHO na wadau wake nao walifanikiwa kufikia hospital mbili zilizoko Gaza Kaskazini Al Shifa na Al Helo una kufikisha misaada ya vifaa tiba pamoja na mafuta ya kuendeshea mitambo ya hospitali. Hata hivyo mkuu wa shirika hilo la WHO Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus kupitia mtandao wa X alisema kuwa Hospitali ya Al Shifa ilikuwa na inafanya kazi sehemu ndogo tu na inahitaji haraka wafanyakazi maalum wa afya.Mahitaji yanasalia kuwa makubwa na ya haraka katika hospitali ya Al Helou, Dkt. Tedros aliongeza, huku huduma zikiwa chache katika idara zote, pamoja na uhaba wa mafuta, chakula, vifaa vya upasuaji na wafanyikazi wa matibabu.
13-3-2024 • 2 minuten, 48 seconden
13 JANUARY 2024
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko Gaza na afya ya watoto chini ya umri wa miaka 5. Makala tunakupeleka nchini Kenya na Mashinani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Wakati kukiwa na ripoti za mashambulizi kwa njia ya anga yanayotekelezwa na Israel huko Gaza usiku wa kuamkia leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limesema idadi ya watoto waliouawa katika miezi ya hivi karibuni ni kubwa kuliko miaka minne ya mizozo duniani kote.Idadi ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 duniani kote imepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi kuwahi kufikiwa katika historia, ambapo takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa mwaka 2022 idadi ya vifo ilikuwa chini ya milioni 4.9, sawa na pungufu kwa asilimia 51 tangu mwaka 2000. Makala inatupeleka Nairobi, Kenya ambako Priscilla Lecomte wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Mratibu wa hatua dhidi ya majanga ya tabianchi na El Niño anazungumza na Mwanamuziki Frida Amani wa Tanzania. Frida Amani anatoa wito kwa watoto wa kike duniani kutokatishwa tamaa kwa kuambiwa “usifanye shughuli fulani kwa kuwa ni ya kiume” kwani kama yeye angekata tamaa asingeweza kuwa msanii wa Hip Hop ambayo imemfikisha katika majukwaa ya kimataifa kiasi cha kuandaa wimbo wa kuhamasisha ushirikiano wa kimataifa katika kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, wimbo ambao umeungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Duniani (UNEP).Katika mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kusikia ujumbe wa mlinda amani mwanamke.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
13-3-2024 • 11 minuten, 42 seconden
13 JANUARY 2024
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko Gaza na afya ya watoto chini ya umri wa miaka 5. Makala tunakupeleka nchini Kenya na Mashinani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Wakati kukiwa na ripoti za mashambulizi kwa njia ya anga yanayotekelezwa na Israel huko Gaza usiku wa kuamkia leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA limesema idadi ya watoto waliouawa katika miezi ya hivi karibuni ni kubwa kuliko miaka minne ya mizozo duniani kote.Idadi ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 duniani kote imepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi kuwahi kufikiwa katika historia, ambapo takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa mwaka 2022 idadi ya vifo ilikuwa chini ya milioni 4.9, sawa na pungufu kwa asilimia 51 tangu mwaka 2000. Makala inatupeleka Nairobi, Kenya ambako Priscilla Lecomte wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Mratibu wa hatua dhidi ya majanga ya tabianchi na El Niño anazungumza na Mwanamuziki Frida Amani wa Tanzania. Frida Amani anatoa wito kwa watoto wa kike duniani kutokatishwa tamaa kwa kuambiwa “usifanye shughuli fulani kwa kuwa ni ya kiume” kwani kama yeye angekata tamaa asingeweza kuwa msanii wa Hip Hop ambayo imemfikisha katika majukwaa ya kimataifa kiasi cha kuandaa wimbo wa kuhamasisha ushirikiano wa kimataifa katika kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, wimbo ambao umeungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Duniani (UNEP).Katika mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kusikia ujumbe wa mlinda amani mwanamke.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
13-3-2024 • 11 minuten, 42 seconden
Juhudi za mashirika zafanikisha kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5
Idadi ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 duniani kote imepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi kuwahi kufikiwa katika historia, ambapo takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa mwaka 2022 idadi ya vifo ilikuwa chini ya milioni 4.9, sawa na pungufu kwa asilimia 51 tangu mwaka 2000. Ama hakika ni mafanikio makubwa kwani video iliyoambatana na habari hizi njema inaonesha madaktari, wakunga, wahudumu wa afya wakiwemo wale wa kijamii huko, Afrika, wakijituma kwa dhati kutoa huduma kuanzia kwa wajawazito, huduma za mama na mtoto hadi chanjo.Mathalani Sierra Leone anaonekana mhudumu wa afya akifika moja ya kaya kutoa huduma ya chanjo dhidi ya Numonia au vichomi.Cambodia, Malawi, Mongolia na Rwanda zimetajwa kuwa ni nchi ambamo idadi ya vifo vya watoto hao imepungua kwa zaidi ya asilimia 75 kati ya 2000 na 2022.Ripoti imetolewa na kundi la mashirika na taasisi ya Umoja wa Mataifa, IGME, linaloongozwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo Mkurugenzi Mtendaji wake Catherine Russell amepongeza juhudi za mtu mmoja mmoja, serikali, wakunga, wahudumu wa afya wakiwemo wale wa kijamii.Amesema kujituma kwao katika kuhakikisha watoto wanafikishiwa huduma bora na fanisi za afya tena kwa gharama nafuu, kumethibitisha kuwa dunia ina ufahamu na mbinu za kuokoa maisha.Licha ya mafanikio hayo, ripoti inaonya kuwa bado safari ni ndefu kufikia lengo la kutokomeza vifo vya watoto vinavyoweza kuzuilika, kwa kuwa mamilioni wanaendelea kufariki dunia kutokana na magonjwa yanayotibika, changamoto za ujautizo, vichomi au numonia, kuhara na malaria.Idadi kubwa ya vifo hivyo ni katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara na kusini mwa Asia, hali inayodhihirisha tofauti za kikanda katika upatikanaji wa huduma bora za afya.Ripoti imetambua pia ukosefu wa utulivu kiuchumi, mizozo, mabadiliko ya tabianchi na changamoto zilizoachwa kutokana na janga la COVID-19, ikisema mambo hayo yanazidi kuchochea tofauti za usawa kwenye utoaji wa huduma za afya.Kundi hilo linaitwa IGME na linajumuisha mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la kuhudumia watoto, UNICEF, la afya, WHO, Benki ya Dunia na kitengo cha Idadi ya Watu cha Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, DESA.IGME ilianzishwa mwaka 2004 kuwezesha wasihrika kubadilishana takwimu na kuboresha mbinu kwa ajili ya takwimu za vifo vya watoto na kufuatilia maendeleo kuelekea kufikia malengo kuhusu uhai wa mtoto.
13-3-2024 • 2 minuten, 8 seconden
Juhudi za mashirika zafanikisha kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5
Idadi ya vifo vya watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 duniani kote imepungua na kufikia kiwango cha chini zaidi kuwahi kufikiwa katika historia, ambapo takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa mwaka 2022 idadi ya vifo ilikuwa chini ya milioni 4.9, sawa na pungufu kwa asilimia 51 tangu mwaka 2000. Ama hakika ni mafanikio makubwa kwani video iliyoambatana na habari hizi njema inaonesha madaktari, wakunga, wahudumu wa afya wakiwemo wale wa kijamii huko, Afrika, wakijituma kwa dhati kutoa huduma kuanzia kwa wajawazito, huduma za mama na mtoto hadi chanjo.Mathalani Sierra Leone anaonekana mhudumu wa afya akifika moja ya kaya kutoa huduma ya chanjo dhidi ya Numonia au vichomi.Cambodia, Malawi, Mongolia na Rwanda zimetajwa kuwa ni nchi ambamo idadi ya vifo vya watoto hao imepungua kwa zaidi ya asilimia 75 kati ya 2000 na 2022.Ripoti imetolewa na kundi la mashirika na taasisi ya Umoja wa Mataifa, IGME, linaloongozwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo Mkurugenzi Mtendaji wake Catherine Russell amepongeza juhudi za mtu mmoja mmoja, serikali, wakunga, wahudumu wa afya wakiwemo wale wa kijamii.Amesema kujituma kwao katika kuhakikisha watoto wanafikishiwa huduma bora na fanisi za afya tena kwa gharama nafuu, kumethibitisha kuwa dunia ina ufahamu na mbinu za kuokoa maisha.Licha ya mafanikio hayo, ripoti inaonya kuwa bado safari ni ndefu kufikia lengo la kutokomeza vifo vya watoto vinavyoweza kuzuilika, kwa kuwa mamilioni wanaendelea kufariki dunia kutokana na magonjwa yanayotibika, changamoto za ujautizo, vichomi au numonia, kuhara na malaria.Idadi kubwa ya vifo hivyo ni katika nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara na kusini mwa Asia, hali inayodhihirisha tofauti za kikanda katika upatikanaji wa huduma bora za afya.Ripoti imetambua pia ukosefu wa utulivu kiuchumi, mizozo, mabadiliko ya tabianchi na changamoto zilizoachwa kutokana na janga la COVID-19, ikisema mambo hayo yanazidi kuchochea tofauti za usawa kwenye utoaji wa huduma za afya.Kundi hilo linaitwa IGME na linajumuisha mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la kuhudumia watoto, UNICEF, la afya, WHO, Benki ya Dunia na kitengo cha Idadi ya Watu cha Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii, DESA.IGME ilianzishwa mwaka 2004 kuwezesha wasihrika kubadilishana takwimu na kuboresha mbinu kwa ajili ya takwimu za vifo vya watoto na kufuatilia maendeleo kuelekea kufikia malengo kuhusu uhai wa mtoto.
13-3-2024 • 2 minuten, 8 seconden
12 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini India ambapo wahandisi wa usanifu majengo waliodhamiria kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kupunguza changamoto ya hewa ukaa katika sekta ya ujenzi kwa kutumia matofali ya matope. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani kama zifuatazo. Meli iliyosheheni misaada ya kibinadamu imeanza safari yake kutoka Cyprus kuelekea Gaza ikiwa na shehena ya tani 200 za misaada ya kuokoa maisha kwa ajili ya wananchi wa Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP hii leo linaonya kuwa litalazimika kusitisha misaada ya kuokoa maisha nchini Chad ifikapo mwezi ujao wa Aprili iwapo litakosa ufadhili wa haraka kwa ajili ya kusaidia wakimbizi. Na mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, ukiendelea hapa jijini New York Marekani hii leo kutakuwa na mikutano ya kujadili mambo mbalimbali ikiwemo hali ya wanawake nchini Afghanistan, kuziba pengo la kujinsia kwenye elimu, athari za umaskini na uhalifu katika huduma ya utoaji mimba pamoja na mkutano wa kuangalia jinsi mabunge yanayozingatia jinsia katika kuendeleza usawa wa kijinsia ili kumaliza umaskini.Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Marynsia Mangu, kijana kutoka Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Success Hands Tanzania anayeshiriki mkutano wa 68 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW68 hapa New York, Marekani akielezea matarajio yake kwenye mkutano huu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
12-3-2024 • 11 minuten, 6 seconden
Mlo shuleni umeongeza idadi ya wanafunzi wangu shule ya Salama: Mwalimu Beatrice Nyakoa Osaka
Shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya UNIS Nairobi amefunga safari hadi shuleni Salama na kuzungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo Beatrice Nyakoa Osaka anayeenza kwa kufafanua umuhimu wa mradi huo shuleni kwake hasa kutokana na eneo walipo.
11-3-2024 • 6 minuten, 7 seconden
Mashambulizi na umwagaji damu vinaendelea Gaza licha ya kuanza kwa Ramadhan mauaji - Guterres
Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo. Hivyo ndivyo alivyoanza Katibu Mkuu katika tarifa yake fupi kwa waandishi wa habari akikumbusha kuwa ni hivi majuzi tuliingia mwezi wa sita tangu shambulio la kigaidi la Hamas nchini Israel na mashambulizi mabaya ya Israel huko Gaza. Ameo leo ana ombi kubwa ambalo ni “kuheshimu dhamira ya Ramadhani kwa kunyamazisha mtutu wa bunduki na kuondoa vikwazo vyote ili kuhakikisha utoaji wa misaada ya kuokoa maisha kwa kasi na kiwango kikubwa kinachohitajika.”Pia ametaka wakati huohuo kwa kuzingatia dhamira ya Ramadhani kuwaachilia mateka wote wanaoshikiliwa mara moja. Katibu Mkuu ameonya kwamba “Macho yadunia yanatazama. Macho ya historia yanatazama. Hatuwezi kuyapa kisogo yanayoendelea ni lazima tuchukue hatua kuepusha vifo vinavyoweza kuzuilika.” Amesema Dunia imeshuhudia mwezi baada ya mwezi mauaji ya raia na uharibifu wa miundombinu ya raia kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea katika miaka yangu yote akiwa Katibu Mkuu. Na kwamba msaada wa kuokoa Maisha kwa raia Gaza unaingia kwa vikwazo vikbwa na wakati mwingine hauingii kabisa.Amesema hivi sasa Sheria ya kimataifa za kibinadamu ziko katika hali mbaya.Na tishio la Israel kushambulia Rafah zinaweza kuwatumbukiza kuzimu zaidi watu wa Gaza.Amesema pamoja na kwamba viongozi wa Dunia na wahudumu wa kibinadamu wamekuwa wakitoa wito wa kusitishwa mapigano wito mahsusi umetoka kwa familia za waathirika wa vita hivi. Sitasahau mikutano yangu pamoja nao na wamesimama kwenye jukwaa hili na kukuhutubia wameungana kwa ujasiri mkubwa na maumivu yasiyopimika. Familia za mateka wa Israeli ambao wameeleza mateso na uchungu wao na wameomba kuachiliwa mara moja kwa wapendwa wao. Pia alikutana na familia za waathirika wa Gaza ambazi zimeomba uhasama kutishishwa mara moja “Kama mmoja wa wanafamilia hao alisema, Hatuko hapa kwa ajili ya rambirambi. Hatupo hapa kwa ajili ya kuomba msamaha. Tuko hapa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za haraka. Je, hili ni kubwa sana kuliomba? Ni lazima tusikilize na kutii sauti hizo.” Amesesisitiza Guterres. Pia amesema leo anatoa ombi la usitishaji uhasama Sudan kwa ajili ya Ramadhani na kukumbusha kwamba hivi karibuni mwezi Aprili kutakuwa na Sikukuu za Pasaka na sikukuu ya Wayahudi ya Passover hivyo huu ni wakati wa kuonyesha huruma, kuchukua hatua na kurejesha Amani.
11-3-2024 • 2 minuten, 53 seconden
Mlo shuleni umeongeza idadi ya wanafunzi wangu shule ya Salama: Mwalimu Beatrice Osaka
Shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Kenya UNIS Nairobi amefunga safari hadi shuleni Salama na kuzungumza na mwalimu mkuu wa shule hiyo Beatrice Nyakoa Osaka anayeenza kwa kufafanua umuhimu wa mradi huo shuleni kwake hasa kutokana na eneo walipo
11-3-2024 • 5 minuten, 8 seconden
11 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu mwezi mktukufu wa Ramadhan, na uwezeshaji wa wanawake wakulima nchini Malawai. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni? Leo ni mwanzo wa mwezi mktukufu wa Ramadhan ambapo Waislamu kote duniani husherehekea na kuchagiza tunu za amani, maridhiano na mshikamano lakini uhasama unaendelea hususani sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Gaza ambako mauaji , na mashambulizi hayajakoma amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza na waandishi wa habari mjini New York Marekani hii leo.Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. Makala inatupeleka katika shule ya Salama iliyo katika eneo la Huruma karibu na mtaa wa mabanda wa Mathare jijini Nairobi Kenya hivi karibuni imeanza programu ya mlo shuleni kupitia mradi wa kampuni ya ‘Food for Education”. Hatua hiyo imenfa idadi ya wanafunzi wanaosoma shule hiyo kuongezeka kutoka 1, 900 hadi 2,300. Mlo shuleni ni moja ya masuala ambayo yanapigiwa debe kubwa na Umoja wa Mataifa sio tu kwa sababu ya kuhakikisha lishe bora kwa mamia ya maelfu ya wanafunzi ambao wengi hawawezi kupata mlo nyumbani bali pia kuongeza idadi ya watoto wanaohudhuria masomo.Na mashinanitunasalia nchini Kenya kumulika jinsi mradi wa FAO umemwezesha msichana mwenye ulemavu kuondokana na msongo wa mawazo na kisha kujikwamua kiuchumi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
11-3-2024 • 13 minuten, 28 seconden
IFAD: Mradi wa ukulima nchini Malawi waboresha maisha ya na usawa kijinsia katika jamii
Nchini Malawi Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo IFAD unatekeleza mradi wa kuwasaidia wanawake wa vijijini kukabiliana na ukosefu wa usawa wa kijinsia na sasa wananachi wanafaidi matunda yake. Mradi huo uitwao TRADE ulioanzishwa mwaka 2022 na serikali ya Malawi kwa kushirikiana na IFAD inalenga kubadilisha kilimo kupitia mpango wake wa Mseto na Ujasiriamali. Amos Mailosi ni Afisa Mazingira wa kanda Mabadiliko ya Tabianchi wa mradi huo wa TRADE na anasema jambo muhimu katika mradi wao ni kuhakikisha familia zinafanya kazi na kufikia maamuzi pamoja. “Moja ya eneo muhimu katika programu yetu ya TRADE ni kuhamasisha suala la ushirikishwaji wa kijinsia ndani ya jamii. Kwa hivyo, tunajaribu kuwawezesha wanawake na wanaume, na wavulana na wasichana, kushiriki kwa usawa katika afua. Ili kwa pamoja waweze kutambua umuhimu wa kufanya maamuzi ya pamoja katika ngazi ya kaya.”Kwa miaka mwili sasa mafanikio yameanza kuoneskana, na mmoja wa wanufaika hao ni Alefu Ofesa na mume wake Lloyd ambao wamekuwa wakulima kwa miaka 20 lakini kwa takriban miaka miwili wamebadili kilimo kuwa biashara. Mabadiliko haya yamefuatitia Alefa na wanawake wenzake kijijini kupatiwa Msaada na mafunzo ya mbinu mpya za kilimo ambazo zimewasaidia kukabiliana na mvua zisizokuwa na uhakika katika ukanda huo. “Mradi huu umekuwa ukihimiza wanawake kushiriki katika kilimo. Kwa ujuzi na maarifa tuliyopatiwa tuna uhakika kuhusu kile kinachohitajika kufanywa ili kuboresha uzalishaji, kwa mfano upandaji kwa kutumia mistari miwili. Wanawake wengi hapa sasa ni wataalam wa shughuli za kilimo na kwa sababu ya faida wanazopata, wengi wametambua umuhimu wa kujiunga pamoja.”Alefa amepanga kutumia mapato ya ziada wanayopata kwa ajili ya kuwapatia elimu watoto wao na kununua kigari cha ng'ombe kwa ajili ya usafiri. Sio tu kwamba familia yake sasa ina chakula cha kutosha kwa mwaka mzima, lakini sasa anaweza pia kuuza sehemu ya kile anachovuna, na anapanga kupanua biashara yake ili kuuza kwenye masoko katika vijiji vya jirani.
11-3-2024 • 2 minuten, 18 seconden
KIGOMa: Mafunzo ya kilimo hifadhi kutoka FAO chaongeza mavuno mahindi kutoka magunia 4 hadi 45
Sasa ni makala inayotupeleka mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limetekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa siku ya wanawake duniani, Wekeza kwa Wanawake, Songesha Maendeleo, kwa kuwapatia mafunzo ya ufugaji bora wa kuku na mbuzi, halikadhalika kilimo hifadhi kisichoharibu mazingira. Sasa manufaa yako dhahiri kwani wanawake wameinuka kiuchumi. Miongoni mwao ni Hadija Alisido, mkazi wa kijiji Muhange, wilaya ya Kakonko. Katika makala hii inayoletwa kwako na Assumpta Massoi wa Idhaa hii, Hadija anaelezea alivyoinuliwa na FAO.
8-3-2024 • 3 minuten, 50 seconden
08 MACHI 2024
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Flora Nducha anamulika siku ya wanawake duniani kuanzia habari ya kwanza hadi ya mwisho maudhui yakiwa Wekeza kwa wanawake - songesha maendeleo.Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani kote Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wanawake na wasichana kwa kupata mafanikio makubwa na kuondoa vikwazo, kuvunja fikra potofu na kuchochea maendeleo kuelekea dunia yenye haki na usawa zaidi.Nchini Afrika Kusini katika jimbo la Western Cape kufuatia mafunzo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia yaliyotolewa na kikundi cha wanawake cha Ilitha Labantu kwa vituo kadhaa vya polisi, sasa kuna ushahidi wa wazi kwamba vituo vya polisi vimeweka mazingira rafiki ya kuwasikiliza wanawake walionyanyaswa kuliko ilivyokuwa hapo awali. Anold Kayanda ameufuatilia mradi huo.Makala inatupeleka Kigoma nchini Tanzania kumsikia shuhuda Hadija Alisido ambaye amenufaika na miradi ya FAO.Mashinani tunabisha hodi Mwanza nchini Tanzania kupata maoni kuhusu siku ya wanawake duniani. Karibu!
8-3-2024 • 11 minuten, 38 seconden
Ukatili dhidi ya wanawake Afrika kusini: Polisi 'wanolewa' sasa mambo ni shwari
Nchini Afrika Kusini katika jimbo la Western Cape kufuatia mafunzo kuhusu unyanyasaji wa kijinsia yaliyotolewa na kikundi cha wanawake cha Ilitha Labantu kwa vituo kadhaa vya polisi, sasa kuna ushahidi wa wazi kwamba vituo vya polisi vimeweka mazingira rafiki ya kuwasikiliza wanawake walionyanyaswa kuliko ilivyokuwa hapo awali. Anold Kayanda ameufuatilia mradi huo. Karibu Anold utueleze zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Asante sana Flora Nducha. Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake (UN Women) linasema kiwango cha unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana nchini Afrika Kusini ni miongoni mwa viwango vya juu zaidi duniani na wanafafanua wakisema kwamba mwanamke mmoja kati ya watano walio katika uhusiano amepitia ukatili wa kimwili uliofanywa na mpenzi wake.Wengi zaidi wameteseka na aina nyingine za vurugu kutoka kwa wanaume wanaowajua na wasiowajua lakini changamoto zaidi ni namna ya kuyashughulikia masuala haya kwani matukio mengi ya unyanyasaji hayaripotiwi kwa mamlaka kutokana na imani ndogo kwa vyombo vya sheria.Ella Mangisa, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo la Ilitha Labantu anasema ulikuwa unakuta mwanamke anayekimbia hali ya vurugu, akifika polisi ataambiwa arudi nyumbani akaelewane na mnyanyasaji wake au kuambiwa haya ni masuala ya kibinafsi wanayohitaji kutatua wao wenyewe."Kupitia ushirikiano na UN Women na wadau wengine ndipo Ilitha Labantu mwaka 2021 ilizindua mpango wa kufanya kazi na Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini (SAPS) kuwaelimisha maafisa kufanya kazi na waathirika wa ukatili wa kijinsia. Mpango umetekelezwa katika vituo 75 vya polisi huko Cape Metro na Cape Winelands katika Mkoa wa Western Cape.Ilitha Labantu inapanga kupanua zaidi mpango huo na kushirikisha mashirika mengine yenye utaalamu tofauti. Shirika hilo pia linatarajia kujumuisha maudhui ya mafunzo yao katika mtaala wa vyuo vya polisi kote nchini Afrika Kusini.
8-3-2024 • 1 minuut, 54 seconden
Kuwekeza kwa wanawake ni jawabu sahihi - Guterres
Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani kote Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapongeza wanawake na wasichana kwa kupata mafanikio makubwa na kuondoa vikwazo, kuvunja fikra potofu na kuchochea maendeleo kuelekea dunia yenye haki na usawa zaidi. Leah Mushi na maelezo zaidi.Katika ujumbe wake kwa siku hii Katibu Mkuu Guterres amesema “Pamoja na juhudi wanazozifanya kila siku bado wanakabiliwa na vikwazo vikubwa. Mabilioni ya wanawake na wasichana wanakabiliwa na kuenguliwa, ukosefu wa haki na ubaguzi, ilhali janga lililojikita la ukatili dhidi ya wanawake lilikimomonyoa ubinamu.”Amesema ni vyema kuongeza juhudi ikiwemo za kisheria katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanawake kwani kwa kasi ya sasa itachukua miaka miatatu kupata usawa.Akieleza nini kifanyike amesema “ tunapaswa kuwekeza kwenye miradi ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na kuchochea ujumuishaji wanawake na uongozi wa wanawake kwenye uchumi, teknolojia za kidijitali, ujenzi wa amani na hatua kwa tabianchi.Yote hii inategemea kupatikana kwa fedha kwa ajili ya maendeleo endelevu ili nchi ziwe na fedha za kuwekeza kwa wanawake na wasichana.”Kauli mbiu ya siku ya wanawake kwa mwaka huu ni wekeza kwa wanawake ili kuharakisha maendeleo na Mkuu huyo wa umoja wa Mataifa amesema inatukumbusha kuwa kutokomeza mfumo dume kunahitaji kuweko kwa fedha mezani.“Tunahitaji pia kuongeza idadi ya wanawake viongozi kwenye sekta ya biashara, Benki Kuu na Wizara za Fedha. Hii inaweza kusaidia kuchochea uwekezaji kwenye sera na miradi inayokidhi mahitaji ya wanawake na wasichana.Haki za wanawake zimedhihirisha kuwa njia ya haki ya jamii zenye haki, amani na ustawi. Hii ni vema kwetu sote. “Kwa Pamoja, hebu na tuchukue hatua za haraka kufanya kuwa halisia.”Usawa kwa woteNalo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women linaadhimisha siku hii kwa kufanya mkutano mkubwa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani utakao wakutanisha pamoja viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa masuala ya wanawake. UN Women wamesema katika mwaka huu ambapo karibu nusu ya watu duniani wanaishi katika nchi zinazoshiriki katika uchaguzi, Siku hii ya Kimataifa ya Wanawake ni fursa muhimu ya kufafanua siku zijazo tunazotaka.Wakati mizozo, mabadiliko ya tabianchi na jamii zenye mgawanyiko zikididimiza miongo kadhaa ya maendeleo katika usawa wa kijinsia, UN Women inatoa wito waku "Wekeza kwa wanawake ili Kuharakisha Maendeleo" ili hatimae dunia iweze kufikia faida ya usawa wa kijinsia kwa wote.
8-3-2024 • 2 minuten, 48 seconden
07 Machi 2024
Hii leo jaridani tunaangazia miradi inayotekelezwa na Umoja wa Mataifa huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo -DRC kusaidia wanawake ikiwa ni kuelekea siku ya wanawake duniani hapo kesho Machi 8. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na kujifunza lugha ya kiswahili ambapo leo ni ufafanuzi wa methali 'AFUNGAYE KIBWEBWE SI BURE ANA MCHEZO'
7-3-2024 • 11 minuten, 43 seconden
Wanawake na wasichana wakiwezeshwa jamii zinanufaika - Wanabiashara Kenya
Wiki hii Ijumaa tarehe 8 Machi 2024, ulimwengu utaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ambapo mwaka huu ina maudhui “Wekeza kwa wanawake: Harakisha maendeleo,” lakini Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women linasema ni dhahiri kwamba ulimwengu bado unakabiliwa na migogoro mingi, kuanzia mizozo ya kijiografia hadi viwango vya umaskini vinavyoongezeka, ukosefu wa usawa na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi.Kwa kuwekeza kwa wanawake, tunaweza kuibua mabadiliko na kuharakisha mpito kuelekea dunia yenye afya, usalama na usawa zaidi kwa wote. Nchini Kenya tunakutana na mama mjasiriamali ambaye alianza kwa kufanya kazi na shirika lisilo la kiserikali liitwalo Sime Food, ambalo linahusika na kilimo endelevu, lishe bora, na stadi za biashara ndogo ndogo ili wawe na maarifa na ujuzi unaohitajika ili kupatia familia zao lishe bora mwaka mzima na kuuza masalio ili kusaidia kulipia mahitaji mengine ya kaya. Baada ya kupata mafunzo hayo na fedha za kuanzisha biashara zake, Lucy anachochea kinamama na vijana wa kike wajiunge naye katika sekta ya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi. Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amefuatilia na kutuandalia makala hii.
6-3-2024 • 4 minuten, 19 seconden
06 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mizozo na janga la kibinadamu nchini Sudan, na kuondoka kwa MONUSCO nchini DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Uganda, kulikoni? Takriban miezi 11 tangu majenerali wapinzani watangaze vita nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo walionya kwamba mzozo huo unaweza kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani.Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, za kuondoka nchini humo zikiendelea, tunamulika hatua chanya zilizochukuliwa na ujumbe huo katika kunusuru vijana waliokuwa wanatumikishwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo. Katika makala na tukielekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo mwaka huu ina maudhui “Wekeza kwa wanawake: Harakisha maendeleo,”, tunatembelea wajasiriamali Kajiado nchini Kenya kusiki ni kwa jinsi gani wanawezakujiumudu kiuchumi.Na mashinani tunaelekea nchini Uganda kumsikia mkimbizi kutoka nchini Sudan Kusini.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
6-3-2024 • 12 minuten, 4 seconden
Mtoto Charles: MONUSCO imenitoa msituni, asanteni sana
Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, za kuondoka nchini humo zikiendelea, tunamulika hatua chanya zilizochukuliwa na ujumbe huo katika kunusuru vijana waliokuwa wanatumikishwa na waasi mashariki mwa nchi hiyo.Miongoni mwao ni Charles, mwenye umri wa miaka 16 ambaye si jina lake halisi. Yeye alitumikishwa msituni na waasi kwa kipindi cha miaka miwili.Akizungumza huku sura yake ikiwa imefichwa kwenye video ya MONUSCO, Charles anakumbuka kuwa walikuwa shambani wanalima wakati waasi wa Mai Mai walipofika na kuwakamata.“Walitueleza kuwa hawana watu wa kuwasaidia mapigano hivyo wakatuchukua. Tulipofika walituona kuwa tuna mawazo ya kutoroka hivyo walitufungia ndani kwa wiki tatu,” anasema Charles.Anasema walipotoka fikra za kutoroka zikatoweka, wakafundishwa kupigana msituni na walipigana mara sita. Lakini haikuwa rahisi kwani wenzake 12 waliuawa huku porini wakati wa mapigano huku yeye mwenyewe akishuhudia.“Niliumia sana. Chakula nacho kilikuwa shida kupata, maisha yalikuwa magumu mno. Nikafikiria nikaona bora nirejee kwa familia yangu.’Walichofanya yeye na wenzake, usiku wa saa saba walitoroka hadi mji wa jirani ambako huko walijisalimisha kwa kiongozi mmoja na kumweleza kuwa wamechoka kuishi na kupigana porini.Kiongozi huyo aliwachukua na kuwapeleka Beni, mji ulioko jimboni Kivu Kaskazini.Charles anasema kiongozi huyo aliwasaidia kuwakutanisha na shirika la kiraia la ACOPE, mdau wa MONUSCO. Hapo walipata mafunzo kwa wiki tatu ikiwemo utengenezaji majiko banifu yasiyochafua mazingira.“Sasa maisha ni mazuri hapa na wito wangu kwa wale watoto na vijana walioko msituni wakipigana ni kwamba waondoke huko waache kupigana, waje wajisalimishe kwa serikali ili waweze kujiendeleza.”
6-3-2024 • 2 minuten, 19 seconden
WFP/UNICEF: Janga kubwa la njaa duniani linanyemelea Sudan miezi 11 baada ya kuzuka vita
Takriban miezi 11 tangu majenerali wapinzani watangaze vita nchini Sudan, wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo walionya kwamba mzozo huo unaweza kusababisha janga kubwa zaidi la njaa duniani. Sudan, nchi iliyo kaskazini mashariki mwa Afrika tayari iko katika mzozo mkubwa zaidi wa watu waliofuriushwa makwao duniani kwa mujibu, Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa, WFP.Na mapigano yanayoendelea kati ya Jeshi la Sudan SAF na kundi hasimu la msaada wa haraka RSF yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine milioni nane kuyahama makazi yao ndani ya nchi na wengine kukimbilia nchi jirani.Hivi sasa watoto milioni 14 wanahitaji haraka msaada wa kuokoa maisha, limesema Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF katika tahadhari yale ya hivi karibuni, huku kukiwa na wasiwasi kwamba mzozo huo unaweza kuenea kwenye mipaka ya Sudan, na kutishia maisha na amani katika eneo hilo, endapo mapigano hayo hayatokoma.Cindy McCain, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa WFP amesema "Miaka ishirini iliyopita, Darfur ilikuwa janga kubwa zaidi la njaa duniani na ulimwengu ulijitolea kuchukua hatua. Lakini leo hii watu wa Sudan wamesahaulika. Mamilioni ya maisha ya watu, amani na utulivu wa eneo zima viko hatarini,” Bi. McCain ameyasema hayo akiwa Sudan Kusini, ambako amekutana na familia zilizokimbia ghasia na hali mbaya ya njaa Sudan na kuingia hiyo jirani zao. Amesema hivi sasa WFP inahaha kutimiza mahitaji ya chakula na kuongeza kuwa "Nimekutana na kina mama na watoto ambao wamekimbia Sudan ili kuokoa maisha yao sio mara moja, lakini mara nyingi, na sasa njaa inawanyemelea. Madhara ya kutochukua hatua yanakwenda mbali zaidi ya mama kushindwa kulisha mtoto wake na yataathili eneo hilo kwa miaka mingi ijayo”.WFP inasema leo hii chini ya mtu mmoja kati ya 20 Sudan ndiye anayeweza kumudu kupata chakula, watu 9 kati ya 10 wanakabiliwa na njaa na mgogoro wa chakula umesambaa hadi nchi jirani zinazohifadhi wakimbizi wa Sudan na kuathiri watu zaidi ya milioni 25 Sudan, Sudan Kusini, na Chad.
6-3-2024 • 2 minuten, 32 seconden
05 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada ambayo inaangazia jitihada za taasisi ya ProjeKt Inspire ya nchini Tanzania katika kuhamasisha masomo ya STEM yaani Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Gaza, haki za binadamu, ukulima na usawa wa kijinsia. Mashinani tukielekea siku ya wanawake duniani tutakupeleka katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya. Baada ya kukosa vibali vya kuingia eneo la Gaza Kaskazini tangu katikati ya mwezi Januari mwaka huu, hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limefanikiwa kuingia eneo hilo na kujionea hali ya wananchi na mahitaji ya afya yalivyo pamoja na kupeleka misaada ikiwemo vifaa vya matibabu na mafuta ya kuendeshea mitambo ya hospitali.Huko Geneva Uswisi mkutano wa 55 wa Baraza La Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeendelea leo ambapo Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu biashara na unyanyasaji wa kingono wa watoto Mama Fatima Singhateh ametaka kutambulika kwa hatua za mtu mmoja mmoja au za pamoja za kupambana na unyanyasaji wa kijinsia na unyonyaji wa watoto katika tasnia ya burudani na vyombo vya habari ili kukomeshwa unyanyasiji huo mara moja. Na tukiwa katika mwezi wa Machi unaoadhimisha siku ya wanawake duniani shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limezitaka nchi kuhakikisha zinashughulikia changamoto za usawa wa kijinsia kwenye kupambana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwani takwimu zinaonesha kuwa familia hususan za vijijini zinazoongozwa na wanawake zinaathirika zaidi na mabadiliko ya tabianchi ikilinganishwa na zile zinazoongozwa na wanaume.Na mashinani Jane Kamenya, Mama wa watoto wawili na mfyanyabiashara ya usukaji nywele kutoka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambaye kando na kupata manufaa na kuweza kujikwamua kiuchumi yeye anatoa wito kwa vijana na kinamama wajiunge naye katika jukumu muhimu ya wanawake la kuhakikisha jamii zao wameondokana na umaskini.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
5-3-2024 • 11 minuten, 24 seconden
Mchango wa wanawake katika kulinda mazingira ni wa thamani sana: Dkt. Josephine Ojiambo
Katika kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo itaadhimishwa Ijumaa wiki hii Machi 8 mchango wa wanawake katika kulinda na kuhifadhi mazingira umeelezwa kuwa ni mkubwa na wa thamani sana. Kandoni mwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 uliofanyika Nairobi Kenya na kukunja jamvi mwishoni mwa wiki, nada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo mchango wa wanawake. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS alizungumza na Balozi na mtafiti katika Mradi wa Green Transition nchini Kenya Dkt. Josephine Ojiambo kuzungumzia mchango huo wa wanawake katika kulinda mazingira.
4-3-2024 • 3 minuten, 57 seconden
UN inaonya kwamba vita ya Gaza yaweza kuchochea machafuko zaidi ya kikanda
Mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza yanaendelea nchini Misri kwa siku ya pili leo huku Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akionya kwamba vita ya Gaza iko katika hatari ya kubadili mweleko na kupanua wigo zaidi utakaoathiri kila nchi Mashariki ya Kati na kwingineko. Asante Anold. Kamishina Mkuu Volker Türk ameliambia Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mjini Geneva Uswisi kuwa "Nina wasiwasi mkubwa kwamba katika janga hili la vita cheche yoyote zaidi inaweza kusababisha moto mkubwa zaidi," Katika taarifa ya hivi karibuni kuhusu migogoro ya kimataifa kwa Nchi 47 Wanachama wa Baraza hilo, Kamishna Mkuu alisisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa inapaswa kufanya "kila linalowezekana ili kuepuka kuenea zaidi kwa vita ya Gaza.”Maoni yake yanakuja huku kukiwa na wito wa "kusitishwa mara moja kwa mapigano kwa angalau wiki sita zijazo ili kuwezesha kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli.’Wito huo umetoka kwa Makamu wa Rais wa Merika Kamala Harris, wakati wa mazungumzo ya kimataifa ya kusitisha mapigano nchini Misri Jumapili, ambayo yanayoripotiwa kuhusisha Marekani wajumbe wa Qatar na Hamas lakini hadi sasa hakuna wawakilishi wa Israel.Bwana Türk amesema “Hatari za kuyumbisha usalama wa kikanda tayari zilionekana kusini mwa Lebanon, akisisitiza kwamba wapiganaji wa wanamgambo wanaoiunga mkono Palestina sasa wanahusika katika hali ya kusikitisha sana ya uhasama na majibizano ya risasi na Israeli, katika msitali wa Bluu wa uangalizi wa Umoja wa Mataifa unaotenganisha nchi zote mbili.Takriban watu 200 wameuawa nchini Lebanon tangu vita ilipozuka Gaza¸ Kamishna Mkuu amesema miongoni mwa waathirika wakubwa ni, watoto, wahudumu wa afya na waandishi wa habari.Mkuu huyo wa haki za binadamu ameongeza kuwa “takriban watu 90,000 nchini Lebanon wamekimbia makazi yao kutokana na ghasia hizo, huku kukiwa na uharibifu mkubwa wa vituo vya afya, shule na miundombinu muhimu. Jamii za Israeli pia zimeshuhudia watu 80,000 wakiondolewa kutoka maeneo ya mpakani kwa sababu ya kuongezeka kwa vurugu.”Mashirika ya kibinadamu yameendelea kuripoti kuhusu hali mbayá na ongezeko la vifo vya raia ambapo lile la kuhudumia watoto UNICEF mwishoni mwa wiki likisema hadi sasa watoto 15 wamepoteza Maisha katika hospitali ya Kamal Adwan mjini Gaza kutokana na utapiamlo na ukosefu wa maji mwilini.UNICEF imeonya kwamba watoto wengi zaidi watapoteza Maisha katika siku zijazo endapo msaada wa haraka unaohitajika hautofikishwa kunusuru Maisha yao.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake UN Women linakadiria kuwa wanawake 9,000 wameshauawa tangu vita ilipozuka Gaza miezi mitano iliyopita. Mamlaka ya afya ya Gaza inasema jumla ya watu waliopoteza Maisha tangu kuanza kwa vita Gaza ni zaidi ya 30,400 na inatarajiwa kuendelea kuongezeka.
4-3-2024 • 1 minuut, 41 seconden
04 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko katika ukanda wa Gaza na uondoaji wa mabomu ya kutegwa ardhini nchini Sudan Kusini. Makala inakupeleka nchini Kenya ambapo hivi karibuni kulifanyika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 na mashinani tutaelekea nhcini DR Congo.Mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza yanaendelea nchini Misri kwa siku ya pili leo huku Kamishina Mkuu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa akionya kwamba vita ya Gaza iko katika hatari ya kubadili mweleko na kupanua wigo zaidi utakaoathiri kila nchi Mashariki ya Kati na kwingineko..Nchini Sudan Kusini kwa mwaka jana pekee wateguaji wa mabomu ya ardhini wa Umoja wa Mataifa wamefanikiwa kusafisha eneo lenye ukubwa sawa na viwanja 64 vya mpira wa miguu, na hivyo kuondoa hatari nyingi za milipuko, inaeleza UNMISS ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini. Makala tukielekea siku ya wanawake duniani ambayo itaadhimishwa Ijumaa wiki hii Machi nane leo tuko Nairobi Kenya kumulika mchango wa wanawake katika kukabiliana na changamoto ya mazingira. Kandoni mwa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS alizungumza na Balozi na mtafiti katika Mradi wa Green Transition nchini Kenya Dkt. Josephine Ojiambo anayeanza kwa kueleza umuhimu wa wanawake katika kulinda mazingira.Na mashinani tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kumsikia mwanafunzi mmoja wa wanufaika wa programu ya (WFP) ya mlo shuleni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
4-3-2024 • 9 minuten, 57 seconden
UNMISS: Kuondoa mabomu ya ardhini Sudan Kusini eneo sawa na viwanja 64 vya soka limesafishwa
Nchini Sudan Kusini kwa mwaka jana pekee wateguaji wa mabomu ya ardhini wa Umoja wa Mataifa wamefanikiwa kusafisha eneo lenye ukubwa sawa na viwanja 64 vya mpira wa miguu, na hivyo kuondoa hatari nyingi za milipuko, inaeleza UNMISS ambao ni Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.Kupitia Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini (UNMAS) asilimia 70 ya vilipuzi ambavyo vilikuwa havijalipuka sasa vimeharibiwa au kuondolewa katika maeneo vilimokuwa na hivyo kuwahakikishia watu makazi salama na maeneo ya kilimo.Mike Fula Rashid, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Sudan ya Hatua dhidi ya Vilipuzi (NMAA) anapeleka shukrani kwa Umoja wa Mataifa akisema,"Tunashukuru kwa msaada ambao UNMAS inatupatia kuhusiana na uondoaji wa vilipuzi kwa sababu ukiangalia uwezo wa kuondoa mabomu nchini Sudan Kusini, asilimia 70 inaungwa mkono na UNMAS huku wafadhili wengine wakichangia asilimia 30 iliyobaki.”
4-3-2024 • 1 minuut, 6 seconden
Mtu 1 kati ya 4 anaishi na utipwatipwa duniani
Utafiti mpya uliotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza Lancet na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO unaonyesha kwamba, mwaka 2022, zaidi ya watu bilioni 1 duniani sasa wanaishi na unene wa kupindukia ama utipwa tipwa. Duniani kote, unene wa kupindukia kwa watu wazima umeongezeka zaidi ya mara mbili tangu mwaka 1990, na umepanda mara nne kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 5 hadi 19. Utafiti huo pia unaonyesha kwamba ingawa viwango vya utapiamlo vimepungua, bado ni changamoto kubwa ya afya ya umma katika maeneo mengi, hasa Asia Kusini Mashariki na Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.Nchi zenye viwango vya juu zaidi vya utipwatipwa na utapiamlo mwaka 2022 zilikuwa ni mataifa ya visiwa katika Pasifiki na Karibea, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema utafiti huu mpya unaangazia umuhimu wa kuzuia na kudhibiti unene wa kupindukia tangu utotoni hadi utu uzima kupitia lishe, mazoezi ya mwili, na huduma za kutosha kadri inavyohitajika.Ghebreyesus ameongeza kuwa ili kupambana na tatizo hilo ni sharti kurejea kwenye mstari ili kufikia malengo ya kimataifa ya kudhibiti unene wa kupindukia itahitaji kazi ya serikali na jamii, ikisaidiwa na sera za WHO na mashirika ya afya ya umma ya kitaifa na sekta binafsi. Kwa mujibu wa WHO, utapiamlo, katika aina zake zote, ni pamoja na kukonda, kudumaa, uzito mdogo, upungufu wa vitamini au madini, uzito kupita kiasi na unene kupita kiasi, hata hivyo ukosefu wa lishe bora huchangia nusu ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 na unene unaweza kusababisha magonjwa yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya moyo na mishipa, kisukari na baadhi ya saratani.Katika Mkutano wa Afya Duniani mwaka 2022, Mataifa Wanachama walikubaliana na Mpango wa WHO wa Kuongeza kasi ya Kusitisha Unene wa Kupindukia, unaounga mkono hatua za ngazi ya nchi hadi 2030. Hadi sasa, serikali 31 zinaongoza njia kudhibiti janga la unene wa kupindukia kwa kutekeleza mpango huo.Mkurugenzi wa Idara ya Lishe na Usalama wa Chakula wa WHO na mmoja wa waandishi wa utafiti huo Dkt. Francesco Branca amesema kuna changamoto kubwa katika utekelezaji wa sera zinazolenga kuhakikisha upatikanaji wa chakula bora kwa wote na kujenga mazingira ambayo yanakuza shughuli za kimwili na maisha ya afya kwa ujumla kwa kila mtu na kutoa wito kwa nchi kuweka mfumo wa kuzuia na kudhibiti utapwitapwi katika huduma za msingiUtafiti huo umeweka bayana kwamba ili kukabiliana na utapiamlo kunahitajika hatua za kisekta mbalimbali katika kilimo, ulinzi wa jamii na afya, ili kupunguza uhaba wa chakula, kuboresha upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira na kuhakikisha upatikanaji wa afua muhimu za lishe kwa wote.
1-3-2024 • 2 minuten, 48 seconden
Tanzania inashikamana na ulimwengu kusongesha ajenda ya mazingira: Waziri Jafo
Mkutanowa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 leo umekunja jamvi jijini Nairobi Kenya baada ya kukutanisha wadau zaidi ya 7000, kutoka nnyanja mbalimbali kwa lengo la kukabiliana na changamoto kubwa tatu zinazoikabili dunia ambazo ni mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa bayoanuai na uchafuzi wa mazingira. Viongozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepata fursa ya kuwasilisha taarifa zao na kushiriki katika mjadiliano. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS hakuachwa nyuma amekuwa akizungumza na wadau mbalimbali wanaoshiriki mkutano huo wa UNEA6 tangu ulipoanza na leo yuko na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wa Tanzania Dkt. Selemani Jafo na kwanza amemuuliza anachokibeba kutoka kwenye mkutano huo
1-3-2024 • 4 minuten, 38 seconden
01 MACHI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 unaokunja chamvi leo, na utafiti mpya uliotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza Lancet na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO kuhusu utipwatipwa. Mkutano wa 6 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 umefunga pazia leo jijini Nairobi, Kenya baada ya siku 5 za majadiliano na shughuli mbalimbali zilizohusisha zaidi ya wajumbe 7,000 kutoka Nchi 182 Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS, Stella Vuzo amekuwa akizungumza na washiriki mbalimbali kuhusu walivyonufaika na mkutano huo na hapa ni mmoja wao kutoka jamii za wafugaji ambao duniani kote mabadiliko ya tabianchi yanawaathiri moja kwa moja.Utafiti mpya uliotolewa leo na jarida la kitabibu la Uingereza Lancet na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO unaonyesha kwamba, mwaka 2022, zaidi ya watu bilioni 1 duniani sasa wanaishi na unene wa kupindukia ama utipwa tipwa. Duniani kote, unene wa kupindukia kwa watu wazima umeongezeka zaidi ya mara mbili tangu mwaka 1990, na umepanda mara nne kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 5 hadi 19. Makala inaturejesha kwenye mkutano wa UNEA6 ambapo Viongozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepata fursa ya kuwasilisha taarifa zao na kushiriki katika mjadiliano mbalimbali kwa lengo la kuisogeza dunia mahala bora zaidi katika upande wa mazingira. Stella Vuzo Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS hakuachwa nyuma amekuwa akizungumza na wadau mbalimbali wanaoshiriki mkutano huo wa UNEA6 tangu ulipoanza na leo yuko na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wa Tanzania Dkt. Selemani Jafo na kwanza amemuuliza anachokibeba kutoka kwenye mkutano huo.”Na mashinani tunamsikia binti Muthoni Truphena, kiongozi wa kikundi cha watoto wanaharakati wa mazingira nchini Kenya ambao wanachochea mabadiliko chanya katika jamii zao wakiungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP, anapazia sauti kizazi chake katika mkutano wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 jijini Nairobi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
1-3-2024 • 12 minuten, 41 seconden
Mkutano wa UNEA 6umekuwa fursa kubwa kwangu – Mfugaji kutoka Tanzania
Mkutano wa 6 WA Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA 6 umefunga pazia leo jijini Nairobi, Kenya baada ya siku 5 za majadiliano na shughuli mbalimbali zilizohusisha zaidi ya waj umbe 7,000 kutoka Nchi 182 Wanachama wa Umoja wa Mataifa. Afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS, Stella Vuzo amekuwa akizungumza na washiriki mbalimbali kuhusu walivyonufaika na mkutano huo na hapa ni mmoja wao kutoka jamii za wafugaji ambao duniani kote mabadiliko ya tabianchi yanawaathiri moja kwa moja.
1-3-2024 • 2 minuten, 14 seconden
Vijana tukipewa nafasi tuna mchango wa kulinda mazingira: UNEA6
Wakati jijini Nairobi Kenya mkutanowa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 ukielekea ukingoni leo ikiwa ni siku yake ya 4, vijana wanaoshiriki mkutano huo wamepaza sauti zai na kusistiza kuwa wakipewa nafasi basi wana mchango mkubwa katika vita dhidi ya uharibifu wa mazingira na kusongesha mbele ajenda ya maendeleo endelevu SDGs. Leo mkutanoni huko Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS amezungumza na vijana wawili wanaoshiriki mkutano huo ambao ni wanaharakati wa mazingira wanaotumia sayansi na sanaa kuleta mabadiliko katika jamii na pia ndio waliobuni sanaa ya jukwaa la mbao ambalo limewekwa kwenye lango la UNEA6 likipewa jina “Get your Seat at the Table”
29-2-2024 • 3 minuten, 49 seconden
Guterres: Umoja wa Mataifa hauondoki Sudan
Ikiwa leo ndio siku ya mwisho ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kipindi cha mpito nchini Sudan (UNITAMS), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema pamoja na kwamba UNITAMS inaondoka Sudan lakini Umoja wa Mataifa hauondoki nchini humo na unaendelea kujitolea kwa dhati kutoa usaidizi wa kibinadamu wa kuokoa maisha na kusaidia watu wa Sudan katika matarajio yao ya mustakabali wenye amani na usalama. Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wake usiku wa jana Februari 28 saa za New York, Marekani, Katibu Mkuu Guterres ameanza kwa kurudia shukrani zake za dhati kwa wafanyakazi wote wa kimataifa na kitaifa wa UNITAMS kwa kujitolea kwao na huduma kwa watu wa Sudan katika muda wote wa majukumu ya Ujumbe huo.Stéphane Dujarric ambaye ni Msemaji wa Katibu Mkuu anaeleza kwamba timu ndogo itasalia mjini Port Sudan ili kusimamia mchakato mzima wa makabidhiano kuanzia tarehe 1 Machi na kwamba Katibu Mkuu anategemea ushirikiano kamili wa mamlaka ya Sudan ili kuhakikisha mchakato huu unakamilika kwa urahisi na haraka iwezekanavyo.Mzozo unaoendelea kupamba moto nchini Sudan unazidi kudidimiza utawala wa sheria na ulinzi wa raia na kuhatarisha nchi nzima na eneo zima. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatoa wito kwa pande zinazozozana kuweka chini silaha zao na kujitolea kwa mazungumzo mapana ya amani yatakayosababisha kuanzishwa tena kwa mpito wa kidemokrasia unaoongozwa na raia.Wazo la kutaka UNITAMS ifungwe lilitoka kwa mamlaka za Sudan na baadaye mwishoni mwa mwaka jana, Baraza la Usalama liliridhia ombi hilo na kupitisha azimio.Mjumbe Binafsi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Sudan, Ramtane Lamamra, ameanza kazi yake ya kuunga mkono juhudi za upatanishi, kwa uratibu na ushirikiano wa karibu na wadau wa Afrika na wengine wa kimataifa. Juhudi hizi za upatanishi zitakamilisha kazi muhimu inayoendelea ya Timu ya Nchi ya Umoja wa Mataifa mashinani, ambayo ni pamoja na kutoa usaidizi wa kibinadamu wa kuokoa maisha. Katibu Mkuu anatoa wito kwa mamlaka za Sudan kuendeleza ushirikiano wao, ikiwa ni pamoja na kuwezesha utoaji wa visa ya kuingia kwa wakati na kutowawekea vikwazo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau nchini humo kutoa msaada unaohitajika.
29-2-2024 • 1 minuut, 57 seconden
29 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya mwisho ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kipindi cha mpito nchini Sudan (UNITAMS), na afya kwa wakimbizi wa DRC jimboni Kivu Kaskazini. Makala na mashinani tunaangazia mkutano huo wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 leo ikiwa ni siku yake ya 4.Ikiwa leo ndio siku ya mwisho ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia kipindi cha mpito nchini Sudan (UNITAMS), Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema pamoja na kwamba UNITAMS inaondoka Sudan lakini Umoja wa Mataifa hauondoki nchini humo na unaendelea kujitolea kwa dhati kutoa usaidizi wa kibinadamu wa kuokoa maisha na kusaidia watu wa Sudan katika matarajio yao ya mustakabali wenye amani na usalama.Nchini Jamhuri ya kidemokrasia kongo DRC Jimboni kivu kaskazini zaidi ya wakimbizi milioni 2.5 wanaishi katika kambi za wakimbizi ambazo zina hali mbaya ambayo ni tishio kwa afya zao. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO linatoa usaidizi kwa wakimbizi hao. Makala tunakupeleka jijini Nairobi, Kenya kunakoendelea mkutano huo wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 leo ikiwa ni siku yake ya 4. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini Nairobi UNIS amezungumza na vijana wawili wanaoshiriki mkutano huo ambao ni wanaharakati wa mazingira wanaotumia sayansi na sanaa kuleta mabadiliko katika jamii na pia ndio waliobuni sanaa ya jukwaa la mbao ambalo limewekwa kwenye lango la UNEA6 likipewa jina “Get your Seat at the Table.”Na mashinani tunasalia nchini Kenya katika mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEA6 kusikia mchango wa vijana katika kusongesha Malengo ya maendeleo endelevu.Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!
29-2-2024 • 11 minuten, 10 seconden
Wakimbizi wanaokimbia machafuko nchini DRC wanapokea huduma za matibabu - WHO
Nchini Jamhuri ya kidemokrasia kongo DRC Jimboni kivu kaskazini zaidi ya wakimbizi milioni 2.5 wanaishi katika kambi za wakimbizi ambazo zina hali mbaya ambayo ni tishio kwa afya zao. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO linatoa usaidizi kwa wakimbizi hao.Kambi ya wakimbizi ya Bulengo iliyoko jimboni kivu kaskazini, Video ya WHO inaonesha maelfu ya mahema meupe chini udongo mweusi wa mfinyazi, mamia ya watu wanaenda huku na kule ndani ya kambi hiyo.WHO inahofia mlundikano huu wa wakimbizi kuleta mlipuko wa magonjwa kama Malaria, magonjwa ya kupumua, ya kuhara na mengine ya kuambukiza. WHO ikishirikiana na wadau wengine wameanzisha vituo vya afya na wagonjwa wanafika kupata huduma, mmoja wao ni Desange Ndamwenge na mwanae. “Nimemleta mtoto wangu hapa asubuhi kwa ajili ya matibabu na ili tupate dawa. Mtoto ana mwaka mmoja na nimgonjwa sana ndio maana nimemleta hapa. Na mimi pia ni mgonjwa. Tumepata dawa wameshatupatia dawa za maji.”Aubedi Dunia Sebirayi ni nesi mkuu katika kambi ya Bulengo na anasema, “Hapa tunatoa huduma ya afya ya msingi, wakimbizi hawa wanapokuja na ninwagonjwa hawana hela ya kwenda hospitali kupata matibabu. Tunatoa huduma bure, kwa siku tunaona wagonjwa kati ya 80 mpaka 120 na kati yao unakuta wagonjwa wawili au watatu tunawapeleka katika hospitali.”Kwa mujibu wa Meneja wa Matukio wa WHO nchini DRC Dkt. Guy Kalambayi wakimbizi hao wa ndani wanakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya lakini kwa kuwapatia dawa, kutoa huduma za kujifungua, kutoa chanjo, na kutibu kipindupindu wanazuia vifo vingi sana na kuokoa maisha.Takwimu za WHO zinaonesha kwa wastani tangu mwezi Februari 2023 kwa mwezi wanawake 100 wanajifungua na hakuna kifo cha mjamzito hata mmoja tangu wameanza kutoa huduma. Kavira Mwaliweka ni mkunga katika kituo cha afya ya Bulengo.“Kama tusingekuwa na wodi hii ya kujifungulia hapa Bulengo tungekuwa na vifo vingi sana vya wajawazito kwasababu kambi hii iko mbali sana na kituo cha afya. Tunajisika kuwa na bahati sana kwa kutokuwa na kifo hata kimoja cha mjamzito.”Elise ni mmoja ya wajawazito waliojifungua salama na sasa anarejea nyumbani kambini na mwanaye kwa furaha.
29-2-2024 • 2 minuten, 23 seconden
UNICEF Rwanda: Je wajua kwamba watoto Rwanda wanaanza kupokea chanjo zao za kawaida karibu na nyumbani?
Katika makala tunaangazia chanjo kwa watoto nchini Rwanda ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaifadhili Rwanda Biomedical Centre (RBC) ambalo ni shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya. Anold Kayanda anasimulia.
28-2-2024 • 3 minuten, 33 seconden
UNMISS: Uongozi wa jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini waomba usaidizi zaidi wa ulinzi
Huku mzozo wa Sudan ukiendelea, wakimbizi na wanaorejea wanamiminika katika mipaka ya nchi jirani ya Sudan Kusini, wengi wamekuwa wakitafuta hifadhi katika jimbo la Upper Nile nchini humo na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umefanya mazungumzo na uongozi wa jimbo hilo kuona namna ya kuwasaidia. Kama ulivyoeleza kutokana na hali hiyo ya ongezeko la wakimbizi katika jimbo la Upper Nile, Anita Kiki Gbeho, Naibu Mwakilishi Maalum mpya wa Katibu Mkuu kwa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Sudan Kusini UNMISS, na ambaye pia ni Mratibu Mkazi wa Misaada ya Kibinadamu nchini humo amefanya ziara yake ya kwanza huko Malakal kujionea hali iliyo. Bi. Anita alijionea wakimbizi wakiandikishwa, aliketi chini na kusikiliza baadhi ya wakimbizi na kuwapongeza wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa kwa kazi kubwa wanayofanya na kisha kuwa na kikao na viongozi wa jimbo la Upper Nile“Itakuwa vyema kusikia kutoka kwako, Kaimu Gavana, na baraza lako jinsi unavyoona mustakabali ulivyo na tena jinsi gani tunaweza kuwaunga mkono kwa sababu hatimaye, tunataka kuona watu wa Sudan Kusini wanaoamua kurejea wanapata usaidizi, na tunachojaribu kufanya ni kukuunga mkono katika safari ya kusonga mbele”.Jeremiah Deng ambaye ni Kaimu Gavana wa jimbo la Upper Nile alimueleza kiongozi huyo wa UNMISS kuwa kazi ya kusimamia watu wanaorejea makwao na wakimbizi katika maeneo yenye watu wengi kama hapo ni kubwa kupita kiasi na imekuwa si rahisi kwa mamlaka za serikali.“Tuna mpaka mrefu ambao uko wazi sana kwamba watu wanaweza kuvuka kutoka upande wowote na kufurika kwa watu kutoka Sudan kuja Sudan Kusini. Watu wengine wanatumia barabara ya mpakani na nyinginezo tofauti, vivukio haramu. Vikosi vyetu vya usalama havina uwezo wa kufunika safu nzima ya mpaka”.UNMISS inatoa usaidizi wa kufanya doria za mara kwa mara ili kufuatilia kituo cha usalama huku mashirika ya kibinadamu yakifanya kazi ya ziada kutoa misaada inayohitajika.
28-2-2024 • 2 minuten, 25 seconden
28 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa chakula nchini Sudan, na ulinzi wa amani katika jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini amabapo idadi ya wakimbizi imeongezeka. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na mashinani nchini Kenya, kulikoni? Msaada wa chakula cha dharura uliotolewa na Ukraine kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ajili ya operesheni zake nchini Sudan, leo umewasili katika bandari ya Port Sudan na kuapakiwa Kwenye malori tayari kwa kuwasambazia mamilioni ya watu wenye uhitaji wa haraka.Huku mzozo wa Sudan ukiendelea, wakimbizi na wanaorejea wanamiminika katika mipaka ya nchi jirani ya Sudan Kusini, wengi wamekuwa wakitafuta hifadhi katika jimbo la Upper Nile nchini humo na wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umefanya mazungumzo na uongozi wa jimbo hilo kuona namna ya kuwasaidia. Makala tunaangazia chanjo kwa watoto nchini Rwanda ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaifadhili Rwanda Biomedical Centre (RBC) ambalo ni shirika kuu la kitaifa la utekelezaji wa afya lenye jukumu la kufanya utafiti wa kisayansi, kutoa huduma za uchunguzi, na kutekeleza afua za kiafya ili kulinda taifa la Rwanda dhidi ya magonjwa na matishio mengine ya kiafya.Na mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ujumbe wa mfugaji kuhusu uwekezaji katika sekta ya uzalishaji wa mifugo unaowezeshwa na Benki ya Dunia.Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!
28-2-2024 • 11 minuten, 18 seconden
WFP: Msaada wa chakula wa dharura kutoka Ukraine wawasili Sudan
Msaada wa chakula cha dharura uliotolewa na Ukraine kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP kwa ajili ya operesheni zake nchini Sudan, leo umewasili katika bandari ya Port Sudan na kuapakiwa Kwenye malori tayari kwa kuwasambazia watu wenye uhitaji wa haraka.Ama kwa hakika wahenga hawakukosea kusema kutoa ni moyo , kwani kwa mujibu wa WFP Ukraine ambayo yenyewe iko katikati ya vita bado imeona umuhimu wa kuwasaidia wenye uhitaji zaidi kwa kuipa WFP ngano ambayo shirika hilo linasema itatosheleza kutoa mgao wa chakula wa mwezi mmoja kwa waathirika wa vita ndani ya Sudan.Kuwasili kwa shehena hiyo ambayo ni sehemu ya mradi wa kibinadamu wa nafaka uliozinduliwa na Rais Zelensky wa Ukraine kumefanikishwa na serikali ya Ujerumani iliyolipia gharama zote ambazo ni Euro milioni 15 sawa na takriban dola milioni 16.2.Vita ikishika kasi Sudan WFP inasema mahitaji ya kibinadamu na hasa chkula yanaongezeka kwa kasi pia. Kwa mujibu wa Eddie Rowe mkurugenzi wa WFP nchini Sudan "Hali ya kibinadamu nchini Sudan ni janga lakini tunahitaji kuchukua hatua sasa ili kuizuia kuendelea kuwa mbaya zaidi. WFP inafanya kazi kwa kasi kuweza kufikisha msaada wa chakula mikononi mwa familia zinazohitaji msaada huo haraka iwezekanavyo.”WFP inasema msaada wa ngano hiyo ambao ni tani 7,600 utagawanywa kwa familia ambazo nyingi zimefurushwa makwao kutokana na mapigano yanayoendelea na zinahaha kila uchao kuweka mlo mezani.Rowe amesema msaada huu umewasili wakati muafaka kwani mapigano yakiendelea mgogoro wa njaa nchini Sudan unajongea hasa kabla ya msimu wa muambo mwezi Mei, wakati chakula kinakuwa haba, na njaa inaongezeka.Amemalizia kwa kusema kuwa "Msaada huu utaiwezesha WFP kusaidia watu ambao maisha yao yamepinduliwa kabisa na vita. Tunaishukuru sana Ukraine na Ujerumani kwa kuwasaidia watu wa Sudan katika wakati ambao uhitaji ni mkubwa.”
28-2-2024 • 2 minuten, 14 seconden
Umoja wa Mataifa sio tatizo – Rais wa Baraza Kuu
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis Pamoja na mambo mengine amesema Umoja wa Mataifa "sio tatizo" bali tatizo linatokana na kwamba baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanahisi wanaweza kukiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa watakavyo na kukiuka sheria za kimataifa bila kuadhibiwa. Anold Kayanda anaeleza zaidi.
27-2-2024 • 4 minuten, 41 seconden
WHO/UNHCR: Asilimia 75 ya vifo vyote duniani vinatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza
Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO na la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR leo yameonya kwamba athari zinazoletwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile saratani, magonjywa na mfumo wa hewa na kisukari kwa maisha ya watu duniani ni kubwa huku yakiwa ni chanzo cha asilimia 75 ya vifo vyote. Katika tarifa yao ya pamoja iliyotolewa mjini Geneva Uswis kwa mashirika hayo yamesema Watu walioathiriwa na dharura za kibinadamu wako katika hatari zaidi ya kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza NCDs huku ikikadiriwa kuwa magonjwa ya kiharusi na shinikizo la damu yana uwezekano wa kuongezeka mara tatu zaidi kunapokuwa na majanga ya kibinadamu.Hata hivyo, yameongeza kuwa huduma na matibabu ya NCDs mara nyingi havijumuishwi kama sehemu ya kawaida ya maandalizi ya hatua za dharura ya kibinadamu, ambayo huzingatia mahitaji ya haraka zaidi.Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema. "Watu wanaoishi na NCDs katika majanga ya kibinadamu wana uwezekano mkubwa wa kuona hali zao zikiwa mbaya zaidi kutokana na kiwewe, msongo wa mawazo, au kutoweza kupata dawa au huduma. Mahitaji ni makubwa, lakini rasilimali hazitoshi. Lazima tutafute njia za kuunganisha vyema huduma za NCD katika kukabiliana na dharura, ili kulinda maisha zaidi kutokana na majanga haya yanayoweza kuepukika na kuboresha usalama wa afya."Wakimbizi wametajwa kwamba mara nyingi wanakabiliwa na ukosefu wa huduma za afya, kutokana na hali mbaya ya maisha, matatizo ya kifedha, na hali mbaya ya kisheria.Filippo Grandi,ambaye ni Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi amesema "Kadiri watu wanaofurushwa makwao wanavyoongezeka, lazima tufanye kazi ili kuhakikisha haki ya afya ya wakimbizi, watu wengine waliolazimika kukimbia na jamii zinazowapokea. Ni muhimu kwamba sera, na rasilimali ziwepo ili kusaidia kujumuishwa kwa wakimbizi katika mifumo ya afya ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na kupata huduma za magonjwa yasiyoambukiza. Lazima tuwe wabunifu, na kufanya kazi na serikali na washirika kutatua changamoto kama hizi."NCDs zilichangia asilimia kubwa ya vifo vyote katika nchi zinazotoa wakimbizi wengi wanaosaidiwa na UNHCRambapoasilimia 75 Syria, asilimia 92 nchini Ukraine, asilimia 50 nchini Afghanistan na asilimia 28 Sudan Kusini.
27-2-2024 • 2 minuten, 40 seconden
27 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hatari ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza na wakimbizi wa Sudan wanaovuka mpaka kuelekea Sudan Kusini. Makala tunakuletea majibu ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis alipohojiwa na UNTV kandoni mwa Kikao cha 55 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea jijini Geneva Uswisi na mashinani tunakupeleka nchini Afghanistan, kulikoni? Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO na la kuhudumia wakimbizi duniani UNHCR leo yameonya kwamba athari zinazoletwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile saratani, magonjywa na mfumo wa hewa na kisukari kwa maisha ya watu duniani ni kubwa huku yakiwa ni chanzo cha asilimia 75 ya vifo vyote.Wananchi waliokimbia makazi yao kutokana na vita inayoendelea nchini Sudan wanasaidiwa nchini Sudan Kusini na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM ambalo limeeleza zaidi ya watu nusu milioni wamevuka mpaka na kuingia eneo la Renk na sasa wanawapatia usaidizi wa usafiri ili kufika kwenye maeneo watakayopata usaidizi. Katika makala Anold Kayanda anaangazia majibu ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Dennis Francis alipohojiwa na UNTV kandoni mwa Kikao cha 55 cha Baraza la Haki za Binadamu kinachoendelea jijini Geneva Uswisi. Pamoja na mambo mengine Balozi Francis amesema Umoja wa Mataifa "sio tatizo" bali tatizo linatokana na kwamba baadhi ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanahisi wanaweza kukiuka mkataba wa Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa watakavyo.Na mashinani tutaelekea nchini Afghanistan kusikia jinsi UNICEF ilivyorejesha huduma za afya, matibabu na mafunzo kwa wataalam ili kuwafikia watoto na wanawake popote walipo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
27-2-2024 • 11 minuten, 13 seconden
Wakimbizi wanaofika mpakani mwa Sudan na Sudan Kusini wanasaidiwa na IOM kusafiri
Wananchi waliokimbia makazi yao kutokana na vita inayoendelea nchini Sudan wanasaidiwa nchini Sudan Kusini na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM ambalo limeeleza zaidi ya watu nusu milioni wamevuka mpaka na kuingia eneo la Renk na sasa wanawapatia usaidizi wa usafiri ili kufika kwenye maeneo watakayopata usaidizi. Maelfu ya watu wanavuka mpaka katika eneo la Renk nchini Sudan Kusini ambako IOM imesema lina hali ngumu kwani hakuna maji, chakula, usafiri wala usalama wa aina yeyote na ni eneo lililo mbali. Maelfu ya watu wameovuka mpaka wanaonekana kuwa ni dhaifu. Wengi wao wana kiwewe. Msemaji wa IOM Afrika Mashariki Yvonne Ndege anasema wamezungumza na wanawake, watoto na wazee ambao wamekimbia ghasia na wametumia wiki na miezi, kujaribu kufikia mpaka huo.“Hali waliyoielezea, waliyo yashuhudia ni ya kutisha kabisa. Wengine wanasema walikimbia vurugu. Wengine wanasema walikimbia risasi. Wengine wanasema walifanyiwa ukatili wa kijinsia wakiwa safarini. Wengine wanasema walitumia siku nyingi sana msituni wakijaribu kufikia mpaka huu. Tulizungumza na familia moja, mama akiwa na binti zake wawili na mama yake mwenyewe, ambaye alisafiri kutoka mji mkuu wa Sudan, Khartoum, mpaka kufika mpaka huu na kuvuka salama. Aliumia sana, alifadhaika sana. Lakini anamshukuru Mungu kwamba alikuwa ametoroka na uhai wake.”Msemaji huyo wa IOM imeeleza wameandaa zaidi ya safari za ndege 1,200 vile vile kuna usafiri wa maji ambapo wakimbizi wengine watasafirishwa kwa siku tatu kutoka Renk kupitia mto Nile mpaka kufika Malakal mji mkuu wa jimbo la Upper Nile. “Usaidizi huu ni muhimu kabisa kwa sababu kile IOM na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa hawataki, ni kambi za wakimbizi kuibuka katika eneo hili kwa sababu liko mbali sana. Hakuna miundombinu. Hakuna hospitali, hakuna vifaa vya matibabu. Hakuna rasilimali za aina yoyote kwa watu.”Pamoja na usaidizi huo unaotolewa na IOM pamoja na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa bado Kuna wasiwasi mkubwa juu ya hatari ya kuibuka kwa magonjwa, njaa na vurugu zaidi.IOM imekuwa ikifanya ukaguzi wa kimatibabu na kutoa chanjo kabla ya kuwasafirishwa.
27-2-2024 • 2 minuten, 41 seconden
Namna ngamia walivyobadili maisha ya wanajamii wa Samburu Kenya
Kwa wafugaji hususan walio katika maeneo ya ukame kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiathirika na athari za mabadiliko ya tabianchi kutokana na mifugo yao kutozalisha kiwango kinachohitajika cha maziwa na nyama cha kuwatosheleza wao wenyewe kula na kingine kuuza na kujipatia fedha. Ni kutokana na changamoto hiyo ndio maana mradi wa Pear Innovation ukaanzishwa huko kaunti ya Samburu nchini Kenya ambao ulilenga kutoa ngamia kwa wanawake ili wawaze kutumia maziwa ya ngamia hao kama lishe kwa familia zao na kisha kuuza mazao mengine na kujipatia fedha. Tuungane na Leah Mushi katika Makala hii.
26-2-2024 • 5 minuten, 9 seconden
UNEA6 ni mwongozo wa kushirikisha pande zote katika kulinda mazingira: Irene Mwoga
Mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 leo umefungua pazia katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Nairobi, nchini Kenya. Mkutano huo utakaodumu kwa siku tano unahudhuriwa na washiriki zaidi ya 6000 ikiwa ni pamoja na viongozi wa Mazingira duniani, asasi za kiraia, wataalamu wa Mazingira, maofisa waserikali za mitaa, wakulima, vyama vinavyowakilisha wafanyakazi, jamii zilizoachwa nyuma pamoja na maofisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.Irene Mwoga mtaalamu wa takwimu wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP kwa bara la Afrika ni Mratibu wa Mkutano huo amezungumza na Stella Vuzo wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Naironi Kenya UNIS na kuhusu mkutano huo dhamira ya mkutano huu unaofanyika kila baada ya miaka miwili, katika mwezi wa Februari akianza kwa kueleza UNEA6 ni nini..
26-2-2024 • 2 minuten, 23 seconden
26 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 jijini Nairobi, na mradi wa kusaidia watoto na vijana ambao walikuwa na changamoto ya masikio na kuongea nchini Rwanda. Makala tunasalia nchin Kenya na mashinani ukanda wa Gaza, kuikoni?Mkutano wa sita wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA6 leo umefungua pazia katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo jijini Nairobi, nchini Kenya. Mkutano huo utakaodumu kwa siku tano unahudhuriwa na washiriki zaidi ya 6000 ikiwa ni pamoja na viongozi wa Mazingira duniani, asasi za kiraia, wataalamu wa Mazingira, maofisa waserikali za mitaa, wakulima, vyama vinavyowakilisha wafanyakazi, jamii zilizoachwa nyuma pamoja na maofisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa.Kupitia mradi wa "Winsiga Ndumva", maneno ya lugha ya Kinyarwanda yanayomaanisha "Usiniache nyuma, ninaweza kusikia”, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wadau wake ikiwemo Wizara ya Afya nchini Rwanda limebadilisha maisha ya watoto wengi na vijana ambao walikuwa na changamoto ya masikio na kuongea kwakuwapatia vifaa maalumu vya kupachika masikioni ili kusaidia masikio kufanya kazi yake ipasavyo. Makala inatupeleka kaunti ya Samburu nchini kenya kuona namna ngamia wanavyoboresha maisha ya wanawake na jamii kwa ujumla.Na mashinani inatupeleka katika ukanda wa Gaza ambapo ongezeko kubwa la utapiamlo miongoni mwa watoto na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha ni tishio kubwa kwa afya zao. Shirika la Mpango wa chakula Duniani, WFP linahaha kuwasambazia lishe yenye virutubisho.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
26-2-2024 • 9 minuten, 57 seconden
UNICEF Rwanda: Programu ya “Winsiga Ndumva” waleta zawadi ya sauti kwa watoto viziwi
Kupitia mradi wa "Winsiga Ndumva", maneno ya lugha ya Kinyarwanda yanayomaanisha "Usiniache nyuma, ninaweza kusikia”, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wadau wake ikiwemo Wizara ya Afya nchini Rwanda limebadilisha maisha ya watoto wengi na vijana ambao walikuwa na changamoto ya masikio na kuongea kwakuwapatia vifaa maalumu vya kupachika masikioni ili kusaidia masikio kufanya kazi yake ipasavyo. Huyo ni Vuguzima Francine, ambaye awali hakujua kuwa mtoto wake kwa kiasi kikubwa ni kiziwi. Mama huyu anasema, “nilikuwa ninamuadhibu kila siku kwa sababu nilikuwa nikimuita haitiki. Nikimwambia aende mahali haiendi. Nilifikiri ni kiburi. Kumbe baadaye ikagundulika hasikii.”UNICEF, kwa zaidi ya watoto na vijana wadogo zaidi ya 500 katika maeneo kadha ya nchini Rwanda imefanya jambo ambalo wazazi na watoto wenyewe wanaona kama miujiza. Manirakora Emmnuel mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika kituo cha viziwi cha Butare akiwa na sura ya furaha na tabasamu pana anasimulia maisha yalivyokuwa magumu kabla hajapata machine ya kusaidia usikivu.“Nilipokuwa ninacheza mpira na watoto wenzangu, mtu akiniambia nielekeze mpira kwake, nilikuwa sisikii. Kwa hiyo kwa kutojua nilikuwa napiga mpira popote.” Pongezi pia ziende kwa Kitengo cha Manunuzi au Ugavi cha UNICEF kilitekeleza jukumu muhimu kuhakikisha wanavipata visaidizi hivi vya masikio kwa dola 118 kila kimoja ingawa bei yake kwa kawaida inafikia dola 2000 za kimarekani.
26-2-2024 • 1 minuut, 40 seconden
Wanawake ili tufanikiwe lazima tujitume: Dkt. Elizabeth Kimani
Mkutano wa wanawake katika nyanja ya diplomasia umefanyika wiki hii katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya. Viongozi wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Nairobi na Geneva Uswisi wamewasilisha mada mbele ya umati wa watu waliohudhuria mkutano huo wakiwemo Mabalozi wastaafu na wanaotumikia nchi zao hivi sasa nchini Kenya kuhusu nafasi ya Mwanamke katika ddiplomasia na katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Dkt. Elizabeth Kimani Murage anayefanyakazi na kituo cha utafiti na idadi ya watu Afrika (African population and research center) kama mtafiri mkuu ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo na amezungumza na Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS katika makala hii na anaanza kwa kumueleza kwanini aliona ni muhimu kuhudhuria mkutano huo.
23-2-2024 • 2 minuten, 59 seconden
Ahunna Eziakonwa: Nimekuja kuona UNDP inavyoweza kuunga mkono maendeleo ya Burundi
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP Kanda ya Afrika, Ahunna Eziakonwa yuko ziarani nchini Burundi ambako amekutana na makundi mbalimbali ya kijamii na hata kufika mpaka wa Burundi na DRC kuona uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo. Pia Bi. Eziakonwa amekutana na Rais Evariste Ndaishimye.“Kwanza kabisa nimemshukuru Rais na nchi kwa kunikaribisha vema katika ziara yangu hii ya kwanza nchini Burundi. Rais na mimi tumejadili mchango wa UNDP katika kuunga mkono maono aliyonayo kwa ajili ya nchi hii. Tunaelewa kwamba kuna maono ya nchi kuwa imechomoza kufikia mwaka 2040 na kuwa imeendelea kufikia 2060. Kama mnavyofahamu UNDP ni shirika la maendeleo na tunataka kuona kile tunachoweza kufanya kuuunga mkono maono haya. Na nimekuja hapa pia kutathimini uimara wa UNDP katika kuisaidia Burundi kwenda katika mwelekeo huu wa maendeleo.”Bi. Eziakonwa anaendelea kueleza waliyoyazungumza na Rais Ndaishimiye akisema,“Pia tumejadili kuhusu vijana. Na nimempongeza Rais kama kinara wa mkutano wa vijana wa Afrika kwa ajili ya amani na usalama ambao ulisababisha kupitisha uamuzi wa Muungano wa Afrika kuhusu mchango wa vijana katika kukuza amani na usalama. Tumezungumza kuhusu vijana kwa ujumla na jinsi ya kuwapa fursa vijana kutumia uwezo wao.”Ni Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP Kanda ya Afrika, Ahunna Eziakonwa akiwa ziarani nchini Burundi. Shukrani kwa washirika wetu Mashariki TV ya mjini Bujumbura kwa kufanikisha kutufikishia sauti hii.
23-2-2024 • 1 minuut, 47 seconden
23 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini DR Congo na hali ya msaada wa kibinadamu kwa wakimbizi wake. Pia tunakupeleka nchini Burundi kufuatilia kazi za makundi ya kijamii. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Ukraine tukielekea miaka mwili kamili ya vita nchini humo.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa kuchukuliwa hatua mara moja kuwalinda watoto na familia zao waliojikuta katikati ya machafuko yanayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, huku lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR likielezea wasiwasi mkubwa kuhusu mustakabali wa zaidi ya raia milioni 7 waliotawanywa na kuomba msaada zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa.Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP Kanda ya Afrika, Ahunna Eziakonwa yuko ziarani nchini Burundi ambako amekutana na makundi mbalimbali ya kijamii na hata kufika mpaka wa Burundi na DRC kuona uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo. Makala inatupeleka katika chuo kikuu cha Nairobi Kenya ulikomalizika mkutano wa wanawake katika nyanja ya diplomasia. Huko viongozi wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Nairobi na Geneva Uswisi wamewasilisha mada mbele ya umati wa watu wakiwemo Mabalozi wastaafu na wa sasa wanaowakilisha mataifa yao Kenya kuhusu nafasi ya mwanamke katika diplomasia na kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Dkt. Elizabeth Kimani Murage anayefanyakazi na kituo cha utafiti na idadi ya watu Afrika kama mtafiti mkuu, ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo.Katika mashinani tukielekea miaka mwili kamili ya vita nchini Ukraine tutamsikia mmoja wa waathirika wa vita hiyo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
23-2-2024 • 10 minuten, 53 seconden
Hali DRC si hali tena, mashirika ya UN yataka msaada zaidi na ulinzi kwa raia
Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuhudumia watoto UNICEF na la mpango wa chakula duniani WFP leo yametoa wito wa kuchukuliwa hatua mara moja kuwalinda watoto na familia zao waliojikuta katikati ya machafuko yanayoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, huku lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR likielezea wasiwasi mkubwa kuhusu mustakbali wa zaidi ya raia milioni 7 waliotawanywa na kuomba msaada zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa.Kwamujibu wa WFP na UNICEF idadi kuwa ya watu wakiwemo watoto wamejeruhiwa au kuawa karibu na makazi ya kambi za wakimbizi na yametoa wito kwa pande zote katika mzozo kuwalinda raia na kuruhusu mashirika ya misaada ya kibinadamu kufanya kazi yao.Mashirika hayo yamesema mapigano ya sasa yamesababisha janga kubwa la kibinadamu na katika wiki mbili zilizopita yamesogea kilometa 25 mwagharibi mwa mji wa Goma kuelekea Sake ambako watoto na familia zao sasa wamezingirwa na mapigano.Mwakilishi wa UNICEF nchini DRC Grant Leaity amesema "Watoto nchini DRC wanahitaji amani sasa. Tunatoa wito kwa watoto kulindwa katika vita hivi na kukomesha ukatili huu kupitia juhudi mpya za kutafuta suluhu za kidiplomasia. Tuna wasiwasi mkubwa kuhusu usalama wa watoto na familia zao walio ndani na karibu na kambi za Goma.”Nalo shirika la UNHCR limesema mapigano haya yamesababisha msongamano mkubwa wa watu kwenye kambi za wakimbizi ambazo tayari zimejaa pomoni watu waliofurushwa makwao. Watu zaidi ya 214,000 wamejiunga na watu wengine 500,000 ambao tayari walikimbia hadi maeneo ya karibu na Goma.Shirika hilo limesema linatiwa hofu kubwa kwani hadi sasa zaidi ya watu milioni 7 wametawanywa nchini DRC ukijumuisha na wengine nusu milioni ambao ni wakimbizi na wengi wanakabiliwa na changamoto za hali duni ya malazi, huduma mbovu za usafi na fursa finyu za kujipatia kipato.Ili kushughulikia changamoto hizo na nyingine nyingi za kibinadamu mwaka huu 2024 ombi la dola bilioni 2.6 lilizinduliwa wiki hii kusaidia watu milioni 8.7 wanaohitaji msaada wa kibinadamu DRC.Lakini jana pia UNHCR na washirika wake walizindua mkakati wa kikanda wa ulinzi na msaada kwa DRC unaohitaji dola milioni 668 kusaidia karibu wakimbizi milioni 1 na jamii zinazowahifadhi hasa nchini Angola, Burundi, Jamhuri ya Congo, Rwanda, Uganda, Tanzania na Zambia.
23-2-2024 • 2 minuten, 31 seconden
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno NDONGOSA
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “NDONGOSA.”
22-2-2024 • 0
22 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ambapo FAO limeutenga mwaka huu wa 2024 kuwa wa wanyama wa jamii ya ngamia kwani mchango na faida zake zinanufaisha zaidi ya mataifa 90 duniani na tunaelekea nchini Kenya kwa makala inayohusu ngamia. Pia tunaangazia DR Congo, Gaza na Ukraine kwa muhtasari ya habari. Katika kujifunza kiswahili tunakuletea uchambuzi wa neno “NDONGOSA”.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) kwa kushirikiana na wadau wake 105 hii leo wamezindua mpango wa kuwasaidia wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, DRC pamoja na jamii zilizowakaribisha. Mpango huo uliozinduliwa hii leo jijini Pretoria, Afrika Kusini utakaogharimu jumla ya dola milioni 668 kwa kipindi cha mwaka 2024-2025 unahusisha wadau kutoka Tanzania, Burundi, Uganda, Rwanda, Angola, Zambia na DRC yenyewe.Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA Philippe Lazzarini na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani Dkt. Tedros Ghebreyesus wakiunga mkono tamko la Kamati ya kudumu ya mashirika ya kimataifa (IASC) lililotolewa jana kuhimiza kusitiza mapigano Gaza, kupitia kurasa zao za mtandao wa X wameeleza hali ilivyo tete Gaza. Lazzarini akihoji ni “mara ngapi zaidi tunapaswa kukumbusha kwamba hakuna mahali salama katika Gaza?” huku Dkt. Tedros akieleza kuwa hospitali zimegeuka uwanja wa vita. Na Uvamizi kamili wa Ukraine uliofanywa na Urusi ukielekea kuingia mwaka wa tatu, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ametoa wito kwa Urusi kuruhusu Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu na mashirika mengine huru ya kimataifa kuwafikia kikamilifu wale wote ambao wamenyimwa uhuru wao katika muktadha wa vita ya kijeshi. Wakati huo huo nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeeleza kuwa asilimia 40 ya idadi ya watu wote wa Ukraine bado wanahitaji aina fulani ya usaidizi wa kibinadamu, wakati wakimbizi milioni 2.2 wanahitaji msaada katika nchi za jirani.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “NDONGOSA”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
22-2-2024 • 11 minuten, 55 seconden
Huku wanakimbia vita wanawake wa Gaza inakuwaje wakiwa katika hedhi?
Kunapozuka mizozo na machafuko wananchi wote wanaathirika kwasababu maisha yao yanaparanganyika kabisa tofauti na walivyokuwa wamezoea. Watoto waliokuwa wakienda shule sasa hawaendi, si wafanyabiashara, wakulima wala viongozi wa dini wanaotekeleza majukumu yao ya kila siku na suala moja lililo kweli kwa kila mtu ni kuwa wanatafuta kila namna ya kuokoa maisha yao na wengi njia hiyo huwa ni kukusanya virango vyao kidogo wanavyoweza kubeba na kukimbia kuokoa nafsi zao. Kwa wananchi wa Gaza hususan wanawake wa Gaza, mwezi Oktoba mwaka 2023 mpaka leo wamekuwa wakikimbia mara kusini, mara kaskazini na sasa wapo Rafah karibu na mpaka wa nchi yao na Misri huku wengine wakiwa wamekwama maeneo mbalimbali ya ukanda huo kutokana na mapigano yanayoendelea baina ya wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na jeshi la Israel IDF. Lakini ki baiolojia kila mwezi wanawake na wasichana waliovunja ungo huona siku zao au huingia katika hedhi , je wanawezaje kujihifadhi wakati huo huo wakiwa leo hapa kesho pale kuokoa nafsi zao? Tuungane na Leah Mushi katika Makala hii.
21-2-2024 • 4 minuten, 35 seconden
21 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mizozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na mabomu ya kutegwa ardhini nchini Ukraine. Makala tukupeleka katika ukanda wa Gaza na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Bintou Keita, ameliambia Baraza la Usalama kwamba ana wasiwasi mkubwa kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa unaofanywa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa M23, ambapo vuguvugu hilo linalenga watendaji wa mashirika ya kiraia, hasa watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari.Umoja wa Mataifa umesema Ukraine sasa ni moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na mabomu ya kutegwa ardhini duniani huku ikadiriwa kwamba karibu thuluthi moja ya nchi hiyo imeghubikwa na vita eneo ambalo ukubwa wake ni mara nne na nusu ya nchi ya Uswisi. Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kazi na serikali ya Ukraine kwa miaka 30 na umekuwa ukiongoza mpango wa utekelezaji wa uteguaji wa mabomu ya kutegwa ardhini tangu 2016. Makala tunaelekea Gaza ambapo tangu Oktoba 7 mwaka jana kulipozuka machafuko huko Ukanda wa Gaza, wanawake wanaume na watoto wamekuwa wakikimbia kutoka eneo moja Kwenda jingina mpaka sasa wengi wao wapo Rafah karibu kabisa na mpaka wan chi ya Misri lakini umeshajiuliza kwa miezi mitano wanawake wa Gaza wanafanyaje wanapoingia katika kipindi cha hedhi kila mwezi?Mashinani ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya lugha ya mama tutaelekea mjini Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania kumsikia kijana anayetumia Kiswahili kama lugha mama.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
21-2-2024 • 12 minuten, 55 seconden
Paul Heslop: Uondoaji wa mabomu ya kutengwa ardhini Ukraine ni mtihani na hatari kubwa
Umoja wa Mataifa umesema Ukraine sasa ni moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na mabomu ya kutegwa ardhini duniani huku ikadiriwa kwamba karibu thuluthi moja ya nchi hiyo imeghubikwa na vita eneo ambalo ukubwa wake ni mara nne na nusu ya nchi ya Uswisi. Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kazi na serikali ya Ukraine kwa miaka 30 na umekuwa ukiongoza mpango wa utekelezaji wa uteguaji wa mabomu ya kutegwa ardhini tangu 2016. Paul Heslop Mshauri Mkuu wa Kiufundi wa utekelezaji wa program ya hatua ya uteguaji mabomu ya kutegwa ardhini ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Ukraine akisema amekuwa akifanya kazi ya uteguzi wa mabomu ya kutegwa ardhini kwa miaka thelathini katika maeneo hatari yenye vita, kuanzia Msumbiji hadi Afghanistan. Lakini aliyoyashuhudia ilikuwa maandalizi tu mtihani kamili ambao sasa uko Ukraine“Ni mazingira magumu sana iwe ya kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiufundi, kwanza kabisa kwa maana ya kieneo, ni nchi kubwa. Kuna mstari wa mbele wa vita ambao sasa ni zaidi ya kilomita elfu moja, kuna uwezekano wa kazi kubwa ya kufanya. theluthi moja ya nchi inashukiwa kuathirika na mabomu ya ardhini. Hiyo ni ukubwa wa kama nchi mbili za Ufaransa.”Mathalani Paul anasema,“Endapo makombora 30,000 yanarushwa kwa siku, hayo ni mabomu 3,000 yasiyolipuka kwa siku. Na, wakati mzozo unafikia siku elfu moja basi, hayo ni mabomu milioni 3 na vilipuzi vingine ambayo hviajalipuka.”Licha a hali kuonekana ni ya kutisha lakini haimkatishi tamaa Paul wala kumfanya ajutie kufanyakazi ya ya Umoja wa Mataifa ya uteguzi mabomu “Nimebaini kwamba kufanya kazi kya kutegua mabomu kuwa ni kazi bora zaidi ambayo ningeweza kuwa nayo. Nimeona ushujaa ambao siwezi hata kuamini na nimeshuhudia matukio ambayo yananitia hofu kubwa.”Kwa mujibu wa UNDP ambayo ni mratibu wa hatua za kutegua mabomu ya ardhini Ukraine hadi kufikia Juni mwaka huu mabomu na vilipuzi 540,000 ambavyo havikulipuka vimeteguliwa, lakini kuifanya Ukraine kuwa salama kabisa ni kibarua kigumu na cha gharama kubwa, huku Benk ya dunia ikikadiria kuwa kutegua vilipuzi na mabomu yote nchini humo kutagharimu dola zaidi ya bilioni 37.
21-2-2024 • 2 minuten, 33 seconden
Bintou Keita: Nina wasiwasi mkubwa na ukikukwaji wa haki za binadamu katika maeneo yanayokaliwa na M23
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Bintou Keita, ameliambia Baraza la Usalama kwamba ana wasiwasi mkubwa kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa unaofanywa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa M23, ambapo vuguvugu hilo linalenga watendaji wa mashirika ya kiraia, hasa watetezi wa haki za binadamu na waandishi wa habari. Akihutubia Baraza la Usalama lililokaa jana kuanzia saa tisa alasiri saa za New York Marekani ili kuijadili hali ya DRC, kwa njia ya video akiwa nchini DRC, Bintou Keita ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, ameeleza kinagaubaga hali ya usalama inavyozidi kudorora mashariki mwa nchi hiyo ya pili kwa ukubwa wa eneo barani Afrika.“Idadi ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na M23 inaendelea kuongezeka, huku takriban raia 150 wakiuawa tangu kuanza tena kwa mapigano Novemba 2023, wakiwemo watu 77 Januari 2024.”Aidha Bi. Keita akasisitiza kuhusu changamoto wanazokutana nazo MONUSCO kutokana na kuendelea kukabiliwa na wimbi la taarifa potofu na za uongo kuhusu uhusika wa MONUSCO kwenye mapigano yanayoendelea hivi sasa. “Kampeni za mtandaoni zinazoilenga MONUSCO zimekuwa zikifanywa na vyanzo ambavyo hasa viko nje ya DRC. Hii imesababisha vitendo vya uhasama dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa na vikwazo vya kutembea vinavyowekwa na makundi yenye silaha na askari wa serikali.”Kwa mujibu wa Mwakilishi huyo maalumu wa Katibu Mkuu nchini, zaidi ya watu 400,000 waliokimbia makazi yao karibu na mji wa Goma sasa wametafuta hifadhi katika mji huo, wakiwemo watu 65,000 katika wiki mbili zilizopita, na hivyo kusababisha ongezeko kubwa la wagonjwa wa kipindupindu kutokana na ukosefu wa maji safi ya kunywa na usafi wa jumla wa mazingira.
21-2-2024 • 2 minuten, 10 seconden
20 FEBRUARI 2024
Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa hii leo ikiwa ni Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kijamii Duniani. Jarida linaletwa kwako na LEAH MUSHI na kubwa hii leo ni mada kwa kina kutoka nchini Kenya ambako serikali na wadau wa wanyamapori wamechukua hatua kulinda moja ya Wanyama walio hatarini kutoweka , Faru. Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari na ujumbe kutoka mashinani. Karibu.
20-2-2024 • 13 minuten, 11 seconden
19 FEBRUARI 2024
Mgogoro wa Sudan ni tishio kwa ukanda mzima huku njaa ya utapiamlo vikiongezeka WFP imeonya.Maelfu ya watu wayakimbia machafuko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya CongoMakala: UNICEF na UNFPA waungana kutokomeza ndoa za utotoni nchini Nepal.Mashinani : Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Sudan Kusini Jean-Pierre Lacroix afanya ziara kutatathimini hali.
19-2-2024 • 10 minuten
Utangazaji wa sasa una walakini japo redio bado ni muhimu - Rose Haji
Ikiwa wiki hii ulimwengu umeadhimisha Siku ya redio Duniani, Mwanahabari gwiji wa siku nyingi nchini Tanzania Rose Haji anakubaliana na mtazamo wa Umoja wa Mataifa kuwa redio bado ni chombo muhimu sana katika mawasiliano ya ulimwengu lakini anaona kwamba kwa upande wa taaluma ya utangazaji wa redio kuna tatizo.
16-2-2024 • 3 minuten, 15 seconden
Guterres: Tunahitaji utaratibu wa kimataifa ambao unafanya kazi kwa kila mtu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo katika mkutano wa usalama unaofanyika mjini Munich Ujerumani ametoa wito wa kuwepo utaratibu wa kimataifa ambao unafanya kazi kwa kila mtu. Asante Evarist Guterres katika hotuba yake amesisitiza wito huo wa amani na utaratibu wa kisasa wa kimataifa akisema utaratibu wa leo wa kimataifa haufanyi kazi kwa kila mtu, "Kwa kweli, ningeenda mbali zaidi na kusema kwamba haufanyi kazi kwa mtu yeyote." Akielezea hali ya kimataifa, Katibu Mkuu amesema hivi sasa dunia inakabiliwa na changamoto lukuki, lakini jumuiya ya kimataifa imegawanyika zaidi kuliko wakati mwingine wowote katika miaka 75 iliyopita.Amesisitiza kwamba "Leo hii tunashuhudia nchi zikifanya chochote wapendacho, bila uwajibikaji." Ameonya kwamba “Kama Ripoti ya Usalama ya Munich inavyoweka bayana mafanikio ya jamii kupitia ushindani kati ya nchi yanapewa kipaumbele badala ya kuangalia faida kwa wote, kupitia ushirikiano”. Ripoti ya Usalama ya Munich huchapishwa kila mwaka kabla ya mkutano na kuchambua masuala muhimu ya sera ya usalama.Guterres ameongeza kuwa migogoro inaongezeka, inayohusishwa na ushindani na kutokujali.Hivyo amesisitiza kuwa utaratibu wa kimataifa ambalo linafanya kazi kwa kila mtu lazima lishughulikie mapungufu haya na kutoa suluhisho."Ikiwa nchi zingetimiza wajibu wao chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa, kila mtu duniani angeishi kwa amani na utu".Katibu Mkuu amegusia pia migogoro inayoendelea duniani mathalan amesema hali ya Gaza ni janga la kutisha la mkwamo katika uhusiano wa kimataifa.Hakuna kinachoweza kuhalalisha mashambulizi ya kiholela yaliyoanzishwa na Hamas tarehe 7 Oktoba, Guterres amesisitiza kwa wakuu wa nchi na serikali kutoka duniani kote mjini Munich na kuongeza kuwa “Na hakuna kinachoweza kuhalalisha adhabu ya pamoja ya watu wa Palestina katika hatua za kijeshi za Israeli.Mashambulizi ya kila upande dhidi ya mji wa Gaza yatakuwa mabaya kwa raia wa Palestina ambao tayari wako kwenye zahma kubwa, ameonya Guterres katika hotuba yake kwa washiriki wa ngazi za juu wa mkutano huo.Masuala mengine aliyozungumzia ni mkutano wa siku zijazo ambao utafanyika Septemba kmwa huu ambapo amesema “tunahitaji kuimarisha usanifu wa amani na usalama wa kimataifa ili kukabiliana na vitisho na changamoto za leo, kama vile mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi, akili bandia au akili mnemba, au kutumia mtandao kama silaha.”Na Jana Alhamisi, siku moja kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Usalama wa Munich, Guterres alitembelea sinagogi la "Ohel Jakob"ambako kuna majina ya Wayahudi zaidi ya 4,500 wa Munich ambao waliuawa wakati wa enzi ya Manazi na kusistiza kuwa chuki dhidi ya Wayahudi inapaswa kukomeshwa kote duniani.
16-2-2024 • 2 minuten, 40 seconden
16 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa usalama unaofanyika mjini Munich Ujerumani, na elimu kwa watoto katika mzozo nchini Afghanistan. Makala tunasikia ujumbe kuhusu matatizo kwa upande wa taaluma ya utangazaji wa redio. Mashinani tunasikia ujumbe wa mkulima nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo katika mkutano wa usalama unaofanyika mjini Munich Ujerumani ametoa wito wa kuwepo utaratibu wa kimataifa ambao unafanya kazi kwa kila mtu.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linafanya kila juhudi kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao ikiwemo elimu. Huko nchini Afghanistan shirika hilo limehakikisha zaidi ya wanafunzi 683,000 wanapata elimu wangali katika mazingira wanayoishi. Katika makala na ikiwa wiki hii ulimwengu umeadhimisha Siku ya redio Duniani, Mwanahabari gwiji wa siku nyingi nchini Tanzania Rose Haji anakubaliana na mtazamo wa Umoja wa Mataifa kuwa redio bado ni chombo muhimu sana katika mawasiliano ya ulimwengu lakini anaona kwamba kwa upande wa taaluma ya utangazaji wa redio kuna tatizo.Mashinani tunakuletea ujumbe wa Agnes, mwanamke mkulima kutoka Kenya ambaye alikuwa anategemea chakula cha msaada kutoka Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP lakini leo, kupitia mtaro wake wa maji inayopeleka maji kwa shamba lake, anavuna mazao yake ya kutosha familia yake na ameweza kujimudu kimaisha kwa kuuza masalio.Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!
16-2-2024 • 10 minuten, 42 seconden
Afghanistan: Watoto 683,000 wanufaika na madarasa ya elimu ya kijamii
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linafanya kila juhudi kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao ikiwemo elimu. Huko nchini Afghanistan shirika hilo limehakikisha zaidi ya wanafunzi 683,000 wanapata elimu wangali katika mazingira wanayoishi. Mtoto Khadija ni mmoja wa wanufaika wa madarasa ya elimu ya kijamii huko nchini Afghanistan. Kabla ya kuanza kwa programu hii inayofadhiliwa na UNICEF mtoto huyu na wenzake walikuwa hawaendi shule.Hapo awali, tulikuwa tunagombana na marafiki zangu sababu hatukujua kile kilicho bora. Mimi na marafiki zangu tulikuwa tunacheza sehemu yoyote ile hata kwenye uchafu, sababu hatukujua kuwa ni tatizo. Lakini baada ya kuandikishwa na kuanza kushiriki katika madarasa ya elimu ya kijamii, Khadija anasema anafurahia mambo anayojifunza shuleni na kushirikiana na wanafunzi wenzake darasani.Nina jisikia furaha na fahari. Napenda kujifunza hisabati, Dari, ujuzi wa kijamii na kuandika. Ninapokuja shuleni najifunza vitu vingi sana. Asilimia 60 ya wanufaika wa programu hii ya madarasa ya elimu ya kijamii inayotolewa kwa wanafunzi 683,000 nchini Afghanistani ni watoto wa kike.
16-2-2024 • 1 minuut, 43 seconden
Jifunze Kiswahili: Uchambuzi wa neno “MBEJAA”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “MBEJAA”.
15-2-2024 • 0
15 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Dkt. Tulia Akson, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, IPU ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania anaeleza yaliyojadiliwa katika mkutano wa pamoja kati ya Umoja wa Mabunge Duniani na Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na uchambuzi wa neno MBEJAA.Leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani limetoa muongozo mpya na nyenzo za kuboresha usambazaji mdogo wa maji. Mwongozo huo wa “ubora wa maji ya kunywa: usambazaji mdogo wa maji”, na vipengele vinavyohusiana vya ukaguzi wa usafi, unalenga kuboresha ubora wa maji hususan ya kunywa, kujenga utoaji wa huduma thabiti zaidi, na kupambana na kuongezeka kwa magonjwa katika jamii zilizo hatarini na zenye uhaba wa rasilimali hiyo muhimu.Gaza, Leo wakati changamoto ya kukatika kwa umeme ikiendelea katika ukanda huo na kwingineko pia mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema mashambulizi ya anga yakiendelea kulenga mji wa kusini mwa Gaza wa Rafah na kusambaa kwa ripoti kwamba vikosi vya Israel vimefanya operesheni ya kijeshi ndani ya jengo la hospitali ya Nasser, wasiwasi juu ya uwezekano wa uvamizi wa ardhini wa mji huo wa mpakani wenye wakazi wengi unazidi kuongezeka. Na leo ni siku ya kimataifa ya saratani ya utotoni ambapo mwaka huu shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO linajikita na jukumu muhimu la wazazi, madaktari wa familia na madaktari wa watoto katika kubaini mapema saratani hiyo ya utotoni.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “MBEJAA”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
15-2-2024 • 12 minuten, 10 seconden
Redio ni chombo cha mawasiliano kilicho rafiki
Licha ya redio ambacho ni chombo cha kuaminiwa kwa miaka mingi katika usambazaji wa taarifa, kukabiliwa na changamoto nyingi katika nyakati hizi ambazo kuna utitiri wa teknolojia za usambazaji wa habari, bado inaonekana watu wana imani kubwa na chombo hiki kwa sababu mbalimbali. Wachache kati ya wengi, ni wadau hawa tuliozungumza kutoka Afrika Mashariki. Kwanza ni Rose Haji, mwanahabari mwandamizi wa siku nyingi nchini Tanzania akieleza kuhusu kazi kuu za redio.
14-2-2024 • 3 minuten, 28 seconden
Ukanda wa Gaza: Uvamizi wa Rafah itakuwa ni janga lisiloelezeka, yaonya UN
Madaktari wa Umoja wa Mataifa leo wamesema wanahofia janga la kibinadamu lisiloelezeka endapo uvamizi kamili wa jeshi la Israeli utatokea Rafah kusini mwa Gaza ambako maelfu ya maelfu ya watu wamekimbilia tangu kuzuka kwa mzozo huu mpya Oktoba 7 mwaka jana. Likiunga mkono wasiwasi huo ulioelezwa pia na mratibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja na mkuu wa shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Mataifa Martin Griffiths kwamba kushambuliwa kwa Rafah "kunaweza kusababisha mauaji makubwa” Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limesema kila liwezekanalo linapaswa kufanyika kuzuia mashambulizi hayo huku pia likikanusha vikali madai ya ushirikiano wa miaka mingi na washirika wasio wa afya ndani au chini ya hospitali za Gaza.Dkt. Teresa Zakaria Msimamizi wa matukio wa WHO katika eneo linalokaliwa la Palestina amesema, "Hatuwezi kupaza sauti zaidi kukanusha kwamba hakuna ushirikiano kati ya WHO na taasisi nyingine yoyote katika sekta ya afya, washirika wa afya, na katika wizara ya afya ya Gaza ambao tunashirikiana nao," Naye Dkt Rik Peeperkorn, Mwakilishi wa WHO katika eneo linalokaliwa la Palestina akizungumza kutoka Gaza amesisitiza kwamba hospitali "hazipaswi kuendeshwa kijeshi na kwamba macho yote sasa yako kwenye uhasama na mashambulizi makubwa yanayohofiwa huko Rafah. Unaona hofu inayowakabili watu. Na watu kila wakati huja na maswali wanauliza tunaweza kufanya nini?"Maendeleo hayo yanakuja wakati vituo vya hospitali "vimelemewa na kutokuwa na uwezo na viko ukingoni kusambaratika kabisa",amesema Dkt Peeperkorn huku akibainisha kuwa Wagaza milioni 1.5 sasa wamesongamana kwenye mahema ya muda na makazi ya UNRWA kila kona ya mkoa wa Rafah.Nao wataalam huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wameonya juu ya athari mbaya za mzozo huo Gaza kwa maisha ya waandishi wa habari wakisema, "Tunasikitishwa na idadi kubwa ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa vyombo vya habari ambao wameuawa, kushambuliwa, kujeruhiwa na kuzuiliwa katika eneo la Palestina linalokaliwa hasa huko Gaza, katika miezi ya hivi karibuni wakipuuza waziwazi sheria za kimataifa. Tunalaani mauaji, vitisho na mashambulizi yote dhidi ya waandishi wa habari na tunatoa wito kwa pande zote kwenye mzozo kuwalinda."
14-2-2024 • 2 minuten, 35 seconden
14 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na jinsi amabvyo watu kote ulimwenguni wanavyokabiliwa na njaa kali inayochochewa na migogoro ya silaha. Makala tuansalia na mada ya mwaka huu wa siku ya redio na mashinani tunakupeleka nchini Chad, kulikoni?Madaktari wa Umoja wa Mataifa leo wamesema wanahofia janga la kibinadamu lisiloelezeka endapo uvamizi kamili wa jeshi la Israeli utatokea Rafah kusini mwa Gaza ambako maelfu ya maelfu ya watu wamekimbilia tangu kuzuka kwa mzozo huu mpya Oktoba 7 mwaka jana.Takriban watu milioni 258 katika nchi na maeneo 58 ulimwenguni wanakabiliwa na njaa kali inayochochewa na migogoro ya silaha, majanga ya kiuchumi, mabadiliko ya tabianchi, umaskini na ukosefu wa usawa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na kutaka wadau kuangalia upya mtindo wa ufadhili. Katika makala, licha ya redio ambacho ni chombo cha kuaminiwa kwa miaka mingi katika usambazaji wa taarifa, kukabiliwa na changamoto nyingi katika nyakati hizi ambazo kuna utitiri wa teknolojia za usambazaji wa habari, bado inaonekana watu wana imani kubwa na chombo hiki kwa sababu mbalimbali. Wachache kati ya wengi, ni wadau hawa tuliozungumza kutoka Afrika Mashariki.Mashinani tunakuletea ujumbe wa mwanamke dereva wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP anayeendesha gari muhimu aina ya sherps lililoundwa kumudu hali tofautitofauti za barabara na hata mito yenye vina vifupi ambalo husaidia kutoa huduma kwa namna yoyote.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
14-2-2024 • 11 minuten, 42 seconden
Tuangalie mtindo mpya wa ufadhili kwa wakulima na wafugaji waathirika wa mizozo - FAO
Takriban watu milioni 258 katika nchi na maeneo 58 ulimwenguni wanakabiliwa na njaa kali inayochochewa na migogoro ya silaha, majanga ya kiuchumi, mabadiliko ya tabianchi, umaskini na ukosefu wa usawa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na kutaka wadau kuangalia upya mtindo wa ufadhili. Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa FAO Bi. Beth Bechdol idadi inayoongezeka ya watu walioathiriwa kutokana na kuongezeka kwa migogoro ya kibinadamu katika maeneo yaliyoathiriwa na migogoro kama vile Ukanda wa Gaza, Ukraine, na Sudan, au walioathirika na mabadiliko ya tabianchi, inahitaji hatua za haraka na za pamoja ili kupatikana kwa suluhu. Akitolea mfano mzozo unaoendelea huko Sudan Bi. Bechdol amesema hali ya kutisha ya ukosefu wa chakula inaonesha wazi kwamba migogoro na njaa "vina uhusiano usioweza kutenganishwa."“Tunaona karibu nusu ya wananchi wote wapo katika mazingira magumu ya uhaba wa chakula, karibu watu milioni 18 ambao wanatatizika. Kumekuwa na idadi kubwa ya watu kupoteza maisha. Watu wengi waliuawa, mamilioni ya watu waliuawa katika vita vya Sudan.”Naibu Mkurugenzi Mkuu huyo wa FAO amekumbusha kuwa ili kukabiliana na changamoto zinazoongezeka na za muda mrefu kama vile mabadiliko ya tabianchi ni lazima wadau kubonga bongo na kufikiria upya mtindo wa ufadhili wa kifedha. “Mizozo inaendelea kwa miaka mingi, mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa yanachukua muda mrefu miaka minane, miaka kumi, ukame, mafuriko ambayo yanaendelea kutokea. Kwa hiyo inatubidi kwa uangalifu, sote, kutafuta njia mpya za kufikiria juu ya uwiano sahihi, mbinu sahihi ya kujumuisha msaada kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wanawake katika majibu haya, kwa sababu nadhani kilimo ndicho kinachoweza kuwa kweli sehemu ya suluhisho la muda mrefu sio tu kufanyia kazi maswala yanayohusiana na njaa, lakini kama tunavyojua, hatimaye inafika mahali ambapo unajaribu sana kujenga ujasiri katika uchumi, maishani, katika hali ambazo ni matokeo ya hali hizi zote ngumu sana.”FAO imetoa ombi la dola bilioni 18 ili iweze kufanikisha usaidizi kwa kibinadamu kwa watu milioni 43 ili nao waweze kuzalisha chakula chao wenyewe kwa mwaka huu wa 2024.
14-2-2024 • 2 minuten, 40 seconden
13 DESEMBA 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ambapo leo ulimwengu unaadhimisha Siku ya kimataifa ya redio duniani, dhima ya mwaka huu ikiwa 'Karne katika kuhabarisha, kuburudisha na kuelimisha'. Pia tunakuletea habari kwa ufupi. Mashinani tunasalia na maadhimisho ya siku redio.Leo ni siku ya Radio duniani na kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa karne moja chombo hicho lkimekuwa kikihabarisha, kuburudisha na kuelimisha jamii kote duniani. Mwaka huu siku hii inaenzi utajiri uliuopita wa Radio, kuendelea kwa umuhimu wake na matarajio ya mustakbali wake ingawa kinaendelea kukabiliwa na changamoto hasa kutoka kwenye majukwaa ya kidijitali na changamoto za kiuchumi. Mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay katika ujumbe wake amesema “Katika siku hii ya Radio, tunasherehekea sio tu historia ya Radio lakini pia jukumu lake muhimu katika jamii zetu sasa na miaka mingi ijayo.”Gaza, Kamishina Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA Philippe Lazzarini akizungumza na nchi wanachama hii leo amewaomba waliokata ufadhili kwa shirika hilo “Kubadili maamuzi yao hususan kwa mtazamo kwamba wafanyakazi waliodaiwa kushiriki uhalifu walifutwa kazi mara moja na uchunguzi unaendelea.” Namalizia na Sudan ambako kaimu mwakilishi wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO nchini humo Peter Graaff, akizungumza mjini Cairo Misri hii leo kuhusu hali ya Sudan amesema miezi kumi ya vita imetumbukiza mamilioni ya watu katika janga lisiloelezeka la kibinadamu huku mapigano yakiendelea kusambaa katika maeneo mapya na kufurusha watu zaidi wengine mara kadhaa.Na katika mashinani tunakutana na mkaazi wa Karen Nairobi nchini Kenya ambaye anasema kupitia matangazo na vipindi vya redio hutaachwa nyuma wakati fursa za biashara au nafasi za ajira zinavyotokea. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
13-2-2024 • 12 minuten, 32 seconden
Benki ya Maendeleo ya Afrika na UNHCR waungana kusaidia wakimbizi nchini Sudan Kusini
Vita vinapotokea wananchi wanalazimika kusaka kila namna ya kujilinda na kuokoa maisha yao. Mambo yanapokuwa mabaya watu hao hulazimika kuacha kila kitu nyuma na kukimbia kwenda kusaka hifadhi sehemu nyingine. Watu hao wanapoondoka wanaondoka na ujuzi wao mfano kama alikuwa muuguzi, mfanya biashara, fundi muashi au taaluma yoyote ile. Mara nyingi sehemu wanazofikia wakimbizi hao iwe ndani au nje ya nchi zao hujikuta wakipata mahitaji muhimu kwa ajili ya kuishi kama vile chakula cha msaada na matibabu, kiufupi watu hawa hugeuka kuwa tegemezi. Huko nchini Sudan Kusini, Benki ya Maendeleo ya Afrika na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR wameamua kwenda mbali zaidi na kuwasaidia wakimbizi kutoka Sudan na wakimbizi wa Sudan Kusini wanaorejea makwao pamoja na jamiii zilizowakaribisha kujiinua kiuchumi kama anavyotujuza Leah Mushi katika Makala hii.
12-2-2024 • 3 minuten, 47 seconden
12 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa wa uhifadhi wa wanyamapori nchini Uzbekistan, na maradi wa maji safi na salama nchini Rwanda. Makala inatupeleka nchini Sudan Kusini na mashinani nchini Kenya, kulikoni? Leo huko Samarkand nchini Uzbekistan, katika ufunguzi wa mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa wa uhifadhi wa wanyamapori (CMS COP14), ripoti ya kwanza ya kihistoria ya Hali ya Aina za Ndege na Wanyama Pori Wanaohamahama imezinduliwa na kuonesha hali ya mashaka kuhusu viumbe hawa duniani. Mradi wa ushirikiano wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na serikali ya Japan umerejesha mautumaini ya maisha kwa maelfu ya wananchi wa wilaya za Rutsiro, Nyamasheke na Rusizi nchi Rwanda kwa kuwajengea na kukarabati visima vya maji na hivyo kuwaepusha na magonjwa yatokanayo na maji machafu na adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kusaka maji. Makala inatupeleka nchini Sudan Kusini ambapo Leah Mushi anatujuza kuwa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya wakimbizi UNHCR limungana na Benki ya Maendeleo ya Afrika kusaidia wakimbizi kutoka sudan na wakimbizi wa sudan Kusini wanaorejea makwao.Na katika mashinani na tukielekea siku ya kimataifa ya redio tunakupeleka katika kijiji cha Kapkoelei iliyoko katika kaunti ya Nandi nchini Kenya kusikia ujumbe kuhusu jinsi ambavyo radio inavyowasaidia watu vijijini. Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!
12-2-2024 • 11 minuten, 16 seconden
Ripoti ya UN: Aina za wanyama na ndege wanaohamahama zinapungua
Leo huko Samarkand nchini Uzbekistan, katika ufunguzi wa mkutano mkubwa wa Umoja wa Mataifa wa uhifadhi wa wanyamapori (CMS COP14), ripoti ya kwanza ya kihistoria ya Hali ya Aina za Ndege na Wanyama Pori Wanaohamahama imezinduliwa na kuonesha hali ya mashaka kuhusu viumbe hawa duniani. Ingawa baadhi ya aina za ndege na wanyama wanaohamahama zilizoorodheshwa chini ya Mkataba wa aina za ndege na wanyama wanaohamahama, CMS zinaboreka, karibu nusu (asilimia 44) zinaonesha kupungua idadi imesema ripoti hiyo ya aina yake.Zaidi ya aina moja kati ya tano (asilimia 22) ya aina za wanyama zilizoorodheshwa na Mkataba wa aina za ndege na wanyama wanaohamahama, CMS zinatishiwa kutoweka. Mathalani takriban samaki wote (asilimia 97) walioorodheshwa kwenye CMS wanatishiwa kutoweka, ripoti imeeleza.Hatari ya kutoweka inaongezeka kwa aina zinazohamahama duniani kote, ikiwa ni pamoja na zile ambazo hazijaorodheshwa chini ya CMS.Nusu (asilimia 51) ya Maeneo Muhimu ya Baionuai yaliyotambuliwa kuwa muhimu kwa wanyama wanaohama walioorodheshwa na CMS hayana hadhi ya kulindwa, na asilimia 58 ya maeneo yanayofuatiliwa yanatambuliwa kuwa muhimu kwa aina zilizoorodheshwa na CMS yanakabiliwa na viwango visivyo endelevu vya shiniko linalosababishwa na binadamu.Vitisho viwili vikubwa kwa aina za wanyama zilizoorodheshwa kwenye Mkataba wa aina za ndege na wanyama wanaohamahama CMS na aina zote zinazohama zinavunwa kupita kiasi na upotezaji wa makazi kwa sababu ya shughuli za wanadamu. Aina tatu kati ya nne zilizoorodheshwa kwenye CMS huathiriwa na upotevu wa makazi, uharibifu na mgawanyiko, na aina saba kati ya kumi zilizoorodheshwa na CMS huathiriwa na uvunwaji kupita kiasi (ikiwa ni pamoja na kuchukua kwa kukusudia na pia kukamata kwa bahati mbaya).Mabadiliko ya tabianchi, uchafuzi wa mazingira na aina vamizi pia zina athari kubwa kwa aina za wanayama zinazohamahama.Ulimwenguni, aina za wanyama 399 zinazohama ambazo zimo hatarini au zinazokaribia kutoweka hazijaorodheshwa kwa sasa chini ya Mkataba wa aina za ndege na wanyama wanaohamahama CMS.Hadi sasa, hakuna tathmini ya kina kama hii iliyofanywa juu ya aina za wanyama zinazohama. Ripoti hiyo inatoa muhtasari wa kimataifa wa hali ya uhifadhi na mienendo ya idadi ya wanyama wanaohama, pamoja na taarifa za hivi karibuni kuhusu matishio yao makuu na hatua zilizofanikiwa za kuwaokoa.Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira Duniani, UNEP, amesema: “Ripoti ya leo inatuonesha wazi kwamba shughuli za binadamu zisizo rafiki kwa mazingira zinahatarisha mustakabali wa viumbe vinavyohamahama - viumbe ambao sio tu wanafanya kama viashiria vya mabadiliko ya mazingira lakini wana jukumu muhimu katika kudumisha mazingira. utendakazi na uthabiti wa mifumo ikolojia changamano ya sayari yetu. Jumuiya ya kimataifa ina fursa ya kutafsiri sayansi hii ya hivi punde zaidi ya shinikizo zinazokabili spishi zinazohama kuwa hatua madhubuti ya uhifadhi. Kwa kuzingatia hali ya hatari ya wengi wa wanyama hawa, hatuwezi kumudu kuchelewesha, na lazima tushirikiane ili kufanya mapendekezo kuwa kweli."Mabilioni ya wanyama hufanya safari za kuhama kila mwaka kwenye nchi kavu, baharini na angani, wakivuka mipaka ya kitaifa na mabara, huku baadhi yao wakisafiri maelfu ya maili kuzunguka dunia ili kula na kuzaliana.Aina za ndege na wanayama zinazohama zina jukumu muhimu katika kudumisha mfumo ikolojia wa dunia, na kutoa manufaa muhimu, kwa kuchavusha mimea, kusafirisha virutubisho muhimu, kuwinda wadudu, na kusaidia kuhifadhi kaboni.
12-2-2024 • 2 minuten, 17 seconden
Wananchi Rwanda washukuru UNICEF kwa kuwarejeshea matumaiani ya maisha kwa maji safi
Mradi wa ushirikiano wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na serikali ya Japan umerejesha mautumaini ya maisha kwa maelfu ya wananchi wa wilaya za Rutsiro, Nyamasheke na Rusizi nchi Rwanda kwa kuwajengea na kukarabati visima vya maji na hivyo kuwaepusha na magonjwa yatokanayo na maji machafu na adha ya kutembea umbali mrefu kwenda kusaka maji. Ni Josephine Mukandanga mkazi na mmoja wa wanufaika wa mradi huo wa maji toka wilaya ya Nyamasheke akisema kabla ya mradi huo upatikanaji wa maji ulikuwa mtihani mkubwa kwao. Kwa Josephine kama ilivyo kwa maelfu ya wakazi wengine mradi huo umemletea nuru kubwa. “Kutokana na maporomoko ya udongo na majanga mengine ya asili mitambo yote ya maji iliharibika na huduma yetu ya maji kukatika. Na hivyo kulazimika kwenda kuchota maji kwenye visima na mabwawa”Kupitia mradi huu wa UNICEF na Japani watu zaidi ya 50,000 katika wilaya tatu wamefaidika kwa maji safi na salama na sio tu umewaletea furaha na kupunguza adha ya umbali mrefu kusaka maji pia umewaepusha na magonjwa yatokanayo na huduma duni za maji , usafi na usafi wa mazingira WASH baada ya miaka mingi.Kwa Josephine huu ni ukurasa mpya kwa maisha yake na jamii yake.“Kwa sasa tatizo limetatuliwa. Sasa tuna maji safi ya kutosha kuosha vyombo, kuogesha watoto wetu, kufua nguo zetu na kuoga kuhakikisha miili yetu iko safi.”Ukosefu wa maji uliwafanya watoto wengi katika wilaya hizo tatu kukosa masomo, kuugua mara kwa mara na kukabiliwa na changamoto nyingine wanapokwenda kuteka maji mbali, lakini sasa wananchi wa wilaya zote tatu wanachosema nishukran kwa serikali yao ya Rwanda, UNICEF na serikali ya Japan kwa kuwapa zawadi ya uhai kupitia maji safi na salama ambayo gharama yake haiwezi kupimika katika maisha yao.
12-2-2024 • 2 minuten, 11 seconden
FAO yawashika mkono wasichana Afrika kuingia katika sayansi ya kilimo
Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi itakayoadhimishwa Jumapili Februari 11 shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema katika Dunia ya sasa inayobadilika kwa kasi, sayansi na ubunifu vina jukumu muhimu katika kushughulikia changamoto zinazoiandama Dunia. Hata hivyo licha ya hatua kubwa zilizopigwa katika kuendeleza sayansi wanawake na wasichana wanaendelewa kukabiliwa na vikwazo vingi kuingia katika tasnia hiyo ndio maana shirika hilo limeamua kuchukua hatua kuendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo hususan wasichana katika sayansi ya takwimu katika kilimo. Leo tunakupeleka Côte D’Ivoire kushuhudia mchango wa FAO katika hilo. Flora Nducha anafafanua zaidi katika makala hii
9-2-2024 • 4 minuten, 15 seconden
09 FEBRUARI 2024
Katika Jarida la habari la Umoja wa Mataifa hii leo Anold Kayanda anakuletea Hali Gaza inazidi kuwa mbaya , mashirika ya Umoja wa Mataifa yaonya kuhusu athari za kiafya, vifo, na njaaNchini Sudan shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF laonya juu ya hatari ya utapiamlo mkali wakati vita ikiendelea katika maeneo mbalimbaliMakala inatupeleka Corte D'Ivoire kumulika mchango wa shirika la chakula na kilimo FAO katika kuwainua wanawake na wasichana katika sayansiNa mashinani inatupeleka Malawi ambako shirika la UNICEF limekuwa likitoa msaada wa vifaa kwa watoto kujifunza
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali “Mjinga akierevuka, mwerevu yupo mashakani.”
8-2-2024 • 0
08 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukimulika hali ya wakimbizi wa ndani na ziara ya Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi nchini Sudan.Pia tunakuletea habari kwa ufupi, na neno la wiki tunakuleleta uchambuzi wa methali “Mjinga akierevuka, mwerevu yupo mashakani.”Huko Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu wamesema wanafanya kila liwezekanalo kuwasaidia waathirika wa mafuriko mabaya zaidi nchini humo yaliyosababisha kina cha mto Congo kufurika katika kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa katika kipindi cha zaidi ya miaka 60. Gaza wakati mashambulizi makubwa ya mambomu ya Israel yakiendelea kwa njia ya anga, aridhini na baharini katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza na hususan Khan Younis na viunga vyake na kuongeza idadi ya vifo, majeruhi na wakimbizi wa ndani shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema jana Februari 7 jeshi la Israel lilitangaza kusitisha kwa muda na kwa kimkakati hii leo operesheni zake za kijeshi katika maeneo ya magharibi mwa Rafah kuanzia saa nne asubuhi hadi saana nane mchana saa za Israel ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia. Mkutano wa maandalizi wa Umoja wa Mataifa wa nchi zinazoendelea zisizo na bandari (LLDCs), unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York umesema nchi hizo kwa kukosa fursa ya moja kwa moja ya kuwa na bahari zinakabiliwa na vikwazo vikubwa vya kibiashara, mawasiliano na maendeleo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali “Mjinga akierevuka, mwerevu yupo mashakani.” Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
8-2-2024 • 11 minuten, 47 seconden
Kampeni ya UNDP Tanzania ya kukabili misimamo mikali yainua vijana kiuchumi Kilwa Masoko mkoani Lindi
Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP linatekeleza mradi wa kukabili misimamo mikali kupitia kampeni ya amani kama njia mojawapo ya kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Tayari kuna wanaufaika na mmoja wao ni Nuru Mbaruku Ramadhani, mwenyekiti wa kikundi cha Masoko 2 Peace Club kilichoko Kilwa Masoko mkoa wa Lindi, kusini mashariki mwa Tanzania. Kikundi hiki kilichoanzishwa mwezi Juni mwaka 2023, kina mabalozi 9 wa amani wakiwemo wanawake 6 na wanaume 3. Nuru akizungumza na Sawiche Wamunza, Afisa mchambuzi wa mawasiliano UNDP Tanzania anaaanza kuelezea kwa nini walianzisha kikundi hiki.
7-2-2024 • 5 minuten, 1 seconde
UNICEF Niger inawasaidia watoto kupona utapiamlo mkali
Nchini Niger shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF linaendesha program mbalimbali za kusaidia kupambana na utapiamlo mkali kwa watoto kwa kutoa virutubisho, kuhakikisha kuna upatikanaji wa huduma bora za lishe na usaidizi wa unyonyeshaji. Mtoto Laoualy miezi miwili iliyopita alikuwa dhofuli hali, bibi yake Sahoura alikuwa na wasiwasi sana na kuamua kumkimbiza katika hospitali inayopatiwa usaidizi na UNICEF nchini Niger ambako huko aligundulika kuwa na utapiamlo mkali.“Mjukuu wangu alikuwa anaugua mafua akapata na homa, alikuwa hali kitu chochote na mdomo wake ukawa umevimba. Nilipowasili hospitali nilikuwa nimekata tamaa, alikuwa hawezi hata kusimama.”Kwasababu ya hali mbaya ya mtoto walilazwa. Pamoja na kupatiwa matibabu mengine hospitali hapo bibi Sahoura anasema mjukuu wake alianza kupatiwa maziwa ya matibabu kwa ajili ya utapiamlo. “Kidogo kidogo maziwa hayo ya matibabu kwa ajili ya utapiamlo yakaanza kurejesha hamu yake ya kula chakula. Na hata tuliporuhusiwa hospitali na kurejea nyumbani akawa anaendelea kula vyakula vingine pia.”Naam, miezi miwili baada ya mtoto Laoualy kuruhusiwa kutoka hospitali, hali yake ikoje? “Mjukuu wangu anaendelea vizuri, amepona na anajisikia vizuri” Mtoto Laoualy anaendelea kupatiwa maziwa ya matibabu. Maziwa haya ya matibabu hutumiwa kulisha watoto wadogo walio katika awamu ya 1 ya kupona kutokana na utapiamlo mkali.
7-2-2024 • 1 minuut, 30 seconden
07 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia vita vinavyoendelea katika ukanda wa Gaza, na afya ya watoto nchini Niger. Makala tunamulika kazi za vijana nchini Tanzania na mashinani tunakuletea ujumbe wa mhudumu wa afya nchini Afghanistan anayejitolea kuchochea afya bora kwa jamii.Vita huko Gaza kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina Hamas ikiingia mwezi wa tano hii leo na kuwa imesababisha vifo va wapalestina 27,585 na takribani 70,000 wamejeruhiwa, Mkuu wa masuala ya misaada ya dharura kwenye Umoja wa Mataifa amekaribisha dalili za mapema za uwezekano wa sitisho la mapigano linaloweza kufanikisha kuachiliwa huru kwa mateka wote waliosalia. Nchini Niger shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF linaendesha program mbalimbali za kusaidia kupambana na utapiamlo mkali kwa watoto kwa kutoa virutubisho, kuhakikisha kuna upatikanaji wa huduma bora za lishe na usaidizi wa unyonyeshaji. Evarist Mapesa anasimulizi ya mmoja wa wanufaika wa huduma hizo za UNICEF. Makala inatupeleka Kilwa Masoko mkoani Lindi, kusini-,mashariki mwa Tanzania, katika bahari ya Hindi ambako Sawiche Wamunza, Afisa Mchambuzi wa Mawasiliano kutoka shirika la Umoja wa MAtaifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP nchini humo anazungumza na Nuru Mbaruku Ramadhani, mwenyekiti wa Kikundi kiitwacho Masoko 2 Peace Club, kinachonufaika na miradi inayotekelezwa na UNDP mkoani humo kama sehemu ya kuwezesha vijana kusongesha amani ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDGs, badala ya vijana kutumbukia kwenye misimamo mikali. Nuru anaanza kwa kuelezea sababu ya kuanzisha kikundi chao.Na mashinani tutaelekea nchini Afghanistan kushuhudia ni kwa jinsi gani wenyeji wanajitolea kuchochea afya bora kwa jamii. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
7-2-2024 • 11 minuten, 43 seconden
Kuelekea mwezi wa 5 wa mapigano Gaza, kuna nuru ya sitisho la mapigano
Vita huko Gaza kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina Hamas ikiingia mwezi wa tano hii leo Jumatano na kuwa imesababisha vifo va wapalestina 27,585 na takribani 70,000 wamejeruhiwa, Mkuu wa masuala ya misaada ya dharura kwenye Umoja wa Mataifa amekaribisha dalili za mapema za uwezekano wa sitisho la mapigano linaloweza kufanikisha kuachiliwa huru kwa mateka wote waliosalia. Martin Griffiths ambaye ni Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kiutu, OCHA ametoa maoni hayo kwa kuzingatia taarifa Chanya zinazotoka kwenye mazungumzo ya hivi karibuni zaidi yanayoendelea kuhusu amani ukanda wa Gaza yakiongozwa na Misri, Qatar na MArekani.Bwana Griffiths anasema kuna uwezekano wa kipindi kirefu cha sitisho la mapigano na hivyo kuruhusu mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas kuachiliwa huru, halikadhalika wafugwa wa kipalestina wanaoshikiliwa huko Israel.Akizungumza na waandishi wa habari hii leo huko Geneva, Uswisi, Mkuu huyo wa OCHA amesema awamu hii inaweza kufuatiwa na kipindi kingine cha utulivu kinachoweza kufungua mlango wa kumalizika kwa vita kati ya Hamas na Israel.Nuru ya sitisho la mapigano inaripotiwa huku OCHA ikisema kuwa mashambulizi makubwa yaliendelea kwenye ukanda wote wa Gaza siku ya Jumanne, hasa mjini Khan Younis.OCHA inasema kwa zaidi ya wiki mbili, mapigano makali yameendelea kuripotiwa karibu na hospitali za Al Amal na Nasser huko Khan Younis na hivyo kuweka hatarini usalama wa madaktari, wauguzi, majeruhi na maelfu ya wakimbizi wa ndani waliosaka hifadhi kwenye hospitali hizo.OCHA pia inasema uhaba wa vifaa vya matibabu ikiwemo upasuaji na kwamba nishati ya siku nne tu ndio imesalia kwa ajili ya kuendesha majenereta yanayozalisha umeme unaotumika hospitalini. Kwa upande wa vifo na majeruhi upande wa Israel, OCHA inasema askari mwingine wa Israel aliuawa wakati wa mapigano ya ardhini yaliyoanza tarehe 5 hadi 6 mwezi huu Gaza na hivyo kufanya idadi ya askari wa Israel waliouawa tangu Oktoba 7, 2023 kufikia 224 na majeruhi 1,304.
7-2-2024 • 2 minuten, 12 seconden
06 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na utamsikia ujumbe wa Careen Joel Mwakitalu ambaye taasisi yake ya No Taka Tanzania inatumia mbinu ya elimu na teknolojia ya Geospatial yaani ramani na mazingira ili kupambana na changamoto ya wanadamu kuhama kutokana na mabadiliko ya tabianchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani.Idadi ya wagonjwa wa kipindipindu hususan Mashariki na kusini mwa Afrika imeongezeka mara mbili mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo jumla ya wagonjwa 26,000 na vifo 7000 vimeripotiwa katika wiki nne za mwanzo wa mwaka huu kutoka nchi 10 zikiongozwA na Zambia na Zimbabwe. Nchini Kenya Bodi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kufanikisha upatikanaji wa dawa na tiba kwa gharama nafuu UNITAID leo limeendelea na ziara yake kukagua faida za miradi bunifu ya kuimarisha sekta ya afya ambayo imeboresha maisha ya maelfu ya wakenya na wakati huo huo kuokoa fedha. Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na watoto aw kike, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwenye ujumbe wake amesema mwaka huu wa 2024 wasichana milioni 4.4 wakiwa hatarini kukeketwa kila mtu achukue hatua maradufu kuepusha kitendo hicho ambacho kinakiuka haki za msingi wa binadamu na kusababisha machungu ya afya ya mwili na akili kwa wanawake na wasichana.Na mashinani tutaelekea nchini Uganda kusikia ni kwa jinsi gani masomo ya teknolojia inatumika katika shule za sekondari. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
6-2-2024 • 11 minuten, 26 seconden
El Niño na janga la tabianchi vyaibua hofu ya ukame Madagascar
El Niño ambao ni mkondo joto, ni hali ya kawaida inayotokea kwenye baharí ikihusisha joto la hewa baharini na wataalamu wanasema unaweza kuvuruga tena kwa kiasi kikubwa mienendo ya hali ya hewa duniani. Hata hivyo dharura ya tabianchi inayosababishwa na shughuli za binadamu zinaongeza ukali na madhara ya El Niño kwa watu na sayari dunia.Nchini Madagascar, kisiwa ambacho kiko eneo ambamo kimo baharini linakiweka kwenye hatari ya kukumbwa na hali mbaya hewa kupindukia, Umoja wa Mataifa unashirikiana na mamlaka kusaidia taifa hilo kuhimili na kukabili.Katika miaka ya karibuni, Madagascar imepigwa na vimbunga vikubwa kupindukia, halikadhalika ukame mkali katika miongo minne iliyopita, na kusababisha njaa na maelfu ya wananchi kukaribia kutumbukia kwenye baa la njaa.Kutokana na hali hiyo, Reena Ghelani, ambaye ni Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Janga la Tabianchi hususan hatua dhidi ya El Niño amezuru Madagascar, ambako anakagua miradi iliyobuniwa kuwezesha jamii kuwa na mnepo, na zisiathiriwe kwa kiasi kikubwa na hali mbaya za hewa. Daniel Dicknson wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Bi. Ghelani na mazungumzo yao ndio makala yetu inayoletwa kwako na Evarist Mapesa wa Idhaa hii. Hapa Bi. Ghelani anaanza kwa kuelezea El Niño.
5-2-2024 • 4 minuten, 16 seconden
05 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na vifaa vya kusikia vizuri vinavyosaidia wanafunzi wenye ulemavu wa kutosikia vizuzi nchini Rwanda. Makala inatupeleka nchini Madagascar, na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa misaada ya kiutu huko Gaza, Mashariki ya Kati, yameripoti kuwa kuwa msafara wa malori yaliyokuwa yamebeba vyakula umeshambuliwa kwa kombora leo baada ya mwisho wa wiki uliogubikwa na uhasama na mapigano yaliyosababisha kuuawa kwa wapalestina 234, na hivyo kuzidisha mvutano zaidi kwenye ukanda huo. Ruzuku inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Rwanda kwenye vifaa vya kusaidia watoto kuweza kusikia vyema imeleta manufaa na kurudisha ndoto za watoto waliokuwa na changamoto ya kusikia. Leah Mushi anatueleza kuhusu mmoja wa watoto wanufaika. Makala inatupeleka Madagascar ambako El Nino inajengea hofu wananchi. Hivyo Reena Ghelani ambaye ni Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Janga la Tabianchi hususan hatua dhidi ya El Niño amezuru taifa hilo kukagua hali ilivyo na amezungumza na Daniel Dickinson wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa, mazungumzo ambayo tumeandaa makala inayoletwa kwako na Evarist Mapesa.Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe wa wakimbizi wanaokimbia machafuko ya mara kwa mara kutoko nchi jirani. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
5-2-2024 • 9 minuten, 57 seconden
Msafara wa vyakula Gaza washambuliwa, wapalestina 234 wauawa mwishoni mwa wiki
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa misaada ya kiutu huko Gaza, Mashariki ya Kati, yameripoti kuwa kuwa msafara wa malori yaliyokuwa yamebeba vyakula umeshambuliwa kwa kombora leo baada ya mwisho wa wiki uliogubikwa na uhasama na mapigano yaliyosababisha kuuawa kwa wapalestina 234, na hivyo kuzidisha mvutano zaidi kwenye ukanda huo.Ripoti za kushambuliwa kwa msafara huo zimetolewa na Tom White, Mkurugenzi wa Masuala katika Shirik ala Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA huko Gaza, ambaye kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X, zamani Twitter, ameambatanisha picha mbili, zikionesha jinsi tela la lori lililosheheni vyakula likiwa limeshambuliwa na kitambaa cha hema kilichotumika kulifunika tela hilo kikiwa kimeraruka.Amesema lori hilo lenye tela lilikuwa linasubiri kuingia Kaskazini mwa Gaza lilipopigwa kwa kombora la Israel kutoka majini.“Tunashukuru hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa,” amesema Bwana White.Kwenye picha hizo, maboksi kadhaa yenye misaada yameonekana kusambaa barabarani, lakini haikufahamika haraka kilichomo kwenye maboksi hayo.Harakati za UNRWA kufikia eneo la kaskazini mwa Gaza zimekuja baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula, WFP kuripoti Ijumaa ya kwamba kwa mara ya tatu limeshindwa kufika kaskazini mwa Gaza.Mkurugenzi wa WFP eneo la Palestina Matthew Hollingworth amesema waliweza kufikisha misafara minne tu mwezi Januari, sawa na malori 35 yenye shehena kwa ajili ya watu 130,000.Afisa huyo wa WFP anasema chakula hicho hakitoshelezi kuepusha baa la njaa Gaza, kwani kiwango cha njaa kinazidi kuongezeka Gaza.Ametumia ukurasa wake kwenye mtandao wa X kuonesha jinsi ilivyo vigumu kwa misafara ya misaada kuingia na kupita eneo lililozingirwa la Gaza baada ya takribani miezi minne ya mashambulizi yasiyokoma kutoka Israel.Anasema, “kuna uharibifu kila mahali, vifusi, Barabara zimefungwa na vile vile kuna mapigano yanaendelea kwenye maeneo kadhaa ya ukanda huu. Inachukua muda kuratibu, kupita kwenye vizuizi.”
5-2-2024 • 2 minuten, 4 seconden
UNICEF Rwanda inaboresha maisha ya watoto wenye ulemavu wa kusikia
Ruzuku inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Rwanda kwenye vifaa vya kusaidia watoto kuweza kusikia vyema imeleta manufaa na kurudisha ndoto za watoto waliokuwa na changamoto ya kusikia. Leah Mushi anatueleza kuhusu mmoja wa watoto wanufaika. Huyu ni Pascaline Uwababyeyi mwanafunzi wa shule ya msingi nchini Rwanda anasema kabla ya kupata vifaa vya kumsaidia kusikia vyema alikuwa hawezi kucheza na watoto wenzake kwani hakuweza kuwasikia kile walichokuwa wakisema. Lakini sasa anaweza kucheza nao kwani anawasikia vyema kabisa.”Pascaline ni mmoja wa wanufaika wa ruzuku inayotolewa na UNICEF nchini Rwanda katika vifaa vya kusaidia kusikia vizuri ambavyo vimepunguzwa bei kwa zaidi ya asilimia 94 kutoka dola 2000 mpaka dola 118. Mama yake Pascaline Bi. Appoline Uwababyeyi anasema anaona mabadiliko katika maisha ya mwanae.“Kitu kipya nilichokiona kutoka kwa mwanangu ni kwamba sasa anafurahia kusoma zaidi kuliko hapo awali. Anapofika darasani, anaweza kusikia, ilhali hapo awali, hakuweza na angeogopa kuuliza maswali, alikuwa ananiambia "Nikiuliza, watanicheka." Lakini sasa, mwalimu anapoeleza jambo lililoandikwa ubaoni, yeye husikia na kuelewa, kama tu wanafunzi wenzake wote.”Pascaline anaeleza faida alizozipata baada ya kuanza kuvaa kifaa cha kumsaidia kusikia vizuri kuwa sasa anaweza kusikiliza muziki, kuwasikia marafiki zake, walimu wake, mama yake na hata mdogo wake wa kiume anasema, “Hii inanifurahisha. Ndoto zangu ni kuwa Waziri. Waziri Mkuu.”
5-2-2024 • 1 minuut, 47 seconden
Muunganisho wa kijamii huondoa upweke na kuboresha afya kwa jamii – WHO
Mwezi Novemba mwaka jana shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO lilizindua Kamisheni ya kuchochea Muunganisho wa Kijamii au Social Connection kwa lengo la kuondokana na tatizo la upweke ambalo limetambuliwa kuwa moja ya tishio kubwa la afya duniani. WHO inasema kutengwa na jamii na kuishi maisha ya upweke ni jambo hatari, chungu, na zaidi hatari kwa afya ya binadamu. Upweke unaweza kuathiri mtu yeyote, wa hali yeyote mahali popote. Kamisheni hiyo sasa kupitia video za Muunganisho wa Kijamii hufikia watu kote ulimwenguni wanaoishi pekee yao lengo kuu likiwa ni kuwapatanisha na kuwashirikisha na jamii pamoja na marafiki ili waondokane na msongo wa mawazo na kuboresha afya yao. Tayari msusururu wa video hizo umeanza kuchapishwa mitandaoni ambapo Selina Jerobon wa Idhaa hii amefuatilia simulizi ya Maria Ondosia Mawero, mama mzee anayeishi katika eneo la mabanda la Kibera jijini Nairobi, nchini Kenya akitueleza ni kwa nini uhusiano wa kijamii ni muhimu kwa afya yetu, ustawi na ubinadamu wetu.
2-2-2024 • 4 minuten, 6 seconden
Hakikisha usalama zaidi ili wahudumu wa kibinadamu waweze kusambaza chakula Sudan - WFP
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limezitaka pande zinazohasimiana nchini Sudan kutoa hakikisho zaidi la usalama kwa shirika hilo ili liweze kusambaza msaada wa chakula kwa wananchi waliokimbia makazi yao na waliokwama katikati ya mapigano ili kuwanusuru watu hao kutokufa njaa. Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao huko Geneva Uswisi, Msemaji wa WFP nchini Sudan, Leonie Kinsley amesema hali ya chakula nchini humo ni mbaya sana, licha ya juhudi zinazofanywa na shirika lao kutoa Msaada kwa watu milioni 6.5, bado watu milioni 18 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.Kinsley amesema “WFP kwa sasa ina uwezo wa kutoa msaada wa haraka wa chakula kwa mtu mmoja kati ya 10 ambao wanakabiliwa na hali ya dharura ya njaa nchini Sudan. Ikimaanisha asilimia 90 ya watu ambao ni wenye njaa zaidi hawapati msaada.”Maeneo yaliyoathirika zaidi ni Khartoum, Darfur and Kordofan na sasa jimbo la Jazeera, ambako mzozo ulisambaa mwezi Desemba mwaka jana.WFP imeeleza kuwa chakula kipo nchini humo lakini inawawia vigumu kukisambaza na wanakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo kuporwa kwa chakula katika ghala lao la chakula huko jimboni Jazeera.“Ili Msaada uweze kuwafikia wananchi, misafara ya misaada ya kibinadamu lazima iruhusiwe kuvuka katika eneo lenye mapigano. Hata hivyo imekuwa vigumu hilo kufanyika kutokana na vitisho vya usalama, mapigano yanayoendelea na kulazimishwa kuwekewa vizuizi barabarani wakidai ada na ushuru. Hali nchini Sudan leo ni janga. Mamilioni ya watu wameathiriwa na mzozo huo.”Angalau juhudi za WFP kusaka hakikisho la usalama ili kusambaza chakula zimezaa matunda wiki iliyopita, na sasa usambazaji wa misaada unaendelea huko Kassala, Gadhafi na jimbo la Blue Nile.Hata hivyo malori mengine 31 ya WFP, ambayo yalipaswa kupeleka misaada ya mara kwa mara huko Kordofan na White Madani, yameegeshwa tupu yakishindwa kuondoka.Hata hivyo malori mengine 31 ya WFP, ambayo yalipaswa kupeleka misaada ya mara kwa mara huko Kordofan na White Madani, yameegeshwa tupu yakishindwa kuondoka.
2-2-2024 • 2 minuten, 14 seconden
02 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia mizozo nchini Sudan, na uvutaji wa cigara. Makala inatupeleka nchini Kenya kumulika madhara ya upweke na programu ya Muunganisho wa Kijamii inayosaidia watu kuondokana na upweke. Mashinani tunakuletea ujumbe kuhusu saratani. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limezitaka pande zinazo hasimiana nchini Sudan kutoa hakikisho la usalama kwa shirika hilo ili liweze kusambaza msaada wa chakula kwa wananchi waliokimbia makazi yao na waliokwama katikati ya mapigano ili kuwanusuru watu hao kutokufa njaa. Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, simulizi ya mtu aliyeanza kuvuta sigara akiwa kijana balehe na sasa ameamua kuacha inamulika ni kwa nini shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO linasisitiza umuhimu wa kampeni za kuacha tumbaku kwani ni miongoni mwa visababishi vikubwa vya maambukizi ya saratani ya mapafu inayooongoza kwa kuua zaidi vifo miongoni mwa wanaume duniani. Makala inaangazia madhara ya upweke, na tunakutana na mama mzee ambaye ameishi pekee yake kwa muda mrefu katika eneo la mabanda la Kibera jijini Nairobi, Kenya, lakini programu ya Muunganisho wa Kijamii (Social Connection) unaofanikishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO imemuondolewa upweke.Mashinani tunaelekea mkoani Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania, kusikia ujumbe wa matibabu ya saratari ya shingo ya kizazi. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
2-2-2024 • 11 minuten, 27 seconden
Acheni sigara haina maana - Thierry
Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, simulizi ya mtu aliyeanza kuvuta sigara akiwa kijana balehe na sasa ameamua kuacha inamulika ni kwa nini shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO linasisitiza umuhimu wa kampeni za kuacha tumbaku kwani ni miongoni mwa visababishi vikubwa vya maambukizi ya saratani ya mapafu inayooongoza kwa kuua zaidi vifo miongoni mwa wanaume duniani. WHO inasema katika ukanda wa Afrika kuna wavuta sigara milioni 73, na kijana balehe 1 kati ya 10 anavuta sigara. Thierry Anatole kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR sasa mtu mzima alikuwa miongoni mwa takwimu hizo.Anasema “nilivuta sigara kwa miaka 30. Nilianza miaka ya 1980 na nilikuwa na umri wa kati ya miaka 11 na 12. Kwa siku nilikuwa navuta pakiti 4.”Kwa mujibu wa WHO, nusu ya watu wanaotumia tumbaku, hufariki dunia. Na Tumbaku husababisha aina lukuki za saratani ikiwemo ya mapafu na njia ya hewa.“Unaweza kuwa na kikohozi mfululizo kwa miezi mitatu, anaendelea Thierry watu wanaweza kukosea na kudhania ni Kifua Kikuu, kumbe ni kikohozi sugu. Na madhara yake ni makubwa.”Thierry akaendelea kuelezea madhara ya uvutaji kiuchumi akisema “hata wakati wa ukata, huwezi kuacha kuvuta sigara. Hata kama ni fedha ya kununulia dawa, unanunulia sigara.”Sasa Thierry yuko uwanjani anafanya mazoezi kwani miaka 7 iliyopita aliamua kuacha kuvuta sigara. Ari ya kulinda watoto wake dhidi ya moshi wa sigara ikaongezeka, “Nilikuwa ninawaumiza bila kutambua.”WHO inasema moshi kutoka kwa mvutaji sigara husababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 1 kila mwaka kwani huathiri afya ya walio karibu nae.Hapo ndipo akili ilinirudia na kuanzia Aprili 2016 hadi leo sijavuta tena sigara. Nimetoka kwenye kifungo cha sigara, Niko huru! Sasa niña fedha kwenye mifuko yangu. Ninaweza kufanya michezo, nakimbia, na ninapumua vizuri.”Thierry akatamatisha na ujumbe.“Kwa wavutaji, na wanaotaka kuvuta, kwa waanzao na wanaovuta mara moja moja, wasikilize sauti ndani ya roho yao inayosema acha kuvuta sigara, usisubiri hadi ukachelewa kwani uvutaji unaua kila siku.”
2-2-2024 • 2 minuten, 26 seconden
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno “MITONGO.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii lleo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “MITONGO.”
1-2-2024 • 1 minuut
01 FEBRUARI 2024
Hii leo jaridani tumekuandalia mada kwa kina ambayo leo inatupeleka katika kijijini Lokujo wilayani Koboko Kusini mwa Uganda kusikia simulizi ya mnufaika wa msaada wa mafunzo, fecda, na pembejeo wa WFP, Pia tunakuletea habari kwa ufipi na uchambuzi wa methali.Kufuatia uamuzi wa nchi 16 wafadhili kusitisha utoaji fedha kwa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA baada ya Israel kulishutumu shirika hilo kuwa wafanyakazi wake 12 walihusika katika shambulio lililotokea tarehe 7 Oktoba mwaka jana, Mkuu wa UNRWA Philipe Lazzarini amesema kuwa iwapo fedha zitaendelea kuzuiliwa, watalazimika kufunga operesheni zao ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa Februari. Wataalamu wa Haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza kusitikishwa na kulaani vitendo vya waandishi wa habari kuuawa, kushambuliwa, kujeruhiwa na kuwekwa vizuizini huko katika eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na kutoa wito kwa pande zote kwenye mzozo kuhakikisha wanalinda waandishi wa habari.Tumalizie na masuala ya afya ambapo Shirika la kimataifa la utafiti wa saratani, IARC ambalo ni shirika tanzu la WHO hii leo limetangaza matokeo ya utafiti wake uliofanyika katika nchi 115 wakiangazia mzigo wa kimataifa wa saratani ambapo wamebaini kuwa nchi nyingi hazitoi kipaumbele na kufadhili ipasavyo huduma za matibabu ya saratani kama sehemu ya mpango wa afya kwa wote.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii lleo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “MITONGO.” Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
1-2-2024 • 11 minuten, 39 seconden
Mwanafunzi Msumbiji: Iwe mvua iwe upepo mkali madarasa yetu ni salama
Kila mwaka, Msumbiji hukabiliwa na matukio ya hali mbaya za hewa kupindukia kama vile vimbunga na mafuriko, matukio ambayo husababisha uharibifu wa shule na hatimaye watoto kushindwa kujifunza. Hata hivyo, ujenzi wa madarasa yanayohimili matukio kama vile pepo kali na mafuriko umeleta nuru na matumiani kwa watoto, wazazi na walimu. Madarasa haya yanawezesha watoto kubakia salama hata wakati wa mvua na upepo mkali. Hali hii ni uwekezaji wa kudumu kwani ni hakikisho kwa watoto kuendelea kupata elimu na mustakabali wao kuwa bora. Selina Jerobon wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anamulika ni kwa vipi hilo limefanyika kupitia mradi uliofadhiliwa na Benki ya Dunia.
31-1-2024 • 4 minuten, 11 seconden
Kamishna Mkuu wa UNHCR akiwa ziarani Ethiopia anasihi wasisahaulike wanaoikimbia Sudan
Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Ethiopia ametoa wito kwa ulimwengu kuwasaidia watu wa Sudan wanaoikimbia nchi yao na kuingia Ethiopia ambayo ni moja ya nchi wenyeji wa wakimbizi na wakimbizi wa ndani wengi zaidi ulimwenguni. “Kuna majanga mengine kote duniani. Mengine makali zaidi na mengine yanaongelewa zaidi. Tusiwasahau watu ambao nimezungumza nao waliokimbia vita Sudan. Hawa wanateseka kila siku na wanahitaji msaada.”Grandi amesafiri hadi magharibi mwa Ethiopia katika mji wa Assosa, ambao ni mji mkuu wa eneo la Benishangul-Gumuz karibu na mpaka wa Sudan, ambako amekutana na baadhi ya wakimbizi na waomba hifadhi zaidi ya 20,000 waliopo katika kituo cha usafiri cha Kurmuk.“Waafrika kamwe hawatupani, wanashikana mkono na ni watu wakarimu kwa walio katika madhila. Hili ni ombi pia kwa jumuiya ya kimataifa. Nchi zote hizo ikiwemo Ethiopia sio nchi tajiri, sio nchi zenye raslimali nyingi, zinahitaji usaidizi wa kimataifa, zinahitaji kugawana uzito wa mzigo na isivyo bahati janga la wakimbizi wa Sudan, janga la kufurushwa, janga la kibinadamu ni moja ya majanga yenye ufadhili mdogo zaidi duniani leo.”
31-1-2024 • 1 minuut, 31 seconden
31 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunafuatilia ziara ya Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi nchini Ethiopia na wakimbizi wa ndani nchini Sudan. Makala tunakupeleka nchini Msumbiji na mashinani nchini Kenya. Kulikoni?Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Filippo Grandi akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Ethiopia ametoa wito kwa ulimwengu kuwasaidia watu wa Sudan wanaoikimbia nchi yao na kuingia Ethiopia ambayo ni moja ya nchi wenyeji wa wakimbizi na wakimbizi wa ndani wengi zaidi ulimwenguni. Islam Mubarak, msichana mwenye umri wa miaka 21 ambaye vita mpya iliyozuka Sudan Aprili mwaka jana ilimlazimisha kufungasha virago na familia yake na kuukimbia mji mkuu Khartoum na sasa amekwama katika kambi ya wakimbizi wa ndani katika jimbo la El-Gedarif, lakini ndoto yake ni kurejea nyumbani siku moja.Makala tunakwenda nchini Msumbiji ambako Selina Jerobon wa Idhaa hii anamulika kabla na baada ya ujenzi wa madarasa yanayohimili hali mbaya za hewa ikiwemo vimbunga vinavyong’oa mapaa.Mashinani tutaelekea katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Kaunti ya Turkana, nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani wazazi wenye ujuzi Chanya wa malezi wanapewa Usaidizi wa Kisaikolojia ili kuwapa watoto msingi muhimu katika ukuaji wao. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
31-1-2024 • 11 minuten, 18 seconden
Simulizi ya Islam Mubarak: Ndoto yangu ni kurejea nyumbani na kuishi kwa amani
Kutana na Islam Mubarak msichana mwenye umri wa miaka 21 ambaye vita mpya iliyozuka Sudan Aprili mwaka jana ilimlazimisha kufungasha virago na familia yake na kuukimbia mji mkuu Khartoum na sasa amekwama katika kambi ya wakimbizi wa ndani katika jimbo la El-Gedarif, lakini ndoto yake ni kurejea nyumbani siku moja.Katika kambi ya wakimbizi wa ndani inayosimamiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ni Islam akiwa amekata tamaa kwa kutouona au kuelezea mustakbali wake .Kabla ya kuzuka mapigano na kukimbia Khartoum Islam alikuwa akisomemea masuala ya fasihi ya Kiingereza, kisha maisha yake yakapinduliwa na ndoto yake kubadilika,“Kama ungeniuliza hapo awali ningekueleza mustakbali wangu utakuwaje , ningemaliza masomo na kisha kwenda zangu Korea Kusini kukutana na kundi la muziki wa pop la BTS, lakini sasa siwezi kusema hivyo.”Kama mmoja wa mashambiki wakubwa Islam anapata faraja kupitia muziki wa kundi maarufu la BTS na kwa kusoma taarifa zao.“Niliingia kwenye Google nikarambaza na kusoma kuhusu maisha yao na ninaweza kulinganisha na maisha yangu kwa kiasi fulani, kwani walipitia changamoto kubwa kabla ya kuwa maarufu. Wanatoka Korea Kusini na walijisukuma sana kujifunza kuongea Kiingereza na hilo ndilo linaloniunganisha mimi na wao.”Kwa mujibu wa UNHCR Islam ni miongoni mwa Wasudan zaidi ya milioni 7 waliofurushwa makwao hadi sasa na kulazimika kuwa wakimbizi ndani ya Sudan na katika nchi jirani na vita bado inaendelea. Islam anasema kambini maisha magumu.“Hali hapa ni ngumu sana kwa wakimbizi wa ndani, ni vigumu kuielezea mtu anahitaji kuishi hapa na kuishuhudia , sijui cha kusema.”Hata hivyo Islam ana matumaini kwamba vita itakwisha hivi karibuni ili akaendelee na masomo na kutimiza ndoto yake.“Maisha yetu Khartoum yalikuwa mazuri, nahisi mambo yatakuwa bora kwangu, hivyo hakuna shida kusubiri kidogo kabla ya kurejea Khartoum “Na hilo ndilo UNHCR inalitaka kwa wakimbizo wote kutoka Sudan kama Islam.
31-1-2024 • 2 minuten, 30 seconden
30 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na inatupeleka kwa wataalam wa afya katika mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania ambao wamekuwa wakitoa elimu ya ugonjwa huo katika jamii na kuhamasisha wanawake kujitokeza katika vituo vya afya vinavyotoa huduma hiyo ili kupima afya zao ili wafahamu iwapo wameambukizwa ugonjwa huo au la. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na sauti za mashinani.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anakutana na wafadhili wakuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ili kuwafahamisha jinsi Umoja wa Mataifa unavyoshughulikia madai ya hivi karibuni dhidi ya UNRWA kuhusika katika mashambulizi ya Oktoba 7 mwaka jana Kusini mwa Israel na pia kuwasihi kuendelea kufadhili misaada ya kibinadamu ya shirika hilo. Leo ni siku ni siku ya magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa duniani. Katika ujumbe wake wa siku hii Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “Magonjwa ya kitropic yaliyopuuzwa au NTDs yanaathiri zaidi ya watu bilioni moja duniani kote hususani katika jamii masikini na zilizotengwa, lakini magonjwa ya NTDs yanazuilika na mara nyingi yanaweza kutokomezwa kabisa katika nchi.Na Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo mjini Geneva Uswisi ametoa ombi la dola milioni 500 kufadhili shughuli za ofisi hiyo kwa mwaka 2024 akionya kwamba ofisi yake inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha zinazohitajika ili kusongesha mbele haki za binadamu duniani.Mashinani tutasalia papa hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani, kusikia kauli ya Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu, ICC kuhusu Sudan. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
30-1-2024 • 11 minuten, 17 seconden
Angola: Mradi wa IFAD umeniheshimisha Kijiji kwetu- Albertina
Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD ni taasisi ya fedha ya kimataifa na pia shirika la Umoja wa Maitafa lililojikita katika kutokomeza umaskini na njaa kwenye maeneo ya vijijini yaliyoko katika nchi zinazoendelea. Miongoni mwa maeneo ambako Mfuko huo unafanya kazi ni nchini Angola barani Afrika ambako huko takwimu zinaonesha ongezeko la vijana wanaohamia mijini kutoka vijijini kwa sababu ya umaskini wa vijijini. Kwa kutambua hilo, na kwa kusaka kuchagiza ufanikishaji wa lengo namba 1 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu kutokomeza umaskini, Mfuko huo ukachukua hatua ya kuanzisha mradi wa kuepusha vijana kukimbilia mijini kwani vijijini nao kuna fursa. Ili kufahamu mradi huo ulioleta matokeo chanya, ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyofanikishwa na IFAD.
29-1-2024 • 4 minuten, 36 seconden
Mashamba darasa yaliyoandaliwa na FAO Syria yainua wanawake wafugaji
Na sasa tuelekee Mashariki ya Kati, Leah Mushi anatueleza jinsi mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo FAO na la Mpango wa chakula duniani WFP yanavyosaidia kuinua maisha ya wananchi katika nchi ya Syria.Mashariki mwa Syria katika mji wa Deir ez-Zor ulioko umbali wa km 450 kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Damascus, mashirika ya UN lile la FAO na WFP yanafanya kila juhudi kuwajengea uwezo na kubadili maisha ya wananchi kupitia miradi mbalimbali.Katika Kijiji cha Al Masrab FAO ilianzisha mafunzo ya mashamba ya wakulima, na wanakijiji wakapewa mafunzo mbalimbali ikiwemo ya ufugaji wa kondoo kwa faida.Bi. Wafaa Al Sydyan anasema mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo WFP ikampa mtaji wa zizi la kondoo. “Chanzo changu kikuu cha mapato kinatokana na ufugaji kondoo, na kipato changu kiliongezeka baada ya kupata uzoefu kutoka kwenye mafunzo mbalimbali ambayo yaliniwezesha mimi na familia yangu kumudu gharama za maisha. Nauza maziwa katika kituo cha ushindikaji cha hapa kijijini kwetu Al Masrab.”Video ya WFP inamuonesha Bi. Baraa Nadal mnufaika wa WFP akiwa na wanawake wenzake wanne katika kituo cha usindikaji maziwa, wakichemsha maziwa na kisha kuchakata mazao yatokanayo na maziwa katika mashine maalum ili kujipatia mazao mbalimbali na anasema si haba biashara inaenda vyema.“Tunauza baadhi ya mazao hapa kijijini kwetu na baadhi tunauza katika soko la Shmatieh. Tunamshukuru Mungu, mapato yetu yamekuwa bora kwa sababu ya kitengo cha usindikaji tulichowezeshwa na WFP.”Miradi hii ya WFP na FAO imepata ufadhili kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwemo Muungano wa Ulaya, Wizara ya mambo ya nje ya Norway na Idara ya maendeleo ya serikali ya Italia.
29-1-2024 • 1 minuut, 42 seconden
Nchi 5 zapokea vyeti kutoka WHO kwa kuchukua hatua kutokomeza vambato hatari kwenye vyakula
Kwa mara ya kwanza leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, limezitunukia vyeti nchi tano kwa hatua kubwa zilizopiga katika kutokomeza viambato vya mafuta katika vyakula vinavyosindikwa viwandani kwa ajili ya kuongeza ladha au Trans Fats. Flora Nducha na maelezo zaidi.Kwa nmujibu wa WHO nchi hizo tano zilizopokea vyeti leo mjini Geneva Uswisi ni Denmark, Lithuania, Poland, Saudi Arabia na Thailand na zimepongezwa kwa kuwa na será bora kwa ajili ya kutokomeza viambato hivyo vya mafuta kwa vyuakula vinavyosindikwa viwandani au iTFA na pia mfumo wa kufuatilia utekelezaji wa serra hizo.Ingawa lengo la WHO lililowekwa mwaka 2018 la kutokomeza viambato vya mafuta y kuongeza ladha katika vyakula vinavyosindikwa viwandani ifikapo mwisho wa mwaka 2023 halikutimia shirika hilo linasema kuna hatua kubwa zimepigwa kuelekea utimizaji wa lengo hilo katika kila kanda duniani.Mathalani limesema mwaka jana pekee nchi saba ziliweka na kuanza kutekeleza será za kutokomeza viambato hivyo vya mafuta ambazo ni Misri, Mexico, Moldova, Nigeria, North Macedonia, Ufilipino na Ukraine.Viambato vya mafuta katika chakula vinahusishwa na athari nyingi za kiafya zikiwa ni pamoja na ongezeko la magonjwa ya kiharusi, shinikizo la damu na vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo.Baadhi ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha viambato hivyo vya mafuta WHO inasema ni vuakula vya kukaangwa, keki na miliambayo imeshatayarishwa na kufungashwa viwandani ambavyo vina viwango vya juu vya sukati, mafuta na chumvi.Akikabidhi vyeti hivyo mkuruhenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanon Ghebreyesus amesema “ Viambato vya mafuta havina faida yoyote mwilini isipokuwa hatari kubwa. Tunafuraha kwamba kuna nchi nyingi zimeweka será za kutokomeza au kupunguza viambato vya mafuta katika chakula. Lakini kuweka será ni suala moja na kuzitekeleza ni suala lingine. Nazipongeza Denmark, Lithuania, Poland, Saudi Arabia na Thailand kwa kuingoza Dunia katika kufuatilia na kutekeleza será dhidi ya viambato vya mafuta katika chakula, tunazichagiza nchi zingine kufuata nyayo zao.”Hivi sasa shirika hilo linasema kuna jumla ya nchi 53 zimeweka será na kuanza kuzitekeleza dhidi ya viambato vya mafuta katika chakula na hivyo kuboresha lishe ya watu bilioni 3.7 sawa na asilimia 46 ya watu wote duniani ikilinganishwa na asilimia 6 tu ya watu miaka mitano iliyopita.
29-1-2024 • 2 minuten, 38 seconden
29 JANUARI 2024
Hii leo kwenye Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa Anold Kayanda anaanzia na masuala ya afya, hususan viambato vya mafuta vinavyohatarisha afya ya mwili, kisha miradi ya UN ilivyosaidia wanawake huko Syria .Makala inakupeleka Angola kuona jinsi Umoja wa Mataifa umenusuru wanawake wa vijijini kwa hohehahe na mashinani atakupeleka katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko Kaunti ya Turkana, nchini Kenya kupata ujumbe kuhusu elimu hasa kwa wasichana.Kwa mara ya kwanza leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO, limezitunukia vyeti nchi tano kwa hatua kubwa zilizopiga katika kutokomeza viambato vya mafuta katika vyakula vinavyosindikwa viwandani kwa ajili ya kuongeza Ladha au Trans Fats. Flora Nducha amefuatilia taarifa hiyo na anatujuza zaidi.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo FAO na la Mpango wa chakula duniani WFP yanasaidia kuinua maisha ya wananchi katika nchi ya Syria kwa kuwapatia miradi mbali mbali ikiwemo ya ufugaji wa kondoo. Leah Mushi anakusimulia kilichofanyikaMakala Assumpta Massoi anakupeleka Angola, kusini mwa Afrika kusikia ni vipi mradi wa Umoja wa Mataifa umeheshimisha wanawake wa vijijini akiwemo mmoja wao aitwaye Albertina.Mashinani: Igiraneza Mixella, msichana mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye amesajiliwa kusoma kwa ufadhili wa Mpesa Foundation Academy ambayo huelemisha wanafunzi mahiri na wenye vipaji lakini wasiojiweza kiuchumi, akielezea jinsi alivyo na furaha isiyo na kifani kwa kutimiza ndoto zake za kuendelea na masomo yake ya sekondari katika shule hiyo.Karibu!
29-1-2024 • 11 minuten, 44 seconden
Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ yaitaka Israeli iepushe mauaji ya kimbari Gaza
Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ hii leo imeamua kuwa Israel lazima ichukue hatua zote za kuzuia vitendo vya mauaji ya kimbari katika mashambulizi yake dhidi ya wapalestina huko, Gaza, uamuzi unaofuatia shauri lililowasilishwa na Afrika Kusini la kutaka Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa ichukue hatua za awali kwa mujibu wa Mkataba wa kimataifa wa kuepusha mauaji ya kimbari wa mwaka 1948. Hakika Leah! Kama unavyofahamu Afrika Kusini katika shauri lake iliyowasilisha tarehe 29 mwezi Desemba mwaka jana wa 2023, Afrika Kusini ilidai kuwa Israeli inakiuka wajibu wake wa kuzingatia Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia mauaji ya Kimbari kuhusiana na wapalestina huko Ukanda wa Gaza na hivyo kutaka ICJ ichukue hatua za awali kuepusha kinachoendelea. Hatua ni pamoja na Israel isitishe mara moja operesheni zake za kijeshi ndani na dhidi ya Gaza, ichukue hatua za kimsingi kuepusha mauaji ya kimbari na pia ichukue hatua zote ndani ya uwezo wake kufuta amri zinazohusiana na mashambulizi ikiwemo za kuzuia au kufukuza na kufurusha watu kutoka makazi yao, halikdhalika watu kunyimwa fursa ya kupata chakula cha kutosha na maji. Hukumu ya ICJ yenye kurasa 29 iliyosomwa na Jaji Phillipe Gautier inasema masharti yote ya kuwezesha kuchukua hatua za dharura yako wakati uamuzi wake wa mwisho ukisubiri wa kutangaza hatua za kulinda haki zinazodaiwa na Afrika Kusini. Ingawa hivyo Mahakama imesema kwa mazingira ya kesi husika, hatua zitakazochukuliwa si lazima zifanane na zile zilizoombwa na Afrika Kusini. Kwa hivyo basi Israeli inapaswa, kwa mujibu wa Mkataba wa kuzuia mauaji ya kimbari ambayo taifa hilo ni mwanachama, itumie uwezo wake wote izuie vitendo vyote kwa mujibu wa ibara ya pili ya mkataba huo ikiwemo mauaji ya kundi hilo yaani wapalestina. Israeli izuie na iadhibu mauaji yoyote ya wapalestina Ukanda wa Gaza na ichukue hatua zote kuwezesha ufikishaji wa misaada ya kibinadamu eneo hilo. Mahakama imetaka Israel iwasilishe ripoti ya utekelezaji wa uamuzi huu wa Mahakama ndani ya mwezi mmoja kuanzia tarehe ya leo ya hukumu, ripoti ambayo itawasilishwa pia kwa Afrika Kusini ili nayo iweze kutoa maoni yake kuhusu utekelezaji. Suala hili lilikuwa miongoni mwa maombi ya Afrika Kusini ya kwamba ripoti ya utekelezaji iwasilishwe. Kwa mujibu wa Mkataba ulioanzisha ICJ, uamuzi unaotolewa na Mahakama hii huwa haukatiwi rufani.
26-1-2024 • 2 minuten, 13 seconden
26 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia maamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ vitendo vya mauaji ya kimbari katika mashambulizi ya Israel dhidi ya wapalestina huko Gaza. Pia tunamulika viwanda vya nishati safi ulimwenguni, makala ikitupeleka nchini India. Mashinani tnakuletea ujumbe wa mhamiaji ambaye ni mchezaji wa musiki, mwalimu na rafiki nchini Burundi.Mahakama ya Kimataifa ya Haki, ICJ hii leo imeamua kuwa Israel lazima ichukue hatua zote za kuzuia vitendo vya mauaji ya kimbari katika mashambulizi yake dhidi ya wapalestina huko, Gaza, uamuzi unaofuatia shauri lililowasilishwa na Afrika Kusini la kutaka Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa ichukue hatua za awali kwa mujibu wa Mkataba wa kimataifa wa kuepusha mauaji ya kimbari wa mwaka 1948. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa ifuatayo. Kilimo ni moja ya shughuli za kibinadamu zinazochangia katika uchafuzi wa hewa. Kwa kulitambua hilo, FAO kote ulimwenguni inachagiza kile inachokiita kwa lugha ya kiingereza Bioeconomy yaani uchumi ambao msingi wake unatokana na matumizi ya rasilimali za kibayolojia zinazopatikana kwenye mazingira; kwa mfano kurejesha taka katika uzalishaji wa nishati safi, mbadala wa mafuta ya kisukuku. Kupitia harakati hizo, FAO inasaidia wakulima kuongeza mapato, kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi na kuchangia kupunguza taka ulimwenguni kwa kubadilisha mifumo ya zamani ya kilimo ambayo ilikuwa inachangia kuharibu mazingira.Na makala ikiwa leo ni maadhimisho ya kwanza kabisa ya siku ya kimataifa ya nishati safi nakupeleka Tanzania kuangazia juhudi zinazofanyika kuhamasisha umma kuhamia kwenye nishati safi au jadidifu kutimiza lengo namba 7 la maendeleo endelevu SDGs. Vijana wako msitari wa mbele katika harakati hizo na miongoni mwao ni Nuzulack Dausen mwanzilishi wa Jukwaa la kidijitali la Jiko point linaloendesha kipindi cha mwanaume jikoni kupitia mtandao wa Youtube. Amezungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Stella Vuzo afisa habari wa Umoja wa Mataifa na kumfafanulia wanavyochangia katika kufanikisha lengo la maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa kuhusu nishati safi . Mashinani tutaelekea katika Jiji la Bujumbura nchini Burundi kumsikia mhamiaji ambaye ni mchezaji wa musiki, mwalimu na rafiki. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
26-1-2024 • 12 minuten, 7 seconden
FAO: Kuna nishati safi na fedha katika kinachoonekana kuwa ni takataka
Kilimo ni moja ya shughuli za kibinadamu zinazochangia katika uchafuzi wa hewa. Kwa kulitambua hilo, FAO kote ulimwenguni inachagiza kile inachokiita kwa lugha ya kiingereza Bioeconomy yaani uchumi ambao msingi wake unatokana na matumizi ya rasilimali za kibayolojia zinazopatikana kwenye mazingira; kwa mfano kurejesha taka katika uzalishaji wa nishati safi, mbadala wa mafuta ya kisukuku. Kupitia harakati hizo, FAO inasaidia wakulima kuongeza mapato, kupunguza uzalishaji wa hewa chafuzi na kuchangia kupunguza taka ulimwenguni kwa kubadilisha mifumo ya zamani ya kilimo ambayo ilikuwa inachangia kuharibu mazingira. FAO iliwatembelea wakulima wa mpunga katika eneo moja nchini India. Kama walivyo wakulima wengine katika maeneo mengine duniani, hawa nao walikuwa wanachoma moto mabaki ya mimea baada ya mavuno ili kuandaa shamba kwa ajili ya msimu mwingine. Njia hiyo isiyofaa ilimaanisha kuwa wakulima hawakufaidika na mabaki ya mimea ya mpunga lakini sasa wakulima na kampuni za biashara wanavuna pia kutoka katika mabaki hayo kwa kuzalisha nishati mbadala ya mafuta ya kuendeshea mitambo na pia vumbi la mabaki linatumika kutengeneza nishati, mbadala wa mkaa wa miti.Profesa Ramesh Chand ambaye ni mmoja wa jopo la fikra la Serikali ya India linalohusika na sera za umma za kuchochea maendeleo ya kiuchumi, anasema, “kwa kuchoma moto tu mabaki ya mazao bila kuyatafutia shughuli mbadala sio tu unaharibu mazingira na afya bali pia kwa namna fulani unachoma moto utajiri.”
26-1-2024 • 1 minuut, 42 seconden
Nuzulack Dausen: Nishati safi inanusuru mazingira na kuinua kipato katika jamii
Leo ni siku ya kimataifa ya nishati safi ambayo lengo lake ni kuzihimiza jamii kote duniani kutekeleza lengo la 7 la maendeleo la Umoja wa Mataifa la kuhakikisha kila mtu anahamia kwenye matumizi ya nishati hiyo ifikapo mwaka 2030. Nchini Tanzania wako msitari wa mbele katika harakati za utekelezaji wa lengo hilo na miongoni mwao ni Nuzulack Dausen mwanzilishi wa Jukwaa la kidijitali la Jiko point linaloendesha kipindi cha mwanaume jikoni kupitia mtandao wa Youtube. Amezungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Stella Vuzo afisa habari wa Umoja wa Mataifa na kumfafanulia wanavyochangia katika kufanikisha lengo la maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa kuhusu nishati safi.
26-1-2024 • 5 minuten, 1 seconde
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno “KUWEKUA.”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KUWEKUA.”
25-1-2024 • 1 minuut, 8 seconden
25 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika hali ya kibinadamu na ya kiafya katika ukanda wa Gaza. Pia tunakuletea habari kwa ufupi tukisalia huko huko Gaza, machafuko nchini Sudan na ya siku ya kimataifa ya wanawake katika ushirikiano wa kimataifa. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakuletea ufafanuzi wa neno “KUWEKUA”.Mashambulizi makubwa dhidi ya majengo Gaza ambayo raia wenye hofu wanakimbilia kupata hifadhi ni "ya kuchukiza na lazima yakome mara moja", amesisitiza Thomas White naibu mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo linalokaliwa la Gaza baada ya leo, kombora kuanguka katika kituo cha mafunzo cha Umoja wa Mataifa.. Sudan inakaribia kuwa moja ya janga baya zaidi la elimu duniani ameonya mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini humo Mandeep O’Brien. Katika mahojiano maalum na UN News kwa njia ya mtandao Bi. O’Brien amesema Sudan inakabiliwa na janga la kibinadamu lisiloelezeka na ni jinamizi kwa watoto kwani watoto "Milioni 14 wanahitaji haraka msaada wa kuokoa maisha wa afya, lishe, elimu, maji na ulinzi. Pili, tunapozungumza, tunajua kwamba zaidi ya watoto milioni 3.5 wamelazimika kukimbia makazi yao tangu vita hii ianze na hii inaifanya Sudan kuwa taifa lenye idadi kubwa zaidi ya watoto waliokimbia makazi yao duniani”. Sudan ina watoto milioni 19 wenye umri wa kwenda shule ambao sasa hawasomi.Na leo ni siku ya kimataifa ya wanawake katika ushirikiano wa kimataifa. Mwaka huu 2024 inaadhimishwa chini ya kaulimbiu “Usawa wa kijinsia katika kutatua dharura ya mabadiliko ya tabianchi.” Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO ambalo linasimamia siku hii, limesema lengo lake ni kutambua wanawake viongozi katika mfumo wa kushirikiano wa kimataifa ili kuchagiza mazungumzo kuhusu suluhu za kimataifa dhidi ya ubaguzi wa kijinsia ambao unakwamisha hatua dhidi ya dharura ya mabadiliko ya tabianchi. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KUWEKUA”. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
25-1-2024 • 13 minuten, 10 seconden
Wakazi wa Ituri, DRC, wazungumzia usaidizi wa MONUSCO kwenye eneo lao
Katika jimbo la Ituri, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, watu waliokimbia makazi yao wanaishi katika takribani kambi 38, ambapo miongoni mwao ni Drodro, Roe, Lodha, Jaiba na Gina. Zaidi ya wakimbizi Laki Nne (400,000) wanafaidika na ulinzi wa moja kwa moja wa ujumbe wa walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO. Walinda amani hao wakiwemo wale wa kutoka Nepal hulinda kambi za watu waliohamishwa kwa kufanya doria za usiku na mchana. Na zaidi ya yote MONUSCO imeweka miundombinu ya kuhakikishia raia usalama wao, moja ya majukumu ya ujumbe huo ambao kwa sasa unaanza kufunga virago taratibu kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia ombi la serikali ya DRC. Katika makla hii mwandishi wetu wa habari mashariki mwa DRC George Musubao alifuatilia mtazamo wa wananchi kuhusu usaidizi wa MONUSCO.
24-1-2024 • 4 minuten, 24 seconden
Siku ya Elimu Duliani 2024 yatumika kukabiliana na kauli za chuki
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeyatumia maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Elimu kuangazia jukumu muhimu la elimu na walimu katika kukabiliana na kauli za chuki, jambo ambalo limekithiri katika miaka ya hivi karibuni kutokana na matumizi ya mitandao ya kijamii na hivyo kuharibu muundo wa jamii kote duniani. UNESCO ambalo ndilo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika moja kwa moja na jukumu la kuratibu maadhimisho ya siku hii ya kimataifa ya elimu inayodhimishwa kila mwaka tarehe 24 Januari, linasema ulimwengu unashuhudia ongezeko la migogoro inayoambatana na ongezeko la kutisha la ubaguzi, ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni, na kauli za chuki. Na kwa kuwa madhara yanavuka mipaka yoyote ya kijiografia, jinsia, rangi, dini, siasa, nje ya mtandao na mtandaoni elimu ni msingi wa kufanikisha kupambana na hali hiyo.Audrey Azoulay ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO kupitia ujumbe wake mahususi kwa siku hii akifafanua kauli mbiu ya mwaka huu ambayo ni ‘Elimu kwa ajili ya amani ya kudumu’ amesema, “kwa sababu kama chuki inaanza kwa maneno, basi amani inaanza na elimu. Tunachojifunza hubadilisha jinsi tunavyouona ulimwengu na huathiri jinsi tunavyowatendea wengine. Kwa hivyo elimu lazima iwe kiini cha juhudi zetu za kufikia na kudumisha amani ya ulimwengu.” Anasisitiza kwamba, katika siku hii, kujitolea kwako kutetea haki ya elimu bora ambayo inatambua haki za binadamu za kila mtu inamaanisha kujitolea kwa mustakabali wa amani kwa wote, ambapo kila mtu anaweza kuishi maisha ya utu, kwa kuelewana na heshima.Ili mawazo haya yawafikie watu wengi zaidi ulimwenguni, UNESCO hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani imewakutanisha wadau wa elimu kutoka kote ulimwenguni ili kujadili mchango muhimu wa elimu katika kufikia amani endelevu duniani. Pia imefanya mafunzo ya mtandaoni ya siku moja kwa maelfu ya walimu kutoka kote ulimwenguni kuhusu utatuzi wa kauli za chuki, ambayo yamewapa zana za kutambua vyema, kukabiliana na kuzuia matukio ya kauli za chuki. Mafunzo haya ni sehemu ya hatua ya UNESCO kusaidia Nchi Wanachama na wataalamu wake wa elimu kushughulikia kauli za chuki kupitia elimu.
24-1-2024 • 2 minuten, 10 seconden
24 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya elimu duniani mada kuu ikiwa ni elimu na mchango wake wa kuleta amani ulimwenguni. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeyatumia maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Elimu kuangazia jukumu muhimu la elimu na walimu katika kukabiliana na kauli za chuki, jambo ambalo limekithiri katika miaka ya hivi karibuni kutokana na matumizi ya mitandao ya kijamii na hivyo kuharibu muundo wa jamii kote duniani. Nchini Uganda katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali wilaya ya Kikuube magharibi mwa taifa hilo, suala la mchango wa elimu kwenye amani liko dhahiri kwani tulipotembelea katika makazi hayo, Yahya Kato ambaye ni Mwalimu Mkuu katika Shule ya msingi Kasonga kwenye makazi hayo ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Sudan aliteueleza kile wanachofanya.Makala inatupeleka huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususan jimboni Ituri mashariki mwa nchi hiyo ambako wakazi wanazungumzia mchango wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wakati huu ambapo ujumbe huo umeanza kufungasha virago. Mashinani tutaelekea katika kaunti ya Garissa nchini Kenya ambapo mvua kubwa inayohusiana na El Niño, imesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao, kuharibu miundombinu na kusababisha kipindupindu na magonjwa mengine yatokanayo na maji yasiyo safi na salama, Mohammed Saidi, Chifu wa kambi ya waislamu waliopoteza makazi yao katika kaunti ya Garissa anasimulia kinachojiri. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
24-1-2024 • 9 minuten, 57 seconden
Uganda: Makazi ya wakimbizi yatumia elimu kusongesha amani miongoni mwa wakimbizi
Nchini Uganda katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali wilaya ya Kikuube magharibi mwa taifa hilo, suala la mchango wa elimu kwenye amani liko dhahiri kwani tulipotembelea katika makazi hayo, Yahya Kato ambaye ni Mwalimu Mkuu katika Shule ya msingi Kasonga kwenye makazi hayo ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Sudan aliteueleza kile wanachofanya.
24-1-2024 • 1 minuut, 15 seconden
23 JANUARI 2024
Hii leo jaridani mada kwa kina, ambapo katika mchakato wa kuleta mabadiliko kwa kuwezesha wanaojifunza kupata ufahamu muhimu, maadili, mienendo, stadi na tabia na hivyo wawe wachagizaji wa amani kwenye jamii zao, tnakupeleka katika makazi ya wakimbizi nchini Uganda kuona ni kwa vipi mchakato huo unafanyika. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya kwamba watu 570,000 wanakabiliwa na janga kubwa la njaa kutokana na kuendelea kwa mapigano makali, wahudumu wa misaada kunyimwa fursa ya kuwafikia wenye uhitaji na kukatwa kwa mawasiliano, sababu ambazo pia zimeathiri uwezo wa shirika hilo kufikisha na kusambaza msaada kwa usalama kwa maelfu ya watu. Hivyo limetoa wito wa kuongezwa haraka fursa za usambazaji na ufikishaji wa misaada ya kibinadamu. Kwingineko wito wa kuchukuliwa hatua za haraka kushughulikia ongezeko kubwa la vifo vya wakimbizi wa Rohingya baharini umetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Kwa mujibu wa shirika hilo wakimbizi wa Rohngya 569 walipoteza maisha au kupotea walipotumia safari hatari za boti katika bahari ya Andaman na Ghuba ya Bengal mwaka 2023, hiyo ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya waliopoteza Maisha tangu mwaka 2014.Na huko Ukraine Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu wa nchi hiyo Denise Brown amelaani vikali wimbi jipya la mashambulizi ya anga ya Urusi dhidi ya miji iliyo na watu wengi nchini Ukraine. Mashinani tutaelekea katika ukanda wa Gaza kusikia ujumbe kuhusu harakati za chanjo kwa watoto ambao tayari wamekumbwa na changamoto ya vita. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
23-1-2024 • 12 minuten, 37 seconden
Hata mimi mwenyewe nilikuwa sijiamini hadi nilipopata mafunzo ya RLabs - Mariam
Mkakati wa Afya ya Uzazi kwa Wasichana, Haki, na Uwezeshaji nchini Tanzania (GRREAT) unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wadau likiwemo shirika lisilo la kiserikali la RLabs Tanzania na serikali ya Canada ni mpango wa miaka mitano (2019-2024) ili kuisaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuboresha ustawi wa wasichana balehe katika mikoa ya Mbeya na Songwe, pamoja na Zanzibar. Kupitia mpango huu wasichana wamepata zana na ujuzi wanaohitaji ili kuboresha maisha yao, familia na jamii zao. Mmoja wao ni Mariam wa Nyanda za juu kusini mwa Tanzania.
22-1-2024 • 3 minuten, 14 seconden
UN: Raia 25, 000 wamepoteza maisha katika vita Gaza na mahitaji ya kibinadamu yanazidi kuongezeka
Mashambulizi makubwa ya mabomu yanayofanywa na Israel Gaza yameendelea tena leo sanjari na maroketi yanayovurumushwa na makundi yenye silaha ya Kipalestina kuelekea Israel, wakati wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wakiripoti kuuawa kwa watu zaidi ya 25,000 Gaza tangu kuanza kwa machafuko hayo mapya Oktoba 7 mwaka jana na mahitaji ya kibinadamu yakiongezeka kila uchao. Hali inazidi kubwa mbaya na hakuna dalili ya kukomesha uhasama Gaza limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA. Likinukuu takwimu za wizara ya afya ya Gaza mbali ya watu waliopoteza maisha Wapalestina zaidi ya elfu 62 wamejeruhiwa, wakati serikali ya Israel kwa upande wake ikisema tangu mwishoni mwa wiki askari wake wawili wameuawa na kufanya jumla ya askari wa Israel waliopoteza Maisha tangu kuanza kwa operesheni ya vita vya ardhini kufikia 193 na majeruhi zaidi ya 1200.Leo mawaziri wa mambo ya nje wa Israel na Palestina wanajiandaa kukutana na wenzao wa Ulaya kwenye mazungumzo ya faragha mjini Brussels Ubeligiji, na hatua hii imekuja baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa G-77 na China uliofanyika Kampala Uganda kulaani vikali umwagaji damu unaoendelea Gaza akisema ni unasikitisha na haukubaliki akisisitiza kufanyika kila linalowezekana kuzuia mgogoro huo kusambaa zaidi kikanda.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mahitaji ya kibinadamu ni makubwa sana na yanaongezeka kila siku, hivi sasa ni maduka 15 pekee ya kuoka mikate ndio yanayofanya kazi sita Rafah na tisa Deir al Balah na hakuna hata moja Kaskazini mwa Wadi Gaza.Nalo shirika la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema kuendelea kutokuwepo kwa mawasiliano kwa siku ya saba sasa kunavuruga usambazaji wa misaada na watu kupata huduma muhimu zikiwemo za matibabu hasa ukizingatia kwamba watu milioni 1.7 wametawanywa na miongoni mwa raia waliouawa 335 walikuwa katika makazi ya UNRWA na wafanyakazi wa shirika hilo waliopoteza Maisha hadi sasa ni 151.
22-1-2024 • 2 minuten, 22 seconden
22 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mradi wa ufugaji nyuki nchini Zimbabwe. Makala tunamuika mkakati wa Afya ya Uzazi kwa Wasichana, Haki, na Uwezeshaji nchini Tanzania na mashinani tunasalia na mada ya elimu bora na tunakupeleka nchini Uganda.Mashambulizi makubwa ya mabomu yanayofanywa na Israel dhidi ya Gaza yameendelea tena leo sanjari na maroketi yanayovurumushwa na makundi yaliyojihami ya kipalestina kuelekea Israel, wakati wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wakiripoti kuuawa kwa watu zaidi ya 25,000 huko Gaza tangu kuanza kwa machafuko hayo mapya Oktoba 7 mwaka jana na mahitaji ya kibinadamu yakiongezeka kila uchao. Nchini Zimbabwe, mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, wa kusongesha ajira rafiki kwa mazingira umeanzisha mashamba darasa ya ufugaji wa nyuki na hivyo kuandaa vijana kuwa wakulima wajasiriamali vijijini. Mradi huo unatekelezwa kwa ubia na shirika la Korea Kusini la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, KOICA.Makala inatupeleka nchini Tanzania kuangazia Mkakati wa Afya ya Uzazi kwa Wasichana, Haki, na Uwezeshaji nchini Tanzania (GRREAT) unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na wadau likiwemo shirika lisilo la kiserikali la RLabs Tanzania na serikali ya Canada. Kupitia mpango huu wasichana wamepata zana na ujuzi wanaohitaji ili kuboresha maisha yao, familia na jamii zao. Mmoja wao ni Mariam wa Nyanda za juu kusini mwa Tanzania. Mashinani tunakupeleka makazi ya wakimbizi ya Kyangwali magharibi mwa Uganda kupata ujumbe wa uhusiano wa elimu na amani. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
22-1-2024 • 10 minuten, 18 seconden
Ufugaji nyuki ‘waua’ ndege zaidi ya mmoja, yasema FAO - Zimbabwe
Nchini Zimbabwe, mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, wa kusongesha ajira rafiki kwa mazingira umeanzisha mashamba darasa ya ufugaji wa nyuki na hivyo kuandaa vijana kuwa wakulima wajasiriamali vijijini. Mradi huo unatekelezwa kwa ubia na shirika la Korea Kusini la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, KOICA. Pasi shaka Assumpta, naanza na Angelina Manhanzva, kijana wa kike akiwa shambani akihudumia mzinga wa nyuki anatanabaisha kuwa…(Nats) fursa inapokufikia usiipuuze kwani inaweza kubadili maisha yako katika fumba na kufumbua. Mjasiriamali kijana huyu kutoka wilaya ya Chegutu jimboni Mashonaland kaskazini-kati mwa Zimbabwe anakiri kuwa baada ya kushiriki kwenye ufugaji wa nyuki kwa miezi kadha wameshuhudia maisha yao yakibadilika. Barnabas Mawire, mtaalamu wa maliasili wa FAO nchini Zimbabwe anasema, “Wazo ni kwamba, eneo moja lenye mizinga ya nyuki linaweza kugeuzwa kuwa shamba darasa ambako vijana kutoka wilaya au kata tofauti wanaweza kuja kujifunza kama waendavvyo shuleni .” FAO inasema kuwa kupatia vijana wa vijijini ajira zisizoharibu au kuchafua mazingira kunaweza kukabili madhara ya mabadiliko ya tabianchi, kuondoa umaskini na kutokomeza umaskini wa vijijini. Mkulima mjasiriamali kijana Evelyne Mutuda naye anakiri faida inapatikana na kwamba, "Tunatarajia kuongeza mizinga mingine ya nyuki kwa kutumia faida ya fedha tuliyopata baada ya kuuza asali. Na pia tutapanda mijakaranda .” Akitamatisha afisa wa FAO, Bwana Mawire anadhihirisha uhusiano wa ufugaji nyuki na ulinzi wa bayonuai. “Nyuki wanafaa sana kwa ajira zisizoharibu mazingira kwa mantiki kwamba wanahitaji aina mbali mbali za mimea . Kwa hiyo nyuki wanasongesha uhifadhi wa bayonuai. Unapotunza miti, unatunza tabianchi yetu, chakula chetu na uhai wetu. Hivyo ufugaji nyuki unanufaisha kwa juhudi kidogo.”
22-1-2024 • 2 minuten, 12 seconden
EmpowerU Cash+; yabadilisha maisha katika Wilaya ya Lamwo nchini Uganda
Kutokana na ushirikiano kati ya serikali ya Uganda na ya Uholanzi, Mradi wa Maendeleo wa Kukabiliana na Athari za Ufurushwaji (DRDIP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kutumia mfumo wa fedha taslimu wa EmpowerU Cash+.limewasaidia walengwa waliochaguliwa katika Wilaya ya Lamwo ambapo mpango uliwalenga wakimbizi na jamii zilizowapokea. Mpango huo wa EmpowerU Cash+ ulikuwa unalenga idadi ya juu ya watoto kufikia wanne kwa kila kaya na kila mtoto kila mwezi alipewa Shilingi 45,000 za Uganda sawa na takribani dola 11 za kimarekani hiyo ikimaainisha kila kaya ilipata jumla ya Shilingi za Uganda 180,000 sawa na takribani dola 47 za kimarekani kwa mwezi. Huduma hiyo ilikuwa kwa muda wa miezi sita katika wilaya za Lamwo, Adjumani, Yumbe, na Obongi lakini hapa ninaangazia wilaya moja tu, Lamwo.
19-1-2024 • 4 minuten, 45 seconden
19 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia vita katika ukanda wa Gaza, na tukielekea siku ya elimu duniani tunabisha hodi nchini Burundi ambako UNICEF inahakikisha watoto wakimbizi wanaorejea nchini humo wanaweza kuendelea na elimu. Makala na mashinani tunasalia na mada ya elimu bora na tunakupeleka nchini Uganda, kulikoni?.Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameeielezea hali inayoendelea Gaza siku 105 baada ya kuzuka vita mpya baina ya wapiganaji wa Hamas na vikosi vya Israel, kuwa ni zahma juu ya zahma. Watu zaidi ya milioni 1.7 wametawanywa huku hofu ya milipuko ya magonjwa, janga la njaa na vifo zaidi likitawala. Nchini Burundi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kuhakikisha watoto wakimbizi wanaorejea nchini humo wanaweza kuendelea na elimu bila uoga na jakamoyo hasa pale wanapokumbana na vizuizi vya tofauti ya lugha waliyotumia ukimbizini na ile inayotumika nyumbani walikorejea.Makala inatupeleka kaskazini mwa Uganda katika wilaya ya Lamwo ambako Kutokana na ushirikiano kati ya serikali ya Uganda na ya Uholanzi, Mradi wa Maendeleo wa Kukabiliana na Athari za Ufurushwaji (DRDIP), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kutumia mpango wa fedha taslimu wa EmpowerU Cash+ limewasaidia wananchi kuboresha hali yao ya maisha. Mashinani Mashinani ttunasalia huko huko Uganda katika makazi ya wakimbizi ya Kyangwali magharibi mwa Uganda kupata ujumbe wa uhusiano wa elimu. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
19-1-2024 • 12 minuten, 24 seconden
Methali: "Aliye na hamu ya kupanda juu hukesha"
Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Aliye na hamu ya kupanda juu hukesha.”
19-1-2024 • 1 minuut, 11 seconden
Nchini Burundi mbinu ya mashangazi na baba wa shuleni yaepusha watoto na kejeli kutoka kwa wenzao
Nchini Burundi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limechukua hatua kuhakikisha watoto wakimbizi wanaorejea nchini humo wanaweza kuendelea na elimu bila uoga na jakamoyo hasa pale wanapokumbana na vizuizi vya tofauti ya lugha waliyotumia ukimbizini na ile inayotumika nyumbani walikorejea. Hebu fikiria baada ya machungu ya ukimbizini, unarejea nyumbani nako shuleni unakumbwa na kejeli kisa tu matamshi ya lugha utumiayo ni tofauti na yale ya wenzako darasani. Pelouse Nibitanga huyu, ambaye amerejea Burundi kutokea Rwanda ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Kamena iliyoko mkoa wa Kirundo kaskazini mwa Burundi barani Afrika anathibitisha. Anasema niliporejea hapa kutangamana hakukuwa rahisi. Kwani wanafunzi wengine walinicheka na kunikejeli kwa matamshi yake ya lugha darasani. Katika mazingira hayo kufaulu ilikuwa ni changamoto. Kupitia mradi wa kuweko kwa mashangazi na wababa wa shuleni, wanafunzi kama Pelouse na wale waliokuweko walipatiwa msaada sio tu wa kielimu bali pia kisaikolojia wa kuwawezesha kuishi na kusoma kwa utangamano. Mwalimu Sandrine Kamutako ni miongoni mwa washauri nasaha na mashangazi wa shuleni. “Usaidizi wa kisaikolojia na kijamii unaongeza zaidi imani ya mtoto kwa mwalimu na mnasihi wake. Mbinu hii ni nzuri kwani inasaidia wanafunzi kuwa na tabia nzuri. Na pia hujenga kuaminiana kati ya mwalimu na mwanafunzi.” Pelouse anathibitisha hilo akisema “shukrani sana kwa ushauri nasaha kwani nilianza kufuatilia masomo vizuri sana na nilimaliza darasa la 6 na sasa nimejiunga na darasa la 7. Sina tena aibu na ninafurahia masomo na wanafunzi wengine. Utangamano wangu unastawi vizuri. Inafurahisha mno.” Mafunzo hayo ya kuleta utangamano yamekuwa na manufaa kwa wanafunzi zaidi ya 18, wakiwemo zaidi ya 7,000 waliorejea Burundi kutoka ukimbizini. Shule nufaika na mafunzo hayo pia zimenufaika na miradi mingine kama ya ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua, madarasa na mafunzo kwa walimu zaidi ya 1,500, UNICEF Burundi ikisema yote yamewezekana kufuatia ufadhili kutoka Muungano wa Ulaya, EU.
19-1-2024 • 2 minuten, 21 seconden
Hali katika ukanda wa Gaza ni zahma juu ya zahma: Mashirika ya UN
Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameeielezea hali inayoendelea Gaza siku 105 baada ya kuzuka vita mpya baina ya wapiganaji wa Hamas na vikosi vya Israel, kuwa ni zahma juu ya zahma. Watu zaidi ya milioni 1.7 wametawanywa huku hofu ya milipuko ya magonjwa, janga la njaa na vifo zaidi likitawala. Asante Anold, nikianza na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO linaonya juu ya mlipuko wa magonjwa ya kuambukiza Gaza watu zaidi ya milioni 1.7 waliotawanywa hivi sasa wanaishi katika makazi ya dharura yaliyofurika pomoni na kwa wastani watu 500 wanatumia choo kimoja huku watu zaidi ya 2000 wakitumia bafu moja kuoga na wakati mwingine kwenye baadhi ya makazi ya dharura hakuna choo kabisa.Hivyo shirika hilo linasema ukosefu wa vyoo na huduma za usafi vimewalazimisha watu kujisaidia haja kubwa kwenye maeneo ya wazi na kuongeza hatari kubwa ya kusambaa kwa magonjwa ya kuambukiza. Tangu katikati ya kwezi Oktoba mwaka jana WHO inasema kumekuwa na makali ya wagonjwa wa kuhara, matatizo ya njia ya mfumo wa hewa, chawa, upele, tetekuanga, homa ya manjano na hata homa ya ini aina ya E.Osisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR inasema ukiukwaji mkubwa wa haki unaendelea katika ukanda huo mkuu wa ofisi ya haki za binadamu kwenye eneo linalokaliwa la Gaza Ajith Sunghay mbaye yuko Gaza tangu Jumatatu anasema “Nimewaona wanaume na watoto wakifukua vifusi kupata matofali ya kujengea mahema ya mifuko ya plastiki, huli ni janga kubwa la haki za binadamu na janga kubwa lililosababishwa na binadamu. Gaza inahitaji ongezeko la misaada ya kibinadamu ikiwemo ulinzi.”Kwa upande wake shirika la kuhudumia watoto UNICEF linaangazia watoto wanaozaliwa wakati vita hii ikiendelea, ikiwa ni sikua ya 105 leo shirika hilo linasema karibu watoto 20,000 wamezaliwa katika hali ya jehanamu ikimaanisha mtoto 1 amezaliwa kila baada ya dakika 10 likionya kwamba wengi huenda wakafariki dunia kutokana na vita na hali mbayá ya Maisha na huduma Gaza.Nahitimisha na Shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA ambalo linasema leo ni siku ya tano mfululizo huduma za mawasiliano zimekatwa Gaza na hali hii inazuia maelfu ya watu kupata tarifa za kuokoa maisha, kukosa fursa ya kuwapigia wahudumu wa afya kupata msaada na inaendelea kuathiri usambasaji wa msaada wa kibinadamu unaohitajika sana.Hadi kufikia sasa kwa mujibu wa takwimu za wizara ya afya ya Gaza takriban watu 25,000 wameuawa tangu Oktoba 7 mwaka jana.
19-1-2024 • 2 minuten
18 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Imesalia miaka 6 kufikia ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015. Dkt. Venance Shillingi Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe nchini Tanzania aliwasilisha pendekezo la utafiti wake utakaoweza kuwa moja ya majawabu ya changamoto barani Afrika. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na uchambuzi wa methali.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamerejea kupaza sauti kuhusu misaada muhimu ya kibinadamu kuendelea kuruhusiwa kuingia Gaza, lile la kuratibu Misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA likisema kwa mara ya kwanza dawa kwa ajili ya mateka wa Israel zimeripotiwa kuruhusiwa kuingia leo sanjari na msaada kwa ajili ya Wapalestina kwa makubaliano maalum yaliyowezeshwa na serikali za Qatar na Ufaransa. Kwingineko ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kutafuta ukweli nchini Sudan umeanza kazi yake kwa ujumbe wa awali kuwasili mjini Geneva wiki hii, ukizitaka pande zinazozozana Sudan kumaliza vita, kutekeleza wajibu wao wa kulinda raia na kuhakikisha kwamba wahusika wa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na uhalifu wanawajibishwa.Na barani Ulaya ambako ripoti mpya iliyochapishwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF inasema takriban watoto nusu milioni kote barani Ulaya na Asia ya Kati wanaishi katika vituo vya makazi ya kulelea watoto pamoja na katika taasisi kubwa. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Aliye na hamu ya kupanda juu hukesha.”. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
18-1-2024 • 11 minuten, 50 seconden
Mbinu 3 za kuhakikisha watoto wanapata chanjo
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto ulimwenguni UNICEF linatumia njia mbalimbali kuhakikisha watoto na familia zao wanapata chanjo stahili hili kuwaepusha kuugua magonjwa ambayo mengine yanaweza kuzuilika kwa kupata chango. Katika Makala hii Leah Mushi anatujuza mbinu tatu zinazotumiwa na UNICEF kuhakikisha jamii inapata chanjo.
17-1-2024 • 3 minuten, 8 seconden
Guterres: Vita, mabadiliko ya tabianchi na AI ni changamoto tunazopaswa kuzishughulikia haraka
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amehutubia jukwaa la uchumi duniani mjini Davos Uswis akigusia changamoto mbalimbali zinazpoikabili dunia hivi sasa kuanzia vita inayoendelea Gaza na kwingineko, hali ya kutochukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na maendeleo ya akili mnemba au AI. Asante Evarist katika hotuba yake Bwana Guterres alianza kwa kuelezea wasiwasi kuhusu changamoto ya tabianchi na ongezeko la joto duniani akisema nchi zimekumbwa na tabia ya kutochukua hatua na ubinafsi katia masuala ya maendeleo na matumizi ya mafuta kisikuku yameifanya dunia kushindwa kushikamana kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na hivyo kuchochea ongezeko la joto duniani “ Nchi zinaendelea kuzalisha hewa chafuzi, sayari yetu inazidi kuchemka kuelekea nyuzi joto 3celisius, ukame, vimbunga, moto wa nyika na mafuriko winaathiri nchi na jamii.”Hotuba hiyo pia imegusa kwa kirefu hofu ya ukiukwaji wa sheria za kimataifa na majanga ya kibinadamu hususan katika mizozo inayoendelea kama vile Gaza na Ukraine akisema kuanzia uvamizi wa Urusi Ukraine hadi Sudan na hivi karibuni kabisa Gaza, pande husika katika mizozo hiyo zinapuuza sheria za kimataifa, zinakiuka mikataba ya Geneva na hata kukiuka katiba ya Umoja wa Mataifa.“Dunia imesismama ikiangangalia raia hususani wanawake na watoto wakiuawa, kulemazwa, kushambuliwa kwa mabonmu, kufurushwa makwao na kunyimwa haki ya misaada ya kibinadamu.”Kwa Gaza mathalani amerejea wito wa usitishwaji mapigano mara moja na kuwa na mchakato ambao utaelekea kuleta amani ya kudmu kwa Israel na Palestina kwa misingi ya kuwa na mataifa mawili akisistiza kwamba “Hii ndio njia pekee ya kukata shina la madhila na kuzuia mzozo huo kusambaa hali ambayo itawasha moto katika ukanda mzima.”Na kuhusu suala la Akili mnemba Katibu Mkuu amezungumzia hatari yake na uwezekano wa kuongeza pengo la usawa na tabia isiyofaa ya makampuni makubwa ya teknolojia "Teknolojia hii ina uwezo mkubwa wa maendeleo endelevu lakini kama Shirika la Fedha Duniani lilivyotuonya hivi karibuni, kuna uwezekano mkubwa wa kuzidisha ukosefu wa usawa duniani. Na baadhi ya makampuni yenye nguvu ya teknolojia tayari yanafuata faida kwa kutozingatia haki za binadamu, faragha kibinafsi na athari za kijamii,"Amehitimisha hotuba yake kwa kwa kusisitiza hali muhimu na inayowezekana ya kujenga upya imani kwa ajili ya dunia iliyo salama na imara zaidi.
17-1-2024 • 2 minuten, 37 seconden
17 JANUARI 2024
Jaridani leo tunamulika jukwaa la uchumi duniani mjini Davos Uswis, na suala la kilimo endelevu. Makala tnakuletea mbinu tatu zinazotumika kuhakikisha watoto na familia zao wanapata chanjo na mashinani tutabisha hodi mkoani Mbeya nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu ujuzi unaohitajika ili kufundisha wanafunzi kwa ufanisi.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amehutubia jukwaa la uchumi duniani mjini Davos Uswis akigusia changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia hivi sasa kuanzia vita inayoendelea Gaza na kwingineko, hali ya kutochukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na maendeleo ya akili mnemba au AI. Kilimo kinaweza kuchukua jukumu kuu katika hatua dhidi ya tabianchi wakati huo huo kikihakikisha uhakika wa chakula duniani, ni maoni ya Mkurugenzi wa Ofisi ya Mabadiliko ya Tabianchi, Bayonuai na Mazingira katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Kaveh Zahedi kufuatia hivi majuzi mwaka 2023 kuthibitishwa kuwa mwaka wa joto zaidi katika rekodi za dunia.Makala hii leo Leah Mushi kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF anatujuza mbinu tatu zinazotumika kuhakikisha watoto na familia zao wanapata chanjo. Na katika mashinani Mwalimu Upendo Mwakapala kutoka Shule ya Msingi ya Uhuru iliyoko mkoani Mbeya Tanzania anatujuza mbinu bunifu za kufundisha ili kusaidia kuboresha elimu kwa watoto kupitia Mpango wa Mafunzo ya Ualimu wa Shule za Msingi unaofanikishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF na wadau wake. Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!
17-1-2024 • 10 minuten, 14 seconden
Kaveh Zahedi wa FAO: Hatuwezi kuwa tu watazamaji wa mabadiliko ya tabianchi, kilimo kina jukumu
Kilimo kinaweza kuchukua jukumu kuu katika hatua dhidi ya tabianchi wakati huo huo kikihakikisha uhakika wa chakula duniani, ni maoni ya Mkurugenzi wa Ofisi ya Mabadiliko ya Tabianchi, Bayonuai na Mazingira katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Kaveh Zahedi kufuatia hivi majuzi mwaka 2023 kuthibitishwa kuwa mwaka wa joto zaidi katika rekodi za dunia. “Kwa hivyo, rekodi hizi ni muhimu. Sasa tunahitajika kuchukua hatua sasa. Hatuwezi tu kuwa aina ya watazamaji tu wa mabadiliko ya tabianchi, na kilimo kina jukumu kuu la kutekeleza". Bwana Zahedi anaongeza kusema kwamba kilimo endelevu kinaweza kuchangia katika kufikia uzalishaji sifuri wa hewa chafuzi.“Mashamba hayapaswi tu kuwa wazalishaji wa chakula. Yanaweza kuwa vyanzo vya nishati mbadala. Nishati inaweza kutumika katika shamashamba ya ndani, kwa ajili ya kusukuma maji, kwa ajili ya umwagiliaji, au nishati ambayo inaweza kugawanywa katika gridi ya taifa, au taka za kilimo kugeuzwa kuwa nishati au nishati ya mimea. Hizi zote ni suluhisho za kilimo bora kwa nishati, na hiyo ndiyo aina ya kazi ambayo sisi FAO tumekuwa tukifanya na nchi."
17-1-2024 • 1 minuut, 18 seconden
16 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika uhakika wa chakula, ambapo FAO imekuwa msitari wa mbele kwa miradi mbali mbali ya kuwasaidia wakulima na wafugaji kwenye mizozo ili kuhakikisha wanapunguza mzigo wa kuwa tegemezi wa msaada wa chakula. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo mauaji wa mlinda amani nchini CAR na sauti za jamii mashinani kama zifuatazo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani mauaji ya jana Januari 15 ambapo aliuawa mlinda amani mmoja wa kutoka Cameroon aliyekuwa anahudumu katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) na kujeruhiwa kwa watu wengine watano, wawili kati yao wakiwa wamejeruhiwa mno kutokana na mlipuko huko Mbindali, katika Mkoa wa Ouham-Pendé, kaskazini-magharibi mwa Paoua. Huku visa vya kipindupindu vikizidi kuongezeka katika maeneo ya Kusini mwa Afrika, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) linataka kuzingatiwa zaidi kwa watoto katika kukabiliana na kipindupindu. Janga la kipindupindu ambalo liliathiri nchi nyingi za Mashariki na Kusini mwa Afrika mwaka 2023 linaendelea kuathiri eneo hilo, na kuweka matatizo ya ziada kwa jamii na vituo vya afya.Na matumizi ya tumbaku yanaoekana kupungua licha ya juhudi za sekta ya tumbaku kuhatarisha maendeleo, imeeleza ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO. WHO inaeleza kwamba mienendo ya kuanzia mwaka 2022 inaonesha takriban mtu mzima 1 kati ya 5 duniani kote anatumia tumbaku ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2000 ambapo ilikuwa ni mtu 1 kati ya 3. Mashinani tunakutana na Bora Meto, mkimbizi na muathirika wa unyanyasaji wa kijinsia nchini DRC akisema amepata usalama na matumaini kupitia mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF na ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uazi, UNFPA ambao umehakikisha usaidizi wa kimatibabu na kisaikolojia, na mafunzo ya stadi za maisha. Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!
16-1-2024 • 11 minuten, 13 seconden
Wahudumu wa afya: Hali katika Hospital ya El-Najar Gaza iko nje ya uwezo wetu
Mashambulio makubwa ya mabomu, vizuizi vya kutembea, na mawasiliano yaliyovurugwa vinafanya iwe karibu kutowezekana kuwasilisha vifaa tiba mara kwa mara na kwa usalama kote Gaza, hasa kaskazini. Kupitia video iliyoratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) huko Rafar, Anold Kayanda anasimulia.
15-1-2024 • 3 minuten, 23 seconden
15 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko katika ukanda wa Gaza na Ufugaji nyukinchini Uganda. Makala tunarejea Gaza na mashinani tunakupeleka nchini Rwanda, kulikoni?Zikiwa ni zaidi ya siku 100 tangu kuibuka upya kwa mzozo huko Mashariki ya Kati, mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo wametoa taarifa inayoeleza kuongezeka kwa hatari ya baa la njaa na milipuko ya magonjwa ya kuambukiza huku yakisisitiza muarobaini pekee kwa sasa ni kuruhusu njia mpya za kuingiza misaada ya kwenda kutatua changamoto zinazowakabili wananchi walioko Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limewapiga jeki wafugaji wa nyuki na usindikaji wa mazao ya asali wilayani NAKAPIRIPIRIT katika jimbo la Karamoja nchini Uganda. Kwa msaada wa vifaa na mafunzo kutoka kwa shirika hilo maisha ya wafuga nyuki wa eneo hilo na familia zao yamebadilika.Makala inatupeleka Gaza ambako mashambulio makubwa ya mabomu, vizuizi vya kutembea, na mawasiliano yaliyovurugwa vinafanya iwe karibu kutowezekana kuwasilisha vifaa tiba mara kwa mara na kwa usalama kote Gaza, hasa kaskazini. Mashinani tutaelekea nchini Rwanda kusikia kuhusu usajili wa watoto wachanga punde wanapozaliwa katika kambi za wakimbizi. Mwenyeji wako ni Evarist Mapesa, karibu!
15-1-2024 • 12 minuten, 41 seconden
UN yaomba kufunguliwe njia nyingine ya kufikisha misaada Gaza
Zikiwa ni zaidi ya siku 100 tangu kuibuka upya kwa mzozo huko Mashariki ya Kati, mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo wametoa taarifa inayoeleza kuongezeka kwa hatari ya baa la njaa na milipuko ya magonjwa ya kuambukiza huku yakisisitiza muarobaini pekee kwa sasa ni kuruhusu njia mpya za kuingiza misaada ya kwenda kutatua changamoto zinazowakabili wananchi walioko Gaza. Hii leo kutoka Geneva Uswisi na New York Marekani Mashariki manne ya UN ambayo ni lile la Mpango wa chakula duniani WFP, Afya ulimwenguni WHO, linalohusika na masuala ya watoto UNICEF na la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA wametoa taarifa ya pamoja inayoeleza zahma zinazowakumba wakazi wa Gaza na nini kifanyike kuwasaidia. WFP, ambao tangu tarehe 7 wamekuwa wakitoa Msaada wa chakula na kuweza kuwafikia zaidi ya wananchi 900,000 mpaka sasa, wanaeleza kuwa wananchi wengi wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula ambapo watu wazima wanapitisha hata siku nzima bila kula chochote ili angalau watoto waweze kuweka chochote tumboni. “Wananchi wa Gaza wapo hatarini kufa njaa wakati maili chache tu toka walipu kuna msururu wa malori yaliyojaa chakula” amesema Mkurugenzi Mkuu wa WFP Cindy McCaini ambaye pia ametoa suluhu akisema “Kila saa inayopotea tunaweka maisha mengi hatarini. Tunaweza kuzuia njaa lakini ikiwa tu tunaweza kutoa vifaa vya kutosha na pia kufikisha misaada hiyo kwa njia zilizo salama ili kula mwenye uhitaji popote alipo afikiwe.”UNICEF, Mkurugenzi Mkuu wake anasema Bi. Catherine Russell anasema watoto huko Gaza mbali na kiwewe cha milipuko na kutakiwa kuhama huku kisha kule na kujeruhiwa na kuuawa wengi wanakabiliwa na utapiamlo mkali na wengine wana uzito mdogo ikilinganishwa na urefu wao. “Watoto walio katika hatari kubwa ya kufa kutokana na utapiamlo na magonjwa wanahitaji sana matibabu, maji safi na huduma za usafi wa mazingira, lakini hali haituruhusu kuwafikia watoto na familia zao, baadhi ya misaada inayohitaji sana kuwasaidia imezuiliwa kuingia Gaza. Maisha ya watoto na familia zao yananing'inia kwenye mizani.”Mkurugenzi wa WHO Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema mbali na kutoa misaada ya vifaa tiba na kusaidia sekta ya afya iliyohemewa na wingi wa wagonjwa lakini wamelazimika kufungua majiko mawili katika hospital maana watu wanaumwa na wana njaa. “Watu huko Gaza wanateseka kutokana na ukosefu wa chakula, maji, dawa na ukosefu wa huduma za afya za kutosha. Njaa itafanya hali mbaya ambayo ipo tayari kuwa janga kwa sababu wagonjwa wana uwezekano mkubwa wa kufa na njaa na watu wenye njaa wana hatari zaidi ya magonjwa. Tunahitaji ufikishaji misaada usiozuiliwa, salama wa kutoa misaada na usitishaji mapigano kwa sababu za kibinadamu ili kuzuia vifo na mateso zaidi.”Mkuu wa UNRWA Phillip Lazzarini amehitimisha taarifa hiyo ya pamoja kwa kusema misaada inayoingia Gaza ni tone la maji katika baharí ya misaada inayohitajika , ombi ni kuwa Israel iruhusu bandari ya Ashdod ambayo ipo umbali wa Km 40 tu kutoka Gaza kaskazini itumike kupitisha misaada ili waweze kuwafikia wananchi wengi wenye uhitaji.
15-1-2024 • 3 minuten, 34 seconden
Wafugaji wa nyuki Karamoja wasema mafunzo ya FAO yamewakomboa wao na familia zao
Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limewapiga jeki wafugaji wa nyuki na usindikaji wa mazao ya asali wilayani Nakapiripirit katika jimbo la Karamoja nchini Uganda. Kwa msaada wa vifaa na mafunzo kutoka kwa shirika hilo maisha ya wakulima wa asali wa eneo hilo na familia zao yamebadilika. Wilaya ya Nakapiripirit ina mamia ya wakulima wa asali wengi wakiwa katika vikundi vya kijamii na wengine wafugaji nyuki binafsi. FAO ilitambua thamani ya mazao ya asli kwa watu wa Kramoja na ikaanza kuwapa mafunzo kupitia mradi maalum wa ufugaji wa nyuki, kuanzia utundikaji mizinga, urinaji, usindikaji wa mazao ya asali na hata kuwasidia kutafuta masoko. Miongoni mwa waliokumbatia fursa hiyo ni John Lopetangor ingawa anasema si kazi rahisi, “Kuna kazi nyingi katika kuezeka mizinga ya nyuki sio watu wote wanaiweza. Kuna wadudu wanapenda kuingia katika mizinga ya nyuki na wakiingia tu hbasi nyuki wanakimbia. Na cha pili ukiwa na mizinginga ni lazima uitembelee kama vile unatembelea ng’ombe na katika mizinga ambayo haina nyuki lazima uhakikishe unajua tatizo ni nini na ufukishe moto hadi uone nyuki wameingia mzingani, usiache tu ukitegemea nyuki wataingia hapo hutopata asali. Na wakati wa ukame mizinga inapaswa kumwagiliwa maji.”Licha ya changamoto hizo John anaipenda kazi hii, “Hii kazi ni kazi ya maana kwa sababu sasa siuzi ng’ombe , siuzi mbuzi kazi yangu sasa hivi ni kuanzia mwezi wa nne mi nashika pesa mkononi tu hadi mwezi wa tisa, nasomesha sasa watoto wangu vizuri kwa sababu ya asali.”Na faida hiyo si kwa John peke yake Susan Chepsugul naye ni mfugaji binasi wa nyuki aliingia katika mradi na sasa matunda ameyaona, “Nilipouza hiyo asali nilipata fedha kidogo ikanisaidia kuweka akiba nikaenda kuongeza mizinga miwili sasa nikapata mizinga mitatu. Na ninapouza hiyo asali pia inanisaidia kulisha watoto, kulima shamba na kununulia watoto nguo. Wakati nilipolima shamba kwa kutumia hela za asali nilipata gunia moja nikaongeza mzinga mwingine nilionunua.”Kwa mujibu wa FAO mradi huu sio tu wa kuwainua kiuchumi wanajamii hawa bali pia kuhakikisha wanakuwa na mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
15-1-2024 • 2 minuten, 28 seconden
Olga muathirika wa vita Ukraine anasema bila UNHCR sijui ningekaa wapi
Kutana na Olga mwathirika wa vita inayoendelea nchini Ukraine ambaye baada ya nyumba yake kushambuliwa na kombora mjini Borodyanka alikataa tamaa ya Maisha lakini sasa mradi wa UNHCR wa kukarabati nyumba zilizoharibiwa na vita Ukraine umemfufulia matumaini ya Maisha yeye na mwanaye. Kwa undani zaidi ungana na Flora Nducha kwa makala hii.
12-1-2024 • 3 minuten, 9 seconden
Israel yaiambia mahakama ya ICJ kwamba vita dhidi ya Hamas huko Gaza ni kitendo cha kujilinda
Israel imekanusha vikali shutuma kuwa ina nia ya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kuwa ipo katika vita ambayo wao hawakuianzisha na wala hawakuitaka kufuatia hapo jana nchi ya Afrika kusini kuwasilisha kesi mbele ya mahakama ya Umoja wa Mataifa ya kimataifa ya haki ICJ wakitaka kukomesha mauaji ya raia huko Gaza.Leo ijumaa ya tarehe 12 Januari ni siku ya pili na ya mwisho ya kusikilizwa kwa kesi ya awali katika Mahakama ICJ ambapo baada ya jana Afrika Kusini kutoa maeleo yale leo timu ya wanasheria wa Israel imesisitiza kwamba wana malengo mawili ambayo mosi ni kutokomeza tishio lililokuwepo la wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas na Pili ni kuwaachilia huru mateka 136 ambao bado wanashikiliwa katika vita inayoendelea huko mashariki ya Kati. kamanda wa Israel Tal Becker aliwaambia majaji wa ICJ huko The Hague nchini Uholanzi kuwa “Israel iko katika vita dhidi ya Hamas, sio dhidi ya watu wa Palestina” kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyoongozwa na Hamas tarehe 7 Oktoba mwaka 2023. Akisoma jumbe za mwisho zilizotumwa na baba wa moja ya familia za wakulima ambao nyumba zao zilichomwa moto na watu wanaodhaniwa kuwa ni Hamas, Bwana Becker amesema “kumekuwa na mateso ya kiraia "ya kutisha" na "ya kuhuzunisha moyo" "katika vita hivi, kama katika vita vyovyote vile.”Becker pia amekataa ombi la Afrika Kusini kwa mahakama chini ya vifungu vya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari la kutoa "hatua za muda" ili kuiamuru Israel kusimamisha mara moja shughuli zake za kijeshi huko Gaza akisema kuwa hatua hiyo ni “jaribio la kuinyima Israel uwezo wake wa kutimiza wajibu wake wa kuwalinda raia wake, mateka, na zaidi ya Waisraeli 110,000 waliokimbia makazi yao ambao hawakuweza kurejea kwa usalama makwao,”Wanasheria wa Israel wamewaeleza majaji wa ICJ kuwa nchi inaposhambuliwa, ina haki ya kujilinda yenyewe na raia wake, “Hakuna nia ya mauaji ya kimbari hapa, haya sio mauaji ya halaiki,” wakili wa Israel Malcolm Shaw aliiambia mahakama hiyo akisisitiza kuwa ukatili uliofanywa na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas “hauhalalishi ukiukwaji wa sheria katika wakujibu mashambulizi na bado ni chini ya mauaji ya halaiki - lakini unahalalisha...utekelezaji wa haki halali na ya asili ya Nchi kujilinda kama ilivyoainishwa katika Mkataba wa Umoja wa Mataifa”.Timu ya wanasheria wa Israel pia imekataa maelezo yaliyowasilishwa hapo jana na timu ya wanasheria ya Afrika kusini ikisema yana “upotoshaji sana” na kwamba wanatumia neno “Mauaji ya kimbari” kama silaha ambapo Wakili Galit Raguan aliiambia mahakama hiyo kuwa “Vita vya mijini daima vitasababisha vifo vya kusikitisha, madhara na uharibifu, lakini huko Gaza matokeo haya yasiyotakikana yanazidishwa kwa sababu ni matokeo yanayotarajiwa ya Hamas.”
12-1-2024 • 3 minuten, 4 seconden
12 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia kesi mbele ya mahakama ya Umoja wa Mataifa ya kimataifa ya haki ICJ inayotaka Israeli kukomesha mauaji ya raia huko Gaza, na haki za wanawake za unyonyeshaji. Makala tunakupeleka nchini Ukraine na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Israel imekanusha vikali shutuma kuwa ina nia ya mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kuwa ipo katika vita ambayo wao hawakuianzisha na wala hawakuitaka kufuatia hapo jana nchi ya Afrika kusini kuwasilisha kesi mbele ya mahakama ya Umoja wa Mataifa ya kimataifa ya haki ICJ wakitaka kukomesha mauaji ya raia huko Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF Rwanda kwa kushirikiana na wadau kama Shirika la Taifa la Maendeleo ya Mtoto nchini humo, NCDA, wanatoa wito kwa sekta binafsi, taasisi za serikali, washirika, asasi za kiraia kuweka mazingira rafiki ya unyonyeshaji mahali pa kazi. Evarist Mapesa anaangazia faida ya moja ya vyumba vya kunyonyeshea mahali pa kazi jijini Kigali Rwanda.Makala leo inakukutanisha na Olga mwathirika wa vita inayoendelea nchini Ukraine ambaye baada ya nyumba yake kushambuliwa na kombora mjini Borodyanka alikataa tamaa ya maisha lakini sasa mradi wa UNHCR wa kukarabati nyumba zilizoharibiwa na vita Ukraine umemfufulia matumaini ya Maisha yeye na mwanaye. Mashinani inatupeleka Kakuma nchini Kenya ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula WFP limejenga ustahimilivu na uwezo wa kujitegemea miongoni mwa wakimbizi na jamii zinazowapokea, kupitia uzalishaji wa mazao na ufugaji unaohimili mabadiliko ya tabianchi”. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
12-1-2024 • 12 minuten, 14 seconden
Wanawake Rwanda: Tunapaswa tufanye kunyonyesha mahali pa kazi kufanye kazi!
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF Rwanda kwa kushirikiana na wadau kama Shirika la Taifa la Maendeleo ya Mtoto nchini humo, NCDA, wanatoa wito kwa sekta binafsi, taasisi za serikali, washirika, asasi za kiraia kuweka mazingira rafiki ya unyonyeshaji mahali pa kazi. Katika moja ya maeneo tulivu ya jiji lenye shughuli nyingi za jiji la Kigali-Rwanda kumetengwa chumba eneo maalumu lenye mazingira yote yanayofaa kwa akina mama kuwanyonyesha Watoto wao au hata kukamua maziwa na kuyahifadhi. Banamwana Yvette Mfanyakazi wa Ofisi za Jiji na Kigali anasema alikuwa anapoteza muda mwingi njiani kutoka kazini kwenda kumnyonyesha mtoto na kurudi kazini. Kayitesi Sophie mwajiriwa wa Benki ya Kigali anasema, “tulikuwa tunakamua maziwa maliwatoni na baadaye kuyamwaga kwa kuwa hatukuwa na pa kuyatunzia.” Vick Mujiji, yeye ni mfanyakazi wa kampuni ya Africa Improved Foods anaeleza kwamba kukitumia chumba cha kunyonyeshea kumeongeza tija kazini kwake kwani ofisi yake haiko mbali na hapa na kwa hivyo anaweza kuja muda wowote akakamua maziwa yake na kurejea kazini. Ingabire Assumpta ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo ya Mtoto Rwanda (NCDA) anasema, “Wengi wa watoto wanaonyonyeshwa katika saa ya kwanza mara tu baada ya kuzaliwa ni watoto wa vijijini kuliko wa mjini. Kwa hiyo ndio hiyo ilifanya tuwawezeshe wazazi kunyonyesha katika maeneo yao ya kazi. Ninawahamasisha mashirika mbalimbali ambao hawajaanzisha vyumba hivi kuanza kwani ni kwa faida yao pindi mama anapokuwa na uhakika kwamba mtoto wake amenyonya vizuri, ana afya na yuko karibu naye, atafanya kazi vizuri na tija inaongezeka.” Baada ya mafanikio haya ya mfano, Mwakilishi wa UNICEF nchini Rwanda, Julianna Lindsey ana ujumbe, “Ujumbe wangu kwetu sote ni kwamba wanawake hawapaswi kuchagua kati ya kazi yao na kuchangia katika uchumi wa Rwanda na utimilifu wa taaluma zao dhidi ya kuhakikisha mtoto anapata lishe muhimu.”
12-1-2024 • 2 minuten, 34 seconden
METHALI: “MSIBA WA MWENZIO NI KANDA LA USUFI”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA anatufafanulia maana ya methali “MSIBA WA MWENZIO NI KANDA LA USUFI”.
11-1-2024 • 0
11 JANUARI 2024
Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo mwezi Desemba mwaka jana nilihudhuria Kongamano la 8 la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) nchini Tanzania na walifanya warsha kuhusu ChatGPT kwa wafundishaji wa lugha ya kiswahili. Dkt. Fillipo Lubua anaeleza zaidi kuhusu jambo hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali. Leo Afrika Kusini imezungumza mbele ya mahakama ya Umoja wa Mataifa ya kimataifa ya haki ICJ baada ya kuwasilisha kesi katika jitihada za kukomesha mauaji ya raia huko Gaza, ikiishutumu Israel kutekeleza mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina madai ambayo Israel imekanusha vikali ikisema kuwa hayana msingi.Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM leo limezindua mpango mkakati wake wa kimataifa wa miaka mitano mjini, N'Djamena Chad unaolenga kutimiza ahadi ya usalama, utaratibu na uhamiaji wa mara kwa mara huku ukisaidia watu walio hatarini zaidi duniani.Na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Misaada nchini Afghanistan UNAMA leo umesema una wasiwasi mkubwa kuhusu kukamatwa kiholela na kuzuiliwa kwa wanawake na wasichana kunakofanywa na maafisa wa serikali ya Afghanistan kwa sababu ya madai ya kutofuata kanuni za mavazi ya Kiislamu. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili nampisha Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA akitufafanulia maana ya methali “MSIBA WA MWENZIO NI KANDA LA USUFI”. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
11-1-2024 • 10 minuten
MINUSCA yachukua hatua kukabili habari potofu n aza uongo CAR
Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kwa muda mrefu imegubikwa na mizozo ya wenyewe kwa wenyewe hususuan maeneo ya kaskazini mwa nchi. Umoja wa Mataifa umekuwa na juhudi mbalimbali za kuleta amani hadi kuwezesha kufanyika kwa uchaguzi mwaka 2016 uliomwezesha Rais wa sasa Faustin Archange Touadera kuwa madarakani. Ingawa hivyo kumekuweko na changamoto za mivutano huku kuenea kwa habari potofu na za uongo kuwa moja ya kichocheo. Kwa kutambua hilo ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MINUSCA umechukua hatua. Je ni zipi hizo? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.
10-1-2024 • 3 minuten, 56 seconden
10 JANUARI 2024
Jaridani leo tunaangazizia ripoti ya ajira ulimwenguni kote, na masuala ya afya nchini Botswana. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Afrika Kati, CAR. Mashinani tunaelekea Zanzibar nchini Tanzania, kulikoni?Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO kuhusu mtazamo wa ajira na kujamii imeonya juu ya kuongezeka kwa ukosefu wa ajira kimataifa kwa mwaka huu wa 2024, sanjari na pengo la usawa na kudumaa kwa kiwango cha uzalishaji hali ambayo inaibua wasiwasi.Botswana iko njiani kutokomeza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI - VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, shukrani kwa msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya WHO kanda ya Afrika wakishirikiana na mashirika ya kiraia.Makala inakupeleka Jamhuri ya Afrika Kati, CAR ambako huko Umoja wa Mataifa umechukua hatua ya kukabiliana na habari potofu, za uongo na chuki kupitia redio. Mashinani tunakuletea ujumbe wa mkulima wa mwani kutoka zanzibar nchini Tanzania kuhusu jinsi ufadhili wa Benki ya Dunia unavyoboresha ukulima wake. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
10-1-2024 • 11 minuten, 49 seconden
Botswana wako mstari wa mbele kutokomeza maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Botswana iko njiani kutokomeza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI - VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, shukrani kwa msaada kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya WHO kanda ya Afrika wakishirikiana na mashirika ya kiraia. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi. Botswana ni moja ya nchi zinazokuwa na changamoto ya maambukizi ya VVU, mwaka 2022 wizara ya afya ya Botwasana wakishirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika na mashirika ya kiraia waliunganisha nguvu kushughulikia changamoto hiyo ambayo ilikuwa ikiwaathiri wajawazito wanaoishi na VVU kwani walikuwa hawajui mengi kuhusu haki zao ikiwemo haki ya faragha, usiri na ruhusa ya kutoa taarifa zao.WHO na wadau wengine walitoa mafunzo kwa wawakilishi 27 wa vikundi vya msaada kwa watu wanaoishi na VVU, wahudumu wa afya katika ngazi ya jamii na watu waliojitolea, na wote hawa walipewa jukumu la kuelimisha wenzao juu ya haki za binadamu, kutoa ridhaa baada ya kuarifiwa na usawa wa kijinsia kama anavyoeleza Layeza Maraya Mbulawa, Muuguzi mkuu katika Kliniki ya Thini iliyoko Tutuma nchini Botswana. “Tumepewa mafunzo ya haki za binadamu, ambayo tunayatekeleza katika ngazi ya wilaya ambapo safari hii kuna mabadiliko makubwa. Watu wanajua haki ya binadamu.”Na sasa wanawake wanaoishi na VVU wanajua zaidi kuhusu haki zao hususan kwenye masuala ya afya kama anavyoeleza mmoja wa wanufaika ambaye jina lake hatutalitaja. “Siku hizi mambo yamekuwa bora sana kwa sababu sasa najua kuhusu haki zangu na hakuna anayefanya maamuzi kwa niaba yangu na mtu unaweza kuamua unachotaka.”Kuimarisha haki ya afya ni kusaidia kuimarisha huduma bora. Afya kwa wote ni kitovu cha mapambano dhidi ya VVU nchini Bostwana.
10-1-2024 • 2 minuten, 1 seconde
Ripoti ya ILO: Ukosefu wa ajira duniani kuongezeka 2024 sanjari na pengo la usawa
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi la Umoja wa Mataifa ILO kuhusu mtazamo wa ajira na kujamii imeonya juu ya kuongezeka kwa ukosefu wa ajira kimataifa kwa mwaka huu wa 2024, sanjari na pengo la usawa na kudumaa kwa kiwango cha uzalishaji hali ambayo inaibua wasiwasi. Ripoti hii ya mwaka 2024 iliyopewa jina Mienendo ya mtazamo wa Dunia wa ajira na kijamii 2024 imegawanyika katika sehemu kuu 4, mosi ni hali halisi ya mtazamo wa ajira duniani kote ambapo inasema ingawa kiwango cha ukosefu wa ajira na pengo katika kusaka ajira vilishuka kidogo chini ya kiwango cha kabla ya COVID-19 kutokana na mnepo uliojitokeza licha ya kuzororta kwa hali ya uchumi lakini matarajio ya kimataifa ndio yanayotia hofu kubwa.Pili ripoti hiyo ya ILO imetaja nini kinachangia hofu hii kwa mwaka 2024, kwanza ni ongezeko la migogoro mipya ambayo mingi inapunguza matarajio ya kijamii ya kupata haki za kijamii ikiwemo ajira ikisema “Mwaka huu wa 2024 wafanyikazi milioni mbili zaidi wanatarajiwa kutafuta kazi, na hivyo kuongeza kiwango cha ukosefu wa ajira duniani kutoka asilimia 5.1 mwaka 2023 hadi asilimia 5.2. Mapato yanayoweza kutumika yamepungua katika nchi nyingi Tajiri duniani za G20 na, kwa ujumla, kuporomoka kwa viwango vya maisha kunaotokana na mfumuko wa bei ambao hauna uwezekano wa kutengamaa haraka".Na pili ripoti inasema ni uwekezaji ambapo tofauti muhimu zinaendelea kati ya nchi za kipato cha juu na cha chini. Sehemu ya tatu ya ripoti ni nani waathirika wakumbwa ambapo imebainisha kuwa “Wakati kiwango cha pengo la ajira mwaka 2023 kilikuwa asilimia 8.2 katika nchi zenye kipato cha juu, kilisimama kwa asilimia 20.5 katika kundi la watu wenye kipato cha chini. Vile vile, wakati kiwango cha ukosefu wa ajira cha 2023 kiliendelea kuwa asilimia 4.5 katika nchi za kipato cha juu, kilikuwa asilimia 5.7 katika nchi za kipato cha chini.”Mwisho ripoti imeongelea kuendelea kwa umasikini hususani katika nchi za kipato cha chini kutokana na ushiriki katika soko la ajira na pengo la usawa ikisema imesema idadi ya wafanyakazi wanaoishi katika umaskini uliokithiri ambao wanapata chini ya dola 2.15 kwa kila mtu kwa siku iliongezeka kwa takriban watu milioni 1 mwaka 2023.Pia idadi ya wafanyakazi wanaoishi katika umaskini wa wastani wakipata chini ya dola 3.65 kwa siku kwa kila mtu iliongezeka kwa watu milioni 8.4 mwaka 2023. Imeonya kwamba ukosefu wa usawa wa mapato umeongezeka, na hii "vinaashiria hali mbaya kwa mahitaji ya jumla na kujikwamua kuliko uendelevu zaidi kiuchumi.” Na katika ushiriki imesema ukosefu wa ajira kwa vijana umeendelea kuwa mtihani mkubwa hasa kwa wasichana na licha ya maendeleo ya teknolojia bado hakuna ongezeko lenye tija la ajira.Mkurugenzi mkuu wa ILO Gilbert F. Houngbo amesema “Inaanza kuonekana kana kwamba kukosekana kwa usawa huku si sehemu tu ya kujikwamua na janga la COVID-19 bali ni suala la kimuundo. Changamoto za wafanyakazi inazotambua ni tishio kwa maisha ya watu binafsi na biashara na ni muhimu kuzishughulikia kwa ufanisi na haraka.”Amesisitiza kuwa “Na bila uadilifu mkubwa wa kijamii kamwe hatutakuwa na ahueni endelevu”.
10-1-2024 • 2 minuten, 47 seconden
Kiswahili kuanza kutumika EAC rasmi mwaka 2024
Lengo namba 17 la Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs linataka uwepo wa Ushirikiano katika kufanikisha malengo. Ushirikiano huo unaweza kuwa baina ya nchi na nchi, wananchi na ushirikiano wa kikanda. Mwezi Desemba mwaka jana 2023 nilifunga safari hadi jijini Arusha nchini Tanzania na kuzungumza na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki kutaka kufahamu namna wanavyoshirikiana na Umoja wa Mataifa katika maeneo mbalimbali ikiwemo ulinzi na usalama pamoja na kukuza lugha ya Kiswahili. Karibu usikilize mazungumzo yetu.
9-1-2024 • 7 minuten, 40 seconden
09 JANUARI 2024
Hii leo jaridani mada kwa kina tukimulika lengo namba 17 la Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs linataka uwepo wa Ushirikiano katika kufanikisha malengo. Ushirikiano huo unaweza kuwa baina ya nchi na nchi, wananchi na ushirikiano wa kikanda. Pia tunaangazia mzizo katika ukanda wa Gaza na Ukraine, na ripoi ya uchumi.Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO na timu yake iliyoko huko idadi ya vifo na majeruhi Gaza kutokana na mzozo unaoendelea baina ya Israel na kundi la Hamas inaongezeka kila uchao na waathirika wakubwa ni wanawake na watoto.Ni karibu miaka miwili sasa tangu Urusi kuivamia Ukraine shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema wakimbizi zaidi ya milioni sita wamefurushwa kutoka makwao nchini Ukraine ambapo Zaidi ya wakimbizi milioni 5.9 wako katika nchi mbalimbali za Ulaya.Na ripoti ya Benki ya Dunia ya matarajio ya uchumi kwa mwaka huu iliyotolewa leo ambapo takwimu zinaonyesha kuwa huu ni nusu muongo uliodorora saana katika ukuaji wa pato la taifa au GDP kwa takribani miaka 30, huku matarajio yakionyesha kushuka kwa ukuaji wa uchumi duniani kwa mwaka wa tatu mfululizo kutoka asilimia 2.6 mwaka jana hadi asilimia 2.4 mwaka huu. Mashinani tunarejea katika ukanda wa Gaza kusikiliza simulizi ya manusura wa vita baina ya Israel na kundi la Hamas. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
9-1-2024 • 10 minuten, 45 seconden
Mradi wa IFAD umenisaidia baada ya kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi – Mkulima Kenya
Mradi wa kilimo endelevu unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kilimo, IFAD na Serikali ya Kenya ambao unalenga kukuza miche ya miti na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi umeleta manufaa kwa wakulima wadogo kutoka eneo la Kaunti ya Kiambu nchini Kenya na kuboresha ukulima wao. Mkulima mdogo Francis Njoroge ni mmoja wa mamilioni ya wakulima wadogo wanaokabiliwa na athari za mabadiliko ya tabianchi lakini kwa bahati nzuri, amefaidika na Mfuko wa Upper Tana Nairobi Water Fund unaolenga kukuza miche ya miti na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Kupitia video iliyoandaliwa na IFAD, Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anasimulia zaidi.
8-1-2024 • 4 minuten, 4 seconden
08 JANUARI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia vita katika ukanda wa Gaza, na huduma za afya na umaskini nchini Nigeria. Makala na mashinani tunamulika ukulima bunifu na wa umwagiliaji unaosaidia wakulima wadogo kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Kenya.Ikiwa leo ni siku ya 93 tangu mapigano yaanze huko Ukanda wa Gaza kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa kipalestina waliojihami, likiwemo kundi la Hamas, mashirika ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kiutu yanazungumzia uwepo wa idadi kubwa ya vifo miongoni mwa wanawake na watoto huku yakisihi timu za madaktari ziruhusiwe kuingia eneo la Gaza ili ziendelee na jukumu la kuokoa maisha. Assumpta Massoi amefuatilia na kutuandalia ripoti hii.Nchini Nigeria katika Jimbo la Anambra shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika kwakushirikiana na mpango wa Bima ya Afya ya Serikali wanabadilisha maisha ya wananchi kwa kulipia sehemu kubwa ya gharama za matibabu ili kuhakikisha kila mtu anaweza kupata huduma za afya bila kudumbukia katika umaskini.Makala leo tunabisha hodi eneo la Murang’a katika kaunti ya Kiambu, nchini Kenya ambapo tunakutana na Francis Njoroge, mkulima mdogo mmoja wa mamilioni ya wakulima wadogo walioathiriwa na mabadiliko ya tabianchi lakini kupitia ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya kilimo, IFAD, anasimulia jinsi ukulima wake umeimarika. Na mashinani tunasalia nchini Kenya mada huo wa ukulima na tunakwenda Kibera, kusikia ujumbe kuhusu mbinu bunifu ya kilimo inayoleta tija kwa wakaazi. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Ikiwa leo ni siku ya 93 tangu mapigano yaanze huko Ukanda wa Gaza kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa kipalestina waliojihami, likiwemo kundi la Hamas, mashirika ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kiutu yanazungumzia uwepo wa idadi kubwa ya vifo miongoni mwa wanawake na watoto huku yakisihi timu za madaktari ziruhusiwe kuingia eneo la Gaza ili ziendelee na jukumu la kuokoa maisha. Naanzia eneo la kati mwa Gaza ambako huko shirika la Umoja wa Mataifa la Afya, WHO limeonya kuwa madaktari katika hospitali pekee inayotoa huduma kwenye jimbo la Deir al Balah ilibidi jana Jumapili waache kutoa huduma baada ya kupokea amri ya kutakiwa kuondoka eneo hilo kutokana na mashambulizi yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel. Na kwenye hospital ya Al-Aqsa ambako timu ya WHO ilipeleka vifaa vya matibabu kusaidia wagonjwa 4,500 wanaohitaji huduma ya kusafisha figo na wengine 500 wanaokabiliwa na kiwewe, idadi ya madaktari waliosalia ni watano pekee. Kupitia mtandao wa X, Afisa wa WHO anayehusika na masuala ya dharura ya afya Sean Casey alichapisha video inayoonesha heka heka kwenye hospitali hiyo ya Al- Aqsa, wagonjwa wakiwa wamefurika sakafuni, madaktari wakiwapatia tiba hapo hapo, huku damu imetapakaa, na mamia ya wagonjwa wengine wakifikishwa hapo kwa ajili ya matibabu. Dkt, Tedros Ghebreyesus ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa WHO naye kupitia mtandao wa X akasema hospitali ina mahitaij makubwa, kama vile wahudumu wa afya, vitanda lakini wafanyakazi wa Al- Aqsa wanasema jambo muhimu zaidi kwao, wagonjwa na familia ni kulindwa dhidi ya mashambulizi ya makombora na uhasama ukome. Huku mashambulizi yakiendelea shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoot, UNICEF linasema magonjwa nayo yanashamiri kwani kila siku kuna wagonjwa wapya 3,200 wa kuhara miongoi mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA imenukuu takwimu mpya kutoka Wizara ya Afya ya Gaza zikionesha kuwa kati ya Ijumaa na jana Jumapili wapalestina 225 wameuawa na 300 wamejeruhiwa huku jeshi la Israel likiripotikuwa tangu lianze operesheni za ardhini, askari wake 174 wameuawa na wengine zaidi ya 1,000 wamejeruhiwa.
8-1-2024 • 2 minuten, 16 seconden
Wananchi wa jimboni Anambra, Nigeria wapata bima ya afya kwa bei nafuu kwa usaidizi wa WHO
Nchini Nigeria katika Jimbo la Anambra shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika kwakushirikiana na mpango wa Bima ya Afya ya Serikali wanabadilisha maisha ya wananchi kwa kulipia sehemu kubwa ya gharama za matibabu ili kuhakikisha kila mtu anaweza kupata huduma za afya bila kudumbukia katika umaskini. Anambra ni jimbo la nane lenye wakazi wengi nchini Nigeria na jimbo la pili kwa idadi kubwa ya watu baada ya jimbo la Lagos. Wananchi wa jimbo hili wanachangamkia kujiandikisha katika mpango wa jimbo hilo wa bima ya afya ambapo WHO inatoa usaidizi kupitia mafunzo na miongozo ya kimkakati.Zaidi ya wananchi 225,000 wameshakata bima ya afya na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Bima ya Afya la jimbo la Anambra Dokta. Simeon Onyemaechi anaeleza malengo yao.“Hakuna mtu anayepaswa kuwa maskini kwa sababu anahitaji huduma ya afya. Tumewapa wananchi ulinzi wa hatari za kifedha ili kuwaokoa kutokana na matumizi makubwa ya afya kwa njia ambayo hakuna hata mtu mmoja anayepaswa kukabiliwa na ugumu wa kifedha au kuwa maskini kwa sababu alilazimika kulipa bili kubwa za hospitali.”Mpango huu unawashirikisha viongozi wa kimila, mmoja wao ni Mfalme Ben Emeka, wa himaya ya Umueri.“Bima ya Afya ni jambo la ajabu ambalo limekuja jimbo la Anambra na limefika kwa watu wangu, watu wa Umueri, kwa sababu kabla ya sasa walikuwa wakilipa kiasi kikubwa sana.”Sio tu Mfalme Emeka anahamasisha wananchi wake kukata bima za afya lakini pia amekatia wananchi wake 300 bima ya afya na anatoa wito kwa watu wenye uwezo wa kifedha na ushawishi kufanya kama yeye.“Matajiri sasa wanaweza kuwasaidia masikini kwa kuwakatia bima za afya. Na masikini pia wanaweza kujilipia wenyewe bima za afya kwakuwa bei imekuwa nafuu.”
8-1-2024 • 2 minuten, 9 seconden
Ukiweka bidii na kuzingatia mwongozo hakuna linaloshindikana: Mary Keitany
Mashirika ya umoja wa Mataifa lile mazingira duniani UNEP na lile la afya WHO nchini Kenya ivi karibuni yalizindua kampeni ya kuhimiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira safi kwa ajili ya afya bora. Kampeni hiyo maalum ilifanyika jijini Nairobi kwa kuwaalika wanaridha kadhaa wa Kenya wa zamani na wa sasa kwenye ofisi za Umoja wa mataifa. Lengo lilikuwa ni kuzungumza na wanariadha hao kuhusu uhusiano uliopo baina ya mazingira na afya bora ili wawe mabalozi wa kuchagiza hilo katika tasnia yao ambayo mara nyingi hufanyika katika maeneo ya wazi na hewa safi ni muhimu. Miongoni wa wanariadha hao ni Mary Jepkosgei Keitany anayeshikilia rekodi kadhaa za mbio ndefu au marathoni. Amezungumza na Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS akianza kwa kutoa historia fupi ya safari yake ya riadha.
5-1-2024 • 3 minuten, 56 seconden
05 JANAURI 2024
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu na hali ya watototo katika ukanda wa Gaza, na ugonjwa wa Saratani ya shingo ya Kizazi na jinsi ambavyo inawezatibika ikigunduliwa mapema. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani tutaelekea huko Lopit nchini Sudan Kusini, kulikoni?Watoa huduma za misaada ya kibinadamu wanatoa wito wa kupatiwa fursa ya kufikisha misaada kwa haraka, kwa usalama, kiendelevu na bila vikwazo huko Kaskazini mwa Gaza, Mashariki ya Kati kwani hali ya kibinadamu inazidi kuwa tete.Mwezi huu wa januari umetangazwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya WHO kuwa ni mwezi wa kujenga ufahamu kuhusu ugonjwa wa Saratani ya shingo ya Kizazi.Makala inatupeleka Nairobi Kenya ambako hivi karibuni mashirika ya umoja wa Mataifa lile mazingira UNEP na lile la afya WHO nchini Kenya yalizindua kampeni ya kuhimiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira safi kwa ajili ya afya bora kwa kushirikisha baadhi ya wanariadha nyota wa zamani na wa sasa nchini humo. Na hapo baadaye ni mashinani na tutaelekea huko Lopit nchini Sudan Kusini kwa mnufaika wa mradi wa Umoja wa Mataifa wa kukabiliana na athari za mabadiliko tabianchi. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
5-1-2024 • 10 minuten, 40 seconden
Saratani ya shingo ya kizazi inatibika ikigundulika mapema – WHO
Mwezi huu wa januari umetangazwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya WHO kuwa ni mwezi wa kujenga ufahamu kuhusu ugonjwa wa Saratani ya shingo ya Kizazi, nami nimemualika mwenzangu Leah Mushi hapa studio ambaye amefuatilia kwa kina suala hilo kupitia wavuti wa WHO.Swali: Leah kwanza tueleze lipi hasa WHO wanalotaka wadau wafanye?Jibu: WHO inahamasisha mambo makuu 3 mosi, kutoa taarifa kuwa kuna ugonjwa huo, pili kuhimiza uchunguzi na tatu kuhamasisha chanjo. Swali: Tuanze na hilo la kwanza taarifa za ugonjwa huo?Jibu: Assumpta ningependwa kuwajuza wasikilizaji wetu kuwa 90% ya wanaougua saratani ya shingo ya kizazi ni kutoka nchi masikini na viwango vya juu vya vifo ni kutoka Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, Amerika ya Kati na Kusini-Mashariki mwa Asia. Swali: Mtu anapataje saratani hii?Jibu: WHO inasema virusi aina ya Human Papiloma (HPV) ambayo huambukizwa kwa njia ya zinaa ndio chanzo, mgonjwa asipopata matibabu au maambukizi ya mara kwa mara ya virusi hivyo vya HPV yanaweza kusababisha seli zisizo za kawaida kukua, ambazo zitaendelea kukua na kuwa saratani.Lakini pia wagonjwa wa UKIMWI wapo katika hatari mara 6 zaidi ya kupata saratani ya shingo ya kizazi. Swali: Mtu anawezaje kujikinga?Jibu: Kubwa ni kupata chanjo ya HPV na inaanza kutolewa kwa wasichana katika umri ambao bado hawajaanza kujamiiaa ndio maana inahimizwa kutolewa kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14.Pia kufanya uchunguzi wa kizazi, mwanamke kuanzia umri wa miaka 35 na kuendelea anapaswa angalau mara 2 kwa mwaka kwenda kufanya uchunguzi. Swali: Tiba sasa ni nini?Jibu: ukigundulika tiba ni zile za wagonjwa wa saratani kama vile upasuaji, tiba ya mionzi na tibakemikali ili kutoa huduma pamoja na udhibiti wa maumivu.
5-1-2024 • 1 minuut, 59 seconden
Uwasilishaji misaada kaskazini mwa Gaza umezuiliwa na vizingiti vya kufikisha misaada ya kibinadamu
Wasaidizi wa kibinadamu wanatoa wito wa fursa ya ufikishaji misaada kwa haraka, salama, endelevu na usiozuiliwa kaskazini mwa Gaza kwani hali ya binadamu inazidi kuwa tete. Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa misaada ya kibinadamu wameshindwa kutoa msaada unaohitajika haraka wa kuokoa maisha kaskazini mwa Wadi Gaza kwa siku nne kutokana na ucheleweshaji na kukataliwa, pamoja na migogoro inayoendelea imeeleza Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura OCHA katika taarifa yake iliyokusanya takwimu za hadi jana Jan 4 na kuchapishwa leo Jan 5. Hii ni pamoja na dawa ambazo zingetoa msaada muhimu kwa zaidi ya watu 100,000 kwa siku 30, pamoja na lori nane za chakula kwa watu ambao kwa sasa wanakabiliwa na uhaba wa chakula unaohatarisha maisha. Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), linasema maelfu ya watoto tayari wamekufariki dunia kutokana na ukatili huo unaoendelea, huku hali ya maisha kwa watoto ikiendelea kuzorota kwa kasi. "Watoto huko Gaza wanakumbwa na jinamizi ambalo linazidi kuwa baya kila kukicha," anasema Catherine Russell, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF na kuongeza kuwa, “Watoto na familia katika Ukanda wa Gaza wanaendelea kuuawa na kujeruhiwa katika mapigano, na maisha yao yanazidi kuwa hatarini kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika na ukosefu wa chakula na maji.” Anatoa wito kwamba watoto na raia wote lazima walindwe dhidi ya unyanyasaji na kupata huduma za kimsingi. Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) linaeleza kamba tangu tarehe 24 Desemba 2023, limethibitisha mashambulizi manane kwenye hospitali ya Al-Amal, mashambulizi yaliyoua watu 7 na kujeruhi 11. Mashambulizi ya karibu zaidi ni ya jana Januari 4. Tangu Oktoba 7 mwaka jana, WHO imethibitisha mashambulio 590 dhidi ya huduma za afya katika ardhi ya Palestina inayokaliwa kwa mabavu. Pamoja na hali hii ngumu, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaendelea kusaidia watu katika kila hali inavyowezekana ijapokuwa ni katika hali hatarishi. Kufikia juzi tarehe 3 Januari, jumla ya wafanyakazi 142 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina (UNRWA) wameuawa tangu kuanza kwa mapigano hapo Oktoba 7.
5-1-2024 • 1 minuut, 50 seconden
Methali: Mla mbegu huvuna vya wenyewe
Karibu kujifunza Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Mla mbegu huvuna vya wenyewe.”
4-1-2024 • 1 minuut, 41 seconden
04 JANUARI 2024
Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa, miongoni wa tuliyokuandalia ni pamoja na mada kwa kina itakayokupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumsikia manusura wa ukatili wa kingono. Lakini kabla ya hiyo utasikia Muhtasari wa Habari na kama ilivyo ada ya kila alhamisi tunajifuza lugha ya kiswahili na leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Mla mbegu huvuna vya wenyewe.” Mwenyeji wako ni Leah Mushi
4-1-2024 • 11 minuten, 7 seconden
Kipaji cha sarakasi chamwezesha mkimbizi kutoka DRC kupata elimu bora Uganda
Umoja wa Mataifa unapazia sauti suala la vijana kutumia vipaji vyao ili kuweza kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu .SDGs. Mmoja wa walioitikia wito huo ni mkimbizi kutoka mjini Bukavu jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye baada ya kuwasili ukimbizini nchini Uganda, kipaji chake cha kucheza sarakasi kimemwezesha kupata elimu bora na hivyo kuwa na uhakika wa ustawi wake na familia yake. Ni kwa vipi kipaji hicho kimemsaidia? John Kibego wa Redio washirika Kazi Njema FM iliyoko Hoima nchini Uganda amezungumza na kijana huyo.
3-1-2024 • 4 minuten, 7 seconden
Si haki kutumia gesi ya Nitrojeni Hypoxia kumuua Kenneth - Wasema wataalam wa UN
Wataalamu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Alice Jill Edwards, anayeshughulikia masuala yanayohusu mateso, na Adhabu nyingine za Kikatili, za kinyume cha utu au za Kushusha hadhi, leo Januari 3 mjini Geneva-Uswisi wameelezea wasiwasi wao kuhusu kukaribia kutekelezwa kwa hukumu ya kifo kwa kutumia gesi ya nitrojeni hypoxia dhidi ya Kenneth Eugene Smith hapa nchini Marekani. Mwenzangu Anold Kayanda amekifuatilia kisa hicho kwa kina… ASSUMPTA: Anold hukumu ya kifo bado inatekelezwa katika maeneo kadha duniani, ni kwa nini hii ya sasa inafuatiliwa zaidi? ANOLD: Assumpta hilo ni swali muhimu hasa na jibu ni kuwa utekelezaji huu wa hukumu ya kifo umepangwa kufanyika kwa kutumia gesi ya Nitrojeni hypoxia ambapo huyu Kenneth Eugine Smith atanyimwa hewa ya Oksijeni lakini atapewa nafasi ya kuvuta hiyo gesi ambayo ndiyo itamuua. Sasa wataalamu hawa wa haki za binadamu wanasema kwa kuwa jambo hili halijawahi kujaribiwa hapo awali, kwa hivyo utekelezaji unaweza kumfanya anayeuawa atendewe ukatili, unyama au udhalilishaji au hata kuteswa na kwamba hakuna ushahidi wa kisayansi wa kuthibitisha vinginevyo. ASSUMPTA: Nikikurudisha nyuma kidogo, huyu anayetarajiwa kuuawa kwa njia hii alifanya kosa gani? Smith alipatikana na hatia ya kuua kwa kukodiwa mwaka wa 1988 na kuhukumiwa kifungo cha maisha bila msamaha kwa kura 11 za kukubali na 1 ya kupinga. Hata hivyo, hakimu aliyetoa hukumu alipuuza pendekezo la jopo la mahakama la kifungo cha maisha na akamhukumu kifo. ASSUMPTA: Na mwisho ikiwa hukumu hii itatekelezwa, ni lini? ANOLD: Kenneth Smith, ambaye amekuwa akisubiri kunyongwa kwa zaidi ya miaka thelathini, amepangwa kunyongwa Januari hii tarehe 25, 2024, katika Jimbo la Alabama hapa Marekani. Mamlaka huko Alabama hapo awali zilijaribu kumuua Smith mnamo Novemba mwaka juzi 2022 kwa kutumia sindano ya sumu, lakini jaribio hilo lilishindikana kwa hiyo na hili ni la kusubiri kuona.
3-1-2024 • 2 minuten, 1 seconde
UN yasema inashikamana na Japan wakati huu taifa hilo limekumbwa na tetemeko kubwa la ardhi
Harakati zikiendelea za kunasua watu waliokwama kwenye vifusi kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililokumba eneo la kati mwa Japan Jumatatu alasiri kwa saa za huko na kusababisha vifo vya watu 62, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea masikitiko yake kufuatia tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 7.6 katika kipimo cha Richa. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah MushiMsemaji wa Umoja wa Mataifa Florencia Soto Nino aliwaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani kwamba, “Katibu mkuu amehuzunishwa sana na taarifa za vifo na uharibifu wa mali uliosababishwa na tetemeko. Na ameelezea mshikamano wake na serikali ya Japan na watu wa Japan. Ametuma pia salamu za rambirambi kwa familia za waliopoteza maisha na kutakia ahueni ya haraka majeruhi.” Vyombo vya habari vinaripoti ya kuwa zaidi ya waokoaji 3,000 wamefika eneo la tukio ambalo ni katikati mwa Japan kwa ajili ya kunasua watu waliokwama kwenye vifusi huku moto ukiripotiwa kulipuka kwenye eneo hilo. Kitovu cha tetemeko hilo ni rasi ya Noto, katikati mwa Honshu ambacho ndio kisiwa kikubwa nchini Japan kinachojumuisha maeneo kama vile Tokyo, Kyoto, Osaka na Hiroshima. Bi. Soto Nino amezungumzia pia ajali ya ndege ya shirika la ndege la Japan na ndege iliyokuwa inaelekea kutoa msaada eneo la tetemeko la ardhi ambapo abiria wote kwenye ndege walinusurika ilhali wafanyakazi watano wa ndege ya misaada wamepoteza maisha. “Mawazo yetu kwa sasa yako na wananchi wa Japan na tunatumai kuwa wataweza kujikwamua kwenye hili.”
3-1-2024 • 1 minuut, 36 seconden
03 JANUARI 2024
Hii leo kwenye jarida la Habari za Umoja wa Mataifa tunamulika tetemeko la ardhi nchini Japan; Matumizi ya gesi aina ya Naitrojeni Hypoxia kuua mfungwa; Makala ni jinsi sarakasi ilivyomwezesha kijana mkimbizi kupata unafuu wa malipo na mashinani tunakwenda Afar nchini Ethiopia.Harakati zikiendelea za kunasua watu waliokwama kwenye vifusi kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililokumba eneo la kati mwa Japan Jumatatu alasiri kwa saa za huko na kusababisha vifo vya watu 62, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea masikitiko yake kufuatia tetemeko hilo lililokuwa na ukubwa wa 7.6 katika kipimo cha Richa. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.Wataalamu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa akiwemo Alice Jill Edwards, anayeshughulikia masuala yanayohusu mateso, na Adhabu nyingine za Kikatili, za kinyume cha utu au za Kushusha hadhi, leo Januari 3 mjini Geneva-Uswisi wameelezea wasiwasi wao kuhusu kukaribia kutekelezwa kwa hukumu ya kifo kwa kutumia gesi ya nitrojeni hypoxia dhidi ya Kenneth Eugene Smith hapa nchini Marekani. Mwenzangu Anold Kayanda amekifuatilia kisa hicho kwa kinaMakala: John Kibego, mwandishi wa redio washirika Kazi Njema FM huko Hoima nchini Uganda anazungumza na mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambaye kipaji chake cha kucheza sarakasi kimwezesha kupata elimu bora. Mashinani: Mama Fatuma, kutoka eneo la Afar, nchini Ethiopia ambaye mwanaye Fatuma ni mnufaika wa huduma za afya ya msingi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto, UNICEF, kwa jamii za wafugaji kuipitia kliniki tembezi ambayo inahakikisha kumfikia kila mama na kila mtoto popote alipo.
3-1-2024 • 9 minuten, 58 seconden
02 JANUARI 2024
Heir ya mwaka mpya 2024 na leo katika jarida letu la kwanza kabisa kwa mwaka huu tunakuletea Habari kwa Ufupi, Mada kwa Kina ikielelea Tanzania na Mashinani tunajikita Kenya. Mwenyeji wako ni Leah Mushi.Habari kwa ufupi: Tetemeko la ardhi Japan; Mashambulizi Ukraine; Mwezi wa Januari kuhamasisha kuhusu saratani ya shingo ya kizazi.Mada Kwa kina: Jinsi gani Umoja wa Mataifa kupitia mfuko wake wa maendeleo ya kilimo, IFAD imesaidia watu wa jamii ya wahadzabe nchini Tanzania kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi.Mashinani: Mratibu wa shirika lisilo la Kiserikali la Center for the Study of Adolescents, linaloendesha programu ya She Leads, lengo lao likiwa ni kuongeza ushawishi endelevu kwa wasichana na wanawake vijana katika kufanya maamuzi na mabadiliko ya kanuni za kijinsia katika kusongesha lengo namba 5 la Umoja wa Mataifa la usawa wa kijinsia..
2-1-2024 • 9 minuten, 58 seconden
Mfumo wa AFCAFIM unaoratibiwa na IFAD wawezesha wakulima Kenya kuhimili mabadiliko ya tabianchi
Kwa miaka 45, mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo , IFAD umekuwa ukifadhili wakulima wadogo wadogo na maendeleo vijijini. IFAD inakuwa kama mratibu kwa kushirikiana na benki binafsi na sasa kuna mfumo wa fedha wa kuwezesha wakulima Afrika kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi au ARCAFIM. Mfumo huo umewezesha kupatikana kwa dola milioni 700 za uwekezaji kutoka sekta binafsi kwenye kwa wakulima wadogo huko Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda, ili kutokomeza umaskini na njaa katika maeneo ya vijijini ya nchi zinazoendelea. Je, ni kwa jinsi gani wameweza kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi? Kupitia video iliyoandaliwa na IFAD, Pamela Awuori wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amefuatilia mafanikio ya wakulima wadogo wadogo nchini Kenya, ungana naye.
29-12-2023 • 2 minuten, 40 seconden
Nchini Niger ILO yanusuru wanawake na mfumo wa utumwa
29-12-2023 • 2 minuten, 16 seconden
Ili kusaidia kukabili mapigano mashariki mwa nchi, kikosi cha kwanza cha SADC chawasili DRC
29-12-2023 • 1 minuut, 37 seconden
29 DESEMBA 2023
Miongoni mwa yaliyomo kwenye Jarida la Habar iza UN:Kikosi cha kwanza cha SADC chawasili DRC.ILO yanusuru wanawake na mfumo wa utumwa nchini Niger.Makala leo tunakwenda Kenya kumulika jinsi mfumo wa fedha wa kuwezesha wakulima kukabiliana na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi.Na mashinani na fursa ni yake Agnes Abisa, Afisa Habari na Mawasiliano wa YUNA ambayo ni Jumuiya ya Vijana ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
29-12-2023 • 9 minuten, 59 seconden
28 DESEMBA 2023
Hujambo na karibu kusikiliza jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ikiwa ni Alhamisi ya tarehe 28 ya mwezi Desemba takribani siku 4 panapo majaliwa kuumaliza mwaka huu wa 2023. Mimi ni ASSUMPTA MASSOI ninakukaribisha kusikiliza mkusanyiko wa matukio machache kati ya mengi yaliyojiri katika mwaka huu ambapo Umoja wa Mataifa ulikuwa na jukumu zito kuhakikisha pamoja na yote bado dunia inasalia kuwa mahali salama pa kuishi.
28-12-2023 • 14 minuten, 9 seconden
Zaidi ya wakazi 500 Beni, DRC wanufaika na matibabu bure kutoka MONUSCO
Mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC takribani watu 500 wamenufaika na matibabu ya bure yanayotolewa na walinda aman iwa Umoja wa Mataifa kutoka India, wanaohudumu kwenye ujumbe wa umoja huo wa kulinda amani nchini humo MONUSCO. Evarist Mapesa na taarifa zaidi.Miongoni mwa wanufaika hao ni Samson Muvu, Mkuu wa kitongoji cha Paida hapa mjini Beni, akizungumza kupitia video ya MONUSCO akiwa kwenye kituo cha matibabu kinachoendeshwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka India anaelezea vile ambavyo waliagizwa na mkuu wa kitongoji cha Ruwenzori kwenda kuhamasisha watu kufika hapa kupata matibabu ya bure.Bwana Muvu anasema, "nikaona na mimi kama kiongozi nije nipate dawa kwa sababu mwili hauko vizuri. »Mwingine ni Kamate Masika ambaye anasema, "mimi ni mkimbizi kutoka Mbao Oicha, Niko hapa Beni. Tangu ile vita ya kila siku wanachinja watu, mimi nasikia mwili unachoka, na mishipa yote inauma. Sina amani. Wakati Niko hapa mwili unaendelea kuuma ndio jirani yangu akanionesha jinsi ya usaidizi wa dawa iko MONUSCO kwani yeye amepata yake. Na ndio niliamua kuja ili nitunzwe.”Kamate alipata pia msongo wa mawazo na kiwewe kwani alishuhudia jamaa zake pia wakichinjwa.Anne- Marie Kave anasema ni mara ya pili amefika hapa. Awali alikwenda kwingineko na kulipa jumla ya dola 180. Anasema jambo jema ni kwamba “nilipofika hapa dawa ya bure ya askari. Naamini nitalima. Nitafanya kazi ya shamba. Sikufanya kazi ya shamba kutokana na maumivu ya kiuno.”Dkt. Kowsalya mlinda amani huyu wa MONUSCO kutoka India ni mshauri mtabibu na anasema “watu wanakuja hapa na magonjwa ya kawaida kama vile Mafua, Malaria, homa ya matumbo, maumivu ya mgongo, kichwa, kisukari na moyo. Tunawapatia matibabu na wanaridhika pian a matibabu.”
27-12-2023 • 2 minuten, 14 seconden
Fahamu jinsi Nukta Fakti ilivyosaidia lishe bora kwa watoto kupitia mtandao
Leo katika makala tunakwenda Tanzania kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Afrika Nuzulack Dausen ambaye pia mwanzilishi wa Jiko point inayojihusisha zaidi na utoaji habari sahihi kuhusu uhakika wa chakula na lishe, jambo ambalo linapigiwa upatu kila uchao na Umoja wa Mataifa. Amezungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Stella Vuzo afisa habari wa Umoja wa Mataifa kufahamu kwa undani wanachokifanya katika kutimiza azma hiyo na anaanza kwa kueleza Jiko point ni nini hasa?
27-12-2023 • 3 minuten, 22 seconden
DRC: Asante MONUSCO kwa kuniepusha kuwa mpiganaji msituni
Bila MONUSCO ningalikuwa bado msituni – Mpiganaji wa zamani DRCNchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kazi ya kuhesabu kura za Rais kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 na kuendelea katika maeneo mengine siku zilizofuata, inaendelea huku nao wanufaka wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO ambao umeanza kufunga virago, wakitoa shukrani zao. Ufafanuzi zaidi anakupataia Anold Kayanda.Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini DRC, CENI, inaendelea kutangaza matokeo ya Urais halikadhalika matokeo ya magavana, wabunge na madiwani, huku mshindi wa kiti cha Urais akitarajiwa kutangazwa tarehe 31 mwezi huu wa Desemba.Kwingineko nchini humo hususan jimboni Kivu Kaskazini, MONUSCO inaanza kufunga ofisi zake kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia ombi la serikali.Ofisi ya hivi karibuni zaidi kufungwa ni ile ya Lubero jimboni humo ambako Gentil Kakule Kombi alishukuru uwepo wa MONUSCO kwenye eneo hilo kwa miaka 21.Amesema ni kwa msaada wa MONUSCO nilitoka porini, nikasalimisha silaha na sasa nimetulia vema kabisa kwenye jamii yangu na ninashikiri kwenye harkati za ujenzi wa amani.”Anakumbuka MONUSCO kumpokea Rutshuru na kisha kusafirishwa kwa basi na kukabidhiwa kwa serikali ambako walipatiwa program ya kujumuishwa tena kwenye jamii.Gentil alijisalimisha mwaka 2015 na sasa ni mwanachama wa klabu ya soka ya Lubero inayocheza kwenye ligi ya jimbo la Kivu Kaskazini.
27-12-2023 • 1 minuut, 31 seconden
27 DESEMBA 2023
Hii leo jarida linajikita barani Afrika likianzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia uchaguzi, wapiganaji wa zamani na MONUSCO, halikdhalika Jiko Point na mashinani ni nchini Kenya.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kazi ya kuhesabu kura za Rais kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 na kuendelea katika maeneo mengine siku zilizofuata, inaendelea huku nao wanufaka wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO ambao umeanza kufunga virago, wakitoa shukrani zao. Ufafanuzi zaidi anakupataia Anold Kayanda.Mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC takribani watu 500 wamenufaika na matibabu ya bure yanayotolewa na walinda aman iwa Umoja wa Mataifa kutoka India, wanaohudumu kwenye ujumbe wa umoja huo wa kulinda amani nchini humo MONUSCO. Evarist Mapesa anafafanua zaidi.Makala: Leo inatupeleka Tanzania kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Afrika Nuzulack Dausen ambaye pia mwanzilishi wa Jiko point inayojihusisha zaidi na utoaji habari sahihi kuhusu uhakika wa chakula na lishe, jambo ambalo linapigiwa upatu kila uchao na Umoja wa Mataifa. Amezungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Stella Vuzo afisa habari wa Umoja wa Mataifa kufahamu kwa undani wanachokifanya katika kutimiza azma hiyo na anaanza kwa kueleza Jiko point ni nini hasa?Mashinani: Tutaelekea katika Kaunti ya Turkana nchini Kenya, kumsikia mvuvi ambaye ameweza kuongeza kipato chake na kupunguza upotevu wa chakula kwa msaada wa Umoja wa Mataifa
27-12-2023 • 9 minuten, 57 seconden
Baada ya mashambulizi kutoka CODECO maisha yarejea hali ya kawaida huko Fataki, Ituri
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kazi ya kuhesabu kura inaendelea baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano na kuendelea katika baadhi ya maeneo jana Alhamisi, huku ikielezwa kwamba jimboni Ituri, maisha yamerejea katika hali ya kawaida kwenye eneo la Fataki baada ya mwaka mmoja wa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo waliojihami wa kundi la CODECO. Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO imegusia zaidi kituo cha biashara cha FATAKI kilichoko mji mkuu wa Ituri, Bunia ambako CODECO kwa mwaka mzima walikuwa wakishambulia mara kwa mara. Mathalani mwezi Mei mwaka huu, CODECO walishambulia eneo la Djugu na kuua raia 38, hali iliyosababisha wakazi wengine kukimbilia eneo la Djahiba lililoko kilometa 5 kutoka kituo cha MONUSCO. Sababu ya maisha kurejea kwenye hali ya kawaida ni doria za magari na za miguu zinazofanywa na askari wa jeshi la serikali, FARDC na walinda amani wa MONUSCO kwenye eneo hilo. Usalama umeimarika, wakazi wanaendelea na biashara sambamba na ukulima mashambani. Wakati huo huo, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini DRC, CENI imesema kazi ya kupiga kura kwenye maeneo yaliyoshindwa kufanya hivyo imekamilika jana Alhamisi na kwamba hakuna eneo lolote lile lililopiga kura leo Ijumaa. Matokeo rasmi ya uchaguzi wa Rais yanatarajiwa kutangazwa tarehe 31 mwezi huu na kisha Rais mteule ataapishwa tarehe 24 Januari mwaka 2024.
22-12-2023 • 0
Baada ya mashambulizi kutoka CODECO maisha yarejea hali ya kawaida huko Fataki, Ituri
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kazi ya kuhesabu kura inaendelea baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano na kuendelea katika baadhi ya maeneo jana Alhamisi, huku ikielezwa kwamba jimboni Ituri, maisha yamerejea katika hali ya kawaida kwenye eneo la Fataki baada ya mwaka mmoja wa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo waliojihami wa kundi la CODECO. Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO imegusia zaidi kituo cha biashara cha FATAKI kilichoko mji mkuu wa Ituri, Bunia ambako CODECO kwa mwaka mzima walikuwa wakishambulia mara kwa mara. Mathalani mwezi Mei mwaka huu, CODECO walishambulia eneo la Djugu na kuua raia 38, hali iliyosababisha wakazi wengine kukimbilia eneo la Djahiba lililoko kilometa 5 kutoka kituo cha MONUSCO. Sababu ya maisha kurejea kwenye hali ya kawaida ni doria za magari na za miguu zinazofanywa na askari wa jeshi la serikali, FARDC na walinda amani wa MONUSCO kwenye eneo hilo. Usalama umeimarika, wakazi wanaendelea na biashara sambamba na ukulima mashambani. Wakati huo huo, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini DRC, CENI imesema kazi ya kupiga kura kwenye maeneo yaliyoshindwa kufanya hivyo imekamilika jana Alhamisi na kwamba hakuna eneo lolote lile lililopiga kura leo Ijumaa. Matokeo rasmi ya uchaguzi wa Rais yanatarajiwa kutangazwa tarehe 31 mwezi huu na kisha Rais mteule ataapishwa tarehe 24 Januari mwaka 2024.
22-12-2023 • 1 minuut, 20 seconden
22 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini DRC na hali ya usalama katika ukanda wa Gaza. Makala tuankuletea ujumbe wa mwanariadha Violah Cheptoo kutoka Kenya na mashinani tuankupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu mazingira na haki za watoto. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kazi ya kuhesabu kura inaendelea baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano na kuendelea katika baadhi ya maeneo jana Alhamisi, huku ikielezwa kwamba jimboni Ituri, maisha yamerejea katika hali ya kawaida kwenye eneo la Fataki baada ya mwaka mmoja wa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo waliojihami wa kundi la CODECO.Njaa imeukumba Ukanda wa Gaza kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na hivyo kutishia ongezeko la magonjwa hususan miongoni mwa watoto, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha na makundi mengine yaliyo hatarini na nishati ya kupikia nayo imeota mbawa.Katika makala Assumpta Massoi anazungumza na mwanariadha wa kimataifa kutoka Kenya wakati alipotembelea hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani mwezi Novemba mwaka huu kwani Umoja wa Mataifa unapigia chepuo michezo kwa afya, ustawi na amani. Mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu haki za Watoto. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
22-12-2023 • 0
22 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini DRC na hali ya usalama katika ukanda wa Gaza. Makala tuankuletea ujumbe wa mwanariadha Violah Cheptoo kutoka Kenya na mashinani tuankupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu mazingira na haki za watoto. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kazi ya kuhesabu kura inaendelea baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano na kuendelea katika baadhi ya maeneo jana Alhamisi, huku ikielezwa kwamba jimboni Ituri, maisha yamerejea katika hali ya kawaida kwenye eneo la Fataki baada ya mwaka mmoja wa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo waliojihami wa kundi la CODECO.Njaa imeukumba Ukanda wa Gaza kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na hivyo kutishia ongezeko la magonjwa hususan miongoni mwa watoto, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha na makundi mengine yaliyo hatarini na nishati ya kupikia nayo imeota mbawa.Katika makala Assumpta Massoi anazungumza na mwanariadha wa kimataifa kutoka Kenya wakati alipotembelea hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani mwezi Novemba mwaka huu kwani Umoja wa Mataifa unapigia chepuo michezo kwa afya, ustawi na amani. Mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu haki za Watoto. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
22-12-2023 • 9 minuten, 58 seconden
WHO inaonya kwamba njaa inaongezeka Gaza hakuna chakula wala nishati ya kupikia na kukaribisha magonjwa zaidi
Njaa imeukumba Ukanda wa Gaza kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na hivyo kutishia ongezeko la magonjwa hususan miongoni mwa watoto, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha na makundi mengine yaliyo hatarini na nishati ya kupikia nayo imeota mbawa. Majira ya mchana mlo unandaliwa katika eneo la Rafah kwa ajili ya wakimbizi wa ndani wakishuhudia kwa hamu kubwa na zana zao mikononi mabakuli , vikombe na hata masufuria. Mlo wenyewe ni uji unaopikwa katika masufuria makubwa na kwa ukosefu wa gesi unapikwa kwenye kuni ambazo sasa ni adimu na ndio nishati pekee inayotegemewa.WHO inaonya kwamba Gaza inakabiliwa na viwango vikubwa vya ukosefu wa chakula na kila siku kuwa hatarini kukumbwa na baa la njaa. Watu hawa hawana chochote kama anavyoema mmoja wa wapishi ambaye pia ni mkimbizi wa ndani,“Vita hii imetudhalilisha kwa kiwango kisichoelezeka, Tunataabika na kudhalilika ili tu tupate mmlo wa mchana. Maisha hapa yamekuwa ghali sana hatuwezi kumudu, hatuli, hatunywi wala kulala vizuri na hakuna kinachopatikana.”Uji sasa tayari na unaanza kugawiwa, mwenye kikombe, mwenye bakuli haya ili mradi kila mtu anagombea maana huenda huu ndio mlo pekee atakaoupata kwa siku hii watu ni wengi. Mpishi huyu anaongeza, “Inachukua dadika 45 kwenda kwa mguu kufuata chakula hii na dakika 45 zingine kurudi ili nipike na kuwagawia , sijui nisema nini zaidi , hali ni ngumu sana.”Katika baadhi ya mitaa ya Rafah kuna vitu vichache vinavyouzwa kama vile vyakula vya makopo na barabarani kina mama na baba lishe wanajitahidi kupika wakipatacho na kuuza. Mkimbizi huyu wa ndani aliyekuja kununua chakula hicho anasema “Leo hii tuko katika hali mbya sana kwenye makazi ya muda, kuna vurugu, machafuko na mambo yasiyowezekana, sisi si watu wabaya , hata msaada wa chakula unaotolewa na UNRWA na mashirika mengine ni gharama kuuandaa na kupika kuliko hata thamani yake. Watu hawawezi kununua au kuandaa chakula kutokana na ukosefu wa gesi.”Wakimbizi hawa wa ndani wanasema watoto wao wengi sasa ni wagonjwa wana mafua, kukohoa matatizo ya tumbo na huduma ni haba. Mafuta pia hayapatikani wenye magari sasa wakilazimika kujaza matanki yao kwa mabaki ya mafuta ya kupikia na si salama kwa afya zao.Kwa mujibu wa WHO kuna wagonjwa zaidi ya 100,000 wa kuhara Gaza tangu katikati ya Oktoba na nusu yao ni watoto wa umri wa chini ya miaka 5 na pia kuna wagonjwa zaidi ya 150,000 wa magonjwa ya mfumo wa hewa, lakini pia uti wa mgongo, upele, wenye chawa na tetekuanga.
22-12-2023 • 0
WHO inaonya kwamba njaa inaongezeka Gaza hakuna chakula wala nishati ya kupikia na kukaribisha magonjwa zaidi
Njaa imeukumba Ukanda wa Gaza kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na hivyo kutishia ongezeko la magonjwa hususan miongoni mwa watoto, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha na makundi mengine yaliyo hatarini na nishati ya kupikia nayo imeota mbawa. Majira ya mchana mlo unandaliwa katika eneo la Rafah kwa ajili ya wakimbizi wa ndani wakishuhudia kwa hamu kubwa na zana zao mikononi mabakuli , vikombe na hata masufuria. Mlo wenyewe ni uji unaopikwa katika masufuria makubwa na kwa ukosefu wa gesi unapikwa kwenye kuni ambazo sasa ni adimu na ndio nishati pekee inayotegemewa.WHO inaonya kwamba Gaza inakabiliwa na viwango vikubwa vya ukosefu wa chakula na kila siku kuwa hatarini kukumbwa na baa la njaa. Watu hawa hawana chochote kama anavyoema mmoja wa wapishi ambaye pia ni mkimbizi wa ndani,“Vita hii imetudhalilisha kwa kiwango kisichoelezeka, Tunataabika na kudhalilika ili tu tupate mmlo wa mchana. Maisha hapa yamekuwa ghali sana hatuwezi kumudu, hatuli, hatunywi wala kulala vizuri na hakuna kinachopatikana.”Uji sasa tayari na unaanza kugawiwa, mwenye kikombe, mwenye bakuli haya ili mradi kila mtu anagombea maana huenda huu ndio mlo pekee atakaoupata kwa siku hii watu ni wengi. Mpishi huyu anaongeza, “Inachukua dadika 45 kwenda kwa mguu kufuata chakula hii na dakika 45 zingine kurudi ili nipike na kuwagawia , sijui nisema nini zaidi , hali ni ngumu sana.”Katika baadhi ya mitaa ya Rafah kuna vitu vichache vinavyouzwa kama vile vyakula vya makopo na barabarani kina mama na baba lishe wanajitahidi kupika wakipatacho na kuuza. Mkimbizi huyu wa ndani aliyekuja kununua chakula hicho anasema “Leo hii tuko katika hali mbya sana kwenye makazi ya muda, kuna vurugu, machafuko na mambo yasiyowezekana, sisi si watu wabaya , hata msaada wa chakula unaotolewa na UNRWA na mashirika mengine ni gharama kuuandaa na kupika kuliko hata thamani yake. Watu hawawezi kununua au kuandaa chakula kutokana na ukosefu wa gesi.”Wakimbizi hawa wa ndani wanasema watoto wao wengi sasa ni wagonjwa wana mafua, kukohoa matatizo ya tumbo na huduma ni haba. Mafuta pia hayapatikani wenye magari sasa wakilazimika kujaza matanki yao kwa mabaki ya mafuta ya kupikia na si salama kwa afya zao.Kwa mujibu wa WHO kuna wagonjwa zaidi ya 100,000 wa kuhara Gaza tangu katikati ya Oktoba na nusu yao ni watoto wa umri wa chini ya miaka 5 na pia kuna wagonjwa zaidi ya 150,000 wa magonjwa ya mfumo wa hewa, lakini pia uti wa mgongo, upele, wenye chawa na tetekuanga.
22-12-2023 • 1 minuut, 56 seconden
Jifunze Kiswahili: Tofouti ya matumizi ya "Habari kwa ufupi na Muhtasari wa habari"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua tofauti ya maneno “HABARI KWA UFUPI NA MUHTASARI WA HABARI”
21-12-2023 • 0
Jifunze Kiswahili: Tofouti ya matumizi ya "Habari kwa ufupi na Muhtasari wa habari"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua tofauti ya maneno “HABARI KWA UFUPI NA MUHTASARI WA HABARI”
21-12-2023 • 1 minuut, 2 seconden
21 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo mwezi Agosti mwaka huu wa 2023, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kutangaza tarehe 21 mwezi Desemba kila mwaka kuwa siku ya mpira wa kikapu duniani. Hii ni kwa kutambua nafasi ya mchezo huu katika kuleta amani, maendeleo na ustawi wa jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na ufafanuzi wa tofouti ya maneno. Mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kusisitiza wito wa usitishwaji mapigano Gaza kwani hali inazidi kuwa mbaya kila uchao, lile la afya duniani WHO limesema timu yake ilifanikiwa kufika katika hospitali za Al Ahil Arab na Al Shifa Gaza kaskasini na uharibifu walioushuhudia hauelezeki. Dkt. Richard Peeperkorn akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo amesema “Wafanyikazi wetu wanakosa maneno ya kuelezea hali mbaya zaidi inayowakabili wagonjwa na wahudumu wa afya waliobaki katika hospitali hizo..Takriban watu 300,000 wamefungasha virago na kukimbia katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Sudan wa Wad Madani kwenye jimbo la Aj Jazirah kwa mujibu wa shirika la umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kufuatia wimbi jipya la mapigano ambayo pia yametawanya maelfu ya watu ndani ya jimbo hilo.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC hapo jana watu wapatao milioni 44 walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na wawakilishi wa serikali za mitaa. Rais wa tume ya uchaguzi nchini humo CENI Denis Kadima amesema wale wote walioshindwa kupiga kura jana kwa sababu mbalimbali ikiwemo mvua leo wamepiga kura zao na matokeo ya awali yameanza kubandikwa katika baadhi ya vituo huku zoezi la kuhesabu kura likiendelea nchi nzima.. Katika kujifunza Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua tofauti ya maneno. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
21-12-2023 • 0
21 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo mwezi Agosti mwaka huu wa 2023, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio la kutangaza tarehe 21 mwezi Desemba kila mwaka kuwa siku ya mpira wa kikapu duniani. Hii ni kwa kutambua nafasi ya mchezo huu katika kuleta amani, maendeleo na ustawi wa jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na ufafanuzi wa tofouti ya maneno. Mashirika ya Umoja wa Mataifa leo yameendelea kusisitiza wito wa usitishwaji mapigano Gaza kwani hali inazidi kuwa mbaya kila uchao, lile la afya duniani WHO limesema timu yake ilifanikiwa kufika katika hospitali za Al Ahil Arab na Al Shifa Gaza kaskasini na uharibifu walioushuhudia hauelezeki. Dkt. Richard Peeperkorn akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi hii leo amesema “Wafanyikazi wetu wanakosa maneno ya kuelezea hali mbaya zaidi inayowakabili wagonjwa na wahudumu wa afya waliobaki katika hospitali hizo..Takriban watu 300,000 wamefungasha virago na kukimbia katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Sudan wa Wad Madani kwenye jimbo la Aj Jazirah kwa mujibu wa shirika la umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM kufuatia wimbi jipya la mapigano ambayo pia yametawanya maelfu ya watu ndani ya jimbo hilo.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC hapo jana watu wapatao milioni 44 walijitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na wawakilishi wa serikali za mitaa. Rais wa tume ya uchaguzi nchini humo CENI Denis Kadima amesema wale wote walioshindwa kupiga kura jana kwa sababu mbalimbali ikiwemo mvua leo wamepiga kura zao na matokeo ya awali yameanza kubandikwa katika baadhi ya vituo huku zoezi la kuhesabu kura likiendelea nchi nzima.. Katika kujifunza Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua tofauti ya maneno. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
21-12-2023 • 10 minuten, 59 seconden
UN: Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Binadamu ni kusherehekea Umoja wetu katika tofauti zetu
DAFI, Mfuko wa Ufadhili wa Kimasomo kwa Wakimbizi, kwa kushirikiana na UNHCR wanawasaidia wakimbizi kutimiza ndoto zao za kupata elimu ya juu katika nchi ya kwanza wanakopata hifadhi baada ya kuzikimbia nchi zao. Idadi ya waliokwisha kunufaika na ufadhili wa DAFI inazidi kuongezeka lakini takwimu za hivi karibuni zinaonesha angalau hadi kufikia mwaka jana 2022 DAFI ilipotimiza miaka 30 tangu kuanziswa kwake, chini ya serikali ya Ujerumani na wadau wengine, tayari imewafadhili wakimbizi zaidi ya 24,000 kusoma elimu za juu iwe vyuo vikuu au vyuo vingine vya ujuzi.Kwa leo tuchukue mfano mdogo tu wa nchini Rwanda. DAFI imewasaidia zaidi ya wanafunzi wakimbizi 500 tangu mwaka 2010 nchini humo. Wanafunzi 154 kati yao hivi sasa wanasoma katika ngazi ya chuo kikuu. Tuchukue wawili tu kuwawakilisha wengine mmoja anamalizia na mwingine ameshahitimu.Eric Nshizirungu, mkimbizi kutoka DR Congo mkazi wa Kambi ya wakimbizi Kiziba nchini Rwanda yuko katika mwaka wake wa mwisho wa masomo akisoma Ufamasia katika Chuo Kikuu cha Rwanda, kampasi ya Remera, "Nia yangu katika masomo yanayohusiana na afya ni kwa sababu kadhaa kama vile kukulia katika kambi ya wakimbizi, kukabiliwa na changamoto nyingi ambapo afya inafunikwa na majanga mengine ya kibinadamu kama vile chakula, malazi na mengine. Kwa hiyo, niliendeleza azma hiyo kwamba siku moja hata kama sitafanikiwa nikiwa kambini, labda nitafanikiwa nikiwa sehemu nyingine, lakini nitaisaidia jamii katika masuala ya afya.”Francois Mbyirukira, naye kutoka DRC, mkazi wa Kigali lakini mwenyeji wa Kambi ya wakimbizi ya Kigeme, kusini mwa Rwanda. Baada ya kuhitimu masomo, akaanzisha biashara yake ya samani: Viti, makochi, meza, masofa mazuri, vyote unapata kwake, “Nilichagua kusomea manunuzi kwa sababu yanaendana na kile ambacho nimekuwa nikifanya kuanzia zabuni hadi ugavi. Yote ni kuhusu kufanya biashara. Kwa maoni yangu, udhamini wa DAFI umefanya kazi kubwa sana. DAFI ilinijengea kujiamini. Leo ninafanya biashara mjini Kigali. Biashara yangu imepanuka sana.”Naam hayo ni matunda ya wanadamu walio katika hali nzuri walioamua kushikamana na walio katika shida kama inavyokumbusha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Kibinadamu kuwa ni siku ya kusherehekea umoja wetu katika utofauti wetu. Mnamo mwaka 2005, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa azimio namba 60/209 lilitambua mshikamano kama moja ya tunu za kimsingi na za ulimwengu ambazo zinapaswa kuwa msingi wa uhusiano kati ya watu katika karne ya 21 na kwa maana hiyo Baraza likaamua kuitangaza tarehe 20 Desemba ya kila mwaka kuwa ya Mshikamano wa Binadamu.
20-12-2023 • 0
UN: Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Binadamu ni kusherehekea Umoja wetu katika tofauti zetu
DAFI, Mfuko wa Ufadhili wa Kimasomo kwa Wakimbizi, kwa kushirikiana na UNHCR wanawasaidia wakimbizi kutimiza ndoto zao za kupata elimu ya juu katika nchi ya kwanza wanakopata hifadhi baada ya kuzikimbia nchi zao. Idadi ya waliokwisha kunufaika na ufadhili wa DAFI inazidi kuongezeka lakini takwimu za hivi karibuni zinaonesha angalau hadi kufikia mwaka jana 2022 DAFI ilipotimiza miaka 30 tangu kuanziswa kwake, chini ya serikali ya Ujerumani na wadau wengine, tayari imewafadhili wakimbizi zaidi ya 24,000 kusoma elimu za juu iwe vyuo vikuu au vyuo vingine vya ujuzi.Kwa leo tuchukue mfano mdogo tu wa nchini Rwanda. DAFI imewasaidia zaidi ya wanafunzi wakimbizi 500 tangu mwaka 2010 nchini humo. Wanafunzi 154 kati yao hivi sasa wanasoma katika ngazi ya chuo kikuu. Tuchukue wawili tu kuwawakilisha wengine mmoja anamalizia na mwingine ameshahitimu.Eric Nshizirungu, mkimbizi kutoka DR Congo mkazi wa Kambi ya wakimbizi Kiziba nchini Rwanda yuko katika mwaka wake wa mwisho wa masomo akisoma Ufamasia katika Chuo Kikuu cha Rwanda, kampasi ya Remera, "Nia yangu katika masomo yanayohusiana na afya ni kwa sababu kadhaa kama vile kukulia katika kambi ya wakimbizi, kukabiliwa na changamoto nyingi ambapo afya inafunikwa na majanga mengine ya kibinadamu kama vile chakula, malazi na mengine. Kwa hiyo, niliendeleza azma hiyo kwamba siku moja hata kama sitafanikiwa nikiwa kambini, labda nitafanikiwa nikiwa sehemu nyingine, lakini nitaisaidia jamii katika masuala ya afya.”Francois Mbyirukira, naye kutoka DRC, mkazi wa Kigali lakini mwenyeji wa Kambi ya wakimbizi ya Kigeme, kusini mwa Rwanda. Baada ya kuhitimu masomo, akaanzisha biashara yake ya samani: Viti, makochi, meza, masofa mazuri, vyote unapata kwake, “Nilichagua kusomea manunuzi kwa sababu yanaendana na kile ambacho nimekuwa nikifanya kuanzia zabuni hadi ugavi. Yote ni kuhusu kufanya biashara. Kwa maoni yangu, udhamini wa DAFI umefanya kazi kubwa sana. DAFI ilinijengea kujiamini. Leo ninafanya biashara mjini Kigali. Biashara yangu imepanuka sana.”Naam hayo ni matunda ya wanadamu walio katika hali nzuri walioamua kushikamana na walio katika shida kama inavyokumbusha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Kibinadamu kuwa ni siku ya kusherehekea umoja wetu katika utofauti wetu. Mnamo mwaka 2005, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa azimio namba 60/209 lilitambua mshikamano kama moja ya tunu za kimsingi na za ulimwengu ambazo zinapaswa kuwa msingi wa uhusiano kati ya watu katika karne ya 21 na kwa maana hiyo Baraza likaamua kuitangaza tarehe 20 Desemba ya kila mwaka kuwa ya Mshikamano wa Binadamu.
20-12-2023 • 3 minuten, 22 seconden
UNICEF Tanzania: Chanjo ya polio sio tu inamlinda mtoto bali inaokoa maisha
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linahimiza kila nchi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wanapatiwa chanjo dhidi ya polio ugonjwa ambao sio tu unasababisha ulemavu kwa watoto lakini pia ukakatili maisha yao. Kwa msaada kutoka wakfu wa Bill na Melinda gates hivi karibuni UNICEF na shirika la afya duniani WHO nchini Tanzania walizindua kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo iliyowafikia watoto zaidi ya milioni 4. Kutana na Therezia Kaminda muhudumu wa afya ya jamii miongoni mwa wahudu wengi walioshiriki kampeni hii chanjo ya nchi nzima mjini Sumbawanga mkoani Rukwa Magharibi mwa Tanzania na anapita nyumba kwa nyumba kutoa chanjo hiyo, "Kitu kinachonifurahisha kabisa ni uelewa walio nao wananchi wangu wameelewa vizuri na wameipokea chanjo hii kwa furaha”.Kwa mujibu wa WHO kila ambukizi 1 kati ya 200 ya polio husababisha ugonjwa wa kupooza ambao hauwezi kubadilishwa na asilimia 5-10 miongoni mwa waliopooza hupoteza maisha. Pascal ni mzazi ameelimika kuhusu ugonjwa huu na amewapeleka mwanawe kupata chanjo sasa anataka elimu zaidi itolewe, “Polio ni ugonjwa unaowapata watoto wa umri wa miaka 15 kushuka chini na una athari kubwa sana, kwa hiyo ni lazima watu waendelee kuelemishwa ili wawapeleke watoto ili wapatiwe chanjo. Watoto wangu wote chanjo walipata hata kuna wakati walitoa kwa watu wazima na hata chanjo ya Corona mimi nilipata”Lengo la kampeni hii ya siku nne ni kumlinda kila mtoto na kwa Terezia uelewa kuhusu chanjo ni kitu cha msingi zaidi, “Kabla ya hata ya kuwapa chanjo kwanza huwa nataka nifahamu wanafahamu nini kuhusu chanjo hii, lakini pia nawapa elimu kwa sababu siwezi kujua kama wote wameshapata tarifa au nini.”Katika kampeni hiyo ya kuhakikisha kila mtoto anafikiwa na chanjo, watoto zaidi ya milioni 4.2 walipokea chanjo ya matone dhidi ya polio.
20-12-2023 • 0
UNICEF Tanzania: Chanjo ya polio sio tu inamlinda mtoto bali inaokoa maisha
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linahimiza kila nchi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wanapatiwa chanjo dhidi ya polio ugonjwa ambao sio tu unasababisha ulemavu kwa watoto lakini pia ukakatili maisha yao. Kwa msaada kutoka wakfu wa Bill na Melinda gates hivi karibuni UNICEF na shirika la afya duniani WHO nchini Tanzania walizindua kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo iliyowafikia watoto zaidi ya milioni 4. Kutana na Therezia Kaminda muhudumu wa afya ya jamii miongoni mwa wahudu wengi walioshiriki kampeni hii chanjo ya nchi nzima mjini Sumbawanga mkoani Rukwa Magharibi mwa Tanzania na anapita nyumba kwa nyumba kutoa chanjo hiyo, "Kitu kinachonifurahisha kabisa ni uelewa walio nao wananchi wangu wameelewa vizuri na wameipokea chanjo hii kwa furaha”.Kwa mujibu wa WHO kila ambukizi 1 kati ya 200 ya polio husababisha ugonjwa wa kupooza ambao hauwezi kubadilishwa na asilimia 5-10 miongoni mwa waliopooza hupoteza maisha. Pascal ni mzazi ameelimika kuhusu ugonjwa huu na amewapeleka mwanawe kupata chanjo sasa anataka elimu zaidi itolewe, “Polio ni ugonjwa unaowapata watoto wa umri wa miaka 15 kushuka chini na una athari kubwa sana, kwa hiyo ni lazima watu waendelee kuelemishwa ili wawapeleke watoto ili wapatiwe chanjo. Watoto wangu wote chanjo walipata hata kuna wakati walitoa kwa watu wazima na hata chanjo ya Corona mimi nilipata”Lengo la kampeni hii ya siku nne ni kumlinda kila mtoto na kwa Terezia uelewa kuhusu chanjo ni kitu cha msingi zaidi, “Kabla ya hata ya kuwapa chanjo kwanza huwa nataka nifahamu wanafahamu nini kuhusu chanjo hii, lakini pia nawapa elimu kwa sababu siwezi kujua kama wote wameshapata tarifa au nini.”Katika kampeni hiyo ya kuhakikisha kila mtoto anafikiwa na chanjo, watoto zaidi ya milioni 4.2 walipokea chanjo ya matone dhidi ya polio.
20-12-2023 • 2 minuten, 17 seconden
Uchaguzi mkuu mwaka 2023 nchini DRC wafanyika kama ilivopangwa
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, uchaguzi mkuu wa Rais, Magavana, wabunge na madiwani umefanyika hii leo kama ilivyopangwa licha ya changamoto zilizojitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Asante Flora. Ni kweli uchaguzi umefanyika kama ilivyopangwa kwani Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO imesema vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa 12 asubuhi kama ilivyopangwa, ingawa kwingine vilichelewa kufunguliwa kwa dakika kadhaa kwa sababu tofauti tofauti. Mathalani kwenye mji mkuu Kinshasa baadhi ya vituo hadi leo asubuhi kwa saa za DRC havikuwa vimepokea vifaa vya uchaguzi. Katika vituo vya Somba ne Lutulu huko Tshikapa, jimbo la Kasaï, upigaji kura ulianza kama ilivyopangwa licha ya mvua kubwa iliyoanza kunyesha saa moja asubuhi kwa saa za huko. Mvua imeripotiwa kusababisha upelekaji vifaa vya upigaji kura kuanza asubuhi huko eneo la Mbuji-Mayi. Huko jimboni Ituri, wakimbizi wa ndani walioko Mudzipela mjini Bunia, walivamia kituo cha kupigia kura na kuharibu vifaa vya kwa kuchukizwa na uamuzi wa CENi wa kuwataka wakapigie kura kwenye makazi yao huko Djugu. Wapiga kura milioni 44 walijiandikisha kupiga kura kuchagua viongozi wao ambapo wagombea wa nafasi ya urais ni 20 akiwemo rais wa sasa Felix Tshisekedi anayesaka awamu ya pili. Mchakato wa uchaguzi umekuwa na changamoto ikiwemo usafirishaji wa vifaa kwenye maeneo ya mashariki mwa nchi ambako jeshi la serikali linakabiliana na vikundi vilivyojihami. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini DRC, CENI iliomba MONUSCO isaidie usafirishaji wa vifaa na ombi liliitikiwa huku Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akisihi mazingira yawe rafiki ili kila mwenye haki ya kupiga au kupigiwa kura afanye hivyo bila vitisho vyovyote. Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi iliyotolewa CENI, matokeo yatatangazwa tarehe 31 mwezi huu wa Desemba na Rais mteule ataapishwa tarehe tarehe 24 mwezi Januari 2024.
20-12-2023 • 0
Uchaguzi mkuu mwaka 2023 nchini DRC wafanyika kama ilivopangwa
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, uchaguzi mkuu wa Rais, Magavana, wabunge na madiwani umefanyika hii leo kama ilivyopangwa licha ya changamoto zilizojitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Asante Flora. Ni kweli uchaguzi umefanyika kama ilivyopangwa kwani Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO imesema vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa 12 asubuhi kama ilivyopangwa, ingawa kwingine vilichelewa kufunguliwa kwa dakika kadhaa kwa sababu tofauti tofauti. Mathalani kwenye mji mkuu Kinshasa baadhi ya vituo hadi leo asubuhi kwa saa za DRC havikuwa vimepokea vifaa vya uchaguzi. Katika vituo vya Somba ne Lutulu huko Tshikapa, jimbo la Kasaï, upigaji kura ulianza kama ilivyopangwa licha ya mvua kubwa iliyoanza kunyesha saa moja asubuhi kwa saa za huko. Mvua imeripotiwa kusababisha upelekaji vifaa vya upigaji kura kuanza asubuhi huko eneo la Mbuji-Mayi. Huko jimboni Ituri, wakimbizi wa ndani walioko Mudzipela mjini Bunia, walivamia kituo cha kupigia kura na kuharibu vifaa vya kwa kuchukizwa na uamuzi wa CENi wa kuwataka wakapigie kura kwenye makazi yao huko Djugu. Wapiga kura milioni 44 walijiandikisha kupiga kura kuchagua viongozi wao ambapo wagombea wa nafasi ya urais ni 20 akiwemo rais wa sasa Felix Tshisekedi anayesaka awamu ya pili. Mchakato wa uchaguzi umekuwa na changamoto ikiwemo usafirishaji wa vifaa kwenye maeneo ya mashariki mwa nchi ambako jeshi la serikali linakabiliana na vikundi vilivyojihami. Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi nchini DRC, CENI iliomba MONUSCO isaidie usafirishaji wa vifaa na ombi liliitikiwa huku Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres akisihi mazingira yawe rafiki ili kila mwenye haki ya kupiga au kupigiwa kura afanye hivyo bila vitisho vyovyote. Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi iliyotolewa CENI, matokeo yatatangazwa tarehe 31 mwezi huu wa Desemba na Rais mteule ataapishwa tarehe tarehe 24 mwezi Januari 2024.
20-12-2023 • 1 minuut, 47 seconden
20 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini DRC, na kampeni ya chanjo ya polio nchini Tanzania. Makala tunamulika DAFI Scholarship Programme nchini Rwanda na mashinani tutaelekea Mkoani Kigoma, nchini Tanzania kumsikia kijina mbunifu wa majiko yanayopunguza hewa ukaa.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, uchaguzi mkuu wa Rais, Magavana, wabunge na madiwani umefanyika hii leo kama ilivyopangwa licha ya changamoto zilizojitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Assumpta Massoi amefuatiliana na kutuandalia ripoti hii.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linahimiza kila nchi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wanapatiwa chanjo dhidi ya polio ugonjwa ambao sio tu unasababisha ulemavu kwa watoto lakini pia ukakatili maisha yao.Katika makala ambayo kwa kuzingatia kuwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Binadamu, Anold Kayanda anaangazia ‘DAFI Scholarship Programme’ ambao ni Mfuko wa Ufadhili wa Kimasomo kwa ajili ya wakimbizi unaopewa nguvu na Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR). Mashinani tunakupeleka Mkoani Kigoma, nchini Tanzania kumsikia kijina mbunifu wa majiko yanayopunguza hewa ukaa. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
20-12-2023 • 0
20 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini DRC, na kampeni ya chanjo ya polio nchini Tanzania. Makala tunamulika DAFI Scholarship Programme nchini Rwanda na mashinani tutaelekea Mkoani Kigoma, nchini Tanzania kumsikia kijina mbunifu wa majiko yanayopunguza hewa ukaa.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, uchaguzi mkuu wa Rais, Magavana, wabunge na madiwani umefanyika hii leo kama ilivyopangwa licha ya changamoto zilizojitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Assumpta Massoi amefuatiliana na kutuandalia ripoti hii.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linahimiza kila nchi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wanapatiwa chanjo dhidi ya polio ugonjwa ambao sio tu unasababisha ulemavu kwa watoto lakini pia ukakatili maisha yao.Katika makala ambayo kwa kuzingatia kuwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Binadamu, Anold Kayanda anaangazia ‘DAFI Scholarship Programme’ ambao ni Mfuko wa Ufadhili wa Kimasomo kwa ajili ya wakimbizi unaopewa nguvu na Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR). Mashinani tunakupeleka Mkoani Kigoma, nchini Tanzania kumsikia kijina mbunifu wa majiko yanayopunguza hewa ukaa. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
20-12-2023 • 11 minuten, 5 seconden
19 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo kesho nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ni uchaguzi mkuu ikiwa ni tamati ya kampeni huku Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umeshiriki kwa kusafirisha sio tu vifaa vya uchaguzi lakini pia kuelimisha wananchi jinsi ya kukabili na kuzia habari potofu na za uongo kwani ni tisho la amani na usalama. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.Leo Umoja wa Mataifa umeonya kwamba Gaza ni mahali hatari zaidi kuishi kwa watoto. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, James Elder amesema, “Siku baada ya siku ukatili wa hali ya juu unadhihirika. Katika saa 48 zilizopita hospitali kubwa Zaidi iliyobaki inafanyakazi imeshambuliwa mara mbili...Nchini Sudan shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limesema linatiwa wasiwasi kubwa na kiwango cha janga la watu wanaoendelea kulazimika kutawanywa ndani ya Sudan na katika nchi Jirani.Na ripoti mpya "Hali ya mifumo ya chakula duniani kote katika kuelekea mwaka 2030", iliyochapishwa leo na mradi wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO unaoangia mifumo hiyo kuelekea ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030 (FSCI), inatoa tathimini ya kwanza ya ufuatiliaji wa kisayansi ili kuwaongoza watoa maamuzi wanapotaka kufanya mabadiliko ya jumla ya kilimo cha kimataifa na mifumo ya chakula. Mashinani tunakupeleka nchini Somalia kusikia ujumbe kuhusu uwezo wa filamu katika simulizi ya hadithi za utamaduni na haki za binadamu. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
19-12-2023 • 0
19 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo kesho nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ni uchaguzi mkuu ikiwa ni tamati ya kampeni huku Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umeshiriki kwa kusafirisha sio tu vifaa vya uchaguzi lakini pia kuelimisha wananchi jinsi ya kukabili na kuzia habari potofu na za uongo kwani ni tisho la amani na usalama. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.Leo Umoja wa Mataifa umeonya kwamba Gaza ni mahali hatari zaidi kuishi kwa watoto. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, James Elder amesema, “Siku baada ya siku ukatili wa hali ya juu unadhihirika. Katika saa 48 zilizopita hospitali kubwa Zaidi iliyobaki inafanyakazi imeshambuliwa mara mbili...Nchini Sudan shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limesema linatiwa wasiwasi kubwa na kiwango cha janga la watu wanaoendelea kulazimika kutawanywa ndani ya Sudan na katika nchi Jirani.Na ripoti mpya "Hali ya mifumo ya chakula duniani kote katika kuelekea mwaka 2030", iliyochapishwa leo na mradi wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO unaoangia mifumo hiyo kuelekea ukomo wa malengo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2030 (FSCI), inatoa tathimini ya kwanza ya ufuatiliaji wa kisayansi ili kuwaongoza watoa maamuzi wanapotaka kufanya mabadiliko ya jumla ya kilimo cha kimataifa na mifumo ya chakula. Mashinani tunakupeleka nchini Somalia kusikia ujumbe kuhusu uwezo wa filamu katika simulizi ya hadithi za utamaduni na haki za binadamu. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
19-12-2023 • 11 minuten, 15 seconden
Wanazuoni waanza utafiti wa kupunguza maneno ya kigeni katika lugha ya kiswahili
Wakati wadau wa lugha ya kiswahili wakikuna vichwa namna ya kuhakikisha lugha hiyo adhimu inasambaa na kuzungumzwa duniani kote, wengine wanaendelea na utafiti kuhakikisha lugha hiyo inakuwa na maneno ya kiswahili fasaha na kupunguza mchanganyiko wa maneno ya kigeni katika lugha hiyo. Leah Mushi aliyehudhuria Kongamano la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili duniani – CHAUKIDU huko jijini Arusha nchini Tanzania ameketi chini na mwanazuoni huyo na kutuandalia makala haya.
18-12-2023 • 0
Wanazuoni waanza utafiti wa kupunguza maneno ya kigeni katika lugha ya kiswahili
Wakati wadau wa lugha ya kiswahili wakikuna vichwa namna ya kuhakikisha lugha hiyo adhimu inasambaa na kuzungumzwa duniani kote, wengine wanaendelea na utafiti kuhakikisha lugha hiyo inakuwa na maneno ya kiswahili fasaha na kupunguza mchanganyiko wa maneno ya kigeni katika lugha hiyo. Leah Mushi aliyehudhuria Kongamano la Kimataifa la Kiswahili lililoandaliwa na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili duniani – CHAUKIDU huko jijini Arusha nchini Tanzania ameketi chini na mwanazuoni huyo na kutuandalia makala haya.
18-12-2023 • 4 minuten, 36 seconden
18 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia vita katika ukanda wa Gaza, na mradi wa UNHC kwa wakimbizi Kigoma Tanzania. Makala tunakuletea mahojiano ya Wanazuoni na wataalamu wa lugha ya Kiswahili na mashinani leo ikiwa ni siku ya wahamiaji duniani tunakupeleka nchini Uganda kupata ujumbe mahsusi.Hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbayá katika Ukanda wa Gaza Mashariki ya Kati, huku hospitali zilizosalia zikiendelea kushambuliwa na kukatili maisha ya watu na kufungwa kwa mawasiliano ya simu na mtandao wa intanet vikizidisha adha yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa..Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na wadau wamewezesha kaya zinazopakana na kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma kujitengenezea mkaa mbadala na hivyo kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji miti kwa ajili ya mkaa.Makala tunakwenda mkoani Arusha kaskazini mwa Tanzania kunakofanyika kongamano la kimataifa la Kiswahili. Wanazuoni na wataalamu wa lugha ya Kiswahili ambayo ni moja kati ya lugha 10 zinazo zungumzwa zaidi duniani wameanza kufanya utafiti wa kupunguza maneno ya kigeni katika lugha hiyo.. Mashinani leo ikiwa ni siku ya wahamiaji duniani tunakupeleka nchini Uganda kupata ujumbe mahsusi. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
18-12-2023 • 0
18 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia vita katika ukanda wa Gaza, na mradi wa UNHC kwa wakimbizi Kigoma Tanzania. Makala tunakuletea mahojiano ya Wanazuoni na wataalamu wa lugha ya Kiswahili na mashinani leo ikiwa ni siku ya wahamiaji duniani tunakupeleka nchini Uganda kupata ujumbe mahsusi.Hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbayá katika Ukanda wa Gaza Mashariki ya Kati, huku hospitali zilizosalia zikiendelea kushambuliwa na kukatili maisha ya watu na kufungwa kwa mawasiliano ya simu na mtandao wa intanet vikizidisha adha yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa..Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na wadau wamewezesha kaya zinazopakana na kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma kujitengenezea mkaa mbadala na hivyo kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji miti kwa ajili ya mkaa.Makala tunakwenda mkoani Arusha kaskazini mwa Tanzania kunakofanyika kongamano la kimataifa la Kiswahili. Wanazuoni na wataalamu wa lugha ya Kiswahili ambayo ni moja kati ya lugha 10 zinazo zungumzwa zaidi duniani wameanza kufanya utafiti wa kupunguza maneno ya kigeni katika lugha hiyo.. Mashinani leo ikiwa ni siku ya wahamiaji duniani tunakupeleka nchini Uganda kupata ujumbe mahsusi. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
18-12-2023 • 13 minuten, 16 seconden
Kaya Kigoma wameweza kuinua kipato na pia kutunza mazingira kupitia Mradi wa UNHCR
Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na wadau wamewezesha kaya zinazopakana na kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma kujitengenezea mkaa mbadala na hivyo kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji miti kwa ajili ya mkaa. Mkoani Kigoma, kaskazini magharibi mwa Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kupitia shirika la Denmark la kuhudumia wakimbizi, DRC wamefanikisha mradi wa kusaidia jamii kutengeneza mkaa kwa kutumia mabaki ya mahindi, maranda, mihogo na mawese. Wanufaika wa mafunzo yaliyotolewa na DRC ni Kikundi cha Tubadilike kinachojihusisha na uchakati wa malighafi za kutengeneza mkaa kilichoko kijiji cha Mvugwe, wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Ayoub Juma Shaban, ni Mwenyekiti wa kikundi hicho ambaye amesema walipatiwa mafunzo ya kutengeneza mkaa huo ambapo wanachanganya maranda ya mbao, magunzi ya mahindi na hutumia mabaki ya unga wa muhogo wa ajili ya kugandisha mkaa huo. Amesema wanatumia mkaa mbadala kama njia ya kuhifadhi mazingira. Badala ya kukata miti sasa wanatumia mabaki kutengeneza mkaa. Mkaa huo wanauza ujazo wa ndoo ya lita 10 kwa shilingi 1,500 sawa na dola senti 65. Bwana Iyege anasema walipatiwa mashine ya kutengeneza mkaa huo mbadala na kutokana na mauzo wanaweza kutunza familia ikiwa ni pamoja na kununulia watoto wao sare za shule.
18-12-2023 • 0
Kaya Kigoma wameweza kuinua kipato na pia kutunza mazingira kupitia Mradi wa UNHCR
Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kushirikiana na wadau wamewezesha kaya zinazopakana na kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu mkoani Kigoma kujitengenezea mkaa mbadala na hivyo kusaidia kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na ukataji miti kwa ajili ya mkaa. Mkoani Kigoma, kaskazini magharibi mwa Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kupitia shirika la Denmark la kuhudumia wakimbizi, DRC wamefanikisha mradi wa kusaidia jamii kutengeneza mkaa kwa kutumia mabaki ya mahindi, maranda, mihogo na mawese. Wanufaika wa mafunzo yaliyotolewa na DRC ni Kikundi cha Tubadilike kinachojihusisha na uchakati wa malighafi za kutengeneza mkaa kilichoko kijiji cha Mvugwe, wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Ayoub Juma Shaban, ni Mwenyekiti wa kikundi hicho ambaye amesema walipatiwa mafunzo ya kutengeneza mkaa huo ambapo wanachanganya maranda ya mbao, magunzi ya mahindi na hutumia mabaki ya unga wa muhogo wa ajili ya kugandisha mkaa huo. Amesema wanatumia mkaa mbadala kama njia ya kuhifadhi mazingira. Badala ya kukata miti sasa wanatumia mabaki kutengeneza mkaa. Mkaa huo wanauza ujazo wa ndoo ya lita 10 kwa shilingi 1,500 sawa na dola senti 65. Bwana Iyege anasema walipatiwa mashine ya kutengeneza mkaa huo mbadala na kutokana na mauzo wanaweza kutunza familia ikiwa ni pamoja na kununulia watoto wao sare za shule.
18-12-2023 • 2 minuten, 43 seconden
UN: Kushambuliwa kwa hospitali na kukatwa kwa mawasiliano ni pigo kubwa kwa mfumo wa afya na raia Gaza
Hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbayá katika Ukanda wa Gaza Mashariki ya Kati, huku hospitali zilizosalia zikiendelea kushambuliwa na kukatili maisha ya watu na kufungwa kwa mawasiliano ya simu na mtandao wa intanet vikizidisha adha yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa. Asante Anold kama ulivyosema hali si hali Gaza Maisha ya watu yanaendelea kupotea kila siku kwanza kutokana na mashambulizi lakini pia kwa kukosa huduma muhimu za afya kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ambaye kupitia ukurasa wake wa X hii leo amesisitiza kwamba “Mashambulizi dhidi ya hospitali , wahudumu wa afya na wagonjwa lazima yakome na usitishwaji mapigano ufanyike sasa”Dkt. Tedros pia amelaani vikali uharibifu mkubwa uliofanyika katika hospitali ya Kamal Adwan Kaskazini mwa Gaza baada ya kuvamiwa na vikosi vya Israel mwishoni mwa wiki ambapo wagonjwa wanane wameuawa akiwemo mtoto wa miaka 9.Ameongeza kuwa wiki iliyopita vikosi vya Israel kwa siku nne viliivamia hospitali hiyo na kuipekua ndani nje huku kukiwa na taarifa za wahudumu wengi wa afya kushikiliwa.Dkt. Tedros ameonya kwamba “Mfumo wa afya wa Gaza ambao tayari ulikuwa taaban sasa kupoteza hospitali nyingine hata kama inafanya kazi kwa kiasi kidogo ni pigo kubwa kwa watu wa Gaza.”Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema “Kutokana na kufungwa kwa mawasiliano ya simu na mtandao wa intanet Gaza nzima sasa hakuna taarifa mpya zinazopatikana za vifo na majeruhi.”Limeongeza kuwa katika Ukingo wa Magharibi tangu kuanza kwa mzozo huu mpya Wapalestina 268 wameuawa na vikosi vya Israel wakiwemo watoto 70 ikiwa ni idadi kubwa Zaidi ya vifo vya Wapalestina kwa mwaka.Shirika hilo limeonya kwamba kuendelesha kwa mashambulizi kwenye Ukanda wa Gaza kunasababisha ugumu mkubwa wa kuafikia wenye uhitaji na hivyo kuwafanya watu waendelee kuwa katikati ya vita, kuzingirwa na kukosa mahitaji.Nimalizie na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo linasema ushitishwaji haraka wa mapigano wa muda mrefu kwa minajili ya kibinadamu ni lazima kwani sasa eneo zima la Gaza ambako Watoto walikuwa wakicheza na Kwenda shuleni kufurahia utoto wao limegeuka kifusi na kuwaacha njiapanda watoto hao.
18-12-2023 • 0
UN: Kushambuliwa kwa hospitali na kukatwa kwa mawasiliano ni pigo kubwa kwa mfumo wa afya na raia Gaza
Hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbayá katika Ukanda wa Gaza Mashariki ya Kati, huku hospitali zilizosalia zikiendelea kushambuliwa na kukatili maisha ya watu na kufungwa kwa mawasiliano ya simu na mtandao wa intanet vikizidisha adha yameonya leo mashirika ya Umoja wa Mataifa. Asante Anold kama ulivyosema hali si hali Gaza Maisha ya watu yanaendelea kupotea kila siku kwanza kutokana na mashambulizi lakini pia kwa kukosa huduma muhimu za afya kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ambaye kupitia ukurasa wake wa X hii leo amesisitiza kwamba “Mashambulizi dhidi ya hospitali , wahudumu wa afya na wagonjwa lazima yakome na usitishwaji mapigano ufanyike sasa”Dkt. Tedros pia amelaani vikali uharibifu mkubwa uliofanyika katika hospitali ya Kamal Adwan Kaskazini mwa Gaza baada ya kuvamiwa na vikosi vya Israel mwishoni mwa wiki ambapo wagonjwa wanane wameuawa akiwemo mtoto wa miaka 9.Ameongeza kuwa wiki iliyopita vikosi vya Israel kwa siku nne viliivamia hospitali hiyo na kuipekua ndani nje huku kukiwa na taarifa za wahudumu wengi wa afya kushikiliwa.Dkt. Tedros ameonya kwamba “Mfumo wa afya wa Gaza ambao tayari ulikuwa taaban sasa kupoteza hospitali nyingine hata kama inafanya kazi kwa kiasi kidogo ni pigo kubwa kwa watu wa Gaza.”Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema “Kutokana na kufungwa kwa mawasiliano ya simu na mtandao wa intanet Gaza nzima sasa hakuna taarifa mpya zinazopatikana za vifo na majeruhi.”Limeongeza kuwa katika Ukingo wa Magharibi tangu kuanza kwa mzozo huu mpya Wapalestina 268 wameuawa na vikosi vya Israel wakiwemo watoto 70 ikiwa ni idadi kubwa Zaidi ya vifo vya Wapalestina kwa mwaka.Shirika hilo limeonya kwamba kuendelesha kwa mashambulizi kwenye Ukanda wa Gaza kunasababisha ugumu mkubwa wa kuafikia wenye uhitaji na hivyo kuwafanya watu waendelee kuwa katikati ya vita, kuzingirwa na kukosa mahitaji.Nimalizie na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo linasema ushitishwaji haraka wa mapigano wa muda mrefu kwa minajili ya kibinadamu ni lazima kwani sasa eneo zima la Gaza ambako Watoto walikuwa wakicheza na Kwenda shuleni kufurahia utoto wao limegeuka kifusi na kuwaacha njiapanda watoto hao.
18-12-2023 • 2 minuten, 32 seconden
Siri ya kuwa sehemu ya tuzo hii ni ushirikiano wetu - Fr. Benedict Ayodi
Hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika hafla la kupatia tuzo washindi wa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, tuzo inayotolewa kwa mtu mmoja mmoja au kundi kwa kuzingatia mchango wao kwenye kusongesha haki za binadamu. Miongoni mwa washindi wa watano ni Ushirikiano wa kimataifa wa mashirika ya kijamii, watu wa asili, harakati za kijamii na jamii za mashinani. Shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la Wafransiskani wakapuchini ni sehemu ya ushirikiano huo. Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Father Benedict Ayodi kutoka shirika hili kufahamu pamoja na mambo mengina sababu ya Ushindi wao. Lakini kwanza anaanza kwa kuelezea jinsi walivyopokea tuzo hii.
15-12-2023 • 0
Siri ya kuwa sehemu ya tuzo hii ni ushirikiano wetu - Fr. Benedict Ayodi
Hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika hafla la kupatia tuzo washindi wa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, tuzo inayotolewa kwa mtu mmoja mmoja au kundi kwa kuzingatia mchango wao kwenye kusongesha haki za binadamu. Miongoni mwa washindi wa watano ni Ushirikiano wa kimataifa wa mashirika ya kijamii, watu wa asili, harakati za kijamii na jamii za mashinani. Shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la Wafransiskani wakapuchini ni sehemu ya ushirikiano huo. Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Father Benedict Ayodi kutoka shirika hili kufahamu pamoja na mambo mengina sababu ya Ushindi wao. Lakini kwanza anaanza kwa kuelezea jinsi walivyopokea tuzo hii.
15-12-2023 • 7 minuten, 46 seconden
Ushirikiano wetu ndio siri ya kuwa sehemu ya tuzo hii – Fr. Ayodi
Hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika hafla la kupatia tuzo washindi wa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, tuzo inayotolewa kwa mtu mmoja mmoja au kundi kwa kuzingatia mchango wao kwenye kusongesha haki za binadamu. Miongoni mwa washindi wa watano ni Ushirikiano wa kimataifa wa mashirika ya kijamii, watu wa asili, harakati za kijamii na jamii za mashinani. Shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la Wafransiskani wakapuchini ni sehemu ya ushirikiano huo. Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Father Benedict Ayodi kutoka shirika hili kufahamu pamoja na mambo mengina sababu ya Ushindi wao. Lakini kwanza anaanza kwa kuelezea jinsi walivyopokea tuzo hii.
15-12-2023 • 0
Ushirikiano wetu ndio siri ya kuwa sehemu ya tuzo hii – Fr. Ayodi
Hii leo kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika hafla la kupatia tuzo washindi wa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, tuzo inayotolewa kwa mtu mmoja mmoja au kundi kwa kuzingatia mchango wao kwenye kusongesha haki za binadamu. Miongoni mwa washindi wa watano ni Ushirikiano wa kimataifa wa mashirika ya kijamii, watu wa asili, harakati za kijamii na jamii za mashinani. Shirika lisilo la kiserikali la kimataifa la Wafransiskani wakapuchini ni sehemu ya ushirikiano huo. Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Father Benedict Ayodi kutoka shirika hili kufahamu pamoja na mambo mengina sababu ya Ushindi wao. Lakini kwanza anaanza kwa kuelezea jinsi walivyopokea tuzo hii.
15-12-2023 • 3 minuten, 48 seconden
15 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tnaangazia ufunguzi wa Kongamano la nane la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), uliofanyika leo jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania, na wanariadha mashujaa wa mazingira nchini Kenya. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini Zimbabwe, kulikoni?.Baada ya Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuitambua lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kimataifa, sasa Tanzania imetangaza kwamba kwa kushirikiana na nchi nyingine wataanza kutoa Tuzo za Kimataifa za Kiswahili. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo wa Tanzania Dkt. Damas Ndumbaro amemweleza hayo mwandishi wa Idhaa hii Leah Mushi aliyehudhuria ufunguzi wa Kongamano la nane la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), uliofanyika leo jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania.Mashirika ya umoja wa Mataifa lile mazingira duniani UNEP na lile la afya WHO nchini Kenya yamehimiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira safi kwa ajili ya afya bora katika kampeni maalum iliyofanyika jana Alhamisi walipowaalika wanaridha kadhaa wa Kenya kwenye ofisi za Umoja wa mataifa jijini Nairobi.Miongoni wa wanariadha hao ni Francis Kipkoech Bowen ambaye kwa takriban miaka 20 amekuwa mkibiaji wa mbio za kawaida na marathon. Amezungumza na Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS kwanza akishukuru Umoja wa Mataifa kumjumuisha. Mashinani tnakuleta ujumbe wa mmoja wa wakimbizi nchini Zimbabwe kuhusu mchango wao katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Mwenyeji wako ni Flora, karibu!
15-12-2023 • 0
15 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tnaangazia ufunguzi wa Kongamano la nane la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), uliofanyika leo jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania, na wanariadha mashujaa wa mazingira nchini Kenya. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini Zimbabwe, kulikoni?.Baada ya Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuitambua lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kimataifa, sasa Tanzania imetangaza kwamba kwa kushirikiana na nchi nyingine wataanza kutoa Tuzo za Kimataifa za Kiswahili. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo wa Tanzania Dkt. Damas Ndumbaro amemweleza hayo mwandishi wa Idhaa hii Leah Mushi aliyehudhuria ufunguzi wa Kongamano la nane la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), uliofanyika leo jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania.Mashirika ya umoja wa Mataifa lile mazingira duniani UNEP na lile la afya WHO nchini Kenya yamehimiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira safi kwa ajili ya afya bora katika kampeni maalum iliyofanyika jana Alhamisi walipowaalika wanaridha kadhaa wa Kenya kwenye ofisi za Umoja wa mataifa jijini Nairobi.Miongoni wa wanariadha hao ni Francis Kipkoech Bowen ambaye kwa takriban miaka 20 amekuwa mkibiaji wa mbio za kawaida na marathon. Amezungumza na Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS kwanza akishukuru Umoja wa Mataifa kumjumuisha. Mashinani tnakuleta ujumbe wa mmoja wa wakimbizi nchini Zimbabwe kuhusu mchango wao katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Mwenyeji wako ni Flora, karibu!
15-12-2023 • 11 minuten, 2 seconden
CHAUKIDU: Ujio wa Tuzo ya Kiswahili ya Mwalimu Nyerere watangazwa
Baada ya Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuitambua lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kimataifa, sasa Tanzania imetangaza kwamba kwa kushirikiana na nchi nyingine wataanza kutoa Tuzo za Kimataifa za Kiswahili. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo wa Tanzania Dkt. Damas Ndumbaro amemweleza hayo mwandishi wa Idhaa hii Leah Mushi aliyehudhuria ufunguzi wa Kongamano la nane la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), uliofanyika leo jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania.“Mwakani 2024 katika kusherehekea siku ya Kiswahili duniani ambayo inatambulika na UNESCO, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine tutazindua rasmi ‘Tuzo ya kimataifa ya Kiswahili ya Mwalimu Nyerere’ ili kuenzi Kiswahili pamoja na mchango wa mwalimu Nyerere katika kuikuza lugha ya Kiswahili Tanzania, Afrika na duniani kote.”Waziri Ndumbaro amesema katika tuzo hiyo watu mbalimbali ambao wametoa mchango katika kukuza na kueneza Kiswahili duniani watatambulika nawatapewa tuzo hiyo kwa heshima ya Mwalimu Nyerere. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni Rais wa kwanza wa taifa la Tanzania ambaye mara baada ya nchi hiyo kupata uhuru alihakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya mawasiliano ya taifa lake na pia kuendelea kukitangaza katika nchi jirani katika ukanda wa Afrika Mashariki. Akiulizwa kwanini tuzo hizo hazitolewi Afrika Mashariki na badala yake zinaenda kutolewa nchini Ufaransa, Waziri huyo wa Utamaduni Sanaa na michezo wa Tanzania amesema “Tuzo hizo zinatolewa Paris kwenye ofisi za UNESCO kwa heshima ya UNESCO kutambua Kiswahili duniani lakini pia kuchagua tarehe 7 ya mwezi wa Saba kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.” Kongamano hilo lililozinduliwa leo tarehe 15 Desemba jijini Arusha, litaendelea mpaka tarehe 17 na linahudhuriwa na washiriki kutoka katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Comorrow, India, Nigeria, Italia, Marekani na Uingereza.Wahudhuriaji wa kongamano hilo ni pamoja na wawakilishi wa vyama na taasisi zinazokuza lugha za Kiswahili, wakalimani pamoja na walimu wa Kiswahili. Rais wa CHAUKIDU Dkt. Fillipo Lubua akizungumza katika uzinduzi huo amewasihi washiriki wa kongamano hilo kuzingatia maendeleo ya kidigitali katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili. Dkt. Lubua ambaye pia ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Pittsburg cha nchini Marekani ametoa mafunzo kwa washiriki wa kongamano hili juu ya kutumia Akili unde (AI) ambapo aliwafundisha matumizi bora na yenye maadili ya ChatGPT pamoja na Adobe Express ambao ni mfumo wa kutengeneza picha.
15-12-2023 • 0
CHAUKIDU: Ujio wa Tuzo ya Kiswahili ya Mwalimu Nyerere watangazwa
Baada ya Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuitambua lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kimataifa, sasa Tanzania imetangaza kwamba kwa kushirikiana na nchi nyingine wataanza kutoa Tuzo za Kimataifa za Kiswahili. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo wa Tanzania Dkt. Damas Ndumbaro amemweleza hayo mwandishi wa Idhaa hii Leah Mushi aliyehudhuria ufunguzi wa Kongamano la nane la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), uliofanyika leo jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania.“Mwakani 2024 katika kusherehekea siku ya Kiswahili duniani ambayo inatambulika na UNESCO, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau wengine tutazindua rasmi ‘Tuzo ya kimataifa ya Kiswahili ya Mwalimu Nyerere’ ili kuenzi Kiswahili pamoja na mchango wa mwalimu Nyerere katika kuikuza lugha ya Kiswahili Tanzania, Afrika na duniani kote.”Waziri Ndumbaro amesema katika tuzo hiyo watu mbalimbali ambao wametoa mchango katika kukuza na kueneza Kiswahili duniani watatambulika nawatapewa tuzo hiyo kwa heshima ya Mwalimu Nyerere. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni Rais wa kwanza wa taifa la Tanzania ambaye mara baada ya nchi hiyo kupata uhuru alihakikisha Kiswahili kinakuwa lugha rasmi ya mawasiliano ya taifa lake na pia kuendelea kukitangaza katika nchi jirani katika ukanda wa Afrika Mashariki. Akiulizwa kwanini tuzo hizo hazitolewi Afrika Mashariki na badala yake zinaenda kutolewa nchini Ufaransa, Waziri huyo wa Utamaduni Sanaa na michezo wa Tanzania amesema “Tuzo hizo zinatolewa Paris kwenye ofisi za UNESCO kwa heshima ya UNESCO kutambua Kiswahili duniani lakini pia kuchagua tarehe 7 ya mwezi wa Saba kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani.” Kongamano hilo lililozinduliwa leo tarehe 15 Desemba jijini Arusha, litaendelea mpaka tarehe 17 na linahudhuriwa na washiriki kutoka katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Comorrow, India, Nigeria, Italia, Marekani na Uingereza.Wahudhuriaji wa kongamano hilo ni pamoja na wawakilishi wa vyama na taasisi zinazokuza lugha za Kiswahili, wakalimani pamoja na walimu wa Kiswahili. Rais wa CHAUKIDU Dkt. Fillipo Lubua akizungumza katika uzinduzi huo amewasihi washiriki wa kongamano hilo kuzingatia maendeleo ya kidigitali katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili. Dkt. Lubua ambaye pia ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Pittsburg cha nchini Marekani ametoa mafunzo kwa washiriki wa kongamano hili juu ya kutumia Akili unde (AI) ambapo aliwafundisha matumizi bora na yenye maadili ya ChatGPT pamoja na Adobe Express ambao ni mfumo wa kutengeneza picha.
15-12-2023 • 1 minuut, 35 seconden
UNEP/WHO: Afya na mazingira ni lila la fila havitengamani
Mashirika ya umoja wa Mataifa lile mazingira duniani UNEP na lile la afya WHO nchini Kenya yamehimiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira safi kwa ajili ya afya bora katika kampeni maalum iliyofanyika jana Alhamisi walipowaalika wanaridha kadhaa wa Kenya kwenye ofisi za Umoja wa mataifa jijini Nairobi. Lengo ni kuzungumza na wanariadha hao kuhusu uhusiano uliopo baina ya mazingira na afya bora ili watambue na kuwa msitari wa mbele kuchagiza hilo katika tasnia yao ambayo mara nyingi hufanyika katika maeneo ya wazi na hewa safi ni muhimu. Miongoni wa wanariadha hao ni Francis Kipkoech Bowen ambaye kwa takriban miaka 20 amekuwa mkibiaji wa mbio za kawaida na marathon. Amezungumza na Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS kwanza akishukuru Umoja wa Mataifa kumjumuisha.“ Nimefurahia sana kuwa hapa UN, kuwa hapa UNEP wakishirikiana na WHO , nimefurahia kmakaribisho, nimeona wanatumikia watu kwa njia nzuri.”Ni kipi ulichojifunza kutokana na mazungumzo yenu na WHOP na UNEP,“Mambo ya hali ya hewa na afya vinaambatana pamoja na kitu kizuri kufundisha hata kizazi kijacho ili tuwe na afya bora wakati wote.”Kitu gani hasa kilichokugusa?“Haswa mambo ya maji na hewa safi “Kama mkimbiaji unafikiri hewa safi ni muhimu sana kwako?“Ni muhimu kwa sababu ile hewa unayovuta ni muhimu nzuri na muhimu kwa afya ya kila mtu na hasa yale mazingira unayoishi kuwa mazuri.”Kwa mujibu wa UNEP na WHO mazingira na afya ni lila na fila havitengamani.
15-12-2023 • 0
UNEP/WHO: Afya na mazingira ni lila la fila havitengamani
Mashirika ya umoja wa Mataifa lile mazingira duniani UNEP na lile la afya WHO nchini Kenya yamehimiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira safi kwa ajili ya afya bora katika kampeni maalum iliyofanyika jana Alhamisi walipowaalika wanaridha kadhaa wa Kenya kwenye ofisi za Umoja wa mataifa jijini Nairobi. Lengo ni kuzungumza na wanariadha hao kuhusu uhusiano uliopo baina ya mazingira na afya bora ili watambue na kuwa msitari wa mbele kuchagiza hilo katika tasnia yao ambayo mara nyingi hufanyika katika maeneo ya wazi na hewa safi ni muhimu. Miongoni wa wanariadha hao ni Francis Kipkoech Bowen ambaye kwa takriban miaka 20 amekuwa mkibiaji wa mbio za kawaida na marathon. Amezungumza na Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS kwanza akishukuru Umoja wa Mataifa kumjumuisha.“ Nimefurahia sana kuwa hapa UN, kuwa hapa UNEP wakishirikiana na WHO , nimefurahia kmakaribisho, nimeona wanatumikia watu kwa njia nzuri.”Ni kipi ulichojifunza kutokana na mazungumzo yenu na WHOP na UNEP,“Mambo ya hali ya hewa na afya vinaambatana pamoja na kitu kizuri kufundisha hata kizazi kijacho ili tuwe na afya bora wakati wote.”Kitu gani hasa kilichokugusa?“Haswa mambo ya maji na hewa safi “Kama mkimbiaji unafikiri hewa safi ni muhimu sana kwako?“Ni muhimu kwa sababu ile hewa unayovuta ni muhimu nzuri na muhimu kwa afya ya kila mtu na hasa yale mazingira unayoishi kuwa mazuri.”Kwa mujibu wa UNEP na WHO mazingira na afya ni lila na fila havitengamani.
15-12-2023 • 1 minuut, 48 seconden
METHALI: MSASI HAOGOPI MIIBA
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalamu wetu Nicholus Makanji, Mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya anatufafanulia maana ya methali MSASI HAOGOPI MIIBA.
14-12-2023 • 0
METHALI: MSASI HAOGOPI MIIBA
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalamu wetu Nicholus Makanji, Mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya anatufafanulia maana ya methali MSASI HAOGOPI MIIBA.
14-12-2023 • 0
14 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamulika kazi za mshindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Julienne Lusenge kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye shirika aliloanzisha la SOFEPADI limenasua wanawake kutoka kwenye ukatili wa kijinsia na kingono, sambamba na utumikishwaji, Mashariki mwa nchi hiyo. Tumekuandalia pia habari kwa ufupi na uchmbuzi wa methali.Mvua kubwa imesababisha maafa mapya huko Gaza huku wasaidizi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wakirudia kueleza wasiwasi wao kuhusu kuzorota kwa hali ya afya katika Ukanda huo,wakati kukiwa bado na mashambulizi yanayoendelea kati ya Israel na makundi yenye silaha ya Palestina. Ofisi ya Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura (OCHA) imesema kuwa maeneo mengi katika eneo hilo yamefurika, "na kuzidisha mahangaiko ya Wapalestina waliokimbia makazi yao.Jukwaa la pili la kimataifa la wakimbizi, GRF, linalowakutanisha takribani watu 4000 kutoka nchi 165 limeingia siku yake ya pili leo huko Geneva, Uswisi ambapo washiriki wanatoa ahadi zao kuhusu namna bora ya kushughulikia suala la wakimbizi. Katika tamko la Kenya lililochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa mkutano huo, Kenya imeeleza namna ilivyotekeleza ahadi yake iliyotoa kwenye mkutano wa kwanza miaka minne iliyopita kwa kuwapa uraia Washona, Wamakonde na Wapemba. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, ili kuwalinda watoto limetoa wito wa kutaka serikali kote duniani zichukue hatua za haraka dhidi ya sigara za kisasa zilizoundwa kwa mfumo wa umeme yaani e-cigarettes. Kupitia wito huo, WHO imeonesha watoto wenye umri wa miaka 13-15 wanatumia sigara za kielektroniki kwa viwango vya juu kuliko watu wazima kote duniani. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalamu wetu leo ni Nicholus Makanji mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya akitufafanulia maana ya methali « MSASI HAOGOPI MIIBA». Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
14-12-2023 • 0
14 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamulika kazi za mshindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu Julienne Lusenge kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye shirika aliloanzisha la SOFEPADI limenasua wanawake kutoka kwenye ukatili wa kijinsia na kingono, sambamba na utumikishwaji, Mashariki mwa nchi hiyo. Tumekuandalia pia habari kwa ufupi na uchmbuzi wa methali.Mvua kubwa imesababisha maafa mapya huko Gaza huku wasaidizi wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wakirudia kueleza wasiwasi wao kuhusu kuzorota kwa hali ya afya katika Ukanda huo,wakati kukiwa bado na mashambulizi yanayoendelea kati ya Israel na makundi yenye silaha ya Palestina. Ofisi ya Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura (OCHA) imesema kuwa maeneo mengi katika eneo hilo yamefurika, "na kuzidisha mahangaiko ya Wapalestina waliokimbia makazi yao.Jukwaa la pili la kimataifa la wakimbizi, GRF, linalowakutanisha takribani watu 4000 kutoka nchi 165 limeingia siku yake ya pili leo huko Geneva, Uswisi ambapo washiriki wanatoa ahadi zao kuhusu namna bora ya kushughulikia suala la wakimbizi. Katika tamko la Kenya lililochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa mkutano huo, Kenya imeeleza namna ilivyotekeleza ahadi yake iliyotoa kwenye mkutano wa kwanza miaka minne iliyopita kwa kuwapa uraia Washona, Wamakonde na Wapemba. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, ili kuwalinda watoto limetoa wito wa kutaka serikali kote duniani zichukue hatua za haraka dhidi ya sigara za kisasa zilizoundwa kwa mfumo wa umeme yaani e-cigarettes. Kupitia wito huo, WHO imeonesha watoto wenye umri wa miaka 13-15 wanatumia sigara za kielektroniki kwa viwango vya juu kuliko watu wazima kote duniani. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalamu wetu leo ni Nicholus Makanji mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya akitufafanulia maana ya methali « MSASI HAOGOPI MIIBA». Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
14-12-2023 • 9 minuten, 58 seconden
Heko Marynsia kwa ushindi wa tuzo COP28
Marynsia Mangu, mmoja wa washiriki wa COP28 au mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC uliofanyika huko Dubai, Falme za Kiarabu, ambaye ameondoka akiwa amebeba tuzo. Tuzo inayodhihirisha utendaji wake yeye kama Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Success Hands Tanzania. Shirika hili linahusika na kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu, tena tangu wakiwa tumboni mwa mama zao. Idhaa ya Umoja wa Mataifa ilitaka kufahamu mengi kutoka kwake ikiwemo ni tuzo gani ameshinda. Ezzat El Feri wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye huko Dubai na kisha Assumpta Massoi akandaa makala hii. Marynsia anaanza kwa kuelezea tuzo aliyonyakua.
13-12-2023 • 0
Heko Marynsia kwa ushindi wa tuzo COP28
Marynsia Mangu, mmoja wa washiriki wa COP28 au mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC uliofanyika huko Dubai, Falme za Kiarabu, ambaye ameondoka akiwa amebeba tuzo. Tuzo inayodhihirisha utendaji wake yeye kama Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la Success Hands Tanzania. Shirika hili linahusika na kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu, tena tangu wakiwa tumboni mwa mama zao. Idhaa ya Umoja wa Mataifa ilitaka kufahamu mengi kutoka kwake ikiwemo ni tuzo gani ameshinda. Ezzat El Feri wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye huko Dubai na kisha Assumpta Massoi akandaa makala hii. Marynsia anaanza kwa kuelezea tuzo aliyonyakua.
13-12-2023 • 3 minuten, 58 seconden
13 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa COP28 ambao unafunga pazia leo. Pia tunamulika Kongamano la Kimataifa la Wakimbizi. Makala tunasalia huko huko Duabai kwenye mkutano wa COP28 na mashinani inamulika afya ya uzazi na haki za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu.Hatimaye mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28, leo umekunja jamvi mjini Dubai Falme za nchi za Kiarabu kwa muafaka ambao Umoja wa Mataifa unasema unatoa ishara ya kuanza kutokomezwa kwa mafuta kisukuku au fosil fuel ingawa baadhi ya nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea ikiwemo Samoa zinaona muafaka huo hautoshelezi kuwalinda kikamilifu dhidi ya tabianchi.Ikiwa leo Kongamano la Kimataifa la Wakimbizi ambalo hufanyika kila baada ya miaka minne linaanza huko Geneva, Uswisi na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo wakimbizi kutafuta suluhu na kuahidi hatua kwa ajili ya wakimbizi duniani na nchi na jamii zinazowahifadhi, nikepeleke sasa nchini Zimbabwe ambako kuna mfano wa wazi namna wakimbizi wanavyoweza kuwa na mchango chanya katika jamii zinazowahifadhi. Makala inatupeleka Dubai, Falme za Kiarabu kwenye mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 ambako huko Marynsia Mangu, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la kiraia la Success Hands la nchini Tanzania linalohusika na kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu ameshinda tuzo. Amezungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya kupokea tuzo na hapa anaelezea mengi ikiwemo alivyoipokea. Mashinani itamulika afya ya uzazi na haki za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
13-12-2023 • 0
13 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa COP28 ambao unafunga pazia leo. Pia tunamulika Kongamano la Kimataifa la Wakimbizi. Makala tunasalia huko huko Duabai kwenye mkutano wa COP28 na mashinani inamulika afya ya uzazi na haki za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu.Hatimaye mkutano wa 28 wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28, leo umekunja jamvi mjini Dubai Falme za nchi za Kiarabu kwa muafaka ambao Umoja wa Mataifa unasema unatoa ishara ya kuanza kutokomezwa kwa mafuta kisukuku au fosil fuel ingawa baadhi ya nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea ikiwemo Samoa zinaona muafaka huo hautoshelezi kuwalinda kikamilifu dhidi ya tabianchi.Ikiwa leo Kongamano la Kimataifa la Wakimbizi ambalo hufanyika kila baada ya miaka minne linaanza huko Geneva, Uswisi na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo wakimbizi kutafuta suluhu na kuahidi hatua kwa ajili ya wakimbizi duniani na nchi na jamii zinazowahifadhi, nikepeleke sasa nchini Zimbabwe ambako kuna mfano wa wazi namna wakimbizi wanavyoweza kuwa na mchango chanya katika jamii zinazowahifadhi. Makala inatupeleka Dubai, Falme za Kiarabu kwenye mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 ambako huko Marynsia Mangu, Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika la kiraia la Success Hands la nchini Tanzania linalohusika na kuwajengea watoto tabia ya kupenda kusoma vitabu ameshinda tuzo. Amezungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya kupokea tuzo na hapa anaelezea mengi ikiwemo alivyoipokea. Mashinani itamulika afya ya uzazi na haki za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
13-12-2023 • 12 minuten, 16 seconden
Wakimbizi vijana dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kambini Tongogara nchini Zimbabwe
Ikiwa leo Kongamano la Kimataifa la Wakimbizi ambalo hufanyika kila baada ya miaka minne linaanza huko Geneva, Uswisi na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo wakimbizi kutafuta suluhu na kuahidi hatua kwa ajili ya wakimbizi duniani na nchi na jamii zinazowahifadhi, nikepeleke sasa nchini Zimbabwe ambako kuna mfano wa wazi namna wakimbizi wanavyoweza kuwa na mchango chanya katika jamii zinazowahifadhi.Kundi la wakimbizi vijana katika Kambi ya Wakimbizi ya Tongogara nchini Zimbabwe wanaongoza juhudi za kurejesha mazingira yao katika hali nzuri wakiungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. EKambi ya wakimbizi ya Tongogara iliyoko kusini mwa Zimbabwe ni makazi ya wakimbizi 16,000, hasa kutoka Burundi, Msumbiji, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. “Miti ina faida nyingi, inavutia mvua, inatupatia kivuli, inakinga vumbi.” Faida alizozitaja Mugisha Everiste, mtoto huyu mkimbizi kutoka Burundi zisingepatikana kambini Tongogara kama si juhudi za vijana wakimbizi kupitia taasisi yao ya Refugee Coalition for Climate Action (RCCA). Elie Nsala Tshikuna, Mkimbizi kutoka DR Congo anaeleza akisema kwamba (Nats)…walianza kupanda miti mwaka 2020. Na kuanzia mwaka huo hadi sasa wamepanda miti zaidi ya 2,000 kambini. Hili limeleta mabadiliko makubwa kwa sababu wameona kwamba jukumu ambalo jamii sasa inalo la kulinda miti limekuwa bora zaidi. Jeanne Muhimundu, yeye ni mkimbizi kutoka Rwanda, mshiriki wa harakati hizi za utunzaji mazingira kambini, ana matumaini makubwa na hatua waliyoichukua, "Natumai kuona miti zaidi. Natumai kuona watu wanachukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.”
13-12-2023 • 0
Wakimbizi vijana dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kambini Tongogara nchini Zimbabwe
Ikiwa leo Kongamano la Kimataifa la Wakimbizi ambalo hufanyika kila baada ya miaka minne linaanza huko Geneva, Uswisi na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo wakimbizi kutafuta suluhu na kuahidi hatua kwa ajili ya wakimbizi duniani na nchi na jamii zinazowahifadhi, nikepeleke sasa nchini Zimbabwe ambako kuna mfano wa wazi namna wakimbizi wanavyoweza kuwa na mchango chanya katika jamii zinazowahifadhi.Kundi la wakimbizi vijana katika Kambi ya Wakimbizi ya Tongogara nchini Zimbabwe wanaongoza juhudi za kurejesha mazingira yao katika hali nzuri wakiungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR. EKambi ya wakimbizi ya Tongogara iliyoko kusini mwa Zimbabwe ni makazi ya wakimbizi 16,000, hasa kutoka Burundi, Msumbiji, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. “Miti ina faida nyingi, inavutia mvua, inatupatia kivuli, inakinga vumbi.” Faida alizozitaja Mugisha Everiste, mtoto huyu mkimbizi kutoka Burundi zisingepatikana kambini Tongogara kama si juhudi za vijana wakimbizi kupitia taasisi yao ya Refugee Coalition for Climate Action (RCCA). Elie Nsala Tshikuna, Mkimbizi kutoka DR Congo anaeleza akisema kwamba (Nats)…walianza kupanda miti mwaka 2020. Na kuanzia mwaka huo hadi sasa wamepanda miti zaidi ya 2,000 kambini. Hili limeleta mabadiliko makubwa kwa sababu wameona kwamba jukumu ambalo jamii sasa inalo la kulinda miti limekuwa bora zaidi. Jeanne Muhimundu, yeye ni mkimbizi kutoka Rwanda, mshiriki wa harakati hizi za utunzaji mazingira kambini, ana matumaini makubwa na hatua waliyoichukua, "Natumai kuona miti zaidi. Natumai kuona watu wanachukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.”
13-12-2023 • 2 minuten
UN: COP28 yafunga pazia kwa muafaka wa kuanza kutokomeza mafuta kisuskuku
Hatimaye mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28, leo umekunja jamvi mjini Dubai huko Umoja w Falme za Kiarabu (UAE) kwa muafaka ambao Umoja wa Mataifa unasema unatoa ishara ya kuanza kutokomezwa kwa mafuta kisukuku au Fossil Fuels, ingawa baadhi ya nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea ikiwemo Samoa zinaona muafaka huo hautoshelezi kuwalinda kikamilifu dhidi ya tabianchi.Ni Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi Simon Stiell akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makubaliano kufikiwa akisema ingawa hawafungua ukurasa mpya kabisa wa kutokomeza mafuta kisukuku Dubai lakini makubaliano hayo yanatoa ishara ya kuanza utokomezaji wa mafuta hayo ambayo ni kichocheo kikubwa cha mabadiliko ya tabianchi. Stiel amesema “makubaliano hayo yameweka msingi wa mpito wa haraka, wa haki na usawa, unaounga mkono kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa uzalishaji wa hewa chafuzi na kuongezwa kwa ufadhili.”Amesisitiza kuwa “sasa serikali na sekta ya biashara wanahitaji kugeuza ahadi hizi kuwa matokeo halisi ya ya uchumi, bila kuchelewa.Akitoa kauli yake baada matokeo ya mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema "licha ya tofauti nyingi, ulimwengu unaweza kuungana na kukabiliana na changamoto ya janga la mabadiliko ya tabianchi. Ushirikiano wa kimataifa unasalia kuwa tumaini bora la ubinadamu." Kwa wale waliopinga kuainisha wazi utokomezaji wa nishati ya mafuta kisukuku katika waraka wa COP28, amesema "utokomezaji wa mafuta kisukuku haiwezi kuepukika watake wasitake. Hebu tutumaini kwamba hautachelewa sana. "Na mgawanyiko wa matokeo hayo ulikuwa bayana hususan kwa visiwa vidogo vinavyoendelea kama Samoa ambayo haikuficha hisia zake kuhusu matokeo na Stiel amekiri hilo akisema, tumesikia wasiwasi wa Samoa na mataifa yote ya visiwa ambayo yameweka wazi kwamba muafaka huu hautoshelezi kulinda watu wao na sayari. Ukweli kwamba ndio walioshangiliwa zaidi ni ishara tosha kwamba hisia zao zinaungwa mkono na wengi.”Washiriki kutoka nchi 199 na takriban pande 200 wamejadiliana Dubai kwa wiki mbili kwa lengo la kudhibiti athari za madiliko ya tabianchi na hasa kuhakikisha joto la duniani haliongezeki zaidi ya nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi.
13-12-2023 • 0
UN: COP28 yafunga pazia kwa muafaka wa kuanza kutokomeza mafuta kisuskuku
Hatimaye mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28, leo umekunja jamvi mjini Dubai huko Umoja w Falme za Kiarabu (UAE) kwa muafaka ambao Umoja wa Mataifa unasema unatoa ishara ya kuanza kutokomezwa kwa mafuta kisukuku au Fossil Fuels, ingawa baadhi ya nchi za visiwa vidogo vinavyoendelea ikiwemo Samoa zinaona muafaka huo hautoshelezi kuwalinda kikamilifu dhidi ya tabianchi.Ni Katibu Mtendaji wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi Simon Stiell akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makubaliano kufikiwa akisema ingawa hawafungua ukurasa mpya kabisa wa kutokomeza mafuta kisukuku Dubai lakini makubaliano hayo yanatoa ishara ya kuanza utokomezaji wa mafuta hayo ambayo ni kichocheo kikubwa cha mabadiliko ya tabianchi. Stiel amesema “makubaliano hayo yameweka msingi wa mpito wa haraka, wa haki na usawa, unaounga mkono kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa uzalishaji wa hewa chafuzi na kuongezwa kwa ufadhili.”Amesisitiza kuwa “sasa serikali na sekta ya biashara wanahitaji kugeuza ahadi hizi kuwa matokeo halisi ya ya uchumi, bila kuchelewa.Akitoa kauli yake baada matokeo ya mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema "licha ya tofauti nyingi, ulimwengu unaweza kuungana na kukabiliana na changamoto ya janga la mabadiliko ya tabianchi. Ushirikiano wa kimataifa unasalia kuwa tumaini bora la ubinadamu." Kwa wale waliopinga kuainisha wazi utokomezaji wa nishati ya mafuta kisukuku katika waraka wa COP28, amesema "utokomezaji wa mafuta kisukuku haiwezi kuepukika watake wasitake. Hebu tutumaini kwamba hautachelewa sana. "Na mgawanyiko wa matokeo hayo ulikuwa bayana hususan kwa visiwa vidogo vinavyoendelea kama Samoa ambayo haikuficha hisia zake kuhusu matokeo na Stiel amekiri hilo akisema, tumesikia wasiwasi wa Samoa na mataifa yote ya visiwa ambayo yameweka wazi kwamba muafaka huu hautoshelezi kulinda watu wao na sayari. Ukweli kwamba ndio walioshangiliwa zaidi ni ishara tosha kwamba hisia zao zinaungwa mkono na wengi.”Washiriki kutoka nchi 199 na takriban pande 200 wamejadiliana Dubai kwa wiki mbili kwa lengo la kudhibiti athari za madiliko ya tabianchi na hasa kuhakikisha joto la duniani haliongezeki zaidi ya nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi.
13-12-2023 • 2 minuten, 47 seconden
12 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunamulika mchango wa vijana katika mkutano wa COP28. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo vita Gaza, na hudam ya afya. Mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini kusikia ni kwa jinsi gani mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyosaidia wafugaji kakabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Katika saa za mwisho za mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 majadiliano yanaendelea kwa matumaini kwamba wajumbe watatoka na makubaliano yatakayoweka ulimwengu kwenye njia ya mustakabali endelevu zaidi. Hata hivyo rasimu ya awali ya makubaliano hayo inaonyesha wito wa kuachana na nishati ya mafuta kiskuku umepewa kisogo, na kusababisha kilio kutoka kwa nchi zilizo katika mazingira magumu ya mabadiliko ya tabianchi na mashirika ya kiraia..Huko Gaza hali ya kibinadamu inazidi kudororora huku mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yakipaza sauti ya kunusuru maisha ya watu wanaopitia adhabu ya jehanamu duniani. Lile la afya WHO linataka ulinzi na fursa ya kufikisha huduma za kibinadamu, wakati la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA likisema karibu Gaza nzima inazingirwa na kusababisha adhabu ya pamoja kwa zaidi ya watu milioni 2 ambapo nusu yake ni watoto. Na leo ni siku ya huduma za afya kwa wote mwaka huu ikibeba maudhui “Afya kwa wote, wakati wa kuchukua hatua” Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO Dkt. Tedross Ghebreyesus katika ujumbe wake wa siku hii amesema “Huduma za afya kwa wote inamaanisha kwamba watu wote wanaweza kupata huduma wanazohitaji bila gharama kubwa lakini bado nusu ya watu wote duniani hawana huduma muhimu za afya. WHO ilizaliwa miaka 75 iliyopita kwa Imani kwamba afya ni haki ya binadamu na njia bora ya kutimiza haki hiyo ni huduma za afya kwa wote. Mashinani tutaelekea nchini Sudan Kusini kusikia ni kwa jinsi gani mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyosaidia wafugaji kakabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
12-12-2023 • 0
12 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunamulika mchango wa vijana katika mkutano wa COP28. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo vita Gaza, na hudam ya afya. Mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini kusikia ni kwa jinsi gani mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyosaidia wafugaji kakabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Katika saa za mwisho za mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 majadiliano yanaendelea kwa matumaini kwamba wajumbe watatoka na makubaliano yatakayoweka ulimwengu kwenye njia ya mustakabali endelevu zaidi. Hata hivyo rasimu ya awali ya makubaliano hayo inaonyesha wito wa kuachana na nishati ya mafuta kiskuku umepewa kisogo, na kusababisha kilio kutoka kwa nchi zilizo katika mazingira magumu ya mabadiliko ya tabianchi na mashirika ya kiraia..Huko Gaza hali ya kibinadamu inazidi kudororora huku mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yakipaza sauti ya kunusuru maisha ya watu wanaopitia adhabu ya jehanamu duniani. Lile la afya WHO linataka ulinzi na fursa ya kufikisha huduma za kibinadamu, wakati la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA likisema karibu Gaza nzima inazingirwa na kusababisha adhabu ya pamoja kwa zaidi ya watu milioni 2 ambapo nusu yake ni watoto. Na leo ni siku ya huduma za afya kwa wote mwaka huu ikibeba maudhui “Afya kwa wote, wakati wa kuchukua hatua” Mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO Dkt. Tedross Ghebreyesus katika ujumbe wake wa siku hii amesema “Huduma za afya kwa wote inamaanisha kwamba watu wote wanaweza kupata huduma wanazohitaji bila gharama kubwa lakini bado nusu ya watu wote duniani hawana huduma muhimu za afya. WHO ilizaliwa miaka 75 iliyopita kwa Imani kwamba afya ni haki ya binadamu na njia bora ya kutimiza haki hiyo ni huduma za afya kwa wote. Mashinani tutaelekea nchini Sudan Kusini kusikia ni kwa jinsi gani mashirika ya Umoja wa Mataifa yanavyosaidia wafugaji kakabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
12-12-2023 • 11 minuten, 10 seconden
Uwekezaji katika elimu kwa watoto utawasaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi
Pazia la mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 likitarajiwa kufungwa hapo kesho huko Dubai Falme za kiarabu tunaangazia suala la jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri watoto hususani katika suala la Afya na kwenye elimu. Tarehe 08 Desemba ratiba ya COP28 ilijikita mahususi kujadili masuala ya vijana na watoto. Mashirika mbalimbali yalitoa takwimu zinazohusiana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa watoto na vijana moja wao ni Mfuko wa kimataifa wa elimu haiwezi kusubiri ECW. Ungana na Leah Mushi katika makala hii anayekujuza zaidi katika makala hii.
11-12-2023 • 0
Uwekezaji katika elimu kwa watoto utawasaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi
Pazia la mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 likitarajiwa kufungwa hapo kesho huko Dubai Falme za kiarabu tunaangazia suala la jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri watoto hususani katika suala la Afya na kwenye elimu. Tarehe 08 Desemba ratiba ya COP28 ilijikita mahususi kujadili masuala ya vijana na watoto. Mashirika mbalimbali yalitoa takwimu zinazohusiana na madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa watoto na vijana moja wao ni Mfuko wa kimataifa wa elimu haiwezi kusubiri ECW. Ungana na Leah Mushi katika makala hii anayekujuza zaidi katika makala hii.
11-12-2023 • 3 minuten, 13 seconden
Guterres kwa washiriki COP28: Epukeni majawabu ya kutia moyo bila ufanisi
Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 ukifikia ukingoni huko Dubai, Falme za Kiarabu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka washiriki waepuke msemo wa “Funika kombe mwanaharamu apite,” na badala yake waje na majawabu ya kina na ya kijasiri ili lengo la kutozidi kwa nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha selsiyasi liweze kufikiwa. Katibu Mkuu Guterres akizungumza na waandishi wa habari hii leo huko Dubai, Falme za Kiarabu amewakumbusha wasongeshaji wa majadiliano hayo kwenye COP28 kuwa mkutano unakunja jamvi kesho lakini bado kuna mapengo makubwa ya kuzibwa. Ni wakati wa kusaka kulegeza misimamo ili kupata majawabu, anasema Guterres, akiongeza kuwa misimamo hiyo ilegezwe bila kupuuza sayansi au kupuuza umuhimu wa kuwa na matamanio makubwa. Anasema katika dunia iliyomeguka na kugawanyika, COP28 inaweza kudhihirisha kuwa ushirikiano wa kimataifa ndio tumaini letu bora la kutatua changamoto za dunia. Ndio hapo Katibu Mkuu akataja maeneo mawili ambayo anasihi pande husika kwenye mkutano huo kuyapatia kipaumbele: Mosi kupunguza utoaji wa hewa chafuzi na kuhakikisha kuna majawabu yanayopatia haki tabianchi. Katibu Mkuu anasema Uhakiki wa kimataifa lazima uwasilishe mpango wa wazi wa kuongeza nishati rejelezi, kuongeza maradufu nishati fanisi, na mpango mmoja wa kushughulikia vyanzo vya janga la tabianchi ambavyo ni uzalishaji na utumiaji wa nishati kisukuku. “Ametamatisha mkutano wake kwa kusema lazima COP28 imalizike kwa kuendeleza azma ya kudhibiti kiwango cha joto kisizidi nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi kama ilivyopitishwa na Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya tabianchi mwaka 2015.
11-12-2023 • 0
Guterres kwa washiriki COP28: Epukeni majawabu ya kutia moyo bila ufanisi
Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 ukifikia ukingoni huko Dubai, Falme za Kiarabu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka washiriki waepuke msemo wa “Funika kombe mwanaharamu apite,” na badala yake waje na majawabu ya kina na ya kijasiri ili lengo la kutozidi kwa nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha selsiyasi liweze kufikiwa. Katibu Mkuu Guterres akizungumza na waandishi wa habari hii leo huko Dubai, Falme za Kiarabu amewakumbusha wasongeshaji wa majadiliano hayo kwenye COP28 kuwa mkutano unakunja jamvi kesho lakini bado kuna mapengo makubwa ya kuzibwa. Ni wakati wa kusaka kulegeza misimamo ili kupata majawabu, anasema Guterres, akiongeza kuwa misimamo hiyo ilegezwe bila kupuuza sayansi au kupuuza umuhimu wa kuwa na matamanio makubwa. Anasema katika dunia iliyomeguka na kugawanyika, COP28 inaweza kudhihirisha kuwa ushirikiano wa kimataifa ndio tumaini letu bora la kutatua changamoto za dunia. Ndio hapo Katibu Mkuu akataja maeneo mawili ambayo anasihi pande husika kwenye mkutano huo kuyapatia kipaumbele: Mosi kupunguza utoaji wa hewa chafuzi na kuhakikisha kuna majawabu yanayopatia haki tabianchi. Katibu Mkuu anasema Uhakiki wa kimataifa lazima uwasilishe mpango wa wazi wa kuongeza nishati rejelezi, kuongeza maradufu nishati fanisi, na mpango mmoja wa kushughulikia vyanzo vya janga la tabianchi ambavyo ni uzalishaji na utumiaji wa nishati kisukuku. “Ametamatisha mkutano wake kwa kusema lazima COP28 imalizike kwa kuendeleza azma ya kudhibiti kiwango cha joto kisizidi nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi kama ilivyopitishwa na Mkataba wa Paris wa Mabadiliko ya tabianchi mwaka 2015.
11-12-2023 • 1 minuut, 56 seconden
Lilly Kiden: Asante FAO kunijengea mnepo sasa najikimu mimi na familia yangu
Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 ukijiandaa kufunga pazia hapo kesho nakupeleka Sudan Kusini jimbo la Equatorial Mashariki ambako wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi sasa wanajengewa mnepo na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na wengi wameweza kujikwamua pamoja na familia zao. Ungana na Flora Nducha akikuletea safari ya mafanikio ya mmoja wa wanuafa wa mradi huo wa FAO. Kutana na Lilly Kiden mama mjasiriamali anayelima na kuchuza mboga za majani katika eneo la Lopit Sudan KusiniLilly anasema ana watoto 7 na jamaa wengine 10 wa familia ambao wote wanamtegemea . Shukran kwa FAO kwa kuwajengea wanawake mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kupitia ufadhili kutoka Benki ya Maendeleo Afrika sasa wana mabwa yanayotumia pampu za sola na kumuwesha Lilly na wanawake wengine wakulima wadogo kumwagilia mashamba yao. Kwa Lilly anasema kibarua ni kigumu kueedesha familia kubwa kama aliyonayo bila msaada mwingine.Ingawa sasa amekuwa mchumia juani anayelia kivulini, ukame wa muda mrefu Sudan umekuwa mwiba kwa wakulima hawa,“Mabadiliko ya tabianchi yametuathiri sana, na mwaka huu umekuwa mbayá zaidi, kila tulichopanda kilikauka na jua hali ikiendelea hivi wanangu hawatakuwa na chakula na wengine watashindwa kwenda shule.”Lilly mwenye umri wa miaka 38 kutokana na kuuza mbogamboga yeye na wenzake 25 wamewekeza fedha wanazopata na sasa wanapena mikopo kupitia jumuiya yao ya akiba ya kijiji. Ama kwa hakika jembe halimtupi mkulima, ”Hela ninayopata kwa kuuza mbogamboga imenisaidia sana naweza kununua chakula kwa ajili ya familia yangu, na kuweka akiba kidogo ambayo imekuwa mkombozi wangu yote ni kwa kulima na kuuza mbogamboga. Ndoto yangu ni kuongeza bidii ili watoto wangu waendelee na masomo.”FAO mbali ya kuwajengea mabwawa kwa ya umwagiliaji wakulima hawa pia inawapa mafunzo, mbegu na mikopo.
11-12-2023 • 0
Lilly Kiden: Asante FAO kunijengea mnepo sasa najikimu mimi na familia yangu
Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 ukijiandaa kufunga pazia hapo kesho nakupeleka Sudan Kusini jimbo la Equatorial Mashariki ambako wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi sasa wanajengewa mnepo na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na wengi wameweza kujikwamua pamoja na familia zao. Ungana na Flora Nducha akikuletea safari ya mafanikio ya mmoja wa wanuafa wa mradi huo wa FAO. Kutana na Lilly Kiden mama mjasiriamali anayelima na kuchuza mboga za majani katika eneo la Lopit Sudan KusiniLilly anasema ana watoto 7 na jamaa wengine 10 wa familia ambao wote wanamtegemea . Shukran kwa FAO kwa kuwajengea wanawake mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kupitia ufadhili kutoka Benki ya Maendeleo Afrika sasa wana mabwa yanayotumia pampu za sola na kumuwesha Lilly na wanawake wengine wakulima wadogo kumwagilia mashamba yao. Kwa Lilly anasema kibarua ni kigumu kueedesha familia kubwa kama aliyonayo bila msaada mwingine.Ingawa sasa amekuwa mchumia juani anayelia kivulini, ukame wa muda mrefu Sudan umekuwa mwiba kwa wakulima hawa,“Mabadiliko ya tabianchi yametuathiri sana, na mwaka huu umekuwa mbayá zaidi, kila tulichopanda kilikauka na jua hali ikiendelea hivi wanangu hawatakuwa na chakula na wengine watashindwa kwenda shule.”Lilly mwenye umri wa miaka 38 kutokana na kuuza mbogamboga yeye na wenzake 25 wamewekeza fedha wanazopata na sasa wanapena mikopo kupitia jumuiya yao ya akiba ya kijiji. Ama kwa hakika jembe halimtupi mkulima, ”Hela ninayopata kwa kuuza mbogamboga imenisaidia sana naweza kununua chakula kwa ajili ya familia yangu, na kuweka akiba kidogo ambayo imekuwa mkombozi wangu yote ni kwa kulima na kuuza mbogamboga. Ndoto yangu ni kuongeza bidii ili watoto wangu waendelee na masomo.”FAO mbali ya kuwajengea mabwawa kwa ya umwagiliaji wakulima hawa pia inawapa mafunzo, mbegu na mikopo.
11-12-2023 • 2 minuten, 8 seconden
11 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mabadiliko ya tabianchi na wakulima nchini Sudan kusini. Makala tunamulika madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa watototo na mashinani tunakupeleka nchini DRC kwa mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa ya Haki za bindamu. Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 ukifikia ukingoni huko Dubai, Falme za Kiarabu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka washiriki waepuke msemo wa “Funika kombe mwanaharamu apite,” na badala yake waje na majawabu ya kina na ya kijasiri ili lengo la kutozidi kwa nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha selsiyasi liweze kufikiwa.Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 ukijiandaa kufunga pazia hapo kesho nakupeleka Sudan Kusini jimbo la Equatorial Mashariki ambako wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi sasa wanajengewa mnepo na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na wengi wameweza kujikwamua pamoja na familia zao. Katika makala wakati pazia la mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 likitarajiwa kufungwa hapo kesho huko Dubai Falme za kiarabu tunaangazia suala la jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri watoto hususani katika suala la Afya na kwenye elimu. Na mashinani tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC kwa mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa ya Haki za bindamu. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
11-12-2023 • 0
11 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mabadiliko ya tabianchi na wakulima nchini Sudan kusini. Makala tunamulika madhara ya mabadiliko ya tabianchi kwa watototo na mashinani tunakupeleka nchini DRC kwa mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa ya Haki za bindamu. Mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP28 ukifikia ukingoni huko Dubai, Falme za Kiarabu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka washiriki waepuke msemo wa “Funika kombe mwanaharamu apite,” na badala yake waje na majawabu ya kina na ya kijasiri ili lengo la kutozidi kwa nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha selsiyasi liweze kufikiwa.Wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 ukijiandaa kufunga pazia hapo kesho nakupeleka Sudan Kusini jimbo la Equatorial Mashariki ambako wakulima walioathirika na mabadiliko ya tabianchi sasa wanajengewa mnepo na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO na wengi wameweza kujikwamua pamoja na familia zao. Katika makala wakati pazia la mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 likitarajiwa kufungwa hapo kesho huko Dubai Falme za kiarabu tunaangazia suala la jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyoathiri watoto hususani katika suala la Afya na kwenye elimu. Na mashinani tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC kwa mshindi wa tuzo ya mwaka huu ya Umoja wa Mataifa ya Haki za bindamu. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
11-12-2023 • 10 minuten, 10 seconden
NENO: Kifandugu
Leo katika Jifunze Kiswahili ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “KIFANDUGU”. Anapochambua neno hili anapatia pia kisawe chake ambacho ni "KITOKONO."
8-12-2023 • 0
NENO: Kifandugu
Leo katika Jifunze Kiswahili ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “KIFANDUGU”. Anapochambua neno hili anapatia pia kisawe chake ambacho ni "KITOKONO."
8-12-2023 • 0
Mafuriko yazidi 'kutikisa' maeneo yaliyokuwa yamegubikwa na ukame Mashariki mwa Afrika
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linaonya kuwa mafuriko makubwa yanatishia kuongeza zaidi tatizo la kukosekana kwa uhakika wa kupatikana kwa chakula katika eneo la Mashariki mwa Afrika licha ya kwamba shirika hilo linajitahidi kusambaza misaada. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuleta maafa katika eneo la Mashariki mwa Afrika, eneo ambalo lina uchangiaji mdogo katika uzalishaji wa hewa chafuzi lakini likiwa eneo ambalo linabeba mzigo mkubwa wa dharura ya tabanchi duniani. Baada ya ukame mkali kati ya mwaka 2020 na 2022, sasa ni mvua asilimia 140 juu ya viwango vya kawaida.Kwa mujibu wa WFP, takriban watu milioni 3 wameathiriwa, huku zaidi ya watu milioni 1.2 wakilazimika kuyahama makazi yao. Somalia, Ethiopia, na Kenya ndizo zinazobeba mzigo mkubwa wa janga hili, zikifuatiwa kwa karibu na Sudan, Sudan Kusini, Burundi, na Uganda na sasa Tanzania ambayo tukio la hivi karibuni ni maporomoko ya udongo katika Mlima Hanang, huko kaskazini mwa nchi. Kwa bahati mbaya, mvua zinatarajiwa kuendelea kote mashariki mwa Afrika hadi mapema mwaka 2024.Petroc Wilton wa WFP Somalia anasema, "El Niño na janga la tabianchi vimepeleka athari mbaya katika maeneo mengi ya Afrika Mashariki. Tumeona mfululizo wa majanga ya tabianchi. WFP hapa Somalia tunatumia boti, tunatumia helikopta kufikisha msaada wa kuokoa maisha kwa watu wenye uhitaji zaidi.”
8-12-2023 • 0
Mafuriko yazidi 'kutikisa' maeneo yaliyokuwa yamegubikwa na ukame Mashariki mwa Afrika
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linaonya kuwa mafuriko makubwa yanatishia kuongeza zaidi tatizo la kukosekana kwa uhakika wa kupatikana kwa chakula katika eneo la Mashariki mwa Afrika licha ya kwamba shirika hilo linajitahidi kusambaza misaada. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuleta maafa katika eneo la Mashariki mwa Afrika, eneo ambalo lina uchangiaji mdogo katika uzalishaji wa hewa chafuzi lakini likiwa eneo ambalo linabeba mzigo mkubwa wa dharura ya tabanchi duniani. Baada ya ukame mkali kati ya mwaka 2020 na 2022, sasa ni mvua asilimia 140 juu ya viwango vya kawaida.Kwa mujibu wa WFP, takriban watu milioni 3 wameathiriwa, huku zaidi ya watu milioni 1.2 wakilazimika kuyahama makazi yao. Somalia, Ethiopia, na Kenya ndizo zinazobeba mzigo mkubwa wa janga hili, zikifuatiwa kwa karibu na Sudan, Sudan Kusini, Burundi, na Uganda na sasa Tanzania ambayo tukio la hivi karibuni ni maporomoko ya udongo katika Mlima Hanang, huko kaskazini mwa nchi. Kwa bahati mbaya, mvua zinatarajiwa kuendelea kote mashariki mwa Afrika hadi mapema mwaka 2024.Petroc Wilton wa WFP Somalia anasema, "El Niño na janga la tabianchi vimepeleka athari mbaya katika maeneo mengi ya Afrika Mashariki. Tumeona mfululizo wa majanga ya tabianchi. WFP hapa Somalia tunatumia boti, tunatumia helikopta kufikisha msaada wa kuokoa maisha kwa watu wenye uhitaji zaidi.”
8-12-2023 • 1 minuut, 48 seconden
GAZA: Misaada ni haba, nyaya za simu zageuzwa kuni
Wakati mashambulizi ya Israel yakiendelea kushika kasi huko Ukanda wa Gaza na mapigano na makundi yaliyojihami ya kipalestina yakiwa kikwazo kikubwa cha kusambaza misaada ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa leo umeonya kwamba jamii inakaribia kusambaratika kabisa watu wakifikia hatua ya kukata nyaya za simu za kuzitumia kama kuni. Flora Nducha amefuatilia na anatusimulia zaidi.Asante Assumpta , Yumkini hali si hali tena Gaza kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswiss hii leo msemaji wa shirika la Afya la Umoja WHO Christian Lindmeier amesema “Watu Gaza wanalazimishwa kutumbukia katika janga kubwa huku kukiwa na kampeni ya kikatili ya Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda huo kulipiza kisasi mashambulizi ya kigaidi ya Hamas tarehe 7 Oktoba.Amesisitiza kuwa “Hali ni mbayá sana na hatuwezi kumudu kupoteza hata gari linguine moja la wagonjwa au hospoitali kwani hadi sasa mashambulizi 212 yamefanyika dhidi ya huduma za afya na kuathiri vituo 56 na magari ya wagonjwa 59.”Wakati huo huo hapa mjini New York, leo mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unafanyika ili kujadili mzozo wa Palestina na Israel na azimio linatarajiwa kupitishwa. Katika mitaa ya Gaza shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linasema utulivu umetoweka hivyo “ Ni muhimu kuhakikisha tunazuia kuporomoka kabisa kwa Gaza na mzozo huu kusambaa kwingineko. Utaratibu wa kiraia unasambaratika Gaza na mitaa sasa ni mahame, haswa baada ya giza kuingia baadhi ya misafara ya misaada inaporwa na magari ya Umoja wa Mataifa kupigwa mawe. Jamii iko kwenye ukingo wa kuporomoka kabisa”.Nalo shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limeonya juu kushindwa kuwafikia watu kwa misaada ya muhimu kama maji, chakula, dawa namingineyo likisema usambazaji wa misaada kwa sasa ni mdogo sana hasa Kusini mwa Ukanda huo na pia hakuna mahali popote palipo salama kwa raia na wahudumu wa misaada.Tangu Oktoba 7 zaidi ya asilimia 85 ya watu Gaza wametawanywa na machafuko ambapo takriban milioni 1.2 wamekuwa wakimbizi Wanjiku ndani wakipatiwa hifadhi katika vituo 151 vya UNRWA. Kwako Assumpta.
8-12-2023 • 0
GAZA: Misaada ni haba, nyaya za simu zageuzwa kuni
Wakati mashambulizi ya Israel yakiendelea kushika kasi huko Ukanda wa Gaza na mapigano na makundi yaliyojihami ya kipalestina yakiwa kikwazo kikubwa cha kusambaza misaada ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa leo umeonya kwamba jamii inakaribia kusambaratika kabisa watu wakifikia hatua ya kukata nyaya za simu za kuzitumia kama kuni. Flora Nducha amefuatilia na anatusimulia zaidi.Asante Assumpta , Yumkini hali si hali tena Gaza kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswiss hii leo msemaji wa shirika la Afya la Umoja WHO Christian Lindmeier amesema “Watu Gaza wanalazimishwa kutumbukia katika janga kubwa huku kukiwa na kampeni ya kikatili ya Israel dhidi ya wakazi wa Ukanda huo kulipiza kisasi mashambulizi ya kigaidi ya Hamas tarehe 7 Oktoba.Amesisitiza kuwa “Hali ni mbayá sana na hatuwezi kumudu kupoteza hata gari linguine moja la wagonjwa au hospoitali kwani hadi sasa mashambulizi 212 yamefanyika dhidi ya huduma za afya na kuathiri vituo 56 na magari ya wagonjwa 59.”Wakati huo huo hapa mjini New York, leo mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa unafanyika ili kujadili mzozo wa Palestina na Israel na azimio linatarajiwa kupitishwa. Katika mitaa ya Gaza shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linasema utulivu umetoweka hivyo “ Ni muhimu kuhakikisha tunazuia kuporomoka kabisa kwa Gaza na mzozo huu kusambaa kwingineko. Utaratibu wa kiraia unasambaratika Gaza na mitaa sasa ni mahame, haswa baada ya giza kuingia baadhi ya misafara ya misaada inaporwa na magari ya Umoja wa Mataifa kupigwa mawe. Jamii iko kwenye ukingo wa kuporomoka kabisa”.Nalo shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limeonya juu kushindwa kuwafikia watu kwa misaada ya muhimu kama maji, chakula, dawa namingineyo likisema usambazaji wa misaada kwa sasa ni mdogo sana hasa Kusini mwa Ukanda huo na pia hakuna mahali popote palipo salama kwa raia na wahudumu wa misaada.Tangu Oktoba 7 zaidi ya asilimia 85 ya watu Gaza wametawanywa na machafuko ambapo takriban milioni 1.2 wamekuwa wakimbizi Wanjiku ndani wakipatiwa hifadhi katika vituo 151 vya UNRWA. Kwako Assumpta.
8-12-2023 • 2 minuten, 27 seconden
08 DESEMBA 2023
Hii leo kwenye jarida Assumpta Massoi anamulika mzozo Mashariki ya Kati hususan huko Gaza, nyaya za simu zageuzwa kuni, kisha anakwenda Mashariki mwa Afrika huko baada ya ukame wa muda mrefu sasa ni mvua za kupindukia zinazosababisha maafa makubwa,; makala anakupeleka Tanzania kusikia uchambuzi wa Ibara ya 15 ya Tamko la Haki za Binadamu la UN, na mashinani utamsikia binti shujaa wa mazingira kutoka visiwani Zanzibar nchini Tanzania.Wakati mashambulizi ya Israel yakiendelea kushika kasi huko Ukanda wa Gaza na mapigano na makundi yaliyojihami ya kipalestina yakiwa kikwazo kikubwa cha kusambaza misaada ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa leo umeonya kwamba jamii inakaribia kusambaratika kabisa watu wakifikia hatua ya kukata nyaya za simu za kuzitumia kama kuni. Taarifa ni ya Flora Nducha.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linaonya kuwa mafuriko makubwa yanatishia kuongeza zaidi tatizo la kukosekana kwa uhakika wa kupatikana kwa chakula katika eneo la Mashariki mwa Afrika licha ya kwamba shirika hilo linajitahidi kusambaza misaada. Anold Kayanda ndiye ameandaa ripoti hii.Makala inamulika ibara ya 15 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75. Mchambuzi wetu ni Mhadhiri na mwanasheria wa Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino SAUT mkoani Mwanza, Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania Shukuru Paul, akihojiwa na Evarist Mapesa wa Idhaa hii.Na mashinani fursa ni yake Nasra, binti huyu shujaa wa mazingira kutoka Zanzibar nchini Tanzania, ambaye ni kiongozi mwenye shauku wa klabu yake ya shule ya upandaji miti na anatumia sauti yake kuhamasisha watu kutunza mazingira na kuhakikisha ulimwengu ulio endelevu zaidi siku za usoni. Karibu!
8-12-2023 • 0
08 DESEMBA 2023
Hii leo kwenye jarida Assumpta Massoi anamulika mzozo Mashariki ya Kati hususan huko Gaza, nyaya za simu zageuzwa kuni, kisha anakwenda Mashariki mwa Afrika huko baada ya ukame wa muda mrefu sasa ni mvua za kupindukia zinazosababisha maafa makubwa,; makala anakupeleka Tanzania kusikia uchambuzi wa Ibara ya 15 ya Tamko la Haki za Binadamu la UN, na mashinani utamsikia binti shujaa wa mazingira kutoka visiwani Zanzibar nchini Tanzania.Wakati mashambulizi ya Israel yakiendelea kushika kasi huko Ukanda wa Gaza na mapigano na makundi yaliyojihami ya kipalestina yakiwa kikwazo kikubwa cha kusambaza misaada ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa leo umeonya kwamba jamii inakaribia kusambaratika kabisa watu wakifikia hatua ya kukata nyaya za simu za kuzitumia kama kuni. Taarifa ni ya Flora Nducha.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linaonya kuwa mafuriko makubwa yanatishia kuongeza zaidi tatizo la kukosekana kwa uhakika wa kupatikana kwa chakula katika eneo la Mashariki mwa Afrika licha ya kwamba shirika hilo linajitahidi kusambaza misaada. Anold Kayanda ndiye ameandaa ripoti hii.Makala inamulika ibara ya 15 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75. Mchambuzi wetu ni Mhadhiri na mwanasheria wa Haki za Binadamu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino SAUT mkoani Mwanza, Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania Shukuru Paul, akihojiwa na Evarist Mapesa wa Idhaa hii.Na mashinani fursa ni yake Nasra, binti huyu shujaa wa mazingira kutoka Zanzibar nchini Tanzania, ambaye ni kiongozi mwenye shauku wa klabu yake ya shule ya upandaji miti na anatumia sauti yake kuhamasisha watu kutunza mazingira na kuhakikisha ulimwengu ulio endelevu zaidi siku za usoni. Karibu!
8-12-2023 • 9 minuten, 45 seconden
07 DESEMBA 2023
Hii leo kwenye jarida Leah Mushi anakuletea Habari kwa Ufupi ikiangazia Tanzania, janga la chakula Afrika na Mkutano wa UN na wanazuoni. Katika Mada kwa Kina tunamulika mshindi wa Tuzo ya UN ya Haki za Binadamu Julienne Lusenge kutoka DRC na Jifunze Kiswahili maana ya neno, Kifandugu.Habari kwa UfupiWakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 ukiendelea Dubai Falme za Kiarabu, nchini Tanzania mafuriko makubwa na maporomoko yameleta janga la kibinadamu katika wilaya ya Hanang mkoani Manyara Kazkazini mwa nchi hiyo, watu zaidi ya 65 wamekufa, zaidi ya 100 kujeruhiwa na maelfu kutawanywa. Serikali imeomba msaada kwa umoja wa Mataifa ambao umesema uko tayari kusaidia.Afrika inakabiliwa na janga kubwa chakula ambao halijawahi kushuhudiwa, kwa mujibu wa ripoti mpya ya pamoja iliyozinduliwa leo na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la chakula na kilimo FAO , la mpango wa chakula duniani WFP, Tume ya Muungano wa Afrika (AUC) na Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika (ECA), Ripoti hiyo, ya uhakika wa chakula na lishe kanda ya Afrika 2023 inaangazia takwimu za kutisha za ukosefu wa chakula na utapiamlo ambazo zinasisitiza haja ya haraka ya hatua za kina kuepusha zahma kubwa. Takribani watu milioni 282 barani Afrika karibu asilimia 20 ya idadi ya watu wote hawana lishe bora, ikiwa ni ongezeko la watu milioni 57 tangu kuanza kwa janga la COVID-19.Na leo mkutano wa Umoja wa Mataifa na wanazuoni kutoka Vyuo Vikuu unakunja jamvi hapa New York, Marekani na mmoja wa washiriki ni Dkt. Venance Shillingi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe nchini Tanzania.Mada kwa Kina: Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zinaelekea ukingoni kwani kilele in tarehe 10 mwezi huu wa Desemba ambayo ni siku ya haki za binadamu duniani. Nayo Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa leo inammulika mmoja wa washindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu ambaye ameweka rehani hata maisha yake kutetea waliokumbwa na ukatili wa kijinsia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC . Akisema SOFEPADI ni kifupi cha shirika la mshikamano wa wanawake kwa ajili ya amani na maendeleo. Jifunze Lugha ya Kiswahili: Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “KIFANDUGU”. Karibu sana!
7-12-2023 • 0
07 DESEMBA 2023
Hii leo kwenye jarida Leah Mushi anakuletea Habari kwa Ufupi ikiangazia Tanzania, janga la chakula Afrika na Mkutano wa UN na wanazuoni. Katika Mada kwa Kina tunamulika mshindi wa Tuzo ya UN ya Haki za Binadamu Julienne Lusenge kutoka DRC na Jifunze Kiswahili maana ya neno, Kifandugu.Habari kwa UfupiWakati mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 ukiendelea Dubai Falme za Kiarabu, nchini Tanzania mafuriko makubwa na maporomoko yameleta janga la kibinadamu katika wilaya ya Hanang mkoani Manyara Kazkazini mwa nchi hiyo, watu zaidi ya 65 wamekufa, zaidi ya 100 kujeruhiwa na maelfu kutawanywa. Serikali imeomba msaada kwa umoja wa Mataifa ambao umesema uko tayari kusaidia.Afrika inakabiliwa na janga kubwa chakula ambao halijawahi kushuhudiwa, kwa mujibu wa ripoti mpya ya pamoja iliyozinduliwa leo na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la chakula na kilimo FAO , la mpango wa chakula duniani WFP, Tume ya Muungano wa Afrika (AUC) na Kamisheni ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Afrika (ECA), Ripoti hiyo, ya uhakika wa chakula na lishe kanda ya Afrika 2023 inaangazia takwimu za kutisha za ukosefu wa chakula na utapiamlo ambazo zinasisitiza haja ya haraka ya hatua za kina kuepusha zahma kubwa. Takribani watu milioni 282 barani Afrika karibu asilimia 20 ya idadi ya watu wote hawana lishe bora, ikiwa ni ongezeko la watu milioni 57 tangu kuanza kwa janga la COVID-19.Na leo mkutano wa Umoja wa Mataifa na wanazuoni kutoka Vyuo Vikuu unakunja jamvi hapa New York, Marekani na mmoja wa washiriki ni Dkt. Venance Shillingi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe nchini Tanzania.Mada kwa Kina: Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zinaelekea ukingoni kwani kilele in tarehe 10 mwezi huu wa Desemba ambayo ni siku ya haki za binadamu duniani. Nayo Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa leo inammulika mmoja wa washindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu ambaye ameweka rehani hata maisha yake kutetea waliokumbwa na ukatili wa kijinsia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC . Akisema SOFEPADI ni kifupi cha shirika la mshikamano wa wanawake kwa ajili ya amani na maendeleo. Jifunze Lugha ya Kiswahili: Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua maana ya neno “KIFANDUGU”. Karibu sana!
7-12-2023 • 11 minuten, 41 seconden
Kituo cha afya cha Mtofaani kwa hisani ya Milele Zanzibar Foundation utekelezaji wa SDG 3
Shirika lisilo la kiserikali la Milele Zanzibar Foundation la Zanzibar Tanzania ambalo limejipambanua kujikita na utekelezaji wa malengo 12 kati ya malengo 17 ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, limetekeleza lengo namba 3 la Afya Bora na Ustawi kwa kujenga kituo cha afya katika Shehia ya Michikichini, Unguja. Hamad Rashid wa redio washirika wetu Mviwata FM ya Morogoro - Tanzania amefika visiwani humo na kutuandalia makala hii.
6-12-2023 • 0
Kituo cha afya cha Mtofaani kwa hisani ya Milele Zanzibar Foundation utekelezaji wa SDG 3
Shirika lisilo la kiserikali la Milele Zanzibar Foundation la Zanzibar Tanzania ambalo limejipambanua kujikita na utekelezaji wa malengo 12 kati ya malengo 17 ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, limetekeleza lengo namba 3 la Afya Bora na Ustawi kwa kujenga kituo cha afya katika Shehia ya Michikichini, Unguja. Hamad Rashid wa redio washirika wetu Mviwata FM ya Morogoro - Tanzania amefika visiwani humo na kutuandalia makala hii.
6-12-2023 • 4 minuten, 25 seconden
Solar Sister watekeleza kwa vitendo nishati safi kwa jamii za pembezoni
Kila uchao, sauti zinapazwa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, tena hasa wakati huu ambapo wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC wakikutana Dubai, huko Falme za Kiarabu kwenye mkutano wao wa 28 au COP28. Tayari hatua zimechukuliwa na shirika la kimataifa la Solar Sister kusaka nishati salama hasa kwa wanawake wa vijijini kama anavyoshuhudia mwanachama na mnufaika wake, Loveness Sabaya wa jamii ya kimasai kutoka Arusha nchini Tanzania kupitia video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X wa mkutano wa COP28.
6-12-2023 • 0
Solar Sister watekeleza kwa vitendo nishati safi kwa jamii za pembezoni
Kila uchao, sauti zinapazwa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, tena hasa wakati huu ambapo wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC wakikutana Dubai, huko Falme za Kiarabu kwenye mkutano wao wa 28 au COP28. Tayari hatua zimechukuliwa na shirika la kimataifa la Solar Sister kusaka nishati salama hasa kwa wanawake wa vijijini kama anavyoshuhudia mwanachama na mnufaika wake, Loveness Sabaya wa jamii ya kimasai kutoka Arusha nchini Tanzania kupitia video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X wa mkutano wa COP28.
6-12-2023 • 1 minuut, 39 seconden
06 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu Gaza na mkutano wa COP28. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tutasalia huko huko COP28, kulikoni?Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo amelaani vikali ukiukaji mkubwa wa haki wa kingono dhidi ya Waisraeli unaodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Hamas wakati wa mashambulizi yao ya kigaidi kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, huku wahudumu wa kibinadamu huko Gaza wakionya kuhusu hali mbaya ya raia, kutokana na kunaendelea kwa mashambulizi ya mabomu na watu kutawanywa eneo la kusini.Kila uchao, sauti zinapazwa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, tena hasa wakati huu ambapo wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC wakikutana Dubai, huko Falme za Kiarabu kwenye mkutano wao wa 28 au COP28. Tayari hatua zimechukuliwa na shirika la kimataifa la Solar Sister kusaka nishati salama hasa kwa wanawake wa vijijini kama anavyoshuhudia mwanachama na mnufaika wake, Loveness Sabaya wa jamii ya kimasai kutoka Arusha nchini Tanzania kupitia video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X wa mkutano wa COP28. Makala inakupeleka Zanzibar, Tanzania ambako Shirika lisilo la kiserikali la Milele Zanzibar Foundation limejenga kituo cha afya katika Shehia ya Michikichini - Unguja ikiwa ni utekelezaji wa lengo namba 3 la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu linalohusu Afya Bora na Ustawi. Na mashinani tunakupeleka katika mkutano wa COP28 huko Dubai, Umoja wa Falme za kiarabu kupata ufafanuzi kuhusu hasara na uharibifu. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
6-12-2023 • 0
06 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu Gaza na mkutano wa COP28. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tutasalia huko huko COP28, kulikoni?Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo amelaani vikali ukiukaji mkubwa wa haki wa kingono dhidi ya Waisraeli unaodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Hamas wakati wa mashambulizi yao ya kigaidi kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, huku wahudumu wa kibinadamu huko Gaza wakionya kuhusu hali mbaya ya raia, kutokana na kunaendelea kwa mashambulizi ya mabomu na watu kutawanywa eneo la kusini.Kila uchao, sauti zinapazwa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, tena hasa wakati huu ambapo wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC wakikutana Dubai, huko Falme za Kiarabu kwenye mkutano wao wa 28 au COP28. Tayari hatua zimechukuliwa na shirika la kimataifa la Solar Sister kusaka nishati salama hasa kwa wanawake wa vijijini kama anavyoshuhudia mwanachama na mnufaika wake, Loveness Sabaya wa jamii ya kimasai kutoka Arusha nchini Tanzania kupitia video iliyochapishwa kwenye ukurasa wa X wa mkutano wa COP28. Makala inakupeleka Zanzibar, Tanzania ambako Shirika lisilo la kiserikali la Milele Zanzibar Foundation limejenga kituo cha afya katika Shehia ya Michikichini - Unguja ikiwa ni utekelezaji wa lengo namba 3 la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu linalohusu Afya Bora na Ustawi. Na mashinani tunakupeleka katika mkutano wa COP28 huko Dubai, Umoja wa Falme za kiarabu kupata ufafanuzi kuhusu hasara na uharibifu. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
6-12-2023 • 10 minuten
Uchunguzi ufanywe Gaza kuhusu madai ya ukatili wa kingono wakati wa shambulio la Hamas - OHCHR
Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo amelaani vikali ukiukaji mkubwa wa haki wa kingono dhidi ya Waisraeli unaodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Hamas wakati wa mashambulizi yao ya kigaidi kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, huku wahudumu wa kibinadamu huko Gaza wakionya kuhusu hali mbaya ya raia. Kamishina mkuu Türk akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis amesisitiza kuhusu hofu yake kwa hatma ya raia akirejea wito wa kukomesha uhasama mara moja kunusuru Maisha ya raia na miundombinu yao. Na kuhusu madai ya Umoja wa Mataifa kuwa na misimamo miwili kunapokuja masuala ya ukatili Gaza amekanusha madai hayo na kubainisha kuwa amefahamishwa kuhusu madai ya unyanyasaji wa kijinsia na kingono wakati wa shambulio la Hamas kwa jamii za kusini mwa Israeli.Amesema kwa uchungu mkubwa kwamba “Ni bayana kwamba mashambulizi ya kikatili yanapaswa kuchunguzwa kikamilifu, kwa uchunguzi huru kwa sababu hilo ni deni letu kwa waathirika.”Juliette Touma, ambaye ni msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, wakati wa mahojiano na vyombo vya habari yaliyochapishwa mtandaoni leo kuhusu hali mbaya ya raia Gaza amesema "Nadhani tumegonga mwamba na ni hatua ya mabadiliko katika vita hivi hali inazidi kuwa mbaya kila dakika tunapokea simu za mara kwa mara za dharura kutoka kwa wafanyakazi wenzetu na marafiki."Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA mapambano yameshika kasi Israel ikishambulia kila kona kwa njia ya anga, baharini na ardhinihususan Mashariki mwa mji wa Gaza kwenye na kuna tarifa za takribani watu 60,000 kuwasili katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia na Khan Younis saa chache zilizopita na Hamas inaendelea kuvurumisha maroketi kwenda Israel kutokea Gaza.Mbali ya changamoto kubwa za kiafya kutokana na mrundikano wa watu na mazingira machafu sasa shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP WFP linaonya kuhusu janga kubwa la njaa.
6-12-2023 • 0
Uchunguzi ufanywe Gaza kuhusu madai ya ukatili wa kingono wakati wa shambulio la Hamas - OHCHR
Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo amelaani vikali ukiukaji mkubwa wa haki wa kingono dhidi ya Waisraeli unaodaiwa kutekelezwa na wanamgambo wa Hamas wakati wa mashambulizi yao ya kigaidi kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, huku wahudumu wa kibinadamu huko Gaza wakionya kuhusu hali mbaya ya raia. Kamishina mkuu Türk akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis amesisitiza kuhusu hofu yake kwa hatma ya raia akirejea wito wa kukomesha uhasama mara moja kunusuru Maisha ya raia na miundombinu yao. Na kuhusu madai ya Umoja wa Mataifa kuwa na misimamo miwili kunapokuja masuala ya ukatili Gaza amekanusha madai hayo na kubainisha kuwa amefahamishwa kuhusu madai ya unyanyasaji wa kijinsia na kingono wakati wa shambulio la Hamas kwa jamii za kusini mwa Israeli.Amesema kwa uchungu mkubwa kwamba “Ni bayana kwamba mashambulizi ya kikatili yanapaswa kuchunguzwa kikamilifu, kwa uchunguzi huru kwa sababu hilo ni deni letu kwa waathirika.”Juliette Touma, ambaye ni msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, wakati wa mahojiano na vyombo vya habari yaliyochapishwa mtandaoni leo kuhusu hali mbaya ya raia Gaza amesema "Nadhani tumegonga mwamba na ni hatua ya mabadiliko katika vita hivi hali inazidi kuwa mbaya kila dakika tunapokea simu za mara kwa mara za dharura kutoka kwa wafanyakazi wenzetu na marafiki."Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA mapambano yameshika kasi Israel ikishambulia kila kona kwa njia ya anga, baharini na ardhinihususan Mashariki mwa mji wa Gaza kwenye na kuna tarifa za takribani watu 60,000 kuwasili katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia na Khan Younis saa chache zilizopita na Hamas inaendelea kuvurumisha maroketi kwenda Israel kutokea Gaza.Mbali ya changamoto kubwa za kiafya kutokana na mrundikano wa watu na mazingira machafu sasa shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP WFP linaonya kuhusu janga kubwa la njaa.
6-12-2023 • 1 minuut, 53 seconden
Tushikamane kwa vitendo kupinga ukatili wa kijinsia - Mwanariadha
Violah Cheptoo au Violah Lagat ni maarufu sana sio tu nchini Kenya bali pia nje ya taifa hilo kutokana na umaarufu wake kwenye mbio za nyika au marathoni. Lakini zaidi ya hivyo, Viola anatambulika pia nje ya michezo kuwa mpeperushaji wa bendera ya kupinga ukatili wa kijinsia. Ni kwa mantiki hiyo katika siku hizi 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alitumia fursa ya uwepo wa mwanariadha huyo hapa Marekani wakati wa mbio za Marathoni jijini New York, Marekani mwezi ulipita wa Novemba kufahamu kwa kina usuli wa harakati hizo nje ya riadha na alianza kwa kumuuliza kuhusu taasisi aliyoanzisha mwaka 2021 inayoitwa Tirop’s Angels.
5-12-2023 • 0
Tushikamane kwa vitendo kupinga ukatili wa kijinsia - Mwanariadha
Violah Cheptoo au Violah Lagat ni maarufu sana sio tu nchini Kenya bali pia nje ya taifa hilo kutokana na umaarufu wake kwenye mbio za nyika au marathoni. Lakini zaidi ya hivyo, Viola anatambulika pia nje ya michezo kuwa mpeperushaji wa bendera ya kupinga ukatili wa kijinsia. Ni kwa mantiki hiyo katika siku hizi 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alitumia fursa ya uwepo wa mwanariadha huyo hapa Marekani wakati wa mbio za Marathoni jijini New York, Marekani mwezi ulipita wa Novemba kufahamu kwa kina usuli wa harakati hizo nje ya riadha na alianza kwa kumuuliza kuhusu taasisi aliyoanzisha mwaka 2021 inayoitwa Tirop’s Angels.
5-12-2023 • 5 minuten, 48 seconden
05 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alitumia fursa ya uwepo wa mwanariadha kutoka nchini Kenya hapa Marekani wakati wa mbio za Marathoni jijini New York, Marekani mwezi ulipita wa Novemba kufahamu kwa kina usuli wa harakati hizo nje ya riadha hasa kuhusu taasisi aliyoanzisha mwaka 2021 inayoitwa Tirop’s Angels. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 unaendelea huko Dubai na leo ukimulika mada mbalimbali ikiwemo kuongeza ufadhili kupambana na janga la tabianchi, kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kujenga mnepo katika sekta ya nishati hasa mifumo ya upoozaji ambayo imeelezwa kuwa ni mzigo mara mbili na inatumia kiwango kikubwa cha nitashi ya umeme hasa kwa viyoyozi na mitambo mingine , pia mkutano huo utasikia kutoka kwa watu wa jamii za asili.Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kuhusu kuendelea kwa hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza yakisema kati ya mchana wa tarehe 3 Desemba na tarehe 4 Desemba Gaza imeshuhudia mashambulizi makubwa Zaidi ya mabomu tangu kuanza kwa mzozo huu mpya kutoka angani, ardhini na baharini, huku maroketo yanayovurumishwa na kundi la Kipalestina la Hamas Kwenda Gaza nayo yakiendelea. Na mkutano wa Umoja wa Mataifa wa ulinzi wa Amani ulifungua pazia hii leo huko Accra Ghana ambako mawaziri na wajumbe kutoka nchi zaidi ya 85 na mashirika ya kimataifa wanakutana kwa siku mbili kwa mara ya kwanza barani Afrika, ili kuwapa fursa nchi wachangiaji wa vikosi vya ulinzi wa Amani kudhihirisha msaada wao wa kisiasa na kuahidi hatua madhubuti za kuimarisha juhudi za ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa kwenda sanjari na mahitaji na changamoto za sasa na zijazo.. Mashinani tunakuletea ujumbe wa mwanaharakati ambaye amezungumza na washirika wetu Radio Dumus katika sherehe za “SHE Leads” nchini Kenya, shirika lisilo la kiserikali linalopazia sauti masuala ya wanawake na wasichana, na anatumia fursa ya kusikilizwa kote duniani kupitia njia ya radio kuwasilisha ujumbe wake kuhusu ukatili wa kijinsia, GBV. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
5-12-2023 • 0
05 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alitumia fursa ya uwepo wa mwanariadha kutoka nchini Kenya hapa Marekani wakati wa mbio za Marathoni jijini New York, Marekani mwezi ulipita wa Novemba kufahamu kwa kina usuli wa harakati hizo nje ya riadha hasa kuhusu taasisi aliyoanzisha mwaka 2021 inayoitwa Tirop’s Angels. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 unaendelea huko Dubai na leo ukimulika mada mbalimbali ikiwemo kuongeza ufadhili kupambana na janga la tabianchi, kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kujenga mnepo katika sekta ya nishati hasa mifumo ya upoozaji ambayo imeelezwa kuwa ni mzigo mara mbili na inatumia kiwango kikubwa cha nitashi ya umeme hasa kwa viyoyozi na mitambo mingine , pia mkutano huo utasikia kutoka kwa watu wa jamii za asili.Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yameonya kuhusu kuendelea kwa hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza yakisema kati ya mchana wa tarehe 3 Desemba na tarehe 4 Desemba Gaza imeshuhudia mashambulizi makubwa Zaidi ya mabomu tangu kuanza kwa mzozo huu mpya kutoka angani, ardhini na baharini, huku maroketo yanayovurumishwa na kundi la Kipalestina la Hamas Kwenda Gaza nayo yakiendelea. Na mkutano wa Umoja wa Mataifa wa ulinzi wa Amani ulifungua pazia hii leo huko Accra Ghana ambako mawaziri na wajumbe kutoka nchi zaidi ya 85 na mashirika ya kimataifa wanakutana kwa siku mbili kwa mara ya kwanza barani Afrika, ili kuwapa fursa nchi wachangiaji wa vikosi vya ulinzi wa Amani kudhihirisha msaada wao wa kisiasa na kuahidi hatua madhubuti za kuimarisha juhudi za ulinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa kwenda sanjari na mahitaji na changamoto za sasa na zijazo.. Mashinani tunakuletea ujumbe wa mwanaharakati ambaye amezungumza na washirika wetu Radio Dumus katika sherehe za “SHE Leads” nchini Kenya, shirika lisilo la kiserikali linalopazia sauti masuala ya wanawake na wasichana, na anatumia fursa ya kusikilizwa kote duniani kupitia njia ya radio kuwasilisha ujumbe wake kuhusu ukatili wa kijinsia, GBV. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
5-12-2023 • 11 minuten, 21 seconden
Walio hatarini zaidi waletwe ‘mbele ya mstari’ wa ufadhili wa tabianchi - COP28
Leo huko Dubai, UAE kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira, COP28, Akaunti ya Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi imezinduliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura (OCHA) ili kutoa njia ya ziada ya kufadhili hatua za kibinadamu kwenye majanga yanayohusiana na tabianchi kama vile mafuriko, ukame, dhoruba na joto kali, na kujenga uwezo wa kustahimili tabianchi. COP28 inaendelea Dubai, na ni dhahiri wadau wa mazingira na tabianchi wameshaona kuna athari mbaa za mabadiliko ya tabianchi zinazoongeza machungu kwa wanadamu ambao wengine tayari wanakabiliwa na changamoto nyingine za kibinadamu. OCHA ambayo ni mdau muhimu wa misaada ya kibinadamu, pia ni sehemu muhimu ya Mfuko Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kukabiliana na Dharura (CERF), ambao kila mwaka, kati ya robo na theluthi ya ufadhili wake unaenda kwenye majanga yanayohusiana na tabianchi. Naibu wa Mkuu wa OCHA, Joyce Msuya amesisitiza umuhimu wa kuongeza ufadhili huu akisema "tunapoingia katika ulimwengu ambao mabadiliko ya tabianchi yanashikilia upanga juu ya kuongezeka kwa idadi ya watu". Jopo la serikali (duniani) kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC, takribani watu bilioni 3.5, karibu nusu ya wanadamu wote duniani, wanaishi katika maeneo ambayo yanaweza kuathiriwa sana na mabadiliko ya tabianchi. Ili kusaidia nchi zilizo hatarini katika kujilinda na matokeo mabaya zaidi ya uharibifu wa tabianchi, mfuko wa hasara na uharibifu ulikubaliwa katika COP27 huko Sharm el-Sheikh mwaka jana na kuidhinishwa kuanza kutumika siku ya ufunguzi wa COP28 umesifiwa kama chombo muhimu cha haki ya tabianchi na. matokeo makubwa ya kwanza ya mkusanyiko huo unaoendelea hadi tarehe 10 mwezi huu. Zaidi ya dola milioni 650 zimeripotiwa kuahidiwa kufikia sasa na watetezi wa jamii zilizo katika mazingira magumu waliopo Dubai wamesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba wale walioathirika zaidi wananufaika na ufadhili huo. Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Filippo Grandi amesisitiz, "Sauti ya wale waliofurushwa na dharura hii lazima isikike, na lazima wajumuishwe katika mipango na ugawaji wa rasilimali.
4-12-2023 • 0
Walio hatarini zaidi waletwe ‘mbele ya mstari’ wa ufadhili wa tabianchi - COP28
Leo huko Dubai, UAE kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira, COP28, Akaunti ya Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi imezinduliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura (OCHA) ili kutoa njia ya ziada ya kufadhili hatua za kibinadamu kwenye majanga yanayohusiana na tabianchi kama vile mafuriko, ukame, dhoruba na joto kali, na kujenga uwezo wa kustahimili tabianchi. COP28 inaendelea Dubai, na ni dhahiri wadau wa mazingira na tabianchi wameshaona kuna athari mbaa za mabadiliko ya tabianchi zinazoongeza machungu kwa wanadamu ambao wengine tayari wanakabiliwa na changamoto nyingine za kibinadamu. OCHA ambayo ni mdau muhimu wa misaada ya kibinadamu, pia ni sehemu muhimu ya Mfuko Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kukabiliana na Dharura (CERF), ambao kila mwaka, kati ya robo na theluthi ya ufadhili wake unaenda kwenye majanga yanayohusiana na tabianchi. Naibu wa Mkuu wa OCHA, Joyce Msuya amesisitiza umuhimu wa kuongeza ufadhili huu akisema "tunapoingia katika ulimwengu ambao mabadiliko ya tabianchi yanashikilia upanga juu ya kuongezeka kwa idadi ya watu". Jopo la serikali (duniani) kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC, takribani watu bilioni 3.5, karibu nusu ya wanadamu wote duniani, wanaishi katika maeneo ambayo yanaweza kuathiriwa sana na mabadiliko ya tabianchi. Ili kusaidia nchi zilizo hatarini katika kujilinda na matokeo mabaya zaidi ya uharibifu wa tabianchi, mfuko wa hasara na uharibifu ulikubaliwa katika COP27 huko Sharm el-Sheikh mwaka jana na kuidhinishwa kuanza kutumika siku ya ufunguzi wa COP28 umesifiwa kama chombo muhimu cha haki ya tabianchi na. matokeo makubwa ya kwanza ya mkusanyiko huo unaoendelea hadi tarehe 10 mwezi huu. Zaidi ya dola milioni 650 zimeripotiwa kuahidiwa kufikia sasa na watetezi wa jamii zilizo katika mazingira magumu waliopo Dubai wamesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba wale walioathirika zaidi wananufaika na ufadhili huo. Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Filippo Grandi amesisitiz, "Sauti ya wale waliofurushwa na dharura hii lazima isikike, na lazima wajumuishwe katika mipango na ugawaji wa rasilimali.
4-12-2023 • 2 minuten, 6 seconden
04 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia yaliyojiri katika Mkutano wa COP28 na miradi ya Benki ya Dunia nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani tunakuletea uchambuzi wa ibara ya 14 ya tamko la haki za binadamu.Leo huko Dubai, UAE kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira, COP28, Akaunti ya Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi imezinduliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura (OCHA) ili kutoa njia ya ziada ya kufadhili hatua za kibinadamu kwenye majanga yanayohusiana na tabianchi kama vile mafuriko, ukame, dhoruba na joto kali, na kujenga uwezo wa kustahimili tabianchi.Tarehe 19 Desemba mwaka 2019, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio namba 74/245, ambalo liliteua tarehe 4 Desemba kuwa Siku ya Kimataifa ya Benki kwa kutambua mchango mkubwa wa benki za maendeleo za kimataifa na benki nyingine za maendeleo za kimataifa katika kuleta maendeleo endelevu na kuchangia uboreshaji wa hali za maisha za wananchi. Makala inamulika siku ya watu wenye ulemavu duniani iliyoadhimishwa jana desemba 3 ikiwa na maudhui Ushirikiano katika hatua ya kuokoa na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, (SDGs) kwa pamoja na watu wenye ulemavu. Na ninakupeleka nchini Kenya kummulika mchezeshaji muziki au DJ mwenye ulemavu wa kutoona John Ndichu al maaruf, DJ Ndichi Kings. Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza naye akiwa eneo la Ruiru, Kaunti ya Kiambu. Na mashinani katika kuelekea siku ya haki za binadamu itakayoadhimishwa tayere 10 Desemba leo Dkt. Anna Henga mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania anatufafanulia kuhusu Ibara ya 14 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
4-12-2023 • 0
04 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia yaliyojiri katika Mkutano wa COP28 na miradi ya Benki ya Dunia nchini Tanzania. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani tunakuletea uchambuzi wa ibara ya 14 ya tamko la haki za binadamu.Leo huko Dubai, UAE kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mazingira, COP28, Akaunti ya Hatua Dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi imezinduliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu na Masuala ya Dharura (OCHA) ili kutoa njia ya ziada ya kufadhili hatua za kibinadamu kwenye majanga yanayohusiana na tabianchi kama vile mafuriko, ukame, dhoruba na joto kali, na kujenga uwezo wa kustahimili tabianchi.Tarehe 19 Desemba mwaka 2019, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio namba 74/245, ambalo liliteua tarehe 4 Desemba kuwa Siku ya Kimataifa ya Benki kwa kutambua mchango mkubwa wa benki za maendeleo za kimataifa na benki nyingine za maendeleo za kimataifa katika kuleta maendeleo endelevu na kuchangia uboreshaji wa hali za maisha za wananchi. Makala inamulika siku ya watu wenye ulemavu duniani iliyoadhimishwa jana desemba 3 ikiwa na maudhui Ushirikiano katika hatua ya kuokoa na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, (SDGs) kwa pamoja na watu wenye ulemavu. Na ninakupeleka nchini Kenya kummulika mchezeshaji muziki au DJ mwenye ulemavu wa kutoona John Ndichu al maaruf, DJ Ndichi Kings. Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza naye akiwa eneo la Ruiru, Kaunti ya Kiambu. Na mashinani katika kuelekea siku ya haki za binadamu itakayoadhimishwa tayere 10 Desemba leo Dkt. Anna Henga mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania anatufafanulia kuhusu Ibara ya 14 ya tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
4-12-2023 • 11 minuten, 1 seconde
Siku ya ulemavu duniani: Kauli kutoka kwa mchezesha muziki mwenye ulemavu wa kutoona
Siku ya watu wenye ulemavu duniani iliadhimishwa jana desemba 3 ikiwa na maudhui Ushirikiano katika hatua ya kuokoa na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, (SDGs) kwa pamoja na watu wenye ulemavu, na leo inakupeleka nchini Kenya kummulika mchezeshaji muziki au DJ mwenye ulemavu wa kutoona John Ndichu al maarufu, DJ NdichiKings. Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza naye akiwa eneo la Ruiru, Kaunti ya Kiambu.
4-12-2023 • 0
Siku ya ulemavu duniani: Kauli kutoka kwa mchezesha muziki mwenye ulemavu wa kutoona
Siku ya watu wenye ulemavu duniani iliadhimishwa jana desemba 3 ikiwa na maudhui Ushirikiano katika hatua ya kuokoa na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, (SDGs) kwa pamoja na watu wenye ulemavu, na leo inakupeleka nchini Kenya kummulika mchezeshaji muziki au DJ mwenye ulemavu wa kutoona John Ndichu al maarufu, DJ NdichiKings. Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza naye akiwa eneo la Ruiru, Kaunti ya Kiambu.
4-12-2023 • 3 minuten, 14 seconden
Nchini Tanzania Benki ya Dunia yasaidia ukuzaji wa rasilimali watu na maendeleo
Tarehe 19 Desemba mwaka 2019, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio namba 74/245, ambalo liliteua tarehe 4 Desemba kuwa Siku ya Kimataifa ya Benki kwa kutambua mchango mkubwa wa benki za maendeleo za kimataifa na benki nyingine za maendeleo za kimataifa katika kuleta maendeleo endelevu na kuchangia uboreshaji wa hali za maisha za wananchi. Afrika ni Bara lenye idadi kubwa ya watoto na vijana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatafsiri maana ya takwimu hizo. “Habari hii ni nzuri na vile vile ni mbaya kwetu, Hali hii inaweza kuwa nzuri na yenye tija iwapo tutawekeza kwenye rasilimali watu kwa kuhakikisha uwepo wa afya bora, elimu bora yenye stadi za maisha.” Benki ya Dunia, kama moja ya wadau wa Maendeleo katika nchi ya Tanzania kupitia chama chake cha maendeleo cha kimataifa IDA ikaitikia wito huo wa Rais Samia kwa kuwekeza katika nyanja mbalimbali na wanufaika wa miradi hiyo wanaeleza matunda ya uwekezaji.Dorice Msafiri wa jijini Dar es Salaam ni mnufaika wa miradi ya kuwainua wanawake “Naweza nikawashauri wanawake wengine ambao wangetamani kujiunga na na kozi za uhandisi ni mambo magumu lakini tunaweza wote. Kama ambavyo wanaweza wanaume na sisi pia tunaweza.”Mradi wau meme vijijini, Sofia Mkuya ni fundi cherehani kutoka Bahi mkoani Dodoma “Tangu umeme ulivyokuja ( katika eneo letu) ninashona mpaka usiku na ninatumia pasi ya umeme kunyoosha nguo situmii mkaa tena.” Mradi wa maji vijijini, Herman Mwendowasa mkazi wa kijiji cha Mtisi Villa mkoani Katavi, “Tumeondokana na changamoto ya maji machafu yenye tope maradhi, shida nyingi.” Na huko visiwani Zanzibar Benki ya Dunia inaendesha miradi mbalimbali ikiwemo wa nishati ya umeme wa Solar ambao utakapo kamilika unatarajiwa kutoa umeme Kilowati 132 kutoka Kilowati 32 zinazo zalisha hivi sasa. Mbali na mchango wao muhimu katika maendeleo ya Tanzania Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Nathan Belete anatoa pongezi, “Tunaipongeza serikali kwa kutoa kipaumbele kwenye elimu kwenye mkakati wao wa ukuaji kwakuzingatia idadi ya watu inaendelea kuongezeka nchini Tanzania hili ni suala muhimu kabisa.”
4-12-2023 • 0
Nchini Tanzania Benki ya Dunia yasaidia ukuzaji wa rasilimali watu na maendeleo
Tarehe 19 Desemba mwaka 2019, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio namba 74/245, ambalo liliteua tarehe 4 Desemba kuwa Siku ya Kimataifa ya Benki kwa kutambua mchango mkubwa wa benki za maendeleo za kimataifa na benki nyingine za maendeleo za kimataifa katika kuleta maendeleo endelevu na kuchangia uboreshaji wa hali za maisha za wananchi. Afrika ni Bara lenye idadi kubwa ya watoto na vijana na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatafsiri maana ya takwimu hizo. “Habari hii ni nzuri na vile vile ni mbaya kwetu, Hali hii inaweza kuwa nzuri na yenye tija iwapo tutawekeza kwenye rasilimali watu kwa kuhakikisha uwepo wa afya bora, elimu bora yenye stadi za maisha.” Benki ya Dunia, kama moja ya wadau wa Maendeleo katika nchi ya Tanzania kupitia chama chake cha maendeleo cha kimataifa IDA ikaitikia wito huo wa Rais Samia kwa kuwekeza katika nyanja mbalimbali na wanufaika wa miradi hiyo wanaeleza matunda ya uwekezaji.Dorice Msafiri wa jijini Dar es Salaam ni mnufaika wa miradi ya kuwainua wanawake “Naweza nikawashauri wanawake wengine ambao wangetamani kujiunga na na kozi za uhandisi ni mambo magumu lakini tunaweza wote. Kama ambavyo wanaweza wanaume na sisi pia tunaweza.”Mradi wau meme vijijini, Sofia Mkuya ni fundi cherehani kutoka Bahi mkoani Dodoma “Tangu umeme ulivyokuja ( katika eneo letu) ninashona mpaka usiku na ninatumia pasi ya umeme kunyoosha nguo situmii mkaa tena.” Mradi wa maji vijijini, Herman Mwendowasa mkazi wa kijiji cha Mtisi Villa mkoani Katavi, “Tumeondokana na changamoto ya maji machafu yenye tope maradhi, shida nyingi.” Na huko visiwani Zanzibar Benki ya Dunia inaendesha miradi mbalimbali ikiwemo wa nishati ya umeme wa Solar ambao utakapo kamilika unatarajiwa kutoa umeme Kilowati 132 kutoka Kilowati 32 zinazo zalisha hivi sasa. Mbali na mchango wao muhimu katika maendeleo ya Tanzania Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Nathan Belete anatoa pongezi, “Tunaipongeza serikali kwa kutoa kipaumbele kwenye elimu kwenye mkakati wao wa ukuaji kwakuzingatia idadi ya watu inaendelea kuongezeka nchini Tanzania hili ni suala muhimu kabisa.”
4-12-2023 • 2 minuten, 5 seconden
SHDEPHA+ yatekeleza kwa vitendo kauli ya UNAIDS ya jamii zishike hatamu kutokomeza Ukimwi
Leo ni siku ya Ukimwi duniani takwimu zikionesha kupungua sio tu kwa asilimia 70 ya vifo ikilinganishwa na mwaka 2004, idadi ilipokuwa kiwango cha juu zaidi duniani, bali pia maambukizi mapya ikilinganishwa na miaka ya 1980. Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la UNAIDS linasema miongoni mwa sababu za kupungua ni ushiriki wa jamii, yaani jamii kushika hatamu za vita dhidi ya Ukimwi. Hilo ni dhahiri huko nchini Tanzania ambako mashirika ya kiraia ikiwemo mtandao wa kitaifa wa maendeleo ya afya, huduma na uegemezi wa watu waishio na Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi, SHDEPHA+, unatekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa siku ya Ukimwi duniani, wa Achia Jamii Ziongoze Harakati dhidi ya Ukimwi. Assumpta Massoi anafafanua kinagaubaga kwenye makala hii kile kinachofanyika.
1-12-2023 • 0
SHDEPHA+ yatekeleza kwa vitendo kauli ya UNAIDS ya jamii zishike hatamu kutokomeza Ukimwi
Leo ni siku ya Ukimwi duniani takwimu zikionesha kupungua sio tu kwa asilimia 70 ya vifo ikilinganishwa na mwaka 2004, idadi ilipokuwa kiwango cha juu zaidi duniani, bali pia maambukizi mapya ikilinganishwa na miaka ya 1980. Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la UNAIDS linasema miongoni mwa sababu za kupungua ni ushiriki wa jamii, yaani jamii kushika hatamu za vita dhidi ya Ukimwi. Hilo ni dhahiri huko nchini Tanzania ambako mashirika ya kiraia ikiwemo mtandao wa kitaifa wa maendeleo ya afya, huduma na uegemezi wa watu waishio na Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi, SHDEPHA+, unatekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa siku ya Ukimwi duniani, wa Achia Jamii Ziongoze Harakati dhidi ya Ukimwi. Assumpta Massoi anafafanua kinagaubaga kwenye makala hii kile kinachofanyika.
1-12-2023 • 5 minuten, 22 seconden
01 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya UKIMWI duniani na Mkutano wa COP28. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani tunasalia hapa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kulikoni?Leo ni siku ya UKIMWI duniani ambapo mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa la kukabili ukimwi UNAIDS limetenga maudhui kuwa “Achia Jamii Ziongoze” kwa lengo la kuzisihi serikali kote duniani kutumia ipasavyo nguvu ya jamii mashinani ili hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi ifikapo mwaka 2030 huku Afrika, Kusini mwa Janga la Sahara ikitajwa kuwa muathirika mkumbwa wa maambukizi mapya ya VVU. Na sasa tuangazie majanga ya asili. Mkutano wa COP28 ukiendelea Dubai, Falme za kiarabu kusaka suluhu dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi, huko Somalia mafurikio makubwa yameendelea kusababisha zahma kwa wananchi ambapo Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA umezungumzia hali halisi na nini kinafanyika.Makala inatupeleka mkoani Shinyanga nchini Tanzania ambako huko mtandao wa kitaifa wa maendeleo ya afya, huduma na uegemezi wa watu waishio na Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi, SHDEPHA+, unatekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa siku ya Ukimwi duniani, Jamii iongoze katika harakati za kutokomeza Ukimwi.Katika mashinani utasikia ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabili Ukimwi UNAIDS. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
1-12-2023 • 0
01 DESEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya UKIMWI duniani na Mkutano wa COP28. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani tunasalia hapa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kulikoni?Leo ni siku ya UKIMWI duniani ambapo mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa la kukabili ukimwi UNAIDS limetenga maudhui kuwa “Achia Jamii Ziongoze” kwa lengo la kuzisihi serikali kote duniani kutumia ipasavyo nguvu ya jamii mashinani ili hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi ifikapo mwaka 2030 huku Afrika, Kusini mwa Janga la Sahara ikitajwa kuwa muathirika mkumbwa wa maambukizi mapya ya VVU. Na sasa tuangazie majanga ya asili. Mkutano wa COP28 ukiendelea Dubai, Falme za kiarabu kusaka suluhu dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi, huko Somalia mafurikio makubwa yameendelea kusababisha zahma kwa wananchi ambapo Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA umezungumzia hali halisi na nini kinafanyika.Makala inatupeleka mkoani Shinyanga nchini Tanzania ambako huko mtandao wa kitaifa wa maendeleo ya afya, huduma na uegemezi wa watu waishio na Virusi Vya Ukimwi na Ukimwi, SHDEPHA+, unatekeleza kwa vitendo ujumbe wa mwaka huu wa siku ya Ukimwi duniani, Jamii iongoze katika harakati za kutokomeza Ukimwi.Katika mashinani utasikia ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kukabili Ukimwi UNAIDS. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
1-12-2023 • 13 minuten, 51 seconden
Katika kutokomeza VVU mchango wa jamii hasa vijana unahitajika sana - Jane
Leo ni siku ya ukimwi duniani ambapo mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa la kukabili ukimwi UNAIDS limetenga maudhui kuwa “Achia Jamii Ziongoze” kwa lengo la kuzisihi serikali kote duniani kutumia ipasavyo nguvu ya jamii mashinani ili hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi ifikapo mwaka 2030 huku Afrika Kusini mwa Janga la Sahara ikitajwa kuwa muathirika mkumbwa wa maambukizi mapya ya VVU. Kwa mujibu wa takwimu za UNAIDS za mwaka huu 2023 wasichana vigori na vijana walichangia zaidi ya asilimia 77 ya maambukizi mapya ya VVU Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara mwaka jana 2022 miongoni mwa vijana wenye umri wa miaka 15-24.Na wasichana wana uwezekano mara tatu zaidi ya kupata VVU kuliko wenzao wa kiume. Kenya ikiwa ndani ya nchi 15 zenye maambukizi makubwa ya VVU Afrika juhudi kubwa zinafanywa kupitia serikali, asasi za kiraia na hata watu binafsi kusongesha mbele vita dhidi ya VVU kwa msaada wa wadau mbalimbali wa kitaifa na kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa ambao leo katia kuadhimisha siku hii jijini Nairobi umeandaa mashindano ya riadha ya kilometa 5 na kuchangisha fedha zitakazowasaidia yatima wa ugonjwa huo kama anavyofafanua Jane Sinyei Afisa Uratibu Msaidisi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Nairobi UNON.“Zile fedha ambayo tutapata itaenda kusaidia watoto wale wasio na wazazi, wasio na kitu chochote hivyo tutakuwa tunafanya kazi ya kusaidia wasiojiweza. Pia tutafanya vipimo vya VVUnkwa wale ambao watakuwa na virudsi hivyo wataelimishwa jinsi ya kufika kwa madaktari, kupata dawa na kwa wale ambao hawatakuwa na virusi vya ukimwi wataelimishwa jinsi ya kuendelea kujikinga na VVU ili wazuie kupata ukimwi na kusambazia wengine ukimwi.” Jane ana ujumbe kwa vijana ambao ndio kundi kubwa la waathirika wa VVU“Vijana tunawasihi mje msitari wa mbele , nyinyini viongozi wa leo na kesho na hapa Kenya mko wengi sana kuliko sisi. Mje mjifunze jinsi mtakavyojikinga na ukimwi, Homa ya ini aina B na magonjwa ya zinaa, na kuelimisha arafiki zenu ili wajikinge na haya magonjwa, muwe na afya bora ili muongize watu wote katika hii nchi yetu.”Nchi za Afrika zinazoongoza kwa VVU kwamujibu wa UNAUDS ni Eswatini inayoshika namba moja ikifuatiwa na Lesotho, Botswana na Zimbabwe. Tanzania inashika namba 11, Kenya 12 na Uganda ya 13.
1-12-2023 • 0
Katika kutokomeza VVU mchango wa jamii hasa vijana unahitajika sana - Jane
Leo ni siku ya ukimwi duniani ambapo mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa la kukabili ukimwi UNAIDS limetenga maudhui kuwa “Achia Jamii Ziongoze” kwa lengo la kuzisihi serikali kote duniani kutumia ipasavyo nguvu ya jamii mashinani ili hatimaye kutokomeza ugonjwa wa Ukimwi ifikapo mwaka 2030 huku Afrika Kusini mwa Janga la Sahara ikitajwa kuwa muathirika mkumbwa wa maambukizi mapya ya VVU. Kwa mujibu wa takwimu za UNAIDS za mwaka huu 2023 wasichana vigori na vijana walichangia zaidi ya asilimia 77 ya maambukizi mapya ya VVU Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara mwaka jana 2022 miongoni mwa vijana wenye umri wa miaka 15-24.Na wasichana wana uwezekano mara tatu zaidi ya kupata VVU kuliko wenzao wa kiume. Kenya ikiwa ndani ya nchi 15 zenye maambukizi makubwa ya VVU Afrika juhudi kubwa zinafanywa kupitia serikali, asasi za kiraia na hata watu binafsi kusongesha mbele vita dhidi ya VVU kwa msaada wa wadau mbalimbali wa kitaifa na kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa ambao leo katia kuadhimisha siku hii jijini Nairobi umeandaa mashindano ya riadha ya kilometa 5 na kuchangisha fedha zitakazowasaidia yatima wa ugonjwa huo kama anavyofafanua Jane Sinyei Afisa Uratibu Msaidisi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Nairobi UNON.“Zile fedha ambayo tutapata itaenda kusaidia watoto wale wasio na wazazi, wasio na kitu chochote hivyo tutakuwa tunafanya kazi ya kusaidia wasiojiweza. Pia tutafanya vipimo vya VVUnkwa wale ambao watakuwa na virudsi hivyo wataelimishwa jinsi ya kufika kwa madaktari, kupata dawa na kwa wale ambao hawatakuwa na virusi vya ukimwi wataelimishwa jinsi ya kuendelea kujikinga na VVU ili wazuie kupata ukimwi na kusambazia wengine ukimwi.” Jane ana ujumbe kwa vijana ambao ndio kundi kubwa la waathirika wa VVU“Vijana tunawasihi mje msitari wa mbele , nyinyini viongozi wa leo na kesho na hapa Kenya mko wengi sana kuliko sisi. Mje mjifunze jinsi mtakavyojikinga na ukimwi, Homa ya ini aina B na magonjwa ya zinaa, na kuelimisha arafiki zenu ili wajikinge na haya magonjwa, muwe na afya bora ili muongize watu wote katika hii nchi yetu.”Nchi za Afrika zinazoongoza kwa VVU kwamujibu wa UNAUDS ni Eswatini inayoshika namba moja ikifuatiwa na Lesotho, Botswana na Zimbabwe. Tanzania inashika namba 11, Kenya 12 na Uganda ya 13.
1-12-2023 • 3 minuten, 17 seconden
Mafuriko makubwa yaathiri wenyeji Somalia baada ya ukame wa miaka minne mfululizo
Mkutano wa COP28 ukiendelea Dubai, Falme za kiarabu kusaka suluhu dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi, huko Somalia mafurikio makubwa yameendelea kusababisha zahma kwa wananchi ambapo Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA umezungumzia hali halisi na nini kinafanyika. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya mtandao kutokea Mogadishu,Somalia, OCHA imebainisha kuwa Somalia inakabiliana na mafuriko yaliyoyaathiri maeneo mengi. Tangu mvua za msimu kuanza mwezi wa Oktoba,zaidi ya watu milioni 2 wameathirika.Milioni wameachwa bila makazi na wengine 100 wameuawa hasa katika maeneo ya Kusini Magharibi, Galmudug, Puntland, Hirshabelle, Banadir na Jubaland. Kwenye mkutano huo, Naibu mwakilishi maalum wa Katibu Mmkuu wa Umoja wa Mataifa,na mratibu wa misaada ya dharura, George Conway, alielezea kuwa ametiwa moyo na mashirika ya kibinadamu yanayoshirikiana na uongozi pamoja na jamii kuokoa maisha katika mazingira magumu. Mvua zinazoendelea na mafuriko yamesababisha mawasiliano kukatika, vijiji kuporomoka na barabara kuharibika. Kwa upande wake,Mkurugenzi wa muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Somalia, Nimo Hassan, amebainisha kuwa uharibifu mkubwa umetokea na ipo haja ya kuwekeza katika suluhu za kudumu za kupambana na mafuriko kadhalika kutoa tahadhari ya mapema ili kuokoa maisha ya Wasomali. Takwimu rasmi zinaashiria kuwa wahudumu wa dharura wamewafikia kiasi ya watu laki Nane na Elfu Ishirini (820,000) na kuwapa usaidizi wa kuokoa maisha ila mahitaji bado yanaongezeka kwasababu ya mafuriko. Kamishna wa mamlaka ya udhibiti wa hali ya dharura nchini Somalia Mahamud Moalim anasema hatua ya muhimu kwa sasa ni kuwaokoa walionasa kwenye mafuriko na kuwapa msaada wa haraka wa kibinadamu. Duru zinaeleza kuwa zahma hiyo inatokea wakati ambapo mamilioni ya raia wa Somalia wanakabiliana na njaa na utapiamlo huku watoto kiasi ya milioni 1.5 walio na umri wa chini ya miaka 5 huenda wakatatizwa na utapiamlo sugu katika kipindi cha agosti 2023 na Julai 2024. Mpango wa usaidizi wa dharura kwa Somalia kwa mwaka huu wa 2023 unahitaji dola bilioni 2.6 kukimu mahitaji ya watu milioni 7.6.
1-12-2023 • 0
Mafuriko makubwa yaathiri wenyeji Somalia baada ya ukame wa miaka minne mfululizo
Mkutano wa COP28 ukiendelea Dubai, Falme za kiarabu kusaka suluhu dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi, huko Somalia mafurikio makubwa yameendelea kusababisha zahma kwa wananchi ambapo Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA umezungumzia hali halisi na nini kinafanyika. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya mtandao kutokea Mogadishu,Somalia, OCHA imebainisha kuwa Somalia inakabiliana na mafuriko yaliyoyaathiri maeneo mengi. Tangu mvua za msimu kuanza mwezi wa Oktoba,zaidi ya watu milioni 2 wameathirika.Milioni wameachwa bila makazi na wengine 100 wameuawa hasa katika maeneo ya Kusini Magharibi, Galmudug, Puntland, Hirshabelle, Banadir na Jubaland. Kwenye mkutano huo, Naibu mwakilishi maalum wa Katibu Mmkuu wa Umoja wa Mataifa,na mratibu wa misaada ya dharura, George Conway, alielezea kuwa ametiwa moyo na mashirika ya kibinadamu yanayoshirikiana na uongozi pamoja na jamii kuokoa maisha katika mazingira magumu. Mvua zinazoendelea na mafuriko yamesababisha mawasiliano kukatika, vijiji kuporomoka na barabara kuharibika. Kwa upande wake,Mkurugenzi wa muungano wa mashirika yasiyo ya kiserikali ya Somalia, Nimo Hassan, amebainisha kuwa uharibifu mkubwa umetokea na ipo haja ya kuwekeza katika suluhu za kudumu za kupambana na mafuriko kadhalika kutoa tahadhari ya mapema ili kuokoa maisha ya Wasomali. Takwimu rasmi zinaashiria kuwa wahudumu wa dharura wamewafikia kiasi ya watu laki Nane na Elfu Ishirini (820,000) na kuwapa usaidizi wa kuokoa maisha ila mahitaji bado yanaongezeka kwasababu ya mafuriko. Kamishna wa mamlaka ya udhibiti wa hali ya dharura nchini Somalia Mahamud Moalim anasema hatua ya muhimu kwa sasa ni kuwaokoa walionasa kwenye mafuriko na kuwapa msaada wa haraka wa kibinadamu. Duru zinaeleza kuwa zahma hiyo inatokea wakati ambapo mamilioni ya raia wa Somalia wanakabiliana na njaa na utapiamlo huku watoto kiasi ya milioni 1.5 walio na umri wa chini ya miaka 5 huenda wakatatizwa na utapiamlo sugu katika kipindi cha agosti 2023 na Julai 2024. Mpango wa usaidizi wa dharura kwa Somalia kwa mwaka huu wa 2023 unahitaji dola bilioni 2.6 kukimu mahitaji ya watu milioni 7.6.
1-12-2023 • 2 minuten, 3 seconden
Methali: "Mwenye kelele hana maneno"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali MWENYE KELELE HANA MANENO.
30-11-2023 • 0
Methali: "Mwenye kelele hana maneno"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali MWENYE KELELE HANA MANENO.
30-11-2023 • 0
30 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 ukiwa umefunguliwa rasmi hii leo huko Dubai, utasikia ujumbe wa Ashraf Nyorano Mugenyi mwenye umri wa miaka 80 mkazi wa Hoima nchini Uganda. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwema za ukanda wa Gaza, mabadiliko ya tabianchi na Malaria, na tunakuletea uchambuzi wa methali MWENYE KELELE HANA MANENO. Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 umefungua pazia rasmi mjini Dubai katika Falme za nchi za Kiarabu kwa kuwaleta Pamoja wajumbe zaidi ya 60,000 kuangalia jinsi ya kuongeza hatua, fursa ya nyenzo za kujenga mnepo ikiwemo makubaliano ya kuanzishwa mfuko wa hasara na uharibifu ambayo yamepitishwa kwenye mkutano huo na pia kutumia ubunifu kudhibiti janga hilo. Tukisalia ma mabadiliko ya tabianchi ripoti mpya iliyotolewa leo kuhusu hali ya hewa duniani na shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO imethibitisha kwamba mwaka 2023 utavinja rekosi ya kuwa mwaka wenye joto Zaidi katika historia huku shirikika hilo likionya kuhusu mwenendo unaoashiria kutokea kwa mafuriko zaidi, moto wa nyika, kuyeyuka kwa barafuna joto la kupindukia katika siku zijazo.Na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO limesema katikia ripoti yake mpya iliyotolewa leo kwamba licha ya hatua kubwa zilizopigwa katika kupanua wigo wa kupata vyandarua vya mbu vyenye dawa pamoja dawa za kusaidia kuzuia malaria kwa watoto na kina mama wajawazito, watu wengi wamekuwa wakiugua malaria. Kwa mujibu wa shirika hilo mwaka 2022 kulikuwa na wagonjwa wa malaria milioni 249 duniani kote ikiwa ni wagonja milioni 16 zaidi ya ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali MWENYE KELELE HANA MANENO. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
30-11-2023 • 0
30 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 ukiwa umefunguliwa rasmi hii leo huko Dubai, utasikia ujumbe wa Ashraf Nyorano Mugenyi mwenye umri wa miaka 80 mkazi wa Hoima nchini Uganda. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwema za ukanda wa Gaza, mabadiliko ya tabianchi na Malaria, na tunakuletea uchambuzi wa methali MWENYE KELELE HANA MANENO. Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP28 umefungua pazia rasmi mjini Dubai katika Falme za nchi za Kiarabu kwa kuwaleta Pamoja wajumbe zaidi ya 60,000 kuangalia jinsi ya kuongeza hatua, fursa ya nyenzo za kujenga mnepo ikiwemo makubaliano ya kuanzishwa mfuko wa hasara na uharibifu ambayo yamepitishwa kwenye mkutano huo na pia kutumia ubunifu kudhibiti janga hilo. Tukisalia ma mabadiliko ya tabianchi ripoti mpya iliyotolewa leo kuhusu hali ya hewa duniani na shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO imethibitisha kwamba mwaka 2023 utavinja rekosi ya kuwa mwaka wenye joto Zaidi katika historia huku shirikika hilo likionya kuhusu mwenendo unaoashiria kutokea kwa mafuriko zaidi, moto wa nyika, kuyeyuka kwa barafuna joto la kupindukia katika siku zijazo.Na Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO limesema katikia ripoti yake mpya iliyotolewa leo kwamba licha ya hatua kubwa zilizopigwa katika kupanua wigo wa kupata vyandarua vya mbu vyenye dawa pamoja dawa za kusaidia kuzuia malaria kwa watoto na kina mama wajawazito, watu wengi wamekuwa wakiugua malaria. Kwa mujibu wa shirika hilo mwaka 2022 kulikuwa na wagonjwa wa malaria milioni 249 duniani kote ikiwa ni wagonja milioni 16 zaidi ya ilivyokuwa kabla ya janga la COVID-19.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali MWENYE KELELE HANA MANENO. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
30-11-2023 • 12 minuten, 20 seconden
Simulizi: Jina langu ni Selemani lakini nilikuwa naitwa Selina
Wakati kila kona ya dunia kwa sasa ikiadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, harakati hizo miaka ya 1987 hazikuwa rahisi kueleweka ndani ya baadhi ya jamii kwani mila na destuli ambazo nyingine zilijikita katika mfumo dume ndizo zilizokuwa zimetamalaki. Lakini wanaharakati walitumia mbinu mbalimbali hata kubadili majina ili waweze kufanya kazi ya kubadilisha mitazamo ndani ya jamii. Mwandishi wa habari nguli Selemani Mkufya kutoka nchini Tanzania anatusimulia alivyofanya kazi na chama cha waandishi wa habari wanawake -TAMWA ambapo huko alikuwa akiitwa Selina badala ya Selemani.
29-11-2023 • 0
Simulizi: Jina langu ni Selemani lakini nilikuwa naitwa Selina
Wakati kila kona ya dunia kwa sasa ikiadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, harakati hizo miaka ya 1987 hazikuwa rahisi kueleweka ndani ya baadhi ya jamii kwani mila na destuli ambazo nyingine zilijikita katika mfumo dume ndizo zilizokuwa zimetamalaki. Lakini wanaharakati walitumia mbinu mbalimbali hata kubadili majina ili waweze kufanya kazi ya kubadilisha mitazamo ndani ya jamii. Mwandishi wa habari nguli Selemani Mkufya kutoka nchini Tanzania anatusimulia alivyofanya kazi na chama cha waandishi wa habari wanawake -TAMWA ambapo huko alikuwa akiitwa Selina badala ya Selemani.
29-11-2023 • 3 minuten, 18 seconden
Tunaadhimisha siku hii nyakati za kiza kwa watu wa Palestina - Guterres
Umoja wa Mataifa leo umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, katika nyakati ambazo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameziita mojawapo ya nyakati za kiza katika historia ya watu wa Palestina na hivyo akasisitiza mshikamano zaidi na kutafuta suluhu ya kudumu. Bwana Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina, kwa njia ya maandishi amesema zaidi ya yote yanayoendelea, hii ni siku ya kuthibitisha mshikamano wa kimataifa na watu wa Palestina na haki yao ya kuishi kwa amani na utu. Guterres ameendelea kusisitiza suluhisho la Serikali mbili, kwa msingi wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa, ili Israeli na Palestina ziishi kwa pamoja kwa amani na usalama na mji wa Jerusalem uwe mji mkuu wa Mataifa yote mawili. “Umoja wa Mataifa hautayumba katika kujitolea kwake kwa watu wa Palestina,” anahitimisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akihimiza kuwa leo na kila siku, ulimwengu usimame katika mshikamano na matarajio ya wananchi wa Palestina kufikia haki zao zisizoweza kupokonywa na kujenga mustakbali wa amani, haki, usalama na utu kwa wote. Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, amesema, "Mshikamano wa kimataifa tunaoueleza leo unathibitisha kwamba hitaji la haki za Wakimbizi wa Kipalestina kama ilivyoainishwa katika maazimio ya Umoja wa Mataifa, ni muhimu zaidi sasa kuliko hapo awali." Kwa hiyo anatoa wito kwa ulimwengu kushirikiana kuelekea, “haki na amani kwa Wakimbizi wa Kipalestina, ambao hawahitaji msaada tu, bali suluhisho la haki na la kudumu." Maadhimisho ya mwaka huu ya Siku hii ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, kwa Umoja wa Mataifa yamefanyika katika makao makuu jijini New York, Marekani, Geneva Uswisi, Vienna Austria na Nairobi Kenya. Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina huadhimishwa na Umoja wa Mataifa kila tarehe 29 Novemba kila mwaka, kwa mujibu wa mamlaka za Baraza Kuu katika maazimio 32/40 B ya 2 Desemba 1977, na 34/65 D ya 12 Desemba 1979 na maazimio yaliyofuata yaliyopitishwa chini ya kipengele cha ajenda "Suala la Palestina." Tarehe 29 Novemba ilichaguliwa kwa sababu ya maana na umuhimu wake kwa watu wa Palestina. Siku hiyo ya 1947, Baraza Kuu lilipitisha azimio namba 181 (II), ambalo lilikuja kuitwa Azimio la Kugawanyika. Azimio hilo lilitoa fursa ya kuanzishwa huko Palestina "Nchi ya Kiyahudi" na "Nchi ya Kiarabu", na Jerusalem kama mji mkuu wa pamoja chini ya utawala maalum wa kimataifa. Kati ya Mataifa mawili yaliyopitishwa kuundwa chini ya azimio hili, ni moja tu, Israeli, ambalo limeundwa hadi sasa.
29-11-2023 • 0
Tunaadhimisha siku hii nyakati za kiza kwa watu wa Palestina - Guterres
Umoja wa Mataifa leo umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, katika nyakati ambazo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameziita mojawapo ya nyakati za kiza katika historia ya watu wa Palestina na hivyo akasisitiza mshikamano zaidi na kutafuta suluhu ya kudumu. Bwana Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina, kwa njia ya maandishi amesema zaidi ya yote yanayoendelea, hii ni siku ya kuthibitisha mshikamano wa kimataifa na watu wa Palestina na haki yao ya kuishi kwa amani na utu. Guterres ameendelea kusisitiza suluhisho la Serikali mbili, kwa msingi wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa, ili Israeli na Palestina ziishi kwa pamoja kwa amani na usalama na mji wa Jerusalem uwe mji mkuu wa Mataifa yote mawili. “Umoja wa Mataifa hautayumba katika kujitolea kwake kwa watu wa Palestina,” anahitimisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akihimiza kuwa leo na kila siku, ulimwengu usimame katika mshikamano na matarajio ya wananchi wa Palestina kufikia haki zao zisizoweza kupokonywa na kujenga mustakbali wa amani, haki, usalama na utu kwa wote. Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, amesema, "Mshikamano wa kimataifa tunaoueleza leo unathibitisha kwamba hitaji la haki za Wakimbizi wa Kipalestina kama ilivyoainishwa katika maazimio ya Umoja wa Mataifa, ni muhimu zaidi sasa kuliko hapo awali." Kwa hiyo anatoa wito kwa ulimwengu kushirikiana kuelekea, “haki na amani kwa Wakimbizi wa Kipalestina, ambao hawahitaji msaada tu, bali suluhisho la haki na la kudumu." Maadhimisho ya mwaka huu ya Siku hii ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, kwa Umoja wa Mataifa yamefanyika katika makao makuu jijini New York, Marekani, Geneva Uswisi, Vienna Austria na Nairobi Kenya. Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina huadhimishwa na Umoja wa Mataifa kila tarehe 29 Novemba kila mwaka, kwa mujibu wa mamlaka za Baraza Kuu katika maazimio 32/40 B ya 2 Desemba 1977, na 34/65 D ya 12 Desemba 1979 na maazimio yaliyofuata yaliyopitishwa chini ya kipengele cha ajenda "Suala la Palestina." Tarehe 29 Novemba ilichaguliwa kwa sababu ya maana na umuhimu wake kwa watu wa Palestina. Siku hiyo ya 1947, Baraza Kuu lilipitisha azimio namba 181 (II), ambalo lilikuja kuitwa Azimio la Kugawanyika. Azimio hilo lilitoa fursa ya kuanzishwa huko Palestina "Nchi ya Kiyahudi" na "Nchi ya Kiarabu", na Jerusalem kama mji mkuu wa pamoja chini ya utawala maalum wa kimataifa. Kati ya Mataifa mawili yaliyopitishwa kuundwa chini ya azimio hili, ni moja tu, Israeli, ambalo limeundwa hadi sasa.
29-11-2023 • 1 minuut, 47 seconden
29 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina na siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Makala tunakupeleka nchini na mashinanini nchini Tanzania, kulikoni? Umoja wa Mataifa leo umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, katika nyakati ambazo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameziita mojawapo ya nyakati za kiza kwa watu wa Palestina na hivyo akasisitiza mshikamano zaidi na kutafuta suluhu ya kudumu.. Wakati dunia ikiendelea na maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza November 25 na zitafikia ukingoni December 10,2023, juhudi za kukabiliana na makovu yatokanayo na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia zimeanza kuzaa matunda kwa wanawake kujua na kutambua haki zao za msingi. Angela Muhindo ni mkazi wa Wilaya ya kasese nchini Uganda,ni miongoni mwa waathirika wa ukatili wa kijinsia na licha ya mikikimikiki aliyokutana nayo amefanikiwa kufungua ukurasa mpya na sasa anawatetea wanawake wengine baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women.Katika makala harakati za kuhakikisha kuna usawa kijinsia zinahitaji mikakati mbalimbali na mmoja kati ya mikakati iliyotumiwa na Chama cha waandishi wa Habari wanawake nchini Tanzani TAMWA ilikuwa ni kufanya kazi na waandishi wanaume na wakawapa majina ya kike.Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kutoka kwa kijana mwanaharakati wa mazingira na mnufaika wa mafunzo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
29-11-2023 • 0
29 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya mshikamano na watu wa Palestina na siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia. Makala tunakupeleka nchini na mashinanini nchini Tanzania, kulikoni? Umoja wa Mataifa leo umeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina, katika nyakati ambazo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameziita mojawapo ya nyakati za kiza kwa watu wa Palestina na hivyo akasisitiza mshikamano zaidi na kutafuta suluhu ya kudumu.. Wakati dunia ikiendelea na maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza November 25 na zitafikia ukingoni December 10,2023, juhudi za kukabiliana na makovu yatokanayo na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia zimeanza kuzaa matunda kwa wanawake kujua na kutambua haki zao za msingi. Angela Muhindo ni mkazi wa Wilaya ya kasese nchini Uganda,ni miongoni mwa waathirika wa ukatili wa kijinsia na licha ya mikikimikiki aliyokutana nayo amefanikiwa kufungua ukurasa mpya na sasa anawatetea wanawake wengine baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women.Katika makala harakati za kuhakikisha kuna usawa kijinsia zinahitaji mikakati mbalimbali na mmoja kati ya mikakati iliyotumiwa na Chama cha waandishi wa Habari wanawake nchini Tanzani TAMWA ilikuwa ni kufanya kazi na waandishi wanaume na wakawapa majina ya kike.Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kutoka kwa kijana mwanaharakati wa mazingira na mnufaika wa mafunzo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
29-11-2023 • 10 minuten, 45 seconden
Simulizi ya Angela Muhindo - Nimejikomboa nataka kila anayekatiliwa kujikomboa pia
Wakati dunia ikiendelea na maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza November 25 na zitafikia ukingoni December 10,2023, juhudi za kukabiliana na makovu yatokanayo na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia zimeanzakuzaa matunda kwa wanawake kujua na kutambua haki zao za msingi. Angela Muhindo ni mkazi wa Wilaya ya kasese nchini Uganda,ni miongoni mwa waathirika wa ukatili wa kijinsia na licha ya mikikimikiki aliyokutana nayo amefanikiwa kufungua ukurasa mpya na sasa anawatetea wanawake wengine baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women.Angela ambaye baada ya kukatiliwa sasa amekuwa mchagizaji mkubwa wa kupambana na ukatili dhidi ya wanawake, anasema, "Wanawake wana nguvu kidogo, lakini kama wewe ni mlemavu uko katika hatari zaidi ya kukatiliwa."Ulimwenguni kote wanawake na wasichana wenye ulemavu wana uwezekano zaidi ya mara mbili ya wanawake wengine kukumbwa na ukatili wa kijinsia, Angela anaeleza jinsi mambo yalivyo badilika, “Baada ya mama kufariki nilirithi ardhi yake lakini wajomba zangu walijaribu kuichukua kwa nguvu, kwani wameamini sina haki, bila ardhi, huna nyumba, chakula, na kipato huna hivyo wanaume watakutumia vibaya.”Angela anaongeza kwamba, “Nilipata mafunzo ya haki za wanawake, haki za walemavu na haki ya ardhi, nilijifunza mimi ni sawa na kila mtu, naweza kumiliki ardhi kama mtu mwingine yeyote, hivyo nilianza mchakato wa kuidai, haikuwa rahisi lakini hatimaye ikawekwa jina langu. Ninakuwa sauti kwa wasio na sauti ili kuwazuia wasipate kile ninachotaka kupitia, natumai wengine watasimamia haki zao kama nilivyofanya, nina ardhi yangu, ardhi hii ndio kila kitu nina nyumba inanipatia chakula na kipato.”Angela baada ya kujikomboa sasa amekuwa mkombozi kwa wanawake wengine. zaidi ya watu 300,000 nchini Uganda wamehudhuria programu za jumuiya kuhusu haki za wanawake tangu 2009, huku wakiungwa mkono na mpango wa uangalizi kupitia UN Women, chombo cha Umoja wa Mataifa kinachopambania usawa wa kijinsia.
29-11-2023 • 0
Simulizi ya Angela Muhindo - Nimejikomboa nataka kila anayekatiliwa kujikomboa pia
Wakati dunia ikiendelea na maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza November 25 na zitafikia ukingoni December 10,2023, juhudi za kukabiliana na makovu yatokanayo na vitendo vya ukatili, unyanyasaji na ubaguzi wa kijinsia zimeanzakuzaa matunda kwa wanawake kujua na kutambua haki zao za msingi. Angela Muhindo ni mkazi wa Wilaya ya kasese nchini Uganda,ni miongoni mwa waathirika wa ukatili wa kijinsia na licha ya mikikimikiki aliyokutana nayo amefanikiwa kufungua ukurasa mpya na sasa anawatetea wanawake wengine baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya Wanawake UN Women.Angela ambaye baada ya kukatiliwa sasa amekuwa mchagizaji mkubwa wa kupambana na ukatili dhidi ya wanawake, anasema, "Wanawake wana nguvu kidogo, lakini kama wewe ni mlemavu uko katika hatari zaidi ya kukatiliwa."Ulimwenguni kote wanawake na wasichana wenye ulemavu wana uwezekano zaidi ya mara mbili ya wanawake wengine kukumbwa na ukatili wa kijinsia, Angela anaeleza jinsi mambo yalivyo badilika, “Baada ya mama kufariki nilirithi ardhi yake lakini wajomba zangu walijaribu kuichukua kwa nguvu, kwani wameamini sina haki, bila ardhi, huna nyumba, chakula, na kipato huna hivyo wanaume watakutumia vibaya.”Angela anaongeza kwamba, “Nilipata mafunzo ya haki za wanawake, haki za walemavu na haki ya ardhi, nilijifunza mimi ni sawa na kila mtu, naweza kumiliki ardhi kama mtu mwingine yeyote, hivyo nilianza mchakato wa kuidai, haikuwa rahisi lakini hatimaye ikawekwa jina langu. Ninakuwa sauti kwa wasio na sauti ili kuwazuia wasipate kile ninachotaka kupitia, natumai wengine watasimamia haki zao kama nilivyofanya, nina ardhi yangu, ardhi hii ndio kila kitu nina nyumba inanipatia chakula na kipato.”Angela baada ya kujikomboa sasa amekuwa mkombozi kwa wanawake wengine. zaidi ya watu 300,000 nchini Uganda wamehudhuria programu za jumuiya kuhusu haki za wanawake tangu 2009, huku wakiungwa mkono na mpango wa uangalizi kupitia UN Women, chombo cha Umoja wa Mataifa kinachopambania usawa wa kijinsia.
29-11-2023 • 2 minuten, 25 seconden
28 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo hivi sasa dunia inaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza tarehe 25 Novemba na zinaendelea mpaka tarehe 10 Desemba ikienda sambamba na Kampeni ya UNGANISHA au UNITE iliyoanzishwa mwaka 2008. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani. Mkimbizi wa zamani na mwandishi wa habari Abdullahi Mire kutangazwa mshindi wa kimataifa wa tuzo ya Nansen ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kuwa kinara wa haki ya elimu kwa wote. Kupitia mradi wake ulioko kambi ya wakimbizi ya Dadaab kaskazini-mashariki mwa Kenya, Mire amefanikiwa kuzindua maktaba iliyo na vitabu laki moja vinavyosomwa na watoto walio ukimbizini. Kwingineko huko Ukanda wa Gaza, ikiwa ni siku ya tano ya sitisho la mapigano msemaij wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF James Elder ambaye ametembelea eneo hilo amesema ameshuhudia hofu waliyo nayo madaktari ya milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu na magonjwa ya njia ya hewa. Taka hazijakusanywa muda mrefu kwenye makazi ya wakimbizi na wagonjwa hawana uwezo wa kufikia huduma.Na kuelekea siku ya Ukimwi duniani tarehe Mosi mwezi ujao wa Desemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kukabili Ukimwi, UNAIDS limetoa ripoti yake leo inayoainisha nafasi muhimu ya jamii mashinani katika kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030. Kwa mantiki hiyo imezitaka serikali kutumia nguvu ya jamii kwenye vita dhidi ya Ukimwi.Na mashinani tutaelekea jijini Geneva, nchini Uswsi, kusikia ujumbe kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa, la Uhamiaji, IOM kuhusu mapambano dhidi ya ukatili sagini kijinsia. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
28-11-2023 • 0
28 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo hivi sasa dunia inaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zilizoanza tarehe 25 Novemba na zinaendelea mpaka tarehe 10 Desemba ikienda sambamba na Kampeni ya UNGANISHA au UNITE iliyoanzishwa mwaka 2008. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani. Mkimbizi wa zamani na mwandishi wa habari Abdullahi Mire kutangazwa mshindi wa kimataifa wa tuzo ya Nansen ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kuwa kinara wa haki ya elimu kwa wote. Kupitia mradi wake ulioko kambi ya wakimbizi ya Dadaab kaskazini-mashariki mwa Kenya, Mire amefanikiwa kuzindua maktaba iliyo na vitabu laki moja vinavyosomwa na watoto walio ukimbizini. Kwingineko huko Ukanda wa Gaza, ikiwa ni siku ya tano ya sitisho la mapigano msemaij wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF James Elder ambaye ametembelea eneo hilo amesema ameshuhudia hofu waliyo nayo madaktari ya milipuko ya magonjwa kama vile kipindupindu na magonjwa ya njia ya hewa. Taka hazijakusanywa muda mrefu kwenye makazi ya wakimbizi na wagonjwa hawana uwezo wa kufikia huduma.Na kuelekea siku ya Ukimwi duniani tarehe Mosi mwezi ujao wa Desemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kukabili Ukimwi, UNAIDS limetoa ripoti yake leo inayoainisha nafasi muhimu ya jamii mashinani katika kutokomeza Ukimwi ifikapo mwaka 2030. Kwa mantiki hiyo imezitaka serikali kutumia nguvu ya jamii kwenye vita dhidi ya Ukimwi.Na mashinani tutaelekea jijini Geneva, nchini Uswsi, kusikia ujumbe kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa, la Uhamiaji, IOM kuhusu mapambano dhidi ya ukatili sagini kijinsia. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
28-11-2023 • 14 minuten, 25 seconden
Misaada tunapata lakini tunachohitaji zaidi ni amani- Mkimbizi wa ndani DRC
Hivi karibuni tulinukuu mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR na lile la kuhudumia watoto UNICEF yakielezea wasiwasi wao mkubwa juu ya kushamiri hivi karibuni kwa mzozo wa kibinadamu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Mapigano makali kati ya jeshi la serikali na vikundi vilivyojihami katika muda wa wiki sita tu yamesababisha watu 450,000 kukimbia makwao kutoka maeneo ya Rutshuru na Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini. Evarist Mapesa wa Idhaa hii ameamua kufuatilia hao waliong’olewa kwenye makazi yao kusikia kile walichopitia na madhila gani yanawakumba. Ukisikia mhusika wakisema mumwezi anamaanisha mwezi, mnane ni nane na saa kenda ni saa tisa. Kwako Evarist.
27-11-2023 • 0
Misaada tunapata lakini tunachohitaji zaidi ni amani- Mkimbizi wa ndani DRC
Hivi karibuni tulinukuu mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR na lile la kuhudumia watoto UNICEF yakielezea wasiwasi wao mkubwa juu ya kushamiri hivi karibuni kwa mzozo wa kibinadamu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC. Mapigano makali kati ya jeshi la serikali na vikundi vilivyojihami katika muda wa wiki sita tu yamesababisha watu 450,000 kukimbia makwao kutoka maeneo ya Rutshuru na Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini. Evarist Mapesa wa Idhaa hii ameamua kufuatilia hao waliong’olewa kwenye makazi yao kusikia kile walichopitia na madhila gani yanawakumba. Ukisikia mhusika wakisema mumwezi anamaanisha mwezi, mnane ni nane na saa kenda ni saa tisa. Kwako Evarist.
27-11-2023 • 3 minuten, 19 seconden
COP28 ihakikishe inamulika jinsi ya kupunguza vifo vitokanavyo na janga la tabianchi- WHO
Kuelekea mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 huko Dubai, Falme za kiarabu tarehe 30 mwezi huu wa Novemba, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, limesema washiriki wanapaswa waelewe kuwa suala la afya ndilo linapaswa kuchochea majadiliano wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kushamiri duniani kote. Dkt, María Neira ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Umma na Mazingira, WHO ameiambia Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi ya kwamba. “wajumbe wanapaswa kuelewa kuwa hawajadili tu punguzo la kiwango cha utoaji wa hewa chafuzi kila mwaka, bali wanajadili pia idadi ya wagonjwa wa pumu, idadi ya wagonjwa wa njia ya hewa, idadi ya wagonjwa wa saratani ya mapafu, idadi ya wagonjwa wa magonjwa yanayohusiana na kukabiliana na hewa chafu au madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Wanahitaji kuelewa wanajadili afya yetu vile vile.” Dkt. Neira amesema pamoja na hilo, wanataka washiriki pia waelewe kuwa iwapo watachukua hatua sahihi, mathalani kushughulikia visababishi vya mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa na miji isiyo na uchafuzi, nishati safi na endelevu, hatua hizo zitakuwa na manufaa kwa afya ya kila mtu. Ndipo akatolea mfano iwapo hatua sahihi za kukabili tabianchi zikichukuliwa na matunda yatakayopatikana ifikapo mwaka 2030, “iwapo tunaangalia afya ya umma, ningependa kupunguza kabisa vifo vya watoto wachanga vinavyosababishwa na uchafuzi wa hewa, ambavyo ni watoto milioni 7 hufia tumboni mwa mama zao. Kwa hiyo tukiongeza upatikanaji wa nishati safi, yaani kwa kuwa tu na hewa safi, tunaweza kupunguza vifo milioni 5 kila mwaka.” Kwa mujibu wa WHO madhara ya mabadiliko ya tabianchi yamekuwa makubwa zaidi kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, halikadhalika nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia na pia nchi za visiwa vidogo. Katika mkutano huo wa COP28 kwa mara ya kwanza kutakuwa na Siku ya Afya ambapo washiriki watajikita zaidi kujadili jinsi tabianchi inarudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya afya.
27-11-2023 • 0
COP28 ihakikishe inamulika jinsi ya kupunguza vifo vitokanavyo na janga la tabianchi- WHO
Kuelekea mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 huko Dubai, Falme za kiarabu tarehe 30 mwezi huu wa Novemba, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, limesema washiriki wanapaswa waelewe kuwa suala la afya ndilo linapaswa kuchochea majadiliano wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kushamiri duniani kote. Dkt, María Neira ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Afya ya Umma na Mazingira, WHO ameiambia Idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi ya kwamba. “wajumbe wanapaswa kuelewa kuwa hawajadili tu punguzo la kiwango cha utoaji wa hewa chafuzi kila mwaka, bali wanajadili pia idadi ya wagonjwa wa pumu, idadi ya wagonjwa wa njia ya hewa, idadi ya wagonjwa wa saratani ya mapafu, idadi ya wagonjwa wa magonjwa yanayohusiana na kukabiliana na hewa chafu au madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Wanahitaji kuelewa wanajadili afya yetu vile vile.” Dkt. Neira amesema pamoja na hilo, wanataka washiriki pia waelewe kuwa iwapo watachukua hatua sahihi, mathalani kushughulikia visababishi vya mabadiliko ya tabianchi kwa kuwa na miji isiyo na uchafuzi, nishati safi na endelevu, hatua hizo zitakuwa na manufaa kwa afya ya kila mtu. Ndipo akatolea mfano iwapo hatua sahihi za kukabili tabianchi zikichukuliwa na matunda yatakayopatikana ifikapo mwaka 2030, “iwapo tunaangalia afya ya umma, ningependa kupunguza kabisa vifo vya watoto wachanga vinavyosababishwa na uchafuzi wa hewa, ambavyo ni watoto milioni 7 hufia tumboni mwa mama zao. Kwa hiyo tukiongeza upatikanaji wa nishati safi, yaani kwa kuwa tu na hewa safi, tunaweza kupunguza vifo milioni 5 kila mwaka.” Kwa mujibu wa WHO madhara ya mabadiliko ya tabianchi yamekuwa makubwa zaidi kwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, halikadhalika nchi za Kusini-Mashariki mwa Asia na pia nchi za visiwa vidogo. Katika mkutano huo wa COP28 kwa mara ya kwanza kutakuwa na Siku ya Afya ambapo washiriki watajikita zaidi kujadili jinsi tabianchi inarudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kwenye sekta ya afya.
27-11-2023 • 2 minuten, 23 seconden
Heko waliofanikisha sitisho la mapigano Gaza - Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezipongeza serikali za Qatar, Misri na Marekani pamoja na kutambua jukumu muhimu la kamati ya Kimataifa ya chama cha msalaba mwekudu kwa juhudi zao za kuhakikisha mapigano yanasitishwa kwa muda, mateka na wafungwa wanaachiwa pamoja na kuingiza misaada huko Ukanda wa Gaza. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Flora NduchaMapigano ya wiki saba huko Gaza na Israel yameleta hali mbaya sana ambayo imeshangaza ulimwengu. Lakini kwa muda wa siku nne sasa, Mapigano hayo yamesitishwa, Mateka wa Israel na mataifa mengine ya kigeni wanaoshikiliwa na Hamas tangu tarehe 7 Oktoba wameanza kuachiliwa na wafungwa wa Kipalestina wanafunguliwa kutoka jela za Israel.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia Msemaji wake Stéphane Dujarric hii leo hapa jijini New York Marekani amewapongeza wahusika wote walioshiriki kufanikisha hayo yanayoendelea kutokea. Umoja wa Mataifa pia umeongeza uingizaji misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza na misaada mingine imetumwa eneo la kaskazini mwa Gaza ambalo kwa wiki kadhaa wananchi waliokosa misaada kutokana na mapigano makali yaliyoendelea katika eneo hilo.Hata hivyo Katibu Mkuu Guterres amesema misaada hiyo haitoshi kukidhi mahitaji ya wananchi milioni 1.7 wenye uhitaji na kusema mahitaji ya kibinadamu kila uchao yanazidi kuongezeka.Ametaka mazungumzo yaliyokuwa chachu ya makubaliano hayo lazima yaendelee, na kufikia usitishaji kamili wa mapigano kwa sababu za kibinadamu, kwa manufaa ya watu wa Gaza, Israel na eneo zima.Katibu Mkuu kwa mara nyingine ametoa wito kwa mateka waliosalia kuachiwa mara moja bila masharti yoyote.Amehitimisha taarifa yake kwa kuyahimiza Mataifa yote kutumia ushawishi wao kumaliza mzozo huu mbaya na kuunga mkono hatua zisizoweza kutenguliwa kuelekea mustakabali pekee endelevu wa eneo hilo ambao ni suluhisho la kuwa na serikali mbili, na Israeli na Palestina kuishi bega kwa bega, kwa amani na usalama.Wakati huo huo wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa hii leo wametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka, wa uwazi na huru kuhusu tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, unaotekelezwa nchini Israel na katika eneo linalokaliwa la Palestina kuanzia tarehe 7 Oktoba mwaka huu wa 2023 na baada ya hapo.Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi imesema wataalamu hao wamezitaka pande zote katika mzozo unaoendelea huko Mashariki ya Kati kuwalinda raia na kuzingatia wajibu wao chini ya sheria za kimataifa.
27-11-2023 • 0
Heko waliofanikisha sitisho la mapigano Gaza - Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezipongeza serikali za Qatar, Misri na Marekani pamoja na kutambua jukumu muhimu la kamati ya Kimataifa ya chama cha msalaba mwekudu kwa juhudi zao za kuhakikisha mapigano yanasitishwa kwa muda, mateka na wafungwa wanaachiwa pamoja na kuingiza misaada huko Ukanda wa Gaza. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Flora NduchaMapigano ya wiki saba huko Gaza na Israel yameleta hali mbaya sana ambayo imeshangaza ulimwengu. Lakini kwa muda wa siku nne sasa, Mapigano hayo yamesitishwa, Mateka wa Israel na mataifa mengine ya kigeni wanaoshikiliwa na Hamas tangu tarehe 7 Oktoba wameanza kuachiliwa na wafungwa wa Kipalestina wanafunguliwa kutoka jela za Israel.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia Msemaji wake Stéphane Dujarric hii leo hapa jijini New York Marekani amewapongeza wahusika wote walioshiriki kufanikisha hayo yanayoendelea kutokea. Umoja wa Mataifa pia umeongeza uingizaji misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza na misaada mingine imetumwa eneo la kaskazini mwa Gaza ambalo kwa wiki kadhaa wananchi waliokosa misaada kutokana na mapigano makali yaliyoendelea katika eneo hilo.Hata hivyo Katibu Mkuu Guterres amesema misaada hiyo haitoshi kukidhi mahitaji ya wananchi milioni 1.7 wenye uhitaji na kusema mahitaji ya kibinadamu kila uchao yanazidi kuongezeka.Ametaka mazungumzo yaliyokuwa chachu ya makubaliano hayo lazima yaendelee, na kufikia usitishaji kamili wa mapigano kwa sababu za kibinadamu, kwa manufaa ya watu wa Gaza, Israel na eneo zima.Katibu Mkuu kwa mara nyingine ametoa wito kwa mateka waliosalia kuachiwa mara moja bila masharti yoyote.Amehitimisha taarifa yake kwa kuyahimiza Mataifa yote kutumia ushawishi wao kumaliza mzozo huu mbaya na kuunga mkono hatua zisizoweza kutenguliwa kuelekea mustakabali pekee endelevu wa eneo hilo ambao ni suluhisho la kuwa na serikali mbili, na Israeli na Palestina kuishi bega kwa bega, kwa amani na usalama.Wakati huo huo wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa hii leo wametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka, wa uwazi na huru kuhusu tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, unaotekelezwa nchini Israel na katika eneo linalokaliwa la Palestina kuanzia tarehe 7 Oktoba mwaka huu wa 2023 na baada ya hapo.Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi imesema wataalamu hao wamezitaka pande zote katika mzozo unaoendelea huko Mashariki ya Kati kuwalinda raia na kuzingatia wajibu wao chini ya sheria za kimataifa.
27-11-2023 • 2 minuten, 40 seconden
27 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani Leah Mushi anamulika Gaza, siku ya nne ya sitisho la mapigano; kisha kauli ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kulekea COP28. Makala ni kauli ya muathirika wa mapigano huko Mashariki mwa DRC na mashinani mnufaika wa kilimo endelevu kutoka Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezipongeza serikali za Qatar, Misri na Marekani pamoja na kutambua jukumu muhimu la kamati ya Kimataifa ya chama cha msalaba mwekudu kwa juhudi zao za kuhakikisha mapigano yanasitishwa kwa muda, mateka na wafungwa wanaachiwa pamoja na kuingiza misaada huko Ukanda wa Gaza.Kuelekea mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 huko Dubai, Falme za kiarabu tarehe 30 mwezi huu wa Novemba, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, limesema washiriki wanapaswa waelewe kuwa suala la afya ndilo linapaswa kuchochea majadiliano wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kushamiri duniani kote.Makala: Evarist Mapesa wa Idhaa hii anafuatilia madhila wanayopitia watu 450,000 waliofurushwa makwao katika kipindi cha wiki sita zilizopita huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na vikundi vilivyojiham.Mashinani:Leo nampa fursa Hannah Karanja, mkulima mnufaika wa mpango wa kilimo endelevu kinachohusisha utandazaji wa majani makavu kama njia ya kuepusha matumizi ya mbolea zenye kemikali, mradi unaofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.
27-11-2023 • 0
27 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani Leah Mushi anamulika Gaza, siku ya nne ya sitisho la mapigano; kisha kauli ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kulekea COP28. Makala ni kauli ya muathirika wa mapigano huko Mashariki mwa DRC na mashinani mnufaika wa kilimo endelevu kutoka Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezipongeza serikali za Qatar, Misri na Marekani pamoja na kutambua jukumu muhimu la kamati ya Kimataifa ya chama cha msalaba mwekudu kwa juhudi zao za kuhakikisha mapigano yanasitishwa kwa muda, mateka na wafungwa wanaachiwa pamoja na kuingiza misaada huko Ukanda wa Gaza.Kuelekea mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 huko Dubai, Falme za kiarabu tarehe 30 mwezi huu wa Novemba, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, limesema washiriki wanapaswa waelewe kuwa suala la afya ndilo linapaswa kuchochea majadiliano wakati huu ambapo janga la tabianchi linazidi kushamiri duniani kote.Makala: Evarist Mapesa wa Idhaa hii anafuatilia madhila wanayopitia watu 450,000 waliofurushwa makwao katika kipindi cha wiki sita zilizopita huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kutokana na mapigano kati ya jeshi la serikali na vikundi vilivyojiham.Mashinani:Leo nampa fursa Hannah Karanja, mkulima mnufaika wa mpango wa kilimo endelevu kinachohusisha utandazaji wa majani makavu kama njia ya kuepusha matumizi ya mbolea zenye kemikali, mradi unaofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.
27-11-2023 • 11 minuten, 57 seconden
Mradi wa kupunguza matumizi ya dawa katika ufugaji kuku wa nyama kuanza mwakani – FAO Tanzania
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Tanzania linakusudia kutekeleza mradi wa kuhamasisha wafugaji kupunguza matumizi ya dawa, mathalani za viuavijiumbemaradhi katika ufugaji wa kuku wa nyama nchini humo. John Kabambala wa redio washirika wetu KidsTime FM anatujuza zaidi kupitia makala hii.
24-11-2023 • 0
Mradi wa kupunguza matumizi ya dawa katika ufugaji kuku wa nyama kuanza mwakani – FAO Tanzania
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Tanzania linakusudia kutekeleza mradi wa kuhamasisha wafugaji kupunguza matumizi ya dawa, mathalani za viuavijiumbemaradhi katika ufugaji wa kuku wa nyama nchini humo. John Kabambala wa redio washirika wetu KidsTime FM anatujuza zaidi kupitia makala hii.
24-11-2023 • 4 minuten, 2 seconden
Guterres aonya kwamba kifanyikacho Antarctica sasa hakisalii tena huko kinasambaa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko ziarani katika eneo la ncha ya kusini mwa dunia, Antarctica amesema eneo hilo limekuwa likijulikana kama eneo lenye manufaa makubwa lakini lililosahaulika, lakini sasa limeamshwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Kauli hiyo imekuwa na mashiko kwa miongo kadhaa kwa msingi kwamba eneo la ncha ya kusini mwa dunia liko mbali na wengi, lakini sasa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa katika ziara ya siku tatu kwenye eneo hilo amejionea akiwa ameambatana na Rais Gabriel Boric wa Chile jinsi kile kinachofanyika maelfu ya maili kinaathiri eneo hilo, na halikadhalika kifanyikacho eneo hilo hakisalii tena eneo hilo kama ambavyo awali watu walidhania. Ametembelea kisiwa cha Kopaitic ambacho ni makazi ya ndege wa baharini aina ya Kiwi na kuona ni kwa jinsi gani mabadiliko ya tabianchi yameathiri eneo hilo. Mathalani nishati kisukuku ambayo ni mafuta yatokanayo na upasuaji na uchomaji wa miamba! Katibu Mkuu amesema uchafuzi utokanao na shughuli hiyo husababisha joto kwenye sayari ya dunia, vivyo hivyo Antarctica. Kielelezo ni ongezeko la joto kwenye baharí kusini mwa dunia ambalo limechochea mkondo joto baharini, El Nino unaosababisha mvua, mafuriko na joto kupindukia. Sasa kwa viongozi na washiriki wa mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 huko Dubai mambo matatu yazingatiwe: Mosi, wachukue hatua wahakikishe kiwango cha joto duniani hakizidi nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi; Pili, walinde binadamu dhidi ya zahma ya tabianchi na tatu waondokane na nishati kisukuku. Guterres amesema tusiache matumaini yote ya sayari endelevu yayoyome. Baadaye leo akiwa na Rais Boric watatembelea kituo cha Frei huko huko Antarctica na kesho Jumamosi atatembelea kituo cha wanasayansi cha Profesa Julio Escudero kupata taarifa kutoka kwa wanasayansi. Atarejea New York, Jumapili.
24-11-2023 • 0
Guterres aonya kwamba kifanyikacho Antarctica sasa hakisalii tena huko kinasambaa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko ziarani katika eneo la ncha ya kusini mwa dunia, Antarctica amesema eneo hilo limekuwa likijulikana kama eneo lenye manufaa makubwa lakini lililosahaulika, lakini sasa limeamshwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Kauli hiyo imekuwa na mashiko kwa miongo kadhaa kwa msingi kwamba eneo la ncha ya kusini mwa dunia liko mbali na wengi, lakini sasa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa katika ziara ya siku tatu kwenye eneo hilo amejionea akiwa ameambatana na Rais Gabriel Boric wa Chile jinsi kile kinachofanyika maelfu ya maili kinaathiri eneo hilo, na halikadhalika kifanyikacho eneo hilo hakisalii tena eneo hilo kama ambavyo awali watu walidhania. Ametembelea kisiwa cha Kopaitic ambacho ni makazi ya ndege wa baharini aina ya Kiwi na kuona ni kwa jinsi gani mabadiliko ya tabianchi yameathiri eneo hilo. Mathalani nishati kisukuku ambayo ni mafuta yatokanayo na upasuaji na uchomaji wa miamba! Katibu Mkuu amesema uchafuzi utokanao na shughuli hiyo husababisha joto kwenye sayari ya dunia, vivyo hivyo Antarctica. Kielelezo ni ongezeko la joto kwenye baharí kusini mwa dunia ambalo limechochea mkondo joto baharini, El Nino unaosababisha mvua, mafuriko na joto kupindukia. Sasa kwa viongozi na washiriki wa mkutano wa 28 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 huko Dubai mambo matatu yazingatiwe: Mosi, wachukue hatua wahakikishe kiwango cha joto duniani hakizidi nyuzijoto 1.5 katika kipimo cha Selsiyasi; Pili, walinde binadamu dhidi ya zahma ya tabianchi na tatu waondokane na nishati kisukuku. Guterres amesema tusiache matumaini yote ya sayari endelevu yayoyome. Baadaye leo akiwa na Rais Boric watatembelea kituo cha Frei huko huko Antarctica na kesho Jumamosi atatembelea kituo cha wanasayansi cha Profesa Julio Escudero kupata taarifa kutoka kwa wanasayansi. Atarejea New York, Jumapili.
24-11-2023 • 2 minuten, 2 seconden
24 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia amani na usalama katika ukanda wa Gaza na msaada wa kibinadamu nchini Chad. Makala tunakupeleka nchini Tanzania, na mashinani tunamulika Ibara ya 13 ya Tamko la Haki za Binadamu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko ziarani katika eneo la ncha ya kusini mwa dunia, Antarctica amesema eneo hilo limekuwa likijulikana kama eneo lenye manufaa makubwa lakini lililosahaulika, lakini sasa limeamshwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Chad ni mwenyeji wa wakimbizi zaidi ya milioni ambao sasa umekuwa mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi na unaokuwa kwa kasi barani Afrika kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. Shirika hilo linasema na vita inayoendelea katika nchi jirani ya Sudan imeongeza shinikizo la rasilimali na mahitaji ya kibinadamu kwani maelfu kwa maelfu ya watu zaidi wanavuka mpaka na kusaka usalama Chad.Katika makala John Kabambala wa redio washirika wetu KidsTime FM ya Morogogo Tanzania anatujuza kuhusu Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Tanzania unaokusudia kuhamasisha wafugaji wa kuku kupunguza matumizi ya dawa, mathalani za viuavijiumbemaradhi wakati wa ufugaji wa kuku wa nyama nchini humo.Na mashinani leo katika mfululizo wetu wa uchambuzi wa Ibara za Tamko la Haki za Binadamu kuelekea Siku ya Haki za Binadamu itakayoadhimishwa hapo Desemba 10 leo tunamulika Ibara ya 13. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
24-11-2023 • 0
24 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia amani na usalama katika ukanda wa Gaza na msaada wa kibinadamu nchini Chad. Makala tunakupeleka nchini Tanzania, na mashinani tunamulika Ibara ya 13 ya Tamko la Haki za Binadamu. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye yuko ziarani katika eneo la ncha ya kusini mwa dunia, Antarctica amesema eneo hilo limekuwa likijulikana kama eneo lenye manufaa makubwa lakini lililosahaulika, lakini sasa limeamshwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Chad ni mwenyeji wa wakimbizi zaidi ya milioni ambao sasa umekuwa mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi na unaokuwa kwa kasi barani Afrika kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. Shirika hilo linasema na vita inayoendelea katika nchi jirani ya Sudan imeongeza shinikizo la rasilimali na mahitaji ya kibinadamu kwani maelfu kwa maelfu ya watu zaidi wanavuka mpaka na kusaka usalama Chad.Katika makala John Kabambala wa redio washirika wetu KidsTime FM ya Morogogo Tanzania anatujuza kuhusu Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) Tanzania unaokusudia kuhamasisha wafugaji wa kuku kupunguza matumizi ya dawa, mathalani za viuavijiumbemaradhi wakati wa ufugaji wa kuku wa nyama nchini humo.Na mashinani leo katika mfululizo wetu wa uchambuzi wa Ibara za Tamko la Haki za Binadamu kuelekea Siku ya Haki za Binadamu itakayoadhimishwa hapo Desemba 10 leo tunamulika Ibara ya 13. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
24-11-2023 • 13 minuten
WFP inasema Chad imewakirimu wakimbizi kwa kila kitu lakini sasa imeishiwa inahitaji msaada
Chad ni mwenyeji wa wakimbizi zaidi ya milioni ambao sasa umekuwa mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi na unaokuwa kwa kasi barani Afrika kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. Shirika hilo linasema na vita inayoendelea katika nchi jirani ya Sudan imeongeza shinikizo la rasilimali na mahitaji ya kibinadamu kwani maelfu kwa maelfu ya watu zaidi wanavuka mpaka na kusaka usalama Chad. Katika kituo cha wakimbizi cha Adre mpakani mwa Chad hekaheka ni nyingi kwani wakimbizi wanamiminika kwa idadi kubwa wakiwa na virago vyao wanakimbia vita inayoendelea Sudan, na miongoni mwao ni Roukaya Yacoub mama wa watoto saba aliyelazimika kukusanya kile alichoweza na wanawe na kuchanja mbuga baada ya mumewe kuawa katika shambulio lilitokea Ardamata.Sasa yuko kambini hapa lakini jinamizi la shambulio hilo linaendelea kumuandama,“Walitushambulia kwa siku tatu mfululizo, ilikuwa mbaya sana, walikwenda mlango kwa mlango wakiwakusanya wanaume wakiwatoa nje na kuwaua. Walimwita baba watoto wangu atoke nje na kisha wakampiga risasi na kumuua. Walichukua kila kitu tulichokuwa nacho na sasa nimesalia mkavu sina chochote cha kuwasaidia wanangu. Hatukuwa na chaguo linguine bali kukimbilia Chad.”Kwa mujibu wa WFP ongezeko hili la wakimbizi limezidisha shinikizo la mahitaji ya kibinadamu kama chakula inachokigawa ambacho ndio tegemeo pekee la wakimbizi hawa na sasa hakitoshelezi tena kwani idadi ya watu inaongezeka kila uchao, rasilimali zinakwisha na kuyaacha mashirika ya misaada ya kibinadamu yakihaha na kukosa la kufanya.Changamoto za wakimbizi hawa pia zinajumuisha masuala ya kiafya ikiwemo utapiamlo kwa watoto, majeruhi na magonjwa mengine ambayo baada ya vipimo wanahitaji msaada. Pierre Honnorat ni mkurugenzi wa WFP nchini Chad anasema,“Wachad wamegawana na wakimbizi kila walichokuwa nacho sasa hawana tena cha kugawana. Wao wenyewe wanahitaji msaada, hivyo tunahitaji kuwasaidia wakimbizi wote 600,000 waliokuja, wakimbizi wa Chad wanaorejea lakini pia sasa tunahitaji kuwasaidia Wachad wanaohifadhi wakimbizi ambao nao wanahaha kama walivyo waliowasili toka Sudan.”WFP inasema zaidi ya watu nusu milioni wamevuka mpaka tangu Aprili wakiwemo wakimbizi 45,000 na watu 80,000 raia wa Chad wanaorejea na idadi ya wanaoingia Chad inatarajiwa kufikia watu 600,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu.
24-11-2023 • 0
WFP inasema Chad imewakirimu wakimbizi kwa kila kitu lakini sasa imeishiwa inahitaji msaada
Chad ni mwenyeji wa wakimbizi zaidi ya milioni ambao sasa umekuwa mgogoro mkubwa zaidi wa wakimbizi na unaokuwa kwa kasi barani Afrika kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. Shirika hilo linasema na vita inayoendelea katika nchi jirani ya Sudan imeongeza shinikizo la rasilimali na mahitaji ya kibinadamu kwani maelfu kwa maelfu ya watu zaidi wanavuka mpaka na kusaka usalama Chad. Katika kituo cha wakimbizi cha Adre mpakani mwa Chad hekaheka ni nyingi kwani wakimbizi wanamiminika kwa idadi kubwa wakiwa na virago vyao wanakimbia vita inayoendelea Sudan, na miongoni mwao ni Roukaya Yacoub mama wa watoto saba aliyelazimika kukusanya kile alichoweza na wanawe na kuchanja mbuga baada ya mumewe kuawa katika shambulio lilitokea Ardamata.Sasa yuko kambini hapa lakini jinamizi la shambulio hilo linaendelea kumuandama,“Walitushambulia kwa siku tatu mfululizo, ilikuwa mbaya sana, walikwenda mlango kwa mlango wakiwakusanya wanaume wakiwatoa nje na kuwaua. Walimwita baba watoto wangu atoke nje na kisha wakampiga risasi na kumuua. Walichukua kila kitu tulichokuwa nacho na sasa nimesalia mkavu sina chochote cha kuwasaidia wanangu. Hatukuwa na chaguo linguine bali kukimbilia Chad.”Kwa mujibu wa WFP ongezeko hili la wakimbizi limezidisha shinikizo la mahitaji ya kibinadamu kama chakula inachokigawa ambacho ndio tegemeo pekee la wakimbizi hawa na sasa hakitoshelezi tena kwani idadi ya watu inaongezeka kila uchao, rasilimali zinakwisha na kuyaacha mashirika ya misaada ya kibinadamu yakihaha na kukosa la kufanya.Changamoto za wakimbizi hawa pia zinajumuisha masuala ya kiafya ikiwemo utapiamlo kwa watoto, majeruhi na magonjwa mengine ambayo baada ya vipimo wanahitaji msaada. Pierre Honnorat ni mkurugenzi wa WFP nchini Chad anasema,“Wachad wamegawana na wakimbizi kila walichokuwa nacho sasa hawana tena cha kugawana. Wao wenyewe wanahitaji msaada, hivyo tunahitaji kuwasaidia wakimbizi wote 600,000 waliokuja, wakimbizi wa Chad wanaorejea lakini pia sasa tunahitaji kuwasaidia Wachad wanaohifadhi wakimbizi ambao nao wanahaha kama walivyo waliowasili toka Sudan.”WFP inasema zaidi ya watu nusu milioni wamevuka mpaka tangu Aprili wakiwemo wakimbizi 45,000 na watu 80,000 raia wa Chad wanaorejea na idadi ya wanaoingia Chad inatarajiwa kufikia watu 600,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu.
24-11-2023 • 3 minuten, 4 seconden
Waepushe watoto wachanga na bidhaa za viwandani – WHO/UNICEF
Kwa mujibu wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Ulimwenguni (WHO) na la Kuhudumia Watoto (UNICEF), tabia za ulishaji wa vyakula visivyo salama kiafya kwa watoto wadogo na wachanga lazima ziepukwe kwasababu zinachangia kuongezeka uzito usio salama kiafya, na vyakula hivyo vinaweza kuchukua nafasi ya vyakula vyenye virutubishi muhimu kwa watoto. Matumizi ya vyakula na vinywaji vitamu kwa watoto wachanga na watoto wadogo huongeza uwezekano wa kuharibika kwa meno na tatizo la kiribatumbo kwa watoto. Kiujumla matumizi ya vyakula visivyo salama kiafya inamaanisha vyakula vyenye sukari nyingi, chumvi na mafuta yasiyo salama kiafya. Edisoni Tumaini Anatory wa redio washirika wetu Karagwe FM ya wilayani Karagwe, mkoani Kagera Magharibi mwa Tanzania ametuandalia makala hii akiangazia mamlaka za afya kwa umma katika hiyo zinavyotoa wito kuhamasisha wananchi kuchukua hatua za kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususani kwa watoto wadogo.
22-11-2023 • 0
Waepushe watoto wachanga na bidhaa za viwandani – WHO/UNICEF
Kwa mujibu wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Ulimwenguni (WHO) na la Kuhudumia Watoto (UNICEF), tabia za ulishaji wa vyakula visivyo salama kiafya kwa watoto wadogo na wachanga lazima ziepukwe kwasababu zinachangia kuongezeka uzito usio salama kiafya, na vyakula hivyo vinaweza kuchukua nafasi ya vyakula vyenye virutubishi muhimu kwa watoto. Matumizi ya vyakula na vinywaji vitamu kwa watoto wachanga na watoto wadogo huongeza uwezekano wa kuharibika kwa meno na tatizo la kiribatumbo kwa watoto. Kiujumla matumizi ya vyakula visivyo salama kiafya inamaanisha vyakula vyenye sukari nyingi, chumvi na mafuta yasiyo salama kiafya. Edisoni Tumaini Anatory wa redio washirika wetu Karagwe FM ya wilayani Karagwe, mkoani Kagera Magharibi mwa Tanzania ametuandalia makala hii akiangazia mamlaka za afya kwa umma katika hiyo zinavyotoa wito kuhamasisha wananchi kuchukua hatua za kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususani kwa watoto wadogo.
22-11-2023 • 3 minuten, 37 seconden
Ngoma za kitamaduni kuleta jamii pamoja Sudan Kusini - UNMISS
Katika kukuza utangamano ndani ya jamii yenye makabila tofauti ambayo hapo awali yalikuwa na misuguano Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wizara ya Utamaduni ya Sudan Kusini imefanya huko katika jimbo la Equatoria Magharibi. Ni sauti za ngoma, marimba, filimbi , vuvuzela na mirindimo mbalimbali ikisikika katika mji wa Yambio ulioko jimboni Equatoria Magharibi hapa Sudan Kusini, mamia ya wananchi wengine wakiwa wamevalia vibwebwe viunoni na mavazi ya asili wakicheza kwa pamoja kufurahia utajiri wao wa utafauti wa makabila. Afisa wa masuala ya kiraia wa UNMISS Emmanuel Dukundane anasema makabila tisa yamekutanishwa hapa, “Shughuli hii ni kwa ajili ya kuonesha tofauti zetu, utofauti wetu kwenye masuala ya utamaduni na lengo ni sote tuwe na furaha. Na kupitia furaha hiyo tunaweza kukuza mshikamano wa kijamii, tunaweza kufahamiana zaidi, kuthaminiana zaidi, na kusahau changamoto zetu za zamani.” Na ama hakika wananchi hapa wamefurahi na hawataki kabisa kukumbuka ya kale kwani yanaumiza kama anavyoeleza Mama Hellen Mading mkazi wa Yambio, "Wakati tunapokuwa na migogoro sisi wanawawake na watoto ndio tunateseka. kwakweli tunahitaji amani, acha tuishi kwa amani kila siku. Tunataka watoto wetu wakue katika mazingira mazuri ili wapate elimu na waje kuwa viongozi wetu wa baadae.” Tamasha hili limeandaliwa na UNMISS wakishirikiana na wizara ya utamaduni, vijana na michezo na kijana James Amabele anasema walikuwa wakisubiri tukio hili kwa hamu, “Matukio kama haya ndio yataleta amani miongoni mwa wanajamii na Sudan Kusini kwa ujumla. Hili ndilo tulikuwa tukilitamani litokee, lazima tuwe na umoja, na ikiwa kila kitu kitaenda vizuri, basi amani itatawala. Hii ndio amani yenyewe. Tulikuwa tukililia amani na hapa tupo katika umoja na amani; makabila yote yameungana.”Kwa UNMISS, hii ni hatua moja kuelekea kujenga amani ya kudumu na endelevu miongoni mwa jamii ambazo zimekumbwa na mgogoro, mmoja baada ya mwingine katika taifa lote la Sudan Kusini.
22-11-2023 • 0
Ngoma za kitamaduni kuleta jamii pamoja Sudan Kusini - UNMISS
Katika kukuza utangamano ndani ya jamii yenye makabila tofauti ambayo hapo awali yalikuwa na misuguano Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wizara ya Utamaduni ya Sudan Kusini imefanya huko katika jimbo la Equatoria Magharibi. Ni sauti za ngoma, marimba, filimbi , vuvuzela na mirindimo mbalimbali ikisikika katika mji wa Yambio ulioko jimboni Equatoria Magharibi hapa Sudan Kusini, mamia ya wananchi wengine wakiwa wamevalia vibwebwe viunoni na mavazi ya asili wakicheza kwa pamoja kufurahia utajiri wao wa utafauti wa makabila. Afisa wa masuala ya kiraia wa UNMISS Emmanuel Dukundane anasema makabila tisa yamekutanishwa hapa, “Shughuli hii ni kwa ajili ya kuonesha tofauti zetu, utofauti wetu kwenye masuala ya utamaduni na lengo ni sote tuwe na furaha. Na kupitia furaha hiyo tunaweza kukuza mshikamano wa kijamii, tunaweza kufahamiana zaidi, kuthaminiana zaidi, na kusahau changamoto zetu za zamani.” Na ama hakika wananchi hapa wamefurahi na hawataki kabisa kukumbuka ya kale kwani yanaumiza kama anavyoeleza Mama Hellen Mading mkazi wa Yambio, "Wakati tunapokuwa na migogoro sisi wanawawake na watoto ndio tunateseka. kwakweli tunahitaji amani, acha tuishi kwa amani kila siku. Tunataka watoto wetu wakue katika mazingira mazuri ili wapate elimu na waje kuwa viongozi wetu wa baadae.” Tamasha hili limeandaliwa na UNMISS wakishirikiana na wizara ya utamaduni, vijana na michezo na kijana James Amabele anasema walikuwa wakisubiri tukio hili kwa hamu, “Matukio kama haya ndio yataleta amani miongoni mwa wanajamii na Sudan Kusini kwa ujumla. Hili ndilo tulikuwa tukilitamani litokee, lazima tuwe na umoja, na ikiwa kila kitu kitaenda vizuri, basi amani itatawala. Hii ndio amani yenyewe. Tulikuwa tukililia amani na hapa tupo katika umoja na amani; makabila yote yameungana.”Kwa UNMISS, hii ni hatua moja kuelekea kujenga amani ya kudumu na endelevu miongoni mwa jamii ambazo zimekumbwa na mgogoro, mmoja baada ya mwingine katika taifa lote la Sudan Kusini.
22-11-2023 • 2 minuten, 26 seconden
22 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia tunaangazia mizozo katika ukanda wa Gaza na hali ya mateka waliochukuliwa wakati wa shambulizi la Hamas huko Israel Kusini Oktoba 7. Pia tunamulika amani nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani Ufalme wa Tonga katika bahari ya Pasifiki, kulikoni? Muafaka uliofikiwa jana jioni wa kuwaachilia mateka waliochukuliwa wakati wa shambulizi la Hamas huko Israel Kusini Oktoba 7 umekaribishwa na Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye amesema Umoja huo uko tayari kutumia hatua hiyo njema kwa ajili ya masuala ya kibinadamu. Katika kukuza utangamano ndani ya jamii yenye makabila tofauti ambayo hapo awali yalikuwa na misuguano Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wizara ya Utamaduni ya Sudan Kusini imefanya huko katika jimbo la Equatoria Magharibi.Katika makala Edisoni Tumaini Anatory wa redio washirika wetu Karagwe FM ya wilayani Karagwe, mkoani Kagera Magharibi mwa Tanzania ameangazia elimu ya lishe kwa watoto dhidi ya bidhaa zenye sukari akizingatia wito wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Ulimwenguni (WHO) na la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwamba tabia za ulishaji wa vyakula visivyo salama kiafya kwa watoto wadogo na wachanga lazima ziepukwe katika kuhamasisha wananchi kuchukua hatua za kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza.Na mashinani tutaelekea katika Ufalme wa Tonga, katika bahari ya Pasifiki kusikia ni kwa jinsi gani wavuvi wameweza kuhimili majanga ya mabadiliko ya tabianchi. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
22-11-2023 • 0
22 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia tunaangazia mizozo katika ukanda wa Gaza na hali ya mateka waliochukuliwa wakati wa shambulizi la Hamas huko Israel Kusini Oktoba 7. Pia tunamulika amani nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani Ufalme wa Tonga katika bahari ya Pasifiki, kulikoni? Muafaka uliofikiwa jana jioni wa kuwaachilia mateka waliochukuliwa wakati wa shambulizi la Hamas huko Israel Kusini Oktoba 7 umekaribishwa na Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye amesema Umoja huo uko tayari kutumia hatua hiyo njema kwa ajili ya masuala ya kibinadamu. Katika kukuza utangamano ndani ya jamii yenye makabila tofauti ambayo hapo awali yalikuwa na misuguano Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwakushirikiana na wizara ya Utamaduni ya Sudan Kusini imefanya huko katika jimbo la Equatoria Magharibi.Katika makala Edisoni Tumaini Anatory wa redio washirika wetu Karagwe FM ya wilayani Karagwe, mkoani Kagera Magharibi mwa Tanzania ameangazia elimu ya lishe kwa watoto dhidi ya bidhaa zenye sukari akizingatia wito wa mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la Afya Ulimwenguni (WHO) na la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwamba tabia za ulishaji wa vyakula visivyo salama kiafya kwa watoto wadogo na wachanga lazima ziepukwe katika kuhamasisha wananchi kuchukua hatua za kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza.Na mashinani tutaelekea katika Ufalme wa Tonga, katika bahari ya Pasifiki kusikia ni kwa jinsi gani wavuvi wameweza kuhimili majanga ya mabadiliko ya tabianchi. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
22-11-2023 • 11 minuten, 24 seconden
Muafaka wa usitishaji mapigano na kuachilia mateka Gaza umefikiwa, UN yakaribisha
Muafaka uliofikiwa jana jioni wa kuwaachilia mateka waliochukuliwa wakati wa shambulizi la Hamas huko Israel Kusini Oktoba 7 umekaribishwa na Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye amesema Umoja huo uko tayari kutumia hatua hiyo njema kwa ajili ya masuala ya kibinadamu. Kwa hakika Assumpta muafaka huo ni habari njema ambayo imepokelewa kwa mikoni miwili na mashirika karibu yote ya Umoja wa Mataifa na wahudumu wa kibinadamu huku Katibu Mkuu Guterres kupitia taarifa yake iliyotolewa leo akisema“Ni hatua muhimu kuelekea kunakostahili na Umoja wa Mataifa utasaidia kwa kila hali kufanikisha hilo lakini mengi zaidi yanahitajika kufanywa.”Tor Wennesland ambaye ni mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati ameunga mkono kauli hiyo ya Guterres akikaribisha usitishaji huo wa mapigano Gaza wa saa 96 au siku nne.Amesisitiza kwamba“Usitishaji maiugano huo lazima utumiwe kikamilifu kuwezesha kuachiliwa kwa mateka na kushughulikia mahitaji makubwa ya Wapalestina Gaza”Na wadau wote wa misaada ya kibinadamu wamesema wako tayari kufanya kila wawezalo kutumia fursa hiyo kusaidia.Baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yametumia fursa hiyo kurejea wito wao mfano lile la afya duniani WHO limetaka fursa ya ukufikia wenye uhitaji lazima ihakikishwe bila vikwazo Ukanda wa Gaza ili kuongeza msaada wa kibinadamu likisisitiza kuwa “Hatuwezi kuendelea kutoa matone tu ya msaada wakati mahitaji yaliyopo ni bahari.”La kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA limesema muafaka huu umeleta matumaini kwa raia wa Gaza likiamini sasa idadi ya malori ya msaada wa mahitaji muhimu ikiwemo mafuta itaongezeka.Habari hii jjema hata hivyo imekuja kukiwa na hofu kubwa ya njaa hasa Kaskazini mwa Gaza kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO, lakini pia mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao kama hospitali yakiendelea kusababisha vifo na uharibifu.Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema tangu kuanza kwa machafuko ya sasa watu 191 wanaopata hifadhi katika vituo vyake wameuawa na wengine 798 kujeruhiwa huku shule mbili za UNRWA zikisambaratishwa kabisa na milipuko. Na jana tu limesema shambulio kwenye hospitali ya Al-Awda Kaskazini mwa Gaza limekatili maisha ya watu 4 wakiwemo madaktari 3 na kumjeruhi muuguzi.
22-11-2023 • 0
Muafaka wa usitishaji mapigano na kuachilia mateka Gaza umefikiwa, UN yakaribisha
Muafaka uliofikiwa jana jioni wa kuwaachilia mateka waliochukuliwa wakati wa shambulizi la Hamas huko Israel Kusini Oktoba 7 umekaribishwa na Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye amesema Umoja huo uko tayari kutumia hatua hiyo njema kwa ajili ya masuala ya kibinadamu. Kwa hakika Assumpta muafaka huo ni habari njema ambayo imepokelewa kwa mikoni miwili na mashirika karibu yote ya Umoja wa Mataifa na wahudumu wa kibinadamu huku Katibu Mkuu Guterres kupitia taarifa yake iliyotolewa leo akisema“Ni hatua muhimu kuelekea kunakostahili na Umoja wa Mataifa utasaidia kwa kila hali kufanikisha hilo lakini mengi zaidi yanahitajika kufanywa.”Tor Wennesland ambaye ni mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati ameunga mkono kauli hiyo ya Guterres akikaribisha usitishaji huo wa mapigano Gaza wa saa 96 au siku nne.Amesisitiza kwamba“Usitishaji maiugano huo lazima utumiwe kikamilifu kuwezesha kuachiliwa kwa mateka na kushughulikia mahitaji makubwa ya Wapalestina Gaza”Na wadau wote wa misaada ya kibinadamu wamesema wako tayari kufanya kila wawezalo kutumia fursa hiyo kusaidia.Baadhi ya mashirika ya Umoja wa Mataifa yametumia fursa hiyo kurejea wito wao mfano lile la afya duniani WHO limetaka fursa ya ukufikia wenye uhitaji lazima ihakikishwe bila vikwazo Ukanda wa Gaza ili kuongeza msaada wa kibinadamu likisisitiza kuwa “Hatuwezi kuendelea kutoa matone tu ya msaada wakati mahitaji yaliyopo ni bahari.”La kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA limesema muafaka huu umeleta matumaini kwa raia wa Gaza likiamini sasa idadi ya malori ya msaada wa mahitaji muhimu ikiwemo mafuta itaongezeka.Habari hii jjema hata hivyo imekuja kukiwa na hofu kubwa ya njaa hasa Kaskazini mwa Gaza kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO, lakini pia mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao kama hospitali yakiendelea kusababisha vifo na uharibifu.Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema tangu kuanza kwa machafuko ya sasa watu 191 wanaopata hifadhi katika vituo vyake wameuawa na wengine 798 kujeruhiwa huku shule mbili za UNRWA zikisambaratishwa kabisa na milipuko. Na jana tu limesema shambulio kwenye hospitali ya Al-Awda Kaskazini mwa Gaza limekatili maisha ya watu 4 wakiwemo madaktari 3 na kumjeruhi muuguzi.
22-11-2023 • 2 minuten, 25 seconden
21 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mada kwa kina ambapo mkutano wa tatu kati ya mitano wa kamati ya kimataifa ya majadiliano baina ya nchi kuhusu uchafuzi wa taka za plastiki INC-3 umekunja jamvi mwishoni mwa wiki jijini Nairobi Kenya, hii ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuanza kwa mkutano wa COP28 utakaofanyika huko Dubai katika Falme za nchi za Kiarabu. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.Tunaanzia Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati ambako mapigano yakiendelea hii leo ikiwa ni siku ya 45 tangu kuanza kwa mzozo eneo hilo kati ya Israeli na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema kila siku watoto takribani 160 wanauawa, ikimaanisha mtoto mmoja kila baada ya dakika 10. WHO inasema wakati huo huo watoto 180 wanazaliwa kila siku eneo hilo na zaidi ya 20 wanahitaji huduma mahsusi ambazo kwa sasa ni changamoto kubwa. Tukisalia Gaza, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF James Elder akizungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi hii leo amesema ukosefu wa maji kwenye eneo hilo unatishia usalama wa watoto. Amegusia pia mateka watoto wanaoshikiliwa na Hamas akisema, “lazima waachiliwe huru. Inachukiza kufikiria kuhusu hofu yao; machungu ya familia zao. Hii lazima ikome.”Na kuelekea mkutano wa mabadiliko ya tabianchi huko Falme za kiarabu mwishoni mwa mwezi huu, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema wanawake wajawazito, watoto wachanga na watoto wanakabiliwa na hatari kubwa za kiafya kutokana na majanga ya mabadiliko tabianchi hivyo hatua za kukabili tabianchi zisiwaengue.Leo ni siku ya uvuvi duniani na hivyo katika mashinani tutamsikia mchakato wa mazao ya uvuvi kutoka Ziwa Tanganyika nchini Tanzania. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
21-11-2023 • 0
21 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mada kwa kina ambapo mkutano wa tatu kati ya mitano wa kamati ya kimataifa ya majadiliano baina ya nchi kuhusu uchafuzi wa taka za plastiki INC-3 umekunja jamvi mwishoni mwa wiki jijini Nairobi Kenya, hii ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuanza kwa mkutano wa COP28 utakaofanyika huko Dubai katika Falme za nchi za Kiarabu. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.Tunaanzia Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati ambako mapigano yakiendelea hii leo ikiwa ni siku ya 45 tangu kuanza kwa mzozo eneo hilo kati ya Israeli na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO linasema kila siku watoto takribani 160 wanauawa, ikimaanisha mtoto mmoja kila baada ya dakika 10. WHO inasema wakati huo huo watoto 180 wanazaliwa kila siku eneo hilo na zaidi ya 20 wanahitaji huduma mahsusi ambazo kwa sasa ni changamoto kubwa. Tukisalia Gaza, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF James Elder akizungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi hii leo amesema ukosefu wa maji kwenye eneo hilo unatishia usalama wa watoto. Amegusia pia mateka watoto wanaoshikiliwa na Hamas akisema, “lazima waachiliwe huru. Inachukiza kufikiria kuhusu hofu yao; machungu ya familia zao. Hii lazima ikome.”Na kuelekea mkutano wa mabadiliko ya tabianchi huko Falme za kiarabu mwishoni mwa mwezi huu, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanasema wanawake wajawazito, watoto wachanga na watoto wanakabiliwa na hatari kubwa za kiafya kutokana na majanga ya mabadiliko tabianchi hivyo hatua za kukabili tabianchi zisiwaengue.Leo ni siku ya uvuvi duniani na hivyo katika mashinani tutamsikia mchakato wa mazao ya uvuvi kutoka Ziwa Tanganyika nchini Tanzania. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
21-11-2023 • 11 minuten, 4 seconden
Mataifa yaongeze kasi ya mabadiliko katika kuhakikisha upatikanaji wa choo safi na salama
Wakati hapo jana Novemba 19 dunia imeadhimisha Siku ya choo Duniani. maudhui yaliyobeba siku hiyo ni ‘Kuongeza kasi ya mabadiliko’. Kampeni hii inazingatia athari za janga la usafi wa mazingira ambalo huwa chanzo cha magonjwa mengi hasa ya kuambukiza. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO watu bilioni 3.6 karibu nusu ya watu wote duniani hawana huduma za msingi za usafi na milioni 494 miongoni mwao wanajisaidia haja kubwa katika maeneo ya wazi kwa kukosa huduma ya choo wengi wakiwa ni kutoka katika nchi masikini. Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Ngong, Kaunti ya Kajiado, nchini Kenya kuhusu changamoto za choo katika eneo hilo unangana naye..
20-11-2023 • 0
Mataifa yaongeze kasi ya mabadiliko katika kuhakikisha upatikanaji wa choo safi na salama
Wakati hapo jana Novemba 19 dunia imeadhimisha Siku ya choo Duniani. maudhui yaliyobeba siku hiyo ni ‘Kuongeza kasi ya mabadiliko’. Kampeni hii inazingatia athari za janga la usafi wa mazingira ambalo huwa chanzo cha magonjwa mengi hasa ya kuambukiza. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO watu bilioni 3.6 karibu nusu ya watu wote duniani hawana huduma za msingi za usafi na milioni 494 miongoni mwao wanajisaidia haja kubwa katika maeneo ya wazi kwa kukosa huduma ya choo wengi wakiwa ni kutoka katika nchi masikini. Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Ngong, Kaunti ya Kajiado, nchini Kenya kuhusu changamoto za choo katika eneo hilo unangana naye..
20-11-2023 • 4 minuten, 33 seconden
Mataifa lazima yaende mbali zaidi kuliko ahadi za sasa kutokomeza uzalishaji wa Hewa Chafuzi - UNEP
Wakati joto la ulimwengu na uzalishaji wa hewa chafuzi vikivunja rekodi katika mwaka huu wa 2023, Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) ya Pengo la Uzalishaji hewa chafuzi iliyotolewa leo Novemba 20 mjini Nairobi Kenya imeeleza kwamba imegundua kuwa ahadi za sasa chini ya Mkataba wa Paris zinaweka ulimwengu kwenye mstari wa ongezeko la joto la nyuzi joto 2.5 hadi 2.9 za Selsiasi zaidi ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda katika karne hii. Ripoti hii iliyotolewa kuelekea mkutano wa tabianchi wa mwaka 2023 unaotarajiwa kufanyika huko Dubai, Falme za Kiarabu mwishoni mwa mwezi huu, inaashiria hitaji la dharura la kuongezeka kwa hatua za kukabiliana na tabianchi kwani rekodi ya viwango vya juu vya joto ilivunjwa na kufikia kiwango kipya mwaka huu lakini wakati huo huo kwa mara nyingine tena ulimwengu umeshindwa kupunguza uzalishaji wa chafuzi. Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP Inger Anderson akisisitiza kuchukua hatua mpya za kudhibiti mwenendo mbaya wa ulimwengu anasema, "Hakuna mtu au uchumi uliosalia kwenye sayari bila kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi, hivyo tunahitaji kuacha kuweka rekodi zisizohitajika kuhusu uzalishaji wa hewa chafuzi, joto la juu duniani na hali mbaya ya hewa.” Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake alioutoa akiwa New York, Marekani amesema yote haya ni kushindwa kwa uongozi duniani, usaliti kwa wanyonge, na fursa kubwa iliyopotea. Guterres anasisitiza uelekeo wa nishati ya jadidifu akisema, “Tunajua bado inawezekana kufanya kikomo cha nyuzi joto 1.5 za Selsiasi kuwa ukweli. Na tunajua jinsi ya kufika huko - tuna ramani kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati na Jopo la serikali (duniani) kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC. Inahitajika kung'oa mzizi wenye sumu wa janga la tabianchi: nishati ya mafuta ya kisukuku.” Kiongozi huyu wa Umoja wa Mataifa anawataka viongozi kuimarisha juhudi zao kwa kiasi kikubwa sasa, wakiwa na matamanio ya juu, hatua za juu na kuweka rekodi za juu za upunguzaji wa hewa ukaa. “Awamu inayofuata ya mipango ya kitaifa ya tabianchi itakuwa muhimu.” Anasema Guterres na kuongeza kuwa, “Mipango hii lazima iungwe mkono na fedha, teknolojia, usaidizi na ushirikiano ili kuifanya iwezekane. Kazi ya viongozi katika COP28 ni kuhakikisha hilo linafanyika.” Hadi mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu, siku 86 zilirekodiwa kuwa na joto ya zaidi ya nyuzi joto 1.5 za Selsiasi juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda. Septemba ulikuwa mwezi wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa, ukiwa na wastani wa halijoto duniani nyuzi 1.8 za selsiasi juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda. Ripoti hiyo imegundua kuwa uzalishaji wa hewa chafuzi duniani (GHG) umeongezeka kwa asilimia 1.2 kutoka 2021 hadi 2022 hadi kufikia rekodi mpya ya Gigatonnes 57.4 ya ‘Carbon Dioxide Equivalent’ (GtCO2e). Uzalishaji wa GHG kote katika nchi za G20 uliongezeka kwa asilimia 1.2 mwaka wa 2022. Mitindo ya utoaji wa hewa chafuzi inaonesha mifumo ya kimataifa ya ukosefu wa usawa. Kwa sababu ya mienendo hii inayotia wasiwasi na juhudi zisizotosheleza za kupunguza hali hiyo, dunia iko kwenye mwelekeo wa kupanda kwa joto zaidi ya malengo ya tabianchi yaliyokubaliwa katika karne hii. Ripoti hii inatoa wito kwa mataifa yote kuwasilisha mabadiliko ya maendeleo ya viwango vya chini vya hewa ukaa kwa kuzingatia mabadiliko ya nishati. Makaa ya mawe, mafuta na gesi inayochimbwa katika kipindi chote cha uzalishaji kwenye migodi vinaweza kuzalisha zaidi ya mara 3.5 ya bajeti ya hewa ukaa inayopatikana ili kupunguza ongezeko la joto hadi nyuzi joto 1.5 za Selsiasi, na karibu bajeti yote iliyopo kwa nyzi joto 2 za Selsiasi. Nchi zilizo na uwezo na wajibu mkubwa wa uzalishaji wa hewa chafuzi - hasa nchi zenye mapato ya juu na zinazotoa hewa chafuzi nyingi miongoni mwa G20 - zitahitajika kuchukua hatua kabambe zaidi na za haraka na kutoa usaidizi wa kifedha na kiufundi kwa mataifa yanayoendelea. Kwa vile nchi…
20-11-2023 • 0
Mataifa lazima yaende mbali zaidi kuliko ahadi za sasa kutokomeza uzalishaji wa Hewa Chafuzi - UNEP
Wakati joto la ulimwengu na uzalishaji wa hewa chafuzi vikivunja rekodi katika mwaka huu wa 2023, Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) ya Pengo la Uzalishaji hewa chafuzi iliyotolewa leo Novemba 20 mjini Nairobi Kenya imeeleza kwamba imegundua kuwa ahadi za sasa chini ya Mkataba wa Paris zinaweka ulimwengu kwenye mstari wa ongezeko la joto la nyuzi joto 2.5 hadi 2.9 za Selsiasi zaidi ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda katika karne hii. Ripoti hii iliyotolewa kuelekea mkutano wa tabianchi wa mwaka 2023 unaotarajiwa kufanyika huko Dubai, Falme za Kiarabu mwishoni mwa mwezi huu, inaashiria hitaji la dharura la kuongezeka kwa hatua za kukabiliana na tabianchi kwani rekodi ya viwango vya juu vya joto ilivunjwa na kufikia kiwango kipya mwaka huu lakini wakati huo huo kwa mara nyingine tena ulimwengu umeshindwa kupunguza uzalishaji wa chafuzi. Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP Inger Anderson akisisitiza kuchukua hatua mpya za kudhibiti mwenendo mbaya wa ulimwengu anasema, "Hakuna mtu au uchumi uliosalia kwenye sayari bila kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi, hivyo tunahitaji kuacha kuweka rekodi zisizohitajika kuhusu uzalishaji wa hewa chafuzi, joto la juu duniani na hali mbaya ya hewa.” Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake alioutoa akiwa New York, Marekani amesema yote haya ni kushindwa kwa uongozi duniani, usaliti kwa wanyonge, na fursa kubwa iliyopotea. Guterres anasisitiza uelekeo wa nishati ya jadidifu akisema, “Tunajua bado inawezekana kufanya kikomo cha nyuzi joto 1.5 za Selsiasi kuwa ukweli. Na tunajua jinsi ya kufika huko - tuna ramani kutoka Shirika la Kimataifa la Nishati na Jopo la serikali (duniani) kuhusu mabadiliko ya tabianchi IPCC. Inahitajika kung'oa mzizi wenye sumu wa janga la tabianchi: nishati ya mafuta ya kisukuku.” Kiongozi huyu wa Umoja wa Mataifa anawataka viongozi kuimarisha juhudi zao kwa kiasi kikubwa sasa, wakiwa na matamanio ya juu, hatua za juu na kuweka rekodi za juu za upunguzaji wa hewa ukaa. “Awamu inayofuata ya mipango ya kitaifa ya tabianchi itakuwa muhimu.” Anasema Guterres na kuongeza kuwa, “Mipango hii lazima iungwe mkono na fedha, teknolojia, usaidizi na ushirikiano ili kuifanya iwezekane. Kazi ya viongozi katika COP28 ni kuhakikisha hilo linafanyika.” Hadi mwanzoni mwa Oktoba mwaka huu, siku 86 zilirekodiwa kuwa na joto ya zaidi ya nyuzi joto 1.5 za Selsiasi juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda. Septemba ulikuwa mwezi wa joto zaidi kuwahi kurekodiwa, ukiwa na wastani wa halijoto duniani nyuzi 1.8 za selsiasi juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda. Ripoti hiyo imegundua kuwa uzalishaji wa hewa chafuzi duniani (GHG) umeongezeka kwa asilimia 1.2 kutoka 2021 hadi 2022 hadi kufikia rekodi mpya ya Gigatonnes 57.4 ya ‘Carbon Dioxide Equivalent’ (GtCO2e). Uzalishaji wa GHG kote katika nchi za G20 uliongezeka kwa asilimia 1.2 mwaka wa 2022. Mitindo ya utoaji wa hewa chafuzi inaonesha mifumo ya kimataifa ya ukosefu wa usawa. Kwa sababu ya mienendo hii inayotia wasiwasi na juhudi zisizotosheleza za kupunguza hali hiyo, dunia iko kwenye mwelekeo wa kupanda kwa joto zaidi ya malengo ya tabianchi yaliyokubaliwa katika karne hii. Ripoti hii inatoa wito kwa mataifa yote kuwasilisha mabadiliko ya maendeleo ya viwango vya chini vya hewa ukaa kwa kuzingatia mabadiliko ya nishati. Makaa ya mawe, mafuta na gesi inayochimbwa katika kipindi chote cha uzalishaji kwenye migodi vinaweza kuzalisha zaidi ya mara 3.5 ya bajeti ya hewa ukaa inayopatikana ili kupunguza ongezeko la joto hadi nyuzi joto 1.5 za Selsiasi, na karibu bajeti yote iliyopo kwa nyzi joto 2 za Selsiasi. Nchi zilizo na uwezo na wajibu mkubwa wa uzalishaji wa hewa chafuzi - hasa nchi zenye mapato ya juu na zinazotoa hewa chafuzi nyingi miongoni mwa G20 - zitahitajika kuchukua hatua kabambe zaidi na za haraka na kutoa usaidizi wa kifedha na kiufundi kwa mataifa yanayoendelea. Kwa vile nchi…
20-11-2023 • 2 minuten, 12 seconden
20 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mazingira na hali ya joto, na pia mzozo katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia hapa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kulikoni?. Wakati joto la ulimwengu na uzalishaji wa hewa chafuzi vikivunja rekodi katika mwaka huu wa 2023, Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) ya Pengo la Uzalishaji hewa chafuzi iliyotolewa leo Novemba 20 mjini Nairobi Kenya imeeleza kwamba imegundua kuwa ahadi za sasa chini ya Mkataba wa Paris zinaweka ulimwengu kwenye mstari wa ongezeko la joto la nyuzi joto 2.5 hadi 2.9 za Selsiasi zaidi ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda katika karne hii. Mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati umesambaratisha kabisa mfumo wa chakula Gaza limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, likisisitiza wakati huu ambapo ni asilimia 10 tu ya bidhaa muhimu za chakula ndizo zinazoingia Gaza tangu kuanza kwa mzozo huo Oktoba 7. Hali ni mbaya na imesababisha njaa kwa karibu wate wote wa eneo hilo na tegemeo lao pekee lililobaki ni msaada wa chakula kutoka WFP.Makala leo tunaangazia umuhimu wa choo wakati hapo jana Novemba 19 dunia imeadhimisha Siku ya choo Duniani. Maudhui yaliyobeba siku hiyo ni ‘Kuongeza kasi ya mabadiliko’. Kampeni hii inazingatia athari za janga la usafi wa mazingira ambalo huwa chanzo cha magonjwa mengi hasa ya kuambukiza. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO watu bilioni 3.6 karibu nusu ya watu wote duniani hawana huduma za msingi za usafi na milioni 494 miongoni mwao wanajisaidia haja kubwa katika maeneo ya wazi kwa kukosa huduma ya choo wengi wakiwa ni kutoka katika nchi masikini. Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Ngong, Kaunti ya Kajiado, nchini Kenya.Katika mashinani tutasikia ujumbe uliotolewa na mshindi wa tuzo ya polisi mwanamke wa mwaka wa Umoja wa Mataifa. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
20-11-2023 • 0
20 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mazingira na hali ya joto, na pia mzozo katika ukanda wa Gaza. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia hapa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kulikoni?. Wakati joto la ulimwengu na uzalishaji wa hewa chafuzi vikivunja rekodi katika mwaka huu wa 2023, Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) ya Pengo la Uzalishaji hewa chafuzi iliyotolewa leo Novemba 20 mjini Nairobi Kenya imeeleza kwamba imegundua kuwa ahadi za sasa chini ya Mkataba wa Paris zinaweka ulimwengu kwenye mstari wa ongezeko la joto la nyuzi joto 2.5 hadi 2.9 za Selsiasi zaidi ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda katika karne hii. Mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati umesambaratisha kabisa mfumo wa chakula Gaza limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, likisisitiza wakati huu ambapo ni asilimia 10 tu ya bidhaa muhimu za chakula ndizo zinazoingia Gaza tangu kuanza kwa mzozo huo Oktoba 7. Hali ni mbaya na imesababisha njaa kwa karibu wate wote wa eneo hilo na tegemeo lao pekee lililobaki ni msaada wa chakula kutoka WFP.Makala leo tunaangazia umuhimu wa choo wakati hapo jana Novemba 19 dunia imeadhimisha Siku ya choo Duniani. Maudhui yaliyobeba siku hiyo ni ‘Kuongeza kasi ya mabadiliko’. Kampeni hii inazingatia athari za janga la usafi wa mazingira ambalo huwa chanzo cha magonjwa mengi hasa ya kuambukiza. Kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO watu bilioni 3.6 karibu nusu ya watu wote duniani hawana huduma za msingi za usafi na milioni 494 miongoni mwao wanajisaidia haja kubwa katika maeneo ya wazi kwa kukosa huduma ya choo wengi wakiwa ni kutoka katika nchi masikini. Pamela Awuori wa Idhaa hii ya Kiswahili amezungumza na baadhi ya wakazi wa eneo la Ngong, Kaunti ya Kajiado, nchini Kenya.Katika mashinani tutasikia ujumbe uliotolewa na mshindi wa tuzo ya polisi mwanamke wa mwaka wa Umoja wa Mataifa. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
20-11-2023 • 13 minuten, 24 seconden
WFP yaonya mfumo wa chakula Gaza umesambaratika kabisa
Mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati umesambaratisha kabisa mfumo wa chakula Gaza limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, likisisitiza wakati huu ambapo ni asilimia 10 tu ya bidhaa muhimu za chakula ndizo zinazoingia Gaza tangu kuanza kwa mzozo huo Oktoba 7. Hali ni mbaya na imesababisha njaa kwa karibu wate wote wa eneo hilo na tegemeo lao pekee lililobaki ni msaada wa chakula kutoka WFP. Watoto wakicheza nje ya majengo ya shule ya umma ya GV katika eneo la Deir El Balah Gaza, kana kwamba hakuna kinachoendelea, wakifurahia utoto wao na kidogo kusahau vita iliyowalazimu kuwa wakimbizi wa ndani katika shule hii iliyogeuzwa makazi ya muda.Inakadiriwa kwamba watu takriban 6,000 wanapata hifadhi katika kila shule kama hii.Hapa mlo ni changamoto, Nattss……Wanawake kwa wanaume wanapika na kujaribu kuoka mikate ambayo ndio chakula kikuu Gaza kwenye majiko ya kuni na mkaa kwani hawana gesi wala umeme. Shifa Al Masri ni mama na mmoja wa wakimbizi wa ndani hapa anasema “Watoto wananjaa na kiu na wote wanaharisha kutapika na kukohoa, hakuna chakula wala matibabu”Kabla ya machafuko ya sasa watu hawa walikuwa walila wawzavyo na kujipatia mahitaji katika maduka ya chakula yanayoendeshwa na WFP lakini sasa maduka haya yamesalia matupu bila chochote.Ni asilimia 25 tu ya maduka yote ya WFP Gaza ndio yaliyosalia wazi na mengine yote yamefunga mlango kwa kuishiwa chakula na yaliyowazi chakula kidogo kilichopo gharama haishikiki hali ambayo imewalazimu watu kula mlo mmoja tu kwa siku.Alaa Younis Mohamed Al-Helw hakuwa na jinsi bali kukimbia na familia yake hadi kwenye makazi haya ambapo sasa analala chini katika nyumba iliyofurika watu 30. Kaja dukani kuangalia mahitaji , lahaula kambulia patupu anatoa wito,“Kama unavyoona tumekuja katika duka hili hakuna chochote tangu asubuhi tumezunguka maduka yote hakuna kitu. Wajuzeni watu ili dunia isikie tuna njaa, tuna njaa tunataka kula, Kuna watoto na mke wangu ana ugonjwa wa moyo anahitaji kula na hakuna hata kipande cha mkate cha kumpa.”Mkate chakula kikuu cha Wapalestina sasa umeadimika kupita kiasi, matumaini yao yote yako kwa WFP. Samer Abdeljaber ni mkurugenzi wa WFP eneo la Palestina,“Watu wanalala njaa. Gaza, watu wanaishi kwa mlo mmoja tu kwa siku ikiwa wana bahati. Uhaba wa mafuta na kutokuwa na mawasiliano kunalemaza operesheni zetu huko Gaza. Ukosefu wa mafuta umekilazimu kiwanda cha mwisho cha kuoka mikate cha WFP kufungwa na pia kinu cha mwisho cha kusagisha unga wa ngano. Hata mkate ambao ni msingi wa kila mlo wa Wapalestina, sasa umeadimika.”Pamoja na changamoto zote hizo WFP imeendelea kuwahakikisha mlo hata kama ni mmoja tu watu hawa, inagawa tende na samaki wa makopo kila siku kwa watu karibu 800,000 wanaohifadhiwa katika shule za shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA na jamii zinazowazunguka.
20-11-2023 • 0
WFP yaonya mfumo wa chakula Gaza umesambaratika kabisa
Mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati umesambaratisha kabisa mfumo wa chakula Gaza limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, likisisitiza wakati huu ambapo ni asilimia 10 tu ya bidhaa muhimu za chakula ndizo zinazoingia Gaza tangu kuanza kwa mzozo huo Oktoba 7. Hali ni mbaya na imesababisha njaa kwa karibu wate wote wa eneo hilo na tegemeo lao pekee lililobaki ni msaada wa chakula kutoka WFP. Watoto wakicheza nje ya majengo ya shule ya umma ya GV katika eneo la Deir El Balah Gaza, kana kwamba hakuna kinachoendelea, wakifurahia utoto wao na kidogo kusahau vita iliyowalazimu kuwa wakimbizi wa ndani katika shule hii iliyogeuzwa makazi ya muda.Inakadiriwa kwamba watu takriban 6,000 wanapata hifadhi katika kila shule kama hii.Hapa mlo ni changamoto, Nattss……Wanawake kwa wanaume wanapika na kujaribu kuoka mikate ambayo ndio chakula kikuu Gaza kwenye majiko ya kuni na mkaa kwani hawana gesi wala umeme. Shifa Al Masri ni mama na mmoja wa wakimbizi wa ndani hapa anasema “Watoto wananjaa na kiu na wote wanaharisha kutapika na kukohoa, hakuna chakula wala matibabu”Kabla ya machafuko ya sasa watu hawa walikuwa walila wawzavyo na kujipatia mahitaji katika maduka ya chakula yanayoendeshwa na WFP lakini sasa maduka haya yamesalia matupu bila chochote.Ni asilimia 25 tu ya maduka yote ya WFP Gaza ndio yaliyosalia wazi na mengine yote yamefunga mlango kwa kuishiwa chakula na yaliyowazi chakula kidogo kilichopo gharama haishikiki hali ambayo imewalazimu watu kula mlo mmoja tu kwa siku.Alaa Younis Mohamed Al-Helw hakuwa na jinsi bali kukimbia na familia yake hadi kwenye makazi haya ambapo sasa analala chini katika nyumba iliyofurika watu 30. Kaja dukani kuangalia mahitaji , lahaula kambulia patupu anatoa wito,“Kama unavyoona tumekuja katika duka hili hakuna chochote tangu asubuhi tumezunguka maduka yote hakuna kitu. Wajuzeni watu ili dunia isikie tuna njaa, tuna njaa tunataka kula, Kuna watoto na mke wangu ana ugonjwa wa moyo anahitaji kula na hakuna hata kipande cha mkate cha kumpa.”Mkate chakula kikuu cha Wapalestina sasa umeadimika kupita kiasi, matumaini yao yote yako kwa WFP. Samer Abdeljaber ni mkurugenzi wa WFP eneo la Palestina,“Watu wanalala njaa. Gaza, watu wanaishi kwa mlo mmoja tu kwa siku ikiwa wana bahati. Uhaba wa mafuta na kutokuwa na mawasiliano kunalemaza operesheni zetu huko Gaza. Ukosefu wa mafuta umekilazimu kiwanda cha mwisho cha kuoka mikate cha WFP kufungwa na pia kinu cha mwisho cha kusagisha unga wa ngano. Hata mkate ambao ni msingi wa kila mlo wa Wapalestina, sasa umeadimika.”Pamoja na changamoto zote hizo WFP imeendelea kuwahakikisha mlo hata kama ni mmoja tu watu hawa, inagawa tende na samaki wa makopo kila siku kwa watu karibu 800,000 wanaohifadhiwa katika shule za shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA na jamii zinazowazunguka.
20-11-2023 • 3 minuten, 42 seconden
Juhudi za pamoja zimesaidia kudhibiti kipindupindu Zanzibar: WHO
Mtazamo wa kujumuisha sekta mbalimbali na kuishirikisha kikamilifu jamii imekuwa chachu kubwa ya kudhibiti milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu iliyokuwa ikikiandama kisiwa cha Zanzibar kwa muda mrefu limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Mtazamo huo ambao unaunganisha kampeni za uelimishaji kwa jamii kupitia ufadhili wa muungano wa chanjo duniani GAVI na msaada wa wadau mbalimbali likiwemo shirika la WHO imekisaidia kisiwa hicho kutokuwa na mgonjwa hata mmoja wa kipindupindu katika miaka mitano iliyopita. Ungana na Flora Nducha kwa makala hii kwa kina.
17-11-2023 • 0
Juhudi za pamoja zimesaidia kudhibiti kipindupindu Zanzibar: WHO
Mtazamo wa kujumuisha sekta mbalimbali na kuishirikisha kikamilifu jamii imekuwa chachu kubwa ya kudhibiti milipuko ya ugonjwa wa kipindupindu iliyokuwa ikikiandama kisiwa cha Zanzibar kwa muda mrefu limesema shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO. Mtazamo huo ambao unaunganisha kampeni za uelimishaji kwa jamii kupitia ufadhili wa muungano wa chanjo duniani GAVI na msaada wa wadau mbalimbali likiwemo shirika la WHO imekisaidia kisiwa hicho kutokuwa na mgonjwa hata mmoja wa kipindupindu katika miaka mitano iliyopita. Ungana na Flora Nducha kwa makala hii kwa kina.
17-11-2023 • 3 minuten, 45 seconden
Umoja wa Mataifa unasimama na Afrika kutatua janga la tabianchi – Joyce Msuya
Ijumaa wiki ijayo yaani tarehe 24 vitaanzaa vikao vya awali kuelekea COP 28 ambao ni Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika Dubai huko Falme za Kiarabu mwishoni mwa mwezi huu kuanzia tarehe 30.Kuelekea mkutano huu, Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Joyce Msuya ameutumia mwezi huu kufanya ziara katika nchi nne za kusini na mashariki mwa Afrika ambako amesisitiza dhamira ya Umoja wa Mataifa ya kusimama na watu na Serikali za ukanda huo wakati janga la tabianchi linafanya mahitaji ya kibinadamu kuwa ya juu zaidi."Na nitamalizia kwa kusema jumuiya ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na NGOs, NGOs za kitaifa na kimataifa, tumejitolea kikamilifu kuendelea kuunga mkono na kukamilisha juhudi za mamlaka zinazojaribu kuokoa maisha, na pia tutaendelea kufanya kazi na wadau wetu wa maendeleo katika mnepo.”Alipokuwa nchini Msumbiji, nchi ya kwanza katika ziara yake kabla ya Kwenda Tanzania, Kenya na Botswana, Bi Msuya alijionea jinsi athari ya pamoja ya vimbunga, migogoro na mabadiliko ya tabianchi yameweka zaidi ya watu milioni 2 katika mahitaji makubwa ya kibinadamu."Nimejawa na matumaini kwa sababu ya ujasiri wa watu niliokutana nao, watoto ambao nimecheza nao, wataalamu wa tiba ambao nimezungumza nao na maafisa wa kibinadamu wa wilaya ambao wanajitoa sana."
17-11-2023 • 0
Umoja wa Mataifa unasimama na Afrika kutatua janga la tabianchi – Joyce Msuya
Ijumaa wiki ijayo yaani tarehe 24 vitaanzaa vikao vya awali kuelekea COP 28 ambao ni Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika Dubai huko Falme za Kiarabu mwishoni mwa mwezi huu kuanzia tarehe 30.Kuelekea mkutano huu, Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Joyce Msuya ameutumia mwezi huu kufanya ziara katika nchi nne za kusini na mashariki mwa Afrika ambako amesisitiza dhamira ya Umoja wa Mataifa ya kusimama na watu na Serikali za ukanda huo wakati janga la tabianchi linafanya mahitaji ya kibinadamu kuwa ya juu zaidi."Na nitamalizia kwa kusema jumuiya ya kibinadamu, Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na NGOs, NGOs za kitaifa na kimataifa, tumejitolea kikamilifu kuendelea kuunga mkono na kukamilisha juhudi za mamlaka zinazojaribu kuokoa maisha, na pia tutaendelea kufanya kazi na wadau wetu wa maendeleo katika mnepo.”Alipokuwa nchini Msumbiji, nchi ya kwanza katika ziara yake kabla ya Kwenda Tanzania, Kenya na Botswana, Bi Msuya alijionea jinsi athari ya pamoja ya vimbunga, migogoro na mabadiliko ya tabianchi yameweka zaidi ya watu milioni 2 katika mahitaji makubwa ya kibinadamu."Nimejawa na matumaini kwa sababu ya ujasiri wa watu niliokutana nao, watoto ambao nimecheza nao, wataalamu wa tiba ambao nimezungumza nao na maafisa wa kibinadamu wa wilaya ambao wanajitoa sana."
17-11-2023 • 1 minuut, 33 seconden
17 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mzozo katika ukanda wa Gaza na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika. Makala na mashinani tunakupeleka viziwani Zanzibar nchini Tanzania, kulikoni?. Wakati mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea na wananchi walioko Gaza wakiwa katika siku ya nne bila mawasiliano kutokana na ukosefu wa mafuta, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya maji salama ya kunywa na usafi ameionya Israel kuwa kuwanyima wananchi maji ni ukiukaji wa haki za binadamu kwani wanatumia maji kama silaha ya vita. Ijumaa wiki ijayo yaani tarehe 24 vitaanzaa vikao vya awali kuelekea COP 28 ambao ni Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika Dubai huko Falme za Kiarabu mwishoni mwa mwezi huu kuanzia tarehe 30.Makala inatupeleka Zanzibar Tanzania ambako juhudi kubwa zilizofanywa na serikali na wadau mbalimbali likiwemo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limesaidia kupambana na kukomesha milipuko ya kipindupindu ya mara kwa mara, kupunguza athari zake vikiwemo vifo na kuelimisha jamii jinsi ya kuzuia milipuko hiyo.Katika mashinani tunakuletea ujumbe kutoka shujaa mwenye umri wa miaka 9 kutoka Visiwani Zanzibar anayeoongoza katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia sauti yake kuhamasisha hatua kwa mustakabali endelevu.” Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
17-11-2023 • 0
17 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mzozo katika ukanda wa Gaza na mabadiliko ya tabianchi barani Afrika. Makala na mashinani tunakupeleka viziwani Zanzibar nchini Tanzania, kulikoni?. Wakati mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea na wananchi walioko Gaza wakiwa katika siku ya nne bila mawasiliano kutokana na ukosefu wa mafuta, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya maji salama ya kunywa na usafi ameionya Israel kuwa kuwanyima wananchi maji ni ukiukaji wa haki za binadamu kwani wanatumia maji kama silaha ya vita. Ijumaa wiki ijayo yaani tarehe 24 vitaanzaa vikao vya awali kuelekea COP 28 ambao ni Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika Dubai huko Falme za Kiarabu mwishoni mwa mwezi huu kuanzia tarehe 30.Makala inatupeleka Zanzibar Tanzania ambako juhudi kubwa zilizofanywa na serikali na wadau mbalimbali likiwemo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limesaidia kupambana na kukomesha milipuko ya kipindupindu ya mara kwa mara, kupunguza athari zake vikiwemo vifo na kuelimisha jamii jinsi ya kuzuia milipuko hiyo.Katika mashinani tunakuletea ujumbe kutoka shujaa mwenye umri wa miaka 9 kutoka Visiwani Zanzibar anayeoongoza katika utunzaji wa mazingira kwa kutumia sauti yake kuhamasisha hatua kwa mustakabali endelevu.” Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
17-11-2023 • 11 minuten, 34 seconden
Israeli yaonywa Maji na mafuta yasitumike kama silaha za vita
Wakati mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea na wananchi walioko Gaza wakiwa katika siku ya nne bila mawasiliano kutokana na ukosefu wa mafuta, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya maji salama ya kunywa na usafi ameionya Israel kuwa kuwanyima wananchi maji ni ukiukaji wa haki za binadamu kwani wanatumia maji kama silaha ya vita. Mwakilishi huyo maalum wa Umoja wa Mataifa Pedro Arrojo- Agudo ameionya Israel hii leo kuwa inapaswa kuruhusu maji safi na mafuta kuingia Gaza ili kuwezesha mtandao wa usambazi wa maji na mitambo ya kuondoa chumvi kwenye maji ifanyekazi mapema kabla ya kuchelewa.Katika taarifa yake iliyotolewa leo huko Geneva Uswisi na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Agudo ameseme “Nataka kuikumbusha Israel kwamba kuzuia vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya maji salama kuingia Ukanda wa Gaza kunakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu. Athari zitakazo jitokeza kwenye afya ya umma haziwezi kufikirika na zinaweza kusababisha vifo vya raia zaidi ya idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na mashambulizi ya Gaza.”Mtaalamu huyo amenukuu kifungu cha 7 cha Mkataba wa Roma kinachohusu kuwanyima raia hali zinazowawezesha kuishi kuwa kunachukuliwa kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu nakusema “Maafa haya ya kivita yanaweza kuzuilika na Israel lazima izuie, Israel lazima iache kutumia maji kama silaha ya vita.”Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA asilimia 70 ya wananchi wa Gaza wanakunywa maji machafu na yenye chumvi na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka iwapo Israel itaendelea kuzuia mafuta kuingia Gaza. UNRWA pia imeeeleza kuwa visima 60 vya kusukuma maji taka huko kusini mwa Gaza pamoja na mitambo ya kuondoa maji chumvi huko Rafah navyo havifanyi kazi suala ambalo limeelezwa kuwa ni hatari kwani linaweza kusababisha milipuko ya magonjwa.Mbali na suala la Maji UNRWA hii leo kupitia mtandao wa kijamii wa X imeeleza kuwa “Watu walioko Ukanda wa Gaza usiku wa jana wametengwa kabisa na ulimwengu kwa sababu ya kukatika kwa mawasiliano kutokana na kutokuwepo kwa mafuta.”Nako huko Ukingo wa Magharibi katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO, limeripoti kuwa na wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya vituo vya afya ambapo tangu tarehe 07 Oktoba mpaka sasa kumekuwa na mashambulizi 170.WHO imeeleza hii leo huko Jenin Ukingo wa Magharibi wahudumu wa afya 6 waliokuwa wakitoka katika hospitali ya Ibn Sina walipekuliwa na kuzuiliwa na magari matatu ya kubeba wagonjwa nayo pia yalipekuliwa. Shirika hilo limekumbusha kuwa wahudumu wa afya sio walengwa katika mizozo na kwamba wanapaswa kulindwa wao navituo vya afya.
17-11-2023 • 0
Israeli yaonywa Maji na mafuta yasitumike kama silaha za vita
Wakati mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea na wananchi walioko Gaza wakiwa katika siku ya nne bila mawasiliano kutokana na ukosefu wa mafuta, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya maji salama ya kunywa na usafi ameionya Israel kuwa kuwanyima wananchi maji ni ukiukaji wa haki za binadamu kwani wanatumia maji kama silaha ya vita. Mwakilishi huyo maalum wa Umoja wa Mataifa Pedro Arrojo- Agudo ameionya Israel hii leo kuwa inapaswa kuruhusu maji safi na mafuta kuingia Gaza ili kuwezesha mtandao wa usambazi wa maji na mitambo ya kuondoa chumvi kwenye maji ifanyekazi mapema kabla ya kuchelewa.Katika taarifa yake iliyotolewa leo huko Geneva Uswisi na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Agudo ameseme “Nataka kuikumbusha Israel kwamba kuzuia vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya maji salama kuingia Ukanda wa Gaza kunakiuka sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu. Athari zitakazo jitokeza kwenye afya ya umma haziwezi kufikirika na zinaweza kusababisha vifo vya raia zaidi ya idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na mashambulizi ya Gaza.”Mtaalamu huyo amenukuu kifungu cha 7 cha Mkataba wa Roma kinachohusu kuwanyima raia hali zinazowawezesha kuishi kuwa kunachukuliwa kuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu nakusema “Maafa haya ya kivita yanaweza kuzuilika na Israel lazima izuie, Israel lazima iache kutumia maji kama silaha ya vita.”Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA asilimia 70 ya wananchi wa Gaza wanakunywa maji machafu na yenye chumvi na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka iwapo Israel itaendelea kuzuia mafuta kuingia Gaza. UNRWA pia imeeeleza kuwa visima 60 vya kusukuma maji taka huko kusini mwa Gaza pamoja na mitambo ya kuondoa maji chumvi huko Rafah navyo havifanyi kazi suala ambalo limeelezwa kuwa ni hatari kwani linaweza kusababisha milipuko ya magonjwa.Mbali na suala la Maji UNRWA hii leo kupitia mtandao wa kijamii wa X imeeleza kuwa “Watu walioko Ukanda wa Gaza usiku wa jana wametengwa kabisa na ulimwengu kwa sababu ya kukatika kwa mawasiliano kutokana na kutokuwepo kwa mafuta.”Nako huko Ukingo wa Magharibi katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO, limeripoti kuwa na wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ya vituo vya afya ambapo tangu tarehe 07 Oktoba mpaka sasa kumekuwa na mashambulizi 170.WHO imeeleza hii leo huko Jenin Ukingo wa Magharibi wahudumu wa afya 6 waliokuwa wakitoka katika hospitali ya Ibn Sina walipekuliwa na kuzuiliwa na magari matatu ya kubeba wagonjwa nayo pia yalipekuliwa. Shirika hilo limekumbusha kuwa wahudumu wa afya sio walengwa katika mizozo na kwamba wanapaswa kulindwa wao navituo vya afya.
17-11-2023 • 2 minuten, 58 seconden
Methali: Ukilima Pantosha utavuna pankwisha
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Nicholus Makanji mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya akitufafanulia maana ya methali, “Ukilima Pantosha utavuna pankwisha.” Karibu!
16-11-2023 • 0
Methali: Ukilima Pantosha utavuna pankwisha
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Nicholus Makanji mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya akitufafanulia maana ya methali, “Ukilima Pantosha utavuna pankwisha.” Karibu!
16-11-2023 • 1 minuut, 6 seconden
16 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo ulimwengu ukijiandaa kuadhimisha siku 16 za harakati kukabiliana na ukatili wa kijinsia katika jamii zinazoendeshwa na Umoja wa Mataifa, baadhi ya sehemu duniani zimeanza kulipa suala Hilo uzito mkubwa ikiwemo Kenya. Kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa mataifa la masuala ya wanawake UN Women na mengine yasiyo ya kiserikali, Kaunti ya Kakamega nchini nchini humo imefanikiwa kuzindua mpango maalum wa kuwapa waathirika wa ukatili wa kijinsia huduma za mahakamani pasi na malipo. UN Women imewashika mkono baadhi ya walioathirika kwa kuwapa bidhaa za matumizi na pia mtaji kuwawezesha kuanza biashara baada ya kuondoka kwenye vituo salama na vya Staha. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka Gaza, Ethiopia n aza WHO kuhusu matumizi ya tumbaku. Katika kujifunza Kiswahili leo tunabisha hodi Chuo Kikuu cha Zetech Limuru nchini Kenya kuchambuliwa maana ya Methali “Ukilima Pantosha utavuna pankwisha”. Kamishina Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) Philippe Lazzarini kupitia ukurasa wake wa X ameandika "Kila siku ni siku ya huzuni kwa Umoja wa Mataifa na UNRWA, na kwamba anasikitika kuthibitisha kwamba wenzake 103 wameuawa Gaza tangu 7 Oktoba. Naye Tom White, Mkurugenzi wa UNRWA Gaza pia kupitia X ameandika kukosekana kwa mafuta inamaanisha ukosefu wa maji ya kunywa na kusababisha ongezeko la asilimia 40 la ugonjwa wa kuhara kwa watu wanaojihifadhi katika shule. Wakati ho huo Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk akisisitiza kuwa njia ya kisiasa inahitajika kuitoa Gaza kwenye janga la kibinadamu. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO), leo limezindua rasmi kampeni ya "Acha uwongo" ikiwa ni hatua muhimu ya kuwalinda vijana dhidi ya sekta ya tumbaku na bidhaa zao. WHO inasema Sekta ya tumbaku ina historia ndefu ya kusema uwongo kwa umma, hata kufikia kusisitiza kwamba uvutaji sigara hausababishi saratani ya mapafu. Pia sekta hiyo inaendelea kutumia njia tofauti kueneza habari potofu, ikijumuisha kupitia watu maarufu katika mitandao ya kijamii, kufadhili matukio, na hata kufadhili wanasayansi na utafiti wenye upendeleo.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema linafufua mfumo wake ulioboreshwa wa operesheni nchini Ethiopia, hatua kubwa ambayo itaanza kuwafikia watu milioni 3.2 kwa msaada wa chakula kwa mara ya kwanza tangu Juni 2023. Msaada wa chakula wa WFP ulisitishwa nchini kote Ethiopia kufuatia ripoti za uporaji wa misaada.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Nicholus Makanji mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya akitufafanulia maana ya methali “Ukilima Pantosha utavuna pankwisha.” Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
16-11-2023 • 0
16 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo ulimwengu ukijiandaa kuadhimisha siku 16 za harakati kukabiliana na ukatili wa kijinsia katika jamii zinazoendeshwa na Umoja wa Mataifa, baadhi ya sehemu duniani zimeanza kulipa suala Hilo uzito mkubwa ikiwemo Kenya. Kwa ushirikiano wa Shirika la Umoja wa mataifa la masuala ya wanawake UN Women na mengine yasiyo ya kiserikali, Kaunti ya Kakamega nchini nchini humo imefanikiwa kuzindua mpango maalum wa kuwapa waathirika wa ukatili wa kijinsia huduma za mahakamani pasi na malipo. UN Women imewashika mkono baadhi ya walioathirika kwa kuwapa bidhaa za matumizi na pia mtaji kuwawezesha kuanza biashara baada ya kuondoka kwenye vituo salama na vya Staha. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka Gaza, Ethiopia n aza WHO kuhusu matumizi ya tumbaku. Katika kujifunza Kiswahili leo tunabisha hodi Chuo Kikuu cha Zetech Limuru nchini Kenya kuchambuliwa maana ya Methali “Ukilima Pantosha utavuna pankwisha”. Kamishina Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) Philippe Lazzarini kupitia ukurasa wake wa X ameandika "Kila siku ni siku ya huzuni kwa Umoja wa Mataifa na UNRWA, na kwamba anasikitika kuthibitisha kwamba wenzake 103 wameuawa Gaza tangu 7 Oktoba. Naye Tom White, Mkurugenzi wa UNRWA Gaza pia kupitia X ameandika kukosekana kwa mafuta inamaanisha ukosefu wa maji ya kunywa na kusababisha ongezeko la asilimia 40 la ugonjwa wa kuhara kwa watu wanaojihifadhi katika shule. Wakati ho huo Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk akisisitiza kuwa njia ya kisiasa inahitajika kuitoa Gaza kwenye janga la kibinadamu. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO), leo limezindua rasmi kampeni ya "Acha uwongo" ikiwa ni hatua muhimu ya kuwalinda vijana dhidi ya sekta ya tumbaku na bidhaa zao. WHO inasema Sekta ya tumbaku ina historia ndefu ya kusema uwongo kwa umma, hata kufikia kusisitiza kwamba uvutaji sigara hausababishi saratani ya mapafu. Pia sekta hiyo inaendelea kutumia njia tofauti kueneza habari potofu, ikijumuisha kupitia watu maarufu katika mitandao ya kijamii, kufadhili matukio, na hata kufadhili wanasayansi na utafiti wenye upendeleo.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema linafufua mfumo wake ulioboreshwa wa operesheni nchini Ethiopia, hatua kubwa ambayo itaanza kuwafikia watu milioni 3.2 kwa msaada wa chakula kwa mara ya kwanza tangu Juni 2023. Msaada wa chakula wa WFP ulisitishwa nchini kote Ethiopia kufuatia ripoti za uporaji wa misaada.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Nicholus Makanji mhadhiri katika chuo Kikuu cha Zetech Limuru Kenya akitufafanulia maana ya methali “Ukilima Pantosha utavuna pankwisha.” Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
16-11-2023 • 12 minuten, 2 seconden
Tiko: Jukwaa la kidijitali linalotumia simu ya mkononi launganisha vijana Kenya
Umoja wa Mataifa nchini Kenya, kupitia ushirikiano unaoongozwa na UNFPA, UNAIDS, WHO, na Jukwaa la Ushirikiano wa SDG, chini ya uratibu wa jumla wa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, kwa ushirikiano na Serikali ya Kenya, shirika la kimataifa la Triggerise, Children's Investment Fund Foundation (CIFF), and Bridges Outcomes Partnerships wanatekeleza mradi wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana nchini Kenya kupitia huduma ya Tiko ya shirika la Triggerise. Kiujumla huduma ya TIKO inalenga kupunguza mimba za utotoni na maambukizi ya VVU miongoni mwa wasichana wenye umri wa miaka 15 - 19Tiko ni jukwaa la kidijitali linalotumia simu ya mkononi ambalo huunganisha vijana waliobalehe kwenye vituo vya karibu vya umma na vya kibinafsi vinavyotoa huduma bila malipo. Mfumo wa Tiko unawaleta pamoja wahusika wakiwemo mitandao ya kliniki za afya, maduka ya dawa, mitandaoni, mashirika ya kijamii, na wahudumu wa afya wanaosaidia vijana katika kufanya uamuzi wao kwa huduma za afya na ustawi wanazohitaji ili kustawi. Kupitia mfumo wa kidijitali, Triggerise inaweza kufuatilia kila senti inakoenda na kutathmini matokeo yake kila siku kwa ripoti za wakati halisi na maarifa yanayotokana na takwimu.
15-11-2023 • 0
Tiko: Jukwaa la kidijitali linalotumia simu ya mkononi launganisha vijana Kenya
Umoja wa Mataifa nchini Kenya, kupitia ushirikiano unaoongozwa na UNFPA, UNAIDS, WHO, na Jukwaa la Ushirikiano wa SDG, chini ya uratibu wa jumla wa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa, kwa ushirikiano na Serikali ya Kenya, shirika la kimataifa la Triggerise, Children's Investment Fund Foundation (CIFF), and Bridges Outcomes Partnerships wanatekeleza mradi wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana nchini Kenya kupitia huduma ya Tiko ya shirika la Triggerise. Kiujumla huduma ya TIKO inalenga kupunguza mimba za utotoni na maambukizi ya VVU miongoni mwa wasichana wenye umri wa miaka 15 - 19Tiko ni jukwaa la kidijitali linalotumia simu ya mkononi ambalo huunganisha vijana waliobalehe kwenye vituo vya karibu vya umma na vya kibinafsi vinavyotoa huduma bila malipo. Mfumo wa Tiko unawaleta pamoja wahusika wakiwemo mitandao ya kliniki za afya, maduka ya dawa, mitandaoni, mashirika ya kijamii, na wahudumu wa afya wanaosaidia vijana katika kufanya uamuzi wao kwa huduma za afya na ustawi wanazohitaji ili kustawi. Kupitia mfumo wa kidijitali, Triggerise inaweza kufuatilia kila senti inakoenda na kutathmini matokeo yake kila siku kwa ripoti za wakati halisi na maarifa yanayotokana na takwimu.
15-11-2023 • 4 minuten, 4 seconden
Waafghanistan wanaorejea kutoka Pakistan wanahitaji msaada - UN
Tangu katikati ya mwezi Septemba mwaka huu kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wananchi wa Afghanistan wanaorejea nchini mwao wakitokea Pakistan ambako wamelazimika kuondoka kutokana na kutokuwa na vibali vya kuishi nchini humo. Ongezeko hilo kubwa la watu limeleta changamoto kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa misaada ya kibinadamu. Wengi wa wananchi hawa wanaorejea Afghanistan wanawasili wakiwa na mali kidogo kwani nyumba na mali zao zote wameziacha nchini Pakistan na sasa wanafika mpakani wakiwa hawajui waende wapi wala mustakabali wa maisha yao. Kaimu Mratibu wa masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Daniel Peter Endres, akimbatana na maafisa wengine wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wamefanya ziara maalum jimboni Nangarhar na kuzungumza na wananchi hao. “Leo niko hapa katika eneo la Torkham mpakani na Pakistani kushuhudia maelfu ya Waafghanistan wakirejea. Wengi wa watu hawa wako katika hali mbaya sana, walisubiri siku kadhaa kabla ya kufika hapa. Nimezungumza na watu wengi, na wameniambia hawana nyumba hapa nchini Afghanistan na majira ya baridi yataanza ndani ya wiki chache zijazo.” Ujumbe unaoongozwa na Bwana Endres pia umetembelea katika kituo cha wasafiri kilichoanzishwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Kuhudumia wahamiaji IOM na la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambapo Waafghanstani wanaorejea wamepiga kambi. Wakiwa kituoni hapo wanafanya tathmini za wanaorejea, mahitaji yao na jinsi bora ya kuwasaidia. “Watu wengi wanahitaji nyumba za kuishi. Na changamoto nikuwa mwezi uliopita kulikuwa na tetemeko kubwa la ardhi katika jimbo la Herat na mablangeti yote na vifaa vingine tulivyokuwa navyo hapa nchini Afghanistan tumevitumia kwa waathirika wa tetemeko. Hii ni changamoto tuliyonayo wakati huu katika kuwasaidia wananchi wanaorejea kutoka Pakistan na wanarejea kwa idadi kubwa. Ni muhimu sana kwanza tukipata suluhisho la muda mfupi. Watu hawa tuwape fedha taslimu, chakula na maji. Itakuwa changamoto kubwa Kwa wanawake na watoto.”Ndani ya kipindi cha miezi miwili Waafghani 327,000 wamerejea kutokea Pakistan na kati yao asilimia 45 ambao ni watu 148,000 wamewasilia kati ya tarehe mosi mpaka 11 mwezi huu wa Novemba wengi wao wakipitia katika jimbo la Nangarhar.
15-11-2023 • 0
Waafghanistan wanaorejea kutoka Pakistan wanahitaji msaada - UN
Tangu katikati ya mwezi Septemba mwaka huu kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wananchi wa Afghanistan wanaorejea nchini mwao wakitokea Pakistan ambako wamelazimika kuondoka kutokana na kutokuwa na vibali vya kuishi nchini humo. Ongezeko hilo kubwa la watu limeleta changamoto kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa misaada ya kibinadamu. Wengi wa wananchi hawa wanaorejea Afghanistan wanawasili wakiwa na mali kidogo kwani nyumba na mali zao zote wameziacha nchini Pakistan na sasa wanafika mpakani wakiwa hawajui waende wapi wala mustakabali wa maisha yao. Kaimu Mratibu wa masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Daniel Peter Endres, akimbatana na maafisa wengine wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wamefanya ziara maalum jimboni Nangarhar na kuzungumza na wananchi hao. “Leo niko hapa katika eneo la Torkham mpakani na Pakistani kushuhudia maelfu ya Waafghanistan wakirejea. Wengi wa watu hawa wako katika hali mbaya sana, walisubiri siku kadhaa kabla ya kufika hapa. Nimezungumza na watu wengi, na wameniambia hawana nyumba hapa nchini Afghanistan na majira ya baridi yataanza ndani ya wiki chache zijazo.” Ujumbe unaoongozwa na Bwana Endres pia umetembelea katika kituo cha wasafiri kilichoanzishwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Kuhudumia wahamiaji IOM na la kuhudumia wakimbizi UNHCR ambapo Waafghanstani wanaorejea wamepiga kambi. Wakiwa kituoni hapo wanafanya tathmini za wanaorejea, mahitaji yao na jinsi bora ya kuwasaidia. “Watu wengi wanahitaji nyumba za kuishi. Na changamoto nikuwa mwezi uliopita kulikuwa na tetemeko kubwa la ardhi katika jimbo la Herat na mablangeti yote na vifaa vingine tulivyokuwa navyo hapa nchini Afghanistan tumevitumia kwa waathirika wa tetemeko. Hii ni changamoto tuliyonayo wakati huu katika kuwasaidia wananchi wanaorejea kutoka Pakistan na wanarejea kwa idadi kubwa. Ni muhimu sana kwanza tukipata suluhisho la muda mfupi. Watu hawa tuwape fedha taslimu, chakula na maji. Itakuwa changamoto kubwa Kwa wanawake na watoto.”Ndani ya kipindi cha miezi miwili Waafghani 327,000 wamerejea kutokea Pakistan na kati yao asilimia 45 ambao ni watu 148,000 wamewasilia kati ya tarehe mosi mpaka 11 mwezi huu wa Novemba wengi wao wakipitia katika jimbo la Nangarhar.
15-11-2023 • 2 minuten, 25 seconden
15 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu katika ukanda wa Gaza na wakimbizi wa Afghanistan wanaorejea nyumbani kutoka Pakistan. Makala tunaelekea nchini Kenya na Mashinani nchini Tanzania, kulikoni? Umoja wa Mataifa leo umesisitiza kwa mara nyingine kwamba kinachoendelea Gaza ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu huku kukiwa na ripoti kwamba vikosi vya Israel vimevamia Hospitali ya Al-Shifa jana usiku ambako mbali ya wagonjwa kuna maelfu ya raia waliotawanywa wanapata hifadhi na umeonya kwamba hospital sio uwanja wa vita na madhila hayo kwa raia wakiwemo watoto lazima yakome kwa kutekeleza mambo 10 ya muhimu. Tangu katikati ya mwezi Septemba mwaka huu kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wananchi wa Afghanistan wanaorejea nchini mwao wakitokea Pakistan ambako wamelazimika kuondoka kutokana na kutokuwa na vibali vya kuishi nchini humo. Ongezeko hilo kubwa la watu limeleta changamoto kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa misaada ya kibinadamu.Makala tunakupeleka nchini Kenya kuangazia mradi ambao unaungwa mkono na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kupitia shirika la kimataifa la Triggerise linalotumia huduma ya simu inayofahamika kama Tiko kwa lengo kuu la kuunguza mimba za utotoni na maambuki ya VVU miongoni mwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 19. Evarist Mapesa anasimulia makala hii iliyoratibiwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Pamoja wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG).Mashinani tunaelekea Mkoani Kigoma-magharibi mwa Tanzania kumsikia ujumbe kutoka kwa mhudumu wa afya mkoani humo kuhusu kampeini ya chanjo ya polio awamu ya pili, lakini kwanza ni makala. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
15-11-2023 • 0
15 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu katika ukanda wa Gaza na wakimbizi wa Afghanistan wanaorejea nyumbani kutoka Pakistan. Makala tunaelekea nchini Kenya na Mashinani nchini Tanzania, kulikoni? Umoja wa Mataifa leo umesisitiza kwa mara nyingine kwamba kinachoendelea Gaza ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu huku kukiwa na ripoti kwamba vikosi vya Israel vimevamia Hospitali ya Al-Shifa jana usiku ambako mbali ya wagonjwa kuna maelfu ya raia waliotawanywa wanapata hifadhi na umeonya kwamba hospital sio uwanja wa vita na madhila hayo kwa raia wakiwemo watoto lazima yakome kwa kutekeleza mambo 10 ya muhimu. Tangu katikati ya mwezi Septemba mwaka huu kumekuwa na ongezeko kubwa la idadi ya wananchi wa Afghanistan wanaorejea nchini mwao wakitokea Pakistan ambako wamelazimika kuondoka kutokana na kutokuwa na vibali vya kuishi nchini humo. Ongezeko hilo kubwa la watu limeleta changamoto kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa misaada ya kibinadamu.Makala tunakupeleka nchini Kenya kuangazia mradi ambao unaungwa mkono na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kupitia shirika la kimataifa la Triggerise linalotumia huduma ya simu inayofahamika kama Tiko kwa lengo kuu la kuunguza mimba za utotoni na maambuki ya VVU miongoni mwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 19. Evarist Mapesa anasimulia makala hii iliyoratibiwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Pamoja wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG).Mashinani tunaelekea Mkoani Kigoma-magharibi mwa Tanzania kumsikia ujumbe kutoka kwa mhudumu wa afya mkoani humo kuhusu kampeini ya chanjo ya polio awamu ya pili, lakini kwanza ni makala. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
15-11-2023 • 13 minuten, 37 seconden
Mambo 10 lazima yatekelezwe kuleta afueni katika ukanda wa Gaza: Griffiths
Umoja wa Mataifa leo umesisitiza kwa mara nyingine kwamba kinachoendelea Gaza ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu huku kukiwa na ripoti kwamba vikosi vya Israel vimevamia Hospitali ya Al-Shifa jana usiku ambako mbali ya wagonjwa kuna maelfu ya raia waliotawanywa wanapata hifadhi na umeonya kwamba hospital sio uwanja wa vita na madhila hayo kwa raia wakiwemo watoto lazima yakome kwa kutekeleza mambo 10 ya muhimu. Hali inaendelea kuwa janga kubwa la kibinadamu kwa watu wa Gaza kwa kumujibu wa mkuu wa masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffis ambaye kupitia tarifa yake iliyotolewa leo amesema “Wakati mauaji ya Gaza yakifikia viwango vipya vya kutisha kila siku, ulimwengu unaendelea kutazama kwa mshtuko huku hospitali zikiteketea, watoto wanaozaliwa njiti wanakufa, na watu wote wananyimwa njia za msingi za kujikimu. Hii haiwezi kuruhusiwa kuendelea.Pande zinazozozana lazima ziheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu, zikubali kusitishwa kwa mapigano kwa minajili ya kibinadamu na kukomesha kabisa mapigano hayo.”Kwa niaba ya jumuiya ya kibinadamu anayowakilisha, Griffiths amehimiza pande zote, wale wote walio na ushawishi juu pande kinzani, na jumuiya pana ya kimataifa kufanya kila liwezalo kuunga mkono na kutekeleza mambo kumi yafuatayo;Mosi: Kuwezesha juhudi za mashirika ya misaada kuwa na mtiririko endelevu wa misafara ya misaada na kufanya hivyo kwa njia ya usalama.Pili: Kufungua sehemu za ziada za kuvuka kwa ajili ya misaada na malori ybiashara kuingia, ikiwa ni pamoja na Kerem Shalom.Tatu: Kuruhusu Umoja wa Mataifa, mashirika mengine ya kibinadamu na mashirika ya umma na ya kibinafsi kupata mafuta kwa wingi wa kutosha ili kutoa misaada na kutoa huduma za msingi.Nnne: Kuwezesha mashirika ya kibinadamu kutoa misaada kote Gaza bila vikwazo au kuingiliwa.Tano: Kuruhusu kupanua wigo wa idadi ya makazi salama kwa watu waliohamishwa katika shule na vituo vingine vya umma kote Gaza na kuhakikisha kwamba wanasalia kuwa sehemu za usalama wakati wote wa vita.Sita: Kuboresha utaratibu wa taarifa za kibinadamu ambao ungesaidia kuwaepusha raia na miundombinu ya kiraia kutokana na uhasama na kusaidia kuwezesha ufikiaji wa kibinadamu.Saba: Kuruhusu kuweka vituo vya usambazaji wa misaada kwa raia, kulingana na mahitaji.Nane: Kuruhusu raia kuhamia maeneo salama na kurudi kwa hiari katika makazi yao.Tisa: Kufadhili ombi la misaada ya kibinadamu, ambalo sasa linafikia dola bilioni 1.2.Kumi: Tekeleza usitishaji mapigano wa kibinadamu ili kuruhusu huduma za msingi kuanza upya na biashara muhimu kuanza tena. Usitishaji huo wa mapigano pia ni muhimu kuwezesha utoaji wa misaada, kuruhusu kuachiliwa kwa mateka, na kutoa afueni kwa raia.Amehitimisha tarifa yake kwa kusema kwamba “Hivi ndivyo vitendo vinavyohitajika kudhibiti mauaji. Mpango huu ni wa kina, na tumedhamiria kusukuma kila hatua, lakini tunahitaji uungwaji mkono mkubwa wa kimataifa.D unia lazima ichukue hatua kabla haijachelewa.”
15-11-2023 • 0
Mambo 10 lazima yatekelezwe kuleta afueni katika ukanda wa Gaza: Griffiths
Umoja wa Mataifa leo umesisitiza kwa mara nyingine kwamba kinachoendelea Gaza ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu huku kukiwa na ripoti kwamba vikosi vya Israel vimevamia Hospitali ya Al-Shifa jana usiku ambako mbali ya wagonjwa kuna maelfu ya raia waliotawanywa wanapata hifadhi na umeonya kwamba hospital sio uwanja wa vita na madhila hayo kwa raia wakiwemo watoto lazima yakome kwa kutekeleza mambo 10 ya muhimu. Hali inaendelea kuwa janga kubwa la kibinadamu kwa watu wa Gaza kwa kumujibu wa mkuu wa masuala ya kibinadamu na msaada wa dharura wa Umoja wa Mataifa Martin Griffis ambaye kupitia tarifa yake iliyotolewa leo amesema “Wakati mauaji ya Gaza yakifikia viwango vipya vya kutisha kila siku, ulimwengu unaendelea kutazama kwa mshtuko huku hospitali zikiteketea, watoto wanaozaliwa njiti wanakufa, na watu wote wananyimwa njia za msingi za kujikimu. Hii haiwezi kuruhusiwa kuendelea.Pande zinazozozana lazima ziheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu, zikubali kusitishwa kwa mapigano kwa minajili ya kibinadamu na kukomesha kabisa mapigano hayo.”Kwa niaba ya jumuiya ya kibinadamu anayowakilisha, Griffiths amehimiza pande zote, wale wote walio na ushawishi juu pande kinzani, na jumuiya pana ya kimataifa kufanya kila liwezalo kuunga mkono na kutekeleza mambo kumi yafuatayo;Mosi: Kuwezesha juhudi za mashirika ya misaada kuwa na mtiririko endelevu wa misafara ya misaada na kufanya hivyo kwa njia ya usalama.Pili: Kufungua sehemu za ziada za kuvuka kwa ajili ya misaada na malori ybiashara kuingia, ikiwa ni pamoja na Kerem Shalom.Tatu: Kuruhusu Umoja wa Mataifa, mashirika mengine ya kibinadamu na mashirika ya umma na ya kibinafsi kupata mafuta kwa wingi wa kutosha ili kutoa misaada na kutoa huduma za msingi.Nnne: Kuwezesha mashirika ya kibinadamu kutoa misaada kote Gaza bila vikwazo au kuingiliwa.Tano: Kuruhusu kupanua wigo wa idadi ya makazi salama kwa watu waliohamishwa katika shule na vituo vingine vya umma kote Gaza na kuhakikisha kwamba wanasalia kuwa sehemu za usalama wakati wote wa vita.Sita: Kuboresha utaratibu wa taarifa za kibinadamu ambao ungesaidia kuwaepusha raia na miundombinu ya kiraia kutokana na uhasama na kusaidia kuwezesha ufikiaji wa kibinadamu.Saba: Kuruhusu kuweka vituo vya usambazaji wa misaada kwa raia, kulingana na mahitaji.Nane: Kuruhusu raia kuhamia maeneo salama na kurudi kwa hiari katika makazi yao.Tisa: Kufadhili ombi la misaada ya kibinadamu, ambalo sasa linafikia dola bilioni 1.2.Kumi: Tekeleza usitishaji mapigano wa kibinadamu ili kuruhusu huduma za msingi kuanza upya na biashara muhimu kuanza tena. Usitishaji huo wa mapigano pia ni muhimu kuwezesha utoaji wa misaada, kuruhusu kuachiliwa kwa mateka, na kutoa afueni kwa raia.Amehitimisha tarifa yake kwa kusema kwamba “Hivi ndivyo vitendo vinavyohitajika kudhibiti mauaji. Mpango huu ni wa kina, na tumedhamiria kusukuma kila hatua, lakini tunahitaji uungwaji mkono mkubwa wa kimataifa.D unia lazima ichukue hatua kabla haijachelewa.”
15-11-2023 • 3 minuten, 30 seconden
Mfumo wa afya Gaza umeelemewa - Mashirika
Licha ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na makazi ya watu katika Ukanda wa Gaza, mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kujitahidi usiku na mchana kuhakikisha watu wanapata huduma ya afya ili kuokoa maisha yao lakini ni wazi kwamba hali inazidi kuwa mbaya kila uchao. Anold Kayanda amefuatilia suala hili na kutuandalia mada hii kwa kina.
14-11-2023 • 0
Mfumo wa afya Gaza umeelemewa - Mashirika
Licha ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na makazi ya watu katika Ukanda wa Gaza, mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kujitahidi usiku na mchana kuhakikisha watu wanapata huduma ya afya ili kuokoa maisha yao lakini ni wazi kwamba hali inazidi kuwa mbaya kila uchao. Anold Kayanda amefuatilia suala hili na kutuandalia mada hii kwa kina.
14-11-2023 • 4 minuten, 2 seconden
14 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo licha ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na makazi ya watu katika Ukanda wa Gaza, mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kujitahidi usiku na mchana kuhakikisha watu wanapata huduma ya afya ili kuokoa maisha yao lakini ni wazi kwamba hali inazidi kuwa mbaya kila uchao. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani. Huko Gaza Mashariki ya Kati madhila kwa raia yanaendelea na leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limepongeza ujasiri wa juhudi za wahudumu wa afya katika hospitali ya Al-shifa na kuelezea hofu yake kwa maelfu ya watu waliotawanywa na mgogoro unaoendelea kufuatia mvua kubwa zinazonyesha ambazo zimesababisha mafuriko na kufanya hali ya ya kibinadamu iliyokuwa mbaya kuwa mbaya zaidi. Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya kuhusu ukosefu wa mafuta likisema sasa akiba yote imekwisha, malori yake hayawezi kufanya kazi na hivyo hayataweza kupokea msaada kutoka kivuko cha Rafah, nusu ya hospital zote Gaza hazifanyikazi kwa kukosa mafuta na 14 zinazoendelea kufanyakazi hazina mafuta ya kutosha na vifaa muhimu vinavyohitajika huku mawasiliano yakiendelea kuwa changamoto kubwa. Tukiendelea na madhila kwingineko nchini Sudan shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema leo kwamba mlipuko mpya wa kipindupindu unaongeza shinikizo katika hali mbaya ya kibinadamu nchini humo.Na leo ni siku ya kisukari duniani miaka 100 tangu kugunduliwa kwa ugonjwa huo shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO linasema takriban watu milioni 422 waliishi na kisukari mwaka 2014 na idadi ya wenye ugonjwa huo imeongezeka karibu mara mbili tangu mwaka 1980 kutoka asilimia 4.7 hadi asilimia 8.5. Na mashinani ikiwa leo ni Siku ya kutokomeza ugonjwa wa kisukari tutakuletea ujumbe wa WHO kuhusu matumizi ya sukari mbadala na madhara yake.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
14-11-2023 • 0
14 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo licha ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na makazi ya watu katika Ukanda wa Gaza, mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kujitahidi usiku na mchana kuhakikisha watu wanapata huduma ya afya ili kuokoa maisha yao lakini ni wazi kwamba hali inazidi kuwa mbaya kila uchao. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani. Huko Gaza Mashariki ya Kati madhila kwa raia yanaendelea na leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limepongeza ujasiri wa juhudi za wahudumu wa afya katika hospitali ya Al-shifa na kuelezea hofu yake kwa maelfu ya watu waliotawanywa na mgogoro unaoendelea kufuatia mvua kubwa zinazonyesha ambazo zimesababisha mafuriko na kufanya hali ya ya kibinadamu iliyokuwa mbaya kuwa mbaya zaidi. Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya kuhusu ukosefu wa mafuta likisema sasa akiba yote imekwisha, malori yake hayawezi kufanya kazi na hivyo hayataweza kupokea msaada kutoka kivuko cha Rafah, nusu ya hospital zote Gaza hazifanyikazi kwa kukosa mafuta na 14 zinazoendelea kufanyakazi hazina mafuta ya kutosha na vifaa muhimu vinavyohitajika huku mawasiliano yakiendelea kuwa changamoto kubwa. Tukiendelea na madhila kwingineko nchini Sudan shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema leo kwamba mlipuko mpya wa kipindupindu unaongeza shinikizo katika hali mbaya ya kibinadamu nchini humo.Na leo ni siku ya kisukari duniani miaka 100 tangu kugunduliwa kwa ugonjwa huo shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO linasema takriban watu milioni 422 waliishi na kisukari mwaka 2014 na idadi ya wenye ugonjwa huo imeongezeka karibu mara mbili tangu mwaka 1980 kutoka asilimia 4.7 hadi asilimia 8.5. Na mashinani ikiwa leo ni Siku ya kutokomeza ugonjwa wa kisukari tutakuletea ujumbe wa WHO kuhusu matumizi ya sukari mbadala na madhara yake.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
14-11-2023 • 10 minuten, 45 seconden
Huduma za afya Al-Shifa zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa rasilimali - WHO
Tangu October 7,2023 mzozo unaoendelea nchini Israel na Wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas umesababisha idadi kubwa ya vifo na majeraha kwa raia na wafanyakazi zaidi ya 100 wa Umoja wa Mataifa. katika ukanda wa Gaza mashambulizi ya anga na ukosefu wa vifaa vya matibabu, chakula, maji na mafuta vimeathiri mfumo wa huduma za afya ambao tayari unakabiliwa na upungufu mkubwa wa rasilimali. Hospitali zimekuwa zikifanya kazi zaidi ya uwezo wake kutokana na ongezeko la idadi ya wagonjwa pamoja na raia waliokimbia makazi yao, utoaji wa huduma muhimu kwa mama na mtoto hadi matibabu ya magonjwa sugu umeathiriwa Vibaya. Tuungane na Evarist Mapesa katika makala hii akiangazia mfumo wa afya.
13-11-2023 • 0
Huduma za afya Al-Shifa zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa rasilimali - WHO
Tangu October 7,2023 mzozo unaoendelea nchini Israel na Wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas umesababisha idadi kubwa ya vifo na majeraha kwa raia na wafanyakazi zaidi ya 100 wa Umoja wa Mataifa. katika ukanda wa Gaza mashambulizi ya anga na ukosefu wa vifaa vya matibabu, chakula, maji na mafuta vimeathiri mfumo wa huduma za afya ambao tayari unakabiliwa na upungufu mkubwa wa rasilimali. Hospitali zimekuwa zikifanya kazi zaidi ya uwezo wake kutokana na ongezeko la idadi ya wagonjwa pamoja na raia waliokimbia makazi yao, utoaji wa huduma muhimu kwa mama na mtoto hadi matibabu ya magonjwa sugu umeathiriwa Vibaya. Tuungane na Evarist Mapesa katika makala hii akiangazia mfumo wa afya.
13-11-2023 • 3 minuten, 39 seconden
13 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangaia hali ya kibinadamu kwa wagonjwa na waliojeruhiwa katika hospital ya Al-Shifa Gaza, na ripoti ya UNICEF kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama kwa watoto. Makala tunasalia huko huko Gaza na masshinani tunakupeleka nchini Nigeria, kulikoni? Hali hatika hospitali za Gaza ni mbayá sana wagonjwa wakiendelea kupoteza maisha wakiwemo watoto njiti katika hospitali ya Al-Shifa ambayo kwa siku ya tatu mfululizo hakuna umeme huku mashambulizi ya Israel yakiongezeka, umesema Umoja wa Mataifa ambao leo unawaomboleza pia wafanyakazi wake 101 waliopoteza maisha katika mzozo huo na kusisitiza kwamba usitishwaji uhasama ni lazima sasa kuliko wakati mwingine wowote. Mtoto mmoja kati ya Watoto watatu au saw ana watoto milioni 739 duniani kote - tayari wanaishi katika maeneo yaliyo na uhaba mkubwa au wa juu sana wa maji, na mabadiliko ya tabianchi yanatishia kufanya hali hii kuwa mbaya zaidi, imebainisha ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwa saa za New York, Marekani. Makala leo inaturejesha Gaza kuangazia changamoto za mfumo wa afya ambazo zinaweka rehani maisha ya mamilioni ya raia wa Gaza wakiwemo kina mama wajawazito na watoto. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mfumo wa afya Gaza karibu unasambaratika kabisa huku huduma muhimu za wagonjwa mahtuti, magonjwa sugu na hata za kujifungua imekuwa mtihani.Na mashinani tunakupeleka jimboni Sokoto nchini Nigeria tumsikilize Rasheeda, mama yake mtoto Nana ambaye ndani ya miezi miwili ameweza kutibiwa utapiamlo mkali ambao uligunduliwa na afisa afya wa mashinani anayefanya kazi chini ya programu zinazofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
13-11-2023 • 0
13 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangaia hali ya kibinadamu kwa wagonjwa na waliojeruhiwa katika hospital ya Al-Shifa Gaza, na ripoti ya UNICEF kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama kwa watoto. Makala tunasalia huko huko Gaza na masshinani tunakupeleka nchini Nigeria, kulikoni? Hali hatika hospitali za Gaza ni mbayá sana wagonjwa wakiendelea kupoteza maisha wakiwemo watoto njiti katika hospitali ya Al-Shifa ambayo kwa siku ya tatu mfululizo hakuna umeme huku mashambulizi ya Israel yakiongezeka, umesema Umoja wa Mataifa ambao leo unawaomboleza pia wafanyakazi wake 101 waliopoteza maisha katika mzozo huo na kusisitiza kwamba usitishwaji uhasama ni lazima sasa kuliko wakati mwingine wowote. Mtoto mmoja kati ya Watoto watatu au saw ana watoto milioni 739 duniani kote - tayari wanaishi katika maeneo yaliyo na uhaba mkubwa au wa juu sana wa maji, na mabadiliko ya tabianchi yanatishia kufanya hali hii kuwa mbaya zaidi, imebainisha ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwa saa za New York, Marekani. Makala leo inaturejesha Gaza kuangazia changamoto za mfumo wa afya ambazo zinaweka rehani maisha ya mamilioni ya raia wa Gaza wakiwemo kina mama wajawazito na watoto. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mfumo wa afya Gaza karibu unasambaratika kabisa huku huduma muhimu za wagonjwa mahtuti, magonjwa sugu na hata za kujifungua imekuwa mtihani.Na mashinani tunakupeleka jimboni Sokoto nchini Nigeria tumsikilize Rasheeda, mama yake mtoto Nana ambaye ndani ya miezi miwili ameweza kutibiwa utapiamlo mkali ambao uligunduliwa na afisa afya wa mashinani anayefanya kazi chini ya programu zinazofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
13-11-2023 • 11 minuten, 19 seconden
Mtoto 1 kati ya 3 anakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji - UNICEF
Mtoto mmoja kati ya Watoto watatu au saw ana watoto milioni 739 duniani kote - tayari wanaishi katika maeneo yaliyo na uhaba mkubwa au wa juu sana wa maji, na mabadiliko ya tabianchi yanatishia kufanya hali hii kuwa mbaya zaidi, imebainisha ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwa saa za New York, Marekani. Ripoti hii iliyotolewa kabla ya mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabianchi wa COP28 unaoanza mwishoni mwa mwezi huu huko Falme za Kiarabu UAE, inaangazia tishio kwa watoto kutokana na mazingira magumu ya upatikanaji maji, mojawapo ya njia ambazo athari za mabadiliko ya tabianchi zinaonekana. Inatoa uchanganuzi wa athari za viwango vitatu vya uhakika wa maji duniani kote - uhaba wa maji, mazingira magumu upatikanaji wa maji, na shinikizo la maji.Ripoti hiyo, nyongeza ya ripoti nyingine ya UNICEF ya mwaka 2021 yenye jina Hatari ya Tabianchi kwa Watoto, pia inaeleza maelfu ya njia nyingine ambazo watoto hubeba mzigo mkubwa wa athari za janga la tabianchi ikiwa ni pamoja na magonjwa, uchafuzi wa hewa, na matukio mabaya ya tabianchi kama vile mafuriko na ukame. Kuanzia wakati wa kutungwa mimba hadi wanapokuwa watu wazima, afya na ukuaji wa akili za watoto, mapafu, mfumo wa kinga na kazi nyingine muhimu huathiriwa na mazingira wanayokulia. Kwa mfano, watoto wana uwezekano mkubwa wa kuteseka kutokana na uchafuzi wa hewa kuliko watu wazima. Kwa ujumla, wanapumua haraka kuliko watu wazima na ubongo wao, mapafu na viungo vingine bado vinakua."Matokeo ya mabadiliko ya tabianchi ni mabaya kwa watoto," Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell anasema na kuongeza kuwa "Miili na akili zao ziko katika hatari ya kipekee kwa hewa chafuzi, lishe duni na joto kali. Sio tu kwamba ulimwengu wao unabadilika - vyanzo vya maji vikikauka na matukio ya tabianchi ya kuogofya yanakuwa yenye nguvu na ya mara kwa mara - hali kadhalika ustawi wao kwani mabadiliko ya tabianchi huathiri afya yao ya kiakili na kimwili. Watoto wanadai mabadiliko, lakini mahitaji yao mara nyingi sana yanawekwa kando.”Kulingana na matokeo ya ripoti hiyo, sehemu kubwa zaidi ya watoto wako katika maeneo ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini na Asia Kusini - ikimaanisha wanaishi katika maeneo yenye rasilimali chache za maji na viwango vya juu vya kutofautiana kwa msimu na mwaka, kupungua kwa maji ya ardhini au hatari ya ukame.Watoto wengi sana - milioni 436 - wanakabiliwa na mzigo maradufu wa uhaba mkubwa au wa juu sana wa maji na viwango vya chini au vya chini sana vya huduma ya maji ya kunywa - inayojulikana kama mazingira magumu sana ya maji - na kuacha maisha yao, afya, na ustawi wao katika hatari. Ni mojawapo ya vichochezi muhimu vya vifo miongoni mwa watoto chini ya miaka mitano kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika.Ripoti hiyo inaonesha kwamba walioathirika zaidi wanaishi katika nchi za kipato cha chini na cha kati katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Asia ya Kati na Kusini, na Mashariki na Kusini-Mashariki mwa Asia. Mnamo mwaka 2022, watoto milioni 436 walikuwa wakiishi katika maeneo yanayokabiliwa na hatari kubwa ya maji. Baadhi ya nchi zilizoathiriwa zaidi ni pamoja na Niger, Jordan, Burkina Faso, Yemen, Chad, na Namibia, ambapo watoto 8 kati ya 10 wako kwenye hatari.Katika mazingira haya, uwekezaji katika huduma za maji safi ya kunywa na usafi wa mazingira ni njia muhimu ya kwanza ya ulinzi kuwalinda watoto dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi pia yanasababisha kuongezeka kwa msongo wa maji - uwiano wa mahitaji ya maji hadi uwepo wa usambazaji endelevu, ripoti inaonya. Ifikapo mwaka 2050, watoto milioni 35 zaidi wanatarajiwa kukabiliwa na viwango vya juu au vya juu sana vya msongo wa maji, huku Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na Asia Kusini kwa sasa zikikabiliwa na mabadiliko makubwa zaidi.Licha ya udhaifu wao wa kipekee, watoto wamepuuzwa au kupuuzwa kwa kiasi kikubwa katika…
13-11-2023 • 0
Mtoto 1 kati ya 3 anakabiliwa na uhaba mkubwa wa maji - UNICEF
Mtoto mmoja kati ya Watoto watatu au saw ana watoto milioni 739 duniani kote - tayari wanaishi katika maeneo yaliyo na uhaba mkubwa au wa juu sana wa maji, na mabadiliko ya tabianchi yanatishia kufanya hali hii kuwa mbaya zaidi, imebainisha ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatatu kwa saa za New York, Marekani. Ripoti hii iliyotolewa kabla ya mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabianchi wa COP28 unaoanza mwishoni mwa mwezi huu huko Falme za Kiarabu UAE, inaangazia tishio kwa watoto kutokana na mazingira magumu ya upatikanaji maji, mojawapo ya njia ambazo athari za mabadiliko ya tabianchi zinaonekana. Inatoa uchanganuzi wa athari za viwango vitatu vya uhakika wa maji duniani kote - uhaba wa maji, mazingira magumu upatikanaji wa maji, na shinikizo la maji.Ripoti hiyo, nyongeza ya ripoti nyingine ya UNICEF ya mwaka 2021 yenye jina Hatari ya Tabianchi kwa Watoto, pia inaeleza maelfu ya njia nyingine ambazo watoto hubeba mzigo mkubwa wa athari za janga la tabianchi ikiwa ni pamoja na magonjwa, uchafuzi wa hewa, na matukio mabaya ya tabianchi kama vile mafuriko na ukame. Kuanzia wakati wa kutungwa mimba hadi wanapokuwa watu wazima, afya na ukuaji wa akili za watoto, mapafu, mfumo wa kinga na kazi nyingine muhimu huathiriwa na mazingira wanayokulia. Kwa mfano, watoto wana uwezekano mkubwa wa kuteseka kutokana na uchafuzi wa hewa kuliko watu wazima. Kwa ujumla, wanapumua haraka kuliko watu wazima na ubongo wao, mapafu na viungo vingine bado vinakua."Matokeo ya mabadiliko ya tabianchi ni mabaya kwa watoto," Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell anasema na kuongeza kuwa "Miili na akili zao ziko katika hatari ya kipekee kwa hewa chafuzi, lishe duni na joto kali. Sio tu kwamba ulimwengu wao unabadilika - vyanzo vya maji vikikauka na matukio ya tabianchi ya kuogofya yanakuwa yenye nguvu na ya mara kwa mara - hali kadhalika ustawi wao kwani mabadiliko ya tabianchi huathiri afya yao ya kiakili na kimwili. Watoto wanadai mabadiliko, lakini mahitaji yao mara nyingi sana yanawekwa kando.”Kulingana na matokeo ya ripoti hiyo, sehemu kubwa zaidi ya watoto wako katika maeneo ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini na Asia Kusini - ikimaanisha wanaishi katika maeneo yenye rasilimali chache za maji na viwango vya juu vya kutofautiana kwa msimu na mwaka, kupungua kwa maji ya ardhini au hatari ya ukame.Watoto wengi sana - milioni 436 - wanakabiliwa na mzigo maradufu wa uhaba mkubwa au wa juu sana wa maji na viwango vya chini au vya chini sana vya huduma ya maji ya kunywa - inayojulikana kama mazingira magumu sana ya maji - na kuacha maisha yao, afya, na ustawi wao katika hatari. Ni mojawapo ya vichochezi muhimu vya vifo miongoni mwa watoto chini ya miaka mitano kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika.Ripoti hiyo inaonesha kwamba walioathirika zaidi wanaishi katika nchi za kipato cha chini na cha kati katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Asia ya Kati na Kusini, na Mashariki na Kusini-Mashariki mwa Asia. Mnamo mwaka 2022, watoto milioni 436 walikuwa wakiishi katika maeneo yanayokabiliwa na hatari kubwa ya maji. Baadhi ya nchi zilizoathiriwa zaidi ni pamoja na Niger, Jordan, Burkina Faso, Yemen, Chad, na Namibia, ambapo watoto 8 kati ya 10 wako kwenye hatari.Katika mazingira haya, uwekezaji katika huduma za maji safi ya kunywa na usafi wa mazingira ni njia muhimu ya kwanza ya ulinzi kuwalinda watoto dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Mabadiliko ya tabianchi pia yanasababisha kuongezeka kwa msongo wa maji - uwiano wa mahitaji ya maji hadi uwepo wa usambazaji endelevu, ripoti inaonya. Ifikapo mwaka 2050, watoto milioni 35 zaidi wanatarajiwa kukabiliwa na viwango vya juu au vya juu sana vya msongo wa maji, huku Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na Asia Kusini kwa sasa zikikabiliwa na mabadiliko makubwa zaidi.Licha ya udhaifu wao wa kipekee, watoto wamepuuzwa au kupuuzwa kwa kiasi kikubwa katika…
13-11-2023 • 1 minuut, 49 seconden
Umoja wa Mataifa yaonya maisha ya watoto yanaendelea kupotea Gaza huku hali ya kukata tamaa ikitawala
Hali hatika hospitali za Gaza ni mbayá sana wagonjwa wakiendelea kupoteza maisha wakiwemo watoto njiti katika hospitali ya Al-Shifa ambayo kwa siku ya tatu mfululizo hakuna umeme huku mashambulizi ya Israel yakiongezeka, umesema Umoja wa Mataifa ambao leo unawaomboleza pia wafanyakazi wake 101 waliopoteza maisha katika mzozo huo na kusisitiza kwamba usitishwaji uhasama ni lazima sasa kuliko wakati mwingine wowote. Asante Leah mashirika yote ya Umoja wa Mataifa yaliyotoa tarifa leo yamerejea wito wa kusitisha machafuko kwani hali inazidi kuwa mbaya zaidi kila uchao, lile la afya duniani WHO limesema watoto sita sita wamefariki dunia leo katika hospitali ya Al-shifa na wengine 37 njiti walilazimika kuhamishiwa katika chumba cha upasuaji mwishoni mwa wiki bila machine zao za kuwapasha joto wakati wahudumu wa afya wakihaha kupasha chumba joto kutokana na ukosefu wa umeme. Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amesisitiza kwamba “Dunia haiwezi kunyamaza kimya wakati hospitali ambazo zinapaswa kuwa mahala salama zimegeuzwa kuwa vituo vya vifo, madhila na kukata tamaa” akirejea wito wa kusitisha uhasama mara moja.Hadi sasa Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu 11,000 wamepoteza Maisha Gaza tangu kuanza kwa mzozo wakiwemo wafanyakazi 101 wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ambao leo wanaombolezwa katika ofisi zote za Umoja wa Mataifa duniani kwa bendera kupepea nusu mlingoti ikiwemo hapa makao makuu jijini New York Marekani.Wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wametoa kauli zao akiwemo mkuu wa shirika la kuhudumia Watoto UNICEF Cindy McCain ambaye amesema “Leo tunaungana na jumuiya ya kimataifa katika wakati wa ukimya kuwakumbuka na kuwaeznzi wafanyakazi wenzetu waliouawa huko Gaza” naye mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Geneva Tatiana Valovaya amewashukuru wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko Gaza kwa kujitolea kwao akiainisha umuhimu wa kazi yao wakati huu mshikamano wa kimataifa ukiwa katika tishio kubwa.Gaza kwa mujibu wa kamishina mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini mashambulizi yanaendelea na leo nyumba ya wageni ya UNRWA iliyoko Rafah imeharibiwa na kombora ingawa hakuna aliyejeruhiwa.Amesema hii inadhihirisha jinsi gani sheria za kimataifa zinavyokiukwa kwa kutojali “ulinzi wa raia, miundombinu yao ikiwemo vifaa vya Umoja wa Mataifa, shule, hospitali, makambi ya wakimbizi na maeneo ya kuabudu.”
13-11-2023 • 0
Umoja wa Mataifa yaonya maisha ya watoto yanaendelea kupotea Gaza huku hali ya kukata tamaa ikitawala
Hali hatika hospitali za Gaza ni mbayá sana wagonjwa wakiendelea kupoteza maisha wakiwemo watoto njiti katika hospitali ya Al-Shifa ambayo kwa siku ya tatu mfululizo hakuna umeme huku mashambulizi ya Israel yakiongezeka, umesema Umoja wa Mataifa ambao leo unawaomboleza pia wafanyakazi wake 101 waliopoteza maisha katika mzozo huo na kusisitiza kwamba usitishwaji uhasama ni lazima sasa kuliko wakati mwingine wowote. Asante Leah mashirika yote ya Umoja wa Mataifa yaliyotoa tarifa leo yamerejea wito wa kusitisha machafuko kwani hali inazidi kuwa mbaya zaidi kila uchao, lile la afya duniani WHO limesema watoto sita sita wamefariki dunia leo katika hospitali ya Al-shifa na wengine 37 njiti walilazimika kuhamishiwa katika chumba cha upasuaji mwishoni mwa wiki bila machine zao za kuwapasha joto wakati wahudumu wa afya wakihaha kupasha chumba joto kutokana na ukosefu wa umeme. Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amesisitiza kwamba “Dunia haiwezi kunyamaza kimya wakati hospitali ambazo zinapaswa kuwa mahala salama zimegeuzwa kuwa vituo vya vifo, madhila na kukata tamaa” akirejea wito wa kusitisha uhasama mara moja.Hadi sasa Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu 11,000 wamepoteza Maisha Gaza tangu kuanza kwa mzozo wakiwemo wafanyakazi 101 wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA ambao leo wanaombolezwa katika ofisi zote za Umoja wa Mataifa duniani kwa bendera kupepea nusu mlingoti ikiwemo hapa makao makuu jijini New York Marekani.Wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa wametoa kauli zao akiwemo mkuu wa shirika la kuhudumia Watoto UNICEF Cindy McCain ambaye amesema “Leo tunaungana na jumuiya ya kimataifa katika wakati wa ukimya kuwakumbuka na kuwaeznzi wafanyakazi wenzetu waliouawa huko Gaza” naye mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa Geneva Tatiana Valovaya amewashukuru wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko Gaza kwa kujitolea kwao akiainisha umuhimu wa kazi yao wakati huu mshikamano wa kimataifa ukiwa katika tishio kubwa.Gaza kwa mujibu wa kamishina mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini mashambulizi yanaendelea na leo nyumba ya wageni ya UNRWA iliyoko Rafah imeharibiwa na kombora ingawa hakuna aliyejeruhiwa.Amesema hii inadhihirisha jinsi gani sheria za kimataifa zinavyokiukwa kwa kutojali “ulinzi wa raia, miundombinu yao ikiwemo vifaa vya Umoja wa Mataifa, shule, hospitali, makambi ya wakimbizi na maeneo ya kuabudu.”
13-11-2023 • 2 minuten, 36 seconden
10 NOVEMBA 2023
Ungana na Leah Mushi kusikia haya jaridani hii leo:Hofu ya uhalifu wa vita ikitanda UN yataka jinamizi linaloghubika Gaza liishe.UNMISS yawajengea wanajeshi wa Sudan Kusini uwezo kulinda haki za watoto.UNCDF na EU katika harakati za kuwakwamua wananchi Gambia dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Na mashinani msichana ambaye ni mkimbizi wa ndani nchini Sudan.
10-11-2023 • 0
10 NOVEMBA 2023
Ungana na Leah Mushi kusikia haya jaridani hii leo:Hofu ya uhalifu wa vita ikitanda UN yataka jinamizi linaloghubika Gaza liishe.UNMISS yawajengea wanajeshi wa Sudan Kusini uwezo kulinda haki za watoto.UNCDF na EU katika harakati za kuwakwamua wananchi Gambia dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Na mashinani msichana ambaye ni mkimbizi wa ndani nchini Sudan.
10-11-2023 • 13 minuten, 7 seconden
09 NOVEMBA 2023
Hii leo Jaridani Evarist Mapesa anakuletea mada kwa akina inayoangazia kazi za majumbani na utasikia kisa cha mtoto wa miaka 11 kutoka nchini Tanzania ambaye akiwa na miaka 10 alikuwa akitumikishwa pamoja na madhila mengine aliyokumbana nayo. Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia masuala ya kibinadamu kwa wananchi wa Gaza na masuala ya mazingira. Na leo katika kujifunza Kiswahili utasikia ufafananuzi wa methali Umekuwa bata akili kwa watoto. Msomaji wako ni Leah Mushi.
9-11-2023 • 0
09 NOVEMBA 2023
Hii leo Jaridani Evarist Mapesa anakuletea mada kwa akina inayoangazia kazi za majumbani na utasikia kisa cha mtoto wa miaka 11 kutoka nchini Tanzania ambaye akiwa na miaka 10 alikuwa akitumikishwa pamoja na madhila mengine aliyokumbana nayo. Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia masuala ya kibinadamu kwa wananchi wa Gaza na masuala ya mazingira. Na leo katika kujifunza Kiswahili utasikia ufafananuzi wa methali Umekuwa bata akili kwa watoto. Msomaji wako ni Leah Mushi.
9-11-2023 • 11 minuten, 36 seconden
Gaza hali ni tete lazima misaada zaidi ipelekwe: WFP
Hali kwa raia walioko Ukanda wa Gaza Mashariki ya Kati inazidi kuwa mbayá kila uchao hasa kutokana na kuendelea kwa operesheni za kijeshi za Israel za agani na ardhini zilizosababisha maelfu ya raia kuendelea kutaabika kwa kukosa mahitaji muhimu ya msingi kama chakula, maji, huduma za afya na mawasiliano limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. Shirika hili ni ambalo ni moja wa wasambazaji wakubwa wa chakula cha msaada sasa wanahaha kuhakikisha malori zaidi yaliyosheheni chakula na maji yanaingia Gaza kupitia mpaka pekee ulio wazi wa Rafah baina ya Gaza na Misri. Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo amefunga safari hadi Rafah kushuhudia hali halisi. Tuungane na Flora Nducha katika makala hii inayoangazia ziara hiyo.
8-11-2023 • 0
Gaza hali ni tete lazima misaada zaidi ipelekwe: WFP
Hali kwa raia walioko Ukanda wa Gaza Mashariki ya Kati inazidi kuwa mbayá kila uchao hasa kutokana na kuendelea kwa operesheni za kijeshi za Israel za agani na ardhini zilizosababisha maelfu ya raia kuendelea kutaabika kwa kukosa mahitaji muhimu ya msingi kama chakula, maji, huduma za afya na mawasiliano limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP. Shirika hili ni ambalo ni moja wa wasambazaji wakubwa wa chakula cha msaada sasa wanahaha kuhakikisha malori zaidi yaliyosheheni chakula na maji yanaingia Gaza kupitia mpaka pekee ulio wazi wa Rafah baina ya Gaza na Misri. Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo amefunga safari hadi Rafah kushuhudia hali halisi. Tuungane na Flora Nducha katika makala hii inayoangazia ziara hiyo.
8-11-2023 • 4 minuten, 10 seconden
Harakati za kujumuisha wanawake kwenye siasa Somalia zaendelea
Catriona Laing, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia amethibitisha kuwa Umoja wa Mataifa unashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Maendeleo ya Wanawake na Haki za Binadamu nchini humo kuhakikisha kwamba sauti za wanawake zinasikika katika Baraza la Ushauri la Taifa (NCC) ambalo kwa sasa linaundwa na wanaume pekee akiwemo Rais wa shirikisho, marais wa majimbo na viongozi wengine wanaume wa ngazi ya juu ya uongozi.Aidha kiongozi mwakilishi hiyo wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ametoa wito wa kutumia mapitio ya katiba yanayoendelea kuhamasisha kupitishwa kisheria kwa asilimia 30 ya mgawo wa wanawake katika Bunge la kitaifa, "Kuhusu asilimia 30, hii lazima iwekwe kisheria. Ni vyema kuwa na dhamira, lakini bila dhamira kisheria, tunajua kutokana na uzoefu katika nchi nyingine kwamba ni vigumu sana kusonga mbele. Nchi barani Afrika ambazo zimefanya vyema zaidi zimefanya nafasi hizi za viti maalumu kulindwa na sheria.”
8-11-2023 • 0
Harakati za kujumuisha wanawake kwenye siasa Somalia zaendelea
Catriona Laing, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia amethibitisha kuwa Umoja wa Mataifa unashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Maendeleo ya Wanawake na Haki za Binadamu nchini humo kuhakikisha kwamba sauti za wanawake zinasikika katika Baraza la Ushauri la Taifa (NCC) ambalo kwa sasa linaundwa na wanaume pekee akiwemo Rais wa shirikisho, marais wa majimbo na viongozi wengine wanaume wa ngazi ya juu ya uongozi.Aidha kiongozi mwakilishi hiyo wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ametoa wito wa kutumia mapitio ya katiba yanayoendelea kuhamasisha kupitishwa kisheria kwa asilimia 30 ya mgawo wa wanawake katika Bunge la kitaifa, "Kuhusu asilimia 30, hii lazima iwekwe kisheria. Ni vyema kuwa na dhamira, lakini bila dhamira kisheria, tunajua kutokana na uzoefu katika nchi nyingine kwamba ni vigumu sana kusonga mbele. Nchi barani Afrika ambazo zimefanya vyema zaidi zimefanya nafasi hizi za viti maalumu kulindwa na sheria.”
8-11-2023 • 1 minuut, 17 seconden
Machungu ya El Nino kuendelea hadi Aprili 2024 kaskazini na kusini mwa dunia
Tukio la mkondo joto la El Niño linalosababisha hivi sasa mvua kubwa, joto kali na ukame kwenye maeneo mbalimbali ya dunia, linatarajiwa kuendelea duniani na kuchochea ongezeko la kiwango cha joto baharini na ardhini, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO hii leo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Taarifa ya WMO iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi inaainisha kuwa El Nino ni mwenendo wa tabianchi unaoambatana na maji ya baharí kuwa ya joto kuliko kawaida kwenye maeneo ya mashariki mwa bahari ya Pasifiki na kusambaa maeneo mengine ya dunia.Hivyo WMO inasema El Nino ilishika kasi mwezi Julai hadi Agosti na kuimarika mwezi Septemba, na kuna uwezekano ikawa na matukio makubwa zaidi mwezi huu wa Novemba hadi Januari 2024.WMO inasema kuna uwezekano wa asilimia 90 kwa El Nino kuendelea kipindi chote cha majira ya baridi kwenye eneo la kaskazini mwa dunia, halikadhalika kipindi cha majira ya joto kwa eneo la kusini mwa dunia.Katibu Mkuu wa WMO Profesa Petteri Taalas anasema kutokana na mwenendo huu, matukio ya kupindukia ya joto kali, ukame, mioto ya nyika, mvua kubwa na mafuriko vinaweza kuimarika kwenye baadhi ya maeneo na kuleta madhara makubwa.Amesema ndio maana WMO inasisitiza mpango wa Utoaji Onyo kwa Haraka kwa Wote ili kuokoa maisha na kupunguza hasara za kiuchumi.Maeneo ambayo yanadokezwa kuwa yatakuwa na mvua kubwa kutokana na El Niño, ni pamoja na Pembe ya Afrika, bonde la Parana Amerika ya Kusini.Mwaka uliotangulia na kuweka rekodi ya kuwa na joto zai kutokana na El Nino ambayo haikuwa ya kawaida ni 2016.
8-11-2023 • 0
Machungu ya El Nino kuendelea hadi Aprili 2024 kaskazini na kusini mwa dunia
Tukio la mkondo joto la El Niño linalosababisha hivi sasa mvua kubwa, joto kali na ukame kwenye maeneo mbalimbali ya dunia, linatarajiwa kuendelea duniani na kuchochea ongezeko la kiwango cha joto baharini na ardhini, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO hii leo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Taarifa ya WMO iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi inaainisha kuwa El Nino ni mwenendo wa tabianchi unaoambatana na maji ya baharí kuwa ya joto kuliko kawaida kwenye maeneo ya mashariki mwa bahari ya Pasifiki na kusambaa maeneo mengine ya dunia.Hivyo WMO inasema El Nino ilishika kasi mwezi Julai hadi Agosti na kuimarika mwezi Septemba, na kuna uwezekano ikawa na matukio makubwa zaidi mwezi huu wa Novemba hadi Januari 2024.WMO inasema kuna uwezekano wa asilimia 90 kwa El Nino kuendelea kipindi chote cha majira ya baridi kwenye eneo la kaskazini mwa dunia, halikadhalika kipindi cha majira ya joto kwa eneo la kusini mwa dunia.Katibu Mkuu wa WMO Profesa Petteri Taalas anasema kutokana na mwenendo huu, matukio ya kupindukia ya joto kali, ukame, mioto ya nyika, mvua kubwa na mafuriko vinaweza kuimarika kwenye baadhi ya maeneo na kuleta madhara makubwa.Amesema ndio maana WMO inasisitiza mpango wa Utoaji Onyo kwa Haraka kwa Wote ili kuokoa maisha na kupunguza hasara za kiuchumi.Maeneo ambayo yanadokezwa kuwa yatakuwa na mvua kubwa kutokana na El Niño, ni pamoja na Pembe ya Afrika, bonde la Parana Amerika ya Kusini.Mwaka uliotangulia na kuweka rekodi ya kuwa na joto zai kutokana na El Nino ambayo haikuwa ya kawaida ni 2016.
8-11-2023 • 1 minuut, 38 seconden
08 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika mwelekeo wa El Nino ya kwamba itaendelea hadi Aprili 2024, halikadhalika madhara yake, Somalia kulekea uchaguzi mkuu na ushiriki wa wanawake; Makala inabisha hodi Mashariki ya Kati usaidizi wa kibinadamu huko Gaza, na mashinani inabisha hodi Armenia.Tukio la mkondo joto la El Niño linalosababisha hivi sasa mvua kubwa, joto kali na ukame kwenye maeneo mbalimbali ya dunia, linatarajiwa kuendelea duniani na kuchochea ongezeko la kiwango cha joto baharini na ardhini, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO hii leo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Catriona Laing, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia amethibitisha kuwa Umoja wa Mataifa unashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Maendeleo ya Wanawake na Haki za Binadamu nchini humo kuhakikisha kwamba sauti za wanawake zinasikika katika Baraza la Ushauri la Taifa (NCC) ambalo kwa sasa linaundwa na wanaume pekee akiwemo Rais wa shirikisho, marais wa majimbo na viongozi wengine wanaume wa ngazi ya juu ya uongozi.Makala inatupeleka Rafah kwenye mpaka wa Ukanda wa Gaza na Misri ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP kama yalivyo mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu linahaha kuingiza msaada Gaza hususan chakula kwa maelfu ya watu wenye uhitaji Gaza. Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo amefunga safari hadi Rafah kushuhudia hali halisi. Tuungane na Flora Nducha katika makala hii inayoangazia alichoshuhudia.Mashinani fursa ni yake Arevik, ambaye ni mama na mkimbizi wa ndani nchini Armenia, akissema licha ya changamoto walizopitia cha muhimu yuko pamoja na familia yake.
8-11-2023 • 0
08 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika mwelekeo wa El Nino ya kwamba itaendelea hadi Aprili 2024, halikadhalika madhara yake, Somalia kulekea uchaguzi mkuu na ushiriki wa wanawake; Makala inabisha hodi Mashariki ya Kati usaidizi wa kibinadamu huko Gaza, na mashinani inabisha hodi Armenia.Tukio la mkondo joto la El Niño linalosababisha hivi sasa mvua kubwa, joto kali na ukame kwenye maeneo mbalimbali ya dunia, linatarajiwa kuendelea duniani na kuchochea ongezeko la kiwango cha joto baharini na ardhini, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO hii leo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.Catriona Laing, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia amethibitisha kuwa Umoja wa Mataifa unashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Maendeleo ya Wanawake na Haki za Binadamu nchini humo kuhakikisha kwamba sauti za wanawake zinasikika katika Baraza la Ushauri la Taifa (NCC) ambalo kwa sasa linaundwa na wanaume pekee akiwemo Rais wa shirikisho, marais wa majimbo na viongozi wengine wanaume wa ngazi ya juu ya uongozi.Makala inatupeleka Rafah kwenye mpaka wa Ukanda wa Gaza na Misri ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP kama yalivyo mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu linahaha kuingiza msaada Gaza hususan chakula kwa maelfu ya watu wenye uhitaji Gaza. Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo amefunga safari hadi Rafah kushuhudia hali halisi. Tuungane na Flora Nducha katika makala hii inayoangazia alichoshuhudia.Mashinani fursa ni yake Arevik, ambaye ni mama na mkimbizi wa ndani nchini Armenia, akissema licha ya changamoto walizopitia cha muhimu yuko pamoja na familia yake.
8-11-2023 • 9 minuten, 49 seconden
07 Novemba 2023
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa ulikuwa na siku tano za kuadhimisha Umoja wa Mataifa kutimiza miaka 78 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945 huko San Fransisco nchini Marekani. Maadhimisho yalifanyika kuanzia tarehe 23 hadi 27 Oktoba kwenye mji mkuu, Kinshasa. Byobe Malenga, mwandishi wetu katika taifa hilo la Maziwa Makuu ndio alikuwa shuhuda wetu wa nini kilifanyika.
7-11-2023 • 0
07 Novemba 2023
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa ulikuwa na siku tano za kuadhimisha Umoja wa Mataifa kutimiza miaka 78 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945 huko San Fransisco nchini Marekani. Maadhimisho yalifanyika kuanzia tarehe 23 hadi 27 Oktoba kwenye mji mkuu, Kinshasa. Byobe Malenga, mwandishi wetu katika taifa hilo la Maziwa Makuu ndio alikuwa shuhuda wetu wa nini kilifanyika.
7-11-2023 • 11 minuten, 45 seconden
Vijana tusiwe watazamaji bali tuchukue hatua kwa kuanza na tulicho nacho- Emmanuel
Vijana wana dhima kubwa katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayofikia ukomo mwaka 2030. Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kutambua nafasi hiyo ya vijana wanatumia vijana wenyewe ili wawe mabalozi wa mashirika hayo mashinani ili kupigia chepuo yale yaliyomo kwenye SDGs. Mathalani nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lina mabalozi na miongoni mwao ni Emmanuel Cosmas Msoka yeye akijikita kwenye masuala ya usafi wa maji, usafi wa mazingira (WASH) na ubunifu. Na ndiye tunammulika leo katika makala ambapo katika mahojiano naFlora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Emmanuel ambaye mwezi Septemba mwaka huu alishiriki vikao vya ngazi ya juu vya vijana kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs alielezea mambo kadhaa akianza na kile alichoondoka nacho.
6-11-2023 • 0
Vijana tusiwe watazamaji bali tuchukue hatua kwa kuanza na tulicho nacho- Emmanuel
Vijana wana dhima kubwa katika kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yanayofikia ukomo mwaka 2030. Mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kutambua nafasi hiyo ya vijana wanatumia vijana wenyewe ili wawe mabalozi wa mashirika hayo mashinani ili kupigia chepuo yale yaliyomo kwenye SDGs. Mathalani nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lina mabalozi na miongoni mwao ni Emmanuel Cosmas Msoka yeye akijikita kwenye masuala ya usafi wa maji, usafi wa mazingira (WASH) na ubunifu. Na ndiye tunammulika leo katika makala ambapo katika mahojiano naFlora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Emmanuel ambaye mwezi Septemba mwaka huu alishiriki vikao vya ngazi ya juu vya vijana kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs alielezea mambo kadhaa akianza na kile alichoondoka nacho.
6-11-2023 • 3 minuten, 33 seconden
Kalavati 'lasogeza' huduma za afya kwa wanajamii Gambia
Nchini Gambia, Magharibi mwa bara la Afrika, kalavati au daraja dogo lililojengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya mitaji, UNCDF kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU)ili kuunganisha maeneo mawili, Pakaliba na Baro Kunda, limesogeza huduma ya afya karibu na wakazi wa maeneo hayo. Anold Kayanda na maelezo zaidiGambia vijijini, Sarata Ceesay, ili kuhudhuria uchunguzi wa baada ya kujifungua hahitaji tena kupita kwenye maji ambako mamba hupenda kukusanyika. Pia halazimiki kulipa nauli kuzunguka kilomita nne kuikwepa adha ya kupita kwenye maji ambayo hujui utaliwa na mamba au utazama maji. Shukrani kwa ujenzi wa kalavati hili jipya.Bi Ceesay, anaweza kujikinga dhidi ya hofu ya kifo cha mtoto mwingine, binti yake Awa ambaye pacha wake alishafariki akiwa kichanga kwa sababu ya changamoto hizi za huduma ya afya, “tulilazimika kuruka kutoka jiwe moja hadi jingine kuvuka mto.” Anasema.Buba Jobe, Muuguzi na Mkunga wa Afya ya Jamii, Kituo cha Afya cha Pakaliba, Gambia anathibitisha mabadiliko haya chanya,"Sasa kwa kuwa wanaweza kutembea kwa urahisi kutoka Baro Kunda hadi Pakaliba bila kulipa nauli yoyote, hiyo imefanya huduma ya afya kufikika. Wanaweza kuja wakati wowote. Kwa hivyo hiyo imeongeza mtiririko wa wagonjwa wetu katika idara ya wagonjwa wa nje.”
6-11-2023 • 0
Kalavati 'lasogeza' huduma za afya kwa wanajamii Gambia
Nchini Gambia, Magharibi mwa bara la Afrika, kalavati au daraja dogo lililojengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya mitaji, UNCDF kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU)ili kuunganisha maeneo mawili, Pakaliba na Baro Kunda, limesogeza huduma ya afya karibu na wakazi wa maeneo hayo. Anold Kayanda na maelezo zaidiGambia vijijini, Sarata Ceesay, ili kuhudhuria uchunguzi wa baada ya kujifungua hahitaji tena kupita kwenye maji ambako mamba hupenda kukusanyika. Pia halazimiki kulipa nauli kuzunguka kilomita nne kuikwepa adha ya kupita kwenye maji ambayo hujui utaliwa na mamba au utazama maji. Shukrani kwa ujenzi wa kalavati hili jipya.Bi Ceesay, anaweza kujikinga dhidi ya hofu ya kifo cha mtoto mwingine, binti yake Awa ambaye pacha wake alishafariki akiwa kichanga kwa sababu ya changamoto hizi za huduma ya afya, “tulilazimika kuruka kutoka jiwe moja hadi jingine kuvuka mto.” Anasema.Buba Jobe, Muuguzi na Mkunga wa Afya ya Jamii, Kituo cha Afya cha Pakaliba, Gambia anathibitisha mabadiliko haya chanya,"Sasa kwa kuwa wanaweza kutembea kwa urahisi kutoka Baro Kunda hadi Pakaliba bila kulipa nauli yoyote, hiyo imefanya huduma ya afya kufikika. Wanaweza kuja wakati wowote. Kwa hivyo hiyo imeongeza mtiririko wa wagonjwa wetu katika idara ya wagonjwa wa nje.”
6-11-2023 • 1 minuut, 30 seconden
"Imetosha!" yasema mashirika ya kimataifa kwa kinachoendelea Gaza
Ikiwa ni siku 30 sasa tangu kuanza kwa mzozo huko Mashariki ya Kati, kati ya Israel na Wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas walioko katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Gaza, mashirika 18 ya Kimataifa ya misaada ya kibinadamu yametoa taarifa ya pamoja hii leo yakisema ‘imetosha’ wakitaka kusitishwa mara moja mzozo huo kwasababu za kibinadamu, mzozo ambao umegharimu maisha ya zaidi ya watu 10,000. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.Mzozo huu alianza Oktoba 7 mwaka huu baada ya wanamgambo wa kipalestina wa Hamas kushambulia Israel, mashambulizi hayo kwa mujibu wa taarifa za Serikali ya Israel yameua takriban waisrael 1,400 huku wengine zaidi ya 200 wakitekwa nyara na Hamas.Katika kujibu mashambulizi, jeshi la Israel lilianza na operesheni ya kurusha makombora kwa njia ya anga na kisha kuongeza operesheni za kijeshi za ardhini ambazo mpaka sasa kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina zimesababisha vifo vya takriban wapalestina 9,500 kati yao 3,900 ni watoto na 2,400 ni wanawake, na 88 ni wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. Zaidi ya watu 23,000 wamejeruhiwa huku maelfu wakiwa hawajapatikana kwani wamefukiwa na vifusi vya nyumba zao ambazo zimelipuliwa na jeshi la Israel.Ufikishaji wa huduma muhimu za misaada ya kibinadamu kwa wananchi milioni 2.2 walioko Ukanda wa Gaza nazo zimekuwa zikisuasua kutokana na mapigano makali yanayoendelea hali ambayo imesababisha uhaba wa chakula, maji, vifaa tiba, mafuta kwa ajili ya kutoa huduma ya nishati hususan ya umeme kwa hospital zinazohudumia wagonjwa. Juhudi mbalimbali za kidiplomasia zimefanyika na zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuazimia kusitishwa kwa mapigano mara moja suala ambalo halijatekelezwa mpaka sasa.Taarifa ya Wakuu wa Kamati ya Kudumu ya Mashirika ya Kimataifa, kuhusu hali ya Israel na eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu hii leo imekuja na kauli moja tu ‘imetosha’, haikubaliki kuendelezwa kwa mauaji yakutisha huko Gaza wakati huo huo wananchi wakikosa huduma muhimu kwani hata miundombinu ya umma inashambuliwa, wakitolea mfano zaidi ya mashambulizi 100 dhidi ya huduma za afya yameripotiwa. Ndani ya kipindi cha siku 10 mawasiliano yamekatika mara 3 huko Gaza hali ambayo si tu imezuia mawasiliano ya raia walioko Gaza bali pia imeliwia vigumu Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA kuwasiliana na wafanyakazi wake walioko Gaza kwa ajili ya kuratibu masuala ya usaidizi. Jeshi la Israel limelipua vyanzo vya maji safi pamoja na hifadhi za maji taka na Ofisi ya moja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu OCHA imeeleza uhaba wa maji hususan Gaza Kaskazini umezua wasiwasi mkubwa wa watu kuwa na upungufu wa maji mwilini na magonjwa yatokanayo na maji kutokana na matumizi ya maji kutoka vyanzo visivyo salama. Tayari UNRWA imeripoti kuwepo kwa wagonjwa kadhaa wenye matatizo ya kupumua, kuhara, tetekuwanga katika maeneo wanayotoa hifadhi. Taarifa hiyo ya pamoja ya mashirika hayo imerejea ombi lao kwa pande zote katika mzozo huo kuheshimu sheria za Kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu, wametoa wito mateka wote waachiliwe bila masharti, raia na miundombinu ya umma isishambuliwe, misaada zaidi ya kibinadamu ambayo ni chakula, maji, dawa iweze kuingia kwa usalama huko Gaza kwa kiwango kinachohitajika na iwafikie wenye uhitaji hasa wanawake na watoto popote walipo. Mashirika ya UN yaliyotia saini taarifa hiyo ni WHO, UN WOMEN, UNFPA, OCHA, UNRWA, UNICEF, IOM, UNHCR, UNDP, UN-HABITAT, OHCHR, mtaalamu maalumu wa UN kuhusu wakimbizi wa ndani, na WFP mashirika yasiyo ya UN ni Care International, Save the Children, Interaction, Mercy Corp na ICVA
6-11-2023 • 0
"Imetosha!" yasema mashirika ya kimataifa kwa kinachoendelea Gaza
Ikiwa ni siku 30 sasa tangu kuanza kwa mzozo huko Mashariki ya Kati, kati ya Israel na Wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas walioko katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Gaza, mashirika 18 ya Kimataifa ya misaada ya kibinadamu yametoa taarifa ya pamoja hii leo yakisema ‘imetosha’ wakitaka kusitishwa mara moja mzozo huo kwasababu za kibinadamu, mzozo ambao umegharimu maisha ya zaidi ya watu 10,000. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.Mzozo huu alianza Oktoba 7 mwaka huu baada ya wanamgambo wa kipalestina wa Hamas kushambulia Israel, mashambulizi hayo kwa mujibu wa taarifa za Serikali ya Israel yameua takriban waisrael 1,400 huku wengine zaidi ya 200 wakitekwa nyara na Hamas.Katika kujibu mashambulizi, jeshi la Israel lilianza na operesheni ya kurusha makombora kwa njia ya anga na kisha kuongeza operesheni za kijeshi za ardhini ambazo mpaka sasa kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina zimesababisha vifo vya takriban wapalestina 9,500 kati yao 3,900 ni watoto na 2,400 ni wanawake, na 88 ni wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. Zaidi ya watu 23,000 wamejeruhiwa huku maelfu wakiwa hawajapatikana kwani wamefukiwa na vifusi vya nyumba zao ambazo zimelipuliwa na jeshi la Israel.Ufikishaji wa huduma muhimu za misaada ya kibinadamu kwa wananchi milioni 2.2 walioko Ukanda wa Gaza nazo zimekuwa zikisuasua kutokana na mapigano makali yanayoendelea hali ambayo imesababisha uhaba wa chakula, maji, vifaa tiba, mafuta kwa ajili ya kutoa huduma ya nishati hususan ya umeme kwa hospital zinazohudumia wagonjwa. Juhudi mbalimbali za kidiplomasia zimefanyika na zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuazimia kusitishwa kwa mapigano mara moja suala ambalo halijatekelezwa mpaka sasa.Taarifa ya Wakuu wa Kamati ya Kudumu ya Mashirika ya Kimataifa, kuhusu hali ya Israel na eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu hii leo imekuja na kauli moja tu ‘imetosha’, haikubaliki kuendelezwa kwa mauaji yakutisha huko Gaza wakati huo huo wananchi wakikosa huduma muhimu kwani hata miundombinu ya umma inashambuliwa, wakitolea mfano zaidi ya mashambulizi 100 dhidi ya huduma za afya yameripotiwa. Ndani ya kipindi cha siku 10 mawasiliano yamekatika mara 3 huko Gaza hali ambayo si tu imezuia mawasiliano ya raia walioko Gaza bali pia imeliwia vigumu Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasaidia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA kuwasiliana na wafanyakazi wake walioko Gaza kwa ajili ya kuratibu masuala ya usaidizi. Jeshi la Israel limelipua vyanzo vya maji safi pamoja na hifadhi za maji taka na Ofisi ya moja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu OCHA imeeleza uhaba wa maji hususan Gaza Kaskazini umezua wasiwasi mkubwa wa watu kuwa na upungufu wa maji mwilini na magonjwa yatokanayo na maji kutokana na matumizi ya maji kutoka vyanzo visivyo salama. Tayari UNRWA imeripoti kuwepo kwa wagonjwa kadhaa wenye matatizo ya kupumua, kuhara, tetekuwanga katika maeneo wanayotoa hifadhi. Taarifa hiyo ya pamoja ya mashirika hayo imerejea ombi lao kwa pande zote katika mzozo huo kuheshimu sheria za Kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu, wametoa wito mateka wote waachiliwe bila masharti, raia na miundombinu ya umma isishambuliwe, misaada zaidi ya kibinadamu ambayo ni chakula, maji, dawa iweze kuingia kwa usalama huko Gaza kwa kiwango kinachohitajika na iwafikie wenye uhitaji hasa wanawake na watoto popote walipo. Mashirika ya UN yaliyotia saini taarifa hiyo ni WHO, UN WOMEN, UNFPA, OCHA, UNRWA, UNICEF, IOM, UNHCR, UNDP, UN-HABITAT, OHCHR, mtaalamu maalumu wa UN kuhusu wakimbizi wa ndani, na WFP mashirika yasiyo ya UN ni Care International, Save the Children, Interaction, Mercy Corp na ICVA
6-11-2023 • 4 minuten, 12 seconden
06 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia Mashariki ya Kati, mapigano huko Gaza siku ya 30, "imetosha" yasema mashirika ya kimataifa, kisha anakwenda Gambia, Magharibi mwa Afrika huko kalavati limeimarisha afya. Makala ni kijana Emmanuel Cosmas Msoka akizungumza na Flora Nducha kuhusu SDGs na mashinani tunakwenda Karamoja nchini Uganda, kilimo cha kisasa kimekomboa wanawake kiuchumi na kijamii. 1. Ikiwa ni siku 30 sasa tangu kuanza kwa mzozo huko Mashariki ya Kati, kati ya Israel na Wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas walioko katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Gaza, mashirika 18 ya Kimataifa ya misaada ya kibinadamu yametoa taarifa ya pamoja hii leo yakisema ‘imetosha’ wakitaka kusitishwa mara moja mzozo huo kwasababu za kibinadamu, mzozo ambao umegharimu maisha ya zaidi ya watu 10,000. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.2. Nchini Gambia, Magharibi mwa bara la Afrika, kalavati au daraja dogo lililojengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya mitaji, UNCDF kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU)ili kuunganisha maeneo mawili, Pakaliba na Baro Kunda, limesogeza huduma ya afya karibu na wakazi wa maeneo hayo. Anold Kayanda na maelezo zaidi3. Makala: Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Emmanuel Cosmas Msoka mchechemuzi kijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kutoka nchini Tanzania ambaye mwezi Septemba mwaka huu alishiriki vikao vya ngazi ya juu vya vijana kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na hapa anaelezea kile alichoondoka nacho.4. Mashinani: Fursa ni yake Rose Lydia, Mkulima na Mwenyekiti wa kundi la wanawake wakulima akisimulia ambavyo wameweza kujimudu kimaisha kutokana na mafunzo ya ukulima waliyoyapata kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP huko Karamoja, Kaskazini Mashariki mwa Uganda.
6-11-2023 • 0
06 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia Mashariki ya Kati, mapigano huko Gaza siku ya 30, "imetosha" yasema mashirika ya kimataifa, kisha anakwenda Gambia, Magharibi mwa Afrika huko kalavati limeimarisha afya. Makala ni kijana Emmanuel Cosmas Msoka akizungumza na Flora Nducha kuhusu SDGs na mashinani tunakwenda Karamoja nchini Uganda, kilimo cha kisasa kimekomboa wanawake kiuchumi na kijamii. 1. Ikiwa ni siku 30 sasa tangu kuanza kwa mzozo huko Mashariki ya Kati, kati ya Israel na Wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas walioko katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Gaza, mashirika 18 ya Kimataifa ya misaada ya kibinadamu yametoa taarifa ya pamoja hii leo yakisema ‘imetosha’ wakitaka kusitishwa mara moja mzozo huo kwasababu za kibinadamu, mzozo ambao umegharimu maisha ya zaidi ya watu 10,000. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.2. Nchini Gambia, Magharibi mwa bara la Afrika, kalavati au daraja dogo lililojengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya mitaji, UNCDF kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU)ili kuunganisha maeneo mawili, Pakaliba na Baro Kunda, limesogeza huduma ya afya karibu na wakazi wa maeneo hayo. Anold Kayanda na maelezo zaidi3. Makala: Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Emmanuel Cosmas Msoka mchechemuzi kijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kutoka nchini Tanzania ambaye mwezi Septemba mwaka huu alishiriki vikao vya ngazi ya juu vya vijana kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na hapa anaelezea kile alichoondoka nacho.4. Mashinani: Fursa ni yake Rose Lydia, Mkulima na Mwenyekiti wa kundi la wanawake wakulima akisimulia ambavyo wameweza kujimudu kimaisha kutokana na mafunzo ya ukulima waliyoyapata kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP huko Karamoja, Kaskazini Mashariki mwa Uganda.
6-11-2023 • 12 minuten, 59 seconden
Ibara ya 12 ya UDHR inatekelezwa Tanzania?
Na sasa tuangazie Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75. Na katika mfululizo wa vipindi vyetu vya kuelimisha umma kuhusu tamko hili kwa kuelezea Ibara kwa Ibara, ninakupeleka nchini Tanzania kwa mwanasheria na wakili Emmanuel Sosthenes kutoka shirika linalotoa msaada wa sheria kwa wanawake nchini humo, WILAC, akichambua Ibara ya 12 ya tamko hilo na jinsi inavyotekelezwa kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki. Kwako Emmanuel.
3-11-2023 • 0
Wanawake na wasichana wafungwa minyororo Sudan
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) imesikitishwa sana na ripoti kwamba huko Darfur nchini Sudan wanawake na wasichana wanatekwa nyara na kushikiliwa katika mazingira ya yasiyo ya kiutu katika maeneo yanayodhibitiwa na wanamgambo waasi (RSF). Anold Kayanda na maelezo zaidi. Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Liz Throssell (Elizabeth Throssel) hii leo Ijumaa asubuhi saa za Geneva, Uswisi akizungumza na waandishi wa Habari anasema, “habari za kuaminika kutoka kwa walionusurika, mashahidi na vyanzo vingine vinaeleza kwamba zaidi ya wanawake na wasichana 20 wametekwa, lakini idadi inaweza kuwa ni kubwa zaidi ya hiyo iliyotajwa.” Bi. Throssel anaendelea kueleza kuwa vyanzo vingine vimeripoti kuwaona wanawake na wasichana wakiwa kwenye minyororo kwenye magari ya kubebea mizigo na magari madogo. Taarifa hizi za kushtua zinakuja huku kukiwa na ongezeko la visa vya unyanyasaji wa kingono nchini humo tangu mapigano yazuke kati ya Jeshi la Sudan na Vikosi hivyo vya wanamgambo wa RSF miezi sita iliyopita. Kwa mujibu wa takwimu walizonazo, Msemaji huyo wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, anasema, “takribani watu 105 wamefanyiwa ukatili wa kingono tangu mapigano hayo yalipoanza tarehe 15 Aprili 2023.” Wanawake wanatekwa, wanalazimishwa kuolewa na kushikiliwa huku watekaji wakidai kikombozi. Kufikia tarehe 2 Novemba, Ofisi ya Haki za Kibinadamu nchini humo Sudan ilikuwa imepokea ripoti za kuaminika za zaidi ya matukio 50 ya unyanyasaji wa kingono yanayohusishwa na uhasama na kuwaathiri wanawake 86, mwanamume mmoja na watoto 18. Matukio 23 kati ya hayo yalihusisha ubakaji, 26 yalikuwa ya ubakaji unaotekelezwa na watu wengi yaani genge na matatu ya kujaribu kubaka. Ofisi hiyo ya haki za binadamu imelaani vikali vitendo hivyo na kuwataka viongozi wa juu wa Jeshi la Sudan na wa Vikosi vya wanamgambo waasi wa RSF pamoja makundi mengine yenye kujihami kwa silaha ambayo yana uhusiano na pande hizi mbili kuchukua hatua za haraka kukomesha unyanyasaji wa kingono ikiwa ni pamoja na kuwaachia huru waliotekwa nyara, kuwapatia huduma ya matibabu na kisaikolojia na kuwafikisha katika mikono ya sheria wahusika wa matukio haya ya kikatili.
3-11-2023 • 0
03 NOVEMBA 2023
Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo hii leo utasikia kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR ambayo imesikitishwa sana na ripoti kwamba huko Darfur nchini Sudan wanawake na wasichana wanatekwa nyara na kushikiliwa katika mazingira ya yasiyo ya kiutu katika maeneo yanayodhibitiwa na wanamgambo waasi (RSF). Pia utapata ufafanuzi wa Ibara ya 12 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75. Makala utasikia utekelezaji wa SDGs nchini Tanzania na mashinani tutasalia kutoka kwa Wakimbizi wa DRC walioko nchini Tanzania.
3-11-2023 • 0
GLAMI Tanzania yasongesha SDG 4 na SDG 5
Harakati za kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa yanatekelezwa kwa mafanikio ifikapo ukomo wake mwaka 2030 zinaendelea katika nchi mbalimbali wanachama wa chombo hicho. Mathalani nchini Tanzania, mashirika ya kiraia yanaunga mkono hatua za serikali kufanikisha malengo hayo. Miongoni mwa mashirika hayo ni lile lisilo la kiserikali la Girls Livelihood and Mentor Initiative (GLAMI) ambalo kupitia mradi wa KISA unatekeleza kwa vitendo lengo namba 4 la Elimu Bora na namba 5 la Usawa wa Kijinsia, kwa kuwakutanisha wanafunzi wa kike 777 wa shule tatu za sekondari; Nuru, Magadini na Oshara katika Mkoa wa Kilimanjaro, kaskazini mwa nchi kutambua taaluma zao kabla ya kufikia katika elimu yao ya juu. Mwandishi wa Habari Hamad Rashid wa Redio washirika ya Mviwata FM kutoka Morogoro alihudhuria tukio hilo na kutuandalia makala hii ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la GLAMI Anande Nnko anaanza kwa kueleza umuhimu wa hii inayoitwa Siku ya Taaluma.
3-11-2023 • 0
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno “INADI”.
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “INADI”.
2-11-2023 • 0
02 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ambapo nchini Tanzania mradi wa Fish4ACP unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya na kutekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kwa kushirikiana n serikali ya Tanzania unaendelea kuleta matunda ya malengo yake ya kuanzishwa. Yaani kuongeza thamani ya mazao yanayotokana na uvuvi na kuimarisha maisha ya wavuvi na wachakataji wa mazao hayo kwa kuongeza thamani. Mradi huu unatekelezwa mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa. Pi atunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za machafuko Gaza, uhalifu unaofanyiwa waandishi wa habari na ripoti ya UNEP kuhusu Tabianchi na mazingira. Katika kujifunza Kiswahili tunakuletea ufafanuzi wa neno “INADI”. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA imeeleza kuwa mashambulizi za ardhini yanatotekelezwa kwa siku kadhaa sasa na Israel huko katika Ukanda wa Gaza yamezuia usafirishaji wa misaada kutoka Gaza Kusini kwenda Gaza Kaskazini hivyo wananchi walioko Gaza Kaskazini hawawezi kufikishiwa misaada ya kibinadamu wakati huu wakikabiliwa na mashambulizi ya anga na ardhini. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP limezindua ripoti hii leo jijini Nairobi nchini Kenya iliyoeleza maendeleo ya harakati za kuhimili mabadiliko ya tabianchi yanasuasua wakati huu ambapo yanapaswa kushika kasi ili kuendana na ongezeko la madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Na leo ni siku ya Kimataifa ya kupinga ukwepaji sheria dhidi ya vitendo vya uhalifu wanavyofanyiwa waandishi wa habari ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amenukuu shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ambalo linasema mwaka 2022 pekee, waandishi wa habari 88 waliuawa.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “INADI”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
2-11-2023 • 0
Simulizi ya Binti Armen Gakani, Mkimbizi Kalobeyei
Migogoro ya miongo na miongo nchini Jamhuri ya kidemocrasia ya Congo, DRC imefurusha watu wengi kutoka makazi yao, wengine kubaki wakimbizi wa ndani na wengnine kukimbilia nchi Jirani. Kenya ni mojawapo wa nchi ambazo zinawahifadhi wakimbizi hao na katika Kaunti ya Turkana, tunakutana na Armen Gakani, msichana mwenye umri wa miaka 23 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambaye alikimbia machafuko nchini humo na sasa yeye, akiwa na mama yake na wadogo wake wawili wenye ulemavu wanaishi katika kambi ya wakimbizi ya Kalibeyei. Je, ni kwa jinsi gani wameweza kujimudu kimaisha? Tuungane na Pamela Awuori wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ili kufahamu zaidi.
1-11-2023 • 0
01 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko Gaza na mafuriko nchini Libya. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni? Umoja wa Mataifa leo umekaribisha uamuzi wa Misri wa kukubali kupokea baadhi ya wagonjwa kutoka eneo la wapalestina la Gaza linalokaliwa na Israeli, kwa ajili ya kuwapatia matibabu, huku mashirika mengine ya Umoja huo yakiendelea kuzungumzia adha inayowakabili maelfu ya watu wa Gaza wakiwemo watoto, uhaba wa mahitaji muhimu, ukosefu wa matfta, kufurika kwa makazi ya dharura na Israeli kuendelea na operesheni ya kijeshi ardhini. Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali yanaendelea kusaidia kuwafikishia misaada watu katika maeneo ya Libya yaliyoathiriwa na mafuriko makubwa yaliyoipiga taifa hilo la Afrika Kaskazini tarehe 10 na 11 mwezi Septemba mwaka huu, hasa wakati huu msimu wa baridi Kali unapojongea. Makala leo tunaelekea Kaunti ya Turkana, nchini Kenya, ambako tunakutana msichana mwenye umri wa miaka 23 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambaye alikimbia machafuko nchini humo na sasa yeye na mama yake na wadogo zake wawili wenye ulemavu, wanaishi katika kambi ya wakimbizi ya Kalobeyei.Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania kusikiliza ujumbe kuhusu afya ya akili na haki za binadamu. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
1-11-2023 • 0
Waathirika wa mafuriko Libya wanaendelea kupokea msaada kutoka UN na wadau wake
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wake yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali yanaendelea kusaidia kuwafikishia misaada watu katika maeneo ya Libya yaliyoathiriwa na mafuriko makubwa yaliyoipiga taifa hilo la Afrika Kaskazini tarehe 10 na 11 mwezi Septemba mwaka huu, hasa wakati huu msimu wa baridi Kali unapojongea. Katika kipindi cha wiki sita tangu mafuriko yaliyosababishwa na kilichotambuliwa kuwa kimbunga kibaya zaidi barani Afrika, mashirika ya misaada ya kibinadamu yamewahudumia takribani watu 164,000 kwa misaada ya kibinadamu na shughuli za usaidizi zinaendelea kwa watu waliopoteza nyumba zao.Video iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA inaonesha mahitaji ya kipaumbele kama ukarabati wa haraka wa mitandao ya maji na maji taka, udhibiti wa taka na uondoaji salama wa uchafu yakifanyiwa kazi."Mahitaji yao makuu sasa ni kuhama kutoka kwenye makazi ya shuleni kwenda kwenye nyumba za muda au kupokea fidia ili kuanza tena maisha yao." Anasema Safina Al Mahjoud, Mwakilishi wa Shirika lisilo la kiserikali linaloitwa Kisa akiwa katika shule ya Al Um Qura huko Derna, Mashariki mwa nchi.Hali ya watu waliokusanyika katika maeneo ya pamoja baada ya kuyakimbia makazi yao bado ni tete. Takriban watu 1,750 wanaendelea kuangaliwa katika maeneo 18. Shughuli ya kuwahamisha watu hawa kwenda kwenye maeneo yenye hali nzuri itaanza ivi karibuni.Hamdi Beleid, ni mfanyakazi wa kujitolea katika Shirika la Mwezi Mwekundu la Libya, anasema, "Mimi ni mmoja wa watu walioathiriwa na janga hili. Nilipoteza wanafamilia wote. Nilipoteza nyumba yangu na chanzo cha mapato. Nilipoteza kila kitu katika maisha haya. Lakini kwa msaada wa Mungu, ninakabiliana nayo na ninaweza kuendelea na kazi yangu. Kwa sababu najua watu wanachopitia, naendelea kutoa msaada. Mungu anisaidie ili nisaidie idadi kubwa ya watu.”Kimbunga Daniel kilipoyakumba maeneo mbalimbali ya Libya, mashirika ya Umoja wa Mataifa yalitathimini kuwa takribani watu 4000 walifariki Dunia na wengine zaidi ya mara mbili ya hao hawakufahamika waliko.
1-11-2023 • 0
Wagonjwa wahamishwa Gaza kwa ajili ya matibabu Misri, UN yakaribisha
Umoja wa Mataifa leo umekaribisha uamuzi wa Misri wa kukubali kupokea baadhi ya wagonjwa kutoka Gaza kwa ajili ya matibabu, huku mashirika mengine ya Umoja huo yakiendelea kuzungumzia adha inayowakabili maelfu ya watu wa Gaza wakiwemo watoto, uhaba wa mahitaji muhimu, ukosefu wa matuta, kufurika kwa makazi ya dharura na kuendelea kwa operesheni ya ardhini ya Israel. Asante Assumpta nianze na hiyo habari njema kwa wagonjwa Gaza hususan wale walio mahtuti na waliojeruhiwa vibaya ambao sasa watakwenda kupata matibabu Misri hatua ambayo imekaribishwa na Umoja wa Mataifa akiwemo mkurugenzi mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO Dkt. Tedross pia amesema “Tumekuwa tukifanyakazi kwa karibu na wizara ya afya ya Misri kupanga uhamishaji wa wagonjwa kwa ajili ya matibabu na tutaendelea kusaidia katika hili”Kauli yake imefuatia taarifa kwamba kivuko cha Rafah baina ya Misri na Gaza kimeruhusiwa kufunguliwa leo mahsusi kwa ajili hiyo ya kuahamisha wagonjwa ikiwa ni mara ya kwanza tangu Oktoba 7, na watakaohamishwa ni wagonjwa lakini pia raia wa kigeni na wenye uraia pacha na hicho ndio kivuko pekee ambacho hakidhibitiwi na Israel.Hata hivyo pamoja na habari hiyo njema bado madhila makubwa yanawaghubika watu wa Gaza shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema kwani uhaba wa mahitaji mengine ya msingi ni mkubwa sana licha ya jana kushuhudia msafara mkubwa zaidi wa misaada wa malori 59 yakiwa na maji, chakula na dawa. Limesema changamoto kubwa zaidi hivi sasa ni mafuta kwa ajili ya kuendesha vifaa vya kuokoa maisha ambayo bado yamepigwa marufuku kuingia Gaza.Hivyo WHO na OCHA yote yamesihi kuingizwa kwa misaada zaidi Gaza ikiwemo mafuta.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limemulika changamoto ya makazi likisema hivi sasa zaidi ya watu milioni 1.4 wamekuwa wakimbizi wa ndani Gaza na wengine zaidi ya 689,000 wanapata hifadhi katika vituo 150 vywa UNRWA ambavyo vimejaa pomoni na kuhatarisha cangamoto zingine zikiwemo za kiafya.Mashirika hayo pia yameonya kuhusu kuendelea kwa operesheni ya ardhini ya jeshi la Israel Gaza ambapo jana kumekuwa na tarifa ya mashambulizi katika makazi ya Jabaliya Kaskazini mwa Gaza mji wenye kambi kubwa zaidi ya wakimbizi inayohifadhi watu 116,000.
1-11-2023 • 0
31 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunabisha hodi nchini Kenya ambako hivi karibuni kumefanyika mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa ya kukabiliana na ueneaji wa hali ya jangwa UNCCD ukishirikisha wadau wengine, kukijadili ni jinsi gani ya kuzishirikisha jamii kwanza kupunguza athari na gharama zinazoletwa na hali ya jangwa na pili kuwajengea mnepo wananchi dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi. Tuanluetea pia habari kwa ufupi zikiwemo za machafuko Gaza, afya nchini Sudan na ujumbe wa Katibu Mkuu wa kuhusu siku ya Miji Duniani. Mashinani tunakupeleka huko Port-au-Prince makao makuu ya taifa la Haiti, kulikoni? 1. Gaza imegeuka "makaburi" ya watoto, kwani maelfu wameuawa kufuatia mashambulizi yanayofanywa na Israel huku zaidi ya Watoto milioni moja wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa mahitaji muhimu na maisha yao ya baadaye yakikabiliwa na kiwewe, amesema Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu na dharura, OCHA, Martin Griffiths kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X, hii leo. 2. Dkt Ni’ma Saeed Abid ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) nchini Sudan, leo ameripoti kuwa Mfumo wa afya nchini humo umezidiwa kiasi cha kufikia hatua mbaya huku mahitaji yakiongezeka kutokana na milipuko ya magonjwa, utapiamlo, na kuongezeka kwa wagonjwa wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambao hawajatibiwa mathalani wenye kisukari, shinikizo la damu, saratani, magonjwa sugu ya kupumua na figo. Kidogo Habari njema ni kuwa WHO Sudan inajiandaa kupokea chanjo ya matone dhidi ya kipindupindu kutoka kwa ICG ambalo ni Kundi la kimataifa la kuratibu usambazaji wa chanjo nyakati za dharura linachoundwa na WHO, UNICEF na wadau wao. 3. Na ikiwa leo ni Siku ya Miji Duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa siku hii ametoa wito kwamba, ‘tunapoadhimisha Siku ya Miji Duniani, tuazimie kufanya kazi pamoja kwa ajili ya maeneo ya mijini ambayo si tu ni injini za ukuaji, bali vinara wa uendelevu, mnepo, na ustawi kwa wote. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN Habitat), Maimunah Mohd Sharif akisisitiza Kaulimbiu ya mwaka huu, Kufadhili Mstakabali wa Miji Endelevu kwa wote, amesema unahitajika mfumo mpya wa ufadhili kwa ajili ya maendeleo endelevu ya miji na kwamba pia inahitajika kuwekeza katika upangaji jumuishi na kuongeza kasi ya kuyafanya makazi na nyumba kuwa haki ya binadamu.4. Mashinani tunakupeleka huko Port-au-Prince makao makuu ya taifa la Haiti kumsikia Duvernise Altema akieleza maishi wanayoishi baada ya kulazimishwa kuyahama makazi yao kutokana na mzozo unaoendelea nchini humo. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
31-10-2023 • 0
UNICEF na Equal Access International, wabuni mbinu za kukabiliana na changamoto katika jamii
Janga la tabianchi limesababisha kupotea kwa upatikanaji wa elimu, huduma muhimu, na ajira kwa vijana nchini Kenya. Hata hivyo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Equal Access International wamewawezesha vijana kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na kutoa ufahamu kuhusu suluhisho la kukabiliana na tatizo hilo. Evarist Mapesa wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anatufafanulia zaidi katika Makala hii.
30-10-2023 • 0
Wanawake na wasichana wajawazito walioko Gaza wasimulia kinachowakumba
Wakati mzozo katika Ukanda wa Gaza ukizidi kuongezeka huku wananchi wakikabiliwa na changamoto nyingine lukuki ikiwemo uhaba wa chakula, maji, mafuta na vifaa vya matibabu vya kuokoa maisha, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu na Afya ya Uzazi UNFPA limesema mfumo wa afya nao uko ukingoni kuanguka. Shirika hilo limezungumza na wanawake wajawazito walioko Gaza kuhusu hali mbaya wanayokabiliana nayo. Thelma mwadzaya anatujuza walichosema wanawake hao. Ukanda wa Gaza makazi ya watu milioni 2.2, wanawake 50,000 ni wajawazito hivi sasa katika eneo ambalo vita inaendelea. UNFPA imesema takriban wanawake 5,500 wanatakiwa kujifungua ndani ya siku 30 zijazo na takwimu za sasa idadi ya wanawake wanaojifungua kila siku ni 160. Wakati wanawake 840 wanaweza kuwa na changamoto wakati wa kujifungua, wengi wa wanawake walioko Gaza wamekatishwa huduma za uzazi salama, kwani hospitali, ambazo zimeelemewa na majeruhi, zinakosa mafuta ya jenereta, dawa na vifaa muhimu ikiwa ni pamoja na usimamizi wa dharura za uzazi.Hizi ndio simulizi za madhila wanayokutana nao wanawake hawa ambao hatutataja majina yao. Wakwanza anatueleza hali ilivyo “Kila mara kuna bomu, naogopa, miguu yangu inapooza, siwezi kutembea, siwezi kusogea, hasa ukizingatia nina watoto na nahitajika kukimbia kwenda kuwafuata, haya ni mateso zaidi ya changamoto zinazo tukabili kwasababu ya ardhi yetu kutwaliwa. Ninaogopa, sababu ya watoto wangu na mtoto wangu aliye tumboni ambaye hajazaliwa.”Huyu wa pili, nyumba yao ililipuliwa na mabomu yanayorushwa na Israel, anasema “Natarajia kujifungua mwezi huu, ninalala mitaani kama ulivyonikuta, hali haivumiliki hapa” Na watatu, naye amepata hifadhi katika shule zinazo endeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina UNRWA.“Hii ndio sehemu pekee ambayo tumeambiwa ina usalama, niña ujauzito wa miezi saba. Hali hapa inasikitisha, unaweza kuisikia hata kwenye sauti yangu. Kifua kinaniuma, niña mafua makali na niña kohoa na hakuna maji kabisa, tunajaribu kuosha vyakula lakini maji si masafi, hata maji kitone tunayofanikiwa kuyapata si masafi. Ninachotaka ni usalama, mazingira salama ya afya, suala kubwa zaidi sasa ni kusafisha vyoo na kupata vifaa vya usafi, maji ni muhimu kwetu hali ni mbaya sana kwetu.”Tayari UNFPA imetuma dawa na vifaa vya afya ya uzazi vya kuokoa maisha nchini Misri kwa ajili ya kuhifadhi na kusafirishwa kuvuka mpaka hadi Gaza. Hadi kufikia tarehe 26 Oktoba, UNFPA ilifikisha nchini Misri vifaa 3,000 vya usafi na kujihifadhi kwa ajili ya wanawake pamoja na wajawazito.
30-10-2023 • 0
30 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu katika eneo linalokaliwa na wapaestina Gaza. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Ethiopia, kulikoni?Huku mzozo wa Israel na Palestina ukiwa katika wiki yake ya nne, wahudumu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo wameonya kuhusu shinikizo linaloongezeka kwenye hospitali za kaskazini mwa Gaza ambako wamesalia wagonjwa na wahudumu wa afya, huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa operesheni za ardhini za jeshi la Israel. Wakati mzozo katika Ukanda wa Gaza ukizidi kuongezeka huku wananchi wakikabiliwa na changamoto nyingine lukuki ikiwemo uhaba wa chakula, maji, mafuta na vifaa vya matibabu vya kuokoa maisha, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu na Afya ya Uzazi UNFPA limesema mfumo wa afya nao uko ukingoni kuanguka. Shirika hilo limezungumza na wanawake wajawazito walioko Gaza kuhusu hali mbaya wanayokabiliana nayo. Katika makala Evarist Mapesa anakupeleka nchini Kenya ambapo mabadiliko tabianchi umesababisha kupotea kwa upatikanaji wa elimu, huduma muhimu, na ajira kwa vijana nchini Kenya, Hata hivyo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini humo kwa kushirikiana na Equal Access International wanawawezesha vijana kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko tabianchi na kutoa ufahamu kuhusu suluhisho la kukabiliana na tatizo hilo.mashinani na tutaelekea nchini Ethiopia, kushuhudia jinsi gani Umoja wa Mataifa unavyasaidia watoto kuondokana na utapiamlo uliokithiri. Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
30-10-2023 • 0
Wahudumu wa misaada wa UN wanasema hospitali za Gaza zimezidiwa na ziko ukingoni mwa huduma
Huku mzozo wa Israel na Palestina ukiwa katika wiki yake ya nne, wahudumu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa leo wameonya kuhusu shinikizo linaloongezeka kwenye hospitali za kaskazini mwa Gaza ambako wamesalia wagonjwa na wahudumu wa afya, huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa operesheni za ardhini za jeshi la Israel. Asante Leah Mashirika yote ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yamesisitiza wito wa misaada zaidi na usitishwaji wa uhasama kwani hali ni mbayá sana , maji yamezidi unga.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema viunga vya hospitali za Shifa na Al Quds katika mji wa Gaza na hospitali ya Indonesia kaskazini mwa Gaza, vimeshambuliwa mwishoni mwa juma na "Hii ilifuatia wito uliotolewa upya na jeshi la Israel la kuhamisha vituo hivyo mara moja."Kupitia ukurasa wake wa X mkuu wa OCHA na mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths akiwa Mashariki ya Kati amesema “Rais wa Palestina na Israel wameteseka vya kutosha.” Griffith amesema anatarajia kukutana na timu ya OCHA kwenye eneo linalokaliwa la Palestina ambayo amesema kazi yao ni ya kishujaa.Shirika hilo linasema takriban watu 117,000 waliokimbia makazi yao wanahifadhiwa katika hospitali 10 ambazo bado zinafanya kazi katika mji wa Gaza na mahali pengine kaskazini mwa Gaza, ambazo zimepokea maagizo ya kurejewa kwa wito wa kuondoka katika siku za hivi karibuni.Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kupitia ukurasa wake a X nalo limesema "kuhamishwa kwa hospitali nzima haiwezekani bila kuhatarisha maisha ya wagonjwa".Kwa upande wake shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi duniani UNFPA limesema hali ni mbaya sana hasa kwa kina mama wanaojifungua kwani hivi sasa upasuaji wa wanawake kujifungua unafanywa bila ganzi huku kukiwa na uhaba mkubwa wa vifaa vya matibabu na nishati, na wakati mwingine madaktari wanabidi kuzalisha watoto njiti wa kina mama wanaofariki dunia.”Huu ni ushuhuda wa kutisha na kusikitisha kutoka kwa wafanyakazi wa Hospitali ya Shifa.UNRWA ambalo ni Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina, lilisema licha ya changamoto zilizopo wafanyakazi wake wa misaada huko Gaza wanaendelea kufanyakazi, wakitoa msaada kwa zaidi ya watu 600,000 ambao wamesaka hifadhi katika makaazi ya UNRWA, ambayo sasa yamefurika mara tatu zaidi ya uwezo."Wafanyakazi hao ni taswira ya ubinadamu katika wakati huu wa jinamizi kubwa” limesongeza shirika hilo.Jana Jumapili shirika hilo lilifanya ibada maalum ya kumbukumbu kwa wafanyakazi wake 59 waliouawa katika mzozo huu hadi sasa na mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres alisisitiza akitoa "shukrani, mshikamano na msaada wake kamili kwa wafanyakazi wenzake hao wanaofanya kazi kuokoa maisha huko Gaza huku wakihatarisha maisha yao.Idadi ya wanaokufa inaongezeka: Hadi kufikia jana Jumapili jioni idadi ya waliofariki dunia Gaza tangu tarehe 7 Oktoba ilifika zaidi ya watu 8,000, kulingana na takwimu za wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas huko Gaza.Kwa mujibu wa mamlaka ya Israel, Waisraeli 239 na raia wa kigeni, wakiwemo watoto 30, wamesalia mateka huko Gaza na watu 40 bado wanaripotiwa kutoweka kufuatia mashambulizi ya kigaidi ya Hamas dhidi ya Israel yaliyofanyika tarehe 7 Oktoba.OCHA imesema jana Jumapili "angalau kulikuwa na mlori 33 yaliyokuwa yamebeba maji, chakula, na vifaa vya matibabu yaliingia Gaza kupitia kivuko cha Rafah na Misri, ikiwa ni idadi kubwa zaidi yangu kuanza tena kwa msafara mdogo wa misaada tena tarehe 21 Oktoba."Wakati ongezeko hili linakaribishwa, kiasi kikubwa zaidi cha misaada kinahitajika mara kwa mara ili kuzuia kuzorota zaidi kwa hali mbaya ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe," OCHA imesisitiza. Kabla ya shambulio la Oktoba 7 la Hamas, karibu malori 500 kwa siku yaliripotiwa kuingia Gaza.Mwishoni mwa wiki huku kukiwa na onyo…
30-10-2023 • 0
Huduma za Posta zisienguliwe kwenye uwekezaji – UPU
Uwekezaji kwenye huduma za posta hasa katika nchi zinazoendelea kama zile za barani Afrika husalia nyuma kutokana na huduma hiyo kutopatiwa kipaumbele sana katikati ya changamoto kama vile afya, elimu, chakula, mabadiliko ya tabianchi. Hali hiyo husababisha huduma za posta kukosa ufadhili unaotakiwa, amesema Mutua Muthusi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika la posta duniani, UPU katika mahojiano yake na Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Bwana Muthusi anasema mizani ya huduma zinazohitajika kwa njia moja au nyingine huacha posta nyuma, licha ya kwamba huduma hiyo ilionekana umuhimu wake wakati wa janga la COVID-19. Je ni kwa vipi, na nini kifanyike kuhakikisha uwekezaji unakuwa wa kutosha na posta ichangie kwenye maendeleo endelevu zama za sasa za maendeleo ya kidijitali? Bwana Muthusi anaanza kwa kuelezea changamoto zinazokumba huduma za posta katika nchi zinazoendelea. (H4) NB: Mahojiano haya yamefanikishwa na Kayla Redstone wa UPU.
27-10-2023 • 0
UN: Pande husika sitisheni huhasama, janga kubwa zaidi la kibinadamu laja Gaza
Hali Mashariki ya Kati inazidi kuwa mbayá. Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo amezisihi pande zote katika mzozo kusitisha uhasana , huku mashirika ya misaada yakionya kuhusu janga kubwa zaidi la kibinadamu, wakati hapa Makao Makuu kikao cha 10 cha dharura kuhusu mzozo huo wa Mashariki ya Kati kikiendelea leo. Kwa hakika hali si hali kwa mujibu wa Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ambaye ameonya leo kwamba adhabu ya pamoja ni uhalifu wa vita akirejea ombi lake la pande zote katika mzozo kusikiliza wito wa amani na kusitisha mapigano hasa wakati huu idadi ya vifo ikongezeka hususan Gaza na pia kukiwa na ripoti kwamba sasa majina ya watoto yanaandikwa kwenye mikono yako ili iwe rahisi kuwatambua endapo watauawa.Turk ameitaka Hamas kuwaachilia mara moja mateka bila masharti na kwa Israel kusitisha mara moja adhabu ya pamoja kwa Wapalestina. Pia amesisitiza kwamba kauli za kukashifu Wapalestina zinapaswa kukoma mara moja. Kwa mashirika ya kibinadu leo yote yanaonya kwamba mambo yanakuwa mabaya zaidi Gaza. Mratibu wa mwasuala ya kibinada wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo linalokaliwa la Palestina Lynn Hastings akizungumza kutoka mjini Jerusalem amesema malori 74 ya msaada yaliyoruhusiwa kuingia Gaza tangu 21 Oktoba na mengine takriban 8 yanayotarajiwa leo hayatoshelezi mahitaji ukizingatia kwamba kabla ya mzozo wa sasa kulikuwa na malozi 450 yaliyokuwa yanaingia kila siku hivyo ameomba msaada zaidi uingine Gaza.Kwa upande wake Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA Philippe Lazzarini amezungumzia idadi ya wanaokufa na hofu ya kuongezeka idadi hiyo kila siku kutokana na mabomu na makombora na pia kwa athari za kuzingirwa Ukanda wa Gaza. Pia ameonya juu ya kukosekana kwa mahitaji ya msingi kama maji, dawa na chakula na amesema idadi ya wafanyakazi wa shirika hilo wanaokufa inaongezeka kufikia leo ni 53.Na mashirika mengine lile la mpango wa chakula duniani WFP limesema limefanikiwa kufikisha asilimia 2 tu ya chakula kinachohitajika huku la afya la Umoja wa Mataifa WHO likisema lita 94,000 za mafuta zinahitajika kila siku kuweza kuendeleza huduma muhimu katika hospital kubwa 12 Gaza na hapa Makao Makuu Kikao cha 10 dharura cha Baraza kuu kinaendelea na kinatarajiwa kupigia kura mswada wa azimio uliowasilishwa na Jordan kuhusu usitishaji uhasama.
27-10-2023 • 0
27 OKTOBA 2023
Hii leojaridani tunaangazia hali ya msaada wa kibinadamu katika eneo linalokaliwa na wapaestina Gaza, na wakimbizi wa Sudan. Makala tunamulika huduma za posta katika nchi zinazoendelea hususan barani Afrika hasa wakati huu wa maendeleo ya kidijitali na mashinani tunakupeleka nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani Umoja wa Mataifa umewasaidia wakulima kuimarisha uhakika wa chakula na kujikwamua kimaisha.Hali Mashariki ya Kati inazidi kuwa mbayá. Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo amezisihi pande zote katika mzozo kusitisha uhasana , huku mashirika ya misaada yakionya kuhusu janga kubwa zaidi la kibinadamu, wakati hapa Makao Makuu kikao cha 10 cha dharura kuhusu mzozo huo wa Mashariki ya Kati kikiendelea leo. Wakati maelfu ya wananchi wakikimbia machafuko nchini Sudan mashirika ya Umoja wa Mataifa nayo yana haha huku na kule kuhakikisha wanatoa usaidizi kwa wakimbizi hao. Katika makala Assumpta Massoi anazungumza na Mutua Muthusi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika la posta duniani, UPU kuhusu changamoto na fursa za huduma za posta katika nchi zinazoendelea hususan barani Afrika hasa wakati huu wa maendeleo ya kidijitali.Na mashinani tunakuletea ujumbe wa Everlyne Lagat kutoka Baringo Kaunti nchini Kenya, mmoja wa wakulima wadogo ambao wameweza kuondokana na hatari ya majanga ya njaa na umasikini kwa kuwa Shirika la Umoja Wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP linanunua chakula cha msaada kutoka kwao Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
27-10-2023 • 0
Sikuwa nataka kurejea nchini mwangu Sudan Kusini - Mkimbizi kutoka Sudan
Wakati maelfu ya wananchi wakikimbia machafuko nchini Sudan mashirika ya Umoja wa Mataifa nayo yana haha huku na kule kuhakikisha wanatoa usaidizi kwa wakimbizi hao. Tangu kuibuka kwa mzozo nchini Sudan miezi sita iliyopita, takriban watu milioni 6 wamelazimika kuyakimbia makazi yao wakisaka hifadhi katika nchi jirani zikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Misri, Ethiopia na Sudan Kusini. Kumekuwa na idadi kubwa ya wakimbizi wa Sudan Kusini ambao walikimbilia Sudan lakini sasa wamamua kurejea katika nchi yao. Mmoja ya watu hao ni Umjuma Achol Mtu mwenye umri wa miaka 26, Mwaka 2016 alikimbia ghasia za kikatili katika kijiji chake cha Bentiu, lakini mgofor unaondelea hivi sasa Sudan umemrejesha Sudan Kusini.“Sikuwa nataka kurejea nyumbani Sudan Kusini kwa sababu ya jinsi tulivyoondoka mwaka 2016. Hali ilikuwa mbaya sana, kumbukumbu bado zinarejea akilini mwangu. Nilikuwa Bentiu vita vilipozuka. Ilitubidi kutembea kilomita 14 kutoka Bentiu hadi Gambella ili kupata usalama. Baadaye tuliishi nchini Sudan.”Ukosefu wa fedha, ufikiaji duni wa watu, na miundombinu duni vinaleta changamoto kubwa kwa mashirika ya Kimataifa kutoa misaada kwa wakimbizi kama anavyoeleza Jimmy Ogwang, Afisa wa Mashinani wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Sudan Kusini.“Mvua imeanza kunyesha, sasa tuna changamoto ya barabara hasa kwa wakimbizi, wataathirika kwa sababu kutakuwa hakupitiki maana eneo hili hufurika wakati mvua inanyesha. Kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa wa watu kukaa kwa muda mrefu hapa, na watu wakikaa kwa muda mrefu basi kutakuwa na msongamano.” Timu za UNHCR, zikiwa pamoja na wadau wengine ziko katika vituo vya kuvuka mpaka nchini Sudan Kusini kufuatilia na kuwasaidia wanaowasili hasa wakimbizi wa Sudan Kusini wanaorejea.Wameanzisha vituo kwa ajili ya wasafiri ambapo wahamiaji wapya hupewa chakula, maji na malazi katika makazi ya jumuiya huku wakiwatafutia usafiri wa kuelekea maeneo yao ya nyumbani au maeneo mengine wanayopendelea. UNHCR pia inasaidia familia kuanzisha mawasiliano na jamaa zao ndani ya Sudan Kusini ili waweze kuunganishwa tena.
27-10-2023 • 0
Methali: MTEGEMEA NUNDU HAACHI KUNONA
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali MTEGEMEA NUNDU HAACHI KUNONA.
26-10-2023 • 0
26 OKTOBA 2023
Hii leojaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunabisha hodi jijini Nairobi nchini Kenya ambako wiki hii kikundi cha wanaharakati wa mazingira cha Mikoko Pamoja kutoka Pwani ya Kenya kimeibuka kidedea na kutwaa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya “mtu mahiri wa mwaka.” Pia tunakuletea habari kwa ufupi, na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali MTEGEMEA NUNDU HAACHI KUNONA.Gaza ambako kipindi cha saa 24 cha siku ya 19 ya mapigano kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas kimekuwa kibaya zaidi kwani watu 756 wameuawa Gaza wakiwemo watoto 344 na kufanya idadi ya waliouawa tangu Oktoba 7 kufikia 6,547 kwenye eneo hilo linalokaliwa la wapalestina, imesema Wizara ya Afya inayoongozwa na Hamas. Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni ,WHO lenyewe linawataka Hamas kutoa hakikisho la hali ya mateka wa kiisraeli wanaoshikiliwa na kundi hilo ikiwemo afya zao na iwapo wanapatiwa huduma za msingi. Hali ya sintofahamu ikiendelea Gaza, hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika kikao cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kufuatia ombi la nchi wanachama baada ya harakati za kusaka kupitisha maazimio Baraza la Usalama kuhusu mzozo Mashariki ya Kati kugonga mwamba. Na kwingineko, hii leo huko Tbilisi, Georgia, shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP na Mfuko wa Tabianchi duniani, GCF wametangaza mradi wa dola milioni 19 utakaotekelezwa mkoani Kigoma nchini Tanzania kwa ajili ya kurejesha mazingira na kujengea mnepo wenyeji na wakimbizi. Mradi utatekelezwa kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Tanzania.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali MTEGEMEA NUNDU HAACHI KUNONA.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
26-10-2023 • 0
UN Women: Mzozo wa Mashariki ya Kati ni jinamizi kwa wanawake na wasichana
Mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati baina ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas na Israel kwa siku 18 sasa umesababisha jinamizi kubwa kwa maelfu ya wanawake na wasichana limesema shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women.Milio ya makombora na risasi vimekuwa vikitawala Gaza, watu kwa maelfu wakipoteza maisha na wengine kulazimika kuwa wakimbizi wa ndani. Akizungumza na Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa Sarah Hendriks naibu mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women Sara Hendricks amesema miongoni mwa waathirika wakubwa ni wanawake na wasichana na ni kutoka pande zote za mzozo.Amesema hali ni mbayá "Kwa kweli huu ni wakati wa giza na mgumu sana. Ni mzozo mkubwa tofauti na wowote ambao eneo hili limewahi kushuhudia katika miongo kadhaa. Tunasikitishwa sana na athari zake kwa maisha ya wanawake na wasichana. Ni wazi kwamba wengi sana tayari wamepoteza maisha au wapendwa wao.” Sara amesema ili kuepusha madhila zaidi kwa wasichana na wanawake hawa UN Women iko msatari wa mbele kuwasaidia kwa kila hali na pia “Wito wa UN women umekuwa ni kuhakikisha ulinzi kwa wanawake na wasichan Israel na eneo linalokaliwa la Palestina na kuhakikisha vita vinasitishwa mara moja kwa sababu za kibinadamu. Kuendelea kwa machafuko haya na athari zake kutaleta hatari za kijinsia kwa wanawake kwenye Ukanda wa Gaza.”Amezitaja hatari hizo kuwa ni pamoja na idadi kubwa ya vifo, ongezeko la wajane, hofu ya ukatili wa kijinsia na kaya nyingi kuendeshwa na wanawake pekee .Sara amesema suluhu pekee ni Amani”Kinachohitajika ni usitishwaji haráka uhasama kwa minajili ya amasuala ya kinidamu, fursa ya bila vikwazo kuingiza misaada ya kibinadamu ikijumuisha mahitaji ya msingi kwa kila kaya, kwa kila maisha chakula, maji, vifaa vya nyumbani na hususani mafuta, ni muhimu kwa Maisha ya wanawake na wasichana kwenye Ukanda wa Gaza.”Amesisitiza kuwa kinachowakabili wanawake na wasicha hawa lazima kiwe kitovu cha suluhu“Ni muhimu sana kwa kipaumbele cha wanawake na wasichana wakati hali hii ikiendelea kieleweke vyema, na ndio sababu UN Women imetoa muhtasari unaotathimini haraka hali ya kijinsia katika mzozo wa sasa.”Afisa huyo wa UN Women amesema kwa muda mrefu kumekuwa na wanawake wanaharakati Gaza ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kusaidia masuala ya kibinadamu kwa wanawake wenzao lakini sasa ukurasa umepinduliwa “Mambo yamebadilika kwa wanawake ambao walikuwa wanaharakati wa kuchagiza hatua za kibinadamu kwa misingi ya kijinsia kwani sasa wamejikuta ni walengwa wa hatua hizo za kibinadamu .” Licha ya changamoto zinazoendelea kwa wanawake hao wa Mashariki ya Kati Sarah ameahidi kwamba UN women haitowapa kisogo wanawake hao “Tutaendelea kusalia hapokusikiliza sauti za wanawake na wasichana, kusikiliza mtazamo wao na kuuwasilisha kwenye jumuiya ya kimataifa ili mahitaji yao yapewe kipaumbele hata wakati suluhu ya mzozo mzima ikiwa inashughulikiwa.”
25-10-2023 • 0
UN Women: Mzozo wa Mashariki ya Kati ni jinamizi kwa wanawake na wasichana
Mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati baina ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas na Israel kwa siku 18 sasa umesababisha jinamizi kubwa kwa maelfu ya wanawake na wasichana limesema shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women.Milio ya makombora na risasi vimekuwa vikitawala Gaza, watu kwa maelfu wakipoteza maisha na wengine kulazimika kuwa wakimbizi wa ndani. Akizungumza na Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa Sarah Hendriks naibu mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women Sara Hendricks amesema miongoni mwa waathirika wakubwa ni wanawake na wasichana na ni kutoka pande zote za mzozo.Amesema hali ni mbayá "Kwa kweli huu ni wakati wa giza na mgumu sana. Ni mzozo mkubwa tofauti na wowote ambao eneo hili limewahi kushuhudia katika miongo kadhaa. Tunasikitishwa sana na athari zake kwa maisha ya wanawake na wasichana. Ni wazi kwamba wengi sana tayari wamepoteza maisha au wapendwa wao.” Sara amesema ili kuepusha madhila zaidi kwa wasichana na wanawake hawa UN Women iko msatari wa mbele kuwasaidia kwa kila hali na pia “Wito wa UN women umekuwa ni kuhakikisha ulinzi kwa wanawake na wasichan Israel na eneo linalokaliwa la Palestina na kuhakikisha vita vinasitishwa mara moja kwa sababu za kibinadamu. Kuendelea kwa machafuko haya na athari zake kutaleta hatari za kijinsia kwa wanawake kwenye Ukanda wa Gaza.”Amezitaja hatari hizo kuwa ni pamoja na idadi kubwa ya vifo, ongezeko la wajane, hofu ya ukatili wa kijinsia na kaya nyingi kuendeshwa na wanawake pekee .Sara amesema suluhu pekee ni Amani”Kinachohitajika ni usitishwaji haráka uhasama kwa minajili ya amasuala ya kinidamu, fursa ya bila vikwazo kuingiza misaada ya kibinadamu ikijumuisha mahitaji ya msingi kwa kila kaya, kwa kila maisha chakula, maji, vifaa vya nyumbani na hususani mafuta, ni muhimu kwa Maisha ya wanawake na wasichana kwenye Ukanda wa Gaza.”Amesisitiza kuwa kinachowakabili wanawake na wasicha hawa lazima kiwe kitovu cha suluhu“Ni muhimu sana kwa kipaumbele cha wanawake na wasichana wakati hali hii ikiendelea kieleweke vyema, na ndio sababu UN Women imetoa muhtasari unaotathimini haraka hali ya kijinsia katika mzozo wa sasa.”Afisa huyo wa UN Women amesema kwa muda mrefu kumekuwa na wanawake wanaharakati Gaza ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kusaidia masuala ya kibinadamu kwa wanawake wenzao lakini sasa ukurasa umepinduliwa “Mambo yamebadilika kwa wanawake ambao walikuwa wanaharakati wa kuchagiza hatua za kibinadamu kwa misingi ya kijinsia kwani sasa wamejikuta ni walengwa wa hatua hizo za kibinadamu .” Licha ya changamoto zinazoendelea kwa wanawake hao wa Mashariki ya Kati Sarah ameahidi kwamba UN women haitowapa kisogo wanawake hao “Tutaendelea kusalia hapokusikiliza sauti za wanawake na wasichana, kusikiliza mtazamo wao na kuuwasilisha kwenye jumuiya ya kimataifa ili mahitaji yao yapewe kipaumbele hata wakati suluhu ya mzozo mzima ikiwa inashughulikiwa.”
25-10-2023 • 0
Guterres: Mzozo wa Mashariki ya Kati sipendelei upande wowote
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa Habari hapa kwenye makao makuu ya Umoja huo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake na amani na usalama. Asante Assumpta, Katibu Mkuu Guterres amezungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo jambo la kwanza alilosema pindi alipofika mbele ya vyombo vya habari ni kuwa ……. Ameshtushwa na taarifa za upotoshaji za baadhi ya kauli alizozitoa hapo jana Katika mkutano wa Baraza la Usalama uliojadili kuhusu mzozo unaoendelea huko mashariki ya kati. Guterres amesema taarifa hizo za upotoshaji zinaonesha kana kwamba alikuwa akihalalisha vitendo vya kigaidi vilivyo fanywa na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas.Guterres amesema “Huu ni uongo, na ilikuwa kinyume chake. “amenukuu taarifa yake akisema…. “Nimelaani bila shaka, vitendo vya kutisha na visivyo na kifani vya Oktoba 7 vya Hamas nchini Israel. Hakuna kinachoweza kuhalalisha mauaji ya makusudi, kujeruhi na kutekwa nyara raia au kurusha roketi kuwalenga raia.”Katika tarifa yake ya jana pia amesema alizungumzia malalamiko ya WaPalestina na ananukuu alichosem…. “Lakini malalamiko ya watu wa Palestina hayawezi kuhalalisha mashambulizi ya kutisha ya Hamas na kisha niliendelea na namna nilivyoingilia mgogoro huo nikimaanisha misimamo yangu yote juu ya nyanja zote za mzozo wa Mashariki ya Kati.” Guterres amehitimisha taarifa yake hiyo fupi ya dakika moja akisema “Ninaamini nilihitajika kuweka kumbukumbu sawa, hasa kwa heshima ya waathiriwa na familia zao.”
25-10-2023 • 0
Guterres: Mzozo wa Mashariki ya Kati sipendelei upande wowote
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa Habari hapa kwenye makao makuu ya Umoja huo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake na amani na usalama. Asante Assumpta, Katibu Mkuu Guterres amezungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo jambo la kwanza alilosema pindi alipofika mbele ya vyombo vya habari ni kuwa ……. Ameshtushwa na taarifa za upotoshaji za baadhi ya kauli alizozitoa hapo jana Katika mkutano wa Baraza la Usalama uliojadili kuhusu mzozo unaoendelea huko mashariki ya kati. Guterres amesema taarifa hizo za upotoshaji zinaonesha kana kwamba alikuwa akihalalisha vitendo vya kigaidi vilivyo fanywa na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas.Guterres amesema “Huu ni uongo, na ilikuwa kinyume chake. “amenukuu taarifa yake akisema…. “Nimelaani bila shaka, vitendo vya kutisha na visivyo na kifani vya Oktoba 7 vya Hamas nchini Israel. Hakuna kinachoweza kuhalalisha mauaji ya makusudi, kujeruhi na kutekwa nyara raia au kurusha roketi kuwalenga raia.”Katika tarifa yake ya jana pia amesema alizungumzia malalamiko ya WaPalestina na ananukuu alichosem…. “Lakini malalamiko ya watu wa Palestina hayawezi kuhalalisha mashambulizi ya kutisha ya Hamas na kisha niliendelea na namna nilivyoingilia mgogoro huo nikimaanisha misimamo yangu yote juu ya nyanja zote za mzozo wa Mashariki ya Kati.” Guterres amehitimisha taarifa yake hiyo fupi ya dakika moja akisema “Ninaamini nilihitajika kuweka kumbukumbu sawa, hasa kwa heshima ya waathiriwa na familia zao.”
25-10-2023 • 0
25 OKTOBA 2023
Hii leojaridani tunaangazia machafuko mashariki ya kati, na kazi za walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa Habari hapa kwenye makao makuu ya Umoja huo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake na amani na usalama. Mwezi huu wa Oktoba ikiwa ni miaka 23 tangu kupitishwa kwa azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake katika harakati za amani na usalama ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia jinsi ujumuishaji wa wanawake walinda amani kwenye kikosi cha India kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo (MONUSCO) kumeleta matumaini kwa wanawake. Na katika makala Flora Nducha anatupeleka Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati ambako kunaendelea mzozo baina ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas na Israel na anamulika jinsi mzozo huo unavyowaathiri wanawake na wasichana.Mashinani tunamsikiliza mkazi mmoja kutoka mji wa Sange, jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akielezea ni kwa jinsi gani uwepo kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Pakistani wanaohudumu kwenye ujumbe wa umoja huo wa kulinda amani nchini humo MONUSCO ulivyosaidia kuleta amani katika eneo hilo. Akisema Absence anamaanisha kutokuweko.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
25-10-2023 • 0
25 OKTOBA 2023
Hii leojaridani tunaangazia machafuko mashariki ya kati, na kazi za walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa Habari hapa kwenye makao makuu ya Umoja huo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake na amani na usalama. Mwezi huu wa Oktoba ikiwa ni miaka 23 tangu kupitishwa kwa azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake katika harakati za amani na usalama ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia jinsi ujumuishaji wa wanawake walinda amani kwenye kikosi cha India kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo (MONUSCO) kumeleta matumaini kwa wanawake. Na katika makala Flora Nducha anatupeleka Ukanda wa Gaza huko Mashariki ya Kati ambako kunaendelea mzozo baina ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas na Israel na anamulika jinsi mzozo huo unavyowaathiri wanawake na wasichana.Mashinani tunamsikiliza mkazi mmoja kutoka mji wa Sange, jimboni Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akielezea ni kwa jinsi gani uwepo kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Pakistani wanaohudumu kwenye ujumbe wa umoja huo wa kulinda amani nchini humo MONUSCO ulivyosaidia kuleta amani katika eneo hilo. Akisema Absence anamaanisha kutokuweko.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
25-10-2023 • 0
Wanawake kwenye INDIBAT-1 waleta matumaini kwa wanawake Nchini DRC
Mwezi huu wa Oktoba ikiwa ni miaka 23 tangu kupitishwa kwa azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake katika harakati za amani na usalama ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia jinsi ujumuishaji wa wanawake walinda amani kwenye kikosi cha India kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo (MONUSCO) kumeleta matumaini kwa wanawake. Sauti hiyo ya Meja Rhandika. Yeye ni Kiongozi la kikosi cha wanawake ndani ya INDIBAT-1 [INDIBAT WAN] ambacho ni kikosi cha India ndani ya MONUSCO kinachohudumu eneo la Rwindi huko Rutshuru jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC. Anasema kupelekwa kufanya kazi kwenye eneo jipya mara nyingi kuna changamoto. Lakini pindi unaposhirikiana na wenyeji inakuwa ni rahisi. Kupitia video ya MONUSCO, Meja Virendra Rathore Mkuu wa INDIBAT-1 anasema walipofika Rwindi baada ya muda, ilibainika kuwa baadhi ya masuala kadhaa ya jamii zilizoathiriwa na mapigano yanayoendelea kwenye eneo hilo, hususan wanawake yalikuwa hayajashughulikiwa. Uwepo wa kikundi cha walinda amani wanawake ndani kikosi hicho ukawa ni jawabu, kama asemavyo Meja Rhandika Kamanda wa kikosi cha wanawake INDIBAT-1. “Katika siku chache zilizopita, timu yangu imekutana na wanajamii hususan viongozi wa wanawake kujadili masuala hasa hofu kuhusu usalama na tumeimarisha juhudi zetu kuwapatia hakikisho la usalama kwa wanawake. Tumefanya doria kadhaa kwenye eneo kudhihirisha uwepo wa wanawake walinda amani na ilionekana kwamba wanawake waliweze kujieleza dhahiri kuhusu matatizo yao. “ Mmoja wa wanawake viongozi kwenye eneo la Kibirizi hapa Rutshuru akaelezea furaha yake. “Sasa mimi nafurahi kuona mama msimamizi wa MONUSCO ambaye tutakuwa tunampatia malalamiko yetu hapa. Na tunakuwa na matumaini kwamba kadri tutaendelea kuhusiana naye tunaweza kupata majawabu ya shida zinazotukabili. Tunashukuru.” Na ndipo Meja Rhandika anatamatisha kwa kusema ,"Watu wa DRC wametukaribisha vema, na kuelezea shukrani yao kwa MONUSCO kwa kuleta walinda amani wanawake kwenye eneo hili. "Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hususan jimboni Kivu Kaskazini yamefurusha watu 410,000 tangu mwanzo wa mwaka huu wa 2023.
25-10-2023 • 0
Wanawake kwenye INDIBAT-1 waleta matumaini kwa wanawake Nchini DRC
Mwezi huu wa Oktoba ikiwa ni miaka 23 tangu kupitishwa kwa azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake katika harakati za amani na usalama ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia jinsi ujumuishaji wa wanawake walinda amani kwenye kikosi cha India kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo (MONUSCO) kumeleta matumaini kwa wanawake. Sauti hiyo ya Meja Rhandika. Yeye ni Kiongozi la kikosi cha wanawake ndani ya INDIBAT-1 [INDIBAT WAN] ambacho ni kikosi cha India ndani ya MONUSCO kinachohudumu eneo la Rwindi huko Rutshuru jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC. Anasema kupelekwa kufanya kazi kwenye eneo jipya mara nyingi kuna changamoto. Lakini pindi unaposhirikiana na wenyeji inakuwa ni rahisi. Kupitia video ya MONUSCO, Meja Virendra Rathore Mkuu wa INDIBAT-1 anasema walipofika Rwindi baada ya muda, ilibainika kuwa baadhi ya masuala kadhaa ya jamii zilizoathiriwa na mapigano yanayoendelea kwenye eneo hilo, hususan wanawake yalikuwa hayajashughulikiwa. Uwepo wa kikundi cha walinda amani wanawake ndani kikosi hicho ukawa ni jawabu, kama asemavyo Meja Rhandika Kamanda wa kikosi cha wanawake INDIBAT-1. “Katika siku chache zilizopita, timu yangu imekutana na wanajamii hususan viongozi wa wanawake kujadili masuala hasa hofu kuhusu usalama na tumeimarisha juhudi zetu kuwapatia hakikisho la usalama kwa wanawake. Tumefanya doria kadhaa kwenye eneo kudhihirisha uwepo wa wanawake walinda amani na ilionekana kwamba wanawake waliweze kujieleza dhahiri kuhusu matatizo yao. “ Mmoja wa wanawake viongozi kwenye eneo la Kibirizi hapa Rutshuru akaelezea furaha yake. “Sasa mimi nafurahi kuona mama msimamizi wa MONUSCO ambaye tutakuwa tunampatia malalamiko yetu hapa. Na tunakuwa na matumaini kwamba kadri tutaendelea kuhusiana naye tunaweza kupata majawabu ya shida zinazotukabili. Tunashukuru.” Na ndipo Meja Rhandika anatamatisha kwa kusema ,"Watu wa DRC wametukaribisha vema, na kuelezea shukrani yao kwa MONUSCO kwa kuleta walinda amani wanawake kwenye eneo hili. "Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hususan jimboni Kivu Kaskazini yamefurusha watu 410,000 tangu mwanzo wa mwaka huu wa 2023.
25-10-2023 • 0
24 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo ni siku ya Umoja wa Mataifa, chombo kilichoanzishwa mwaka 1945 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia ikiwa na wanachama waanzilishi 51, bara la Afrika likiwa na nchi nne tu ambazo ni Misri, Liberia, Ethiopia na Afrika Kusini enzi hizo ikijulikana kama Muungano wa Afrika Kusini. Kwa mujibu wa Chata iliyoanzisha chombo hicho, lengo ni kuendeleza amani na usalama duniani, kusongesha uhusiano wa kirafiki baina ya nchi, kufanikisha ushirikiano wa kimataifa na kuwa kitovu cha kuratibu vitendo vya mataifa. Dkt. Kaanaeli Kaale, Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT nchini Tanzania, na pia Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimataifa anaeleza iwapo malengo ya kuanzishwa bado yana mantiki. Pia tunakuletea habari kwa ufupi, na mashinani ambapo tunasikiliza ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya UN.Ni siku ya 17 ya kuendelea mzozo wa karibuni baina ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas huko Mashariki ya Kati Masharikika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na kilio cha kuongeza misaada zaidi kuingia Gaza kwani iliyowasili hadi sasa haikidhi mahitaji.Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa inaadhimishwa kumbukumbu ya kuanza kutumika kwa chata iliyoanzisha Umoja huo mwaka 1945. Katika ujumbe wake wa siku hii Clementine Nkweta-Salami naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan na kaimu mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu amesema “Mwaka huu tunaadhimisha siku hii wakati Sudan ikikabiliwa na moja ya mgogoro wa kibinadamu unaokuwa kwa kasi ukiambatana na mahitaji makubwa. Mapigano yamegeuza mgogoro huo kuwa janga kubwa. Zaidi ya watu milioni 5.6 wamefurushwa makwao, milioni 25 wanahitaji msaada, zaidi ya wanawake na wasichana milioni 4.2 wako katika hatari ya ukajtili wa kijinsia na mtoto 1 kati ya 3 hana fursa ya kwenda shule. Na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema theluthi mbili ya watoto wakimbizi nchini Armenia wameandikiswa katika mifumo ya kitaifa ya shule mwezi mmoja baada ya watoto 21, 000 wenye umri wa kwenda shule kukimbia makwao. UNICEF imesema sasa juhudi ni kuhakikisha watoto walioasalia 1 kati ya 3 ambao hawahudhurii shule wanapata fursa hiyo.Na katika mashinani tunasalia katika siku ya Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa chombo hicho anazungumzia nafasi ya kila mtu katika kusongesha malengo ya Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
24-10-2023 • 0
24 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo ni siku ya Umoja wa Mataifa, chombo kilichoanzishwa mwaka 1945 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia ikiwa na wanachama waanzilishi 51, bara la Afrika likiwa na nchi nne tu ambazo ni Misri, Liberia, Ethiopia na Afrika Kusini enzi hizo ikijulikana kama Muungano wa Afrika Kusini. Kwa mujibu wa Chata iliyoanzisha chombo hicho, lengo ni kuendeleza amani na usalama duniani, kusongesha uhusiano wa kirafiki baina ya nchi, kufanikisha ushirikiano wa kimataifa na kuwa kitovu cha kuratibu vitendo vya mataifa. Dkt. Kaanaeli Kaale, Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT nchini Tanzania, na pia Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimataifa anaeleza iwapo malengo ya kuanzishwa bado yana mantiki. Pia tunakuletea habari kwa ufupi, na mashinani ambapo tunasikiliza ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya UN.Ni siku ya 17 ya kuendelea mzozo wa karibuni baina ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas huko Mashariki ya Kati Masharikika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na kilio cha kuongeza misaada zaidi kuingia Gaza kwani iliyowasili hadi sasa haikidhi mahitaji.Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa inaadhimishwa kumbukumbu ya kuanza kutumika kwa chata iliyoanzisha Umoja huo mwaka 1945. Katika ujumbe wake wa siku hii Clementine Nkweta-Salami naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan na kaimu mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu amesema “Mwaka huu tunaadhimisha siku hii wakati Sudan ikikabiliwa na moja ya mgogoro wa kibinadamu unaokuwa kwa kasi ukiambatana na mahitaji makubwa. Mapigano yamegeuza mgogoro huo kuwa janga kubwa. Zaidi ya watu milioni 5.6 wamefurushwa makwao, milioni 25 wanahitaji msaada, zaidi ya wanawake na wasichana milioni 4.2 wako katika hatari ya ukajtili wa kijinsia na mtoto 1 kati ya 3 hana fursa ya kwenda shule. Na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema theluthi mbili ya watoto wakimbizi nchini Armenia wameandikiswa katika mifumo ya kitaifa ya shule mwezi mmoja baada ya watoto 21, 000 wenye umri wa kwenda shule kukimbia makwao. UNICEF imesema sasa juhudi ni kuhakikisha watoto walioasalia 1 kati ya 3 ambao hawahudhurii shule wanapata fursa hiyo.Na katika mashinani tunasalia katika siku ya Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa chombo hicho anazungumzia nafasi ya kila mtu katika kusongesha malengo ya Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
24-10-2023 • 0
Mshtakiwa ana haki ya kuhesabiwa kuwa hana hatia hadi athibitishwe kuwa na hatia – Ibara 11
“Kila mtu aliyehukumiwa kwa kosa la adhabu ana haki ya kuhesabiwa kuwa hana hatia hadi athibitishwe kuwa ana hatia kwa mujibu wa sheria katika kesi ya hadhara ambapo amekuwa na dhamana zote zinazohitajika kwa ajili ya utetezi wake, na Hakuna mtu atakayepatikana na hatia ya kosa lolote la adhabu kwa sababu ya kitendo au kutotenda jambo ambalo halikuwa ni kosa la adhabu, chini ya sheria ya kitaifa au kimataifa, wakati lilipotendwa, wala haitatolewa adhabu kubwa kuliko ile ambayo ilitumika wakati kosa la adhabu lilipotendwa.” Linasema tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75, na Je Ibara hii ina maanisha nini ? na inatekelezwa? Ili kupata majibu hayo Pamela Awuori wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Wakili Fridah Jausiku wa mahakama kuu ya Kenya anayeanza kwa kufafanua haki za mshtakiwa nchini humo....
23-10-2023 • 0
Mshtakiwa ana haki ya kuhesabiwa kuwa hana hatia hadi athibitishwe kuwa na hatia – Ibara 11
“Kila mtu aliyehukumiwa kwa kosa la adhabu ana haki ya kuhesabiwa kuwa hana hatia hadi athibitishwe kuwa ana hatia kwa mujibu wa sheria katika kesi ya hadhara ambapo amekuwa na dhamana zote zinazohitajika kwa ajili ya utetezi wake, na Hakuna mtu atakayepatikana na hatia ya kosa lolote la adhabu kwa sababu ya kitendo au kutotenda jambo ambalo halikuwa ni kosa la adhabu, chini ya sheria ya kitaifa au kimataifa, wakati lilipotendwa, wala haitatolewa adhabu kubwa kuliko ile ambayo ilitumika wakati kosa la adhabu lilipotendwa.” Linasema tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75, na Je Ibara hii ina maanisha nini ? na inatekelezwa? Ili kupata majibu hayo Pamela Awuori wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Wakili Fridah Jausiku wa mahakama kuu ya Kenya anayeanza kwa kufafanua haki za mshtakiwa nchini humo....
23-10-2023 • 0
23 OKTOBA 2023
Hii leojaridani tunaangazia machafuko mashariki ya kati na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan. Makala tuanakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wamesihi wanasheria wanaoishauri serikali ya Israeli inayoendelea na mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa kipalestina Hamas huko Ukanda wa Gaza, wakatae kuidhinisha kisheria vitendo ambavyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita. Kulikoni?Nchi ya Afghanistan hivi karibuni imekumbwa na matetemeko makubwa ya ardhi na kusababisha watu kupoteza maisha pamoja na uharibifu mkubwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP linasema hadi kufikia Oktoba 14, zaidi ya watu 19,250 waliathirika na matetemeko katika jimbo la Herat. Makala tunaendelea na mwendelezo wa chambuzi wa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75, leo tunabisha hodi nchini Kenya ambapo Pamela Awuori wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Fridah Jausiku, Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya, kufafanua Ibara ya 11 ya tamko hilo inayotaka kila mtu aliyehukumiwa kwa kosa la adhabu kupatiwa haki yake ya kuhesabiwa kuwa hana hatia hadi athibitishwe kuwa na hatia.Na katika mashinani tutaelekea nchini Tanzania kufuatilia ni kwa vipi huduma za afya kwa wote zinahakikishwa husuani za magonjwa yasiyoambukizwa.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
23-10-2023 • 0
23 OKTOBA 2023
Hii leojaridani tunaangazia machafuko mashariki ya kati na tetemeko la ardhi nchini Afghanistan. Makala tuanakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wamesihi wanasheria wanaoishauri serikali ya Israeli inayoendelea na mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa kipalestina Hamas huko Ukanda wa Gaza, wakatae kuidhinisha kisheria vitendo ambavyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita. Kulikoni?Nchi ya Afghanistan hivi karibuni imekumbwa na matetemeko makubwa ya ardhi na kusababisha watu kupoteza maisha pamoja na uharibifu mkubwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP linasema hadi kufikia Oktoba 14, zaidi ya watu 19,250 waliathirika na matetemeko katika jimbo la Herat. Makala tunaendelea na mwendelezo wa chambuzi wa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75, leo tunabisha hodi nchini Kenya ambapo Pamela Awuori wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Fridah Jausiku, Wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya, kufafanua Ibara ya 11 ya tamko hilo inayotaka kila mtu aliyehukumiwa kwa kosa la adhabu kupatiwa haki yake ya kuhesabiwa kuwa hana hatia hadi athibitishwe kuwa na hatia.Na katika mashinani tutaelekea nchini Tanzania kufuatilia ni kwa vipi huduma za afya kwa wote zinahakikishwa husuani za magonjwa yasiyoambukizwa.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
23-10-2023 • 0
UNDP inahaha kuwasaidia waathirika wa matetemeko ya ardhi Afghanistan
Nchi ya Afghanistan hivi karibuni imekumbwa na matetemeko makubwa ya ardhi na kusababisha watu kupoteza maisha pamoja na uharibifu mkubwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP linasema hadi kufikia Oktoba 14, zaidi ya watu 19,250 waliathirika na matetemeko katika jimbo la Herat. Video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP inaanza kwa kuonesha taswira kutoka angani ambapo ni eneo kubwa la wazi likionekana kama makazi ya watu, lakini video hiyo ikiendelea, taswira inabadilika ardhini si nyumba tena bali vifusi kimejirundika pamoja na maghofu. Haya ni madhara ya matetemeko ya ardhi kadhaa katika jimbo hili la Herat ambapo takribani watu 20,000 wameathirika, asilimia 90 kati yao wakiwa ni wanawake na watoto. Manusura wanajaribu kuokoteza chochote kile kinachoweza kupatikana baada ya tetemeko, wengine wakiokote sinia, wengine spika na wengine wakiondoka na vifurushi kwenye viroba kwani ndivyo walivyoweza kupata. Kamera inamuonesha bibi huyu aitwaye Reza Gul akiangalia mabaki ya iliyokuwa nyumba yake, machozi yakimtoka, anasimulia hali ilivyokuwa, “Ilikuwa saa 11 alfajiri. Sote tulikuwa tumeketi pamoja tunakunywa chai. Nilitoka nje ya nyumba ili kuangalia kondoo. Ghafla, nikasikia mngurumo wa sauti na nikaanguka chini. Mkwe wangu mmoja alikimbia nje wakati paa likiporomoka. Mkwe wangu mwingine na watu wengine wote wa familia yangu walikuwa bado ndani”.Mwingine ni Bi. Mahzada, akiwa anapanga baadhi ya vitu vyake nje ya iliyokuwa nyumba yake sasa ni kifusi, anasema, “Hakuna kitu ndugu, tuko gizani, hakuna kitu. Hatuna taa, hatuna nyumba, hatuna maisha, tumekuwa watu wa kutanga-tanga. Tuko hai lakini tuko gizani, hatuna taa, hatuna nishati ya umeme wa jua na tunaishi gizani.”Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Afghanistan Stephen Rodrigues akiwa ameambatana na maafisa wengine wametembelea jimboni Herat na kuzungumza na wananchi walioathirika. “Tumewaona wanawake na watoto wengi wakiishi kwenye mahema, na hiyo ndiyo hali ya kijiji hiki hivi sasa, na vijiji vingine vingi kama hivi katika eneo lote la Herat. Watu wanauhitaji sana wa makazi kwani msimu wa baridi unakuja”.UNDP imetangaza kutenga dola milioni 1.5 kama hatua ya awali ya kusaidia juhudi za haraka za misaada na mipango ya kuokoa maisha. Pamoja na mambo mengine fedha hizo zitasaidia katika ujenzi wa nyumba mpya na nishati mbadala kwa jamii zilizoathiriwa na matetemeko ya ardhi.
23-10-2023 • 0
UNDP inahaha kuwasaidia waathirika wa matetemeko ya ardhi Afghanistan
Nchi ya Afghanistan hivi karibuni imekumbwa na matetemeko makubwa ya ardhi na kusababisha watu kupoteza maisha pamoja na uharibifu mkubwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP linasema hadi kufikia Oktoba 14, zaidi ya watu 19,250 waliathirika na matetemeko katika jimbo la Herat. Video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP inaanza kwa kuonesha taswira kutoka angani ambapo ni eneo kubwa la wazi likionekana kama makazi ya watu, lakini video hiyo ikiendelea, taswira inabadilika ardhini si nyumba tena bali vifusi kimejirundika pamoja na maghofu. Haya ni madhara ya matetemeko ya ardhi kadhaa katika jimbo hili la Herat ambapo takribani watu 20,000 wameathirika, asilimia 90 kati yao wakiwa ni wanawake na watoto. Manusura wanajaribu kuokoteza chochote kile kinachoweza kupatikana baada ya tetemeko, wengine wakiokote sinia, wengine spika na wengine wakiondoka na vifurushi kwenye viroba kwani ndivyo walivyoweza kupata. Kamera inamuonesha bibi huyu aitwaye Reza Gul akiangalia mabaki ya iliyokuwa nyumba yake, machozi yakimtoka, anasimulia hali ilivyokuwa, “Ilikuwa saa 11 alfajiri. Sote tulikuwa tumeketi pamoja tunakunywa chai. Nilitoka nje ya nyumba ili kuangalia kondoo. Ghafla, nikasikia mngurumo wa sauti na nikaanguka chini. Mkwe wangu mmoja alikimbia nje wakati paa likiporomoka. Mkwe wangu mwingine na watu wengine wote wa familia yangu walikuwa bado ndani”.Mwingine ni Bi. Mahzada, akiwa anapanga baadhi ya vitu vyake nje ya iliyokuwa nyumba yake sasa ni kifusi, anasema, “Hakuna kitu ndugu, tuko gizani, hakuna kitu. Hatuna taa, hatuna nyumba, hatuna maisha, tumekuwa watu wa kutanga-tanga. Tuko hai lakini tuko gizani, hatuna taa, hatuna nishati ya umeme wa jua na tunaishi gizani.”Mwakilishi mkazi wa UNDP nchini Afghanistan Stephen Rodrigues akiwa ameambatana na maafisa wengine wametembelea jimboni Herat na kuzungumza na wananchi walioathirika. “Tumewaona wanawake na watoto wengi wakiishi kwenye mahema, na hiyo ndiyo hali ya kijiji hiki hivi sasa, na vijiji vingine vingi kama hivi katika eneo lote la Herat. Watu wanauhitaji sana wa makazi kwani msimu wa baridi unakuja”.UNDP imetangaza kutenga dola milioni 1.5 kama hatua ya awali ya kusaidia juhudi za haraka za misaada na mipango ya kuokoa maisha. Pamoja na mambo mengine fedha hizo zitasaidia katika ujenzi wa nyumba mpya na nishati mbadala kwa jamii zilizoathiriwa na matetemeko ya ardhi.
23-10-2023 • 0
UN: Wanasheria mnaoshauri Israeli muwe makini na ushauri wenu
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wamesihi wanasheria wanaoishauri serikali ya Israeli inayoendelea na mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa kipalestina Hamas huko Ukanda wa Gaza, wakatae kuidhinisha kisheria vitendo ambavyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita. Msingi wa kauli ya wataalamu hao ni kwamba tangu tarehe 7 mwezi huu wa Oktoba wanamgambo wa Hamas waliposhambulia Israeli, jeshi la ulinzi la Israeli, IDF limekuwa likiripotiwa kuwa linajipanga kuanza uvamizi wa ardhini baada ya kutekeleza mashambulizi ya angani huko Kaskazini mwa Gaza yaliyosababisha vifo vya wapalestina zaidi ya 3,400 na majeruhi 12,000 wakiwemo watoto. Uvamizi huo wa ardhini inaelezwa ni kulipiza kisasi cha mashambulizi yaliyofanywa na Hamas na wanamgambo wengine wa kipalestina nchini Israeli na kuua raia, halikadhalika kuteka na kushikilia wengine mateka hadi leo hii. Wataalamu hao kupitia taarifa yao waliyoitoa hii leo mjini Geneva, Uswisi wanasema bila shaka vitendo vya Hamas dhidi ya raia wa Israeli vilikuwa mauaji. Lakini sasa mashambulizi ya Israeli yamekuwa yakielekezwa kwenye maeneo yenye makazi ya watu wengi, yakiharibu makazi, hospitali, masoko huku ikizidi kuweka vizuizi na kuzingira Gaza, imekata usambazaji wa vyakula, maji, umeme na mafuta. Sasa wataalamu wanasema kadri ambavyo Israeli inajibu kitendo cha Hamas na kuendesha operesheni zake Gaza, wanasheria wote wanaoshauri kijeshi serikali ya Israeli lazima wabainishe na wasake ushauri ambao utaepusha vitendo ambavyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita. Wamesema wanasheria wana wajibu kwa mujibu wa kazi yao kukataa kuidhinisha kisheria vitendo vya kihalifu, vitendo ambavyo vitakiuka sheria ya kimataifa. Ifahamike kuwa sheria ya kimataifa pamoja na mambo mengine inataka pande kinzani kulinda raia kwenye mapigano na kuepuka kushambulia miundombinu ya kiraia kama vile mifumo ya maji, hospitali na shule.
23-10-2023 • 0
UN: Wanasheria mnaoshauri Israeli muwe makini na ushauri wenu
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu wamesihi wanasheria wanaoishauri serikali ya Israeli inayoendelea na mashambulizi dhidi ya wanamgambo wa kipalestina Hamas huko Ukanda wa Gaza, wakatae kuidhinisha kisheria vitendo ambavyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita. Msingi wa kauli ya wataalamu hao ni kwamba tangu tarehe 7 mwezi huu wa Oktoba wanamgambo wa Hamas waliposhambulia Israeli, jeshi la ulinzi la Israeli, IDF limekuwa likiripotiwa kuwa linajipanga kuanza uvamizi wa ardhini baada ya kutekeleza mashambulizi ya angani huko Kaskazini mwa Gaza yaliyosababisha vifo vya wapalestina zaidi ya 3,400 na majeruhi 12,000 wakiwemo watoto. Uvamizi huo wa ardhini inaelezwa ni kulipiza kisasi cha mashambulizi yaliyofanywa na Hamas na wanamgambo wengine wa kipalestina nchini Israeli na kuua raia, halikadhalika kuteka na kushikilia wengine mateka hadi leo hii. Wataalamu hao kupitia taarifa yao waliyoitoa hii leo mjini Geneva, Uswisi wanasema bila shaka vitendo vya Hamas dhidi ya raia wa Israeli vilikuwa mauaji. Lakini sasa mashambulizi ya Israeli yamekuwa yakielekezwa kwenye maeneo yenye makazi ya watu wengi, yakiharibu makazi, hospitali, masoko huku ikizidi kuweka vizuizi na kuzingira Gaza, imekata usambazaji wa vyakula, maji, umeme na mafuta. Sasa wataalamu wanasema kadri ambavyo Israeli inajibu kitendo cha Hamas na kuendesha operesheni zake Gaza, wanasheria wote wanaoshauri kijeshi serikali ya Israeli lazima wabainishe na wasake ushauri ambao utaepusha vitendo ambavyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita. Wamesema wanasheria wana wajibu kwa mujibu wa kazi yao kukataa kuidhinisha kisheria vitendo vya kihalifu, vitendo ambavyo vitakiuka sheria ya kimataifa. Ifahamike kuwa sheria ya kimataifa pamoja na mambo mengine inataka pande kinzani kulinda raia kwenye mapigano na kuepuka kushambulia miundombinu ya kiraia kama vile mifumo ya maji, hospitali na shule.
23-10-2023 • 0
Makala: Je akili mnemba AI ni faida au athari katika sekta ya filamu?
Hii leo makala inamulika Akili Mnemba au AI ambayo imebadili fani mbali mbali ikiwemo ya sanaa. Ni kwa kutambua umuhimu wa suala hili shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limeandaa mjadala maalum kuhusu akili mnemba kwenye sekta ya filamu unaoendelea huko Paris Ufaransa. Ajenda inajikita ni manufaa na changamoto kwa sekta ya sanaa ukizingatia maadili na ubunifu. Yvonne Muinde mchanganya picha za filamu ni msanii aliyebobea kwenye sekta ya ubunifu na dijitali na mshiriki wa mjadala huo wa UNESCO ulioanza jana. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya alimtembelea ofisini kwake mjini Nairobi na kuandaa makala hii.
20-10-2023 • 0
Makala: Je akili mnemba AI ni faida au athari katika sekta ya filamu?
Hii leo makala inamulika Akili Mnemba au AI ambayo imebadili fani mbali mbali ikiwemo ya sanaa. Ni kwa kutambua umuhimu wa suala hili shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limeandaa mjadala maalum kuhusu akili mnemba kwenye sekta ya filamu unaoendelea huko Paris Ufaransa. Ajenda inajikita ni manufaa na changamoto kwa sekta ya sanaa ukizingatia maadili na ubunifu. Yvonne Muinde mchanganya picha za filamu ni msanii aliyebobea kwenye sekta ya ubunifu na dijitali na mshiriki wa mjadala huo wa UNESCO ulioanza jana. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya alimtembelea ofisini kwake mjini Nairobi na kuandaa makala hii.
20-10-2023 • 0
Mazungumzo yanaendelea kupata ufafanuzi wa vikwazo na vizuizi kabla ya misaada kuingia Gaza
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko nchini Misri leo ametembelea mpaka wa Rafah, kivuko pekee cha kuingia na kutoka Ukanda wa Gaza, ambako hivi sasa kuna mashambulizi yanaendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na kusema hivi sasa wanaendelea na mazungumzo kupata ufafanuzi wa vikwazo na vizuizi vya masharti yaliyowekwa na Israel kabla ya kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Ukanda wa Gaza. Ni vigumu uwepo hapa na usivunjike moyo, ndivyo Katibu Mkuu Guterres alivyowaeleza wanahabari walioko mji wa mpakani wa Rafah ambako msururu wa malori ya misaada ya kibinadamu unasubiri kuingia Gaza ambako takriban watu milioni 2 wanasubiri kwa udi na uvumba Msaada huo kwani hawana maji, chakula, dawa wala umeme huku wakiendelea kukabiliwa na mashambulizi kwa takriban wiki mbili sasa.Ingawa Marekani, Israel na Misri zote zimeeleza kuwa mpaka huo utafunguliwa lakini hilo bado halijatendeka na Guterres anasema.“Matangazo haya yalitolewa kwa masharti na vikwazo vingine. Na kwa hivyo sasa tupo tukishirikisha wahusika wa pande zote kikikamilifu, tunashirikiana kikamilifu na Misri, na Israel, na Marekani ili kuhakikisha tunaweza kufafanua masharti hayo, na tunaweza kupunguza vizuizi hivyo ili malori haya yaweze kuelekea kwa haraka iwezekanavyo mahali yanapohitajika.”Guterres amesema kinachohitaji si tu misaada hiyo iweze kufika haraka lakini pia zoezi hilo liwe endelevu kwani mzozo unaoendelea Gaza si wa kawaida.“Kwa bahati mbaya, hii sio operesheni ya kawaida ya kibinadamu. Ni operesheni katika eneo la vita na ndiyo sababu nimetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano ya kibinadamu, sio kwamba ninaona kuwa usitishaji mapigano wa kibinadamu ni sharti la utoaji wa misaada ya kibinadamu lakini hatutaki kuwaadhibu watu wa Gaza mara mbili. Kwanza kwa sababu ya vita na pili kwa sababu ya ukosefu wa misaada ya kibinadamu. Lakini ni wazi kwamba usitishaji mapigano wa kibinadamu utafanya mambo kuwa rahisi zaidi na salama zaidi kwa kila mtu.”Pamoja na kuishukuru nchi ya Misri na shirika la kimataifa la hilal nyekundu kwa kuendelea kushughulikia suala hili kwa karibu, Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amehitimisha mkutano wake na wanahabari kwa kusema anatumai ipo siku Israel na Palestina wataishi kwa amani.“Natumai kwamba kutakuwa na mustakabali na matumaini kwamba siku moja kutakuwa na amani na suluhisho la Serikali mbili, huku Wapalestina na Waisraeli wakiishi kwa amani katika Mataifa mawili, upande mmoja hadi mwingine.”
20-10-2023 • 0
Mazungumzo yanaendelea kupata ufafanuzi wa vikwazo na vizuizi kabla ya misaada kuingia Gaza
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko nchini Misri leo ametembelea mpaka wa Rafah, kivuko pekee cha kuingia na kutoka Ukanda wa Gaza, ambako hivi sasa kuna mashambulizi yanaendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na kusema hivi sasa wanaendelea na mazungumzo kupata ufafanuzi wa vikwazo na vizuizi vya masharti yaliyowekwa na Israel kabla ya kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Ukanda wa Gaza. Ni vigumu uwepo hapa na usivunjike moyo, ndivyo Katibu Mkuu Guterres alivyowaeleza wanahabari walioko mji wa mpakani wa Rafah ambako msururu wa malori ya misaada ya kibinadamu unasubiri kuingia Gaza ambako takriban watu milioni 2 wanasubiri kwa udi na uvumba Msaada huo kwani hawana maji, chakula, dawa wala umeme huku wakiendelea kukabiliwa na mashambulizi kwa takriban wiki mbili sasa.Ingawa Marekani, Israel na Misri zote zimeeleza kuwa mpaka huo utafunguliwa lakini hilo bado halijatendeka na Guterres anasema.“Matangazo haya yalitolewa kwa masharti na vikwazo vingine. Na kwa hivyo sasa tupo tukishirikisha wahusika wa pande zote kikikamilifu, tunashirikiana kikamilifu na Misri, na Israel, na Marekani ili kuhakikisha tunaweza kufafanua masharti hayo, na tunaweza kupunguza vizuizi hivyo ili malori haya yaweze kuelekea kwa haraka iwezekanavyo mahali yanapohitajika.”Guterres amesema kinachohitaji si tu misaada hiyo iweze kufika haraka lakini pia zoezi hilo liwe endelevu kwani mzozo unaoendelea Gaza si wa kawaida.“Kwa bahati mbaya, hii sio operesheni ya kawaida ya kibinadamu. Ni operesheni katika eneo la vita na ndiyo sababu nimetoa wito wa kusitishwa kwa mapigano ya kibinadamu, sio kwamba ninaona kuwa usitishaji mapigano wa kibinadamu ni sharti la utoaji wa misaada ya kibinadamu lakini hatutaki kuwaadhibu watu wa Gaza mara mbili. Kwanza kwa sababu ya vita na pili kwa sababu ya ukosefu wa misaada ya kibinadamu. Lakini ni wazi kwamba usitishaji mapigano wa kibinadamu utafanya mambo kuwa rahisi zaidi na salama zaidi kwa kila mtu.”Pamoja na kuishukuru nchi ya Misri na shirika la kimataifa la hilal nyekundu kwa kuendelea kushughulikia suala hili kwa karibu, Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amehitimisha mkutano wake na wanahabari kwa kusema anatumai ipo siku Israel na Palestina wataishi kwa amani.“Natumai kwamba kutakuwa na mustakabali na matumaini kwamba siku moja kutakuwa na amani na suluhisho la Serikali mbili, huku Wapalestina na Waisraeli wakiishi kwa amani katika Mataifa mawili, upande mmoja hadi mwingine.”
20-10-2023 • 0
20 AGOSTI 2023
Hii leojaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mashariki ya kati na kilichojiri hapa makao makuu baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huko kugonga mwamba. Makala tunaangazia akili mnemba katika filamu na mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza nchini Palestina na utamsikia ujumbe wa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuhusu machungu wanayopitia wanawake na wasichana katika eneo hilo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko nchini Misri leo ametembelea mpaka wa Rafah, kivuko pekee cha kuingia na kutoka Ukanda wa Gaza, ambako hivi sasa kuna mashambulizi yanaendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na kusema hivi sasa wanaendelea na mazungumzo kupata ufafanuzi wa vikwazo na vizuizi vya masharti yaliyowekwa na Israel kabla ya kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Ukanda wa Gaza.Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa kipalestina, Hamas, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kusimamia amani na usalama liko njiapanda baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huo kugonga mwamba! Makala leo inamulika Akili mnemba ambayo imebadili fani ya sanaa na utamaduni kwa njia ambazo hazikutarajiwa na mabadiliko hayo ni ya muda mrefu. Na kwa kutambua umuhimu wa suala hili shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limeandaa mjadala maalum kuhusu akili mnemba kwenye sekta ya filamu. Ajenda inajikita kwenye manufaa na changamoto zitakazokumba sekta za utamaduni na sanaa ukizingatia maadili na ubunifu. Yvonne Muinde mchanganya picha za filamu ni msanii aliyebobea kwenye sekta ya ubunifu na dijitali na mshiriki wa mjadala huo wa UNESCO ulioanza jana.Na katika mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza nchini Palestina na utamsikia ujumbe wa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuhusu machungu wanayopitia wanawake na wasichana katika eneo hilo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
20-10-2023 • 0
20 AGOSTI 2023
Hii leojaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mashariki ya kati na kilichojiri hapa makao makuu baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huko kugonga mwamba. Makala tunaangazia akili mnemba katika filamu na mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza nchini Palestina na utamsikia ujumbe wa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuhusu machungu wanayopitia wanawake na wasichana katika eneo hilo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko nchini Misri leo ametembelea mpaka wa Rafah, kivuko pekee cha kuingia na kutoka Ukanda wa Gaza, ambako hivi sasa kuna mashambulizi yanaendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na kusema hivi sasa wanaendelea na mazungumzo kupata ufafanuzi wa vikwazo na vizuizi vya masharti yaliyowekwa na Israel kabla ya kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Ukanda wa Gaza.Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa kipalestina, Hamas, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kusimamia amani na usalama liko njiapanda baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huo kugonga mwamba! Makala leo inamulika Akili mnemba ambayo imebadili fani ya sanaa na utamaduni kwa njia ambazo hazikutarajiwa na mabadiliko hayo ni ya muda mrefu. Na kwa kutambua umuhimu wa suala hili shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limeandaa mjadala maalum kuhusu akili mnemba kwenye sekta ya filamu. Ajenda inajikita kwenye manufaa na changamoto zitakazokumba sekta za utamaduni na sanaa ukizingatia maadili na ubunifu. Yvonne Muinde mchanganya picha za filamu ni msanii aliyebobea kwenye sekta ya ubunifu na dijitali na mshiriki wa mjadala huo wa UNESCO ulioanza jana.Na katika mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza nchini Palestina na utamsikia ujumbe wa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuhusu machungu wanayopitia wanawake na wasichana katika eneo hilo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
20-10-2023 • 0
Fahamu nini kinaweza kufuatia pindi maazimio yanagonga mwamba Baraza la Usalama la UN
Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa kipalestina, Hamas, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kusimamia amani na usalama liko njiapanda baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huo kugonga mwamba! Marekani ikitumia kura turufu. Sasa nini kinafuatia? Rasimu mpya au kikao cha dharura cha Baraza Kuu? Bila shaka Assumpta! Ikumbukwe kuwa mzozo wa sasa huko Mashariki ya Kati alianza tarehe 7 mwezi huu wa Oktoba kwa Hamas kurusha makombora Israel.Hali hiyo ikatinga kwenye rada za Baraza la Usalama lenye wanachama 15, watano wakiwa wa kudumu, Baraza lenye wajibu wa kusimamia amani na usalama duniani. Rasimu mbili ziliandaliwa zote zikiwa na lengo la pamoja na mambo mengine sitisho la mapitano na kupatikana kwa njia ya kupitisha misaada ya kibinadamu. Ya kwanza ikiwasilishwa na Urusi haikupata kura za kutosha kuweza kupitishwa, ya pili iliyowasilishwa na Brazili, ilipigiwa kura turufu na Marekani. Marekani, China, Urusi, Ufaransa na Uingereza zina ujumbe wa kudumu Barazani hivyo zina kura turufu au veto ambayo ikitumika rasimu haipiti hata ikipata kura tisa ambazo zinahitajika azimio kupita. Kura turufu ilipatiwa wajumbe hao wa kudumu punde tu baada ya Baraza kuanzishwa mwishoni mwa vita kuu ya pili ya dunia. Hadi sasa harakati za kupanua wigo wa umiliki wa kura hiyo zimegonga mwamba. Lakini wajumbe wa Baraza wanaweza pia kumaliza tofauti zao kwenye lugha ya rasimu na kisha kuwasilisha rasimu nyingine Barazani ili ipigiwe kura. Hiyo itakuwa heri!! Nafasi ya Baraza Kuu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa nalo lina nafasi yake ambapo kwa ombi la nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Baraza hilo Kuu anaweza kuitisha kikao rasmi ndani ya siku 10 tangu mjumbe mmoja au zaidi atumie kura tufuru kuzuia azimio. Na kumbuka Marekani ilitumia turufu yake kuzuia rasimu ya azimio juu ya mzozo wa Israel na Palestina, hivyo Baraza lina hadi tarehe Mosi mwezi ujao wa Novemba kuitisha kikao hicho. Hatua nyingine pia inayoweza kufuatia ni kwa nchi wanachama kumuomba Rais wa Baraza Kuu kuitisha mjadala kuhusu mazingira ambamo kwayo kura hiyo turufu ilitumika. Lakini ni vema kutambua kuwa Baraza hilo halikutani kwa kile ambacho aghalabu huitwa kikao maalum cha dharura juu ya suala moja. Lengo ni kutoa mapendekezo ikiwemo uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi, kuendeleza au kurejesha amani na usalama kwenye eneo husika. Halikadhalika kusitisha mapigano na mahitaji yafikie walio kwenye shida. Na ukiangalia ongezeko la idadi ya vifo huko Mashariki ya Kati, iwapo Rais wa Baraza ataombwa kuitisha kikao kutokana na kura ya wajumbe wowote 7 au zaidi wa Baraza la Usalama au kwa idadi kubwa ya nchi 193 wanachama wa UN, basi Rais huyo lazima aitishe kikao maalum cha dharura ndani ya saa 24. Tangu Umoja wa Mataifa uanzishwe mwaka 195 kumekuweko na vikao vya aina hiyo 11 pekee, na kati ya hivyo, vitano (5) vilihusu Mashariki ya Kati. Kikao cha mwisho kilikuwa Februari mwaka 2022, siku 6 baada ya Urusi kuvamia Ukraine. Lakini wengine wanauliza, mkwamo ndani ya Baraza la Usalama unamaanisha Umoja wa Mataifa umefungwa mikono hauwezi kutekeleza majukumu yake? La hasha! Kwa sasa harakati za kidiplomasia na kibinadamu zinaendelea tangu kulipuka kwa mzozo huo ambapo Katibu Mkuu na wasaidizi wake wako tayari Mashariki ya Kati, huku mashirika yakiendelea kuhakikisha misaada ya kiutu inafikia wahusika.
20-10-2023 • 0
Fahamu nini kinaweza kufuatia pindi maazimio yanagonga mwamba Baraza la Usalama la UN
Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa kipalestina, Hamas, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kusimamia amani na usalama liko njiapanda baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huo kugonga mwamba! Marekani ikitumia kura turufu. Sasa nini kinafuatia? Rasimu mpya au kikao cha dharura cha Baraza Kuu? Bila shaka Assumpta! Ikumbukwe kuwa mzozo wa sasa huko Mashariki ya Kati alianza tarehe 7 mwezi huu wa Oktoba kwa Hamas kurusha makombora Israel.Hali hiyo ikatinga kwenye rada za Baraza la Usalama lenye wanachama 15, watano wakiwa wa kudumu, Baraza lenye wajibu wa kusimamia amani na usalama duniani. Rasimu mbili ziliandaliwa zote zikiwa na lengo la pamoja na mambo mengine sitisho la mapitano na kupatikana kwa njia ya kupitisha misaada ya kibinadamu. Ya kwanza ikiwasilishwa na Urusi haikupata kura za kutosha kuweza kupitishwa, ya pili iliyowasilishwa na Brazili, ilipigiwa kura turufu na Marekani. Marekani, China, Urusi, Ufaransa na Uingereza zina ujumbe wa kudumu Barazani hivyo zina kura turufu au veto ambayo ikitumika rasimu haipiti hata ikipata kura tisa ambazo zinahitajika azimio kupita. Kura turufu ilipatiwa wajumbe hao wa kudumu punde tu baada ya Baraza kuanzishwa mwishoni mwa vita kuu ya pili ya dunia. Hadi sasa harakati za kupanua wigo wa umiliki wa kura hiyo zimegonga mwamba. Lakini wajumbe wa Baraza wanaweza pia kumaliza tofauti zao kwenye lugha ya rasimu na kisha kuwasilisha rasimu nyingine Barazani ili ipigiwe kura. Hiyo itakuwa heri!! Nafasi ya Baraza Kuu Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa nalo lina nafasi yake ambapo kwa ombi la nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Baraza hilo Kuu anaweza kuitisha kikao rasmi ndani ya siku 10 tangu mjumbe mmoja au zaidi atumie kura tufuru kuzuia azimio. Na kumbuka Marekani ilitumia turufu yake kuzuia rasimu ya azimio juu ya mzozo wa Israel na Palestina, hivyo Baraza lina hadi tarehe Mosi mwezi ujao wa Novemba kuitisha kikao hicho. Hatua nyingine pia inayoweza kufuatia ni kwa nchi wanachama kumuomba Rais wa Baraza Kuu kuitisha mjadala kuhusu mazingira ambamo kwayo kura hiyo turufu ilitumika. Lakini ni vema kutambua kuwa Baraza hilo halikutani kwa kile ambacho aghalabu huitwa kikao maalum cha dharura juu ya suala moja. Lengo ni kutoa mapendekezo ikiwemo uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi, kuendeleza au kurejesha amani na usalama kwenye eneo husika. Halikadhalika kusitisha mapigano na mahitaji yafikie walio kwenye shida. Na ukiangalia ongezeko la idadi ya vifo huko Mashariki ya Kati, iwapo Rais wa Baraza ataombwa kuitisha kikao kutokana na kura ya wajumbe wowote 7 au zaidi wa Baraza la Usalama au kwa idadi kubwa ya nchi 193 wanachama wa UN, basi Rais huyo lazima aitishe kikao maalum cha dharura ndani ya saa 24. Tangu Umoja wa Mataifa uanzishwe mwaka 195 kumekuweko na vikao vya aina hiyo 11 pekee, na kati ya hivyo, vitano (5) vilihusu Mashariki ya Kati. Kikao cha mwisho kilikuwa Februari mwaka 2022, siku 6 baada ya Urusi kuvamia Ukraine. Lakini wengine wanauliza, mkwamo ndani ya Baraza la Usalama unamaanisha Umoja wa Mataifa umefungwa mikono hauwezi kutekeleza majukumu yake? La hasha! Kwa sasa harakati za kidiplomasia na kibinadamu zinaendelea tangu kulipuka kwa mzozo huo ambapo Katibu Mkuu na wasaidizi wake wako tayari Mashariki ya Kati, huku mashirika yakiendelea kuhakikisha misaada ya kiutu inafikia wahusika.
20-10-2023 • 0
Neno: KIPA MKONO”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIPA MKONO”.
19-10-2023 • 0
Neno: KIPA MKONO”
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIPA MKONO”.
19-10-2023 • 0
19 OKTOBA 2023
Hii leo tunakuletea mada kwa kina ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO nchini Tanzania kwa ushirikiano na wadau wengine ikiwemo serikali ya Tanzania, waliamua hitimisho la maadhimisho ya siku ya chakula huko Kigoma, Magharibi mwa Tanzania, lifanyike kwenye mwalo wa Kibirizi – Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji kwa kufanya mashindano ya ngalawa, washiriki wakiwa mashujaa wa chakula kitokacho kwenye maji, ziwani Tanganyika, yaani wavuvi na wale waongezao thamani ya mazao ya ziwani kwani wote wanasongesha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kutokomeza umaskini halikadhalika njaa. Pia tunakuleta habari zifuatazo kwa ufupi na katika kujifunza Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla anafafanua maana ya neno “KIPA MKONO”.Kuna matumaini huko Gaza ambako wahudumu wa misaada ya kibinadamu wanaendelea kusubiri ruksa kwa hamasa kubwa kuingiza misaada ya kuokoa maisha kufuatia ripoti za makubaliano yaliyosimamiwa na Rais wa Marekani ya kuingiza Gaza malori 20 ya misaada kupitia mpaka wa Misri umesema leo Umoja wa Mataifa. Tani 3,000 za vifaa zimekuwa zikisubiri kuingia upande wa Misri wa kivuko cha Rafah tangu Jumamosi na shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limesema liko tayari kusambaza msaada huo.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, leo limetoa wito wa ufadhili mpya na kujitolea kwa muda mrefu kwa ajili ya kusambaza mlo shuleni katika mkutano muhimu wa kimataifa unaofanyika mjini Paris Ufaransa kuhusu mlo shuleni. Na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO leo limeanza majadiliano ya ngazi ya juu mjini Paris Ufanrasa kuhusu akili mnemba au AI na sekta ya filamu. Ajenda kubwa ni kuangalia jinsi gani maendeleo ya AI yanavyoathiri sekta hiyo na jinsi sekta hiyo inavyoweza kukumbatia maendeleo hayo kupata ufanisi na manufaa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIPA MKONO”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
19-10-2023 • 0
19 OKTOBA 2023
Hii leo tunakuletea mada kwa kina ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO nchini Tanzania kwa ushirikiano na wadau wengine ikiwemo serikali ya Tanzania, waliamua hitimisho la maadhimisho ya siku ya chakula huko Kigoma, Magharibi mwa Tanzania, lifanyike kwenye mwalo wa Kibirizi – Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Ujiji kwa kufanya mashindano ya ngalawa, washiriki wakiwa mashujaa wa chakula kitokacho kwenye maji, ziwani Tanganyika, yaani wavuvi na wale waongezao thamani ya mazao ya ziwani kwani wote wanasongesha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kutokomeza umaskini halikadhalika njaa. Pia tunakuleta habari zifuatazo kwa ufupi na katika kujifunza Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla anafafanua maana ya neno “KIPA MKONO”.Kuna matumaini huko Gaza ambako wahudumu wa misaada ya kibinadamu wanaendelea kusubiri ruksa kwa hamasa kubwa kuingiza misaada ya kuokoa maisha kufuatia ripoti za makubaliano yaliyosimamiwa na Rais wa Marekani ya kuingiza Gaza malori 20 ya misaada kupitia mpaka wa Misri umesema leo Umoja wa Mataifa. Tani 3,000 za vifaa zimekuwa zikisubiri kuingia upande wa Misri wa kivuko cha Rafah tangu Jumamosi na shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limesema liko tayari kusambaza msaada huo.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, leo limetoa wito wa ufadhili mpya na kujitolea kwa muda mrefu kwa ajili ya kusambaza mlo shuleni katika mkutano muhimu wa kimataifa unaofanyika mjini Paris Ufaransa kuhusu mlo shuleni. Na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO leo limeanza majadiliano ya ngazi ya juu mjini Paris Ufanrasa kuhusu akili mnemba au AI na sekta ya filamu. Ajenda kubwa ni kuangalia jinsi gani maendeleo ya AI yanavyoathiri sekta hiyo na jinsi sekta hiyo inavyoweza kukumbatia maendeleo hayo kupata ufanisi na manufaa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KIPA MKONO”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
19-10-2023 • 0
Tunashukuru TANZBATT10 kwa vifaa vya shule lakini pia watusaidie majengo
Hii leo katika makala ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 10, TANZBATT 10 kinachohudumu kwenye ujumbe wa UN wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, hususan kile cha kujibu mashambulizi, FIB wamefika shule ya msingi Ushindi mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini na kutoa msaada wa vifaa vya shule wakilenga kufanikisha lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu. SDGs hukusan kipengele kinachohusu ujumuishi. Afisa Habari wa kikosi hicho Luteni Abubakari Muna ameandaa makala hii kutoka na ziara hiyo, ikianza na Meja Neema Neligwa mwakilishi wa Kamanda kikosi cha TANZBATT 10, Luteni Kanali John Peter Kalabaka akifafanua walengwa kwa msaada huo.
18-10-2023 • 0
Tunashukuru TANZBATT10 kwa vifaa vya shule lakini pia watusaidie majengo
Hii leo katika makala ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 10, TANZBATT 10 kinachohudumu kwenye ujumbe wa UN wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, hususan kile cha kujibu mashambulizi, FIB wamefika shule ya msingi Ushindi mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini na kutoa msaada wa vifaa vya shule wakilenga kufanikisha lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu. SDGs hukusan kipengele kinachohusu ujumuishi. Afisa Habari wa kikosi hicho Luteni Abubakari Muna ameandaa makala hii kutoka na ziara hiyo, ikianza na Meja Neema Neligwa mwakilishi wa Kamanda kikosi cha TANZBATT 10, Luteni Kanali John Peter Kalabaka akifafanua walengwa kwa msaada huo.
18-10-2023 • 0
Umoja wa Mataifa unaendelea kuwapatia msaada wananchi waliosalia nchini Ukraine
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umefurusha makwao mamilioni ya watu kwenda kusaka hifadhi maeneo ya mikoani na hata nchi jirani. Katika Mkoa wa Donetsk asilimia 90 ya wananchi walikimbia tu vita ilipoanza, na zaidi ya wananchi 1,000 walioamua kusalia hawana huduma za maji, umeme na gesi na Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kila juhudi kuhakikisha wanapata huduma hizo muhimu.Wakazi wa Chasiv Yar mkoani Donetsk tangu kuibuka kwa vita kati ya Ukraine na Urusi wamekuwa wakiishi katika hali ya taabu na kujificha katika mahandaki chini ya nyumba zao.Mapigano yameharibu nyumba zao pamoja na miundombinu na kuwaacha wakazi zaidi ya 1,000 wakiwa katika hali ngumu.Mfanyakazi wa kujitolea aitwaye Oleksandr anasema baadhi ya walioamua kubaki katika eneo hilo wanawasaidia wananchi wenzao kwani kuna kundi kubwa la wazee wake kwa waume ambao hawataki kuondoka na wanahitaji msaada, “Kwa wakati huu, tuseme, hali si rahisi. Naweza kusema kuwa ni ngumu kwa wenyeji. Kwa nini? Hakuna umeme, gesi, taa, wala miundombinu ya kuletajoto kwenye nyumba. Ndio maana shirika letu linafanya kila liwezalo kusaidia watu kuboresha nyumba zao.”Mratibu mkazi wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine Denise Brown amefika katika mkoa huo akiwa na msafara wa 31 uliosheheni misaada ya kibinadamu kutoka kwa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na kugawa misaada hiyo kwa wananchi.Miongoni mwa waliopokea msaada ni Bi. Lyubove, “Tumepokea misaada ya kibinadamu leo, sijui imetoka wapi, lakini kila mtu amepata chupa tatu za maji pamoja na masanduku mawili ya bidhaa.”Pamoja na kushukuru kwa msaada huo Bi.Lyubove akatoa ombi kwa wadau wa misaada ya kibinadamu, “Kodi ya nyumba ni ghali sana kwa sasa. Watu wameanza kurejea Chasiv Yar. Ingawa ni ngumu sana na inatisha kuishi hapa lakini wanajaribu kurudi nyumbani hasa wale wenye nyumba zao binafsi zilizo ambazo zina majiko. Majira ya baridi yanakuja, na watu hawana pesa za kulipa… Pensheni ni ndogo, na hakuna mishahara.”Kiujumla kwa mwaka huu Umoja wa Mataifa na wadau wake wamefanikiwa kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wakazi zaidi ya milioni 8.3 nchini Ukraine.
18-10-2023 • 0
Umoja wa Mataifa unaendelea kuwapatia msaada wananchi waliosalia nchini Ukraine
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umefurusha makwao mamilioni ya watu kwenda kusaka hifadhi maeneo ya mikoani na hata nchi jirani. Katika Mkoa wa Donetsk asilimia 90 ya wananchi walikimbia tu vita ilipoanza, na zaidi ya wananchi 1,000 walioamua kusalia hawana huduma za maji, umeme na gesi na Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kila juhudi kuhakikisha wanapata huduma hizo muhimu.Wakazi wa Chasiv Yar mkoani Donetsk tangu kuibuka kwa vita kati ya Ukraine na Urusi wamekuwa wakiishi katika hali ya taabu na kujificha katika mahandaki chini ya nyumba zao.Mapigano yameharibu nyumba zao pamoja na miundombinu na kuwaacha wakazi zaidi ya 1,000 wakiwa katika hali ngumu.Mfanyakazi wa kujitolea aitwaye Oleksandr anasema baadhi ya walioamua kubaki katika eneo hilo wanawasaidia wananchi wenzao kwani kuna kundi kubwa la wazee wake kwa waume ambao hawataki kuondoka na wanahitaji msaada, “Kwa wakati huu, tuseme, hali si rahisi. Naweza kusema kuwa ni ngumu kwa wenyeji. Kwa nini? Hakuna umeme, gesi, taa, wala miundombinu ya kuletajoto kwenye nyumba. Ndio maana shirika letu linafanya kila liwezalo kusaidia watu kuboresha nyumba zao.”Mratibu mkazi wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine Denise Brown amefika katika mkoa huo akiwa na msafara wa 31 uliosheheni misaada ya kibinadamu kutoka kwa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na kugawa misaada hiyo kwa wananchi.Miongoni mwa waliopokea msaada ni Bi. Lyubove, “Tumepokea misaada ya kibinadamu leo, sijui imetoka wapi, lakini kila mtu amepata chupa tatu za maji pamoja na masanduku mawili ya bidhaa.”Pamoja na kushukuru kwa msaada huo Bi.Lyubove akatoa ombi kwa wadau wa misaada ya kibinadamu, “Kodi ya nyumba ni ghali sana kwa sasa. Watu wameanza kurejea Chasiv Yar. Ingawa ni ngumu sana na inatisha kuishi hapa lakini wanajaribu kurudi nyumbani hasa wale wenye nyumba zao binafsi zilizo ambazo zina majiko. Majira ya baridi yanakuja, na watu hawana pesa za kulipa… Pensheni ni ndogo, na hakuna mishahara.”Kiujumla kwa mwaka huu Umoja wa Mataifa na wadau wake wamefanikiwa kufikisha misaada ya kibinadamu kwa wakazi zaidi ya milioni 8.3 nchini Ukraine.
18-10-2023 • 0
18 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu Gaza na ya wakimbizi wa ndani Ukraine. Makala tunakupeleka nchini DRC na mashini tuanarejea huko Gaza kusikia ushuhuda wa waathirika, salía papo hapo tafadhali!Hali Mashariki ya Kati inaendelea kuwa mbayá hasa baada ya shambulio dhidi ya Hospitali ya Al-Ahli lililokatili maisha ya zaidi ya watu 500. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelazimika kukatisha ziara yake nchini China na kuelekea Cairo Misri atakakozungumza na wadau kuhusu jinsi ya kupunguza madhila kwa waathirika wa mzozo wa Israel na Hamas huko Gaza, lakini kabla ya kuondoka ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano kwa ajili ya masuala ya kibinadamu, huku mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths tayari ameshawasili Cairo ili kuhakikisha misaada ya kibinadamu inaruhusiwa kuingia Gaza.Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umefurusha makwao mamilioni ya watu kwenda kusaka hifadhi maeneo ya mikoani na hata nchi jirani. Katika Mkoa wa Donetsk asilimia 90 ya wananchi walikimbia tu vita ilipoanza, na zaidi ya wananchi 1,000 walioamua kusalia hawana huduma za maji, umeme na gesi na Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kila juhudi kuhakikisha wanapata huduma hizo muhimu. Makala inatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 10, TANZBATT 10 kinachohudumu kwenye ujumbe wa UN wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, hususan kile cha kujibu mashambulizi, FIB wamefika shule ya msingi Ushindi mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini na kutoa msaada wa vifaa vya shule. Afisa Habari wa kikosi hicho Luteni Abubakari Muna ameandaa makala hii kutoka na ziara hiyo, ikianza na Meja Neema Neligwa mwakilishi wa Kamanda kikosi cha TANZBATT 10, Luteni Kanali John Peter Kalabaka akifafanua walengwa kwa msaada huo.Na mashinani tuaelekea katika ukanda wa Gaza, eneo linalokaliwa la Palestina huko Mashariki ya Kati, kusikia ushuhuda wa waathirika wa mapigano yanayoendelea kati ya wanamgambo wa Hamas wa kipalestina na jeshi la Israel kati ya Hamas na Israeli.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
18-10-2023 • 0
18 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya kibinadamu Gaza na ya wakimbizi wa ndani Ukraine. Makala tunakupeleka nchini DRC na mashini tuanarejea huko Gaza kusikia ushuhuda wa waathirika, salía papo hapo tafadhali!Hali Mashariki ya Kati inaendelea kuwa mbayá hasa baada ya shambulio dhidi ya Hospitali ya Al-Ahli lililokatili maisha ya zaidi ya watu 500. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelazimika kukatisha ziara yake nchini China na kuelekea Cairo Misri atakakozungumza na wadau kuhusu jinsi ya kupunguza madhila kwa waathirika wa mzozo wa Israel na Hamas huko Gaza, lakini kabla ya kuondoka ametoa wito wa kusitishwa mara moja mapigano kwa ajili ya masuala ya kibinadamu, huku mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths tayari ameshawasili Cairo ili kuhakikisha misaada ya kibinadamu inaruhusiwa kuingia Gaza.Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umefurusha makwao mamilioni ya watu kwenda kusaka hifadhi maeneo ya mikoani na hata nchi jirani. Katika Mkoa wa Donetsk asilimia 90 ya wananchi walikimbia tu vita ilipoanza, na zaidi ya wananchi 1,000 walioamua kusalia hawana huduma za maji, umeme na gesi na Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kila juhudi kuhakikisha wanapata huduma hizo muhimu. Makala inatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 10, TANZBATT 10 kinachohudumu kwenye ujumbe wa UN wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, hususan kile cha kujibu mashambulizi, FIB wamefika shule ya msingi Ushindi mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini na kutoa msaada wa vifaa vya shule. Afisa Habari wa kikosi hicho Luteni Abubakari Muna ameandaa makala hii kutoka na ziara hiyo, ikianza na Meja Neema Neligwa mwakilishi wa Kamanda kikosi cha TANZBATT 10, Luteni Kanali John Peter Kalabaka akifafanua walengwa kwa msaada huo.Na mashinani tuaelekea katika ukanda wa Gaza, eneo linalokaliwa la Palestina huko Mashariki ya Kati, kusikia ushuhuda wa waathirika wa mapigano yanayoendelea kati ya wanamgambo wa Hamas wa kipalestina na jeshi la Israel kati ya Hamas na Israeli.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
18-10-2023 • 0
Guterres: Mapigano lazima yasite mara moja Gaza kwa sababu za kibinadamu
Hali Mashariki ya Kati inaendelea kuwa mbayá hasa baada ya shambulio dhidi ya Hospitali ya Al-Ahli na kukatili Maisha ya zaidi ya watu 500. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelazimika kukatisha ziara yake nchini China na kuelekea Cairo Misri lakini kabla ya kuondoka ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano Mashariki ya kwa ajili ya masuala ya kibinadamu. Naye mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths ameshawasili Cairo Misri katika juhudi za kuhakikisha misaada inaruhusiwa kuingia Gaza. Akizungumza mjini Beijing China, kabla ya kuondoka kuelekea Cairo Misri hii leo Bwana Guterres hakutafuna maneno, amesema kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anawajibika kutoa kauli hii ili kupunguza madhila makubwa yanayowaghubika watu katika mzozo wa Masharikiya Kati Mashariki ya Kati ni "mateso makubwa ya kibinadamu" Hivyo amesema “Natoa wito wa usitishaji mapigano haraka kwa sababu za kibinadamu ili kutoa wakati na fursa ya kutosha kusaidia kutimiza maombi yangu mawili na kupunguza mateso makubwa kwa binadamu tunayoshuhudia. Maisha ya watu wengi na hatma ya ukanda mzima viko njiapanda.”Guterres ameonya kwamba eneo mzima liko katika hatari ya janga kubwa akisisitiza umuhimu wa kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.Wakati huohuo mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths ameshawasili Cairo Misri kwa ajili ya kuhakikisha misaada hiyo ya kibinadamu ambayo iko tayari mpakani mwa Gaza inaruhusiwa kuingia ili kuokoa maisha ya watu wengi. Kupitia ukurasa wake wa X amesema “ Kutoa misaada kwa watu wa Gaza popote walipo ni suala la uhai au kifo. Kufanya hivyo kwa njia endelevu, isiyozuiliwa, na inayotabirika ni sharti la kibinadamu.”Naye Phillippe Lazzarini kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA amewaomba mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya ya ushirikiano wa nchi za Kiislamu OIC "kuunga mkono kwa dhati na bila masharti juhudi za kibinadamu za kuwalinda raia huko Gaza" akisema kwani hadi sasa “Hakuna shehena hata moja ya msaada imeruhusiwa kuingia Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa mzozo huu kutokana na hali iliyowekwa na Israel ya kuzingizwa. Watu wanalazimika kunywa maji ambayo hayafai kwa matumizi, kwani maji safi ya kunywa hayapatikani. Akiba ya chakula, vifaa vya usafi na dawa vinapungua kwa kasi. Tuko ukingoni mwa janga kubwa la afya na usafi wa mazingira”.Hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama limekutana kujadili mgogoro huo na huko Israel Rais wa Marekani Joe Biden amewasili na kukutana na waziri mkuu Benjamin Netanyahu ambapo ameahidi msaada wa Marekani kwa Israel na kusema ameshtushwa na kughadhibishwa na mlipuko wa jana katika hospital mjini Gaza.
18-10-2023 • 0
Guterres: Mapigano lazima yasite mara moja Gaza kwa sababu za kibinadamu
Hali Mashariki ya Kati inaendelea kuwa mbayá hasa baada ya shambulio dhidi ya Hospitali ya Al-Ahli na kukatili Maisha ya zaidi ya watu 500. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelazimika kukatisha ziara yake nchini China na kuelekea Cairo Misri lakini kabla ya kuondoka ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano Mashariki ya kwa ajili ya masuala ya kibinadamu. Naye mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths ameshawasili Cairo Misri katika juhudi za kuhakikisha misaada inaruhusiwa kuingia Gaza. Akizungumza mjini Beijing China, kabla ya kuondoka kuelekea Cairo Misri hii leo Bwana Guterres hakutafuna maneno, amesema kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anawajibika kutoa kauli hii ili kupunguza madhila makubwa yanayowaghubika watu katika mzozo wa Masharikiya Kati Mashariki ya Kati ni "mateso makubwa ya kibinadamu" Hivyo amesema “Natoa wito wa usitishaji mapigano haraka kwa sababu za kibinadamu ili kutoa wakati na fursa ya kutosha kusaidia kutimiza maombi yangu mawili na kupunguza mateso makubwa kwa binadamu tunayoshuhudia. Maisha ya watu wengi na hatma ya ukanda mzima viko njiapanda.”Guterres ameonya kwamba eneo mzima liko katika hatari ya janga kubwa akisisitiza umuhimu wa kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.Wakati huohuo mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths ameshawasili Cairo Misri kwa ajili ya kuhakikisha misaada hiyo ya kibinadamu ambayo iko tayari mpakani mwa Gaza inaruhusiwa kuingia ili kuokoa maisha ya watu wengi. Kupitia ukurasa wake wa X amesema “ Kutoa misaada kwa watu wa Gaza popote walipo ni suala la uhai au kifo. Kufanya hivyo kwa njia endelevu, isiyozuiliwa, na inayotabirika ni sharti la kibinadamu.”Naye Phillippe Lazzarini kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA amewaomba mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya ya ushirikiano wa nchi za Kiislamu OIC "kuunga mkono kwa dhati na bila masharti juhudi za kibinadamu za kuwalinda raia huko Gaza" akisema kwani hadi sasa “Hakuna shehena hata moja ya msaada imeruhusiwa kuingia Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa mzozo huu kutokana na hali iliyowekwa na Israel ya kuzingizwa. Watu wanalazimika kunywa maji ambayo hayafai kwa matumizi, kwani maji safi ya kunywa hayapatikani. Akiba ya chakula, vifaa vya usafi na dawa vinapungua kwa kasi. Tuko ukingoni mwa janga kubwa la afya na usafi wa mazingira”.Hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama limekutana kujadili mgogoro huo na huko Israel Rais wa Marekani Joe Biden amewasili na kukutana na waziri mkuu Benjamin Netanyahu ambapo ameahidi msaada wa Marekani kwa Israel na kusema ameshtushwa na kughadhibishwa na mlipuko wa jana katika hospital mjini Gaza.
18-10-2023 • 0
17 OKTOBA 2023
Hii leo jaridanitunakuletea mada kwa kina na ukulima wa kisasa hususani mijini umeelezwa kuchangia si tu upatikanaji wa chakula bali pia unatumia maji kidogo hivyo unapigiwa chepuo hususan wakati huu dunia ikikabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Taasisi ya Malembo Farm iliyofanya kazi nchini Tanzania na Kenya inatoa mafunzo ya kilimo cha kisasa mijini ambapo tumezungumza na wanufaika wa mafunzo hayo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wake Lucas Elias Malembo akiwa nchini Tanzania anayeanza kwa kueleza namna wanavyoienzi kauli mbiu ya mwaka huu. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani, zinahusu nini? Salía papo hapo tafadhali!Asante Leah naazia Mashariki ya Kati ambako mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine yameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu hatma raia huko Gaza na Ukingo wa Magaribi yakisistiza fursa ya kufikisha misaada kwa wenye uhitaji likiwemo shirika la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linalohifadhi wakimbizi wa ndani takribani 400,000 kati ya laki sita sasa katika vituo vyake.Katika taarifa nyingine leo UNHCR, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi limetoa tahadhari kuhusu kukithiri kwa ghasia na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika majimbo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambazo zimesababisha wimbi jipya la watu kukimbia makazi yao, ndani na nje ya nchi. Licha ya makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano katika jimbo la Kivu Kaskazini, UNHCR imeripoti kuwa zaidi ya watu 90,000 katika maeneo ya Rutshuru na Masisi wamelazimika kukimbia makazi yao katika wiki za kwanza za Oktoba. Nchini Sudan kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Takriban watu 4,000 wameuawa huku mali na miundombinu ya raia vikiharibiwa vibaya katika vita inavyoendelea Darfur na watu wengine 8,400 wamejeruhiwa, kati ya Aprili 15 na mwisho wa Agosti, huku wengi wao wakilengwa kutokana na sababu za kikabila, hasa eneo la Darfur Magharibi.Na mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza nchini Palestina kushuhudia jinsi ambavyo watoto na jamii zao wanavyoathirika kufuatia vita kati ya Hamas na Israeli.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
17-10-2023 • 0
17 OKTOBA 2023
Hii leo jaridanitunakuletea mada kwa kina na ukulima wa kisasa hususani mijini umeelezwa kuchangia si tu upatikanaji wa chakula bali pia unatumia maji kidogo hivyo unapigiwa chepuo hususan wakati huu dunia ikikabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Taasisi ya Malembo Farm iliyofanya kazi nchini Tanzania na Kenya inatoa mafunzo ya kilimo cha kisasa mijini ambapo tumezungumza na wanufaika wa mafunzo hayo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wake Lucas Elias Malembo akiwa nchini Tanzania anayeanza kwa kueleza namna wanavyoienzi kauli mbiu ya mwaka huu. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani, zinahusu nini? Salía papo hapo tafadhali!Asante Leah naazia Mashariki ya Kati ambako mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine yameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu hatma raia huko Gaza na Ukingo wa Magaribi yakisistiza fursa ya kufikisha misaada kwa wenye uhitaji likiwemo shirika la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA linalohifadhi wakimbizi wa ndani takribani 400,000 kati ya laki sita sasa katika vituo vyake.Katika taarifa nyingine leo UNHCR, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi limetoa tahadhari kuhusu kukithiri kwa ghasia na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika majimbo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambazo zimesababisha wimbi jipya la watu kukimbia makazi yao, ndani na nje ya nchi. Licha ya makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha mapigano katika jimbo la Kivu Kaskazini, UNHCR imeripoti kuwa zaidi ya watu 90,000 katika maeneo ya Rutshuru na Masisi wamelazimika kukimbia makazi yao katika wiki za kwanza za Oktoba. Nchini Sudan kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Takriban watu 4,000 wameuawa huku mali na miundombinu ya raia vikiharibiwa vibaya katika vita inavyoendelea Darfur na watu wengine 8,400 wamejeruhiwa, kati ya Aprili 15 na mwisho wa Agosti, huku wengi wao wakilengwa kutokana na sababu za kikabila, hasa eneo la Darfur Magharibi.Na mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza nchini Palestina kushuhudia jinsi ambavyo watoto na jamii zao wanavyoathirika kufuatia vita kati ya Hamas na Israeli.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
17-10-2023 • 0
Asante FAO kwani sasa nimeweza kujipatia zaidi ya dola Elfu 3 kupitia kilimo cha kisasa
Wanawake wa vijijini wanatambuliwa kimataifa kupitia siku yao ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 15 mwezi Oktoba. Mwaka huu maadhimisho yamefanyika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania, huko Afrika Mashariki. Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula, FAO liliandaa tukio maalum la kutambua mchango wa wanawake hao hasa kwa kuzingatia mchango wao katika uzalishaji chakula, kwani shirika la Umoja wa Mataifa la kazi, ILO linasema wanawake ni zaidi ya asilimia 40 ya nguvukazi kwenye sekta ya kilimo. Ingawa hivyo tija itokanayo na kilimo hicho mara nyingi huwa ni ya chini sana na ndio maana FAO nchini Tanzania kupitia Mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP, wameendesha miradi kama vile kilimo cha kisasa kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, halikadhalika ufugaji wa kisasa. Baadhi ya wanawake wanufaika wa miradi hiyo wamekuwa mashujaa wa chakula, maudhui ya siku hiyo ya mwanamke wa Kijijini. Sasa wamefanya nini? John Kabambala wa Radio Washirika Kids Time FM ya mkoani Morogoro nchini Tanzania alikuwa shuhuda wetu wa tukio hilo mkoani Kigoma.
16-10-2023 • 0
Asante FAO kwani sasa nimeweza kujipatia zaidi ya dola Elfu 3 kupitia kilimo cha kisasa
Wanawake wa vijijini wanatambuliwa kimataifa kupitia siku yao ya kimataifa inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 15 mwezi Oktoba. Mwaka huu maadhimisho yamefanyika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo mkoani Kigoma, magharibi mwa Tanzania, huko Afrika Mashariki. Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula, FAO liliandaa tukio maalum la kutambua mchango wa wanawake hao hasa kwa kuzingatia mchango wao katika uzalishaji chakula, kwani shirika la Umoja wa Mataifa la kazi, ILO linasema wanawake ni zaidi ya asilimia 40 ya nguvukazi kwenye sekta ya kilimo. Ingawa hivyo tija itokanayo na kilimo hicho mara nyingi huwa ni ya chini sana na ndio maana FAO nchini Tanzania kupitia Mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP, wameendesha miradi kama vile kilimo cha kisasa kinachohimili mabadiliko ya tabianchi, halikadhalika ufugaji wa kisasa. Baadhi ya wanawake wanufaika wa miradi hiyo wamekuwa mashujaa wa chakula, maudhui ya siku hiyo ya mwanamke wa Kijijini. Sasa wamefanya nini? John Kabambala wa Radio Washirika Kids Time FM ya mkoani Morogoro nchini Tanzania alikuwa shuhuda wetu wa tukio hilo mkoani Kigoma.
16-10-2023 • 0
Matarajio ya OCHA ni misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuingia Gaza
Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths, ameeleza wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa mzozo wa kibinadamu huko Gaza, Mashariki ya Kati, kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina, Hamas, halikadhalika hatma ya mateka wa Israel, huku pia akieleza matarajio yake ya kupokea habari njema za misaada kuruhusiwa kuingia Gaza. Akihojiwa jijini Geneva nchini Uswisi hii leo, na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Mkuu huyo wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA amezungumzia hali inayoendelea huko Mashariki ya Kati na kutaja mambo matatu.Mosi, ametaka mateka wa Israel wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto waliochukuliwa na wapiganaji wa Hamas waachiliwe mara moja. Pili, ametaka kuheshimiwa kwa sheria za kibinadamu kwenye vita akieleza kuwa “Huwezi kuwaeleza watu wahame kutoka kwenye hatari bila ya kuwasaidia kwenda mahali wanapotaka, ambako wanataka kuwa salama na kuwapa misaada ya kibinadamu ikayofanya safari yao hiyo kuwa salama. Akifafanua suala la misaada ya kibinadamu Griffiths amesema kwa sasa hospitali hazina nishati ya kujiendeesha, na wanakabiliwa na upungufu wa misaada hivyo watu hawawezi kuhama kutoka Gaza Kaskazini Kwenda Gaza Kusini bila ya Msaada. “Suala la tatu tunahitaji misaada”, amesisitiza Griffiths akieleza kuwa wanaendelea na mazungumzo na nchi za Israel, Misri na nyinginezo huku wakitarajia kupata habari njema.“Na ninatumai kusikia habari njema asubuhi ya leo kuhusu misaada kuruhusiwa kuingia huko Gaza kupitia mpaka wa Rafah, (Ulioko nchini Misri) kusaidia watu milioni moja waliohamia eneo hulo wakitokea Kaskazini pamoja na wakazi wa eneo hilo la kusini waliokuwepo muda wote. Na kumesisitiza katika hili “sheria za vita, misaada, na kuruhusiwa kupita” lazima zizingatiwe.Mkuu huyo wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa hapo kesho yeye mwenyewe ataenda Mashariki ya Kati ili kusaidia kwenye mazungumzo pamoja na kuonesha mshikamano na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu ambao wamesalia kuendelea kutoa usaidizi kwa watu. Amehitimisha taarifa yake kwa kueleza kueleza kuna maisha baada ya vita. “Ninataka kuwaacha na wazo moja la mwisho. Historia inatuambia kwamba kitendo cha vita vina athari ambazo mara nyingi hazizingatiwi wakati watu wakiingia vitani. Tumeona filamu hii kwa mara nyingi sana. Tunahitaji kuwa na wasiwasi na kuunda hali ambayo kwa sasa itaonekana kama ya kipuuzi - ambapo Waisraeli na Wapalestina wanaweza kuishi kama majirani, kama marafiki, kwa hakika, kama wanaoingiliana, ambapo hawahitaji kupeana mafunzo kupitia vita. Asante.”
16-10-2023 • 0
Matarajio ya OCHA ni misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuingia Gaza
Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths, ameeleza wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa mzozo wa kibinadamu huko Gaza, Mashariki ya Kati, kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina, Hamas, halikadhalika hatma ya mateka wa Israel, huku pia akieleza matarajio yake ya kupokea habari njema za misaada kuruhusiwa kuingia Gaza. Akihojiwa jijini Geneva nchini Uswisi hii leo, na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Mkuu huyo wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA amezungumzia hali inayoendelea huko Mashariki ya Kati na kutaja mambo matatu.Mosi, ametaka mateka wa Israel wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto waliochukuliwa na wapiganaji wa Hamas waachiliwe mara moja. Pili, ametaka kuheshimiwa kwa sheria za kibinadamu kwenye vita akieleza kuwa “Huwezi kuwaeleza watu wahame kutoka kwenye hatari bila ya kuwasaidia kwenda mahali wanapotaka, ambako wanataka kuwa salama na kuwapa misaada ya kibinadamu ikayofanya safari yao hiyo kuwa salama. Akifafanua suala la misaada ya kibinadamu Griffiths amesema kwa sasa hospitali hazina nishati ya kujiendeesha, na wanakabiliwa na upungufu wa misaada hivyo watu hawawezi kuhama kutoka Gaza Kaskazini Kwenda Gaza Kusini bila ya Msaada. “Suala la tatu tunahitaji misaada”, amesisitiza Griffiths akieleza kuwa wanaendelea na mazungumzo na nchi za Israel, Misri na nyinginezo huku wakitarajia kupata habari njema.“Na ninatumai kusikia habari njema asubuhi ya leo kuhusu misaada kuruhusiwa kuingia huko Gaza kupitia mpaka wa Rafah, (Ulioko nchini Misri) kusaidia watu milioni moja waliohamia eneo hulo wakitokea Kaskazini pamoja na wakazi wa eneo hilo la kusini waliokuwepo muda wote. Na kumesisitiza katika hili “sheria za vita, misaada, na kuruhusiwa kupita” lazima zizingatiwe.Mkuu huyo wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuwa hapo kesho yeye mwenyewe ataenda Mashariki ya Kati ili kusaidia kwenye mazungumzo pamoja na kuonesha mshikamano na wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu ambao wamesalia kuendelea kutoa usaidizi kwa watu. Amehitimisha taarifa yake kwa kueleza kueleza kuna maisha baada ya vita. “Ninataka kuwaacha na wazo moja la mwisho. Historia inatuambia kwamba kitendo cha vita vina athari ambazo mara nyingi hazizingatiwi wakati watu wakiingia vitani. Tumeona filamu hii kwa mara nyingi sana. Tunahitaji kuwa na wasiwasi na kuunda hali ambayo kwa sasa itaonekana kama ya kipuuzi - ambapo Waisraeli na Wapalestina wanaweza kuishi kama majirani, kama marafiki, kwa hakika, kama wanaoingiliana, ambapo hawahitaji kupeana mafunzo kupitia vita. Asante.”
16-10-2023 • 0
16 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu Gaza, na siku ya chakula duniani. Makala tunakupeleka nchini Tanzania kushuhudia jinsi ambavyo FAO nchini humo umeinua wanawake wa kijijini. Mashinani tunasalia katika siku ya chakula duniani na tutasikia ujumbe kuhusu jinsi ambavyo wahamiaji wanavyoweza kusaidiwa kuhimili madhila ya mabadiliko ya tabianchi.Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths, ameeleza wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa mzozo wa kibinadamu huko Gaza, Mashariki ya Kati, kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina, Hamas, halikadhalika hatma ya mateka wa Israel, huku pia akieleza matarajio yake ya kupokea habari njema za misaada kuruhusiwa kuingia Gaza.Leo ni siku ya chakula duniani na maadhimisho ya mwaka huu kwa mujibu wa shirika na chakula na kilimo FAO yanasherehekea moja ya rasilimali muhimu zaidi kwa maisha ya binadamu ambayo ni maji, kwani yanachukua asilimia 50 ya uso wa dunia, yanazalisha chakula na kuwezesha watu kuishi. Makala leo inatupeleka Kigoma, magharibi mwa Tanzania ambako huko mradi wa pamoja wa Kigoma, KJP unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini humo umeinua wanawake wa kijijini, na mwenyeji wetu ni John Kabambala wa Radio Washirika Kids Time FM ya Morogoro nchini Tanzania.Na mashinani leo ikiwa ni siku ya chakula duniani tutasikia ujumbe kuhusu mifumo ya kilimo na njia mbadala ya kuwezesha jamii waathirika kuhimili changamoto za mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Flora, karibu !
16-10-2023 • 0
16 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu Gaza, na siku ya chakula duniani. Makala tunakupeleka nchini Tanzania kushuhudia jinsi ambavyo FAO nchini humo umeinua wanawake wa kijijini. Mashinani tunasalia katika siku ya chakula duniani na tutasikia ujumbe kuhusu jinsi ambavyo wahamiaji wanavyoweza kusaidiwa kuhimili madhila ya mabadiliko ya tabianchi.Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths, ameeleza wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa mzozo wa kibinadamu huko Gaza, Mashariki ya Kati, kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina, Hamas, halikadhalika hatma ya mateka wa Israel, huku pia akieleza matarajio yake ya kupokea habari njema za misaada kuruhusiwa kuingia Gaza.Leo ni siku ya chakula duniani na maadhimisho ya mwaka huu kwa mujibu wa shirika na chakula na kilimo FAO yanasherehekea moja ya rasilimali muhimu zaidi kwa maisha ya binadamu ambayo ni maji, kwani yanachukua asilimia 50 ya uso wa dunia, yanazalisha chakula na kuwezesha watu kuishi. Makala leo inatupeleka Kigoma, magharibi mwa Tanzania ambako huko mradi wa pamoja wa Kigoma, KJP unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini humo umeinua wanawake wa kijijini, na mwenyeji wetu ni John Kabambala wa Radio Washirika Kids Time FM ya Morogoro nchini Tanzania.Na mashinani leo ikiwa ni siku ya chakula duniani tutasikia ujumbe kuhusu mifumo ya kilimo na njia mbadala ya kuwezesha jamii waathirika kuhimili changamoto za mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Flora, karibu !
16-10-2023 • 0
FAO inasisitiza kwamba maji ni uhai, maji ni chakula tusimwache yeyote nyuma katika hili
Leo ni siku ya chakula duniani na maadhimisho ya mwaka huu kwa mujibu wa shirika na chakula na kilimo FAO yanasherehekea moja ya rasilimali muhimu zaidi kwa maisha ya binadamu ambayo ni maji, kwani yanachukua asilimia 50 ya uso wa dunia, yanazalisha chakula na kuwezesha watu kuishi. Maudhui ya siku ya mwaka huu ni “Maji ni uhai, maji ni chakula, usimwache yeyote nyuma”.Pamoja na kwamba maji ndio kila kitu FAO imekumbusha kwamba rasilimali hiyo haidumu milele na dunia inahitaji kuacha kuichukulia kama mazoea kwani chakula kinacholiwa duniani na jinsi kinavyozalishwa vinaathiri rasilimali ya maji.Hivyo shirika hilo limesisitiza kwamba dunia “Kwa pamoja tunaweza kuchukua hatua kwa ajili ya chakula na kuwa mabadiliko yanayohitajika, kwani maji ni msingi kwa ajili ya maisha na chakula.”Akisisitiza umuhimu huo mkurugenzi mkuu wa FAO Qu Dongyu (TAMKA KYU DONGYU) amesema, "Mgogoro wa madadiliko ya tabianchi, ongezoko la idadi ya watu, ukuaji wa miji, maendeleo ya viwanda na maendeleo ya kiuchumi na kijamii vinaongeza shinikizo katik rasilimali ya maji.”Na kuongeza kuwa theluthi moja ya watu wote duniani wanaishi bila rasilimali hiyo muhimu hivyo changamoto hizo zinaleta athari kubwa kwa uhakika wa chakula na ametoa wito wa kugeukia sayansi, ubunifu na teknolojia kuzitatua, “Lazima tukumbatie uwezo wa sayansi, ubunifu, takwimu na teknolojia kuzalisha zaidi kwa kutumia maji kidogo ili kufanya kila tone la maji kuwa na maana. Sote tunapswa kutumia na kudhibiti maji kwa ufanisi.”Ili kuendeleza azma hiyo ametaka sekta ya kilimo inayotumia asilimia 70 ya maji duniani kufanya mabadiliko ya mifumo yake ya chakula na ndio maana leo mjini Roma Italia FAO limenaza kongamano la siku nne litakalokamilika 20 Oktaba kujadili umuhimu wa sayansi, uvumbuzi na teknolojia katika kubadili mifumo ya chakula kuwa sehemu ya suluhu ya mabadiliko ya tabianchi.Ismahane Elouafi ni mkuu wa kitengo cha sayansi ya chakula na kilimo wa FAO anasema, “Kuanzia uvumbuzi wa teknolojia hadi uvumbuzi wa kifedha, uvumbuzi wa kitaasisi, uvumbuzi wa sera, ni katika wigo mzima wa uvumbuzi, na tunatumai kwamba mjadala kati ya wadau tofauti utaleta matokeo, je tunajua nini hadi sasa, tunaweza kuongeza nini kwa sasa na ni wapi tunapaswa kuwekeza katika siku za usoni ili kuwa na msingi bora wa sayansi na ushahidi kwa ajili ya utungaji sera na kwa ajili ya mabadiliko ya mifumo ya kilimo ya chakula.”FAO inasema kampeni ya siku ya chakula mwaka huu ni kuelimisha dunia kuhusu umuhimu wa kutumia maji kwa ufanisi kwa sababu rasilimali hiyo iko katika tishio kubwa na huu ni wakati wa kufanyakazi pamoja na kujenga mustakbali bora, na endelevu kwa wote.
16-10-2023 • 0
FAO inasisitiza kwamba maji ni uhai, maji ni chakula tusimwache yeyote nyuma katika hili
Leo ni siku ya chakula duniani na maadhimisho ya mwaka huu kwa mujibu wa shirika na chakula na kilimo FAO yanasherehekea moja ya rasilimali muhimu zaidi kwa maisha ya binadamu ambayo ni maji, kwani yanachukua asilimia 50 ya uso wa dunia, yanazalisha chakula na kuwezesha watu kuishi. Maudhui ya siku ya mwaka huu ni “Maji ni uhai, maji ni chakula, usimwache yeyote nyuma”.Pamoja na kwamba maji ndio kila kitu FAO imekumbusha kwamba rasilimali hiyo haidumu milele na dunia inahitaji kuacha kuichukulia kama mazoea kwani chakula kinacholiwa duniani na jinsi kinavyozalishwa vinaathiri rasilimali ya maji.Hivyo shirika hilo limesisitiza kwamba dunia “Kwa pamoja tunaweza kuchukua hatua kwa ajili ya chakula na kuwa mabadiliko yanayohitajika, kwani maji ni msingi kwa ajili ya maisha na chakula.”Akisisitiza umuhimu huo mkurugenzi mkuu wa FAO Qu Dongyu (TAMKA KYU DONGYU) amesema, "Mgogoro wa madadiliko ya tabianchi, ongezoko la idadi ya watu, ukuaji wa miji, maendeleo ya viwanda na maendeleo ya kiuchumi na kijamii vinaongeza shinikizo katik rasilimali ya maji.”Na kuongeza kuwa theluthi moja ya watu wote duniani wanaishi bila rasilimali hiyo muhimu hivyo changamoto hizo zinaleta athari kubwa kwa uhakika wa chakula na ametoa wito wa kugeukia sayansi, ubunifu na teknolojia kuzitatua, “Lazima tukumbatie uwezo wa sayansi, ubunifu, takwimu na teknolojia kuzalisha zaidi kwa kutumia maji kidogo ili kufanya kila tone la maji kuwa na maana. Sote tunapswa kutumia na kudhibiti maji kwa ufanisi.”Ili kuendeleza azma hiyo ametaka sekta ya kilimo inayotumia asilimia 70 ya maji duniani kufanya mabadiliko ya mifumo yake ya chakula na ndio maana leo mjini Roma Italia FAO limenaza kongamano la siku nne litakalokamilika 20 Oktaba kujadili umuhimu wa sayansi, uvumbuzi na teknolojia katika kubadili mifumo ya chakula kuwa sehemu ya suluhu ya mabadiliko ya tabianchi.Ismahane Elouafi ni mkuu wa kitengo cha sayansi ya chakula na kilimo wa FAO anasema, “Kuanzia uvumbuzi wa teknolojia hadi uvumbuzi wa kifedha, uvumbuzi wa kitaasisi, uvumbuzi wa sera, ni katika wigo mzima wa uvumbuzi, na tunatumai kwamba mjadala kati ya wadau tofauti utaleta matokeo, je tunajua nini hadi sasa, tunaweza kuongeza nini kwa sasa na ni wapi tunapaswa kuwekeza katika siku za usoni ili kuwa na msingi bora wa sayansi na ushahidi kwa ajili ya utungaji sera na kwa ajili ya mabadiliko ya mifumo ya kilimo ya chakula.”FAO inasema kampeni ya siku ya chakula mwaka huu ni kuelimisha dunia kuhusu umuhimu wa kutumia maji kwa ufanisi kwa sababu rasilimali hiyo iko katika tishio kubwa na huu ni wakati wa kufanyakazi pamoja na kujenga mustakbali bora, na endelevu kwa wote.
16-10-2023 • 0
Tanzania tumepiga hatua kubwa kupambana na kifua kikuu: Waziri Ummy Mwalimu
Kifua kikuu au TB ni moja ya changamoto kubwa za kiafya duniani na janga ni kubwa zaidi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO duniani kote, TB ni sababu ya 13 inayoongoza kwa vifo na ya pili muuaji wa magonjwa ya kuambukiza baada ya COVID-19 ikiwa juu ya VVU na Ukimwi. Shirika hilo linakadiria kwamba mwaka 2021, takriban watu milioni 10.6 waliugua kifua kikuu kote duniani wakiwemo wanaume milioni sita, wanawake milioni 3.4 na watoto milioni 1.2. Na shirika hilo loimesisitiza kuwa TB iko katika nchi zote na inaathiri makundi ya umri wote ndio maana wakati wa mkutano mkuu wa Baraza Kuu mwezi septemba TB ilikuwa moja wa mada zilizojadiliwa kandoni na mjadala wa Baraza Kuu ukizitaka nchi kuchukua hatua kuutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030. Tanzania ilishiriki mkutano huo na waziri wake wa afya ummy Mwalimu alimweleza Flora Nducha wa idhaa hii ya Kiswahili hatua wanazochukua katika vita dhidi ya TB.
13-10-2023 • 0
Tanzania tumepiga hatua kubwa kupambana na kifua kikuu: Waziri Ummy Mwalimu
Kifua kikuu au TB ni moja ya changamoto kubwa za kiafya duniani na janga ni kubwa zaidi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO duniani kote, TB ni sababu ya 13 inayoongoza kwa vifo na ya pili muuaji wa magonjwa ya kuambukiza baada ya COVID-19 ikiwa juu ya VVU na Ukimwi. Shirika hilo linakadiria kwamba mwaka 2021, takriban watu milioni 10.6 waliugua kifua kikuu kote duniani wakiwemo wanaume milioni sita, wanawake milioni 3.4 na watoto milioni 1.2. Na shirika hilo loimesisitiza kuwa TB iko katika nchi zote na inaathiri makundi ya umri wote ndio maana wakati wa mkutano mkuu wa Baraza Kuu mwezi septemba TB ilikuwa moja wa mada zilizojadiliwa kandoni na mjadala wa Baraza Kuu ukizitaka nchi kuchukua hatua kuutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030. Tanzania ilishiriki mkutano huo na waziri wake wa afya ummy Mwalimu alimweleza Flora Nducha wa idhaa hii ya Kiswahili hatua wanazochukua katika vita dhidi ya TB.
13-10-2023 • 0
Raia katika ukanda wa Gaza hawana pa kukimbilia, milioni 1 waambiwa waondoke ndani ya saa 24: UN
Leo ni siku nyingine ambapo hali imeendelea kuwa tete na mbayá zaidi kwenye Ukanda wa Gaza, kwani Israel imetangaza watu wote wanaoishi katika eneo la Kaskazini mwa Wadi Gaza kuondoka na kwenda Kusini mwa Gaza ndani ya saa 24 na hivyo kuwaacha njiapanda maelfu kwa maelfu ya watu wanaoishi eneo hilo yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo ambayo yanahaha kuwasaidia na kuwanusuru watu hao. Umoja wa Mataifa umesema amri hiyo ya watu kuondona inawaathiri zaidi ya Wapalestina milioni moja wakiwemo watoto, wazee na wagonjwa ikiwalazimisha kuhamia kwingine wakati hawana chochote na hata usafiri, pia kukiwa na hakikisho dogo sana kwa ajili ya usalama wao wakati mashambulizi yakiendelea.Umoja wa Mataifa unasema unadhani itakuwa vigumu sana kuendesha shughuli hiyo ya kuhama bila kuleta madhara makubwa ya kibinadamu, hivyo umeto ombi la kufuta amri hiyo ili kuepuka zahma kubwa zaidi katika hali ambayo tayari ni mbayá.Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ametoa wito kwa mataifa yote kusisitiza na kuzisaidia pande kinzani katika mzozo kutekeleza utoaji mwanya wa fursa ya misaada ya kibinadamu ili kuhakikisha msaada unaohitajika haraka unawafikia wenye uhitaji.Pia ameonya kwamba katika nchi nyingi hivi sasa kumekuwa na ongezeko la chuki dhidi ya Wayahudi na kauli za chuki dhidi ya Uislam amelaani vikali hayo.Ndani ya Gaza kamisha mkuu wa shirika laumoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA Philippe Lazzarini amezitaka pande zote na wale wenye ushawishi juu ya pande hizo kukomesha madhila yanayoendelea na kuhakikisha msaada na ulinzi kwa raia wote.Amesisitiza kwamba amri iliyotangazwa na Israel kutaka zaidi ya watu milioni moja kuondoka” Hii itasababisha janga kubwa ambalo halijawahi kushuhudiwa na kuwasukuma zaidi jehanamu watu wa Gaza.”Ili kutoa msaada ipasavyo Umoja wa Mataifa unasema fedha zinahitajika ndio maana leo shirika lake la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limezindua ombi la dola milioni 249 kwa ajili ya washirika wake wa kibinadamu 77 watakaokuwa wakihudumia mahitaji ya haraka ya watu milioni 1.26 Gaza na kwenye Ukingo wa Magharibi.Na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeonya kuhusu vifo, majeruhi na machungu wanayopitia watoto wasio na hatia katika mzozo huu , huku lile la afya duniani WHO likisema mfumo wa afya Gaza hauana uwezo tena wa kutoa huduma zinazohitajika hasa kutokana na hospital nyingi kusambaratishwa na makombora na kutokuwa na vifaa vinavyohitajika.Wito wa mashirika haya ni mmoja tu, mgogoro huu lazima ukome mara moja kunusuru maisha ya raia wa pande zote mbili.
13-10-2023 • 0
Raia katika ukanda wa Gaza hawana pa kukimbilia, milioni 1 waambiwa waondoke ndani ya saa 24: UN
Leo ni siku nyingine ambapo hali imeendelea kuwa tete na mbayá zaidi kwenye Ukanda wa Gaza, kwani Israel imetangaza watu wote wanaoishi katika eneo la Kaskazini mwa Wadi Gaza kuondoka na kwenda Kusini mwa Gaza ndani ya saa 24 na hivyo kuwaacha njiapanda maelfu kwa maelfu ya watu wanaoishi eneo hilo yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo ambayo yanahaha kuwasaidia na kuwanusuru watu hao. Umoja wa Mataifa umesema amri hiyo ya watu kuondona inawaathiri zaidi ya Wapalestina milioni moja wakiwemo watoto, wazee na wagonjwa ikiwalazimisha kuhamia kwingine wakati hawana chochote na hata usafiri, pia kukiwa na hakikisho dogo sana kwa ajili ya usalama wao wakati mashambulizi yakiendelea.Umoja wa Mataifa unasema unadhani itakuwa vigumu sana kuendesha shughuli hiyo ya kuhama bila kuleta madhara makubwa ya kibinadamu, hivyo umeto ombi la kufuta amri hiyo ili kuepuka zahma kubwa zaidi katika hali ambayo tayari ni mbayá.Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ametoa wito kwa mataifa yote kusisitiza na kuzisaidia pande kinzani katika mzozo kutekeleza utoaji mwanya wa fursa ya misaada ya kibinadamu ili kuhakikisha msaada unaohitajika haraka unawafikia wenye uhitaji.Pia ameonya kwamba katika nchi nyingi hivi sasa kumekuwa na ongezeko la chuki dhidi ya Wayahudi na kauli za chuki dhidi ya Uislam amelaani vikali hayo.Ndani ya Gaza kamisha mkuu wa shirika laumoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA Philippe Lazzarini amezitaka pande zote na wale wenye ushawishi juu ya pande hizo kukomesha madhila yanayoendelea na kuhakikisha msaada na ulinzi kwa raia wote.Amesisitiza kwamba amri iliyotangazwa na Israel kutaka zaidi ya watu milioni moja kuondoka” Hii itasababisha janga kubwa ambalo halijawahi kushuhudiwa na kuwasukuma zaidi jehanamu watu wa Gaza.”Ili kutoa msaada ipasavyo Umoja wa Mataifa unasema fedha zinahitajika ndio maana leo shirika lake la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limezindua ombi la dola milioni 249 kwa ajili ya washirika wake wa kibinadamu 77 watakaokuwa wakihudumia mahitaji ya haraka ya watu milioni 1.26 Gaza na kwenye Ukingo wa Magharibi.Na shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limeonya kuhusu vifo, majeruhi na machungu wanayopitia watoto wasio na hatia katika mzozo huu , huku lile la afya duniani WHO likisema mfumo wa afya Gaza hauana uwezo tena wa kutoa huduma zinazohitajika hasa kutokana na hospital nyingi kusambaratishwa na makombora na kutokuwa na vifaa vinavyohitajika.Wito wa mashirika haya ni mmoja tu, mgogoro huu lazima ukome mara moja kunusuru maisha ya raia wa pande zote mbili.
13-10-2023 • 0
13 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia athari za majanga na ujumuishwaji katika utoaji wa maonyo ya mapema, na pia machafuko mashariki ya kati. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunasalia hapa makau makuu, kulikoni?Leo ni siku nyingine ambapo hali imeendelea kuwa tete na mbayá zaidi kwenye Ukanda wa Gaza, kwani Israel imetangaza watu wote wanaoishi katika eneo la Kaskazini mwa Wadi Gaza kuondoka na kwenda Kusini mwa Gaza ndani ya saa 24 na hivyo kuwaacha njiapanda maelfu kwa maelfu ya watu wanaoishi eneo hilo yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo ambayo yanahaha kuwasaidia na kuwanusuru watu hao. Ufilipino ni mojawapo ya nchi zinazokabiliwa zaidi na hatari za majanga duniani, jimboni Samar Kaskazini, hatari kwa watoto ni kubwa zaidi ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linafanya kazi na serikali za mtaa ili kuwashirikisha watoto na vijana katika hatua za kujiandaa na hatari pamoja na kupunguza athari za majanga. Makala leo inamulika jitihada za kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu au TB nchini Tanzania.Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO watu milioni 10.6 walikufa kwa TB mwaka 2021 na nchi za afrika Kusini mwa janga la Sahara ndizo zinazobeba mzigo mkubwa wa ugonjwa hu. Flora Nducha wa Idhaa akizungumza na waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu wakati wa mkutano kuhusu kifua kuu kandoni ya mjada mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba alitaka kufahamu nchi hiyo inafanya nini kutokomeza TB ifikapo 2030.Na mashinani tunakuletea ujumbe kuhusu athari za majanga kwa watu wasiojiweza..Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu !
13-10-2023 • 0
13 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia athari za majanga na ujumuishwaji katika utoaji wa maonyo ya mapema, na pia machafuko mashariki ya kati. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunasalia hapa makau makuu, kulikoni?Leo ni siku nyingine ambapo hali imeendelea kuwa tete na mbayá zaidi kwenye Ukanda wa Gaza, kwani Israel imetangaza watu wote wanaoishi katika eneo la Kaskazini mwa Wadi Gaza kuondoka na kwenda Kusini mwa Gaza ndani ya saa 24 na hivyo kuwaacha njiapanda maelfu kwa maelfu ya watu wanaoishi eneo hilo yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo ambayo yanahaha kuwasaidia na kuwanusuru watu hao. Ufilipino ni mojawapo ya nchi zinazokabiliwa zaidi na hatari za majanga duniani, jimboni Samar Kaskazini, hatari kwa watoto ni kubwa zaidi ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linafanya kazi na serikali za mtaa ili kuwashirikisha watoto na vijana katika hatua za kujiandaa na hatari pamoja na kupunguza athari za majanga. Makala leo inamulika jitihada za kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu au TB nchini Tanzania.Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO watu milioni 10.6 walikufa kwa TB mwaka 2021 na nchi za afrika Kusini mwa janga la Sahara ndizo zinazobeba mzigo mkubwa wa ugonjwa hu. Flora Nducha wa Idhaa akizungumza na waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu wakati wa mkutano kuhusu kifua kuu kandoni ya mjada mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba alitaka kufahamu nchi hiyo inafanya nini kutokomeza TB ifikapo 2030.Na mashinani tunakuletea ujumbe kuhusu athari za majanga kwa watu wasiojiweza..Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu !
13-10-2023 • 0
Tushirikishe watoto katika kujiandaa na athari za majanga unamanufaa - UNICEF
Ufilipino ni mojawapo ya nchi zinazokabiliwa zaidi na hatari za majanga duniani, jimboni Samar Kaskazini, hatari kwa watoto ni kubwa zaidi ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linafanya kazi na serikali za mtaa ili kuwashirikisha watoto na vijana katika hatua za kujiandaa na hatari pamoja na kupunguza athari za majanga kama anavyotujuza Leah Mushi katika taarifa hii aliyotuandalia.Manispaa ya Mapanas iliyoko jimboni Samar Kaskazini nchini Ufilipino kutokana na kuathirika mara kwa mara na vimbunga pamoja na dhoruba mwaka 2014 UNICEF na Kituo cha Kukabiliana na Majanga kwa wananchi walizindua kituo cha Kupunguza Hatari za Majanga kwa Watoto- CCDRR. Gary Lavin ni Makamu Ganava wa jimbo la Samar Kaskazini anasema lengo la kituo hicho ni kuwajengea watoto na vijana uelewa kuhusu majanga na kuwashirikisha katika kusaka majawabu wakati wa majanga. “Lazima tuwalinde watoto na vijana kwa mustakabali si wa jamii yetu na jimbo letu pekee, bali taifa zima ndio maana tunatakiwa kuhakikisha wanakuwa salama wakati wa majanga na wanapewa ulinzi unaostahili.”Kituo hicho kinawafundisha hatua kwa hatua namna ya kupunguza athari za majanga kama anavyoeleza Faye Anne Bandilla Rais wa Kituo hicho ambaye pia ni kijana. Faye Anne Bandilla – Msichana “Kituo hiki kinahusishwa watoto na vijana kuanzia kwenye ngazi zote kuanzia kwenye kupanga, kwasababu kuna hatari ambazo watoto wanaziana lakini watu wazima hawazioni” Kupitia Program hiyo inayofadhiliwa na UNICEF shule pia zilifundishwa namna ya kuunganisha kujikinga na majanga kwenye mitaala yao kama anavyoeleza mwalimu Mayla Bricio. “Programu ya Kupunguza Hatari za Majanga kwa Watoto ilipokuja tulianza kuunganisha kujiandaa na majanga katika karibu masomo yote. Kwakufanya hivyo tunahakikisha kwamba kila mtoto anajua jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya majanga.”Kupitia shirika lisilo la kiserikali la KKK watoto na vijana walihamasishwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kupunguza maafa ikiwemo upandaji miti na kuandaa ramani shirikishi 3D Mapping ambayo inaeleza waende wapi na wafanye nini majanga yanapotokea.Vijana pia wamepata nafasi katika Baraza la Manispaa, wanapaza sauti zao kueleza nini wanahitaji na hii imewezesha manispaa kutekeleza mahitaji yao na kutunga sera zenye kuzingatia mahitaji ya watoto na vijana. Jolan Baguo ni kijana mwanachama wa KKK na anasema …. “Kabla ya programu hii, majanga yalipotokea tulikuwa tunakimbilia kwenye vituo vya kujiokoa tukiwa na wasiwasi bila ya kujua tutafanya nini, lakini baada ya CCDRR hatimaye nikawa mmoja wa vijana waliowezesha kuwahamisha watu na kuwaweka maeneo salama.”Programu hii iliyowezeshwa na UNICEF imethibitisha umuhimu wa ushirikishaji wa jamii nzima kwenye kila ngazi ya maamuzi na kubwa zaidi imetengenezwa kwa namna ambayo hata uongozi wa kisiasa ukibadilika na ufadhili wa programu ukiisha bado watoto na vijana wataendelea kushiriki kwenye kufanya maamuzi kwa masuala yahusuyo maslahi yao.
13-10-2023 • 0
Tushirikishe watoto katika kujiandaa na athari za majanga unamanufaa - UNICEF
Ufilipino ni mojawapo ya nchi zinazokabiliwa zaidi na hatari za majanga duniani, jimboni Samar Kaskazini, hatari kwa watoto ni kubwa zaidi ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linafanya kazi na serikali za mtaa ili kuwashirikisha watoto na vijana katika hatua za kujiandaa na hatari pamoja na kupunguza athari za majanga kama anavyotujuza Leah Mushi katika taarifa hii aliyotuandalia.Manispaa ya Mapanas iliyoko jimboni Samar Kaskazini nchini Ufilipino kutokana na kuathirika mara kwa mara na vimbunga pamoja na dhoruba mwaka 2014 UNICEF na Kituo cha Kukabiliana na Majanga kwa wananchi walizindua kituo cha Kupunguza Hatari za Majanga kwa Watoto- CCDRR. Gary Lavin ni Makamu Ganava wa jimbo la Samar Kaskazini anasema lengo la kituo hicho ni kuwajengea watoto na vijana uelewa kuhusu majanga na kuwashirikisha katika kusaka majawabu wakati wa majanga. “Lazima tuwalinde watoto na vijana kwa mustakabali si wa jamii yetu na jimbo letu pekee, bali taifa zima ndio maana tunatakiwa kuhakikisha wanakuwa salama wakati wa majanga na wanapewa ulinzi unaostahili.”Kituo hicho kinawafundisha hatua kwa hatua namna ya kupunguza athari za majanga kama anavyoeleza Faye Anne Bandilla Rais wa Kituo hicho ambaye pia ni kijana. Faye Anne Bandilla – Msichana “Kituo hiki kinahusishwa watoto na vijana kuanzia kwenye ngazi zote kuanzia kwenye kupanga, kwasababu kuna hatari ambazo watoto wanaziana lakini watu wazima hawazioni” Kupitia Program hiyo inayofadhiliwa na UNICEF shule pia zilifundishwa namna ya kuunganisha kujikinga na majanga kwenye mitaala yao kama anavyoeleza mwalimu Mayla Bricio. “Programu ya Kupunguza Hatari za Majanga kwa Watoto ilipokuja tulianza kuunganisha kujiandaa na majanga katika karibu masomo yote. Kwakufanya hivyo tunahakikisha kwamba kila mtoto anajua jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya majanga.”Kupitia shirika lisilo la kiserikali la KKK watoto na vijana walihamasishwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kupunguza maafa ikiwemo upandaji miti na kuandaa ramani shirikishi 3D Mapping ambayo inaeleza waende wapi na wafanye nini majanga yanapotokea.Vijana pia wamepata nafasi katika Baraza la Manispaa, wanapaza sauti zao kueleza nini wanahitaji na hii imewezesha manispaa kutekeleza mahitaji yao na kutunga sera zenye kuzingatia mahitaji ya watoto na vijana. Jolan Baguo ni kijana mwanachama wa KKK na anasema …. “Kabla ya programu hii, majanga yalipotokea tulikuwa tunakimbilia kwenye vituo vya kujiokoa tukiwa na wasiwasi bila ya kujua tutafanya nini, lakini baada ya CCDRR hatimaye nikawa mmoja wa vijana waliowezesha kuwahamisha watu na kuwaweka maeneo salama.”Programu hii iliyowezeshwa na UNICEF imethibitisha umuhimu wa ushirikishaji wa jamii nzima kwenye kila ngazi ya maamuzi na kubwa zaidi imetengenezwa kwa namna ambayo hata uongozi wa kisiasa ukibadilika na ufadhili wa programu ukiisha bado watoto na vijana wataendelea kushiriki kwenye kufanya maamuzi kwa masuala yahusuyo maslahi yao.
13-10-2023 • 0
METHALI: SHIMO LA ULIMI MKONO HAUFUTIKI
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali Jino la P Na leo katika kujifunza lugha ya kiswahili tunakuletea maana ya methali methali SHIMO LA ULIMI MKONO HAUFUTIKI, KARIBU!
12-10-2023 • 0
METHALI: SHIMO LA ULIMI MKONO HAUFUTIKI
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali Jino la P Na leo katika kujifunza lugha ya kiswahili tunakuletea maana ya methali methali SHIMO LA ULIMI MKONO HAUFUTIKI, KARIBU!
12-10-2023 • 0
12 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunaangazia moja ya miradi ya Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) unaotelelezwa katika kisiwa cha Pemba nchini Tanzania. Evarist Mapesa anatupitisha katika Bahari ya Hindi hadi visiwani humo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na kataika kujifunza lugha ya Kiswahili leo tunakuletea maana ya methali methali SHIMO LA ULIMI MKONO HAUFUTIKI.Hii leo ikiwa ni siku ya 6 ya mapigano huko Mashriki ya Kati, kati ya Israeli na Palestina idadi ya waliouawa upande wa Palestina inatajwa kuwa ni 1,100 ihali Israeli ni 1,200, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, likiongeza kuwa miongoni mwa waliouawa ni wafanyakazi wake 12.Tukisalia huko Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP linasema kuna hatari ya eneo hilo kukosa chakula, maji, umeme na vifaa muhimu kutokana na ukata, hivyo usaidizi wa kifedha kwa shirika hilo unahitajika. Tayari WFP na UNRWA wamesambaza mikate, na chakula kwa wakimbizi 137,000 wanaoishi kwenye makazi ya muda, na mpango ni kufikia watu 800,000 katika eneo lote la Palestina.Na huko nchini Tanzania kuelekea siku ya chakula duniani tarehe 16 mwezi huu wa Oktoba, shirika la Umoja wa Mataifa chakula na kilimo, FAO limeanza kuelimisha watoto kuhusu lishe bora kupitia mafunzo ya mapishi, Alfonsina Paul ni miongoni mwa wanafunzi walionufaika na na ujumbe.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali Jino la P Na leo katika kujifunza lugha ya kiswahili tunakuletea maana ya methali methali SHIMO LA ULIMI MKONO HAUFUTIKI.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
12-10-2023 • 0
12 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunaangazia moja ya miradi ya Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) unaotelelezwa katika kisiwa cha Pemba nchini Tanzania. Evarist Mapesa anatupitisha katika Bahari ya Hindi hadi visiwani humo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na kataika kujifunza lugha ya Kiswahili leo tunakuletea maana ya methali methali SHIMO LA ULIMI MKONO HAUFUTIKI.Hii leo ikiwa ni siku ya 6 ya mapigano huko Mashriki ya Kati, kati ya Israeli na Palestina idadi ya waliouawa upande wa Palestina inatajwa kuwa ni 1,100 ihali Israeli ni 1,200, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, likiongeza kuwa miongoni mwa waliouawa ni wafanyakazi wake 12.Tukisalia huko Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP linasema kuna hatari ya eneo hilo kukosa chakula, maji, umeme na vifaa muhimu kutokana na ukata, hivyo usaidizi wa kifedha kwa shirika hilo unahitajika. Tayari WFP na UNRWA wamesambaza mikate, na chakula kwa wakimbizi 137,000 wanaoishi kwenye makazi ya muda, na mpango ni kufikia watu 800,000 katika eneo lote la Palestina.Na huko nchini Tanzania kuelekea siku ya chakula duniani tarehe 16 mwezi huu wa Oktoba, shirika la Umoja wa Mataifa chakula na kilimo, FAO limeanza kuelimisha watoto kuhusu lishe bora kupitia mafunzo ya mapishi, Alfonsina Paul ni miongoni mwa wanafunzi walionufaika na na ujumbe.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali Jino la P Na leo katika kujifunza lugha ya kiswahili tunakuletea maana ya methali methali SHIMO LA ULIMI MKONO HAUFUTIKI.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
12-10-2023 • 0
Usambazaji wa misaada ya chakula kwa wahitaji Gaza umeanza - WFP
Ikiwa leo ni siku ya tano ya mzozo kati ya Israeli na Palestina huko Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan, mashirika ya Umoja wa Mataifa yamepiga kambi kuhakikisha yanafikisha misaada kwa wahitaji wakati huu ambapo mapigano hayo yamefurusha takribani watu 246, 000 kutoka ukanda wa Gaza pekee. Mashirika hayo ni pamoja na lile la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP ambalo limeanza kugawa mikate, vyakula vya makopo na vingine vilivyo tayari kuliwa kwa takribani watu 100,000 waliosaka hifadhi kwenye maeneo ya hifadhi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA huko Gaza. Lengo la UNRWA ni kwamba operesheni hii ya dharura ifikishe misaada kwa zaidi ya watu 800,000. Ikumbukwe kuwa idadi hii ni pamoja na wakimbizi wa zamani waliokuwa wanahifadhiwa na UNRWA.Mkurugenzi Mkazi wa WFP huko Palestina Samer Abdeljaber anasema tuko hapa kwenye enep na tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha wahitaji waliofurushwa makwao ambao wanaishi kwenye makazi ya muda wanapata chakula na msaada wanaohitaji ili waweze kuishi. Tutaanza pia kutoka vocha za fedha ili watu waweze kununua chakula kutoka kwenye maduka yaliyo bado wazi.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nalo pia liko Gaza likisambaza misaada ya kiutu.WFP inasihi pande kinzani kuhakikisha njia za usambazaji chakula ziko wazi ili misaada ifikie wahitaji huku ikitoa ombi la dola milioni 17.3 ili kufanikisha operesheni zake za dharura kwa wiki nne zijazo kwani mzozo huu umelipuka wakati tayari ukata ulikuwa unalikabili na kulazimu mwezi Juni kukata misaada kwa maelfu ya familia za kipalestina zisizo na uwezo.Wakati huo huo UNRWA kupitia mtandao wa X inasema tangu Jumamosi hadi hii leo watumishi wake 9 wameuawa kwenye mashambulizi hayo huko Gaza.
11-10-2023 • 0
Usambazaji wa misaada ya chakula kwa wahitaji Gaza umeanza - WFP
Ikiwa leo ni siku ya tano ya mzozo kati ya Israeli na Palestina huko Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan, mashirika ya Umoja wa Mataifa yamepiga kambi kuhakikisha yanafikisha misaada kwa wahitaji wakati huu ambapo mapigano hayo yamefurusha takribani watu 246, 000 kutoka ukanda wa Gaza pekee. Mashirika hayo ni pamoja na lile la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP ambalo limeanza kugawa mikate, vyakula vya makopo na vingine vilivyo tayari kuliwa kwa takribani watu 100,000 waliosaka hifadhi kwenye maeneo ya hifadhi ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA huko Gaza. Lengo la UNRWA ni kwamba operesheni hii ya dharura ifikishe misaada kwa zaidi ya watu 800,000. Ikumbukwe kuwa idadi hii ni pamoja na wakimbizi wa zamani waliokuwa wanahifadhiwa na UNRWA.Mkurugenzi Mkazi wa WFP huko Palestina Samer Abdeljaber anasema tuko hapa kwenye enep na tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha wahitaji waliofurushwa makwao ambao wanaishi kwenye makazi ya muda wanapata chakula na msaada wanaohitaji ili waweze kuishi. Tutaanza pia kutoka vocha za fedha ili watu waweze kununua chakula kutoka kwenye maduka yaliyo bado wazi.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nalo pia liko Gaza likisambaza misaada ya kiutu.WFP inasihi pande kinzani kuhakikisha njia za usambazaji chakula ziko wazi ili misaada ifikie wahitaji huku ikitoa ombi la dola milioni 17.3 ili kufanikisha operesheni zake za dharura kwa wiki nne zijazo kwani mzozo huu umelipuka wakati tayari ukata ulikuwa unalikabili na kulazimu mwezi Juni kukata misaada kwa maelfu ya familia za kipalestina zisizo na uwezo.Wakati huo huo UNRWA kupitia mtandao wa X inasema tangu Jumamosi hadi hii leo watumishi wake 9 wameuawa kwenye mashambulizi hayo huko Gaza.
11-10-2023 • 0
11 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko mashariki ya kati, na mradi wa maji Baringo nchini Kenya. Makala tunakuletea uchambuzi wa Ibara ya 10 ya tamko la haki za binadamu na mashinani tunamulika siku ya mtoto wa kike duniani inayoadhimishwa kila mwaka Oktoba 11 kila mwaka ambayo ni leo. Ikiwa leo ni siku ya tano ya mzozo kati ya Israeli na Palestina huko Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan, mashirika ya Umoja wa Mataifa yamepiga kambi kuhakikisha yanafikisha misaada kwa wahitaji wakati huu ambapo mapigano hayo yamefurusha takribani watu 246, 000 kutoka ukanda wa Gaza pekee..Uhakika wa upatikanaji wa maji ni moja ya majawabu ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi hususan katika maeneo yanayokabiliwa na ukame. Ni kwa kutambua hilo, huko nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP kwa kushirikiana na serikali wamewezesha wananchi wa kaunti ya Baringo kuondokana na adha ya maji..Makala leo inaangaza Ibara ya 10 ya tamko la haki za binadamu. Je ibara hiyo inasema nini? Na Inatekelezwa ipasavyo hasa barani Afrika? Kujibu maswali hayo Pamela Awuori wa Idhaa hii amezungumza na wakili wa mahakama kuu ya Kenya Kevin Ngetich.Katika mashinani tunamulika siku ya mtoto wa kike duniani inayoadhimishwa kila mwaka Oktoba 11 kila mwaka ambayo ni leo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
11-10-2023 • 0
11 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko mashariki ya kati, na mradi wa maji Baringo nchini Kenya. Makala tunakuletea uchambuzi wa Ibara ya 10 ya tamko la haki za binadamu na mashinani tunamulika siku ya mtoto wa kike duniani inayoadhimishwa kila mwaka Oktoba 11 kila mwaka ambayo ni leo. Ikiwa leo ni siku ya tano ya mzozo kati ya Israeli na Palestina huko Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan, mashirika ya Umoja wa Mataifa yamepiga kambi kuhakikisha yanafikisha misaada kwa wahitaji wakati huu ambapo mapigano hayo yamefurusha takribani watu 246, 000 kutoka ukanda wa Gaza pekee..Uhakika wa upatikanaji wa maji ni moja ya majawabu ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi hususan katika maeneo yanayokabiliwa na ukame. Ni kwa kutambua hilo, huko nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP kwa kushirikiana na serikali wamewezesha wananchi wa kaunti ya Baringo kuondokana na adha ya maji..Makala leo inaangaza Ibara ya 10 ya tamko la haki za binadamu. Je ibara hiyo inasema nini? Na Inatekelezwa ipasavyo hasa barani Afrika? Kujibu maswali hayo Pamela Awuori wa Idhaa hii amezungumza na wakili wa mahakama kuu ya Kenya Kevin Ngetich.Katika mashinani tunamulika siku ya mtoto wa kike duniani inayoadhimishwa kila mwaka Oktoba 11 kila mwaka ambayo ni leo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
11-10-2023 • 0
Wenyeji Baringo nchini Kenya wanufaika kufuatia mradi wa maji wa WFP
Uhakika wa upatikanaji wa maji ni moja ya suluhisho za kupambana na mabadiliko ya tabianchi hususan katika maeneo yanayokabiliwa na ukame. Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP kwakushirikiana na serikali wamewezesha wananchi wa kaunti ya Baringo kuondokana na adha ya maji. Kwa miaka takriban 40 wananchi wa Kaunti ya Baringo nchini Kenya wamekuwa wakitaabika na uhaba wa maji kutokana na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Hali hiyo imewafanya wananchi hao kuwa tegemezi wa chakula kwa kwakuwa wamekosa maji ya kulisha mifugo yao na kilimo. Kutokana na adha hiyo WFP kwa kushirikiana na wadau wake na serikali ya Kenya imetekeleza mradi wa kuchimba visima mradi ambao Naibu gavana wa kaunti ya Baringo Felix Kimaiyo anasema unaenda kubadili maisha ya wananchi. “Mradi huu utakuwa muhimu sana kwa sababu unaenda kugusa maisha ya watu hawa na kuweza kupunguza maswala mengi na kuhakikisha kuwa eneo hili kuna uhakika wa upatikanaji wa chakula”Naam, na WFP mpaka sasa imefanikisha kuchimba visima 74 na vingine 22 vikiendelea kuchimvwa. Na mabadiliko yanaonekana kwani mifugo imepata maji, kilimo cha umwagiliaji kinaendelea na matumizi mengine ya majumbani pamoja na shuleni kama anavyothibitisha Lilian Ruto Mkazi wa Kijiji cha Kapkut ambaye pia ni mkulima wa mbogamboga wa kikundi cha kina mama wa Eitui. “Mahali tulikuwa tunatoa maji kulikuwa mbali sana na ilikuwa inatuchukua muda ili uweze kufikisha maji nyumbani ndio uende kuendelea na kazi zako za nyumbani. Kwahiyo tunashukuru sana kwasababu maji yamefika.“ Bi.Ruto anasema sasa hawategemeai tena chakula cha msaada kwani wanaweza kulima wenyewe na lishe za watoto wao zimeimarika. “Sasa kwasababu tumepata maji tunajua sasa tuta tengeneza bustani tupande vyakula vyenye lishe ili kuhakikisha watoto wetu wanapata lishe bora.”WFP inafanya kazi kwa karibu na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa ikiwemo UNICEF, UNEP, FAO na IFAD kuhamasisha matumizi bora ya maji kwa afya, uhakika wa upatikanaji wa chakula na ustawi bora wa maisha yao.
11-10-2023 • 0
Wenyeji Baringo nchini Kenya wanufaika kufuatia mradi wa maji wa WFP
Uhakika wa upatikanaji wa maji ni moja ya suluhisho za kupambana na mabadiliko ya tabianchi hususan katika maeneo yanayokabiliwa na ukame. Nchini Kenya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani WFP kwakushirikiana na serikali wamewezesha wananchi wa kaunti ya Baringo kuondokana na adha ya maji. Kwa miaka takriban 40 wananchi wa Kaunti ya Baringo nchini Kenya wamekuwa wakitaabika na uhaba wa maji kutokana na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Hali hiyo imewafanya wananchi hao kuwa tegemezi wa chakula kwa kwakuwa wamekosa maji ya kulisha mifugo yao na kilimo. Kutokana na adha hiyo WFP kwa kushirikiana na wadau wake na serikali ya Kenya imetekeleza mradi wa kuchimba visima mradi ambao Naibu gavana wa kaunti ya Baringo Felix Kimaiyo anasema unaenda kubadili maisha ya wananchi. “Mradi huu utakuwa muhimu sana kwa sababu unaenda kugusa maisha ya watu hawa na kuweza kupunguza maswala mengi na kuhakikisha kuwa eneo hili kuna uhakika wa upatikanaji wa chakula”Naam, na WFP mpaka sasa imefanikisha kuchimba visima 74 na vingine 22 vikiendelea kuchimvwa. Na mabadiliko yanaonekana kwani mifugo imepata maji, kilimo cha umwagiliaji kinaendelea na matumizi mengine ya majumbani pamoja na shuleni kama anavyothibitisha Lilian Ruto Mkazi wa Kijiji cha Kapkut ambaye pia ni mkulima wa mbogamboga wa kikundi cha kina mama wa Eitui. “Mahali tulikuwa tunatoa maji kulikuwa mbali sana na ilikuwa inatuchukua muda ili uweze kufikisha maji nyumbani ndio uende kuendelea na kazi zako za nyumbani. Kwahiyo tunashukuru sana kwasababu maji yamefika.“ Bi.Ruto anasema sasa hawategemeai tena chakula cha msaada kwani wanaweza kulima wenyewe na lishe za watoto wao zimeimarika. “Sasa kwasababu tumepata maji tunajua sasa tuta tengeneza bustani tupande vyakula vyenye lishe ili kuhakikisha watoto wetu wanapata lishe bora.”WFP inafanya kazi kwa karibu na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa ikiwemo UNICEF, UNEP, FAO na IFAD kuhamasisha matumizi bora ya maji kwa afya, uhakika wa upatikanaji wa chakula na ustawi bora wa maisha yao.
11-10-2023 • 0
10 OKTOBA 2023
Ungana na Leah Mushi kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo hii leo ikiwa ni siku ya Kimataifa ya Afya ya Akili Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limehimiza serikali na jamii kuhakikisha wanalinda haki za wale wanao ugua afya ya akili na pia kulinda jamii isiathirike na hatari za afya ya akili. Pia utasikia habari kwa ufupi zikijikita katika vita inayoendelea mashariki ya kati na kuna ujumbe uliotolewa na mashirika matano ya Umoja wa Mataifa. Mashinani hii leo tunakupeleka nchini Sudan kuona mradi wa maji safi na salama ulivyowanufaisha wananchi wana Puntland.
10-10-2023 • 0
10 OKTOBA 2023
Ungana na Leah Mushi kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo hii leo ikiwa ni siku ya Kimataifa ya Afya ya Akili Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limehimiza serikali na jamii kuhakikisha wanalinda haki za wale wanao ugua afya ya akili na pia kulinda jamii isiathirike na hatari za afya ya akili. Pia utasikia habari kwa ufupi zikijikita katika vita inayoendelea mashariki ya kati na kuna ujumbe uliotolewa na mashirika matano ya Umoja wa Mataifa. Mashinani hii leo tunakupeleka nchini Sudan kuona mradi wa maji safi na salama ulivyowanufaisha wananchi wana Puntland.
10-10-2023 • 0
UPU na harakati za kusaidia nchini kusongesha posta za kidijitali
Leo ni siku ya posta duniani ambapo maudhui ni Pamoja kwa kuaminiana:Ushirikiano kwa mustakabali salama na uliounganika. Lengo la maudhui hay ani kuchagiza serikali na huduma zao za posta kusaidia maendeleo ya posta ya kidijitali ambayo itaboresha mtandao wa kale wa posta ulioendelezwa karne na karne, ukihitaji kwa kiasi kikubwa mtoa huduma na mhudumiwa kuonana uso kwa uso, jambo ambalo sasa kwa kiasi kikubwa limebadilika, huduma za posta mtandao zikichukua fursa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU linataka ofisi za posta zichochee uchumi wa kidijitali. Katika kufahamu UPU inafanya nini kusongesha hilo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika hilo, Mutua Muthusi anazungumza na Evarist Mapesa wa Idhaa hii na anaanza kwa kuelezea hali ya huduma ya posta hususan katika nchi zinazoendelea au maskini katika zama za sasa za maendeleo ya kidijitali. Mahojiano haya yamefanikishwa na Kayla Redstone wa UPU.
9-10-2023 • 0
UPU na harakati za kusaidia nchini kusongesha posta za kidijitali
Leo ni siku ya posta duniani ambapo maudhui ni Pamoja kwa kuaminiana:Ushirikiano kwa mustakabali salama na uliounganika. Lengo la maudhui hay ani kuchagiza serikali na huduma zao za posta kusaidia maendeleo ya posta ya kidijitali ambayo itaboresha mtandao wa kale wa posta ulioendelezwa karne na karne, ukihitaji kwa kiasi kikubwa mtoa huduma na mhudumiwa kuonana uso kwa uso, jambo ambalo sasa kwa kiasi kikubwa limebadilika, huduma za posta mtandao zikichukua fursa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU linataka ofisi za posta zichochee uchumi wa kidijitali. Katika kufahamu UPU inafanya nini kusongesha hilo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika hilo, Mutua Muthusi anazungumza na Evarist Mapesa wa Idhaa hii na anaanza kwa kuelezea hali ya huduma ya posta hususan katika nchi zinazoendelea au maskini katika zama za sasa za maendeleo ya kidijitali. Mahojiano haya yamefanikishwa na Kayla Redstone wa UPU.
9-10-2023 • 0
Mashirika ya kibinadamu nayo yanahitaji msaada ili kusaidia wakimbizi wa Armenia
Mashirika ya kibinadamu nayo yanahitaji msaada ili kusaidia wakimbizi wa Armenia Ili kuhakikisha mahitaji ya muda mfupi, kati na ya muda mrefu yanatimizwa, mashirika ya kibinadamu yanaendelea kuhaha kutafuta ufadhili wa haraka ili kuongeza msaada kwa zaidi ya wakimbizi 100,000 nchini Armenia waliokimbia eneo la Karabhak kufuatia kuongezeka kwa uhasama mwezi Septemba. Anold Kayanda na maelezo zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linaeleza kuwa takribani wakimbizi 100,000 waliwasili Armenia ndani ya muda wa chini ya wiki moja kufuatia kuongezeka kwa uhasama unaoendelea kwenye eneo la Karabakh linalogombaniwa na Armenia na Azerbaijan huko barani Asia.UNHCR inasema miongoni mwa wakimbizi wapya waliowasili, ni watoto wapatao 30,000 na watu wengi wenye uhitaji ikiwa ni pamoja na wazee, wanawake wajawazito, watu wenye ulemavu na wengine wenye magonjwa ya kudumu. Zaidi ya nusu ya wakimbizi ni wanawake na wasichana.Huyu ni Vika, mmoja wa wakimbizi anasema, (Sauti ya Vika) – Evarist/sauti ya kike“Hali yetu hapa si ya uhakika. Huko, nilikuwa nikifanya kazi shuleni, nilikuwa muuguzi pale. Kila kitu kilikuwa kikienda sawa, tulikuwa tukiishi na wazazi wangu baada ya kifo cha mume wangu. Lakini hapa, hatuna chochote, hatuna kazi, hakuna kitu, hata nguo. Wasamaria wema wanaleta vitu sasa, hivi au vile, kutoka hapa na pale… la sivyo hatuna kitu, binti yangu hana nguo nyingine, hana chochote cha kuvaa kumpa joto.”UNHCR inaisaidia Serikali ya Armenia kwa vifaa vya kiufundi, kama aina mbalimbali za kompyuta ili kurahisisha usajili na imetoa msaada wa vitu muhimu kama vitanda vya kukunja na magodoro kwa ajili ya wakimbizi, huku misaada muhimu zaidi ikiwa njiani.Tags: Armenia, UNHCR, Karabhak
9-10-2023 • 0
Mashirika ya kibinadamu nayo yanahitaji msaada ili kusaidia wakimbizi wa Armenia
Mashirika ya kibinadamu nayo yanahitaji msaada ili kusaidia wakimbizi wa Armenia Ili kuhakikisha mahitaji ya muda mfupi, kati na ya muda mrefu yanatimizwa, mashirika ya kibinadamu yanaendelea kuhaha kutafuta ufadhili wa haraka ili kuongeza msaada kwa zaidi ya wakimbizi 100,000 nchini Armenia waliokimbia eneo la Karabhak kufuatia kuongezeka kwa uhasama mwezi Septemba. Anold Kayanda na maelezo zaidi.(Taarifa ya Anold Kayanda)Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linaeleza kuwa takribani wakimbizi 100,000 waliwasili Armenia ndani ya muda wa chini ya wiki moja kufuatia kuongezeka kwa uhasama unaoendelea kwenye eneo la Karabakh linalogombaniwa na Armenia na Azerbaijan huko barani Asia.UNHCR inasema miongoni mwa wakimbizi wapya waliowasili, ni watoto wapatao 30,000 na watu wengi wenye uhitaji ikiwa ni pamoja na wazee, wanawake wajawazito, watu wenye ulemavu na wengine wenye magonjwa ya kudumu. Zaidi ya nusu ya wakimbizi ni wanawake na wasichana.Huyu ni Vika, mmoja wa wakimbizi anasema, (Sauti ya Vika) – Evarist/sauti ya kike“Hali yetu hapa si ya uhakika. Huko, nilikuwa nikifanya kazi shuleni, nilikuwa muuguzi pale. Kila kitu kilikuwa kikienda sawa, tulikuwa tukiishi na wazazi wangu baada ya kifo cha mume wangu. Lakini hapa, hatuna chochote, hatuna kazi, hakuna kitu, hata nguo. Wasamaria wema wanaleta vitu sasa, hivi au vile, kutoka hapa na pale… la sivyo hatuna kitu, binti yangu hana nguo nyingine, hana chochote cha kuvaa kumpa joto.”UNHCR inaisaidia Serikali ya Armenia kwa vifaa vya kiufundi, kama aina mbalimbali za kompyuta ili kurahisisha usajili na imetoa msaada wa vitu muhimu kama vitanda vya kukunja na magodoro kwa ajili ya wakimbizi, huku misaada muhimu zaidi ikiwa njiani.Tags: Armenia, UNHCR, Karabhak
9-10-2023 • 0
Mashariki ya Kati bado hali si shwari, UNHCR yapaza sauti
Mashariki ya Kati bado hali si shwari, UNHCR yapaza sauti Mapigano huko Mashariki ya Kati yakiingia siku ya tatu kati ya Israel na wapalestina, huko Geneva, hii leo wajumbe wa mkutano wa 54 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka mamia ya watu waliopoteza maisha katika mapigano hayo yaliyoanza baada ya wanamgambo wa Hamas kurusha makombora kuelekea upande wa Israel. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. (Taarifa ya Assumpta Massoi) Nats.. Ni katika ukumbi wa Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu, jijini Geneva, Uswisi kunakoendelea mkutano wa 54 wa Baraza hilo ambako mwenyekiti alitaka wajumbe kusimama kwa dakika moja kukumbuka waliopoteza maisha kwenye mapigano hayo yanayoendelea huko Mashariki ya Kati, kati ya wanamgambo wa Hamas kutoka Palestina na jeshi la Israel. Takwimu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA zinasema hadi sasa watu 370 wakiwemo watoto 20 wameuawa huku zaidi ya 2,200 wamejeruhiwa upande Palestina ihali kwa Israel waliouawa ni takribani 650. Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amenukuliwa hii leo huko Geneva, Uswisi akisema shirika hilo linakabiliwa na moja ya nyakati ngumu zaidi katika historia yake ya miaka 70. Amesema watu milioni 110 ni wakimbizi duniani kote na ukata ndio umekumba zaidi UNHCR. Bwana Grandi amesema picha za kutisha na kusikitisha za mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Hamas dhidi ya raia wa Israel zimegubika skrini za televisheni kwa saa 48. Mkuu huyo wa UNHCR amesema “tunashuhudia vita nyingine Mashariki ya Kati, vita ambayo bila shaka itasababisha machungu zaidi kwa raia, pande zote za Israel na Palestina, na kuhatarisha kuleta ukosefu mkubwa wa utulivu kwenye ukanda huo ambao tayari umegubikwa na mvutano.” Bwana Grandi amesema iwapo hatua hazitachukuliwa haraka kudhibiti, kuna hatari mzozo huo ukasambaa na kudumaza amani duniani. Jana Jumapili, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana kwa faragha kujadili mapigano hayo Mashariki ya Kati huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa taarifa Jumamosi akilaani mashambulizi hayo ya Hamas dhidi ya Israel huku akitaka diplomasia itumike kumaliza mzozo huo. TAGS: Amani na Usalama Additional: Amani na Usalama News: Israel, Palestina, Hamas Region: Mashariki ya Kati UN/Partner: UNRWA, UNHCR
9-10-2023 • 0
Mashariki ya Kati bado hali si shwari, UNHCR yapaza sauti
Mashariki ya Kati bado hali si shwari, UNHCR yapaza sauti Mapigano huko Mashariki ya Kati yakiingia siku ya tatu kati ya Israel na wapalestina, huko Geneva, hii leo wajumbe wa mkutano wa 54 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka mamia ya watu waliopoteza maisha katika mapigano hayo yaliyoanza baada ya wanamgambo wa Hamas kurusha makombora kuelekea upande wa Israel. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. (Taarifa ya Assumpta Massoi) Nats.. Ni katika ukumbi wa Baraza la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu, jijini Geneva, Uswisi kunakoendelea mkutano wa 54 wa Baraza hilo ambako mwenyekiti alitaka wajumbe kusimama kwa dakika moja kukumbuka waliopoteza maisha kwenye mapigano hayo yanayoendelea huko Mashariki ya Kati, kati ya wanamgambo wa Hamas kutoka Palestina na jeshi la Israel. Takwimu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA zinasema hadi sasa watu 370 wakiwemo watoto 20 wameuawa huku zaidi ya 2,200 wamejeruhiwa upande Palestina ihali kwa Israel waliouawa ni takribani 650. Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Filippo Grandi amenukuliwa hii leo huko Geneva, Uswisi akisema shirika hilo linakabiliwa na moja ya nyakati ngumu zaidi katika historia yake ya miaka 70. Amesema watu milioni 110 ni wakimbizi duniani kote na ukata ndio umekumba zaidi UNHCR. Bwana Grandi amesema picha za kutisha na kusikitisha za mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Hamas dhidi ya raia wa Israel zimegubika skrini za televisheni kwa saa 48. Mkuu huyo wa UNHCR amesema “tunashuhudia vita nyingine Mashariki ya Kati, vita ambayo bila shaka itasababisha machungu zaidi kwa raia, pande zote za Israel na Palestina, na kuhatarisha kuleta ukosefu mkubwa wa utulivu kwenye ukanda huo ambao tayari umegubikwa na mvutano.” Bwana Grandi amesema iwapo hatua hazitachukuliwa haraka kudhibiti, kuna hatari mzozo huo ukasambaa na kudumaza amani duniani. Jana Jumapili, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana kwa faragha kujadili mapigano hayo Mashariki ya Kati huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa taarifa Jumamosi akilaani mashambulizi hayo ya Hamas dhidi ya Israel huku akitaka diplomasia itumike kumaliza mzozo huo. TAGS: Amani na Usalama Additional: Amani na Usalama News: Israel, Palestina, Hamas Region: Mashariki ya Kati UN/Partner: UNRWA, UNHCR
9-10-2023 • 0
09 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani Leah Mushi anamulika Mashariki ya Kati, Ulaya, siku ya posta duniani na mashinani anaelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumsikia mnufaika wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.1. Mapigano huko Mashariki ya Kati yakiingia siku ya tatu kati ya Israel na wapalestina, huko Geneva, hii leo wajumbe wa mkutano wa 54 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka mamia ya watu waliopoteza maisha katika mapigano hayo yaliyoanza baada ya wanamgambo wa Hamas kurusha makombora kuelekea upande wa Israel.2. Ili kuhakikisha mahitaji ya muda mfupi, kati na ya muda mrefu yanatimizwa, mashirika ya kibinadamu yanaendelea kuhaha kutafuta ufadhili wa haraka ili kuongeza msaada kwa zaidi ya wakimbizi 100,000 nchini Armenia waliokimbia eneo la Karabhak kufuatia kuongezeka kwa uhasama mwezi Septemba.3. Makala ni siku ya Posta Duniani ambapo Evarist Mapesa wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU Mutua Muthusi anaelezea nafasi ya maendeleo ya kidijitali katika kusongesha huduma za posta. 4. Mashinani ni mnufaika wa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani, WFP nchini DR Congo.
9-10-2023 • 0
09 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani Leah Mushi anamulika Mashariki ya Kati, Ulaya, siku ya posta duniani na mashinani anaelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumsikia mnufaika wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP.1. Mapigano huko Mashariki ya Kati yakiingia siku ya tatu kati ya Israel na wapalestina, huko Geneva, hii leo wajumbe wa mkutano wa 54 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka mamia ya watu waliopoteza maisha katika mapigano hayo yaliyoanza baada ya wanamgambo wa Hamas kurusha makombora kuelekea upande wa Israel.2. Ili kuhakikisha mahitaji ya muda mfupi, kati na ya muda mrefu yanatimizwa, mashirika ya kibinadamu yanaendelea kuhaha kutafuta ufadhili wa haraka ili kuongeza msaada kwa zaidi ya wakimbizi 100,000 nchini Armenia waliokimbia eneo la Karabhak kufuatia kuongezeka kwa uhasama mwezi Septemba.3. Makala ni siku ya Posta Duniani ambapo Evarist Mapesa wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Posta, UPU Mutua Muthusi anaelezea nafasi ya maendeleo ya kidijitali katika kusongesha huduma za posta. 4. Mashinani ni mnufaika wa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani, WFP nchini DR Congo.
9-10-2023 • 0
Madarasa yajengwa Sofala, Msumbiji kuhimili majanga ya asili ikiwemo vimbunga
Hii leo Umoja wa Mataifa umetoa ripoti ya kwanza ya uchambuzi wa aina yake kuhusu matukio ya watoto kulazimika kukimbia makwao kutokana na majanga yasababishwayo na hali ya hewa ikisema zaidi ya watoto milioni 43 walijikuta wakimbizi wa ndani kwenye nchi 44 katika kipindi cha miaka sita iliyopita, ikitafsiri kuwa ni watoto 20,000 kila siku.Makadirio ya ripoti hiyo ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, yanaonesha kuwa kufurika kwa mito pekee kutafurusha watoto milioni 96 katika miaka 30 ijayo.Kwa kutambua hilo, mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Idai nchini Msumbiji mwaka 2019 tayari yamekuwa somo na hatua zimechukuliwa, hatua ambazo zinaweza kuwa somo pia kwa maeneo mengine. Je ni hatua zipi hizo? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyofanikishwa na UNICEF.
6-10-2023 • 0
Madarasa yajengwa Sofala, Msumbiji kuhimili majanga ya asili ikiwemo vimbunga
Hii leo Umoja wa Mataifa umetoa ripoti ya kwanza ya uchambuzi wa aina yake kuhusu matukio ya watoto kulazimika kukimbia makwao kutokana na majanga yasababishwayo na hali ya hewa ikisema zaidi ya watoto milioni 43 walijikuta wakimbizi wa ndani kwenye nchi 44 katika kipindi cha miaka sita iliyopita, ikitafsiri kuwa ni watoto 20,000 kila siku.Makadirio ya ripoti hiyo ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, yanaonesha kuwa kufurika kwa mito pekee kutafurusha watoto milioni 96 katika miaka 30 ijayo.Kwa kutambua hilo, mafuriko yaliyosababishwa na kimbunga Idai nchini Msumbiji mwaka 2019 tayari yamekuwa somo na hatua zimechukuliwa, hatua ambazo zinaweza kuwa somo pia kwa maeneo mengine. Je ni hatua zipi hizo? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyofanikishwa na UNICEF.
6-10-2023 • 0
Tuzo ya amani ya Nobel yaenda kwa mfungwa Iran, UN yasifu wanawake wa Iran kwa kuongoza vuguvugu
Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu imemtunuku mfungwa mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu wa Iran Narges Mohammadi na Umoja wa Mataifa umepongeza uamuzi huo. Flora Nducha na taarifa zaidiBaada ya kutangazwa tu leo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema “ Kumpatia tuzo Narges Mohammadi mwanaharakati shupavu wa haki za binadamu ambaye hivi sasa anatumikia kifongo cha miaka 16 kwenye gereza la Evin mjini Tehran nchini Iran kunasisitiza ijasiri na dhamira waliyonayo wanawake wa Iran.”Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa ofisi hiyo ya haki za binadamu Liz Throssell amesema “ Nadhani kilicho bayan ani kwamba wanawake wa Iran wamekuwa chanzo cha hamasa ulimwenguni . Tumeshuhudia ujasiri na kujizatiti kwao katika wakati wa ukiukwaji wa haki, vitisho, machafuko na watu kuswekwa vizuizini. Na ujasiri huu na kujizatiti huku ni kwa hali ya juu, kwani wamekuwa wakibughudhwa kwa kile wanachovaa au kutovaa, wanabanwa kisheria, kijamii na kiuchumi kwa hatua zinazochukuliwa dhidi yao.”Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameongeza sauti yake akisema “Narges kupewa tuzo hiyo ni kumbusho muhimu kwamba haki za wanawake na wasichana zinakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo kupitia kushitakiwa kwa wanawake watetezi wa haki za binadamu nchini Iran na kwingineko.Na hivyo “ Tuzo hiyo ya Amani ya Nobel ni “Utambuzi wa wanawake wote ambao wanapambana kwa ajili ya haki za binadamu huku wakihatarisha uhuru wao, afya zao n ahata Maisha yao.”Narges amefanyakazi kwa miaka mingi kama muandishi wa habari na pia ni mwandishi wa vitabu na pia naibu mkurugenzi wa shirika la kiraia la Defenders of Human rights Center lililoko mjini Tehran.MweZi mei mwaka huu alipata tuzo ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari inayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO
6-10-2023 • 0
Tuzo ya amani ya Nobel yaenda kwa mfungwa Iran, UN yasifu wanawake wa Iran kwa kuongoza vuguvugu
Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu imemtunuku mfungwa mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu wa Iran Narges Mohammadi na Umoja wa Mataifa umepongeza uamuzi huo. Flora Nducha na taarifa zaidiBaada ya kutangazwa tu leo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema “ Kumpatia tuzo Narges Mohammadi mwanaharakati shupavu wa haki za binadamu ambaye hivi sasa anatumikia kifongo cha miaka 16 kwenye gereza la Evin mjini Tehran nchini Iran kunasisitiza ijasiri na dhamira waliyonayo wanawake wa Iran.”Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis msemaji wa ofisi hiyo ya haki za binadamu Liz Throssell amesema “ Nadhani kilicho bayan ani kwamba wanawake wa Iran wamekuwa chanzo cha hamasa ulimwenguni . Tumeshuhudia ujasiri na kujizatiti kwao katika wakati wa ukiukwaji wa haki, vitisho, machafuko na watu kuswekwa vizuizini. Na ujasiri huu na kujizatiti huku ni kwa hali ya juu, kwani wamekuwa wakibughudhwa kwa kile wanachovaa au kutovaa, wanabanwa kisheria, kijamii na kiuchumi kwa hatua zinazochukuliwa dhidi yao.”Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameongeza sauti yake akisema “Narges kupewa tuzo hiyo ni kumbusho muhimu kwamba haki za wanawake na wasichana zinakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo kupitia kushitakiwa kwa wanawake watetezi wa haki za binadamu nchini Iran na kwingineko.Na hivyo “ Tuzo hiyo ya Amani ya Nobel ni “Utambuzi wa wanawake wote ambao wanapambana kwa ajili ya haki za binadamu huku wakihatarisha uhuru wao, afya zao n ahata Maisha yao.”Narges amefanyakazi kwa miaka mingi kama muandishi wa habari na pia ni mwandishi wa vitabu na pia naibu mkurugenzi wa shirika la kiraia la Defenders of Human rights Center lililoko mjini Tehran.MweZi mei mwaka huu alipata tuzo ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari inayotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO
6-10-2023 • 0
Mtoto kuzaliwa njiti humtia hatarini kukumbwa na kifo, hatua zichukuliwe- WHO
Inakadiriwa watoto milioni 13.4 njiti (wanaozaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito) walizaliwa mwaka 2020 idadi hii ikiwa ni takriban mtoto 1 kati ya 10 na wengi wa watoto hao ni kutoka Ukanda wa jangwa la Sahara na Asia ya Kusini imesema ripoti iliyochapishwa leo kwenye jarida la masuala ya afya la Lancet. Leah Mushi na maelezo zaidi.Ripoti hiyo inafuatia utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kwakushirikiana na lile la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF pamoja na Chuo kikuu cha London kitivo cha usafi na dawa za kitropiki (London School of Hygiene and Tropical Medicine.)Mkurugenzi wa WHO idara ya masuala ya watoto wachanga, watoto, afya za barubaru na wazee Dkt. Anshu Banerjee amesema kwa kuwa watoto kuzaliwa kabla ya muda ni sababu kubwa ya vifo vya watoto wachanga suala hili linapaswa kushughulikiwa kwa udharura.“Idadi hii inaonesha uhitaji wa uwekezaji wa maana ili kuweza kusaidia familia na watoto wao pamoja na kuweka mkazo katika katika kuhakikisha kuna upatikanaji wa huduma bora za afya kabla na wakati wa ujauzito.”Sababu za kujifungua mtoto njitiHatari za afya ya uzazi, kama vile mimba za utotoni, maambukizi, lishe duni, na hali ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito ni sababu zinazo husishwa na mama mjamzito kujifungua mtoto njiti.Upatikanaji wa huduma bora wakati wa ujauzito ni suala muhimu kwani linawezesha kufanya utambuzi na udhibiti wa matatizo wakati wa ujauzito, kuhakikisha kuna uhesabuji sahihi wa ujauzito kwakuazia wakati mimba upo ndogo kupitia uchunguzi wa kutumia ultrasound na pale inapohitajika kuchelewesha mwanamke kupata uchungu wa kujifungua itawezekana kupitia matibabu yaliyo idhinishwaAthari za kuzaliwa njitiTaarifa ya WHO iliyotolewa leo kutoka huko Jijini Geneva Uswisi imebainisha kuwa mbali na suala la watoto kupoteza maisha, watoto njiti wanakabiliwa na ukuwaji wenye changamoto ikiwemo kupata magonjwa makubwa, ulemavu na ukuaji kwa kuchelewa na hata wakiwa wakiwa watu wazima wanaweza kupata magonjwa sugu kama kisurari na magonjwa ya moto.“Watoto njiti wapo hatarini sana kupata matatizo ya afya yanayo hatarisha maisha na wanahitaji uangalizi maalum” amesema Dr. BanerjeeMatokeo ya utafitiUtafiti huo Makadirio ya kwenye karatasi, ya Kitaifa, kikanda na kimataifa ya watoto njiti kwa mwaka wa 2020, yenye muelekeo kuanzia mwaka 2010: uchambuzi wa kiutaratibu,umeonesha kuna utofauti baina ya kanda na mataifa.Asilimia 65 ya watoto njiti waliozaliwa mwaka 2020 walitokea…
6-10-2023 • 0
Mtoto kuzaliwa njiti humtia hatarini kukumbwa na kifo, hatua zichukuliwe- WHO
Inakadiriwa watoto milioni 13.4 njiti (wanaozaliwa kabla ya wiki 37 za ujauzito) walizaliwa mwaka 2020 idadi hii ikiwa ni takriban mtoto 1 kati ya 10 na wengi wa watoto hao ni kutoka Ukanda wa jangwa la Sahara na Asia ya Kusini imesema ripoti iliyochapishwa leo kwenye jarida la masuala ya afya la Lancet. Leah Mushi na maelezo zaidi.Ripoti hiyo inafuatia utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kwakushirikiana na lile la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF pamoja na Chuo kikuu cha London kitivo cha usafi na dawa za kitropiki (London School of Hygiene and Tropical Medicine.)Mkurugenzi wa WHO idara ya masuala ya watoto wachanga, watoto, afya za barubaru na wazee Dkt. Anshu Banerjee amesema kwa kuwa watoto kuzaliwa kabla ya muda ni sababu kubwa ya vifo vya watoto wachanga suala hili linapaswa kushughulikiwa kwa udharura.“Idadi hii inaonesha uhitaji wa uwekezaji wa maana ili kuweza kusaidia familia na watoto wao pamoja na kuweka mkazo katika katika kuhakikisha kuna upatikanaji wa huduma bora za afya kabla na wakati wa ujauzito.”Sababu za kujifungua mtoto njitiHatari za afya ya uzazi, kama vile mimba za utotoni, maambukizi, lishe duni, na hali ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito ni sababu zinazo husishwa na mama mjamzito kujifungua mtoto njiti.Upatikanaji wa huduma bora wakati wa ujauzito ni suala muhimu kwani linawezesha kufanya utambuzi na udhibiti wa matatizo wakati wa ujauzito, kuhakikisha kuna uhesabuji sahihi wa ujauzito kwakuazia wakati mimba upo ndogo kupitia uchunguzi wa kutumia ultrasound na pale inapohitajika kuchelewesha mwanamke kupata uchungu wa kujifungua itawezekana kupitia matibabu yaliyo idhinishwaAthari za kuzaliwa njitiTaarifa ya WHO iliyotolewa leo kutoka huko Jijini Geneva Uswisi imebainisha kuwa mbali na suala la watoto kupoteza maisha, watoto njiti wanakabiliwa na ukuwaji wenye changamoto ikiwemo kupata magonjwa makubwa, ulemavu na ukuaji kwa kuchelewa na hata wakiwa wakiwa watu wazima wanaweza kupata magonjwa sugu kama kisurari na magonjwa ya moto.“Watoto njiti wapo hatarini sana kupata matatizo ya afya yanayo hatarisha maisha na wanahitaji uangalizi maalum” amesema Dr. BanerjeeMatokeo ya utafitiUtafiti huo Makadirio ya kwenye karatasi, ya Kitaifa, kikanda na kimataifa ya watoto njiti kwa mwaka wa 2020, yenye muelekeo kuanzia mwaka 2010: uchambuzi wa kiutaratibu,umeonesha kuna utofauti baina ya kanda na mataifa.Asilimia 65 ya watoto njiti waliozaliwa mwaka 2020 walitokea…
6-10-2023 • 0
06 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akimulika pamoja na mambo mengine mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Mabadiliko ya Tabianchi, vijana na siasa pamoja na majiko sanifu.1.Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu imemtunuku mfungwa mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu wa Iran Narges Mohammadi na Umoja wa Mataifa umepongeza uamuzi huo2. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na Umoja wa wanafunzi wa nchini humo wanaendesha midahalo ya wanafunzi lengo likiwa ni kuchagiza vijana waweze kushiriki kikamilifu katika masuala ya siasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Desemba 2024.3. Makala inakupeleka Msumbiji ambako huko UNICEF imejenga majengo ya shule yanayoweza kuhimili mvua kubwa na mafuriko.4 .Mashinani ni mfinyanzi mkimbizi kutoka DRC akijiinua si yeye peke yake bali pia jamii kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.
6-10-2023 • 0
06 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akimulika pamoja na mambo mengine mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Mabadiliko ya Tabianchi, vijana na siasa pamoja na majiko sanifu.1.Kamati ya tuzo ya amani ya Nobel mwaka huu imemtunuku mfungwa mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu wa Iran Narges Mohammadi na Umoja wa Mataifa umepongeza uamuzi huo2. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na Umoja wa wanafunzi wa nchini humo wanaendesha midahalo ya wanafunzi lengo likiwa ni kuchagiza vijana waweze kushiriki kikamilifu katika masuala ya siasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwezi Desemba 2024.3. Makala inakupeleka Msumbiji ambako huko UNICEF imejenga majengo ya shule yanayoweza kuhimili mvua kubwa na mafuriko.4 .Mashinani ni mfinyanzi mkimbizi kutoka DRC akijiinua si yeye peke yake bali pia jamii kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.
6-10-2023 • 0
Mwalimu binafsi aanzisha maktaba inayosaidia watoto katika maeneo duni Kenya
Siku ya walimu duniani huadhimishwa tarehe 5 Oktoba kila mwaka.Mada kuu kwa mwaka huu ni walimu tunaohitaji kwa elimu tunayoitaka. Kenya imepiga hatua kwenye sekta ya elimu kwa kuzindua mfumo unaojikita katika kukuza vipaji na uwezo wa mwanafunzi, CBC,ila uhaba wa walimu ni kikwazo cha utekelezaji. Baadhi ya walimu wa kujitegeme wamechukua hatua mikononi mwao na kuanzisha maktaba za binafsi ili kuwapa watoto nafasi ya kusoma nje ya mazingira ya shule.Maktaba ya Little Voice Deep Within iko mtaani Kariobangi South jijini Nairobi katikati ya makaazi ya umma.Hii ndiyo taswira unayokumbana nayo unapowasili.Watoto wanacheza nje au kusoma vitabu wakiwa ndani.Kila siku ina ratiba yake ima ni kusoma, sanaa au kujifunza kutumia kompyuta .Eric Odhiambo ni mwalimu wa kujitegemea na muasisi wa maktaba binafsi ya Little Voice Deep Within na anaamini kuwa kila mtoto ana haki ya kupata elimu mujarab nje ya mazingira ya shule kwani,”Watoto wa mtaani hawana maktaba.Unakuta mtoto anafikiria tu kutazama vibonzo kwenye televisheni hakuna kingine cha kufanya.Hakuna kituo ambapo mtoto anaweza kupitisha muda au kusoma na kufanya kitu fulani.Niliona ni bora kuwaletea maktaba karibu ili mtoto akitaka kusoma au ambaye hajui kusoma anapata msaada.”Kusoma vitabu ni njia mujarab ya kuepusha utunduMaktaba hii ina vitabu vya lugha na mada tofauti mahsusi kwa watoto wa kila rika.Siku ya walimu duniani huadhimishwa tarehe 5 Oktoba kila mwaka na mada kuu mwaka huu ni walimu tunaowahitaji kwa elimu tunayoitaka.Kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Sayansi na utamaduni,UNESCO, walimu milioni 44 bado wanahitajika ili kutimiza lengo la kusambaza elimu ya msingi na sekondari kwa wote ifikapo 2030.Walimu wana mchango muhimu kwenye maisha ya wanafunzi na ni sawa na walezi. Evelyne Wambui ni mzazi na binti yake Joy anapata mafunzo kwenye kituo cha Little Voice Deep Within , anakiri kwa mba mwanawe amebadilika na kwa sasa,”Mwanzo wa mwaka mwalimu aliwaandikia vile vitabu vinavyohitajika kununuliwa. Mimi kama mzazi niliweza kununua vitabu vinne....hivyo vyengine vilinunuliwa na viko huko Vinamsaidia. Akipewa kazi ya ziada ya nyumbani.Yeye ana vitabu vya msingi vya Kiswahili, Hesabu na Sayansi.Vingine anavipata huku.”Watoto hujifunza pia vitu vingine kama kufuma mitandio na vitambaa wanapokuja kwenye kituo hiki.Kadhalika wanapata ujuzi wa kuchora kulingana na uwezo na umri wao.Ili kuiongeza kasi ya kutimiza lengo la 4 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa,SDGs ya elimu bora,UNESCO inashirikiana na mataifa hasa ya eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara na kusini mwa Asia ili kuimarisha sera zinazowahusu na kuunga mkono mifumo ya kutoa mafunzo kwa walimu.Susan Muthoni ni mwalimu wa hiari kwenye kituo hiki cha watoto na anawafunza kufuma vitambaa na mitandio kwa upande wake anaamini kuwa masomo ya kutengeza bidhaa kwa mikono yana umuhimu mkubwa katika maisha ya usoni lakini,”Kwanza ni kuwa na walimu wanaowaelewa watoto.Kwenye shule kama hizi za umma,unapata kuwa kama mtoto wako huwa wa kwanza ataendelea hivyo na kama huwa wa mwisho anaendelea kuvuta mkia. Kwahiyo upo umuhimu wa kuwa na njia maalum ya kuwasomesha hawa watoto...kuwe na walimu wa kuwasomesha masomo mengine.Ukiona mtoto haelewi masomo ya kuandika anaweza kupata ujuzi wa kazi za mikono.”UNESCO,shirika la lazi la Umoja wa Mataifa ILO,shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF na Education International ndiyo mashirika yanayosimamia siku ya walimu duniani na dhamira ni kuzishajiisha serikali na mashirika ya kijamii kuipa fani ya ualimu sifa nzuri zaidi ili kuwavutia wengi kujiunga hasa vijana.UNESCO imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa haki ya elimu inakuwa mchango muhimu kwenye misingi ya haki za binadamu na kulinda amani.Hata hivyo,kwa mujibu wa UNESCO nadharia hii itatimia iwapo walimu wanaungwa mkono kuwafunza…
5-10-2023 • 0
Mwalimu binafsi aanzisha maktaba inayosaidia watoto katika maeneo duni Kenya
Siku ya walimu duniani huadhimishwa tarehe 5 Oktoba kila mwaka.Mada kuu kwa mwaka huu ni walimu tunaohitaji kwa elimu tunayoitaka. Kenya imepiga hatua kwenye sekta ya elimu kwa kuzindua mfumo unaojikita katika kukuza vipaji na uwezo wa mwanafunzi, CBC,ila uhaba wa walimu ni kikwazo cha utekelezaji. Baadhi ya walimu wa kujitegeme wamechukua hatua mikononi mwao na kuanzisha maktaba za binafsi ili kuwapa watoto nafasi ya kusoma nje ya mazingira ya shule.Maktaba ya Little Voice Deep Within iko mtaani Kariobangi South jijini Nairobi katikati ya makaazi ya umma.Hii ndiyo taswira unayokumbana nayo unapowasili.Watoto wanacheza nje au kusoma vitabu wakiwa ndani.Kila siku ina ratiba yake ima ni kusoma, sanaa au kujifunza kutumia kompyuta .Eric Odhiambo ni mwalimu wa kujitegemea na muasisi wa maktaba binafsi ya Little Voice Deep Within na anaamini kuwa kila mtoto ana haki ya kupata elimu mujarab nje ya mazingira ya shule kwani,”Watoto wa mtaani hawana maktaba.Unakuta mtoto anafikiria tu kutazama vibonzo kwenye televisheni hakuna kingine cha kufanya.Hakuna kituo ambapo mtoto anaweza kupitisha muda au kusoma na kufanya kitu fulani.Niliona ni bora kuwaletea maktaba karibu ili mtoto akitaka kusoma au ambaye hajui kusoma anapata msaada.”Kusoma vitabu ni njia mujarab ya kuepusha utunduMaktaba hii ina vitabu vya lugha na mada tofauti mahsusi kwa watoto wa kila rika.Siku ya walimu duniani huadhimishwa tarehe 5 Oktoba kila mwaka na mada kuu mwaka huu ni walimu tunaowahitaji kwa elimu tunayoitaka.Kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Sayansi na utamaduni,UNESCO, walimu milioni 44 bado wanahitajika ili kutimiza lengo la kusambaza elimu ya msingi na sekondari kwa wote ifikapo 2030.Walimu wana mchango muhimu kwenye maisha ya wanafunzi na ni sawa na walezi. Evelyne Wambui ni mzazi na binti yake Joy anapata mafunzo kwenye kituo cha Little Voice Deep Within , anakiri kwa mba mwanawe amebadilika na kwa sasa,”Mwanzo wa mwaka mwalimu aliwaandikia vile vitabu vinavyohitajika kununuliwa. Mimi kama mzazi niliweza kununua vitabu vinne....hivyo vyengine vilinunuliwa na viko huko Vinamsaidia. Akipewa kazi ya ziada ya nyumbani.Yeye ana vitabu vya msingi vya Kiswahili, Hesabu na Sayansi.Vingine anavipata huku.”Watoto hujifunza pia vitu vingine kama kufuma mitandio na vitambaa wanapokuja kwenye kituo hiki.Kadhalika wanapata ujuzi wa kuchora kulingana na uwezo na umri wao.Ili kuiongeza kasi ya kutimiza lengo la 4 la maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa,SDGs ya elimu bora,UNESCO inashirikiana na mataifa hasa ya eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara na kusini mwa Asia ili kuimarisha sera zinazowahusu na kuunga mkono mifumo ya kutoa mafunzo kwa walimu.Susan Muthoni ni mwalimu wa hiari kwenye kituo hiki cha watoto na anawafunza kufuma vitambaa na mitandio kwa upande wake anaamini kuwa masomo ya kutengeza bidhaa kwa mikono yana umuhimu mkubwa katika maisha ya usoni lakini,”Kwanza ni kuwa na walimu wanaowaelewa watoto.Kwenye shule kama hizi za umma,unapata kuwa kama mtoto wako huwa wa kwanza ataendelea hivyo na kama huwa wa mwisho anaendelea kuvuta mkia. Kwahiyo upo umuhimu wa kuwa na njia maalum ya kuwasomesha hawa watoto...kuwe na walimu wa kuwasomesha masomo mengine.Ukiona mtoto haelewi masomo ya kuandika anaweza kupata ujuzi wa kazi za mikono.”UNESCO,shirika la lazi la Umoja wa Mataifa ILO,shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF na Education International ndiyo mashirika yanayosimamia siku ya walimu duniani na dhamira ni kuzishajiisha serikali na mashirika ya kijamii kuipa fani ya ualimu sifa nzuri zaidi ili kuwavutia wengi kujiunga hasa vijana.UNESCO imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa haki ya elimu inakuwa mchango muhimu kwenye misingi ya haki za binadamu na kulinda amani.Hata hivyo,kwa mujibu wa UNESCO nadharia hii itatimia iwapo walimu wanaungwa mkono kuwafunza…
5-10-2023 • 0
Jifunze Kiswahili - "KUMBITI"
Katika jifunze Kiswahili hii leo tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA Je wajua maana ya neno “KUMBITI”? Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua.
5-10-2023 • 0
Jifunze Kiswahili - "KUMBITI"
Katika jifunze Kiswahili hii leo tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA Je wajua maana ya neno “KUMBITI”? Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA anafafanua.
5-10-2023 • 0
05 OKTOBA 2023
Mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya ametembelea maktaba ya Little Voice Deep iliyoko jijini Nairobi kujionea jinsi gani kupitia waalimu walioko inavyochangia kuhakikisha watoto wanapata elimu wanayoitaka na kusongesha lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa linalohusu elimu bora.
5-10-2023 • 0
05 OKTOBA 2023
Mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya ametembelea maktaba ya Little Voice Deep iliyoko jijini Nairobi kujionea jinsi gani kupitia waalimu walioko inavyochangia kuhakikisha watoto wanapata elimu wanayoitaka na kusongesha lengo namba 4 la malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa linalohusu elimu bora.
5-10-2023 • 0
Uchumi wa dunia uko njiapanda: UNCTAD
Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD, imezindua leo ripoti yake kuu ya Biashara na Maendeleo ya mwaka 2023 ambayo inachunguza kuimarika kwa uchumi wa dunia na kutoa utabiri wa kinachotarajiwa. Ripoti inaeleza hatua za kisera zinazopaswa kuchukuliwa ili kulinda uchumi wa dunia kutokana na matatizo ya kimfumo ya siku zijazo. Hii ni ripoti ambayo hutolewa kila mwaka ikitathimini mwenendo wa ukuaji wa uchumi kote duniani, changamoto zinazojitokeza na nini kifanyike ili kuhakikisha uchumi unaendelea kukua na kuepusha athari kubwa kwa nchi lakini pia kwa Dunia nzima.Ripoti hiyo iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi safari hii imeonya kwamba uchumi wa Dunia unadorora na kuna tofauti kubwa za ukuaji wa uchumi huo miongoni mwa nchi na kanda duniani. Inasema “Ukuaji wa uchumi wa dunia unatarajiwa kupungua kutoka asilimia 3 mwaka jana hadi asilimmia 2.4 mwaka huu huku kukiwa na dalili chache za kuimarika tena mwaka ujao.”Hivyo imeweka bayana kwamba “Uchumi wa dunia uko katika njia panda.”Ripoti hiyo ya UNCTAD imeendelea kueleza kwamba “Njia tofauti za ukuaji uchumi, kuongezeka kwa ukosefu wa usawa, kukua kwa hali ya kujikita na masoko na mzigo wa madeni vinahatarisha mustakabali wake wa uchumi wa dunia.” Mathalani ripoti imesema wakati nchi zilizoendelea kama Marekani, Uchina na nyinginezo za Ulaya zikijaribu kujikwamua kiuchumi kutokana na athari za janga la COVID-19 katika nchi zinazoendelea mchanganyiko wa viwango vya riba vinavyoongezeka, kudhoofika kwa sarafu zao na ukuaji duni wa mauzo ya nje vinabana nafasi ya kifedha inayohitajika kwa serikali kutoa huduma muhimu, na kubadilisha mzigo unaokua wa huduma ya madeni kuwa changamoto ya maendeleo inayojitokeza.Takriban watu bilioni 3.3 karibu nusu ya binadamu wote duniani sasa wanaishi katika nchi ambazo hutumia zaidi fecha kwa ajili ya malipo yenye riba ya madeni kuliko katika huduma za elimu au afya.Na nchi ambazo zimeathirika zaidi ni nchi zinazoendelea zenye kipato cha chini au ambazo zilianza kupata masoko ya mitaji ya kimataifa baada ya msukosuko wa kifedha duniani.Kwa mantiki hiyo UNCTAD inatoa wito wa “Kutaka mageuzi ya kitaasisi katika usimamizi wa fedha duniani, sera za kiutendaji zaidi za kukabiliana na mfumuko wa bei, ukosefu wa usawa, madeni katika nchi na uangalizi thabiti wa masoko muhimu ili kufikia uthabiti wa kifedha, kuongeza uwekezaji wenye tija na kuunda nafasi bora za kazi.
4-10-2023 • 0
Uchumi wa dunia uko njiapanda: UNCTAD
Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD, imezindua leo ripoti yake kuu ya Biashara na Maendeleo ya mwaka 2023 ambayo inachunguza kuimarika kwa uchumi wa dunia na kutoa utabiri wa kinachotarajiwa. Ripoti inaeleza hatua za kisera zinazopaswa kuchukuliwa ili kulinda uchumi wa dunia kutokana na matatizo ya kimfumo ya siku zijazo. Hii ni ripoti ambayo hutolewa kila mwaka ikitathimini mwenendo wa ukuaji wa uchumi kote duniani, changamoto zinazojitokeza na nini kifanyike ili kuhakikisha uchumi unaendelea kukua na kuepusha athari kubwa kwa nchi lakini pia kwa Dunia nzima.Ripoti hiyo iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi safari hii imeonya kwamba uchumi wa Dunia unadorora na kuna tofauti kubwa za ukuaji wa uchumi huo miongoni mwa nchi na kanda duniani. Inasema “Ukuaji wa uchumi wa dunia unatarajiwa kupungua kutoka asilimia 3 mwaka jana hadi asilimmia 2.4 mwaka huu huku kukiwa na dalili chache za kuimarika tena mwaka ujao.”Hivyo imeweka bayana kwamba “Uchumi wa dunia uko katika njia panda.”Ripoti hiyo ya UNCTAD imeendelea kueleza kwamba “Njia tofauti za ukuaji uchumi, kuongezeka kwa ukosefu wa usawa, kukua kwa hali ya kujikita na masoko na mzigo wa madeni vinahatarisha mustakabali wake wa uchumi wa dunia.” Mathalani ripoti imesema wakati nchi zilizoendelea kama Marekani, Uchina na nyinginezo za Ulaya zikijaribu kujikwamua kiuchumi kutokana na athari za janga la COVID-19 katika nchi zinazoendelea mchanganyiko wa viwango vya riba vinavyoongezeka, kudhoofika kwa sarafu zao na ukuaji duni wa mauzo ya nje vinabana nafasi ya kifedha inayohitajika kwa serikali kutoa huduma muhimu, na kubadilisha mzigo unaokua wa huduma ya madeni kuwa changamoto ya maendeleo inayojitokeza.Takriban watu bilioni 3.3 karibu nusu ya binadamu wote duniani sasa wanaishi katika nchi ambazo hutumia zaidi fecha kwa ajili ya malipo yenye riba ya madeni kuliko katika huduma za elimu au afya.Na nchi ambazo zimeathirika zaidi ni nchi zinazoendelea zenye kipato cha chini au ambazo zilianza kupata masoko ya mitaji ya kimataifa baada ya msukosuko wa kifedha duniani.Kwa mantiki hiyo UNCTAD inatoa wito wa “Kutaka mageuzi ya kitaasisi katika usimamizi wa fedha duniani, sera za kiutendaji zaidi za kukabiliana na mfumuko wa bei, ukosefu wa usawa, madeni katika nchi na uangalizi thabiti wa masoko muhimu ili kufikia uthabiti wa kifedha, kuongeza uwekezaji wenye tija na kuunda nafasi bora za kazi.
4-10-2023 • 0
04 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNCTAD na elimu kwa watoto wote. Makala tunarejelea uchambuzi wa ibara ya 10 ya Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Mashinani tunakupeleka nchini DRC, kulikoni? Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD, imezindua leo ripoti yake kuu ya Biashara na Maendeleo ya mwaka 2023 ambayo inachunguza kuimarika kwa uchumi wa dunia na kutoa utabiri wa kinachotarajiwa. Ripoti inaeleza hatua za kisera zinazopaswa kuchukuliwa ili kulinda uchumi wa dunia kutokana na matatizo ya kimfumo ya siku zijazo.Katika kuhakikisha hakuna mtoto yeyote anayeachwa nyuma kupata elimu Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linatekeleza mradi wa kutoa mafunzo kwa walimu nchini Ghana na tayari wanafunzi 37,000 wamenufaika na mafunzo waliopewa walimu wao. Leah Mushi anatuletea taarifa ya Mwalimu Sam mnufaika wa mafunzo yanayofadhiliwa na UNICEF.Katika mwendelezo wa uchambuzi wa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75, leo tunaangazia ibara ya 10 ambayo inasema kwamba “Kila mtu mwenye kesi ana haki ya kusikilizwa kwa haki katika mahakama iliyo wazi kwa umma, yenye kujitegemea, huru na isiyo na upendeleo. Ili kufahamu zaidi kuhusu Ibara hii niliwahi kuzungumza na Dkt. Elifuraha Laltaika, Mhadhiri Mwandamizi wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira nchini Tanzania na alianza kwa kuelezea historia ya ibara hiyo.Katika mashinani Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kushuhudia jinsi masomo ya kujua kusoma na kuandika inavyoelimisha wananchi kuendesha biashara zao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
4-10-2023 • 0
04 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNCTAD na elimu kwa watoto wote. Makala tunarejelea uchambuzi wa ibara ya 10 ya Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Mashinani tunakupeleka nchini DRC, kulikoni? Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD, imezindua leo ripoti yake kuu ya Biashara na Maendeleo ya mwaka 2023 ambayo inachunguza kuimarika kwa uchumi wa dunia na kutoa utabiri wa kinachotarajiwa. Ripoti inaeleza hatua za kisera zinazopaswa kuchukuliwa ili kulinda uchumi wa dunia kutokana na matatizo ya kimfumo ya siku zijazo.Katika kuhakikisha hakuna mtoto yeyote anayeachwa nyuma kupata elimu Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linatekeleza mradi wa kutoa mafunzo kwa walimu nchini Ghana na tayari wanafunzi 37,000 wamenufaika na mafunzo waliopewa walimu wao. Leah Mushi anatuletea taarifa ya Mwalimu Sam mnufaika wa mafunzo yanayofadhiliwa na UNICEF.Katika mwendelezo wa uchambuzi wa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75, leo tunaangazia ibara ya 10 ambayo inasema kwamba “Kila mtu mwenye kesi ana haki ya kusikilizwa kwa haki katika mahakama iliyo wazi kwa umma, yenye kujitegemea, huru na isiyo na upendeleo. Ili kufahamu zaidi kuhusu Ibara hii niliwahi kuzungumza na Dkt. Elifuraha Laltaika, Mhadhiri Mwandamizi wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira nchini Tanzania na alianza kwa kuelezea historia ya ibara hiyo.Katika mashinani Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kushuhudia jinsi masomo ya kujua kusoma na kuandika inavyoelimisha wananchi kuendesha biashara zao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
4-10-2023 • 0
UNICEF yafanikisha mbinu bunifu za ufundishaji na zimeongeza uelewa wa wanafunzi Ghana
Katika kuhakikisha hakuna mtoto yeyote anayeachwa nyuma kupata elimu Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linatekeleza mradi wa kutoa mafunzo kwa walimu nchini Ghana na tayari wanafunzi 37,000 wamenufaika na mafunzo waliopewa walimu wao. Leah Mushi anatuletea taarifa ya Mwalimu Sam mnufaika wa mafunzo yanayofadhiliwa na UNICEF.Video ya UNICEF inaanza kwa kumuonesha mwalimu Sam anaendesha baiskeli akielekea shuleniWalimu Sam anasema yeye ana falsafa yake ya ufundishaji, “Ukitaka kupanga kwa mwaka mmoja utapanda mpunga, kwa muongo mmoja utapanda miti lakini ukitaka kupanga kwa maisha yote unachotakiwa kufanya ni kuelimisha watu na hiyo ndio falsafa yangu kama mwalimu.” Mwalimu Sam anasema katika kila darasa uelewa wa watoto unatofautiana ndio maana huwaweka katika makundi tofauti. “Nawapa kila kikundi zoezi fulani kutokana na uwezo wao wa kujifunza, na natenga muda wangu ili kuhakikisha nafikia kila kikundi ili kufikia kiwango fulani, na kila mtu ataweza kuelewa nafundisha nini.”Na manufaa yameonekana kwani, “Darasani kwangu asilimia 80 mpaka 90 wanaweza kusoma vizuri kutokana na mbinu ninayotumia kuwafundisha.” Na huu ndio ushauri wa mwalimu Sam kwako.“Ukitaka kufanya jambo lolote kwenye maisha inakubidi ufanye msingi kwenye kila somo ili kupata uelewa mpana wa kukuwezesha kukabiliana na changamoto unazokumbana nazo kwenye maisha.”
4-10-2023 • 0
UNICEF yafanikisha mbinu bunifu za ufundishaji na zimeongeza uelewa wa wanafunzi Ghana
Katika kuhakikisha hakuna mtoto yeyote anayeachwa nyuma kupata elimu Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linatekeleza mradi wa kutoa mafunzo kwa walimu nchini Ghana na tayari wanafunzi 37,000 wamenufaika na mafunzo waliopewa walimu wao. Leah Mushi anatuletea taarifa ya Mwalimu Sam mnufaika wa mafunzo yanayofadhiliwa na UNICEF.Video ya UNICEF inaanza kwa kumuonesha mwalimu Sam anaendesha baiskeli akielekea shuleniWalimu Sam anasema yeye ana falsafa yake ya ufundishaji, “Ukitaka kupanga kwa mwaka mmoja utapanda mpunga, kwa muongo mmoja utapanda miti lakini ukitaka kupanga kwa maisha yote unachotakiwa kufanya ni kuelimisha watu na hiyo ndio falsafa yangu kama mwalimu.” Mwalimu Sam anasema katika kila darasa uelewa wa watoto unatofautiana ndio maana huwaweka katika makundi tofauti. “Nawapa kila kikundi zoezi fulani kutokana na uwezo wao wa kujifunza, na natenga muda wangu ili kuhakikisha nafikia kila kikundi ili kufikia kiwango fulani, na kila mtu ataweza kuelewa nafundisha nini.”Na manufaa yameonekana kwani, “Darasani kwangu asilimia 80 mpaka 90 wanaweza kusoma vizuri kutokana na mbinu ninayotumia kuwafundisha.” Na huu ndio ushauri wa mwalimu Sam kwako.“Ukitaka kufanya jambo lolote kwenye maisha inakubidi ufanye msingi kwenye kila somo ili kupata uelewa mpana wa kukuwezesha kukabiliana na changamoto unazokumbana nazo kwenye maisha.”
4-10-2023 • 0
03 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na inatupeleka Kibokoni, Kaunti ya Kilifi nchini Kenya ambako mabwawa ya samaki yamebadili kabisa maisha ya wavuvi wa eneo hilo walioathirika na mabadiliko ya tabianchi yaliyosabisha samaki kutoweka baharini na kuwakatisha tamaa ya Maisha. Lakini sasa kupitia mradi wa ufugaji samaki ulio chini ya mwamvuli wa Umoja Self-Help Group jamii hiyo ina mabwawa 17 ya samaki yanayozalisha samaki aina ya milkfish, kamba, kaa, sandfish, rabbitfish na perege au tilapia. Mshiani tanakuletea ujumbe kusu afya ya uzazi na uswa wa kijinsia. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo limeonya kwamba hali ya njaa inaibuka kwenye mpaka kati ya Sudan Kusini na Sudan huku familia zinazokimbia mapigano nchini Sudan zikiendelea kuvuka mpaka kila siku. Takwimu mpya zilizokusanywa na WFP zinaonesha kuwa kati ya karibu watu 300,000 ambao wamewasili Sudan Kusini katika miezi mitano iliyopita, mtoto mmoja kati ya watano ana utapiamlo na asilimia 90 ya familia wanasema wanakaa siku nyingi bila kula.Leo imetimia miaka 10 kamili tangu ajali ya meli iliyokuwa imebeba wahamiaji zaidi ya 500 kutoka Libya barani Afrika kuelekea nchini Italia ilipozama kwenye eneo la Lampedusa. Katika taarifa ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, Amy E. Pope, na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,(UNHCR) Filippo Grandi wamesema tukio hilo baya lilipotokea dunia iliahidi, “isitokee tena” lakini hilo halijatekelezeka. Mwaka huu pekee kufikia jana Oktoba pili tayari watu 2,517 wameshahesabiwa kuwa wamefariki dunia au kupotea katika bahari ya Mediterania.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema leo kuwa Armenia inakabiliwa na changamoto za kiafya kutokana na wimbi la wakimbizi ambalo halijawahi kushuhudiwa. Lakini wakati huo huo mashirika ya Umoja wa Mataifa kama la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu duniani UNFPA limepeleka vifaa vya afya ya uzazi na la Kuhudumia Watoto UNICEF limeanzisha eneo salama huko Goris, kusini mwa Armenia.Katika mashinani Dk. Natalia Kanem, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA anatoa ujumbe kuhusu upatikanaji wa afya Uzazi kwa wote, na usawa wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
3-10-2023 • 0
03 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na inatupeleka Kibokoni, Kaunti ya Kilifi nchini Kenya ambako mabwawa ya samaki yamebadili kabisa maisha ya wavuvi wa eneo hilo walioathirika na mabadiliko ya tabianchi yaliyosabisha samaki kutoweka baharini na kuwakatisha tamaa ya Maisha. Lakini sasa kupitia mradi wa ufugaji samaki ulio chini ya mwamvuli wa Umoja Self-Help Group jamii hiyo ina mabwawa 17 ya samaki yanayozalisha samaki aina ya milkfish, kamba, kaa, sandfish, rabbitfish na perege au tilapia. Mshiani tanakuletea ujumbe kusu afya ya uzazi na uswa wa kijinsia. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo limeonya kwamba hali ya njaa inaibuka kwenye mpaka kati ya Sudan Kusini na Sudan huku familia zinazokimbia mapigano nchini Sudan zikiendelea kuvuka mpaka kila siku. Takwimu mpya zilizokusanywa na WFP zinaonesha kuwa kati ya karibu watu 300,000 ambao wamewasili Sudan Kusini katika miezi mitano iliyopita, mtoto mmoja kati ya watano ana utapiamlo na asilimia 90 ya familia wanasema wanakaa siku nyingi bila kula.Leo imetimia miaka 10 kamili tangu ajali ya meli iliyokuwa imebeba wahamiaji zaidi ya 500 kutoka Libya barani Afrika kuelekea nchini Italia ilipozama kwenye eneo la Lampedusa. Katika taarifa ya pamoja ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, Amy E. Pope, na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,(UNHCR) Filippo Grandi wamesema tukio hilo baya lilipotokea dunia iliahidi, “isitokee tena” lakini hilo halijatekelezeka. Mwaka huu pekee kufikia jana Oktoba pili tayari watu 2,517 wameshahesabiwa kuwa wamefariki dunia au kupotea katika bahari ya Mediterania.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema leo kuwa Armenia inakabiliwa na changamoto za kiafya kutokana na wimbi la wakimbizi ambalo halijawahi kushuhudiwa. Lakini wakati huo huo mashirika ya Umoja wa Mataifa kama la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu duniani UNFPA limepeleka vifaa vya afya ya uzazi na la Kuhudumia Watoto UNICEF limeanzisha eneo salama huko Goris, kusini mwa Armenia.Katika mashinani Dk. Natalia Kanem, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA anatoa ujumbe kuhusu upatikanaji wa afya Uzazi kwa wote, na usawa wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
3-10-2023 • 0
02 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya makazi, na simulizi ya wakimbizi wa Armania kutoka Karabakh. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoniMipango ya jamii kudhibiti taka katika maeneo yao inaunga mkono uundaji wa mzunguko wa uchumi, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya leo ya Kimataifa ya Makazi na anaongeza kuwa “juhudi za umma za kupanua maeneo safi ya kijani yanasaidia kupoza maeneo ya mijini nyakati za mawimbi ya joto.”Nchini Armenia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linahaha kusaidia wakimbizi wanaoendelea kumiminika nchini humo kutoka eneo la Karabakh linalogombewa kati ya Armenia na Azerbaijan ambako sasa idadi ya wakimbizi waliowasili katika kipindi kisichozidi wiki moja ni zaidi ya laki moja na wako taabani.Makala makala inatupeleka Kenya ambako Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, Nairobi Kenya UNIS amezungumza na mmoja wa wazee wastaafu wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho maalum yaliyofanyika leo kuadhimisha siku ya wazee duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba Mosi.Katika mashinani Benedicto Kapaya, mfanyakazi wa kujitolea kutoka Tanzania ambaye ameitikia wito wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO wa kuhamasisha wenyeji wa vijiji vya Muzee na Kalakala kuhakikisha watoto wote wamepatiwa chanjo ya polio katika kampeni ya chanjo inayoendelea nchini humo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
2-10-2023 • 0
02 OKTOBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya makazi, na simulizi ya wakimbizi wa Armania kutoka Karabakh. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya, kulikoniMipango ya jamii kudhibiti taka katika maeneo yao inaunga mkono uundaji wa mzunguko wa uchumi, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya leo ya Kimataifa ya Makazi na anaongeza kuwa “juhudi za umma za kupanua maeneo safi ya kijani yanasaidia kupoza maeneo ya mijini nyakati za mawimbi ya joto.”Nchini Armenia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linahaha kusaidia wakimbizi wanaoendelea kumiminika nchini humo kutoka eneo la Karabakh linalogombewa kati ya Armenia na Azerbaijan ambako sasa idadi ya wakimbizi waliowasili katika kipindi kisichozidi wiki moja ni zaidi ya laki moja na wako taabani.Makala makala inatupeleka Kenya ambako Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, Nairobi Kenya UNIS amezungumza na mmoja wa wazee wastaafu wa Umoja wa Mataifa katika maadhimisho maalum yaliyofanyika leo kuadhimisha siku ya wazee duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba Mosi.Katika mashinani Benedicto Kapaya, mfanyakazi wa kujitolea kutoka Tanzania ambaye ameitikia wito wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO wa kuhamasisha wenyeji wa vijiji vya Muzee na Kalakala kuhakikisha watoto wote wamepatiwa chanjo ya polio katika kampeni ya chanjo inayoendelea nchini humo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
2-10-2023 • 0
Wakimbizi kutoka Kabarakh wasimulia yaliyowasibu
Nchini Armenia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linahaha kusaidia wakimbizi wanaoendelea kumiminika nchini humo kutoka eneo la Karabakh linalogombewa kati ya Armenia na Azerbaijan ambako sasa idadi ya wakimbizi waliowasili katika kipindi kisichozidi wiki moja ni zaidi ya laki moja na wako taabani.Tuko eneo la Goris, jimboni Syunik kusini mwa Armenia, taifa hili la Ulaya Mashariki, wakimbizi wake kwa waume, vijana na watoto wakiwasili kutoka Karabakh, magari yamesheheni virago vyao. Marine mmoja wa wakimbizi hao anasema, “leo tunakwenda Yerevan kusajiliwa na kupata pahala pa kuishi, tuko wanne, Nahitaji kumhudumia binti yangu mdogo.” Mkimbizi mwingine anakumbuka safari yao akisema “ilikuwa ngumu sana, tulikuwa barabarani kwa saa kati ya 26 hadi 29. Kulikuwa na msururu mrefu wa magari, ilikuwa vigumu sana kufika hapa. Mama yangu ni mgonwa, na kaka yangu ana watoto na wajukuu.” Serikali ya Armenia kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na mashirika yakiraia imebeba jukumu la kuwalinda na kusaidia wakimbizi. “Niko hapa mji wa Goris ambako zaidi ya wakimbizi 100,000 wamewasili hapa Armenia, baada ya kutumia siku kadhaa njiani. Wamewasili hapa wamechoka, wameacha kila kitu chao nyumbani. Watu wanahitaji msaada wa dharura. UNHCR imekuweko kwenye eneo hili mapema kuwapatia wahitaji misaada ya dharura, vitanda na magodoro. Tunayo malori ambayo yatawasili na kuendelea kutoa msaada kwa wale wenye uhitaji zaidi.”
2-10-2023 • 0
Wakimbizi kutoka Kabarakh wasimulia yaliyowasibu
Nchini Armenia, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, linahaha kusaidia wakimbizi wanaoendelea kumiminika nchini humo kutoka eneo la Karabakh linalogombewa kati ya Armenia na Azerbaijan ambako sasa idadi ya wakimbizi waliowasili katika kipindi kisichozidi wiki moja ni zaidi ya laki moja na wako taabani.Tuko eneo la Goris, jimboni Syunik kusini mwa Armenia, taifa hili la Ulaya Mashariki, wakimbizi wake kwa waume, vijana na watoto wakiwasili kutoka Karabakh, magari yamesheheni virago vyao. Marine mmoja wa wakimbizi hao anasema, “leo tunakwenda Yerevan kusajiliwa na kupata pahala pa kuishi, tuko wanne, Nahitaji kumhudumia binti yangu mdogo.” Mkimbizi mwingine anakumbuka safari yao akisema “ilikuwa ngumu sana, tulikuwa barabarani kwa saa kati ya 26 hadi 29. Kulikuwa na msururu mrefu wa magari, ilikuwa vigumu sana kufika hapa. Mama yangu ni mgonwa, na kaka yangu ana watoto na wajukuu.” Serikali ya Armenia kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na mashirika yakiraia imebeba jukumu la kuwalinda na kusaidia wakimbizi. “Niko hapa mji wa Goris ambako zaidi ya wakimbizi 100,000 wamewasili hapa Armenia, baada ya kutumia siku kadhaa njiani. Wamewasili hapa wamechoka, wameacha kila kitu chao nyumbani. Watu wanahitaji msaada wa dharura. UNHCR imekuweko kwenye eneo hili mapema kuwapatia wahitaji misaada ya dharura, vitanda na magodoro. Tunayo malori ambayo yatawasili na kuendelea kutoa msaada kwa wale wenye uhitaji zaidi.”
2-10-2023 • 0
Viongozi wa UN wanasema safisha mji wako ili kuunga mkono mzunuko wa uchumi
Mipango ya jamii kudhibiti taka katika maeneo yao inaunga mkono uundaji wa mzunguko wa uchumi, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya leo ya Kimataifa ya Makazi na anaongeza kuwa “juhudi za umma za kupanua maeneo safi ya kijani yanasaidia kupoza maeneo ya mijini nyakati za mawimbi ya joto.”Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN Habitat), Maimunah Mohamed Sharif anasisitiza kauli hiyo ya Guterres akisema, “Safisha mji wako. Ondoa uchafu wako. Safisha mitaro. Ufanye mji wako kuwa msafi wa kijani. Hiki ndicho ninataka. Kubadilisha tabia. Usitupe taka kwenye mitaro. Unapokuwa na mvua kunafurika, unalaumu mabadiliko ya tabianchi. Ninafurahi kwamba hapa Kenya kumezuiliwa mifuko ya plastiki kwenye maduka lakini ukiangalia nje bado kuna mifuko ya plastiki kwenye mitaro. Kwa hiyo ninafiriki hicho ndicho mtu binafsi anaweza kufanya kama yeye.”Siku ya Kimataifa ya Makazi ya mwaka huu 2024 inaangazia 'Uchumi Mijini Wenye Mnepo’ na uwezekano wa miji kuwa vichochezi vya ukuaji jumuishi, wa kijani na endelevu.
2-10-2023 • 0
Viongozi wa UN wanasema safisha mji wako ili kuunga mkono mzunuko wa uchumi
Mipango ya jamii kudhibiti taka katika maeneo yao inaunga mkono uundaji wa mzunguko wa uchumi, anasema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya leo ya Kimataifa ya Makazi na anaongeza kuwa “juhudi za umma za kupanua maeneo safi ya kijani yanasaidia kupoza maeneo ya mijini nyakati za mawimbi ya joto.”Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani (UN Habitat), Maimunah Mohamed Sharif anasisitiza kauli hiyo ya Guterres akisema, “Safisha mji wako. Ondoa uchafu wako. Safisha mitaro. Ufanye mji wako kuwa msafi wa kijani. Hiki ndicho ninataka. Kubadilisha tabia. Usitupe taka kwenye mitaro. Unapokuwa na mvua kunafurika, unalaumu mabadiliko ya tabianchi. Ninafurahi kwamba hapa Kenya kumezuiliwa mifuko ya plastiki kwenye maduka lakini ukiangalia nje bado kuna mifuko ya plastiki kwenye mitaro. Kwa hiyo ninafiriki hicho ndicho mtu binafsi anaweza kufanya kama yeye.”Siku ya Kimataifa ya Makazi ya mwaka huu 2024 inaangazia 'Uchumi Mijini Wenye Mnepo’ na uwezekano wa miji kuwa vichochezi vya ukuaji jumuishi, wa kijani na endelevu.
2-10-2023 • 0
Simulizi ya kijana mkimbizi Gad Harindimana Mnyarwanda nchini Uganda - FAO inavyofungua uwezo
Makala inatupeleka nchini Uganda kumsikiliza Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi Nakivale mnufaika wa programu ya Huduma za Ajira Vijijini inayoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO kupitia shirika lisilo la kiserikali la AVSI Foundation. Gad Harindimana amepata kazi ya ufundi pikipiki baada ya kukamilisha programu ya Huduma hizo. Anasimulia kwa lugha ya Kinyakole inayotafsiriwa na Anold Kayanda.
29-9-2023 • 0
Simulizi ya kijana mkimbizi Gad Harindimana Mnyarwanda nchini Uganda - FAO inavyofungua uwezo
Makala inatupeleka nchini Uganda kumsikiliza Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi Nakivale mnufaika wa programu ya Huduma za Ajira Vijijini inayoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO kupitia shirika lisilo la kiserikali la AVSI Foundation. Gad Harindimana amepata kazi ya ufundi pikipiki baada ya kukamilisha programu ya Huduma hizo. Anasimulia kwa lugha ya Kinyakole inayotafsiriwa na Anold Kayanda.
29-9-2023 • 0
FAO waeleza kwa nini kuzuia upotevu na utupaji wa chakula ni muhimu na jukumu la kila mtu
Katika siku ya kimataifa ya uhamasishaji kuhusu uelewa wa Upotevu na utupaji wa chakula, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO linataka kila mtu atambue ni kwanini kuzuia na kupumguza upotevu na utupaji wa chakula ni muhimu hasa katika kuchangia mabadiliko ya mifumo ya chakula na utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Siku yam waka huu ambayo imebeba mauadhui “Komesha upotevu na utupaji wa chakula kwa ajili ya watu na sayari” inaadhimishwa huku kati ya watu milioni 691 na 783 walikabiliwa na njaa mmwaka 2022 limesema shirika hilo.Likisisitiza jinsi hali inavyohitaji kubadilika haraka shirika hilo linasema wakati njaa na kutokuwa na uhakika wa chakula kukiendelea duniani mwaka 2022 inakadiriwa kuwa asilimia 13 ya chakula duniani ilipotea kwenye mnyororo wa thamani kuanzia baada ya kuvunwa na kabla ya kufika sokoni, na asilimia 17 nyingine ilitupwa majumbani, kwenye sehemu za utoaji huduma za chakula na kwenye masoko ya chakula.Hivyo FAO inatatoa mwito wa kuchukua hatua kwa mashirika ya umma, sekta binafsi, na kila mtu ili kupunguza upotevu na utupaji wa chakula (FLW) na kuelekea kubadilisha mifumo ya kilimo kwa ajili ya kuweza kuchangia katika mafanikio ya utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya 2030. Kwani limesema Kupunguza upotevu na utupaji wa chakula kunaweza kuwa na jukumu muhimu katika sio tu kwa mabadiliko ya mifumo ya chakula ya kilimo bali pia kwa kuongeza upatikanaji wa chakula, kuchangia uhakika wa chakula, lishe bora, na kujenga mnepo. Upunguzaji wa upotevu na utupaji wa chakula kwa mujibibu wa FAO pia hutumika kama mkakati muhimu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi (GHGs). Kwa hivyo unaweza kusaidia nchi na biashara kuongeza hamasa ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi, huku zikihifadhi na kulinda mifumo yetu ya ikolojia na maliasili ambayo mustakabali wa chakula huitegemea.FAO inasema hivi sasa, mifumo mingi ya kilimo ya chakula duniani sio endelevu, kwani inaharibu ardhi ya kilimo, inachangia uzalishaji wa gesi chafu na upotevu wa bioanuwai na hutumia maji mengi ya ardhini. Mifumo ya chakula pia iko hatarini kwa majanga ya hali ya hewa na mishtuko mingine, kwa sababu ya athari kwa mazingira.
29-9-2023 • 0
FAO waeleza kwa nini kuzuia upotevu na utupaji wa chakula ni muhimu na jukumu la kila mtu
Katika siku ya kimataifa ya uhamasishaji kuhusu uelewa wa Upotevu na utupaji wa chakula, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO linataka kila mtu atambue ni kwanini kuzuia na kupumguza upotevu na utupaji wa chakula ni muhimu hasa katika kuchangia mabadiliko ya mifumo ya chakula na utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Siku yam waka huu ambayo imebeba mauadhui “Komesha upotevu na utupaji wa chakula kwa ajili ya watu na sayari” inaadhimishwa huku kati ya watu milioni 691 na 783 walikabiliwa na njaa mmwaka 2022 limesema shirika hilo.Likisisitiza jinsi hali inavyohitaji kubadilika haraka shirika hilo linasema wakati njaa na kutokuwa na uhakika wa chakula kukiendelea duniani mwaka 2022 inakadiriwa kuwa asilimia 13 ya chakula duniani ilipotea kwenye mnyororo wa thamani kuanzia baada ya kuvunwa na kabla ya kufika sokoni, na asilimia 17 nyingine ilitupwa majumbani, kwenye sehemu za utoaji huduma za chakula na kwenye masoko ya chakula.Hivyo FAO inatatoa mwito wa kuchukua hatua kwa mashirika ya umma, sekta binafsi, na kila mtu ili kupunguza upotevu na utupaji wa chakula (FLW) na kuelekea kubadilisha mifumo ya kilimo kwa ajili ya kuweza kuchangia katika mafanikio ya utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya 2030. Kwani limesema Kupunguza upotevu na utupaji wa chakula kunaweza kuwa na jukumu muhimu katika sio tu kwa mabadiliko ya mifumo ya chakula ya kilimo bali pia kwa kuongeza upatikanaji wa chakula, kuchangia uhakika wa chakula, lishe bora, na kujenga mnepo. Upunguzaji wa upotevu na utupaji wa chakula kwa mujibibu wa FAO pia hutumika kama mkakati muhimu dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi (GHGs). Kwa hivyo unaweza kusaidia nchi na biashara kuongeza hamasa ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi, huku zikihifadhi na kulinda mifumo yetu ya ikolojia na maliasili ambayo mustakabali wa chakula huitegemea.FAO inasema hivi sasa, mifumo mingi ya kilimo ya chakula duniani sio endelevu, kwani inaharibu ardhi ya kilimo, inachangia uzalishaji wa gesi chafu na upotevu wa bioanuwai na hutumia maji mengi ya ardhini. Mifumo ya chakula pia iko hatarini kwa majanga ya hali ya hewa na mishtuko mingine, kwa sababu ya athari kwa mazingira.
29-9-2023 • 0
29 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia utupaji wa chakula, na uchaguzi ujao nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Uganda na mashinani nchini DRC, kulikoni?.Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, Baraza la Usalama limejadili hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo awali Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja huo kuhusu misaada ya kiutu Joyce Msuya anataja changamoto zinazokumba taifa hilo.Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza kabisa tangu ipate uhuru, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendesha makongamano na vyama vya siasa nchini humo.Makala inatupeleka nchini Uganda kumsikiliza Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi Nakivale mnufaika wa programu ya Huduma za Ajira Vijijini inayoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO kupitia shirika lisilo la kiserikali la AVSI Foundation. Harindimana anasimulia kwa lugha ya Kinyakole inayotafsiriwa na Anold Kayanda.Katika mashinani tutammsikia mwanamke ambaye aliweza kujifungua salama, na bila malipo, kwa usaidizi wa wakunga katika kliniki tembezi inayohifadhiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu, UNFPA katika kambi ya wakimbizi wa ndani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
29-9-2023 • 0
29 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia utupaji wa chakula, na uchaguzi ujao nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Uganda na mashinani nchini DRC, kulikoni?.Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, Baraza la Usalama limejadili hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo awali Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja huo kuhusu misaada ya kiutu Joyce Msuya anataja changamoto zinazokumba taifa hilo.Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza kabisa tangu ipate uhuru, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendesha makongamano na vyama vya siasa nchini humo.Makala inatupeleka nchini Uganda kumsikiliza Gad Harindimana, kijana mkimbizi kutoka Rwanda anayeishi katika makazi ya wakimbizi Nakivale mnufaika wa programu ya Huduma za Ajira Vijijini inayoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani, ILO kupitia shirika lisilo la kiserikali la AVSI Foundation. Harindimana anasimulia kwa lugha ya Kinyakole inayotafsiriwa na Anold Kayanda.Katika mashinani tutammsikia mwanamke ambaye aliweza kujifungua salama, na bila malipo, kwa usaidizi wa wakunga katika kliniki tembezi inayohifadhiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu, UNFPA katika kambi ya wakimbizi wa ndani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
29-9-2023 • 0
UNMISS wataka wanasiasa Sudan Kusini wapatie wanachi elimu ya kisiasa
Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza kabisa tangu ipate uhuru, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendesha makongamano na vyama vya siasa nchini humo. Ikiwa imesalia miezi 15 mpaka uchaguzi ufanyike hapo Desemba 2024 UNMISS wanasema lengo la kuandaa makongamano hayo nikujenga utamaduni wa kuwa na mazungumzo thabiti, kutatua changamoto zinazowakabili kuhusu utawala bora na kujenga kuaminiana miongoni mwa wanasiasa na jamii wanazozitumikia. Akiwa katika moja ya majukwaa huyo katika mji mkuu wa Juba Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ambaye pia ni Mkuu wa UNMISS, Nicholas Haysom aliwaambia washiriki kuwa, “Uchaguzi hauwezi kufanyika ikiwa hakuna makubaliano ya masuala ya kiufundi. Hisia za uharaka walizonazo jumuiya ya kimataifa kuhusu uchaguzi hazisaidii. Udharura unawahusu Wasudan Kusini — wananchi, na hasa vyama vya siasa, ndiyo maana tutawaomba nyinyi kufanya kazi na kutusaidia sisi katika kuunda na kuelewa asili ya chaguzi mnazotaka kufanya ili na sisi tuweze kuhamasisha kupatikana kwa misaada kwa ajili ya mambo hayo.”Si wanasiasa pekee wanaohudhuria makongamano hayo bali pia wasomi ambao wamehimiza umuhimu wa kuwa na ushiriki mkubwa wa umma katika michakato ya amani, pamoja vyama vya siasa kuwa na ushindani imara kama anavyoeleza Adwak Nyaba, “Vyama vya siasa vinapaswa kuhimiza elimu ya kisiasa ili kuongeza ufahamu wa kijamii na ufahamu wa kisiasa wa wananchi. Ni kutokana na kuwepo kwa ufahamu wa kisiasa na watu wanaozingatia siasa kunakowezesha uwepo wa serikali za kidemokrasia. Ikiwa watu hawana ufahamu kabisa wa kisiasa, huwezi kuzungumzia utawala wa kidemokrasia, au huwezi kuzungumzia demokrasia.”Wanasiasa wamehimizwa kufikia makubaliano ya masuala muhimu haswa kuhusu uanzishwaji wa taasisi muhimu ambazo ni Baraza la Vyama vya Siasa, Tume ya Kitaifa ya Marekebisho ya Katiba na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi.
29-9-2023 • 0
UNMISS wataka wanasiasa Sudan Kusini wapatie wanachi elimu ya kisiasa
Wakati nchi ya Sudan Kusini ikijiandaa kushiriki katika uchaguzi mkuu kwa mara ya kwanza kabisa tangu ipate uhuru, Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS unaendesha makongamano na vyama vya siasa nchini humo. Ikiwa imesalia miezi 15 mpaka uchaguzi ufanyike hapo Desemba 2024 UNMISS wanasema lengo la kuandaa makongamano hayo nikujenga utamaduni wa kuwa na mazungumzo thabiti, kutatua changamoto zinazowakabili kuhusu utawala bora na kujenga kuaminiana miongoni mwa wanasiasa na jamii wanazozitumikia. Akiwa katika moja ya majukwaa huyo katika mji mkuu wa Juba Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ambaye pia ni Mkuu wa UNMISS, Nicholas Haysom aliwaambia washiriki kuwa, “Uchaguzi hauwezi kufanyika ikiwa hakuna makubaliano ya masuala ya kiufundi. Hisia za uharaka walizonazo jumuiya ya kimataifa kuhusu uchaguzi hazisaidii. Udharura unawahusu Wasudan Kusini — wananchi, na hasa vyama vya siasa, ndiyo maana tutawaomba nyinyi kufanya kazi na kutusaidia sisi katika kuunda na kuelewa asili ya chaguzi mnazotaka kufanya ili na sisi tuweze kuhamasisha kupatikana kwa misaada kwa ajili ya mambo hayo.”Si wanasiasa pekee wanaohudhuria makongamano hayo bali pia wasomi ambao wamehimiza umuhimu wa kuwa na ushiriki mkubwa wa umma katika michakato ya amani, pamoja vyama vya siasa kuwa na ushindani imara kama anavyoeleza Adwak Nyaba, “Vyama vya siasa vinapaswa kuhimiza elimu ya kisiasa ili kuongeza ufahamu wa kijamii na ufahamu wa kisiasa wa wananchi. Ni kutokana na kuwepo kwa ufahamu wa kisiasa na watu wanaozingatia siasa kunakowezesha uwepo wa serikali za kidemokrasia. Ikiwa watu hawana ufahamu kabisa wa kisiasa, huwezi kuzungumzia utawala wa kidemokrasia, au huwezi kuzungumzia demokrasia.”Wanasiasa wamehimizwa kufikia makubaliano ya masuala muhimu haswa kuhusu uanzishwaji wa taasisi muhimu ambazo ni Baraza la Vyama vya Siasa, Tume ya Kitaifa ya Marekebisho ya Katiba na Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi.
29-9-2023 • 0
Methali: Umekuwa Jeta Hubanduki!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali Umekuwa Jeta Hubanduki!
28-9-2023 • 0
Methali: Umekuwa Jeta Hubanduki!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali Umekuwa Jeta Hubanduki!
28-9-2023 • 0
28 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake wamewezesha hatua ya upimaji wa udongo katika wilaya sita ambako mradi wa kulinda na kuhifadhi baiyonuai unatekelezwa. Kazi hiyo imefanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA, na sasa utafiti huo umekamilika, Je umebaini nini? John Kabambala wa redio washirika KidsTime ya Morogoro-Tanzania amehudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo ya vipimo vya udongo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za ulinzi wa amani, haki za binadamu na ubaguzi wa rangi. Na katika kujifunza lugha ya kiswahili tunakuletea maana ya methali “UMEKUWA JETA HUBANDUKI”.Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, Baraza la Usalama limejadili hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo awali Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja huo kuhusu misaada ya kiutu Joyce Msuya anataja changamoto zinazokumba taifa hilo.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk, ametoa wito wa ujumbe wa kimataifa wa kusaidia polisi wa kitaifa nchini Haiti kutokomeza mzunguko wa ghasia uliojikita kwenye ngazi zote za jamii na kuchochea janga la ukosefu wa usalama na haki za binadamu.Na mfumo wa kibaguzi dhidi ya wamarekani weusi wenye asili ya Afrika umepenyezwa hadi kwenye utendaji wa jeshi la polisi na mfumo wa mahakama nchini Marekani na hivyo lazima marekebisho ya haraka yafanywe ili kuondokana na madhila yanayokumba wananchi hao, imesema ripoti mpya ya wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali “Umekuwa Jeta Hubanduki!”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
28-9-2023 • 0
28 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake wamewezesha hatua ya upimaji wa udongo katika wilaya sita ambako mradi wa kulinda na kuhifadhi baiyonuai unatekelezwa. Kazi hiyo imefanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA, na sasa utafiti huo umekamilika, Je umebaini nini? John Kabambala wa redio washirika KidsTime ya Morogoro-Tanzania amehudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo ya vipimo vya udongo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za ulinzi wa amani, haki za binadamu na ubaguzi wa rangi. Na katika kujifunza lugha ya kiswahili tunakuletea maana ya methali “UMEKUWA JETA HUBANDUKI”.Hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani, Baraza la Usalama limejadili hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambapo awali Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja huo kuhusu misaada ya kiutu Joyce Msuya anataja changamoto zinazokumba taifa hilo.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk, ametoa wito wa ujumbe wa kimataifa wa kusaidia polisi wa kitaifa nchini Haiti kutokomeza mzunguko wa ghasia uliojikita kwenye ngazi zote za jamii na kuchochea janga la ukosefu wa usalama na haki za binadamu.Na mfumo wa kibaguzi dhidi ya wamarekani weusi wenye asili ya Afrika umepenyezwa hadi kwenye utendaji wa jeshi la polisi na mfumo wa mahakama nchini Marekani na hivyo lazima marekebisho ya haraka yafanywe ili kuondokana na madhila yanayokumba wananchi hao, imesema ripoti mpya ya wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali “Umekuwa Jeta Hubanduki!”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
28-9-2023 • 0
Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine na FAO Tanzania wapima udongo katika wilaya 6 Tanzania
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake wamewezesha hatua ya upimaji wa udongo katika wilaya sita ambako mradi wa kulinda na kuhifadhi baiyonuai unatekelezwa. Kazi hiyo imefanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA, na sasa utafiti huo umekamilika, Je umebaini nini? John Kabambala wa redio washirika KidsTime ya Morogoro-Tanzania amehudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo ya vipimo vya udongo.
28-9-2023 • 0
Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine na FAO Tanzania wapima udongo katika wilaya 6 Tanzania
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wake wamewezesha hatua ya upimaji wa udongo katika wilaya sita ambako mradi wa kulinda na kuhifadhi baiyonuai unatekelezwa. Kazi hiyo imefanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine - SUA, na sasa utafiti huo umekamilika, Je umebaini nini? John Kabambala wa redio washirika KidsTime ya Morogoro-Tanzania amehudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo ya vipimo vya udongo.
28-9-2023 • 0
27 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tuanaangazia usafirishaji baharini, na ulinzi wa amani. Makala tunakupeleka mjini Roma na mashinani tutasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kuikoni?Usafirishaji baharini unapaswa kuangaliwa upya ili kupunguza hewa ya ukaa au kaboni inayochafua mazingira, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara duniani, UNCTAD.Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA, Jenerali Humphrey Nyone amewataka walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu nchini humo chini ya MINUSCA kuendelea na moyo wa uchapa kazi huku wakizingatia kuepuka unyanyasaji na unyonyaji wa kingono.Katika makala Evarist Mapesa anayetuletea makala kutoka nchini Thailand ikiangazia mradi unaotekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO wakusaidia wafanyabiashara kupunguza upotevu na utupaji wa chakula.Mashinani tunasalia katika ajenda 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu kusikia ujumbe wa Orlando Bloom, Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
27-9-2023 • 0
27 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tuanaangazia usafirishaji baharini, na ulinzi wa amani. Makala tunakupeleka mjini Roma na mashinani tutasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kuikoni?Usafirishaji baharini unapaswa kuangaliwa upya ili kupunguza hewa ya ukaa au kaboni inayochafua mazingira, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara duniani, UNCTAD.Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA, Jenerali Humphrey Nyone amewataka walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu nchini humo chini ya MINUSCA kuendelea na moyo wa uchapa kazi huku wakizingatia kuepuka unyanyasaji na unyonyaji wa kingono.Katika makala Evarist Mapesa anayetuletea makala kutoka nchini Thailand ikiangazia mradi unaotekelezwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO wakusaidia wafanyabiashara kupunguza upotevu na utupaji wa chakula.Mashinani tunasalia katika ajenda 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu kusikia ujumbe wa Orlando Bloom, Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
27-9-2023 • 0
Mradi wa FAO wa kupunguza upotevu wa chakula wazaa matunda nchini Thailand
Kupunguza upotevu wa chakula na taka kuna jukumu muhimu katika kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula.Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs inataka kupunguza nusu ya upotevu wa chakula duniani kwa kila mtu katika viwango vya rejareja na walaji wa mwisho na pia inapigia chepuo kuimarisha minyororo ya uzalishaji na usambazaji wa chakula.Nchini Thailand shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo FAO linatekeleza mradi wa kuwapatia ujuzi wafanyabiashara wadogo na wa kati ili waweze kupunguza upotevu na uharibifu wa chakula na pia kuongeza thamani ya mazao yao na hatimaye kujipatia kipato zaidi. Tuungane na Evarist Mapesa katika Makala hii akitujuza ziadi kuhusu mradi huo.
27-9-2023 • 0
Mradi wa FAO wa kupunguza upotevu wa chakula wazaa matunda nchini Thailand
Kupunguza upotevu wa chakula na taka kuna jukumu muhimu katika kubadilisha mifumo ya kilimo na chakula.Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa SDGs inataka kupunguza nusu ya upotevu wa chakula duniani kwa kila mtu katika viwango vya rejareja na walaji wa mwisho na pia inapigia chepuo kuimarisha minyororo ya uzalishaji na usambazaji wa chakula.Nchini Thailand shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo FAO linatekeleza mradi wa kuwapatia ujuzi wafanyabiashara wadogo na wa kati ili waweze kupunguza upotevu na uharibifu wa chakula na pia kuongeza thamani ya mazao yao na hatimaye kujipatia kipato zaidi. Tuungane na Evarist Mapesa katika Makala hii akitujuza ziadi kuhusu mradi huo.
27-9-2023 • 0
UNCTAD: Hatua za kijasiri zahitajika kukabili hewa ya ukaa kwenye usafiri baharini
Usafirishaji baharini unapaswa kuangaliwa upya ili kupunguza hewa ya ukaa au kaboni inayochafua mazingira, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara duniani, UNCTAD. Ikipatiwa jina Usafiri wa Baharini mwaka 2030, ripoti inahimiza hatua za kijasiri na ushirikiano wa mfumo mzima kwa kuzingatia umuhimu wake duniani lakini vile vile uchafuzi wake wa mazingira sababu kuu ikiwa vyombo hivyo vya usafiri maji kuwa kuukuu. Mkurugenzi wa UNCTAD anayehusika na teknolojia Shamika N. Sirimanne anasema, “Usafiri wa baharini ni tegemeo kuu la uchumi wa dunia ukibeba asilimia 80 ya biashara yote. Sekta hii muhimu inachangia asilimia 3 ya hewa chafuzi zinazotolewa duniani. Na kadri biashara kupitia usafiri wa baharíni unakua, vivyo utoaji wa hewa chafuzi ambao umeongezeka kwa asilimia 20 muongo mmoja uliopita.” Sasa jawabu ni nini? “Tunahitaji hatua za kijasiri duniani za kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa wakati wa usafirishaji baharini. Na ili kuhakikisha mpito wenye haki na sawia katika kuelekea nishati salama ni lazima tushirikishe wadau wote kwenye sekta ya usafiri majini. UNCTAD tunatoa wito mifumo ya udhibiti ya kimataifa itumike kwa meli zote bila kujali ni ya nchi gani au inamilikiwa na nani.” UNCTAD inasisitiza mfumo wa ushirikiano mpana zaidi, uingiliaji kati haraka kuchukua hatua na uwekezaji thabiti kwenye teknolojia za usafirishaji zisizochafua mazingira, halikadhalika ununuzi wa vyombo vipya vya usafiri baharini.
27-9-2023 • 0
UNCTAD: Hatua za kijasiri zahitajika kukabili hewa ya ukaa kwenye usafiri baharini
Usafirishaji baharini unapaswa kuangaliwa upya ili kupunguza hewa ya ukaa au kaboni inayochafua mazingira, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara duniani, UNCTAD. Ikipatiwa jina Usafiri wa Baharini mwaka 2030, ripoti inahimiza hatua za kijasiri na ushirikiano wa mfumo mzima kwa kuzingatia umuhimu wake duniani lakini vile vile uchafuzi wake wa mazingira sababu kuu ikiwa vyombo hivyo vya usafiri maji kuwa kuukuu. Mkurugenzi wa UNCTAD anayehusika na teknolojia Shamika N. Sirimanne anasema, “Usafiri wa baharini ni tegemeo kuu la uchumi wa dunia ukibeba asilimia 80 ya biashara yote. Sekta hii muhimu inachangia asilimia 3 ya hewa chafuzi zinazotolewa duniani. Na kadri biashara kupitia usafiri wa baharíni unakua, vivyo utoaji wa hewa chafuzi ambao umeongezeka kwa asilimia 20 muongo mmoja uliopita.” Sasa jawabu ni nini? “Tunahitaji hatua za kijasiri duniani za kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa wakati wa usafirishaji baharini. Na ili kuhakikisha mpito wenye haki na sawia katika kuelekea nishati salama ni lazima tushirikishe wadau wote kwenye sekta ya usafiri majini. UNCTAD tunatoa wito mifumo ya udhibiti ya kimataifa itumike kwa meli zote bila kujali ni ya nchi gani au inamilikiwa na nani.” UNCTAD inasisitiza mfumo wa ushirikiano mpana zaidi, uingiliaji kati haraka kuchukua hatua na uwekezaji thabiti kwenye teknolojia za usafirishaji zisizochafua mazingira, halikadhalika ununuzi wa vyombo vipya vya usafiri baharini.
27-9-2023 • 0
Mkuu wa MINUSCA kwa TANBAT6 - Zingatieni uhusiano mwema na raia
Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA, Jenerali Humphrey Nyone amewataka walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu nchini humo chini ya MINUSCA kuendelea na moyo wa uchapa kazi huku wakizingatia kuepuka unyanyasaji na unyonyaji wa kingono. Akitokea katika makao makuu ya MINUSCA yaliyoko kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Bangui (tamka Bongii) takribani kilometa 292 magharibi mwa Mambéré-Kadéï, Jenerali Humphray Nyone ametua katika uwanja wa ndege wa mjini wa Berberati na baadaye akiambatana na wanadhimu wa kijeshi akazungumza na askari wa Kikosi cha 6 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT6 wanaohudumu chini ya MINUSCA, "Askari mila na desturi yake ni nidhamu na kufuata maelekezo. Hapa mlipo nimempata taarifa kutoka kwa kamanda Kikosi hiki Luteni Kanali Ramadhani Shaaban Ramadhani jinsi mnavyo jituma katika utendaji kazi wenu nimefurahi sana kusikia hivyo. Aidha hii ni kweli kwamba kikosi hiki kinasaidia kikundi changu vyema katika kutekeleza na kukamilisha jukumu la MINUSCA hapa Jamhuri ya Afrika ya Kati ninawasihi kuendelea hivyo bila kusahau kuzidi kuepuka suala zima la unyanyasaji wa kingono. Asante sana."Naye Kamanda wa TABAT6 Luteni Kanali Ramadhani Shaaban Ramadhani amesema amepokea na kuahidi kudumisha aliyoelekezwa katika katika utendaji wa kikosi hicho cha walinda amani kutoka Tanzania.
27-9-2023 • 0
Mkuu wa MINUSCA kwa TANBAT6 - Zingatieni uhusiano mwema na raia
Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA, Jenerali Humphrey Nyone amewataka walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu nchini humo chini ya MINUSCA kuendelea na moyo wa uchapa kazi huku wakizingatia kuepuka unyanyasaji na unyonyaji wa kingono. Akitokea katika makao makuu ya MINUSCA yaliyoko kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Bangui (tamka Bongii) takribani kilometa 292 magharibi mwa Mambéré-Kadéï, Jenerali Humphray Nyone ametua katika uwanja wa ndege wa mjini wa Berberati na baadaye akiambatana na wanadhimu wa kijeshi akazungumza na askari wa Kikosi cha 6 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT6 wanaohudumu chini ya MINUSCA, "Askari mila na desturi yake ni nidhamu na kufuata maelekezo. Hapa mlipo nimempata taarifa kutoka kwa kamanda Kikosi hiki Luteni Kanali Ramadhani Shaaban Ramadhani jinsi mnavyo jituma katika utendaji kazi wenu nimefurahi sana kusikia hivyo. Aidha hii ni kweli kwamba kikosi hiki kinasaidia kikundi changu vyema katika kutekeleza na kukamilisha jukumu la MINUSCA hapa Jamhuri ya Afrika ya Kati ninawasihi kuendelea hivyo bila kusahau kuzidi kuepuka suala zima la unyanyasaji wa kingono. Asante sana."Naye Kamanda wa TABAT6 Luteni Kanali Ramadhani Shaaban Ramadhani amesema amepokea na kuahidi kudumisha aliyoelekezwa katika katika utendaji wa kikosi hicho cha walinda amani kutoka Tanzania.
27-9-2023 • 0
MONUSCO na ufanikishaji wa uchaguzi mkuu wa 2023 DRC
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, (MONUSCO) unashiriki katika maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ambapo tayari umeshasaidia usafirishaji wa nyaraka za uchaguzi, halikadhalika mafunzo kwa polisi wa kitaifa ili uchaguzi huo uwe huru na ufanyike kwa amani.Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita, Rais wa DRC Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani alithibitisha kuwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge, magavana na madiwani utafanyika kama ilivyopangwa na Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo, CENI tayari imeshaanza kuchapisha majina ya wagombea.Tumesafirisha nyaraka nyeti za CENIAkizungumza George Musubao wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC, Msemaji wa MONUSCO mjini Beni-Lubero Bwana Jean Tobie Okala amesema “CENI inatuambia inabidi zifanyike kwa hali ya usalama na amani. Jambo la kwanza ni kuungwa mkono kwa CENI. Nakujulisha kwamba tangu Januari 2023 MONUSCO imesafirisha maelfu ya tani za shehena nyeti sana za uchaguzi ambazo ni za CENI na ambazo zimewezesha shughuli za kurekodi na kuandikisha wapiga.”
26-9-2023 • 0
MONUSCO na ufanikishaji wa uchaguzi mkuu wa 2023 DRC
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, (MONUSCO) unashiriki katika maandalizi ya uchaguzi mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu ambapo tayari umeshasaidia usafirishaji wa nyaraka za uchaguzi, halikadhalika mafunzo kwa polisi wa kitaifa ili uchaguzi huo uwe huru na ufanyike kwa amani.Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita, Rais wa DRC Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani alithibitisha kuwa uchaguzi mkuu wa rais, wabunge, magavana na madiwani utafanyika kama ilivyopangwa na Tume Huru ya Uchaguzi nchini humo, CENI tayari imeshaanza kuchapisha majina ya wagombea.Tumesafirisha nyaraka nyeti za CENIAkizungumza George Musubao wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC, Msemaji wa MONUSCO mjini Beni-Lubero Bwana Jean Tobie Okala amesema “CENI inatuambia inabidi zifanyike kwa hali ya usalama na amani. Jambo la kwanza ni kuungwa mkono kwa CENI. Nakujulisha kwamba tangu Januari 2023 MONUSCO imesafirisha maelfu ya tani za shehena nyeti sana za uchaguzi ambazo ni za CENI na ambazo zimewezesha shughuli za kurekodi na kuandikisha wapiga.”
26-9-2023 • 0
26 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo alihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kutangaza kuwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwishoni mwa mwaka huu, utafanyika kama ilivyopangwa. Alisema tayari Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC, CENI [SENI] imeshachapisha majina ya wagombea na michakato mingine inaendelea. Kufuatia kauli hiyo, mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini humo, George Musubao amezungumza na msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO ofisi ya Beni-Lubero jimboni Kivu Kaskazini Tobi Okala, kufahamu MONUSCO inafanya nini kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru na amani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani, baki nasi!Hii leo Mjadala Mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umekunja jamvi ambapo viongozi na wawakilishi kutoka nchi 15 wamehutubia wakiwemo kutoka India, Zambia na Morocco. Mjadala huo umefungwa na Rais wa Baraza Kuu Balozi Dennis Francis.Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Kabisa Silaha za Nyuklia inatukumbusha kwamba wakati ujao wenye amani unategemea kukomeshwa kwa tishio la nyuklia, ndivyo António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alivyouanza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 26 Septemba. Kwa msingi huo Guterres anatoa wito mataifa yenye silaha za nyuklia yaongoze kwa kutimiza wajibu wao wa kupokonya silaha, na kujitolea kamwe kutotumia silaha za nyuklia kwa hali yoyote.Na Leo, ili kusaidia kulinda afya ya Watoto, Shirika la Umoja wa Matafa la Afya Ulimwenguni limetoa machapisho mawili mapya, “Uhuru dhidi ya tumbaku na nikotini: mwongozo kwa shule,” na “zana za shule zisizo na nikotini na tumbaku.” Lengo la machapisho hayo ni kuzuia hali ambayo inazidi kuenea ya matumizi ya sigara hasa za kielektroniki kwa vijana hasa wanafunzi.Katika mashinani Samuel Eto’o Rais wa shirikisho la soka Cameroon anasema mchezaji atamulika mbinu za kuepusha soka kutumika kusafirisha kiharamu binadamu.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
26-9-2023 • 0
26 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Félix-Antoine Tshisekedi Tshilombo alihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kutangaza kuwa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika nchini humo mwishoni mwa mwaka huu, utafanyika kama ilivyopangwa. Alisema tayari Tume Huru ya Uchaguzi nchini DRC, CENI [SENI] imeshachapisha majina ya wagombea na michakato mingine inaendelea. Kufuatia kauli hiyo, mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini humo, George Musubao amezungumza na msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO ofisi ya Beni-Lubero jimboni Kivu Kaskazini Tobi Okala, kufahamu MONUSCO inafanya nini kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uhuru na amani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani, baki nasi!Hii leo Mjadala Mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa umekunja jamvi ambapo viongozi na wawakilishi kutoka nchi 15 wamehutubia wakiwemo kutoka India, Zambia na Morocco. Mjadala huo umefungwa na Rais wa Baraza Kuu Balozi Dennis Francis.Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Kabisa Silaha za Nyuklia inatukumbusha kwamba wakati ujao wenye amani unategemea kukomeshwa kwa tishio la nyuklia, ndivyo António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alivyouanza ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 26 Septemba. Kwa msingi huo Guterres anatoa wito mataifa yenye silaha za nyuklia yaongoze kwa kutimiza wajibu wao wa kupokonya silaha, na kujitolea kamwe kutotumia silaha za nyuklia kwa hali yoyote.Na Leo, ili kusaidia kulinda afya ya Watoto, Shirika la Umoja wa Matafa la Afya Ulimwenguni limetoa machapisho mawili mapya, “Uhuru dhidi ya tumbaku na nikotini: mwongozo kwa shule,” na “zana za shule zisizo na nikotini na tumbaku.” Lengo la machapisho hayo ni kuzuia hali ambayo inazidi kuenea ya matumizi ya sigara hasa za kielektroniki kwa vijana hasa wanafunzi.Katika mashinani Samuel Eto’o Rais wa shirikisho la soka Cameroon anasema mchezaji atamulika mbinu za kuepusha soka kutumika kusafirisha kiharamu binadamu.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
26-9-2023 • 0
Tuna imani Tanzania tutafikia lengo la huduma za afya kwa yote 2030: Waziri Ummy
Tanzania taifa lililo Afrika Mashariki limesema limejipanga vyema katika kutekeleza azimio la kuchukua hatua kuhusu huduma za afya kwa wote lililoidhinishwa kwa kauli moja mwishoni mwa juma na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu alikuwa miongoni mwa waliohudhuria na ameketi chini na Flora Nducha wa Idhaa hii na kumfafanulia mikakati yao ya kutekeleza azimio hilo.
25-9-2023 • 0
Tuna imani Tanzania tutafikia lengo la huduma za afya kwa wote 2030: Waziri Ummy
Tanzania taifa lililo Afrika Mashariki limesema limejipanga vyema katika kutekeleza azimio la kuchukua hatua kuhusu huduma za afya kwa wote lililoidhinishwa kwa kauli moja mwishoni mwa juma na nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Waziri wa afya wa Tanzania Ummy Mwalimu alikuwa miongoni mwa waliohudhuria na ameketi chini na Flora Nducha wa Idhaa hii na kumfafanulia mikakati yao ya kutekeleza azimio hilo.
25-9-2023 • 0
Vitendo vya kikatili vya Urusi nchini Ukraine vinasikitisha - Tume ya UN
Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ukraine imeripoti leo kwa Baraza la Haki za Kibinadamu kwamba kuna ushahidi kuwa wanajeshi wa Urusi wanaendelea wanafanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.Katika taarifa yao waliyoiwasilisha leo katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi, Tume hiyo ya Huru ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kinagaubaga kwamba wanajeshi wa Urusi wanafanya mashambulizi haramu ya kutumia silaha za milipuko, mateso, unyanyasaji wa kingono na kijinsia, na mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati.Wakati wa uwasilishaji kwa Baraza la Haki za Kibinadamu, Tume imeripoti kwamba imerekodi mashambulizi ya silaha za milipuko kwenye majengo ya makazi, kituo cha matibabu kinachofanya kazi, kituo cha reli, mgahawa, maduka na maghala ya biashara. Mashambulizi haya yalisababisha vifo vya raia, uharibifu wa miundombinu muhimu, na kukatizwa kwa huduma muhimu.Taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya Habari imeeleza kuwa Tume inachunguza sababu ya uvunjaji wa bwawa la Nova Kakhovka na athari zake kwa raia.Wakati huo huo Tume imeeleza kuwa uchunguzi wake huko Kherson na Zaporizhzhia unaonesha matumizi makubwa na yaliyoratibiwa ya utesaji yanayotekelezwa na vikosi vya jeshi la Urusi dhidi ya watu wanaoshutumiwa kuwa watoa habari wa vikosi vya jeshi la Ukraine. Katika matukio fulani, mateso yalifanywa kwa ukatili kiasi kwamba yalisababisha kifo.Mtu mmoja ambaye aliteswa kwa kupigwa na mshtuko wa umeme aliiambia tume kwamba kila wakati alipojibu kwamba hajui wala hakumbuki jambo Fulani, walimpiga shoti za umeme na hajui hali hiyo ilidumu kwa muda gani kwani kwake aliona ni kama milele. Katika eneo la Kherson, askari wa Urusi waliwabaka na kufanya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake wa umri wa kuanzia miaka 19 hadi 83, Tume iligundua. Mara kwa mara, wanafamilia waliwekwa katika chumba cha karibu na hivyo kulazimika kusikia ukiukaji unaofanyika.Tume imeendelea kuchunguza hali za kibinafsi za uhamisho wa madai ya kuhamishwa watoto wa Ukraine bila usimamizi wowote na kuwapeleka Urusi. Tume pia ina wasiwasi kuhusu madai ya mauaji ya kimbari nchini Ukraine. Kwa mfano, baadhi ya matamshi yanayosambazwa katika Urusi na vyombo vingine vya habari yanaweza kujumuisha uchochezi wa mauaji ya kimbari. Tume inaendelea na uchunguzi wake kuhusu masuala hayo.Tume inasisitiza wasiwasi wake mkubwa juu ya ukubwa na uzito wa ukiukaji ambao umefanywa nchini Ukraine na vikosi vya kijeshi vya Urusi na inasisitiza haja ya uwajibikaji. Pia inakumbuka hitaji la mamlaka ya Ukraine kuchunguza kwa haraka na kwa kina visa vichache vya ukiukaji wa sheria uliofanywa na vikosi vyao wenyewe. Taarifa hii mpya ya Tume kwa Baraza la Haki za Kibinadamu ni mwendelezo wa ripoti zake za awali, ikijumuisha Waraka wake wenye matokeo ya uchunguzi wa kina, iliyotolewa tarehe 29 Agosti 2023.Tangu kuanzishwa kwake, Tume imesafiri zaidi ya mara kumi Kwenda Ukraine. Wakati wa uchunguzi wake, wanachama na wachunguzi wake walikutana na mamlaka za serikali, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kiraia, na wadau wengine husika.Tume Huru ya Kimataifa ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine ni chombo huru kilichopewa mamlaka na Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, pamoja na mambo mengine, kuchunguza ukiukwaji wote wa haki za binadamu na ukiukwaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu, na uhalifu unaohusiana nao katika muktadha wa uchokozi dhidi ya Ukraine unaofanywa na Shirikisho la Urusi. Tume itawasilisha ripoti za shughuli zake kwa Baraza Kuu mwezi Oktoba mwaka huu 2023, na kwa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mnamo Machi mwaka kesho 2024.
25-9-2023 • 0
Vitendo vya kikatili vya Urusi nchini Ukraine vinasikitisha - Tume ya UN
Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ukraine imeripoti leo kwa Baraza la Haki za Kibinadamu kwamba kuna ushahidi kuwa wanajeshi wa Urusi wanaendelea wanafanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.Katika taarifa yao waliyoiwasilisha leo katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Geneva, Uswisi, Tume hiyo ya Huru ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kinagaubaga kwamba wanajeshi wa Urusi wanafanya mashambulizi haramu ya kutumia silaha za milipuko, mateso, unyanyasaji wa kingono na kijinsia, na mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati.Wakati wa uwasilishaji kwa Baraza la Haki za Kibinadamu, Tume imeripoti kwamba imerekodi mashambulizi ya silaha za milipuko kwenye majengo ya makazi, kituo cha matibabu kinachofanya kazi, kituo cha reli, mgahawa, maduka na maghala ya biashara. Mashambulizi haya yalisababisha vifo vya raia, uharibifu wa miundombinu muhimu, na kukatizwa kwa huduma muhimu.Taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya Habari imeeleza kuwa Tume inachunguza sababu ya uvunjaji wa bwawa la Nova Kakhovka na athari zake kwa raia.Wakati huo huo Tume imeeleza kuwa uchunguzi wake huko Kherson na Zaporizhzhia unaonesha matumizi makubwa na yaliyoratibiwa ya utesaji yanayotekelezwa na vikosi vya jeshi la Urusi dhidi ya watu wanaoshutumiwa kuwa watoa habari wa vikosi vya jeshi la Ukraine. Katika matukio fulani, mateso yalifanywa kwa ukatili kiasi kwamba yalisababisha kifo.Mtu mmoja ambaye aliteswa kwa kupigwa na mshtuko wa umeme aliiambia tume kwamba kila wakati alipojibu kwamba hajui wala hakumbuki jambo Fulani, walimpiga shoti za umeme na hajui hali hiyo ilidumu kwa muda gani kwani kwake aliona ni kama milele. Katika eneo la Kherson, askari wa Urusi waliwabaka na kufanya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake wa umri wa kuanzia miaka 19 hadi 83, Tume iligundua. Mara kwa mara, wanafamilia waliwekwa katika chumba cha karibu na hivyo kulazimika kusikia ukiukaji unaofanyika.Tume imeendelea kuchunguza hali za kibinafsi za uhamisho wa madai ya kuhamishwa watoto wa Ukraine bila usimamizi wowote na kuwapeleka Urusi. Tume pia ina wasiwasi kuhusu madai ya mauaji ya kimbari nchini Ukraine. Kwa mfano, baadhi ya matamshi yanayosambazwa katika Urusi na vyombo vingine vya habari yanaweza kujumuisha uchochezi wa mauaji ya kimbari. Tume inaendelea na uchunguzi wake kuhusu masuala hayo.Tume inasisitiza wasiwasi wake mkubwa juu ya ukubwa na uzito wa ukiukaji ambao umefanywa nchini Ukraine na vikosi vya kijeshi vya Urusi na inasisitiza haja ya uwajibikaji. Pia inakumbuka hitaji la mamlaka ya Ukraine kuchunguza kwa haraka na kwa kina visa vichache vya ukiukaji wa sheria uliofanywa na vikosi vyao wenyewe. Taarifa hii mpya ya Tume kwa Baraza la Haki za Kibinadamu ni mwendelezo wa ripoti zake za awali, ikijumuisha Waraka wake wenye matokeo ya uchunguzi wa kina, iliyotolewa tarehe 29 Agosti 2023.Tangu kuanzishwa kwake, Tume imesafiri zaidi ya mara kumi Kwenda Ukraine. Wakati wa uchunguzi wake, wanachama na wachunguzi wake walikutana na mamlaka za serikali, mashirika ya kimataifa, mashirika ya kiraia, na wadau wengine husika.Tume Huru ya Kimataifa ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine ni chombo huru kilichopewa mamlaka na Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, pamoja na mambo mengine, kuchunguza ukiukwaji wote wa haki za binadamu na ukiukwaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu, na uhalifu unaohusiana nao katika muktadha wa uchokozi dhidi ya Ukraine unaofanywa na Shirikisho la Urusi. Tume itawasilisha ripoti za shughuli zake kwa Baraza Kuu mwezi Oktoba mwaka huu 2023, na kwa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa mnamo Machi mwaka kesho 2024.
25-9-2023 • 0
25 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Ukraine na mkutano wa kimataifa huko Rome kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa wanyama. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Poland, kulikoni?Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ukraine imeripoti leo kwa Baraza la Haki za Kibinadamu kwamba kuna ushahidi unaoendelea kuwa wanajeshi wa Urusi wanafanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.Mkutano wa kwanza kabisa wa kimataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa Wanyama umeanza hii leo kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO lengo likiwa ni kusaka mbinu za kuwezesha ufugaji huo uwe na mnepo zaidi, usiharibu mazingira na uchangie katika maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii, halikadhalika sayari yenye afya.Katika makala Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu aliketi chini na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili kuzungumzia mikakati ya nchi hiyo katika kulitekeleza azimio la Umoja wa Mataifa la kuchukua hatua kuhusu huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030.Mashinani tunakupeleka nchini Poland kusikia jinsi ambavyo wakimbizi wa Ukraine walivyoshindwa kuendelea na matibabu ya kifua kikuu baada ya kulazimika kukimbia makwao.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
25-9-2023 • 0
25 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Ukraine na mkutano wa kimataifa huko Rome kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa wanyama. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Poland, kulikoni?Tume ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ukraine imeripoti leo kwa Baraza la Haki za Kibinadamu kwamba kuna ushahidi unaoendelea kuwa wanajeshi wa Urusi wanafanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine.Mkutano wa kwanza kabisa wa kimataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa Wanyama umeanza hii leo kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO lengo likiwa ni kusaka mbinu za kuwezesha ufugaji huo uwe na mnepo zaidi, usiharibu mazingira na uchangie katika maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii, halikadhalika sayari yenye afya.Katika makala Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu aliketi chini na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili kuzungumzia mikakati ya nchi hiyo katika kulitekeleza azimio la Umoja wa Mataifa la kuchukua hatua kuhusu huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030.Mashinani tunakupeleka nchini Poland kusikia jinsi ambavyo wakimbizi wa Ukraine walivyoshindwa kuendelea na matibabu ya kifua kikuu baada ya kulazimika kukimbia makwao.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
25-9-2023 • 0
FAO: Ufugaji endelevu unaonufaisha jamii bila kuharibu mazingira wamulikwa huko Roma, Italia
Mkutano wa kwanza kabisa wa kimataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa Wanyama umeanza hii leo kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO lengo likiwa ni kusaka mbinu za kuwezesha ufugaji huo uwe na mnepo zaidi, usiharibu mazingira na uchangie katika maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii, halikadhalika sayari yenye afya. Mkutano huo wa siku tatu unaleta pamoja wawakilishi wanachama wa FAO, mashirika yanayohusika n uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo, watafiti, wanazuoni, mashirika ya maendeleo, mashirika ya kiraia na sekta binafsi ambapo watapata fursa kujadili mbinu bunifu na za ugunduzi ili hatimye sekta ya mifugo iweze kuzalisha mazao yenye lishe bora zaidi, gharama nafuu huku ikichangia kidogo katika uchafuzi wa mazingira. Thanawat Tiensin, Mkurugenzi wa Kitengo cha FAO kinachohusika na Uzalishaji wa Mifugo na Afya anafafanua maana ya ufugaji endelevu wa Wanyama. "Ufugaji endelevu unahusisha mwenendo unaolenga kukidhi mahitaji ya kufuga wanyama kwa ajili ya chakula huku ukipunguza uharibifu wa mazingira. Ufugaji endelevu unasongesha uwepo wa mifumo ya kilimo cha mazao ya chakula, hulinda maliasili, huboresha mnepo wa kiuchumi na huchangia kwenye mustakabali endelevu na wenye mnepo zaidi.” Wakati huu ambapo mahitaji ya mazao yatokanayo na mifugo duniani yakitarajiwa kuongezeka kwa asilimia 20 ifikapo mwaka 2050, nyama, mayai na bidhaa za maziwa zitakuwa dhima muhimu katika kuhakikisha uhakika wa upatikanaji wa chakula na mlo wenye afya na endelevu. Bwana Tiensin anaelezea zaidi jukumu la mkutano. "Ili kuzalisha mifugo huku unapunguza madhara, kwanza lazima tujitike katika mifumo fanisi ya ufugaji. Hii inajumuisha kubadili na kutumia vema chakula cha mifugo, kupunguza utupaji wa chakula hicho, matumizi mazuri ya virutubisho, kupunguza umomonyoaji wa udongo na vyanzo vya maji, kupunguza utoaji wa hewa chafuzi na kupunguza uharibifu wa mazingira. Halikadhalika, kupatia kipaumbele mifumo ya kilimo na ufugaji wa kisasa unaokidhi tabianchi.” Na zaidi ya yote, "Mkutano huu wa kimataifa utatoa fursa ya kuangazia tafiti na ujumbe muhimu, na kuchangia katika mazungumzo ya dunia kuhusu ufugaji endelevu na nafasi yake katika kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi. Kwa ujumla mkutano huu una dhima muhimu katika kusongesha ajenda ya ufugaji endelevu na kuendeleza mbinu zote ambazo zinashughulikia masuala ya kimazingira, kijamii na kiuchumi ya mifumo ya ufugaji.” Mambo yanayomulikwa ni pamoja na chakula na afya ya mifugo, lishe ya binadamu, matumizi ya teknolojia, na nafasi ya mifugo katika kuwezesha wafugaji wadogo kuendesha maisha yao na pia uhusiano kati ya ufugaji na uendelevu wa mazingira, uchumi na jamii.
25-9-2023 • 0
FAO: Ufugaji endelevu unaonufaisha jamii bila kuharibu mazingira wamulikwa huko Roma, Italia
Mkutano wa kwanza kabisa wa kimataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa Wanyama umeanza hii leo kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO lengo likiwa ni kusaka mbinu za kuwezesha ufugaji huo uwe na mnepo zaidi, usiharibu mazingira na uchangie katika maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii, halikadhalika sayari yenye afya. Mkutano huo wa siku tatu unaleta pamoja wawakilishi wanachama wa FAO, mashirika yanayohusika n uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo, watafiti, wanazuoni, mashirika ya maendeleo, mashirika ya kiraia na sekta binafsi ambapo watapata fursa kujadili mbinu bunifu na za ugunduzi ili hatimye sekta ya mifugo iweze kuzalisha mazao yenye lishe bora zaidi, gharama nafuu huku ikichangia kidogo katika uchafuzi wa mazingira. Thanawat Tiensin, Mkurugenzi wa Kitengo cha FAO kinachohusika na Uzalishaji wa Mifugo na Afya anafafanua maana ya ufugaji endelevu wa Wanyama. "Ufugaji endelevu unahusisha mwenendo unaolenga kukidhi mahitaji ya kufuga wanyama kwa ajili ya chakula huku ukipunguza uharibifu wa mazingira. Ufugaji endelevu unasongesha uwepo wa mifumo ya kilimo cha mazao ya chakula, hulinda maliasili, huboresha mnepo wa kiuchumi na huchangia kwenye mustakabali endelevu na wenye mnepo zaidi.” Wakati huu ambapo mahitaji ya mazao yatokanayo na mifugo duniani yakitarajiwa kuongezeka kwa asilimia 20 ifikapo mwaka 2050, nyama, mayai na bidhaa za maziwa zitakuwa dhima muhimu katika kuhakikisha uhakika wa upatikanaji wa chakula na mlo wenye afya na endelevu. Bwana Tiensin anaelezea zaidi jukumu la mkutano. "Ili kuzalisha mifugo huku unapunguza madhara, kwanza lazima tujitike katika mifumo fanisi ya ufugaji. Hii inajumuisha kubadili na kutumia vema chakula cha mifugo, kupunguza utupaji wa chakula hicho, matumizi mazuri ya virutubisho, kupunguza umomonyoaji wa udongo na vyanzo vya maji, kupunguza utoaji wa hewa chafuzi na kupunguza uharibifu wa mazingira. Halikadhalika, kupatia kipaumbele mifumo ya kilimo na ufugaji wa kisasa unaokidhi tabianchi.” Na zaidi ya yote, "Mkutano huu wa kimataifa utatoa fursa ya kuangazia tafiti na ujumbe muhimu, na kuchangia katika mazungumzo ya dunia kuhusu ufugaji endelevu na nafasi yake katika kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi. Kwa ujumla mkutano huu una dhima muhimu katika kusongesha ajenda ya ufugaji endelevu na kuendeleza mbinu zote ambazo zinashughulikia masuala ya kimazingira, kijamii na kiuchumi ya mifumo ya ufugaji.” Mambo yanayomulikwa ni pamoja na chakula na afya ya mifugo, lishe ya binadamu, matumizi ya teknolojia, na nafasi ya mifugo katika kuwezesha wafugaji wadogo kuendesha maisha yao na pia uhusiano kati ya ufugaji na uendelevu wa mazingira, uchumi na jamii.
25-9-2023 • 0
Msukumo dhidi ya TB ufanane na ule wa COVID-19- Waziri Wafula
Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya Kifua Kikuu au TB ukifanyika leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030 inawezekana endapo dunia itashikamana na kuweka msokumo mkubwa kwa ugonjwa huo kama ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19. Waziri Wafula alizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa.
22-9-2023 • 0
Msukumo dhidi ya TB ufanane na ule wa COVID-19- Waziri Wafula
Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya Kifua Kikuu au TB ukifanyika leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030 inawezekana endapo dunia itashikamana na kuweka msokumo mkubwa kwa ugonjwa huo kama ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19. Waziri Wafula alizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa.
22-9-2023 • 0
Kliniki tembezi nchini Tanzania yasaidia kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu
Hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani, wakuu wa nchi na serikali wamekutana katika mkutano wa pili wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa kutathmini mwelekeo wa Kifua Kikuu au TB kufuatia azimio la kisiasa la mwaka 2018 ambalo pamoja na mambo mengine linalenga kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030. Mkutano huo ni muhimu katika kukabiliana na vikwazo ikiwemo hatua za dharura za kutengeneza na kusambaza aina mpya ya chanjo dhidi ya Kifua Kikuu, huku ikibebwa na maudhui ya “kusongesha sayansi, ufadhili na ugunduzi na faida zake, kumaliza haraka kifua kikuu duniani kwa kuhakikisha kupata kwa usawa huduma za kinga, tiba na malezi.” Licha ya changamoto ya kudhibiti ugonjwa huo, tayari matunda yanaonekana ikiwemo huko Kanda ya Ziwa nchini Tanzania ambako kliniki tembezi zinafikia wagonjwa kule waliko. Evarist Mapesa wa Idhaa hii amezungumza na Dokta Abdallah Keresa kutoka kitengo cha Kliniki ya Kifua Kikuu na Virusi vya Ukimwi (VVU) Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza nchini Tanzania ambapo pamoja na kueleza mafanikio ya kudhibiti TB, anaanza kwa kueleza umhimu wa mkutano huu.
22-9-2023 • 0
Kliniki tembezi nchini Tanzania yasaidia kudhibiti ugonjwa wa Kifua Kikuu
Hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani, wakuu wa nchi na serikali wamekutana katika mkutano wa pili wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa kutathmini mwelekeo wa Kifua Kikuu au TB kufuatia azimio la kisiasa la mwaka 2018 ambalo pamoja na mambo mengine linalenga kutokomeza ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030. Mkutano huo ni muhimu katika kukabiliana na vikwazo ikiwemo hatua za dharura za kutengeneza na kusambaza aina mpya ya chanjo dhidi ya Kifua Kikuu, huku ikibebwa na maudhui ya “kusongesha sayansi, ufadhili na ugunduzi na faida zake, kumaliza haraka kifua kikuu duniani kwa kuhakikisha kupata kwa usawa huduma za kinga, tiba na malezi.” Licha ya changamoto ya kudhibiti ugonjwa huo, tayari matunda yanaonekana ikiwemo huko Kanda ya Ziwa nchini Tanzania ambako kliniki tembezi zinafikia wagonjwa kule waliko. Evarist Mapesa wa Idhaa hii amezungumza na Dokta Abdallah Keresa kutoka kitengo cha Kliniki ya Kifua Kikuu na Virusi vya Ukimwi (VVU) Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza nchini Tanzania ambapo pamoja na kueleza mafanikio ya kudhibiti TB, anaanza kwa kueleza umhimu wa mkutano huu.
22-9-2023 • 0
22 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazi ugonjwa wa kifua kikuu na haki za wanawake nchini Iran. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu wa Umoja wa Mataifa, kulikoni?Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya Kifua Kikuu au TB ukifanyika leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030 inawezekana endapo dunia itashikamana na kuweka msokumo mkubwa kwa ugonjwa huo kama ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19.Hatua ya Bunge la Iran kupitisha mswada mpya utakaowabana zaidi wanawake kuhusu uhuru wa miili yao na pia uvaaji wao hususani vazi la Hijab imepokelewa kwa masikitiko makubwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR.Katika makala hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika mkutano wa pili wa ngazi ya juu kutathmini azimio la kisiasa la mwaka 2018 kuhusu kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu ifikapo mwaka 2030. Evarist Mapesa wa Idhaa hii amezungumza na Dokta Abdallah Keresa kutoka kitengo cha Kliniki ya Kifua Kikuu na Virusi vya Ukimwi (VVU) Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza nchini Tanzania ambapo pamoja na kueleza mafanikio ya kudhibiti TB, anaanza kwa kueleza umhimu wa mkutano huu.Mashinani tutasalia hapa Makao Makuu kupata ujumbe wa Rais wa Guinea kwa viongozi wa Dunia.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
22-9-2023 • 0
22 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazi ugonjwa wa kifua kikuu na haki za wanawake nchini Iran. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu wa Umoja wa Mataifa, kulikoni?Mkutano wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya Kifua Kikuu au TB ukifanyika leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030 inawezekana endapo dunia itashikamana na kuweka msokumo mkubwa kwa ugonjwa huo kama ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19.Hatua ya Bunge la Iran kupitisha mswada mpya utakaowabana zaidi wanawake kuhusu uhuru wa miili yao na pia uvaaji wao hususani vazi la Hijab imepokelewa kwa masikitiko makubwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR.Katika makala hii leo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika mkutano wa pili wa ngazi ya juu kutathmini azimio la kisiasa la mwaka 2018 kuhusu kutokomeza ugonjwa wa Kifua Kikuu ifikapo mwaka 2030. Evarist Mapesa wa Idhaa hii amezungumza na Dokta Abdallah Keresa kutoka kitengo cha Kliniki ya Kifua Kikuu na Virusi vya Ukimwi (VVU) Hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza nchini Tanzania ambapo pamoja na kueleza mafanikio ya kudhibiti TB, anaanza kwa kueleza umhimu wa mkutano huu.Mashinani tutasalia hapa Makao Makuu kupata ujumbe wa Rais wa Guinea kwa viongozi wa Dunia.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
22-9-2023 • 0
OHCHR: Mswada Hijabu na ‘usafi’ kwa wanawake wa Iran unasikitisha
Hatua ya Bunge la Iran kupitisha mswada mpya utakaowabana zaidi wanawake kuhusu uhuru wa miili yao na pia uvaaji wao hususani vazi la Hijab imepokelewa kwa masikitiko makubwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR. Tunasikitika sana Bunge la Iran kupitisha Mswada mpya wa Usafi na Hijabu ambao unaongeza kwa kiasi kikubwa vifungo vya jela na faini ya kuwakandamiza wanawake na wasichana ambao hawatatii kanuni za lazima za uvaaji, imesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kupitia kwa Msemaji wake Ravina Shamdasani alipozunguza na waandishi wa Habari jijini Geneva, Uswisi. Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu, Volker Türk, ametuma ujumbe kwamba mswada huu wa kikatili unaopeperushwa waziwazi mbele ya uso wa sheria za kimataifa lazima usitishwe. Wale wanaopuuza kanuni kali ya mavazi ya Kiislamu ya kufunika kichwa na mavazi yanayoitwa ya heshima wako hatarini kukumbwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela, kuchapwa viboko pamoja na kutozwa faini ya hadi rial za Iran milioni 360 sawa na takribani dola za kimarekani 8,522. Kwa hatua mswada huu ulipofikia, kinachosubiriwa ni kupitishwa na Baraza la Uongozi linaloundwa na wazee 12 walioidhinishwa kikatiba ambao wana nguvu na ushawishi mkubwa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Chini ya sheria ya awali, kosa kama hilo lilibeba kifungo cha hadi miezi miwili jela, au faini ya hadi rial 500,000 za Iran sawa na takribani dola 11.84 za kimarekani.
22-9-2023 • 0
OHCHR: Mswada Hijabu na ‘usafi’ kwa wanawake wa Iran unasikitisha
Hatua ya Bunge la Iran kupitisha mswada mpya utakaowabana zaidi wanawake kuhusu uhuru wa miili yao na pia uvaaji wao hususani vazi la Hijab imepokelewa kwa masikitiko makubwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR. Tunasikitika sana Bunge la Iran kupitisha Mswada mpya wa Usafi na Hijabu ambao unaongeza kwa kiasi kikubwa vifungo vya jela na faini ya kuwakandamiza wanawake na wasichana ambao hawatatii kanuni za lazima za uvaaji, imesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu kupitia kwa Msemaji wake Ravina Shamdasani alipozunguza na waandishi wa Habari jijini Geneva, Uswisi. Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu, Volker Türk, ametuma ujumbe kwamba mswada huu wa kikatili unaopeperushwa waziwazi mbele ya uso wa sheria za kimataifa lazima usitishwe. Wale wanaopuuza kanuni kali ya mavazi ya Kiislamu ya kufunika kichwa na mavazi yanayoitwa ya heshima wako hatarini kukumbwa na kifungo cha hadi miaka 10 jela, kuchapwa viboko pamoja na kutozwa faini ya hadi rial za Iran milioni 360 sawa na takribani dola za kimarekani 8,522. Kwa hatua mswada huu ulipofikia, kinachosubiriwa ni kupitishwa na Baraza la Uongozi linaloundwa na wazee 12 walioidhinishwa kikatiba ambao wana nguvu na ushawishi mkubwa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Chini ya sheria ya awali, kosa kama hilo lilibeba kifungo cha hadi miezi miwili jela, au faini ya hadi rial 500,000 za Iran sawa na takribani dola 11.84 za kimarekani.
22-9-2023 • 0
Waziri wa Afya Kenya atoa wito kwa wadau kutengeneza chanjo ya TB
Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mapambano dhidi ya kifua kikuu au TB ukifanyika leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030 inawezekana endapo Dunia itashikama na kuweka msokumo mkubwa kwa ugonjwa huo kama ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19.Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Waziri Wafula amesema “Najiuliza, mbona sisi watu wote, kwanza wafadhili na wale wazalishaji wa hizo dawa na vifaa, mbona tusifikirie lile jambo moja ambalo tunastahili kufanya ili kumaliza ugonjwa wa TB?” Akifafanua zaidi Waziri huyo amesema jambo la muhimu ni kupata kinga ili watu wasipata ugonjwa wa TB kwakuwa kwa kiasi kikubwa wanaoambukizwa ni watu walio katika maeneo duni. “Kulikuwa na COVID-19, muda mfupi tu kumekuwa na chanjo na sasa watu tunatembea kwa uhuru kabisa na watu wanatangamana, pale mwanzo COVID-19 ilikuwa imefanya watu hawatembeleani. Ninauhakika kwamba tukiweka fedha kwenye sayansi, kufanya utafiti na maendeleo tutapata chanjo ya hii TB ama pia tupate tiba ya mara moja.”Waziri huyo wa Afya kutoka nchini Kenya amesema pamoja na taifa hilo kutibu ugonjwa wa TB bure kwa wananchi wake lakini changamoto wanayokutana nayo ni uhaba wa vifaa tiba katika baadhi ya hospitali na kutoa wito kwa wafanyabiashara kupunguza bei za vifaa tiba hivyo ili waweze kusambaza katika hospital zote nchini Kenya. Kuhusu namna watakavyotekeleza Azimio la kisiasa kuhusu Afya kwa wote nchini Kenya ambayo wanaiita “Afya Mashinani” Waziri Wafula amesema Kenya imejipanga kutekeleza katika vipengele vifuu vinne ambavyo ni: kuhakikisha kuna dawa na vifaa tiba, kuhakikisha kuna watoa huduma katika vituo vya afya, matumizi ya teknolojia kufikisha afya mashinani na ufadhili wa afya kupitia bima ya afya ya taifa.
22-9-2023 • 0
Waziri wa Afya Kenya atoa wito kwa wadau kutengeneza chanjo ya TB
Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mapambano dhidi ya kifua kikuu au TB ukifanyika leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani, Waziri wa Afya wa Kenya Susan Nakhumicha Wafula amesema kutokomeza TB ifikapo mwaka 2030 inawezekana endapo Dunia itashikama na kuweka msokumo mkubwa kwa ugonjwa huo kama ilivyofanya wakati wa mlipuko wa janga la COVID-19.Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Waziri Wafula amesema “Najiuliza, mbona sisi watu wote, kwanza wafadhili na wale wazalishaji wa hizo dawa na vifaa, mbona tusifikirie lile jambo moja ambalo tunastahili kufanya ili kumaliza ugonjwa wa TB?” Akifafanua zaidi Waziri huyo amesema jambo la muhimu ni kupata kinga ili watu wasipata ugonjwa wa TB kwakuwa kwa kiasi kikubwa wanaoambukizwa ni watu walio katika maeneo duni. “Kulikuwa na COVID-19, muda mfupi tu kumekuwa na chanjo na sasa watu tunatembea kwa uhuru kabisa na watu wanatangamana, pale mwanzo COVID-19 ilikuwa imefanya watu hawatembeleani. Ninauhakika kwamba tukiweka fedha kwenye sayansi, kufanya utafiti na maendeleo tutapata chanjo ya hii TB ama pia tupate tiba ya mara moja.”Waziri huyo wa Afya kutoka nchini Kenya amesema pamoja na taifa hilo kutibu ugonjwa wa TB bure kwa wananchi wake lakini changamoto wanayokutana nayo ni uhaba wa vifaa tiba katika baadhi ya hospitali na kutoa wito kwa wafanyabiashara kupunguza bei za vifaa tiba hivyo ili waweze kusambaza katika hospital zote nchini Kenya. Kuhusu namna watakavyotekeleza Azimio la kisiasa kuhusu Afya kwa wote nchini Kenya ambayo wanaiita “Afya Mashinani” Waziri Wafula amesema Kenya imejipanga kutekeleza katika vipengele vifuu vinne ambavyo ni: kuhakikisha kuna dawa na vifaa tiba, kuhakikisha kuna watoa huduma katika vituo vya afya, matumizi ya teknolojia kufikisha afya mashinani na ufadhili wa afya kupitia bima ya afya ya taifa.
22-9-2023 • 0
Tunaelimisha wanafunzi na vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi - Madina Jubilate Kimaro
Wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi. Miongoni mwa vijana walioshiriki ni Madina Jubilate Kimaro, Balozi wa Mazingira wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF nchini Tanzania. Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye kufahamu masuala kadhaa ikiwemo nini anafanya kuhakikisha mazingira yanasalia salama.
21-9-2023 • 0
Tunaelimisha wanafunzi na vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi - Madina Jubilate Kimaro
Wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi. Miongoni mwa vijana walioshiriki ni Madina Jubilate Kimaro, Balozi wa Mazingira wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF nchini Tanzania. Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye kufahamu masuala kadhaa ikiwemo nini anafanya kuhakikisha mazingira yanasalia salama.
21-9-2023 • 0
Methali: "Mshale mzuri haukai ziakani"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Mshale mzuri haukai ziakani.”
21-9-2023 • 0
Methali: "Mshale mzuri haukai ziakani"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Mshale mzuri haukai ziakani.”
21-9-2023 • 0
21 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi. Miongoni mwa vijana walioshiriki ni Madina Jubilate Kimaro, Balozi wa Mazingira wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF nchini Tanzania. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiangazia Afya, amani na yanayoendelea katika UNGA78. Katika kujifinza lugha ya Kiswahili Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Mshale mzuri haukai ziakani.”. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
21-9-2023 • 0
21 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo wiki hii hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa tathmini ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs kuona wapi nchi wanachama, kampuni, watu binafsi wamefikia kusongesha maendeleo hayo yanayofikia ukomo mwka 2030. Vijana nao walikuwa na siku zao mbili za kuelezea wanafanya nini kule waliko na wanataka nini kifanyike kusongesha malengo hayo likiwemo namba 13 la tabianchi. Miongoni mwa vijana walioshiriki ni Madina Jubilate Kimaro, Balozi wa Mazingira wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF nchini Tanzania. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiangazia Afya, amani na yanayoendelea katika UNGA78. Katika kujifinza lugha ya Kiswahili Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Mshale mzuri haukai ziakani.”. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
21-9-2023 • 0
Guterres: Tumieni vizuri Mjadala wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu kuhusu ufadhili wa maendeleo
Viongozi wa ulimengu wanaohudhuria Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wamefanya Mjadala wa Ngazi ya Juu kujadili ufadhili kwa ajili ya maendeleo ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewasihi kuitumia fursa ya majadiliano haya ili kufanya marekebisho katika mfumo wa ufadhili duniani. Evarist Mapesa na taarifa zaidi.“Waheshimiwa, Mabibi na mabwana…Katika masuala yote tutakayojadili wiki hii, ufadhili unaweza kuwa muhimu zaidi.” Ndivyo alivyoanza hotuba yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mbele ya viongozi wa ulimwengu kwa lengo la kutafuta suluhisho la ufadhili wa maendeleo unaosuasua duniani. Akitumia mfano wa nishati isukumavyo mitambo, Guterres amesema kwa sababu ufadhili wa maendeleo ndio nishati inayosukuma maendeleo kwenye Ajenda ya mwaka 2030 na Mkataba wa Paris. Leo, nishati hiyo inaisha na injini ya maendeleo endelevu inadumaa, inakwama, na inarudi nyuma.Bwana Guterres ameweka wazi kuwa kuna mgawanyiko mkubwa na unaokua kati ya nchi ambazo zinaweza kupata ufadhili kwa masharti yanayokubalika na zile ambazo haziwezi na zinaachwa nyuma zaidi akitoa mfano mchungu kwamba nchini zinazoendelea zinakabiliwa na gharama za kukopa hadi mara nane zaidi ya nchi zilizoendelea – kitu ambacho amekiita mtego wa madeni na hapo akatoa wito,“Ninakuombeni mtumie mjadala huu wa ngazi ya juu kama jukwaa la ushirikiano wenye kujenga, kwa kuzingatia suluhisho za ufadhili za kiubunifu na vitendo ambazo zinaweza kuendelezwa katika miezi na miaka ijayo.”
20-9-2023 • 0
Guterres: Tumieni vizuri Mjadala wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu kuhusu ufadhili wa maendeleo
Viongozi wa ulimengu wanaohudhuria Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wamefanya Mjadala wa Ngazi ya Juu kujadili ufadhili kwa ajili ya maendeleo ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewasihi kuitumia fursa ya majadiliano haya ili kufanya marekebisho katika mfumo wa ufadhili duniani. Evarist Mapesa na taarifa zaidi.“Waheshimiwa, Mabibi na mabwana…Katika masuala yote tutakayojadili wiki hii, ufadhili unaweza kuwa muhimu zaidi.” Ndivyo alivyoanza hotuba yake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres mbele ya viongozi wa ulimwengu kwa lengo la kutafuta suluhisho la ufadhili wa maendeleo unaosuasua duniani. Akitumia mfano wa nishati isukumavyo mitambo, Guterres amesema kwa sababu ufadhili wa maendeleo ndio nishati inayosukuma maendeleo kwenye Ajenda ya mwaka 2030 na Mkataba wa Paris. Leo, nishati hiyo inaisha na injini ya maendeleo endelevu inadumaa, inakwama, na inarudi nyuma.Bwana Guterres ameweka wazi kuwa kuna mgawanyiko mkubwa na unaokua kati ya nchi ambazo zinaweza kupata ufadhili kwa masharti yanayokubalika na zile ambazo haziwezi na zinaachwa nyuma zaidi akitoa mfano mchungu kwamba nchini zinazoendelea zinakabiliwa na gharama za kukopa hadi mara nane zaidi ya nchi zilizoendelea – kitu ambacho amekiita mtego wa madeni na hapo akatoa wito,“Ninakuombeni mtumie mjadala huu wa ngazi ya juu kama jukwaa la ushirikiano wenye kujenga, kwa kuzingatia suluhisho za ufadhili za kiubunifu na vitendo ambazo zinaweza kuendelezwa katika miezi na miaka ijayo.”
20-9-2023 • 0
20 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea maoni kuhusu matumizi ya lugha ya kiswahili kutokwa kwa viongozi wanaoshiriki UNGA78, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mjadala kuhusu malengo ya maendeleo endelevu. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia hapa makao makuu, kulikoni? Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki ambaye yuko hapa New York, Marekani kushiriki vikao vya ngazi ya juu vya Umoja wa Mataifa amesema ili kuongeza ushawishi na kukuza lugha ya Kiswahili duniani ambayo sasa inatambulika kimataifa, ni vyema viongozi wa jumuiya hiyo wakawa mfano kwa kuhutubia kwa lugha hiyo mathalani kwenye mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa au UNGA78.Viongozi wa ulimwengu wanaohudhuria Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wamekuwa na Mjadala wa Ngazi ya Juu kujadili ufadhili kwa ajili ya maendeleo hususan katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewasihi kuitumia fursa ya majadiliano hayo ili kurekebisha mfumo wa ufadhili duniani. Na katika makala wakati hapa Makao Makuu hii leo kukifanyika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu tabianchi na jinsi ya kudhibiti athari zake, wakazi wa Kibokoni kaunti ya Kilifi nchini Kenya, wamechukua hatua kwani baada ya kuathirika wamejijengea mnepo na kuendelea kujikimu kimaisha kwa kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki kwenye mabwawa.Mashinani inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mjadala wa Baraza Kuu kunafanyika mkutano kuhusu hali ya Sudan. Naibu msaidizi wa Katibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Joyce Msuya anasema kwa upande wa kibinadamu hali ni tete. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
20-9-2023 • 0
20 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea maoni kuhusu matumizi ya lugha ya kiswahili kutokwa kwa viongozi wanaoshiriki UNGA78, na yaliyojiri hapa makao makuu katika mjadala kuhusu malengo ya maendeleo endelevu. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani tunasalia hapa makao makuu, kulikoni? Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki ambaye yuko hapa New York, Marekani kushiriki vikao vya ngazi ya juu vya Umoja wa Mataifa amesema ili kuongeza ushawishi na kukuza lugha ya Kiswahili duniani ambayo sasa inatambulika kimataifa, ni vyema viongozi wa jumuiya hiyo wakawa mfano kwa kuhutubia kwa lugha hiyo mathalani kwenye mjadala mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa au UNGA78.Viongozi wa ulimwengu wanaohudhuria Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wamekuwa na Mjadala wa Ngazi ya Juu kujadili ufadhili kwa ajili ya maendeleo hususan katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewasihi kuitumia fursa ya majadiliano hayo ili kurekebisha mfumo wa ufadhili duniani. Na katika makala wakati hapa Makao Makuu hii leo kukifanyika mkutano wa ngazi ya juu kuhusu tabianchi na jinsi ya kudhibiti athari zake, wakazi wa Kibokoni kaunti ya Kilifi nchini Kenya, wamechukua hatua kwani baada ya kuathirika wamejijengea mnepo na kuendelea kujikimu kimaisha kwa kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki kwenye mabwawa.Mashinani inaturejesha hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mjadala wa Baraza Kuu kunafanyika mkutano kuhusu hali ya Sudan. Naibu msaidizi wa Katibu Mkuu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Joyce Msuya anasema kwa upande wa kibinadamu hali ni tete. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
20-9-2023 • 0
Mradi wa ufugaji wa Samaki umenikombia mimi na familia yangu: Michael Chiwayi
Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mabadiliko ya tabianchi unafanyika leo kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu , UNGA78 lengo likiwa kuzihamasisha nchi wanachana kuchukua hatua zaidi kuzinusuru nchi zinazobeba mzigo mkubwa wa athari za janga hilo. Eneo la Kibokoni kaunti ya Kilifi nchini Kenya ni moja ya maeneo ya wavuvi yaliyoathirika na mabadiliko ya tabianchi na kuwalazimu wavufi kutafuta mbinu mbadala ya kuweza kujikimu kimaisha. Na ndipo chini ya mwamvuli wa shirika lisilo la kiserikali la Umoja Self-Help Group likiwa na wanachama 40 wakaanzisha mabwa 17 ya ufugaji wa Samaki aina ya milkfish, dagaa kamba, kaa, sandfish, rabbitfish na tilapia wa baharini. Mradi huu unaihakikisha jamii uzalishaji, kuwainua kiuchumi na kuwajengea mnepo. Tuungane Flora Nducha na mmoja wa wanaufaika wa mradi huo katika makala hii iliyofanikishwa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIS, Nairobi Kenya.
20-9-2023 • 0
Mradi wa ufugaji wa Samaki umenikombia mimi na familia yangu: Michael Chiwayi
Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mabadiliko ya tabianchi unafanyika leo kwenye makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kandoni mwa mjadala mkuu wa Baraza Kuu , UNGA78 lengo likiwa kuzihamasisha nchi wanachana kuchukua hatua zaidi kuzinusuru nchi zinazobeba mzigo mkubwa wa athari za janga hilo. Eneo la Kibokoni kaunti ya Kilifi nchini Kenya ni moja ya maeneo ya wavuvi yaliyoathirika na mabadiliko ya tabianchi na kuwalazimu wavufi kutafuta mbinu mbadala ya kuweza kujikimu kimaisha. Na ndipo chini ya mwamvuli wa shirika lisilo la kiserikali la Umoja Self-Help Group likiwa na wanachama 40 wakaanzisha mabwa 17 ya ufugaji wa Samaki aina ya milkfish, dagaa kamba, kaa, sandfish, rabbitfish na tilapia wa baharini. Mradi huu unaihakikisha jamii uzalishaji, kuwainua kiuchumi na kuwajengea mnepo. Tuungane Flora Nducha na mmoja wa wanaufaika wa mradi huo katika makala hii iliyofanikishwa na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, UNIS, Nairobi Kenya.
20-9-2023 • 0
Tuzungumze Kiswahili kwenye UNGA78 - Viongozi wa EAC
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki amesema ili kuongeza ushawishi na kukuza lugha ya Kiswahili duniani ni vyema viongozi wa jumuiya wakazungumza lugha hiyo wakiwa katika mikutano mikubwa duniani akitolea mfano mjadala Mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa au UNGA78. “Katika vikao vyetu vya jumuiya (EAC) tumewaomba marais pia wakija vikao kama hivi (UNGA78) wazungumze kwa lugha ya Kiswahili ndio sasa wananchi waanze kuwasikia wanasema nini lakini pia itakuwa mchango wao kuendelea kusukuma lugha ya Kiswahili iweze kwenda mbele kama lugha zingine.” Amesema Dkt. Mathuki katika mahojiano yake na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Dkt. Mathuki amesema tayari jumuiya hiyo imeanza kutekeleza mambo mbalimbali ya kusongesha lugha hiyo kimataifa. “Katika kikao cha baraza la mawaziri cha 43 kilichofanyika mwezi Machi mwaka huu 2023 tumekubaliana mambo yote tunayofanya katika jumuiya ya Afrika Mashariki lazima yawe kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza. Tumeanza kutafuta wataalamu watusaidie kutafrisi nyaraka zote tunazofanya na ujumbe wowote tunaotoa lazima pia uwe kwa lugha ya Kiswahili.” Ili kusongesha zaidi lugha hiyo amesema wameanza mchakato wa kuanzisha vituo vya Kiswahili kwenye kila balozi za nchi wanachama ughaibuni ili kuvutia wageni pia watake kujifunza lugha hiyo adhimu. Amlipoulizwa inakuwaje viongozi wengi wa kisiasa wanaposimama katika majukwaa ya kimataifa wanazungumza kwa kingereza Dkt Mathuki alisema hiyo ni kutokana na uzoefu wao wakuwa wanazungumza lugha ya kigeni lakini kuna juhudi zinafanyika akitolea “mfano nchini Uganda, katika baraza la mawaziri mafunzo ya lugha ya Kiswahili ni lazima.”
20-9-2023 • 0
Tuzungumze Kiswahili kwenye UNGA78 - Viongozi wa EAC
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Peter Mathuki amesema ili kuongeza ushawishi na kukuza lugha ya Kiswahili duniani ni vyema viongozi wa jumuiya wakazungumza lugha hiyo wakiwa katika mikutano mikubwa duniani akitolea mfano mjadala Mkuu wa Mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa au UNGA78. “Katika vikao vyetu vya jumuiya (EAC) tumewaomba marais pia wakija vikao kama hivi (UNGA78) wazungumze kwa lugha ya Kiswahili ndio sasa wananchi waanze kuwasikia wanasema nini lakini pia itakuwa mchango wao kuendelea kusukuma lugha ya Kiswahili iweze kwenda mbele kama lugha zingine.” Amesema Dkt. Mathuki katika mahojiano yake na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Dkt. Mathuki amesema tayari jumuiya hiyo imeanza kutekeleza mambo mbalimbali ya kusongesha lugha hiyo kimataifa. “Katika kikao cha baraza la mawaziri cha 43 kilichofanyika mwezi Machi mwaka huu 2023 tumekubaliana mambo yote tunayofanya katika jumuiya ya Afrika Mashariki lazima yawe kwa lugha ya Kiswahili na kiingereza. Tumeanza kutafuta wataalamu watusaidie kutafrisi nyaraka zote tunazofanya na ujumbe wowote tunaotoa lazima pia uwe kwa lugha ya Kiswahili.” Ili kusongesha zaidi lugha hiyo amesema wameanza mchakato wa kuanzisha vituo vya Kiswahili kwenye kila balozi za nchi wanachama ughaibuni ili kuvutia wageni pia watake kujifunza lugha hiyo adhimu. Amlipoulizwa inakuwaje viongozi wengi wa kisiasa wanaposimama katika majukwaa ya kimataifa wanazungumza kwa kingereza Dkt Mathuki alisema hiyo ni kutokana na uzoefu wao wakuwa wanazungumza lugha ya kigeni lakini kuna juhudi zinafanyika akitolea “mfano nchini Uganda, katika baraza la mawaziri mafunzo ya lugha ya Kiswahili ni lazima.”
20-9-2023 • 0
19 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Leo ni siku ya pili na ya mwisho wa mkutano kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs lakini leo pia ndio pazia la mjadala Mkuu wa 78, UNGA78 limefunguliwa na pamoja na na hotuba za viongozi pia kutakuwa na mikutano itakayo jadili hali za ulinzi na usalama katika mataifa mbalimbali na hapo kesho kutakuwa na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Sudan. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na nashinani ikimulika hotuba za viongozi katika Baraza Kuu na kazi za vijana katika utekelezaji wa DGs. Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu Malengo ya maendeleo endelevu SDGs, limefungua pazia leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuja na azimio la kisiasa la kuhakikissha wanayanusuru malengo hayo ambayo mengi yanakwenda mrama kwani ni asilimia 15 pekee kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ndio yametimizwa huku ikiwa imesalia chini ya miaka 7 kufikia mwaka 2030 ukomo wa utimizaji wa malengo hayo.Tarehe 17 na 18 Septemba yani leo na kesho hapa katika makao Makuu viongozi wanakutana kuangalia vipi wametekeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanatarajiwa kufikia kilele mwaka 2030. Makala nampisha Thelma Mwadzaya na makala kuhusu apu iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iitwayo oKy ya kuwezesha wasichana kufuatilia hedhi, moja ya vipengele vya SDGs.Kama kawaida Rais wa kwanza kuhutubia ni wa Brazil akifuatiwa na Marekani. Pia Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine yuko hapa akiwa miongoni mwa wanaoutubia leo. Aidha ratiba inaonesha kwa leo siku ya ufunguzi marais kutoka bara la Afrika watakaohutubia ni Rais wa Afrika Kusini, Msumbiji, Nigeria, Senegal. Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wanaonekana kwenye ratiba ya kesho.Mashinani tunasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York kusikia jinsi ambavyo vijana wanavyochangia katika mchakato wa kusongesha ajenda ya malengo ya malengo endelevu. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
19-9-2023 • 0
19 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Leo ni siku ya pili na ya mwisho wa mkutano kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs lakini leo pia ndio pazia la mjadala Mkuu wa 78, UNGA78 limefunguliwa na pamoja na na hotuba za viongozi pia kutakuwa na mikutano itakayo jadili hali za ulinzi na usalama katika mataifa mbalimbali na hapo kesho kutakuwa na mkutano wa ngazi ya juu kuhusu Sudan. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na nashinani ikimulika hotuba za viongozi katika Baraza Kuu na kazi za vijana katika utekelezaji wa DGs. Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu Malengo ya maendeleo endelevu SDGs, limefungua pazia leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuja na azimio la kisiasa la kuhakikissha wanayanusuru malengo hayo ambayo mengi yanakwenda mrama kwani ni asilimia 15 pekee kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ndio yametimizwa huku ikiwa imesalia chini ya miaka 7 kufikia mwaka 2030 ukomo wa utimizaji wa malengo hayo.Tarehe 17 na 18 Septemba yani leo na kesho hapa katika makao Makuu viongozi wanakutana kuangalia vipi wametekeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanatarajiwa kufikia kilele mwaka 2030. Makala nampisha Thelma Mwadzaya na makala kuhusu apu iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iitwayo oKy ya kuwezesha wasichana kufuatilia hedhi, moja ya vipengele vya SDGs.Kama kawaida Rais wa kwanza kuhutubia ni wa Brazil akifuatiwa na Marekani. Pia Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine yuko hapa akiwa miongoni mwa wanaoutubia leo. Aidha ratiba inaonesha kwa leo siku ya ufunguzi marais kutoka bara la Afrika watakaohutubia ni Rais wa Afrika Kusini, Msumbiji, Nigeria, Senegal. Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wanaonekana kwenye ratiba ya kesho.Mashinani tunasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York kusikia jinsi ambavyo vijana wanavyochangia katika mchakato wa kusongesha ajenda ya malengo ya malengo endelevu. Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
19-9-2023 • 0
UNICEF: Apu ya OKY na hedhi salama yasongesha SDG 3
Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limezindua apu maalum ya wasichana kufuatilia maelezo wakati wa hedhi. Apu hiyo ni mahsusi kwa wasichana wa mataifa yanayoinukia na yaliyo masikini. Apu hii inaleta matumaini wakati huu ambapo viongozi wa dunia wanakutana New York, Marekani kutathmini maendeleo ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Thelma Mwadzaya amefuatilia na kutuletea makala kuhusu apu hiyo, iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.
18-9-2023 • 0
UNICEF: Apu ya OKY na hedhi salama yasongesha SDG 3
Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, limezindua apu maalum ya wasichana kufuatilia maelezo wakati wa hedhi. Apu hiyo ni mahsusi kwa wasichana wa mataifa yanayoinukia na yaliyo masikini. Apu hii inaleta matumaini wakati huu ambapo viongozi wa dunia wanakutana New York, Marekani kutathmini maendeleo ya malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Thelma Mwadzaya amefuatilia na kutuletea makala kuhusu apu hiyo, iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF.
18-9-2023 • 0
Guterres: Badala ya kutomwacha yeyote nyuma tunahatarisha kuyaacha malengo ya SDGs nyuma
Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu Malengo ya maendeleo endelevu SDGs, limefungua pazia leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuja na azimio la kisiasa la kuhakikissha wanayanusuru malengo hayo ambayo mengi yanakwenda mrama kwani ni asilimia 15 pekee kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ndio yametimizwa huku ikiwa imesalia chini ya miaka 7 kufikia mwaka 2030 ukomo wa utimizaji wa malengo hayo.Muda wa kuchukua hatua ni sasa kuhakikisha tunayaokoa malengo ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanasuasua na kuwa kwenye hatari kubwa ya kutotimizwa amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika ufunguzi wa jukwaa hilo hapa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa chini ya mwamvuli wa Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa au UNGA78.Katibu Mkuu amesema ahadi iliyotolewa na viongozi wa Dunia miaka 8 iliyopita kwa watu ya kuwa na Dunia yenye afya, maendeleo na fursa kwa wote inakwenda mrama na hadi sasa ni asilimia 15 pekee ya malengo 17 yaliyopitishwa ndio yako kwenye msitari unaotakiwa menggine yanarudi nyuma na mengi yanajikongoja.Viongozi wa Dunia waliafikiana na kupitisha malengo hayo 17 mwaka 2015 wakiahidi kutomwacha yeyote nyuma.Malengo hayo yanajumuisha kutokomeza umasikini, kutokomeza njaa, kuhakikisha fursa ya upatikanaji wa maji safi na usafi lakini pamoja na kutoa elimu bora kwa wote na fursa za muda mrefu za kusoma. Kila lengo kuu lina vipengele vyake na jumla ya ni asilimia 15 pekee ya malengo hayo na vipengele vyake ndio viko kwenye msitari unaotakiwa.vipengele vya malengo hayo ni 169, lakini Katibu Mkuu ameonya kwamba ni malengo mengi yako nje ya msitari.Hivyo amesisitiza kuwa azimio la kisiasa ndio dawa mujarabu wa kusongesha mbele utimizaji na ufikiaji wa malengo hayo ikiwa imesalia chini ya miaka 7 kufika ukomo wake mwaka 2030.Azimio hilo linajumuisha “ahadi ya kufadhli kwa nchi zinazoendelea ili kusongesha malengo hayo na msaada mkubwa wa kuunga mkono mapendekezo yake kwa ajili ya SDGs angalu dola bilioni 500 kila mwaka , na pia mkakati wa upunguzaji wa madeni.Azimio hilo pia linatoa wito wa kubadili mtindo wa biashara wa benki za maendeleo za kimataifa ili kutoa fedha za kibinafsi kwa viwango vya riba nafuu zaidi kwa nchi zinazoendelea, na kuunga mkono mageuzi ya usanifu wa fedha wa kimataifa ambao ameuita umepitwa na wakati, haufanyi kazi vizuri na sio wa haki.
18-9-2023 • 0
Guterres: Badala ya kutomwacha yeyote nyuma tunahatarisha kuyaacha malengo ya SDGs nyuma
Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu Malengo ya maendeleo endelevu SDGs, limefungua pazia leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuja na azimio la kisiasa la kuhakikissha wanayanusuru malengo hayo ambayo mengi yanakwenda mrama kwani ni asilimia 15 pekee kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ndio yametimizwa huku ikiwa imesalia chini ya miaka 7 kufikia mwaka 2030 ukomo wa utimizaji wa malengo hayo.Muda wa kuchukua hatua ni sasa kuhakikisha tunayaokoa malengo ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanasuasua na kuwa kwenye hatari kubwa ya kutotimizwa amesema leo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza katika ufunguzi wa jukwaa hilo hapa kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa chini ya mwamvuli wa Kikao cha 78 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa au UNGA78.Katibu Mkuu amesema ahadi iliyotolewa na viongozi wa Dunia miaka 8 iliyopita kwa watu ya kuwa na Dunia yenye afya, maendeleo na fursa kwa wote inakwenda mrama na hadi sasa ni asilimia 15 pekee ya malengo 17 yaliyopitishwa ndio yako kwenye msitari unaotakiwa menggine yanarudi nyuma na mengi yanajikongoja.Viongozi wa Dunia waliafikiana na kupitisha malengo hayo 17 mwaka 2015 wakiahidi kutomwacha yeyote nyuma.Malengo hayo yanajumuisha kutokomeza umasikini, kutokomeza njaa, kuhakikisha fursa ya upatikanaji wa maji safi na usafi lakini pamoja na kutoa elimu bora kwa wote na fursa za muda mrefu za kusoma. Kila lengo kuu lina vipengele vyake na jumla ya ni asilimia 15 pekee ya malengo hayo na vipengele vyake ndio viko kwenye msitari unaotakiwa.vipengele vya malengo hayo ni 169, lakini Katibu Mkuu ameonya kwamba ni malengo mengi yako nje ya msitari.Hivyo amesisitiza kuwa azimio la kisiasa ndio dawa mujarabu wa kusongesha mbele utimizaji na ufikiaji wa malengo hayo ikiwa imesalia chini ya miaka 7 kufika ukomo wake mwaka 2030.Azimio hilo linajumuisha “ahadi ya kufadhli kwa nchi zinazoendelea ili kusongesha malengo hayo na msaada mkubwa wa kuunga mkono mapendekezo yake kwa ajili ya SDGs angalu dola bilioni 500 kila mwaka , na pia mkakati wa upunguzaji wa madeni.Azimio hilo pia linatoa wito wa kubadili mtindo wa biashara wa benki za maendeleo za kimataifa ili kutoa fedha za kibinafsi kwa viwango vya riba nafuu zaidi kwa nchi zinazoendelea, na kuunga mkono mageuzi ya usanifu wa fedha wa kimataifa ambao ameuita umepitwa na wakati, haufanyi kazi vizuri na sio wa haki.
18-9-2023 • 0
Mazao ya asili yaliyo puuzwa yatasaidia kutokomeza njaa
Tarehe 17 na 18 Septemba yani leo na kesho hapa katika makao Makuu viongozi wanakutana kuangalia vipi wametekeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanatarajiwa kufikia kilele mwaka 2030Wadau wa Maendeleo wamejaa hapa katika makao Makuu hakika na rangi za malengo 17 zikiwa zimetaradadi kila kona kuanzia nje mpaka ndani ya Baraza Kuu, mwaka huu wakija na maudhui yasemayo, Kujenga upya kuaminiana na kuchochea mshikamano wa dunia.Mikutano ya SDGs imekuwa na ubunifu tofauti mwaka baada ya mwaka, na mwaka huu katika eneo la wazi baada tu ya kuingia makao makuu kuna milango midogo 17 inayoonesha malengo 17 na kila mlango una mchechemuzi na umeandikwa namna anavyopambana kutekeleza lengo.Mlango namba mbili ni kutokomeza njaa, na ukifungua mlango unakutana na Pierre Thiam raia wa Senegali na mpishi mwenye makazi yake hapa jijini New York Marekani, yeye anaamini kuwa dunia inaweza kutokomeza njaa iwapo itageukia katika mazao ambayo hayatumiwi sana na yamekuwa yakipuuzwa.Thiam alihojiwa na mwenzangu Florence Westergard wa Idhaa ya Kifaransa ya Umoja wa Mataifa na anasema,“Kwa hiyo kupambana na njaa kutanza kwa kubadili mifumo yetu ya chakula na kurejea katika aina ya kilimo kinachosaidia wakulima wadogo na mazao yao ambayo hayatumiki, na kutafuta njia za kuongeza thamani katika mazao hayo na kuyafanya yaweze kupatikana masokoni.”Thiam yeye ananena na anatenda kwani anahamasisha zao la Forno ambalo linapatikana maeneo mengi ya ukanda wa Sahel. Ukanda ambao nchi nyingi zinatakabiliwa na uhaba wa chakula.Kwakweli Flora mara baada ya kumsikia mchechemuzi huyu nami nikakumbuka kule kwetu Kilimanjaro Tanzania tumehamasika kula ndizi lakini kuna mazao kama viazi vikuu ambavyo ndio hayo yanayoelezwa kuwa yamepuuzwa na tunapaswa kurejea kwayo.
18-9-2023 • 0
Mazao ya asili yaliyo puuzwa yatasaidia kutokomeza njaa
Tarehe 17 na 18 Septemba yani leo na kesho hapa katika makao Makuu viongozi wanakutana kuangalia vipi wametekeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanatarajiwa kufikia kilele mwaka 2030Wadau wa Maendeleo wamejaa hapa katika makao Makuu hakika na rangi za malengo 17 zikiwa zimetaradadi kila kona kuanzia nje mpaka ndani ya Baraza Kuu, mwaka huu wakija na maudhui yasemayo, Kujenga upya kuaminiana na kuchochea mshikamano wa dunia.Mikutano ya SDGs imekuwa na ubunifu tofauti mwaka baada ya mwaka, na mwaka huu katika eneo la wazi baada tu ya kuingia makao makuu kuna milango midogo 17 inayoonesha malengo 17 na kila mlango una mchechemuzi na umeandikwa namna anavyopambana kutekeleza lengo.Mlango namba mbili ni kutokomeza njaa, na ukifungua mlango unakutana na Pierre Thiam raia wa Senegali na mpishi mwenye makazi yake hapa jijini New York Marekani, yeye anaamini kuwa dunia inaweza kutokomeza njaa iwapo itageukia katika mazao ambayo hayatumiwi sana na yamekuwa yakipuuzwa.Thiam alihojiwa na mwenzangu Florence Westergard wa Idhaa ya Kifaransa ya Umoja wa Mataifa na anasema,“Kwa hiyo kupambana na njaa kutanza kwa kubadili mifumo yetu ya chakula na kurejea katika aina ya kilimo kinachosaidia wakulima wadogo na mazao yao ambayo hayatumiki, na kutafuta njia za kuongeza thamani katika mazao hayo na kuyafanya yaweze kupatikana masokoni.”Thiam yeye ananena na anatenda kwani anahamasisha zao la Forno ambalo linapatikana maeneo mengi ya ukanda wa Sahel. Ukanda ambao nchi nyingi zinatakabiliwa na uhaba wa chakula.Kwakweli Flora mara baada ya kumsikia mchechemuzi huyu nami nikakumbuka kule kwetu Kilimanjaro Tanzania tumehamasika kula ndizi lakini kuna mazao kama viazi vikuu ambavyo ndio hayo yanayoelezwa kuwa yamepuuzwa na tunapaswa kurejea kwayo.
18-9-2023 • 0
18 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tuanaangazia malengo ya maendeleo endelevu na tutasalia hapa makao makuu ya umoja wa Mataifa kwenye Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo hayo.Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu Malengo ya maendeleo endelevu SDGs, limefungua pazia leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuja na azimio la kisiasa la kuhakikissha wanayanusuru malengo hayo ambayo mengi yanakwenda mrama kwani ni asilimia 15 pekee kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ndio yametimizwa huku ikiwa imesalia chini ya miaka 7 kufikia mwaka 2030 ukomo wa utimizaji wa malengo hayo.Tarehe 17 na 18 Septemba yani leo na kesho hapa katika makao Makuu viongozi wanakutana kuangalia vipi wametekeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanatarajiwa kufikia kilele mwaka 2030. Katika makala Thelma Mwadzaya amefuatilia na kukuletea makala kuhusu apu iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iitwayo oKy ya kuwezesha wasichana kufuatilia hedhi, moja ya vipengele vya SDGs.Mashinani tunasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani kusikia kile ambacho vijana wanataka kifanyike ili malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaweze kufanikiwa, lakini kwanza ni makala nampisha Thelma Mwadzaya na makala kuhusu apu iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iitwayo oKy ya kuwezesha wasichana kufuatilia hedhi, moja ya vipengele vya SDGs. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
18-9-2023 • 0
18 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tuanaangazia malengo ya maendeleo endelevu na tutasalia hapa makao makuu ya umoja wa Mataifa kwenye Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo hayo.Jukwaa la siku mbili la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu Malengo ya maendeleo endelevu SDGs, limefungua pazia leo kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani. Lengo kubwa la jukwaa hilo ni kuja na azimio la kisiasa la kuhakikissha wanayanusuru malengo hayo ambayo mengi yanakwenda mrama kwani ni asilimia 15 pekee kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ndio yametimizwa huku ikiwa imesalia chini ya miaka 7 kufikia mwaka 2030 ukomo wa utimizaji wa malengo hayo.Tarehe 17 na 18 Septemba yani leo na kesho hapa katika makao Makuu viongozi wanakutana kuangalia vipi wametekeleza malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yanatarajiwa kufikia kilele mwaka 2030. Katika makala Thelma Mwadzaya amefuatilia na kukuletea makala kuhusu apu iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iitwayo oKy ya kuwezesha wasichana kufuatilia hedhi, moja ya vipengele vya SDGs.Mashinani tunasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani kusikia kile ambacho vijana wanataka kifanyike ili malengo ya maendeleo endelevu, SDGs yaweze kufanikiwa, lakini kwanza ni makala nampisha Thelma Mwadzaya na makala kuhusu apu iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF iitwayo oKy ya kuwezesha wasichana kufuatilia hedhi, moja ya vipengele vya SDGs. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
18-9-2023 • 0
Tunakumbatia wito wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo - Vijana Bongoyo Tanzania
Wakati macho na masikio ya Dunia yakielekezwa hapa New York Marekani kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumatatu wiki ijayo kujadili mada mbalimbali ikiwemo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , tunaelekea Tanzania ambako katika pitapita zake, Flora Nducha alipokuwa jijini Dar es Salaama alikutana na mmoja wa vijana wajasiriamali kwenye kisiwa cha Bongoyo waliokumbatia wito wa kupambana na jinamizi la mabadiliko ya tabianchi, akamweleza Flora kuwa mbali ya kujipatia kipato kutokana na utalii endelevu ana jukumu kubwa pamoja na baadhi ya vijana wenzie la kulinda msitu wa Bongoyo na matumbawe ya Kisiwa hicho kilicho katika Bahari ya Hindi. Tusikilize mahojiano na kijana huyo anayeanza kwa kujitambulisha.
15-9-2023 • 0
Tunakumbatia wito wa kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo - Vijana Bongoyo Tanzania
Wakati macho na masikio ya Dunia yakielekezwa hapa New York Marekani kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumatatu wiki ijayo kujadili mada mbalimbali ikiwemo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , tunaelekea Tanzania ambako katika pitapita zake, Flora Nducha alipokuwa jijini Dar es Salaama alikutana na mmoja wa vijana wajasiriamali kwenye kisiwa cha Bongoyo waliokumbatia wito wa kupambana na jinamizi la mabadiliko ya tabianchi, akamweleza Flora kuwa mbali ya kujipatia kipato kutokana na utalii endelevu ana jukumu kubwa pamoja na baadhi ya vijana wenzie la kulinda msitu wa Bongoyo na matumbawe ya Kisiwa hicho kilicho katika Bahari ya Hindi. Tusikilize mahojiano na kijana huyo anayeanza kwa kujitambulisha.
15-9-2023 • 0
WHO: Msizike marehemu wa majanga kwenye makaburi ya halaiki
Kunapotokea majanga au vita na kusababisha watu wengi kupoteza maisha kunakuwa na hofu kuhusu miili ya marehemu kuwa inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa hivyo baadhi ya jamii kwa kutokuwa na taarifa sahihi hujikuta wakizika miili hiyo katika makaburi ya halaiki ili kuepuka mlipuko wa magonjwa lakini shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linasema hiyo si sahihi. Kuzika marehemu ni ibada, ni heshima na kubwa zaidi husaidia wafiwa kuponya nafsi zao kwa kufunga ukurasa wa mpendwa wao wakibaki na matumaini kuwa wamempumzisha katika nyumba yake ya milele. Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa leo na WHO pamoja na shirika la chama cha Msalaba mwekundu ICRC na Mwezi mwekundu IFRC imeeleza kuwa miili ya watu ambao wamekufa kutokana na majeraha, katika majanga ya asili au vita kamwe haileti hatari ya kiafya kwa jamii. Hii ni kwa sababu watu hao ambao wamekufa kutokana na kiwewe, kuzama au moto hawahifadhi katika miili yao vinavyosababisha magonjwa ambayo yatahitaji jamii kuchukua tahadhari za kawaida.Dkt. Kazunobu Kojima ni Afisa Tiba wa ulinzi na usalama wa katika Mpango wa Dharura wa Afya wa WHO na ametoa ombi kwa mamlaka zote duniani. “Tunahimiza mamlaka katika jamii zilizoguswa na msiba kutoharakisha mazishi ya halaiki au kuchoma maiti. Usimamizi wenye heshima ni muhimu kwa familia na jamii, na katika maeneo yaliyo na migogoro, mara nyingi, ni sehemu muhimu ya kukomesha haraka mapigano.”WHO imeeleza kuwa eneo ambalo kuna magonjwa kama Ebola, Marburg au kipindupindu, au wakati maafa mengine yanapotokea katika eneo lenye magonjwa hayo ya kuambukiza hapo ni vyema kuzika marehemu haraka kwani magonjwa ya mlipuko yanaweza kutokea.Naye Mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa ICRC Pierre Guyomarch amesema “Imani kwamba maiti yoyote itasababisha magonjwa ya mlipuko haiungwi mkono na ushahidi wowote” na kutoa wito kwa wanao elimisha jamii kuzingatia utoaji taarifa sahihi.“Tumekuwa tukiona ripoti nyingi za vyombo vya habari na hata wataalamu wakikosea katika kushughulikia suala hili, ukweli ni kwamba wale wanaookoka kwenye matukio kama msiba wa asili wana uwezekano mkubwa wa kueneza magonjwa kuliko maiti.” Amesema Guyomarch. Mashirika hayo kwa pamoja yamehimiza jamii kupatiwa zana na taarifa sahihi ili kupunguza hofu na ili waweze kudhibiti na kuhifadhi maiti kwa usalama na heshima. Na wale wanaohusika katika kushughulikia majanga wanapaswa kufuata kanuni zilizowekwa za usimamizi wa maiti, kwa manufaa ya jamii yote, na watoe msaada zaidi kama inahitajika.
15-9-2023 • 0
WHO: Msizike marehemu wa majanga kwenye makaburi ya halaiki
Kunapotokea majanga au vita na kusababisha watu wengi kupoteza maisha kunakuwa na hofu kuhusu miili ya marehemu kuwa inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa hivyo baadhi ya jamii kwa kutokuwa na taarifa sahihi hujikuta wakizika miili hiyo katika makaburi ya halaiki ili kuepuka mlipuko wa magonjwa lakini shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linasema hiyo si sahihi. Kuzika marehemu ni ibada, ni heshima na kubwa zaidi husaidia wafiwa kuponya nafsi zao kwa kufunga ukurasa wa mpendwa wao wakibaki na matumaini kuwa wamempumzisha katika nyumba yake ya milele. Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa leo na WHO pamoja na shirika la chama cha Msalaba mwekundu ICRC na Mwezi mwekundu IFRC imeeleza kuwa miili ya watu ambao wamekufa kutokana na majeraha, katika majanga ya asili au vita kamwe haileti hatari ya kiafya kwa jamii. Hii ni kwa sababu watu hao ambao wamekufa kutokana na kiwewe, kuzama au moto hawahifadhi katika miili yao vinavyosababisha magonjwa ambayo yatahitaji jamii kuchukua tahadhari za kawaida.Dkt. Kazunobu Kojima ni Afisa Tiba wa ulinzi na usalama wa katika Mpango wa Dharura wa Afya wa WHO na ametoa ombi kwa mamlaka zote duniani. “Tunahimiza mamlaka katika jamii zilizoguswa na msiba kutoharakisha mazishi ya halaiki au kuchoma maiti. Usimamizi wenye heshima ni muhimu kwa familia na jamii, na katika maeneo yaliyo na migogoro, mara nyingi, ni sehemu muhimu ya kukomesha haraka mapigano.”WHO imeeleza kuwa eneo ambalo kuna magonjwa kama Ebola, Marburg au kipindupindu, au wakati maafa mengine yanapotokea katika eneo lenye magonjwa hayo ya kuambukiza hapo ni vyema kuzika marehemu haraka kwani magonjwa ya mlipuko yanaweza kutokea.Naye Mkuu wa kitengo cha uchunguzi wa ICRC Pierre Guyomarch amesema “Imani kwamba maiti yoyote itasababisha magonjwa ya mlipuko haiungwi mkono na ushahidi wowote” na kutoa wito kwa wanao elimisha jamii kuzingatia utoaji taarifa sahihi.“Tumekuwa tukiona ripoti nyingi za vyombo vya habari na hata wataalamu wakikosea katika kushughulikia suala hili, ukweli ni kwamba wale wanaookoka kwenye matukio kama msiba wa asili wana uwezekano mkubwa wa kueneza magonjwa kuliko maiti.” Amesema Guyomarch. Mashirika hayo kwa pamoja yamehimiza jamii kupatiwa zana na taarifa sahihi ili kupunguza hofu na ili waweze kudhibiti na kuhifadhi maiti kwa usalama na heshima. Na wale wanaohusika katika kushughulikia majanga wanapaswa kufuata kanuni zilizowekwa za usimamizi wa maiti, kwa manufaa ya jamii yote, na watoe msaada zaidi kama inahitajika.
15-9-2023 • 0
15 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea habari kuhusu magonjwa ya mlipuko baada ya majanga, na makaburi ya wafalme wa Uganda. Makala tunakupeleka nchini Tanzania kusikia matarajio wa wananchi tukielekea mkutano wa UNGA78 na mashinani tutasalia hapa hapa Makao Makuu kusikia ujumbe kuhusu kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika juma lijalo. Kunapotokea majanga au vita na kusababisha watu wengi kupoteza maisha kunakuwa na hofu kuhusu miili ya marehemu kuwa inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa hivyo baadhi ya jamii kwakutokuwa na taarifa sahihi hujikuta wakizika miili hiyo katika makaburi ya halaiki ili kuepuka mlipuko wa magonjwa lakini shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linasema hiyo si sahihi.Baada ya kunusurika kwa moto na hatimaye kuwekwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini kuharibika, makaburi ya wafalme wa Buganda huko Kasubi nchini Uganda sasa yako salama na yameondolewa kwenye orodha hiyo baada ya ukarabati uliofanywa na Uganda kwa usaidizi wa Umoja wa Mataifa na wadau. Katika makala na wakati macho na masikio ya Dunia yakielekezwa New York Marekani kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumatatu ijayo kujadili mada mbalimbali ikiwemo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na tunaelekea Tanzania.Mashinani tutasalia hapa makao Makuu kusikia ujumbe wa Mwakilishi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Linda Thomas-Greenfield kuhusu kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika juma lijalo. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
15-9-2023 • 0
15 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea habari kuhusu magonjwa ya mlipuko baada ya majanga, na makaburi ya wafalme wa Uganda. Makala tunakupeleka nchini Tanzania kusikia matarajio wa wananchi tukielekea mkutano wa UNGA78 na mashinani tutasalia hapa hapa Makao Makuu kusikia ujumbe kuhusu kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika juma lijalo. Kunapotokea majanga au vita na kusababisha watu wengi kupoteza maisha kunakuwa na hofu kuhusu miili ya marehemu kuwa inaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa hivyo baadhi ya jamii kwakutokuwa na taarifa sahihi hujikuta wakizika miili hiyo katika makaburi ya halaiki ili kuepuka mlipuko wa magonjwa lakini shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linasema hiyo si sahihi.Baada ya kunusurika kwa moto na hatimaye kuwekwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini kuharibika, makaburi ya wafalme wa Buganda huko Kasubi nchini Uganda sasa yako salama na yameondolewa kwenye orodha hiyo baada ya ukarabati uliofanywa na Uganda kwa usaidizi wa Umoja wa Mataifa na wadau. Katika makala na wakati macho na masikio ya Dunia yakielekezwa New York Marekani kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utakaoanza Jumatatu ijayo kujadili mada mbalimbali ikiwemo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na tunaelekea Tanzania.Mashinani tutasalia hapa makao Makuu kusikia ujumbe wa Mwakilishi wa kudumu wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Linda Thomas-Greenfield kuhusu kikao cha ngazi ya juu cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kitakachofanyika juma lijalo. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
15-9-2023 • 0
UNESCO imeondoa makaburi ya wafalme wa Buganda kwenye orodha, kulikoni?
Baada ya kunusurika kwa moto na hatimaye kuwekwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini kuharibika, makaburi ya wafalme wa Buganda huko Kasubi nchini Uganda sasa yako salama na yameondolewa kwenye orodha hiyo baada ya ukarabati uliofanywa na Uganda kwa usaidizi wa Umoja wa Mataifa na wadau. Mwaka 2010 moto mkubwa uliharibu kwa kiasi kikubwa Makaburi ya Wafalme wa Buganda kwenye vilima vya wilaya ya Kampala nchini Uganda, hali iliyosababisha Umoja wa Mataifa kuingilia kati kwa kuwa makaburi hayo yaliorodheshwa mwaka 2001 na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni kuwa eneo la urithi wa dunia. Lazare Eleoundou Assomo Mkurugenzi wa Kituo cha UNESCO cha Maeneo ya Urithi wa Dunia akizungumza akiwa kwenye eneo hilo anasema, ni siku ya kihistoria. Kamati ya Urithi wa Dunia imeondoa makaburi ya Kasubi kutoka orodha ya maeneo yaliyo hatarini. Miezi michache iliyopita nilitembelea eneo hili, na niliweza kuona kazi nzuri na ya kina iliyofanywa na wanajamii na watu wa Uganda. Napenda kumpongeza kila mtu kwa kazi hii kubwa. Hongereni sana nyote.” Makaburi hayo yako kwenye eneo la ukubwa wa ekari 30 na kwa kiasi kikubwa eneo hilo ni shamba ambalo kilimo chake hutumia mbinu za kiasili. Ujenzi wake umetumia vitu vya asili kama miti, nyasi na matete. Eneo la kati ni kasri ya zamani ya wafalme Kabaka wa Buganda iliyojengwa mwaka 1882 na kugeuzwa kuwa makaburi mwaka 1884. Wanajamii ndio waliokuwa kitovu cha mafanikio ya ukarabati wa makaburi hayo kwa ushirikiano na serikali na wataalamu ambapo walifanikisha ujenzi mpya wa Muzibu Azaala Mpanga ambalo ndilo jengo kuu lenye makaburi, na urejeshaji wa Bujjabukala, ambayo ni nyumba ya muangalizi na uwekaji wa mfumo wa kisasa wa kutoa onyo la kuzima moto. Mradi huo ulihusisha pia mafunzo kwa wazima moto kutoka eneo hilo ili kuzuia janga kama la 2010 lisitokee tena. Kikao cha 45 cha Kamati ya UNESCO ya maeneo ya urithi wa dunia kinafanyika huko Riyadhi, Saudi Arabia kuanzia tarehe 10 hadi 25 mwezi huu ambako pamoja na mambo mengine kinatathmini uhifadhi wa maeneo ya urithi wa dunia. Bofyahapakutambua maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini.
15-9-2023 • 0
UNESCO imeondoa makaburi ya wafalme wa Buganda kwenye orodha, kulikoni?
Baada ya kunusurika kwa moto na hatimaye kuwekwa kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini kuharibika, makaburi ya wafalme wa Buganda huko Kasubi nchini Uganda sasa yako salama na yameondolewa kwenye orodha hiyo baada ya ukarabati uliofanywa na Uganda kwa usaidizi wa Umoja wa Mataifa na wadau. Mwaka 2010 moto mkubwa uliharibu kwa kiasi kikubwa Makaburi ya Wafalme wa Buganda kwenye vilima vya wilaya ya Kampala nchini Uganda, hali iliyosababisha Umoja wa Mataifa kuingilia kati kwa kuwa makaburi hayo yaliorodheshwa mwaka 2001 na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni kuwa eneo la urithi wa dunia. Lazare Eleoundou Assomo Mkurugenzi wa Kituo cha UNESCO cha Maeneo ya Urithi wa Dunia akizungumza akiwa kwenye eneo hilo anasema, ni siku ya kihistoria. Kamati ya Urithi wa Dunia imeondoa makaburi ya Kasubi kutoka orodha ya maeneo yaliyo hatarini. Miezi michache iliyopita nilitembelea eneo hili, na niliweza kuona kazi nzuri na ya kina iliyofanywa na wanajamii na watu wa Uganda. Napenda kumpongeza kila mtu kwa kazi hii kubwa. Hongereni sana nyote.” Makaburi hayo yako kwenye eneo la ukubwa wa ekari 30 na kwa kiasi kikubwa eneo hilo ni shamba ambalo kilimo chake hutumia mbinu za kiasili. Ujenzi wake umetumia vitu vya asili kama miti, nyasi na matete. Eneo la kati ni kasri ya zamani ya wafalme Kabaka wa Buganda iliyojengwa mwaka 1882 na kugeuzwa kuwa makaburi mwaka 1884. Wanajamii ndio waliokuwa kitovu cha mafanikio ya ukarabati wa makaburi hayo kwa ushirikiano na serikali na wataalamu ambapo walifanikisha ujenzi mpya wa Muzibu Azaala Mpanga ambalo ndilo jengo kuu lenye makaburi, na urejeshaji wa Bujjabukala, ambayo ni nyumba ya muangalizi na uwekaji wa mfumo wa kisasa wa kutoa onyo la kuzima moto. Mradi huo ulihusisha pia mafunzo kwa wazima moto kutoka eneo hilo ili kuzuia janga kama la 2010 lisitokee tena. Kikao cha 45 cha Kamati ya UNESCO ya maeneo ya urithi wa dunia kinafanyika huko Riyadhi, Saudi Arabia kuanzia tarehe 10 hadi 25 mwezi huu ambako pamoja na mambo mengine kinatathmini uhifadhi wa maeneo ya urithi wa dunia. Bofyahapakutambua maeneo ya urithi wa dunia yaliyo hatarini.
15-9-2023 • 0
Mradi wa "Football for the Goals" kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu Rwanda - UN Rwanda
Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia chepuo mbinu mbali mbali halali za kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, na miongoni mwa mbinu hizo ni mpira wa miguu, soka, wengine wakisema kabumbu au kandanda! Sasa wenyewe wabobezi au manguli wa soka wameitikia wito na Umoja wa Mataifa hususan nchini Rwanda ukaitikia Naam!!! Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ameketi na Mkuu wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa UN, Rwanda Josephine Marealle-Ulimwengu na anafafanua kitendawili hicho.
14-9-2023 • 0
Mradi wa "Football for the Goals" kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu Rwanda - UN Rwanda
Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia chepuo mbinu mbali mbali halali za kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, na miongoni mwa mbinu hizo ni mpira wa miguu, soka, wengine wakisema kabumbu au kandanda! Sasa wenyewe wabobezi au manguli wa soka wameitikia wito na Umoja wa Mataifa hususan nchini Rwanda ukaitikia Naam!!! Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ameketi na Mkuu wa Ofisi ya Mratibu Mkazi wa UN, Rwanda Josephine Marealle-Ulimwengu na anafafanua kitendawili hicho.
14-9-2023 • 0
Jifunze Kiswahili - "Nyamba"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA akieleza maana ya neno “NYAMBA”.
14-9-2023 • 0
Jifunze Kiswahili - "Nyamba"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA akieleza maana ya neno “NYAMBA”.
14-9-2023 • 0
14 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia chepuo mbinu mbali mbali halali za kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, na miongoni mwa mbinu hizo ni mpira wa miguu, soka, wengine wakisema kabumbu au kandanda na tunabisha hodi nchini Rwanda kushuhudia jinzi ambavyo wameitikia. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kuhusu ombi la msaada kusaidia waathirika Libya, utabiri wa hali ya hewa na usalama wa afya ya mgonjwa. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tuankuletea ufafanuzi wa neno “NYAMBA”. Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths amesema kufuatia zahma kubwa ya mafuriko yaliyoikumba Libya na kuathiri maelfu kwa maelfu ya waltu leo ametoa dola milioni 10 kutoka kwenye mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF huku ombi la msaada zaidi likitarajiwa kwa lengo la kufikisha msaada unaohitajika haraka kwa waathirika na kuwaepushia janga zaidi la kiafya.Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika mbalimbali na kuratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO imesema wakati dunia imeshafikia nusu ya muda wa utimizaji wa ajenda ya maendeleo ya 2030, sayansi iko bayana kwamba lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi linakwenda kombo, hali ambayo inaathiri juhudi za kimataifa za kupambana na njaa, umasikini, afya, kuboresha fursa za upatikanaji wa maji na nishati na maeneo mengine ya malengo ya maendeleo endelevu SDG’s , kwani hadi sasa ni asilimia 15 pekee ya malengo hayo 17 ndio yakk kwenye mstari unaotakiwa. Na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limehitimisha mkutano wa kimataifa kuhusu ushirikishwaji na usalama wa afya ya mgonjwa kwa makubaliano ya mkataba wa kwanza kabisa wa haki za usalama wa mgonjwa ambao unabainisha haki za msingi za wagonjwa wote katika muktadha wa usalama wa huduma za afya na unataka kusaidia serikali na wadau wengine wa sekta ya afya kuhakikisha kwamba sauti za wagonjwa zinasikika na haki yao ya kupata huduma salama za afya inalindwa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili nampisha mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA akieleza maana ya neno “NYAMBA”. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
14-9-2023 • 0
14 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa ukipigia chepuo mbinu mbali mbali halali za kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, na miongoni mwa mbinu hizo ni mpira wa miguu, soka, wengine wakisema kabumbu au kandanda na tunabisha hodi nchini Rwanda kushuhudia jinzi ambavyo wameitikia. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kuhusu ombi la msaada kusaidia waathirika Libya, utabiri wa hali ya hewa na usalama wa afya ya mgonjwa. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tuankuletea ufafanuzi wa neno “NYAMBA”. Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths amesema kufuatia zahma kubwa ya mafuriko yaliyoikumba Libya na kuathiri maelfu kwa maelfu ya waltu leo ametoa dola milioni 10 kutoka kwenye mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF huku ombi la msaada zaidi likitarajiwa kwa lengo la kufikisha msaada unaohitajika haraka kwa waathirika na kuwaepushia janga zaidi la kiafya.Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika mbalimbali na kuratibiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO imesema wakati dunia imeshafikia nusu ya muda wa utimizaji wa ajenda ya maendeleo ya 2030, sayansi iko bayana kwamba lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi linakwenda kombo, hali ambayo inaathiri juhudi za kimataifa za kupambana na njaa, umasikini, afya, kuboresha fursa za upatikanaji wa maji na nishati na maeneo mengine ya malengo ya maendeleo endelevu SDG’s , kwani hadi sasa ni asilimia 15 pekee ya malengo hayo 17 ndio yakk kwenye mstari unaotakiwa. Na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limehitimisha mkutano wa kimataifa kuhusu ushirikishwaji na usalama wa afya ya mgonjwa kwa makubaliano ya mkataba wa kwanza kabisa wa haki za usalama wa mgonjwa ambao unabainisha haki za msingi za wagonjwa wote katika muktadha wa usalama wa huduma za afya na unataka kusaidia serikali na wadau wengine wa sekta ya afya kuhakikisha kwamba sauti za wagonjwa zinasikika na haki yao ya kupata huduma salama za afya inalindwa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili nampisha mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA akieleza maana ya neno “NYAMBA”. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
14-9-2023 • 0
Mradi wa stadi za maisha waleta manufaa kwa wanafunzi wa kike Tanzania
Shirika la Campaign for Female Education au CAMFED kwa kushirikiana na wizara za Elimu Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania wanatekeleza mradi wakutoa elimu ya stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike katika shule za sekondari za serikali lengo likiwa ni kuboresha stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike na kuwapa fursa zaidi za elimu na ujifunzaji.Mradi huo unaotekeleza lengo namba 4 na namba 5 la Malengo ya Maendeleo endelevu SDGs yanayohimiza elimu bora na usawa wa kijinsia mtawalia umeanza kuzaa matunda kama anavyotujuza John Kabambala wa redio washirika KidsTime FM nchini Tanzania.
13-9-2023 • 0
Mradi wa stadi za maisha waleta manufaa kwa wanafunzi wa kike Tanzania
Shirika la Campaign for Female Education au CAMFED kwa kushirikiana na wizara za Elimu Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nchini Tanzania wanatekeleza mradi wakutoa elimu ya stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike katika shule za sekondari za serikali lengo likiwa ni kuboresha stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike na kuwapa fursa zaidi za elimu na ujifunzaji.Mradi huo unaotekeleza lengo namba 4 na namba 5 la Malengo ya Maendeleo endelevu SDGs yanayohimiza elimu bora na usawa wa kijinsia mtawalia umeanza kuzaa matunda kama anavyotujuza John Kabambala wa redio washirika KidsTime FM nchini Tanzania.
13-9-2023 • 0
Mwanafunzi Malawi: Asante UNICEF, sasa kuoga si tatizo tena
Nchini Malawi, hofu ya wanafunzi wa kike kunuka wakati wakiwa kwenye hedhi kutokana na uhaba wa maji shuleni kwao imepatiwa jawabu baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kufunga kisima cha maji kinachotumia nishati ya sola kuvuta maji kutoka ardhini. Noria Kanyama, mwanafunzi huyu wa shule moja ya msingi wilaya ya Chikwawa, mkoa wa Kusini nchini Malawi akikumbuka siku ambayo mafuriko yalikumba eneo lao. Anasema ililazimu wakimbilie maeneo ya mwinuko ambako ndiko aliko hivi sasa. Anasema, hapa ndipo tulalapo, mimi, mama yangu na wadogo zangu watatu. Pahala penyewe ni chumba kimoja na kidogo. Vimbunga ikiwemo Idai na Fredy vilisambaratisha miundombinu ya maji kwenye eneo lao.Kwa hiyo kando ya zahma ya malazi, ni zahma ya maji, akisema walitembea mwendo mrefu kwenda kuteka maji mtoni ambapo walitumia saa moja kwenda na kurudi. Maji yenyewe anasema hayakuwa masafi na si salama na watu wengine waliugua kuhara kwa kunywa maji hayo. Lakini zaidi ya yote, “Ninapokuwa kwenye hedhi, wavulana shuleni huwa wanatucheka. Wanasema wasichana wananuka, wako kwenye hedhi. Hii inatufanya tusiende shuleni, tunabakia nyumbani hadi tumalize hedhi. Hii inatuacha nyuma kwa sababu wenzetu wanaendelea na masomo wakati sisi tuko nyumbani.” UNICEF kwa kutambua zahma hii imejenga kisima cha maji kinachotumia nishati ya sola kusukuma maji kutoka ardhini, kisima kinachohudumia watoto 504 na familia zao. Sasa Noria mwenye umri wa miaka 14 anasema, “Ujio wa kisima hiki umebadili maisha yangu mno. Kuoga si tatizo, halikadhalika maji ya kunywa. Magonjwa nayo yametoweka. Tunapenda kuwashukuru wale waliotuletea hii huduma ya maji. Kinachonifurahisha zaidi mama yangu ananiruhusu niende shuleni. Ndoto yangu ni kuwa daktari.”
13-9-2023 • 0
13 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea habari kutoka UNICEF na Benki ya Dunia. Makala tunamulika lengo namba nne na tano la malengo ya maendeleo endelevu SDGs ya Umoja wa Mataifa yanazungumzia upatikanaji wa elimu bora kwa wote na usawa wa kijinsia na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni?Ripoti mpya iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Benki ya Dunia inasema zaidi ya watoto milioni 333 duniani kote wanaishi katika ufukara, huku kudorora kwa uchumi kulikochangiwa na janga la COVID-19 kwa miaka mitatu kukichochea zaidi janga hilo.Nchini Malawi, hofu ya wanafunzi wa kike kunuka wakati wakiwa kwenye hedhi kutokana na uhaba wa maji shuleni kwao imepatiwa jawabu baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kufunga kisima cha maji kinachotumia nishati ya sola kuvuta maji kutoka ardhini. Makala tunamulika lengo namba nne na tano la malengo ya maendeleo endelevu SDGs ya Umoja wa Mataifa yanazungumzia upatikanaji wa elimu bora kwa wote na usawa wa kijinsia ambapo serikali zinahimizwa kushirikiana na wadau kuhakikisha yote yanatimia ifikapo mwaka 2030 na nchini Tanzania shirika la CAMFED linatekeleza malengo hayo katika mradi wa kutoa elimi ya Stadi za maisha kwa wanafunzi wa kike wa shule za serikali za sekondari na tayari faida zimeanza kuonekana.Na mashinani tutakupeleka nchini Sudan ambapo licha ya migogoro ambayo imesababisha watu wengi nchini humo kukimbia makazi yao, wahudumu wa afya wanaendelea kutoa huduma kwa wananchi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
13-9-2023 • 0
UNICEF/Benki ya Dunia: Watoto milioni 333 duniani kote wanaishi katika ufukara
Ripoti mpya iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Benki ya Dunia inasema zaidi ya watoto milioni 333 duniani kote wanaishi katika ufukara, huku kudorora kwa uchumi kulikochangiwa na janga la COVID-19 kwa miaka mitatu kukichochea zaidi janga hilo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo “Mwenendo wa kimataifa wa umaskini wa kifedha wa mtoto kulingana na mistari ya kimataifa ya umaskini” iliyotolewa mjini New York na Washington mtoto 1 kati ya 6 kote duniani anaishi kwa chini dola 2 na senti 15 kwa siku ikiwa imepungua kutoka watoto milioni 383 hadi milioni 333 sawa na asilimia 13 kati ya mwaka 2013 na 2022.Ripoti imesema athari za kiuchumi za janga la COVID-19 zimechangia kupotea kwa miaka mitatu ya kupiga hatua za kiuchumi na kuwaacha watoto milioni 30 zaidi kusalia katika umasikini ambao waliotarajiwa kuondolewa kwenye jinamizi hilo.Tathimini hii iliyotolewa kuelekea mjadala wa Baraza Kuu la umoja wa Mataifa wa ngazi ya juu wiki ijayo ambao pamoja na mambo mengine viongozi wa dunia watatthimini hatua za mchakato wa utekelezaji wa malengo ya malengo ya maendeleo endelevu SDG’s inaonya kwamba lengo la kutokomeza umasikini kwa watuto ifikapo mwaka 2030 halitotimia.Mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Catherine Russell amesema "Miaka saba iliyopita, dunia ilitoa ahadi ya kumaliza umaskini uliokithiri kwa watoto ifikapo mwaka 2030. Tumepiga hatua, tukionyesha kwamba kwa uwekezaji na utashi sahihi, kuna uwezekano wa kuwainua mamilioni ya watoto kutoka katika hali mbaya ya maisha ya umaskini. Lakini majanga yanayoongezeka kuanzia athari za COVID-19, migogoro, mabadiliko ya tabianchi na majanga ya kiuchumi, yamezuia maendeleo, na kuwaacha mamilioni ya watoto katika umaskini uliokithiri. Hatuwezi kuwaangusha watoto hawa sasa. Kutokomeza umaskini wa watoto ni chaguo la kisera. Juhudi lazima ziongezwe maradufu ili kuhakikisha watoto wote wanapata huduma muhimu, ikiwa ni pamoja na elimu, lishe, huduma za afya na hifadhi ya jamii, huku tukishughulikia chanzo cha umaskini uliokithiri.”Naye Luis-Felipe Lopez-Calva mkurugenzi wa kimataifa wa Benki ya Dunia wa masuala ya umaskini na usawa amesema"Dunia ambapo watoto milioni 333 wanaishi katika umaskini uliokithiri na kunyimwa sio tu mahitaji ya msingi lakini pia utu, fursa au matumaini hali hii haiwezi kuvumiliwa. Ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwamba watoto wote wawe na fursa bayana ya kutoka katika umaskini kupitia upatikanaji sawa wa elimu bora, lishe bora, afya, ulinzi wa hifadhi ya jamii, pamoja na ulinzi na usalama. Ripoti hii inapaswa kuwa kumbusho tosha kwamba hatuna muda wa kupoteza katika vita dhidi ya umaskini na ukosefu wa usawa, na kwamba watoto lazima wawe kipaumbele katika juhudi zetu.”Tathimini ya ripoti hiyo inaonyesha kuwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ndizo zinazobeba mzigo mkubwa zaidi wa watoto masikini kwani asilimia 40 wanaishi katika ufukara, na ilichangia ongezeko kubwa la Watoto masikini katika muongo uliopita, ikipanda kutoka asilimia 54.8 mwaka 2013 hadi asilimia 71.1 mwaka 2022.Wakati huo huo, ripoti inasema maeneo mengine yote duniani yameshuhudia kupungua kwa kasi kwa viwango vya umaskini uliokithiri, isipokuwa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.
13-9-2023 • 0
12 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani leo inatupeleka nchini Kenya kupata tathmini ya wanamazingira kufuatia kumalizika kwa mkutano wa siku tatu wa viongozi wa Afrika kuhusu tabianchi, mkutano uliotamatishwa kwa kupitishwa kwa azimio la Nairobi ambalo lilikuwa na vipengele 10 vya hatua za kuchukua ikiwemo wito kwa viongozi wa dunia kutambua kuwa uwepo wa shughuli za kiuchumi zitoazo kiwango kidogo cha hewa ya ukaa, ni fursa pia ya kuchangia katika usawa na ustawi wa watu wote duniani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwema za WHO na WMO. Mashinani tunakupeleka nchini nchini Sudan Kusini kusikia simulizi ya mkimbizi kutoka nchini Sudan.Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Usalama wa Mgonjwa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, Dkt. Tedros Ghebreyesus ameuambia Mkutano wa Kimataifa wa WHO mjini Geneva, Uswisi kuwa ushahidi unaonesha kwamba mitazamo ambayo wagonjwa na familia zao huleta husababisha huduma bora, uzoefu bora wa wagonjwa, na matokeo bora.Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani (WMO) limeeleza kuwa maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa kupindukia siku mbili zilizopita nchini Libya yamesisitiza haja ya kampeni ya kimataifa ya Maonyo ya Mapema kwa Wote iliyozinduliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres mapema mwaka jana. Na Leo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limezindua miongozo miwili iliyoundwa ili kuimarisha juhudi za kuzuia watu kujiua. Mmoja ni muongozo ulioboreshwa kwa ajili wataalamu wa vyombo vya habari na pili Muhtasari wa sera kuhusu vipengele vya afya vya kuyafanya majaribio ya kujiua na kujiua yasiwe jinai.Na mashinani leo Aziza Harba Idriss, mkimbizi kutoka Sudan ambaye alikimbilia nchi jirani ya Sudan Kusini kupitia njia hatarishi akisaka usalama anasimulia changamoto alizozipitia.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
12-9-2023 • 0
Türk: Haki ya makazi bado ni ndoto kwa wengi duniani
Mkutano wa 54 wa Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu umeanza hii leo huko Geneva, Uswisi ambapo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Volker Türk pamoja na mambo mengine amesisitiza suala la makazi kama moja ya haki za msingi za binadamu na haki inayopigiwa chepuo pia kwenye malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Mwakilishi wa kudumu wa Gambia kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi, anaomba wajumbe kusimama kwa dakika moja kukumbuka watu waliopoteza maisha kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililokumba Morocco usiku wa kuamkia jumamosi. Kisha hotuba zikaanza na ulipowadia wakati wa Kamishna Mkuu Volker Türk, yeye amemulika masuala mbali mbali ikiwemo mahitaji na haki za watu kuishi kwenye mazingira bora ya maisha, makazi na kupata chakula na huduma za afya wakati wowote wanapohitaji, hivyo vyote vikisalia ndoto kwa wengi. Bwana Türk amesema “lakini katika nchi nyingi, makazi, mathalani yanaonekana kama bidhaa ya uwekezaji kulingana na mahitaji ya soko: mchezo wa soko la fedha badala ya kuwa haki ya msingi. Janga la kuweko kwa makazi yenye unafuu linabinya vipato vya familia, linaongeza kasi ya ukosefu usawa, linadhuru afya ya watoto, linafanya vijana wawe hohehahe, na kuchochea zaidi janga la watu kutokuwa na makazi. Janga hili limesambaa pia katika nchi zilizoendelea.” Bwana Türk amesema anaangazia zaidi janga la watu kukosa makazi au pahala pa kuishi kwa sababu suala hilo ndio msingi wa mkataba wa kijami. Amesema nchini Marekani, zadi ya watu 500,000 hawakuwa na makazi mwezi Januari mwaka 2022, kwa mujibu wa takwimu rasmi, ambapo asilimia 40 kati yao hao ni watu wenye asili ya Afrika, ambao ni asilimia 12 ya wanachi wote wa Marekani. Bwana Türk amekumbusha kuwa kutokomeza ukosefu wa makazi na kuhakikisha upatikanaj wa makazi nafuu vimejumuishwa kwenye malengo ya maendleeo endelevu na pia ni haki ya msingi wa binadamu. Ametoa wito kwa nchi zote hususan zilizoendelea kuelekeza rasilimali ili kukidhi haki hiyo kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
11-9-2023 • 0
Mradi wa UNCDF Tanzania wawezesha kaya kuondakana na nishati hatarishi ya kupikia
Nchini Tanzania kuna kaya nyingi ambazo zinatumia mkaa, kuni na mafuta ya taa kama tegemeo kuu la mapishi ya nyumbani, nishati ambazo si rafiki sio tu kwa mazingira bali pia afya ya mamilioni ya binadamu. Lakini sasa kuna mabadiliko,wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo nishati jadidifu na salama; wakati huu ambapo pia wakuu wa nchi watakutana jijini New York, Marekani kutathmini hatua zipi zimechukuliwa kubadili mwelekeo wa mabadiliko ya tabianchi. Shukrani kwa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya mitaji, UNCDF uitwao COOK FUND unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya. Mradi huu unalenga kuchangia katika ahadi za Tanzania katika kukabili athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kuongeza idadi ya watu wanaopata nishati safi ya kupikia hadi asilimia 80 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2023. Evarist Mapesa anafafanua kwenye makala hii..
11-9-2023 • 0
11 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia haki ya makazi na mkutano wa G20. Makala na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Mkutano wa 54 wa Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu umeanza hii leo huko Geneva, Uswisi ambapo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Volker Türk pamoja na mambo mengine amesisitiza suala la makazi kama moja ya haki za msingi za binadamu na haki inayopigiwa chepuo pia kwenye malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.Mkutano wa kila mwaka wa Kundi la Nchi 20 zenye Maendeleo Makubwa ya Kiuchumi Duniani (G20) umehitimishwa jana katika mji mkuu wa India New Delhi huku Umoja wa Mataifa ukiwa umekaribisha kupitishwa kwa Azimio la Viongozi wa Kundi hilo kukubali kujumuisha Muungano wa Afrika (AU) kama mwanachama wake mpya wa kudumu. Katika makala Evarist Mapesa kutoka Tanzania amefuatilia mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa unaoleta majawabu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania kwa kuwezesha kaya kutumia nishati jadidifu katika kupikia.Na mashinani tunasalia nchini Tanzania kusikia ni kwa jinzi gani mashirika wanasaidia wasichana waathririka wa mimba za utotoni kurejea shuleni na hatimaye kufikia ndoto zao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
11-9-2023 • 0
African Union kukubaliwa katika G20 ni taswira ya kuongezeka kwa umuhimu wa Afrika kimataifa - Guterres
Mkutano wa kila mwaka wa Kundi la Nchi 20 zenye Maendeleo Makubwa ya Kiuchumi Duniani (G20) umehitimishwa jana katika mji mkuu wa India New Delhi huku Umoja wa Mataifa ukiwa umekaribisha kupitishwa kwa Azimio la Viongozi wa Kundi hilo kukubali kujumuisha Muungano wa Afrika (AU) kama mwanachama wake mpya wa kudumu. "Hii ni taswira ya kuongezeka kwa ushawishi na umuhimu wa Afrika katika hatua ya kimataifa," alieleza Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema kupitia Msemaji wake mara tu baada ya uamuzi huo wa G20 kuujumuisha muungano wa Afrika kama mwanachama wake wa kudumu na akaongeza kuwa, "Wakati sehemu kubwa ya usanifu wa kimataifa uliopo ulipojengwa, sehemu kubwa ya Afŕika ilikuwa bado inatawaliwa na ukoloni na haikuwa na fuŕsa ya kusikilizwa sauti zao. Hii ni hatua nyingine ya kurekebisha usawa huo." Baadhi ya viongozi wa Afrika haraka baada ya uamuzi huo walijitokeza kuonesha furaha yao ambapo kwa upande wake Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye pia alihuduria mkutano huo aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa X akisema, "Tuna furaha kwamba G20 imekubali AU kama mwanachama wa G20. Mabadiliko ya tabianchi, uharibifu wa mazingira, matumizi yasiyo endelevu na uzalishaji na uhaba wa rasilimali ni changamoto zinazoweza kutatuliwa kwa pamoja na kwa mshikamano mkubwa." Naye Rais wa Kenya William Ruto akitumia pia ukurasa wake wa X aliandika, "Kenya inakaribisha kuongezwa katika G20 Muungano wa Afrika - bara linalokua kwa kasi zaidi duniani. Hii itaongeza sauti ya Afrika, kuonekana, na ushawishi katika jukwaa la kimataifa na kutoa jukwaa la kuendeleza maslahi ya pamoja ya watu wetu. Hii inaendana kikamilifu na maazimio ya Mkutano wa Afrika kuhusu Tabianchi uliokamilika hivi karibuni.” Katika Mkutano wa G20, chini ya Kauli Mbiu “Dunia Moja, Familia Moja, Mstakabali Mmoja,” masuala muhimu kama vile uhakika wa chakula, tabianchi na nishati, maendeleo, afya na digitali yalijadiliwa.
11-9-2023 • 0
Dola Bil 360 zinahitajika kwa mwaka ili kufikia usawa wa kijinsia 2030
Takwimu mpya zilizokusanywa na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa zimeonesha kuwa kuna haja ya uwekezaji wa ziada wa dola bilioni 360 kwa mwaka ili kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake ifikapo 2030. Hapo jana mchana kwa saa za New York Marekani shirika la Umoja wa Mataifa la UN WOMEN linalohusika na masuala ya wanawake na UNDESA ambayo ni Idara ya Umoja wa Mataifa ya uchumi na kijamii, walizindua ripoti yao ya kila mwaka ya Maendeleo kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu: Muhtasari wa jinsia 2023 inayotathimini namna malengo 17 ya maendeleo endelevu SDGs yanavyotekelezwa kwa kuzingatia usawa wa kijinsia.Utafiti wa mwaka huu ulihusisha nchi 116 pamoja na mambo mengine uliweka mkazo kwa wanawake wazee ambapo ripoti ilionesha kuwa kundi hilo ndani ya jamii linakabiliwa na viwango vikubwa si tu vya umasikini na kutokuwa na pensheni, bali pia ukatili, ikilinganishwa na wanaume wazee. Wakati huu ambapo utelekezaji wa SDGs umefika nusu ya muda uliopangwa kabla ya kufikia kilele hapo mwaka 2030, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women Bi. Sarah Hendriks anasema ripoti ya mwaka huu ni wito mkubwa wa kuchukua hatua. Bi. Hendriks aliongeza kuwa “ni lazima kwa pamoja na kwa dhamira ya dhati tuchukue hatua sasa kusahihisha changamoto zilizopo ili tuwe na ulimwengu ambao mwanamke na msichana wana haki sawa, fursa na uwakilishi. Ili kufikia hili, tunahitaji dhamira isiyoyumba, suluhu bunifu, na ushirikiano katika sekta zote na washikadau.”Ripoti hii imesisitiza hitaji la dharura la juhudi madhubuti za kuharakisha maendeleo kuelekea usawa wa Kihansi ifikapo mwaka 2030 na kueleza kwamba zaidi ya dola bilioni 360 kwa mwaka zinahitajika ili kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika malengo muhimu ya kimataifa.Pamoja kupigiwa chepuo kila kwenye majukwaa makubwa hususani ya wafanya maamuzi, pengo la kijinsia katika madaraka na nyadhifa za uongozi bado limekita mizizi, na, kwa kasi ya sasa ya maendeleo, ripoti imeeelza kizazi kijacho cha wanawake bado kitatumia wastani wa saa 2.3 zaidi kwa kila siku bila ujira wakati wakifanya kazi za nyumbani kuliko wanaume.Ripoti ya mwaka huu pia iliangazia suala la mabadiliko ya tabianchi na takwimu zilizokusanywa zimeonesha kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaweza kusukuma hadi wanawake na wasichana milioni 158.3 katika umasikini. Idadi hiyo zaidi ya milioni 16 ikilinganishwa na wanaume na wavulana. Ripoti hiyo pia inajumuisha wito wa kuwa na mtazamo jumuishi na wa kiujumla, ushirikiano mkubwa kati ya wadau, ufadhili endelevu, na hatua za kisera kushughulikia tofauti za kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana duniani kote, ikihitimisha kwamba kushindwa kuweka kipaumbele kwa usawa wa kijinsia sasa kunaweza kuhatarisha Ajenda nzima ya 2030 ya SDGs.
8-9-2023 • 0
08 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia habari za masikitiko kuhusu watototo katika migogoro nchini DRC. Pia tunamulika pengo katika usawa wa kijinsia. Makala tunarejelea ufafanuzi wa ibara ya 9 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu na mashinani tunakuletea ujumbe wa vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi.Ukatili dhidi ya watoto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC umepindukia, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo likitolea mfano watoto mapacha ambao hivi karibuni walikutwa wamefungwa mkanda wenye mabomu kiunoni ili yeyote atakayejaribu kuufungua uwezo kulipuka na kusababisha maafa.Takwimu mpya zilizokusanywa na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa zimeonesha kuwa kuna haja ya uwekezaji wa ziada wa dola bilioni 360 kwa mwaka ili kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake ifikapo 2030. Katika makala Anold Kayanda akizungumza na Jebra Kombole, Mwanasheria na Wakili kutoka TAnzania akifafanua Ibara ya 9 ya Tamko la Kimataifa la Haki za binadamu ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75 tangu lipitishwe.Na mashinani Balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto, UNICEF kutoka Uganda ni mmoja wa vijana ambao wanahudhuria Wiki ya Tabianchi ya Afrika nchini Kenya inayokunja jamvi hii leo, wiki iliyoambatana na Mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi, uliofunga pazia tarehe 6 mwezi huu wa Septemba nchini Kenya na anatoa ujumbe wa vijana.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
8-9-2023 • 0
Nchini DRC watoto wamefungwa mitego ya mikanda ya mabomu
Ukatili dhidi ya watoto mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC umepindukia, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo likitolea mfano watoto mapacha ambao hivi karibuni walikutwa wamefungwa mkanda wenye mabomu kiunoni ili yeyote atakayejaribu kuufungua uwezo kulipuka na kusababisha maafa.Ni Grant Leaity mwakilishi wa UNICEF nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC akieleza kuwa hivi karibuni alitembelea kituo kimoja jimboni Kivu Kaskazini kinachohifadhi watoto walioachiliwa huru na vikundi vilivyojihami na kukuta watoto wawili mapacha wenye umri wa mwaka mmoja waliokuwa wametelekezwa kwenye Kijiji wakiwa na mkanda kiunoni wenye mabomu. Amewaambia waandishi wa Habari mjini Geneva USwisi hii leo kuwa kitendo hicho ni miongoni mwa ukatili dhidi ya watoto nchini DRC na kwamba ni taifa lenye matukio makubwa ya ukatili dhidi ya watoto yaliyothibitishwa na Umoja wa Mataifa. Katika kipindi cha mwaka mmoja, ongezeko la ghasia mashariki mwa DRC limesababisha ukimbizi mkubwa zaidi Afrika, watoto zaidi ya milioni 2.8 wakibeba mzigo wa janga hilo. Bwana Leity anasema niko hapa leo, natumai nitapaza sauti nisikike. Kila siku watoto wanabakwa, na wanauawa, wanatekwa, wanatumikishwa vitani na wanatumiwa na makundi yaliyojihami na tunajua ripoti tulizo nazo ni kidogo kulinganisha na matukio halisi.” Alipoulizwa nini kilitokea baada ya kubaini watoto hao, Mwakilishi huyo wa UNICEF DRC amesema “tuliwasiliana na wenzetu wataalamu wa kutegua mabomu ambao walikuja na kuweza kuondoa mtego huo wa mabomu kwa usalama.” Amesema matumizi ya vilipuzi vya kutengeneza yanazidi kuongezeka DRC. na hivyo UNICEF inatoa wito kwa hatua zichukuliwe ili kumaliza mzozo na familia zirejee nyumbani. Pamoja na ghasia ya kiwango cha juu dhidi ya watoto, Afisa huyo amesema maisha ya watoto mashariki mwa DRC yanatishiwa na milipuko ya magonjwa na utapiamlo. Takribani watoto milioni 1.2 wenye umri wa chini ya miaka mitano wanakabiliwa na utapiamlo uliokithiri kwenye eneo hilo. UNICEF inasema dunia inawaangusha watoto wa DRC kwani imewasahau, ikisema kuna matumaini lakini bado msaada unahitaji kwenye maeneo mawili. Mosi, rasilimali kuweza kukidhi mahitaji ya kibinadamu ya watoto inahitaji dola milioni 400. Pili ni utashi wa kisiasa kumaliza mzozo unaoendelea DRC na hivyo inatoa wito kwa serikali, mataifa ya Afrika na jamii ya kimataifa kushirikiana kusaka suluhisho la amani ya kudumu kwenye janga hilo ili familia zirejee nyumbani.
8-9-2023 • 0
Methali: "Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali "KIVULI CHA FIMBO HAKIMFICHI MTU JUA"
7-9-2023 • 0
07 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Magavana Dkt. Wilber Ottichilo wa Kaunti ya Vihiga na Gavana wa Kaunti ya Narok, Patrick Ole Ntutu hivi karibuni walipohudhuria Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu SDGs lijulikanalo kama HLPF hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, waliketi na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ili waeleze mipango yao ya kutimiza Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs katika majimbo yao huko nchini Kenya. Pia tunakuletea habari kwa fupi kuhusu Akili mnemba au AI, Siku ya Polisi na mkutano wa ASEAN. Katika kujifunza lugha ya kiswahili tunakuletea maana ya methali KIVULI CHA FIMBO HAKIMFICHI MTU JUA.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezipongeza nchi za kusini-mashariki mwa Asia kwa mchango wake wa kujenga maelewano duniani kote wakati huu ambapo ulimwengu umegubikwa na mivutano ya kisiasa na kijiografia.Ikiwa leo ni siku ya Kimataifa ya Ushirikiano na Polisi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewatumia salamu za pongezi polisi ulimwenguni kote kwa kujitolea kwao kuhakikisha jamii inakuwa na amani, usalama na haki. Amewakumbusha pia upolisi unaolenga katika kusaka suluhisho za kijamii husaidia zaidi kujenga uaminifu na kuboresha usalama. Na tuhitimishe na masuala ya teknolojia, wakati muhula mpya wa masomo ukianza maeneo mengi duniani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limetoa muongozo wenye vipengele saba unaotaka nchi kudhibiti matumizi ya akili mnemba au -AI mashuleni.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali KIVULI CHA FIMBO HAKIMFICHI MTU JUA.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
7-9-2023 • 0
Amini Sayansi na sikilizeni sauti za watoto na vijana - Vijana katika mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi
Mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi uliokunja chamvi hii leo jijini Nairobi nchini Kenya, umeleta pamoja vijana wanaharakati wa tabianchi kutoka nchi zote barani Afrika. Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIS Nairobi amekutana na baadhi ya vijana hao kandoni mwa mkutano huo na wanaeleza mawazo yao na walichojifunza.
6-9-2023 • 0
Azimio la Nairobi kuhusu mabadiliko ya tabianchi lapitishwa na viongozi wa Afrika
Mkutano wa siku tatu wa viongozi wa Afrika kuhusu tabianchi umekunja jamvi hii leo huko Nairobi Kenya kwa viongozi hao kupitisha Azimio la Nairobi kuhusu mabadiliko ya tabianchi likiwa na vipengele 10 vya hatua za kuchukua ikiwemo wito kwa viongozi wa dunia kutambua kuwa uwepo wa shughuli za kiuchumi zitoazo kiwango kidogo cha hewa ya ukaa, ni fursa pia ya kuchangia katika usawa na ustawi wa watu wote duniani. Azimio hilo limepitishwa kwa kutambua mambo kadhaa ikiwemo ripoti ya IPCC ya kwamba joto linaongezeka kwa kasi kubwa barani Afrika kuliko mabara mengine na iwapo hatua hazitachukuliwa, mabadiliko ya tabianchi yatakuwa na madhara makubwa kwa uchumi wa Afrika na jamii zake, halikadhalika kukwamisha ukuaji na ustawi wa watu wake. Hivyo azimio hilo linakaribisha wadau wa maendeleo kutoka pande zote usaidizi wao wa kiufundi na kifedha kwa Afrika ili kusongesha matumizi endelevu ya maliasili zilizomo kwenye bara hilo ili kutoa kiwango kidogo cha hewa ya ukaa na hivyo kuchangia katika upunguzaji wa hewa hiyo duniani. Halikadhalika linataka hatua za kina dhidi ya janga la madeni ili kuepusha nchi kutumbukia kwenye mtego wa kushindwa kulipa na badala yake kuwekwe mfumo unaokidhi mahitaij ya nchi zinazoendelea katika kupata fedha za maendeleo na hatua kwa tabianchi. Azimio linapendekeza kuanzishwa kwa mfumo mpya wa ufadhili unaokidhi mahitaji ya Afrika, ikiwemo marekebisho ya mfumo wa madeni na msamaha kupitia kuanzishwa kwa Chata ya kimataifa ya ufadhili kwa tabianchi kupitia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ifikapo mwaka 2025. Pamoja na kuamua kuwa Azimio hili litakuwa msingi wa msimamo wa mchakato wa Afrika kwa tabianchi kuelekea mkutano wa 28 wa mabadiliko ya tabianchi, COP28 baadaye mwaka huu, azimio hilo pia limeitaka Kamisheniya Muunganowa Afrika kuandaa mpango wa utekelezaji na kufanya Mabadiliko ya Tabianchi kuwa maudhumi ya Muungano wa Afrika kwa mwaka 2025 au 2026. Mkutano huo wa siku tatu umemazilika leo lakini Wiki ya Tabianchi Afrika iliyoanza tarehe 4 itamalizika tarehe 8 mwezi huu wa Septemba.
6-9-2023 • 0
06 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi nchini Kenya leo hii ikifunga pazia. Pia tunamulika kazi za walinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR. Makala na mashinani tunasalia nchini Kenya katika mkutano wa Afrika kuhusu kukuletea ujumbe wa vijana.Mkutano wa siku tatu wa viongozi wa Afrika kuhusu tabianchi umekunja jamvi hii leo huko Nairobi Kenya kwa viongozi hao kupitisha Azimio la Nairobi kuhusu mabadiliko ya tabianchi likiwa na vipengele 10 vya hatua za kuchukua ikiwemo wito kwa viongozi wa dunia kutambua kuwa uwepo wa shughuli za kiuchumi zitoazo kiwango kidogo cha hewa ya ukaa, ni fursa pia ya kuchangia katika usawa na ustawi wa watu wote duniani. Walinda amani wa Tanzania wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA wametoa misaada mbalimbali kwa jamii wanazo zilinda. Katika Makala Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIS Nairobi anawapa fursa vijana wengine waliohudhuria mkutano huo uliofikia tamati leo kueleza mawazo yao na walichojifunza.Na katika mashinani Mohammed Abbas, Mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania ambaye pia ni mmjoa wa vijana waliohudhuria Mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi anatoa ujumbe wake akizungumza na Kituo hicho hicho cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIS Nairobi kandoni mwa mkutano huo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
6-9-2023 • 0
Walinda amani kutoka Tanzania TANBAT 6 wafanya usafi na kutoa msaada wa vifaa tiba CAR
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutokaTanzania wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, MINUSCA wametoa misaada mbalimbali kwa jamii wanazolinda kama moja ya sehemu ya kuimarisha utangamano na maelewano kati yao na jamii wanayoilinda. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Kapten Mwijage Inyoma. Taarifa ya Kapten Mwijage Inyoma Wanajeshi wa TANBAT 6 ambacho ni Kikosi cha sita cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wamefanya usafi na kukabidhi baadhi ya vifaa tiba Kwa Mganga Mkuu wa hospitali ya Mkoa wa Mambéré-Kadéï ikiwa ni namna mojawapo ya kusherehekea kilele cha maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 59 ya kuundwa Kwa Jeshi la Ulinzi la wananchi Tanzania JWTZ, ambalo limekuwa mstari wa mbele kuchangia kwenye ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa. Bi. Atheo Mathible ni Mkuu wa hospitali hiyo. “Nawapongeza walinda Amani wa jeshi laTanzania kwa jeshi lao kutimiza miaka 59 Kwa kweli si kazi ndogo toka mwaka 1964 mpaka sasa likiwa imara, lakini pia tunawashukuru kutumia maadhimisho hayo kusaidia jamii Kwa kufanya usafi eneo la hospitali yetu” Akihitimisha maadhimisho hayo Mkuu wa kikosi TANBAT6 Luten kanali Ramadhani Shaaban Ramadhani anasema, “Ujumbe wangu kwa wanajeshi wenzangu hasa wanaohudumu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya kazi kwa bidhii na weledi wa hali ya juu ili kuweza kufikia lengo kuu la MINUSCA ambalo ni amani ya kudumu”
6-9-2023 • 0
05 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mada kwa kina ikimulika Siku ya kimataifa ya hisani au kuwaonea huruma wagonjwa na maskini. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo yanayojiri katika mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi nchini Kenya na ujumbe wa Rais wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Kőrösi akitamatisha awamu yake hii leo. Katika mashinani tunakupeleka nchini DRC, kulikoni?Mkutano wa Afrika kuhusu tabianchi ukiingia siku ya pili hii leo huko Nairobi, Kenya, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bara la Afrika lina asilimia 30 ya akiba ya madini ambayo ni muhimu katika kuzalisha nishati jadidifu na teknolojia zinazotoa kiwango kidogo cha hewa ya ukaa, rasilimali ambazo zinaweza kuifanya Afrika kuwa kitovu cha nishati jadidifu duniani iwapo zitatumika kiuendelevu na kwa haki.Tukisalia kwenye mkutano huo, mmoja wa washiriki ni Dkt. Victor Yamo kutoka shirika la World Animal Protection la kulinda haki za wanyama na anasisitizia umuhimu wa kuwa na mifumo endelevu ya ufugaji. Na Rais wa mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Kőrösi ametamatisha awamu yake hii leo kwa kuwaeleza wajumbe kuwa mivutano ya kisiasa katu haiwezi kuisha duniani, lakini mivutano hiyo ipatiwe suluhu si kwa mmoja kushinda na mwingine kupoteza bali kwa kuridhiana kupitia maazimio yanayopitishwa na Baraza hilo.Na mashinani tutakupeleka nchini Jamhuri ya Kiemokrasia ya Congo, DRC ambapo mizozo na ongezeko la idadi ya watu wanaokimbia makazi yao mashariki mwa nchi hiyo linawafanya watoto kuingia katika janga kubwa la kipindupindu kuwahi tokea tangu mwaka 2017”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
5-9-2023 • 0
Ndoto za kuwa daktari au Mwalimu Mkuu kwa watoto hawa zitatimia?
Ijapokuwa ni wakimbizi wa ndani na wanaishi kwenye kituo cha kuhifadhi wakimbizi wa ndani cha Bushagara, mjini Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mtoto Irene anataka kuwa daktari, na Christelle anataka kuwa Mwalimu Mkuu. Ingawa hivyo, elimu bado ni changamoto kubwa kwa watoto milioni 2.4 wakimbizi wa ndani nchini DRC hususan majimbo ya Kivu Kaskazini, Ituri na Kivu Kusini ambao wanahitaji elimu kwa haraka. Hoja ni iwapo ndoto zao hizo zitatimia au ndio zitapeperushwa na vita inayoendelea nchini mwao na kuwafurusha kila uchao? Assumpta Massoi kupitia Makala hii iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura anakuletea simulizi za watoto hao wakiwa Bushagara.
1-9-2023 • 0
Nchini Kenya mkutano wa Mabadiliko ya tabianchi utaanza Septemba 4
Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kukutana jijini Nairobi, kenya wiki ijayo kwa ajili ya mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi ambako watajadili njia mbalimbali za kupunguza utoaji wa gesi chafuzi huku wakija na mbinu za kukabiliana na athari za hali ya hewa. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Thelma Mwadzaya. Taarifa ya Thelma Mwadzaya akiwa jijini Nairobi inafafanua zaidi.Mkutano huo unaoanza tarehe 04 mpaka 6 Septemba mwaka huu unawaleta pamoja watunga sera, viongozi wafanyabiashara na wanaharakati wa mazingira kutoka kila pembe ya bara la Afrika. Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya Stephen Jackson akizungumzia mkutano huo ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Muungano wa Afrika na Serikali ya Kenya anaeleza sababu za mkutano huo kufanyikia nchini Kenya. “Kenya ipo mstari wa mbele katika kuathirika na changamoto ya Mabadiliko ya Tabia Nchi, Kenya ipo hatua ya mbele katika kupendekeza suluhu. Hii ni sawa kwa bara la Afrika. Afrika ndilo bara litakalotupa suluhu kuhusiana na tatizo hili la Mabadiliko ya Tabia Nchi. Afrika ina pafu la pili la dunia katika msitu mkubwa nchini Congo wenye hulka ya kuwa na mvua za mara kwa mara. Afrika inautajiri mkubwa wa dunia wa rasilimali za nishati jadidifu. Kenya, ninapofanyia kazi, tayari ipo katika ngazi kubwa ya kutumia asilimia 93 ya nishati ya umeme unozalishwa na nishati jadidifu. Afrika ina sehemu kubwa ya ardhi asilia yenye uwezo wa kuilisha dunia. Kwa sababu hizi zote, Afrika ndiyo mahala panapofaa kupatia suluhu kuhusiana na janga la Mabadiliko ya Tabia Nchi. Na Kenya ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kubadili mitizamo.“Mratibu Mkaazi huyu anaeleza pamoja na kuwa na suluhu lakini Afrika inahitaji ufadhili wa kifedha, “Tunahitaji uwezeshwaji wa kifedha wenye masharti nafuu ili kuliwezesha bara la Afrika kutatua janga la Mabadiliko ya Tabia Nchi linalolikabili bara hili ili pia tutatue tatizo la dunia nzima. Hivi sasa hakuna fedha na ambapo fedha zikikosekana gharama zinakuwa ni za juu sana. Hivyo maono ya Rais Ruto kuhusu Kilele cha Mkutano huu na maono ya Umoja wa Afrika kuhusiana na bara hili kuhusu Mkutano huu wa Bara la Afrika ni kwenda mbali zaidi ya kuangalia ajenda ya upotevu na uharibifu na agenda kuhusiana na uwezeshwaji ili kukabiliana na janga hili la mabadiliko ya `tabia nchi. Ajenda ambazo bado zinabaki kuwa ni za umuhimu sana na na kuangalia ni jinsi gani tutashirikiana kuchanga fedha nyingi kwa Pamoja ili kuleta suluhu za kudumu za afrika katika soko la dunia.”Mkutano huu umeundwa rasmi ili kuongeza kasi ya ushawisi kabla ya viongozi hao kushiriki katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi COP28 huko Dubai baadae mwaka huu.
1-9-2023 • 0
01 SEPTEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mabadiliko ya tabianchi na malelengo ya maendeleo endelevu kupitia mchezo wa mpira wa miguu. Makala tutaelekea nchini DRC kusikia simulizi ya wakimbizi na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania kusikia ni kwa vipi wanawake wameweza kufanya kazi zao na kunyonyesha watoto wao ipasavyo.Viongozi wa Afrika wanatarajiwa kukutana jijini Nairobi, kenya wiki ijayo kwa ajili ya mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi ambako watajadili njia mbalimbali za kupunguza utoaji wa gesi chafuzi huku wakija na mbinu za kukabiliana na athari za hali ya hewa.Mwaka jana 2022 mwezi Julai, katika siku ya kwanza ya Michuano ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Barani Ulaya chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani humo (UEFA Women's EURO 2022), Umoja wa Mataifa uliitumia siku hiyo kuzindua mradi wa ‘Football for the Goals’ yaani Mpira wa Miguu kwa ajili ya Malengo ukiwa ni mpango mpya wa Umoja wa Mataifa ambao unatoa jukwaa kwa jumuiya ya soka duniani kujihusisha na kuhamasisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Nchi ziliitikia na mradi huo unaendelea duniani kote. Makala tunakupeleka nchiniJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikiliza simulizi ya watoto wawili wakimbiziwa ndani juu ya kile wanachopitia sasa, ndotoyao na watamanicho kukipata hivi sasa. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi katikamakala hii iliyofanikishwa na Ofisi ya Umojawa Mataifa ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA nchini DRC.Na mashinani hivi karibuni katika maadhimisho ya wiki wa unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Umoja wa Mataifa ulithirihirisha kwamba kunyonyesha si tu jukumu la mama pekee, bali ni jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha tunaheshimu jitihada za mama kunyonyesha kwa amani, na Lilian Nyachama, mfanyakazi wa kuchuna majani chai kutoka Tanzania anatoa shuhuda.”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
1-9-2023 • 0
Global Youth Forum na UNIS Nairobi watekeleza mradi wa ‘Football for the Goals’ kwa vitendo
Mwaka jana 2022 mwezi Julai, katika siku ya kwanza ya Michuano ya Mpira wa Miguu ya Wanawake Barani Ulaya chini ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani humo (UEFA Women's EURO 2022), Umoja wa Mataifa uliitumia siku hiyo kuzindua mradi wa ‘Football for the Goals’ yaani Mpira wa Miguu kwa ajili ya Malengo ukiwa ni mpango mpya wa Umoja wa Mataifa ambao unatoa jukwaa kwa jumuiya ya soka duniani kujihusisha na kuhamasisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Nchi ziliitikia na mradi huo unaendelea duniani kote. Peter Omondi kutoka shirika la vijana la Global Youth Forum nchini Kenya ni mmoja wa vijana ambao mapema mwezi huu kwa kushirikiana na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIS Nairobi waliandaa mechi ya mpira wa miguu iliyohusisha zaidi ya vijana 100 katika Kaunti ya Siaya ili kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu. Omondi Peter akihojiwa na Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi Kenya anaeleza ushiriki wao katika mradi huu akisema, “Kulingana na ripoti, mambo ya Malengo ya Maendeleo Endelevu yanafaa yazingatiwe kila mahali kuhakikisha kila mtu katika ulimwengu anajumuika katika kuendeleza hii miradi ya SDGs.” “Huu mradi (Mpira wa Miguu kwa ajili ya Malengo) ,” Kijana huyo kutoka shirika la vijana la Global Youth Forum nchini Kenya anaendelea kueleza, “inahakikisha kujumuisha wachezaji wote katika michezo ya mpira, kuwa pamoja, na kuunganisha vijana wote, wazee na akina mama kuja pamoja.” Omondi Akieleza kitu kilichomfurahisha anasema ni watu kuja pamoja na hii michezo kuandaliwa katika miji iliyoko ndani au pembezoni na hivyo watu wa vijijini kushiriki katika mazungumzo ya Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu. “Kama kijana ningependa kuhamasisha vijana wenzangu pale nyumbani na katika maeneo ya ndani kwenye jamii waendelee kujumuika kwa ajili ya SDGs. Hiyo yote itahakikisha kwamba hakuna aliyeachwa nyuma katika haya mazungumzo ya Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu.” Anahitimisha kijana Omondi Peter.
1-9-2023 • 0
Methali: “Lakesho huonekana leo ila la jana halipingi la leo.”
Hii leo katika kujifunza Lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “La kesho huonekana leo ila la jana halipingi la leo.”
31-8-2023 • 0
31 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo mradi wa msaada wa maendeleo ya biashara ndogo-ndogo na za kati wa Benki ya Dunia, unaoendeshwa na mshirika wake, shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women, unaaminika kuleta manufaa mengi katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo Siku ya Kimataifa ya Watu wa Asili ya Afrika na afya nchini Yemen. Katika kujifunza Lugha ya Kiswahili, Dkt. Josephat Gitonga anafafanua maana ya methali “Lakesho huonekana leo ila la jana halipingi la leo.”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Watu wa Asili ya Afrika inayoadhimishwa leo amehimiza Mataifa kuchukua hatua madhubuti, kwa ushirikishwaji kamili wa watu wa asili ya Afrika na jamii zao, kukabiliana na aina za zamani na mpya za ubaguzi wa rangi; na kuondoa ubaguzi wa rangi wa kimuundo na kitaasisi uliokita mizizi na kupaza sauti bila kuchoka dhidi ya mawazo yote ya ubora wa rangi ili kukomboa jamii zote kutoka kwenye balaa la ubaguzi wa rangi.” Wakati huo huo, Mshauri Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kupinga ubaguzi pahala pa kazi, Mojankunyane Gumbi akizungumza kuhusu siku hii ya Kimataifa ya Watu wa Asili ya Afrika amesema Timu ya kupinga Ubaguzi inapenda kutambua michango ya waafrika walioko ughaibuni. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeeleza leo wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa surua na rubela miongoni mwa watoto nchini Yemen. Hadi kufikia tarehe 31 mwei jana, Julai, mwaka huu, idadi ya wanaoshukiwa kuwa na surua na rubela nchini Yemen imefikia karibu watu 34,300 na vifo 413, ikilinganishwa na wagonjwa 27,000 na vifo 220 vilivyohusishwa na magonjwa hayo mwaka 2022.Katika kujifunza Lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Lakesho huonekana leo ila la jana halipingi la leo.”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
31-8-2023 • 0
Watoto Kakuma wafikishiwa msaada wa kuwanusuru na utapiamlo
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF nchini Kenya linatekeleza mradi wa matibabu kwa watoto wenye utapiamlo, mradi ambao umeanza kuzaa matunda kwani afya za watoto zimeanza kuimarika. Leah Mushi na taarifa zaidi.Sabina Naboi mwenye umri wa miaka 28 mama wa watoto watatu, alizaliwa ndani ya kambi ya Kakuma iliyoko katika kaunti ya Turkana nchini Kenya.Misimu sita mfululizo ya ukame uliochochewa na mabadiliko ya tabianchi umekuwa na athari hasi hususan kwenye suala la lishe kwa watu wengi katika kaunti hii ya Turkana na mmoja wao ni Sabina ambaye mtoto wake mwenye umri chini ya miaka mitano alipata utapiamlo.Changamoto alizopitia SabinaSabina anasema,“sisi tunategemea chakula hiki cha msaada wa wakimbizi ambacho tunakipata mara moja kwa mwezi na huwa hatuwezi kufika nacho mwisho wa mwezi mwingine. Wakati nimejifungua binti yangu analia alikuwa sawa lakini alipofika miezi sita akaanza kuumwaumwa mara kuharisha yani afya yake haikuwa sawa. Nilikuwa nampeleka hospitali anapewa dawa lakini mtoto alikuwa anakonda sana.”Mtoto wa Sabina aligundulika kuwa na utapiamlo na hivyo akapewa lishe maalum kwa ajili ya watoto wenye utapiamlo.Vicent Opinya ni meneja wa programu ya afya katika kambi ya Kakuma anasema, “tunahudumia takribani watu 246,000 ambapo wahudumu wetu wa afya wanawapatia matibabu ya chakula maalum kilicho tayari kwa ajili ya kutibu watoto walio na utapiamlo mkali bila shida nyingine yoyote katika vituo vyetu vya wagonjwa wanje.”Mgao wa fedha taslimu, lishe na huduma ya matibabuChini ya ufadhili wa Muungano wa Ulaya UNICEF na wadau wake wanatoa lishe, msaada wa fedha taslimu na matibabu kwa watoto wenye upatiamlo waliochini ya umri wa miaka mitano kwa wakazi wa Kalobeyei pamoja na Kambi ya wakimbizi ya Kakuma. Kwa sasa watoto zaidi ya 22,000 wamefikiwa na misaada hiyo ya kuokoa maisha.Susan Jobando ni Afisa afya wa UNICEF nchini Kenya na anasema mbali na kusaidia serikali ya Kaunti ya kakuma katika masuala ya afya kwa watoto pia wanawajengea uwezo wahudumu wa afya na kuimarisha mfumo wa afya na kuhakikisha kuna mnyororo thabiti wa usambazaji matibabu ya utapiamlo kuweza kumfikia kila mtoto mwenye uhitaji.’Tukiwa na wadau kama ECHO tunaweza kuwafikia watoto wengi zaidi sio tu kama mkakati wa matibabu bali pia ni mkakati wa kujikinga ili waweze kukabiliana vyema na athari za mabadiliko ya tabianchi.”Tabasamu sasa kwa SabinaSasa Sabina ana furaha kwa kuwa mtoto wake ameanza kupata nafuu na anasema, “vile ninaona afya yake iko sawa hata mimi hufurahi. Na ninaamini mwezi ujao mwili wake utarudi kama zamani (atanenepa) na utaendelea kuongezeka mpaka atoke kwenye hiyo programu ( ya kula chakula cha watoto wenye utapiamlo) na aende kwenye programu nyingine . Kila mama anataka mtoto wake awe na afya nzuri, awe na mwili mzuri.”
30-8-2023 • 0
Msaada kutoka TANZBATT 10 umenusuru wagonjwa wanaokabiliwa na njaa
Mgeni njoo mwenyeji apone ni methali iliyodhihirisha huko eneo la Mbau jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC baada ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania kikosi cha 10, TANZBATT 10 walipotembelea hospitali ya La Grace kutoa msaada si tu wa chakula bali pia dawa. Walinda amani hawa wanahudumu kwenye kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO. Mwenyeji wetu ni Afisa Habari wa TANZBATT 10, Luteni Abubakari Muna ambapo katika makala hii Meja Neema Neligwa mwakilishi wa Kamanda kikosi cha TANZBATT 10, Luteni Kanali John Peter Kalabaka anaanza kwa kufafanua kilichojiri kwenye ziara hiyo.
30-8-2023 • 0
Wataalamu wa haki waongeza sauti kwenye suala la utoweshwaji wa watu
Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa na wa kanda mbalimbali ikiwemo Afrika na Asia wameyasihi mataifa yote kutoa haki kwa waathirika wa utoweshwaji wa watu, ikiwa ni pamoja na mtu yeyote ambaye amepata madhara kama matokeo ya moja kwa moja ya utoweshwaji wa watu. Anold Kayanda na maelezo zaidi. "Kuhakikisha haki ya waathiriwa kunahitaji kuchukua hatua zote muhimu ili kufichua ukweli," wataalam hao wamesema katika taarifa walioitoa jana mjini Geneva, Uswisi kuelekea leo ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Waathiriwa wa Kutoweshwa kwa watu. Wataalamu hao wanasema kwamba kuhakikisha upatikanaji wa kutosha wa haki na uwajibikaji ipasavyo kwa wahalifu katika ngazi zote za mnyororo mzima wa amri ni muhimu ili kuwasilisha ujumbe mzito kwamba kutowesha watu ni uhalifu chini ya sheria ya kimataifa ya haki za binadamu, hairuhusiwi au kuvumiliwa. Kwa mujibu wa Azimio la Ulinzi wa Watu Wote dhidi ya Kutoweshwa kwa Watu, lililotangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika azimio lake la 47/133 la tarehe 18 Desemba 1992 kutoweshwa ni pindi "Watu wanakamatwa, kuwekwa kizuizini au kutekwa nyara bila hiari yao au kunyimwa uhuru wao kwa njia nyingine na maafisa wa matawi au ngazi mbalimbali za Serikali, au na makundi yaliyopangwa au watu binafsi kwa niaba ya, au kwa msaada, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, ridhaa au kukubaliana na Serikali, ikifuatiwa na kukataa kufichua hatima au mahali walipo watu waliokamatwa au kukataa kukiri kunyimwa uhuru wao, jambo ambalo linawaweka watu hao nje ya ulinzi wa sheria." Wataalamu wa haki za binadamu wanasema "Katika mapambano yao ya kila siku ya haki, waathiriwa mara nyingi wanakabiliwa na vitisho, kisasi na unyanyapaa. Hili lazima likomeshwe, na waathiriwa lazima wapate msaada wa kisheria bila malipo ili kuhakikisha kuwa hali yao ya kifedha haiwazuii kutafuta haki na upatikanaji wa haki lazima usiwe wa kinadharia tu bali uhakikishwe kivitendo kupitia hatua madhubuti zinazokuza na kuthamini kikamilifu ushiriki wa kweli na wa maana wa waathiriwa na wawakilishi wao katika mchakato wote."
30-8-2023 • 0
30 AGOSTI 2023
Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo miongoni mwa utakayoyasikia ni pamoja na Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa na wa kanda mbalimbali ikiwemo Afrika na Asia wameyasihi mataifa yote kutoa haki kwa waathirika wa utoweshwaji wa watu, ikiwa ni pamoja na mtu yeyote ambaye amepata madhara kama matokeo ya moja kwa moja ya utoweshwaji wa watu. Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya watoto UNICEF nchini Kenya linatekeleza mradi wa matibabu kwa watoto wenye utapiamlo ambao umeanza kuzaa matunda kwa afya za watoto kuimarika. Makala hii leo inatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 10 wanaohudumu kwenye ujumbe wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wametembelea wagonjwa katika hospitali ya La Grace iliyoko Mbau jimboni Kivu Kaskazini. Na katika mashinani ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya watu kutoweshwa tunakwenda SriLanka kusikia changamoto anazopitia Jeyatheepa Ponniyamoorthi ambaye mumewe alitoweshwa mwaka 2009 na kumuacha na mtoto wao wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu na sasa mtoto huyo ana umri wa miaka 14.
30-8-2023 • 0
29 AGOSTI 2023
Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo leo tunamulika kilimo cha parachini na jinsi kinavyo changia kutekeleza malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo endelevu hususan la kutokomeza umaskini. Pia utasikia habari kwa ufupi kuhusu matumizi ya silaha za nyuklia, hali ya usalama nchini Niger na haki za binadamu nchini Ethiopia. Mashinani hii leo utamsikilia Luteni Kanali Kevin Byabato, Msemaji wa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO akieleza jinsi ushirikiano kati ya MONUSCO na jeshi la serikali FARDC umezaa matunda kwani katika siku 15 za hivi karibuni waliweza kuzuia mashambulizi matano toka kwa waasi wa ADF jimboni Ituri na Kivu Kaskazini.
29-8-2023 • 0
Walinda amani wanaondoka Mali lakini Umoja wa Mataifa unabakia
Baada ya kuweko nchini Mali kwa muongo mmoja, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani na kuweka utulivu nchini humo umeanza kufunga virago. Hii ni baada ya mamlaka nchini humo kutaka ujumbe huo uondoke, ombi ambalo liliridhiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Sasa MINUSMA inatakiwa iwe imeondoka ifikapo tarehe 31 mwezi Agosti mwaka huu. Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Mali, El-Ghassim Wane ambaye pia ni Mkuu wa MINUSMA amezungumza na Jerome Bernard wa Idhaa ya Kifaransa ya Umoja wa Mataifa, mazungmzo ambayo ndio msingi wa makala hii inayoletwa kwako na Assumpta Massoi.
28-8-2023 • 0
Botswana: Mkutano wa 73 wa Kamati ya Kanda ya Afrika ya WHO waanza Gaborone
Mkutano wa Sabini na tatu wa Kamati ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) umeanza hii leo katika mji mkuu wa Botswana, Gaborone huku tukio hilo likishuhudia pia Maabara ya Kitaifa ya Marejeleo ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ya Botswana ikipewa hadhi ya kuwa Kituo Kishiriki cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) cha kufuatilia Ubora. Mkutano huu utakaoendelea hadi tarehe Mosi ya mwezi ujao Septemba unawakutanisha Mawaziri wa afya wa Afrika na wawakilishi wa serikali pamoja na wadau wengine wa sekta ya afya kutoka kote barani Afrika ili kujadili na kukubaliana kuhusu hatua muhimu za kushughulikia changamoto za afya za kanda ya Afrika, kuendeleza na kukuza afya bora na ustawi wa watu. Na kuhusu Maabara ya Kitaifa ya Botswana kuwa Kituo Kishiriki cha Ubora cha WHO, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza asubuhi ya leo ya Botswana baada ya yeye na Rais Dkt Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi wa Botswana kutia saini makubaliano amesema,"WHO inajivunia kuhesabu maabara hii kama Kituo cha Kushirikiana na inatarajia kufanya kazi pamoja kwa karibu zaidi katika kutoa msaada na huduma zinazohitajika kwa watu wanaoishi na VVU." Kwa upande wake Rais Masisi wa Botswana amesema kuteuliwa kwa maabara hii kama Kituo Kishiriki cha Ubora cha WHO kunaipa nchi ya Botswana imani kwamba wako kwenye njia sahihi ya kufikia lengo la WHO la mwaka 2030 la kudhibiti Virusi Vya Ukimwi (VVU). Wengine walioko nchini Botswana kuhudhuria Mkutano huo unaofanyika kwa njia ya ana kwa ana na mtandaoni ni Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti ambaye kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano huu, anatarajiwa kutoa taarifa kuhusu hali ya afya barani Afrika.
28-8-2023 • 0
Baada ya uchaguzi mkuu Zimbabwe Guterres aomba amani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema anafuatilia kwa karibu kinachoendelea kwenye mchakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Zimbabwe tarehe 23 mwezi huu wa Agosti. Taarifa iliyotolewa Jumapili jioni na ofisi ya msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inasema Katibu Mkuu Guterres katika ufuatiliaji wa kinachoendelea nchini humo, hofu yake kubwa ni ripoti za kukamatwa kwa waangalizi wa uchaguzi, vitisho dhidi ya wapiga kura, vitisho vya ghasia, halikadhalika manyanyaso na matumizi ya nguvu. Hofu ya Guterres inakuja wakati ambapo tayari vyombo vya habari vinaripoti kuwa Rais wa sasa Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa ameibuka na ushindi kwenye kinyang’anyiro cha urais kilichokuwa kinawaniwa na wagombea 11. Katibu Mkuu ametoa wito kwa viongozi wa kisiasa na wafuasi wao kuepuka aina yoyote ya ghasia au kuchochea ghasia, na badala yake wahakikishe haki za binadamu na utawala wa sheria vinaheshimiwa. Ametoa wito pia kwa washiriki wote kwenye siasa kutatua mizozano yoyote ile kupitia njia za kisheria na taasisi zilizowekwa kwa ajili hiyo. Bwana Guterres amezitaka taasisi husika zitatue migogoro yoyote itakayoibuka kwa njia ya haki, uwazi na haraka ili kuhakikisha matokeo ya uchaguzi huo yanaakisi utashi wa wananchi wa Zimbabwe. Vyombo vya habari vinaripoti kuwa wagombea kutoka upinzani wamekataa matokeo ya uchaguzi yaliyompatia ushindi Rais Mnangagwa kwa asilimia 52.6, matokeo yaliyotangazwa Jumamosi na Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe. Bwana Mnangagwa aliingia madarakani kufuatia uchaguzi wa mwaka 2018.
28-8-2023 • 0
28 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani jaridani tunaangazia hali ya usalama nchini Zimbabwe baada ya uchaguzi na masuala ya afya nchini Botswana. Makala tunakupeleka nchini Mali na mashinani nchini Rwanda, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema anafuatilia kwa karibu kinachoendelea kwenye mchakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Zimbabwe tarehe 23 mwezi huu wa AgostiMkutano wa Sabini na tatu wa Kamati ya Kanda ya Afrika ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) umeanza hii leo katika mji mkuu wa Botswana, Gaborone huku tukio hilo likishuhudia pia Maabara ya Kitaifa ya Marejeleo ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ya Botswana ikipewa hadhi ya kuwa Kituo Kishiriki cha Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) cha kufuatilia Ubora. Katika makala Assumpta Massoi anamulika harakati za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Mali, MINUSMA kuwa umeondoka nchini humo ifikapo tarehe 31 mwezi Desemba mwaka huu kufuatia ombi la mamlaka nchini Mali.Mashinani tunakupeleka nchini Rwanda kusikia ni kwa jinsi gani wazazi wameweza kutokomeza udumavu na kuhakikisha afya njema kwa watoto wao.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
28-8-2023 • 0
Wakati wa mafuriko nilipoteza mtoto, na sasa sina uhakika nitakayejifungua ataishi- Mkazi Pakistani
Mwaka mmoja tangu mafuriko ya kihistoria yakumbe Pakistani, na hali ya dharura nchini humo kutangazwa, mamilioni ya watoto bado wanaendelea kuhitaji misaada ya dharura huku operesheni za ukarabati zikisalia kukumbwa na ukata kwani fedha zinazotakiwa hazijapatikana. Hii leo katika Makala Assumpta Massoi anakupeleka Pakistani kusikia waathirika na kumbukumbu za hali ilivyokuwa, shaka na shuku zao hivi sasa na nini Umoja wa Mataifa unafanya kuleta angalau ahueni.
25-8-2023 • 0
Griffiths: Vita na njaa vinaweza kusambaratisha Sudan
Vita inayoendelea nchini Sudan inachochea dharura kubwa ya kibinadamu ambapo vita na njaa, magonjwa na watu kufurushwa makwao vilivyofuatia sasa inatishia ‘kutafuna’ nchi nzima, amesema Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Martin Griffiths. Taarifa iliyotolewa na OCHA hii leo jijini New York, Marekani imemnukuu mkuu wa ofisi hiyo Martin Griffiths akisema kuwa mapigano makali yaliyoanzia mji mkuu wa Sudan, Khartoum na jimbo la Darfur katikati ya mwezi Aprili mwaka huu yamesambaa hadi Kordofan. Amesema katika mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kusini, Kadugli hifadhi ya vyakula imekwisha kwa kuwa mapigano na vizuizi njiani vinasababisha wahudumu wa misaada washindwe kufikia wenye njaa. Huko El Fula, mji mkuu wa jimbo la Kordofan Magharibi, ofisi za watoa misaada zimevamiwa na misaada imeporwa. Bwana Griffiths amesema hofu yake sasa ni usalama wa raia kwenye jimbo la Al Jazira wakati huu ambapo mzozo huo unasogelea eneo hilo tegemewa kwa uzalishaji wa chakula Sudan. Mkuu huyo wa OCHA amesema kadri mapigano yanavyoendelea, vivyo hivyo madhara yanayongezeka. Mamia ya maelfu ya watoto wana utapiamlo uliokithiri na wako hatarini kufa iwapo hawatapata tiba. Magonywa ya kuambukizwa kwa vimelea kama vile Malaria, Kifaduro, Kidingapopo yanasambaa nchi nzima na yanatishia uhai kwa wale wenye waliodhoofishwa tayari na utapiamlo. Wagongwa hao hawawezi kupata matibabu kwani mapigano yamesambaratisha mfumo wa afya. Bwana Griffiths amesema vita ya muda mrefu itapoteza kizazi cha watoto kwani mamilioni hawaendi shuleni, na watakumbwa na kiwewe na kusalia na kovu la vita katika maisha yao. Amesema ripoti za kwamba watoto wanatumika pia kwenye mapigaon ni za kuchukiza. Mkuu huyo wa OCHA ametaka pande kinzani kuweka mbele maslahi ya wananchi Sudan badala ya uroho wao wa madaraka, watoa misaada wapatiwe ruhusa ya kufikisha mahitaji na zaidi ya yote jamii ya kimataifa ipatie janga la Sudan udharura unaohitajika.
25-8-2023 • 0
25 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani jaridani tunaangazia haki za binadamu nchini Sudan na utaifa wa Wapemba nchini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Pakistan na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Vita inayoendelea nchini Sudan inachochea dharura kubwa ya kibinadamu ambapo vita na njaa, magonjwa na watu kufurushwa makwao vilivyofuatia sasa inatishia ‘kutafuna’ nchi nzima, amesema Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Martin GriffithsMwishoni mwa mwezi uliopita Rais wa Kenya William Ruto akiwa Kilifi mashariki mwa Kenya alitangaza kutambulika rasmi kwa jamii ya Wapemba ambao kwa miaka mingi waliishi nchini humo wakikosa hadhi ya utaifa kwa kuwa vizazi vyao vya nyuma vilitoka nje ya Kenya. Makala tunakwenda Pakistani ambako leo ni mwaka mmoja tangu mafuriko makubwa yaliyozua zahma nchini humo.Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania kushuhudia jinsi ambavyo ukulima wa mboga mboga na matunda unavyosaidia wanawake kupatia jamii zao mapato thabiti na kuwapeleka watoto wao shuleni.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
25-8-2023 • 0
Mdau wa UNHCR Haki center, moja ya mashirika yaliyosaidia Wapemba kutambulika rasmi Kenya
Mwishoni mwa mwezi uliopita Rais wa Kenya William Ruto akiwa Kilifi mashariki mwa Kenya alitangaza kutambulika rasmi kwa jamii ya Wapemba ambao kwa miaka mingi waliishi nchini humo wakikosa hadhi ya utaifa kwa kuwa vizazi vyao vya nyuma vilitoka nje ya Kenya. Nyuma ya mafanikio haya zimekuwepo harakati za muda mrefu za kuitafuta haki hiyo zikifanywa na wananchi na mashirika yasiyo ya kiserikali. Moja ya mashirika hayo ni Haki Center ambalo ni mdau wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) katika eneo la pwani na kaskazinimashariki mwa Kenya. Barke Hamisi kutoka jamii ya wapemba anatambua mchango wa shirika hili na anakumbuka hali ilivyokuwa kabla ya hatua ya juzi ya kutambulika,“Mimi nimezaliwa hapa watamu na nikalelewa hapa watamu na pia nilisoma shule ya msingi watamu. Nilikuwa najumuika vizuri na jamii zingine lakini shida ilikuwa ni mtu anakwambia wewe ni mpemba. Sasa mtu akikuambia wewe ni mpemba, hiyo ni kama mtu amekudunga mkuki. Unakosa morali (ari).” Na ni kwa vipi basi shirika la Haki Center lilichangia harakati hizi? Barke anaeleza, “Haki Center ilikuwa na mchango mkubwa katika utetezi wetu kwa sababu walituwezesha sana kutojificha tena kupigania haki yetu kupitia msaada wao, ndipo tuliposhirikiana na wabunge na kutoka kwenye mazungumzo na majadiliano tuliyokuwa nayo pamoja nao tuliandika ombi.”
25-8-2023 • 0
Methali - Mnywa Maji kwa Mkono Mmoja Kiu yake I pale pale
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA nchini Tanzania anachambua methali, "Mnywa Maji kwa Mkono Mmoja Kiu yake I pale pale."
24-8-2023 • 0
Wanawake wapatiwe nafasi katika sayansi na teknolojia, watasongesha agenda 2030- Mwanaisha Ulenge
Ikiwa imesalia takribani miaka 6 ushehe kufika mwaka 2030 muda ambao ulimwengu ulijiwekea lengo la kuwa umetimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), mapema mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiamini wanawake wanasayansi wana uwezo wa kuchangia haraka katika maendeleo ya ulimwengu, alieleza namna kuwanyima fursa za sayansi wanawake kunarudisha maendeleo nyuma na hivyo akashauri wanawake wanasayansi wapewe nafasi kuanzia darasani, maabara na katika vyumba vya maamuzi.Mwanaisha Ulenge ni Mwanamke Mwanasayansi Mhandisi, Mbunge nchini Tanzania vilevile Mjumbe wa Shirikisho la Mabunge Duniani (IPU) na hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa nilipata fursa ya kujadiliana naye kuhusu nafasi ya mwanamke katika sayansi na teknolojia.
24-8-2023 • 0
24 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na Mwanaisha Ulenge ni Mwanamke Mwanasayansi Mhandisi, Mbunge nchini Tanzania vilevile Mjumbe wa Shirikisho la Mabunge Duniani (IPU) na hivi karibuni akiwa katika ziara ya kikazi hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa Anold Kayanda alipata fursa ya kujadiliana naye kuhusu nafasi ya mwanamke katika sayansi na teknolojia. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ziara za Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa nchini Afrika Kusini, kazi za umoja wa mataifa nchini Sudan na hali ya kibinadamu ya wakimbizi wa Rohingya baada ya miaka 6 ya kukimbia makazi yao nchini Myanmar. Katika kujifunza Kiswahili Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA nchini Tanzania anachambua methali “Mnywa Maji kwa Mkono Mmoja Kiu yake I pale pale”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amehutubia mkutano wa viongozi kundi la Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini au BRICS huko Johannesburg Afrika Kusini na kusema katika dunia ya sasa iliyogawanyika na kugubikwa na majanga hakuna mbadala mwingine wa kuwezesha kusonga mbele zaidi ya mshikamano hasa kwenye masuala lukuki ikiwemo marekebisho ya mfumo wa kimataifa wa fedha duniani.Ikiwa kesho ni miaka 6 tangu serikali ya kijeshi nchini Myanmar ianze msako wa kufurusha waislamu wa kabila la Rohingya kutoka jimbo la Rakhine nchini humo, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Volker Türk amesema jamii ya kimataifa isisahau warohingya na wale wanaowahifadhi, na zaidi ya yote juhudi za kimataifa ziongezwe maradufu ili wahusika wawajibishwe. Na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linaonya kuwa bila amani nchini Sudan, hatma ya watoto iko mashakani wakati huu ambapo zaidi ya watoto milioni 2 wamefurushwa makwao tangu mapigano yaanze kwenye mji mkuu Khartoum mwezi Aprili mwaka huu na sasa mapigano hayo yanaenea kwenye maeneo mapya.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA nchini Tanzania anachambua methali Mnywa Maji kwa Mkono Mmoja Kiu yake I pale pale.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
24-8-2023 • 0
UNEP: Majitaka yawe jawabu la changamoto ya maji na tabianchi duniani
Maadhimisho ya Wiki ya Maji yakiendelea huko Stockholm nchini Sweden, shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira duniani, (UNEP) leo limezindua ripoti yenye lengo la kugeuza majitaka kuwa jawabu la uhaba wa maji na changamoto ya tabianchi duniani.UNEP kupitia taarifa yake iliyotolewa leo Nairobi nchini Kenya inasema majitaka yanaendelea kuwa tishio la afya na mazingira yakichangia utoaji wa hewa chafuzi kama ilivyo sekta ya anga. Hata hivyo ripoti hiyo inasema kwa kutunga será sahihi, majitaka yanaweza kuwa chanzo mbadala cha nishati kwa watu nusu bilioni duniani na kusambaza mara 10 zaidi ya maji ya baharini yanayotolewa chumvi kwa matumizi ya binadamu na wakati huo huo kuepusha zaidi ya asilimia 10 ya matumizi ya mbolea duniani. Ripoti hiyo ikipatiwa jina Majitaka. Kubadili tatizo kuwa jawabu, imeandaliwa na UNEP kwa ushirikiano na taasisi ya GRID-Arendal na Mpango wa Kimataifa kuhusu majitajika, (GWWI) na inazisihi serikali na sekta ya biashara kutumia tena na tena majitaka kama fursa ya kiuchumi, badala ya kuyageuza kuwa tatizo la kuondokana nalo. Faida za kukusanya, kusafisha na kutumia tena na tena maji hayo ni lukuki, kwa mujibu wa ripoti hiyo, ikiwemo fursa mpya za ajira na vyanzo vipya vya mapato, halikadhalika kupunguza kiwango cha majitaka yanayozalishwa. Leo hii ni asilimia 11 tu ya majitaka duniani kote ndio yanatumika ten ana tena na takribani nusu ya majitaka yasiyosafishwa yanaingia kwenye mito, maziwa na bahari. Akizungumzia ripoti hiyo, Leticia Carvalho kutoka UNEP anasema duniani kote, majitaka yana fursa kubwa lakini kwa sasa yanaachiwa yachafue mfumo anuai tunaotegemea. Tusipoteze fursa hii: ni wakati wa kutimiza ahadi ya majitaka kuwa chanzo mbadala cha maji safi, nishati na virutubisho muhimu.”
23-8-2023 • 0
23 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia wiki ya maji na kazi ya Umoja wa mataifa katika utoaji wa huduma za maji. Makala tunakuletea uchambuzi wa Ibara ya 8 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na mashinani tunakupeleka jijini Mbeya nchini Tanzania, kulikoni? Maadhimisho ya Wiki ya Maji yakiendelea huko Stockholm nchini Sweden, shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira duniani, (UNEP) leo limezindua ripoti yenye lengo la kugeuza majitaka kuwa jawabu la uhaba wa maji na changamoto ya tabianchi dunianiTukiwa bado katika Wiki ya Maji ambayo imeanza tarehe 20 na itaendelea hadi kesho tarehe 24, TANBAT 6 ambacho ni Kikosi cha sita cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), kwa kutumia magari wametoa msaada wa maji safi na salama kwa wanawake wa vijiji vinavyokabiliwa na uhaba wa maji mjini Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï. Hii leo katika makala tunakuletea uchambuzi wa Ibara ya 8 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu. Makala hii iliyoandaliwa na Grace Kaneiya ni marejeo na ilirushwa tarehe 12 Novemba 2018. Grace Kaneiya alizungumza na Robi Chacha akiwa Afisa Kampeni usalama na Haki za binadamu Amnesty International nchini Kenya. Ibara inasema kila mtu ana haki ya kupata msaada wa kisheria na kutumia mfumo wa kisheria iwapo haki zake haziheshimiwi.Na mashinani tunakupeleka jijini Mbeya nchini Tanzania ambako ujenzi wa vyoo na vituo vya maji ambavyo ni muhimu kwa afya na ustawi wa watoto vimewezesha wanafunzi kunawa mikono na kunywa maji safi na salama.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
23-8-2023 • 0
Walinda amani kutoka Tanzania TANBAT6 watoa huduma ya maji kwa wanakijiji nchini CAR
Tukiwa bado katika Wiki ya Maji ambayo imeanza tarehe 20 na itaendelea hadi kesho tarehe 24, TANBAT 6 ambacho ni Kikosi cha sita cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA), kwa kutumia magari wametoa msaada wa maji safi na salama kwa wanawake wa vijiji vinavyokabiliwa na uhaba wa maji mjini Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï. Siku ya leo ni shangwe isiyo na kifani kwa wananchi wa kijiji cha Bisa na kijiji cha Diforo vilichopo mkoani Mambéré-Kadéï kusini magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR. Ni baada ya kikosi cha TANZBAT 6 kutoa msaada wa kuwagawia maji waliyobeba kwenye magari yao maalum hasa msaada ukiwaalenga wanawake na watoto ambao ndio waathirika wakubwa kwenye tatizo hilo.Bi. Yakele Stella mmoja wa wanawake wanufaika wa msaada huu wa maji ametoa shukrani kwa walinda amani hawa wa Umoja wa Mataifa akisema, "Mimi kama mama nimefurahi sana leo kwa msaada wa kupewa maji maana sisi akinamama tunakwenda mbali kuchota maji lakini pia maji hayo si maji salama. Lakini leo hii walinda amani hawa kutoka Tanzania wanazidi kutusaidia jamii zetu kwa kutupatia maji safi na salama."Mwingine aliyetoa shukrani kwa niaba ya wananchi wengine ni chifu wa eneo la Difolo Bwana Mamadour Soh Papy, "Tunashukuru sana kwa walinda amani kutoka Tanzania kwa jinsi walivyoamua kutupa msaada wa maji safi hapa nyumbani maana hatuna maji safi hapa kwetu. Huwa tunapata maji ya bomba mara mbili tu kwa wiki na huwa tunanunua. Watu tunakuwa wengi sana, wanasukumana mpaka kuumia. Lakini leo tunajisikia amani kupata maji bila fujo yeyote. Mungu awabariki walinda amani wa Tanzania kwa upendo wao wanaouonyesha hapa kwetu."Aidha TANBAT 6 sabamba na wiki hii ya maji, wanautumia wakati huu kusaidia jamii za hapa CAR ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuelekea kuadhimisha miaka mitano tangu kuundwa kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Shughuli nyingine zinazotarajiwa kufanyika kwenye jamii katika kuelekea wiki hii ya maadhimisho ya kuundwa kwa JWTZ ni pamoja na kutoa elimu ya ujasiliamali Kwa vikundi mbalimbali na matibabu kwenye zahanati zilizopo karibu na kikosi hicho.
23-8-2023 • 0
22 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Mapigano yanayoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC yakiendeshwa na vikundi vilivyojihami vya waasi yanaendelea kufurusha watu kutoka makwao, na hivyo wakimbizi hao wa ndani kushindwa kujikimu maisha yao ya kila siku. Malazi ni shida, makazi ni shida, halikadhalika chakula. Maisha yanakuwa ni changamoto kila uchao. Hali hiyo iko dhahiri kabisa jimboni Kivu Kaskazini ambako hata hivyo hatua za shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula duniani, WFP kwa wakimbizi Oicha zimeleta ahueni. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za msaada wa kibinadumu, malaria na maji. Mashinani tunakwenda Tanzania hususan mkoani Kilimanjaro.Mamilioni ya watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wako hatarini kukumbwa na njaa huku ufadhili ukiwa katika hali mbali ametahadharisha leo Peter Musoko ambaye ni Mkurugenzi wa Nchi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP) nchini DRC alipozungumza leo na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi. Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Kőrösi amehutubia mkutano wa Wiki ya Maji huko Stockholm nchini Sweden na kutaka mabadiliko makubwa ya hatua za kufanikisha upatikanaji wa maji duniani akisema kwa kasi ya sasa muda uliosalia hautawezesha kufanikisha lengo la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu maji.Na Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) umetangaza Mbinu Mpya ya Kuongeza Upatikanaji wa Vyandarua Vizuri Zaidi ili Kuzuia Malaria. Na mashinai Anna Assey, mkulima kutoka mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania akielezea ni kwa vipi yeye anahifadhi mbegu za kiasili wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa unasisitiza matumizi ya mbinu za kiasili kama njia ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
22-8-2023 • 0
Lebanon - Mabomu yateguliwa na kuwezesha wamiliki kurejea kwenye ardhi baada ya kutelekeza miaka ya 1970
Huko nchini Lebanon, Mashariki ya Kati, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNIFIL kwa ushirikiano na wadau wameteketeza mabomu 4,000 yaliyokuwa yametegwa kwenye eneo la ukubwa wa mita 44,000 za mraba na hivyo kuwezesha ianze kutumika tena kwa kilimo baada ya kushindikana tangu miaka ya 1970 kwa hofu ya milipuko ya mabomu.Ni katika eneo la Mess el Jebal, kusini mwa Lebanon eneo hili la ukubwa wa meta 44,000 za mraba ni kichaka lakini salama. Wamiliki wa eneo hili wamerejea bila hofu ya kulipukiwa na mabomu na mmojawao ni Jaffar Ghadban, “Zamani miaka ya 70 mababu zetu walikuwa wanalima hapa na zao kuu kwenye eneo hili lilikuwa kunde. Jeshi la Lebanon, walinda amani wa UNIFIL [YUNIFIL] kutoka Cambodia wamesafisha ardhi kwa kutegua mabomu.Tumekuja leo hapa kumiliki tena ardhi yetu. Mungu akipenda tutaanza kulima tena kama walivyofanya watangulizi wetu. Tutarejesha upya eneo hili liwe bora kuliko zamani.” Luteni Kanali Zang Dongjie, Mkuu wa kitengo cha uhandisi UNIFIL anasema mabomu 4,000 ya kutegwa ardhini yaliteketezwa hivyo “sasa naweza kuthibitisha kuwa eneo hili ni salama kwa kilimo.” Kazi hii iliyoendeshwa kwa ushirikiano katiya UNIFIL, ofisi ya Umoja wa Mataifa ya hatua dhidi ya mabomu, UNMAS na Kituo cha Lebanon cha hatua dhidi ya mabomu, LMAC haikuwa rahisi kwani wakati wa operesheni mteguaji mmoja wa mabomu alifariki dunia. Julie Mayers, Mkuu wa Programu ya uteguaji mabomu, UNIFIL anatamatisha akisema baada ya miaka miwili ya kutegua mabomu kwenye maeneo 10 sasa wana furaha kwamba “kilichofanyika kina uhusiano moja kwa moja na dira ya kituo cha Lebanon cha hatua dhidi ya mabomu ya ardhini ya kuona jamii inastawi na kuondokana na tishio la vilipuzi.”
21-8-2023 • 0
Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi Waathirika wa Ugaidi
Ikiwa leo tarehe 21 Agosti ni Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi Waathirika wa Ugaidi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii amewasihi watu wote ulimwenguni kuhakikisha kwamba wale waliofariki au kukumbwa na athari za muda mrefu za ugaidi hawasahauliki kamwe. Kama sehemu ya kuadhimisha Siku hii, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kukabiliana na Ugaidi (UNOCT) kupitia Kampeni ya Kumbukumbu, kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii inasambaza kumbukumbu za waathirika wa ugaidi kupitia filamu na picha ili kuwaenzi waliofariki na pia kuwapa waathirika fursa ya kutoa ya moyoni. Mmoja wao ni Nigeel Namai alikuwa na umri wa miezi 4 baba yake alipouawa katika shambulio la mwaka 1998 kwenye Ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, Kenya. Wakati wowote Nigeel anapovaa suti, inaleta kumbukumbu na simulizi kuhusu baba yake, ambaye kila mara alikuwa nadhifu.“Kila wakati ninapovaa suti inarejesha kumbukumbu ya simulizi ambazo mama alikuwa ananisimulia kuhusu baba. Ningependa baba yangu ajivunie. Popote alipo aangalie aseme: “Oo, ingawa siwezi kuwa naye kimwili ninajivunia yeye kama mvulana mdogo na pia mwanaume mdogo.”
21-8-2023 • 0
Mifumo madhubuti ya kuwasiliana Sierra Leone imeimarisha uthibiti wa milipuko ya magonjwa
Takriban miaka 10 iliyopita nchi kadhaa za Afrika zilikumbana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa ebola uliogharimu maisha ya mamilioni ya watu. Moja ya nchi hizo ni Sierra Leone ambayo wakati mlipuko wa Ebola ukiikumba nchi hiyo walikuwa hawana njia bora za kuwasiliana kama taifa na kujua ukubwa wa ugonjwa huo na namna ya kudhibiti. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika mbali na kuisaidia nchi hiyo kupamba na Ebola lakini iliwasaidia kuweka mifumo madhubuti ya kuwasiliana nchi nzima kujua iwapo kuna mlipuko wa ugonjwa wowote. Ni kutokana na mfumo huo thabiti nchi hiyo imefanikiwa kuongoza katika utambuzi wa haraka wa milipuko ya magonjwa na kushughulikia kwa wakati. Leah Mushi anatujuza zaidi katika Makala hii.
21-8-2023 • 0
21 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya waathirika wa ugaidi duniani na mabomu ya kutegwa ardhini. Makala tunakupeleka nchini Siarra Leone na mashinani nchini Msumbiji, kulikoni? Ikiwa leo tarehe 21 Agosti ni Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka na Kuwaenzi Waathirika wa Ugaidi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii amewasihi watu wote ulimwenguni kuhakikisha kwamba wale waliofariki au kukumbwa na athari za muda mrefu za ugaidi hawasahauliki kamwe. Huko nchini Lebanon, Mashariki ya Kati, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNIFIL kwa ushirikiano na wadau wameteketeza mabomu 4,000 yaliyokuwa yametegwa kwenye eneo la ukubwa wa mita 44,000 za mraba na hivyo kuwezesha ianze kutumika tena kwa kilimo baada ya kushindikana tangu miaka ya 1970 kwa hofu ya milipuko ya mabomu.Katika makala Leah Mushu anatujuza namna nchi ya Sierra Leone ilivyoweza kubadilika kutoka nchi yenye ugunduzi dhaifu wa magonjwa hususan ya mlipuko mpaka kuwa nchi yenye ugunduzi thabiti na unaofanya kazi.Mashinai tunakwenda mjini Maputo nchini Msumbiji kusikia jinsi huduma ya maji ilivyoleta furaha kwa wafanyabiashara.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
21-8-2023 • 0
Kutana na Nafi Aïsha Diop mtaalamu wa usalama na ubora wa chakula wa WFP DRC
Ikiwa kesho Agosti 19 ni Siku ya watoa misaada ya kibinadamu, ambapo ulimwengu unawatambua na kuwasherehekea watu wote ambao waliojitolea au wanajitolea maisha yao kusaidia wanadamu wengine walio katika changamoto, leo tunakukutanisha na Nafi Aïsha Diop mtaalamu wa usalama na ubora wa chakula wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) anayehudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC). Msimulizi ni Anold Kayanda.Nafi Aïsha Diop akieleza kuhusu kazi yake hiyo katika WFP kwamba ni kuhakikisha usalama na ubora wa chakula ambacho WFP inakisambaza kwa wahitaji kuanzia shambani hadi mezani. Anafafanua anachomaanisha anaposema usalama na ubora wa chakula kwamba chakula lazima kiwe salama kwa matumizi ya binadamu. Na kuhusu ubora ni kwamba chakula hiki inabidi kiwe na lishe ndani yake kama vitamini na madini na kwa hiyo kiwape walaji kila kitu kinachohitajika katika mlo wao. Je ni kitu gani Nafi Aïsha Diop anakipenda zaidi katika kazi yake?Anasema, "Ninachopenda zaidi kuhusu kazi yangu ni kwamba ninafanya kazi na watu tofauti, mazingira, na aina tofauti za chakula. Ninajihisi kuridhishwa hasa na matokeo kwenye mnyororo mzima wa usambazaji kwa sababu unaweza kuona wazi matokeo. Kwa mfano tunapofanya mafunzo ya usalama na ubora wa chakula kwenye ghala, hatugusi tu wafanyakazi kwenye ghala. , lakini pia tunagusa jamii zao.”
18-8-2023 • 0
Wahisani msichoke kukirimu wenye uhitaji – Gregory Akall wa OCHA
Siku ya watoa misaada ya kibinadamu huadhimishwa kila Agosti 19, na maudhui mwaka huu ni “kwa vyovyote vile,” ikimaanisha misaada lazima iendelewe kutolewa katika mazingira yoyote yale. Gregory Akall wa Ofisa wa usaidizi wa kibinadamu katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya binadamu na ya dharura (OCHA), anahudumu kaskazini mwa Kenya. Akiwa naye mshiriki kwenye jukumu hili anatumia mazungumzo yake na mwandishi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini Kenya kutia shime wahisani wasichoke kwa vyovyote vile bali waendelee kunyoosha mikono yao kukirimu walio na uhitaji. Gregory anahudumu kaskazini mwa Kenya, eneo ambalo limezongwa na uhaba wa mvua, njaa na maafa ya mifugo. Hapa anaanza kufafanua jukumu la OCHA.
18-8-2023 • 0
UNICEF DRC: Mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu watishia uhai wa watoto
Kipindupindu chatishia uhai wa watoto DRC, UNICEF na wadau wachukua hatua.Heshima kwa Nafi Aïsha Diop mtaalamu wa usalama na ubora wa chakula wa WFP DRC.Makala leo tunaendelea na Gregory Akall, Msaidizi wa kibinadamu nchini Kenya hususan eneo la kaskazini mwa nchi akihudumu kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la uratibu wa misaada ya kibinadamu na dharura.Na mashinani, ili kukabiliana na tatizo la utapiamlo na uhaba wa chakula katika mkoa wa Karamoja nchini Uganda Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP linatumia vijana kama mawakala wa kuleta mabadiliko katika jamii zao.
18-8-2023 • 0
Methali: "Ukubwa jalala"
Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Ukubwa ni jalala.”
17-8-2023 • 0
17 AGOSTI 2023
Siku ya watoa misaada ya kibinadamu huadhimishwa tarehe 19 ya mwezi Agosti kila mwaka kwa lengo la kutambua wale waliojitolea maisha yao kusaidia walio katika changamoto.Thomas Nyambane kutoka Kenya amekuwa mratibu wa misaada ya binadamu kwa zaidi ya miongo miwili na amehudumu kwenye mazingira magumu. Anaipenda kazi yake ila changamoto ni tishio la usalama na kila anapokuwa nje anaikumbuka sana familia yake kwani anapitwa na mengi. Hata hivyo, majukumu yake katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya binadamu na ile ya dharura, UNOCHA yanampa faraja kubwa kwani anapata nafasi ya kubadili maisha ya watu walio taabani.Mwandishi wetu wa Kenya ,Thelma Mwadzaya alikutana naye mjini Nairobi alipokuwako kwa muda mfupi kabla kurejea Somalia ambako ndiko kituo chake cha kazi. Hapa Thomas anaanza kwa kusimulia ilikoanzia safari yake.
17-8-2023 • 0
Sikufahamu jinsi ya kuzungumza na mwanangu kumuepusha na mimba za utotoni - Mzazi Haiti
Hebu fikiria kutarajia kupata mtoto wakati ambapo hata hufahamu neno ujauzito lina maana gani. Hicho ndicho kilichomfika mtoto mwenye umri wa miaka 14 nchini Haiti ambaye alijikuta anapewa ujauzito na kaka wa rafiki ya kiume wa rafiki yake. Hakuwa anajitambua akakubali kumsindikiza rafiki yake na zaidi ya yote akakubali urafiki na kijana huyo mwenye umri wa miaka 16. Mama yake binti huyu naye anasema hakufahamu ni kwa jinsi gani azungumze na mtoto wake ili kumuepusha na uhusiano na wavulana kwa lengo la kumuepusha kupata ujauzito. Maji yameshamwagika hayazoleki lakini shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya watu, UNFPA nchini Haiti linachukua hatua kutoa eliu ya viungo vya uzazi na afya ya uzazi kwa wasichana na watoto wa kike ili kuepusha maji kumwagika zaidi ilhali hayazoleki. Simulizi ya mtoto huyo na kinachofanyika kuwasaidia ndio makala yetu ya leo inayoletwa kwako na Assumpta Massoi.
16-8-2023 • 0
WFP na mradi wa kushughulikia utapiamlo na kuinua kipato nchini Kenya
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP nchini Kenya linatekeleza mradi wa Mchepuko Chanya au Positive Deviance (PD) Heart unaolenga kuwasaidia kinamama kushughulikia na kuzuia utapiamlo kwa kutumia vyakula salama na vyenye lishe ambavyo vinalimwa na wanajamii wenyewe. Evarist Mapesa na maelezo zaidi.Katika Kaunti ya Baringo mradi wa PD Heart unaotekelezwa na WFP nchini Kenya umesaidia watoto kukarabati afya zao kwa kuwapatia kinamama ujuzi wa kuweza kushughulikia utapiamlo wakiwa majumbani pamoja na kuwafundisha wazazi wote namna bora yakupika vyakula vyenye virutubisho kwakutumia viungo vinavyopatikana katika maeneo yao. Mafanikio yamepatikana tayari kwa watoto kuongezeka uzito kutoka gramu 200 hadi 800 katika muda wa siku 12 hadi 30 shuhuda wa hilo ni Irene Menjo. “Kile kilinifanya nijiunga na PD Heart ni mtoto wangu alikuwa na uzito mdogo nikamlisha mboga za majani kwa siku 12 na naona sasa hivi mtoto wangu amepata afya.”Mradi huo pia unawaunganisha wakulima na masoko kama anavyoeleza Caroline chedu Afisa mradi wa WFP. “Kila wiki wanapeleka mboga za majani katika shule mbalimbali lengo letu linalotuongoza ni kuongeza utofauti wa mlo kwa wanafunzi wanaoenda shule” Kwa watoto wengi wa Kaunti hiyo ya Baringo wanapoenda shuleni wanakuwa hawajala kitu chochote na Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Maji Moto Ann Mungai anasema wanashukuru pogramu za mlo shuleni. “Tuna bahati nzuri ya kuwa na programu ya mlo shuleni inayotolewa na serikali. Mboga za majani zilizoongezwa kwenye vyakula vya watoto ni muhimu sana mosi vinafanya kuwa kitamu na pili kuwa na muonekano mzuri, utatamani kukila kwa jinsi kinavyoonekana. Na wakinamama nao wanafuraha kwani wananufaika na mradi huu kwakupata fedha kutokana na kuuza mboga za majani na pia kwa lishe.”WFP wanasema programu hii ni mbinu ya gharama nafuu ya kupunguza utapiamlo kwani imepunguza idadi kubwa ya watoto wanaopelekwa kwenye vituo vya kusaidia wenye utapiamlo.
16-8-2023 • 0
Ripoti ya UNCTAD - Afrika inaweza kuwa kiungo muhimu katika minyororo ya ugavi duniani
Afrika inaweza kuwa kiungo muhimu katika minyororo ya ugavi duniani - Ripoti ya UNCTAD.Mradi wa PD wa WFP Kenya washughulikia utapiamlo na kuinua kipato cha wakulima.Sikufahamu jinsi ya kuzungumza na mwanangu kumuepusha na mimba za utotoni - Mzazi HaitiMashinani ni ushauri wa Issa Ibrahim Shauri anayefahamika kama mgonjwa wa mwisho nchini Tanzania wa virusi vya polio aina ya 1.
16-8-2023 • 0
15 AGOSTI 2023
Tarehe 19 mwezi huu wa Agosti siku ya ubinadamu duniani ikilenga kutambua watu wanaojitoa kwa moyo wao wote kusaidia wale walio kwenye uhitaji. Miongoni mwa watu hao ni Gregory Akall, Afisa huyu wa ubinadamu kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya binadamu,UNOCHA. Eneo lake la kufanyia kazi ni kaskazini mwa Kenya ambako ukame, uhaba wa maji na njaa ni matatizo makubwa yanayowazonga wakaazi kila uchao. Gregory Akall mwenyewe ni mturkana kutoka eneo hilo la kaskazini mwa Kenya, hivyo kufanya kazi eneo hilo ni sawa na mcheza kwao. Je, kama mratibu wa misaada ya binadamu kwenye shirika la UNOCHA, siku yake huanza vipi? Hilo ndilo swali mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya aliloanza kumuuliza alipokutana naye mjini Nairobi, Kenya.
15-8-2023 • 0
Kamishna Susan aelezea ambacho hatosahau wakati wa huduma yake Abyei
Hii leo katika makala nakukutanisha na Kamishna Susan Kaganda, Mkuu huyu wa Utawala na Raslimali watu katika Jeshi la Polisi Tanzania ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Operesheni kwenye ujumbe wa muda wa Umoja wa Mataifa wa mpito kwenye eneo la Abyei lililoko katikati ya Sudan na Sudan Kusini, UNISFA. Katika mahojiano yake na Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC Dar es salaam nchini Tanzania anasimulia mambo kadhaa ikiwemo hili analoanza nalo la jambo gani anakumbuka zaidi wakati akihudumu UNISFA.
15-8-2023 • 0
Tiba asilia duniani: Takriban nusu ya nchi wanachama wa WHO wanazitambua na kuzitumia
14-8-2023 • 0
Wataalam UN: Watalibani wanazidi kukandamiza raia kinyume na madai yao
14-8-2023 • 0
14 AGOSTI 2023
Watalibani wanazidi kukandamiza raia kinyume na madai yao - Wataalam UN.Takriban nusu ya nchi wanachama wa WHO wanatambua na kutumia tiba asilia.Kwenye makala ni Suzan Kaganda, Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu katika Jeshi la Polisi Tanzania ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Operesheni kwenye ujumbe wa muda wa Umoja wa Mataifa kwenye eneo la Abyei lililoko katikati ya Sudan na Sudan Kusini, UNISFA. Mashinani ni ujumbe wa mama mnufaika wa huduma za afya hususan za uzazi nchini Rwanda.
14-8-2023 • 0
Wakazi wa Darfur Magharibi hatimaye wafikishiwa chakula – WFP
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hatimaye limethibisha hofu yake juu ya viwango vya juu vya njaa nchini Sudan baada ya kuweza kwa mara ya kwanza kufikisha msaada wa chakula kwa wakazi wa Darfur Magharibi nchini humo tangu kuzuka kwa vita mwezi Aprili mwaka huu huku mamilioni ya watu wakiwa hawana chakula. Punde tu baada ya vita kuanza mwezi APrili mwaka huu nchini Sudan, WFP ilitabiri kuwa njaa inaweza kuongezeka na kukumba zaidi ya watu milioni 19 katika miezi ijayo. Eddie Rowe Mkurugenzi wa WFP nchini Sudan akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kwa njia ya video kutoka mji wa Port Sudan amesema, "sasa ikiwa ni miezi takribani minne tangu vita ianze, utabiri huo mchungu umethibitika kuwa ukweli mchungu." Amenukuu taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) kwamba ripoti mpya ya uhakika wa kupata chakula (IPC) imeonesha kuwa vita imetumbukiza zaidi ya watu milioni 20 kwenye njaa kali. Idadi hiyo ni sawa na asilimia 42 ya wananchi wa Sudan. Watu milioni 6.3 kati yao hao milioni 20 wenye njaa Sudan, wako katika kiwango cha juu zaidi cha njaa, ikiwa ni hatua moja kabla ya kuwa na baa la njaa. Licha ya changamoto ya usalama, Bwana Rowe amesema wiki iliyopita wameweza kwa mara ya kwanza kufikishia wakazi wa Darfur Magharibi msaada wa chakula kupitia mpaka wa mashariki mwa Chad, msaada ulionufaisha watu 15,400 kwenye vijiji vya Adikong, Shukri, na Jarabi. Amesema ni matumaini yake njia hiyo itaendelea kutumika kwa ajili ya kupitishia misaada huko Geneina, mji muu wa jimbo la Darfur MAgharibi ambako miji na vijijii vimetelekezwa na waliosalia ni wanawake na watoto bila huduma za afya na miundombinu mingine muhimu.
11-8-2023 • 0
Manusurua kutoka Gambia: Sitamani tena kuzamia kwenda ulaya
Kila mwaka maelfu ya wahamiaji kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Afrika hujaribu kufika Ulaya wakivuka Bahari ya Mediterania wakieleza kwenda kusaka maisha bora lakini safari hiyo inaelezwa kuwa ni hatari sana kwani maelfu ya watu hufa maji au kutoweka. Ni Amadou Jobe kijana ambaye akiwa na umri wa miaka 25 alianza safari ya hatari kutoka nchini Kwake Gambia kupitia kaskazini mwa Afrika lengo likiwa Kwenda nchini Italia kusaka maisha bora kwani alikuwa akiishi katika hali ya umasikini na alitamani kuja kuisaidia familia yake iwapo angefanikiwa kufika Ulaya. Safari ya Amadou haikuwa rahisi kwa zaidi ya miaka miwili alikuwa safarini kutoka nchini mwake Gambia alienda mpaka nchi ya Mauritani, kisha Mali, akaingia Niger na mwisho nchini Libya nchi ambayo baada ya kukaa zaidi ya mwaka mmoja alifanikiwa kupata boti ambayo ndio ingetimiza ndoto yake ya Kwenda Ulaya. “Ndani ya boti yetu, kulikuwa na zaidi ya watu 100 kutoka Gambia, watu wengine niliowakuta ni Wanigeria na wengine wanatoka Liberia kiufupi kulikuwa na nchi kutoka barani Afrika. Siku tulipojaribu kuvuka Kwenda Ulaya, boti yetu ilikuwa na matatizo na hali ya hewa pia haikuwa nzuri. Tuliona maji yakijaa ndani ya boti yetu. Kwa hivyo tuliamua kurudi kwa sababu kama tukitaka kuendelea, tungaweza wote kufamaji huko.” Bahati haikuwa yake kwani alipojaribu kusafiri awamu ya pili walikamatwa na kufingwa jela nchini Libya anasema maisha jela yalikuwa mabaya na baadae Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM liliwatembelea gerezani na kuwapa fursa ya kurejeshwa makwao na Amadou naye alirejea.“Sikuwa nataka kurudi hapa. Nilitaka kuendelea na safari yangu. Nina huzuni sana kwa sababu pesa zote nilizotumia, nilipoteza kila kitu na kuja kuanza upya kutoka sifuri. Nimetumia karibu dola 1700. Lakini hakuna la kufanya. Mahali tulipokuwa tusingeweza kwenda kokote na hauwezi kutoroka.” Marie Stella Ndiaye ni meneja program wa IOM nchini Gambia anaeleza baada ya kuwajeresha makwao hawawaachi pia wa programu za kuwasaidia. “Tumejikita kwenye kuwatafuta na kuokOa maisha yao. Pia tunatoa usaidizi kwenye vituo vya rasilimali za wahamiaji vilivyo katika nchi ambazo wahamiaji hawa hupita wakitaka kusafiri Kwenda ulaya. Mara tu wanaporejea, IOM inatoa usaizi wa kila aina kuanzia masuala ya ushauri nasaha, ujumuishaji wa kiuchumi, ujumuishaji upya wa kijamii, lakini pia, muhimu zaidi, usaidizi wa kisaikolojia.” Mara bada ya kurejea nchini Gambia Amadou alipata ufundi stadi kutoka mashirika ya UN ambayo ni IOM na UNCDF na sasa anafanya kazi ya fundi uashi, ameoa na ana watoto wawili. Ameapa kutojaribu tena kuzamia kwenda ulaya, ataenda bara hilo kwa kupanda ndege kihalali nasi vinginevyo.
11-8-2023 • 0
Kijana Florent: Vijana DRC tunahaha kujikwamua kiuchumi lakini usalama unatukwamisha
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, vijana kesho wataadhimisha siku yao duniani huku kiza kinene cha ukosefu wa usalama kikiwa kimetanda mashariki mwa taifa hilo la ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika. Wakati Umoja wa Mataifa ukipigia chepuo vijana kushika hatamu ya kusongesha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ikiwemo hatua kwa tabianchi, kutokomeza umaskini na ajira zenye hadhi, kwa vijana wa mashariki mwa DRC vuguvugu hilo linakumbwa na kikwazo cha usalama hata kama wawe wamepata elimu. Shuhuda wa changamoto hizo ni kijana Florent Muhindo Nambura mkazi wa Beni jimboni Kivu Kaskazini na amefunguka hali halisi ilivyo akizungumza na George Musubao, mwandishi wetu DRC. Florent anaanza kwa kuelezea kile anachofanya.
11-8-2023 • 0
11 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Vijana Duniani ambayo inaadhimishwa tarehe 12 Agosti 2023 kila mwaka na tutafuatilia kazi za vijana waliorejea nyumbani Gambia kutoka Ulaya. Pia tuanaangazia msaada wa kibinadamu Sudan. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, salía papo hapo!Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP hatimaye limethibisha hofu yake juu ya viwango vya juu vya njaa nchini Sudan baada ya kuweza kwa mara ya kwanza kufikisha msaada wa chakula kwa wakazi wa Darfur Magharibi nchini humo tangu kuzuka kwa vita mwezi Aprili mwaka huu huku mamilioni ya watu wakiwa hawana chakula. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. Kila mwaka maelfu ya wahamiaji kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Afrika hujaribu kufika Ulaya wakivuka Bahari ya Mediterania wakieleza kwenda kusaka maisha bora lakini safari hiyo inaelezwa kuwa ni hatari sana kwani maelfu ya watu hufa maji au kutoweka. Evarist Mapesa anatupeleka nchini Gambia kusikia simulizi wa kijana ambaye chupuchupu apoteze maisha.Hii leo katika Makala tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mwandishi wetu George Musubao amezungumza na kijana Florent Muhindo Nambura mkazi wa Beni jimboni Kivu Kaskazini ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya vijana duniani tarehe 12 mwezi huu wa Agosti. Florent anaanza kwa kuelezea kile afanyacho.Mashinai tunakupeleka katika kambi ya wakimbizi ya Birau nchini CAR, ambako kijana mkimbizi kutoka Sudan hajafa moyo na anatarajia kutimiza ndoto zake na zile za watoto wakibizi walioko kambini humo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
11-8-2023 • 0
Methali: "Mchakacho ujao haulengwi jiwe."
Katika kujifunza lugha ya kiswahili Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA nchini Tanzania anachambua methali "Mchakacho ujao haulengwi jiwe."
10-8-2023 • 0
10 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikimulika kazi ya vijana katika kusongesha malengo ya maendeleao endeleu na tunaelekea huko mkoani Mwanza kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambapo kijana Mbunifu Kelvin Paul amekuwa akibuni vifaa mbalimbali vya kiteknolojia ili kufanikisha lengo namba 4 linalozungumzia Elimu kwa wote ifikapo Mwaka 2030. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka nchini Chad, Niger na Ethiopia. Katika kujifunza Kiswahili tunapata uchambuzi wa methali “Mchakacho ujao haulengwi jiwe.” Huku duru za habari zikiripoti kuwa Rais wa Niger Mohamed Bazoum na familia yake wanashikiliwa na walinzi wa Rais bila huduma kama umeme, dawa chakula na maji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza kusikitishwa na hali hiyo na kutaka wanaomshikilia wamwachilie huru bila masharti. Kamisheni ya kimataifa ya wataalamu wa haki za binadamu kuhusu Ethiopia leo imesema ina wasiwasi mkubwa kuhusu ripoti ya kudorora kwa hali ya usalama kwenye ukanda wa kaskazini-magharibi mwa Ethiopia hususan jimbo la Amhara ambako huko Baraza la Mawaziri lilitangaza hali ya dharura tarehe 4 mwezi huu kinyume na katiba ya nchi.Na nchini Chad, zaidi ya watu 50 waliokimbia machafuko nchini Sudan wamepata hifadhi kwenye nyumba ya Fatna Hamid, jambo linalofanywa na raia wengi wa Chad wakati huu ambapo zaidi ya wakimbizi 320,000 wameingia mashariki mwa Chad tangu mapigano yaanze Sudan mwezi April mwaka huu. Fatna anasema, “Wengi wananifahamu tangu zamani na baadhi ni wagonjwa hawana mtu wa kuwahudumia. Wanahitaji msaada kwa sababu hawana chochote.”Na katika kujifunza kiswahili Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA nchini Tanzania anachambua methali Mchakacho ujao haulengwi jiwe.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
10-8-2023 • 0
Vijana wa jamii ya asili tuna nafasi kubwa kusongesha jamii zetu
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya jamii ya watu wa asili hii leo, ambayo maudhui yake yanalenga vijana na nafasi yao katika kusongesha tamaduni na ufahamu wa jamii hizo Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa ilibisha hodi nchini Kenya, Mashariki mwa Afrika ambako kuna vijana wa jamii ya asili wanachukua hatua. Lengo ni kufahamu nafasi yao hivi sasa na nini wanafanya kuona mustakabali wao unaimarika. Vijana hao Virginia Sintanai wa jamii ya Ilchamus na pia mwanachama wa Mtandao wa vijana wa jamii ya asili nchini Kenya (KIYN). Mwingine ni Bernard Loolasho wa jamii ya Yiaku kutoka mpango wa hifadhi ya jamii ya Laikipia kaskazini, (LANCCI). Tunaanza na Virginia.
9-8-2023 • 0
09 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya watu wa asili ambapo umoja wa mataifa umepongeza vijana wa jamii hizo kwa kazi zao za kusongesha malengo ya maendeleo endelevu. Pia tunakupeleka nchini Rwanda na Kenya, kulikoni?Hii leo ni siku ya jamii ya watu wa asili duniani ambapo maudhui ni vijana, ikisherehekea vijana wa jamii ya asili na dhima yao katika kuleta mabadiliko na kuumba mustakabali wa dunia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa ujumbe wake. Wakati dunia ikiwa na maono mbalimbali juu ya ukuaji wa mtandao wa intaneti na namna unavyoweza kuwasaidia, Mwakilishi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda Ozzonia Ojielo amesema ni vyema maono hayo kuhakikisha hakuna mtu anaachwa nyuma.Makala tunakupeleka Kenya kupata ujumbe kutoka kwa vijana wa jamii ya asili ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya jamii ya asili ikimulika zaidi vijana.Na katika mashinani Hapo baadaye ni mashinani na ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya watu wa asili tutakuletea ujumbe kuhusu haki za wasichana na wanawake, hususan wanaolelewa katika jamii za watu wa asili.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu sana!
9-8-2023 • 0
Wananchi wakipatiwa elimu ya kidigital watakuza maendeleo ya Taifa
Wakati dunia ikiwa na maono mbalimbali juu ya ukuaji wa mtandao wa intaneti na namna unavyoweza kuwasaidia, Mwakilishi Mkaazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda Ozzonia Ojielo amesema ni vyema maono hayo kuhakikisha hakuna mtu anaachwa nyuma. Ni Mwakilishi Mkaazi wa UN nchini Rwanda akizungumza katika jukwaa la kujadili utawala wa mtandao lililofanyika huko nchini Rwanda likikutanisha wadau wa masuala ya mtandao ili kuangalia namna bora ya kuhakikisha jamii nzima inanufaika na maendeleo ya kiteknolojia yanayoletwa na huduma ya mtandao. Katika hotuba yake Ojielo amesema, “Ahadi yetu ya kumjumuisha kila mtu inaanza kwa kuhakikisha kuna upatikanaji sawa wa mtandao kote nchini Rwanda kuanzia mijini mpaka vijijini. Kuunganishwa na mtandao haipaswi kuwa fursa bali haki ya msingi inayopatikana kwa wote.” Mkuu huyo wa UN nchini Rwanda amesema pamoja na kufikishiwa huduma ya mtandao lakini pia wananchi wapatiwe elimu.“Kwa kukuza elimu ya kidigitali, tutawawezesha watu binafsi kuchangamkia fursa katika elimu, ujasiriamali, na ushiriki wa kiraia, hatimaye hivi vyote vitasaidia kuendeleza maendeleo ya taifa letu.” Katika hotuba yake hiyo pia ameipongeza serikali ya Rwanda kwa kupitisha sheria ya kulinda taarifa za watumia mitandao ya mwaka 2021 pamoja na sera ya kitaifa ya Akili Mnemba au AI ya mwaka 2022 na kusema juhudi hizo zinaonesha nia ya dhati ya serikali ya Rwanda ya kuendelea kidijitali, kibunifu na kuwalinda wananchi wake.
9-8-2023 • 0
UN wawapongeza vijana wa jamii ya asili kwa kutokubali ukandamizaji wa jamii zao
Hii leo ni siku ya jamii ya watu wa asili duniani ambapo maudhui ni vijana, ikisherehekea vijana wa jamii ya asili na dhima yao katika kuleta mabadiliko na kuumba mustakabali wa dunia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa ujumbe wake. Katika ujumbe wake wa siku hii iadhimishwayo tarehe 9 mwezi Agosti ya kila mwaka, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anasema duniani kote watu wa jamii ya asili wanakabiliwa na changamoto, ardhi na rasilimali zao zikitishiwa haki zao zikikandamizwa na changamoto yao ya kila uchao ya kuenguliwa na kutengwa. Hata hivyo amesema vijana wa jamii ya asili wanapambana kupinga vitisho hivyo kwa kuchukua hatua. Katibu Mkuu amesema wao ni viongozi wa vuguvugu la hatua kwa tabianchi duniani. Ni wachechemuzi wa haki, wanafurahia tamaduni zao, wanasongesha haki za binadamu na kuhamasisha uelewa wa watu kuhusu historia ya watu wa jamii ya asili na masuala yao duniani kote. Kama hiyo haitoshi, Bwana Guterres amesema vijana hao wanajifunza kutoka kwa wazee wao, wakihakikisha tamaduni za watu jamii ya asili, busara na utambulisho wao vinasonga mbele badala ya kutoweka. Ufahamu wa watu wa jamii ya asili na tamaduni zao zimejikita mizizi katika maendeleo endelevu na vinaweza kusaidia kutatua changamoto nyingi za pamoja. Ni kwa sababu hiyo Katibu Mkuu anasema ni muhimu vijana wa jamii ya asili, wote wake kwa waume, wavulana na wasichana washiriki katika upitisha wa maamuzi. Bwana Guterres amesema chaguo lifanyikalo leo litaamua dunia ya kesho hivyo ametaka kila mtu apatie msisitizo ahadi yake ya kuhakikisha haki za mtu mmoja mmoja na za kijamii kwa watu wa asili na wakati huo huo kusaidia ushiriki wao katika mijalada dunian ina upitishaji wa maamuzi. Ametamatisha ujumbe wake akisma kwa pamoja hebu tujenge mustakabli bora kwa sisi sote.
9-8-2023 • 0
Watoto wanaonyonyeshwa maziwa ya mama wana afya bora - UNICEF Kenya
Wiki ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama duniani, imehitimishwa Agosti 7, au jana Jumatatu, wiki iliyosheheni matukio ya kuonesha hatua za kuhakikisha watoto wanapozaliwa wananyonyeshwa maziwa ya mama kwa faida sio tu ya mtoto bali pia mama. Nchini Kenya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Wizara ya Afya, walikuwa na tukio la aina hiyo na shuhuda wetu alikuwa mwandishi wetu nchini Kenya, Thelma Mwadzaya.
8-8-2023 • 0
08 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kinaambapo wiki ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama duniani, imehitimishwa Agosti 7, au jana Jumatatu, wiki iliyosheheni matukio ya kuonesha hatua za kuhakikisha watoto wanapozaliwa wananyonyeshwa maziwa ya mama kwa faida sio tu ya mtoto bali pia mama. Nchini Kenya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Wizara ya Afya, walikuwa na tukio la aina hiyo na shuhuda wetu alikuwa mwandishi wetu nchini Kenya. Mashinani tutakupeleka kijijini Mauratou nchini Fiji kushuhudia jinsi wakulima wanawake wanavyoweza kukabiliana na tatizo la kupanda kwa bei ya chakula na bidhaa zingine. Wakati idadi ya watu wanaokimbia machafuko nchini Sudan ikifikia milioni 4, Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na masuala ya wakimbizi UNHCR limesema lina wasiwasi mkubwa kuhusu kuzorota kwa afya za wakimbizi hao ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi katika kambi za wakimbizi. Tukisalia na vita vya Sudan, nalo shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO limeeleza kukabiliwa na uhaba wa vifaa tiba pamoja na huduma za maji na umeme katika maeneo yaliyoathirika na vita.Na katika pwani ya Lampedusa nchini Italia Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limesikitishwa na ajali nyingine ya meli katika bahari hiyo ya Mediterania.Na katika mashinani wanawake wakulima nchini Fiji, kufuatia mafunzo yanoyotolewa na Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo duniani, IFAD wameweza kubadilisha bidhaa zinazotoka nje kama vile unga na aina zinazozalishwa nyumbani.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
8-8-2023 • 0
OCHA: Maisha ya kila siku nchini Sudan ni jinamizi
Mkuu wa kitengo cha Operesheni na Uchechemuzi kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu na kuratibu masuala ya dharura OCHA Edem Wosornu amesema maisha ya kila siku ya wananchi nchini Sudan yamegubikwa na sintofahamu kutokana na vita inayoendelea hivyo amesihi pande husika kukomesha mapigano na wakati huo huo wahisani waongeze ufadhili wa kibinadamu. Akihojiwa na Idhaa ya kiarabu ya Umoja wa Mataifa Bi. Wosornu ambaye alikuwa ziarani nchini humo hivi karibuni, amesema hali ya sintofahamu imekumba wananchi akitolea mfano Hawaa, mama, bibi na mfanyabiashara ambaye alikuwa mchuuzi nje kidogo ya mji mkuu wa Sudan Khartoum ambaye sasa tangu vita ianze hawezi kujikimu bali anategemea malipo kidogo ya fedha kila mwezi ili anunue dawa za kujitibu kisukari. Na kwa watoa misaada ya dharura nao hali ni mbayá, “Na niliwauliza maisha yako vipi kwa mtu wa kawaida mjini Khartoum? Na wakasema ni kama jinamizi kwa sababu hufahamu kama upande wowote ule utakukamata na kukuweka ndani. Hufahamu iwapo utatoweshwa. Lakini wanaendelea na maisha kwa sababu wameazimia kuliko wakati wowote ule kusambaza misaada ya kiutu.” Afisa huyo wa OCHA ametoa wito kwa wahisani wengine zaidi wajitokeza kuchangia ili kufanikisha mahitaji ya wananchi wa Sudan huku akipeleka ujumbe kwa pande kinzani ambazo ni jeshi la serikali, (SAF) na wanamgambo waasi wa kikundi cha Rapid Support Forces (RSF), “Ujumbe wangu kwa pande kinzani ni ujumbe ambao wasudan wamenieleza nilipotembelea Sudan. Acheni vita. Acheni mapigano ma tuacheni turejee majumbani mwetu na tuishi maisha yetu.”
7-8-2023 • 0
Mauritius waelekeza mbinu wanazotumia kutokomeza uvutaji wa tumbaku nchini mwao
Mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Afya WHO walitoa ripoti ya 9 kuhusu janga la uvutaji tumbaku na kueleza kuwa mafanikio yameanza kuonekana kwa nchi wanachama kutekeleza sera ya kulinda umma kutoathirika na uvutaji wa sigara unaofanywa na mtu mwingine ambapo zaidi ya watu bilioni 5.6 wamenufaika na sera hiyo ulimwenguni kote. Nchi ya Mauritius ilipongezwa kwa kuwa nchi pekee iliyotekeleza vyema sera zote sita za kupambana na athari za tumbaku. Je waliwezaje? Tuungane na Hapinness Palangyo wa redio washirika akitusomea makala hii iliyoandaliwa hapa studio.
7-8-2023 • 0
07 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mizozo Sudan na ukulima wa mboga mboga nchini Benin. Makala tunakupeleka nchini Mauritius na mashinani nchini Kenya, kulikoni? Mkuu wa kitengo cha Operesheni na Uchechemuzi kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya kibinadamu na kuratibu masuala ya dharura OCHA Edem Wosornu amesema maisha ya kila siku ya wananchi nchini Sudan yamegubikwa na sintofahamu kutokana na vita inayoendelea hivyo amesihi pande husika kukomesha mapigano na wakati huo huo wahisani waongeze ufadhili wa kibinadamu. Nchini Benin, mradi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji, UNCDF umewezesha vijana waliokuwa wanazurura wakati wa msimu wa mwambo nchini humo kuweza kuendelea na shughuli za kilimo kutokana na mradi huo kuwapatia pampu za kusukuma maji ya umwagiliaji kwa kutumia nishati ya sola.Makala tuankupeleka nchini Mauritius ambapo hivi karibuni imepongezwa kwa kuwa nchini ya kwanza Barani Afrika kupunguza kwa kiasi kikumbwa athari za matumizi ya tumbaku kwa umma.Na katika mashinani tutakupeleka nchini Kenya kusikia ujumbe wa mwanaharakati wa mazingira na tabianchi kuhusu vijana wa vijijini na jukumu lao muhimu katika kukabiliana na ukosefu wa chakula na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
7-8-2023 • 0
Mradi wa maji unaotumia sola Benin waepusha vijana na uzururaji wakati wa mwambo
Nchini Benin, mradi unaofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mfuko wa Maendeleo ya Mitaji, UNCDF umewezesha vijana waliokuwa wanazurura wakati wa msimu wa mwambo nchini humo kuweza kuendelea na shughuli za kilimo kutokana na mradi huo kuwapatia pampu za kusukuma maji ya umwagiliaji kwa kutumia nishati ya sola. Ni Issotina Nala huyo kijana mkulima wa mboga mboga mwenye umri wa miaka 32 akizungumza kwa furaha juu ya manufaa ya pampu inayotumia nishati ya jua au sola na mfumo wa umwagiliaji maji uliofanikihswa na UNCDF hapa Kijiji cha Wekete jimbo la Ouake, kaskazini magharibi mwa Benin, huko Afrika Magharibi. “Ndio, inaleta tofauti kubwa sasa na kwa siku za usoni, kwa kuwa hatutakosa kipato. Kwa sababu mimi nina wake wawili na Watoto. Kwa pampu hii Watoto wangu wataweza Kwenda shuleni, na familia yangu itakuwa na ahueni.” Cossova Nanako, Mkuu wa Programu za UNCDF Benin anasema suala kwamba kuna uhaba wa maji kutokana na mabadiliko ya tabianchi tunabaini kuwa vijana wengi wanakuwa hawana cha kufanya msimu wa ukame kuanzia mwezi Oktoba hadi Aprili. Bwana Nala akiwa kwenye bustani yake ya mboga anakiri.. “Hakuna maji kuanzia Oktoba hadi Machi kwa hiyo tunabakia nyumbani. Na unaweza kufanya nini bila maji? Ukiwa na bustani ya mboga unapaswa kuwepo bustani kila wakati.” UNCDF inasema hali hiyo inalazimu vijana kuondoka vijijini na kuelekea mijini kutafuta vibarua lakini kupitia mradi huu uitwalo LoCAL wa kuwezesha wakazi kuhimili mabadiliko ya tabiachi nchi sasa kuna nuru na Bwana Nala anasema, “Sasa na mfumo huu wa umwagiliaji, hakuna tena kupumzika na tutakuwa na muda wa kufanya kazi wakati wowote.” UNCDF inasema sasa wakulima wanaweza kulima misimu yote hata wakati wa ukame na hivyo kuwa na uhakika sio tu wa chakula bali pia kipato kwa ajili ya familia zao.
7-8-2023 • 0
Amina J. Mohammed ziarani Amazon: Nimesikia maombi yenu na tutapaza sauti
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed anaendele ana ziara yake ya siku tano nchini Brazil ambapo siku ya Alhamisi Agosti 3, 2023 alizuru jamii ya watu wa asili ya Mapuera kwenye ukanda wa Amazon jimboni Para ambako huko alipata fursa ya kuzungumza na wanajamii hao na kusikia maombi yao, ziara ambayo anafanya kufuatilia utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuelekea mkutano wa viongozi kuhusu SDGs mwezi Septemba mwaka huu. Thelma Mwadzaya anatusimulia kilichojiri.
4-8-2023 • 0
Türk asikitishwa baada ya ofisi ya UN ya Haki za Binadamu Uganda yafungwa
Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu UN Volker Türk, hii leo ameelezea masikitiko yake makubwa kufuatia kufungwa kwa ofisi yake nchini Uganda kufuatia uamuzi wa serikali hiyo kutotia saini mkataba wa kuendelea kuweko kwa ofisi hiyo nchini humo. Taarifa iliyotolewa leo huko Geneva, Uswisi na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imesema tayari ofisi ndogo za Gulu na Maroto zilifungwa tarehe 30 Juni na 31 Julai mtawalia, huku ofisi kuu ya jijini Kampala ikifungwa kesho Jumamosi Agosti 5. Bwana Türk amesema “nasikitika ofisi yetu Uganda inafungwa baada ya kuweko nchini humo kwa miaka 18, ambapo tuliweza kushirikiana na mashirika ya kiraia, watu kutoka pande mbalimbali nchini Uganda pamoja na taasisi za serikali kusongesha na kulinda haki za binaamu za waganda wote.” Amesema tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo mwaka 2005 wameshirikiana na serikali na wadau kwenye masuala kama vile kujumuisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kwenye mipango ya kitaifa na kushauri juu ya kuoanisha sheria za nchi na sheria za kimataifa za haki za binadamu. Hata hivyo amesema licha ya maendeleo makubwa yaliyopatikana kwenye haki za binadamu Uganda bado kuna changamoto kubwa za haki za binadmau, akitaja hususan hofu juu ya haki za binadamu kuelekea uchaguzi mkuu wa Uganda mwaka 2026 ambako watetezi wa haki, wawakilishi wa mashirika ya kiraia na waandishi wa habari wanafanya kazi katika mazingira magumu. Bwana Türk ameonya juu ya uwezekano wa kudorora kwa ahadi za Uganda kwenye mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu iliyoridhia, ikiwemo kupitishwa kwa sheria dhidi ya ushoga ambayo tayari imekuwa na madhara kwa waganda. Kamishna huyo Mkuu wa Haki za Binadamu ameisihi serikali ya Uganda ihakikishe kuwa taasisi ya kitaifa ya haki za binadamu inafanya kazi kwa ufanisi, kwa uhuru kama chombo chenye jukumu la kusimamia haki nchini humo. Amesema kwa upande wake, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu inasalia kuendelea kushughulikia haki za binadamu Uganda kwa mujibu wa mamlaka ya kimataifa.
4-8-2023 • 0
04 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu na Akili Mnemba au ‘Artificial Intelligence’. Makala tunakupeleka nchini Brazil na mashinani tutasikia ujumbe wa kijana kutoka Tanzania, salía papo hapo! Kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu UN Volker Türk, hii leo ameelezea masikitiko yake makubwa kufuatia kufungwa kwa ofisi yake nchini Uganda kufuatia uamuzi wa serikali hiyo kutotia saini mkataba wa kuendelea kuweko kwa ofisi hiyo nchini humo. Hatimaye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametimiza ahadi yake ya kuunda Bodi ya Umoja wa Mataifa ya Ushauri wa Kisayansi wakati huu ambapo teknolojia ya Akili Mnemba au ‘Artificial Intelligence’ imeshaanza kugonganisha vichwa vya watu kuhusu nafasi yake katika maendeleo duniani.Katika makala Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed akiwa ziarani nchini Brazil amewahakikishia watu wa jamii ya asili ya Mapuera kwenye jimbo la Pará nchini humo kwamba amesikia kilio chao na zaidi ya yote Umoja wa Mataifa utahakikisha sauti zao zinasikilizwa kwani wanachodai ni haki zao za msingi.Na katika mashinani na ikiwa tunaelekea siku ya vijana duniani nampisha tutasikia ujumbe wa kijana Najma Mohamed kutoka Tanzania ambaye ni bingwa wa haki za watoto kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia watoto UNICEF.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
4-8-2023 • 0
António Guterres aunda Bodi ya Ushauri wa Kisayansi
Hatimaye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametimiza ahadi yake ya kuunda Bodi ya Umoja wa Mataifa ya Ushauri wa Kisayansi wakati huu ambapo teknolojia ya Akili Mnemba au ‘Artificial Intelligence’ imeshaanza kugonganisha vichwa vya watu kuhusu nafasi yake katika maendeleo duniani. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Guterres Bodi hii mpya aliyoiunda ni kwa ajili ya kuwashauri viongozi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mafanikio katika sayansi na teknolojia na jinsi ya kutumia manufaa ya maendeleo haya na kupunguza hatari zinazoweza kutokea. Bwana Guterres anaamini maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia yanaweza kuunga mkono juhudi za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu lakini pia yanaleta wasiwasi wa kimaadili, kisheria na kisiasa, wasiwasi ambao unahitaji ufumbuzi wa kimataifa. Bodi ya Umoja wa Mataifa ya Ushauri wa Kisayansi ambayo Bwana Guterres anaamini pia kuwa itaimarisha jukumu la Umoja wa Mataifa kama chanzo cha kuaminika cha data na ushahidi wa kisayansi itajumuisha kundi la Maprofesa wanasayansi saba mashuhuri duniani. Maprofesa hao ni Profesa Yoshua Bengio, Profesa Sandra Díaz, Profesa Saleemul Huq, Profesa Fei-Fei Li, Profesa Alan Lightman, Profesa Thuli Madonsela, na Profesa Thomas C. Südhof. Pia kundi jingine ni Wanasayansi Wakuu wa mashirika tofauti ya Umoja wa Mataifa, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Umoja wa Mataifa, na Mjumbe wa Katibu Mkuu kuhusu Teknolojia. Mmoja wa wanaounda Bodi hiyo, Profesa Yoshua Bengio, Mkurugenzi wa Kisayansi wa Taasisi ya Mila - Quebec AI ambaye pia ni Mkufunzi katika Chuo Kikuu cha Montréal anatoa ahadi akisema, “Uamuzi wa Katibu Mkuu wa kuanzisha Bodi ya Ushauri wa Kisayansi unasisitiza kujitolea bila kuyumba kwa viongozi wa Umoja wa Mataifa kwa kanuni za mbinu za kisayansi. Ninatazamia kumuunga mkono Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika kupaza sauti kwa ajili ya sera zinazotegemea sayansi na kufanya uamuzi.” Kupitia juhudi zao za ushirikiano, Bodi na Mtandao wake utawaunga mkono viongozi wa Umoja wa Mataifa katika kutazamia, kuzoea, na kutumia maendeleo ya hivi karibuni ya kisayansi katika kazi yao kwa watu, sayari na ustawi. Bodi itafanya kazi kama kitovu cha mtandao wa mitandao ya kisayansi. Lengo ni kuwa na muunganiko bora kati ya jumuiya ya kisayansi na kufanya uamuzi katika Umoja wa Mataifa. Kwa upande wake Bi. Ismahane Elouafi, Mwanasayansi Mkuu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo anasema, "Kwa kuhakikisha kwamba sera na programu za Umoja wa Mataifa zimeanzishwa kwa msingi wa ushahidi na utaalamu bora wa kisayansi uliopo, Bodi itachukua jukumu muhimu katika kutatua matatizo changamano ya kimaadili, kijamii na kisiasa yanayowasilishwa na maendeleo ya haraka ya kisayansi na kiteknolojia." Ikumbukwe mwezi Julai mwaka huu, kwa mara ya kwanza Baraza la Usalama lilikuwa na mjadala mahususi kuhusu Akili Mnemba na mstakabali wake katika amani na usalama duniani na kabla yake, Katibu Mkuu Antonio Guterres kupitia moja ya matamko yake ya kisera ya Ajenda Yetu ya Pamoja, alitoa ahadi ambayo imetimia kwa kuunda Bodi hii ya kumshauri katika masuala ya kisayansi.
4-8-2023 • 0
03 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunakupeleka nchini DRC ambako MONUSCO, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC uko kwenye mchakato wa kuondoka nchini humo na kukabidhi jukumu la ulinzi na usalama kwa serikali. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kutoka UNITAMS, FAO na nchini Haiti. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na nitakupeleka kwake Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili Zanzibar, BAKIZA nchini Tanzania, salía papo hapo tafadhali! Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia kipindi cha mpito nchini Sudan, (UNITAMS) umesema una wasiwasi mkubwa kuhusu athari kubwa kwa raia katika eneo la Darfur kutokana na mapigano kati ya Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vinavyoungwa mkono na wanamgambo wa Kiarabu dhidi ya Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan (SAF). Ripoti zinaonesha kuwa raia wanazuiwa kuondoka kwenda maeneo salama.Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) limetahadharisha kuhusu kuongezeka kwa janga la chakula nchini Sudan. Kulingana na tathimini ya hivi karibuni ya hali ya uhakika wa chakula (IPC), zaidi ya watu milioni 20.3, wanaowakilisha zaidi ya asilimia 42 ya watu wote nchini humo wanakabiliwa na viwango vya juu vya uhaba wa chakula (IPC ngazi ya 3 au zaidi) kati ya Julai na Septemba mwaka huu 2023.Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na wanasheria Margaret Satterthwaite leo ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusu shambulio la kikatili lililomlenga Jaji wa nchini Haiti Haiti Wilner Morin, ambaye gari lake lilipigwa risasi katika mji mkuu wa Port-au-Prince miezi michache iliyopita. Morin ni jaji wa Mahakama ya Mwanzo ya Port-au-Prince, ambaye anachunguza kesi kadhaa za ufisadi zenye hadhi ya juu.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili nampisha Dkt. Mwanahija Ally Juma Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA akitufafanualia maana ya neno “NDEKWA”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
3-8-2023 • 0
Jifunze Lugha ya Kiswahili: Neno "NDEKWA"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA anatufafanualia maana ya neno “NDEKWA”.
3-8-2023 • 0
Maji ya kisima hiki ni jawabu kwa afya na kipato – Mwananchi Sudan Kusini
Kwa siku tatu, viongozi wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Mpango wa Chakula (WFP), Chakula na Kilimo (FAO) na Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo duniani, IFAD walikuwemo nchini Sudan Kusini kuona ni kwa jinsi gani miradi wanayotekeleza kwa pamoja ya kujenga mnepo na kuhakikisha lishe ya uhakika na bora imeleta mabadiliko. Wakazi wa Apada Boma jimboni Bahr el Ghazal Kaskazini nchini humo walikuwa taswira ya manufaa ya miradi hiyo ambayo wakuu hao walikagua kama inavyofafanua Makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi.
2-8-2023 • 0
02 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama nchini Sudan Kusini na mradi wa maji nchini Rwanda. Makala tunasalia huko huko Sudan Kusini na Mashinani tunakupeleka nchini Zimbabwe, kulikoni? Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Nicholas Haysom ametahadharisha kwamba muda unazidi kuyoyoma kuelekea Sudan Kusini kufanya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Desemba mwaka ujao wa 2024 lakini bado masuala muhimu ya kuufanya uchaguzi huo uende kama ulivyopangwa bila kuchelewa hayajakamilika.Balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF Vanessa Nakate amefanya ziara nchini Rwanda kujionea namna mradi wa pampu ya kuvutia maji inayotumia nishati ya umeme wa jua au Sola ilivyoleta manufaa kwa wanawake na wasichana barubaru 11,000 waliokuwa wakitembea umbali mrefu kusaka hmaji.Katika makala Assumpta Massoi anafuatilia ziara ya wakuu wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini.Na tunakupeleka nchini Zimbabwe ambako vijana wameweza sio tu kijikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini bali pia kuhifadhi mazingira na tutasikia kutoka kwa mmoja wao.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
2-8-2023 • 0
Nicholas Haysom: Hatua inahitajika sasa kwa ajili ya uchaguzi kwa wakati na wa huru na haki nchini Sudan Kusini
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS), Nicholas Haysom ametahadharisha kwamba muda unazidi kuyoyoma kuelekea Sudan Kusini kufanya uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwezi Desemba mwaka ujao wa 2024 lakini bado masuala muhimu ya kuufanya uchaguzi huo uende kama ulivyopangwa bila kuchelewa hayajakamilika."Ikiwa imesalia miezi 17 tu kwenye ratiba ya kuelekea uchaguzi wa mwaka 2024, narudia kile nilichokisema katika mkutano wa awali na waandishi wa habari, kwamba mwaka 2023 ni mwaka wa 'kutengeneza au kuvunja'," amesema Bwana Haysom mapema leo Agosti pili alipozungumza na vyombo vya Habari mjini Juba ambao ni mji mkuu wa nchi hiyo changa zaidi duniani. Ghasia miongoni mwa jamii za Sudan Kusini zinaendelea kuongezeka pamoja na shinikizo la kuongezeka kwa ufinyu wa rasilimali huku maelfu ya watu wakiendelea kuingia nchini humo wakikimbia mapigano katika nchi jirani ya Sudan. Kwa mujibu wa Bwana Haysom, miongoni mwa hatua muhimu ambazo inabidi zichukuliwe ni pamoja na hitaji la kuunda upya vyombo vitatu muhimu, ambavyo ni, Tume ya Kitaifa ya Marekebisho ya Katiba, Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi, na Baraza la Vyama vya Kisiasa; kukamilisha mipango ya mpito ya usalama; kuendeleza mchakato wa kudumu wa kutengeneza katiba; na kuunda nafasi za kiraia na kisiasa ambapo kila raia ana uhuru wa kujadili na kujihusisha na uchaguzi wa kisiasa na kikatiba bila woga. "Kufanya uchaguzi tu hakutoshi - uaminifu, uwazi na ushirikishwaji wa mchakato ndio unaoleta uhalali. Hii ni pamoja na kwamba vyama vya siasa lazima viweze kujiandikisha na kufanya kampeni kwa uhuru; asasi ya kiraia kwa ajili ya elimu ya uraia na kuwa waangalizi wa mchakato. Inajumuisha vyombo vya habari vinavyoweza kuripoti kuhusu mchakato huo na kutoa nafasi kwa sauti na maoni mbalimbali kwa wapiga kura kufanya uamuzi sahihi,” amesema Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini. Aidha Bwana Haysom amesisitiza kuwa UNMISS itaendelea kuiunga mkono Sudan Kusini katika michakato ya uchaguzi na uundaji wa katiba kwa kushirikiana na wadau wa kikanda kama vile Muungano wa Afrika (AU) na mamlaka ya pamoja ya kitaifa kwa ajili ya maendeleo kwenye eneo la Pembe ya Afrika (IGAD).
2-8-2023 • 0
Vanessa Nakate: Matumizi ya nishati safi yanasaidia wasichana kusalia shuleni
Balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto UNICEF Vanessa Nakate amefanya ziara nchini Rwanda kujionea namna mradi wa pampu ya kuvutia maji inayotumia nishati ya umeme wa jua au Sola ilivyoleta manufaa kwa wanawake na wasichana barubaru 11,000 waliokuwa wakitembea umbali mrefu kusaka hmaji. Ni Vanessa Nakate Balozi mwema wa UNICEF, raia wa Uganda ambaye pia ni mwanaharakati wa mabadiliko ya tabianchi akiwa Nyagashankara nchini Rwanda alikokwenda kutembelea mradi wa maji ambao hapo awali ulikuwa ukitumia mafuta ya diseli lakini saa unatumia nishati safi ya Sola. Akiwa kijijini hapo Vanessa alikutana na mabinti wawili Adele na Graciela ambao kabla ya mradi huu walikuwa wakitembea umbali mrefu kusaka maji …… na anaeleza kuwa, “Ilikuwa hatari kwao, tunajua kuwa kwa uwiano, wasichana na wanawake wanaathirika pakubwa na majanga ya tabianchi, kwa hiyo ni muhimu sana kuelewa kuwa tunavyopamba kupata haki kutokana na athari za mabadilko ya tabianchi ni kuwa pia tunapambana kwa haki ya kijinsia.”Vanessa anaikumbusha jamii kuwa wasichana hawana changamoto moja tu ndani ya jamii, utakuja binti ambaye anaathirika na mabadiliko ya tabianchi, huyo huyo anaweza kuacha shule au kukosa masomo hivyo kuleta majawabu mtambuka kunasaidia kutatua changamoto nyingi ndani ya jamii. “Kuwa na mashine ya kuvuta maji inayotumia umeme wa Sola ambao unawarahisishia kupata maji sio tu unasaidia kuhakikisha wasichana wanasalia shuleni lakini pia inawasaidia kuwa na maono ya dunia bora zaidi. “Vanessa anahitimisha kwa kueleza kuwa ili kuhakikisha wanajamii wengi zaidi wananufaika na miradi kama hii ya maji lazima kuwepo na miradi mingi kama hii na hilo litawezekana iwapo watapata uwezeshaji wa kifedha na rasilimani nyingine nah apo wasichana wengi watakuwa wamehakikishiwa kuendelea kusalia shuleni.
2-8-2023 • 0
01 AGOSTI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo mradi wa serikali ya DRC na UN Women wajengea uwezo wajasiriamali Goma. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kutoka IFAD, FAO, WHO na UNICEF ikiwa ni pamoja na Tamko la Haki za binadamu. Mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni? Ikiwa leo ni mwanzo wa Wiki ya Kimataifa ya Unyonyeshaji Maziwa ya Mama kwa mtoto, kaulimbiu ikiwa, "Tufanye unyonyeshaji kazini, ufanye kazi" Mashirika ya Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) na la Afya Ulimwenginu (WHO) wanasisitiza haja ya usaidizi mkubwa wa unyonyeshaji katika sehemu zote za kazi ili kuendeleza na kuboresha maendeleo katika viwango vya unyonyeshaji duniani kote huku ushauri wao ukijumuisha likizo ya uzazi yenye malipo ikiwezekana kwa muda wa miezi sita au zaidi baada ya kujifungua.Wakuu wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa, lile la Chakula na Kilimo (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wameonya leo walipokuwa wakihitimisha ziara ya siku tatu nchini Sudan Kusini kuwa madhara ya kutochukua hatua katika kushughulikia majanga tata ya chakula, tabianchi na ukosefu wa usalama nchini humo yatajitokeza katika kupoteza maisha, ustawi na mustakabali wa mamilioni ya watu katika taifa hilo changa duniani.Na tukiendelea na ufafanuzi wa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75, Mwanasheria wa Haki za Binadamu nchini Tanzania, Wakili Jebra Kambole anafafanua ibara ya 6 ya tamko hilo.Na mashinani tutamsikia Mkuu wa Operesheni wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya kibinadamu pamoja na kuratibu masuala ya dharura OCHA aliyetembelea kambi za wakimbizi wa ndani nchini Sudan.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
1-8-2023 • 0
Je unafahamu kuwa kuna fursa ya ufadhili katika nishati safi na salama Tanzania?
Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mfuko wa maendeleo ya mitaji UNCDF wakizingatia Utafiti wa Bajeti ya Kaya Tanzania Bara (2017/18), upatikanaji wa nishati safi na teknolojia ya kupikia ni asilimia 17.1 tu ya wakazi wa mijini na asilimia 2 ya wakazi wa vijijini. Kuongezeka kwa mahitaji ya nishati ya kuni kunatokana na ukuaji wa haraka wa miji, bei ya juu, na upatikanaji mdogo wa nishati mbadala. Ili kuondokana na changamoto hizi, Programu ya CookFund ambayo inatekelezwa chini ya UNCDF kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati nchini Tanzania, ina nia kuongeza idadi ya watu kwa kutumia suluhu endelevu za nishati safi ya kupikia katika maeneo ya mijini. Tayari awamu ya kwanza ya ufadhili imeenda kwa makampuni 16 kama anavyosimulia Anold Kayanda katika makala hii.
31-7-2023 • 0
Sera za MPOWER zaepusha watu kuvutishwa sigara bila ridhaa yao- WHO
Miaka 15 baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO kuanzisha sera ya kulinda umma kutoathirika na uvutaji wa sigara unaofanywa na mtu mwingine, zaidi ya watu bilioni 5.6 wamenufaika na sera hiyo ulimwenguni kote, imesema ripoti mpya ya shirika hilo iliyotolewa leo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Assumpta Massoi. Idadi hiyo ni sawa na kusema kuwa asilimia 71 ya watu ulimwengu kose sasa wamelindwa na athari ambazo wangeweza kuzipata kutokana na mtu mwingine kuvuta sigara karibu yake. Na iwapo kusingekuwa na sera hizo zaidi ya watu milioni 300 wangekuwa wametumbukia katika uvutaji moshi wa sigara bila wao kuvuta wenyewe. Akizindua ripoti hiyo ya 9 ya janga la uvutaji tumbaku ulimwengu hii leo jijini Geneva Uswisi, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema mikakati 6 iliyopendekezwa kuwa sera imeanza kuleta mafanikio ambapo watu 7 kati ya 10 ulimwenguni wanalindwa na angalau Sera moja. Dkt. Tedros amesema “takwimu hizi zinaonesha japo ni polepole lakini kwa hakika, watu wengi zaidi wanalindwa dhidi ya madhara ya tumbaku kwa kutumia sera za utendaji bora za WHO zilizotungwa kwa msingi wa ushahidi.” Sera hizo ziitwazo MPOWER zinataka serikali kuweka mikakati sita ya kudhibiti tumbaku ambayo ni Mosi; Fuatilia sera za matumizi na uzuiaji wa tumbaku, Pili; kuweka kinga ya kulinda watu dhidi ya moshi wa tumbaku, Tatu; kutoa usaidizi wa wale wanaotaka kuacha matumizi ya tumbaku; Nne,kuelimisha watu kuhusu hatari za tumbaku, Tano; kuweka marufuku ya utangazaji, ukuzaji na udhamini wa bidhaa za tumbaku na sita; kuongeza ushuru kwa bidhaa za tumbaku. Nchi za Brazil na Uturuki zilifanikiwa kutekeleza sera hizo kwa viwango vya juu na leo Mkuu huyo wa WHO amezipongeza nchi ya Mauritius kwa kuwa nchi ya kwanza barani Afrika, na Uholanzi kwa kuwa ya kwanza katika Muungano wa Ulaya kutekeleza mpango kamili wa sera hizo za kudhibiti matumizi ya tumbaku. WHO pia imeeleza ipo tayari kuunga mkono nchi zote kufuata mfano wao na kuwalinda watu wao kutokana na janga hili baya.
31-7-2023 • 0
Mradi wa "Njoo shuleni" nchini Kenya warejesha matumaini kwa familia
Elimu ni moja ya nyenzo zenye nguvu zaidi za kuleta mabadiliko kwa watu binafsi na jamii na ndio maana katika miongo miwili iliyopita, serikali ya Kenya imefanya mageuzi mengi ili elimu ya msingi iwe bure na ya lazima kwa watoto wote walio katika umri wa kwenda shule. Hata hivyo, watoto wengi bado hawako shuleni kutokana na umaskini, miundombinu duni, kutelekezwa na wazazi na matatizo ya kiafya hasa katika maeneo masikini. Sasa shirika la Umoja la kuhudumia watoto UNICEF limeamua kuingilia kati kwa kushirikiana na wadau kusaidia. Flora Nducha na maelezo zaidi.Katika Kaunti ya Dandora jijini Nairobi ambako wakazi wengi ni walala hoi, watoto kwenda shule ni mtihani unaoanzia kwa wazazi kama Wambui Kahiga mama wa Octavia mtoto mwenye umri wa miaka 10.Wambui anasema, “shida zangu kubwa sasa hivi ni chakula, mavazi , kulipa gharama za shule na ghara za kulipia nyumba. Kibarua ninachopata wakati huu ni cha kufua nguo na hakiaminiki kuna wakati napata na kuna wakati nakosa. Najihisi vibaya kwani ingekuwa mapenzi yangu , Octavia angekuwa alianza shule kitambo.”Kwa mujibu wa UNICEF umasikini ndio sababu kubwa inayowafanya wazazi kushindwa kuwapeleka watoto shule na sasa shirika hilo linashirikiana na wakfu wa Elimisha mtoto (EAC) na wanaendesha programu ya elimu zaidi ya yote kupitia mradi wa “Njoo shuleni” ili kuwafikia watoto wote kama Octavia na kuhakikisha wanapata haki ya elimu.Elizabeth Waitha ni afisa elimu wa UNICEF Kenya anasema “mara tunapobaini watoto ambao hawana fursa ya elimu, tunawasajili na tunaweza kuwasaidia na vifaa vya shule ambavyo vinapunguza mzigo kwa wazazi kuweza kuwasaidia watoto wao kwa ajili ya kusoma”.Na hii inaleta faja na matumaini kwa watoto na wazazi kama kwa mama wa Octavia akisema, “Octavia yuko shuleni , na sasa ambavyo anasoma naona maisha yake yatabadilika , yatakuwa maziri hata mimi atakuja kuniinua.”Kwa UNICEF “Elimu ni haki ya msingi ya binadamu na kila mtoto anapaswa na anahitaji fursa ya kupata elimu na uelimishaji mkubwa unahitajika kuhakikisha kwamba kila mtoto anasoma.”Kulingana na takwimu za Educate A Child (EAC) kuna watoto milioni 1.3 wa umri wa kati ya miaka 6 hadi 13 ambao hawasomi nchini Kenya.Mradi huu unafadhiliwa na mfuko kwa ajili ya maendeleo wa serikali ya Qatar na unatekelezwa katika kaunti 16 nchini Kenya ambazo ni Baringo, Bungoma, Garissa, Isiolo, Kajiado, Kilifi, Kwale, Mandera, Marsabit, Narok, Samburu, Tana River, Turkana, Wajir, West Pokot, na katika makazi yasiyo rasmi ya jijini Nairobi.
31-7-2023 • 0
31 JULAI 2023
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akimulika masuala ya afya hususan mafanikio ya será za kudhibiti uvutaji sigara na tumbaku; elimu kwa watoto waliokosa fursa huko Kenya; nishati salama nchini Tanzania na ujumbe wa Romeo George mwanaharakati wa SDGs.Miaka 15 baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO kuanzisha sera ya kulinda umma kutoathirika na uvutaji wa sigara unaofanywa na mtu mwingine, zaidi ya watu bilioni 5.6 wamenufaika na sera hiyo ulimwenguni kote, imesema ripoti mpya ya shirika hilo iliyotolewa leo.Nchini Kenya, UNICEF na wadau wameibuka na mradi wa kusaidia watoto waliokosa fursa ya elimu kurejea tena shuleni.Makala: Mradi wa COOKFUND unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mfuko wa mitaji ya maendeleo, UNCDF nchini Tanzania wasongesha nishati safi na salama.Mashinani: Romeo George ajulikanye kama RJ, Mwigizaji na mwanaharakati wa malengo ya maendeleo endelevu nchini Tanzania anayehudumu chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR akitaka wakimbizi wapatiwe fursa sawa katika ufanikishwaji wa malengo hayo.
31-7-2023 • 0
Kutoka Dodoma Tanzania Bara hadi Paje, Zanzibar kukabiliana na umaskini
Moja ya malengo ya Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu, SDGs ni kutokomeza umaskini ifikapo mwaka 2030. Ikiwa imesalia miaka 7 kabla ya kufikia ukomo, nchi, jamii na kila mtu mmoja mmoja anachukua hatua kutokomeza umaskini hasa kuanzia ngazi ya familia. Umaskini unasababisha watu washindwe sio tu kupata mlo bali pia kupeleka watoto wao shuleni kupata elimu bora. Nchini Tanzania, hususan visiwani Zanzibar katika mkoa wa Kusini Unguja Assumpta Massoi katika pita ya hapa na pale alikutana na mwananchi mmoja ambaye ameamua kuvuka baharí ya Hindi kutoka Bara hadi visiwani kukabiliana na umaskini. Ungana naye basi Assumpta Massoi katika makala hii.
28-7-2023 • 0
Hali si swari Burkina Faso msirejeshe wakimbizi wake: UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, leo limetoa mwongozo mpya juu ya ulinzi wa watu wanaokimbia Burkina Faso, na wito wa haraka kwa mataifa yote kuacha kuwarudisha kwa nguvu watu wote wanaotoka katika ukanda huo ulioathiriwa zaidi na mgogoro unaoendelea nchini humo na badala yake kuwaruhusu raia wanaokimbia Burkina Faso kuingia katika mipaka yao. Huku hali ya usalama nchini Burkina Faso ikiendelea kuzorota, UNHCR imesema ina wasiwasi mkubwa kutokana na kuenea kwa hali ya ukosefu wa usalama na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofanywa dhidi ya raia.Ukwiukwaji huo ni pamoja na mauaji, kutoweshwa kwa lazima, mateso na utekaji nyara. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva uswis hii leo Elizabeth Tan, mkurugenzi wa ulinzi wa kimataifa wa UNHCR amesema: “Katika matukio kadhaa, raia wamekuwa wakilengwa na kuuawa, na hivyo kusababisha vifo vingi vya raia na watu kutawanywa. Watoto pia wanakabiliwa na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, kama vile kuajiriwa kwa nguvu vitani na makundi yenye silaha, ajira ya watoto, pamoja na aina nyingine za unyanyasaji, ukatili, unyonyaji na unyanyasaji wa kijinsia."Ameongeza kuwa asilimia kubwa ya watu wanaotawanywa ni watoto, shule nyingi zimelazimika kufungwa na takriban asilimia 82 ya wasichana wanakabiliwa na ukatili wa kijinsia, lakini pia mamilioni wanahitaji msaada.Anasema "Takriban watu milioni 4.7 kote nchini wanahitaji msaada wa kibinadamu, na ikiwa ni zaidi ya asilimia 20 ya wakazi wote wa nchi hiyo."Kwa mujibu wa UNHCR vita na machafuko pia vimesambaratisha mioundombinu na kuathiri huduma za serikali na taasisi ikiwemo katika maeneo yaliyoathirika na vita na hali ni mbayá zaidi kwa watu wanaoishi katika miji ambayo makundi yenye itikadi Kali yanazuia watu ikiwemo idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani.Hadi kufikia Juni mwaka huu wa 2023, zaidi ya watu 67,000 kutoka Burkina Faso wamesaka hifadhi katika nchi jirani kama vile Mali, Niger, Ivory Coast, Togo, Benin na Ghana, huku zaidi ya watu milioni 2 wakiwa wakimbizi wa ndani katika nchi yao, na kuufanya mzozo huo kuwa moja ya mizozo mibaya zaidi yawakimbizi wa ndani katika bara la Afrika.
28-7-2023 • 0
28 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia afya na hali ya usalama na msaada wa kibinadamu nchini Burkina Faso. Makala tnamulika harakati za kufanikisha SDGs na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni? Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, leo limetoa mwongozo mpya juu ya ulinzi wa watu wanaokimbia Burkina Faso, na wito wa haraka kwa mataifa yote kuacha kuwarudisha kwa nguvu watu wote wanaotoka katika ukanda huo ulioathiriwa zaidi na mgogoro unaoendelea nchini humo na badala yake kuwaruhusu raia wanaokimbia Burkina Faso kuingia katika mipaka yao.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus kupitia ujumbe wake kwa Siku ya Kimataifa ya Homa ya Ini inayoadhimishwa kila Julai 28, amesema kwa kuwa wanadamu tunaishi mara moja na tuna ini moja, WHO imejitolea kushirikiana na nchi zote na wadau wote ili kutimiza maono ya pamoja ya kutokomeza virusi vya homa ya ini ifikapo 2030.Katika makala Assumpta Massoi anaangazia harakati za kufanikisha malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs hususan kutokomeza umaskini na kujiinua kiuchumi.Na mashinani tutaelekea kaunti ya Turkana nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani ukame umeathiri utoaji wa huduma za afya ya uzazi kwa wanawake na wasichana.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
28-7-2023 • 0
Dkt. Tedros - Tunaishi mara moja na tuna ini moja, tutokomeze Homa ya Ini
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus kupitia ujumbe wake kwa Siku ya Kimataifa ya Homa ya Ini inayoadhimishwa kila Julai 28, amesema kwa kuwa wanadamu tunaishi mara moja na tuna ini moja, WHO imejitolea kushirikiana na nchi zote na wadau wote ili kutimiza maono ya pamoja ya kutokomeza virusi vya homa ya ini ifikapo 2030. “Kila mwaka, homa ya ini inayosababishwa na virusi inaua zaidi ya watu milioni moja, na zaidi ya watu milioni tatu wapya wanaambukizwa. Tunajua namba hizi ni za chini ya makadirio. Mamilioni ya watu ulimwenguni kote wana homa ya ini ambayo haijatambuliwa na ambayo haijatibiwa. Mara nyingi, ugonjwa huendelea bila kutambuliwa mpaka dalili zinakuwa mbaya.” Hata hivyo Dkt. Tedros anaeleza habari njema akisema, “Sasa tuna zana bora zaidi za kuzuia, kutambua na kutibu homa ya ini. Duniani kote, WHO inaunga mkono nchi kupanua matumizi ya zana hizo, ili kutokomeza homa ya ini na kuokoa maisha.” Anayoyasema Mkuu huyu wa WHO tayari yameanza kuzaa matunda katika baadhi ya nchi. Mathalani barani Afrika, wizara ya Afya ya Uganda, kwa msaada wa kiufundi kutoka WHO, ilibuni mkakati wa kudhibiti homa ya ini ya B, ikijumuisha uhamasishaji wa umma, upimaji na matibabu nchini kote. Hadi kufikia sasa watu milioni 4 wamefanyiwa uchunguzi wa ugonjwa huo na zaidi ya asilimia 30 ya watu walioambukizwa homa ya ini ya B wanafahamu hali zao na wanaweza kupata huduma za matibabu ya kina, ikiwa ni pamoja na dawa za bure. Tags: Homa ya Ini, Virusi vya Homa ya Ini, Hepatitis, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus, Siku za UN
28-7-2023 • 0
27 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Jacqueline Woiso, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania anafafanua ni malengo yapi ya Maendeleo Endelevu yaliyoipa Multichoice Tanzania Ushindi wa Tuzo ya UN Global Compact. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya hali ya hewa, jaribio la kutaka kutwaa madaraka kijeshi nchini Niger na uhifadhi wa bioanuwai barani Afrika. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakuletea maana ya neno “NDOFYA". Kufuatia ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa WMO kwa kushirikiana na lile la Kamisheni ya Muungano wa Ulaya ambayo imethibitisha kuwa mwezi huu wa Julai utavunja rekodi ya dunia ya kuwa na joto kali ulimwenguni kote, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema takwimu hizi mpya ni uthibitisho kuwa ubinadamu umeketi katika kiti cha moto na kwamba lazima hatua zichukuliwe haraka.Tukitoka Marekani tuelekee Geneva Uswisi ambako Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ameshtushwa, amehuzunishwa na kulaani vikali jaribio la kutaka kutwaa madaraka kijeshi nchini Niger lililofanyika hapo jana.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limekaribisha mchango wa zaidi ya dola milioni 27 uliotolewa na Muungano wa Ulaya kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya uhifadhi wa bioanuwai barani Afrika.Na Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili nampisha Dkt. Mwanahija Ally Juma Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA akitufafanualia maana ya neno “NDOFYA".Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
27-7-2023 • 0
Je wajua maana ya neno "NDOFYA?" - Dkt. Mwanahija Ally Juma
Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili nampisha Dkt. Mwanahija Ally Juma Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA akitufafanualia maana ya neno “NDOFYA".
27-7-2023 • 0
Kutana na Timu ya Taifa ya Kandanda ya Wanawake ya Afghanistan - Wakimbizi katika Michezo
“Tunajaribu kuleta michezo na nguvu zake katika mazingira magumu sana ya watu wasiojiweza. Mchezo ni mzuri kwa kuwapa watu matumaini ya siku zijazo.” Anasema Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) akirejelea Timu ya mpira wa miguu ya wanawake wakimbizi wanaoishi nchini Australia baada ya kuokoa maisha yao yaliyokuwa hatarini nchini mwao Afghanistan. Anold Kayanda anasimulia zaidi.
26-7-2023 • 0
Hospitali Sudan zaomba usaidizi
Vita nchini Sudan ambayo sasa imedumu kwa zaidi ya siku 100 imeshuhudia zaidi ya watu milioni 3 wakiyakimbaia makazi yao kwenda kusaka hifadhi katika miji mingine pamoja na nchi Jirani. Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA inaanza kwa kuonesha chupa cha upasuaji ambako mjamzito amefanyiwa upasuaji na kujifungua salama huko katika mji Port Sudan jimboni Red Sea mashariki mwa nchi ya Sudan.Hapo awali, hospitali hiyo ilikuwa ikipokea wajawazito 300 mpaka 450 wanaojifungua kwa njia ya kawaida na wale wanaohitaji upasuaji walikuwa takriban 300 kwa mwezi. Daktari Randa Osman ni Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo ya Wazazi ya Port Sudan anasema “Idadi ya sasa ni kubwa zaidi kwa sababu ya ongezeko la watu wanaokimbilia katika jimbo hili.” Dokta Randa anaendelea kwa kusema wajawazito na watoto wachanga wanakabiliwa na ufikiaji finyu wa huduma muhimu za afya. “Hospitali hii ya kujifungulia ndio pekee iliyopo katika mji huu na inatoa huduma za dharura za uzazi, uangalizi baada ya kujifungua na upasuaji. Hospitali imekuwa ikipokea idadi kubwa ya wagonjwa na mzigo wa kazi umeongezeka mara mbili. Watendaji wetu wanafanya kazi bila kuchoka kuwahudumia wakimbizi wanaokaa katika makazi ya muda ya wakimbizi.” Daktari huyu anahitimisha kwa kueleza kile wanachohitaji? “Tunahitaji vifaa tiba zaidi kwakuwa idadi ya wagonjwa ni zaidi ya mara mbili. Na pia tunahitaji kuongeza juhudi ili kukabiliana na hitaji hili kubwa linalozidi kuongezeka.”Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA linafanya kila juhudi kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa na wadau kuhakikisha wanawasaidia watu wote wenye uhitaji.
26-7-2023 • 0
UNESCO inasema teknolojia itumike kwa manufaa ya mwanadamu na sio kuwa mbadala wake: Ripoti
Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO kuhusu ufuatiliaji wa teknolojia katika elimu GEM 2023 imetaka mifumo ya elimu kote duniani siku zote kuhakikisha kwamba matakwa ya wanaojifunza yanakuwa katika kitovu cha teknolojia na kwamba teknolojia zitumike kusaidia elimu inayotokana na mwingiliano wa binadamu badala ya kulenga kuwa mbadala wake. Ripoti hiyo mwaka 2023 ya GEM inashughulikia matumizi ya teknolojia katika elimu duniani kote kupitia muktadha wa umuhimu, usawa, uthabiti na uendelevu.UNESCO inasema teknolojia inabadilika haraka kuliko inavyowezekana kutathminiwa na bidhaa za teknolojia ya elimu hubadilika kila baada ya miezi 36, kwa wastani huku ushahidi mkubwa ukitoka katika nchi tajiri zaidi.Mathalani ripoti inasema “Nchini Uingereza, asilimia 7 ya makampuni ya teknolojia ya elimu yalikuwa yamefanya majaribio yaliyodhibitiwa bila mpangilio, na asilimia 12 yalikuwa yametumia uthibitishaji wa watu wengine. Pia utafiti uliofanywa kwa walimu na wasimamizi katika majimbo 17 ya Marekani ulmeonyesha kuwa ni asilimia 11 tu waliomba tathimini ya ushahidi kabla ya kupitishwa.Katika miaka 20 iliyopita, wanafunzi, waelimishaji na taasisi wamepitisha na kukumbatia kwa kiasi kikubwa zana za teknolojia ya kidijitali.Audrey Azoulay, mkurugenzi mkuu wa UNESCO anaonya kwamba "Mapinduzi ya kidijitali yana uwezo usiopimika lakini, kama vile onyo ambavyo limekuwa likitolewa kuhusu jinsi yanavyopaswa kudhibitiwa katika jamii, tahadhari sawa lazima izingatiwe jinsi mapinduzi hayo yanavyotumiwa katika elimu. Matumizi yake lazima yawe kwa ajili ya uzoefu ulioimarishwa wa kujifunza na kwa ajili ya ustawi wa wanafunzi na walimu, si kwa madhara kwao. Matakwa ya mwanafunzi yawe kipaumbele cha kwanza na yawasaidie walimu. Kuunganishwa mtandaoni sio mbadala wa mwingiliano wa wanadamu.”Azoulay amesisitiza kuwa “Kutumia teknolojia kunaweza kuboresha baadhi ya aina za kujifunza katika baadhi ya miktadha. Ripoti hiyo inataja ushahidi unaoonyesha kuwa manufaa ya kujifunza hutoweka ikiwa teknolojia itatumiwa kupita kiasi au kutokuwepo kwa mwalimu aliyehitimu. Kwa mfano, kusambaza kompyuta kwa wanafunzi hakuboreshi hali ya kujifunza ikiwa walimu hawatahusika katika tajriba ya ufundishaji. Simu za rununu shuleni pia zimeonekana kuwa kero katika kujifunza, lakini ni chini ya robo ya nchi tu ndizo zimepiga marufuku matumizi ya simu hizo shuleni.”Duniani kote ripoti imesema idadi ya watu wanaotumia mtandao wa intaneti imeongezeka kutoka asilimia 16 mwaka 2005 hadi asilimia 66 mwaka 2022.
26-7-2023 • 0
26 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNESCO kuhusu teknolojia na pia afya ya wanawake wajawazito nchini Sudan. Makala tunakupeleka nchini Australia na mashinani Roma nchini Italia, kulikoni? Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO kuhusu ufuatiliaji wa teknolojia katika elimu GEM 2023 imetaka mifumo ya elimu kote duniani siku zote kuhakikisha kwamba matakwa ya wanaojifunza yanakuwa katika kitovu cha teknolojia na kwamba teknolojia zitumike kusaidia elimu inayotokana na mwingiliano wa binadamu badala ya kulenga kuwa mbadala wake.Vita nchini Sudan ambayo sasa imedumu kwa zaidi ya siku 100 imeshuhudia zaidi ya watu milioni 3 wakiyakimbaia makazi yao kwenda kusaka hifadhi katika miji mingine pamoja na nchi Jirani.Makala tunaangazia Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wanawake ambao wako ukimbizini Australia baada ya kuukimbia utawala wa Taliban nchini mwao Afghanistan.Na katika mashinani ikiwa mkutano wa viongozi kuhusu mifumo ya upatikanaji wa chakula unakunja jamvi leo huko Roma nchini Italia tutasikia ujumbe unaotaka jumuiya ya kimataifa kubuni njia mpya za kukabiliana na changamoto za ukosefu wa chakula.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
26-7-2023 • 0
25 JULAI 2023
Hii leo jaridani mada kwa kina ambapo wakimbizi kutoka nchini Rwanda na Burundi wanaopata hifadhi katika nchi Jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wamepata matumaini mapya ya maisha baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na shirika lisilo la kiserikali ya AIDES kuwawezesha kuanzisha mradi wa kazi za Sanaa ambao unawasidia kujikimu kimaisha pamoja na familia zao. Ashinani tutaelekea Bahari ya Shamu au Red Sea, kulikoni? Hatimaye operesheni kubwa imeanza leo huko Yemen ya kupakua mapipa ya mafuta ghafi kutoka meli ya FSO Safer iliyoanza kuoza kwenda meli ya Nautica au Yemen katika pwani ya bahari ya Shamu.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuzuia watu kuzama majini, shirika la Umoja wa MAtaifa la chakula na kilimo, FAO limesema linatumia siku hii kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kuelimisha umma juu ya kuzama majini hasa katika sekta ya uvuvi.Nchini Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA linaendesha semina kuhusu ukatili wa kijinsia na kingono ili kusaidia manusura ambao wanakabiliwa na vitendo hivyo wakati wakirejea nyumbani kutokana na mapigano yanayoendelea nchini Sudan.Mashinani tutamsikia Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNEP hatua iliyoanza asubuhi ya leo kwa saa za Yemen ya kuhamisha mafuta yaliyokuwa yanahatarisha usalama kwenye Bahari ya Shamu au Red Sea.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
25-7-2023 • 0
WD2023 imeonesha kuwa wanawake tunachukua hatua mashinani - Martha Wanza
Mkutano wa kimataifa wa Women Deliver 2023 (WD2023) au wanawake wanatekeleza umekunja jamvi mwishoni mwa wiki mjini Kigali nchini Rwanda baada ya kuwaleta pamoja washiriki 6,000 ana kwa ana na wengine zaidi ya 200,000 mtandaoni. Lengo kuu la mkutano huo mkubwa kabisa uliozanza Julai 17 hadi 20 na kubeba kaulimbiu “Nafasi, mshikamano na suluhu” lilijikita katika ujumuishwaji ili kusongesha usawa endelevu wa kijinsia kwa kuhusisha sekta mbalimbali. Wadau wakiwemo wakuu wa nchi na serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo linalohusika na masuala ya wanawake UN-Women na la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA walikuwa mstari wa mbele katika mkutano huo Martha Wanza alikuwa miongoni mwa washiriki kutoka Kenya , anafanyakazi na shirika lijulikanalo kama Jumuiya ya wanawake vijana Wakristo nchini humo YWCA. Amezungumza na Eugene Uwimana Afisa uratibu msaidizi wa maendeleo, mawasiliano na mipango katika ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda , maswali yake ynarejewa studio na Flora Nducha na Martha akianza kwa kumfafanulia kuhusu shirika lao
Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF limekunja jamvi mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya siku 10 za tathimini ya utekelezaji wa malengo hayo au SDGs. Mhandisi Mwanaisha Ulenge ambaye ni Mbunge katika Bunge la Tanzania na pia Mjumbe wa Bunge la Dunia IPU, mmoja wa walioshiriki Jukwaa hilo la Umoja wa Mataifa la Ngazi ya juu la kisiasa kuhusu SDGs, akihojiwa na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York, Marekani ametoa wito kwa wanawake ulimwenguni kote kwamba wao pia wanapaswa kuwa na mchango katika kuleta usawa wa kijinsia kwanza kwa wao wenyewe kutojiwekea mipaka. Lakini kwanza Mwanaisha Ulenge anaanza kwa kueleza ushiriki wa wabunge katika jukwaa hili la HLPF akisema, “Kikao hiki ambacho tumeshiriki hapa katika Umoja wa Mataifa (New York, Marekani) ni kikao ambacho kinaangazia namna ambavyo Bunge la Tanzania limeweza kuisimamia serikali katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Ndilo lilikuwa lengo kubwa kama Bunge kuangalia ni namna gani ambavyo serikali imeweza kutekeleza. Kwa hiyo serikali pia wameleta watu wao wamewasilisha lakini na Bunge sisi tumewasilisha namna ambavyo tumeisimamia serikali katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia.” Na kwa kuwa yeye ni mbunge mwanamke na wakati huo huo bado kuna changamoto kwa wanawake kuzifikia nafasi hizo za kushiriki katika ngazi za maamuzi, Mhandisi Mwanaisha Ulenge ana ujumbe kwa wasichana na wanawake kote ulimwenguni kuhusu mchango wao kufanikisha kuondoa pengo la usawa wa kijinsia. “Hakika usawa wa jinsia ni sehemu ya yale Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.” Anasema Mwanaisha akiongeza, “Kwa hiyo mimi niwaambie wanawake kwamba tuna uwezo sawa wa kuweza kuhudumu na kuweza kufanya makubwa kama jinsia nyingine. Mahali popote pale mwanamke ukiweka dhamira ya dhati kabisa katika kulifanya jambo kwa dhamira kubwa na pana inawezekana. Anahitimisha kwa kusema, “Tusijiwekee mipaka na wala tusiwe na woga.”
24-7-2023 • 0
Guterres ataja mambo matatu ya kufanikisha mifumo bora ya chakula duniani
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amezungumza kwenye mkutano wa viongozi kuhusu Mifumo ya Upatikanaji wa Chakula huko Roma, Italia hii leo akisema bado inastaajabisha kuwa katika dunia yenye utajiri bado kuna watu hawana chakula au wanakufa njaa, huku akipendekeza mambo makuu matatu ya kuzingatia ili kurekebisha mifumo hiyo. Assumpta Massoi na maelezo zaidiKatika hotuba yake ya kurasa 6, Katibu Mkuu amechambua ni kwa jinsi gani mifumo ya chakula duniani kuanzia shambani hadi mezani imesambaratika na kusababisha zaidi ya watu bilioni tatu wakose mlo wenye lishe, huku zaidi ya bilioni mbili wakiwa matipwatipwa na zaidi ya milioni 780 hawana chakula.Guterres amesema “bila ufadhili na msamaha wa madeni, nchi zinazoendelea zinahaha kuwekeza kwenye mifumo ya chakula itakayowezesha kufikishia wananchi wao lishe wanayohitaji kwa Maisha yenye afya. Kwingineko uzalishaji, ufungishaji na ulaji usio endelevu wa chakula unazidisha janga la tabianchi na kuzalisha theluthi moja ya hewa chafuzi, unatumia asilimia 70 ya maji na kupoteza bayonuai.”Ameenda mbali kuelezea jinsi hatua ya Urusi kujiondoa kwenye makubaliano ya kusafirisha nafaka na mbolea kupitia Bahari Nyeusi kumesababisha bei za vyakula kupanda na hivyo kuisihi Urusi kurejea kwenye makubaliano hayo.Ameieleza hadhira ya mkutano huo ulioandaliwa na Italia kuwa licha ya changamoto kwenye mifumo ya chakula, kuna nuru katika kuiboresha kwani tayari nchi zinaitikia wito wa mwaka 2021 wa kuboresha mifumo ya chakula.Nchi 100 zimewasilisha ripoti zao za jinsi ambavyo zinatunga sera na kujumuisha katika mipango ya kitaifa hatua za kuimarisha mifumo hiyo.Hata hivyo ili dunia iwe na mifumo bora na endelevu ya kuzalisha na kusambaza chakula na itakayofanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, Katibu Mkuu amependekeza mambo makuu matatu.Mosi; uwekezaji wa kiwango kikubwa kwenye mifumo ya chakula endelevu, yenye uwiano, afya na mnepo. Pili; serikali na sekta binafsi zishirikiane kujenga mifumo ya chakula itakayojali watu badala ya faida na tatu; kuhakikisha mifumo ya chakula haiharibu mazingira ya sayari dunia.
24-7-2023 • 0
24 JULAI 2023
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Leah Mushi akimulika mkutano wa mifumo ya chakula ulioanza leo Roma, Italia; Kauli ya mshiriki kutoka Tanzania kwenye mkutano uliomalizika hivi karibuni hapa makao makuu ya UN; Makala anabisha hodi Rwanda ilhali mashinani anakupeleka Tunisia.1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amezungumza kwenye mkutano wa viongozi kuhusu Mifumo ya Upatikanaji wa Chakula huko Roma, Italia hii leo akisema bado inastaajabisha kuwa katika dunia yenye utajiri bado kuna watu hawana chakula au wanakufa njaa, huku akipendekeza mambo makuu matatu ya kuzingatia ili kurekebisha mifumo hiyo.2. Mwanaisha Ulenge ambaye ni Mbunge katika Bunge la Tanzania na pia Mjumbe wa Bunge la Dunia IPU, mmoja wa walioshiriki Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Ngazi ya juu la kisiasa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs, lililokamilika wiki iliyopita akihojiwa na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa hapa jijini New York, Marekani ametoa wito kwa wanawake ulimwenguni kote kwamba wao pia wanapaswa kuwa na mchango katika kuleta usawa wa kijinsia kwanza kwa wao wenyewe kutojiwekea mipaka.3. Makala: Leo inatupeleka mjini Kigali Rwanda ambako mwishoni mwa wiki umekamilika mkutano wa kimataifa wa Women Deliver 2023 (WD2023) au wanawake wanatekeleza. Mkutano ulijikita na suala la ujumuishwaji ili kusongesha usawa endelevu wa kijinsia. Ulihudhuriwa na washiriki zaidi ya 200,000 mtandaoni na ana kwa ana, miongoni mwao ni Martha Wanza kutoka Kenya, anayefanyakazi na shirika la Jumuiya ya wanawake vijana Wakristo nchini humo YWCA.4. Mashinani: Jinsi mkopo na mafunzo kutoka mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umemuinua kiuchumi Hayet Aouida nchini Tunisia.
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC, Shirika la Umoja wa Mataifa la kutegua Mabomu ya ardhini (UNMAS) Jumanne Julai 18 mwaka huu wa 2023 lilitegua bomu lenye uzito wa kilo 250 lililogunduliwa wiki iliyopita na wakulima katika eneo la Kididiwe, wilayani Beni. Jimboni Kivu Kaskazini. Wakazi wanaonesha furaha yao kwa Umoja wa Mataifa kwa kutegua bomu hilo linalosababisha vifo. Mwandishi wetu wa nchini DRC, George Musubao amefuatilia na kuandaa makala hii.
21-7-2023 • 0
WHO: Nusu ya watu duniani hatarini kuugua Dengue
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limesema takriban nusu ya idadi ya watu ulimwenguni hivi sasa wapo hatarini kuungua ugonjwa wa Dengue huku ikikadiriwa kila mwaka watu kati ya milioni 100 mpaka 400 wanapata maambukizi. Dengue ni ugonjwa unaoenezwa na mbu aina ya Aedes. Ugonjwa huo hutokea zaidi katika nchi zenye hali ya hewa ya kitropiki na ya joto. Mkuu wa Kitengo kinachohusika na magonjwa ya Kitropiki yasiyopewa kipaumbele ambaye pia ni mratibu wa mpango wa magonjwa ya Dengue na Arbovirus katika shirika la Afya ulimwenguni WHO Dkt. Raman Velayudhan, akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Geneva Uswisi amesema ugonjwa huu wa Dengue “Umeongezeka kwa kasi duniani kote katika miongo ya hivi karibuni, huku idadi ya wagonjwa wanaoripotiwa WHO wakiongezeka kutoka nusu milioni mwaka 2000 hadi zaidi ya milioni 4.2 mwaka 2022. Hiyo ni takriban mara 8 zaidi katika miongo miwili.”Ugonjwa wa Dengue, ambao pia huitwa homa ya mfupa, ni maambukizi ya kawaida ya virusi ambayo huenea kutoka kwa mbu hadi kwa binadamu. Watu wengi walio na ugonjwa huu hawana dalili na hupata nafuu baada ya wiki 1 mpaka 2. Hata hivyo Dkt. Velayudhan amesema “Kwa wengine hupata dalili za kawaida ikiwemo homa kali, maumivu ya kichwa, maumivu ya mwili, kichefuchefu na vipele. Iwapo mtu ataugua na kupona na kisha kuugua kwa mara ya pili ana uwezekano mkubwa kupata dalili za dengue kali.”Watu ambao hupata Dengue kali wanahitaji kupatiwa matibabu hospitalini kwani wakichelewa wanaweza kupoteza maisha.Ingawa hakuna matibabu kamili ya ugonjwa huu mpaka sasa , wale wanaogundulika hupatiwa dawa za kupunguza joto na maumivu ya mwili. Watu wanaweza kupunguza hatari ya kupata dengue kwa kuepuka kuumwa na mbu, hasa mchana.Wakati takriban asilimia 70 ya wagonjwa wengi wakiripotiwa kutoka Barani Asia, Ukanda wq Jangwa la Sahara idadi kubwa ya wagonjwa wameripotiwa kutoka nchini Sudan ambapo kulikuwa na wagonjwa 8239 na vifo 45 tangu Julai 2022. Katika wiki za hivi karibuni WHO imepokea ripoti za uwepo wa wagonjwa wa dengue nchini Misri.WHO imezitaka wizara za Afya kuchukua hatua kwani wakati kuna milipuko, dengue inaweza kuchukua rasilimali za thamani kutoka kwenye mfumo wa afya, na kuongeza mzigo zaidi kwa taifa.
21-7-2023 • 0
21 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia Afya na malengo ya maendeleo endelevu. Makala tunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Rwanda, kulikoni? Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limesema takriban nusu ya idadi ya watu ulimwenguni hivi sasa wapo hatarini kuungua ugonjwa wa Dengue huku ikikadiriwa kila mwaka watu kati ya milioni 100 mpaka 400 wanapata maambukizi..Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF limekunja jamvi jana hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya siku 10 za tathimini ya utekelezaji wa malengo hayo au SDGs. Waakilishi wa nchi na serikali, wanazuoni, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wanaharakati na vijana ni miongoni mwa waliohudhuria. Kenya haikubaki nyuma katika jukwaa hilo.Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC, ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la kutegua Mabomu ya ardhini (UNMAS) Jumanne Julai 18 mwaka huu wa 2023 lilitegua bomu lenye uzito wa kilo 250 lililogunduliwa wiki iliyopita na wakulima katika eneo la Kididiwe, wilayani Beni. Jimboni Kivu Kaskazini. Wakazi wanaonesha furaha yao kwa Umoja wa Mataifa kwa kutegua bomu hilo linalosababisha vifo. .Mashinani tutaelekea nchini Rwanda kusikia ni kwa jinsi gani programu ya remedial ambayo imewafikia watoto zaidi ya 10,000 katika shule 200 na vituo 10 vya vijana imeboresha masomo kwa wanafunzi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
21-7-2023 • 0
Susan Mang’eni: Serikali imesikia kilio chenu Wakenya ina mikakati chonde chonde kuweni na subira
Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF limekunja jamvi jana hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani baada ya siku 10 za tathimini ya utekelezaji wa malengo hayo au SDGs. Waakilishi wa nchi na serikali, wanazuoni, mashirika ya Umoja wa Mataifa, wanaharakati na vijana ni miongoni mwa waliohudhuria. Kenya haikubaki nyuma katika jukwaa hilo. Susan Auma Mang’eni katibu mkuu wa wizara ya ushirika na biashara ndogondogo wa Kenya alibeba bendera yataifa hilo miongoni mwa waliowasilisha tarifa katika mkutano wa vijana kandoni mwa jukwaa hilo amenieleza kuwa moja ya changamoto kubwa ya utekelezaji wa malengo hayo hasa kwa nchi zinazoendelea kama Kenya ni ufadhili ulioahidiwa na mataifa tajiri ya G20 ambao bado haujatolewa kwa nchi zinazoendelea, “Zikitusaidia sasa tutaweza kuweka mikakati ambayo inatakikana ili tuweze kupunguza hali ngumu ya Maisha na kando ya hapo katika kuangalia masuala ya mabadiliko ya tabianchi tumejitoa ndio maana kuanzia tarehe 4 hadi tarehe 6 mwezi ujao tutakuwa na kongamano kubwa sana la Afrika la kuweza kuangazia mambo ya hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi tukijiandaa kwenye kwenye kongamano la COP28.”Susan amekiri kwamba changamoto za hali ngumu ya maisha zinazochangiwa na sababu lukuki ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, na vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine hususa kwa Kenya zimechochea hali ya uchumi hasa mifukoni mwa watu kuwa mbayá zaidi wengi wakishindwa kumudu Maisha ya kila siku na kuzusha maandamano, hata hivyo amesema serikali imesikia kilio chao na inajitahidi kuleta afueni amewasihi Wakenya kuwa na subirá, “Ningependa kuwaambia Wakenya kwamba serikali ina mikakati tulieni, tufanye bidii , tupange pamoja hali itakuwa nzuri, tukiendelea kwenda kufanya maandamano ambayo ni maharibifu katika hiyo hali watu wanapoteza maisha, watu wanaumia hata askari pia wanaumia tuanendelea kufanya hii hali iwe hata ghali kiasi. Ugali hauko barabarani, ugali uko mashambani kwetu , ugali uko kwenye bidii yetu ya biashara ndogondogo. Niwaomba Wakenya kwamba msikubali kupelekwa barabarani bila msimamo kwa sababu hizo changamoto sio za Kenya peke yake.”Mapema wiki hii ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilitoa tarifa ikisema inatiwa hofu na maandamano yanayoendelea Kenya baada ya watu 23 kuuawa katika maandamano hayo huku ikivisihi vyombo vya ulinzi na usalama kutotumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji kwani kuandamana ni haki yao ya msingi ya kiraia.
21-7-2023 • 0
Ujumuishwaji ni msingi mkuu katika kusongesha malengo ya maendeleo endevu - Waheshimiwa Baraza na Mugabe
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF linafikia tamati hii leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wamekutana kuanzia tarehe 10 Julai kujadili hatua za kuchukua ili kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030. Leah Mushi ameketi chini na Gavana wa Kauti ya Kakamega Fernandes Baraza pamoja na Mbunge wa Likuyani Innocent Mugabe wote kutoka nchini Kenya kuzungumza nini wanaondoka nacho baada ya Siku 10 za mkutano huu.
20-7-2023 • 0
20 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF linafikia tamati hii leo hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wamekutana kuanzia tarehe 10 Julai kujadili hatua za kuchukua ili kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030. Leah Mushi ameketi chini na Gavana wa Kauti ya Kakamega Fernandes Baraza pamoja na Mbunge wa Likuyani Innocent Mugabe wote kutoka nchini Kenya kuzungumza nini wanaondoka nacho baada ya Siku 10 za mkutano huu. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ajenda ya Katibu Mkuu, ubaguzi nchini Libya, Mafuta katika meli nchini Yemen. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili nakupeleka kwake Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA upate uchambuzi wa neno NAZAA. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kupitia mfululizo wa mapendekezo yake yanayojulikana kama “Ajenda Yetu ya Pamoja” ambayo yanaonesha maono yake kwa miongo ijayo, hii leo akiwa amejikita na Ajenda Mpya ya Amani, ametoa mapendekezo kadhaa na hatua miongoni mwake ikiwa ni kuondoa silaha za nyuklia; kuboresha mbinu ya shughuli za amani na kushughulikia uhusiano kati ya tabianchi, amani na usalama.Wataalamu wa Umoja wa Mataifa leo wameelezea wasiwasi wao kuhusu sera ya kibaguzi iliyotangazwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya (GNU) mwezi Aprili mwaka huu 2023 ambayo inazuia haki za wanawake na wasichana kusafiri nje ya nchi bila msimamizi wa kiume au Mahram. Wataalamu hao wamesema, "Siyo tu sera hii ni ya kibaguzi, lakini pia inazuia uhuru wa kutembea ikiwa ni pamoja na wanafunzi wanaoondoka nchini kwenda kusoma nje ya nchi," na kwamba wanawake na wasichana wanaokataa kujaza au kuwasilisha fomu wanazuiwa kuondoka nchini Libya.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la UNDP limetangaza kwamba tayari Meli inayofahamika kwa jina Nautica au Yemen, tayari imeifikia meli nyingine ya FSO Safer katika katika ufukwe wa Yemen tayari kuanza kupakua mapipa milioni 1.14 ya mafuta ghafi ambayo kutokana na hali mbaya ya usalama katika ukanda huo yamekwama katika FSO Safer na yanatishia usalama kwani yanaweza kuvuja au kulipuka.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA anatufafanualia maana ya neno “NAZAA.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
20-7-2023 • 0
Pata ufafanuzi wa Neno NAZAA - Dkt. Mwanahija Ally Juma
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA anitufafanualia maana ya neno “NAZAA”.
20-7-2023 • 0
Vijana wanaweza kutumia elimu yao kusongesha SDGs iwapo watapata ufadhili wa miradi yao - Gibson
Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu kwa kifupi HLPF linakaribia kufikia ukingoni na leo Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana aliitisha kikao cha kando kuzungumza na vijana kuhusu tathmini yao ya utekelezaji wa Mkakati wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Miongoni mwa walioshiriki ni Gibson Kawago, mmoja wa viongozi vijana wa kusongesha SDGs. Nimezungumza naye kufahamu mambo kadhaa ikiwemo alichowasilisha kwenye mkutano huu.
19-7-2023 • 0
Sitaki kuwa mkimbizi wa ndani nataka wanangu wasome - Nurta
Wakati ukame mkali ukiendelea kuathiri Afrika hususan Ukanda wa jangwa la Sahara na kusababisha mamilioni ya watu kuyakimbia makazi yao kwenda kusaka misaada, baadhi ya wananchi waliosalia kwenye maeneo yao wanasema hali ni mbali lakini wamebaki kwa mustakabali wa watoto wao. Miaka 40 ya jua kali na ukame katika pembe ya Afrika, imekuwa na athari kubwa kwa wananchi wengi wasijue hali yao ya kesho itakuwaje kama mama huyo aitwaye Nurta Andow Nurinye mkazi wa Kaunti ya Garissa nchini Kenya. “Nina watoto watano, kabla ya ukame tulikuwa na mifugo, maziwa na nyama. Tangu ukame uje hakuna mvua, Wanyama wamekufa mbuzi, ngamia kila kitu kimekwenda. Maisha yamebadilika, hakuna chakula hakuna maziwa, hatuna kitu chochote, watoto wakirejea kutoka shuleni hakuna kitu chochote.” Lakini kwanini Bi.Nurta na familia yake hawaendi kusaka msaada zaidi kwenye kambi za wakimbizi wa ndani? “Tungeweza kuondoka na kwenda kusaka chakula sehemu nyingine lakini hatuwezi kwenda. Hapa watoto wapo shule, na hapa watoto wanaenda Madrasa na kwa sababu hiyo hatuwezi kufungasha virago na kwenda sehemu nyingine, ni lazima tubaki hapa.” Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa ikiwemo lile la idadi ya watu duniani na afya ya uzazi UNFPA yanafanya kila juhudi kuhakikisha wanawafikia wananchi kama Nurta Nurinye ili kuwafikishia misaada ya kuokoa maisha.
19-7-2023 • 0
Sauti za asasi za kiraia katika utekelezaji wa SDGs ni muhimu: UNA
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF, linaendelea hapa Makao Makuu jijini New York Marekani likitathimini utekelezaji wa malengo hayo yaliyosaliza chini ya miaka 7, kabla ya kufikia ukomo hapo mwaka 2030. Mbali ya tathimini ya utekelezaji wake jukwaa hilo limetoa fursa kwa nchi 39 zilizojitolea kuwasilisha ripoti za kitaifa za utekelezaji wa malengo hayo. Tanzania ni miongoni mwa nchi hizo na iliwasilisha ripoti yake jana Jumanne. Reynald Maeda, Mkurugenzi wa asasi ya Umoja wa Mataifa Tanzania, UNA ni miongoni mwa waliochangia katika ripoti hiyo kwa sasa yuko hapa New York akishiriki jukwaa hilo lakini kabla hajaondoka Tanzania alizungumza na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC Dar es salaam akianza kwa kumueleza mchango wa asasi hiyo katika ripoti iliyowasilishwa.
19-7-2023 • 0
19 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa la Umoja wa Mataifa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu kwa kifupi HLPF ambalo linakaribia kufikia ukingoni na pia ukame nchini Kenya. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na mashinani tunakupeleka nchini Yemen, kulikoni? Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
19-7-2023 • 0
18 JULAI 2023
Hii leo Jumanne ya Julai 18, siku ya kimataifa ya Mandela mwenyeji wako ni Leah Mushi akikuletea Habari kwa Ufupi zikisomwa na Anold Kayanda, kisha anakupeleka Iringa nchini Tanzania kumulika harakati za shirika la kiraia la Afya Plus za kusongesha lengo namba 6 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu maji safi na kujisafi kupitia maabara za hedhi salama, mradi unaofadhiliwa na Mfuko wa Malala. Kisha mashinani anakurejesha hapa makao makuu ya UN kusikia wito wa kwamba kufanikisha SDGs lazima uwe na moyo kama wa mama. Karibu!
18-7-2023 • 0
Kesho isiyo na saratani ya shingo ya kizazi kwa Wanawake Tanzania
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni kanda ya Afrika linaeleza kuwa Saratani ya shingo ya kizazi ni moja ya sababu kuu za vifo vinavyotokana na saratani kwa wanawake nchini Tanzania. Kawaida saratani ya shingo ya kizazi huathiri wanawake wenye zaidi ya umri wa miaka 25 ambao wameambukizwa virusi vya papilloma ya binadamu na hawajapata chanjo. Makala hii iliyoandaliwa na WHO na kusimuliwa na Anold Kayanda inaeleza jinsi uchunguzi wa afya wa mara kwa mara ni njia nzuri ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi..
17-7-2023 • 0
Watu wa jamii ya asili ni muarobaini wa majanga yanayokumba dunia-Türk
Watu wa jamii ya asili wanaweza kutuongoza katika harakati za kukabiliana na misukosuko na majanga yanayokabili zama zetu hivi sasa, amesema hii leo huko mjini Geneva, Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk akihutubia mkutano wa 16 wa wataalamu wa haki za watu wa jamii ya asili. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.Bwana Türk amesema uwezo wao katika kunusuru dunia hivi sasa ni dhahiri shahiri kwa kuzingatia ziara yake ya mapema mwaka huu huko Kenya, Colombia, Ecuador na Venezuela ambako watu wa jamii ya asili walimwelezea sio tu changamoto wanazokumbana nazo kama vile kupokonywa ardhi za asili za mababu zao bali pia harakati zao wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Mathalani uchimbaji madini unavyoharibu mazingira yao ya asili na kukiuka haki zao na maeneo yao kuvamiwa kijeshi, akisema vitendo hivyo lazima vikome kwa kuwa kusongesha haki za watu wa jamii ya asili na kulinda na kupaza sauti zao ni jukumu muhimu la ofisi yake ya kutetea haki.Ametolea mfano jinsi watoto wa jamii ya asili ya Huitoto nchini Colombia ambao mama yao alikufa kwenye ajali ya ndege mwezi uliopita, lakini kwa muongozo waliopata wakati wa makuzi kutoka kwa mama na bibi yao ya jinsi ya kuishi kwenye mazingira na mimea, wanyama na misitu ya mvua, wameweza kuishi bila kutetereka.Bwana Turk amesema ni wazi kuwa simulizi hiyo ya Watoto inadhihirisha kuwa ufahamu wa mababu, hasa wa jamii ya asili una mafunzo mengi kwa dunia ya sasa hasa wakati huu inapozidi kukabiliwa na misukosuko ikiwemo ya mabadiliko ya tabianchi.Ametanabaisha kuwa ajabu ni kwamba wanawake wa jamii ya asili ambao ndio wana uhusiano mahsusi na mazingira huwa wa kwanza kuenguliwa pindi miradi mikubwa inapoanzishwa kwenye jamii zao.Hivyo Kamishna Mkuu huyo wa Haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa amesisitiza umuhimu wa kujumuisha sauti zao katika harakati za kitaifa, kikanda na kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili hatimaye hoja ya hakuna chochote kuhusu sisi bila sisi iweze kuwa ya uhalisia.Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa duniani kote kunakadiriwa kuweko kwa watu milioni 476 wa jamii ya asili.Idadi hiyo ni sawa na asilimia 6.2 ya watu wote duniani na wanakabiliwa na umaskini, ubaguzi, kutengwa na kupokonywa mali zao. Kutokana na mazingira hayo, shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO linasema watu wa jamii ya asili ni asilimia 18.2 ya watu hohehahe duniani.
17-7-2023 • 0
UNICEF na wadau wafanikisha elimu kwa watoto wakimibizi Kakuma nchini Kenya
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linashirikiana na wadau kuisaidia serikali ya Kenya katika kaunti ya Turkana kuhakikisha elimu ya awali inawafikia watoto wote hususan kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma. Flora Nducha anatupasha zaidi katika taarifa hii.Asubuhi mapema katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, ni wakati wa watoto kwenda shule tayari kuanza siku kwa masomo darasani “Mimi jina langu ni Nyota Plamedy Baraka nina miaka sita, napenda kusoma, napenda wageni , napenda vitabu na nawapenda marafiki zangu.”Nyota ni miongoni mwa mamia ya watoto wakimbizi kutoka nchi mbalimbali walioko katika kambi hii na baba yake Baraka Munange mkimbizi mwenye watoto watano anasema elimu hii ni ya muhimu na ndio tegemeo pekee la mustakbali bora kwa watoto wao “Watoto wangu wanasoma shule ya msingi ya Morning Star , na shule ya chekechea ni nzuri sana kwa mwanzo wa mtoto kwa sababu inamfanya mtoto ajue kuongea, ajifunze kuandika na zaidi.”Kambini hapa kuna shule nyingi ambazo kwa msaada wa ufadhili kutoka kwa kanisa la Jesus Christ of the Latter-day Saints Charities, UNICEF inaweza kuhakikisha elimu inatolewa ikiwepo katika shule ya msingi ya Kalemchuch “Jina langu ni Joyce Lotenga niña umri wa miaka 8, nasoma katika shule ya Kalemchuch.”Joyce ni mmoja kati ya watoto tisa wa Francis Lomoi “Mimi ni babaye Joyce, Joyce yuko darasa la pili katika shule ya Kalemchuch kwa sababu tunakubali watoto wakimbizi kusoma pamoja na wengine, ili wote waweze kusoma kwenye shule pamoja ndio maana watoto wamekuwa wengi”Watoto hawa wanafaidika na elimu chini ya program inayoendeshwa na serikali ya “Kujifunza Maisha yote” na mbali ya elimu pia wanashiriki shughuli mbalimbali za michezo ikiwemo kuimba.Kwa mujibu wa serikali ya kaunti ya Turkana, ukame umekuwa changamoto kubwa kwa watoto hawa wanaotoka mataifa mbalimbali kupata elimu lakini jitihada zinafanyika.Afisa wa elimu wa UNICEF Kenya Sarah Musengya paul anasela licha ya changamoto hizo “Hatua kubwa zimepigwa katika elimu ya awali kwenye kaunti ya Turkana, katika usaili wa watoto sasa ikiwa imefikia asilimia 166 ambayo ni juu ya kiwango cha wastan cha serikali, pili tumepiga hatua katika vifaa vya kusomea kama madawati na viti na vifaa vingine ambavyo vimewafanya wanafunzi kufurahia kuendelea kusoma. Lakini bado kuna changamoto katika kaunti ya Turkana ikiwemo mlo shuleni katika shule zinazotoa mlo kiwango bado ni kidogo hakikidhi mahitaji ya watoto hata wa chekechea.”Kwa wazazi elimu hii inayotolewa ni baraka na matumaini kwa watoto wao “Mimi mzazi nikishakuja nyumbani nawakuta watoto wanazungumza walichofundishwa shuleni ni kiytu kimoja ambacho kinanifurahisha sana na kuonyesha kwamba watoto wanasoma vizuri.”UNICEF limeahidi kuongeza juhudi zaidi hasa za kupata wafadhili ili kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa.
17-7-2023 • 0
17 JULAI 2023
Hii leo katika jarida la Habar iza UN, mwenyeji wako Leah Mushi anamulika haki za binadamu za watu wa jamii ya asili, haki ya elimu kwa watoto wakimbizi, saratani ya shingo ya kizazi na hatimaye jinsi kampeni ya boma kwa boma inasongesha utoaji chanjo kwa jamii ya wamasai nchini Tanzania.Watu wa jamii ya asili wanaweza kutuongoza katika harakati za kukabiliana na misukosuko na majanga yanayokabili zama zetu hivi sasa, amesema hii leo huko mjini Geneva, Uswisi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk akihutubia mkutano wa 16 wa wataalamu wa haki za watu wa jamii ya asili.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linashirikiana na wadau kuisaidia serikali ya Kenya katika kaunti ya Turkana kuhakikisha elimu ya awali inawafikia watoto wote hususan kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma.Katika makala, Anold Kayanda anatupeleka nchini Tanzania ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) kwa kushirikiana na serikali nchini Tanzania linafanya juhudi za kutoa elimu ya uchunguzi wa mapema ili kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake nchini humo.Na mashinani, Edward Ngobei, Mzee kiongozi wa kimasai wilayani Monduli mkoani Arusha nchini Tanzania, anaeleza jinsi yeye pamoja na jamii za eneo hilo wamepokea chanjo mbalimbali kupitia kampeni ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO na wadau wake inayopeleka huduma za chanjo mashinani. Karibu!
17-7-2023 • 0
Amani ikitawala kutakuwa na matokeo chanya katika hatua za kufikia SDGs - Lawrence
Lawrence Oluwaseun Adeniyi, raia wa Nigeria anayefanya shughuli zake Houston Marekani amewakilisha taasisi hii ya International Association of World Peace Advocates (IAWPA) inayojitambulisha kwa kazi kuu mbili ambazo ni Utetezi wa Amani na Kuhakikisha Maendeleo Endelevu. Je analoondoka nalo kwenye Jukwaa hili ni lipi? Karibu!
14-7-2023 • 0
Mkimbizi kutoka Rwanda anayahakikisha wasichana wakimbizi hawaachi nyuma kidigitali: Deline
Malengo ya maendeleo endelevu SDGs yanahimiza kuwa wakati wa utekelezaji wake hakuna mtu anapaswa kuachwa nyuma. Tukiwa katika ulimwengu wa kidijitali jamii za wakimbizi zilizopo kwenye makambi zinafikiwaje kwenye masuala kama ya kupata elimu ya kidijitali ili wasiachwe nyuma. Nchini Kenya katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma mshichana Deline anafanya juhudi zote kuhakikisha wasichana wengine hawaachwi nyuma. Katika video ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na masuala ya wakimbizi UNHCR inamuonesha Deline, ambaye ni mkimbizi kutoka nchini Rwanda akijiandaa kuanza safari yake ya kuelekea kazini. Anasema “Ninaenda kazini, na hii ndio njia ninayopita kila siku ninavyoenda kazini, anasema Deline huku akisimama njiani na kusalimia majirani zake. Hawa ni majirani zangu, na kisha anapanda pikipiki kuelekea kazini. Deline anaendelea kueleza "Ninafanya kazi katika shirika liitwalo Solidarity iniatiative for refugees, shirika la kijamii linalojihusisha na kuwajengea uwezo wanawake kuweza kutumia teknolojia ya kidijitali ili kuboresha maisha yao. Tunafanya kazi na wanawake wa jamii za wenyeji na jamii za wakimbizi tukiwapa ujuzi wa kidigitali.” Mwalimu huyu kijana anasema kitu anachopenda zaidi kuhusu ajira yake ni fursa aliyonayo ya kuwajengea uwezo wasichana wengine kuchangamkia fursa ziletwazo na ujuzi wa kidigitali. Mbali na kuwa mwalimu Deline pia ni kiongozi “Nina timu ninayoiongoza na majukumu yangu yamegawanyika katika makundi matatu, usimamizi wa watu, usimamizi wa mradi, na usimamizi wa kituo na hayo ni baadhi ya majukumu ninayo yafanya.”Na baada ya kumaliza kufundisha na siku ndefu ya majukumu yake, Deline anahakikisha kila kitu kipo sawa kwa ajili ya darasa jingine hapo kesho na kisha anafunga kituo tayari kurejea nyumbani. “Asanteni wote kwakuwa nami leo katika siku hii hapa katika kutuo chetu kilichopo kambi ya wakimbizi ya Kakuma, tutaonana siku nyingine, kwaherini“
14-7-2023 • 0
Ukatili dhidi ya wanawake na wasicha Mashariki mwa DRC umeongezeka - UNHCR
Hali ya kusikitisha inajitokeza Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambapo ghasia zilizozuka upya kati ya makundi yasiyo ya kiserikali yenye silaha na vikosi vya serikali zimerejea katika majimbo ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Ituri zikiambatana na ukatili mkubwa dhidi ya wanawake na wasichana na kutawanya maelfu ya watu , limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR. Katika taarifa yalke iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis kamishina msaidizi wa masuala ya ulinzi wa UNHCR Gillian Triggs amesema kutokana na hali hiyo, watu milioni 2.8 wamekimbia makazi yao katika majimbo hayo tangu mwezi Machi 2022. Miongoni mwa orodha ya sheria za kibinadamu na ukiukaji wa haki za binadamu, unaoendelea ni raia kuuawa na kuteswa, huku kukamatwa kiholela, uporaji wa vituo vya afya, nyumba za raia, na uharibifu za shule pia vimeripotiwa.Triggd ameongeza kuwa “Pia tunasikitishwa sana na kuongezeka kwa ripoti za ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana waliolazimika kukimbia makwao, ikiwa ni pamoja na vitendo vya ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.Cha kusikitisha, zaidi takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba kati ya zaidi ya watu 10,000 waliopata huduma za unyanyasaji wa kijinsia (GBV) huko Kivu Kaskazini katika robo ya kwanza ya mwaka, asilimia 66 ya kesi hizi zilikuwa za ubakaji.”Ameendelea kusema kwamba visa vingi vya ukiukaji huu mbaya wa GBV vimeripotiwa kufanywa na watu wenye silaha. Hata hiuvyo amesema anaamini takwimu hizo ni sehemu ndogo tu ya kile kinachoendelea kwani nmanusura wengi wa GBV hawaripoti ukatili huo au kufuata msaada wa huduma kutokana na hofu ya unyanyapaa kwenye jamii lakini pia fursa ya kuwafikia waathirika bado ni finyu kutokana nna hali ya usalama na masuala ya kiufundi.Kwa mujibu wa afisa huyo wa UNHCR hali ngumu ya maisha imewasukuma wanawake na wasichana wengi kugeukia mbinu za hatari kama biashara ya ngono hasa Goma Kivu Kaskazini ili kujikimu kimaisha na familia zao hasa wakati huu ambapo changamoto ya kutokuwa na uhakika wa chakula inaongezeka.Lakini pia amesema wanawake na wasichana wengi wanabakwa wakati wakienda kusenya kuni na kuteka maji.Amehitimisha taarifa yake kwa kusema “Tunatoa wito kwa serikali na mamlaka za mitaa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na janga hili la kutisha la GBV. Wale waliohusika na ukiukaji huu mbaya wa haki za binadamu na sheria za kibinadamu lazima wawajibishwe.”
14-7-2023 • 0
14 JULAI 2023
Hii leo jaridani machafuko nchini DRC na mjadala kuhusu malaengo ya maendeleo endelevu unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Makala tunasalia hapa hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni? Hali ya kusikitisha inajitokeza Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambapo ghasia zilizozuka upya kati ya makundi yasiyo ya kiserikali yenye silaha na vikosi vya serikali zimerejea katika majimbo ya Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Ituri zikiambatana na ukatili mkubwa dhidi ya wanawake na wasichana na kutawanya maelfu ya watu , limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.Malengo ya maendeleo endelevu SDGs yanahimiza kuwa wakati wa utekelezaji wake hakuna mtu anapaswa kuachwa nyuma. Makala tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF limeingia siku yake ya 5. Tunaendelea kuzungumza na washiriki wa Jukwaa hili na leo ni zamu ya Lawrence Oluwaseun Adeniyi ambaye ni afisa wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wachechemuzi wa Amani Ulimwenguni anayehusika na Malengo ya Maendeleo Endelevu.Na katika mashinani tuatelekea Arusha nchini Tanzania kusikia ujumbe wa mhudumu wa afya ambaye anatembea boma kwa boma mashinani kutoa huduma za chanjo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
14-7-2023 • 0
Vijana wachukue hatua kuhakikisha malengo ya maendeleo endelevu yanatimizwa - Job Nyangenye Omanga
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeingia siku yake ya nne hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wanakutana kujadili hatua za kuchukua ili kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030. Mmoja wa wanaoshiriki ni Job Nyangenye Omanga, raia wa Kenya anayeishi Texas-Marekani akijishughulisha na sekta ya afya hapa Marekani na nyumbani Kenya. Mwenzangu Anold Kayanda amezungumza naye na kwanza Omanga anaanza kueleza ujumbe aliokuja nao kwenye Jukwaa hili.
13-7-2023 • 0
Je wafahamu maana ya neno UKUMBIZAJI?
Katika kujifunza Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA akieleza maana ya neno “UKUMBIZAJI."
13-7-2023 • 0
13 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeingia siku yake ya nne hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York-Marekani. Wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa, asasi mbalimbali na vijana wanakutana kujadili hatua za kuchukua ili kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikapo mwaka 2030. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo migogoro nchini Sudan, ripoti ya UNAIDS na msaada wa kibinadamu nchini Zimbabwe. Katika kijifunza Kiswahili tunataungana na mtaalam wetu Onni Sigalla kutoka BAKITA Tanzania. Miili ya takriban watu 87 ya kabila la Masalit na wengine wanaodaiwa kuuawa mwezi uliopita na vikosi vya msaada wa haraka RSF na washirika wao huko Darfur Magharibi nchini Sudan, imezikwa kwenye kaburi la pamoja huko El-Geneina kwa amri ya vikosi hivyo kulingana na taarifa za kuaminika ambazo Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa imezipata.Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya UKIMWI UNAIDS imeeleza kuna njia ya wazi kabisa ya kumaliza UKIMWI ulimwenguni ifikapo mwaka 2030 na njia hiyo inaweza kusaidia kujiandaa na majanga mengine makubwa yasiyo tazamiwa na hivyo kuwezesha ufikiaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu. Na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limekaribisha mchango wa dola milioni 2 uliotolewa na shirika la Marekani la msaada wa kimataifa USAID ili kusaidia wananchi wa miji mitatu nchini Zimbabwe.Katika kujifunza Kiswahili leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA akieleza maana ya neno “UKUMBIZAJI”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
13-7-2023 • 0
12 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia utapiamlo na msaada wa kibidamu. Makala tunasalia hapa marekani na mashinani tutaelekea Geneva nchini Uswisi, kulikoni?Zaidi ya watu milioni 122 wanakabiliwa na njaa duniani tangu mwaka 2019 kutokana na majanga mbalimbali, mishtuko ya hali ya hewa pamoja na migogoro ya mara kwa mara ikiwa ni pamoja na vita vya Ukraine hayo yapo kwenye ripoti iliyotolewa leo ya hali ya usalama wa chakula na lishe duniani SOFI.Baada ya jana Jumanne nia ya Baraza la Usalama kupitisha azimio ambalo ningeruhusu uvushaji misaada ya kibinadamu katika kivuko cha Bab al-Hawa kwenye mpaka wa Syria na Uturuki kaskazini-magharibi mwa Syria ili ikaokoe maisha ya wananchi wa nchi hiyo ambao wamekuwa kwenye zaidi ya miaka 12 ya vita kukwama kutokana na Urusi kupiga kura ya turufu kulipinga azimio hilo lingerefusha operesheni hiyo kwa miezi tisa mbele baada ya kufikia ukomo juzi tarehe 10 Julai, hofu sasa ni kuwa matokeo yake yatakuwa maumivu zaidi kwa wananchi wa Syria. Katika ya makala Flora Nducha anazungumza na kijana Omesa Mukaya miongoni mwa vijana wanaohudhuria jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo maendeleo endelevu HLPF linaloendelea hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kwanza Omesa ambaye hivi karibuni amehitimu shahada ya kwanza katika masuala ya sayansi ya mazingira na será katika chuo kikuu cha Clark Massachusetts amemweleza Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili nini nkilichomleta.Na mashinani Rebeca Grynspan, Katibu Mkuu wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo ya biashara duniani, UNCTAD anatoa onyo kuhusu hatua za kuelekea utekelezaji wa malendo ya maendeleo endelevu ifikapo mwaka 2023 katika nchi maskini.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
12-7-2023 • 0
Vijana tusipoteze matumaini bado tuna fursa ya kukabili changamoto ya tabianchi: Omesa Mukaya
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu HLPF linaendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo wawakilishi wa nchi na serikali, wanasayansi, wanazuoni, mashirika ya umoja wa Mataifa asasi mbalimbali na vijana wanashiriki kukuna vichwa kujadili nini cha kufanyua kuhakikisha malengo hayo muhimu ya maendeleo yanatimizwa ifikpo mwaka 2030 na nini kifanyike kuzisaidia nchi zinazosuasua. Miongoni mwa washiriki ni kijana Omesa Mukaya kutoka Kenya ambaye mwezi Mei mwaka huu amehitimu shahada ya kwanza ya masuala ya sayansi ya mazingira na será katika chuo kikuu cha Clark Jimboni Massachussets hapa Marekani, amemweleza Flora Nducha wa Idhaa hii kilichomleta katika jukwaa hili.
12-7-2023 • 0
Watu milioni 122 wanakabiliwa na njaa duniani: Ripoti ya SOFI
Zaidi ya watu milioni 122 wanakabiliwa na njaa duniani tangu mwaka 2019 kutokana na majanga mbalimbali, mishtuko ya hali ya hewa pamoja na migogoro ya mara kwa mara ikiwa ni pamoja na vita vya Ukraine hayo yapo kwenye ripoti iliyotolewa leo ya hali ya usalama wa chakula na lishe duniani SOFI. Utafiti uliofanywa kwa ushirikiano wa mashirika matano ya Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 2019 mpaka 2022 umebaini kuwa takriban watu milioni 735 wanaokabiliwa na njaa kwa sasa, ikilinganishwa na watu milioni 613 mwaka 2019 hali inayofanywa ufikiaji wa lengo namba 2 la Malengo ya Maendeleo Endelevu SDG la kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2030 kutoweza kufikiwa. Ripoti hiyo ilizinduliwa katika majiji matatu Roma Italia, Geneva Uswisi na New York Marekani imeeleza kuwa ingawa maendeleo yameonekana katika kupunguza njaa barani la Asia na Amerika ya Kusini, Afrika inasalia kuwa eneo lililoathiriwa zaidi ambapo mtu mmoja kati ya watano anakabiliwa, na kwa wastani njaa ipo katika kiwango ambacho ni zaidi ya mara mbili ya wastani wa kimataifa.Katika ujumbe wake kwa njia ya video Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumzia ripoti hiyo ya SOFI amesema ingawa kuna miale ya matumaini katika baadhi ya mabara lakini kwa kwa ujumla, tunahitaji juhudi kubwa na za haraka za kimataifa ili kuokoa Malengo ya Maendeleo Endelevu. “Ni lazima tujenge uthabiti dhidi ya migogoro na mishtuko inayosababisha uhaba wa chakula kuanzia kwenye migogoro hadi kwenye hali ya hewa” amesema Katibu Mkuu Guterres.Kwa upande wa njaa na utapiamlo ripoti hiyo imeeleza kuwa uwezo wa watu kupata lishe bora umeshuka kote ulimwenguni kote, zaidi ya watu bilioni 3.1 sawa na asilimia 42 hawakuweza kumudu lishe bora mnamo 2021. Hii inawakilisha ongezeko la jumla la watu milioni 134 ikilinganishwa na 2019.Watoto hususan walio chini ya miaka mitano ni waathirika wakubwa wa utapiamlo. Watu wa vijijini ndio waathirika zaidi wa njaa ikilinganishwa na watu wa mijini lakini nchi zinapaswa kujipanga kwa sera bora kwani idadi kubwa ya watu wanahamia mijini na hivyo tatizo la njaa linaonekana kuongezeka hata mijini.Wakuu wa mashirika matano ya Umoja wa Mataifa ambayo ni Shirika la Chakula na Kilimo FAO, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD, lile la kuhudumia watoto UNICEF, la afya duniani WHO pamoja na la mpango wa chakula duniani WFP katika dibaji yao kwenye ripoti hiyo yenye kurasa 313 wameandika kuwa “Bila shaka, kufikia lengo la Maendeleo Endelevu la kutokomeza njaa ifikapo mwaka 2030 kunaleta changamoto kubwa. Inakadiriwa kuwa takriban watu milioni 600 bado watakuwa wakikabiliwa na njaa ifikapo mwaka 2030. Vichochezi vikuu vya uhaba wa chakula na utapiamlo vimekuwa jambo la kawaida na hivyo hakuna chaguo jingine isipokuwa kuongeza juhudi za kubadilisha mifumo ya chakula kwenye kilimo na kuwasidia ili kufikia lengo hilo namba 2. “Ripoti hiyo inapendekeza ili kukuza uhakika wa wa chakula na lishe kwa ufanisi, lazima kuwe na uingiliaji kati wa sera, na hatua zichukuliwe, uwekezaji lazima uongozwe na uelewa wa kina wa uhusiano mtambuka na unaobadilika kati ya mwendelezo wa vijijini na mijini na mifumo ya kilimo cha chakula.
12-7-2023 • 0
Azimio la Baraza la Usalama kutopitishwa ni hatari kwa Wasyria
Baada ya jana Jumanne nia ya Baraza la Usalama kupitisha azimio ambalo ningeruhusu uvushaji misaada ya kibinadamu katika kivuko cha Bab al-Hawa kwenye mpaka wa Syria na Uturuki kaskazini-magharibi mwa Syria ili ikaokoe maisha ya wananchi wa nchi hiyo ambao wamekuwa kwenye zaidi ya miaka 12 ya vita kukwama kutokana na Urusi kupiga kura ya turufu kulipinga azimio hilo lingerefusha operesheni hiyo kwa miezi tisa mbele baada ya kufikia ukomo juzi tarehe 10 Julai, hofu sasa ni kuwa matokeo yake yatakuwa maumivu zaidi kwa wananchi wa Syria. Huyo ni Priscilla Gomes mmoja wa maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR akiwa huko kaskazini-magharibi mwa Syria anasema…kwa sasa yuko Atma, katika moja ya vituo vya jamii vinavyoungwa mkono na UNHCR. Priscilla Akieleza umuhimu wa misaada ya kibinadamu huko anasema, "Hapa, watoto na watu wazima ambao wameathiriwa na migogoro na tetemeko la ardhi wanaweza kupata huduma muhimu za ulinzi, ikiwa ni pamoja na ushauri wa kisheria, msaada wa kisaikolojia, na upatikanaji wa shughuli za jamii na mafunzo ya ufundi.” Takribani watu milioni 4.1, ambapo inakadiriwa milioni 2.7 ni wakimbizi wa ndani, wanaendelea kuhitaji msaada muhimu wa kuokoa maisha. Wakati Umoja wa Mataifa na wadau wake wametayarisha mpango wa mwendelezo wa utoaji misaada, pengo lililoletwa na kutopitishwa mwendelezo wa azimio la kuvusha misaada kutoka Türkiye hadi kaskazini-magharibi mwa Syria kunaweza kuongeza mateso ya wanadamu kwa haraka. Priscilla Gomes afisa huyu wa UNHCR akiwa bado kaskazini magharibi mwa Syria anahitimisha akisema, "Ni muhimu kutoa msaada wa haraka wa kuokoa maisha. Na ni muhimu pia kuunga mkono mwitikio katika muda wa kati na mrefu, kushughulikia mahitaji makubwa.
12-7-2023 • 0
11 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo ninatupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kama ilivyo sehemu nyingi za Afrika Mashariki nako lugha ya kiswahili inatajwa kuwa chombo chenye nguvu sana kinachoingilia kati ujenzi wa amani na pia katika biashara hasa kwa wakaazi wa mji wa Goma katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Kiswahili ndio lugha ya kwanza nchini DRC yenye idadi kuwa ya wazungumzaji katika mikoa ya Mashariki na Magharibi mwa nchi ambako inatumiwa hata kwenye vyombo vya habari kama Redio na televisheni. Pia tunaangazi ripoti ya UNFPA ya idadi ya watu Duniani. Mashinani tunakupeleka nchini Haiti, kulikoni?Mwenyenji wako ni Leah Mushi, karibu!
11-7-2023 • 0
Walinda amani Bunia DRC watumia maigizo kuelimisha umma dhidi ya unyanyasaji wa kingono
Ili kudhibiti unyanyasaji wa kingono ambao wakati mwingine unafanywa na baadhi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, huko jimboni Ituri katika mji wa Bunia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo – MONUSCO wanatumia ubunifu wa sanaa za maigizo ya jukwaani kuelimisha umma. Wanafunzi na wananchi wakiangalia, igizo linaendelea, mwanafunzi aliyefanyiwa unyanyasaji wa kingono hakukaa kimya amekuja katika mamlaka zinazohusika na kupokea malalamiko kueleza kilichotokea na anaambiwa amefika mahali salama na kwanza atapewa huduma ya kisaikolojia. Aliyekuwa anaongoza igizo hilo ni Debora Barugahara, yeye ni Ofisa wa MONUSCO anayehusika na tabia na nidhamu katika eneo la Bunia. Anasema “Tunafanya kuelimisha umma ili kuzuia unyanyasaji wa kingono. Tunawalenga wanafunzi wanaosoma na kuishi katika eneo la Bankoko hapa Bunia eneo ambalo ni mwenyeji wa kambi kubwa kabisa ya MONUSCO. Tumetumia maigizo ya jukwaani ili kukuza uelewa. Igizo fupi limeonesha askari wa MONUSCO na raia wakihusika katika unyanyasaji wa kiongo kwa wanafunzi. Kila mmoja alikuwa makini akifuatilia igizo lililoonesha matokeo mabaya ya unyanyasaji wa kingono. Tumehisi kwamba ujumbe umefika.” Marie Zaire Baguma ni Rais wa Mtandao wa Kijamii wa Malalamiko Bunia anasema, “Tunataka jamii kuchukua kwanza umiliki wa jambo hili. Inapokuwa hivyo tunakuwa na matumaini kutakuwa na matukio machache ya unyanyasaji wa kingono.”
10-7-2023 • 0
10 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu na walinda amani nchini DRC. Makala tuankupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Chad, kulikoni? Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani chini ya mwamvuli wa baraza la kiuchumi na kijamii ECOSOC.Ili kudhibiti unyanyasaji wa kingono ambao wakati mwingine unafanywa na baadhi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, huko jimboni Ituri katika mji wa Bunia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo – MONUSCO wanatumia ubunifu wa sanaa za maigizo ya jukwaani kuelimisha umma. Katika Makala Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA nchini Kenya Anders Tomsen, ameeleza shirika hilo linatekeleza ipasavyo tamko la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu ambalo mwaka huu linafikisha miaka 75 hususan ibara ya Tano ambayo inasema Haki ya mtu ya kwamba asitumbukizwe kwenye vitendo vya mateso, ukatili, au adhabu dhalili.Mashinani tutaelekea Chad ambapo Maelfu ya wananchi wa Chad wanarejea nyumbani wakikimbia mzozo unaoendelea nchini SudanMwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
10-7-2023 • 0
UNFPA Kenya yaeleza mipango yake ya kutetea haki za wanawake
Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na idadi ya watu UNFPA nchini Kenya Anders Tomsen, ameeleza shirika hilo linatekeleza ipasavyo tamko la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu ambalo mwaka huu linafikisha miaka 75 hususan ibara ya Tano ambayo inasema Haki ya mtu ya kwamba asitumbukizwe kwenye vitendo vya mateso, ukatili, au adhabu dhalili.Akihojiwa na mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya Tomsen anaanza kwa kusema shirika hilo limeundwa kwa kuzingatia misingi ya haki.
10-7-2023 • 0
UN: Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa HLPF kuhusu SDG’s limengoa nanga leo
Jukwaa la ngazi ya juu la kisiasa kuhusu ,malengo ya maendeleo endelevu lijulikanalo kama HLPF limeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani chini ya mwamvuli wa baraza la kiuchumi na kijamii ECOSOC.Jukwaa hilo ambalo litakunja jamvi 20 Julai mwaka huu limebeba maudhui "Kuharakisha kujikwamua kutokana na janga la ugonjwa wa virusi vya corona au COVID-19 na utekelezaji kamili wa ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu katika ngazi zote".Mbali ya viongozi wa ngazi ya juu katikia jukwaa hilo kutakuwa na siku tatu za majadiliano katika ngazi ya mawaziri.Kwa mujibu wa ECOSOC jukwaa hilo “litajumuisha mapitio ya mada ya malengo ya maendeleo endelevu namba 6 kuhusu maji safi na usafi wa mazingira, namba 7 kuhusu nishati nafuu na safi, namba 9 linalohusu viwanda, uvumbuzi na miundombinu, namba 11 linalohusu miji na jamii endelevu, na namba 17 linalohusu ubia kwa ajili ya malengo.”Pia jukwaa hili ltashughulikia changamoto maalum zinazokabili nchi zilizo katika hali maalum. Zaidi ya hapo litathimini vipimo vya kikanda na vya ndani ya nchi kuhusu kujikwamua kutoka kwaenye janga la COVID-19 na hali kuhusu malengo ya maendeleo endelevu SDGs. Na kisha litaunga mkono mapitio ya muda wa kati wa malengo ya SDGs na maandalizi ya mkutano wa mwa ka huu 2023 wa SDG mutaotarajiwa kufanyika Septemba.Leo katika siku ya kwanza ya jukwaa hilo mada kuu zitakazopewa kipaumbele ni “kushinda majanga, kuleta mabadiliko kwa aajili ya SDGs, na kutomwacha mtu yeyote nyuma, Kufadhili hatua zetu za kukabiliana na majanga na kuwekeza katika SDGs.”Nchi 39 zikiwemo Tanzania, Rwanda na Zambia zitafanya mapitio ya kitaifa ya hiari (VNRs) ya utekelezaji wao wa ajenda ya 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu katika katika jukwaa hilo la HLPF 2023.Miongoni mwa wazungumzaji wa leo katika jukwaa hilo ni wasaidizi wa Katibu Mkuu Li Junhua, Qu Dongyu ambaye ni mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO, Guy Ryder ambaye ni msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya sera, Mami Mizutori msaidizi wa Katibu Mkuu na mkuu wa ofisi ya Umoja wa Msataifa ya upunguzaji wa hatari ya majanga UNDDR, na Filippo Grandi ambaye ni Kamisha mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR.
10-7-2023 • 0
07 JULAI 2023
Ni ijumaa ya tarehe 07 mwezi Julai mwaka 2023 siku ya lugha ya Kiswahili Duniani. Mimi ni Leah Mushi.Wahenga walinena leo ni leo asemaye kesho muongo na asiye na mwana aeleke jiwe, kila kona ya Dunia palipo na wadau wa Kiswahili siku hii inaadhimishwa kwa shughuli mbalimbali. Nasi tunakuletea kipindi maalum kwa ajili ya maadhimisho hayo na tunaanzia hapa makao makuu ambako kunafanyika hafla maalum kuienzi siku hii.
7-7-2023 • 0
06 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Eugene Uwimana mmoja wa maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda amemtembelea mhamasishaji wa lugha ya Kiswahili nchini humo Profesa Pacifique Malonga ambaye ameanzisha eneo maalumu la vitabu vya Kiswahili katika Maktaba Kuu ya mji wa Kigali. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za uhamiaji, usafirishaji haramu wa binadamu na Akili Bandia. Katika jifunze Kiswahili hii leo tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kupata ujumbe maalum kuhusu umuhimu wa lugha. Katika kipindi cha miezi 3 ya vita nchini Sudan idadi ya wakimbizi wanaoenda kusaka usalama nchi jirani imefikia milioni 3 limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya uhamiaji IOM.Nusu ya idadi ya watoto wahanga wa usafirishaji haramu wa binadamu husafirishwa ndani ya nchi zao na wale wanaosafirishwa kimataifa hupelekwa nchi jirani ambazo ni tajiri. Na leo pamoja na Kesho julai 6 na 7, katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Geneva Uswisi kunafanyika mkutano unaojadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya Akili Bandia AI pamoja na roboti.Katika jifunze Kiswahili hii leo tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kupata ujumbe maalum kuhusu umuhimu wa lugha.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
6-7-2023 • 0
05 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea kipindi maalum kuelekea siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili itakayoadhimishwa wiki hii na leo tutakuwa nchini Kenya ambapo mada kuu ya mwaka huu ya Siku ya Kiswahili inampa faraja Wangari Grace, Mwandishi wa vitabu vya kiswahili, msimulizi wa hadithi na msanii kwani amefanikiwa kusimulia hadithi kwa watu walioko kwenye mataifa mbalimbali kupitia majukwaa ya kijamii kama vile Youtube, TikTok, podcast na hata pia kuandika vityabu vya dijitali yaani e-book. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za UNICEF, Baraza la haki za binadamu na UNHCR. Mashinani tutaelekea nchini Tanzania, kulikoni? Nchi 12 barani Afrika zinatazamiwa kupokea dozi milioni 18 za chanjo ya kwanza ya malaria katika kipindi cha miaka miwili ijayo imeeleza leo taarifa ya pamoja iliyotolewa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya ulimwenguni WHO na lilanoshughulika na watoto UNICEF huku wakishirikiana na Ubia wa chanjo duniani, GAVI.Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya wakimbizi wa ndani Paula Gaviria ameliambia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kufurutu ada na huo ni ukweli wa kutisha. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,UNHCR limeeleza kunasikitishwa na ripoti zinazoendelea za raia nchini Sudan, wakiwemo wakimbizi wa ndani na wakimbizi waliokumbwa na mzozo unaoendelea, wamekuwa wahanga wa mauaji ya kiholela wa mapigano na kuzuiwa kutafuta usalama.Na katika mashinani leo tunaelekea katika Wilaya ya Mbozi nchini Tanzania kusikiliza ni kwa jinsi gani wazazi na walezi wanaweza kuweka nyumba zao salama dhidi ya ukatili kupitia malezi bora toka mtoto anapozaliwa hadi anapokuwa kijana barubaru.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
5-7-2023 • 0
Mahojiano maalum kuelekea siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili - BAKITA
Kuelekea siku ya lugha ya Kiswa duniani itakayoadhimishwa Ijumaa wiki hii Afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam amefunga safari hadi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini humo BAKITA lenye wajibu mkubwa wa kuendelea na kukuza lugha hiyo adhimu sio Tanzania na Afrika tu bali duniani kote na kuketi chini na mhariri mwandamizi wa Baraza hilo Onni Sigalla. Wamejadili mengi lakini Onni anaanza kufafanua jukumu lake BAKITA.
3-7-2023 • 0
03 JULAI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea kipindi maalum kuelekea siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili itakayoadhimishwa wiki hii na leo tutakuwa nchini Tanzania katika Baraza la Kiswahili la taifa BAKITA. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za WHO, UNAIDS na IAEA. Mashinani tutaelekea nchini Afrika Kusini, kulikoni? Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) limetoa mwongozo mpya kuhusu sera za kuwalinda watoto dhidi ya athari mbaya za matangazo ya vyakula.Shirika la Umoja wa Mataifa kukotokomeza Virusi vya Ukimwi na UKIMWI (UNAIDS) katika ripoti yake mpya iliyopewa jina ‘Njia Inayomaliza UKIMWI, limeonesha kuwa kuna ongezeko la idadi ya nchi zinazothibitisha kwamba UKIMWI unaweza kukomeshwa ikiwa kuna utashi wa kisiasa ambao unamaanisha kutoa ufadhili wa kutegemewa na wa kutosha; kufuata data na ushahidi; kupunguza kukosekana kwa usawa na ubaguzi unaonyima huduma za watu, kutumia zana za kisayansi zinazolinda ustawi, na kipengele muhimu cha kutambua na kushirikisha afua zinazoongozwa na jamii.Na baada ya miezi minne, Mtambo wa Nishati ya Nyuklia wa Zaporizhzhya nchini Ukraine (ZNPP) umeunganishwa tena katika njia yake pekee ya dharura lakini hali ya nishati ya eneo hilo bado ni tete wakati wa mzozo wa kijeshi unaoendelea na sio endelevu, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Mariano Grossi ameeleza leo.Mashinai tutakupeleka nchini Afrika Kusini ambapo video fupi iliyopewa jina "A Thousand Colours" yaani 'Rangi Elfu Moja' iliyoandaliwa na taasisi ya Khalili Foundation kwa kushirikiana na UNESCO inaeleza umuhimu wa utofauti wa kitamaduni.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
3-7-2023 • 0
Wananchi wahamasishwa kuyalinda mazingira baada ya mafuriko Kalehe, DRC.
Muungano wa mashirika ya kiraia katika eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuchukua hatua nyingine zitakazosaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa mapema mwezi Mei Mwaka huu. Mwandishi wetu wa DRC George Musubao amefika huko na kutuandalia makala ifuatayo. Kwako George.
30-6-2023 • 0
Walinda amani kutoka Tanzania watoa mafunzo ya mapishi na ujasiriamali kwa wanawake wanakijiji cha Moro, CAR
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR (MONUSCO) wametoa mafunzo ya upishi kwa vikundi vya wanawake wa Kijiji cha Moro kilichoko takribani kilometa 50 kutoka Mji wa Berberati, jimboni Mambere Kadei yalipo makao makuu ya kikosi hicho. Wakiwa na shangwe na nderemo wanakijiji cha Moro wanawapokea walinda amani kutoka Tanzania chini ya MINUSCA katika Kijiji hicho...Kisha walinda amani hao wanaanza kutoa elimu ya mapishi kwa vitendo kwa wanawake ili kuwapa njia ya kujipatia kipato na lishe kupitia utengenezaji wa vitafunwa kama vile mandazi. Wanawake wameona kuanzia jinsi ya kuchanganya unga, kukoroga, kuumua hadi mwisho kupata Chifu wa Kijiji cha Moro Jack Bambakyr anatoa shukrani zake kwa TANBAT6 kwa elimu waliyotoa akisema, "Ninatoka shukrani kwa walinda amani kutoka Tanzania kwa sababu ya mambo mapya ambayo wamekuja kuwaonesha wake zetu hapa. Wamepata ujuzi wa kutengeneza vitu mbalimbali kwa mikono Ili kujipatia kipato. Asante sana, asante sana kwa kuja kwetu." Naye Mwenyekiti wa vikindi vya ujasiliamali vya wanawake wa kijiji Cha Moro Bi. Marie Aghateanatoa shukrani zake kwa TANBAT6 huku akiwasihi wapatapo nafasi warudi tena kuwapatia elimu zaidi, "Kwa niamba ya kinamama nashukuru sana Kwa kutupa uelewa zaidi wa kujipatia kipato. Asanteni watanzania tunaomba mnapopata nafasi msisite kuja tena Kijiji hapa"Sasa ni matunda ya kile walichofundishwa wanakijiji, wanakula na kunywa uji na mandazi.
30-6-2023 • 0
UNFPA inasaidia kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake na wasichana wanaokimbia ghasia Khartoum
Wanawake na wasichana wanaokimbia machafuko yanayoendelea mjini Kharthoum nchini Sudan wanakabiliwa na changamoto lukuki hususan kwa wajawazito wanaohitaji msaada wa kujifungua, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambalo sasa limechukua jukumu la kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake hao. Miongoni mwa wanawake hao ni Omnia hili si jina lake halisi amepewa ili kulinda usalama wake, akiwa na ujauzito wa miezi tisa, alilazimika kuacha nyumba yake na kila kitu alichojua ili kuepuka vita kali iliyoukumba mji mkuu wa Sudan, Khartoum kuokoa maisha yake.Kwa uchumngu mkubwa anasema "Nimepoteza kila kitu katika vita hii. Lakini sikutaka kumpoteza mtoto wangu ambaye bado hajazaliwa.”Ingawa kusafiri katika hali yake ilikuwa hatari, alihisi hakuwa na chaguo, ukosefu wa usalama, risasi zinazorindima, uporaji na uharibifu wa vituo vya afya ulimaanisha kuwa hakuweza kumuona daktari kwa wiki kadhaa, ilikuwa safari ngumu ya siku tano, hatimaye mapema Juni alifanikiwa kufika Port Sudan, kwenye ufuo wa jimbo la bahari ya Sham.Omnia alikuwa akilia njia nzima kutoka Khartoum na aliogopa kwamba angepata uchungu na kujifungulia njiani kuelekea Port Sudan.Kwa mujibu wa UNFPA Omnia ni kisa kimoja tu lakini maelfu ya wanawake na wasichana wanapitia changamoto hiyo hivi sasa Sudan. Alikuwa na bahati kwani aliwasili katika hospitali ya mafunzo ya Port Sudan ambako alianza kuumwa uchungu na kusaidiwa kujifungua salama mtoto wa kike kwa njia ya upasuaji. Hata hivyo UNFPA inasema “hiyo ni hospital pekee ya serikali inayotoa huduma za uzazi kwa watu milioni 1.6 na sasa shirika hilo la idadi ya watu na wadau wa bahari ya Sham wanaisaidia hospitali hio kwa vifaa, dawa na mafunzo kwa wahudumu ili kuhakikisha wakina mama wajawazito kama Omnia waliotawanywa na vita na kuwasili Port Sudan kutoka nchi nzima wanajifungua salama.”Mkurugenzi mkuu wa hospitali hiyo Dkt. Randa Osman anasema “Timu yetu imejitolea kikamilifu kusaidia wanawake na wasichana wanaowasili kutoka Khartoum, lakini tunahitaji vifaa zaidi vya dharura, ikiwa ni pamoja na mafuta na vifaa vya kuokoa maisha na dawa. “Kwa mujibu wa UNFPA takriban vituo 46 vya afya nchini Sudan vimeshambuliwa, na karibu theluthi mbili havifanyi kazi tena.Mpango wa hivi karibuni wa msaada wa kibinadamu Sudan unalenga kuwasaidia waty milioni 24.7 ambapo milioni 11 kati yao wanahitaji msaada wa dharura wa huduma za afya na wanawake na wasicha milioni 2.6 miongoni mwao wako katika umri wa kuzaa.
30-6-2023 • 0
30 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia wanawake na wasichana nchini Sudan na kazi ya walinda amani nchini CAR. Makala tutakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Misri, kulikoni?Wanawake na wasichana wanaokimbia machafuko yanayoendelea mjini Kharthoum nchini Sudan wanakabiliwa na changamoto lukuki hususan kwa wajawazito wanaohitaji msaada wa kujifungua, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA ambalo sasa limechukua jukumu la kuhakikisha uzazi salama kwa wanawake hao.Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) wanaohudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR (MONUSCO) wametoa mafunzo ya upishi kwa vikindi vya wanawake wa Kijiji cha Moro kilichoko takribani kilometa 50 kutoka Mji wa Berberati, jimboni Mambere Kadei yalipo makao makuu ya kikosi hicho. Makala tunakupeleka nchini DRC ambapo Muungano wa mashirika ya kiraia katika eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wako katika harakati za kuhamasisha wananchi kupanda miti na kuchukua hatua nyingine zitakazosaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi baada ya eneo hilo kukumbwa na mafuriko yaliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa mapema mwezi Mei Mwaka huu.Katika mashinani na leo tutaelekea nchini Misri ambapo wanawake waliokimbia migogoro nchini Sudan kuelekea nchini humo wanapokea huduma za afya ya akili baada ya kupitia machungu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
30-6-2023 • 0
29 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tukiwa tunaelekea maadhimisho ya pili ya siku ya kimataifa ya lugha ya Kiswahili duniani leo tunaelekea nchini Uganda kuangazia hatua zinazopigwa kufuta kabisa usemi wa mitaani kuwa Kiswahili kilizaliwa Tanzania, kikafa Kenya na kisha kuzikwa Uganda. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za WHO, UNICEF na FAO. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo nampisha Dkt. Mwanahija Ally Juma akitujuza walivyojiandaa kuadhimisha siku ya lugha ya Kiswahili duniani ambayo kilele chake ni Julai 7.Ripoti mpya ya maendeleo yam toto iliyozindiliwa leo mjini Geneva Uswisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO na la kuhudumia Watoto duniani UNICEF inaelezea haja ya kutenga uwekezaji katika huduma ya lishe hususan katika nchi masikini na dhaifu zaidi huku miaka ya kwanza ya maisha ya mtoto ikitoa fursa zisizoweza kuelezeka za kuboresha afya ya maishani, lishe na ustawi.Tukisalia na masuala ya afya nusu ya watu wote duniani bado hawana huduma ya kutosha ya maji safi ya kunywa, usafi wa mazingira na kujisafi yaani WASH ambayo ingeweza kuzuia vifo vya watu milioni 1.4 na Maisha yaliyoboreshwa ya watu milioni 74 wenye ulemavu hadi mwaka 2019 kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya kimataifa iliyotolewa na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO na makala iliyochapishwa katika jarida la afya la Uingereza The Lancet. Na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO pamoja na mashirika manne wadau, wamepewa jukumu la kuongoza mpango wa pamoja wa bahari safi na zenye afya, anmbao ni mradi unaolenga kuanzia kwenye chanzo taka hadi baharini ambao utaelekeza ruzuku ya hadi dola milioni 115 kuzisaidia nchi kukabiliana na uchafuzi wa mazingira ya pwani na mfumo mzima wa Maisha ya baharí.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo nampisha Dkt. Mwanahija Ally Juma akitujuza walivyojiandaa kuadhimisha siku ya lugha ya Kiswahili duniani ambayo kilele chake ni Julai 7.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
29-6-2023 • 0
27 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo inaturejesha hapa Makao makuu ya umoja wa Mataifa kusiki maandalizi ya maadhimisho ya pili ya siku ya Lugha ya Kiswahili duniani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu watoto katika migogoro ya silaha, msaada kwa wakimbizi nchini Sudan na maadili ya akili bandia. Katika mashinani tunakupeleka nchini Mali, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Biashara Ndogondogo na za Kati, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amewapigia chepuo wanawake na wajasiriamali wadogo kwamba wanahitaji kusaidiwa ili kukabiliana na changamoto nyingi ambazo mara nyingi huzuia ukuaji wa biashara zao, na kuwakwamisha wengi wao katika ujasiriamali usio rasmi.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeeleza kuwa linazidi kutishwa na kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu miongoni mwa walioathirika na vita nchini Sudan. Kamishna Mkuu Msaidizi wa Operesheni za UNHCR, Raouf Mazou hii leo mjini Geniva Uswisi amesema wafanyakazi wa UNHCR wanafanya juhudi za kusaidia wananchi lakini ukosefu wa usalama unazuia kufika katika baadhi ya maeneo ili kuwasaidia wenye uhitaji. Na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Kamisheni ya Ulaya wametia saini makubaliano ya kuharakisha utekelezaji wa kimataifa wa Pendekezo la UNESCO kuhusu maadili ya akili bandia. Bajeti ya Euro milioni 4 itatolewa kusaidia nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani ili zifanikishe uundaji wa sheria zao za kitaifa. Takriban nchi 30 tayari zimeanza kutumia Pendekezo hili kutunga sheria za kitaifa zinazohakikisha kwamba matumizi ya akili bandia yanaheshimu uhuru wa kimsingi na haki za binadamu na kuwanufaisha wanadamu wote.Mashinani tutakupeleka nchini Mali ambapo tutaskikiliza jinsi vita inavyoathiri watoto.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
27-6-2023 • 0
Mariam: Dawa za kulevya zilinifanya kupoteza mtoto na mume
Tatizo la dawa za kulevya duniani ni suala tata ambalo linaathiri mamilioni ya watu duniani kote. Watu wengi wanaotumia dawa za kulevya hukumbana na unyanyapaa na ubaguzi, jambo ambalo linaweza kudhuru zaidi afya yao ya kimwili na kiakili na kuwazuia kupata usaidizi wanaohitaji.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu UNODC inatambua umuhimu wa kuchukua mtazamo unaozingatia watu kuhusu sera za dawa za kulevya, kwa kuzingatia haki za binadamu, huruma na mazoea yanayotegemea ushahidi. Miongoni mwa shuhuda nzuri katika jamii ni kuwa wale waliotumia dawa za kulevya wanaweza kurejea kwenye afya zao na maisha yao ya awali iwapo wataacha na kukaaa kwenye vituo vya matibabu ya uraibu na matibabu. Mariam, sio jina lake halisi alikubali na kukaa kituoni na hii ni simulizi yake iliyoandaliwa na UNODC na inasomwa kwako na Evarist Mapesa wa redio washirika SAUTFM iliyoko Mwanza nchini Tanzania.
26-6-2023 • 0
Usambazaji wa Dawa za Kulevya umezidisha mizozo ya kimataifa, ripoti ya UNODC yaonya
Kuendelea kwa ongezeko la usambazaji haramu wa dawa za kulevya na mitandao ya usambazaji inayoendelea kukua inazidisha mizozo ya kimataifa na changamoto za huduma za afya na utekelezaji wa sheria, imesema Ripoti ya Dunia ya Dawa za kulevya mwaka huu 2023 iliyozinduliwa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC). Ulimwenguni kote, zaidi ya watu milioni 296 walitumia dawa za kulevya mwaka 2021, ongezeko la asilimia 23 katika miaka 10 iliyopita imeeleza ripoti hiyo ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na kupambana na dawa za kulevya na uhalifu, UNODC. Takwimu mpya zinaweka makadirio ya kimataifa ya watu wanaojidunga dawa za kulevya kwa mwaka 2021 kuwa milioni 13.2, asilimia 18 juu kuliko ilivyokadiriwa hapo awali. Ripoti hiyo inaeleza zaidi kwamba idadi ya watu wanaougua matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya imepanda kufikia watu milioni 39.5, sawa na ongezeko la asilimia 45 katika kipindi cha miaka 10. Vilevile ripoti hii ya UNODC ina ukurasa maalumu kuhusu ulanguzi wa dawa za kulevya na uhalifu unaoathiri mazingira katika Bonde la Amazon kusini mwa Amerika pamoja na sehemu za majaribio ya kimatibabu yanayohusisha dawa zinazovuruga akili na pia matumizi ya matibabu ya bangi; matumizi ya madawa ya kulevya katika mazingira ya kibinadamu; ubunifu katika matibabu ya dawa na huduma zingine; na madawa ya kulevya na migogoro. Aidha ripoti hiyo ya Dunia ya Dawa za Kulevya pia inaangazia jinsi ukosefu wa usawa wa kijamii na kiuchumi unavyosukuma na pia unavyosukumwa na changamoto za dawa za kulevya; uharibifu wa mazingira na ukiukwaji wa haki za binadamu unaosababishwa na uchumi haramu wa dawa za kulevya; na kuongezeka kwa dawa za kulevya zinazotengenezwa viwandani. Mahitaji ya kutibu magonjwa yanayohusiana na dawa za kulevya bado hayajafikiwa, ripoti hiyo inaeleza na kwamba ni mtu mmoja tu kati ya watano wanaougua matatizo yanayohusiana na madawa ya kulevya waliokuwa katika matibabu ya matumizi ya madawa ya kulevya mwaka wa 2021, na tofauti zinazoongezeka katika upatikanaji wa matibabu katika maeneo yote ulimwenguni. Vijana ndio walio hatarini zaidi kutumia dawa za kulevya na pia huathiriwa zaidi na ugonjwa wa matumizi ya dawa katika maeneo kadhaa ulimwenguni. Barani Afrika, asilimia 70 ya watu wanaopata matibabu dhidi ya dawa za kulevya wako chini ya umri wa miaka 35. Ripoti imeshauri kwamba afya ya umma, kinga, na ufikiaji wa huduma za matibabu lazima zipewe kipaumbele duniani kote vingiunevyo changamoto za dawa za kulevya zitawaacha watu wengi nyuma. Ripoti pia inasisitiza zaidi hitaji la hatua za utekelezaji wa sheria ili kuendana na miundo ya kisasa ya biashara ya uhalifu na kuenea kwa dawa za kulevya za bei nafuu zinazotengenezwa viwandani ambazo ni rahisi kuletwa sokoni. Akitoa maoni yake kuhusu matokeo ya ripoti hii, Mkurugenzi Mtendaji wa UNODC, Ghada Waly amesema, “Tunashuhudia kuendelea kuongezeka kwa idadi ya watu wanaokabiliwa na matatizo ya matumizi ya dawa za kulevya duniani kote, huku matibabu yakishindwa kuwafikia wote wanaohitaji. Wakati huo huo, tunahitaji kuongeza hatua dhidi ya makundi ya biashara ya madawa ya kulevya ambayo yanatumia mizozo na migogoro ya kimataifa ili kupanua kilimo na uzalishaji haramu wa madawa ya kulevya, hasa ya madawa ya kulevya ya viwandani, kuchochea masoko haramu na kusababisha madhara makubwa kwa watu na jamii. Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambao ameutumia kuisihi jamii kutowatenga waathirika wa dawa za kulevya, amehitimisha kwa kusisitiza jumuiya ya kimataifa kuendelea na kazi ya kukomesha matumizi mabaya na ulanguzi haramu wa dawa za kulevya.
26-6-2023 • 0
26 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia lugha ya Kiswhaili na ripoti ya dawa za Kulevya ya UNODC 2023. Makala tunakupeleka nchini Pakistan na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kuendelea kwa ongezeko la usambazaji haramu wa dawa za kulevya na mitandao ya usambazaji inayoendelea kukua inazidisha mizozo ya kimataifa na changamoto za huduma za afya na utekelezaji wa sheria, imesema Ripoti ya Dunia ya Dawa ya mwaka huu 2023 iliyozinduliwa leo na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC).Maadhimisho ya pili ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani yatafanyika wiki ijayo Julai 7 na sasa maandali zi yanafanyika katika kila kona kuhakikisha siku hiyo iliyopewa uzito mkubwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO lakini pia inatumika kama jukwaa la kuziunganisha jamii sio za Afrika tu zinazozungumza Kiswahili ali na nyinginezo zinazokumbatia Kiswahili. Katika makala na leo ikiwa ni siku ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Matumizi Mabaya ya dawa Za Kulevya na Usafirishaji Haramu kauli mbiu ya mwaka huu inasema, “Watu kwanza: acha unyanyapaa na ubaguzi, imarisha kinga”. Tunaelekea nchini Pakistan kusikia kisa cha binti aliyedumbukia kwenye uraibu wa dawa za kulevya na kupoteza kila kitu.Mashinani tutaelekea Kalobeyei huko Kakuma nchini Kenya kusikiliza jinsi ambavyo wakimbizi wanavyoishi kwa utengamano na jamii za wenyeji nchini humo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
26-6-2023 • 0
UNESCO inaungana na Afrika kuenzi Kiswahili - Estelle Zadra
Maadhimisho ya pili ya siku ya lugha ya Kiswahili duniani yatafanyika wiki ijayo Julai 7 na sasa maandali zi yanafanyika katika kila kona kuhakikisha siku hiyo iliyopewa uzito mkubwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO lakini pia inatumika kama jukwaa la kuziunganisha jamii sio za Afrika tu zinazozungumza Kiswahili ali na nyinginezo zinazokumbatia Kiswahili.Estelle Zadra Afisa Uhusiano wa ofisi ya UNESCO hapa New York. ameeleza kwamba kuna mambo mengi yatakayojiri siku hiyo, “Kuanzia hapa New York hadi Paris, Dar es salaam hadi Nairobi na katika miji mbalimbali ya Afrika tutakuwa na mijadala na matukio ya kitamaduni ili kuwafanya washiriki kuwa sehemu ya lugha hii iliyosheheni ya Kiswahili. Mbali ya matukio ya kijamii kama mazungumzo na mijadala tutakuwa na hafla mbalimbali za kitamaduni, kama dansi, muziki na hata chakula cha kitamaduni.”Hata hivyo nilitaka kufahamu nini maudhui ya mwaka huu na kwanini wameyachagua hayo Etelle hakutafuna maneno, “Kiswahili ni lugha ya umoja na mawasiliano kwa watu wengi sana barani Afrika na nje ya Afrika lakini tunataka kuonyesha kwa jinsi gani Kiswahili kilivyo na uwzekao mkubwa katika zama za kidijitali, hivi sasa jamii zetu zimeunganishwa sana na ni muhimu kila mtu kuwa na fursa ya nyenzo hizo na tunazihitaji kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na mijadala katika jamii zetu na kila mtu kushiri hivyo maudhui ya mwaka huu ni “Kuibua uwezo wa Kiswahili katika zama za kidijitali kwa sababu tunauhakika kwamba Kiswahili kinaweza kutumika kama daraja kuunganisha jamii mbalimbali na kuwezesha ujumuishwaji katika ulimwengu wa kidijitali.”Na ili kuhakikisha maudhui haya yanatimia Estelle amesema wanashirikiana kwa karibu n anchi zote za Afrika Mashariki na za Jumuiya ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa afrika SADC ambazo pia zimekikumbatia Kiswahili lakini pia amesema lengo kuu ni kuwafikia vijana hususan wajasiriamali ambao wana hamu ya kutumia nyenzo za kidijitali kujiendeleza na lugha mujarabu kwao ni Kiswahili. Na mwisho Estelle akasema ujumbe wa UNESCO kwa dunia kuhusu siku hii ni kwamba, “Kiswahili sio lugha tu bali ni mkusanyiko mahiri wa urithi uliosheheni wa kitamaduni wa Afrika Mashariki na tunadhani kwa kukumbatia Kiswahili katika zama za kidijitali tunatoa fursa ya kubadilishana utamaduni, kuchagiza ukuaji wa uchumi na uwezeshaji wa kielimu. “ Siku ya lugha ya kiswahili duniani huadhimishwa kila mwaka tareje 7 Julai tangu ilipopitishwa rasmi na UNESCO miaka mwili iliyopita.
26-6-2023 • 0
Fahamu Umuhimu wa yoga katika kujenga mwili
Aina nyingi za mazoezi zinaweza kusaidia kuimarisha maisha yako, lakini hapa tunazingatia zoezi ya yoga kwa sababu ni wiki hii tarehe 21 Juni ambapo ulimwengu umeazimisha siku ya Yogan Duniani.Maudhui ya mwaka huu ya siku hii “Yoga kwa ajili ya ustawi wa sayari moja, familia moja.” Kufahamu zoezi hii kwa undani pamoja na faida zake mwilini, tunamsikiliza mwalimu wa Yoga kutoka Kenya Zepline Ouma.
23-6-2023 • 0
CAR: Walinda amani wa UN kutoka Tanzania na Senegal wafanya mazoezi ya pamoja
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) na wenzao kutoka kikosi cha polisi kinachotoka Senegal wote wakihudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamuhuri wa Afrika ya Kati (MINUSCA), kwa wiki nzima wamefanya mazoezi ya pamoja ya ulinzi wa amani na kutuliza ghasia hususani wakati nchi hiyo ikijiandaa na uchaguzi wa ngazi mbalimbali ikiwemo kura ya maoni kuhusu katiba.Wakiwa wamevalia mavazi maalumu na vifaa vingine vya kujikinga, walinda amani wako katika uwanja wa wazi wanajikumbusha nini kinatakiwa kufanyika pale ambapo watu wenye nia ovu wanapowafanyia vurugu wananchi kwa kuziba barabara na hivyo kukwamisha shughuli za kijamii. Kiongozi wa zoezi hilo Kapteni Boniface Issack ambaye ni Afisa wa mafunzo wa TANBAT 06 anaeleza lengo la zoezi hilo, Naye Mkuu wa uangalizi kwa wanajeshi walioko chini ya MINUSCA Kanali Mussa Abdalla anafafanua zaidi akisema, "Zoezi hili linaonesha kunapokuwa na tatizo wakati wa uchaguzi waandamanaji wanapokuja kwa lengo la kuharibu, kuzuia mchakato wa uchaguzi na kama wana nguvu sana, kikosi cha kuchua hatua za haraka cha Tanzania na Senegal wanaitwa kufanya kazi na kuwaondosha waandamanaji kwenye eneo na uchaguzi kufanyika sawasawa.” Nikiripoti kutoka Beriberati, Mambere Kadei nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, mimi ni Kapteni Mwijage Inyoma, TANBAT 6. TAGS: TANZABAT 06, Jamhuri ya Afrika ya Kati
23-6-2023 • 0
Watumishi wa umma wanachangia ujenzi wa mustakbali bora kwa wote: Guterres
Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ya watumishi wa umma, ambapo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mchango wao ni muhimu sana katika ufanikishaji wa malengo ya maendeleo endelevu na kuhakikisha mustakbali bora kwa wote.Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii amesema lengo lake ni kuwaenzi wanawake na wanaume kote duniani ambao huwajibika kwa jukumu muhimu zaidi la kutoa huduma kwa umaa.Amesema maadhimisho ya siku ya mwaka huu yanakuja wakati Dunia iko katikati ya kuelekea ukomo wa ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu na hivyo amesisitiza kuwa “ Watumishi wa umma na taasisi wanazoziunga mkono zitakuwa muhimu zaidi huku ulimwengu ukiharakisha hatua za kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu, ambayo yako yanakwenda kombo.”Ameichagiza dunia kwamba ili kutimiza malengo hayo “ Teknolojia lazima iwe kiini cha kuongeza kasi hii ya utekelezaji. Kila siku, teknolojia mpya zinaibuka ambazo zinashikilia uwezo wa kubadilisha jinsi tunavyoishi na kufanya kazi. Inapotumiwa na utumishi wa umma wenye ujuzi, uliowezeshwa na wenye vifaa, teknolojia inaweza kuboresha ufikiaji na ufanisi wa huduma za umma, huku ikisukuma maendeleo kuelekea utimizaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu.”Amehitimisha ujumbe wake kwa wito kwamba “Wakati tukiadimisha siku hii muhimu hebu tusherehekee sio tu kazi ya utumishi wa umma kote duniani lakini tutafute njia mpya za kutumia ubunifu katika kazi zetu na kuenzi uwajibikaji wa watumishi hao wa kufanyakazi kwa ushirikiano ili kujenga mustakbali bora kwa watu wote.”
23-6-2023 • 0
23 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia umuhimu wa watumishi wa umma na walinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya kati. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Afrika Kusinin, kulikoni?Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa ya watumishi wa umma, ambapo katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema mchango wao ni muhimu sana katika ufanikishaji wa malengo ya maendeleo endelevu na kuhakikisha mustakbali bora kwa wote. Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) na wenzao kutoka kikosi cha polisi kinachotoka Senegal wote wakihudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamuhuri wa Afrika ya Kati (MINUSCA), kwa wiki nzima wamefanya mazoezi ya pamoja ya ulinzi wa amani na kutuliza ghasia hususani wakati nchi hiyo ikijiandaa na uchaguzi wa ngazi mbalimbali ikiwemo kura ya maoni kuhusu katiba. Katika makala wiki hii tarehe 21 Juni ulimwengu umeadhimisha Siku ya Yoga Duniani na leo tupo nchini Kenya kumsikiliza Zepline Ouma ambaye kwa miaka mitano sasa anafundisha watu kuhusu mazoezi ya Yoga ambayo uhusisha mtu kutuliza mwili sehemu moja au wakati mwingine kunyoosha viungo na kutafakari kwa utulivu.Na leo katika mashinani tuankuletea ujumbe wa Nomzamo Mbatha, Mwigizaji na Balozi mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kutoka nchini Afrika Kusini ambaye kwake, mamilioni ya wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao barani Afrika ni kiini cha moyo wake.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
23-6-2023 • 0
Jifunze Kiswahili: Neno "TATABISI"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo tunafafanuliwa maana ya neno "TATABISI" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.
22-6-2023 • 0
22 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inatupeleka Kenya kuangazia awamu ya pili ya mradi wa PLEAD unaoendesha na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa na uhalifu UNODC nchini Kenya. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za msaada kwa wakulima nchini Ukraine, ripoti ya UNICEF kuhusu watoto katika hatari kubwa ya athari za janga la tabianchi na hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mkataba Mpya wa Ufadhili wa Kimataifa Paris. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kufafanuliwa maana ya neno"TATABISI", salía hapo hapo!Zaidi ya watoto bilioni moja wako katika hatari kubwa ya athari za janga la tabianchi, kwa mujibu wa ripoti mpya kuhusu Hatari za Tabianchi kwa Watoto iliyofanywa na Muungano wa Mpango wa Haki za Mazingira za Watoto (CERI) ambao unahisisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF, Plan International na Save the Children. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo mjini Paris, Ufaransa kupitia hotuba yake kwenye hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Mkataba Mpya wa Ufadhili wa Kimataifa amerelea ombi lake la mageuzi makubwa ya muundo wa fedha wa kimataifa na kuwasilisha mapendekezo yake ikiwa ni pamoja na kichocheo cha Malengo ya Maendeleo Endelevu, (SDG) ili kusaidia nchi zinazoendelea na zinazoibukia kiuchumi ili kuurudisha ulimwengu kwenye mstari wa kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wamezindua mpango wa pamoja kwa ushirikiano na shirika la FSD (Fondation Suisse de Déminage) kusaidia wakulima wadogo na familia za vijijini zilizoathiriwa zaidi na vita huko nchini Ukraine.Na leo katika jifunze Kiswahili tunafafanuliwa maana ya neno "TATABISI" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
22-6-2023 • 0
Mradi wa ALiVE awamu ya pili kupima stadi za watoto nje ya masomo ya kawaida Zanzibar
Baada ya kufanya tathmini ya upimaji Stadi za maisha na maadili kwa vijana wenye umri wa miaka 13 hadi 17 nchini Kenya, Uganda na Tanzania, mradi wa ALiVE katika awamu ya pili umepanga kuwafikia watoto wenye umri wa miaka 6 hadi 12 ambao bado wako shule ili kuwapima viwango vyao vya Stadi za maisha na maadili ikiwa ni katika jitihada za kuchechemua fikra tunduizi na kusongeza malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu, SDGs. Kama ambavyo mradi huu utatekelezwa katika maeneo mengine ya Afrika Mashariki, Visiwani Zanzibar nako uzinduzi umefanyika na hapa Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM kutoka Morogoro, Tanzania amesafiri hadi Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi visiwani humo Zanzibar na kutuandalia na kutuandalia Makala hii.
21-6-2023 • 0
21 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia Migogoro nchini Ukraine na wakimbizi nchini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Tanznai na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa, kulikoni? Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine Matthew Hollingworth amelaani vikali shambulio lililofanywa na Urusi kwenye eneo la Kherson lililoathirika vibaya na mafuriko ya bwawa la Kakhovka, na kukatili maisha ya mfanyakazi wa ukoaji na kujeruhi wengine.Serikali ya Kenya inaendesha mradi wa “shiriki” ambao unawapa fursa wakimbizi wanaosihi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko katika kaunti ya Turkana nchini humo kujitegemea kwa kufanya kilimo cha mbogamboga kupitia chama cha ushirika wa wakulima. Serikali hiyo imetenga ekari 21katika kambi ya Kakuma ili kutumika katika mradi huo ambao sio tu unawapa lishe bora wakimbizi, matumaini na kipato lakini pia umekuwa neema kwa jamii za wenyeji. Katika makala Mwandishi wa redio washirika wetu MVIWATA FM ya Tanzania anatupeleka visiwani Zanzibar ambako umezinduliwa mradi wa AliVE awamu ya pili unaolenga kupima stadi za maisha na maadili kwa wanafunzi Watoto wa umri wa miaka 6 hadi 12.Na mashinani leo ikiwa ni siku ya Yoda duniani tunarejea makao makuu ya Umoja wa Mataifa kusikia ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo alieleza kwa nini yoga ni muhimu katika maisha ya mwanadamu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
21-6-2023 • 0
Umoja wa Mataifa imelaani vikali shambulio lililoua na kujeruhi wafanyakazi wa ukoaji Kherson Ukraine
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine Matthew Hollingworth amelaani vikali shambulio lililofanywa na Urusi kwenye eneo la Kherson lililoathirika vibaya na mafuriko ya bwawa la Kakhovka, na kukatili maisha ya mfanyakazi wa ukoaji na kujeruhi wengine. Katika tarifa yake iliyotolewa leo mjini Kyiv Ukraine mratibu huyo Hollingworth amesema “Inasikitisha sana kwamba waokoaji wameuawa na kujeruhiwa jana huko Kherson walipokuwa wakisaidia jamii zilizoathiriwa na uharibifu mkubwa wa bwawa la Kakhovka.”Kwa mujibu wa duru za habari mfanyakzi mmoja wa uokoaji wa ofisi ya huduma za dharura za Ukraine ameuawa katika shambulio hilo wakati waokoaji wengine wanane wamejeruhiwa huku sita wakielezwa kuwa katika hali mbayá.Imeleezwa kuwa shambulio hilo lililtokea wakati vikosi vya jeshi la Urusi vilipowafyatulia risasi wafanyakazi hao wa uokoaji wakiwa wakiwa katika operesheni za kusafisha matope yaliyotokana na uharibifu katika bwawa la Kakhovka.Kwa niaba ya jumuiya ya masuala ya kibinadamu bwana Hollingworth ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu na kuwatakia majeruhi wote ahuweni ya haraka akiongeza kuwa “Fikra zetu pia ziko na ofisi ya huduma za dharura za Ukraine, inayofanya kazi katika mazingira magumu sana kusaidia watu wake.”Mratibu huyo wa masuala ya kibinadamu amekumbusha kuwa “Tukio hili ni mfano mwingine wa athari mbayá za kibinadamu za uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.” Na amesisitiza kwamba raia wote wakiwemo wafanyakazi wa ukoaji wanalindwa chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu na kuwashambulia na kuwaua ni jambo lisilokubalika.
21-6-2023 • 0
Wakimbizi Kenya: Mradi wa shiriki ni neema kwetu na jamii inayotuhifadhi
Serikali ya Kenya inaendesha mradi wa “shiriki” ambao unawapa fursa wakimbizi wanaosihi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko katika kaunti ya Turkana nchini humo kujitegemea kwa kufanya kilimo cha mbogamboga kupitia chama cha ushirika wa wakulima. Serikali hiyo imetenga ekari 21katika kambi ya Kakuma ili kutumika katika mradi huo ambao sio tu unawapa lishe bora wakimbizi, matumaini na kipato lakini pia umekuwa neema kwa jamii za wenyeji.Katika makazi ya Kalobeyei kambini Kakuma maisha yanaendelea kama kawaida kwa maelfu ya wakimbizi yakighubikwa na pilika nyingi kikiwemo kilimo cha mchicha, Sukuma na mbogamboga zingine chini ya mradi wa shiriki. Abdulazizi Lugazo ni mkimbizi kutoka Somalia na mwenyekiti wa chama hicho cha ushirika wa wakulima anasema, Abdulazizi anasema mradi huu ulianza kidogokidogo lakini sasa umepanuka na kujumuisha wakimbizi wengi zaidi, Kenya imekuwa mwenyeji wa wakimbizi kwa zaidi ya miaka 30 na inaamini kuwapa fursa hii wakimbizi sio tu inawapa matumaini badi inawajengea uwezo. Mkimbizi kutoka Congo DRC anayeshiriki mradi huu Muhawe Selene ambaye ni mchuuzi wa mbogamboga sokoni anaafiki, Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR mtazamo kama huu wa Kenya unapaswa kuigwa na mataifa mengine kwani unawajumuisha wakimbizi na kusaidia kuleta utangamno baina ya wakimbizi na jamii zinazowahifadhi.Kwa Abdulazizi mradi huu umemfungulia njia mpya ya matumaini akiwa mbali na nyumbani.UNHCR Imeishukuru Kenya kwa kuwapa matumaini wakimbizi hawa wakiwa mbali na nyumbani, na Kenya inasema huu ni mwanzo tu kwani iko katika mipango ya kutekeleza sera ambazo ni bunifu na jumuishi zitakazowaruhusu baadhi ya wakimbizi hao nusu milioni na waomba hifadhi nchini humo kufanya kazi na kuishi na Wakenya.
21-6-2023 • 0
HABARI ZA UN 20 JUNI 2023
Ikiwa leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani tutawasikia wakimbizi wa ndani DRC wanavyozungumzia harakati za Umoja wa Mataifa katika kutekeleza Kauli mbiu ya mwaka huu:"Matumaini Mbali na Nyumbani.".Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia ujumbe wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwa siku hii ya wakimbizi duniani akihimiza mshikamano na ushirikiano na wakimbizi. Naye kamishna wa wakimbizi Filippo Grandi ameadhimisha siku hii akiwa katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma iliyoko nchini kenya ambapo ametoa wito kwa wadau kuunga mkono wakimbizi lakini pia kuzisaidia nchi zinazopokea na kuwahifadhi wakimbizi kama Kenya.
20-6-2023 • 0
Viwavi jeshi vimerejea Afrika Mashariki, FAO kusaidia kuvikabili
Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, limetahadharisha kuwa viwavijeshi ambavyo vimeripotiwa kuonekana kwenye mbuga na hifadhi za wanyama nchini Kenya vimerejea.Wadudu hao pia wameonekana kwenye mataifaJirani ya Eritrea, Sudan Kusini,Ethiopia, Somalia na Uganda. Ifahamike kuwa mwaka 2016 viwavijeshi vilionekana kwenye mataifa 6 pekee barani Afrika.Viwavijeshi vina uwezo wa kuvamia na kukomba mazao ya mahindi, ngano, mtama, shayiri na nyasi. Kwa undani zaidi wa juhudi hizo ungana na mwandishi wetu wa Kenya Thelma Mwadzaya katika Makala hii.
19-6-2023 • 0
Kina mama wa Srebenica waeleza athari za kauli za chuki
Hapo jana juni 18 dunia iliadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga kauli za chuki ambapo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kumefanyika maonesha ya athari ziletwazo na kauli za chuki. Wawakilishi watatu wa taasisi ya Kina mama wa Srebrenica walitembelea maonesho hayo na kuzungumzia maswahibu yaliyowakumba miaka 28 iliyopita na kuacha vidonda katika mioyo yao. Taarifa ya Leah MushiMwaka 1995 katikati ya vita vya Bosnia Umoja wa Mataifa ulianzisha eneo la usalama huko Srebrenica, lakini ilipofika mwezi Julai mji huo ulizidiwa na vikosi vya wanamgambo wa Bosnia-Serb ambao walitekeleza mauaji ya wavulana na wanaume wa kiislamu wapatao 8,000 ndani ya wiki moja.Mauaji hayo ya kimbari ya Srebrenica yanachukuliwa kuwa ukatili mkubwa zaidi barani Ulaya tangu Vita vya pili vya dunia. Mwaka 2002 Chama cha kina mama wa Srebrenica kilianzishwa na kuunganisha maelfu ya wanawake waliopoteza wapendwa wao.Watatu kati ya wanachama wa chama hicho wametembelea Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani na kueleza kwa zaidi ya miaka 20, shirika hilo limekuwa likitafuta watu waliopotea, kutafuta makaburi ya halaiki, nakujaribu kutambua kila mwathiriwa na maiti, kusaidia walionusurika, na kutafuta haki.Akiwa ameshikilia picha mkononi mwake Kada Hotić, anaeleza mpaka sasa hajafanikiwa kuona maiti za wapendwa wake.Kada Hotić – Sauti ya Happines Palangyo“Huyu ni mume wangu, mwanangu, na ndugu zangu wawili…. Mwaka 2013, nilizika mifupa miwili ya mguu mmoja wa mwanangu. Uchunguzi wa DNA ulithibitisha kwamba mifupa hii miwili ilikuwa mwanangu. Ndivyo nilivyozika. Nina umri wa miaka 79 sasa. Bado sijachoka na bado napigana. Na nitaendelea kupigana. Kwa jina la haki na kwa jina la ubinadamu.”Naye Rais wa chama cha hicho cha kina mama wa Srebenica Munira Subašić, anaeleza ingawa alinusurika katika mauaji hayo ya halaiki yaliyogharimu maisha ya wanafamilia yake 22 kuna namna na yeye amekufa.Munira Subašić – Sauti ya Devotha Songorwa“Mwanangu alikuwa mtoto mzuri sana. Alikuwa mwanafunzi mzuri. Alipenda maisha. Alipenda hesabu. Alijali marafiki zake kwa dhati. Hata hivyo, hatima ilichukua mkondo wake. Kila wakati ninapozungumza juu yake, nafsi inanirejesha wakati ule, mwaka 1995. Kilichotokea ni kwamba hawapo tena. Ninajua tu kwamba kila mama ambaye amefiwa na mtoto wake pia kwa njia fulani naye amekufa. “Kwa masikitiko Munira anatuma ujumbe akisemaMunira Subašić – Sauti ya Devotha Songorwa“Ujumbe wangu kwa kina mama wote duniani ni kujaribu kuwalea watoto kwa upendo na kuwafundisha kupenda na kupendwa na sio kuleta madhara kwa mtu yeyote kwa njia yeyote”Mwenyeji wa kina mama hawa katika Makao Makuu ya UN alikuwa ni Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari Alice Wairimu Nderitu ambaye anasema pamoja na uwepo wao kina mama hawa bado kuna baadhi ya watu wanaendelea kuamini mauaji haya hayakutokeaAlice Wairimu Nderitu – sauti ya Sarah Oleng’“Uwepo wao hapa ni ukumbusho wa kile ambacho hakipaswi kutokea tena. Uwepo wao hapa unamaanisha kuwa hadithi huwekwa hai. Ina maana kwamba tunaweza kuendelea kujiuliza, ni kitu gani tunaweza kufanya vizuri zaidi ili mauaji haya ya kimbari yasitokee tena. Bado tunasikia, hadi leo, watu wanakataa mauaji ya kimbari, watu wakisema kuwa hayakufanyika. Umoja wa Mataifa ulianzishwa kwa ahadi ya kuzuia mauaji kutokea tena. Ahadi hii ni ngumu kutimiza, lakini lazima tuendelee kujaribu kuitimiza.”
19-6-2023 • 0
Ukatili wa kingono katika mizozo ni jinamizi lililokita mizizi katika pengo la usawa: UN
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono katika mizozo ya vita Umoja wa Mataifa umesenma jinamizi hilo ni janga lililokita mizizi katika kukosekana kwa usawa na kanuni na tamaduni kali za masuala ya kijinsia. Tupate maelezo Zaidi kutoka kwa Flora Nducha(TAARIFA YA FLORA NDICHA)Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa leo mjini Brussells na New York na mwakilishi wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kingono katika mizozo Pramila Patten na mwakilishi wa Muungano wa Ulaya kwa ajili ya mambo yan je na sera za usalama Josep Borrell wametoa wito wa hatua madhubuti zaidi za kuzuia na kukomesha unyanyasaji wa kingono, na kuendeleza usawa wa kijinsia kama kipaumbele cha kisiasa. Wamesema “Tunasikitishwa na kuongezeka kwa matumizi ya unyanyasaji wa kingono kama mbinu ya kikatili ya vita, mateso, ugaidi na ukandamizaji wa kisiasa, na tishio kwa usalama wa pamoja. Hatari ya kuwa mlengwa wa unyanyasaji wa kingono leo inazidishwa na ukweli kwamba uhalifu huu unaweza pia kuwezeshwa na kukuzwa mtandaoni, kwa kutumia chaneli za kidijitali.”Badala ya kutumika vibaya wamekumbusha kuwa “Wakati huo huo, majukwaa ya kidijitali yanaweza kuwa na jukumu muhimu na kuwa chombo chenye nguvu cha kuboresha usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana, na kuchangia katika kujenga uwezo wao wa kustahimili nyakati za shida. Wanaweza pia kusaidia katika kuzuia unyanyasaji wa kingono na kijinsia, na hatua zinazohitajika, kupitia tahadhari za mapema na kuunganisha waathiriwa na njia za kuwatambulisha kwenye huduma, na kuwezesha kuripoti..”Viongozi hao wameonya kwamba badala ya kuwa msaada kwa waathirika leo hii “Mitandao hiyo inatumika vibaya kusambala kauli za chuki na kuchochea ukatili wa kijinsia na ubaguzi, kwani kauli za chuki za kijinsia zinaendelea kuongezeka kutumika kuwanyamazisha watetezi wa haki za binadamu, na wanaharakati wa kisiasa kwa kuchagiza utekelezaji wa ukatili wa kingono. Katika mazingira yaliyoathiriwa na migogoro, majukwaa ya kidijitali yanatumiwa kusafirisha kiharamu wanawake na wasichana kwa madhumuni ya unyanyasaji wa kingono. Walanguzi wa ngono wanatumia mtandao kama zana ya kuajiri wanawake na haswa Watoto na kutangaza huduma za kinyonyaji.”Wameongeza kuwa na katika mazingira mabaya zaidi wanawake na wasichana wanauzwa mtandaoni kama ilivypoainishwa kwenye maenmeo yanayodhibitiwa na kundi la kigaidi la ISILZaidi ya hayo wamesema “ upotoshaji wa habari kwa makusudi na udhibiti kupitia kampeni za kutoa taarifa potofu unaathiri uwezo wa mataifa kulinda raia na kushughulikia unyanyasaji wa kingono. Matumizi ya intaneti kama silaha katika maeneo yenye migogoro pia huzuia waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro kupata taarifa kuhusu huduma za kuokoa maisha na kupata usaidizi wa mtandaoni kama vile usaidizi wa kisaikolojia.”Kwa mantiki hiyo wametoa wito wa kuwa na “Majukwaa salama ya kidijitali yanayotii sheria za kimataifa, ili waathirika wa unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro na wale wanaowaunga mkono watumie mifumo hii kupambana na ukwepaji wa sheria na kudai uwajibikaji ulioboreshwa. Ni muhimu kukuza mazingira ya ulinzi mtandaoni na nje ya mtandao, ambayo yanazuia unyanyasaji wa kijinsia na vile vile kuwezesha kuripoti kwa usalama na makuchukuliwa hatua zinazofaa.”Pia wameitaka Jumuiya ipambane kwa Pamoja dhidi ya tishio linaloongezeka kila mara linaloletwa na teknolojia ya kidijitali na kuziba pengo la mgawanyiko wa kidijitali wa kijinsia ili kuruhusu waathiriwa kupata rasilimali na kupambana na ukwepaji wa sheria kwa kuzingatia kujenga usawa wa kijinsia kwa kuzuia na kupambana na unyanyasaji wa kingono katika migogoro.Wamehitimisha ujumbe wao kwa kusema kuwa “Kwa kushughulikia mgawanyiko wa kidijitali wa kijinsia, tunaweza kuunda ulimwengu ambapo wanawake na watoto wanaweza kuishi bila woga na vurugu.”Siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono katika mizozo…
19-6-2023 • 0
19 JUNI 2023
Leo jarida la Umoja wa Mataifa linaangazia siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono katika mizozo ya vita, Umoja wa Mataifa umesema jinamizi hilo ni janga lililokita mizizi katika kukosekana kwa usawa, kanuni na tamaduni kali za masuala ya kijinsia.Utasikia pia kuhusu maonesha ya athari ziletwazo na kauli za chuki ambapo wawakilishi watatu wa taasisi ya Kina mama wa Srebrenica walitembelea maonesho hayo na kuzungumzia maswahibu yaliyowakumba miaka 28 iliyopita na kuacha vidonda katika mioyo yao.Makala hii leo inaangazia taarifa za viwavi jeshi kuibuka tena nchini Kenya na juhudi za FAO kukabiliana navyo ikiwemo kuwapatia mafunzo maafisa wa nchi za pembe ya Afrika wanaohusika na kupambana na wadudu hao.Na mashinani tunaenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC ambapo utamsikia afisa wa jeshi la polisi anayehakikisha ulinzi wa wanawake na wasichana wanaokabiliwa na vitendo kwa ukatili wa kijinsia.
19-6-2023 • 0
WMO kuimarisha mifumo ya tahadhari ya mapema dhidi ya majanga Afrika Mashariki
Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani WMO kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupunguza hatari za majanga UNDRR wiki hii wamezindua mradi mpya wa kuimarisha mifumo ya tahadhari ya mapema ya kikanda. Mradi huo uliopewa jina “Kuimarisha huduma za hali ya hewa na tahadhari ya mapema katika Ukanda wa Afrika Mashariki” utafanya kazi katika nchi sita za ukanda huo ambazo ni Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda, Burundi na Sudan Kusini.Uzinduzi huo umefanyika katika katika mji mkuu wa Rwanda Kigali, nchi ambayo hivi karibuni ilishuhudia athari mbayá za hali ya hewa kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na mafuriko yaliyogharimu maisha ya zaidi ya watu 135. Umoja wa Mataifa na serikali wanasema mifumo ya tahadhari ya mapema inaweza kuwa na jukumu muhimu katika kuzuia athari za matukio mabaya kama hayo. Eugene Uwimana Afisa uratibu msaidizi wa maendeleo, mawasiliano na mipango katika ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda amezungumza na Macklin Merchades, kutoka ofisi ya utabiri wa hali ya hewa ya Tanzania (TMA) atakayeongoza mradi huo kwa Tanzania na hapa anaanza kwa kufafanua kuhusu mradi huo.
16-6-2023 • 0
16 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia manufaa ya utumaji pesa kutoka nchi moja kwenda nyingine, na uwezeshaji wa wavuvi nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na mashinani nchini Colombia, kulikoni? Leo ni Siku ya Kimataifa ya Utumaji fedha kwa familia ambapo maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia manufaa ambayo ujumuishaji wa kidijitali na kifedha unapohusishwa na utumaji pesa kutoka nchi moja kwenda nyingine, huzisaidia familia zinazopokea fedha kufikia Malengo yao ya Maendeleo Endelevu, SDGs.Mkuu wa Mpango wa umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS ambaye pia ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom amefanya ziara maalum ya kutembelea visiwa vilivyopo katika kaunti ya Terekeka na kujionea utekelezaji wa miradi ya stadi za maisha inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO. Makala leo inatupeka mji mkuu wa Rwanda Kigali ambako shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO wiki hii limezindua mradi mpya wa “Kuimarisha huduma za hali ya hewa na tahadhari ya mapema katika Ukanda wa Afrika Mashariki” ukijumuisha nchi zote sita za ukanda huo ambazo ni Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda, Burundi na Sudan Kusini.Na katika mashinani na tukielekea siku ya wakimbizi Duniani, tutakupelekea nchini Combia kusikia jinsi mwansheria ambaye amelelewa katika kambi ya wakimbizi wa ndani Maisha yake yote na hatimaye kuweza kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanasheria ameamua kuzihudumia jamii zilizo chini ya tishio la kigaidi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
16-6-2023 • 0
Manufaa ya ujumuishaji wa kidijitali na kifedha unapohusishwa na utumaji pesa kutoka nchi moja kwenda nyingine
Leo ni Siku ya Kimataifa ya Utumaji fedha kwa familia ambapo maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia manufaa ambayo ujumuishaji wa kidijitali na kifedha unapohusishwa na utumaji pesa kutoka nchi moja kwenda nyingine, huzisaidia familia zinazopokea fedha kufikia Malengo yao ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD, asilimia 14 ya idadi ya watu duniani, au watu bilioni 1, hutuma au kupokea fedha. Hiyo ni sawa na wafanyakazi wahamiaji milioni 200 wanaotuma fedha kwa wanafamilia milioni 800 kote duniani. David Casian ni mwanadiaspora wa Tanzania anayeishi kwa miaka mingi nchini Marekani anaeleza namna matumizi ya dijitali yamesaidia sana katika utumaji fedha nyumbani, “Teknolojia ya kidijitali kitu cha kwanza walichofanya ni kuondoa mambo ya katikati mengi ambayo yalikuwa yanatuzuia na imeleta ufanisi. Katika muda mdogo tu unaweza ukatuma pes ana mpokeaji akapokea kule nyumbani na kama kuna tatizo la haraka likatatuliwa. Kwa hiyo hivi ni vitu vya muhimu sana tunapenda dijitali kwa sababu kweli imeleta mapinduzi makubwa na tumeweza kufanya mambo mengi kwa wakati mchache.” Aidha Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaeleza kuwa mwaka jana 2022, utumaji fedha kimataifa kwa mataifa ya kipato cha chini na cha kati ulifikia dola bilioni 626. Wastani wa kila mwezi wa dola za Marekani 200 hadi 300 zinazotumwa na wafanyakazi wahamiaji husaidia familia nyingi duniani kote na mwanadiaspora huyu David Casian ni shuhuda wa hilo, “Pesa tunazotuma nyumbani zinasaidia wanafamili kwa upande wa mmoja mmoja lakini pia zinasaidia jamii nzima ya watu wetu. Mtu anaweza akawa anaumwa ukatuma pesa akaweza kutibiwa. Ukatuma pesa mtoto amerudishwa kwa ada shuleni unatuma. Unatuma pesa kwa ajili ya mambo ya uchumi labda mtu anahitaji hela kwa ajili ya kufungua kabiashara kidogo ili aweze kujikimu na hii inasaidia kuchangia uchumi wa mtu mmoja mmoja na vile vile kwa taifa kuijumla. Kwa hiyo ni kitu kizuri na ni kitu cha kukiendeleza na kushukuru kwamba dijitali kwakweli imeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya utumaji pesa.”
16-6-2023 • 0
Jamii ya Wavuvi Sudan Kusini wawezeshwa na FAO kutengeneza mnyororo wa thamani
Mkuu wa Mpango wa umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS ambaye pia ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom amefanya ziara maalum ya kutembelea visiwa vilivyopo katika kaunti ya Terekeka na kujionea utekelezaji wa miradi ya stadi za maisha inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO. Katika ziara hiyo maalum, Mkuu wa UNMISS aliambatana na wawakilishi wa FAO pamoja na Benki ya Dunia ambao ni miongoni mwa wahusika wa moja kwa moja wa kuendesha Mradi wa Kuimarisha Ustahimilivu wa Jamii ya Wavuvi -FICREP ambao unawajengea uwezo wananchi wa visiwani ambao kwa kiasi kikubwa wanajishughulisha na biashara ya Samaki. Mwakilishi wa FAO nchini Sudan Kusini Meshack Malo anasema malengo ya miradi yao ni kuziwezesha jumuiya za wavuvi kutengeneza mnyororo wa thamani na kuwa na biashara stahimilivu kwakutumia vyema uwepo wao katika ukanda wa mto Nile, “Unakuta kwamba changamoto walizonazo Wasudan Kusini na wakazi wa Terekeka ni kuongeza muda wa kuhifadhi samaki. Hapo awali walikuwa wakipata samaki asubuhi na ikifika jioni chochote kile ambacho hakijauzwa wanatupa. Kwa hivyo, tumeanzisha ukaushaji wa Samaki ili waweze kuchukua hadi miezi minane. Kwa teknolojia ya usindikaji tunatumai kuwa wananchi hawa wanaweza kupata thamani ya pesa.”Mbali na kuwapatia vifaa vya kuvulia pamoja na kusindika samaki, FAO inaendesha mafunzo ya kutunza na kuhifadhi Samaki, kutafuta masoko na kutengeneza uhusiano mwema. Vijana nao wanafundishwa kutengeneza mitumbwi ya kuvulia samaki ambayo inadumu na haiingizi maji.Miradi hii tayari imeanza kuwa na matokeo chanya, mfano wanawake wamewezeshwa kujenga mtandao wa kimataifa na kujikwamua kiuchumi, wamepelekwa katika ziara za kimasomo kwenye nchi za Kenya, Uganda na Ghana, ambako wamejifunza njia za gharama nafuu na zenye afya za kuendesha biashara zao suala lililo mfurahisha mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini Nicholas Haysom, “Nimepata uzoefu muhimu san,a sio tu kwa kutoka nje ya mji wa Juba na kuja kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi wa kawaida wa Sudani Kusini, lakini kujionea mradi huu wenye mafanikio makubwa yamradi huu unaotekelezwa na Wasudan Kusini wa kawaida. Nadhani kuna utambuzi mpana kwamba huko Sudan Kusini hakuwezi kuwa na amani bila maendeleo, lakini tunajua kuwa hakuwezi kuwa na maendeleo bila amani. Kwa maana hii, kaunti hii inawakilisha jaribio la kweli, la kusitawisha amani, lakini pia mradi ambao matunda ya amani yanaweza kuhisiwa na watu wote.”Mkuu huyo wa UNMISS amehitimisha ziara yake kwakusema jumuiya zinazofanya maamuzi na kuyasimamia zinafanikiwa na kuwa mfano bora kwa jamii zote za nchini Sudan Kusini.
16-6-2023 • 0
Jifunze kiswahili: Je, wajua maana ya neno "KUYEYESA"?
Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunafafanuliwa maana ya neno "KUYEYESA" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, karibu!
15-6-2023 • 0
15 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo inatupeleka Congo DRC kusikia kinachowasibu wakimbizi wa ndani waliofurishwa na waasi wa ADF na kinachofanywa na Umoja wa Mataifa kuwasaidia. Pia tunakuletea habari kwa ufupi za IOM, UNITAMS na WMO. Katika kujifunza lugha ya tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kufafanuliwa maana ya neno "KUYEYESA" Tangu mwaka huu uanze mwezi Januari mpaka mwezi huu wa Juni, Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limerekodi takriban watu milioni 1 walioyahama makazi yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC kutokana na machafuko yanayotekelezwa na vikundi vya wanangambo.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia kipindi cha mpito nchini SUDAN, UNITAMS umelaani vikali mauaji ya Gavana wa jimbo la Darfur Magharibi Khamis Abdullah Abbaker yaliyotekelezwa hapo jana na kutaka wale wote waliohusika kufikishwa mbele ya sheria. Na tarifa ya kila mwaka ya ‘Kutoa tahadhari mapema kwa kila mtu” iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO imeeleza kuwa juhudi kubwa zilizofanywa na nchi mbalimbali mwaka jana 2022 za kuweka mifumo ya kutoa taarifa za mapema kuhusu majanga ya hali ya hewa zinakadiria kuwa wastani wa watu milioni 111 wapo katika mazingira mazuri ya kujulishwa mapema kuchukua tahadhari.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunafafanuliwa maana ya neno "KUYEYESA" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
15-6-2023 • 0
Taasisi 16 zakutana Morogoro Tanzania kusongesha SDG 4
Taasisi 16 zikiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia na vyuo vikuu ambao kwa pamoja ni wanachama wa Mtandao wa Elimu Afrika Mashariki (RELI) wamekutana mjini Morogoro, Tanzania kujengewa uwezo wa namna ya kuimarisha juhudi za kuchochea mabadiliko ya elimu na kuhamasisha ujengaji fikra tunduizi kwa vijana ili kusongesha lengo namba 4 la Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu SDGs. Mafunzo haya yameratibiwa na Shirika lisilo la kiserikali la GESCI (The Global e-Schools and Communities Initiative) kutoka nchini Kenya linalotekeleza mradi wa ADAPT Kenya na Tanzania, Mwandishi wa Habari Hamad Rashid wa Redio washirika wetu MVIWATA FM ya Morogoro Tanzania amefuatilia mafunzo hayo ya siku tatu na kutuandalia makala ifuatayo.
14-6-2023 • 0
UNICEF: Idadi ya watoto waliotawanywa duniani imevunja rekodi na kufikia milioni 43.3
Katika kuelekea siku ya wakimbizi duniani itakayoadhimishwa wiki ijayo, ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imeonya kwamba idadi inayoongezeka ya watoto kutawanywa duniani, inadhihirisha jinsi gani dunia ilivyoshindwa kushughulikia mizizi ya watu kutawanywa na kutoa suluhu ya muda mrefu hususan kwa watoto wanaolazimika kukimbia makwao.Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa leo mjini New York hadi kufikia mwisho wa mwaka jana 2022 makadirio ya UNICEF yanaonyesha kwamba watoto milioni 43.3 walilazimika kuishi maisha ya kutawanywa na wengi wao katika utoto wao wote.Ripoti inasema idadi ya watoto waliofurushwa kwa lazima kutoka makwao iliongezeka maradufu katika muongo uliopita, na hivyo kupita juhudi za kuweza kuwajumuisha na kuwalinda wakimbizi na watoto ambao ni wakimbizi wa ndani. Na vita nchini Ukraine imechochea hali kuwa mbaya zaidi ikiwalazimu zaidi ya watoto milioni 2 wa Ukraine kuikimbia nchi hiyo na kkuwafanya wengine zaidi ya milioni 1 kuwa wakimbizi ndani.Akizungumzia jinamizi hili mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Catherine Russell amesema."Kwa zaidi ya muongo mmoja, idadi ya watoto wanaolazimika kuhama makwao imeongezeka kwa kasi ya kutisha, na uwezo wetu wa kimataifa wa kukabiliana na hali hiyo bado uko katika shinikizo kubwa. Ongezeko hilo linakwenda sambamba na mashambulizi ya mara kwa mara ya migogoro, changamoto na majanga ya tabianchi duniani kote. Lakini pia inadhihirisha hali duni za serikali katika kuhakikisha kila mkimbizi na mtoto aliyetawanywa ndani ya nchi anaweza kuendelea kusoma, kuwa na afya njema na kuendelea ili kufikia uwezo wake kamili.”Miongoni mwa watoto hai milioni 43.3 waliolazimika kutawanywa takribani asilimia 60 sawa na watoto milioni 25.8 walikuwa ni wakimbizi wa ndani waliotokana na mizozo na machafuko.Na idadi ya watoto wakimbizi na wasaka hifadhi ilifikia kiwango cha juu cha watoto milioni 17.5 bila kujumuisha watoto waliotawanywa mwaka huu wa 2023.Kwa mantiki hiyo UNICEF imetoa wito kwa serikali zote kutomwacha mtoto yeyote nyuma kwa kutambua watoto wakimbizi, wahamiaji na waliotawanywa cha kwanza ni watoto na wana haki ya kulindwa, kujumuishwa na kushirikishwa. Pili imezitaka serikali kutoa njia salama na za kisheria kwa watoto kuweza kuhama, kuomba hifadhi na kujumuishwa na familia zao.Tatu kuhakikisha hakuna mtoto anayeshikiliwa kwa sababu ya hali yake ya uhamiaji au kurejeshwa bila mazingira salama isipokuwa tu pale ambapo imebainika kuwa ni kwa maslahi ya mtoto.Nne imezitaka serikali kuimarisha mifumo ya kitaifa ya elimu, afya, ulinzi kwa watoto na mifumo ya hifadhi ya jamii ili kujumuisha watoto waliotawanywa bila ubaguzi.Tano kuwekeza katika mifumo ya ulinzi kwa watoto ili kuweza kuwalinda vyema watoto walio safarini dhidi ya hatari za kunyanyaswa na ukatili hususan watoto wanaokimbia peke yao bila walezi au wazazi.Na mwisho imezitaka serikali kusikiliza na kuwahusisha watoto katika kusaka suluhu ambazo ni endelevu na jumuishi na ambazo zinaweza kuwasaidia watoto hao kufikia uwezo wao.
14-6-2023 • 0
Sudan: Watoto 297 wafanikiwa kuhamishwa kutoka eneo la vita mpaka eneo salama
Kufuatia vita inayoendelea nchini Sudan, watoto 297 wamehamishwa kwa usalama kutoka kituo cha watoto yatima cha Mygoma huko Khartoum nchini Sudan hadi kituo cha muda katika eneo salama zaidi nchini humo. Mafundi uashi wakichomelea vyuma na wengine wakiwa wanachomelea nguzo varandani…… Nje wahandisi wanaonekana wakijadili jambo eneo la genereta… haya yote yakiendelea ndani ya eneo ambalo linaonekana kama ukumbi mkubwa wenye viti vichache wakionekana wanawake wameketi wengine wamesimama na watoto wadogo wakicheza katika mikeka na zulia jekundu. Hapa ni Madani, mji mkuu wa jimbo la Al Jazirah lililoko mashariki ya kati mwa nchi ya Sudan. Eneo hili ndio makazi mapya salama ya watoto 297 waliotolewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mygoma huko Khartoum ambapo sasa hali si shwari, vita vime taradadi. Kituo hichi ni cha mpito, watoto hapa wako chini ya uangalizi wa wizara za Ustawi wa Jamii na Afya ya Sudan wakishirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto, UNICEF ambalo linasaidia kwenye matibabu ya watoto, lishe, msaada wa kisaikolojia, michezo na shughuli za elimu, na huku wakiwasaidia walezi wa watoto waliohamishwa.Uhamisho wa watoto hawa umefanyika kwa kutumia magari ya kubebea wagonjwa ndani ya magari hayo watoto wamewekwa kwenye mabeseni ama hakika vita kitu kibaya sana. Na pia mabasi makubwa ya kubeba abiria yametumika, watoto wanaojiweza wakiwa wameshikiliwa na wazazi wao wanaonekana kupiga hatua ndogo ndogo kuingia kwenye kituo hicho ambacho bado kinatengenezwa, na wale wasiojiweza na watoto wachanga, wazazi na wahudumu wa UNICEF wanaonekana kuwabeba wakiwa katika mwendo wataratibu wakiingia nao ukumbini hapo. Mwakilishi wa UNICEF nchini Sudan Mandeep O'Brien anasema kufanikiwa kwa uhamisho huu wa watoto kutoka eneo la vita kuja eneo salama kumeleta mwanga katikati ya vita vinavyoendelea nchini Sudan. Hata hivyo O’Brien anasema “Mamilioni mengi ya watoto, bado wako hatarini kote nchini Sudan, wanatishwa na mapigano, wanakimbia makazi yao na kuendelea kupata athari za vita kama vile kukosa huduma za kuokoa maisha yao. Mustakabali wa watoto unahatarishwa na vita hivi kila siku.”Mbali na kutoa huduma za matibabu na lishe, UNICEF wanashirikiana na mamlaka husika katika kutambua watoto wasio na walezi.Mpaka sasa takwimu za UNICEF zinaonesha kote nchini Sudan, zaidi ya watoto milioni 13.6 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu wa kuokoa maisha, hii ni idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa nchini humo. Athari za vita zinaendelea kutishia maisha na mustakabali wa familia na watoto, na kuacha huduma za kimsingi zikiwa zimekatishwa na vituo vingi vya afya kufungwa au kuharibiwa.UNICEF imetoa ombi la dola milioni 838 kushughulikia mzozo huo, fedha hii ikiwa ni ongezeko la dola milioni 253 tangu mzozo wa sasa uanze mwezi Aprili 2023.
14-6-2023 • 0
14 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia watoto katika migogoro ya silaha na wale wanaokimbia makazi yao. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunasalia huko huko Tanzania, kulikoni? Katika kuelekea siku ya wakimbizi duniani itakayoadhimishwa wiki ijayo, ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imeonya kwamba idadi inayoongezeka ya watoto kutawanywa duniani, inadhihirisha jinsi gani dunia ilivyoshindwa kushughulikia mizizi ya watu kutawanya na kutoa suluhu ya muda mrefu hususan kwa watoto wanaolazimika kukimbia makwao.Kufuatia vita inayoendelea nchini Sudan, watoto 297 wamehamishwa kwa usalama kutoka kituo cha watoto yatima cha Mygoma huko Khartoum nchini Sudan hadi kituo cha muda katika eneo salama zaidi nchini humo. Katika makala taasisi 16 nchini Tanzania zikiwemo mashirikia yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia na vyuo vikuu ambao kwa pamoja ni wanachama wa Mtandao wa Elimu Afrika Mashariki (RELI) wamekutana mjini Morogoro, Tanzania kujengewa uwezo wa namna ya kuimarisha juhudi za kuchochea mabadiliko ya elimu na kuhamasisha ujengaji fikra tunduizi kwa vijana ili kusongesha lengo namba 4 la Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu SDGs.Na katika mashinani tutaelekea katika shule ya msingi ya Mazimbua-A nchini Tanzania kusikiliza jinsi ambavyo elimu shirikishi inanvyowasaidia wanafunzi sio tu kuelewa kile wanachofundishwa bali pia kujua umuhimu wa kutunza misitu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
14-6-2023 • 0
13 JUNI 2023
Hii leo ni Siku ya Kimataifa ya Uelewa Kuhusu Ualbino na kama ilivyo ada ya kila Jumanne tunakuletea mada kwa kina ambapo tutamsikia mwanamuziki Roben X akieleza kuhusu maisha yake ya Ualbino. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za DRC, Myanmar na Ukraine. Mashinani tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tukikuletea ujumbe kuhusu ujumuishaji na uajiri wa watu wenye ualbino.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limesema imeshtushwa na shambulio dhidi ya kambi ya wakimbizi wa ndani lililofanyika jana Jumatatu katika jimbo la Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.Nchini Ukraine Umoja wa Mataifa unashirikisha serikali ya taifa hilo na ya Shirikisho la Urusi ili kuhakikisha upatikanaji wa fursa ya kuwafikia raia wote walioathiriwa na uharibifu mkubwa wa bwawa la Kakhovka.Na mwezi mmoja baada ya kimbunga Mocha kupiga Magharibi mwa Myanmar, mratibu mkazi na wa misaada ya kibinadamu wa umoja wa Mataifa Ramanathan Balakrishnan amesema leo kwamba baraza la uongozi wa jimbo la Rakhine limesitisha fursa ya kufikisha misada ya kibinadamu katika jimbo hilo na hivyo kuathiri usambazaji wa misaada ya kuokoa Maisha katika jamii zilizoathirika.Na katika mashinani leo nampisha Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wenye ualbino.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
13-6-2023 • 0
TANBAT 6, walinda amani wa UN kutoka Tanzania wapokea pongezi kutoka JWTZ na MINUSCA
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha 6 cha kutoka Tanzania TANBAT 06 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) wamepokea ugeni na salamu kutoka Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia ujumbe uliongozwa na Brigedia Jenerali George Mwita Itang’are aliyewakilisha salamu za Mkuu wa Majeshi ya Tanzania kutokana na sifa nzuri anazozipokea kutoka MINUSCA kuhusu kikosi hicho. Afisa Habari wa TANBAT 06 Kapteni Mwijage Inyoma ameshiriki na kutuandalia makala hii..
12-6-2023 • 0
Kambini Za’atari, mkimbizi kutoka Syria ageuza takataka kuwa hazina nchini Jordan
Katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari iliyoko nchini Jordan, roho ya ubunifu ya mtu mmoja na dhamira yake isiyoyumba imebadilisha vitu mbalimbali vinavyotupwa na kuonekana havifai tena kuwa nyenzo muhimu za urembo.Ziyad Al-Awaji, al maarufu Abu Jihad, kila siku huamka alfajiri kuaza shughuli zake za kutafuta plastiki iliyotupwa na vifaa vingine kwenye dampo za taka katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari huko nchini Jordan.Mkimbizi huyu kutoka nchini Syria mwenye umri wa miaka 64, mume na baba wa watoto 12 pamoja na kupitia magumu ikiwa ni pamoja na kupoteza nyumba yake na kipato sababu ya vita nchini mwake, hajakata tamaa na amedhamiria kuleta athari chanya kwa jamii yake na mazingira.Tangu awasili kambini hapo mwaka 2013 Abu Jahid alianza kujenga nyumba yake na kuiremba na vitu vya kipekee kutoka majalalani. Mapenzi yake ya kuchakata malighafi zilizotupwa yalichochewa na rasilimali chache zinazopatikana kambini, na punde si punde akawa gwiji wa kutafuta matumizi mapya ya vitu vya zamani na kugeuza taka anazo okota kuwa vitu muhimu na vizuri."Hii ni Chandelier, lakini bado haijakamilika, hii hapa ni mashine ya kusagia kahawa. "Ninatumia tena nyenzo zozote zinazokuja mikononi mwangu. Ninapenda kutoa maisha ya pili kwa vitu ambavyo tunadhani ni upotevu. Kila kitu kina matumizi ya pili,”Mbali na ubunifu wake wa kutengeneza vitu kama meza, taa, matanki ya kuhifadhi maji ya mvua na mifuko lakini Abu Jahid ni mfano mzuri wa namna wakimbizi wanaweza kuwa na athari chanja katika jamii zao.“Jordan inatuchukulia kama raia wake, tumekumbatiwa na kuungwa mkono kwa namna ambazo zinatufanya tujisikie kama sehemu ya jamii ya Jordan.”Wakati dunia inapambana na athari mbaya za uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na plastiki, shauku ya Abu Jihad ya kuchakata tena taka ni mfano mzuri wa namna uwezo na vitendo vya mtu binafsi unavyoletwa kuleta mabadiliko katika dunia.
12-6-2023 • 0
Watoto Tanzania wapaza sauti yao katika maadhimisho dhidi ya utumikishaji watoto
Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa dhidi ya Ajira au Utumikishaji wa Watoto ambayo inakusudia kutumika kama kichocheo cha kuongeza harakati za kimataifa dhidi ya ajira au utumikishwaji kwa watoto na ikisisitiza uhusiano kati ya haki za kijamii na ajira kwa watoto, kama ilivyo kwa nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania nayo imeungana na mataifa mengine kuadhimisha siku hii ambapo maadhimisho hayo yamefanyika Kitaifa katika kijiji cha Gua, Kata ya Gua katika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Mkoani Songwe. Kupitia siku hii muhimu kwa Watoto ulimwenguni kote, baadhi ya watoto kutoka Shule ya Msingi Gua wametoa maoni yao kuhusu umuhimu wa maadhimisho haya, miongoni mwao ni, Grace yeye ni muelimishaji jamii kuhusu utumikishwaji wa mtoto kwenye mashamba ya tumbaku, hapa anazungumzia hali ya utumikishwaji ilivyo kwa sasa, Kwa upande wake Innocent David Pesa amewashauri wazazi na walezi juu ya athari za utumikishwaji wa mtoto, Maadhimisho ya mwaka huu yanaenda Sambamba na kauli mbiu isemayo “Haki za Jamii kwa Wote, Tokomeza utumikishwaji wa Mtoto”
12-6-2023 • 0
12 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia ajira kwa watoto na wakimbizi nchini Jordan. Makala tunakupeleka nchini CAR na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa dhidi ya Ajira au Utumikishaji wa Watoto ambayo inakusudia kutumika kama kichocheo cha kuongeza harakati za kimataifa dhidi ya ajira au utumikishwaji kwa watoto na ikisisitiza uhusiano kati ya haki za kijamii na ajira kwa watoto, kama ilivyo kwa nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania nayo imeungana na mataifa mengine kuadhimisha siku hii ambapo maadhimisho hayo yamefanyika Kitaifa katika kijiji cha Gua.Katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari iliyoko nchini Jordan, roho ya ubunifu ya mtu mmoja na dhamira yake isiyoyumba imebadilisha vitu mbalimbali vinavyotupwa na kuonekana havifai tena kuwa nyenzo muhimu za urembo.Katika makala leo Afisa Habari wa Kikosi cha 6 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT 6 wanaohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, anatupeleka katika ziara ya walinda amani hao kukagua miradi ambayo wameianzisha kwa ajili ya wananchi.Na mashinani tutakupeleka kijinini Kareman katika kaunti ya Turkana nchini Kenya kushuhudia jinsi ambavyo wenyeji wanajitolea kuhakikisha wanawake na watoto wanaweza kufikia huduma za afya licha ya ukame ambao umezikumba jamii za kaunti hiyo kwa muda mrefu.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
12-6-2023 • 0
Sitisha uhasama miongoni mwa wakimbizi wa ndani Sudan Kusini: UNMISS
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umetoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uhasama miongoni mwa wakimbizi wa ndani katika Kambi ya Umoja wa Mataifa ya Ulinzi wa Raia nchini humo kufuatia tukio la jana Alhamis ambapo watu kadhaa waliripotiwa kujeruhiwa na wengine kuuawa.Video iliyorekodiwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) inaonesha gari la wagonjwa la Umoja wa Mataifa likisindikizwa na walinda amani likipita katika barabara ya vumbi katikati ya umati wa wakimbizi wa ndani katika eneo la Malakal nchini Sudan Kusini. Kila mmoja aliyefanikiwa kusalia na chochote katika anavyovimiliki, amekibebeba kichwani, mgongoni au mkononi. Jana muda wa mchana ghasia zilizuka kati ya jamii mbili za wakimbizi wa ndani ambazo zimehifadhiwa katika Kambi ya Umoja wa Mataifa ya Ulinzi wa Raia. UNMISS inasema vurugu hizo zilichochewa na tukio la kuchomana visu huku ripoti za awali zikitaja raia watatu kuuawa na wengine 20 kujeruhiwa hadi kufikia jana Alhamisi mchana. Kabla ya hapo, hiyo-hiyo jana Alhamis asubuhi, milio ya risasi ilitanda alfajiri katika mji mkuu wa jimbo la Upper Nile, Malakal, karibu na makazi ya UNMISS.Walinda amani wa UNMISS waliingia kazini haraka kwa kuwa hali ya wasiwasi imekuwa ikiendelea hapa tangu mwisho wa wiki iliyopita, wakati mzozo katika kituo cha maji uliongezeka haraka na kuwa mzozo kamili ambapo mtu mmoja mwenye umri wa miaka 32 aliuawa. Kwa kuwa kambi ya walinda amani iko karibu na kambi ya Umoja wa Mataifa ya ulinzi kwa raia, mara zote walinda amani wako chonjo kuchukua hatua ya haraka pindi tu wanapopokea taarifa ya vurugu. Wakati wa mapigano ya mwezi uliopita, wanajeshi na polisi walinda amani walitumwa mara moja ili kutuliza hali hiyo. Polisi na walinda amani wa kijeshi kwa sasa wanashika doria ndani ya eneo hilo na kuzunguka eneo la nje, kwa ushirikiano na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini ili kuondoa hofu miongoni mwa jamii iliyokimbia makazi yao. Zaidi ya hayo, walinda amani matabibu katika hospitali ya UNMISS wanatoa huduma ya dharura kwa baadhi ya waliojeruhiwa. Kwa mujibu wa usajili wa kibayometriki wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM), kufikia Desemba mwaka jana 2022, baadhi ya watu 37,032 waliokimbia makazi yao wanajihifadhi katika Eneo la Ulinzi la Umoja wa Mataifa la Malakal.
9-6-2023 • 0
OHCHR yapokea ripoti za raia kuuawa na wanawake kubakwa nchini Sudan
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binaadamu, OHCHR imeeleza kusikitishwa na athari mbaya za mapigano kwa raia zinazoendelea nchini Sudan ambapo mpaka hizi sasa wamepokea taarifa za kuuawa kwa raia ikiwemo watoto na wajawazito na ubakaji huku waandishi wa habari wakiwa katika hali mbaya kutokana na kauli za chuki hususani mitandaoni.Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini Geneva Uswisi msemaji wa Ofisi hiyo ya Haki za Binadamu Jeremy Laurence amesema, “Kwa wiki hii pekee limetokea shambulio katika soko la mifugo lenye shughuli nyingi katika mji mkuu Khartoum lilisababisha vifo vya raia wanane, miongoni mwao takriban watatu wanatoka familia moja. Mashambulizi ya anga kwenye soko la Al-Muwaliyyah tarehe 7 Juni yalidaiwa kutekelezwa na Jeshi la Sudan.”Jeremy pia amezungumzia tukio la mtoto kuuawa akiwa nyumbani kwao na pia uwepo wa ripoti za unyanyasaji wa kingono.“Tangu mapigano yalipoanza, Ofisi yetu imepokea ripoti za kuaminika za matukio 12 ya unyanyasaji wa kingono yanayohusiana na mzozo huo, dhidi ya angalau wanawake 37, ingawa idadi inaweza kuwa kubwa zaidi. Katika angalau matukio matatu, waathirika walikuwa wasichana wadogo. Katika kisa kimoja, wanawake 18 hadi 20 waliripotiwa kubakwa.”Ripoti za watu kutoweka na waandishi wa habari kukabiliwa na ongezeko la matamshi ya chuki mitandaoni pia zimeripotiwa.
9-6-2023 • 0
09 JUNI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mizozo nchini Sudan ka pia nchi jirani Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Somalai na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binaadamu, OHCHR imeeleza kusikitishwa na athari mbaya za mapigano kwa raia zinazoendelea nchini Sudan ambapo mpaka hizi sasa wamepokea taarifa za kuuawa kwa raia ikiwemo watoto na wajawazito na ubakaji huku waandishi wa habari wakiwa katika hali mbaya kutokana na kauli za chuki hususani mitandaoni.Na tukitokea huko Sudan tuelekee katika nchi jirani, Sudan Kusini. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umetoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uhasama miongoni mwa wakimbizi wa ndani katika Kambi ya Umoja wa Mataifa ya Ulinzi wa Raia nchini humo kufuatia tukio la jana Alhamis ambapo watu kadhaa waliripotiwa kujeruhiwa na wengine kuuawa.Makala ambayo leo inatupeleka katika majimbo ya Hijraan na Galmudug nchini Somalia yaliyoathirika vibaya na ukame ulioleta changamoto ya maji kwa wakulima na wafugaji, lakini sasa asante kwa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO mradi wake wa maji unaleta nuru.Na katika tunakupeleka nchini Tanzania kusikia ni kwa jinsi gani mashirika ya Umoja wa Mataifa wanashirikiana na wadau wake kupambana na magonjwa ya kuambukiza.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
9-6-2023 • 0
Asante FAO kwa kutunusuru na ukame: Wafugaji Somalia
Somalia ambayo imekuwa katika machafuko kwa miongo zaidi ya mitatu sasa inaendelea kukabiliana na janga lingine kubwa la ukame ambao haujawahi kushuhudiwa kwa miaka takriban 40 na kuathiri mamilioni ya watu wakiwemo wakulima na wafugaji wa majimbo ya Hijraan na Galmudug. Katika majimbo hayo jamii zimepoteza karibu kila kitu kutokana na ukame huo na kupoteza matumaini. Lakini sasa asante kwa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO kurejesha matumaini ya jamii hizo kwa kuzindua mradi wa maji ambao sio tuu utazinusuru jamii hizo na mifugo yao lakini pia utazipa matumaini mapya ya maisha. Tuambatane na Flora Nducha katika makala hii kwa ufafanuzi zaidi
9-6-2023 • 0
Jifunze Kiswahili: Uchambuzi wa neno, "RUWI"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo tunafafanuliwa maana ya neno "RUWI" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, Karibu!
8-6-2023 • 0
08 JUNI 2023
Hii leo ni siku mada kwa kina na jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya bahari inayohimiza kuhakikisha bahari inakuwa safi na yenye afya ili iweze kuihudumia vyema jamii tutaangalia namna taka zinazotolewa baharini zinavyoweza kutumika kama malighafi bora ndani ya jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo …. Na katika kujifunza kiswahili tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kufafanuliwa maana ya neno"RUWI", salía hapo hapo!Katika siku ya bahari duniani ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akisema bahari ni msingi wa maisha na binadamu tunaitegemea bahari lakini je bahari inaweza kututegemea? Ethiopia inakabiliwa na dharura nyingi huku kukiwa na changamoto kubwa ya ufadhili duni limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na kuongeza kuwa huku kukiwa na watu wapya na wanaoendelea kutawanywa na kuteseka kutokana na ukame, nchi hiyo ya Afrika Mashariki inahaha kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya watu waliokimbia makazi yao nchini kote.Na tukamilishe na habari Njema. Mlipuko wa homa ya Marburg nchini Equatorial Guinea umemalizika leo kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO huku kukiwa hakuna mgonjwa yeyote mpya aliyeripotiwa katika muda wa siku 42 zilizopita baada ya mgonjwa wa mwisho kuruhusiwa kutoka baada ya matibabu. Mlipuko huo, ambao ulitangazwa tarehe 13 Februari, ulikuwa wa kwanza wa aina yake nchini Equatorial Guinea. Jumla ya wagonjwa 17 walithibitishwa na maabara na vifo 12 vilirekodiwa.Na katika kujifunza Kiswahili, leo tunafafanuliwa maana ya neno "RUWI" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
8-6-2023 • 0
Wakimbizi zaidi wa Sudan nchini CAR, UNHCR yakimbizana na muda kuiwahi mvua
Zaidi ya watu 13,000 kutoka Sudan wamewasili katika Kijiji cha Am Dafock kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kuepuka madhila ya mgogoro unaoendelea nchini mwao. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi linasema wengi wa waliowasili ni wanawake na watoto kutoka Nyala mji ulioko kusini magharibi mwa Sudan ambako wanasema walikabiliwa na matatizo kadhaa njiani kuelekea kuvuka mpaka hadi kufika Am Dafock, kama vile vitisho kutoka kwa watu wenye silaha, unyang'anyi wa bidhaa, unyanyasaji wa kimwili na unyanyasaji wa kijinsia. Zaidi kuhusu hili, Anold Kayanda ameandaa makala hii.
7-6-2023 • 0
Bahari ni sehemu ya suluhisho la matatizo lukuki katika jamii - FAO
Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya habari duniani hapo kesho Juni nane shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limesema ni vyema jamii kuzingatia afya ya baharí kwani umuhimu wake kamwe hauwezi kupuuzwa.Bahari, ni makazi ya asilimia 80 ya majani ya wanyama, ambayo yanatumika kama chanzo muhimu cha wananchi kujipatia riziki na pia lishe kwa mamilioni ya watu ulimwenguni.Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Rasilimali za Uvuvi na Ufugaji wa samaki kutoka FAO Manuel Barange, anasema kwa utajiri uliopo baharini, “Hakuna tatizo hata moja ambalo tunalo ulimwenguni iwe kwenye mabadiliko ya tabianchi, umasikini au uhakika wa chakula ambalo linaweza kutatuliwa bila kuzingatia baharí kama sehemu ya suluhisho” Manuel anasema kwa sasa zaidi ya watu milioni 800 wameathiriwa na njaa kote ulimwenguni, vyakula vya baharini vilivyo sheheni lishe ya hali ya juu ni suluhisho la kushughulikia njaa na utapiamlo, “Ufugaji wa samaki umekuwa mfumo wa uzalishaji wa chakula unaokua kwa kasi zaidi katika kipindi cha miongo mitano iliyopita. Ulaji pia wa vyakula vya majini umekuwa ukiongezeka maradufu ya kiwango cha ongezeko la watu katika miongo ya hivi karibuni.”Katika kuhakikisha kila nchi inajitosheleza na kuweza kuhimili ongezeko la uhitaji wa vyakula vya majini FAO inahamasisha utekelezaji wa mkakati wa Mabadiliko ya Buluu Blue Transformation unaolenga kuimarisha mifumo ya vyakula vya majini katika kulisha idadi ya watu inayoongezeka duniani kwa kutoa mifumo ya kisheria, sera na usaidizi wa kiufundi inayohitajika ili kuendeleza ukuaji na uvumbuzi, “Mpango wa Mabadiliko ya Bluu ni dira kutoka FAO ambayo imeanza na kanuni mbili kubwa. Kwanza ni kukubali kwamba vyakula vya majini ni sehemu ya suluhisho la njaa na utapiamlo. Pili ni utambuzi kwamba mabadiliko yanafanyika hata bila sisi kufanya lolote.”Mpango wa Mabadiliko ya Buluu umependekeza msururu wa hatua zilizoundwa kusaidia ustahimilivu katika mifumo ya chakula cha majini na kuhakikisha uvuvi na ufugaji wa samaki unakuwa kwa njia endelevu huku hakuna mtu anayeachwa nyuma, hususan jamii zinazotegemea sekta hiyo.Masuala mengine yanayoangaziwa na mabadiliko hayo ni pamoja na sera na desturi zinazofaa kwa mabadiliko ya tabianchi na mazingira, pamoja na ubunifu wa kiteknolojia.
7-6-2023 • 0
Siku ya usalama wa chakula duniani yaadhimishwa na UM ikihimiza viwango bora huokoa maisha
Leo ni siku ya usalama wa chakula duniani mwaka huu ikibeba kaulimbiu “Viwango vya chakula huokoa Maisha” ikilenga kuchagiza mwenendo na viwango vya usalama ambavyo hupunguza hatari ya uchafuzi wa chakula.Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO na lile la chakula na kilimo FAO ambao huibeba siku hii lengo kubwa ni kuongeza habari na taarifa kuhusu hatari ya sumu ya chakula na uchafuzi, ambayo inaua watu 420,000 kila mwaka huku vifo 125,000 miongoni mwao vikiwa ni vya Watoto wa umri wa chini ya miaka mitano.Na takwimu za mashirika hayo zinaonyesha kuwa kila mwaka kuna angalau kesi 600,000 za magonjwa unaosababishwa na chakula ambacho huandaliwa bila hata usalama mdogo.Pia mashirika hayo yamesema watu mafukara na walio hatarini zaidi mara nyingi ndio wanaoathirika zaidi wakiwemo wanawake na watoto.FAO imetoa wito wa “kuitumia siku hii muhimu kutanabaisha kuhusu umakini na kuhamasisha hatua za kusaidia kuzuia, kugundua na kudhibiti hatari zinazotokana na chakula, kuchangia uhakika wa chakula, afya ya binadamu, ustawi wa kiuchumi, kilimo, upatikanaji wa soko, utalii na maendeleo endelevu.”Nalo shirika la WHO limesisitiza kuwa “Siku hii ya kimataifa ni fursa ya kuimarisha juhudi za kuhakikisha kuwa chakula tunachokula ni salama, usalama wa chakula katika mfumo wa umma wa chakula na kupunguza mzigo wa magonjwa yanayotokana na chakula duniani.”Kwa kutambua umuhimu wa kuhakikisha usalama kwa chakula duniani kote FAO pia imezindua imezindua nyenzo za kina, za vitendo na zinachoweza kufikiwa zilizoundwa ili kuwasaidia wale wote wanaofanya kazi katika sekta ya chakula kuzingatia viwango vya kimataifa vya usafi wa chakula.Siku ya usalama wa chakula duniani huazimishwa kila mwaka Juni 7 tangu ilipopitishwa rasmi mwaka 2018.
7-6-2023 • 0
07 JUNI 2023
Jaridani hii leo tunaangazia siku za Umoja wa Mataifa na wawakimbizi wa Sudan wanaolelekea nchi jirani. Makala tunakupeleka nchini CAR na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Leo ni siku ya usalama wa chakula duniani, mwaka huu ikibeba kaulimbiu “Viwango vya chakula huokoa maisha” ikilenga kuchagiza mwenendo na viwango vya usalama ambavyo hupunguza hatari ya uchafuzi wa chakula. Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya habari duniani hapo kesho Juni nane shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limesema ni vyema jamii kuzingatia afya ya baharí kwani umuhimu wake kamwe hauwezi kupuuzwa.Katika makala Anold Kayanda anatupeleka katika kijiji cha Am Dafock kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linafanya kila namna kuwasaidia wakimbizi waliovuka mpaka wakitokea Sudan.Na katika mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe wa mshikamano kutoka kwa wanaharakati wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs unaopigia chepuo utokomezaji wa ukatili wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, Karibu!
7-6-2023 • 0
06 JUNI 2023
Jaridani hii leo tunaangazia ni mada kwa kina na nakupeleka mwambao wa Ziwa Tanganyika nchini Tanzania, hususan mkoani Rukwa ambako huko utasikia harakati za Umoja wa Mataifa za kujumuisha wanawake kwenye uvuvi. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Nishati jadidifu, mabadiliko ya tabianchi na afya. Katika mashinani tunakupeleka nchini Sudan Kusini kusikia ni kwa jinsi gani vijana wanachangia katika mchakato wa utengenezaji wa katiba ukielekea uchaguzi mkuu nchini humo.Ripoti mpya iliyozinduliwa leo kuhusu hatua zilizopigwa katika ufikiaji wa lengo namba 7 la maendeleo endelevu SDGs ifikapo mwaka 20230 lihusulo nishati, inasema pengo la nishati duniani bado linaendelea kwani watu milioni 675 hawana umeme, huku watu wengine bilioni 2.3 wanategemea nishati za kupikia ambazo ni hatari kwa afya zao na mazingira. Umoja wa Mataifa umezindua mradi wa miaka miatatu wa kuimarisha mnepo wa jamii dhidi ya mabadiliko ya tabianchi mkoani Kigoma nchini Tanzania ambako mamia kwa maelfu ya wakimbizi wanahifadhiwa.Na kuelekea siku ya usalama wa chakula duniani hapo kesho Juni 7 mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani WHO na la mpango wa chakula duniani WFP kwa kushirikiana na sekretarieti ya Codex Alimentarius wamesema kila siku takriban watu milioni 1.6 duniani kote wanaugua kutokana na kula chakula kisicho salama.Na katika mashinani Elizabeth Acu, Mwanaharakati wa vijana ambaye pia ni mwanauchumi nchini Sudan Kusini, anaeleza jukumu la vijana katika uundaji na uimarishaji wa katiba, na pia changamoto zinazoikumba nchi hiyo huku mchakato wa uchaguzi mkuu unapokaribia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
6-6-2023 • 0
UDHR75: Utekelezaji wa Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu
Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu mwaka huu linatimiza miaka 75 tangu kupitishwa kwake. Katika kutathmini utekelezaji wake, tunachambua ibara kwa ibara kuona iwapo kuna mafanikio, halikadhalika changamoto. Na kwa mantiki hiyo leotunamulika Ibara ya Tatu ya Tamko hilo inayosema Kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya kuwa huru na kulindwa . Na mchambuzi wetu ni Getrude Dyabene Afisa Mwandamizi wa Dawati la Jinsia kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania, LHRC akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani. Bi. Dyabene anaanza kwa kuelezea jinsi Katiba ya Tanzania inatambua haki ya kuishi.
5-6-2023 • 0
05 JUNI 2023
Jaridani hii leo tunaangazia siku ya mazingira duniani na ukiukwaji haki dhidi ya watoto walio katika migogoro inayotumia silaha. Makala tunakuletea uchambuzi wa Ibara ya Tatu ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu, na mashinani tunakupeleka nchini Kenya kusikia ujumbe kutoka kwa mwanaharakati wa mazingira kuhusu taka za plastiki.Ikiwa leo ni siku ya mazingira duniani Umoja wa Mataifa imetoa wito kwa kila mtu kusaidia vita ya kutokomeza plastiki kwa faida ya mustakbali wa mazingira ya dunia na viumbe vyake. Zaidi ya matukio laki tatu ya ukiukwaji haki dhidi ya watoto walio katika migogoro inayotumia silaha yamethibitishwa na Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 2005 na 2022, hicho kikiwa ni kielelezo tosha cha athari mbaya za vita na migogoro kwa Watoto, imeeleza taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF iliyotolewa.Makala, katika kuadhimisha miaka 75 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za binadamu tunaendelea na uchambuzi wa wa Ibara kwa Ibara na leo tunamulika Ibara ya Tatu ya Tamko hilo inayosema Kila mtu ana haki ya kuishi, haki ya kuwa huru na kulindwa . Na mchambuzi wetu ni Getrude Dyabene Afisa Mwandamizi wa Dawati la Jinsia kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania, LHRC akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, jijini New York, Marekani..Na katika mashinani Nasenya Kutoka Kenya, ambaye ni Muigizaji na pia Balozi Mwema wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani UNEP anasema anaamini kwamba tunaweza kukomesha uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na taka za plastiki.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, Karibu!
5-6-2023 • 0
Hatua zichukuliwe kutokomeza taka za plastiki: UN
Ikiwa leo ni siku ya mazingira duniani Umoja wa Mataifa imetoa wito kwa kila mtu kusaidia vita ya kutokomeza plastiki kwa faida ya mustakbali wa mazingira ya dunia na viumbe vyake.Maudhui ya siku ya mazingira mwaka huu ni “tokomeza taka za plastiki” utajiuliza kwa nini? Jibu analo Inger Anderson mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira duniani UNEP kupitia ujumbe wake wa siku hii anasema ni, “Kwa sababu taka za plastiki Kwa sababu zinasonga mifumo yetu ya ikolojia, zinapasha joto hali ya hewa yetu na kuna uwezekano mkubwa wa kuharibu afya zetu. Urejelezaji sio mazingaombwe. Mifumo yetu haiwezi kuhimili. Mabadiliko lazima yafanyike katika mzunguko mzima wa maisha wa plastiki. Ni lazima kukataa vitu visivyo vya lazima vya matumizi ya mara moja. Tupange upya bidhaa na vifungashio ili kutumia plastiki kidogo, tutumie tena, turejeleze, tuelekeze upya na tubadilishe mifumo yetu.”Amesema kwa njia hiyo ndio Dunia itaweza kuengua plastiki katika mifumo ya ikolojia na uchumi na hilo amsisitiza ni jukumu la kila mtu, “ Kila mtu lazima atimize wajibu wake. Serikali zinaweza kutoa matokeo madhubuti kwenye mpango huo wa kukomesha uchafuzi wa plastiki kwa majadiliano. Biashara zinaweza kuchukua mtazamo mpya, sekta ya fedha inaweza kuweka mtaji wake katika kusongesha mabadiliko, na wananchi wanaweza kutumia sauti, kura na pochi zao kuleta mabadiliko.Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiunga mkono wito huo amesema, “Kila mwaka, zaidi ya tani milioni 400 za plastiki huzalishwa duniani kote - theluthi moja ambayo hutumiwa mara moja tu. Kila siku, zaidi ya lori 2000 za takataka zilizojaa plastiki hutupwa katika bahari, mito na maziwa yetu. Matokeo yake ni janga. Chembechembe za plastiki huishia kwenye chakula tunachokula, maji tunayokunywa, na hewa tunayopumua.”Ameongeza kuwa plastiki imetengenezwa kutokana na nishati ya kisukuku na kadiri tunavyozalisha plastiki zaidi, ndivyo mafuta ya kisukuku tunavyoyachoma, na ndivyo tunavyofanya mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi kuwa mbaya zaidi.Hata hivyo amesema kuna suluhu “Mwaka jana, jumuiya ya kimataifa ilianza kujadili makubaliano ya kisheria ya kukomesha uchafuzi wa taka za plastiki. Hii ni hatua ya kwanza ya matumainii, lakini tunahitaji kila hatua kutekelezwa.”Ameongeza kuwa ripoti mpya ya UNEP inaonyesha, “tunaweza kupunguza uchafuzi wa taka za plastiki kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2040 ikiwa tutachukua hatua sasa kurejeleza, kuchakata tena, kuelekeza upya, na kutenganisha plastiki.”Kwa mantiki hiyo amesisitiza “Ni lazima tufanye kazi kama kitu kimoja, serikali, kampuni na watumiaji kwa pamoja ili kuondokana na uraibu wetu wa matumizi ya plastiki, kuchagiza kutokuwa na taka za plastiki na kujenga uchumi wa kweli. Kwa pamoja, tutengeneze maisha safi, yenye afya na endelevu zaidi kwa wote.”Siku ya mazingira duniani huadhimishwa kila mwaka Juni 5.
5-6-2023 • 0
Matukio ya ukatili dhidi ya watoto kwenye migogoro inayotumia silaha katika mwaka 2002-2022 ni zaidi ya 300,000: UNICEF
Zaidi ya matukio laki tatu ya ukiukwaji haki dhidi ya watoto walio katika migogoro inayotumia silaha yamethibitishwa na Umoja wa Mataifa kati ya mwaka 2005 na 2022, hicho kikiwa ni kielelezo tosha cha athari mbaya za vita na migogoro kwa Watoto, imeeleza taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF iliyotolewa.Wakati mataifa, wafadhili na jumuiya ya misaada ya kibinadamu wakikutana hii leo na kesho katika mji mkuu wa Norway, Oslo kwa ajili ya Mkutano wa Kulinda Watoto katika Migogoro yenye kutumia Silaha, UNICEF imeripoti kwamba, tangu ufuatiliaji wa matukio ya ukikukwaji wa haki za Watoto katika maeneo yenye mizozo uanze mwaka 2005, Umoja wa Mataifa umethibitisha matukio 315,000 ya ukikukwaji mkubwa wa haki za watoto uliofanywa na pande zinazozozana katika zaidi ya maeneo 30 ya migogoro barani Afrika, Asia, Mashariki ya Kati na Amerika Kusini. Matukio haya ya ukatili dhidi ya watoto ni pamoja na, zaidi ya watoto 120,000 kuuawa au kulemazwa, takribani watoto 105,000 waliandikishwa au kutumiwa na vikosi vya kijeshi au vikundi vyenye silaha, zaidi ya watoto 32,500 walitekwa nyara, na zaidi ya watoto 16,000 walifanyiwa ukatili wa kijinsia. Umoja wa Mataifa pia umethibitisha zaidi ya mashambulizi 16,000 dhidi ya shule na hospitali, na zaidi ya matukio 22,000 ya kunyimwa haki za kibinadamu kwa watoto. Zaidi ya hayo, UNICEF inaeleza kuwa mamilioni ya watoto zaidi wamefurushwa kutoka katika nyumba na jumii zao, wamepoteza marafiki au familia au wametenganishwa na wazazi au walezi. "Vita yoyote ile hatimaye ni vita dhidi ya watoto," anasema Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell akiongeza kwamba "Kukabiliwa na migogoro kuna athari mbaya na kunabadilisha maisha kwa watoto.” “Ingawa tunajua nini kifanyike ili kuwalinda watoto dhidi ya vita, ulimwengu haufanyi vya kutosha. Mwaka baada ya mwaka, Umoja wa Mataifa unaandika njia zinazoonekana, za kutisha na zinazoweza kutabirika ambazo maisha ya watoto yanasambaratika. Ni wajibu wetu sote kuhakikisha kwamba watoto hawalipi gharama ya vita ya watu wazima, na kuchukua hatua madhubuti zinazohitajika ili kuboresha ulinzi wa baadhi ya watoto walio hatarini zaidi duniani.” Anasema Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF. Idadi hii iliyowekwa wazi ni visa vile tu ambavyo vimethibitishwa, vinginevyo UNICEF inadhani kwamba idadi inaweza kuwa ni ya juu zaidi.
5-6-2023 • 0
UNHCR watembelea DRC kutathimini hali ya wakimbizi
Tangu kuanza kwa hali mbaya ya usalama mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Shirika la Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limekuwa likifanya kazi ya kuboresha hali ya maisha ya wakimbizi na kwa wakimbizi wa ndani. Ujumbe mkuu wa shirika hilo la UNHCR upo katika ziara ya siku kadhaa katika jimbo la Kivu kaskazini na umekuwa ukibadilishana mawazo na watu waliokimbia makazi yao nchini humo. Moja ya maeneo ambayo Ujumbe huo wa UNHCR umetembelea ni eneo la wakimbizi la Rusayo. Mwandishi wa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, Byobe Malenga ameandaa makala hii kuhusu ziara hiyo.
2-6-2023 • 0
IAEA: Matumizi ya nyuklia katika kuhakikisha jamii inakula chakula kilicho salama
Usalama wa chakula ni suala muhimu kwa afya ya umma na usalama wa chakula duniani, hata hivyo walaji hawawezi kugundua kwa kuona, kuonja au kunusa chakula kisicho salama, na ndio maaana maabara za usalama wa chakula zinazotumia sayansi ya nyuklia kuhakikisha wananchi wanalindwa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO linakadiria watu milioni 600 kila mwaka wanapata madhara kutokana na kula chakula kisicho salama, idadi hii ni sawa na mtu mmoja kati ya kila watu 10 au mara mbili ya idadi yote ya wananchi wa Marekani.Usalama wa chakula ina maanisha chakula kinacholiwa linatakiwa kisilete madhara kwa mlaji na pale chakula kinapobainika kuwa si salama basi wataalamu hukataza wananchi kula chakula hicho.Maendeleo ya sayansi yamewezesha nyuklia kutumika katika ukuaji wa chakula na mbogamboga na pia nyuklia hutumika kupima kiasi cha virutubisho vinavyofyonzwa. Swali ni je nyuklia inawezaje kuhakikisha chakula tunachokula ni salama?Na anayejibu ni Carl Blackburn, mtaalamu kutoka kituo cha pamoja cha Mbinu za Nyuklia katika Chakula na Kilimo kinachosimamiwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo FAO na la nguzu za Atomiki IAEA.“Kisayansi tuna viwango vya kimataifa vya chakula ambapo tunatoa kikomo kwa vyakula vinavyochafua.Zimewekwa kanuni nzuri za kuanzia uchakataji wa chakula, usindikaji, mpaka uhifadhi wa chakula. Mamlaka ya udhibiti wa chakula kwa kila nchi zinaweka viwango na sheria zinazosaidia usambazaji wa chakula kukidhi viwango vya kimataifa na ni muhimu kwa nchi zote kukidhi viwango hivyo kwa usawa kwani hatutaki viwe kizuizi kwa watu kufanya biashara ya chakula duniani kote.”Zaidi ya nchi 200 zinahusika katika utungaji wa sheria hizo zinazosimamia kuhakikisha chakula kinakuwa salama na IAEA ndio muangalizi wa sheria hizo. Moja ya maabara zinazopima usalama wa chakula kwakutumia nyuklia zipo nchini Botswana, nchi inayofahamika zaidi kwa usambazaji wa nyama duniani kote, Sandy Mookantsa, ni afisa katika maabara ya Kitaifa ya Mifugo ya Botswana na anasema mbali na kupima nyama lakini pia wanasaidia kutoa mafunzo kwa nchi jirani.“Maabara yetu ni ya usalama wa chakula, ilianzishwa mwaka 1989, tunashirikiana na IAEA katika kutujengea uwezo, rasilimali na kiufundi. Kwakupitia IAEA tumeweza kutengeneza mtandao ambapo tumekuwa tukitoa mafunzo kwa wanasayansi kutoka nchini Nigeria, Lesoth, Burundi na Uganda kwakutaja nchi chache tu."
2-6-2023 • 0
WFP: Uporaji wa chakula cha msaada Sudan waweka rehami Maisha ya watu milioni 4.4
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, leo limelaani vikali uporaji katika moja ya maghala yake ya msaada wa kiufundi na chakula Eil Obeid nchini Sudan na kusema uporaji huo unaweka hatarini maisha ya watu milioni 4.4 wanaotegemea msaada wa chakula katika maeneo yaliyoathirika na vita. Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Roma Italia WFP imesema inafanyakazi usiku na mchana ili kuongeza operesheni zake nchini Sudan ili kuwafikia mamilioni ya watu ambao sasa wako katika hali ya sintofahamu na kukabiliwa na njaa kufuatia machafuko yaliyozuka katikati ya mwezi Aprili.Hivyo limesema “Uporaji huo wa cjakula cha msaada wa kibinadamu na mali zingine za shirika hilo unaweza rehani maisha ya mamilioni ya watu wanaoitegemea WFP kuweza kuishi na pia kuathiri operesheni zetu katika wakati huu muhimu kwa watu wa Sudan, vitendo hivi lazima vikome.”El Obeid ni mwenyeji wa moja ya kituo kikubwa zaidi cha masuala ya kiufundi cha WFP katika bara la Afrika na kinatumika kama njia muhimu ya operesheni nchini Sudan na Sudan Kusini.Shirika hilo limeongeza kuwa “Mamilioni ya watu wataathiriwa na shambulio hili la uporaji.”Ripoti za awali zinaonyesha kuwa vifaa vilivyoporwa katika tukio hilo ni pamoja na chakula na lishe, magari, mafuta na jenereta.WFP imekumbusha kuwa “Hii si mara ya kwanza kwa chakula na mali za msaada wa kibinadamu za WFP na washirika wetu kuvamiwa na kuporwa. WFP pekee hadi sasa imerekodi hasara inayokadiriwa kuwa ya zaidi ya dola milioni 60 tangu ghasia kuzuka Aprili 15.”Hivyo WFP imetoa witio kwa pande zote katika mzozo kuhakikisha usalama na ulinzi wa misaada ya kibinadamu , wahudumu wa kibinadamu na mali zao ili kazi yao ya kuokoa maisha iweze kuendelea.Inakadiriwa kuwa takriban watu milioni 2 hadi milioni 2.5 nchini Sudan wanatarajiwa kutumbukia katika janga la njaa katika miezi michache ijayo kwa sababu ya vita inayoendelea.Na hali hiyo kwa mujibu wa WFP “Itafanya hali mbaya ya uhakika wa chakula Sudan kufikia viwango vya juu zaidi huku zaidi ya watu milioni 19 wakiathirika saw ana asilimia 40 ya watu wote wa taifa hilo.”
2-6-2023 • 0
02 JUNI 2023
Jaridani hii leo tunaangazia msaada wa chakula nchini Sudan na matumizi ya Nyuklia katika maabara nchini Botswana kuhakikisha usalama wa chakula. Makala tunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, leo limelaani vikali uporaji katika moja ya maghala yake ya msaada wa kiufundi na chakula Eil Obeid nchini Sudan na kusema uporaji huo unaweka hatarini maisha ya watu milioni 4.4 wanaotegemea msaada wa chakula katika maeneo yaliyoathirika na vita. Usalama wa chakula ni suala muhimu kwa afya ya umma na usalama wa chakula duniani, hata hivyo walaji hawawezi kugundua kwa kuona, kuonja au kunusa chakula kisicho salama, na ndio maaana maabara za usalama wa chakula zinazotumia sayansi ya nyuklia kuhakikisha wananchi wanalindwa.Katika makala mwandishi wetu wa DRC, Byobe Malenga anatupeleka katika ziara ya ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa wa kuhudumia wakimbizi UNHCR ukiongozwa na Kamishna Mkuu Msaidizi wa UNHCR ulipotembelea kambi ya wakimbizi ya Rusayo, Jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC.Na mashinani tutaelekea Dandora nchini Kenya kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu ujenzi wa barabara jumuishi ili kuhakikisha usalama kwa watu wote barabarani.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, Karibu!
2-6-2023 • 0
Jifunze Kiswahili: "Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt. Mwanahija Ally Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili visiwani Zanzibar, BAKIZA anachambua methali: Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama!
1-6-2023 • 0
01 JUNI 2023
Jaridani hii leo mada kwa kina na nakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia maoni ya wananchi kuhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO ikiwa tunaendelea na maadhimisho ya miaka 75 ya tangu kuanzishwa kwa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo wakimbiz nchini Chad, WMO na uondoaji na upokonyaji silaha kwa makundi mbalimbali nchini DRC. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt. Mwanahija Ally Juma anachambua methali: Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama!Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia haraka wakimbizi nchini Chad, kwani idadi ya waliowasili imevuka 100,000. Taarifa ya UNHCR iliyotolewa leo katika mji mkuu wa Chad, Ndjamena imeeleza tangu kuanza kwa mzozo nchini Sudan tarehe 15 Aprili, takriban wakimbizi 100,000 wanaokimbia ghasia wamesaka hifadhi mashariki mwa Chad, hasa katika mikoa ya Ouaddaï, Sila, na Wadi Fira. Profesa Celeste Saulo wa Argentina ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa kwanza mwanamke wa shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa duniani (WMO), akichukua usukani wa shirika hilo liloanzishwa miaka 73 iliyopita na lililo mstari wa mbele katika juhudi za kimataifa za kufuatilia na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa inayozidi kuwa mbayá.MONUSCO inaendelea na programu ya uondoaji na upokonyaji silaha kwa makundi mbalimbali nchini humo DRC ikiwemo kuwaunganisha tena kwenye jamii wale wanaoridhia kuachana na maisha ya mapigano. Chance SEBAYINZI ni mmoja wa wanufaika wa program hiyo aambaye ameamua kuondoka msituni na kurejea maisha ya kiraia baada ya miaka 8 kutumikia kundi la waapiganaji wanaojihami kwa silaha huko Beni, kaskazini mashariki mwa DRC jimboni Kivu Kaskazini.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na ninampisha Dkt. Mwanahija Ally Juma akichambua methali Mama ni Mama Hata Kama ni Rikwama!.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, Karibu!
1-6-2023 • 0
Tuzo kwa Sprina mkulima aliyeachana na na kilimo cha tumbaku na kugeukia maharage
Tuzo hiyo imetolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, (WHO) kwa kutambua mchango wa Sprina wa sio tu katika kukata shauri kuachana na kilimo cha tumbaku bali pia kuchukua hatua ya kukuza jamii yenye afya kupitia mlo wa maharage ambayo yana protini. Kufahamu kwa undani harakati za Sprina, ungana na Thelma Mwadzaya katika makala hii.
31-5-2023 • 0
WFP Tanzania kupunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi kutokana na ukata
Zaidi ya wakimbizi 200,000 walioko nchini Tanzania wataanza kupokea nusu mgao wa chakula wanachopatiwa kutokana na ukata unaokabili shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP. Asilimia 70 ya wakimbizi hao wanatoka Burundi ilhali asilimia 30 wanatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Taarifa iliyotolewa jijini Dar es salaam nchini Tanzania na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP, imesema uamuzi huo unakuja wakati tayari tangu mwaka 2020 walilazimika kupunguza mgao wa chakula.WFP inasema kwa kawaida kila mkimbizi anatakiwa kupata mlo wa siku wenye kiwango cha chini pendekezwa cha lishe chenye kalori 2,100, lakini kutokana na ukata kuanzia mwezi Machi mwaka huu, mgao ulipunguzwa kutoka kukidhi asilimia 80 ya mahitaji ya kalori hadi asilimia 65.Kutokana na hali fedha kuwa mbaya, kuanzia mwezi ujao wa Juni mgao utapunguzwa zaidi hadi asilimia 50 na hivyo wakimbizi kuwa hatarini kukidhi mahitaji yao ya lishe.Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Tanzania Sarah Gordon – Gibson amesema wamepokea kiwango kidogo cha fedha hivyo wanalazimika kuchukua uamuzi mgumu wa kupunguza mgao wakati huu ambapo mahitaji yameongezeka.Amesema wanahitaji kwa dharura dola milioni 21 kupatia msaada wa chakula zaidi ya wakimbizi 200,000 kwa kipindi cha miezi sita ijayo, halikadhalika kuepusha njaa kwenye kambi za wakimbizi Tanzania.Hofu ya Bi. Gordon-Gibson ni kwamba kupunguza mgao kwa kiasi kikubwa kutaweka wakimbizi hatarini hivyo amesihi jamii ya kimataifa, wahisani na sekta binafsi kuchukua hatua haraka za usaidizi ili wakimbizi waweze kukidhi mahitaji yao ya lishe.Kwa sasa Tanzania inashuhudia ongezeko la wimbi la wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao wanakimbia mapigano jimboni Kivu Kaskazini.
31-5-2023 • 0
WHO: Watu milioni 8 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na tumbaku:
Ikiwa leo ni siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, limezitaka nchi kuacha kutoa ruzuku kwa kilimo cha tumbaku na badala yake kuunga mkono na kusaidia kilimo cha mazao endelevu yatakayoweza kulisha mamilioni ya watu wenye uhitaji wa chakula. Kupitia ujumbe wake wa siku hii mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema “Tumbaku inawajibika kwa vifo milioni 8 kila mwaka lakini bado serikali duniani kote zitatumia mamilioni ya dola kuunga mkono mashamba ya tumbaku. Watu duniani kote wanakabiliwa na njaa wakati ekari milioni 300 za dunia yetu zinatumika kulima tumbaku.”Akaenda mbali zaidi na kusistiza kwamba “Ni wakati wa kubadili mwelekeo wa juhudi zetu na kujikita na kilimo ambacho kinastawisha siha yetu na mazingira yetu.”Hivi sasa kwa mujibu wa WHO zaidi ya watu milioni 300 duniani kote wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na uhakika wa chakula wakati ambapo Zaidi ya ekari milioni 300 katika nchi zaidi ya 120 duniani zinatumika kulima tumbaku hata kwenye nchi ambazo watu wana njaa kali.WHOWHO imesema tumbaku inagharimu maisha wa watu milioni 8 kila mwaka.Dkt. Tedros amesema WHO inafanyakazi kwa karibu na mashirika mengi ya Umoja wa Mataifa likiwemo la chakula na kilimo FAO na la mpango wa chakula duniani WFP kuwasaidia wakulima kuhamia kwenye kilimo mbadala wa tumbaku kwani “kwa kuchagua kulima chakula badala ya tumbaku tutatoa kipaumbele kwa afya, kulinda mfumo wa maisha na kuimarisha uhakika wa chakula kwa wote.”Lengo la maadhimisho ya mwaka huu ni kuujulisha umma hatari za matumizi ya tumbaku, mwenendo wa biashara wa makampuni ya tumbaku, nini kinachofanywa na WHO kupambana na janga la tumbaku na nini watu duniani kote wanaweza kufanya ili kudai haki yao ya afya, maisha yenye afya na kuvilinda vizazi vijavyo.Siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani huadhimishwa kila mwaka Mei 31 na mwaka huu imebeka maudhui “Lima chakula sio tumbaku.”
31-5-2023 • 0
31 MEI 2023
Hii leo katika jarida Anold Kayanda anamulika kwa kiasi kikubwa siku ya kutokomeza matumizi ya tumbaku duniani halikadhalika hatua ya kupunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi walioko nchini Tanzania.Ikiwa leo ni siku ya kupinga matumizi ya tumbaku duniani shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, limezitaka nchi kuacha kutoa ruzuku kwa kilimo cha tumbaku na badala yake kuunga mkono na kusaidia kilimo cha mazao endelevu yatakayoweza kulisha mamilioni ya watu wenye uhitaji wa chakula.Zaidi ya wakimbizi 200,000 walioko nchini Tanzania wataanza kupokea nusu mgao wa chakula wanachopatiwa kutokana na ukata unaokabili shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP. Asilimia 70 ya wakimbizi hao wanatoka Burundi ilhali asilimia 30 wanatoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.Makala: Harakati za mkulima Sprina Robi Chacha, wa nchini Kenya za kuondokana na kilimo cha tumbaku na sasa analima maharage. Ameshinda tuzo ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO.Mashinani: Harakati huko Cabo Verde za kukabiliana na uvutaji wa sigara
31-5-2023 • 0
30 MEI 2023
Jaridani hii leo ni mada kwa kina leo tunaelekea nchini DRC kuangazia kikosi cha pili cha walinda amani kutoka Kenya cha kuchukua hatua za haraka KEN QRF 2 kinachohudumu mjini Beni, Jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, DRC-MONUSCO. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za matumaini kwa familia zilizokata tamaa zilizokwama katika kitovu cha mzozo nchini Sudan, msaada wa kibinadamu kwa watoto nchini humo, na wakimbizi wanaohama kwa nchi jirani. Mashinani tutakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo Jumanne limeeleza kuwa kwa mara ya kwanza tangu mapigano yazuke nchini Sudan tarehe 15 Aprili, wahudumu wa kibinadamu sasa wameweza kufikisha msaada wa chakula kwa familia zilizokata tamaa zilizokwama katika kitovu cha mzozo huo, Khartoum. Tukisalia na taarifa kuhusu hali ya Sudan, hii leo pia Msemaji wa UNICEF James Elder amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba "watoto wengi zaidi nchini Sudan wanahitaji usaidizi wa kuokoa maisha kuliko hapo awali", huku watoto milioni 13.6 wakihitaji msaada wa haraka. Na akifanya kulinganisha idadi hiyo akasema kwamba, "Hii ni zaidi ya idadi ya watu wote wa Sweden, Ureno au Rwanda,"Na Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) Filippo Grandi akihitimisha ziara ya siku tatu nchini Misri ametoa wito wa dharura wa msaada kwa watu wanaokimbia Sudan na akazisihi nchi zinazowapokea wakimbizi wa Sudan kuendelea kuacha mipaka yao wazi kwa ajili ya wale wanaotoroka vita.Katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Kamishna Suzan Kaganda ambaye anahusika na Utawala na Raslimali watu katika Jeshi la Polisi Tanzania akizungumzia mikakati ya Jeshi la Polisi la Tanzania kushiriki katika shughuli za ulinzi wa amani duniani.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, Karibu!
30-5-2023 • 0
The Africa Soft Power Rwanda ujumuishe wanawake katika mkutano wao: UN
Viongozi, watafiti, vijana, na wanawake kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika Kigali kwa ajili ya mkutano wa pili wa Africa Soft Power kuanzia tarehe 23 hadi 27 Mei 2023.Mkutano huu umeandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa nchini Rwanda. Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Rwanda ni Ozonnia Ojielo anasema“ Mkutano wa Soft Power Africa, ni mradi mzuri unaohusu ukweli kwamba tunahitaji wote wanaume na wanawake ili kusaidia kuleta mabadiliko katika jamii, ni kuhusu kuwawezesha wanawake kufikia uwezo wao na hivyo majadiliano haya yanaangazia machaguo mbalimbali lakini hususani kuhusu jukumu la sekta binafsi , nafasi ya uwezeshaji wa kiuchumi kama nyenzo kwa ajili ya mabadiliko, na ndio sababu mfumo wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda unafuha kushirikiana na mradi huu wa Soft Power Africa “Mkutano wa Africa Soft Power ni tukio kuu ambalo lengo lake ni kukuza viwanda vya ubunifu vya Afrika, uchumi wa maarifa, na kutumia nguvu yake laini kwa maendeleo. Balozi Amina Mohamed kutoka Kenya alikuwa na haya ya kusema kuhusu mradi huu" Nadhani hili ni jukwaa zuri sana na ninafurahi kwamba hii ni mara ya pili tu linafanyika, na hivyo matarajio yangu ni kwamba nitahudhuria pia lijalo, ili tuweze kuona kwamba tunachokizungumzia ni athari za maendeleo katika bara zima.”Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Rwanda aliongoza majadiliano ya jopo ambalo lilichunguza jukumu la taasisi za jadi za Kiafrika katika kukuza maendeleo ya bara hilo, na mifano ni mingi kama asemavyo Mfalme wa Onitsha jimbo la Anambra Kusini Mashariki mwa Nigeria Mfalme Nnaemeka Alfred Achebe“ Tukisukumwa na janga la COVID-19 tuliharakisha mpango tulioanzisha mnamo 2017 mwanzoni mwa jukwaa la maendeleo yetu ya jamii. Tulipata takriban vijana 100 wa kike na wa kiume, ambao miaka minne iliyopita, walikuwa hawafanyi lolote, leo wanaendesha biashara zao kwa mafanikio.”Majadiliano ya kushirikiana katika Mkutano wa Africa Soft Power yalilenga maeneo ya mada matatu: uongozi wa wanawake, nguvu ya ubunifu na uchumi wa kisasa, na kusherehekea sauti za Kiafrika na za diaspora ya kisasa.
26-5-2023 • 0
Fulgence Kayishema, Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari huenda atahukumiwa nchini Rwanda - Serge Brammertz
Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka ya mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari, IRMCT iliyoko Arusha Tanzania, Serge Brammertz ameeleza kuwa Fulgence Kayishema, mmoja wa watuhumiwa vinara waliokuwa wanasakwa zaidi kwa kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda, aliyekamatwa juzi Mei 24 huko Paarl nchini Afrika Kusini huenda akapelekwa nchini Rwanda kukabiliana na mkono wa sheria kutokana na tuhuma za kushiriki kuwaua watu zaidi ya 2000 wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994. Anold Kayanda amezungumza na Mwendesha Mashitaka huyo na kutuandalia makala ifuatayo.
26-5-2023 • 0
26 MEI 2023
Jaridani hii leo tunaangazia ripoti kuhusu matumizi ya tumbaku na wakimbizi wa Sudan. Makala tunaangazia mauaji ya kimbari nchini Rwanda na mashinani tutakupeleka nchini Chad, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limezisihi nchi kuacha kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku na badala yake kuelekeza usaidizi wao kwenye mazao endelevu yatakayo wanufaisha mamilioni ya watu. Walimuua mume wangu, walijeruhi mwanangu na mimi walinipiga, ni simulizi ya mama ambaye sasa yuko na watoto wake nchini Chad akitokea Sudan kwani nchini mwake ni kama wasemavyo wahenga, Amkani si shwari kufuatia mapigano yaliyoanza tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu ambayo pamoja na kuua zaidi ya watu 700 wengine zaidi ya 300,000 wamekimbilia nchi jirani ikiwemo Chad na miongoni mwao ni Hawaye Ibrahim.Makala Mwendesha Mashitaka Mkuu wa ofisi ya mwendesha mashtaka ya mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari, IRMCT iliyoko Arusha Tanzania, Serge Brammertz ameeleza ni kwa nini ilichukua muda mrefu wa zaidi ya miaka 20 kumtia mbaroni Fulgence Kayishema, mmoja wa watuhumiwa vinara waliokuwa wanasakwa zaidi kwa kuhusika na mauaji ya kimbari nchini Rwanda, aliyekamatwa juzi Mei 24 huko Paarl nchini Afrika Kusini na leo kufikishwa katika mahakama ya Afrika Kusini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kumrejesha nchini Rwanda ili akabiliane na mkono wa sheria.Katika mashinani na tukiwa tunaelekea siku ya walinda amani duniani leo tutaelekea nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR kusikiliza ujumbe kutoka kwa mlinda amani akilezea umuhimu wa siku ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
26-5-2023 • 0
Mama akiwa na wanae ukimbizini Chad asimulia yaliyomsibu Sudan
Walimuua mume wangu, walijeruhi mwanangu na mimi walinipiga, ni simulizi ya mama ambaye sasa yuko na watoto wake nchini Chad akitokea Sudan kwani nchini mwake ni kama wasemavyo wahenga, Amkani si shwari kufuatia mapigano yaliyoanza tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu ambayo pamoja na kuua zaidi ya watu 700 wengine zaidi ya 300,000 wamekimbilia nchi jirani ikiwemo Chad na miongoni mwao ni Hawaye Ibrahim.Sura isiyo na matumaini na iliyopauka!!! Hawaye Ibrahim yuko na watoto wake watatu hapa Koufroune nchini Chad kwenye kituo cha mpito cha wakimbizi kutoka Sudan, lakini mawazo hayako hapa kabisa. Hawaye anasema “Ni mapigano yamenileta hapa. Wanamgambo waliingia nyumbani kwetu, walimuua mume wangu na wakamjeruhi mtoto wangu wa kiume .Mimi mwenyewe walinitesa, hivyo nikakimbia na kuja hapa Chad.” Anamnyanyua mwanae aliyejeruhiwa kuonesha kovu, anaitwa Manane, ameshonwa nyuzi 7 juu ya kitovu na 3 chini ya kitovu, angalau jeraha limepona. Hawaye huku sasa akionesha sikio lake anaendelea kusema, “walinipiga kwa fimbo na hadi sasa sikio langu la kushoto halifanyi kazi ,hivyo siwezi kusikia vizuri.” Kutoka kuishi kwenye nyumba yao huko Darfur nchini Sudan hadi kwenye kibanda hiki kilichoegeshewa na kuzungushiwa nailoni, hapa jua ni lao! na mvua ni yao. Akikumbuka safari yao, Hawaye anasema “nilikimbia saa tano za usiku nikiwa nimembeba mgongoni mwanangu aliyejeruhiwa. Sikuwa hata na usafiri wa punda. Ilibidi watoto wengine niwaache. Waliletwa hapa na watu wengine.” Hawaye akiendelea kuwaza na kuwazua akiwa na wanawe, kwingineko hapa wanawake wanaonekana wakisubiri mgao wa vifaa vya huduma za msingi huku wengine wakizidi kuwasili na virago vyao kwa kutumia punda. Brice Degla Mratibu Mwandamizi wa masuala ya dharura wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Chad anasema, “Wamekimbia sio tu kwa sababu ya vita mjini Khartoum, bali pia kwa sababu ya mapigano ya kikabila baina ya jamii huko Tendalti. Halikadhalika hofu ya kushambuliwa kwa sababu ya vita, imewalazimu wakimbie na ndio wote sasa wamefika hapa.” Katika vibanda vingine, akina mama wako na watoto wao, njaa ni dhahiri. Ingawa tayari kuna usalama tofauti na kule Darfur alikotoka bado Hawaye ana mahitaji akisema, “nahitaji chakula, nahitaji nguo, nahitaji pia malazi na sabuni na vitu vingine ili niweze kutulia.” Mgao wa bidhaa muhimu unaendelea huku wakimbizi wengine wakipanda magari wakipungiwa na wenzao waliosalia. Bwana Delga anasema , “UNCHR inabaini maeneo yaliyo mbali, angalau kilometa 50 kutoka hapa, ambako inahamishia wakimbizi kutoka hapa mpakani, ili hatari ya ukosefu wa usalama iwe imepatiwa jawabu, lakini vile vile kuwapatia msaada.” Baada ya muda, walioondoka Koufroune wamewasili Gaga nchini Chad hapa wamepatiwa angalau makazi yenye staha na sasa wanaanza maisha upya ugenini wakiwa matumaini mapigano yaliyoanza tarehe 15 Aprili nchini mwao Sudan yatamalizika ili waweze kurejea nyumbani.
26-5-2023 • 0
WHO: Nchi ziache kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO limezisihi nchi kuacha kutoa ruzuku kwa wakulima wa tumbaku na badala yake kuelekeza usaidizi wao kwenye mazao endelevu yatakayo wanufaisha mamilioni ya watu.Katika kuelekea sikuya kupinga matumizi ya tumbaku duniani itakayoadhimishwa Mei 31 WHO inasema , watu milioni 300 ulimwenguni wanakabiliwa na uhaba wa chakula wakati huo huo zaidi ya hekta milioni 3 katika nchi 120 zinatumika kulima tumbaku, hata katika zile nchi zenye tatizo la njaa.WHO katika taarifa yao kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo huko Geneva Uswisi imeeleza kuwa kwa kuchagua kulima mazao ya chakula badala ya tumbaku inamaanisha jamii inatoa kipaumbele kwenye afya, kulinda baianowai na kuimarisha uhakika wa chakula.Akizungumzia athari za tumbaku, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema “tumbaku imesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 8 kwa mwaka, na bado serikali duniani kote zinatumia mamilioni ya kuwasaidia wakulima wa zao hilo.” Ripoti mpya iliyotolewa na WHO kuelekea siku ya kupinga matumizi ya tumbaku iitwayo “Lima chakula sio tumbaku” imeeleza madhara ya kulima tumbaku na faidi ambazo wakulima, jamii, uchumi, mazingira na dunia kwa ujumla itapata iwapo itahamia kwenye ukulima wa mazao mengine. Ripoti hiyo pia inafichua tasnia ya tumbaku kuwa inawaingiza wakulima katika changamoto mbalimbali ikiwemo mzunguko mbaya wa madeni, wakulima kupata magonjwa na watoto zaidi ya milioni 1 wametumbukia kwenye kilimo hicho na kukosa fursa ya kupata elimu.Katika kuhakikisha wakulima wanasaidiwa kuhamia kwenye kilimo cha mazao ya chakula WHO kwa kushirikiana na mashirika mengine ya UN lile la Mpango wa chakula duniani WFP na la chakula na kilimo FAO wanawasaidia wakulima 5000 nchini Kenya na Zambia kulima mazoa ya chakula endelevu badala ya tumbaku.Katika juhudi hizo WHO kila mwaka katika siku ya Kutotumia tumbaku huwaenzi wale wanaoleta mabadiliko chanya katika udhibiti wa tumbaku na mwaka huu mmoja wa washindi wa Tuzo hizo, Bi. Sprina Robi Chacha, mkulima wa kike kutoka nchini Kenya ambaye anatambulika si tu kwa kuachana na kilimo cha tumbaku kuhamia kwenye maharagwe yenye protini nyingi, bali pia kutoa mafunzo kwa mamia ya wakulima wengine ili na wao waweze kutoka kwenye kilimo cha tumbaku na kujenga jamii yenye afya bora.
26-5-2023 • 0
Methali: Aanguae huanguliwa
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Aanguae huanguliwa.”
25-5-2023 • 0
25 MEI 2023
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina na katika kuelekea siku ya walinda Amani duniani itakayoadhimishwa Mei 29 leo tunakupeleka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR kumulika jinsi mchango wa kusongesha maendeleo wa kikosi cha walindamani kutoka Tanzania TANBAT6 unavyopokelewa na wananchi wa taifa hilo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za masuala ya jinsia, biashara huru na haki za binadamu. Katika kujifunza kiswahili tutasikia maana ya methali “Aanguae huanguliwa.”Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres amemtangaza Kapteni Cecilia Erzuah kutoka Ghana kuwa mshindi wa tuzo ya kila mwaka ya Mchechemuzi wa Masuala ya jinsia kwenye operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa. Leo ni siku ya Afrika ikiwa ni kumbukizi ya kuanzishwa kwa Umoja wa nchi huru za Afrika, OAU sasa Muungano wa Afrika (AU) tarehe 25 mwezi Mei mwaka 1963 ambapo Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo, UNCTAD imesema eneo la biashara huru la Afrika, AfCFTA linatoa fursa ya kukuza biashara ya ndani barani humo.Na baada ya kuwa mtoro kwa zaidi ya miaka 20, hatimaye Fulgence Kayishema, mmoja wa watuhumiwa vinara waliokuwa wanasakwa zaidi kwa kuhusika na mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi nchini Rwanda, amekamatwa jana huko Paarl nchini Afrika Kusini kufuatia ushirikiano baina ya ofisi ya mwendesha mashtaka ya mfumo wa kimataifa wa kushughulikia mabaki ya kesi za mauaji ya kimbari, IRMCT na serikali ya Afrika Kusini.Katika kujifunza Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Aanguae huanguliwa.”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
25-5-2023 • 0
Huduma za fedha mtandao zamwondolea mwanafunzi adha ya kufuata fedha benki
Misri, taifa lenye watu milioni 100 hivi sasa, lakini ni asilimia 30 tu ya watu hao yani watu milioni 36.8 ndio wenye akaunti za benki. Katika zama hizo za huduma za fedha kimtandao, mashirika ya mawasiliano ya simu yanaingia ubia na benki ili kupanua wigo wa huduma hizo. Ukosefu wa huduma za fedha kimtandao zinakuwa kikwazo kwani wananchi hupoteza muda mwingi benki kusubiria malipo ambayo wangaliweza kuyapokea kupitia simu za kiganjani au rununu. Shuhuda pande zote mbili hizo ni msichana mmoja mkazi wa Cairo nchini Misri kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mawasiliano duniani, ITU.
24-5-2023 • 0
Ukame: Dola bilioni 7 zinahitaji kusaidia pembe ya Afrika
Hii leo jijini New York Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwakushirikiana na nchi saba wanachama wa UN wanaendesha tukio la uchangishaji fedha lengo likiwa ni kukusanya dola bilioni 7 kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu kwa nchi zilizopo pembe ya Afrika. Kwa miongo kadhaa pembe ya Afrika imekuwa ikikabiliwa na ukame mkali hali iliyofanya takriban watu milioni 43.3 kuhitaji usaidizi wa kuokoa maisha na kustahimili changamoto zinazo wakabali hususan katika nchi za Kenya, Somalia na Ethiopia.Ukame umeleta njaa, kutokuwa na uhakika wa upatikanaji wa chakula na shida ya maji ambayo inachangia katika kuleta magonjwa.Hivi karibuni mvua zimeanza kunyesha, wananchi wamekuwa wakitarajia zitasaidia kupunguza changamoto zao lakini kama waswahili wasemavyo ‘ngombe wa masikini hazai’ ndicho kilichotokea kwa nchi hizo kwani mvua kubwa zimeleta mafuriko na kwa mujibu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA zaidi ya watu 900,000 wameathiriwa na mvua hizo.Mmoja wa watu hao ni Abdirahaman Ali Sheikh kutoka nchini Somalia, “Angalia hali ilivyo sasa, maji yametapakaa kwenye nyumba yangu yote na watoto wangu.”Bi. Qiyaas Axmed Farax amelazimika kuyakimbia makazi yake sababu ya mafuriko na sasa anahitaji msaada wa kibinadamu.“Tunahitaji chakula, malazi na maji, hatuna kitu, nguo zetu, vyakula na vingine vyote vimesombwa na maji. Watoto wangu walikuwa hatarini lakini namshukuru Mungu kwasasa tupo salama.”Mkutano huu wa ngazi za juu unaofanyika hapa jijini New York Marekani unatarajia kusaidia zaidi ya watu milioni 32 ikiwemo hawa waliathirika na mafuriko.Nchi saba zinazoshirikiana na Katibu Mkuu Guterres katika kendesha tukio hilo la ahadi ni Marekani, Uingereza, Qatar, Italia pamoja na nchi ambazo zinauhitaji wa haraka wa misaada hiyo ambazo ni Ethiopia, Somalia na Kenya.
24-5-2023 • 0
24 MEI 2023
Jaridani leo tunaangazia machafuko nchini Sudan na ukame uliokithiri katika pembe ya Afrika. Makala tunakupeleka nchini Misri na mashinani nchini DRC, kulikoni? Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, ambaye pia ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia kipindi cha mpito SUDAN, UNITAMS amesema bila kujali ni nani anayehusika na janga la kibinadamu nchini Sudan, Umoja wa Mataifa utaendelea kuwasaidia wananchi. Hii leo jijini New York Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwakushirikiana na nchi saba wanachama wa UN wanaendesha tukio la uchangishaji fedha lengo likiwa ni kukusanya dola bilioni 7 kwa ajili ya usaidizi wa kibinadamu kwa nchi zilizopo pembe ya Afrika.Makala tunaelekea Misri, taifa lenye watu milioni 100 hivi sasa, lakini ni asilimia 30 tu ya watu hao yani watu milioni 36.8 ndio wenye akaunti za benki. Katika zama hizo za huduma za fedha kimtandao, mashirika ya mawasiliano ya simu yanaingia ubia na benki ili kupanua wigo wa huduma hizo.Katika mashinani na tukiwa tunaelekea siku ya walinda amani duniani leo tutaelekea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kusikiliza ni kwa jinsi gani tasnia ya michezo ya kuigiza na vipaji vya wenyeji vimesaidia kuzuia unyanyasaji na ukatili wa kingono unaosababishwa na walinda amani na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
24-5-2023 • 0
Bila kujali upande, Umoja wa Mataifa mara zote utasaidia watu Sudan - Volker Perthes
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes, ambaye pia ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia kipindi cha mpito SUDAN, UNITAMS amesema bila kujali ni nani anayehusika na janga la kibinadamu nchini Sudan, Umoja wa Mataifa utaendelea kuwasaidia wananchi.Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, Volker Perthes ameyasema hayo jijini New York Marekani katika mahojiano na Abdelmonem Makki wa Idhaa wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa muda mfupi baada ya kiongozi huyo kulieleza Baraza la Usalama hali ya Sudan. “Tumepaza sauti kimataifa. Tumetoa mpango mpya wa misaada ya kibinadamu na kutoa wito kwa ulimwengu kusaidia kifedha, kusaidia watu. Na kabla ya vita, na mashirika mengine ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa yalishakadiria kuwa tuna watu milioni 15 wenye uhitaji nchini Sudan na sasa tunakadiria watu milioni 18 au milioni 19 kwa hiyo tunahitaji fedha zaidi kwa ajili hiyo na mtiririko wa misaada umeanza.” Bwana Parthes alipoulizwa kwamba sasa ni zaidi ya wiki tano tangu kuzuka kwa mapigano haya ya Sudan na kwamba usitishaji mapigano umechukua muda mrefu na kwa hiyo inaonekana kwamba wahusika wa pande zinazohasimiana hawako tayari kuacha mapigano, Je, ni motisha au kichocheo gani pande hizo kinzani zitapewa ili kuacha kabisa kupigana, anasema mazungumzo ndio suluhu pekee, "Nadhani motisha kubwa ni kukosekana kwa ushindi katika uwanja wa vita. Katika siku za kwanza za vita, Aprili 15 na Aprili 16 tulisikia pande zote mbili zikisema kwamba wanatarajia ushindi wa haraka dhidi ya upande mwingine. Hapana, hilo halijatokea. Na kila mtu anaweza kuona kwamba halijatokea. Kwa hivyo, nadhani kuna utambuzi unaokua kwa pande zote mbili kwamba ushindi wa vita hii hautakuwa wa kijeshi, angalau sio kwa ushindi rahisi. Na hata kama kungekuwa na ushindi, unaweza kuja kwa gharama ya kuharibu nchi au mji mkuu au sehemu kubwa ya nchi.” Licha ya kinachoendelea Sudan, Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu nchini Sudan, ana matumaini, kwamba hivi karibuni vita itakwisha na mchakato wa mpito unaweza kuanza tena na kwamba ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia kipindi cha mpito SUDAN, UNITAMS watasalia nchini humo kufanya kila wawezalo kusaidia katika mchakato wa mpito kwa njia yoyote ile wanayoiweza.
24-5-2023 • 0
23 MEI 2023
Hii leo ni siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Fistula na jaridani kama ilivyo ada ya kila Jumanne leo tunakuletea mada kwa kina ikimulika juhudi za kutokomeza Fistula zinazofanywa na Hospitali ya CCBRT nchini Tanzania. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za utapiamlo kwa watoto katika Pembe ya Afrika na msaada wa kibinadamu nchini Myanmar. Mashinani tunakuletea ujumbe kuhusu hatua zinapaswa kuchukuliwa ili kuzuia fistula itokanayo na uzazi. Fistula ya uzazi ni shimo kati ya njia ya uzazi na kibofu cha mkojo au rektamu, inayosababishwa na uchungu wa kujifungua wa muda mrefu, bila kupata matibabu ya wakati, na ya hali ya juu. Maudhui ya mwaka huu ni “Miaka 20 ya vita dhidi ya ugonjwa huu kuna maendeleo lakini hayatishi, hivyo hatua zhitajika sasa kutokomeza Fistula ifikapo 2030”. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limeonya kwamba Watoto zaidi ya milioni 7 wa umri wa chini ya miaka mitano katika Pembe ya Afrika wana utapiamlo na wanahitaji msaada wa haraka wa lishe huku wengine zaidi ya milioni 1.9 wakiwa katika hatari ya kifo kutokana na unyafuzi.Na jumuiya ya kimataifa nchini Myanmar leo imezindua ombi la dola milioni 333 ili kuwasaidia watu millioni 1.6 walioathirika na kimbunga Mocha kilichoikumba nchi hiyo Mei 14.Katika mashinani tunajiunga na mshauri wa kanda ya Afrika katika masuala ya afya ya jinsia na uzazi kufahamu ni hatua gani zinapaswa kuchukuliwa ili kuzuia fistula itokanayo na uzazi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
23-5-2023 • 0
Mradi wa Binti Shupavu wasongesha SDG4 nchini Tanzania
Nchini Tanzania Shirika la lisilo la kiserikali la Girls Livelihood and Mentorship Initiative (GLAMI) kupitia Mradi wake wa Binti Shupavu, unaowajengea Stadi za Maisha ikiwemo uwezo wa kujitambua, mabinti walioko Shule, unaendelea na juhudi za kufanikisha Lengo la Nne la maendeleo endelevu SDG’s linalohusu Elimu, ambapo Jumla ya wasichana 824 wananufaika kutoka katika Shule Tisa zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, ambapo Mwezi huu wa Tano limekamilisha Programu ya kufanya vikao na wazazi katika Shule hizo ili kuwajengea uwezo wa malezi ya watoto wao. Hamad Rashid wa Redio washirika MVIWATA FM kutoka Morogoro, mashariki mwa Tanzania amehudhuria baadhi ya vikao vya wazazi na GLAMI kisha kutuandalia makala ifuatayo.
22-5-2023 • 0
22 MEI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya ukatili wa kijinsia nchini DRC na msaada wa kibinadamu nchini Myanmar. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunakupeleka Ureno, kulikoni? Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Bruno Lemarquis amezungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi hii leo na kusema vitendo vya ukatili wa kijinsia na kingono dhidi ya wanawake na wasichana kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani nchini DRC vimeongezeka kwa asilimia 37 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana, huku akitaka hatua za haraka zichukuliwe ili kurekebisha kinachoendelea. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linasema hadi kufikia mwisho wa mwaka huu 2023 linahitaji dola za Marekani milioni 60 ili kutoa msaada wa chakula cha kuokoa maisha nchini Myanmar kwa watu milioni 2.1 walioathiriwa na majanga mengi na magumu kikiwemo kimbunga Mocha.Makala tunakwenda Morogoro, mashariki mwa Tanzania kusikiliza harakati za shirika lisilo la kiserikali la Girls Livelihood and Mentorship Initiative (GLAMI) kupitia Mradi wake wa Binti Shupavu, wa kuwajengea Stadi za Maisha wasichana ili kusonga mbele kielimu.Na katika mashinani leo tutakuwa Ureno kwa mtaalam wa sayansi na baolojia ya baharí ambaye pia ni mvuvi na mwanzilishi mwenza wa Ocean alive, Raqel Gaspar akizungumzia umuhimu wa kulinda viumbe wa baharini kama Pomboo na mazingira yao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
22-5-2023 • 0
Wakimbizi wa ndani DRC wakabiliwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kingono
Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC Bruno Lemarquis amezungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi hii leo na kusema vitendo vya ukatili wa kijinsia na kingono dhidi ya wanawake na wasichana kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani nchini DRC vimeongezeka kwa asilimia 37 mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana, huku akitaka hatua za haraka zichukuliwe ili kurekebisha kinachoendelea.Katika mkutano wake huo uliomulika hali ya kibinadamu nchini DRC, Bwana Lemarquis ambaye pia ni Naibu Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC amesema mwaka jana pekee kwenye makazi ya wakimbizi katika jimbo la Kivu Kaskazini, kulikuwa na matukio zaidi ya 38,000 ya ukatili wa kingono na kwamba katika miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka huu pekee, kumekuweko na ongezeko kwa asilimia 37. Amesema “wanawake na watoto walio hatarini zaidi ambao wanasaka hifadhi kwenye makazi hayo, wanajikuta wakikabiliwa na ukatili na machungu zaidi na hili halivumiliki.” Hivyo amesema hatua zaidi zinahitajika kuchukuliwa na serikali pamoja na wadau ili kudhibiti hali hiyo. Lemarquis amesema ongezeko la wakimbizi wa ndani kwenye makazi linatokana pia na ombwe la ulinzi kwenye maeneo ya kaskazini mwa jimbo la Kivu Kaskazini, Ituri na Kivu Kusini kutokana na vikosi vya usalama kuhamishwa ili kwenda kukabiliana na waasi wa M23. Amesema baadhi ya makundi yaliyojihami kama vile ADF, Zaire na CODECO yametumia fursa hiyo kushamirisha mashambulizi yao dhidi ya raia hususan Ituri. Naibu Mwakilishi huyo wa Katibu Mkuu nchini DRC amegusia pia jimbo la Mai-Ndombe lililoko magharibi mwa DRC, ambako amesema ghasia zilizoibuka mwezi Juni mwaka jana zimeendelea na zinasambaa kwenye maeneo ya jirani na kwamba kwa kuwa DRC inaelekea kwenye uchaguzi ni vema kuchukua hatua kudhibiti ili ghasia hizo zisijekuwa chanzo cha janga lingine la kibinadamu nchini humo.
22-5-2023 • 0
WFP inasaka fedha kuendelea kuwasaidia waathirika wa Kimbunga Mocha
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) linasema hadi kufikia mwisho wa mwaka huu 2023 linahitaji dola za Marekani milioni 60 ili kutoa msaada wa chakula cha kuokoa maisha nchini Myanmar kwa watu milioni 2.1 walioathiriwa na majanga mengi na magumu kikiwemo kimbunga Mocha.Kwa mujibu wa WFP, kimbunga Mocha, dhoruba kali zaidi kuwahi kutokea katika Ghuba ya Bengal katika kipindi cha muongo mmoja, kimesababisha maafa kwa mamilioni ya watu walio tayari kwenye wakati mgumu, hasa nchini Myanmar. Kimbunga Mocha kimeacha uharibifu katika Jimbo la Rakhine kaskazini mwa Myanmar ambapo kaya katika vitongoji vingi na maeneo ya watu waliohama katika maeneo ya mabondeni wamepoteza akiba kubwa ya chakula na na vyanzo vingine vya kipato. Miundo muhimu kama hospitali na shule vimeharibiwa hasa katika mji mkuu wa jimbo la Rakhine, Sittwe. Mawasiliano na njia za umeme katika eneo hili la Myanmar zimevurugwa. Stephen Anderson ni Mkurugenzi wa WFP nchini Myanmar anaeleza wanachokifanya, "WFP tayari imeanza usambazaji wa haraka wa chakula kwa watu wenye mahitaji makubwa huko Rakhine na Magwe na iataongeza zaidi katika siku zijazo. Tunatumai kuwafikia angalau watu 800,0000 ambao wanachukuliwa kuwa wenye uhitaji mkubwa zaidi. Timu zetu ziko kwenye eneo kufanya kazi mchana na usiku kufanya lolote wawezalo ili kuongeza msaada ili kuwafikia wale wote wanaohitaji popote walipo.” Wakati wa mchana Mei 14 kimbunga kikali kilipiga Mynmar karibu na mpaka wa Bangladesh kwa upepo unaokadiriwa kuwa na kasi ya karibu kilomita 280 kwa saa na hivyo kukifanya kuwa moja ya vimbunga vikali zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kwenye ukanda huo.
22-5-2023 • 0
IOM yaeleza ilivyo hatari kuvuka eneo la msitu wa Darién
UN wachukua hatua kuokoa watoto Malawi hatarini kukumbwa na utapiamlo
Takribani watoto 573,000 wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Malawi wako hatarini kukumbwa na utapiamlo, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto duniani, UNICEF huku likisema linahitaji dola milioni 87.7 kukidhi mahitaji ya watu milioni 6.5 wakiwemo watoto milioni 3.3 nchini humo, ikiwa ni ombi jipya la fedha lililotolewa leo.Assumpta Massoi na taarifa kwa kina.UNICEF kupitia taarifa yake iliyotolewa jijiini Lilongwe Malawi hii leo, inasema maendeleo yaliyopatikana hivi karibuni ya kukabili utapiamlo yanayoyoma kutokana na uhaba mkubwa wa chakula ukigubikwa na matukio ya mara kwa mara ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi, milipuko ya magonjwa yanayozuilika, ukosefu wa utulivu wa kiuchumi na ukosefu mkubwa wa ufadhili kwenye sekta za kijamii.Taarifa hiyo inasema Malawi bado inazingirwa na kiza kinene cha athari mbaya za kimbunga Fredy kilichokumba taifa hilo mwezi Machi na kuacha hadi leo hii watu 659,000 wakimbizi wa ndani wakiwemo watoto.Halikadhalika mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu bado unaendelea na tayari umesababisha vifo vya watu 1,759.UNICEF/Thoko ChikondiDalitso Dines mwenye umri wa miaka 14 in mwanafunzi wa darasa la 8 na manusura wa kimbunga Freddy. Hapa yuko darasani kwenye shule ya msingi ya Chumani huko Mulanje kusini mwa Malawi akijisomea. Hii ni tarehe 23 Machi 2023.Mwakilishi wa UNICEF nchini Malawi Gianfranco Rotigliano anasema watoto nchini Malawi wanakabiliwa na mlolongo wa majanga. Ukosefu wa uhakika wa kupata chakula ukichochewa na janga la mabadiliko ya tabianchi, mlipuko wa magonjwa na kutwama kwa uchumi duniani, vyote vinatishia maisha ya mamilioni ya watoto.Amerejelea ombi la Hatua za Kiutu kwa Watoto, HAC lililozinduliwa leo na UNICEF likionesha ongezeko la matukio ya utapiamlo miongoni mwa watoto katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ambapo mwaka 2023 pekee watoto 62,000 wenye umri wa kati ya miezi 6 hadi miaka 5 wako hatarini kukumbwa na unyafuzi au udumavu.Ni kwa mantiki hiyo UNICEF imeongeza ombi lake kwa usaidizi Malawi kutoka zaidi ya dola milioni 52 hadi dola milioni 87 ili kukidhi mahitaji ya watu milioni 6.5 wakiwemo watoto milioni 3.3.Fedha hizo zitatumika kununua mahitaji ya vyakula vilivyo tayari kuliwa ili kutibu unyafuzi, kupata huduma za maji safi na salama, huduma za kujisafi, afya, lishe, elimu, ulinzi dhidi ya watoto na miradi ya fedha taslimu.Bwana Rotigliano amesema bila usaidizi wa kifedha, kaya maskini na za Watoto walio hatarini watasalia bila huduma za msingi na zaidi ya yote amesema pamoja na misaada hiyo ni lazima kujengea mnepo ili kupunguza madhara makubwa ya milipuko na dharura za kiutu.
19-5-2023 • 0
Tunapatia UNHCR dola milioni 3 kusaidia dharura ya elimu kwa wakimbizi wa Sudan: ECW
Vita inayoendelea nchini Sudan mbali ya kukatili uhai wa mamia ya watu imesambaratisha na kupindua maisha ya mamilioni ya watu ikiwa ni pamoja na kuathiri huduma za msingi kama vile chakula, malazi, afya na elimu. Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yanahaha kukidhi mahitaji ya dharura ya maelfu ya wakimbizi ndani na nje ya Sudan.Asilimia kubwa ya waathirika ni wanawake na watoto ambao sasa mustakabali wao uko njia panda kwani elimu yao imekatizwa na vita hiyo. Kwa kutambua umuhimu wa elimu yao hata wakiwa ukimbizini mfuko wa kimatifa wa elimu haiwezi kusubiri ECW unashikamana na mashirika hayo kusaidia kunusuru elimu ya watoto hao kutoka Sudan. Juma hili ECW, imetangaza kuchagia dola milioni 3 kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ili ziwasaidie watoto wakimbizi wa Sudan walioko nchini Chad kuweza kupata elimu ya dharura. Makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha inafafanua zaidi
19-5-2023 • 0
19 MEI 2023
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Anold Kayanda akianzia barani Afrika, kisha Amerika ya Kusini na kurejea tena Afrika na kutamatishia barani Asia.1. Nchini Malawi Umoja wa Mataifa waomba fedha zaidi kunusuru watoto dhidi ya udumavu na unyafuzi kutokana na changamoto lukuki kama vile magonjwa ya milipuko, madhara ya tabianchi na ufadhili duni kwenye sekta za kijamii.2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) linaongeza juhudi za msaada wa kibinadamu kwenye mipaka ya Colombia, Costa Rica na Panama ili kusaidia wahamiaji wanaovuka kuelekea eneo la kaskazini mwa Amerika hasa kupitia msitu hatari wa Darien unaounganisha Amerika kusini na kaskazini. 3. Makala anakurejesha Afrika mpakani mwa Sudan na Chad kwenye kambi inayohifadhi wakimbizi wanaokimbia mapigano Sudan wakiwemo maelfu ya watoto.4. Mashinani anakupeleka nchini Sri Lanka kusikia ujumbe kuhusu ukulima wa chai na njia za kuipanda upya ili ilete mapato mazuri, ikiwa ni kuelekea siku ya chai duniani.
19-5-2023 • 0
18 MEI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamulika juhudi za wanawake wa jamii ya kifugaji mkoani Arusha ambao wameamua kujihusisha na ufugaji nyuki. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za siku za UN, msaada wa kibinadamu nchini Sudan na ulizi wa amani nchini DRC. Na katika jifunze lugha ya tunakuletea maana ya methali JINO LA PEMBE SI DAWA YA PENGO, karibu!.Hii leo ni siku ya kimataifa ya wanawake katika sekta ya usafirishaji baharini ambapo Katibu Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la usafirishaji baharini, IMO, Kitack Lim ametoa ujumbe ambao pamoja na mambo mengine unatambua mchango wa wafanyakazi hao baharini na nje ya bahari katika kusaidia mpito wa kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa, matumizi ya dijitali na mustakabli endelevu wa tasnia hiyo. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP limefikishia jumla ya watu 54,000 msaada wa dharura wa chakula kwenye vituo viwili vya mpakani huko Aswan na Misri wakati huu ambapo familia zinazidi kuingia Misri zikikimbia mapigano nchini Sudan.Na huko Bukavu, jimboni Kivu Kusini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo unaendesha mafunzo kwa polisi wa DRC juu ya ulinzi wa raia ambacho ni kipaumbele muhimu cha kupatia polisi hao usaidizi muhimu wa kuongeza uelewa wa jukumu hilo kuelekea mpito wa MONUSCO kuondoka nchini humo.Na katikajJifunze Kiswahili Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali Jino la Pembe si dawa ya pengo.Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, Karibu!
18-5-2023 • 0
METHALI: JINO LA PEMBE SI DAWA YA PENGO
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua methali, "Jino la Pembe si dawa ya pengo".
18-5-2023 • 0
Makala: Mradi wa NICHE wa afya na malezi umekua mkombozi kwa familia Kilifi Kenya
Kaunti ya Kilifi iliyoko Pwani ya Kenya ni moja ya maeneo ambako mradi wa majaribio wa elimu ya malezi na lishe kwa watoto unaendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ukifanyika kwa ushirikiano na serikali na wadau wengine,lengo kubwa likiwa ni kuzisaidia familia zisizojiweza na zilizo hatarini kupitia program ya lishe na elimu ya afya ziweze kutoa malezi bora kwa watoto wao huku zikikabiliana na ukatili katika familia hasa dhidi ya watoto.Mradi huu umeleta faraja kubwa kwa familia nyingi za kauti hiyo tuungane na Flora Nducha katika Makala hii kwa undani zaidi.
17-5-2023 • 0
Mijadala kuhusu utengenezaji wa Katiba ya Kudumu Sudan Kusini - UNMISS
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umefanya warsha za majadiliano katika mji wa Torit na Magwi mashariki mwa mji mkuu Juba jimboni Equatorial Mashariki ili kujadili kuhusu utungaji katiba na michakato ya uchaguzi.Sudan Kusini kwa sasa inatayarisha katiba yake ya kudumu ambayo si tu ni muhimu bali pia ni sharti la kufanya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliopangwa kufanyika mwakani, 2024. Makundi mbalimbali ya kijamii yaliyoshiriki katika majadiliano haya yaliyoratibiwa na UNMISS ni pamoja na wanawake, vijana, waliorejea kutoka ukimbizini, wakimbizi wa ndani, na viongozi wa kimila. Jessica Kalmas, mkimbizi aliyerejea ambaye sasa ni Msemaji wa Umoja wa Vijana, Equatoria Mashariki anasema, “Kunapaswa kuwa na uzingatiaji wanaorejea. Pia, suala la ukatili wa majumbani na kijinsia likomeshwe. Hili pia lijumuishwe kwenye katiba ya kudumu.”Masuala ambayo washiriki wameyapa uzito katika majadiliano yao ni nafasi sawa kwa wanawake katika maisha ya umma, kuhakikisha wasichana wote wana haki ya kupata elimu, na kukomesha desturi ya ndoa za kulazimishwa au za utotoni. Angel Omex, Mwanafunzi ni Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Sudan Kusini anaeleza, “Nimehudhuria huu mchakato wa kutengeneza katiba, na nina furaha kuwa sehemu yake. Na, kulingana na maoni yangu binafsi nadhani kinachopaswa kujumuishwa katika mchakato wa kutengeneza katiba ya kudumu ni suala la asilimia 35 ya jinsia. Wanawake wanatakiwa kupewa asilimia 35. Haifai kuwa kusema tu bali inapaswa kutekelezwa. Na sio tu kwamba wanaorejea kutoka ukimbizini ni muhimu sana, lakini pia wanapaswa kurejeshwa katika jamii na kusajiliwa.”Kwa pamoja, waliohudhuria walifikia mapendekezo kuhusiana na katiba ya kudumu na uchaguzi unaofuata, ikiwa ni pamoja na ushiriki wenye nguvu Zaidi wa vijana. UNMISS inashirikiana na mamlaka za serikali na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Fedha na Mipango ili kuandaa warsha kama hizo kote Sudan Kusini.
17-5-2023 • 0
Mashirika wafanyia marekebisho ombi la fedha kusaidia Sudan ili kukidhi mahitaji
Mzozo nchini Sudan ukiingia mwezi wa pili, hii leo Umoja wa Mataifa na wadau wake wamefanyia marekebisho ombi la usaidizi kwa nchi hiyo na sasa linafikia dola bilioni 3 kwa ajili ya kusaidia mamilioni ya watu nchini humo na mamia ya maelfu wengine waliokimbilia nchi jirani kusaka usalama.Uzinduzi wa ombi hilo lililorekebishwa umefanywa kwa pamoja hii leo huko Geneva Uswisi na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR. Hivi sasa jumla ya dola bilioni 2.56 zinahitajika kwa mwaka 2023, ikiwa ni nyongeza ya dola milioni 800 kutoka miezi michache iliyopita, ili kusaidia watu milioni 18 hadi mwishoni mwa mwaka huu na hivyo kufanya ombi hili kuwa ombi kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa Sudan. Marekebisho hayo yanazinagatia ongezeko la mahitaji lililochochewa na mapigano yanayoendelea ambapo Mkuu wa ofisi ya OCHA mjini Geneva, Ramesh Rajasingham amewaambia waandishi wa habari kuwa, “mahitaji nchini Sudan ni ya msingi na yamesambaa kama unavyoweza kufikiria kutokana na majanga: kulindwa dhidi ya mapigano, matibabu, chakula, maji, huduma za kujisafi, malazi na huduma dhidi ya kiwewe. Tunapata pia taarifa za ongezeko la ukatili wa kingono na waathirika hawawezi kupata huduma. Watoto wako hatarini zaidi katika janga hili linalozidi kuibuka.” Akifafanua kuhusu ombi la usaidizi kwa wakimbizi waliosaka hifadhi Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Misri, Ethiopia, Sudan Kusini na wakimbizi waliorejea nyumbani kutokana na changamoto Sudan, Kamishna Msaidizi wa UNHCR akihusika na operesheni, Raouf Mazour amesema, “hii leo tunatoa ombi la takribani dola milioni 472 ili kukidhi mahitaji ya zaidi ya watu milioni 1 katika kipindi cha miezi 6 ijayo.” Mapigano yalizuka Sudan tarehe 15 mwezi Aprili mwaka huu na hadi sasa mamia ya watu Sudan wameuawa, zaidi ya 5,000 wamejeruhiwa na mamilioni wamejificha majumbani mwao bila uwezo wa kupata huduma muhimu kama vile matibabu. UNHCR na OCHA wanasema leo hii, watu milioni 25 nchini Sudan, zaidi ya nusu ya idadi ya watu Sudan wanahitaji misaada ya kibinadamu na ulinzi.
17-5-2023 • 0
17 MEI 2023
Jaridani hii leo tunaangazia machafuko nchini Sudan na mchakato wa uchaguzi nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Kenya na Mashinani yunasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu idadi ya watu duniani.Mzozo nchini Sudan ukiingia mwezi wa pili, hii leo Umoja wa Mataifa na wadau wake wamefanyia marekebisho ombi la usaidizi kwa nchi hiyo na sasa linafikia dola bilioni 3 kwa ajili ya kusaidia mamilioni ya watu nchini humo na mamia ya maelfu wengine waliokimbilia nchi jirani kusaka usalama. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) umefanya warsha za majadiliano katika mji wa Torit na Magwi mashariki mwa mji mkuu Juba jimboni Equatorial Mashariki ili kujadili kuhusu utungaji katiba na michakato ya uchaguzi.Makala leo inatupeleka Kaunti ya Kilifi Pwani ya Kenya ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linashirikiana na serikali na wadau wengine kuzisaidia familia zisizojiweza na zilizo hatarini kupitia program ya lishe na elimu ya afya na malezi bora ijulikanayo kama NICHE.Katika mashinani tutasikia ujumbe kuhusu idadi ya watu duniani na jinsi ambavyo inatofoutiana kulingana na nchi.Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, Karibu!
17-5-2023 • 0
16 MEI 2023
Hii leo siku ya kimataifa ya kuishi pamoja kwa amani, halikadhalika siku ya kimataifa ya mwanga na nitakuletea mada kwa kina ikimulika jinsi njaa inavyotumbukiza wanawake kwenye ukatili wa kingono huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za mkutano ujao wa G-7, afya na uzalishaji. Mashinani tunakupeleka Port Sudan kusikiliza ujumbe kutoka mkuu wa operesheni za dharura za UNICEF nchini Sudan Jill Lawler. Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limewataka viongozi wa kundi la nchi saba tajiri zaidi duniani G-7 zitakazokutana siku chache zijazo nchini Japan kuendelea kudumisha ahadi yao ya mwaka 2022 ya kuhakikisha uhakika wa chakula duniani ukizingatia kwamba mwaka huu migogoro mipya ya Sudan, Haiti na Sahelinawatumbukiza watu wengi zaidi katika janga la njaa. Benini na Mali zimethibitishwa na kupongezwa leo na shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani kwa kufanikiwa kutokomeza ugonjwa wa vikope kama tatizo la afya ya umma. Hatua hiyo inazifanya Benin na Mali kuwa nchi za tano na sita katika kanda ya Afrika kufikia hatua hiyo. Zingine zilizofanikiwa kutokomeza ugonjwa huo Afrika ni Ghana, Gambia, Togo na Malawi. Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedross Ghebreyesus amesema “Kwa mafanikio hayo ya Benin na Mali sasa zimesalia nchi 23 Afrika na kutusogeza karibu katika kutimiza lengo la kuutokomeza kabisa ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.Na kamati ya biashara na maendeleo ya Umohja wa Mataifa UNCTAD leo imeanza uzinduzi wa ngazi ya juu wa tathimini ya pengo la uwezo wa uzalishaji wa kitaifa (NPCGA) na mpango wa kuendeleza uwezo wa uzalishaji nchini Kenya.Katika mashinani leo fursa ni yake mkuu wa operesheni za dharura za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF nchini Sudan Jill Lawler, akizungumzia shehena ya pili ya msaada wa shirika hilo iliyowasili mwishoni mwa wiki kwa ajili ya waathirika wa vita.Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, Karibu!
16-5-2023 • 0
Ingawa kuna changamoto najitahidi kutunza familia yangu- Tsinduka
Hii leo ni siku ya kimataifa ya familia duniani ambapo maudhui ya mwaka huu ni mienendo ya makundi ya watu na familia wakati huu ambapo idadi ya watu inaongezeka ingawa kwa kiwango cha chini. Umoja wa Mataifa unasema kupungua kwa idadi ya wanafamilia hutoa fursa ya familia kupatia huduma bora zaidi watoto, mathalani elimu na afya.Lakini ni ndivyo sivyo kwa familia moja huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako pamoja na baba na mama kuhaha kupatia mahitaji familia yao, waasi wanaleta changamoto kwani hata mazao shambani yanavunwa na waasi badala ya kunufaisha familia. Je nini kinafanyika? George Musubao amefika kwenye kaya hiyo.
15-5-2023 • 0
WHO imetoa onyo kwamba matumizi ya vikoleza utamu visivyo sukari hayapunguzi uzito
Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, hii leo limetoa mwongozo unaoshauri watu wasitumie vikoleza utamu visivyo sukari halisia (NSS) kwa lengo la kupunguza uzito na kuepusha magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs.Taarifa ya WHO iliyotolewa leo Geneva, Uswisi inasema mwongozo huo unafuatia mapitio ya ushahidi unaodokeza kwamba kutumia sukari isiyo halisia kwa ajili ya kupunguza uzito hauna manufaa ya muda mrefu katika kupunguza mafuta mwilini miongoni mwa watoto na watu wazima. Sukari hizo zisizo halisia na ambazo zinatumika ni pamoja na aspartame, advantame, cyclamates, neotame, saccharin, sucralose na stevia. Kitu kibaya zaidi ambacho mapitio hayo yamebaini ni kwamba sukari hizo zisizo halisia zinaongeza hatari ya kupata uognjwa wa kisukari aina ya 2, magonjwa ya moyo na vifo miongoni mwa watu wazima. Mkurugenzi wa WHO Idara ya Lishe na Usalama wa Chakula Dkt. Francesco Branca amesema kuacha kutumia sukari ya kawaida na badala yake kutumia sukari zisizo halisia kwa muda mrefu hakusaidii kupunguza uzito. Amesema “watu wanapaswa kufikiria njia mbadala za kupunguza matumizi ya sukari kwa kula vyakula vyenye sukari ya asili kama vile matunda au vinywaji na vyakula visivyo na sukari.” Amesema “vikoleza utamu visivyo na sukari havina lishe yoyote. Watu wapunguze vyakula vitamu kwenye mlo wao tangu utotoni ili kuimarisha afya zao.” WHO inasema pendekezo hilo linahusu watu wote isipokuwa wale wanaougua kisukari.
15-5-2023 • 0
Kiliniki za UNICEF zinazotembea msaada kwa waathirika wa kimbunga Freddy nchini Malawi
Wananchi wa Malawi walioathirika na Kimbunga Freddy wamepongeza mbinu ya kutumia kilniki za kuhama kwa njia ya magari iliyotumiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kuwahudumia wanawake na watoto nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kilicholipiga eneo hilo takribani miezi mwili iliyopita.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) linasema kimbunga Freddy kilichotokea kati ya Februari 5 na Machi 14 kiliwaacha watoto wa Malawi milioni 2.9 hatarini na katika uhitaji mkubwa wa msaada wa kibinadamu. Na katika msingi huo bado UNICEF inawaomba wahisani duniani kote kuichangia dola za Marekani milioni 52.4 kupitia ombi la Hatua ya Kibinadamu kwa ajili ya kufanikisha kutoa msaada wa kuokoa maisha ya watoto na wanawake nchini Malawi, ikiwa ni pamoja na wale walioathiriwa na Kimbunga Freddy hicho. Hata hivyo UNICEF katika hali hiyo hiyo ya uhaba wa ufadhili bado ilifanikiwa kutoa msaada kwa watu walioalazimika kuishi kwenye makambi baada ya kimbunga hicho. Mary Kwatani ni mmoja wao, “Nilikuja kambini kwa sababu nilipoteza nyumba yangu kutokana na mafuriko. Nilikuja hapa kutafuta makazi kwa sababu afya ya watoto wangu ilikuwa mbaya kutokana na lishe duni.” Kwa haraka UNICEF ilichukua hatua ikaleta kiliniki za kwenye magari ili kuleta huduma tiba kwa ajili ya, wajawazito na wanaonyesha na watoto chini ya umri wa miaka mitano. Mary Kwatani ni mnufaika anasema, "Kiliniki hizi zinazotembea zimekuwa msaada kwangu kwa sababu nilikuwa nasafiri umbali mrefu kufika hospitalini lakini sasa wahudumu wa afya wanaweza kutufikia kupitia kiliniki zinazohama." Kimbunga Freddy ambacho kilizipiga nchi kadhaa kusini mwa Afrika, kwa Malawi kiliathiri moja kwa moja wilaya 15 zilizopo kusini mwa nchi ya Malawi na kuathiri maisha ya watu na makazi.
15-5-2023 • 0
15 MEI 2023
Hii leo jaridani tuanaangazi ripoti ya WHO ya vikoleza utamu visivyo sukari halisia, na huduma za afya zizazotolewa nchini Malawai kupitia kilniki za kuhama kwa njia ya magari. Makala tunakupeleka nchini DRC na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, hii leo limetoa mwongozo unaoshauri watu wasitumie vikoleza utamu visivyo sukari halisia (NSS) kwa lengo la kupunguza uzito na kuepusha magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs. Wananchi wa Malawi walioathirika na Kimbunga Freddy wamepongeza mbinu ya kutumia kilniki za kuhama kwa njia ya magari iliyotumiwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kuwahudumia wanawake na watoto nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kilicholipiga eneo hilo takribani miezi mwili iliyopita.Katika Mkala, leo ikiwa ni siku ya familia duniani nakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mwandishi wetu George Musubao amemulika ni vipi familia inajitahidi kukidhi mahitaji licha ya changamoto za usalama.Katika mashinani na tutaelekea nchini Tanzania kusikiliza jinsi ambavyo hakikisho la maji safi na salama linavyokuza nidhamu na kuboresha usafi shuleni.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
15-5-2023 • 0
UN na wadau waimarisha usaidizi kwa waathirika wa mafuriko huko Kalehe, DRC
Ni takribani wiki moja tangu eneo la Kalehe lililoko jimbo la Kivu Kusini nchini DRC, likumbwe na mafuriko kufuatia kuongezeka kwa kina cha maji katika mito kulikosababishwa na mvua kubwa. Serikali ya DRC na mashirika yasiyo ya kiserikali yametuma wajumbe mbalimbali papo hapo kwenda kufanya uchunguzi ili kutoa misaada ya kibinadamu kwa wahanga. Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini DRC George Musubao amezungumza kwa njia ya simu na Yvon Edoumou ambaye ni msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA nchini humo ili kufahamu hali inaendeleaje.
12-5-2023 • 0
Khadija Khalid Ismail na Ebenezer Suleiman Mathew kuwawakilisha vijana wa Tanzania katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Mwezi Septemba mwaka huu wakuu wa serikali na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kama ilivyo ada ya kila mwaka watakutana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kujadili masuala mbalimbali ya Ulimwengu. Wakati wa mkutano huu wa juu kabisa katika Diplomasia ya Umoja wa Mataifa, vijana pia hushiriki katika mikutano ya kando ili kuchangia mawazo yao katika mstakabali wa ulimwengu. Vijana wawili kutoka Tanzania Khadija Khalid Ismail na Ebenezer Suleiman Mathew watawakilisha vijana wenzao wakati wa Baraza hili. Ili kufahamu mipango yao, Stell Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa, UNIC, jijini Dar es salaam nchini Tanzania amezungumza na mmoja wao.
12-5-2023 • 0
TANBAT 6, Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wapokea pongezi kutoka JWTZ na MINUSCA
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha 6 cha kutoka Tanzania TANBAT 06 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) wamepokea ugeni na salamu kutoka Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia ujumbe uliongozwa na Brigedia Jenerali George Mwita Itang’are aliyewakilisha salamu za Mkuu wa Majeshi ya Tanzania kutokana na sifa nzuri anazozipokea kutoka MINUSCA kuhusu kikosi hicho. Kutoka mjini Berbérati mkoani Mambéré-Kadéï, Afisa Habari wa TANBAT 06 Kapteni Mwijage Inyoma ameshiriki mapokezi ya ugeni huo, anaripoti. Kwanza ni gwaride la ukaguzi…na kisha baadaye ukumbini ni nyimbo za morali. Brigedia Jenerali Itangare katika ziara hii aliyoambatana na Brigedia Jenerali Robert William Mtafungwa ambaye ni Mwambata Jeshi katika Uwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa akizungumza na maafisa na askari walinda amani baada ya ziara yake ya kutembea kikosi hicho amesema kuwa lengo la ziara ya ujumbe huo ni kuangalia utayari wa kikosi lakini pia kuwapongeza kwa kazi nzuri na utayari pale wanapopewa jukumu. Aidha Brigedia Jenerali Itang’are amewataka walinda amani hao kuzingatia maadili ili wasiuchafue Umoja wa Mataifa, Jeshi la Tanzania na taifa lao. Kwa upande wake Mkuu wa TANBAT 06 Luteni Kanali Amini Stephen Mshana ameshukuru Jeshi la Tanzania kufanya ziara ya kutembelea kikosi hicho nchini CAR lakini pia akawakumbusha askari yaliyozungumzwa amehahidi kuendeleza mafanikio waliyoyaona ikiwemo kutekeleza maelekezo ambayo wameyapokea.
12-5-2023 • 0
12 MEI 2023
Jaridani hii leo tunakuletea mahojiano kuhusu masuala ya vijana, na pi tunaangazia kazi ya walinda amani TANBAT 6 nchini DRC. Makala tunaangazia maafuriko Kalehe nchini DRC, na mashinani tunaakuletea ujumbe kuhusu watoto wanaozaliwa njiti.Mwezi Septemba mwaka huu wakuu wa serikali na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kama ilivyo ada ya kila mwaka watakutana katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kujadili masuala mbalimbali ya Ulimwengu. Walinda amani wa Umoja wa Mataifa Kikosi cha 6 cha kutoka Tanzania TANBAT 06 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) wamepokea ugeni na salamu kutoka Jeshi la Ulinzi wa Wananchi Tanzania (JWTZ) kupitia ujumbe uliongozwa na Brigedia Jenerali George Mwita Itang’are aliyewakilisha salamu za Mkuu wa Majeshi ya Tanzania kutokana na sifa nzuri anazozipokea kutoka MINUSCA kuhusu kikosi hicho.Katika Mkala, George Musubao mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa huko nchini Jamhuri akizungumza na msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA nchini humo, Yvon Edoumou kuhusu mafuriko ya maji yaliyokumba eneo la Kalehe jimboni Kivu Kusini hivi karibuni.Katika masshinani tutasikia ujumbe wa Muuguzi, ambaye alilazimika kuacha kazi yake kwa muda ili aweze kuwalea watoto wake ambao walizaliwa njiti.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
12-5-2023 • 0
Jifunze Kiswahili: Ufafanuzi wa neno "KONGO"
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo tunapata ufafanuzi wa neno "KONGO" kutoka kwa mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.
11-5-2023 • 0
11 MEI 2023
Jaridani hii leo tunakuletea mada kwa kina ikimulika harakati za shirika moja la kiraia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC za kuitikia wito wa Umoja wa Mataifa wa kuona mitandao ya kidijitali inatumika kuimarisha afya hasa ya wajawazito na watoto. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Sudan na Afghanistan, na changamoto za utoaji wa msaada wa chakula katika eneo la Palestina. Katika jifunze Kiswahili hii leo tuko Tanzania kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kupata ufafanuzi wa neno"KONGO"Baraza Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa leo linafanya kikao maalum kushughulikia athari za vita inayoendelea nchini Sudan dhidi ya haki za binadamu. Katika taarifa yake kwenye kikao hicho Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa amesema mapigano hayo "yanaitumbukiza nchi hiyo yenye mateso mengi katika janga kubwa".Tukisalia na masuala ya haki za binadamu, Wataalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wameeleza kusikitishwa kwao na tangazo la hivi karibuni la Mahakama ya juu zaidi nchini Afghanistan la kuidhinisha matumizi ya adhabu ikiwa ni pamoja na kupigwa mawe, kuchapwa viboko na kuzikwa chini ya ukuta.Na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP limetangaza leo kwamba kufikia mwezi ujao watu 200,000 sawa na asilimia 60 ya watu wanaosaidiwa na shirika hilo katika eneo linalokaliwa la Palestina hawatapokea tena msaada wa chakula kutokana na ukata unaolikabili shirika hilo.Katika jifunze Kiswahili hii leo tuko Tanzania kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kupata ufafanuzi wa neno"KONGO".Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
11-5-2023 • 0
Jamii msimkatae msichana akipata ujauzito bila kutarajia. Si mwisho wa maisha - Ashley Toto
Ripoti iliyopewa jina Kuzaliwa kabla ya wakati: muongo wa hatua dhidi ya kuzaliwa kabla ya wakati, iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) pamoja na PMNCH ambao ni Ushirikiano wa mkubwa zaidi unaoangazia Afya ya Mama, watoto na vijana inaeleza kwamba mwaka 2020 takriban watoto milioni 13.4 duniani walizaliwa kabla ya wakati yaani njiti, huku karibu milioni 1 kati yao wakifariki kutokana na matatizo yanayotokana na hali hiyo ya kuzaliwa kabla ya wakati. Aidha miongoni mwa sababu zinazotajwa na ripoti hiyo kuwa zinachangia kwa kiasi kikubwa watoto kuzaliwa njiti ni pamoja na mimba za utotoni na shinikizo kubwa la damu wakati wa ujauzito (pre-eclampsia). Katika muktadha huo Anold Kayanda anatupeleka nchini Kenya kumwangazia mama mwenye umri mdogo Ashley Toto akieleza changamoto alizozipitia kutokana na kujifungua mtoto njiti.
10-5-2023 • 0
10 MEI 2023
Jaridani hii leo tunaangazia machafuko nchini Sudan na hali ya wakimbizi wa ndani na wale wanaosaka hifadhi katika nchi jirani. Makala tunaangazia afya ya uzazi na watoto wanaozaliwa njiti na mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Takriban watu milioni 2 hadi milioni 2.5 wanatarajiwa kutumbukia kwenye janga la njaa nchini Sudan katika miezi michache ijayo kwa sababu ya vita inayoendelea nchini humo limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP.Nchini Chad, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeanza kazi ya kusajili wakimbizi walioingia nchini humo kutoka Sudan kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF kwenye mji mkuu wa taifa hilo Khartoum. Wakimbizi sasa pamoja na kusajiliwa wanapatiwa mahitaji muhimu.Makala tunaangazia Ripoti mpya iliyotolewa hii leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na PMNCH ambao ni Ushirikiano wa mkubwa zaidi unaoangazia Afya ya Mama, watoto na vijana kuhusu Kuzaliwa kabla ya wakati inazitaja sababu kama vile mimba za utotoni na shinikizo kubwa la damu wakati wa ujauzito (pre-eclampsia), kuhusika kwa karibu na watoto kuzaliwa njiti.Mashinani tutakupeleka nchini Tanzania ambapo mwanaharakati wa wasichana anatoa ujumbe kuhusu changamoto ambazo wasichana wanazipitia.Mwenyeji wako ni Assumta Massoi, Karibu!
10-5-2023 • 0
Takriban wakimbizi 30,000 kutoka Sudan wasajiliwa Chad- UNHCR
Nchini Chad, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeanza kazi ya kusajili wakimbizi walioingia nchini humo kutoka Sudan kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF kwenye mji mkuu wa taifa hilo Khartoum. Wakimbizi sasa pamoja na kusajiliwa wanapatiwa mahitaji muhimu. Ving’ora! purukushani za hapa na pale! Wanawake wanaume na watoto wakipita huku na kule! Ni harakati zenye ahueni miongoni mwa wakimbizi 30,000 kutoka Sudan ambao wameona nuru baada ya kufika hapa Midjilita, jimbo la OUADDAÏ nchini Chad. Wakimbizi hawa wako hoi na miongoni mwao ni Raouda Abdallah Jaffar akiwa amebeba mtoto mmoja huku wengine wakiambatana naye! Wanajongea kwenye dawati la usajili lililoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR. Baada ya usajili, Raoud anasema, “ nimesajiliwa leo na UNHCR. Nahitaji sasa matandiko, blanketi, chakula na mahitaji mengine.” Usajili ukikamilika, wakimbizi wanaelekea sehemu ya kupatiwa vifaa muhimu kama alivyosema Raoud. Mmoja baada ya mwingine anapatiwa matandiko, vifaa vya jikoni na kadha wa kadha. Huku wakimbizi wakisajiliwa na kupatiwa vifaa vya msaada, kwingineko hapa ujenzi unaendelea wa makazi ya wakimbizi sambamba na vyoo ili kuhakikisha huduma za kujisafi na usafi zinapatikana. Jerome Sebastien Naibu Mwakilishi wa UNHCR nchini Chad anasema iwapo mzozo Sudan utaendelea kuna uwezekano wa Chad kupokea hadi wakimbizi 100,000 (Laki Moja) na mahitaji ya fedha kwa ajili ya kufanikisha operesheni za usaidizi yanaweza kufikia dola milioni 130. Hivyo ametoa ombi kwa jamii ya kimataifa kusaidia Chad na mashirika ya kiutu yanayoshiriki katika harakati za kusaidia wakimbizi. Amesema “ni wakati huu tunahitaji uhamasishaji wa fedha ili tuweze kuwahamishia wakimbizi hawa maeneo ya ndani zaidi kwa ajili ya usalama na pia wapate usaidizi makini.”
10-5-2023 • 0
Takriban watu milioni 2.5 wako hatarini kukabiliwa na njaa Sudan: WFP
Takriban watu milioni 2 hadi milioni 2.5 wanatarajiwa kutumbukia kwenye janga la njaa nchini Sudan katika miezi michache ijayo kwa sababu ya vita inayoendelea nchini humo limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP.Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo iliyotolewa mjini Roma Italia na Port Sudan , hii itafanya hali mbaya ya kutokuwa na uhakika wa chakula Sudan kufikia rekodi ya juu kabisa huku kukiwa na watu milioni 19 ambao ni theluthi mbili ya watu wote nchini humo wakiwa wameathirika.Majimbo yanayotarajiwa kuathirika zaidi ni Darfur Magharibi, Kordofan Magharibi, Blue Nile, Red Sea na Darfur Kaskazini.Shirika hilo la mpango wa chakula linasema bei ya chakula imeongezeka mara dufu nchi nzima na sasa bei ya kikapu kimoja cha chakula kitatazamiwa kupanda kwa asilimia 25 katika miezi mitatu hadi sita ijayo.Kutokana na mapigano yanayoendelea wakulima wengi inasema WFP hawawezi Kwenda mashambani mwao kupanda katika msimu wa mvua kati ya Mei na Julai hali ambayo itapandisha hata zaidi bei za vyakula.Shirika hilo baada ya kusitisha kwa muda operesheni zake sasa imerejea kugawa msaada wa kuokoa Maisha na wiki iliyopita pekee imewafikia watu 35,000, lengo likiwa kuwafikia watu 384,000 walioathirika na mapigano mapya, wakimbizi wa zamani, wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi katika majimbo ya Gedaref, Gezira, Kassala na White NileKatika miezi ijayo WFP pia itaongeza operesheni zake ili kuwasaidia watu milioni 4.9 katika maeneo ambayo usalama unaruhusu, ikiwa ni Pamoja na kuzuia na kutibu utapiamlo kwa Watoto 600,000 wa chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wanaonyonyesha.Pia WFP ikishirikiana na wadau wengine likiwemo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na la kuhudumia Watoto UNICEF inasaidia nchi jirani ambako watu wanakimbilia kwa msaada wa chakula na maji ikiwemo Chad, Sudan Kusini, Misri na Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.
10-5-2023 • 0
09 MEI 2023
Jaridani hii leo tunakuletea mada kwa kina ikimulika jitihada za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuendeleza lugha ya Kiswahili kimataifa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo machafuko nchini Sudan, uzazi salama na masuala ya afya . Mashinani tunakupeleka nchini Ethiopia.Idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan waliotawanywa na machafuko mapya ynayoendelea imeongezeka zaidi ya mara mbili wiki iliyopita na sasa kufikia watu 700,000 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO, leo limezindua ripoti mpya inayoelezea hatua zilizopigwa kuhusu kuokoa maisha wakati wa kujifungua, na vifo vya watoto wachanga.Katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Baraza kuu kunafanyika mkutano wa siku mbili wa ulioandaliwa kwa pamoja na Baraza Kuu la umoja wa Mataifa na WHO, ukiwaleta pamoja wadau mbalimbai kuzungumzia masuala muhimu ya afya ikiwemo na huduma za afya kwa wote.Mashinani tutaelekea Tigray nchini Ethiopia kushuhudia kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua na harakati za kusaidia watoto ambao wako hatarini kuathirika na utapiamlo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
9-5-2023 • 0
Wahudumu wa afya wa vijiji Uganda wapambana na malaria kwa msaada wa UNICEF.
Malaria ni moja ya magonjwa hatari zaidi duniani ikielezwa na ripoiti ya mwaka 2022 ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kuwa ilikatili maisha ya watu 619,000 duniani kote mwaka 2021 na waliougua ugonjwa huo kufikia milioni 247.Shirika hilo linasema asilimia kubwa ya vifo na wagonjwa wako barani Afrika hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara. Uganda ni moja ya mataifa yaliyoathirika na ugonjwa huo na wahanga wakubwa ni watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano. Kwa kulitambua hilo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau limeanzisha program ya kuziwezesha timu za wahudumu wa afya wa vijijini VHT kushiriki katika vita dhidi ya malaria ikiwemo kwenye wilaya ya Ntungamo. Je wanafanya nini na program hiyo ina tija gani? Ungana na Selina Jerobon katika Makala hii kwa undani zaidi.
8-5-2023 • 0
UNAIDS: Ili kutokomeza ukimwi ifikapo 2030 kila mtu lazima ajumuishwe hata watumia mihadarati
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na vita dhidi ya ukimwi UNAIDS limesema ili kuhakikisha ukimwi unatokomezwa ifikapo mwaka 2030 basi kila mtu anapaswa kujumuishwa katika vita hivyo ikiwemo wafungwa na wanaotumia mihadarati, kwani Mifumo mingi ya magereza inajitahidi kukabiliana na msongamano, rasilimali duni, ufikiaji mdogo wa huduma za afya na huduma zingine za msingi, vurugu na matumizi ya dawa za kulevya.Nchini Moldova, gereza namba 16 la Pruncul moja ya magereza ambako UNAIDS inashirikiana na serikali na mamlaka za afya kuhakikisha wafungwa na hasa wanaotumia mihadarati wanapata huduma za kudhibiti virusi vya ukimwi au VVU na kukabiliana na athari za matumizi ya mihadarati.Shirika hilo linasema mwaka 2021, idadi ya wafungwa magerezani duniani kote iliongezeka kwa asilimia 24 ikilinganishwa na mwaka wa 2020 hadi kufikia zaidi ya watu milioni 10.Kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya Umoja wa Mataifa ya dawa za kulevya na uhalifu UNODC katika baadhi ya nchi hadi asilimia 50 ya watu walio gerezani hutumia au hujidunga dawa za kulevya ambayo ni moja ya sababu kubwa ya maambukizi ya magonjwa yatokanayo na damu kama vile VVU na hepatitis C.Moldova ni miongoni mwa nchi zilizathirika na matatizo haya kwani tangu mwaka2000, ni magereza machache tu nchini humo yaliyokuwa yakitoa huduma za kupunguza madhara. Lakini sasa kwa msaada wa UNAIDS magereza yote 17 yana huduma na mfungwa yeyote mpya katika jela za nchi hiyo anawajibika kumuona daktari wa magonjwa ya akili, na daktari wa kawaida kwa vipimo na ikihitajika basi anajumuishwa katika mpango wa matibabu.Mfungwa Alexander Godin ni miongoni mwa waathirika anapitia katika milango kadhaa iliyofungwa katika gereza namba hili huku akisindikizwa na mlinzi hadi kwenye duka la dawa gerezani hapo. Hii ni sehemu ya utaratibu wake wa kila siku. Anakuja kuchukua dawa yake ya maji ya methadone baada ya kuacha uraibu wa dawa za kulevya, "Nimekuwa kwenye matibabu mbadala ya methadone kwa miaka 10. Familia yangu ilifanya uamuzi huu. Kabla ya hapo, nilitumia dawa za kulevya, afuni. Kwa hili, pesa zilihitajika, na hapo ndipo shida zilianza katika familia. Familia ilipendekeza niende kujiorodhesha kwenye zahanati inayotoa matibabu na tangu hapo nimekuwa kwenye mpango huo.” Methadone ni tiba inayosaidia watu kukabiliana na dalili za athari za mihadarati, msongo wa mawazo, kupunguza utegemezi wa heroini na kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwenye sindano zenye maambukizi.Maria Potrimba, mkuu, idara ya magonjwa ya kuambukiza, Gereza hapa anasema "Ikiwa mgonjwa yuko kwenye matibabu haya mbadala, anafahamu zaidi kuhusu athari na anazingatia zaidi matibabu yake."Maambukizi ya VVU ni asilimia 11 kati ya watu wanaojidunga dawa za kulevya nchini Moldova ambao ni zaidi ya asilimia 0.36 ya watu wote. Na ni moja ya makundi yaliyoathirika zaidi nchini humo.Svetlana Plamadeala, ni mkurugenzi wa UNAIDS nchini Moldova amasema, "Nchini Moldova mzigo wa VVU ni mkubwa zaidi miongoni mwa makundi muhimu na pia huathiri wafungwa. Ofisi UNAIDS nchini humu iliunga mkono serikali kufanya majaribio ya programu za kupunguza madhara na matibabu ya mbadala wa afyuni magerezani tangu mapema mwaka wa 2000. Leo tunasherehekea ukweli kwamba tumepanua wigo wa huduma hizo kutoka kwenye mradi wa majaribio hadi kwenye mfumo mzima wa magereza au kila gereza lina huduma hizo. Ni katika kutoa kipaumbele kwa watu na pia ni kuhusu mtazamo wa afya ya umma.”UNAIDS, na washirika wengine wa Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu wamekuwa wakiunga mkono kupanua huduma hizi kwenye magereza yote.Kwa sasa, kulingana na Harm Reduction International, ni nchi 59 pekee duniani ndio zinazotoa huduma hizo katika magereza yake.
8-5-2023 • 0
Makao Makuu ya UM: Jukwaa la 18 la Umoja wa Mataifa la misitu limeng’oa nanga leo
Jukwaa la 18 la Umoja wa Mataifa la misitu limeanza leo kwenye makao Makuu ya Umoja huo mjini New York Marekani likiwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mfumo wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa na kikanda na wadau wa misitu ili kujadili thamani ya rasilimali hiyo muhimu kwa binadamu na mazingiraKwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO misitu ni chanzo kikubwa cha nishati, chakula na malisho, na hutoa riziki kwa mamilioni ya watu, ikiwa ni pamoja na wengi ambao ni maskini zaidi duniani.Watu bilioni 2.4 duniani bado wanatumia nishati inayotokana na kuni kupikia. Lakini misitu pia husaidia kupunguza mabadiliko ya tabianchi na kuboresha rutuba ya udongo, hewa na maji.Shirika hilo linasema ikisimamiwa kwa uendelevu, misitu pia ni chanzo cha malighafi inayoweza kurejelewa, na hivyo kutoa mchango muhimu katika mzunguko wa ujenzi wa uchumi.Jukwaa hili lililoandaliwa na idara ya masuala ya kiuchumi na kijamii ya Umoja wa Mataidfa DESA linataka kila mtu duniani afahamu mambo matano muhimu kuhusu misitu ambayo ni mosi misitu inachukua asilimia 31 ya eneo la dunia,ina asilimia 80 ya bayoanuai ya dunia na inahifadhi hewa ukaa kiasi kikubwa zaidi ya kilichopo hewani.Pili, misitu inasaidia ustawi na maisha ya viumbe duniani, kwani watu zaidi ya bilioni 1.6 wanategemea mistu ili kuishi, kuendesha Maisha yao, ajira na kipato na Afrika takriban watu bilioni 2 na kaya theluthi mbili bado wanategemea misitu kwa kuni kama nishati ya kupikiaTatu misitu yenye afya inasaidia afya ya watu kwani misitu na miti inatoa hewa safi na maji na maji ni Uhai bila kujali mtu anakoishi.Nne misitu inaendelea kuwa hatarini kila mwaka dunia inapoteza ekati milioni 10 za misitu sababu ya uktaji haramu wa magogo, moto wa nyika, uchafuzi wa mazingira, magonjwa, wadudu na athari za mabadiliko ya tabianchi.Na tano kurejesha misitu ni ufunguo wa kuwa na mustakbali endelevu na kurejesha ardhi iliyomomonyoka kutasaidia kufikia malengo ya maendeleo endelevu hasa ya kuongeza eneo la mistu duniani kwa asilimia 3 ifikapo mwaka 2030.Kongamano hilo la siku 5 litakunja jamvi Ijumaa Mei 12
8-5-2023 • 0
08 MEI 2023
Hii leo jaridani tanaangazia Jukwaa la Umoja wa Mataifa la misitu linaloendelea hapa makao makuu, vita dhidi ya ukimwi Moldova. Makala tunakupeleka nchini Uganda na Mashinani nchini Rwanda, kulikoni?Jukwaa la 18 la Umoja wa Mataifa la misitu limeanza leo kwenye makao Makuu ya Umoja huo mjini New York Marekani likiwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, mfumo wa Umoja wa Mataifa, mashirika ya kimataifa na kikanda na wadau wa misitu ili kujadili thamani ya rasilimali hiyo muhimu kwa binadamu na mazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na vita dhidi ya ukimwi UNAIDS limesema ili kuhakikisha ukimwi unatokomezwa ifikapo mwaka 2030 basi kila mtu anapaswa kujumuishwa katika vita hiyo ikiwemo wafungwa na wanaotumia mihadarati, kwani mifumo mingi ya magereza inajitahidi kukabiliana na msongamano, rasilimali duni, ufikiaji mdogo wa huduma za afya na huduma zingine za msingi, vurugu na matumizi ya dawa za kulevya.Makala inatupeleka Uganda kumulika juhudi zinazofanywa na shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kupambana na malaria.Mashinani tutaeleke nchini Rwanda kumsikia mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa ana matumaini baada ya kupokea msaada wa kibinadamu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
8-5-2023 • 0
Makala: Mchoro wa Ashraf Kuku waibuka kidedea kwenye “Amani Yaanza Nami”
Kwa wiki nne katika Chuo Kikuu cha Juba nchini Sudan Kusini, kulifanyika mashindano ya sanaa yakihusisha wanafunzi 20 kutoka chuo hicho. Maudhui yalikuwa ni Amani Yaanza Nami yakienda sambamba na miaka 75 ya operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa.Mashindano hayo yaliandaliwa kwa pamoja kati ya Chuo Kikuu Juba na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS. Washindi watatu, kazi zao za sanaa zitawekwa kwenye lango la ofisi ya Mkuu wa Operesheni za Ulinzi wa Amani za Umoja wa Mataifa Pierre Lacroix, iliyoko makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Je nani aliibuka mshindi? Ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.
5-5-2023 • 0
05 MEI 2023
Jaridani leo tunaangazia siku ya urithi duniani hasa barani Afrika na wakimbizi wa Sudan. Makala tunakupeleka nchini Sudan Kusini na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa leo ni siku ya uruthi wa dunia wa Afrika, shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO linasema urithi huo ambao thamani yake ya kipekee inaadhimisha leo, bado haujatambuliwa kulingana na umuhimu wake wa kihistoria, wa kibinadamu na wa asili. Maelfu ya watu wamevuka na kuingia Sudan Kusini wakikimbia mzozo unaoendelea nchini Sudan. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) liko linawasaidia wanaowasili lakini mzigo huu wa ziada unaweka shinikizo katika shughuli za shirika hilo ambazo tayari ziko katika hali mbaya ya ufadhili.Makala tutakupeleka nchini Sudan Kusini ambapo katika Chuo Kikuu cha Juba nchini Sudan Kusini, kulifanyika mashindano ya sanaa yakihusisha wanafunzi 20 kutoka chuo hicho. Maudhui yalikuwa ni Amani Yaanza Nami yakienda sambamba na miaka 75 ya operesheni za ulinzi wa amani kwenye Umoja wa Mataifa.Na katika mashinani na tutakupeleka Kasulu mkoani Kigoma nchini Tanzania kusikia ujumbe wa mwanafunzi wa shule kuhusu haki ya maji safi na salama.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
5-5-2023 • 0
Watu wanaoikimbia Sudan kuingia Sudan Kusini waendelea kupata msaada wa kibinadamu: WFP
Maelfu ya watu wamevuka na kuingia Sudan Kusini wakikimbia mzozo unaoendelea nchini Sudan. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) liko linawasaidia wanaowasili lakini mzigo huu wa ziada unaweka shinikizo katika shughuli za shirika hilo ambazo tayari ziko katika hali mbaya ya ufadhili.Video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) inatupeleka katika Kaunti ya Renk iliyoko kaskazinimashariki mwa nchi ya Sudan Kusini inakopakana na Sudan. Hapa ni kila mtu anajaribu kukumbatia kile alichofanikiwa kutoroka nacho akikwepa mabaya ambayo yangemkumba ikiwa angesalia Sudan ambako tangu tarehe 15 mwezi jana Aprili kunafukuta mapigano makali. Wanaobahatika wanabebwa na magari ya Umoja wa Mataifa, wengine punda na wengine wametembea mwendo mrefu kufika hapa. Kwa mujibu wa WFP, zaidi ya watu 30,000 hadi sasa wamevuka mpaka kutoka Sudan na kuingia Sudan Kusini. Wengi wao ni waliorejea kwani walikimbia madhila hapa Sudan Kusini lakini nako ugenini Sudan kumechafuka, wamerejea. Naimat Khamis, ni mmoja wa waliorejea anasema, "Tulilazimika kuja hapa kwa sababu ya mapigano ya Khartoum…tulilazimika kukimbia haraka iwezekanavyo kwa sababu ya vita…ilikuwa safari ngumu…tunataka kubaki na jamaa zetu hapa kwa sababu tumeteseka sana.” Hassan Abdallaziz, kijana mwenye umri wa miaka 17 huyu yeye ni raia wa Sudan kwa hiyo kwa Sudan Kusini yuko ukimbizi anasema, “Hali ya nchi ilinilazimu kuja hapa. Hakuna kitu kizuri kilichobaki nchini, hakuna kazi, ni machafuko. Mtu yeyote anaweza kupora mali yako, ni kama msitu." WFP tayari inawasaidia waliowasili na wanaowasili ikiwa ni pamoja na kuwapa chakula, kuwapima watoto, wajawazito na wanaonyonyesha, lakini mzigo huu wa ziada unaongeza chumvi kwenye kidonda. Mary-Ellen McGroarty ni Mkurugenzi wa WFP nchini Sudan Kusini akiwa mjini Juba anasema, "Mgogoro huu umekuja katika wakati mbaya zaidi. Unajua nchini Sudan Kusini tunaingia katika msimu wa muambo na msimu wa mvua. Tayari tuna watu milioni 7.4 wanaohitaji msaada wa chakula. Hatuwezi kuwafikia wote kwa sababu ya changamoto za rasilimali. Tumelazimika kupunguza programu zetu kwa sababu ya vikwazo vikali vya ufadhili. Na sasa tena tunalazimika kuweka vipaumbele upya kati ya watu wenye njaa, hawa wapya wanaowasili, ambao wako hatarini sana.”
5-5-2023 • 0
UNESCO: Urithi wa Kiafrika bado haujatambuliwa kulingana na umuhimu wake wa kihistoria
Ikiwa leo ni siku ya urithi wa dunia wa Afrika, shirika la elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO linasema urithi huo ambao thamani yake ya kipekee inaadhimisha leo, bado haujatambuliwa kulingana na umuhimu wake wa kihistoria, wa kibinadamu na wa asili.Kupitia ujumbe wake wa siku hii mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema baada ya kupitishwa mkataba wa urithi wa dunia miaka 50 iliyopita na kuanza kutekelezwa rasmi mwaka 1978, miongoni mwa maeneo 12 ya kwanza kuingizwa kwenye orodha ya urithi wa duniani matatu yalikuwa barani Afrika hii ikimaanisha kwamba robo ya maeneo ya awali yaliyochaguliwa yalikuwa barani huo.Hata hivyo amesema “Leo, hii, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara inachukua takriban moja ya kumi ya maeneo yote yaliyoorodheshwa ingawa thamani ya urithi wake wa kipekee, bado haijatambuliwa.Ili kukabiliana na hali hii, na kuupa heshima ipasavyo kutokana na fikra za binadamu na kazi za asili zinazopatikana barani Afrika, UNESCO imeliweka bara hili kuwa kitovu cha mkakati wake wa urithi wa dunia.”Mkuu huyo wa UNESCO amesisitiza kuwa kuna haja ya kufikiria upya utekelezaji wa mkataba wa urithi wa dunia ili kukabiliana na changamoto zitakaoukabili miaka mingine 50 ijayo na hatimaye kufanikisha msingi wa mkataba huo wa urithi wa kipekee kwa dunia nzima.Ameongeza kuwa “Ni kwa sababu ya upekee wake wa kina, utofauti wake na utajiri wake ndiyo maana urithi wa Kiafrika ni wa ulimwengu wote na unahitaji tuutilie maanani. Mifano ya urithi huu ni pamoja na misikiti minane ya mtindo wa Wasudan nchini Côte d'Ivoire ambayo iliingizwa kwenye orodha ya urithi wa dunia mwaka jana, mbuga ya taifa ya wanyama ya Ivindo Gabon ambayo inahifadhi wanyama wengi walio hatarini kutoweka wakiwemo tembo.”Azoulay amehitimisha ujumbe wake kwa ahadi kwamba “Ili kutambua vyema urithi huu wa Kiafrika na kuwezesha mchango wake kwa urithi wetu wa dunia, tutahakikisha kwamba kufikia mwaka wa 2025, mataifa yote ya Afrika yanayotaka kufanya hivyo yatakuwa yamewasilisha angalau ombi moja la kujumuishwa kwenye orodha ya urithi wa dunia kwa msaada wa kisayansi na kiufundi kutoka kwa Shirika la UNESCO.”Shirika hilo linasema “ingawa Afrika ina uwakilishi mdogo kwenye orodha ya urithi wa dunia mali za Kiafrika zinachukua takribani asilimia 12 ya maeneo yote yaliyoorodheshwa duniani, na asilimia 39 ya mali hizi ziko kwenye orodha ya urithi wa dunia ulio hatarini.”Ukikabiliwa na vitisho mbalimbali vya kisasa, mabadiliko ya tabianchi, maendeleo yasiyodhibitiwa, ujangili, machafuko ya kiraia na ukosefu wa utulivu, maajabu mengi ya urithi wa Afrika yana hatari ya kupoteza thamani yake bora ya ulimwengu.“Kwa hiyo ni suala la dharura zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwamba urithi huu usioweza kubadilishwa ulindwe na kuhifadhiwa kwa ajili ya kufurahiwa na vizazi vijavyo.”Siku hii huadhimishwa kila mwaka Mei 5 na UNESCO inasema ni fursa kwa watu kote duniani, na hasa Waafrika, kusherehekea urithi wa kipekee wa kitamaduni na wa asili wa bara hilo.
5-5-2023 • 0
04 MEI 2023
Tathmini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP, inaashiria kuwa fani ya mitindo huchangia asimilia kati ya 2 hadi 8 ya gesi ya ukaa kwenye mazingira.Shughuli ya kutia rangi vitambaa ina mchango mkubwa kwenye vyanzo vya uchafuzi wa mifumo ya maji kote ulimwenguni. Na ni kwa mantiki hiyo ,mwandishi wetu wa Nairobi, Kenya Thelma Mwadzaya amefuatilia harakati za kuepusha uchafuzi wa mazingira kwa kutumia nguo tena na tena huko nchini Kenya.
4-5-2023 • 0
Uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki zote za binadamu
Hii leo ikiwa ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani maudhui yakiwa Kuumba mustakabali wa Haki: Uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki zote za binadamu tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mwandishi wetu George Musubao amezungumza na waandishi wa habari kufahamu uzingatiaji wa maudhui ya siku hii halikadhalika kile ambacho wangependa kuona kinafanyika ili haki hiyo ya kupata habari iweze kuzingatiwa na hatimaye iwe kichocheo cha wananchi kupata haki zote.
3-5-2023 • 0
03 MAI 2023
Jaridani leo tunaangazia Siku ya Uhuru wa vyombo vy habari duniani na machafuko nchini Sudan.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari , waandishi wa habari watatu wanawake nchini Iran ambao kwa sasa wanatumikia kifungo wametangazwa kuwa washindi wa tuzo ya uhuru wa vyombo vya habari ya shirika la umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO/Guillermo Cano kufuatia mapendekezo ya jopo la majaji wa kimataifa wa tasnia ya habari. Hayo yakiendelea, msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA Jens Laerke amezungumza na waandishi wa habari huko Geneva Uswisi hii leo na kusema mashirika ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kiutu yanakabiliwa na pengo la dola bilioni 1.5 la kufanikisha operesheni zake Sudan wakati huu mahitaji yanaongezeka kutokana na mapigano yanayoendelea, maelfu ya watu wakifurushwa makwao.Katika makala George Musubao mwandishi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC anangumza na waandishi wa habari hii leo ikiwa ni siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari maudhui yakiwa Kuumba mustakabali wa Haki: Uhuru wa kujieleza kama kichocheo cha haki zote za binadamu.Na katika mashinani tutelekea nchini Sudan kupata ujumbe kuhusu changamoto zinazowakabili wanawake na wasichana nchini humo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
3-5-2023 • 0
Guillermo Cano: Waandishi wanawake watatu wa Iran wanaotumikia kifungo watwaa tuzo ya UNESCO
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari , waandishi wa habari watatu wanawake nchini Iran ambao kwa sasa wanatumikia kifungo wametangazwa kuwa washindi wa tuzo ya uhuru wa vyombo vya habari ya shirika la umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO/Guillermo Cano kufuatia mapendekezo ya jopo la majaji wa kimataifa wa tasnia ya habari. Washindi hao Niloofar Hamedi, Elaheh Mohammadi and Narges Mohammadi ushindi wao umetanmgzwa na Audrey Azouley mkurugenzi mkuu wa UNESCO katika hafla maalum iliyofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani."Sasa kuliko wakati mwingine wowote, ni muhimu kutoa pongezi kwa waandishi wa habari wanawake wote ambao wanazuiwa kufanya kazi zao na ambao wanakabiliwa na vitisho na mashambulizi dhidi ya usalama wao. Leo tunaenzi kujitolea kwao kwa dhati na uwajibikaji”.Naye alisema Zainab Salbi, mwenyekiti wa Baraza la Kimataifa la wanataaluma wa vyombo vya habari. Amesema "Tumejizatiti kuenzi kazi ya ujasiri ya waandishi wa habari wanawake wa Iran ambao kuripoti kwao kulisababisha mapinduzi ya kihistoria yaliyoongozwa na wanawake. Wamelipa gharama kubwa kwa kujitolea kwao kuripoti na kueleza ukweli. Na kwa ajili hiyo, tumedhamiria kuwaenzi na kuhakikisha sauti zao zitaendelea kusikika duniani kote hadi wawe salama na huru,” Niloofar Hamedi anaandikia gazeti la kila siku la Shargh la wanamageuzi. Alitangaza habari za kifo cha Masha Amini kufuatia kuzuiliwa kwake chini ya ulinzi wa polisi tarehe 16 Septemba 2022.Niloofar anashikiliwa kizuizini kwenye kifungo cha upweke katika Gereza la Evin la Iran tangu Septemba 2022.Elaheh Mohammadi anaandikia gazeti la wanamageuzi, Ham-Mihan, linaloangazia masuala ya kijamii na usawa wa kijinsia.Aliripoti kuhusu mazishi ya Masha Amini, naye pia amezuiliwa katika Gereza la Evin tangu Septemba 2022.Hapo awali alikuwa alipigwa marufuku kuripoti kwa mwaka mmoja mwaka 2020 kutokana na kazi yake.Niloofar Hamedi na Elaheh Mohammadi ni washindi wa pamoja wa tuzo ya kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2023, tuzo ya wanahabari ya Canada ya uhuru wa kujieleza (CJFE), na Tuzo ya Harvard ya Louis M. Lyons 2023 ya dhamiri na uadilifu katika uandishi wa Habari.Pia wametajwa kama wawili miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi zaidi wa Jarida la Time la mwaka 2023.Narges Mohammadi amefanya kazi kwa miaka mingi kama mwandishi wa habari wa magazeti mbalimbali na pia ni mwandishi na makamu mkurugenzi wa kituo cha asasi ya kiraia cha watetezi wa haki za binadamu (DHRC) chenye makao yake mjini Tehran.Kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 16 jela katika Gereza la Evin. Ameendelea kuripoti kwa maandishi kutoka gerezani, na pia amewahoji wafungwa wengine wanawake.Mahojiano haya yalijumuishwa katika kitabu chake "White Torture" mwaka 2022, alishinda tuzo ya ujasiri ya waandishi wasio na mipaka (RSF).Kwa mujibu wa UNESCO ulimwenguni kote, wanahabari wanawake na wafanyikazi wa vyombo vya habari wanakabiliwa na ongezeko la mashambulizi ya nje ya mtandao na mtandaoni na wanakabiliwa na vitisho maalum na visivyo vya kawaida.Unyanyasaji wa kijinsia wanaokabiliwa nao ni pamoja na unyanyapaa, kauli za chuki za kijinsia, kukandamizwa, kushambuliwa kimwili, ubakaji na hata mauaji. UNESCO inatetea usalama wa waandishi wa habari wanawake na inashirikiana na wadau wengine kutambua na kutekeleza mazoea mazuri na kushirikiana mapendekezo na pande zote zinazohusika katika kukabiliana na mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari wanawake, kama inavyotambuliwa na maazimio mengi ya Umoja wa Mataifa.UNESCO pia inashirikiana na mashirika maalumu kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa vyombo vya habari wanawake mashinani na kupitia kozi za mafunzo ya mtandaoni, na inafanya kazi na vikosi vya usalama ili kuwahamasisha kuhusu uhuru wa kujieleza kwa kuzingatia jinsia.
3-5-2023 • 0
UNICEF Ripoti: Ndoa za utotoni zimepungua lakini kasi ni ndogo mno
Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) imeeleza kwamba vitendo vya ndoa za utotoni vimeendelea kupungua duniani ingawa upunguzaji huo hauna kasi ya kutosha kufikia lengo la kutokomeza ndoa za utotoni ifikapo mwaka 2030 kama yalivyo Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu, SDGs.Kupitia ripoti hiyo ya UNICEF iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatano kwa saa za New York, Marekani, takwimu zinazoonesha kupungua kwa ndoa za utotoni duniani zimechangiwa zaidi na kupungua kwa vitendo hivyo nchini India nchi yenye watu wengi zaidi na ambayo imekuwa ikiukumbatia utamaduni huu. Pamoja na kupungua huko kwa vitendo vya kuozesha watoto, UNICEF inasema India inasalia kuwa na idadi kubwa zaidi duniani ya watoto wanaoolewa. Hata hivyo ripoti hiyo inaeleza kuwa ingawa baadhi ya maeneo ya dunia yameshudia kupungua kwa vitendo vya ndoa katika umri mdogo, mataifa mengine yamekwama hasa zaidi katika eneo la Afŕika Maghaŕibi na Kati, kanda inayotajwa kuwa yenye matukio mengi zaidi ya ndoa za utotoni. Nchi nyingi katika kanda hii, hasa zile za Sahel, zimekumbwa na migogoro inayoendelea ambayo inazidisha mazingira magumu kwa wasichana. Kanda nyingine yenye maendeleo madogo katika ndoa za watoto ni Amerika Kusini na Karibea. Katika eneo hili, mapungufu makubwa katika makundi ya kijamii na kiuchumi yanaonesha kuwa ndoa za utotoni ni suala lililokita mizizi miongoni mwa jamii maskini. Aidha ripoti hii imeeleza kwamba nchi nyingine zaidi ya India ambazo zimeonesha kupunguza ndoa za utotoni ingawa kwa miaka mingi zilishamiri kwa matukio haya ni Bangladesh na Ethiopia huku Rwanda na Maldives zikitajwa kuwa nchi ambazo tangu awali zimekuwa na matukio machache ya ndoa za utotoni na wanakaribia kuvitokomeza kabisa vitendo hivyo. Ingawa ripoti inasema kuwa licha ya maendeleo haya kiasi yaliyopatikana kimataifa kasi bado ni ndogo mno na ikiendelea hivi inaweza kuchukua miaka 300 hadi kutokomeza kabisa ndoa za utotoni, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell ana matumaini akisema, "Tumethibitisha kwamba maendeleo ya kukomesha ndoa za utotoni yanawezekana. Inahitaji msaada usioyumba kwa wasichana na familia zilizo katika mazingira hatarishi. Ni lazima kuzingatia kuwaweka wasichana shuleni na kuhakikisha wanapata fursa za kiuchumi."
3-5-2023 • 0
02 May 2023
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina na leo tunamulika juhudi za kumkwamua mjasiriamali hasa nchini Kenya. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ziara za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Qatar, haki za binadamu na misaada kutoka mashirika nchini Sudan. Katika mashinani na kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari hapo kesho, tunakuletea ujumbe wa Mwandishi wa Habari kutoka Uingereza kuhusu changamoto zinazowakumba waandishi wa habari.Mratibu Mkuu wa Umoja Mataifa kuhusu misaada ya dharura, Martin Griffiths ambaye yuko Kenya kusaka suluhu ya kufikisha misaada ya kiutu nchini Sudan, amemshukuru Rais William Ruto kwa uongozi na usaidizi wake kuona hatua za dharura za kiutu zinachukuliwa ili misaada ifikie nchini Sudan. Ametoa kauli hiyo baada ya Rais Ruto kuongoza mkutano uliohudhuriwa na viongozi waandamizi wa Umoja wa Mataifa wakiwemo Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina Mohammed, Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi na Bwana Griffiths.Hayo yakiendelea, msemaji wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya uratibu wa misaada ya dharura, OCHA Jens Laerke amezungumza na waandishi wa habari huko Geneva Uswisi hii leo na kusema mashirika ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa kiutu yanakabiliwa na pengo la dola bilioni 1.5 la kufanikisha operesheni zake Sudan wakati huu mahitaji yanaongezeka kutokana na mapigano yanayoendelea, maelfu ya watu wakifurushwa makwao.Naye msemaji wa shirila la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR mjini Geneva, Uswisi Olga Sarrado Mur amewaambia waandishi wa habari hii leo kwamba shirika hilo litazindua Mpango wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wa kuchukua hatua za usaidizi Sudan, wakati huu ambapo takwimu za serikali, wadau na UNHCR zinaonesha zaidi ya watu 800, 000 wamekimbia Sudan na kuelekea Chad, Ethiopia, Sudan Kusini, na kwingineko, ambapo 600,000 ni wasudan na 200,000 ni wasudan kusini na wengineo waliokuwa wanapatiwa hifadhi Sudan.Na katika mashinani na kuelekea siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari hapo kesho, tunakuletea ujumbe wa Mwandishi wa Habari kutoka Uingereza kuhusu changamoto zinazowakumba waandishi wa habari.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
2-5-2023 • 0
Nchini Chad WFP na wadau wahaha kusaidia wakimbizi wa Sudan
Chad inashuhudia wimbi jipya la wakimbizi wanaouvuka mpaka kutoka Sudan kuingia nchini humo kufuatia mapigano yaliyoanza tarehe 15 mwezi huu kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum, hali inayofanya mahitaji ya kibinadamu kuongezeka kwa kuzingatia Chad tayari inahifadhi wakimbizi ilhali rasilimali za kuwapatia ni chache.Msafiri kafiri, walinena wahenga! Na katika video hii ya shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, wasafiri hawa, wakitembea kuingia Chad, hawakuwa wamepanga safari, bali imewalazimu kutokana na mapigano nchini mwao Sudan. Kila mmoja na kirago chake kichwani, wakitembea kwa miguu, punda nao wakitumika kubebea mizigo. WFP inasema wakimbizi 20,00 wameingia Chad na kati yao takribani asilimia 70 ni wanawake na watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano, wengi wao wakisaka hifadhi chini ya miti au vibanda chakavu. Miongoni mwao ni Beské Abdoulaye, mama huyu akiwa kwenye moja ya vibanda chakavu kwenye kijiji hiki cha Koufroun, mpakani na Sudan anasimulia, “Vita imetufurusha majumbani mwetu. Tulikuwa na watoto wetu pindi watu wenye silaha walipofika na hivyo ilibidi tukimbilie kichakani. Hii yawezekana vipi?” Maisha yasiyo na staha yakiendelea katika eneo hili walikofikia wakimbizi, WFP inasema wakimbizi wengine wapya wanawasili karibu na Farchana, mashariki mwa Chad na maeneo mengine ya mpakani. Tathmini ya pamoja ya WFP na wadau imebaini mahitaji ya kipaumbele huku Mkurugenzi Mkazi wa shirika hilo nchini Chad Pierre Honnorat akiwa kwenye bohari wakipakia shehena za misaada anasema, “Sasa tunapakia shehena kwenye malori kwa sababu kw a mujibu wa takwimu za UNHCR na serikali tayrai watu kati ya 10,000 na 20,000 wameingia kutoka Sudan. Ni muhimu sana kwani kabla ya janga hili tayari tulikuwa na wakimbizi 400,000 kutoka Sudan tuliokuwa tunawapatia msaada. Ni muhimu sana kusambaza sasa kwani katika wiki 6 au 8 zijazo hatutaweza kufikia maeneo kutokana na mvua”Msafara wa malori 10 ukiwa na tani za ujazo 340 unaondoka na hatimaye kufika eneo la Adré mashariki mwa Chad, ambako wakimbizi wanapokea mgao wao wa chakula kama vile maharage. WFP inasema ili kuweza kuendelea kusaidia wakimbizi wapya wanaoingia, jamii zinazowahifadhi na wakimbizi 470,000 walioko tayari Chad, na jamii zilizo hatarini, inahitaji dola milioni 162.4. Iwapo haitopata fedha zaidi, usaidizi kwa makundi hayo utakoma ifikapo mwezi ujao wa Mei.
1-5-2023 • 0
McCain: WFP inaanza mara moja operesheni zake Sudan baada ya kuzisitisha kwa muda
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limesema linarejelea mara moja operesheni zake za msaada wa kibinadamu nchini Sudan baada ya kuzisitisha kwa muda wafanyakazi watatu wa shirika hilo walipouawa Aprili 15 mwaka huu.Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Roma Italia hii leo mkurugenzi mtendaji wa WFP Cindy McCain ugawaji wa chakula unatarajiwa kuanza katika siku chache zijazo kwenye majimbo ya Gedaref, Gezira, Kassala na White Nile kwa lengo la kutoa msaada wa kuokoa Maisha kwa maelfu ya watu ambao wanauhitaji msaada huo kwa udi na uvumba.Bi. McCain amesema mgogoro unaoendelea nchini Sudanunawssukuma mamilioni ya watu katika janga la njaa na hali ya usalama bado ni tete.Mkuu huyop amesema pamoja na kuwa wanaanza tena operesheni zao lakini wanafikiria maeneo ambayo wana fursa ya kuyafikia lakini pia suala la usalama, uwezo wao na masuala mingine ya muhimu ya ufikiaji.“Tutachukua kila tahadhari kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wetu na washirika wetu wakati tukikimbizana kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya watu walio hatarini zaidi.”Amesisitiza Bi. McCain na kuongeza kuwa “Ili kuwalinda vyema wahudumu wetu wanaohitajika sana na watu wa sudan mapigano lazima yakome.”Zaidi ya watu milioni 15 walikuwa wanakabiliwa na hali mbayá ya kutokuwa na uhakika wa chakula Sudan hata kabla ya kuanza kwa mgogoro wa sasa.Mkuu huyo wa WFP amehitimisha taarifa yake kwa kusema kuwa “Tunatarajia idadi hii kuongezeka kwa kiasi kikubwa n ani wakati kama huu ambapo WFP na washirika wake wa Umoja wa Matifa wanapohitajika sana.”
1-5-2023 • 0
01 MAY 2023
Jaridani leo tunaangazi machafuko nchini Sudana na msaada ya kibinadamu kwa waathirika. Makala tu tunamulika ibara namba 2 ya haki za binadamu na mashinani tunakupeleka mkoani Rukwa nchini Tanzania, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limesema linarejelea mara moja operesheni zake za msaada wa kibinadamu nchini Sudan baada ya kuzisitisha kwa muda wafanyakazi watatu wa shirika hilo walipouawa Aprili 15 mwaka huu.Chad inashuhudia wimbi jipya la wakimbizi wanaouvuka mpaka kutoka Sudan kuingia nchini humo kufuatia mapigano yaliyoanza tarehe 15 mwezi huu kwenye mji mkuu wa Sudan, Khartoum, hali inayofanya mahitaji ya kibinadamu kuongezeka kwa kuzingatia Chad tayari inahifadhi wakimbizi ilhali rasilimali za kuwapatia ni chache.Katika makala leo tunamulika ibara ya pili ya tamko la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu, inayosema Kila mtu anastahili kuwa na haki zote na uhuru wote ambao umeelezwa katika tamko bila ubaguzi wa aina yoyote kama vile rangi, taifa,jinsia, lugha,,dini,siasa,fikra,asili ya taifa la mtu,miliki, kuzaliwa au kwa hali nyingine yoyote. Na katika ufafanuzi huu tunarejelea makala ya mwaka jana ambamo kwayo Balozi Getrude Mongella kutoka Tanzania alifafanua kipengele cha ubaguzi wa rangi.Na katika mashinani tutaelekea Sumbawanga mkoani Rukwa nchini Tanzania kusikia jinsi wenyeji wamehamasika na kuamini kwamba chanjo zinaweza kuleta matokeo chanya.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
1-5-2023 • 0
Mwambata wa jeshi wa Tanzania nchini atembelea Kikosi cha Tanzania TANBAT 6 wanaohudumu chini ya MINUSCA nchini CAR.
Mwambata jeshi wa Tanzania anayehudumu kazi yake Jamhuri ya Afrika ya kati Brigedia Jenerali Absolomon Lyanga Shausi amefanya ziara ya kutembelea kikosi cha walinda amani wa Tanzania TANBAT6 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA ili kujitambilisha tangu kikosi hicho kianze shughuli ya ulinzi wa amani kikipokea majukumu kutoka kwa kikosi cha TANBAT5 mwishoni mwa mwaka.Kapteni Mwijage Inyoma aliyeko nchini Afrika ya Kati anaeleza zaidi..
28-4-2023 • 0
Mashirika yashirikiana kusambaza chakula Sudan
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Sudan limesema linaendelea kufanya kazi kwa karibu na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP ili kuona ni kwa vipi chakula kilichomo nchini humo kinawza kusambazwa kwa wahitaji na wakati huo huo misaada mingine inaweza kutolewa kwa ushirikiano na wadau wengine wakati huu ambapo uhasama unashamiri na kuathiri raia wakiwemo wakimbizi, wakimbizi wa ndani na raia nchini kote.Sauti hiyo ya Axel Bisshop, Mwakilishi wa UNHCR nchini Sudan akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kwa njia ya video kutoka mji wa Port Sudan nchini Sudan akisema changamoto kubwa sasa ni kuhakikisha ni vipi mgao wa chakula utaendelea. Anasema wamewasiliana na WFP na leo asubuhi wamekuwa na mazungumzo na WFP ambao wamewahakikishia kuwa watasalia na UNHCR ili kuendelea kugawa chakula maeneo ambayo bado yanafikika. Miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo ni kwamba wanashindwa kupata taarifa au kupatia taarifa jamii za wakimbizi katika baadhi ya maeneo. Hata hivyo amesema ofisi za UNHCR zimeendelea kuwa na mawasiliano na viongozi wa jamii za wakimbizi na wajumbe wa kamati za wakimbizi na kwamba wanawapatia ushauri nasaha na usaidizi kwa kadri inavyowezekana. Bwana Bisshop amesema wamepokea ripoti ya kwamba takribani wakimbizi 33,000 wamekimbia mji mkuu Khartoum kusaka hifadhi kwenye kambi za wakimbizi kwenye majimbo ya White Nile, ilhali wakimbizi 2,000 kambi zilizoko Gedaref na wengine 5,000 wamesaka hifadhi huko Kassala tangu mapigano yaanze tarehe 15 mwezi huu wa Aprili. Mwakilishi huyo wa UNHCR Sudan anasema “tuna hofu pia ya kwamba kasi ya mapigano inaweza kuongezeka na tunaweza kuwa na hali ambayo itarudia mazingira ambayo tulikuwa nayo miaka iliyopita.” Hata hivyo amesisitiza kuwa UNHCR itasalia nchini Sudan kulinda wakimbizi kutoka nje ya nchi hiyo, wakimbizi wa ndani na raia wanaohifadhi wakimbizi huku akitoa wito kwa pande kwenye mapigano kusitisha uhasama ili huduma za usaidizi wa kibinadamu ziweze kufikia wahitaji.
28-4-2023 • 0
28 APRILI 2023
Jaridani leo tunaangazi machafuko nchini Sudan, na watoto katika ukanda wa Sahel. Makala tu tuakupeleka nchini CAR na mashinani tunasalia hapa Makao Makuu, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Sudan limesema linaendelea kufanya kazi kwa karibu na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP ili kuona ni kwa vipi chakula kilichomo nchini humo kinawza kusambazwa kwa wahitaji na wakati huo huo misaada mingine inaweza kutolewa kwa ushirikiano na wadau wengine wakati huu ambapo uhasama unashamiri na kuathiri raia wakiwemo wakimbizi, wakimbizi wa ndani na raia nchini kote.Mgogoro uliodumu kwa muda sasa katika eneo la Sahel barani Afrika umekuwa ukisababisha mzigo mkubwa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wao lakini shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema kwa namna yoyote halitakoma kuendelea kuwasaidia watoto wanaojikuta katikati ya madhila.Katika makala nakupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, ambako huko mwambata wa jeshi wa Tanzania Brigedia Jenerali Absolomon Lyanga Shausi anayehudumu nchini humo alizuru kikosi cha walinda amani wa Tanzania TANBAT6 wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, ziara aliyotamatisha jana.Na katika mashinani tutasikia kauli ya mjumbe wa Kenya kwenye jukwaa la vijana lililokunja jamvi jana hapa New York, Marekani.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
28-4-2023 • 0
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "NDUI"
Katika kujifunza Kiswahili, leo tunapata ufafanuzi wa neno "NDUI" kutoka kwa mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.
27-4-2023 • 0
27 APRILI 2023
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ikimulika harakati za kufanikisha kilimo hifadhi nchini Tanzania. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ripoti ya UNICEFya wasichanan katika ICT, watoto katika mizozo nchini Sudan na chanjo kwa watoto katika ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Na katika jifunze Kiswahili hii leo tuko Tanzania kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kupata ufafanuzi wa neno"NDUI".Hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya wasichana katika TEHAMA,shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema asilimia 90 ya wasichana vijana na barubaru hawatumii mtandao wa intaneti hasa katika nchi za kipato cha chini wakati wenzao wa kiume wana fursa karibu mara mbili ya kuwa mtandaoni, ndio maana maudhui ya mwaka huu ya siku hii ni “Ujuzi wa kidijitali kwa Maisha” ili kuchagiza wasichana na wanawake kushamiri katika sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati au STEM.Wakati makubaliano ya usitishaji uhasama yakikaribishwa nchini Sudan, mashirika ya Umoja wa Mataifa na ya kimataifa yameendelea kuonya kuhusu hatari inayowakabili watoto na kuathirika kwa mfumo wa afya. Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, taasisi iliyo ya kiserikali ya Worls Vision na Save the children wameelezea jinsi gani watoto walivyo katika hatari kubwa endapo muafaka huo wa kusitisha uhasama hautotekelezwa na kuheshimiwa na pande zote, huku shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO likionya kuhusu kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya miundombinu ya afya ikiwemo kukaliwa na wapiganaji hospital kadhaa mjini Kharthoum pamoja na maabara kuu.Na zaidi ya watoto milioni 4.3 katika ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (MENA) hawajapokea hata chanjo moja ya surua kati ya mwaka 2019 hadi 2021 limeonya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na kuongeza kwamba watoto wengine takriban milioni 3.8 walipata chanjo pungufu za donda koo, pepo punda na pertussis(DTP) katika kipindi hicho.Na katika jifunze Kiswahili leo tuko Tanzania kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa BAKITA kupata ufafanuzi wa neno"NDUI".Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
27-4-2023 • 0
Jukwaa la vijana limetukutanisha na watunga sera za mataifa mbalimbali
Tayari tangu jana Aprili 25, Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) la mwaka 2023 limeng’oa nanga ambapo maelfu ya viongozi vijana kutoka duniani kote wanakusanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York kujadili pamoja na mambo mengine, masuala yanayolenga kuharakisha kujikwamua kutoka janga la COVID-19 na utekelezaji kamili wa Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu. Jukwaa la Vijana ndilo jukwaa kuu la vijana kuchangia mijadala ya sera katika Umoja wa Mataifa, ambapo wanaweza kutoa maoni yao, wasiwasi wao, na kuzingatia suluhu zao za kibunifu ili kukabiliana na changamoto zinazokabili ulimwengu.Mmoja wa vijana wanaohudhuria Jukwaa hili ni Gibson Kawago anayechakata betri chakavu za kompyuta na kuzirejesha katika matumizi mengine ya uzalishaji nishati. Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na kijana huyu. .
26-4-2023 • 0
Nakimayak: Makazi ni moja ya changamoto kubwa kwa jamii ya watu wa asili wa Inuit wa Eskimo
Jamii ya Inuit ya watu wa asili wa Eskimo ni miongoni mwa jamii za walio wachache sana kutoka jimbo la Inuvik nchini Canada. Jamii hiyo ambayo ina jumla ya watu 180,000 kwa asili ni ya wawindaji, wavuvi na wafugaji wa kuhamahama, lakini sasa kutokana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi wamelazimika kubadili mfumo wa maisha na kuishi mahali pamoja katika vijiji, hata hivyo mabadiliko hayo yamewaletea changamoto kubwa kama anavyosema Herbert Angiki Nakimayak, Makamu wa rais wa Baraza la jamii ya Inuit nchini humo anayehudhuria jukwaa la 22 la watu wa asili la Umoja wa Mataifa hapa Marekani alipozungumza na Idhaa hii ya Kiswahili..“Nyumba siku zote imekuw ni changamoto kubwa tunayokabiliana nayo katika maeneo ya vijijini na tunafanyakazi kwa karibu na uongozi ili kuhakikisha kwamba tuna nyumba zinazojitosheleza ili familia zetu ziewe kukuwa pamoja na kuwa zenye afya. Pia sidhani kama nchi au serikali zimejikwamua vyema kutoka kwenye janga la COVID-19, hivyo kuna huduma ambazo hazipatikani kwa watu wa jamii ya asili ya Inuit. Na baharini tuna msongamano wa meli ndogo na kubwa , pia linapokuja suala la umwagaji wa mafuta hatuna uwezo wa kukabiliana nalo hali itakayoathiri uhamaji wa viumbe kama nyangumi na samaki , Ndege na bata maji ambao wanahama ambao tunawtegemea.”Nakimayak ameongeza kuwa changamoto hizo anaamini suluhu itapatikana endapo jamii husika za asili zitajumuishwa na huo ndio ujumbe aliouleta kwenye jukwaa hili la watu wa asili, “Serikali , nchi na mataifa wanaandaa será na sheria kwa ajili ya watu wa asili, lakini sasa wakati umefika kwa nchi hizo kufanyakazi na watu wa asili ili kuunda sheria na taratibu na watu wa asili kwa ajili ya watu wa jamii zetu hasa wa vijijini ambao hawawakilishwi vya kutosha.”Na kwa jumuiya ya kimataifa ana wito,“Tungependa nchi na wanasayansi kuelewa kwamba sisi ni sehemu ya mfumo wa maisha na chochocte kitakachotokea katika mfumo wa maisha baharini au nchi kavu kitatuathiri pia, kitaathiri afya zetu na uwezo wetu wa kuendelea na mfumo wetu wa maisha wa kitamaduni na tunataka kulinda hilo kwa kadri tuwezavyo. Tunataka kuhakikisha kwamba tunalinda utamaduni wetu kwa ajili ya leo, kesho na wakati ambao watunga será na sheria watakapokuja kuweka sheria, será na kanuni ili wanafanye hivyo pamoja nasi na kwa ajili yetu hivyo ujumuishwaji ni ufunguo.”
26-4-2023 • 0
FAO, UNWTO: Utalii milimani unaweza kuimarisha baiyonuai na vipato vya wakazi wa maeneo hayo
Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau imeeleza bayana jinsi utalii kwenye maeneo ya milimani unaweza kuwa na manufaa sio tu kwa baiyonuwai bali pia kwa jamii zinazoishi kwenye maeneo hayo.Taarifa iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO mjini Roma, Italia hii leo imesema chapisho hilo limetolewa ili kwenda sambamba na hitimisho la mwaka wa kimataifa wa maendeleo endelevu ya milima ulioanza mwaka jana wa 2022. Chapisho hilo linasema utalii wa milimani iwapo utasimamiwa kwa uendelevu, una nafasi kubwa ya kuinua vipato vya jamii zinazozingira maeneo hayo na kusaidia kulinda maliasili na utamaduni. Hata hivyo imebainika kuwa ukosefu wa data na ufahamu kuhusu fursa za kiuchumi na mazingira zitokanazo na utalii wa milimani umezuia jamii nyingi kunufaika na fursa hizo. FAO kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la utalii duniani, UNWTO na shirika la Mountain Partnership, MP, wametoa ripoti hiyo kama njia ya kuondoa pengo ili hatimaye jamii za maeneo ya milimani zipate kunufaika na fursa zilizoko. Mathalani chapisho linataka kusongesha upatikanaji wa takwimu za utalii wa milimani ambako ni makazi ya watu wapatao bilioni 1.1, baadhi yao wakiwa ni wale hohehahe zaidi na waliotengwa. Milima ina maeneo ambako watalii wanaweza kutembea, kupanda na kufanya michezo nyakati za majira ya baridi kali. Maeneo hayo yanaweza pia kuvutia wageni kutokana na taswira zake, utajiri wa baiyonuai na tamaduni za kipekee. Hata hivyo takwimu za karibuni zaidi za mwaka 2019 zinaonesha nchi 10 zenye milima zaidi duniani zilipokea asilimia 8 pekee ya watalii wa kimataifa duniani kote. Mkurugenzi Mkuu wa FAO QU Dongyu na Katibu Mkuu wa UNWTO Zurab Pololikashvili kupitia utangulizi wa ripoti hiyo wamesema kupata takwimmu za watalii wa milimani ni hatua ya kwanza muhimu tunayopaswa kuchukua. Uwepo wa takwimu sahihi utawezesha kufuatilia mienendo ya utalii kwenye maeneo hayo na kisha kutumia takwimu kusaidia mipango na kuandaa bidhaa endelevu kulingana na mahitaji ya watalii kwenye kila eneo husika na hatimaye sera za kuchochea utalii wenye manufaa kwa jamii.
26-4-2023 • 0
26 APRILI 2023
Jaridani leo ripoti ya utalii wa milima na jamii ya watu wa asili wa Inuit. Makala tunakuletea tunasalia hapa Makao Makuu na mashinani tunakupeleka Kisiwa cha Jamhuri ya Kiribati, kulikoni?Ripoti mpya iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau imeeleza bayana jinsi utalii kwenye maeneo ya milimani unaweza kuwa na manufaa sio tu kwa baiyonuwai bali pia kwa jamii zinazoishi kwenye maeneo hayo.Jamii ya Inuit ya watu wa asili wa Eskimo ni miongoni mwa jamii za walio wachache sana kutoka jimbo la Inuvik nchini Canada.Katika Makala Flora Nducha anazungumza na Kijana Mtanzania Gibson Kawago aliyeko hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa akihudhuria Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) la mwaka 2023.Na mashinani mashinani na tutaelekea katika Kisiwa cha Jamhuri ya Kiribati kilichoko Oceania katika Bahari ya Pasifiki ya Kati kusikia ujumbe kuhusu umuhimu wa chanjo.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
26-4-2023 • 0
25 APRILI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ikimulika Malaria nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo tarifa ya WHO ya siku ya malaria duniani, wakimbizi wa Sudan na ripoti mpya ya FAO. Mashinani tunakuletea ujube kuhusu maambukizi ya malaria.Leo ni siku ya malaria duniani mwaka huu ikibeba kmaudhui “Wakati wa kutokomeza kabisa malaria:Kuwekeza kubuni na kutekeleza”. Kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataoifa duniani WHO mwaka huu linajikita zaidi katika utekelezaji na hasa umuhimu wa kuwafikiwa watu walio hatarini Zaidi kwa mikakati na nyenzo zilizopo ili kutokomeza ugonjwa huo unaokatili Maisha ya mamilioni ya watu kila mwaka.Shirika la Umoja wa Matyaifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limesema linaongeza jitihada kuwasaidia maelfu ya watu wanaokwenda kusaka usalama katika nchi za jirani na Sudan wakikimbia nchini mwao ambayo yanaonekana kuendelea kutawanya watu ndani na nje ya nchi.Na nyama, mayai na maziwa vimeelezwa katika ripoti mpya ya shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO kuwa ni chanzo muhimu cha vitutubisho vinavyohitajika mwili ambavyo haviwezi kupatikana kwa urahisi katika lishe itokanayo na mimea.Mashinani na tutakuletea ujumbe kuhusu usugu wa vimelea vya malaria na njia za kuudhibitiMwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
25-4-2023 • 0
UNICEF Ghana yarahisisha vijana kupata huduma za afya ya uzazi na masuala ya kujamiiana
Huduma za afya ya uzazi na masuala ya kujamiiana mara nyingi hupata vikwazo hasa pale zinapolenga vijana na barubaru. Hii ni kwa kuzingatia kuwa penginepo pahala ambapo huduma hizo zinatolewa si rafiki kwa vijana na hivyo kuhofia kufuata huduma hizo kunaweza kuwa chanzo kwa wao kubainika jambo ambalo wanadhani si jema kwao.Ni kwa kutambua hilo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Ghana imeibuka na mbinu mbadala inayowapatia vijana uhakika wa usalama wa taarifa zao na yale wanayotaka kufahamu ili kuwe na afya bora ya uzazi. Je ni mbinu gani hiyo? Fuatana na Assumpta Massoi kwenye makala hii iliyoandaliwa na UNICEF Ghana.
24-4-2023 • 0
24 APRILI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea habari kutoka UNICEF na WHO. Makala tunaangazia huduma za afya ya uzazi na mashinani maji na ujasiriamali, kulikoni?Wiki ya chanjo ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, inaanza leo ikichagiza juhudi kubwa kufanyika ili kuziba pengo la chanjo duniani kote.Msikilizaji, Usemi ambao umekuwa ukielezwa mara zote watu wanapozungumzia suala la amani ni kwamba, vita inapotokea wanaotesema ni wanawake na watoto. Kwa zaidi ya wiki moja nchi ya Sudan imekuwa katika vita ya madaraka baina ya majeshi ya nchi hiyo.Katika makala tunaangazia huduma za afya ya uzazi.Na katika mashini tutakupeleka Kibondo nchini Tanzania kusikiliza jinsi ambavyo hakikisho la maji safi na salama limeboresha ujasiriamali.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
24-4-2023 • 0
UNICEF: Sudan sitisheni mzozo hali ya watoto inazidi kuwa mbaya
Msikilizaji, Usemi ambao umekuwa ukielezwa mara zote watu wanapozungumzia suala la amani ni kwamba, vita inapotokea wanaotesema ni wanawake na watoto. Kwa zaidi ya wiki moja nchi ya Sudan imekuwa katika vita ya madaraka baina ya majeshi ya nchi hiyo. Je hali ya watoto ipoje?Hata kabla ya kuanza kwa mzozo wa hivi karibuni nchini Sudan, mahitaji ya kibinadamu kwa watoto yalikuwa juu sana. Takwimu zikionesha robo tatu ya watoto walikadiriwa kuishi katika umaskini uliokithiri, na watoto milioni 11.5 na wanajamii walihitaji huduma za dharura za maji na usafi wa mazingira.Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Geneva Uswisi msemaji wa Shirika la moja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF James Elder anaeleza hali ilivyo sasa.“Kwasasa tuna ripoti zinazoonesha angalau watoto 9 waliuawa na wengine 50 wamejeruhiwa. Idadi hiyo itaendelea kuongezeka maadamu mapigano yanaendelea. Lakini jambo la muhimu sana kukumbuka ni kwamba katika mapigano haya, idadi kubwa ya watu wamekwama hawawezi Kwenda kokote hivyo hawana huduma ya umeme, na wana wasiwasi wa kuishiwa chakula, maji na dawa.”Watoto waliokuwa na utapiamlo mkali kabla ya vita kuanza, walikuwa wamelazwa hospitalini hali ikoje huko?“Hivi sasa tupo katika hali ambayo misaada muhimu ya kuokoa maisha kwa zaidi ya watoto 50,000 iko hatarini, hawa ni watoto wenye utapiamlo mkali. Kwasasa watoto hawa wapo mahospitalini kwa sababu wanahali mbaya zaidi, kwa hiyo wanalishwa kwa mirija kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee ya kulishwa, na wakati mashambulizi ya mabomu au makombora yanapoanza nje ya hospitali, watoa huduma za matibabu wanahitaji kukimbia kujificha. Halafu nini sasa kinaendelea?”Ama hakika suluhu ya haraka inahitajika ili si tu kukomesha vita bali pia kuokoa maisha ya watoto hawa na wanajamii kwa ujumla ikiwemo wafanyakazi wa misaada yakibinadamu.Tangu kuibuka kwa mapigano, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amekuwa akisema, inahitajika nguvu ya pamoja kukomesha mara moja uhasama, na pande zote zinazo zozana zinahitajika kuheshimu majukumu yao ya kimataifa ya kuwaweka watoto mbali na madhara. Na msemaji wa UNICEF anarejea wito huo wa Guterres akieleza nini kifanyike.“Nini sasa kifanyike, kwasasa ni kuendelea kukazia wito wa Katibu Mkuu kwamba inahitajika kusitishwa kwa mapigano kwa sababu mapigano yamekuwa ya kiholela na watumishi wengi na wadau wa mashirika yasiyo ya kiserikali yakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotegemewa na wengi kwa sasa wamejificha, na wengine wamekwenda kwenye Mto Nile kujaribu kupata maji licha ya ukosefu wa usalama, iwe kupata maji safi na usafi wa mazingira au kupigwa na silaha za moto.”
24-4-2023 • 0
Wakati wa COVID-19 watoto milioni 25 walikosa chanjo, ni wakati wa kuziba pengo hilo: WHO
Wiki ya chanjo ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, inaanza leo ikichagiza juhudi kubwa kufanyika ili kuziba pengo la chanjo duniani kote.Wiki hiyo itakayo kamilika Aprili 30 huadhinmishwa kila wiki ya mwisho ya mwezi Aprili lengo likiwa ni kuainisha juhudi za pamoja zinazohitajika ili kuwalinda watu dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.Katika wiki hii ambayo imebeba kaulimbiu “The Big Catch-Up” ikisisitiza juhudi kubwa zinazohitajika katika kibarua kilichopo kufikia lengo la chanjo, WHO inashirikiana na wadau mbalimbali kuzisaidia nchi kurejea katika msitari unaotakiwa kuhusu chanjo ili kuhakikisha watu wengi zaidi wanalindwa dhidi ya magonjwa yanayozuilika.WHO inasisitiza kwamba “Tunahitaji kuchukua hatua sasa ili ili kuwafikia mamilioni ya Watoto ambao walikosa chanjo wakati wa janga la COVID-19, kurejesha usambazaji wa chanjo muhimu kwa kiwango cha angalau mwaka 2019 na kuimarisha huduma za msingi za afya ili kuweza kutoa chanjo.”Kwa mujibu wa shirika hilo la afya duniani lengo kubwa la wiki ya chanjo duniani ni kwa watoto wengi, watu wazima na jamii zao kulindwa dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kama polio, surua, pepopunda na mengine na kuwaruhusu kuishi kwa furaha na kuwa na maisha yenye afya.
24-4-2023 • 0
Jifunze Kiswahili: "KITENDAWILI NI NINI."
Katika kujifunza Lugha ya Kiswahili leo tunaye Mwenyekiti wa idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki Aida Mutenyo akiwa Kampala Uganda anatufafanulia "KITENDAWILI NI NINI."
20-4-2023 • 0
20 APRILI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa ambapo leo katika mada kwa kina tunakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa wameweka silaha kando na kubeba dawa na vipima mapigo ya moyo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo gazia ripoti ya UNICEF kuhusu uaminifu kwa chanjo za watoto, UNFPA Sudan Kusini, uvumbuzi na ubunifu. Katika kujifunza Kiswahili Mwenyekiti wa Idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki Aida Mutenyo, anatueleza maana ya “KITENDAWILI”.Ripoti ya Hali ya Watoto Ulimwenguni mwaka 2023 iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF imefichua kuwa mtazamo chanya kuhusu umuhimu wa chanjo kwa watoto ulipungua hadi asilimia 44 wakati wa janga la COVID-19 katika nchi 52 kati ya nchi 55 zilizofanyiwa utafiti. UNICEF inasema mara nyingi mtazamo kuhusu chanjo huwa ni suala linalobadilikabadilika kulingana na wakati maalum na hivyo ukusanyaji wa taarifa zaidi na uchanganuzi mwingine utahitajika ili kubaini kama matokeo haya ya sasa yataonesha mwelekeo wa muda mrefu na inasisitiza umuhimu wa watu kuendelea kuwapa haki ya chanjo watoto ili kuwalinda dhidi ya magonjwa.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu duniani UNFPA nchini Sudan lina wasiwasi mkubwa kuhusu ghasia kubwa zinazoendelea nchini humo ambazo zimesababisha kukwama kwa huduma za afya na kuwaweka watu hatarini hususani wanawake wajawazito wanaofikia 219,000. Laila Baker, Mkurugenzi wa UNFPA wa Ukanda wote wa Uarabuni akihojiwa na Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa ameeleza kuwa hali ni tete na UNFPA inafanya kila namna kuokoa maisha hata imefikia kulazimika kufanya huduma ya matibabu kwa “maelekezo ya kitabibu kwa njia ya simu pale inapowezekana.” Na kuelekea kesho tarehe 21 Aprili ambayo ni Siku ya Kimataifa ya Ubunifu na Uvumbuzi ili kukuza ufahamu wa jukumu la ubunifu na uvumbuzi katika nyanja zote za maendeleo ya binadamu kwa kutafuta majawabu ya changamoto za kijamii, Mvumbuzi kijana raia wa Tanzania Gibson Kawago ameshukuru Umoja wa Mataifa kuwa na siku kama hii na akaeleza mipango yake ya kupambana na uchafuzi wa hali ya hewa duniani.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili Mwenyekiti wa Idara za Kiswahili katika vyuo vikuu Afrika Mashariki Aida Mutenyo, anatueleza maana ya “KITENDAWILI”.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, Karibu!
20-4-2023 • 0
Wananchi wa Sudan Kusini washerehekea tamasha la utamaduni la amani
Mwanzoni mwa mwezi huu wa April dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya michezo kwa maendeo na amani, nchini Sudan Kusini kwa siku mbili mfululizo maelfu ya wananchi walikusanyika kusherehekea tamasha la utamaduni la amani lililoandaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni ya jimbo la Kaskazini la Bahr El Ghazal.Maelfu ya wananchi walikusanyika kwa ajili ya sherehe hizo katika mji wa Aweil, wakitazama na kushiriki kuimba na kucheza nyimbo na ngoma za kitamaduni. Leah Mushi anasimulia hali ilivyokuwa
19-4-2023 • 0
Uzazi wa Mpango usidhoofishe haki za wengine hususan wanawake - Ripoti UNFPA
Tangu tarehe 15 Novemba 2022 Umoja wa Mataifa ulipotangaza idadi ya watu ulimwenguni kuwa imefika watu bilioni 8 mjadala katika mataifa mbalimbali umekuwa Je, haw ani watu wengi sana duniani? Je, ni wachache sana? Ni kutokana na hilo, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu duniani UNFPA limetoa ripoti mpya ambayo imeshauri kuwa badala ya kuuliza jinsi watu wanavyozaliana, viongozi duniani wanapaswa kuuliza kama watu hasa wanawake, wanaweza kujiamulia wao na kwa uhuru kuhusu uzazi, swali ambalo jibu lake, mara nyingi sana, ni hapana. Zaidi kuhusu ripoti hii ya leo iliyowekwa wazi usiku wa kuamkia leo kwa saa za Marekani, tumezungumza na Meneja Mawasiliano wa UNFPA ofisi ya Tanzania, Warren Bright.
19-4-2023 • 0
COVID-19 ilidhihirisha kila mkazi wa dunia ana thamani yake - Susan Mang'eni
Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ufadhili kwa ajili ya maendeleo 2023 FfD linaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika jaribio la kubadilisha mfumo wa fedha wa kimataifa na kurejesha ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 katika mstari unaotakiwa ikiwa imesalia chini ya miaka saba kufikia ukomo.Nchi, hususan zinazoendelea zinahaha kuhakikisha zinatimiza malengo yake kwa kila hali na miongoni mwao ni Kenya ambapo Susan Auma Mang’eni Katibu Mkuu wa Idara ya Ukuzaji wa Biashara Ndogondogo iliyo ndani ya Wizara Mpya ya Ushirika na Ukuzaji wa Biashara Ndogondogo au Ujasiriamali nchini humo anahudhuria kongamano hilo na amemweleza Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amekuja na ujumbe maalum kutoka Kenya.“Kwanza nimekuja hapa ili kuwasilisha ujumbe wetu wa Kenya hasa tunavyoona ufadhili wa maendeleo, kwa sababu lile janga la COVID-19 limedhihirisha bayana kwamba hakuna sehemu yoyote hapa duniani ambayo haina faida ya mambo ya uchumi, hakuna binadamu yeyote ambaye hana uzuri wake, hana thamani ya kiuchumi. Na limeonyesha ya kwamba wakati ule ambao tulikuwa katika zile hekaheka tukijaribu kujiuliza ni jinsi gani tutakabvyoliangamiza hili janga la COVID tulijiuliza maswali lakini hatukuwa na majibu , sasa ilibidi ya kwamba kila sehemu duniani kila nchi ianze kujifikiria kuona ya kwamba ni lipi sisi tunaweza fanya kuangamiza COVID-19. Na tunaona ya kwamba kuna nchi nyingi sana katikia hii dunia ambazo ziliweza kushinda haya madhara ya COVID -19 na sasa hivi imeonesha ya kwamba kama dunia sasa lazima tuanze kujiuliza ni jinsi gani sasa tutakavyoweza kukuza uchumi wetu, ili tuweze kuboresha Maisha ya wananchi wetu ili hapo baadaye litakapotokea tena janga kama hili tusife sana kama jinsi tulivyopoteza wananchi wetu.”Akaenda mbali zaidi na kusema rasilimali watu ipo wanachohitaji sasa na wanachokiomba kwenye mkutano huu ni ufadhili ili kufikia malengo ya maendeleo na ukuzaji uchumi wao.“Tunaweza kusema kwamba majibu mengi yako katika urithi wetu kama nchi na hasa sisi hapo Kenya tunatambua ya kwamba urithi wetu uko katika wananchi wetu, kwa watu wetu ambao wana bidii, wana ndoto nzuri na wameonesha kwamba wao wanaweza kufanya lolote ili kuendelea kimaisha. Na tumeona kwamba ukienda popote pale utaona rasilimali ipo, na hii rasilimali utaitambua kupitia utamaduni wetu, jinsi ambayo tunaishi na jinsi ambavyo tunashirikiana na wengine kwa vyakula vyetu, kwa kilimo chetu , kwa bidii yetu, ndio inaonesha kuwa hiyi ndio rasilimali yetu.”
19-4-2023 • 0
19 APRILI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNFPA na ujasiriamali. Makala tunaelekea nchini Sudan Kusini na mashinaninchini Kenya, kulikoni?Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu duniani UNFPA limetoa ripoti mpya ambayo imeshauri kuwa badala ya kuuliza jinsi watu wanavyozaliana, viongozi duniani wanapaswa kuuliza kama watu hasa wanawake, wanaweza kujiamulia wao na kwa uhuru kuhusu uzazi, swali ambalo jibu lake, mara nyingi sana, ni hapana.Jukwaa la Umoja wa Mataifa la ufadhili kwa ajili ya maendeleo 2023 FfD linaendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika jaribio la kubadilisha mfumo wa fecha wa kimataifa na kurejesha ajenda ya maendeleo endelevu ya 2030 katika msitari unaotakiwa ikiwa imesalia miaka chini ya sabakifikia ukomo.tuelekee nchini Sudan Kusini ambako kumefanyika tamasha la utamaduni kwa amani lililondaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS kwakushirikiana na serikali ya jimbo la Kaskazini la Bahr El Ghazal.Na katika mashini tutaelekea tutaelekea nchini Kenya kupat aujumbe kuhusu lugha ya Kiswahili.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, Karibu!
19-4-2023 • 0
18 APRILI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina aambapo tutasalia hapa makao makuu kusikiliza msimamo wa Tanzania kuhusu Umoja wa Mataifa kufuatia mazungumzo yetu na Mwakilishi mpya wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Hussein Kattanga. Pia tunaluletea habari kwa ufupi zikiwemo za machafuko nchini Sudan, njaa uliokithiri katikati mwa Afrika na ukosefu wa elimu ka wasichana nchini Afghanistan. Mashinani tunakupeleka nchini Malawi, kulikoni?Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk, ametoa wito wa kusitishwa uhasama mara moja nchini Sudan akilisihi jeshi la serikali SAF na vikosi vya upinzani Rapid Support Forces RSF kurejea katika meza ya mazungumzo.Kiwango cha kutokuwa na uhakika wa chakula katika nchi za Magharibi na katikati mwa afrika kinaratajiwa kuwa cha juu Zaidi mwaka huu katika kipindi cha miaka 10 huku kikitishia kusambaza njaa katika nchi nyingine za pwani na zile zinazokabiliwa na mizozo kama Burkina Faso na Mali kwa mujibu wa utafiti mpya uliotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP.Na utafiti mpya uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP unaonyesha kwamba bila wasichana kuendelea na masomo na wanawake kufanya kazi nchini Afghanistan matarajio ya kujikwamua kiuchumi kwa taifa hilo yatasalia kuwa ndoto.Na katika mashini tutaelekea nchini Malawi kushuhudia furaha ya wenyeji baada ya kupata hakikisho la chakula kufuatia kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
18-4-2023 • 0
Upandaji wa miti ya migunga yarejesha matumaini kwa wakazi wa msitu wa Congo
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa kupanda miti aina ya migunga umeondoa tishio la ukataji miti holela kwenye msitu.wa bonde la mto Congo, ambao ni wa pili kwa ukubwa duniani katika kufyonza hewa ya ukaa na sasa wananchi wananufaika sio tu kwa kupata mkaa bali pia hata watu wa jamii ya asili wanaweza kupata kitoweo porini.Video ya Benki ya Dunia inaanzia kwenye msitu wa bonde la Mto Congo ambako yaelezwa ekari nusu milioni ya misitu ya asili hutoweka kila mwaka kutokana na ukataji miti kwa ajili ya shughuli za kilimo, kuni na kuchoma mkaa.Tunalima ardhi na kila siku nakata matawi ya miti na kuchanja ndoo moja ya kuni,” anasema Nzaka Ilanga akiwa porini akikata kuni akiendelea kusema zikiisha kesho tena narudi nakata nyingine kupikia chakula kwa ajili ya watoto.”Kwingineko anaoneka Guysha Izemengwe akichoma mkaa akisema anatumia miti midogo midogo kuchoma mkaa akisema anapata magunia 22 ya mkaa na kila moja anauza faranga 7,000 za DRC sawa na dola 3 na senti 50 na hiyo ndio chanzo cha kipato kwa familia yake.Kwa mujibu wa Benki ya Dunia ni asilimia 3.7 tu ya wananchi wa DRC ndio wanapata nishati ya kisasa ya kupikia.Shinikizo la ukataji miti holela linaweka mashakani wale wanaotegemea zaidi kwa chakula kama vile watu wa asili jimboni Mai- Ndombe ambapo Deko Louis akiwa anatembea msituni anasema…mitego yangu iko porini. Nawinda wanyama kwa ajili ya familia yangu. Siku hizi ni vigumu sana kupatawanyama. Si unaona leo nzima hatujapata mnyama. Zamani tungalikuwa tumepata hata Kobe.”Benki ya Dunia ikaja na mradi wa kupanda misitu mipya kwa kutumia miti ya migunga. Wakulima awali walikuwa na wasiwasi lakini sasa ndani ya misitu hiyo wamepanda na mihogo.Mayasa Mpime mkulima huyu akiwa kwenye msitu huo wa kupanda anasema uyoga ambao awali ilikuwa vigumu kupata sasa inachipuka tena. Na hata tunaweza kuwinda swala ndani ya msitu huu. Hivyo tunakula vizuri. Pia tunarina asali ambayo tunatumia na pia tunauza.”
17-4-2023 • 0
Tuhamasishe mawazo chanya duniani – Mchechemuzi wa SDGs, Chioma Ogbonna “Cill”
Mwanamuziki wa Nigeria Chioma Ogbonna akifahamika kwa jina la usanii “Cill” ni mchechemuzi wa Kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG Action Campaign ambaye hivi karibuni alihudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zenye maendeleo duni Duniani, LDC5. Moja ya nyimbo zake maarufu ni Woman alioutoa mwaka 2021 ukiwa mahususi kwa ajili ya Siku ya Mwanamke Duniani. Ni wimbo ambao unaeleza nguvu ya mwanamke licha ya kukatishwa tamaa. Nyimbo zake nyingine maarufu za Cill ni pamoja na Tatarata, Kachifo, Permit me na nyinginezo kadhaa. Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alipata fursa ya kuzungumza na msanii huyu mjini Doha nchini Qatar.
17-4-2023 • 0
Guterres: Tumieni elimu za watu wa asili kutatua changamoto za ulimwengu
Hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani Jukwaa la kudumu la watu wa asili limeanza rasmi ambapo katika ufunguzi wa jukwaa hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema pamoja na majukumu muhimu ya jamii za asili hususan katika kulinda mazingira na mbinu nyingine mbadala za maisha, watu hawa wanazidi kuwa masikini na kuzitaka nchi zote duniani zihakikishe zinawasaidia kuondokana na umasikiniAkizungumza katika jukwaa hilo la 22 Guterres amesema jamii za watu wa asili zinawasilisha utofauti mzuri na mkubwa duniani kwani kuna tamaduni tofauti zaidi ya 5000 zinazo zungumza zaidi ya lugha 4000 tofauti.Hata hivyo pamoja utajiri huu wa mila na destuli duniani lakini bado watu hawa wanakabiliwa na changamoto lukuki tena zinazo fanana.Ametaja changamoto hizo kuwa ni kutengwa, kukandamizwa, kunyimwa haki za binadamu, unyonywaji, kuchukua kiharamu maeneo yao yenye rasilimali nyingi, kuondolewa kwenye ardhi zao za asili na hata mashambulizi ya kimwili na kufanyiwa vurugu.Kwa bahati mbaya zaidi pamoja na wanawake wa jamii ya asili kuwa ndio watunzaji wa urithi tajiri sana wa asili zao lakini wao ndio mara nyingi huteseka zaidi.Guterres amesema “Udhalimu wa vizazi kwa vizazi vya ubaguzi unajidhihirisha katika ukosefu wa usawa ambao unashangaza. Jamii za watu wa asili ni takribani asilimia tano ya idadi ya watu duniani, pamoja na uchache wao lakini wao ni asilimia 15 ya watu maskini zaidi duniani.”Guterres amesema ujumbe wake uko wazi kabisa, Umoja wa Mataifa unasimama nao katika kudai haki zao na ametaka washirikishwe kwenye kutafuta suluhu za changamoto za ulimwengu kwenye masuala mbalimbali akitolea mfano afya na mabadiliko ya tabianchi ambapo dunia sasa inahamasishwa kujikita kwenye uchumi wa kijani.Amesema “Hii dhana ya uchumi wa kijani sio mpya kwa watu wa asili wamekuwa wakiitumia kwa zaidi ya milenia. Tuna mengi ya kujifunza kutoka kwenye hekima, ujuzi, uongozi, uzoefu, na mifano yao.”Amezipongeza pia jamii za asili kwa ushiriki wao kwenye masuala kadhaa kama vile Mkataba wa Anuwai za Kibiolojia na Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi.Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amezitaka nchi zote kuiga mfano wa UN na kufanyakazi pamoja na jamii za watu wa asili katika kutokomeza changamoto za uhaba wa chakula na kupunguza pengo la kidijitali kwa kuhakikisha huduma zinawafikia.Pia ametaka washirikishwe kwenye utungaji wa sera na utekelezaji wa programu mbalimbali katika ngazi zote huku wakitoa fursa kwa watu wa asili kupaza sauti zao.
17-4-2023 • 0
17 APRILI 2023
Hii leo jaridani tunasalia hapa makao makuu kukuletea yaliyojiri kwenye Jukwaa la kudumu la watu wa asili, na pia kukupeleka nchini DRC kumulika faida ya mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa kupanda miti aina ya migunga. Makala tunaangazia SDG 17 na Mashinani tunakupeleka nchini Tanzania, kulikoni?Hii leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani Jukwaa la kudumu la watu wa asili limeanza rasmi ambapo katika ufunguzi wa jukwaa hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema pamoja na majukumu muhimu ya jamii za asili hususan katika kulinda mazingira na mbinu nyingine mbadala za maisha, watu hawa wanazidi kuwa masikini na kuzitaka nchi zote duniani zihakikishe zinawasaidia kuondokana na umasikini.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mradi unaofadhiliwa na Benki ya Dunia wa kupanda miti aina ya migunga imeondoa tishio la ukataji miti holela kwenye msitu wa bonde la mto Congo, ambao ni wa pili kwa ukubwa duniani katika kufyonza hewa ya ukaa na sasa wananchi wananufaika sio tu kwa kupata mkaa bali pia hata watu wa jamii ya asili wanaweza kupata kitoweo porini.Katika makala Mwanamuziki Chioma Ogbonna (tamka Obona) “Cill” au Cillsoul wa Nigeria ambaye ni Mchechemuzi wa Kampeni ya Umoja wa Mataifa ya kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs na anaeleza anavyoutumia kipaji chake kusongesha malengo hayo 17.Na katika mashini tutaelekea nchini Tanzania kusikiliza jinsi ambavyo hakikisho la maji safi na salama limeboresha elimu shuleni.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
17-4-2023 • 0
Nguo hizi za binti yangu ni ushahidi tosha kuwa mauaji ya kimbari yapo: Manusura mauaji ya Rwanda
Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika maonesho yaliyopatiwa jina Simulizi za Manusura na Kumbukizi: Wito wa kuchukua hatua kuzuia mauaji ya kimbari. Katika maonesho haya vifaa mbali mbali vinavyohusiana na mauaji ya kimbari, mathalani ya Rwanda au kule Bosnia Hezergovina na Srebenica vinaoneshwa, yakiwemo mavazi ya wale waliokumbwa na mauaji hayo. Mauaji ya kimbari nchini Rwanda yalifanyika kwa siku 100 kuanzia Aprili 7 hadi Julai 15 mwaka 1994. Hadi leo hii manusura na wale waliopoteza ndugu na jamaa zao bado machungu yako moyoni mwao na wanatumia maonesho haya kupata sauti. Hicho ndio msingi wa makala hii kama ilivyoandaliwa na kusimuliwa na Assumpta Massoi.
14-4-2023 • 0
14 APRILI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia wasichana waliotekwa nyara katika shule ya bweni huko Chibok Nigeria ambapo mpaka sasa 96 bado wapo utumwani, na matokeo ya mradi wa FISH4ACP nchini Tanzania. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na Mashinani nchini Jamhuri ya Congo, Brazaville, kulikoni?Ikiwa ni miaka tisa imepita tangu wasichana 276 kutekwa nyara wakiwa katika shule ya bweni huko Chibok Nigeria ambapo mpaka sasa 96 bado wapo utumwani, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetaka wadau kusaidia katika kuwekeza zaidi katika usalama wa wanafunzi mashuleni kwani bado vitendo vya utekaji vinaendelea nchini humo.Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kupitia mradi wake FISH4ACP limepokea matokeo ya Utafiti kuhusu Usawa wa Kinjisia katika Masuala ya Uvuvi, moja ya hoja ambayo ikitekelezwa vema itasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hasa la kutokomeza njaa na kuondokana na umaskini. Devotha Songorwa wa Redio washirika Kids Time FM nchini Tanzania ndio shuhuda wetu wa uzinduzi huo uliofanyika katika Mkoa wa Kigoma, Magharibi mwa Taifa hilo la Afrika Mashariki.Katika tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kusikiliza simulizi ya manusura wa mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, ikiwa leo Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lina kumbukizi maalum ya mauaji hayo.Na katika mashini tutaelekea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, Brazaville kusikia ushauri kutoka kwa mwanamke ambaye amekuwa akiishi na Virusi vya Ukimwi, VVU kwa miaka 24.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!
14-4-2023 • 0
Wanafunzi nchini Nigeria wahitaji ulinzi zaidi: UNICEF
Ikiwa ni miaka tisa imepita tangu wasichana 276 kutekwa nyara wakiwa katika shule ya bweni huko Chibok Nigeria ambapo mpaka sasa 96 bado wapo utumwani, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetaka wadau kusaidia katika kuwekeza zaidi katika usalama wa wanafunzi mashuleni kwani bado vitendo vya utekaji vinaendelea nchini humo.Mwakilishi wa UNICEF nchini Nigeria Cristian Munduate amesema vitendo vya utekaji nyara wanafunzi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria vimefurutu ada ambapo taarifa za hivi karibuni kutoka vyombo vya habari zinasema wanafunzi 80 wametekwa nyara na wana mgambo huko Tsafe jimboni Zamfara.Bi. Muduate amesema “Hatuwezi kufumbia macho mateso ya watoto wa Nigeria. Lazima tufanye kila tunachoweza katika uwezo wetu kuhakikisha watoto hawa wanakuwa katika mazingira salama, wanapata elimu na fursa nyingine kadri ya uwezo wao.”Tangu mwaka 2014 zaidi ya wanafunzi 6800 wameathirika. Lakini si wanafunzi pekee, Tangu mwaka 2009 takriban walimu 2300 wameuawa, 1900 hawajulikani walipo na shule 1500 zimefungwa kutokana na kukosa usalama.Akieleza zaidi changamoto wanazokutana nazo wanafunzi na walimu nchini humo ameeleza kuwa “takwimu zinaogofya, ikiwa imepita miaka 9 tangu utekaji nyara wa kutisha wa wasichana wa Chibok, lakini jinamizi hilo linaendelea kwani watoto bado wanatekwa, wanasajiliwa kinguvu kushiriki kwenye kupigana vita, kuuawaa, kujeruhiwa na wanaharibiwa maisha yao ya baadae.”UNICEF imekaribisha utiaji saidi wa serikali ya Nigeria na ahadi yake ya kutenga dola milioni 314.5 ambazo zitaelekezwa katika usalama kwenye shule na kuahidi kushirikiana nayo kwenye kutekekeza mpango wa shule salama na kuhakikisha watoto wote waliotekwa na wanamgambo wanarejeshwa salama kuungana na familia zao.UNICEF pia imezitaka pande zote kwenye mzozo nchini humo kuheshimu sheria za kimataifa na haki za binadamu na kulinda haki na ustawi wa watoto.
14-4-2023 • 0
Kupitia FISH4ACP, FAO Tanzania yachukua hatua kukwamua wavuvi wanawake na wanaume
Nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kupitia mradi wake FISH4ACP limepokea matokeo ya Utafiti kuhusu Usawa wa Kinjisia katika Masuala ya Uvuvi, moja ya hoja ambayo ikitekelezwa vema itasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hasa la kutokomeza njaa na kuondokana na umaskini.Uzinduzi wa matokeo hayo umefanyika wakati wa kikao cha siku mbili hapa mkoani Kigoma na unatoka na Utafiti kuhusu Usawa wa kijinsia katika mnyororo wa thamani wa mazao ya Uvuvi Ziwa Tanganyika ukishirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wavuvi, wachakataji, wasafarishaji, Jeshi la Polisi, serikali na wadau wa maendeleo.Devotha Songorwa wa Redio washirika Kids Time FM nchini Tanzania ndio shuhuda wetu wa uzinduzi huo uliofanyika katika Mkoa wa Kigoma, Magharibi mwa Taifa hilo la Afrika Mashariki amezungumza na Afisa Mtaalamu Mnyororo wa Thamani wa Uvuvi na Ufugaji Viumbe Maji, kutoka FAO nchini Tanzania anayesimamia mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma nchini Tanzania, Hashim Muumin, ambaye amempatia muhtasari wa matokeo ya utafiti huo kutokana na mradi huo wa miaka mitano unaotekelezwa katika nchi 12 za Afrika ikiwemo Tanzania .“Imeonekana uvuvi ni suala la kiume zaidi kuliko wanawake lakini kwa utafiti tulioufanya tuliona asilimia 78 ya wachakataji ni wanawake na asilimia 99 ya wavuvi ni wanaume na kuna masuala ambayo yanawakwaza kina wanawake na wanaume wavuvi katika kujikwamua kiuchumi,” amesema Afisa huyo.Ameeleza kuwa utafiti huo utasaidia kubaini changamoto zinazokabili masuala ya Jinsia na fursa zake katka Ziwa Tanganyika ili kutoa mwamko kwa wanawake na watu wenye ulemavu kujihusisha na Uvuvi kuinua kipato chao.“Shirika la FAO limeanzisha dawati la jinsia katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambalo linafanya kazi na sisi kama mradi wa FISH4ACP tunafanya kazi kwa karibu sana kuhakikisha sera, mikakati na sheria za Serikali zinatekelezwa,” amebainisha Hashim.
14-4-2023 • 0
13 Aprili 2023
Miongoni mwa yaliyomoRipoti mpya ya FAO imesema kuweko kwa usawa kwa jinsia kwenye mifumo ya kilimo ya uzalishaji chakula kunaweza kuchochea uchumi wa dunia kwa dola trilioni 1 na kupunguza ukosefu wa uhakika wa kupata chakula kwa watu milioni 45.Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu wafanyakazi wahamiaji yazinyoshea kidole Nigeria, Morocco, El Salvado na Ufilipino.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Volker Türk ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali mbaya wanayokumbana nayo wasaka hifadhi na wahamiaji wanaojaribu kuelekea Ulaya kupitia njia ya Mediteranea ya Kati.Mada kwa kina inaangazia tangazo la ufadhili au ruzuku kutoka UNESCO kwa ajili ya kukuza tofauti za utamaduni hasa katika nchi zinazoendelea.Na katika Jifunze Kiswahili utafahamu maana na "BAHATI YA MTENDE KUOTEA JANGWANI".
13-4-2023 • 0
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, laisaidia Botswana kuanzisha kituo cha ufuatiliaji polio
12-4-2023 • 0
Utiaji alama silaha utafanikisha amani na usalama mashariki mwa DRC
Mashambulizi dhidi ya raia yanayoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC yanachochewa pia na kitendo cha makundi ya waasi kumiliki silaha. Silaha zinaripotiwa kupatikana kiholela na kutishia usalama wa rai ana mali zao. Ni kwa kutambua hilo, hivi karibuni ofisi ya Umoja wa Mataifa ya huduma ya kutegua mabomu UNMAS kwa ushirikiano na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, DRC MONUSCO waliendesha operesheni ya wiki mbili ya kutia alama kwenye silaha lengo likiwa ni kuhakikisha usimamizi bora wa silaha hizo. Je nini kilifanyika? George Musubao, mwadishi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nchini DRC alikuwa shuhuda wetu na ametuma makala hii.
12-4-2023 • 0
Antonio Guterres ziarani Somalia awatia moyo wananchi kuendelea na mnepo
Katika siku ya pili na ya mwisho ya ziara yake nchini Somalia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewapongeza watu wa Somalia akisema licha ya changamoto lukuki zinazowaandama wameendelea kuwa imara na kuonyesha mnepo wa hali ya juu, akiwataka kuendelea kufanya hivyo kwa ajili ya kizazi hiki na kijacho. Flora Nducha na tarifa zaidiAntonio Guterres ametoa pongezi hizo katika mkutano na waandishi wa habari wa kuhitimisha zira yake ya mshikamano mjini Moghadishu akisema tangu alipofika mara ya mwisho nchini humo miaka sita iliyopita kuna mabadiliko kwani sasa Somalia hatua kubwa zimepigwa katika mchakato wa amani , usalama na maendeleo endelevu.Amempongeza pia Rais wa taifa hilo la Pembe ya Afrika Hassan Sheikh Mohamud kwa juhudi zake za kusongesha mchakato wa amani na usalama na kuainisha umuhimu wa kuwa na ushirikiano imara sio tun a Umoja wa Mataifa bali nan chi wanachama wa serikali ya shirikisho ili kushughulikia tishio la magaidi wa Al-Shabaab.Katibu Mkuu amewahakikishia Wasomali dhamira ya Umoja wa Mataifa kulisaidia juhudi za taifa hilo na za kikanda katika kulinda haki za binadamu na kupambana na ugaidi na uhalifu wa itikadi kali ikiwemo kupitia mpango wa muungano wa Afrika nchini humo.Guterres ameongeza kuwa “Ziara yangu ya mwisho mwaka 2017 ilikuwa wakati wa operesheni kubwa ya kuepusha baa la njaa. Leo hii hali kwa mara nyingie ni ya kutia hofu, kwani mabadiliko ya tabianchi yameleta zahma kubwa, misimu 5 isiyo na mvua ambayo si kawaida na ukame tayari umeshakatili Maisha ya watu 43,000 2022 pekee na kutawanya watu wengine milioni 1.4 huku asilimia 80 wakiwa ni wanawake na Watoto.”Amesem changamoto hizo na ukiongeza na mfumuko wa bei ya chakulaumezifanya jamii za masikini kusukumwa kwenye ukingo wa njaa akikadiria kwamba kati ya sasa na Juni Wasomali milioni 6.5 watakabiliwa na viwango vya juu vya kutokuwa na uhakika wa chakula hali inayodhihirisha kwamba baa la njaa bado linanyemelea.Amesisitiza kuwa hatua lazima zichukuliwe sasa kuepusha janga kubwa Zaidi hasa akiwasihi wahisani kunyoosha mkono Zaidi kwani ombi la kibinadamu kwa ajili ya Somalia 2023 ambalo n idola bilioni 2.6 zimefadhiliwa kwa asilimia 15 pekee hadi sasa.
Hata hivyo Katibu Mkuu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani amewapa matumaini Wasomali kwa ahadi ya Umoja wa Mataifa kushikamana nao katika kusongesha amani na usalama, maendeleo endelevu, haki za binadamu na ujenzi wa mustakbali bora kwa Wasomali wote.
12-4-2023 • 0
12 APRILI 2023
Miongoni mwa tuliyokuandalia hii leo:Licha ya changamoto lukuki watu wa Somalia wanaendelea kuonyesha mnepo wa hali ya juu, asema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.WHO yaisaidia Botswana kuanzisha kituo cha ufuatiliaji polio.Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mwandishi wetu George Musubao amefuatilia kazi ya utiaji alama kwenye silaha ili kuepusha silaha hizo kutumbukia mikononi mwa waasi.Na katika mashinani unakutana na mmoja wa wanasayansi wa masuala ya anga za juu wanaotumia mfumo wa taarifa za kijiografia (GIS).Karibu.
12-4-2023 • 0
11 APRILI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tutaangazia jitihada za serikali na wadau nchini Kenya kupambana na saratani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kutoka Somalia, Ethiopia, Hatay na Kahramanmaraş. Na mashinani tunakwenda nchini Syria, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko Somalia kwa ziara ya mshikamano na taifa hilo wakati huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ametoa wito kwa wahiasani na jamii ya kimataifa nao kuonesha mshikamano wao kwa kufanikisha ombi la usaidizi wa kiutu Somalia kwa mwaka huu wa 2023 ambalo limefadhiliwa kwa asilimia 15 pekee.Tukisalia na Pembe ya Afrika, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR huko Geneva Uswisi Olga Sarrado amesema uhamishaji wa wakimbizi wapya waliowasili kwenye mkoa wa Somali nchini Ethiopia baada ya kukimbia mapigano mji wa Lascanood nchini Somalia tayari ambapo wakimbizi 1,036 walio hatarini zaidi wamehamishwa kutoka maeneo ya mipakani kwenye maeneo ya ndani zaidi katika siku tatu zilizopita.Na katika jitihada za kulinda urithi wa kitamaduni nchini Uturuki ambao hauwezi kupatiakna tena kufuatia matetemeko ya ardhi nchini humo, shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP limefikisha shehena ya kwanza ya kontena 20 kwenye makumbusho ya malikale huko Hatay na Kahramanmaraş.Na katika mashini tutakupeleka Aleppo Hatay na Kahramanmaraş katika hospitali kuu ambayo inatoa huduma mbalimbali zikiwemo za watoto na wamama wajawazito ambao pia ni waathirika wa tetemeko la ardhi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!
11-4-2023 • 0
Athari za utupaji wa taka za plastiki kwenye maziwa na baharí
Uchafuzi wa mazingira katika maeneo ya bahari unatajwa kuwa na athari kwa viumbe hai waishio chini ya maji kutokana na baadhi ya taka ikiwemo plastiki kuwa na madhara ya moja kwa moja kwa viumbe hao.Umoja wa Mataifa umekuwa ukizitaka nchi wanachama kuhakikisha wanadhibiti taka hizo katika mataifa yao ili kuokoa Maisha ya viumbe hai waishio chini ya maji pamoja na mfumo wa Ikolojia.Kutoka jijini Mwanza kaskazini-magharibi mwa Tanzania, Evarist Mapesa alikutana na Mhadhiri Msaidizi wa Shule Kuu ya Sayansi wa Maji na Mazingira yake na Teknolojia za Uvuvi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bahati Mayoma, akitaka kufahamu athari za taka za plastiki kwa viumbe hai waishio kwenye maji na hapa mhadhiri huyo anaeleza.
10-4-2023 • 0
Asante ILO: Kutoka kutumikishwa kitumwa hadi mfanyabiashara ajitegemea
Nchini Nepal mradi wa BRIDGE unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO umewezesha familia moja ya kimaskini kuondokana na sio tu kutumikishwa kwenye ajira za kitumwa bali pia kuepusha baba wa familia kuondokana na kwenda nchi za nje kusaka vibarua.Tuko wilaya ya Bajura magharibi mwa Nepal barani Asia, tunakutana na Shanti Devi Lohar, mama wa familia mwenye umri wa miaka 50. Akifungua redio kujiburudisha akiwa anauza mboga mboga na maboga huku akikumbuka maisha yalivyokuwa awali.Shanti anasema mume wangu amekwenda India kusaka kibarua kutokana na hali mbaya ya kifedha ya familia yetu. Peke yangu nyumbani ilikuwa vigumu kupata kazi. Fedha ilikuwa changamoto kwani hatukuwa na ardhi.Punde anapata mteja na anauza boga moja kwa dola tatu. Msingi wa biashara hii ni nini?Shanti anasema “nilibaini kuwa kituo cha rasilimali watu kilikuwa kinaanzisha mafunzo ya kilimo cha mboga mboga nje ya msimu husika wa mazao hayo kwa wafanyakazi waliokuwa wanatumikishwa. Nilijiunga ili nipate mafunzo ya kilimo na niwe mfanyabiashara ninayejitegemea.”Mafunzo yalifanyika na kisha Shanti alimweleza mumewe ambaye alimtumia mtaji wa dola 343 wa kuanzisha kilimo biashara cha mboga mboga. ILO na mdau wake waliwapatia makaratasi ya nailoni ya kuezekea bustani hizo, madumu ya kumwagilia pamoja na mbegu.Faida ni dhahiri na anasema kwa kuuza viazi faida ni kati ya dola 86 hadi 129 kwa mwaka. Mapato kutokana na kuuza nyanya ni kati ya dola 258 hadi 300.”Ingawa watoto wake wa kiume wanasoma bweni na gharama ni dola 429 kwa mwaka, Shanti hana tena hofu kwani anapata fedha hizo kupitia kilimo biashara na binti zake wawili wanasoma shahada ya kwanza. Na zaidi ya yote anachofurahia Shanti ni kwamba mumewe hatokwenda tena nje ya Nepal kusaka kibarua.
10-4-2023 • 0
Kambi ya Kamango huko Beni, DRC yafungwa na MONUSCO
Kambi ya Kamango iliyokuwa inamilikiwa na kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO imefungwa baada ya kukamilisha jukumu lake.Kambi hiyo iliyoko kilometa 80 kaskazini-magharibi mwa mji wa Beni jimbo la Kivu Kaskazini ilianzishwa miaka 10 iliyopita kukabili vitisho kutoka waasi wa ADF na imefungwa rasmi tarehe 6 mwezi huu. Kwa mujibu wa chapisho la MONUSCO, kambi hiyo sasa imekabidhiwa kwa mamlaka za eneo hilo ambapo Chifu wa Kata ya WAtalinga ilimo kambi hiyo ameshukuru kwa kazi nzuri iliyofanywa na MONUSCO ya kurejesha usalama kwa raia. Ijapokuwa kituo hicho kimefungw,a MONUSCO itaendelea kusalia kwenye eneo hilo kwa ajili ya kuimarisha mawasiliano na usalama kwa raia. MONUSCO inasema vifaa na miundombinu iliyokuwemo itatumiwa na mamlaka za eneo hilo na kufungwa kwa kambi hiyo kunakwenda sambamba na mpango wa mpito wa kuanza kukabidhi majukumu ya usalama kwa serikali ili hatimaye ujumbe huo uondoke DRC. Chifu wa Watalinga, Mwami Saambili Bamukoka akizungumzia hatua ya kufungwa kwa kituo hicho amesema “kwa kiasi kikubwa MONUSCO imesaidia kuimarisha usalama eneo hili. Tunashukuru kwa kazi ya vikosi mbali mbali vilivyoshirikiana nasi hapa. Tunaweza kusema sasa hali ya usalama ni nzuri.” Ameongeza kuwa wao ni sehemu ya mji wa Beni na ingawa kwingineko wanakumbwa na changamoto za usalama, wao enoe lao ni tulivu. Kwa upande wale Odette Zawadi ambaye ni Rais wa shirika la kiraia la kuchochea maendeleo Watalinga amesema mchango wa MONUSCO kwenye usalama wa eneo lao ni dhahiri kwa kuwa hivi sasa raia wanaweza kuendesha shughuli zao bila hofu, wanawake wanaweza kwenda shambani bila kushambuliwa. Amesema “ninavyozungumza, hapa kuna amani, wananchi wanaenda mashambani, kila mtu anafanya shughuli zake kwa uhuru. Hii ni kumbukumbu nzuri sana ya uwepo wa MONUSCO hapa, kwa sababu sasa tunajua bila amani hakuna kinachoweza kufanyika.”
10-4-2023 • 0
10 APRILI 2023
Hii leo jaridani tunamulika kazi ya walinda amani nchini DRC na kilimo cham boga nchini Nepal. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Bolivia, kulikoni?Kambi ya Kamango iliyokuwa inamilikiwa na kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO imefungwa baada ya kukamilisha jukumu lake.Nchini Nepal mradi wa BRIDGE unaotekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO umewezesha familia moja ya kimaskini kuondokana na sio tu kutumikishwa kwenye ajira za kitumwa bali pia kuepusha baba wa familia kuondokana na kwenda nchi za nje kusaka vibarua.Makala tunaelekea jijini Mwanza, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania ambapo Mhadhiri msaidizi wa shule kuu ya sayansi akua na teknolojia za uvuvi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Bahati Mayoma, anatueleza athari za taka za plastiki kwa viumbe hai waishio chini ya maji.Na katika mashini tutakupeleka katika Kijiji cha Oruro nchini Bolivia ambapo mafunzo ya shirika la mpango wa chakula duniani WFP yamesaidia wanawake wa jamii ya watu wa asili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuondokana na utapiamlo”.Mwenyeji wako Anold Kayanda, karibu!
10-4-2023 • 0
Asante walinda amani wa UN kutoka Tanzania kwa kutupima afya zetu- Wakazi Beni, DRC
Leo ni siku ya afya duniani ujumbe ukiwa ni Afya kwa Wote ambapo walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, wametumia siku hii kuwapima magonjwa yasiyo ya kuambukiza, NCDs, wakazi wa Beni-Mavivi jimboni Kivu. Taarifa zaidi na Afisa habari wa kikundi hich cha tatu cha kikosi cha Tanzania cha kutoa msaada wa haraka, TANZ-QRF-3 ndani ya MONUSCO, Luteni Abubakar Muna.Mganga Mkuu wa TANZQRF-3 Luteni Hussen Sinda amesema “tumeona tuadhimishe siku hii kwa kuwapima afya ndugu zetu wa Nzuma na kuwashauri kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari na saratani mbalimbali. Magonjwa haya hayaambukizi kutoka mtu mmoja kwenda kwa mwingine, lakini ni magonjwa tunayapata kulingana na namna tunavyoishi maisha yetu.” Tunawashukuru waliobuni siku hii Jusue Kapisa ambaye ni Chifu wa Kata ya Nzuma eneo la Beni-Mavivi anasema ushirikiano kati ya walinda amani wa UN kutoka Tanzania na eneo lao umekuwa ni mzuri tangu kuanza kuweko kwa walinda amani hao. Na zaidi ya yote, tunashukuru viongozi wa afya ulimwenguni kwa kuwazia na kupanga siku ya leo ya kuzungumzia siku ya afya. Sasa hawa viongozi wa afya duniani waone jinsi ya kuendelea kufanya utafiti ili magonjwa yaliyoko duniani na hayana tiba, yapate tiba na wakazi wa dunia waone mambo ya afya yanasonga mbele.” Upatikanaji wa dawa ni shida, waasi wanatukwamisha Alphonsine Muhindi, mkazi wa kata ya Nzuma ameshiriki pia huduma hii ya kupima afya na baada ya kupata huduma hiyo anafunguka kuhusu changamoto akisema, “tunapitia shida ya afya hapa Nzuma kwa sababu kwenye afya hatuna dawa kwa kuwa hatuna fedha. Ukisema ulime ili upate fedha, sasa ukiwa shambani unasikia waasi wamefika shambani. Hii inaleta dhiki kwa jamaa kwanza, njaa na magonjwa yanazidi kusambaa kwa kuwa hatuna dawa.” Ameshukuru kuweko kwa huduma hii kwa sababu angalau akishapima atajua hali ya afya yao inakuwa ni rahisi kwenda kupata dawa kwani tayari wanafahamu hali yao ya afya na pia kushughulikia watoto. Hoja ya wananchi yajibiwa na TANZ-QRF-3 Kwa Luteni Martha Mapunda, mtaalamu wa masuala ya saikolojia ndani ya TANZ -QRF -3 ombi lake ni kwa MONUSCO kuongeza idadi ya maafisa wa Jinsia zote wenye taaluma ya saikolojia ili waweze kuwasaidia wakazi wa Beni jimboni Kivu kaskazini. Hoja ya uhaba wa dawa unaokabili wakazi wa kata ya Nzuma ikajibiwa na Kapteni Damasi Khaza, Afisa Uhusiano wa TANZ-QRF -3 kwa niaba ya kamanda kikosi Luteni Kanali Adson Mwashifungwe ambapo amesema, utaratibu wa ugawaji dawa utafanyika kwa kuzipeleka kwenye vituo vya afya na hospitali ili zipatiwe wakazi hao. Taarifa hii imeandaliwa kwa pamoja na Luteni Abubakar Muna Afisa Habari TANZ-QRF -3 na George Musubao
7-4-2023 • 0
Jifunze kiswahili - Methali: "Mshale kwenda msituni haukupotea"
Katika kujifunza Lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Mshale kwenda msituni haukupotea.” Karibu!
6-4-2023 • 0
06 APRILI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunaangazia afya ya uzazi na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya afya ya uzazi salama kwa wanawake kutoka hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Dk. Elieza Chibwe akizungumzia juu ya kukoma kwa hedhi kwa wanawake anasema “Ukihisi dalili za menopause mapema nenda hospitali.” Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo salamu za sikukuu za Pasaka na Eid El Fitr kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ombi la UNICEF la msaada kwa watoto waathirika wa matetemeko ya ardhi huko mashariki ya kati, na haki za watu wa jamii asili. Leo katika kujifunza kiswahili Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya uchambuzi wa methali isemayo “Mshale kwenda msituni haukupotea.”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa watu wa imani zote duniani kote "kuunganisha sauti zao katika maombi ya pamoja ya amani", wakati huu dunia ikijiandaa kusherehekea sikukuu za Pasaka na Eid El Fitr huku akikiri kwamba amani imekosekana.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF limesema miezi miwili baada ya metetemeko ya ardhi yaliyopiga Uturuki na kaskazini mwa Syria, bado watoto milioni 2.5 nchini Uturuki wanahitaji msaada na wako hatarini kutumbukia kwenye umaskini, kutumikishwa kwenye ajira au kuozwa utotoni.Na mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa jamii ya asili hii leo amekaribisha hatua ya Vatican kutupilia mbali Nyaraka ya Ugunduzi, ambayo ni amri ya Kanisa Katoliki ya Zaidi ya miaka 500 iliyotumika kuhalalisha wakoloni kutwaa ardhi ya watu wa jamii ya asili.Na katika kujifunza kiswahili mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia methali isemayo “Mshale kwenda msituni haukupotea.”.Mwenyeji wako Leah Mushi, karibu!
6-4-2023 • 0
Nimejifunza watu wenye Down Syndrome wanaweza kuishi maisha ya kawaida wakijumuishwa – Elly Kitaly
Hivi karibuni katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa umefanyika mkutano wa Siku ya Kimataifa ya Down Syndrome. Mkutano huo uliokuwa na kauli mbiu “Pamoja nasi, kwa ajili yetu” uliandaliwa na taasisi ya Down Syndrome International (DSI) kwa kushirikiana na taasisi ya The International Disability Alliance (IDA), Uwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Mataifa wa Brazil, Japan na Poland. Mmoja wa waliohudhuria mkutano huo ni Elly Kitaly, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa asasi ya kijamii iitwayo Chadron’s Hope Foundation inayohusika na kujenga mazingira bora kwa watu wenye hali ya Down Syndrome nchini Tanzania anaeleza aliyojifunza katika mkutao huo.
5-4-2023 • 0
05 MACHI 2023
Hii leo jaridani tuanaangazi waendeshaji wa pikipiki, na kazi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania TANBAT 6 nchini CAR. Makala na mashinani tunasalia hapa makao, kulikoni?Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kwa kutambua majeraha ya kichwa ndio sababu inayoongoza ya vifo vya waendesha pikipiki duniani, limezindua mwongozo mpya utakaowezesha mamlaka kuongeza matumizi ya helmeti kwa waendeshaji na watumiaji wa pikipiki.Kikosi cha sita cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati – MINUSCA wametoa huduma ya maji safi na salama kwa vijiji vinavyokabiliwa na uhaba wa maji mjini Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï.Katika makala Bi. Elly Kitaly, Mkurugenzi na Mwanzilishi wa asasi ya kijamii iitwayo Chadron’s Hope Foundation inayojihusisha na kujenga mazingira bora kwa watu wenye changamoto ya Down Syndrome ambayo ni hali mtu anayozaliwa nayo na inaathiri uwezo wa kujifunza, anaeleza aliyojifunza katika mkutano wa Siku ya Kimataifa ya Down Syndrome uliofanyika hivi karibuni hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa ili kuhamasisha kuwahusisha watu wenye changamoto hiyo katika masuala yote ya kijamii.Na mashinani Naibu msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu Ilze Brands Kehris akisisitiza kwamba kila binadamu ana haki ya maji safi na salama.Mwenyeji wako Flora Nducha, karibu!
5-4-2023 • 0
Kikosi cha Tanzania TANZBAT6 watoa huduma ya maji kwa wananchi nchini CAR
Kikosi cha sita cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati – MINUSCA wametoa huduma ya maji safi na salama kwa vijiji vinavyokabiliwa na uhaba wa maji mjini Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï. Siku ya leo ni shangwe isiyo na kifani kwa wananachi wa kijiji cha Savaderi Kilichoko mkoani Mambéré-Kadéï baada ya kikosi cha TANZBAT6 kutoa msaada wa kuwagawia maji waliyobeba kwenye magari yao maalum.Wananchi hawa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji safi na salama. Afisa jamii na walinda amani kutoka Tanzania Luteni Alyoice Tyraphone Deusi, kwa niaba ya Mkuu wa TANZBAT06 Luteni kanali Amin Stephen Mshana, baada ya kutoa huduma hiyo ya maji katika vijiji kadhaa akasema wameona ni njia rahisi ya uhusiano bora na jamii.Kwa upande wake Bi Christin Mamaduu, mmoja wa akina mama wa eneo hilo baada ya kutua ndoo ya maji kichwani alitoa shukrani zake kwa walinda amani kutoka Tanzania chini ya MINUSCA. “Tunashukuru sana kwa walinda amani kutoka Tanzania kwa jinsi walivyo amua kutupa msaada wa maji safi hapa nyumbani maana hatuna maji safi hapa kwetu. Huwa tunapata maji ya bomba mara mbili tu kwa wiki na huwa tunanunua. Watu tunakuwa wengi sana, wanasukumana mpaka kuumia. Lakini leo tunajisikia amani kupata maji bila fujo yeyote. Mungu awabariki walinda amani wa Tanzania kwa upendo wao wanaouonyesha hapa kwetu."
5-4-2023 • 0
WHO: Mwongozo mpya kusaidia kupunguza vifo vya watumiaji pikipiki
Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kwa kutambua majeraha ya kichwa ndio sababu inayoongoza ya vifo vya waendesha pikipiki duniani, limezindua mwongozo mpya utakaowezesha mamlaka kuongeza matumizi ya helmeti kwa waendeshaji na watumiaji wa pikipiki.Mwongozo huo umepitishwa hii leo huko Mumbai nchini India kunakofanyika mkutano wa siku mbili wa kanda ya Asia kuhusu Usalama Barabarani Duniani ukijikita katika matumizi ya helmeti bora kwa ajili ya kupunguza vifo na majeraha. WHO inasema mwongozo utasaidia mamlaka kutunga sheria, kanuni na hatua zinazotakiwa ili kuongeza usalama, ubora wa helmeti na hatimaye kuokoa maisha. Taarifa ya WHO iliyochapishwa leo inasema matumizi ya helmeti zenye ubora hupunguza hatari ya vifo mara sita zaidi ilhali hatari ya ubongo kuathirika hupungua kwa hadi asilimia 74. Ukosefu wa helmeti bora, salama na zenye gharama nafuu, vinatajwa kuwa sababu za watu kutotumia helmeti, halikdhalika ukosefu wa helmeti za watoto, kutokusimamiwa kwa sheria zilizoko na joto. WHO inasema helmeti ambayo haijavaliwa na kufungwa vizuri huongeza pia hatari ya kifo na majeraha iwapo ajali itatokea. Ingawa hivyo bado matumizi ya helmeti kwenye nchi nyingi za kipato cha chini na kati ni kidogo licha ya ongezeko la kasi la pikipiki. Dkt. Matts-Ake Belin, kiongozi wa Muongo wa Umoja wa Mataifa wa usalama barabarani mwaka 2021 hadi 2030 anasema kwa kuwa pikipiki zinaongezeka kwa kasi kubwa kwenye nchi za kipato cha chini na cha kati, hatua za dharura zinahitajika kuondokana na vifo na majeraha katika miaka ijayo. Dkt. Belin anasisitiza kuwa mamlaka lazima ziweke sheria, mifumo na hatua za kuchagiza uwepo na uvaaji wa helmeti bora na mwongozo uliozinduliwa leo umetaja viwango vya ubora. Mwongozo utasaidia kuanzisha mfumo wa kuchagiza matumizi ya helmeti, ikiwemo sheria ya kimataifa kuhusu helmeti, viwango vya ubora, usimamizi wa sheria na elimu. WHO inasema mfumo wa matumizi ya helmeti zenye ubora na salama umesaidia Norway na Sweden kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo na majeraha yatokanayo na ajali za pikipiki.
5-4-2023 • 0
04 APRILI 2023
Hii leo ni siku ya mada kwa kina ambapo leo tutasafiri pamoja hadi visiwani Zanzibar nchini Tanzania kusikia harakati binafsi za mke wa Rais katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu ili kusaidia wanawake, wasichana, vijana na watoto. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za afya uzazi , athari za mabomu ya ardhini na ubaguzi dhidi ya raia weusi nchini Tunisia. Mashinani tunakuletea ujumbe kuhusu athari za mabomu ya ardhini.Idadi kubwa ya watu wameathiriwa na utasa kwenye maisha yao, imeeleza ripoti mpya iliyochapishwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni WHO.Leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji na usaidizi dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini maudhui yakisema “Hatua dhidi ya mabomu haiwezi kusubiri”. Katika ujumbe wake wa mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kwa mamilioni ya watu wanaoishi katika maeneo yenye migogoro ya silaha hata pale ambapo migogoro hiyo itamalizika bado maeneo yao yanasalia kutokuwa salaama.Na tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inayopiga vita ubaguzi wa rangi CERD imeitaka mamlaka ya ngazi za juu nchini Tunisia kulaani hadharani na kujitenga na kauli za chuki na kibaguzi zinazotolewa na wanasiasa, watu mashuhuri na watu binafsi dhidi ya Waafrika weusi, hasa wahamiaji kutoka kusini mwa jangwa la Sahara na raia weusi wa Tunisia.Na mashinani tutakuletea ujumbe wa Danel Craig, Balozi Mwema wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya huduma za kutegua mabomu ya kutegwa ardhini, UNMAS kuhusu athari za mabomu ya ardhini.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
4-4-2023 • 0
OCHA: Wadau wa kibinadamu wahitaji dola milioni 194.2 kuisaidia Burundi 2023
Wadau wa masuala ya kibinadamu kwa kushirikiana na serikali ya Burundi leo wamezindua ombi la pamoja wakihitaji dola milioni 194.2 kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya kibinadamu nchini humo kwa mwaka huu wa 2023.Ombi hilo lililozinduliwa mjini Bujumbura Burundi katika hafla maalum iliyoandaliwa na serikali ya Burundi na wadau wa kimataifa linadhihirisha ushirikiano wa muda mrefu baina ya jumuia ya misaada ya kibinadamu na serikali ya nchi hiyo na linalenga watu milioni 1.5 watakaohitaji msaada wa kibinadamu kwa mwaka huu wa 2023 na watu milioni 1.1 miongoni mwao ni wale walio hatarini wanaohitaji msaada maalum.Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA Burundi iko katika hatari kubwa ya mabadiliko ya taianchi na majanga ya asili yamesababisha wimbi kubwa la watu kutawanywa.Kaimu mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi John Agbor amesema “Hatua zetu za kibinadamu kwa Burundi mwaka 2023 ni matokeo ya uchambuzi wa kina wa mahitaji na changamoto zinazowakabili watu walio hatarini zaidi. Kwa pamoja, tukishirikiana na Serikali, washirika wa kibinadamu na wa maendeleo, tunaweza kufanya kazi kufikia suluhisho endelevu ili kuboresha hali ya maisha ya watu hawa na kujenga mustakabali thabiti zaidi. Sote tumeunganishwa na sababu moja, kuokoa maisha na kutomwacha mtu yeyote nyuma.”Mwaka 2021 na 2022, changamoto mbalimbali, ikiwa ni pamoja na janga la COVID-19, milipuko ya magonjwa, na vita nchini Ukraine, vilizidisha mahitaji yaliyopo ya kibinadamu, na kuathiri idadi ya watu walio hatarini kama vile wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao.OCHA imeongeza kuwa rasilimali za kutosha, zinazolingana na mpango wa hatua, bado ni changamoto.Iwapo halitashughulikiwa, ukosefu wa ufadhili unaweza kuwa na madhara makubwa, na kuwaacha watu walio hatarini kukabili hatari za mabadiliko ya tabianchji, magonjwa, na hatari za kutokuwa na ulinzi na hivyo kuhatarisha juhudi za kuwarudisha nyumbani na Maisha yao. Pia kuvunja mzunguko wa janga la magonjwa itakuwa vigumu bila hatua za dharura ya afya na msaada wa maji, usafi wa mazingira na kujisafi. Limesisitiza shirika hilo.Kushughulikia mahitaji ya kibinadamu Burundi ni muhimu sana na kwa kushauriana na Serikali, jumuiya ya misaada ya kibinadamu inaongoza harakati za misaada tangu 2016 ili kushughulikia mahitaji muhimu ya watu walioathirika na mwaka jana pekee watu 673,714 walipokea msaada wa kibinadamu ikiwa ni asilimia 71 ya lengo la awali.Hata hivyo OCHA inasema bado kulikuwa na pengo kubwa la ufadhili la karibu asilimi 50 hali ambayo iliathiri kiwango cha msaada wa kibinadamu uliotolewa.
3-4-2023 • 0
Nyanduga: Ibara ya 1 inabeba tamko la haki za binadamu kila nchi inawajibika kuitekeleza
Mwaka huu 2023 tamko la haki za binadamu lililopotishwa katika azimio la mwaka 1948 linatimiza miaka 75. Msingi wa azimio la tamko hilo ilikuwa ni vita ya pili ya Dunia ambayo iliifanya dunia kutafakari nje ya kuhakikisha haki, Amani na utulivu vinadumishwa duniani. Kwa kutambua mchango wa tamko hiloleo tunaangazia ibara ya kwanza. Kuchambua ibara hiyo Stella Vuzo afisa habari wa kitucho cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es slaam ameketi na mwanasheria au wakili Bahame Tom Nyanduga ambaye pia aliwahi kuwa mwakilishi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia. Kwako Stella!
3-4-2023 • 0
Nchini Colombia mfuko wa Elimu haiwezi kusubiri wapanua uwekezaji
Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kuchagiza elimu kwenye maeneo ya mizozo, Education Cannot Wait, ECW, au Elimu Haiwezi Kusubiri umetangaza nia yake ya kupanua uwekezaji nchini Colombia kwa kuwekeza dola milioni 12 ili uweze kuwafikia watoto wengi zaidi raia wa Colombia na wakimbizi kutoka nchini Venezuela.Nia hiyo imetangazwa na Mkurugenzi mtendaji wa Mfuko wa Elimu haiwezi kusubiri Yasmine Sherif akiwa ziarani nchini Colombia wiki iliyopita ambako alijionea utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo shirika hilo limetekeleza kwa miaka mitatu.ECW wametangaza kutenga dola million 12, wakati tayari walishawekeza miradi mbalimbali ambayo inafanya jumla ya uwekezaji nchini humo kufikia zaidi ya dola milioni 28 na kuweza kuwafikia zaidi ya watu 107,000 kwa takwimu zilizoishia mwezi Novemba 2022.Miradi inayotelezwa wamekuwa wakishirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa pamoja na wadau wengine na Bi Sherif anasema“Inafurahisha sana kurejea hapa na kujionea matokeo yaliyofikiwa, kuona jinsi UNICEF, Save the Children, World Vision, Shirika la kimataifa la Plan, na Shirika la kuwasaidia wakimbizi la Norway wnavyofanya kazi bega kwa bega katika kusaidia, maendeleo ya kibinadamu wakishirikiana na serikali ya Colombia.”Mbali na nchi ya Colombia kuwa na wakimbizi wa ndani milioni 5.6, lakini nchi hiyo pia imewapatia makazi zaidi ya wakimbizi milioni 2.5 kutoka nchi jirani ya Venezuela hali inayoongeza mzigo kwa serikali kwenye kutekeleza haki ya kupata elimu hususan kwa watoto.Mkurugenzi huyo wa ECW anasema wanatambua jukumu zito lililobebwa na serikali. “Tunajua kuwa serikali ya Colombia kwa ukarimu wake wame wajumuisha Wavenezuela 500,000 katika mfumo wa kitaifa wa umma. Washirika wetu nao wameweza kuwafikia zaidi ya watu 110,000, na sasa sisi Elimu Haiwezi kusubiri tunafuata na mpango wetu ulioboreshwa na wakuweza kusonga mbele zaid maendeleoi.”Msaada wa haraka wa dola milioni 46.4 zinahitajika nchini Colombia ili kuweza kuziba pengo la ustahimilivu la miaka mingi nchini humo.Programu zilizotekelezwa nchini Colombia ni pamoja na kuhakikishwa watoto wanafikiwa na elimu rasmi na isiyo rasmi katika mazingira salama, huduma za afya ya akili na usaidizi wa kisaikolojia, huduma maalum za kusaidia mabadiliko ya mfumo wa kitaifa wa elimu kwa watoto walio katika hatari ya kuachwa nyuma wakati wengine wakisonga mbele kielimu, pamoja na hatua mbalimbali za kuimarisha uwezo wa mamlaka za elimu za mitaa na kitaifa ili kusaidia elimu kuanzia ngazi ya elimu ya awali hadi shule za sekondari.
3-4-2023 • 0
03 APRILI 2023
Jaridani leo tunaangazia mahitaji ya kibinadamu nchini Burundi, na uwekezaji wa elimu nchini Colombia. Makala tunaelekea tunaku[eleka nchini Tanzania na mashinani tunasalia huko huko nchini Tanzania, kulikoni?Wadai wa masuala ya kibinadamu kwa kushirikiana na serikali ya Burundi leo wamezindua ombi la pamoja wakihitaji dola milioni 194.2 kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya kibinadamu nchini humo kwa mwaka huu wa 2023.Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kuchagiza elimu kwenye maeneo ya mizozo, Education Cannot Wait, ECW, au Elimu Haiwezi Kusubiri umetangaza nia yake ya kupanua uwekezaji nchini Colombia kwa kuwekeza dola milioni 12 ili uweze kuwafikia watoto wengi zaidi raia wa Colombia na wakimbizi kutoka nchini Venezuela.Katika makala leo tunaanza mfululizo wa vipindi vitavyoendelea hadi tarehe 10 Desemba kilele cha siku ya haki za binadamu, mwaka huu ikiwa ni miaka 75 tangu kupitishwa kwa azimio la tamko la haki za binadamu. Tamko hilo lina ibara 30 na leo tunaanza na ibara ya kwanza. Kuchambua ibara hiyo Stella Vuzo afisa habari wa kitucho cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es slaam ameketi na mwanasheria au wakili Bahame Tom Nyanduga ambaye pia aliwahi kuwa mwakilishi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia.Na mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia jinsi ambavyo programu iliyofanikishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA imewasaidia watu wenye ulemavu.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
3-4-2023 • 0
MuDa Africa washindi wa ufadhili wa UNESCO wahamasisha wasichana kutoficha vipaji vyao
Wasanii kutoka Taasisi ya Muda Africa ya nchini Tanzania, kundi ambalo ni washindi wa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) wanatoa wito kwa wasichana na wanawake kutoficha vipaji vyao ili waweze kutimiza ndoto zao na jamii iwasaidie kuyatimiza malengo hayo kwani hiyo itasaidia kuondoa pengo la usawa wa kijinsia katika tasnia mbalimbali ambazo kwa muda mrefu zinahodhiwa na wanaume. Wasanii hao wameyasema hayo hivi karibuni katika mazungumzo yao na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa walipopata walipopata nafasi ya kutumbuiza wakati wa Mkutano wa nchi zenye maendeleo duni uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu wa Machi mjini Doha Qatar.
31-3-2023 • 0
Kuna wasiwasi kuhusu kesi dhidi ya Jaji Kisaakye wa Mahakama Kuu nchini Uganda - UN
Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na mawakili Margaret Satterthwaite ameonesha wasiwasi wake mkubwa kuwa kesi za kinidhamu zilizoendeshwa dhidi ya Jaji wa Mahakama Kuu nchini Uganda Esther Kisaakye huenda zikawa sawa na kulipiza kisasi dhidi yake kwa kutekeleza majukumu yake ya kimahakama.
Katika taarifa yake iliyotolewa kwa waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi hii leo Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na mawakili Bi. Margaret Satterthwaite amesema Jaji Esther Kisaakye mwaka 2021 alitoa uamuzi katika ombi la uchaguzi kati ya kiongozi mkuu wa chama cha upinzani Bobi Wine na Rais aliye madarakani Yoweri Museveni, uamuzi wa kumpa kiongozi huyo wa upinzani muda zaidi wa kurekebisha malalamiko yake ya kupinga matokeo ya uchaguzi.
31-3-2023 • 0
31 machi 2023
Jaridani leo tunakuletea ujumbe wa Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji ambao aliutoa akiwa hapa Marekani, na habari za WFP kuhusu wakimbizi nchini Burundi. Makala tunaelekea Doha Qatar na mashinani kaunti ya Kajiado Kenya, kulikoni?Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji akiwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani amezungumza na Idhaa ya Umoja na kufafanua kile ambacho wanafanya kusaidia wakimbizi wanaotokana na mashambulizi yanayofanywa na makundi yaliyojihami kaskazini mwa nchi hiyo hususan mpakani mwa nchi yake na Tanzania tangu mwaka 2017.Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa majaji na mawakili Margaret Satterthwaite ameonesha wasiwasi wake mkubwa kuwa kesi za kinidhamu zilizoendeshwa dhidi ya Jaji wa Mahakama Kuu nchini Uganda Esther Kisaakye huenda zikawa sawa na kulipiza kisasi dhidi yake kwa kutekeleza majukumu yake ya kimahakama.Katika makala wasanii kutoka Taasisi ya MuDa Africa ya nchini Tanzania, kundi ambalo ni washindi wa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na ambao ndio kundi pekee lilipata nafasi ya kutumbuiza wakati wa Mkutano wa nchi zenye maendeleo duni uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu mjini Doha Qatar nilipozungumza nao walitoa wito kwa wasichana na wanawake kutoficha vipaji vyao ili waweze kutimiza ndoto zao na jamii iwasaidie kuyatimiza malengo hayo.Na mashinani na tutaelekea kaunti ya Kajiado Kenya kumsikia mama mwenye mtoto mwenye ulemavu aliyefaidika na msaada wa UNICEF kwa Watoto wanaoishi na ulemavu!Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
31-3-2023 • 0
Tunashirikiana na nchi Jirani kusaidia wakimbizi wa ndani na wa nje- Rais Nyusi
Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji akiwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani amezungumza na Idhaa ya Umoja na kufafanua kile ambacho wanafanya kusaidia wakimbizi wanaotokana na mashambulizi yanayofanywa na makundi yaliyojihami kaskazini mwa nchi hiyo hususan mpakani mwa nchi yake na Tanzania. “Mvua zilizonyesha kama kutokana na kimbunga Freddy kuna watu wengi wanaondoka kutoka nchi nyingine pia. Tuna mikataba kama kupitia SADC ambapo wengi wakitoka kwenda Tanzania lazima wahakikishwe kuwa wao ni wananchi na si watu wanaotaka kuleta fujo,”amesema Rais Nyusi. Amesema kinachohitajika ni wakimbizi hao kupokelewa ili wakae pale na kupatiwa usaidizi unaotakiwa, “lakini kikubwa ni mawasiliano kati ya sisi na Tanzania.” Rais Nyusi amesema wamepokea pia wakimbizi kutoka eneo la Nyasa nchini Malawi kutokana na kimbunga Freddy. “Tumewapokea na tunajaribu kutafuta njia ndogo za kusaidia maisha yao kama vile blanketi, maturubai, malazi, chakula na tunafanya hivyo kwa sababu tunafahamu kuwa kila mara vitu hivyo hutokea hivyo tuko pamoja tunashirikiana,” amefafanua Rais Nyusi. Tunakushukuru sana Rais Nyusi na zaidi y ayote Eleuterio Guevane kwa mahojiano hayo.
31-3-2023 • 0
30 MACHI 2023
Ni Alhamisi ya tarehe 30 ya mwezi Machi mwaka 2023, mwezi Machi siku ya kimataifa ya kutotupa taka na ni siku ya mada kwa kina ambayo leo inatupeka Kenya kumulika jitihada za shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO za kumuinua mwanamke mkulima kwa kutumia ubunifu na teknolojia. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na katika kipengele cha Jifunze Kiswahili tutamsikia Profesa Aldin Mutembei, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Kiswahili cha Mwalimu Nyerere.Ikiwa leo ni maadhimisho ya kwanza ya siku ya kimataifa ya kutozalisha na kutupa taka kiholela, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema wakati umefika wa kuacha kugeuza sayari dunia dampo na badala yake kila mtu azingatie matumizi ya ten ana tena ya bidhaa kadri inavyowezekana. Guterres amesema huu ni wakati wa kuamka na kusongesha harakati za kiuchumi zisizozalisha taka na wakati huo huo wateja na walaji wajenge tabia ya kutumia bidhaa tena na tena kabla ya kuitupa ili kupunguza kiwango cha taka kinachozalishwa.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP limesema halina budi kupunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi nchini Burundi kwa sababu ya ukata unaolikabili.Na huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tunakuletea ripoti kutoka kwa mwandishi wetu George Musubao kuhusu ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO.Katika katika kipengele cha Jifunze Kiswahili tutamsikia Profesa Aldin Mutembei, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Kiswahili cha Mwalimu Nyerere!Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
30-3-2023 • 0
Jifunze Kiswahili: Kongamano za Idhaa za Kiswahili Duniani
Katika Jifunze Kiswahili Profesa Aldin Mutembei Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Kiswahili cha Mwalimu Nyerere hivi karibuni nilipokutana naye visiwani Zanzibar Tanzania ambako kulifanyika Kongamano za Idhaa za Kiswahili Duniani, alinidokeza kuhusu jitihada wanazozifanya ili kuwashawishi viongozi wa Bara la Afrika hususani wa Afrika Mashariki kuanza kutumia lugha ya Kiswahili katika hotuba zao wanapokuwa katika majukwaa makubwa ya kimataifa mathalani Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
30-3-2023 • 0
Hakikisho la maji safi na salama lachochea jamii kuishi na utangamano Mkoani Kigoma nchini Tanzania
Ufumbuzi wa ubunifu wa maji unaotumia teknolojia ya nishati ya jua ambao unafanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na wadau wake ukiwemo ule wa utekelezaji, Water Mission, na ule wa kutoa msaada wa fedha Grundfos Foundation kutoka nchini Denmark umesaidia serikali ya Tanzania kubuni suluhisho la msingi na la kudumu la maji katika jamii 15 za mkoa wa Kigoma ulioko magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Lengo lao kubwa ni kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa watu 99,107 mkoani humo ifikapo Machi 2024. Miongoni mwa wanufaika ni jamii, wanafunzi na wahudumu wa afya katika hospitali, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikumbwa na changamoto za ukosefu wa maji na migogoro kati yao inayotokea mara kwa mara wakati kundi kubwa la watu linapokutana katika mto moja ulioko mbali kuteka maji. Hali ilikuwa vipi kabla na baaannoda ya mradi huo? Ungana basi na Selina Jerobon katika makala hii iliyofanikishwa na UNICEF.
29-3-2023 • 0
Walinda amani wa UN kutoka Tanzania watoa msaada wa matibabu na dawa nchini CAR
Mbali na shughuli za ulinzi wa amani chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati MINUSCA, walinda amani wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania TANBAT6 wameshiriki huduma ya kutoa matibabu na kukabidhi msaada wa dawa katika zahanati ya WAPO iliyoko mkoa wa mjini Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï.Kwa kutambua ulinzi wa amani unahusika pia na kusaidia jamii kuwa bora, Mkuu wa kikosi cha TANBAT6, Luteni kanali Amini Setephen Mshana anaendesha kampeni ya afya kwa kuruhusu watabibu wa kikosi hicho kutoa za matibabu katika vijiji vya mkoa wa Mambéré-Kadéï.Katika Zahanati ya WAPO mjini Berberati, Mganga mkuu wa kikundi cha TANBAT6 kapten Nashiru Bakari Mzego kwa niaba ya Mkuu wa TANBAT6 luteni kanali Amin Stephen Mshana anakabidhi msaada wa dawa za matibabu huku akiwa ameambatana na timu ya matabibu wa kikosi hicho wakiwa tayari kutoa huduma kwa wagonjwa wa kituoni hapo.“Tupo katika muendelezo wa kampeni ya utoaji wa huduma za afya, awali tulitoa katika zahanati ya POTOPOTO sasa tupo WAPO. Hii ni muendelezo wa utoaji huduma katika maeneo yetu ya uwajibikaji.” Amesema Kapten Nashiru Bakari Mzego ambaye ni Mganga Mkuu wa TANZBAT6.
29-3-2023 • 0
Kamati ya UN yaitaka Angola ibadili sheria ya kuengua watu wenye ulemavu kusimamia haki zao
29-3-2023 • 0
29 Machi 2023
Katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo:Angola yatakiwa kubadili sheria ya kuengua watu wenye ulemavu katika kusimamia haki zao.TANBATT 6 wanaohudumu chini ya MINUSCA washiriki huduma ya kutoa matibabu na kukabidhi msaada wa dawa katika zahanati ya WAPO, Berberati, Mambéré-Kadéï.Mradi wa ufumbuzi wa tatizo la maji kwa kutumia teknolojia ya nishati ya jua wahakikisha upatikanaji wa maji safi na salama mkoani Kigoma, Magharibi mwa Tanzania.UNICEF yafadhili mafunzo ya kuwaelimisha walimu nchini Rwanda ili kuwashauri wanafunzi.
29-3-2023 • 0
28 MACHI 2023
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo tutamsikia Spika wa Bunge la Tanzania. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka UNICEF, ILO na OHCHR. Mashinani tunakupeleka nchini Malawi.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limetoa ombi la dola milioni 171 ili liweze kusaidia watu milioni 28 wanaokabiliwa na ugonjwa wa kipindupindu katika nchi 11 zilizoko Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika.Shirika la Umoja wa Mataifa la ajira ulimwenguni ILO limesema matetemeko yaliyozikumba nchi za Syria na Uturuki mapema mwaka huu yamesababisha biashara nyingi kufungwa na kuharibika kwa kiasi kikubwa na matokeo yake mamia kwa maelfu ya watu katika nchi hizo hawana ajira za kuwapatia kipato ili waweze kujikimu.Na kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za binadamu Volker Turk hii leo jijini Geneva nchini Uswisi ametoa ripoti ya kina inayoonesha mateso yanayoendelea ya waathirika wa kutoweshwa na kutekwa nyara nchini Korea Kaskazini na kutaka wale wote wanaohusika wachukuliwe hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani ndani ya nchi au mahakama za kimataifa.Katika mashinani Shorai Nyambalo Ng'ambi afisa wa UNICEF akiwa amembeba mtoto katika kambi ya Naotcha mjini Blantyre nchini Malawi inayohifadhi waathirika wa mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na kimbunga Freddy nchini Malawi akitoa wito wa usaidizi kwa shirika hilo kwani mahitaji ya watoto ni makubwa na wanakumbwa na kiwewe!Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
28-3-2023 • 0
FAO, WHO, UNEP na WOAH: Usalama wa ulimwengu kiafya unahitaji hatua ya pamoja
Mashirika manne ya kimataifa yakiwemo matatu ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza mpango wa kimataifa wa ‘Afya Moja’ au ‘One Health’, hii leo yametoa wito wa ushirikiano wa kimataifa ili kujenga mifumo imara ya afya kufanikisha kukabiliana na changamoto ngumu za kiafya zinazoukabili ulimwengu. Taarifa iliyotolewa hii leo mjini Roma-Italia, Paris-Ufaransa, Geneva-Uswisi na Nairobi-Kenya imeeleza kuwa katika mkutano wao wa kila mwaka uliofanyika kwa mara ya kwanza ana kwa ana, wakuu wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo (FAO), la Mpango wa Mazingira (UNEP), la Afya Ulimwenguni (WHO) pamoja na mdau wao Shirika la Afya ya Wanyama Ulimwenguni (WOAH) wameeleza kuwa changamoto za kiafya zinazoukabili ulimwengu zimeonesha hitaji la mifumo thabiti ya afya na hatua za haraka za kimataifa. Kwa pamoja mashirika hayo manne yanalenga kufanikisha kwa pamoja kile ambacho sekta moja haiwezi kukifanikisha peke yake yaani mpango wa Afya Moja ambao unaonekana kuwa njia kuu ya kukabiliana na changamoto ngumu zinazokabili ulimwengu kama vile dharura za kiafya kimataifa za hivi hivi karibuni kama vile janga la COVID-19, Mpox, milipuko ya Ebola, na kuendelea kwa vitisho vya magonjwa mengine yanayotokana na Wanyama, uhakika wa chakula, usugu wa vijiumbe maradhi, uharibifu wa mfumo wa ikolojia na mabadiliko ya tabianchi. Wakisisitiza haja ya kuimarishwa kwa ushirikiano wa kimataifa na kujitolea kutafsiri mbinu ya Afya Moja katika utekelezaji wa sera katika nchi zote, viongozi wa Mashirika hayo manne yanayoshirikiana wanahimiza nchi zote na wadau wakuu kuendeleza na kuchukua hatua saba za kipaumbele: Mosi, kuupa mpango wa Afya Moja katika ajenda ya kimataifa ya kisiasa, kuongeza ufahamu na kuhamasisha kupitishwa na kukuza utawala bora wa afya kati ya sekta mbalimbali.Pili, kuimarisha sera, mikakati na mipango ya kitaifa ya Afya Moja. Tatu, kuharakisha utekelezaji wa mipango ya Afya Moja. Nne, kujenga nguvu kazi za Afya Moja zinayoshirikisha sekta mbalimbali. Tano, kuimarisha na kudumisha uzuiaji wa magonjwa ya milipuko na matishio ya kiafya katika chanzo. Sita, kuhimiza na kuimarisha maarifa ya kisayansi ya Afya Moja na uundaji na ubadilishanaji wa ushahidi. Na saba, kuongeza uwekezaji na ufadhili wa mikakati na mipango ya Afya Moja. Afya Moja ni mbinu jumuishi iliyoundwa na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa ambapo wadau mbalimbali wanashirikiana katika kutatua changamoto za kiafya kwa wanadamu, wanyama na mazingira.
27-3-2023 • 0
Ukame Turkana Umeathiri elimu, UNICEF yahaha kusadia watoto kusalia shuleni
Ukame unaoendelea Pembe ya Afrika umeathiri shule zaidi ya 100 katika kaunti ya Turkana Kenya na kusababisha watoto wengi kuacha shule. Sasa shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya kwa ushirikiano na mradi wa Educate a Child wanaisaidia serikali kusajili watoto shuleni na kuhakikisha waliosajiliwa wanasalia shuleni."Niliacha shule nikaenda mitaani, Maisha mitaani yalikuwa magumu sana, njaa kila siku na nilikosa mahali pa kula na kulala.”Huyo ni Emmanuel Ekiru mwenye umri wa miaka 10 mmoja wa wanafunzi walioathirika katika kaunti hii ya turkana na kulazimika kuacha shule, ambapo takwimu za UNICEF zinaonyesha kwamba zaidi ya wanafunzi 22,200 wameathirika na ukame huo na karibu shule 40 hivi sasa hazina huduma za kutosha za maji safi na salama.Ukame huo pia umesababisha hali ngumu ya maisha na kushindwa kujikimu kwa familia nyingi, Teresa Asinyen ni mama wa Emanuel anasema ili kukidhi mahitaji ya familia “ Imeniladhimu kusenya kuni na kuuza na pia kufanyakazi za ndani kwenye nyumba za watu. Natumia fedha ninazopata kulisha watoto wangu . Kulikuwa na ukame mbaya wati wa janga la COVID-19, na shule zilizpofungwa watoto walikwenda kusaka chakula, nilihaha kulisha watoto wangu na mara nyingi walijilisha wenyewe.”Lakini sasa UNICEF kwa kushirikiana na mradi wa Educate a child au elimisha mtoto wanaisaidia serikali kurejesha shuleni watoto kama Emmanuel na kusajili wapya huku pia wakiwapa mlo shuleni .
Hadi kufikia sasa Watoto 157,000 wamefaidika na mradi huo akiwemo Emmanuel. Mwalimu Mary Ikay kutoka shule ya msingi ya Nakwamekwi ndiye aliyeenda kuzungumza naye, “Niliweza kukutana na Emmanuel nikajaribu kuzungumza naye kama mwanangu , nikamuuliza shida ilikuwa ni nini , ndipo nikaweza kumleta shuleni na mwalimu mkuu alichukua hatua kumsaidia, kuzungumza naye na kumpatia mahitaji ambayo hakuwa nayo ili aweze kuendelea na masomo na pia kumuingiza kwenye program yam lo shuleni.”UNICEF inasema lengo ni kufikia watoto 48,000 walioacha shule na kuwarejesha shuleni katika kaunti nne ikiwemo Turkama, West Pokot, Baringo na Samburu.Lakini kwa Emmanuel sasa mambo yamebadilika hata ana ndoto, “Nikienda shule sasa nafurahia masomo , nikiwa mkubwa nataka kuwa daktari"
27-3-2023 • 0
27 MACHI 2023
Jaridani leo tunaangazia Afya na elimu. Makala tunasalia hapa makao makuu kufuatilia kazi ya vijana katika kutafuta suluhisho endelevu la upatikanaji wa maji barani Afrika na mashinani tutaelekeanchini Tanzania, kulikoni?Mashirika manne ya kimataifa yakiwemo matatu ya Umoja wa Mataifa yanayotekeleza mpango wa kimataifa wa ‘Afya Moja’ au ‘One Health’, hii leo yametoa wito wa ushirikiano wa kimataifa ili kujenga mifumo imara ya afya kufanikisha kukabiliana na changamoto ngumu za kiafya zinazoukabili ulimwengu.Ukame unaoendelea Pembe ya Afrika umeathiri shule zaidi ya 100 katika kaunti ya Turkana Kenya na kusababisha watoto wengi kuacha shule. Sasa shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya kwa ushirikiano na mradi wa Educate a child wanaisaidia serikali kusajili watoto shuleni na kuhakikisha waliosajiliwa wanasalia shuleni.Katika makala Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na Lauriel Kivuyo, Mwanaharakati kijana huyu wa tabianchi kutoka Tanzania ambaye alishiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji.Na katika mashinani tunaelekea nchini Tanzania kusikiliza shairi ambalo limeandikwa na kukaririwa kwa ajili ya kutetea haki za watoto hususani wasichana.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
27-3-2023 • 0
Vijana ni wakati wetu sasa kufanikisha upatikanaji wa maji- Laurel
Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji ulifanyika kwa siku tatu kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani kuanzia tarehe 22 mwezi huu wa Machi. Mkutano huu ulichukuliwa kama fursa ya kipekee ya kizazi hiki ya kuharakisha maendeleo kuelekea upatikanaji wa maji salama na usafi wa mazingira ifikapo mwaka 2030 kwa kuzingatia kuwa mara ya mwisho ya mkutano kama huu kufanyika ilikuwa mwaka 1977.Cha kutia moyo zaidi, katika mkutano huu vijana walipatiwa fursa ya kushiriki kwa kutambua kuwa wao si tu taifa la kesho bali ni kizazi cha sasa kinachohitajiwa zaidi katika kujenga mustakabali bora wa kesho. Miongoni mwa vijana walioshiriki ni Laurel Kivuyo, mwanaharakati wa tabianchi kutoka Tanzania akiwakilisha Bunge la Vijana la Maji Afrika. Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alipata fursa ya kuzungumza na Laurel mwishoni mwa mkutano huo na kumuuliza mambo kadhaa ikiwemo ni kipi alichoondoka nacho kutoka mkutano huu.
27-3-2023 • 0
Chonde chonde UN tusaidie tujue ukweli kuhusu mauaji ya jamaa zetu- Mkazi Beni, DRC
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC mashambulizi yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo kwenye jimbo la Kivu Kaskazini yanasababisha sio tu vifo bali machungu yasiyoisha kwa familia za waliouawa kwa kushindwa kufahamu ukweli wa nini kiliwafika jamaa zao, nani aliwaua, na haki gani imetendeka na sheria dhidi ya waliohusika. Hii leo katika makala na ikiwa ni siku ya kimataifa ya haki ya kupata ukweli kuhusu ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na utu kwa waathirika mwandishi wetu nchini DRC, George Musubao amefunga safari hadi kwenye makazi ya mmoja wa waliopoteza jamaa zao na kufahamu hali iko vipi na zaidi ya yote Umoja wa Mataifa unafanya nini.
24-3-2023 • 0
24 MACHI 2023
Jaridani leo tunaangazia siku ya kifua kikuu duniani na tunaelekea nchini Kenya. Pia tunakuletea yaliyojiri makao makuu katika mkutano wa maji. Makala tunakupeleka DRC na Mashinani tunarejea makao makuu, kulikoni?Leo ni siku ya kifua kikuu duniani maudhui yakiwa “ndio inawezekana kuitokomeza TB.” Takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO zinaonyesha kuwa tangu mwaka 2000 watu milioni 74 wamesalimika baada ya Kupona kifua kikuu na ni kwasababu ya harakati za ulimwengu za kupambana na ugonjwa huo hatari.Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji ukifikia tamati kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huku moja ya mikakati ni kuhakikisha kunakuweko matumizi endelevu ya maji, mmoja wa washiriki kutoka Rwanda amezungumzia vile ambavyo teknolojia ya kusafisha maji taka ili yaweze kutumika tena na tena inaweza kuwa mkombozi kwenye eneo lao.Makala George Musubao, mwandishi wetu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akiwa Beni amekutana na muathirika wa kuuawa kwa wanafamilia lakini hadi sasa haki haijatendeka, ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupata ukweli kwa makosa ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na utu kwa waathiriwa hao.Na katika mashinani tunakuletea ujumbe wa Danielle Kamtie, Makamu wa Rais wa Bunge la Vijana Duniani katika Maswala ya Maji ambaye ni mmoja wa vijana wanaohudhuria mkutano wa maji hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
24-3-2023 • 0
Naibu Meya wa Musanze asema teknolojia ya kusafisha maji itatuokoa Rwanda
Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji ukifikia tamati kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huku moja ya mikakati ni kuhakikisha kunakuweko matumizi endelevu ya maji, mmoja wa washiriki kutoka Rwanda amezungumzia vile ambavyo teknolojia ya kusafisha maji taka ili yaweze kutumika tena na tena inaweza kuwa mkombozi kwenye eneo lao. Mshiriki huyo Andrew Mpuhwe Rucyahana ambaye ni Naibu Meya wa wilaya ya Musanze katika jimbo la Kaskazini nchini Rwanda amesema hayo akihojiwa na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa. Bwana Rucyahana anasema kule Musanze anakotoka ni eneo lenye shughuli nyingi za kitalii na likipokea wageni wengi wanaofika hivyo ni lazima kuwe na kiasi kikubwa cha maji tena maji safi. “Ushiriki wangu kwenye huu mkutano utaniwezesha kukutana na watu wengine na kufahamu ni vipi tunaweza kufanikisha wilaya ya Musanze iwe na maji safi na salama hasa kwa kuzingatia eneo letu liko milimani na tunapokea watalii wengi,” amesema Naibu Meya huyu wa Musanze. Hapa kwenye mkutano tunaweza kubadilishana mawazo ni vipi watu wanajenga miundombinu ya maji. Tuna maji mengi lakini hayatoshi, tungali na kazi kubwa ya kufanya ili tufikishe maji safi kwa watu wote, anasema Bwana Rucyahana akitaja changamoto ni uhaba wa fedha za kuwezesha kujenga miundombinu ya kufikisha maji milimani. “Tunahitaij kupata maji yaliyo safi. Mfano tupate teknolojia ya kupeleka maji milimani ambako kuna hoteli zinazopokea wageni wengi. Tuna malengo ya kufikisha maji kwa wakazi wote wa wilaya ya Musanze ifikapo mwaka 2024.” Hoja ya kutumia maji tena na tena ilitajwa na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Csaba Kőrösi, ambaye alisema teknolojia hiyo ni moja ya mambo muhimu ya kuepusha kupoteza maji. “Tunatakiwa kukomesha haraka upotevu wa maji. Kuwa na mzungumko wa matumizi ya maji, yaani kuyatumia tena na tena badala ya kuchimba mengine, huo ndio unapaswa kuwa mwelekeo,” Naibu Meya huyu wa Musanze anasema katika eneo lao watu wanatumia maji mara moja tu “unaona maji mengi yanaharibika. Lakini tayari kuna teknolojia ya kusafisha maji ili yatumike tena na tena mara mbili au tatu. Teknolojia hii ni gharama kubwa Afrika. Kwa Musanze teknolojia hiyo inatumika kwenye hotel za gharama ya juu . Lakini si katika hoteli za bei ya gharama ya chini au kwenye makazi ya watu wenye uwezo mdogo ambao ni wengi.” Ni kwa mantiki hiyo anaamini kuwa kupitia mkutano wa maji anaweza kupata watu wenye teknolojia wanaweza kuipeleka na kuiuza huko Musanze. Lakini juu ya yote wito wake ni kwa watu kutambua kuwa maji ni maisha yetu, kukosa maji ni kukosa maisha. Watu wote tusaidiane ili tuwe na maji safi na mengi barani Afrika.
24-3-2023 • 0
Inawezekana kutokomeza kabisa TB kwa kuongeza juhudi dhidi ya ugonjwa huo
Leo ni siku ya kifua kikuu duniani maudhui yakiwa “ndio inawezekana kuitokomeza TB.” Takwimu za shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO zinaonyesha kuwa tangu mwaka 2000 watu milioni 74 wamesalimika baada ya Kupona kifua kikuu na ni kwasababu ya harakati za ulimwengu za kupambana na ugonjwa huo hatari. Kifua kikuu husababishwa na bakteria wanaosambaa kupitia kukohoa, kucheua, kuimba na hata kucheka. Kifua kikuu ni ugonjwa hatari unaosababishwa na bakteria. Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kikohozi ambacho kinaweza kutoka na damu, kupungua uzito wa mwili, joto mwilini hasa wakati wa usiku na maumivu ya viungo.Kulingana na WHO, watu milioni 10 waliambukizwa kifua kikuu mwaka 2021. Geoffrey Murage aliugua kifua kikuu mwaka 2015 na ishara za kikohozi kisichokwisha pamoja na kuishiwa nguvu ndivyo vilivyomsukuma kusaka vipimo.Murage anasema, "nilianza kukohoa na kusikia mwili uko na uchovu.Nilifikiria kwenda kwa madaktari kuangaliwa na nikapimwa magonjwa tofauti tofauti ndipo wakaiona TB.Baada ya hapo ndio nikapewa dawa za wiki moja na kuagizwa kwenda kwenye hospitali iliyokuwa karibu ya Kayole kuchukua nyengine.Nilipewa maagizo ya kumeza dawa na nikichelewa itabidi nirudie kwahiyo nilitii.Nilikuwa napewa za mwezi mmoja kisha narejea kuongezea hadi ikatimia miezi sita.” anasimulia.Janga la covid 19 lilimulika matatizo yanayowakabili wakaazi wa mataifa masikini ukizingatia mifumo ya afya na utoaji huduma.Wagonjwa wa kifua kikuu ni baadhi ya wanaohitaji huduma mujarab za afya na matibabu kwani vikwazo ni vingi.Kwa Kenya, dawa za kifua kikuu hutolewa bure kwenye hospitali za umma. Hilo lilimuwezesha Geoffrey Murage kujipa moyo kwenye safari ya matibabu.Tathmini imebaini kuwa kifua kikuu kinawaathiri zaidi wanaume ikilinganishwa na wanawake kwani mienendo na tabia ina mchango mkubwa kwani, "kuepuka TB kitu cha kwanza ni usafi. Cha pili mambo ya kuombana sigara na pombe ni muhimu kuachana na hayo kwani mimi nahisi huko ndiko nilikookota TB.Hii ni kwasababu hivyo vikombe wanavyotumia havioshwi vizuri na vinatumiwa na kila mtu,” anafafanua.Mada kuu ya siku ya Kifua kikuu mwaka huu ni Ndio! Tunaweza kuitokomeza TB!.Dhamira ya siku hii ni kuwatia imani viongozi na kuwatia shime kuimarisha uwekezaji kwenye sekta ya afya kwenye vita dhidi ya Kifua Kikuu. Geoffrey Murage ana imani TB inaweza kutokomezwa kwani yeye ni mfano mzuri.Kwa mtazamo wake, "TB ni kama homa ukitii.Ukitii mawaidha ya daktari utapona kwani ni kama homa. Ukikosa kutii utakufa tu.Ukinywa dawa mara kadhaa mwili unazowea. Ni lazima unywe hizo dawa. Ukiacha kuzitumia utaumia.Maisha sio ya daktari, ni yako tu.” anasisitiza.Mwaka wa 2023 una umuhimu mkubwa katika vita dhidi ya Kifua Kikuu na Umoja wa Mataifa uko mstari wa mbele kwenye harakati hizo. Kongamano la pili la Kifua kikuu la ngazi ya juu limepangwa kufanyika tarehe 22 mwezi wa Septemba mwaka huu. Ajenda kuu ni manufaa ya sayansi, teknolojia na uwekezaji kupambana na TB. Takwimu za shirika la Afya la Umoja wa Mataifa,WHO, zinaashiria kuwa Kenya ni moja ya mataifa 22 yanayochangia 80% ya wagonjwa wa Kifua kikuu ulimwenguni.Kwa mantiki hii, Kenya ni ya 15 katika orodha hiyo ya mataifa 22 yanayozongwa naTB. …
24-3-2023 • 0
Jifunze Lugha ya Kiswahili: HAKIBIZA
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo tunapata ufafanuszi wa neno "HAKIBIZA" kutoka kwa mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA.
23-3-2023 • 0
23 MACHI 2023
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo Mkutano wa 67 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW67 umekunja jamvi baada ya kufanyika kwa takribani wiki mbili! Maudhui yalikuwa ni vipi teknolojia na uvumbuzi vinaweza kumkwamua mwanamke na msichana katika zama za kidijitalitunaangazia, na Getrude Dyabene, Afisa kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria na haki za binadamu nchini Tanzania atakueleza washiriki waliondoka na ujmbe gani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi za afya, maji safi na salama na biashara. Katika jifunze Kiswahili leo tunataungana na mtaalam wetu ni Onni Sigalla kutoka BAKITA,Tanzania salia papo hapo?Kuelekea siku ya Kifua Kikuu au TB duniani hapo kesho shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO hii leo limetangaza kupanua wigo wa mpango wa Mkurugenzi wa shirika hilo wa kusaidia mchakato wa ufuatiliaji wa ugonjwa huo ili kuutokomeza na kufanikisha afya kwa wote ifikapo mwaka 2030. Mpango huo uliokuwa wa 2018 hadi 2022 sasa umeongezwa kutoka 2023 hadi 2027 na unajumuisha utoaji wa tiba za muda mfupi mfupi dhidi ya TB yenye usugu wa dawa.Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maji ukiendelea hapa Umoja wa Mataifa mmoja wa washiriki Mana Omar ambaye ni Mkurugenzi wa shirika la kiraia la SASAL Kaunti ya Kajiado nchini Kenya amezungumzia changamoto za maji zinazokabili jamii yake ya wafugaji.Na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara, UNCTAD imetoa ripoti yake hii leo inayoonesha ingawa ukuaji uchumi duniani ulidorora mwishoni mwa mwaka jana na kuwa hasi, mwanzoni mwa mwaka huo kuwa kiwango cha biashara kilivunja rekodi na kufikia thamani ya dola trilioni 32 na kichocheo kilikuwa uzalishaji wa bidhaa rafiki kwa mazingira.Na katika jifunze lugha ya Kiswahili , leo tunapata ufafanuszi wa neno "HAKIBIZA" kutoka kwa mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
23-3-2023 • 0
Maji ni zawadi toka kwa mungu hivyo ni haki ya kila mtu: Fr. Benedict Ayodi
Mkutano wa maji wa Umoja wa Mataifa unaanza leo Machi 22 hapa makao makuu ukibeba maudhui hatua za ajenda ya kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wote, kwani hatua hizo za maji zinaongeza uhakika wa chakula, usawa miongoni mwa jinsia, zinahakikisha watoto wanasalia shuleni, zinafanya jamii kuishi kwa amani na kuchangia mazingira yenye afya.Umoja wa Mataifa unamtaka kila mtu kuchukua hatua na sasa na shirika la kimataifa lisilo la kiserikalia la Wakapuchini wa Fraciscan ni miongoni mwa wanaochukua hatua hizo ili kuhakikisha rasilimali hii muhimu inamfikia kila mtu.Kufahamu zaidi kuhusu shirika hilo na wanachokifanya Flora Nducha amemezungumza na Fr Benedict Ayodi wa shirika hilo ambaye anaanza kwa kueleza kuhusu shirika lao
22-3-2023 • 0
Vikosi vya usaidizi wa haraka nchini DRC kutoka Tanzania vyakabidhiana majukumu
Mashambulizi dhidi ya raia huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC yanaripotiwa kila uchao ambapo Umoja wa Mataifa kupitia ujumbe wake wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO unaendelea kujiimarisha ili kuimarisha pia usalama wa raia ambalo ndilo jukumu lake. Harakati za kulinda raia na kukabiliana na waasi zinaendeshwa na walinda amani kutoka mataifa mbali mbali ikiwemo Tanzania ambapo hivi karibuni kikundi kipya cha kutoa usaidizi wa haraka kimewasili kuendeleza jukumu la kikundi cha awali. Je kilichofanyika ni nini? Wanaoondoka wana ujumbe gani na wale wanaoingia wana matarajio yapi? Basi ungana na Luteni Abubakari Muna Afisa Habari wa kikundi kipya kilichoingia.
22-3-2023 • 0
22 MACHI 2022
Jaridani leo tunaangazia mkutano wa maji hapa makao makuu na kusalia kwenye siku ya maji tukimulika upatikanaji wa maji nchini DRC. Makala na mashinani tutasalia huko huko DRC, kulikoni?Ikiwa leo ni siku ya maji duniani Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti sasa iki kuhakikisa rasilimali hiyo adhimu inalindwa, kudhibitiwa ipasavyo na kupatikana kwa kila mtu.Hii leo ni siku ya maji duniani na ninakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mtoto Liesse mwenye umri wa miaka 17 amefuatilia upatikanaji wa maji safi ya kunywa kwenye eneo la Goma jimboni Kivu Kaskaizini baada ya kupatiwa mafunzo ya uandishi wa habari na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF na hatimaye taarifa yake kutangazwa na Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo.Makala tunakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwenye makabidhiano ya vikosi vya Tanzania vya kutoa usaidizi wa haraka kupitia ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO. Shuhuda wetu ni Luteni Abubakar Muna, Afisa Habari wa walinda amani hao wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania.Na katika mashinani namleta kwako Ghislane, mama huyu wa familia mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC akizungumzia jinsi maji wanayoteka ziwa Kivu ni machafu na yanasababisha magonjwa kwa mtoto wale mdogo. Akisema madayareee akimaanisha kuhara. Anatoa wito watu wasitupe taka kwani ziwa ni chanzo cha samaki, chakula na usafiriMwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
22-3-2023 • 0
Takribani watu bilioni 2.4 hawatakuwa na maji mijini ifikapo mwaka 2050: UN
Mkutano wa maji wa Umoja wa Mataifa unaanza leo ukibeba maudhui “kushikamana kwa ajili yam aji kwa wote” Ikiwa pia ni siku ya maji duniani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti sasa ili kuhakikisa rasilimali hiyo adhimu inalindwa, kudhibitiwa ipasavyo na kupatikana kwa kila mtu.Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema maji ni kama damu ya Maisha ya dunia, kwani kuanzia katika suala la afya na lishe, hadi elimu na miundombinu maji ni muhimu katika kila nyanja ya mwanadamu kuishi na ustawi wake lakini pia yanachangia pakubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kushamiri kwa kila taifa.Pamoja na umuhimu wake wote huo amesema lakini “Tone kwa tone rasilimali hii muhimu inaharibiwa na uchaguzi wa mazingira na kukaushwa kwa kutumiwa kupita kiasi, huku mahitaji yam aji yakitarajiwa kupita uwezo wa rasilimali hiyo kwa asilimia 40 ifikapo mwisho wa muongo huu.”Wakati huo huo, Katibu Mkuu amesema mabadiliko ya tabianchi yanaharibu mzunguko wa asili wa maji.Uchafuzi wa gesi ya viwandani unaendelea kuongezeka hadi viwango vya kuvunja rekodi ya wakati wote ule , ongezeko la joto duniani likifurutu ada kwa viwango vya hatari.“Hii inazidisha majanga yanayohusiana na maji, milipuko ya magonjwa, uhaba wa maji na ukame, huku ikisababisha uharibifu wa miundombinu, uzalishaji wa chakula, na minyororo ya usambazaji.”Guterres ameongeza kuwa kati ya kila watu 100 duniani, 25 huchota maji yao yote kutoka kwenye vijito vya wazi na madimbwi au hulipa bei ya juu kununua maji yenye usalama wa kutiliwa shaka. Watu 22 kujisaidia nje au kutumia vyoo vichafu, vilivyo hatari au vilivyobomoka. Na 44 wanaona maji yao machafu yakitiririka kurudi kwenye vyavyo vya maji vya asili bila kutibiwa, na kusababisha matokeo mabaya ya kiafya na kimazingira.”Umoja wa Mataifa unasema “watu wanaoishi mijini wanaotarajiwa kuwa kwenye mgogoro wa kukosa maji itaongezeka mara mbili kutoka watu milioni 930 mwaka 2016 hadi kufikia watu kati ya bilioni 1.7 na bilioni 2.4 mwaka 2050.”Kwa kifupi mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema “Dunia yetu inakwenda kombo katika kufikia lengo letu la maji yanayodhibitiwa kwa usalama na usafi wa mazingira kwa wote ifikapo 2030 na hii ni hatari sana.”Amesisitiza kuwa hakuna mud awa kupoteza akimtaka kila mmoja kuchukua hatua Madhubuti ili kuleta mabadiliko mwaka huu na kuwekeza katika brasilimali hii ambayo uhai wa waytu na dunia unaitegemea.Amehitimisha kwa kusema kwamba “Maudhui ya siku ya maji mwaka huu yanatukumbusha gharama ya kushindwa huku kuchukua hatua kwa mabilioni ya watu ambao wanakosa maji safi na salama.”
22-3-2023 • 0
Wanahabari watoto wapasha umma kuhusu changamoto za maji DRC kwa kuwezeshwa na UNICEF
Hii leo ni siku ya maji duniani na ninakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko mtoto Liesse mwenye umri wa miaka 17 amefuatilia upatikanaji wa maji safi ya kunywa kwenye eneo la Goma jimboni Kivu Kaskaizini baada ya kupatiwa mafunzo ya uandishi wa habari na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani, UNICEF na hatimaye taarifa yake kutangazwa na Radio Okapi ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo.Video ya UNICEF inaanza kwa kuonesha msikilizaji akirekebisha redio yake kupata masafa ya Radio Okapi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na kisha anaonekana Liesse na kamera yake akikutana na Sostine, mchuuzi huyu wa maji akikokota kwa baiskeli madumu yaliyojaa maji aliyoteka kutoka Ziwa Kivu hapa Goma, jimboni Kivu kaskazini. Sostine anamweleza mwanahabari mtoto Liesse ya kuwa “Kila asubuhi nachukua baiskeli yangu na kisha nakwenda ziwani kuteka maji. Kutokana na taka zilizotupwa kwenye ziwa inabidi niweka dawa ya kusafisha maji kwenye madumu halafu hayo maji nakwenda kuuza. Nafanya hii kazi hapa kwenye mji wetu wa Goma kwa sababu katika huu mji wetu kuna shida ya kupata maji safi na salama.” Dawa anayosema anaweka ni Klorini ya kutakatisha maji kwani kwenye ziwa kuna uchafu. Ripoti hii ya Liesse iko hewani kupitia Radio Okapi kwa ufadhili wa UNICEF kwa kuwa kila wiki watu milioni 24 huwasha redio zao kusikiliza na sasa wasikilizaji wametegesha redio zao na Liesse kupitia matangazo hayo anasema, “habari zenu nyote mimi ni Liesse. Nimekuwa kwenye mji wa Goma kwa miaka mitatu. Tunahitaji maji na tunahitaji mabomba yanayotoa maji vizuri.” Na kisha ana ujumbe “mimi mwanahabari kijana napenda Waziri wa Mazingira ajaribu kutatua haya matatizo kwa sababu tukiwa na maji safi na salama itatusaidia, au sio? Kwa sababu wanasema maji ni uhai. Tunahitaji maji kila mahali. Hospitalini, nyumbani, shuleni ambako kuna wasichana wengi. Naona maji ni mtambuka katika maisha yetu, ni kila kitu.”
22-3-2023 • 0
21 MACHI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina nitasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika maandalizi ya mkutano wa maji wa mwaka 2023, unaoanza kesho kumsikia Fr. Benedict Ayodi kutoka shirika la kiamatifa la Wakapuchini wa Fraciscan ambao watakuwa na mjadala maalum kuhusu haki ya maji kwa wote katika mkutano huo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo zikiwemosiku za UN, UNCTAD na Burundi. Mashinani tunakuletea ujumbe kuhusu misitu.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupinga ubaguzi wa rangi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kila mtu aazimie kutokomeza ubaguzi huu ambao unaendelea kuathiri kila nchi duniani.Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara, UNCTAD imetoa ripoti hii leo inayotaka nchi za Afrika zilizo kusini mwa Sahara zishirikiane kuchagiza matumizi ya nishati ikiwemo rejelezi kama njia ya kuimarisha huduma za afya, elimu na kupunguza umaskini.Na ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa hii leo imesema ina hofu kubwa juu ya ongezeko la msako dhidi ya watetezi wa haki nchini Burundi kufuatia kuswekwa korokoroni hivi karibuni kwa watetezi watano wa haki za binadamu na kufungwa jele kwa mwandishi wa Habari.Na katika mashinani tutausikia ujumbe kuhusu uhifadhi wa misitu na faida zake.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
21-3-2023 • 0
Waandishi wa habari wana fursa kubwa ya ushawishi chanya kwa jamii: Fatma Hamad – Zanzibar
Tangu shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni lilipoitangaza lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kimataifa, taasisi mbalimbali zimeendelea kuhamasisha makundi mbalimbali kuitumia lugha hiyo katika masuala mbalimbali ya kijamii kama vile elimu kuhusu mabadiliko ya tabianchi, uchumi, ukatili wa kijinsia na kadhalika. Miongoni mwa makundi muhimu kufanikisha hayo ni waandishi wa habari ambao wana fursa kubwa ya ushawishi kwa jamii kama asemavyo Fatma Hamad,Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Vijana na Utamaduni katika serikali ya mapinduzi, Zanzibar alipozungumza baada ya kukamilika kwa Kongamano la Idhaa za Kiswahili lililofanyika kwa siku mbili visiwani humo. Fatma Hamad anaanza kumweleza mwenzetu Anold Kayanda aliyehudhuria Kongamano hilo tathmini ya Kongamano lilivyokuwa.
20-3-2023 • 0
20 MACHI 2023
Hii leo katika jarida tunamulika upatikanaji wa huduma za maji na za usafi, siku ya furaha, kongamano la kiswahili Zanzibar, Tanzania na changamoto za maji yatokanyo ziwa Kivu mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.Wakati viongozi wa dunia wakijiandaa kuhudhuria mkutano wa kihistoria wa maji wa Umoja wa Mataifa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF llimetoa wito wa uwekezaji wa haraka katika huduma za maji, usafi na usafi wa mazingira (WASH) zilizo na mnepo ili kuwalinda watoto. Leo ni siku ya furaha duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni siku ya kutabua umuhimu wa furaha kwa watu wote ulimwenguni kwani ni msingi wa lengo la ubinadamu na pia huchagiza ukuaji wa kiuchumiAnold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Fatma Hamad, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Michezo, Vijana na Michezo katika serikali ya mapinduzi Zanzibar kuhusu Kongamano la Idhaa za Kiswahili lililofanyika visiwani humo. Mashinani: Paschal, mtoto mwenye umri wa miaka 15 ambaye kila siku kabla ya kwenda shule anadamkia Ziwa Kivu jimboni Kivu Kaskazini nchini DR Congo kuokota taka ili kuhakikisha wanaoteka maji hawapati magonjwa.
20-3-2023 • 0
UNICEF: Tishio la migogoro inayohusiana na maji linahatarisha maisha ya watoto milioni 190
Wakati viongozi wa dunia wakijiandaa kuhudhuria mkutano wa kihistoria wa maji wa Umoja wa Mataifa, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF llimetoa wito wa uwekezaji wa haraka katika huduma za maji, usafi na usafi wa mazingira (WASH) zilizo na mnepo ili kuwalinda watoto. kulingana na tathimini mpya ya UNICEF “Watoto milioni 190 katika nchi 10 za Afrika wako katika hatari kubwa zaidi kutokana na mchanganyiko wa matishio matatu yanayohusiana na maji ambayo ni ukosefu wa maji ya kutosha, hudumza za usafi na usafi wa mazingira (WASH), magonjwa yanayohusiana na maji na hatari za mabadiliko ya tabianchi.”Shirika hilo limeongeza kuwa tishio hilo la mara tatu limegundulika kuwa baya zaidi katika nchi za Benin, Burkina Faso, Cameroon, Chad, Côte d'Ivoire, Guinea, Mali, Niger, Nigeria na Somalia, na kuifanya Afrika Magharibi na Kati kuwa miongoni mwa nchi zenye uhaba mkubwa wa maji na changamoto za mabadiliko ya tabianchi duniani.Nchi nyingi zilizoathiriwa zaidi, hasa katika Sahel, pia zinakabiliwa na ukosefu wa amani na migogoro ya silaha, ambayo inazidisha changamotpo ya upatikanaji wa maji safi na vyoo kwa watoto.Kwa mujibu wa mkurugenzi wa program wa UNICEF Sanjay Wijesekera "Afrika inakabiliwa na janga la maji. Wakati mabadiliko ya tabianchi na majanga yanayohusiana na maji yanaongezeka duniani kote, hakuna mahali popote duniani ambapo hatari zinazidi kuwa mbaya kwa Watoto kama afrika. Dhoruba, mafuriko ya kihistoria na ukame tayari vinaharibu vifaa na nyumba, yanachafua vyanzo vya maji, kunasababisha njaa na kueneza magonjwa. Lakini kwa jinsi hali ya sasa ilivyo changamoto, bila hatua za haraka, siku zijazo zinaweza kuwa mbaya zaidi."Uchambuzi huu wa kimataifa ambao umetathimini katika ngazi ya kaya fursa za huduma za WASH, mzigo wa vifo vinavyotokana na ukosefu wa huduma za WASH miongoni mwa watoto wa chini ya umri wa miaka mitano, na kukabiliwa na hatari za mabadiliko ya tabianchi na mazingira unaonyesha ni wapi watoto wanakabiliwa na tishio kubwa na ambapo uwekezaji katika suluhu unahitajika sana ili kuzuia ulazima wa vifo zaidi.Katika maeneo 10 yaliyo hatari zaidi, karibu theluthi moja ya watoto hawana japo huduma ya maji ya msingi nyumbani, na theluthi mbili hawana huduma za msingi za usafi wa mazingira.Robo ya watoto hawana chaguo ila kujisaidia haja kubwa katika maeneo ya wazi. Usafi wa mikono pia ni mdogo, ambapo robo tatu ya watoto hawawezi kunawa mikono kwa sababu ya ukosefu wa maji na sabuni nyumbani.Tathimini hiyoi inasema “Kutokana na hali hiyo, nchi hizi pia hubeba mzigo mkubwa zaidi wa vifo vya watoto kutokana na magonjwa yanayosababishwa na huduma zisizotosheleza za WASH, kama vile magonjwa ya kuhara. Kwa mfano watoto 6 kati ya 10 wamekabiliwa na milipuko ya kipindupindu katika mwaka uliopita. Ulimwenguni, zaidi ya watoto 1,000 wa chini ya miaka mitano hufa kila siku kutokana na magonjwa yanayohusiana na huduma za WASH, na karibu Watoto 2 kati ya 5 wapo katika nchi hizi 10 pekee.”Uchambuzi huo mpya umekuja kabla ya mkutano wa maji wa Umoja wa Mataifa wa 2023 utakaofanyika New York Marekani kuanzia tarehe 22-24 Machi. Viongozi wa dunia, mashirika husika na washiriki wengine watakutana kwa mara ya kwanza baada ya miaka 46 kukagua maendeleo ya kuhakikisha upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira kwa wote.
20-3-2023 • 0
Tusaidieni huko DRC ili nasi tuwe na furaha, Wakazi Beni waomba Umoja wa Mataifa
Leo ni siku ya furaha duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni siku ya kutabua umuhimu wa furaha kwa watu wote ulimwenguni kwani ni msingi wa lengo la ubinadamu na pia huchagiza ukuaji wa kiuchumi. Mwandishi wetu wa Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Wa kwanza kuzungumza mjini Beni ambako vikundi vya waasi vimekuwa vikishabulia raia, ni Vakekya Kaswera mama huyu wa watoto 7 akiwa shambani anasema furaha kwake yeye ni shamba lake analolima mihogo. Shambani anapata sombe au kwa kiswahili kisamvu na pia anapata unga wa muhogo. Hata hivyo anasema “furaha yangu inapotea pale mbuzi wanapokuja na kuharibu mazao yangu. Napenda kazi ya kilimo kwa sababu ndio kazi yangu tangu mdogo na inaniweza kutunza familia. Wazazi walitufundisha kulima na pia walitupeleka shuleni.” Mkazi mwingine Serge Kyamundu kwake yeye furaha ni pale enzi hizo ilikuwa inawezekana kupata starehe mjini Beni. “Kwangu ni furaha ni pale ninaona mji wangu uko katika starehe. Miaka iliyopita katika mji wetu wa Beni muziki ulipigwa ilikuwa furaha hakika. Lakini leo hii wakati usalama umemalizika katika mji wetu furaha kwangu imekwisha.” Ametoa wito kwa watu wengine wa nje na serikali za mbali zisaidie kurejesha usalama ili furaha irejee Beni kwani katika siku ya leo ya furaha“watoto wa Beni hatuna hakika furaha kwani tunakosa usalama katika mji wetu.” Naye Sylvie Mbakania, mkulima amesema “furaha yangu ni kutazama mazingira yakiwa mazuri. Ninapoona mbegu zimechipuka hunipatia furaha.” Hata hivyo hivi sasa furaha yake si kamilifu “kwa sababu ya vita katika nchi yetu. Natoa wito kwa Umoja wa Mataifa kufanya juhudi zaidi kurejesha amani ili kukamilisha furaha yangu kama vile mahali pengine wanasherehekea siku hii.” Tarehe 12 mwezi Julai mwaka 2012, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha tarehe 20 ya kila mwaka kuwa siku ya furaha duniani kwa kutambua mchango wake furaha na ustawi kama malengo ya kimataifa na matamanio ya kila binadamu.
20-3-2023 • 0
Wasichana wapatiwe haki zao za elimu bora na wajengewe uwezo wa teknoljia - Elionaora
Kikao cha 67 cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW67 kielekea tamati, mwaka huu 2023 kikiwa kimebeba mada uvumbuzi, mabadiliko ya kiteknolojia, na elimu katika zama hizi za kidigitali kwa ajili ya kufikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana wote. Mijadala mingi katika mkutano huu imelenga kuwawezesha na kuhakikisha watoto wa kike wanaingia kwenye masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati au STEM ili hapo baadaye waweze kuchangia katika ubunifu wa teknolojia katika enzi hizi za dunia ya kidijitali. Kwa muktadha huo, kamisheni hali ya wanawake wakishirikiana na serikali za nchi mbalimbali na mashirika yasio ya kiserikali iliwaalika na kuwajuimisha watoto wa kike katika kikao hicho ili waweze kuwakilisha wanafunzi wenzao, na mmoja wa wanafunzi hao kutoka Tanzania amepata fursa ya kuzungumza na Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa mataifa katika mahojiano kandoni mwa mkutano huo na kumuelezea matarajio yake katika ulimwengu huu wa kidijitali ni yapi, na ana ujumbe gani kwa wasichana wenzake lakini anaanza kwa kujitambulisha..
17-3-2023 • 0
UNICEF: Watoto milioni 10 Sahel ya Kati hatarini, huku ukosefu wa usalama ukitishia janga kusambaa nchi jirani.
Watoto milioni 10 nchini Burkina Faso, Mali na Niger wana uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu, idadi ambayo ni maradufu ikilinganishwa na mwaka 2020, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto duniani, UNICEF hii leo, chanzo kikiwa ni mizozo inayoshamiri kila uchao na kwamba Watoto wengine million 4 nchi Jirani wako hatarini Zaidi kwani mapigano kati ya makundi yaliyojihami na majeshi ya serikali yanavuka mipaka.Tuko Benin na sauti ni ya Abasse, Dahani, mtoto mkimbizi mwenye umri wa miaka 8 kutoka Burkina Faso anasema tulikuja hapa Tanguieta Benin kwa mguu. Tulikimbia nyumbani kwa sababu tulifukuzwa.Abasse anawakilisha mamilioni ya watoto wanaokimbia makwao ukanda wa Sahel kwani Mkurugenzi wa UNICEF kanda ya Afrika Magharibi na Kati Marie – Pierre Poirier anasema “watoto wanazidi kukumbwa kwenye mapigano kama waathirika wa mapigano au walengwa kutoka vikundi vilivyojihami ambavyo si vya kiserikali.”Afisa huyo anatolea mfano Burkina Faso akisema watoto waliothibitishwa kuuawa katika miezi tisa ya mwanzo yam waka 2022 walikuwa mara tatu zaidi kuliko mwaka 2021.Wengi wa watoto hao walikufa kutokanana majerara ya risasi, vijiji vyao kushambuliwa au kulipuka kwa vilipuzi vya kutengeneza au masalia ya mabomu yatumikayo vitani. Bi. Poirier amesema mwaka 2022 ulikuwa wa kikatili Zaidi kwa Watoto Sahel ya Kati na hivyo pande zote kwenye mzozo lazima zikomeshe mashambulizi kwa Watoto, shule zao, vituo vya afya na makazi yao.UNICEF inasema mapigano yanazidi kuwa ya kikatili ambapo baadhi ya vikundi vilivyojihami vinaendesha operesheni zao katika maeneo ya Mali, Burkina Faso na Niger ambako wanatumia mbinu kama vile kuweka vizuizi mijini na vijijini na hata kuharibu mitandao yam aji.Kama hiyo haitoshi, UNICEF inasema kutokana na mashabulizi hayo zaidi ya watu 20,000 kwenye maeneo ya mpaka baina ya Burkina Faso, Mali na Niger watakuwa na kiwango cha kutisha cha ukosefu wa chakula ifikapo mwezi Juni mwaka huu.Vikundi vilivyojihami ambavyo vinapinga elimu inayotolewa na serikali vinatia moto majengo ya shule na kupora mali, vinaweka vitisho, vinateka nyara au kuua walimu.Zaidi ya shule 8,300 zimefungwa katika shule zote kwa sababu zilishambuliwa moja kwa moja na walimu kukimbia au kwa sababu wazazi walikimbia au wanahofia kupeleka watoto wao shuleni.Sasa Abasse na familia yake wako Benin na akiwa darasani akiandika anasema “kwa kuwa sasa naenda shuleni, nimepata marafiki. Napenda kifaransa, nazungumza kidogo. Na mwalimu wangu ni mzuri.”UNICEF inasema janga la Sahel ya Kati bado halijapata ufadhili wa kutosha kuweza kufanikisha operesheni zake kwani mwaka 2022 ilipokea theluthi moja tu ya dol amilioni 391 na kwamba mwaka huu imeomba dola milioni 473 kufanikisha operesheni za kiutu Sahel ya Kati na nchi Jirani. TAGS: Usaidizi wa kibinadamuAdditional: Usaidizi wa kibinadamuNews: Sahel ya KatiRegion: AfrikaUN/Tags: UNICEF
17-3-2023 • 0
Mlipuko wa polio type 2 Burundi yatangaza: WHO
Mamlaka ya afya nchini Burundi leo imetangaza mlipuko na kusambaa kwa virusi vya polio type 2 baada ya wagonjwa wanane kuthibitishwa , ikiwa ni mara ya kwanza kuthibitishwa kwa virusi hivyo baada ya zaidi ya miongo 3 kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO.Taarifa ya WHO iliyotolewa mjini Bunjumbura na Brazzaville imesema virusi hivyo vimethibitishwa kwa mtoto wa kiume wa umri wa miaka minne katika wilaya ya Isale Magharibi mwa Burundi ambaye hajawwahi kupewa chanjo ya polio na pia kwa Watoto wengine wawili waliokutana na mvulana huyo.Pia shitika hilo limeongeza kuwa sampuli tano kutoka kwenye mazingira yam aji machafu zimethiribisha uwepo wa kusambaa kwa virusi hivyo vya polio type 2.Akizungumzia mlipuko huo wa polio mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti amesema “ Kubainika kusambaa kwa vitusi hivyo vya polio Burundi kunadhihirisha ufanisi ya mfumo wa ufuatiliaji wa magonjwa. Polio inaambukiza sana na kuchukuliwa hatua kwa wakati ni muhimu katika kuwalinda watoto kupitia chanjo inayofaa. Tunaunga mkono juhudi za kitaifa za kuongeza chanjo ya polio ili kuhakikisha kuwa hakuna mtoto anayekosa na hakabiliwi na hatari ya kupooza inayotokana na athari za polio.”Serikali ya Burundi ambayo imetangaza mlipuko wa virusi hivyo kuwa ni dharura ya kitaifa ya afya ya umma inapanga kutekeleza kampeni ya chanjo ya kukabiliana na polio katika wiki zijazo, inayolenga kuwalinda watoto wote wanaostahiki wenye umri wa miaka 0 hadi 7 dhidi ya virusi hivyo.Mamlaka za afya, kwa msaada kutoka kwa WHO na washirika wa kimataifa wa mradi wa kutokomeza polio (GPEI), pia wameanza uchunguzi zaidi wa magonjwa, ikiwa ni pamoja na tathmini za hatari ili kubaini ukubwa wa mlipuko huo.Burundi inaimarisha zaidi ufuatiliaji wa polio, huku wataalam wa WHO katika uwanja huo wakiunga mkono ukusanyaji wa sampuli za ziada pamoja na kutathmini uwezekano wa kufunguliwa kwa maeneo mapya ya uchunguzi wa mazingira kwa ajili ya kugunduliwa mapema kwa virusi vya polio vinavyosambaa kimya kimya.Polio type 2 ni virusi vinavyopatikana sana Afrika na kuripotiwa zaidi ambapo kumekuwa na wagonjwa 400 walioripotiwa katika nchi 14 kwa mwaka 2022 pekee.
17-3-2023 • 0
17 MACHI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea habari za WHO nchini Burundi na UNICEF eneo la Sahel. Makala tutamsikia mwanafunzi kutoka Tanzania ambaye ni mshiriki wa mkutano wa 67 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW67 na mashinani tutasalia hapa makao makuu kusikia ujumbe kuhusu haki ya maji.Mamlaka ya afya nchini Burundi leo imetangaza mlipuko na kusambaa kwa virusi vya polio type 2 baada ya wagonjwa wanane kuthibitishwa , ikiwa ni mara ya kwanza kuthibitishwa kwa virusi hivyo baada ya zaidi ya miongo 3 kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO.Watoto milioni 10 nchini Burkina Faso, Mali na Niger wana uhitaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu, idadi ambayo ni maradufu ikilinganishwa na mwaka 2020, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto duniani, UNICEF hii leo, chanzo kikiwa ni mizozo inayoshamiri kila uchao na kwamba Watoto wengine million 4 nchi Jirani wako hatarini Zaidi kwani mapigano kati ya makundi yaliyojihami na majeshi ya serikali yanavuka mipaka.Katika Makala mwanafunzi kutoka Tanzania ambaye ni mshiriki wa mkutano wa 67 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW67 unaomalizika leo, amezungumza na Selina Jerobon wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa mataifa kuhusu kilichomleta kwenye mkutano huu na matarajio yake katika ulimwengu huu wa kidijitali.Na katika mashinani ikimulika ujumbe kuhusu haki ya maji ikiwa ni kuelekea mkutano wa Umoja wa Mataifa wa maji utakaofanyika wiki ijayo hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
17-3-2023 • 0
Jifunze lugha ya Kiswahili: Tofouti ya maneno Yeyote na Yoyote
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tuaelekea visiwani Zanzibar nchini Tanzania ambako mchambuzi wetu Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA anafafanua matumizi ya maneno Yeyote na Yoyote, karibu!
16-3-2023 • 0
16 MACHI 2023
Hii leo jaridani tunanasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kusikiliza mahojiano yetu na viongozi waandamizi wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto huko Zanzibar Tanzania wanaoshiriki mkutano wa 67 wa hali ya wanawake duniani, CSW67 maudhui yakiwa matumizi ya dijitajitali katika zama za sasa za teknolojia kwa lengo la kusaidia wanawake na wasichana na hatimaye jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo hali nchini Malawi baada ya kimbunga Freddy kuzuka nchini humo, Wakimbizi Ethiopia WHO na teknolojia UNCTAD. Katika kjifunza Klugha ya Kiswahili Dkt. Mwanahija Ali Juma anafafanua matumizi ya maneno Yeyote na Yoyote, baki nasi!Nchini Malawi, Umoja wa Mataifa umeendelea kuchukua hatua za usaidizi baada ya Rais wa nchi hiyo Lazarus Chikwera kutangaza hali ya hatari kwenye mkoa wa kusini kufuatia mvua kubwa zilizosababishwa na kimbunga Freddy na katika wiki hii pekee zaidi ya watu 170 wamekufa na 178 wameokolewa.Nchini Ethiopia, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO linaimarisha harakati zake za kuhakikisha wakimbizi wanaokimbia ghasia Somalia na kuingia ukanda wa Dollo ulioko mkoa wa Somali nchini Ethiopia wanapata huduma za afya pamoja na wenyeji wao, wakati huu ambapo idadi yao inaongezeka kila uchao kwani tangu mwezi Februari mwaka huu idadi ya wakimbizi walioingia imefikia takribani laki moja.Na Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara duniani, UNCTAD imesema teknolojia rafiki kwa mazingira ambazo zinatumika kuzalisha bidhaa na huduma zinazidi kushamiri kila uchao na kuongeza fursa za kiuchumi, lakini nchi zinazoendelea ziko hatarini kutonufaika nazo iwapo serikali na jamii ya kimataifa hazitachukua hatua madhubuti.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na tunasalia visiwani Zanzibar nchini Tanzania ambako mchambuzi wetu Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar, BAKIZA anafafanua matumizi ya maneno Yeyote na Yoyote..Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
16-3-2023 • 0
Tumejadili mambo mengi katika Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani - Spika wa Bunge la Tanzania Dkt Tulia Ackson.
Mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani ulioanza tarehe 11 mwezi huu wa Machi na kujumuisha Mabunge ya Nchi Wanachama, Waangalizi wa Kimataifa na Majukwaa mbalimbali ya Kibunge ili kuchagiza Amani na kujenga Jamii Jumuishi na Kuvumiliana umehitimishwa leo tarehe 15 Machi 2023. Katika Mkutano huu Mabunge yameeleza namna ambavyo yameweza kufikia ushirikishwaji wa Vijana, Wanawake na Jamii kwa ujumla katika kulinda amani sambamba na kusisitiza kuheshimu mipaka ya kila mmoja wao. Dhima hii ni msisitizo wa malengo ya Maendeleo Endelevu hususani lengo namba 16 la Umoja wa Mataifa. Zaidi kuhusu yaliyojadiliwa Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson ambaye ni Rais wa Kundi la Kijiografia na Kisiasa la Mabunge ya Afrika anatueleza yale waliyoyajadili katika Mkutano huo halikadhalika mtazamo wake kuhusu ripoti ya hivi karibuni ya IPU kuhusu idadi ya wabunge wanawake duniani.
15-3-2023 • 0
15 MACHI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea tunaangazia vurugu nchini Syria ambapo ni miaka 12 kamili tangu machafuko yalipozuka; na ripoti ya ILO inayosihi nchi zote duniani ziboreshe mazingira ya kazi ya watendaji hao. Makala tutaelekea nchini Bahrain na mashinani nchini Geneva, kulikoni?.Leo ni miaka 12 kamili tangu machafuko yalipozuka Syria na kusababisha vita inayoendelea tangu mwaka 2011 iliyosambaratisha nchi hiyo na mamilioni ya raia wake. Maelfu wamepoteza maisha, mamilioni wamekuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi yao na majanga mengine ya kila uchao yanazidi kuwaondelea matumaini raia wa taifa hilo la Mashariki ya Kati.Baada ya janga la COVID-19 kufichua ni kwa kiasi gani jamii ilikuwa haipatii wafanyakazi muhimu thamani wanayotakiwa ikiwemo malipo ya kutosha na mazingira bora ya kazi, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO limetoa ripoti inayosihi nchi zote duniani ziboreshe mazingira ya kazi ya watendaji hao.Makala tunakupeleka nchini Bahrain katika mji mkuu wa nchi hiyo, Manama ambako mkutano wa 146 wa Umoja wa Mabunge Duniani ulioanza tarehe 11 mwezi huu wa Machi umehitimishwa leo tarehe 15. Spika wa Bunge la Tanzania Dkt. Tulia Ackson ambaye ni Rais wa Kundi la Kijiografia na Kisiasa la Mabunge ya Afrika amezungumza na Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuhusu mambo kadhaa ikiwemo waliyoyajadili katika Mkutano huo.Na mashinani tunakupeleka Geneva, Uswisi kwa Neema Lugangira mshindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mradi bingwa wa kutumia TEHAMA kuboresha afya na lishe miongoni mwa wazee.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
15-3-2023 • 0
Vita ya miaka 12 vimetuacha taaban tukipoteza matumaini: Raia Aleppo Syria
Leo ni miaka 12 kamili tangu machafuko yalipozuka Syria na kusababisha vita inayoendelea tangu mwaka 2011 iliyosambaratisha nchi hiyo na mamilioni ya raia wake. Maelfu wamepoteza maisha, mamilioni wamekuwa wakimbizi ndani na nje ya nchi yao na majanga mengine ya kila uchao yanazidi kuwaondelea matumaini raia wa taifa hilo la Mashariki ya Kati.Adhana hiyo inaashiria ni siku nyingine isiyo na nuru bali iliyoghubikwa na machungu na kupoteza matumaini kwa wakaazi wa Aleppo ambayo ilikuwa mstari wa mbele wa vita, majengo yamesalia magofu ingawa bado kuna watu wanaoishi katika magofu haya.Wwatu wengi waliosalia hap ani wale waliotawanywa na vita inayoendelea kwa mwaka wa 12 sasa akiwemo Sabaha mkimbizi wa ndani aliyepoteza matumaini ya mustakbali bora akisema “Vita ilikuwa ngumu, tumepitia kila zahma kama njaa na mashambulizi ya mabomu. Mume wangu na kaka yangu waliuawa lakini hata wakati huo Maisha yalikuwa kidogo rahisi kuliko sasa”.Kweli yumkini hali si hali, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani nusu ya watu wa silia wanakabiliwa na njaa na wanaishi kwa kutegemea msaada wa wahisani likiwemo shirika hilo wengi wakiishi katika maeneo ya wazi na katika shule. Kenn Crossely ni mkurugenzi wa WFP nchini Syria, "Kuna vitongoji Aleppo ambavyo vimesambaratishwa kabisa na kusalia kuwa vifusi. Maisha yao yote yenye tija, majengo, makazi yao, na maeneo ambayo watu walikuwa wakiishi havipo tena. Kisha tetemeko la ardhi likaja, na watu kutoka huko walilazimika kuhama tena, ilibidi wahamie kwenye mashule, wengine wahamie misikitini. Kulikuwa na jumuiya yenye nguvu ya kiraia, washirika wanaoshirikiana nao, NGO’s zinazofanya kazi ya kuwapa chakula cha moto na makazi, lakini kwa hakika watu wanachokitaka ni maisha yenye tija ,watu waweze kujikimu tene, lakini kila siku wamekuwa wakitegemea kwa kiasi kikubwa misaada ya kibinadamu.”Mdororo wa kiuchumi, ukosefu wa ajira na mfumuko wa bei vimekuwa ni kuongeza chumvi juu ya kidonda kwa wakimbizi hawa wa ndani kama Nawal Shaban “ Hatuwezi kununua chakula cha kutosha kwa watoto wetu vyakula vingi bei haishikiki kama vile nyama na kuku na umeme gharama imekuwa juu pia.”Hata hivyo kuna wale ambao bado wana imani ya nuru kurejea siku moja kama muna ambaye pia ni mkimbizi wa ndani Aleppo “Sasa kilichosalia ni matumaini kwamba vita hii, mgogoro huu ipo siku utakwimu. Nina matumaini makubwa kwamba watoto wangu wataendelea na elimu yao Mungua akipenda.”
15-3-2023 • 0
Boresheni mazingira ya kazi kwa wafanyakazi muhimu: ILO
Baada ya janga la COVID-19 kufichua ni kwa kiasi gani jamii ilikuwa haipatii wafanyakazi muhimu thamani wanayotakiwa ikiwemo malipo ya kutosha na mazingira bora ya kazi, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO limetoa ripoti inayosihi nchi zote duniani ziboreshe mazingira ya kazi ya watendaji hao.Ripoti hiyo ikipatiwa jina Mwelekeo wa Ajira Jamii mwaka 2023: Thamani ya kazi muhimu, inataja makundi manane ambamo kwayo wafanyakazi hao wanapatikana kuwa ni sekta ya afya, chakula, biashara ya rejareja, usafi na huduma za kujisafi, usafirishaji, kazi za mikono, ufundi na ukarani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watendaji katika sekta hizo walitegemewa kuliko ilivyotarajiwa wakati wa janga la COVID-19. Hata hivyo mazingira duni ya kazi na kutothaminiwa kwao kulisababisha wengi kuacha kazi na hivyo huduma za msingi kuvurugika. Ripoti inataka kuboreshwa kwa mazingira ya kazi na uwekezaji mkubwa kwenye sekta hizo kama njia mojawapo ya kujenga mnepo wa mtikisiko wowote. Mathalani katika nchi 90 ambako takwimu zimepatikana, asilimia 52 ya kazi hizo zinafanywa na wafanyakazi hao muhimu ingawa katika nchi za kipato cha juu kiwango ni asilimia 34 pekee. Kutokana na mazingira duni ya kazi wakati wa janga la COVID-19, wafanyakazi wengi muhimu walikufa kuliko wale wasio muhimu. Wanafanya kazi kwa muda mrefu huku ujira ukiwa ni chini ya theluthi mbili ya ujira wa wastani kwa saa. Na katika nchi za kipato cha juu, waajiriwa wengi kwenye sekta hii ni wahamiaji. Mkurugenzi Mkuu wa ILO Gilbert F. Houngbo anasema “watumishi wa sekta ya afya, makeshia wa maduka makubwa ya bidhaa, wasafishaji, mabaharia, wafanyakazi wa afya na wengine kwenye mnyororo wa usambazaji chakula waliendelea kufanya kazi usiku na mchana hata wakati janga lilipokuwa kiwango cha juu na wakati mwingine kwenye mazingira hatari. Kuthamini kazi yao ni kuhakikisha wanapata ujira sahihi na mazingira bora ya kazi. Kazi yenye utu ni lengo kwa wafanyakazi wote lakini ni muhimu zaidi kwa wafanyakazi hawa muhimu ambao wanatoa huduma muhimu nyakati za raha na shida.”
15-3-2023 • 0
14 MACHI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mkutano wa 67 wa hali ya wanawake duniani, CSW67 ukiendelea maudhui yakiwa nafasi ya teknolojia na ugunduzi katika kumsongesha mwanamke tunapata mgeni studio ambaye ni John Nyirenda, kijana huyu, Muasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali la kusongesha ustawi wa vijana nchini Malawi, YouthWAVE Malawi. Pia tunakuletea habari kwa ufupi za UNIDO, WHO na AFSD. Mashinani tutaelekea nchini Ethiopia, kulikoni?.Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda duniani UNIDO kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania Jumatatu wamezindua kiwanda cha kutengeneza barakoa aina ya N95.Tukisalia na afya, shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO limesema mameya na maafisa wengine kutoka Zaidi ya miji 50 kote duniani wanakutana London Uingereza kuanzia leo Machi 14 hadi Machi 16 kushughilikia magonjwa yasio ya kuambukiza NCDs na kuzuia majeraha, katika mkutano wa kwanza wa ushirikiano kwa ajili ya miji yenye afya.Na jukwaa la mataifa la nchi za Kiarabu kwa ajili ya maendeleo endelevu AFSD na kusongesha ajenda ya mwaendeleo ya mwaka 2030, limeanza leo, mwaka huu likibeba mada “Suluhu na Hatua".Na mashinani tutasikia ujumbe kutoka wenyeji nchini Ethiopia kuhusu changamoto zinazowakumba sio tu wakimizi bali pia wenyeji hao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
14-3-2023 • 0
Mitandao ya intaneti kwenye ngazi ya jamii ndio jawabu la kufikisha teknolojia kwa walio pembezoni- Bi. Lugangira
Mkutano wa 67 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW67 ukiendelea na maudhui makuu yakiwa ni namna ugunduzi na teknolojia ya dijitali inaweza kuchangia kumkwamua mwanamke, Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa nayo inaendelea kuzungumza na washiriki ili kufahamu kule watokako hali iko namna gani na nini kinafanyika ili kuhakikisha teknolojia ya kidijitali inatumika kivitendo badala ya kusalia kwenye makabrasha au kumilikiwa na wachache na hivyo kuzidi kuongeza pengo la kidijitali. Miongoni mwa washirii ambao Idhaa hii imezungumza nao ni Neema Lugangira, mbunge wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, nchini Tanzania akiwakilisha mashirika yasiyo ya kiserikali. Katika mahojiano yake na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Bi. Lugangira amezungumzia ni kwa kiwango gani teknolojia ya kidijitali inatumika Bungeni na zaidi ya yote mikakati yake ya kuona intaneti inafikia wengi walio pembezeno. Lakini kwanza anamulika matumizi ya teknolojia kwa ujumla wake nchini Tanzania.
13-3-2023 • 0
Wajumbe wa Baraza la Usalama watamatisha ziara DRC
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametamatisha ziara yao ya siku tatu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC iliyolenga kujadili kwa kina majukumu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO halikadhalika kujionea hali halisi ya amani na usalama.Kupitia mtandao wa Twitter, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, Bintou Keita amesema wajumbe wa Baraza pamoja na kuwa na mazungumzo na viongozi wa ngazi ya juu wa serikali na MONUSCO, walipata pia fursa ya kutembelea maeneo ya Mashariki wa taifa hilo ambako kumegubikwa na mashambulizi kutoka makundi ya waasi. Mathalani walipata fursa ya kusikiliza shuhuda kutoka kwa wawakilishi wa vikundi vya wanawake jimboni Kivu Kaskazini, vikundi ambavyo vinapambania kuheshimiwa kwa haki za wanawake na wasichana waliokumbwa na ukatili wa kingono. Halikadhalika walitembelea kambi ya wakimbizi ya ndani ya Bushagara – Nyiragongo ambako iko karibu na Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.Bi. Bintou ambaye pia ni Mkuu wa MONUSCO amesema katika kambi hiyo maelfu ya wakimbizi wa ndani wako hatarini na mazingira yao yanakabiliwa na changamoto lukuki. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ina takribani wakimbiz iwa ndani milioni 5 na mashambulizi kutoka makundi ya waasi yanazidi kukwamisha maisha yao.
13-3-2023 • 0
13 MACHI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia hitimisho la ziara ya Baraza la Usalama DRC na UN Global Compact Tanzania. Makala tutasalia tunakurejesha hap makao makuu katika mkutano wa CSW67 na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa.Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wametamatisha ziara yao ya siku tatu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC iliyolenga kujadili kwa kina majukumu ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO halikadhalika kujionea hali halisi ya amani na usalama.Nchini Tanzania Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kushirikisha kampuni kuzingatia será na misingi endelevu na inayojali jamii, au kwa kiingereza UN Global Compact Tanzania umeanza kuona mabadiliko katika kushirikisha kampuni kuzingatia misingi 7 ya kumwezesha mwanamke kwenye sekta ya biashara.Makala inaturejesha hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa ambako mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani SCW iumeingia wiki ya pili na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amepata fursa ya kuzungumza na mbunge anayewakilisha asasi za kiraia kutoka Tanzania Neema Lugangira ambaye anashiriki mkutano huo wa kikao cha 67 kuhusu mada kuu ya kikao hicho ubunifu na teknolojia katika kusongesha mbele maendeleo ya wanawake akitaka kufahamu suala hilo linapewa uzito gani Tanzania.Na mashinani tutasikia ujumbe kuhusu unyanyasaji wa kijinsia utokanao na mfumo dume ambao bado umesalia kuwa kikwazo cha maendeleo katika nchi nyingi duniani.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
13-3-2023 • 0
Misingi ya uwezeshaji wanawake yachagizwa na UN Global Compact Tanzania
Nchini Tanzania Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kushirikisha kampuni kuzingatia será na misingi endelevu na inayojali jamii, au kwa kiingereza UN Global Compact Tanzania umeanza kuona mabadiliko katika kushirikisha kampuni kuzingatia misingi 7 ya kumwezesha mwanamke kwenye sekta ya biashara.Jijini Dar es salaam, mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania nashiriki kwenye tukio la Gonga Kengele kwa usawa wa jinsia, mwezi huu wa Machi ambao unamulika masuala ya wanawake. Tukio limeandaliwa na UN Global Compact Tanzania na Mkurugenzi wake Masha Makatta akaeleza sababu. Akimaanisha gonga kengele kwa usawa wa kijinsia katika taifa hili ambalo takwimu za mwaka 2019 kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, NBS zinaonesha ni asilimia 18 tu ya wataalamu walioajiriwa katika Sayansi na Uhandisi ni wanawake. Bi. Makatta akaelezea walichojumuisha kwenye tukio la mwaka huu kwa lengo la kumjumuisha mwanamke. Na je kulikuwa na mafanikio yoyote? Kwa Women Empowerment Principles anamaanisha Kanuni za Uwezeshaji mwanamka ambazo kwa mujibu wa UN Global Compact ziko 7 na miongoni mwao ni kuendeleza elimu, mafunzo na ueledi kwa wanawake. Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Zlatan Milišić, akanieleza hatua ya muda mrefu itakayomuinua zaidi mtoto wa kike, “Umoja wa Mataifa nchini Tanzania una miradi mbalimbali inayoelekea kwenye vipaumbele tofauti vya kazi zetu zinazogusa wanawake. Kuna ambayo ni mahsusi kwa wanawake kwa minajili kwamba hatutaki waachwe nyuma katika maeneo fulani. Lakini mingine ni ya jumla lakini bila shaka inapatia kipaumbele wanawake pale ambako idadi yao ni ndogo.”
13-3-2023 • 0
UNICEF: Watoto katika nchi 11 za Mashariki na Kusini mwa Afrika wako hatarini sababu ya kipindupindu
Nchi 11 Mashariki na Kusini mwa Afrika zinakabiliwa na hali mbaya ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambako hadi sasa kumeripotiwa wagonjwa 67,822 na vifo 1, 788 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.Taarifa ya UNICEF iliyotolewa leo mjini Nairobi, Johannesburg na New york inasema huenda idadi kamili ya wagonjwa na vifo ikawa kubwa zaidi kutokana na changamoto ya mifumo ya ufuatiliaji, utoaji taarifa na unyanyapaa.Nchi mbili ambazo zina mzigo mkubwa zaidi ni Malawi na Msumbuji ambazo shirika hilo linasema “kwa pamoja zaidi ya watu milioni 5.4 wanahitaji msaada wakiwemo watoto zaidi ya milioni 2.8.”Naibu mkurugenzi wa kinanda wa UNICEF Lieke van de Wiel ambaye amehudhuria mkutano wa mawaziri kuhusu kipindupindu mjini Lilongwe Malawi amesema “Tulifikiri ukanda huu hautoshuhudia mlipuko wa kipindupindu wa kiwango hiki cha kusambaa kwa zama hizi. Mifumo duni yam aji na usafi, matukio mabaya ya hali ya hewa, mizozo inayoendelea na mifumo duni ya afya vimezidisha adha na kuweka rehani maisha ya mamilioni ya watoto kote Kusini mwa Afrika.”Msaada wa UNICEF katika ngazi za kitaifa unajumuisha “utoaji wa maji safi na huduma ya usafi, kuweka tembe za kusafisha maji, sabuni za kunawia mikono,dawa za kuongeza maji mwilini, huduma ya kubadili mwenendo wa tabia, na kusambaza ujumbe wa kampeni ya kuishirikisha jamii na zaidi ya hayo UNICEf na washirika wake pia wanatoa msaada wa vifaa vya afya na mahema kwa ajili ya kukabiliana na kiwango kikubwa cha wagonjwa.”Kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali hususani katika nchi zilizoathirika zaidi na kipindupindu sasa “UNICEF inaomba dola milioni 150 kwa aajili ya kuzisaidia nchi zote 11 zilizoathirika ikiwemo dola milioni 34.9 kwa ajili ya Malawi, na milioni dola 21.6 kwa ajili ya Msumbiji kuweza kutoa huduma za kuokoa Maisha kwa watu walioathirika na mlipuko huo.”Hadi sasa washirika wa UNICEF wameshachangia dola milioni 2.9 kukabiliana na mlipuko nchini Malawili na dola 550,000 kwa ajili ya Msumbiji.
10-3-2023 • 0
Kuna haja ya kusaka amani kwa njia ya majadiliano, lasema Baraza la usalama la UN wakiwa ziarani nchini DRC
Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya kutathmini hali ya usalama na utekelezaji wa majukumu ya vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda mamani nchini humo MONUSCO. Mara tu baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa jijini Kinshasa, bwana Nicolas de Rivière, Balozi wa kudumu wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa makundi yenye silaha, vyovyote vile yalivyo, lazima yasitishe operesheni zao ili kushiriki katika mchakato wa amani, “Ni wakati muhimu wakuchukua hatua na kwamba vikundi vyote vyenye silaha, kwa hali yao lazima visitishe shughuli zao na washiriki katika mchakato wa kisiasa. Naomba makundi ya kigeni yajiondoe na makundi yanayoungwa mkono na mataifa ya kigeni pia yajiondoe ili hatimaye amani irejee katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo”.Ujumbe huo umekuja nchini DRC wakati kukitarajiwa kuwa na uchaguzi mkuu wa raisi pamoja na wabunge mwezi decembe mwaka huu huku bwana Michel Xavier Biang Balozi wa Gabon kwenye Umoja wa Mataifa akisisitiza lazima uchaguzi huo uwe wa haki, wa uwazi na salama, “ Tuko katika mwaka ambao utakuwa mwaka wa uchaguzi, ujumbe wetu ni wakuhimiza wanasiasa wa pande zote kushiriki katika mchakato wa uchaguzi ambao ni wa uwazi, na wa kuaminika kwa mujibu wa Katiba ya DRC na sheria ya uchaguzi. Tuko hapa kuunga mkono hatua ya MONUSCO na kukumbusha kwamba MONUSCO ni sehemu ya fursa ya suluhu”.Wajumbe hao watakutana na watu kutoka tabaka mbali mbali ikiwemo mashirika ya kiraia na Rais wa DRC Félix Tshisekedi jijini Kinshasa na baadae watakwenda mjini Goma jimboni Kivu Kaskazini, ambako mapigano yamezidi kurindima kwa miezi kadhaa sasa kati ya jeshi la serikali na kundi la wanamkambo wa M23.
10-3-2023 • 0
Walinda amani wa UN kutoka Tanzania huko DRC wakabidhiana lindo
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC walinda amani kutoka Tanzania kikosi cha 9 wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wanaendelea kushika doria na kulinda raia katika jimbo la Kivu Kaskazini ambapo wiki hii kikosi cha 9, TANZBATT 9 kimemaliza muda wake na kukabidhi majukumu kwa kikosi cha 10, TANZBATT 10. Je nini kimejiri katika makabidhiano hayo ? Kapteni Denisia Lihaya, Afisa habari wa TANZBATT 9 kabla ya kurejea nyumbani ametuandalia ripoti hii ya makabidhiano.
10-3-2023 • 0
10 MACHI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia taarif aya UNICEF kuhusu kipindupindu, na ziara ya Baraza la Usalama DR Congo. Makala tutasalia huko huko DR Congo kushuhudia maadhimisho wa makabidhiano kati ya TANZBATT 9 na TANZBATT 10, na mashinani tukuletea ujumbe kutoka CSW67.Nchi 11 Mashariki na Kusini mwa Afrika zinakabiliwa na hali mbaya ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambako hadi sasa kumeripotiwa wagonjwa 67,822 na vifo 1, 788 kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa umewasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya kutathmini hali ya usalama na utekelezaji wa majukumu ya vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda mamani nchini humo MONUSCO. Mwandishi wetu wa Kinshasa Byobe Malenga amefuatilia kuhusu ziara hiyo na kutuandalia taarifa ifuatayo.Makala tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako huko kikosi cha 9 cha Tanzania kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO kimetamatisha jukumu lake na sasa kimekabidhi majukumu kwa TANZABATT-10 kama anavyoripoti Afisa habari wa kikosi hicho Kapteni Denisia Lihaya.Na mashinani tukuletea ujumbe wa mbunge kutoka Tanzania ambaye anashiriki mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW kikao cha 67 hapa makao makuu wa Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
10-3-2023 • 0
Jifunze Lugha ya Kiswahili: MANYEZI
Katika kujifunza Kiswahili, leo tukipata ufafanuzi wa neno "MANYEZI" kutoka kwa mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA, karibu!
9-3-2023 • 0
09 MACHI 2023
Ni Alhamisi tulivu kabisa ya tarehe Tisa ya mwezi Machi mwaka 2023, siku ya mwisho ya mkutano wa 5 hapa Qatar wa nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani ambapo leo ni mada kwa kina na tutasalia hapa Doha, Qatar ambako katika mkutano waw a 5 wa nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani, LDC5, miongoni mwa washiriki ni vijana ambao walifika hapa kuhakikisha sauti zao zinakuwa sehemu ya maazimio ya mkutano huo. Miongoni mwa vijana hao ni Jadot Nkurunziza ambaye kwa kushirikiana na wenzake wanaunga mkono mkono mradi unaotekelezwa na Rais wa kurejesha misitu nchini Burundi kwa kupanda miti. Pia tunakuletea habari kwa ufupi za kutokoa LDC5 na ripoti ya dawa za kulevya. Katika kujifunza kujifunza Kiswahili , leo tukipata ufafanuszi wa neno "MANYEZI" kutoka kwa mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA.Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Nchi Zenye Maendeleo Duni zaidi duniani, uliokuwa unafanyika mjini Doha Qatar umemalizika jioni ya leo kwa saa za Qatar kwa nchi kuidhinisha hatua madhubuti za kutekeleza Mpango wa Utekelezaji wa Doha (DPoA) - unaolenga kuhuisha na kuimarisha ahadi kati ya nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani LDCs na wadau wao wa maendeleo kuashiria mageuzi kwa nchi zilizo hatarini zaidi duniani.Tukisalia huko huko Doha vijana walikuwa sehemu kubwa ya mkutano huo wa tano wa nchi masikini zaidi duniani LDC ili kuhakikisha sauti zao zinasikika. Humphrey Mrema kutoka taasisi isiyo ya kiserikali ya vijana ijulikanayo kama Youth Survivour Organization ni miongoni mwao na anasema nini ametoka nacho kwenye mkutano huo.Na ripoti mpya ya mwaka 2022 iliyotolewa leo na bodi ya kimataifa ya kudhibiti dawa za kulevya INCB inaonya kwamba kuhalalisha matumizi yasiyo ya kitabibu ya bangi ambayo yanakwenda kinyume na mkataba wa mwaka 1961 wa matumizi ya dawa za kulevya kunaonekana kuongeza kwa kiasi kikubwa matumizi ya dawa hizo na kupunguza uelewa wa hatari zake hususan miongoni mwa vijana.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili ambapo leo nakuleta ufafanuzi wa neno "MANYEZI" kutoka kwa mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
9-3-2023 • 0
Ukiweza kutokomeza umasikini kwa wanawake, basi umeutokomeza kwa jamii: Paricia Makau
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya wanawake, moja ya changamoto kubwa inayowakabili wanawake kote duniani ni umasikini na ndio maana Umoja wa Mataifa uliuweka kutokomeza umasikini kama lengo namba 1 la maendeleo endelevu SDGs. Na unashirikisha na kualika wadau mbalimbali kushirikia katika vita hiyo na wengi wameitikia wito likiwemo shirika la kimataifa la kujitolea lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Voluntary service Overseas (VSO).Patricia Makau ni afisa wa shirika hilo nchini Kenya ambayo yuko hapa kwenye Umoja wa Mataifa kushiriki mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW kikao cha 67. Ameketi na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa na kumueleza ujumbe aliokuja nao katika mkutano huu wa cw67, lakini kwanza anafafanua shirika lao linajikita na nini
8-3-2023 • 0
Chuo Kikuu cha Mtandao cha LDCs kukwamua wanawake
Hii leo ikiwa ni siku ya wanawake duniani maudhui yakilenga ushiriki wa wanawake katika ugunduzi na teknolojia kama njia muhimu ya kuwakwamua kutoka lindi la umaskini, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii amesema ni lazima kuziba pengo la mgawanyiko wa matumizi ya teknolojia kati ya wanawake na wanaume kwa kuwa katika Nyanja hiyo hivi sasa wanawake ni chini ya theluthi moja ya nguvu kazi katika ajira za sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.Amesema Teknolojia inaweza kufungua njia za kupata elimu na fursa kwa wanawake na wasichana. Lakini vile vile inaweza kutumiwa kupazia ukatili na chuki. Nimezungumza na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa aliyeko Doha nchini Qatar kwenye mkutano wa 5 wa nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani, LDC5 kutaka kufahamu iwapo leo siku ya wanawake hoja hii ya Katibu Mkuu imepigiwa chepuo kwa njia moja au nyingine!
8-3-2023 • 0
08 MACHI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia siku ya wanawake duniani, na kilimo Somaliland nchini Ethiopia. Makala tutatatasalia hapa Makao Makuu na mashinani na tutasikia ujumbe wa kutoka kwa FAO kwa ajili ya wanawake hususan wa vijijini kwa siku hii ya wanawake duniani.Hii leo ikiwa ni siku ya wanawake duniani maudhui yakilenga ushiriki wa wanawake katika ugunduzi na teknolojia kama njia muhimu ya kuwakwamua kutoka lindi la umaskini, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake wa siku hii amesema ni lazima kuziba pengo la mgawanyiko wa matumizi ya teknolojia kati ya wanawake na wanaume kwa kuwa katika Nyanja hiyo hivi sasa wanawake ni chini ya theluthi moja ya nguvu kazi katika ajira za sayansi, teknolojia, uhandisi na hisabati.Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO linaendesha mradi wa miaka minne wa mnepo wa uhakika wa upatikanaji wa chakula katika maeneo yaliyoathirika na migogoro pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi katika pembe ya Afrika lengo likiwa ni kujenga amani na kutatua changamoto wanazo kabiliana nazo.Makala inaturejesja makao makuu ya Umoja wa Mataifa panakofanyika mkutano wa 67 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW. Mkutano huo umewaleta Pamoja wadau mbalimbali yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali au NGO. Patricia Makau ni miongoni mwa washiri kutoka Kenya katika shirika la kimataifa la kujitolea lisilo la kiserikali lijulikanalo kama Voluntary service Overseas (VSO)..Na katika mashinani Husna Mbarak Msimamizi wa haki, maliasili na jinsia kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Kenya ametuma ujumbe kwa wanawake duniani kote wahakikishe wanashiriki kwenye kila nyanja ya maisha ili kuleta maendeleo hususan kwenye kilimo..Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
8-3-2023 • 0
Jamii Somaliland zasaidiwa kupambana na uhaba wa chakula: FAO
Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO linaendesha mradi wa miaka minne wa mnepo wa uhakika wa upatikanaji wa chakula katika maeneo yaliyoathirika na migogoro pamoja na athari za mabadiliko ya tabianchi katika pembe ya Afrika lengo likiwa ni kujenga amani na kutatua changamoto wanazo kabiliana nazo.Video ya FAO ikimuonesha Asha Mohammed Ali mama wa watoto 8 na mkulima kutoka wilaya ya Wadaamago huko Somaliland akiwa shambani anapalilia mazao yake huku akisimulia namna ukame ulivyowaathiri wakulima na kuharibu kabisa mustakabali wa maisha yao.Anasema “Mifugo imeathiriwa na ukame na kilimo kimeathiriwa na ukame na hata sisi wenyewe tumeathiriwa sana na ukame”Ili kutatua changamoto zote hizo, FAO inaendesha mradi wa miaka minne kwa ufadhili wa fedha kutoka Uholanzi ambapo wanasaidia kaya 13,000 zilizoko Sool na Sanaang huko Somaliland kwa kuwapatia malisho ya mifugo yao, usaidizi kwenye kilimo pamoja na mbinu bora za kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi.“Kupitia mradi huu katika eneo letu, tulipewa mafunzo ya kuzalisha mazao na matunda, na pia tulikuwa tunapewa trekta kwa saa kadhaa, walituletea mashine za lishe na vifaa vingine na kutujengea kituo cha kuhifadhi mazao. Tulipatiwa ujuzi wa kufanyakazi, kuongeza juhudi, tumefundishwa kuungana na kushirikiana yani tufanye kazi pamoja. Kwakweli tumejifunza mengi kutoka FAO.”Juhudi kama hizi zinawasaidia watu kama Asha kuweza kuendesha maisha yao hata kama wanakabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
8-3-2023 • 0
07 MACHI 2023
Ni Jumanne ya tarehe Saba ya mwezi Machi mwaka 2023, Siku ya pili ya mkutano wa wa 67 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW hapa Umoja wa Mataifa ambapo leo ni mada kwa kina na tutasalia hapa hapa kusikia mbunifu wa teknolojia ya kusaidia wanawake wa pembezeoni kupata haki zao hususan za ardhi. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kimbunga Freddy nchini Msumbiji, wakimbizi Rohingya na machafuko Sudani Kusini. Mashinani tunasalia hapa makao makuu, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO limetoa onyo la mvua kubwa katika saa 36 zijazo Kusini mwa Madagascar wakati kimbunga Freddy kilichoondoka nchini humo kuelekea nchini Msumbiji.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wake 116 wametoa ombi la dola milioni 876 ili waweze kuwasaidia wakimbizi wa Rhohinghya pamoja na jamii za Bangladesh zilizowakaribisha wakimbizi hao.Na Tume ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini Sudan Kusini imetoa ripoti yake hii leo na kueleza kuwa kutokujali ni kichocheo kikubwa cha mgogoro wa haki za binadamu nchini Sudan Kusini, ambao unaendelea kusababisha kiwewe na mateso makubwa kwa raia nchini humo.Na katika mashinani Bi. Sima Bahous, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN Women anatumia mkutano wa 67 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW67 unaoendela hapa makao maku ya Umoja wa Mataifa kupaza sauti juu ya aina mpya ya umaskini.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
7-3-2023 • 0
Tunachotegemea baada ya LDC5 ni ushirikishwaji zaidi wa sisi vijana - Humphrey Mrema na Cosmas Msoma
Kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 50 ya mkutano wa nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani, LDCs, vijana wamepewa kipaumbele cha juu baada ya mkutano huo kushirikisha vijana kutoka katika nchi mbalimbali ili wasaidie kuchangia mawazo ya namna bora ya kuondoa tatizo la uduni wa maendeleo duniani. Miongoni mwa vijana hao ni Cosmas Msoka na Humphrey Mrema ambao ni wawakilishi wa vijana wa Tanzania katika mkutano huo unaofanyika kila baada ya miaka 10 na sasa ukifanyika huko Doha, Qatar. Anold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza nao.
6-3-2023 • 0
06 MACHI 2023
Jaridani leo tunaangazia mkutano wa CSW67 hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa na amani na usalama nchi i DRC. Makala tutaelekea Doha nchini Qatar na mashinani tunasalia hapa makao makuu, kulikoni?Mkutano wa 67 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ukileta pamoja wawakilishi kutoka serikali, mashirika ya kiraia yanayotambuliwa na Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC pamoja na vijana.Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Bintou Keita amesema kwamba mpango wa Umoja wa Mataifa nchini huomo MONUSCO unasisitiza wito wa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa makundi yenye silaha yanayoendesha operesheni zao DRC kuweka chini silaha zao mara moja pasi na masharti yoyote.Katika makala Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa aliyeko Doha Qatar kunakofanyika mkutano wa 5 wa nchi zenye maendeleo duni zaidi duniani, LDCs, yeye amezungumza na vijana Cosmas Msoka na Humphrey Mrema ambao wako kwenye ujumbe wa vijana wanaoshiriki mkutano huo.Na katika mashinani tunasalia hapa hapa Umoja wa Mataifa kukuletea matarajio ya kijana kutoka Tanzania aliyekuja kushiriki mkutano wa hali ya wanawake duniani.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
6-3-2023 • 0
Makundi yenye silaha DRC waweweke chini silaha zao: Keita
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Bintou Keita amesema kwamba mpango wa Umoja wa Mataifa nchini huomo MONUSCO unasisitiza wito wa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa makundi yenye silaha yanayoendesha operesheni zao DRC kuweka chini silaha zao mara moja pasi na masharti yoyote.Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC Bintou Keita amesema kwamba mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO unasisitiza wito wa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa makundi yenye silaha yanayoendesha operesheni zao DRC kuweka chini silaha zao mara moja pasi na masharti yoyote. Mwandishi wetu wa Kinshasa BYOBE MALENGA na tarifa zaidi.Bi Bintou Keita, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini DRC ametoa kauli hio wakati wa mkutano na waandishi wa habari wakati ahitimisha ziara yake mwishoni mwa wiki katika majimbo matatu ya Mashariki mwa nchi amambapo amesema amehuzunishwa sana na hali ya wakimbizi wa ndani,“Nilikuja kuona kwa uhakika athari za kuzorota kwa hali ya usalama katika maisha ya mamia kwa maelfu ya watu walio katika mazingira magumu, wakiwemo wanawake na watoto. Nimetembelea maeneo ya Bushagara na mugwera huko Kivu Kaskazini na KISOGE huko Ituri. Nimekutana na wanawake na wanaume walio katika dhiki lakini ambao bado wana matumaini. Wana nia moja tu ya kurejea kwa amani ili warudi majumbani kwao salama. Haya ni matakwa yetu ya pamoja.” Keita amewataka waasi wa kundi la M23 kuheshimu mkataba wa mwisho wa mkutano mdogo wa kilele uliofanyika mjini Launda nchini Angola ambao unaowataka waasi hao kuondoka na kurejea katika nafasi yao ya awali kwenye Mlima Sabinyo kabla ya Jumanne ya Machi 7 mwaka huu bila masharti kabla ya kutaka mazungumzo yoyote na serikali ya DRC, “Ninakaribisha hatua ya mpatanishi wa Umoja wa Afrika, Rais wa Angola Joao Lourenço, ambayo imefanya Ijumaa kutolewa ahadi ya M23 ya kusitisha mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia Jumanne tarehe 7 Machi saa 12 Jioni. Ninatoa wito kwa vuguvugu hili la waasi wa M23 kuheshimu bila masharti au kusita, masharti ya tamko la Luanda la Novemba 23, ambalo linadai wajiondoe katika maeneo yanayokaliwa, kusitishwa kwa mapigano yote, kuwaondoa wapiganaji wao na kurudi katika eneo lao la awali kwenye Mlima Sabino “. Wito huo unakuja wakati waasi wa M23 wakiteka vijiji kadhaa katika maeneo ya Masisi, Rutshuru na Nyiragongo, hali iliyosababisha zaidi ya watu 600,000 kuyahama makazi yao.
6-3-2023 • 0
Mkutano wa CSW67 yafungua pazia, Mwenyekiti asema hitimisho litakuwa la kijasiri
Mkutano wa 67 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ukileta pamoja wawakilishi kutoka serikali, mashirika ya kiraia yanayotambuliwa na Baraza la Kiuchumi na Kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC pamoja na vijana.Mwenyekiti wa mkutano huo Balozi Mathu Joyini ambaye ni Mwakilishi wa kudumu wa Afrika Kusini kwenye Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari kuwa washiriki ni wanawake kutoka kona mbali mbali za dunia pamoja na vijana na zaidi ya yote na maudhui ni mabadiliko ya ugunduzi na teknolojia na nafasi yake katika zama hizi za kidijitali ili kufanikisha usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake na maudhui amesema yamekuja wakati muafaka.. "Teknolojia za kidijitali zinaleta fursa za kipekee katika kuwezesha wanawake na wasichana. Lakini vilevile zinaleta changamoto mpya kubwa kwa haki za wanawake na wasichana. Teknolojia inaenda kwa kasi lakini mfumo wa maadili duniani bado haujarekebishwa." Hivyo amesema, "Tunatumaini kuwa na hitimisho la kijasiri ambalo linaweka maadili na viwango vya kusongesha mbele ili kuhakikisha wanawake wanawakilishwa kwenye nyanja ya teknolojia. Elimu pia ambayo inawaruhusu kushiriki katika ubunifu na mifumo anuai iliyoko, na kwamba wanawake na wasichana wanapatiwa fursa ya kubuni, kuendeleza na kutumia teknolojia." Mkutano huo ulioanza leo tarehe 6 Machi utamalizika tarehe 17 mwezi huu wa Machi ambapo pia wajumbe watatathmini changamoto na fursa za kufikia usawa wa kijinsia kwa wanawake na wasichana wa vijijini, maudhui yatokanayo na mkutano wa 62 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW62.
6-3-2023 • 0
Matunda ya ubia katika kuhifadhi wanyamapori wazaa matunda pori la Waga Tanzania
Nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa Jumuiya za Hifadhi za WAnyamapori, WMAs, unaotekelezwa kwa pamoja kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii nchini humo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP wa kuzuia ujangili na uhifadhi wa wanyamapori umesaidia jamii kunufaika sio tu na uwepo wa wanyamapori kwenye maeneo yao lakini pia kuishi kwa utangamano na wanyama kwa kuzingatia kuwa leo ni siku ya wanyamapori duniani na ujumbe ni ushirikishaji jamii katika hifadhi ya wanyamapori.Mwenyeji wetu ni Sawiche Wamunza, Mkuu wa Mawasiliano UNDP Tanzania akizungumza na Mwenyekiti na Katibu wa Jumuiya ya eneo la hifadhi ya wanyamapori ya Waga inayojumuisha vijiji vilivyoko mkoa wa Iringa na Mbeya.
3-3-2023 • 0
WHO linasema mtu 1 kati ya 15 duniani wana matatizo ya uwezo wa kusikia
Ikiwa leo ni siku ya kusikia duniani, shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limesema maelfu ya watu duniani wanakabiliwa na changamoto ya kupoteza uwezo wa kusikia katika kiwango cha kuhitaji vipimo na matibabu.Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswis kuhusu siku hii Dkt. Shelly Chadha afisa wa program ya WHO ya kuzuia uziwi na kupoteza uwezo wa kusikia amesema “Karibu mtu 1 katika kila watu 15 duniani kote wanakabiliwa na changamoto ya kiwango fulani cha kupoteza uwezo wa kusikia unaohitaji kufanyiwa vipimo na kupata matibabu. Na kila Watoto 3 kati ya 4 wakati wanapofikisha umri wa miaka 15 ya kuzaliwa wanakuwa wamepata angalau mara moja au zaidi maambukizi ya magonjwa ya masikio ambayo endapo hayatopatiwa tiba yanaweza kusababisha matatizo ya muda mrefu ya masikio, kupoteza uwezo wa kusikia na wakati mwingine athari zinazotishia maisha yao.” Dkt. Chadha ameoneza kuwa ijapokuwa matatizo ya masikio na kusikia ni baadhi ya hali zinazojitokeza sana katika jamii, huduma za matatizo haya hubakia tu katika ngazi ya kiwango cha juu na hutolewa na wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu kama vile wa sikio, pua na koo (ENT) na wataalam wa sauti. “Hii ina maana kwamba watu wanaopata magonjwa haya ya masikio au kupata upotevu wa uwezo wa kusikia mara nyingi hulazimika kusafiri umbali mrefu na kuingia gharama kubwa mifukoni mwao ili kupata huduma wanazohitaji katika kliniki na hospitali maalum.” Na kwa mujibu wa WHO kinachoongeza changamoto hii “ni ukweli kwamba duniani kote, kuna uhaba wa wataalamu wa huduma ya masikio na kusikia wenye ujuzi unaofaa.” Mathalani shirika hilo limesema nchi nyingi za kipato cha chini au cha kati zina chini ya mtaalam mmoja wa masikio na kuiskia ENT na mtaalam mmoja wa masuala ya sauti katika kila watu milioni 1 hali ambayo inaleta tishio kubwa la kiafya ambalo linaweza kushughulikiwa tu kupitia urekebishaji wa mfano wa utunzaji na ujumuishaji wa huduma zinazohitajika katika kiwango cha msingi. Limependekeza kuwa “Wahudumu wa afya wanaofanya kazi katika ngazi ya msingi, kama vile madaktari, wauguzi, na wahudumu wa afya wa jamii lazima wawezeshwe kwa mafunzo, maarifa, ujuzi na zana husika ili kukidhi mahitaji ya wagonjwa.” Na ili kuunga mkono juhudi hizi, WHO leo imetoa mwongozo mpya wa mafunzo ya huduma ya masikio na usikivu ambayo inaweza kuzisaidia nchi katika kujenga uwezo wa wafanyakazi wao wa afya kutoa huduma hizi katika ngazi ya jamii. Maudhui ya siku ya kusikia duniani mwaka huu ni “ Sikio na huduma ya masikio kwa wote hebu tuifanye kuwa hali halisi” na siku hii huadhimishwa kila mwaka Machi 3.
3-3-2023 • 0
Misaada sio jibu kwa nchi zenye maendeo duni - Rahab
Kuanzia siku ya jumapili tarehe 5 mpaka 9 ya mwezi huu wa Machi, huko Doha nchini Qatar viongozi kutoka kila pembe ya dunia watakutana katika mkutano wa tano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zenye maendeleo duni- LDC5 ili kukubaliana na kuangalia namna ya kuzisaidia nchi hizo ziweze kustawi wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na changamoto lukuki.Kimsingi mkutano huo wa LDC5 unazileta pamoja nchi 46 zenye maendeleo duni zaidi duniani, na kuzikutanisha na nchi nyingine duniani pamoja na wadau wa maendeleo.Akizungumza katika mahojiano maalum na idhaa ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kuelekea mkutano huo, Bi. Rabab Fatima, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa nchi zenye maendeleo duni, zisizo na bahari na visiwa vidogo amesema dunia inapaswa kujali masuala ya nchi hizo kwani zimeachwa nyuma zaidi.Bi. Rabab anasema “Ni muhimu sana kwa dunia nzima kusaidia LDCs kuwa endelevu zaidi na zisiwe tegemezi kwa misaada. Na ni muhimu sana tuwasaidie kupata nafuu, kuwajengea uwezo wa kustahimili, ili waweze kupunguza utegemezi wao kwa dunia nzima.”Mwakilishi huyo wa Umoja wa Mataifa kwa nchi hizo duni amesema kwa miaka mingi zimekuwa zikitegea misaada zaidi, na imedhihirika misaada sio jibu la maendeleo.“Bila shaka jibu ni, kujenga uwezo wa LDCs wenyewe kuwa wanazalisha mapato yao wenyewe. Mapato ya ndani, mapato yote. Biashara ni jibu linalofuata. Uwekezaji ni jibu linalofuata. Nchi hizo nyingi zimejaliwa kuwa na wingi wa maliasili pamoja na rasilimali watu, idadi kubwa ya vijana duniani wako katika nchi hizo zenye maendeleo duni.”Wakati mkutano huo ukianza hapo kesho kutwa Bi. Rabab Fatima ametoa wito kwa nchi zenye maendeleo duni sio tu kuhudhuria mkutano huo bali kushika usukani wa kuendesha mijadala na kushughulikia ahazi zao za kusonga mbele pamoja na kuhakikisha wadau wao na jumuiya ya kimataifa nazo zinashiriki kikamilifu na kuweka ahadi za kuwasaidia kusonga mbele.Nchi hizo ni Afghanistan; Angola; Bangladesh; Benin; Bhutan; Burkina Faso; Burundi; Kambodia; Jamhuri ya Afrika ya Kati- CAR; Chad; Comoro; Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo -DRC; Djibouti; Eritrea; Ethiopia; Gambia; Guinea; Guinea-Bissau.Nyingine ni Haiti; Kiribati; Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Lao; Lesotho; Liberia; Madagascar; Malawi; Mali; Mauritania; Msumbiji; Myanmar; Nepal; Niger; Rwanda; Sao Tome na Principe; Senegal; Sierra Leone; Visiwa vya Solomon; Somalia; Sudan Kusini; Sudan; Timor-Leste; Togo; Tuvalu; Uganda; Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Yemen na Zambia.Vanuatu ilikuwa nchi ya hivi karibuni kutoka katika orodha ya nchi hizo na iliondolewa mwishoni mwa mwaka 2020.
3-3-2023 • 0
03 MACHI 2023
Jaridani leo tunaangazia afya na hali ya kiuchumi katika nchi zenye maendeleo duni- LDC5. Makala tutaelekea nchini Tanzania na mashinani nchini Sudan, kulikoni?Ikiwa leo ni siku ya kusikia duniani , shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limesema maelfu ya watu duniani wanakabiliwa na changamoto ya kupoteza uwezo wa kusikia katika kiwango cha kuhitaji vipimo na matibabu.Kuanzia siku ya jumapili tarehe 5 mpaka 9 ya mwezi huu wa Machi, huko Doha nchini Qatar viongozi kutoka kila pembe ya dunia watakutana katika mkutano wa tano wa Umoja wa Mataifa wa nchi zenye maendeleo duni- LDC5 ili kukubaliana na kuangalia namna ya kuzisaidia nchi hizo ziweze kustawi wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na changamoto lukuki.Katika makala tunakwenda nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori, WMAs, unaotekelezwa kwa pamoja kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii nchini humo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo duniani, UNDP wa kuzuia ujangili na uhifadhi wa wanyamapori umesaidia jamii kunufaika sio tu na uwepo wa wanyamapori kwenye maeneo yao lakini pia kuishi kwa utangamano na wanyama kwa kuzingatia kuwa leo ni siku ya wanyamapori duniani na ujumbe ni ushirikishaji jamii katika hifadhi ya wanyamapori.Na katika mashinani na tutaelekea nchini Sudan kusikia njia mbadala za kuhakikisha usalama wa chakula na kuondokana na umaskini kwa jamii ambazo zilikuwa zinategemea upatikanaji wa ardhi, maji na malisho ya mifugo wengi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
3-3-2023 • 0
Msemo: Kauka nikuvae sanduku msumari
Katika kujifunza Kiswahili, leo tunafafanuliwa maana ya msemo "KAUKA NIKUVAE SANDUKU MSUMARI" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Karibu!
2-3-2023 • 0
02 MACHI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia mada kwa kina na ninakupeleka nchini Zimbabwe kumulika harakati za uhifadhi wa wanyamapori, ikiwa ni kuelekea siku ya wanyamapori duniani hapo kesho. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo UNICEF, WHO na UNECE. Na leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, je wajua maana ya msemo "KAUKA NIKUVAE SANDUKU MSUMARI"? Baki nasi!Watoto milioni 3.7 ambao walinusurika na matetemeko ya ardhi ya tarehe 6 Februari mwaka huu katika maeneo yaliyoathirika nchini Syria wanakabiliwa na ongezeko la vitisho kadhaa vya janga kubwa, amesema leo Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF, Catherine Russell akihitimisha ziara yake ya siku mbili nchini humo.Shirika la Afrya la Umoja wa Mataifa duniani WHO limesema limeonya leo kwamba ingawa idadi ya wagonjwa wa kipindupindu ya kila wiki katika nchi zilizoathirika na mlipuko wa ugonjwa huo barani Afrika inapungua, lakini mafuriko makubwa yanayotokana na mvua za msimu na vimbunga vya kitropiki kusini mwa Afrika yanaongeza hatari ya ugonjwa huo kuenea na kutishia kudhoofisha juhudi za kuudhibiti.Na tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi barani Ulaya UNECE leo imesema kufuatia mfano wa nchi kadhaa katika za ukanda wa Ziwa Chad barani Afrika , Niger imethibitisha rasmi nia yake ya kujiunga na mkataba wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya ulinzi na matumizi ya maji ya ya mipaka na maziwa ya mimataifa, unaojulikana zaidi kama “Mkataba wa Maji”. Na katika kujifunza Kiswahili , leo tunafafanuliwa maana ya msemo "KAUKA NIKUVAE SANDUKU MSUMARI" na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania , BAKITA.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
2-3-2023 • 0
Baada ya hofu kubwa ya soko Peru, IFAD yaleta matumaini makubwa
Miaka miwili iliyopita, wakulima nchini Peru walikuwa na hofu ya kwamba janga la COVID-19 lingalifuta kabisa masoko yao waliyozoea kuuza mazao kama vile kakao na malimao. Walizoea kuuza sokoni lakini COVID-19 ilifuta masoko hayo kutokana na vizuizi vya kutembea.Hata hivyo Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD kupitia mradi wa kuchechemua kilimo vijijini baada ya COVID-19 ulileta nuru na sasa wakulima hawaamini kile wakipatacho. Ni kwa vipi basi? Ungana na Assumpta kwenye makala hii iliyoandaliwa na IFAD.
1-3-2023 • 0
UNICEF: Kila msichana anastahili fursa nyingine ya elimu hata kama alijifungua akiwa shuleni
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na serikali ya Uganda kupitia msaada wa serikali ya Ireland, unawapa fursa ya pili ya kurejea shuleni wasicha waliopata ujauzito na waliojifungua kabla ya kumaliza masono katika jimbo la Karamoja nchini Uganda. Lengo kuu la mradi huo ni kuhakikisha hakuna msichana yeyote anayesalia nyuma kielimu hata kama amekuwa mama katika umri mdogo.Jimbo la Karamoja lililoko Kaskzini Mashariki mwa Uganda linakabiliwa na changamoto kubwa ya wasichana kupata mimba za utotoni na wengi hujikuta wakikatisha ndoto zao za kuendelea na masomo baada ya kujifungua. Lakini sasa mradi wa UNICEF wa “Kutomwacha msichana yeyote nyuma” umewapa nafasi ya pili ya kutimiza ndoto zao kielimu. Joyce Opel ni mwalimu mkuu katika shule ya Napak ambayo ni miongoni mwa shule zinazoshiriki mradi huo wa UNICEF anasema, “Nina kina mama hawa wenye umri mdogo13 , lakini wanapaswa kuwa 17, bado nasubiri wengine kujiunga, baadhi yao walipewa mimba na kutelekezwa bwana zao hawako wamebaki wakilea watoto peke yao, na hicho ndicho kilichonisukuma Kwenda kuongea nao , na nikisha ongea nao na wakaelewa wanarejea shuleni"Ameongeza kuwa pamoja na fursa hiyo kuna changamoto, “Changamoto zinazowakabili kina mama hawa wadogo shuleni ni moja, watoto wao wakiugua basi inabidi wakose masomo, na ndio maana nawachagiza waalimu kuwavumilia ili wakati wanaporejea basi wawasaidie kuanzia pale walipoishia.” Mradi huu umeleta tija Karamoja kwani kufikia mwishoni mwa mwaka 2022 julma ya kina mama watoto 1226 na wasichana wajawazito 296 walisaidiwa kurejea shuleni jimboni humo. kwa mujibu wa Sambey Logira mtaalam wa elimu wa UNICEF “miongoni mwa wasichana hao waliorejea shuleni walifanya mitihani ya kumaliza elimu ya msingi na walifanya vizuri kuliko hata wale waliokuwepo shuleni wakati wote. Na tumaini ni kuhakikisha wanapiga hatua nyingine zaidi katika elimu yao.”. La msingi kwa Solome Aisia ambaye ni mkufunzi katika kituo cha uratibu wa mradi huo Napak ni kutowahukumu wasicha hawa kwa kufanya makosa ya kuzaa utotoni”...anassema ni muhimu sana kutoangalia makosa ya mtu bali suluhu au jinsi gani ya kumsaidia mtu huyo, na daima kuna fursa ya pili. Kama tusingewapa kina mama hawa watoto fursa basi tungekuwa tumewapoteza.” Kwa UNICEF lengo ni kuhakikisha mradi huu unawafikia wasichana wengi zaidi na kurejesha matumaini na ndoto zao za maisha.
1-3-2023 • 0
01 MACHI 2023
Hii leo jaridani tunaangazia ziara za Guterres nchini Iraq na mimba za utotoni nchini Uganda. Makala tunaangazia matumaini kwa wakulima ambao walikuwa wamekata tamaa na mashinani tamko la watoto…Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefanya ziara nchini Iraq lengo likiwa ni kusisitiza mshikamano na kuunga mkono juhudu za nchi za kuleta amani ,haki za binadamu na maendeleo endelevu.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kushirikiana na serikali ya Uganda kupitia msaada wa serikali ya Ireland, unawapa fursa ya pili ya kurejea shuleni wasicha waliopata ujauzito na waliojifungua kabla ya kumaliza masono katika jimbo la Karamoja nchini Uganda.Makala tunaangazia ni kwa vipi mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD umerejesha matumaini kwa wakulima waliokuwa wametaka tamaa.Na katika mashinani tutaelekea nchini Tanzania kupata tamko la watoto kutoka nchi 80 waliowakilisha watoto wa dunia nzima katika mkutano wao Septemba mwaka jana nchini Demark.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
1-3-2023 • 0
Katibu Mkuu Guterres ziarani nchini Iraq
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amefanya ziara nchini Iraq lengo likiwa ni kusisitiza mshikamano na kuunga mkono juhudu za nchi za kuleta amani ,haki za binadamu na maendeleo endelevu.Ziara ya mwisho ya Katibu Mkuu Guterres nchini Iraq ilikuwa miaka sita iliyopita, na alipofika Baghdad alipokelewa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya nje Fued Hussein ambapo walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari.Katika hotuba yake Katibu Mkuu Guterres aliipongeza serikali ya Iraq kwa kuwaruhusu wananchi wa Iraq walio nje ya nchi hiyo kurejea na kusema Umoja wa Mataifa unaunga mkono kikamilifu juhudi zote za kuhakikisha nchi hiyo inakuwa na mustakabali wa amani na ustawi na taasisi zake zinaunganishwa na demokrasia.Katika mkutano huo pia alizungumzumzia changamoto zinazowakabili wananchi wa nchi hiyo ikiwemo uhaba wa maji na athari za mabadiliko ya tabianchi na kusema “Moyo wangu unavunjika nikiona wakulima wanaacha ardhi zao na mazao ambayo wamekuwa wakilima kwa milenia. Uhaba wa maji nchini Iraq umechangiwa na kupungua kwa uingiaji kutoka nje, usimamizi usio endelevu wa maji, na sasa athari za mabadiliko ya tabianchi. Ni tishio linalohitaji umakini wa kimataifa.”Katika kupata suluhu kwenye changamoto hiyo amesema mkutano Umoja wa Mataifa wa Maji utakaofanyika baadae mwezi huu jijini New York, Marekani utajadili mengi kuhusu changamoto ya maji huku akidhibitisha kuelewa ni kwa namna gani suala ya uhakika wa maji ni muhimu kwa nchi hiyo.Katika ziara yake hiyo, Katibu Mkuu atakutana na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Waziri Mkuu Mohammed Shia’ Al Sudani.Akiwa katika mji mkuu, Katibu Mkuu pia atakutana na kuwasikiliza wawakilishi wa vikundi vya haki za vijana na wanawake na kufanya mkutano na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.Hapo kesho Katibu Mkuu Guterres atatembelea kambi ya Wakimbizi wa Ndani na Kituo cha Urekebishaji kilichoko kaskazini mwa nchi hiyo na kufanya mazungumzo na wakazi wa kituoni hapo.Kisha ataenda Erbil na kukutana na maafisa wa Serikali ya Mkoa wa Kurdistan.
1-3-2023 • 0
28 FEBRUARI 2023
Hii leo jaridani mada kwa kina ambayo leo inatupeleka Kenya kuangazia umuhimu na faida za lugha mama. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo ukame Pembe ua Afrika, wakimbizi nchini Somalia na watoto waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Uturuki . Mashinani tutakupeleka nchini Yemen, kulikoni?.Ukanda wa Pembe ya Afrika ukiingia msimu wa sita bila mvua, ukimbizi wa ndani unazidi kushamiri kwa kuwa mamilioni ya watu kutoka Somalia, Ethiopia na Kenya wanaendela kuhaha katikati ya uhaba wa maji, njaa, ukosefu wa usalama na mizozo, amesema Olga Sarrado, msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR akizungumza na waandishi wa habari hii leo huko Geneva, Uswisi.Tukisalia Pembe ya Afrika, hususan Somalia, shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM limesema idadi ya wakimbizi wa ndani nchini Somalia ikifikia kiwango cha juu cha watu milioni 3.8, shirika hilo linategemea uwekezaji wa wahisani kwenye majawabu ya kuepusha zaidi ukimbizi wa ndani na kushughulikia mazingira duni ya maisha kwa mamilioni ya walioathiriwa na ukame na mzozo unaoendelea nchini humo.Na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Catherine Russell amehitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Uturuki na kusema watoto milioni 2.5 wanahitaji msaada wa dharura kufuatia matetemeko makubwa ya ardhi yaliyokuba kusini-mashariki mwa nchi hiyo na kaskazini mwa Syria mapema mwezi huu.Na katika mashinani tutaelekea Aden nchini Yemen ambako huko Bi. Fatima Muhammed Saeed mkimbizi wa ndani mwenye umri wa miaka 35 na mama wa watoto 9 anasema hapo awali kabla ya kukimbia vita maisha yalikuwa mazuri lakini sasa wanaishi maisha ya aibu na magumu mpaka hata kupata utapiamlo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
28-2-2023 • 0
Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wametufundisha kutumia majembe – Wakulima CAR
Wananchi wa Kijiji cha Difolo katika viunga vya mji wa Berberati mkoa wa Mambéré-Kadéï nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wamewashukuru walinda amani wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania kinachohudumu chini ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo (MINUSCA) baada ya wanalinda amani hao kuwafundisha wananchi hao kulima kwa kutumia jembe la mkono badala ya kulima kwa kutumia panga. Kapteni Mwijage Francis Inyoma ni Afisa Habari wa kikosi hicho ameandaa makala hii.
27-2-2023 • 0
Mradi wa ILO wawezesha wanawake wa kimasai Kenya kujua kusoma, kuandika na kuanzisha biashara
Nchini Kenya, mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO wa ubia wa maendeleo kati ya sekta ya umma na binafsi, PPDP umewezesha wanawake wa jamii ya kimasai katika eneo la Rift Valley kujiinua kiuchumi na kijamii. Thelma Mwadzaya na ripoti kamili kama ilivyoandaliwa na ILO.Mmoja wa wanufaika hao ni Mary Nkisonkoi kutoka kijiji cha Oloshaiki kilichoko eneo la Rift Valley au Bonde la Ufa nchini Kenya.Mary kupitia video ya ILO anasema alikuwa na bahati sana kuchaguliwa kuwa mwezeshaji wa jamii katika mradi wa PPDP.“Kabla ya mradi huu kuanza, wanawake katika eneo letu hawakuwa wanakutana na kuzungumza kwa uwazi na kina matatizo na changamoto zinazowakabili. Hatukuruhusiwa kufanya hivyo labda pale tu ambapo waume zetu walifahamu kile ambacho kinajadiliwa,” anasema Mary.Walikuwa wamezoea kusalia kijijini na kukutana kanisani na baada ya ibadi kila mtu anarejea nyumbani na kuendelea na wajibu wake wa kifamilia. Hatukufahamu kuwa sisi wanawake na akina mama tunaweza kufanya kitu na kusaidia kama jamii au kama wanawake.PPDP ikabisha hodi OloshaikiMradi wa PPDP ukaingia na ukaanza kufundisha wanawake kuhusu jinsia, haki za wanawake na tofauti kati ya mke na mume.“Hii ilituhamasisha kuzungumza na wanaume wetu,” anasema Mary huku akiongeza kwamba alifundishwa kuwa mwezeshaji ili kuwaleta pamoja wanawake na wanaume katika majukwaa ya umma. “Niliwaita wazee wa kijiji, wanawake, viongozi wa vikundi vya kijamii ili kujadili ni jambo gani lifanyike ili kuinua eneo letu.”Mabadiliko chanya ya kujivuniaMary anasema mabadiliko ya kwanza kutokea na ambayo anajivunia ni pale wanawake walipoweza kupata elimu ya watu wazima. “Tulifundishwa na mwalimu kutoka mradi wa PPDP. Tulifundishwa pia jinsi ya kuendesha biashara.”Wanawake wengi walijiunga na darasa kwa sababu “hatukuwa na njia nyingine ya kujipatia kipato. Kwa asili, wanawake hawawezi kuuza ng’ombe au mahindi kwa sababu shamba ni mali ya mume.”Walijipanga vema ili wasikose darasaMary anasema mwanzoni ilikuwa changamoto, lakini walijifunza kujipanga mapema kuhakikisha majukumu ya nyumbani na uchungaji wa mbuzi na ng’ombe unafanyika asubuhi. Ikifika saa 8 adhuhuri watoto wanaporejea nyumbani kutoka shuleni, wanawake walienda darasani.“Wanawake walijifunza alfabeti pamoja nan amba na matokeo yake waliweza kutumia simu za rununu au za kiganjani,” anasema Mary.Baada ya kujua kusoma na kuandika, nini kilifuatia?Mwezashaji huyu wa jamii anasema baada ya darasa la elimu ya watu wazima, walifikiria ni nini tena wanaweza kufanya na kuleta mabadiliko zaidi.“Tulianzisha kikundi cha upatu. Siku yetu ya soko ni jumatano ambako wanawake wanauza maharage, viazi au mboga za majani. Tuliamua kukutana kila Alhamisi baada ya siku ya soko na kila mwanamke alete dola senti 40 au dola senti 81. Na iwapo mwanamke anataka kukopa fedha kukuza biashara yake, tunamkopesha na atarejesha na riba. Kisha tutampatia tena mwanamke mwingine akuze biashara yake.” Mafanikio mengine sasa wanaume wamepata uelewa wa kuwapatia wake zao nafasi na fursa kwa sababu Mary anasema, “nilipoketi nao kama mwezeshaji, niliwaeleza kuwa akina mama nao wanaweza kuleta kipato nyumbani, wakalipa karo na hata kununua chakula.”Sasa anasema wako huru kuanzisha na kumiliki biashara. Kila mwanamke anaweza kupeleka kitu nyumbani na kuweka mezani, hata kiwe kidogo kiasi gani.Hata shilingi 500 za Kenya saw ana dola 4.10. Tunawaambia waume zetu hiki ndicho nilichopata,” anasema Mary akiongeza kuwa hayo ni mabadiliko makubwa na hatuishi kama tulivyokuwa tunaishi zamani. Mary anasema “ninajiambia katika biashara yangu siku moja nitakuwa miongoni mwa nyota zinazong’ara kwenye eneo hili.” Kupitia ujasiriamali wa kukuza ng’ombe bora, Mary ameweza kujenga nyumba yake na anatamatisha akisema, “wanawake si watu wa kukandamizwa. Pale mwanamke anapoelimishwa, jamii itanufaika zaidi. Kwa hiyo…
Wahisani wa kimataifa wanakutana leo mjini Geneva UswisI kwa ajili kutanabaisha kuhusu zahma ya kibinadamu inayoendelea nchini Yemen na kuchangisha fedha za kufadhili operesheni za kibinadamu nchini humo. Mkutano huo wa ngazi ya juu wa kuchangisha fedha kwa ajili ya Yemen umeandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na serikali za Sweden na Uswis. Flora Nducha na taarifa kamili Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa Yemen inasalia kuwa moja ya migogoro mikubwa zaidi ya kibinadamu duniani , na baada ya miaka mingi ya vita inaendelea kuwa na dharura kubwa kibinadamu kwani watu zaidi ya milioni 21 au theluthi mbili ya watu wote katika taifa hilo la Mashariki ya Kati watahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi mwaka huu 2023. Sababu kubwa za kuendelea kwa mgogoro wa kibinadamu mbali ya vita ni kudorora kwa uchumi na kusambaratika kwa huduma za msingi. Umoja wa mataifa pia umesema Yemen iko katika kitovu cha mgogoro wa mabadiliko ya tabianchi ikikabiliwa na majanga ya asili ya mara kwa mara kama ukame wa kupindukia na mafuri yanayotishia maisha ya watu, usalama na ustawi wao. Mashirika ya misaada ya kibinadamu “Yanahitaji dola bilioni 4.3 mwaka huu 2023 ili kusaidia watu milioni 17.3 kote nchini kwani bila msaada endelevu kwa operesheni ya misaada nchini Yemen, maisha ya mamilioni ya Wayemen yatabaki hatarini na juhudi za kumaliza mzozo huo mara moja zitakuwa ngumu zaidi.” Amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na kuongeza kuwa "Jumuiya ya kimataifa ina uwezo na mbinu za kumaliza mgogoro huu. Na huanza kwa kufadhili ombi letu kikamilifu na kuahidi kutoa fedha haraka. Kwa pamoja, hebu hatimaye tugeuze wimbi hili la mateso. Tuwape matumaini watu wa Yemen.” Kwa upande wake, mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura, Martin Griffiths, amesema: "Ulimwengu unakutana tena leo kudhihirisha dhamira yake ya kuwasaidia watu wa Yemen kujinasua kutoka katika mgogoro huu mbaya. Hiyo ina maanisha ni kuendelea, na kwa kweli kuongeza maradufu, juhudi za kutafuta suluhu ya amani. Inamaanisha kufadhili operesheni za misaada ili programu za kuokoa maisha ziweze kuendelea kuzuia hali mbaya zaidi. Na inamaanisha kusaidia mashirika ya misaada yanapofanya kazi kuchukua hatua za kukabiliana na mgogoro huo nchini kote.” Mwaka 2022 wahisani walitoa dola zaidi ya bilioni 2.2 ambazo ziliwezesha mashirika ya misaada ya kibinadamu kuwafikia karibu watu milioni 11 nchini humo kila mwezi kwa misaada ya kuokoa maisha ikiwemo chakula, maji safi, malazi, ulinzi na elimu.
27-2-2023 • 0
27 FEBRUARI 2023
Hii leo katika jarida la UN Anold Kayanda anamulika:Mkutano wa kimataifa wa kuchangisha fedha kwa ajili ya Yemen unaofanyika Geneva, USwisiNchini Kenya mradi wa ILO wajengea wanawake wa kimasai uwezo wa kushiriki shughuli za kiuchumi na kijamii na sasa wanaweza sio tu kusoma bali pia ni wajasiriamali.Makala anakupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR huko walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wafundisha wakulima matumizi ya jembe la mkono kwenye kilimo badala ya panga.Mashinani Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri nchini Tanzania na ujumbe wake kwa wazazi kuhusu malezi sahihi kwa watoto.Karibu!
27-2-2023 • 0
Mwaka mmoja wa uvamizi wa Urusi Ukraine, UN yataka vita ikome
Hii leo ni mwaka mmoja tangu Urusi ivamie Ukraine! Ndani ya mwaka mmoja wa uvamizi huo, zaidi ya watu 8,000,000 wamekimbia nchi hiyo, zaidi ya 5,000,000 ni wakimbizi wa ndani ilhali theluthi moja ya wananchi wote hawako kwenye makazi yao. Watu milioni 17.6 wanahitaji msaada wa dharura wa kibinadamu ambapo zaidi ya milioni 16 wameshafikiwa na msaada muhimu. Nini kimetokea katika mwaka huo mmoja? Umoja wa Mataifa umechukua hatua gani kufikia wahitaji? Assumpta Massoi anasimulia katika makala hii.
24-2-2023 • 0
Viongozi watoa maoni yao dhidi ya Urusi baada ya uamuzi wa Baraza Kuu la UN
Vita ya Ukraine ikiwa inaingia mwaka wake wa pili, wawakilishi mbalimbali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wametoa maoni yao kufuatia uamuzi kwa njia ya kura uliofanywa na Kikao Maalumu cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio jipya la kutaka amani ya haki na ya kudumu nchini Ukraine na kwamba Urusi bila masharti yoyote iondoe mara moja majeshi yake katika ardhi ya Ukraine. Umaalumu wa kikao hiki cha siku mbili kilichokamilika jana jijini, New York, Marekani ni kwa mujibu wa azimio lilipotishwa mwaka 1950 na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwamba Baraza hilo linaweza kushughulikia masuala ya kimataiafa yanayohusu amani na usalama pale ambapo Baraza la Usalama linakuwa limeshindwa kufanya hivyo. Kwa msingi huo kutokana na mara kwa mara Urusi kutumia kura ya turufu katika Baraza la Usalama kuzuia uamuzi wa kuibana, ndipo kikao hiki cha Baraza Kuu kikaitishwa kwa siku mbili Jumatano na Alhamis katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ili nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wapige kura kuiambia Urusi iondoke Ukraine.Awali kabla ya azimio kupigiwa kura, Vassily Nebenzia Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi aliliambia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa kufanya uamuzi kwa kuangalia tu yaliyotokea Februari 24 mwaka jana 2022 ni jaribio la makusudi la nchi za Magharibi kuficha sababu za kweli za mzozo huo. Hata hivyo matokeo ya kura yakaonesha kuwa walioinga mkono Urusi ni nchi 7 tu, 31 zikionesha kutokuwa upande wowote huku 141 zikiliunga mkono Azimio. Vita ikome, Urusi iondoke Ukraine.Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba, mara tu baada ya kupitishwa kwa azimio… anasema “nchi yangu imeridhika na matokeo na ujumbe uko wazi; Haijalishi ni nini Urusi inajaribu na jinsi inavyojaribu kudhoofisha utaratibu wa kimataifa, inashindwa kila mara.” Naye Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa aliwasisitizia wajumbe akisema, “uchokozi ni kinyume cha sheria. Kumvamia jirani ni kinyume cha sheria. Kujimegea kipande cha nchi nyingine ni kinyume cha sheria.” Miongoni mwa nchi 32 ambazo zimepiga kura isiyoonesha kama zinaunga mkono azimio au la pamoja na Burundi, Msumbiji, Ethiopia, Congo, Zimbabwe, Afrika Kusini, China, India na Pakistan. Na zile ambazo zimeiunga mkono Urusi kwa kulipinga azimio hilo la kumaliza vita Ukraine ni Belarus, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea, Eritrea, Mali, Nicaragua, Urusi yenyewe na Syria.
24-2-2023 • 0
Hofu ya athari yatanda huku kimbunga Freddy chabisha hodi Msumbiji: WMO
Kimbunga Freddy moja ya vimbunga vilivyodumu kwa muda mrefu na kusababisha athari kubwa sehemu mbalimbali sasa kimeondoka Madagascar na kubisha hidi Msumbiji ambako kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kinaleta tishio kubwa kwa sababu ya kiwango cha mvua kinachoambatana nacho.WMO inasema kimbunga Freddy kimeshika kasi kwenye mkondo wa Msumbiji kikitokea Madagascar huku kikiambatana na upepo mkali na mvua na kinatarajiwa kupiga kikamilifu Msumbiji mchana wa leo Ijumaa Machi 24 na uwezekano mkubwa ni katika maeneo kati ya Beira na Inhambane. Hata hivyo shirika hilo la utabiri wa hali ya hewa limesema tahadhari za mapema na hatua zilizochukuliwa mapema zimesaidia kudhibiti idadi ya vifo hasa Madagascar na sasa Msumbiji hali ambayo inadhihirisha umuhimu wa kampeni inayoendelea kote duniani ya kuhakikisha tahadhari ya mapema inatolewa kwa wote. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA imeonya kwamba “tishio la kimbunga hicho litasababisha janga kubwa la kibinadamu nchini Msumbiji.” Taasisi ya kitaifa ya kudhibiti majanga Msumbiji inakadiria kwamba mafuriko makubwa katikati na Kusini mwa Msumbiji kutokana na kimbunga hicho yanaweza kuathiri hadi watu milioni 1.75. Hatari kubwa ya kimbunga Freddy Msumbiji imeelezwa kuwa uwezekano mkubwa wa mvua kubwa inayopaswa kunyeksha kwa muda wa mwezi mmoja kunyesha kwa siku kadhaa na hivyo kusababisha mafuriko katika taifa ambalo tayari udongo wake umejaa maji na mito imefurika kutokana na msimu wa mvua usiotarajiwa.
WMO inasema kimbunga Freddy ni cha aina yake kwa sababu ya umbali kinachoweza kusafiri na muda kinachoweza kudumu. Kilianza Februari 6 kwenye mwambao wa Kaskazini Magharibi mwa Australia na kuathiri mataifa kadfhaa ya visiwani ikiwemo Mauritius na Réunion, wakati wa safari yake ndefu kupitia Kusini mwa bahari ya Hindi nah ii ni nadra sana linasema shirika hilo kwani kimbunga cha karibuni cha aina hiyo kilichorekodiwa ni Leon-Eline na Huda vyote vilitokea mwaka 2000.
24-2-2023 • 0
24 FEBRUARI 2023
Hii leo jaridani linaangazia vita vya mwaka mmoja nchini Ukraine na kimbunga Freddy. Makala na mashinani tunasalia huko huko Ukraine.Vita ya Ukraine ikiwa inaingia mwaka wake wa pili, wawakilishi mbalimbali wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wametoa maoni yao kufuatia uamuzi kwa njia ya kura uliofanywa na Kikao Maalumu cha dharura cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio jipya la kutaka amani ya haki na ya kudumu nchini Ukraine na kwamba Urusi bila masharti yoyote iondoe mara moja majeshi yake katika ardhi ya Ukraine.Kimbunga Freddy moja ya vimbunga vilivyodumu kwa muda mrefu na kusababisha athari kubwa sehemu mbalimbali sasa kimeondoka Madagascar na kubisha hodi Msumbiji ambako kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO kinaleta tishio kubwa kwa sababu ya kiwango cha mvua kinachoambatana nacho.Katika makala tunamulika mwaka mmoja wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.Na katika mashinani mashinani tutasalia nchini Ukraine katika kituo cha muda cha watoto wakimbizi wa ndani nchini Ukraine kusikia ni jinsi gani wafanyakazi wa kujitolea wanavyowasaidia watoto hao kurejesha afya yao ya kiakili.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
24-2-2023 • 0
Jifunze Lugha ya Kiswahili: MBWANDA
Katika kujifunza Lugha ya Kiswahili leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania, BAKITA anafafanua neno MBWANDA.
23-2-2023 • 0
23 FEBRUARI 2023
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunabisha hodi kaunti ya Makueni Kenya kuangazia mchango na faida za mikunde kwa mazingira, wakulima na jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo afya ya uzazi, intaneti, na msaada wa kibinadamu mashariki ya katiKatika kujifunza Lugha ya Kiswahili tunakwenda Baraza la Kiswahili Tanzania BAKITA kuchambua neno MBWANDA.Kila baada ya dakika 2 mwanamke mwanamke mmoja anafariki dunia kutokana na ujauzito au wakati wa kujifungua duniani kote, imesema leo ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa ikifichua vikwazo vya kutisha dhidi ya afya ya wanawake katika miaka ya karibuni wakati huu ambapo vifo vya wajawazito vimeongezeka au bado viwango vyake vimepungua katika takribani maeneo yote duniani.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa MAtaifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Audrey Azoulay amefungua mkutano wa kimataifa kuhusu Intaneti kwa ajili ya Kuaminiana huko Paris, Ufaransa na kusema kuzidi kuyoyoma kwa mpaka kati ya ukweli na uongo na kukataliwa kwa taarifa za ukweli za kisayansi, hakukuanzia kwenye mitandao ya kijamii bali kukosekana kwa kanuni za udhibiti na usimamizi na ndio maana uongo unashamirishwa kuliko ukweli.Na nchini Syria, hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limesafirisha kutoka Gazientep nchini Uturuki, shehena ya tani 34.5 ya vifaa vya matibabu kuingia kaskazini-magharibi mwa Syria kupitia vituo vya mpaka vya Bab Al-Hawa na Bab Al-Salama vikiwa na zaidi ya thamani ya dola milioni 353 ili kuimarisha huduma katika vituo vya afya ambavyo sasa vimezidiwa uwezo kufuatia tetemeko la ardhi lililokumba taifa hilo zaidi ya wiki mbili zilizopita.Na katika Lugha ya Kiswahili na leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa Tanzania, BAKITA anafafanua neno MBWANDA.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
23-2-2023 • 0
Kulima tunalima lakini lishe bado ni changamoto tuchukue hatua- Mkulima Sarah
Jamii ya mikunde! Wengi wanaitambua zaidi kama ni kunde zenyewe, na maharagwe lakini ni zaidi ya hiyo. Kuna choroko, mbaazi, dengu, njegere na kadha wa kadha ambapo kutokana na umuhimu wake katika lishe ya binadamu, kurutubisha udongo na pia kuhimili mabadiliko ya tabianchi, ndio maana Umoja wa Mataifa unapigia chepuo.Mathalani nchini Tanzania, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO linafadhili mradi wa AgriConnect ambao pamoja na mambo mengine unapatia wananchi, wake kwa waume stadi za mapishi sahihi ya jamii ya mikunde.Hivi karibuni wakati wa siku ya mikunde duniani tarehe 10 mwezi huu wa Februari, FAO ilishindanisha washiriki wa mradi huo kufahamu ni nani bingwa zaidi wa mapishi ya mikunde kwa kutambua kuwa Tanzania ni mmoja wa wazalishaji wakubwa wa mikunde lakini ulaji wake bado unachangamoto. Sasa makala hii inamulika harakati za kuchagiza ulaji wa mikunde pamoja na majani yake na mwenyeji wetu ni John Kabambala wa redio washirika Kids Time FM ya Morogoro, Tanzania. Kwako John!
22-2-2023 • 0
22 FEBRUARI 2023
Hii leo jaridani tunakuletea habari kuhusu mwelekeo wa matumizi ya maji barani Afrika, na elimu kwa watoto waliotumikishwa jeshini nchini DR Congo. Makala tutakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunarudi tena nchini DR Congo.Ni wakati kufikiria upya jinsi ya kutumia maji kwa njia endelevu na yenye uwiano huku ubunifu katika kilimo ukiwa kitovu cha mipango yote, amesema Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO limesema Qu Dongyu hii leo wakati akizungumza na viongozi na wataalamu wa Afrika kwenye warsha ya kwanza ya kikanda kuhusu mwelekeo wa matumizi ya maji barani Afrika, warsha inayofanyika nchini Zimbabwe.Mradi mpya wa shule nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC uliozinduliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wake kwa ufadhili kutoka mfuko wa Umoja wa Mataifa wa kuchagiza elimu kwenye maeneo ya mizozo, Education Cannot Wait, ECW, au Elimu Haiwezi Kusubiri umewezesha watoto waliokuwa wametumikishwa vitani kuanza kurejea kwenye masomo na hata kutangamana na wenzao kwa amani.Katika makala tunakupeleka Njombe mkoa ulioko kusini mwa Tanzania kusikia harakati za Umoja wa Mataifa na wadau za kusongesha ulaji wa mazao ya jamii ya mikunde ili kuboresha lishe.Na katika mashinani tutaelekea tena Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumsikia mvulana aliyekuwa ametumikishwa vitani.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!