Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Kukabiliana na tatizo la kiafya la kungatwa na nyoka katika ukanda wa Afrika
Kungatwa na nyoka imeorodheshwa miongoni mwa matatizo ya kiafya yaliyotengwa Takwimu za shirika la afya duniani ,WHO zinasema kila dakika nne ,watu nne duniani, hupoteza maisha kutokana na sumu ya nyoka.Hii ni kutokana na gharama ya juu ya matibabu ,ugumu wa kupatikana na matibabu haya na raia kutofahamu hatua sahihi ya kufuata ukiumwa au kutemewa sumu na nyoka.Nchini Sudan Kusini ,visa vya wagonjwa wanaongatwa imeongezeka maradufu kutokana na mafuriko ya miezi kadhaa kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka,MSFMSF hata hivyo kudhibiti hali ,inatumia mfumo wa akili mnemba au AI kurahisisha ubainishaji wa ainya ya nyoka na sumu yake vile vile matibabu yake,mradi unaoendeshwa na MSF katika baadhi ya vituo vyake jimbo la Warrap na Abyei.
10/22/2024 • 10 minutes, 14 seconds
ICRC yapambana kutoa huduma za afya za dharura ndani ya saa 96
Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC mara nyingi hubidi kuhudumu katika maeneo yenye mizozo kutoa huduma za dharura ,msaada wa kibinadaam ikiwemo afya Ili kukabiliana na changamoto za kuafikia malengo yake ya kutoa huduma za afya za dharura katika uwanja wa vita ,maeneo yenye majanga ,imebidi kufumbua mbinu ya kuwa na hospitali za muda ambazo zinajengwa kutumia hema na zinaweza kufanya kazi ndani ya saa 96ICRC inaendelea na mafunzo ya kuwaandaa wahudumu wa afya wanaohudumu katika mazingira hatarishi ,ili wapate kuhudumu ipasavyoMafunzo hayo yanatolewa kwenye hospitali halisi ambazo hutumika katika maeneo ya mizozo ,ambapo wahudumu hao hutakiwa kushughulikia mazingira tofauti ya dharuraMafunzo hayo yamefanyika nchini Kenya mara mbili ambapo wahudumu hao kutoka maeneo tofauti wanawekwa kwenye makundi na kutakiwa kutangamana na kushughulikia dharura tofauti kabla kuanza kutumwa kwenye maeneo ya mizozo
10/8/2024 • 10 minutes, 17 seconds
Ugonjwa wa Selimundu maarufu Sickle Cell unavyowaathiri wengi
10/7/2024 • 9 minutes, 45 seconds
Ubunifu kutatua changamoto za miundombinu kwenye usafi na maji taka
Mashirika ya nchini Kenya kwa ushirikiano na serikali za kaunti ,yamezindua mfumo mpya na wa kisasa wa vyoo bunifu visivyotumia maji wala kuunganishwa na mabomba ya maji taka Hatua Ambayo imeonekana kupunguza msambao wa magonjwa kama vile kipindupindu.
9/24/2024 • 10 minutes, 18 seconds
Ukosefu wa Ufahamu wa haki za afya ya uzazi ni kikwazo kikubwa ukanda wa Afrika
Raia wengi bado hawawezi kufurahia haki zao za afya ya uzazi kutokana na ukosefu wa ufahamu Haki hizo ni pamoja na haki ya kuwa mzazi au la,kupata habari kuhusu afya ya uzazi ,kupata huduma bora za uzazi ,kushiriki mapenzi kwa njia stahiki na kuhudumiwa katika vituo vya afya kwa heshima
9/17/2024 • 10 minutes, 19 seconds
Matatizo ya kupata uja uzito miongoni mwa wanafamilia yanazidi kuongezeka
Ripoti nyingi zinaonesha wanawake pamoja na wanaume wanakabiliwa na changamoto za uzazi Wanandoa nyingi wanalazimika kukaa miaka mingi kabla kupata watoto ,kitu ambacho bado kinazingatiwa na jamii za Afrika kuwa ukamilifu katika kila ndoa au familia.Daktari bingwa wa uzazi dkt Dennis Miskella anaeleza juhudi za kutafuta mtoto zinastahili kuwa ushirikiano kati ya mke na mumeweBaadhi ya sababu zinazohusishwa na hali hii ni kushiriki tendo la ndoa visivyo ,athari za baadhi ya mbinu za kupanga uzazi ,uvutaji sigara na pia unene wa kupitiliza
9/3/2024 • 10 minutes, 26 seconds
Wanawake wawafuga samaki kukwepa msambao hatari wa Ukimwi ziwa Victoria
Mashirika ya kiraia yanayofanya kazi maeneo ya Kisumu nchini Kenya wanawasaidia wanawake kuachana na mpango wa kuuza miili yao ili kupata samaki Tabia hiyo inayofahamika kama ngono samaki kwa wakazi imekuwa ikichangia msambao wa virusi vya HIV
8/28/2024 • 9 minutes, 37 seconds
WHO imetoa mwongozo wa kupambana na MPOX katika mataifa ya Afrika
Mikakati ambayo WHO inahimiza nchi za Afrika kukumbatia ni ubadilishanaji wa taarifa kuhusu ugonjwa wa Mpox ,ubainishaji sahihi na kampeni za chanjo Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,kuna hofu ya msambao hatari wa MPox unaohuishwa na vitendo vya ngonoWatalaam wa afya nchini DRC pia wanahimiza uhamasisho zaidi kuhusu ugonjwa huo ambao umesababisha vifo zaidi ya 500
8/20/2024 • 10 minutes, 1 second
MPOX yatangazwa janga la dharura la kiafya baada ya kasi ya maambukizi kuzidi
Shirika la afya duniani ,WHO na taasisi ya kudhibiti magonjwa ya umoja wa Afrika ,CDC zililazimika kuchukua uamuzi mzito wa kutangangaza MPOX dharura ya kiafya Mataifa 16 ya Afrika kati ya 55 yameripoti visa vya MPOX mwaka huu ,CDC ikisema maambukizo yamepanda hadi asilimia 160 mwaka huu ukilinganishwa na mwaka 2023Virusi vya MPOX vimeripotiwa kujibadilisha na kwa sasa msambao hatari wa virusi sugu zaidi unahusishwa na ngono
8/20/2024 • 9 minutes, 36 seconds
Bidhaa mpya za tumbaku zinauzwa kwa mwoneko bora, ladha ya kuvutia kuficha madhara yake
Kuuza bidhaa za tumbaku za kisasa ,kama bidhaa zisizo na madhara ,kutumia ladhaa tamu na kutumia mitandao ya kijamii kuuza bidhaa hizi ni mbinu ambao kampuni za kutengeneza tumbaku zinatumia kuwavutia vijana na kuwa wateja wao wa kudumu. Kampuni hizi zinafadhili pia utafiti ambao unakinzani na utafiti wa taasisi za afya kuhusu madhara ya Tumbaku.Isitoshe kampuni hizi zinazalisha bidhaa ambazo mtumiaji anaweza kutumia zaidi ya moja .
8/6/2024 • 9 minutes, 59 seconds
Mbinu fiche zinazotumia sekta ya kuzalisha tumbaku kuendelea kudumu soko
Kumeshuhudia juhudi makhsusi kutoka sekta ya Tumbaku zinazopinga sheria zinazodhibiti Tumbuka kama vile kupitia ushuri au sheria zenye adhabu kali Sekta hii pia imeonekana kurubuni serikali tofauti kwa kutoa msaada bila wao kufahamu lengo la sekta hiyo. Aidha kuna tafiti za kisayansi zinazofadhiliwa na sekta hii kukabili sayansi zinazorodhesha tumbaku na bidhaa za sigara kuwa zenye madhara makubwa ya kiafya
8/1/2024 • 10 minutes, 21 seconds
Simulizi kuhusu ugonjwa wa Endometriosis unaowasababishia wanawake maumivu
Ugonjwa wa Endometriosis hudhihirika msichana anapovunja ungo na huja na maumivu makali kabla ,wakati na hata baada ya hedhi Lilian Leley ameishi na maumivu hayo kwa zaidi ya miaka thelathini.Amefanya upasuaji mara mbili na anatazamiwa kwenda kwenye operesheni nyingine hivi karibuni katika kujaribu kutafuta tiba ya ugonjwa wa EndometriosisAnasimulia masaibu yake ,ambapo anasema ndani ya mwezi huenda ni mzimu tu kwa siku 10
7/24/2024 • 10 minutes, 16 seconds
Fahamu kuhusu ugonjwa wa Endometriosis na changamoto za afya zinazofungamana nao
Endometriosis hutokea wakati tishu kwenye ukuta wa tumbo la uzazi zinapopatikana katika maeneo mengine ya mwili ikiwemo mapafu ,utumbo na hata ubongo Endemotriosis huwa na dalili zinazofanana magonjwa mengine ya uzazi na unaweza kubainika kupitia kipimo cha Laparoscopy ambapo tishu hizo zinachunguzwa moja kwa moja
7/16/2024 • 10 minutes, 23 seconds
Maandishi yenye tahadhari yatasaidia mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukizwa
Bidhaa za vyakula au vinywaji zikiwa na machapisho ya kuonesha kuwa vina sukari nyingi ,chumvi nyingi au mafuta mengi mnunuzi anakuwa na fursa ya kuchagua vema Watalaam wamesema lishe ni kiungo muhimu katika kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa ambayo yanazidi kuongezeka na kuwa mzigo kubwa kwa jamii na mifumo ya afya
7/10/2024 • 10 minutes, 22 seconds
Mashujaa wa kupambana na Vitiligo wana matumaini makubwa ya jamii kuwaelewa
Jamii nyingi bado hazielewi kuwa ugonjwa wa Vitiligo hauwezi kuambukizwa kwa kutangamana ,kugusana au hata kushiriki mlo
7/10/2024 • 9 minutes, 50 seconds
Dunia yaadhimisha siku ya ugonjwa wa ngozi - Vitiligo
Vitiligo ni hali ya ngozi ambapo madoa meupe au mabaka yanaonekana. Inaweza kuathiri mtu yeyote, ikiwa ni pamoja na watoto na vijana. Sio hatari, si kama saratani ya ngozi au maambukizi unayoweeza kupata na kwa hiyo huwezi kuipata kutoka kwa mtu mwingine. Watu wengi wenye vitiligo wana afya nzuri. Baada ya muda, mabaka zaidi yanaweza kuonekana kwenye sehemu tofauti za mwili, hata kwenye nywele au ndani ya kinywa na pua. Mara nyingi huanza katika maeneo yaliyopigwa na jua. Takriban 1% ya dunia ina vitiligo
6/29/2024 • 10 minutes, 33 seconds
Muguka inaweza kusababisha madhara ya afya mtu anapokuwa mraibu
Kumekuwa na mvutano kati ya serikali ,uongozi wa kaunti za Pwani ya Kenya ,kuhusu Muguka kupigwa marufuku kwa sababu za kiafya Wakulima ,wafanyabiashara na wenyeji wa Embu wanaozalisha Muguka kwa kiasi kikubwa hata hivyo wanasema hawajapata madhara yoyoteHata hivyo watalaam wa afya wanaonya uraibu wa Muguka unaweza kudhuru afya
6/21/2024 • 10 minutes, 19 seconds
Sera kuhusu idadi ya watu inavyoathiri uchumi ,afya na hali ya maisha
Mataifa ya Afrika bado yanaendelea kushuhudia kasi ya ongezeko la watu ijapokuwa chumi za Afrika hazifanyi vizuri inavyotakikana Watalaam wanaonya iwapo idadi ya watu haitodhibitiwa ,kupangiwa huenda mataifa mengi yakalemewa na idadi ya watu wanaowategemea wengineAidha kuna hatari ya sera za serikali kushindwa kukidhi mahitaji ya raia wake ,idadi inapokuwa kubwa
6/11/2024 • 9 minutes, 58 seconds
Juhudi za kuukabili ugonjwa wa Mycetoma kutumia dawa zilizofanyiwa utafiti Sudan
Mycetoma ni mojawapo ya magonjwa yaliyopuuzwa ingawa unaendelea kuwaathiri wengi haswa watu wanaokaa maeneo kavu na jamii zilizotengwa Mycetoma hujidhihirisha kama donda ambalo haliponi bali linaendelea kukua na kuchimba sehemu athirika katika mwili
6/8/2024 • 10 minutes, 8 seconds
Mataifa ya Afrika yashinikiza mwongozo wa kukabiliana na hali ya dharura
Mataifa wanachama wa shirika la afya duniani ,WHO yanayokongamano katika kongamano la afya ya 77 jijini Geneva yanataka kuwepo mwongozo wa afya kukabiliana na hali ya dharura baada ya janga la COVID 19 Mataifa haya yanasisitiza kuwepo usawa kwenye kuzalisha na matumizi ya sampuli za kutengeneza sampuli zinazochangiwa na nchi mbali mbaliAidha usawa kwenye ufadhili ,usambazaji wa chanjo mpya na chanjo zinazotumika wakati wa majanga Kongamano hilo pia linatazamiwa kuja na mwafaka kuhusu marekebisho kwenye sheria za afya za mwaka 2005
5/29/2024 • 9 minutes, 32 seconds
Matatizo ya afya ya akili yasipotatuliwa huwaathiri mustakabali wa watoto
Watoto na vijana walioshuhudia dhulma , kupata kiwewe,mara nyingi wanajikuta hawaamini katika uhusiano ,huwa waathiriwa wa dhulma za kimapenzi
5/22/2024 • 10 minutes, 9 seconds
Changamoto za afya ya akili miongoni mwa watoto na vijana Afrika
Kumekuwa na ongezeko la idadi ya watoto na vijana wanaokabiliwa na changamoto za afya ya akili Kila mwezi Mei dunia huungana kufanya kampeni ya watu kuwa makini na afya zao za akili ili kuzuia changamoto zaidi za akili ambazo wakati mwingi huishia kwenye umauti na matatizo zaidi ya kiafyaWatalaam wa afya wanasema watoto na vijana pia nao hupatwa na changamoto hizi zinazohusishwa na afya ya akili ,matatizo hayo yakiwemo kiwewe na msongo wa mawazo.Daktari bingwa wa afya ya akili katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta kitengo cha watoto ,Dkt Josephine Omondi anasema mazingira yanayochochea hali hii ni mizozo ya kifamilia ,matumizi mabaya ya mitandao ,shinikizo kutoka mazingira ya shule na pia matatizo ya kiafya yanayohusishwa na miaka ya awali ya mtotoMshauri Nasaha Naomi Ngugi anasema ni wakati wazazi wakakumbatia ukweli kuwa watoto na vijana huhitaji washauri nasaha na matibabu mengine ya matatizo ya afya ya akili
5/14/2024 • 10 minutes, 14 seconds
Mimba za utotoni zaendelea kuongezeka ukanda wa Afrika Mashariki
Idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimbo za utotoni wapo katika nchi za Afrika kwa mujibu wa shirika la afya duniani pia UNFPA Sababu zinazochangia mimba za utotoni ni pamoja na umaskini ,dhulma za kimapenzi ,ngono biashara na tamaduni hasi
5/8/2024 • 10 minutes, 20 seconds
Methadone yatumika kuwasaidia waraibu wa dawa za kulevya kupambana na Ukimwi
Kenya imeanza kutumia Methadone kupambana na Ukimwi baada ya Tanzania
5/7/2024 • 8 minutes, 40 seconds
Ajali za barabara Afrika huchangiwa na utepetevu, kasi na msongo wa mawazo
Ajali za barabara huchangia vifo vingi vya watu walio katika umri kati ya miaka mitano hadi 29 kwa mujibu wa WHO Uchunguzi unaofanywa baada ya ajali huonesha madereva wengi hulaumi kufeli kwa breki ilhali wengi wana msongo wa mawazo ,imesema mamlaka ya usalama barabarani nchini Kenya ,National Transport and Safety Authority. Ongezeko la magari,mchipuko wa miundo mbinu bora na ongezeko la watu yanazidi kufanya uwezekano wa mtu kuhusika kwenye ajali kuwa mkubwa.
4/23/2024 • 10 minutes, 25 seconds
Watu wengi wanajikuta na magonjwa ya figo na ini,watoto wengi Sudan wakiaga
Kuna ongezeko la magonjwa ya figo na ini kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO inabashiri kuwa ongezeko hilo litakuwa juu zaidi kufikia mwaka 2030 ,hali hii ikichangiwa na hali ya maisha haswa ya raia katika nchi zinazoendeleaUgonjwa wa ini maarufu Hepatitis pia ni tishio kubwa haswa kwa raia wa Afrika ambayo inachangia asilimia 63 ya visa vya HepatatisNchini Sudan watoto wengi haswa walio chini ya umri wa miaka mitano wanazidi kupoteza maisha kutokana na utapiamlo unaohusishwa na ukosefu msaada wa kibinadaam wakati huu vita vikiendelea kurindima
4/17/2024 • 10 minutes, 9 seconds
Uhitaji wa huduma za dharura za afya washika kasi ukanda wa Afrika
Shirika la AMREF Flying doctors linaonya kuwa mlipuko wa magonjwa yasiyoambukizwa yanazidi kuongeza uhitaji huku wigo la kupanua biashara likitanuka pia
4/10/2024 • 9 minutes, 55 seconds
Wanawake waongoza juhudi za kampeni za Afya bora ,DRC ikizidisha mapambano ya Kipindu Pindu
Wawawake kutoka ukanda wa Afrika wanajumuika Dar Salaam mwishoni mwa juma kupiga jeki kampeni za kuboresha afya Nchini DRC mikakati iliyoweka kudhibiti mlipuko wa Kipindu Pindu ulioripotiwa katika mataifa ya Afrika ya Kusini ,inaendelea kulipa na hata kuwa msaada kwa mataifa jirani kama vile Zambia
4/2/2024 • 9 minutes, 59 seconds
Mataifa ya Afrika yanayoendelea bado yanachangia mzigo mkubwa wa TB
Usalama mdogo nchini Sudan Kusini umesababisha wagonjwa wengi kuchelewa kubainishwa TB na kupata matibabu ya mapema Watalaam wa afya wanashauri ulimwengu kukumbatia teknolojia za kisasa kama vile Akili Mnemba kurahisisha ubainishaji na kuongeza usahihi wa vipimo
3/29/2024 • 10 minutes, 23 seconds
Mageuzi yanayoletwa na nishati bunifu kisiwa cha Ndeda magharibi mwa Kenya
3/20/2024 • 10 minutes, 14 seconds
Wanawake mbele kuinua sekta ya sayansi na utafiti nchini Kenya
Idadi ya wanawake wanaongoza katika sekta mbali mbali bado ni ndogo barani Afrika. Kauli mbinu mwaka huu wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake ni kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuongeza kasi ya maendeleo,tunaangazia wanawake wanasayansi na watafiti nchini Kenya ,wakijikita kwenye utafiti wa magonjwa yaliyotengwa
3/13/2024 • 10 minutes, 14 seconds
Jamii ya Kibera jijini Nairobi inavyopambana na mimba za utotoni
Mimba za utotoni ni kizingiti kikubwa kinachoathiri elimu ya wasichana barani Afrika
3/10/2024 • 10 minutes, 3 seconds
UNITAID mbioni kurahisisha upatikanaji wa dawa nadra sokoni
UNITAID imekuwa ikishirikiana na mataifa kuleta dawa mpya na za bei nafuu Upatikanaji wa dawa zilizo za viwango vya juu na kwa bei nafuu bado ni changamoto kubwa kwa mataifa yanayoendelea.Matibabu ambayo bado ni mapya hukumbwa na vikwazo vingi kuingia soko la kimataifa na sasa UNITAID imekuwa mbioni kuziba pengo hilo
2/28/2024 • 9 minutes, 21 seconds
Ushirikiano kati ya shirika la Village Reach na wizara ya afya nchini Kenya na nchi za ukanda wa Afrika
Village Reach ambayo kwa tafsiri rahisi ni kufikia maeneo ya vijijini, imefungua ofisi za kikanda jijini Nairobi kujaribu kusaidia serikali kusimamia namba ya dharura,usafirishaji wa sampuli za Polio na kuboresha utendakazi wa wahudumu wa afya wanaofanya kazi katika jamii tofauti Baada ya kupata mafanikio makubwa katika nchi za Msumbiji, Malawi ,Village Reach inapanga kutumia mafunzo hayo kusaidia kuboresha huduma za afya katika mataifa ya Afrika.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,Village reach imeimarisha huduma za utoaji chanjo ,usafirishaji wa chanjo kutumia ndege zisizo na rubani katika maeneo yasiyo na miundo mbinu ikiwemo mkoa wa Equateur.Aidha shirika hilo linatoa huduma kwa ushirikiano na serikali katika mataifa mengine yenye mzozo kama vile Niger na Sudan Kusini.Afisa mkuu mtendaji Emily Bancroft amesisitiza mifumo ya afya inastahili kuwa thabiti ili kuwa na uwezo wa kustahimili majanga na hali za dharura kama ilivyoshuhudiwa wakati wa Uviko 19
2/6/2024 • 10 minutes, 7 seconds
Changamoto za afya ya akili katika mitaa ya mabanda nchini Kenya
Shirika la afya duniani limeorodhesha ongezeko la watu wanaokumbwa na changamoto za afya ya akili hususan tangu kuzuka janga la Corona,kupanda gharama ya maisha na mfumuko wa bei
1/24/2024 • 9 minutes, 54 seconds
Mikakati kuboresha matibabu ya TB
Juhudi zinaendelea kuhakikisha dawa mwafaka ya TB miongoni mwa watoto zinaendelea Licha ya kuwa TB inaweza kuambukiza watu wa umri wowote ,watoto kwa miaka wamekuwa wakiachwa nyuma katika matibabu ya TB. Watoto kwa miaka walilazimika kutumia donge za watu wazima.
1/15/2024 • 8 minutes, 31 seconds
Muendelezo wa ugonjwa wa Kisukari nchini Kenya na Sudan Kusini
Nchi zinazoendelea zinashuhudia ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa ukiwemo Kisukari
1/5/2024 • 9 minutes, 43 seconds
Wadau wa afya wapaza sauti kuhusu ongezeko la magonjwa tengwa wakionya ni tishio katika mifumo ya afya
Wadau katika sekta ya afya wana wasi wasi kuhusu ongezeko la magonjwa yaliyotengwa ambayo mengi yao hayana tiba au matibabu yao hayapatikani kwa urahisi au ni bei juu Wawekezaji katika sekta ya uzalishaji dawa ,chanjo hawavutiwi kuzitengeneza dawa za magonjwa hayo. Magonjwa hayo ni kama vile ugonjwa wa malale,matende ,Chikukungunya na Dengue.
12/22/2023 • 10 minutes, 20 seconds
Matumizi ya Akili mnemba au AI kuboresha huduma za Afya
Ulimwengu umeanza kukumbatia matumizi ya akili mnemba au AI kuboresha huduma muhimu licha ya kuwa bado kukamilika mchakato wa kudhibiti matumizi ya teknolojia hiyo. Katika sekta ya afya mfumo wa AI umeanza kutumika kwenye ubainishaji wa magonjwa na ufuatiliaji wa matibabu.
12/22/2023 • 10 minutes, 6 seconds
Ugonjwa wa Utindio wa Ubongo almaarufu Celebral Palsy
Ugonjwa unaofahamika kama Utindio wa ubongo au Cerebral Palsy kwa lugha ya kimombo ni ugonjwa unaoathiri ubongo, namara nyingi unatokea kwa watoto na husababishwa wakati damu inapovuja kwenye ubongo au hakuna hewa yakutosha.Unaweza kutokea wakati Mtoto anapoanza kupoteza fahamu punde baada ya kuzaliwa au mwezi wa kwanza wa kuzaliwa.Vilevile Jeraha kwenye ubongo linaweza kusababisha matatizo ya kuongea na ugumu wa kufahamu mambo.Sikiliza makala haya kutambua zaidi kuhusu ugonjwa huu.
12/22/2023 • 10 minutes, 14 seconds
Afya ya umma barani Afrika
Kongamano la tatu la CPHIA kuhusu huduma za afya barani Afrika.
12/1/2023 • 9 minutes, 7 seconds
Mpango wa afya kwa wote barani Afrika
Mataifa mengi yana matamanio ya kuhakikisha raia wake wanapata huduma bora za afya kwa bei nafuu,safari hii ikiwa bado ina panda shuka kwa mataifa mengi. Huduma za afya barani Afrika zina mfungamano na hali ya kisiasa,uchumi na pia utawala bora.
11/21/2023 • 10 minutes, 19 seconds
Faida za mazoezi ya Yoga kwenye mwili wa mwanadamu
Yoga ni mazoezi ya mwili yanayoongeza nguvu kwa misuli na kunyoosha mifupa lakini pia yoga inalenga kuunganisha mwili, ufahamu, na akili kwa pamoja. Hivyo ni tofauti kabisa na aina nyingine za mazoezi.Sikiliza makala haya kwa ufahamu zaidi.
11/16/2023 • 10 minutes
Ongezeko la visa vya mdomo Sungura
Watalaam wanahofu kuhusu ongezeko la watoto wanaozaliwa na mdomo sungura au Cleft Clip Licha ya kuwa utafiti haujabainisha moja kwa moja sababu ya mdomo sungura ,lishe,urithi na matumizi ya sigara zimetajwa kuchangia hali hii
11/3/2023 • 9 minutes, 46 seconds
Hofu kuhusu hatma ya mchakato wa amani DRC unaoratibiwa na AU
Umoja wa mataifa umeonya uwezekano wa kuibuka vita kati ya DRC na Rwanda Rwanda na DRC zimeendelea kulaumiana kuhusu hali mbaya ya usalama mashariki mwa DRC. Rwanda imeongeza usalama katika mipaka yake na DRC baada ya raia wake kujeruhiwa na risasi iliyotokea upande wa Congo.
10/25/2023 • 10 minutes, 8 seconds
Mpango wa afya kwa wote nchini Kenya ambapo wafanyikazi watachangia 2.75 ya mishahara
Kenya katika sherehe za hivi karibuni za mashujaa ,imezindua mpango wa afya kwa wote. Mpango huu wa afya unazingatia raia kupata huduma bora kuanzia vituo vya afya vya daraja la kwanza hadi hospitali kubwa bila malipo .
10/24/2023 • 10 minutes, 18 seconds
Ongezeko la akina baba wanaowalea watoto pekee yao
10/23/2023 • 9 minutes, 4 seconds
Shirika la madaktari wasio na mpaka lataka wanawake waliodhulumiwa kingono kupata msaada zaidi ya matibabu
Wanawake wakimbizi jijini Goma waliokimbia vita wameathirika afya ya akili na mwili na wanahitaji msaada hata baada ya kupata matibabu.Wengi wamebakwa zaidi ya mara moja wakienda kutafuta chakula na mahitaji mengine
10/10/2023 • 9 minutes, 56 seconds
Wauguzi wanaowahudumia wagonjwa wa saratani walia kubeba mzigo mkubwa unaowaathiri hata afya zao
Idadi ya wagonjwa wanaougua saratani inazidi kupanda kila siku,katika mataifa ya ulimwengu,vile vile idadi ya vifo vinavyosababishwa na saratani Wauguzi wanaowahudumia wagonjwa hao hulazimika kutembea na mgonjwa ambaye mara nyingi huwa na maumivu makali , kudhurika wakati wa matibabu ,wengine kufariki na inapotokea ,muuguzi ndiye anayehitajiwa kuwashughulikia pia familia zao.
9/26/2023 • 9 minutes, 48 seconds
Wanawake wakimbizi eneo la Goma DRC wanakabiliwa na changamoto za kiafya na dhulma za kingono
Wanawake waliokimbia mapigano mashariki mwa DRC ,wamepitia dhulma za kijinsia zaidi ya mara moja ,hata baada ya kuwepo kwenye kambi za wakimbizi Shirika la madaktari wasio na mipaka ,MSF limesema kila siku ,kuna wanawake 70 wanaotibiwa katika vituo vyao kutokana na kukithiri dhulma za kingono.MSF huwapa huduma za dharura,kupanga uzazi na wengine wanalazimika kupewa huduma za kuavya mimba kwa njia salama.Hali ya kambi wanazokaa,inawaweka kwenye hatari ya kushambuliwa ,kubakwa huku wengine wakipitia dhulma hizo wanapokwenda nje ya kambi kutafuta mahitaji mengine ya kila siku.
9/19/2023 • 10 minutes, 14 seconds
Je matumizi ya sukari mbadala inafaa?
Mwezi Septemba dunia inapojiunga kuleta hamasa kuhusu afya ya akili,idadi ya vijana wanaojiua bado iko juu. Na watalaam vile vile wanaonya kuhusu sukari mbadala au artificial sweeteners ambazo japo zinadhaniwa kuwa salama ,zina madhara katika viungo vya mwili na utendakazi wa mwili
9/15/2023 • 9 minutes, 59 seconds
Ongezeko kwa maambukizi ya HIV miongoni mwa vijana ni tishio kwa mapambano dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi
Ngono zembe miongoni mwa vijana inawaweka wengi kwenye hatari ya kupata HIV na saratani ya shingo ya uzazi
8/29/2023 • 9 minutes, 42 seconds
Soko huru ya sigara za kisasa ni tishio kubwa la afya
Kasi ya watumiaji wa sigara za kisasa kama vile Nicotine Pouches na Sigara ya Kielectroniki imezidi kupanda ,vile vile uraibu miongoni mwa vijana na wanafunzi Wanaotumia sigara za kisasa wanahoji kuwa hazina moshi au harufu mbaya ,hali ambayo watalaam wanasema inachangia uraibu wa haraka na madhara zaidi kwa viungo vya mwili
8/22/2023 • 9 minutes, 57 seconds
Upandikizaji viungo vya mwili Afrika Mashariki
Kupandikiza au kuhamisha viungo vya mwili kama njia mojawapo ya matibabu inazidi kushika kasi .Mataifa mengi yanafanya upandikizaji wa figo ,moyo ,ini ,Cornea na sehemu za umme. Kuna hata hivyo changamoto katika hili,mataifa bado hayana sheria za kutosha kusimamia zoezi hili. Kwa sasa upandikizaji unafanyika kwa watu wanaohusiana huku kukiwa na hitaji kubwa ya viungo muhimu vya mwili.Hii ni kutokana na kuwepo wagonjwa wengi wanaopata viungo vyao muhimu vimefeli kutokana nao kuwa na magonjwa yasiyoambukizwa.
8/15/2023 • 10 minutes, 18 seconds
Chanjo ya Kipindu Pindu na changamoto za akina mama wanaonyonyesha
Juma la kwanza la Agosti ,ulimwengu huungana kupigia upatu juhudi za akina mama kuweza kuwanyonyesha wanao bila vikwazo katika miezi sita ya kwanza. Katika juhudi za kupambana na Kipindu Pindu ,Kenya inaendelea na kampeni ya kuchoma chanjo dhidi ya Kipindu Pindu chanjo ambayo imeshuhudia uhaba kutokana na uhitaji mkubwa katika mataifa mengi.
8/8/2023 • 10 minutes, 15 seconds
Mataifa ya Afrika yanavyopambana kukabili usugu wa vimelea,Antimicrobial Resistance
Tatizo la usugu wa vimelea ni changamoto kubwa katika sekta ya afya ,watalaam wakihitajika kutumia gharama kubwa kwenye matibabu
8/1/2023 • 9 minutes, 42 seconds
Mlipuko wa Magonjwa yanayohusishwa na wanyama
Mlipuko wa magonjwa yenye asili ya wanyama wa Pori na hata wale wa kufugwa nyumbani umeendelea kushuhudiwa ukanda wa Afrika Mashariki Magonjwa haya ni pamoja na Marburg ,Homa ya Mgunda , Ebola na Covid 19
7/13/2023 • 9 minutes, 31 seconds
Ushirikiano kati ya sekta binafsi na ya umma kuboresha huduma za afya
Mataifa mengi barani Afrika bado yana changamoto ya kuwahakikishia raia wao huduma za kisasa za afya na ambazo haziwagharimu zaidi Katika makala haya tunaangazia mjadala wa kushirikisha sekta binafsi kuboresha huduma za afya barani Afrika.Aidha tunaangazia mpango wa kupunguza idadi ya vifo vya watoto walio chini ya umri ya miaka mitano kaunti ya Kwale ,Pwani ya Kenya kwa kuorodhesha habari zao muhimu kwa mfumo wa kidijitali tangu wanapozaliwa
7/5/2023 • 9 minutes, 59 seconds
Ugonjwa wa Kipindu Pindu Homabay nchini Kenya
Mataifa mengi barani Afrika yameripoti mlipuko wa Kipindu Pindu Katika makala haya ,tunaangazia Kipindu Pindu katika kaunti ya Homabay ,magharibu mwa Kenya ,karibu na ziwa Victoria .Pia tutakufahamisha kuhusu juhudi za kupambana na ugonjwa huo
6/29/2023 • 10 minutes, 11 seconds
Ugonjwa wa Matende
Magonjwa yaliyotengwa kama Matende bado yanawapa changamoto nyingi raia wengi Matende au Elephantiasis ni baadhi ya magonjwa yaliyotengwa au kusahaulika ijapokuwa madhara yake ni makubwa.Mara nyingi matibabu yake huwa gharama juu wakati kinga kupitia dawa za minyoo imeendelea kupuuzwa na raia wengi kutokana na dhana kuwa dawa zinazosambazwa bila malipo na serikali si vya viwango vya juu
6/22/2023 • 9 minutes, 51 seconds
Juhudi za kupunguza gharama katika matibabu ya macho
Raia wengi nchini Kenya wana uhitaji wa miwani kutokana na matatizo ya macho.Wengi wao hata hivyo hawapati miwani kutokana na gharama ya juu Katika makala haya tunaangazia mchango wa kampuni ya Mamy Eye Wear kupunguza gharama ya miwani huku ikizingatia ubora.
6/16/2023 • 9 minutes, 57 seconds
Matumizi ya Dawa za Kulevya Sudan Kusini
Watu walioacha kutumia dawa za kulevya nchini Sudan wanasaidia juhudi za kupambana na dawa za kulevya
6/6/2023 • 9 minutes, 29 seconds
Mapambano kupunguza matumizi ya Tumbaku na mchango wa sekta binafsi katika afya
Mataifa ya ulimwengu yanapoadhimisha siku ya Tumbaku Mei 31,kuna hofu juhudi za kupunguza matumizi ya tumbaku zinaonekana kurudishwa nyuma na ukiukaji wa sheria za kupambana na matumizi ya tumbaku Sheria kuhusu ushuru unaotozwa kwenye bidhaa za tumbaku bado haifuatwi kikamilifu .Wafanyibiashara wanaouza sigara chini ya pakiti moja wanatuhumiwa vile vile kurudisha mapambano ya kupunguza matumizi ya tumbaku.Isitoshe kampuni zinazotengeneza bidhaa hizo zimekuja na bidhaa mpya ambazo zinawavutia watumizi wa umri mdogo na pia wanawake .Aidha kwenye makala haya tunakufahamisha kuhusu juhudi za sekta binafsi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kuchangia kupunguza idadi ya raia wanaoumwa kwa kuwatuza na kuwasaidia kuepukana na magonjwa haswa yasiyoambukizwa.
5/31/2023 • 10 minutes, 7 seconds
Kuipa hedhi heshima kama haki ya msingi miongoni mwa wanawake
Umaskini umechangia wasichana wengi kukosa Sodo na kushindwa kwenda shule
Ukosefu wa sodo ndio umeonekana kuchangia wasichana wengi nchini Kenya kutoudhuria shule hasa maeneo ya mashinani.Utamaduni pamoja na ufukara ndivyo vimeonekana kuchangia halii hii kwa asilimia kubwa.
Utafiti uliofanywa na shirika la Borgen, asilimia 65 ya wasichana na wanawake nchini kenya hukumbwa na ukosefu wa sodo hivyo kuathiri masomo na shughuli zao za kila siku.
Lakini hata hivyo katika kaunti ya kwale ,idadi ya wasichana imeanza kuongezeka shuleni baada ya jamii pamoja na mashirika mbalimbali kuanzisha mpango wa ugavi wa sodo kwa wasichana.
5/25/2023 • 9 minutes, 28 seconds
Nafasi ya wauguzi kwenye mkondo wa huduma za afya na huduma za afya kwa wanaoishi na ulemavu
Kila Mei kati ya tarehe 8- 14 dunia huwaenzi wauguzi ambao ni kiungo muhimu kwenye huduma za afya.
Kwenye makala haya tunaangazia wauguzi na mchango wao kutoa huduma za afya .Tumezungumza na nesi Caroline Mwangi anayehudumu katika chumba cha dharura katika shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF,nchini Kenya.
Tumezungumza pia na Faustin Chepchirchir kutoka shirika linalowashughulikia watu wanaoishi na ulemavu kuhusu namna ya kuboresha ubora wa huduma za afya kwa watu wa makundi tengwa
5/16/2023 • 10 minutes, 3 seconds
Mchango wa Wakunga katika utoaji huduma za kimsingi kwenye jamii
Kila Mei tarehe tano ,ulimwengu huadhimisha siku ya kimataifa ya wakunga
Jamii ya Wapemba wanaoishi kaunti ya Kwale ,Pwani ya Kenya kwa kuwa hawana uraia,imekuwa ikitegemea pakubwa huduma za mkunga.
5/9/2023 • 10 minutes, 3 seconds
Mpango wa afya kwa wananchi wa Zanzibar
Zanzibar inaanza kutekeleza mpango wa mfuko wa bima wa afya kwa raia wote kupata huduma za afya bila malipo.
Waziri wa Afya, Nassor Ahmed Mazrui anasisitiza ndio njia pekee itakayowawezesha Wananchi wote yakiwamo makundi yasiyokuwa na uwezo kufaidika na huduma za Afya kikamilifu.
5/2/2023 • 10 minutes, 1 second
Dunia yaadhimisha siku ya Malaria
Ulimwengu huadhimisha siku ya malaria kila tarehe 25 mwezi wa nne. Malaria ni ugonjwa wa kuambukiza ambao unaenezwa na mbu wa jenasi anayefahamika kama Anopheles na kusababishwa na kidubini aina ya Plasmodium.
Kulingana na shirika la afya duniani Nigeria inasajili visa hivyo kwa asilimia 31.3, DRC asilimia 12.3,Tanzania kwa asilimia 4.1 na Niger kwa asilimia 3.9.
Vilevile Kulingana na ripoti ya shirika la maendeleo ya Ufaransa nchini Kenya AFD ni kwamba Kisumu inaongoza kwa visa vya malaria kwa hadi asilimia 40.
Na Kwenye makala haya tunazungumzia ugonjwa huu na jinsi ya kupambana nao. Nimezungumza nae Peris Oloo ambae anaugua malaria na anaelezea baadhi ya dalili alizokua nazo.kisha Daktari anaezungumzia Ugonjwa huu kwa kina na jinsi mtu anaeza uepuka.
4/26/2023 • 9 minutes, 56 seconds
Jinsi mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri afya na haki za akina mama
Mabadiliko ya tabia nchi yameendelea kufifiza usalama wa chakula chenye lishe,kupunguza uwezo wa akina mama wanaotegemea kilimo asili kulisha familia zao na kuongeza idadi ya magonjwa yasiyoambukizwa
Kwenye makala haya tunaangazia kilimo cha wimbi ambacho japo ni cha asili,ni chakula chenye lishe na kinachohitajika kwa sasa kwa ajili ya wagonjwa wa kisukari.Kupungua kwa uzalishaji wa wimbi kutokana na ukame,gharama ya juu ya mbegu na mashamba yanayotumika kwa mara ya kwanza ,yamechangia akina mama wengi hawawezi kuwalisha familia zao kwa kuwa wimbi ni kipato cha wanawake,inatumika kuwalisha watoto na watu wenye umri uliokwenda wengi wao wakiwa wanauguza ugonjwa wa kisukari.
Tunaangazia vile vile kilimo cha sasa cha wimbi ambacho wanawake katika kaunti ya Bomet ,kusini mwa bonde la ufa ,nchini Kenya wamebidi kukumbatia ili kuendelea na kilimo cha wimbi wakati huu ulimwengu unapokumbwa na athari haasi ya mabadiliko ya tabia nchi.
4/18/2023 • 10 minutes, 12 seconds
Afya ya kinywa na tabia za kuzingatia kuchochea afya ya kinywa
Afya ya kinywa ni muhumi ilivyo afya ya sehemu zingine za mwili.
Katika makala haya ,tunakupa ufahamu zaidi kuhusu afya ya kinywa ;usafi wa meno,ulimi na ufizi .Daktari David Amenya anaelezea namna ya kupiga mswaki,mswaki sahihi,matibabu ya meno miongoni mwa maswala mengine.
4/11/2023 • 10 minutes, 21 seconds
Mpango wa Car Free jijini Kigali unaolenga kuboresha afya na usafi wa jiji
Kila Jumapili ya kwanza ya kila mwezi na ya tatu wakazi wa Kigali hujumuika kufanya mazoezi ya pamoja
Car Free jijini Kigali imezidi kupata umaarufu,raia wanajumuika kufanya mazoezi pamoja na kuja pamoja kama jamii,huku wakifurahia mandhari ya mji huo ,usafi na mpangilio mzuri.Watalaam wa afya wanasema kuwa kuondoa pia magari barabarani husaidi kupunguza uchafuzi wa hewa kaa na kuwapa wananchi nafasi ya kuvuta hewa safi. Kwenye makala haya tunakupa mengi zaidi kuhusu mkakati wa Car Free.
4/5/2023 • 10 minutes, 12 seconds
Ugonjwa wa Marburg unavyosambaa Afrika na mapambano ya TB nchini Kenya
Mataifa zaidi barani Afrika yameripoti virusi vya Marburg . Na kwenye mapambano ya TB nchini Kenya,ingawaje bado kuna idadi kubwa ya TB Sugu ,teknolojia mpya ya Gene expert iliyoboreshwa imeendelea kuchangia ubainishaji wa haraka
Equitoria Guinea imeripoti vifo 8 vinavyohusishwa na ugonjwa wa Marburg,huku Tanzania ikiwa imeripoti vifo vya watu watano.
Na kwenye mapambano ya TB nchini Kenya Michael Macharia mshauri wa kiufundi katika kanisa katoliki na pia Peter Muchui shujaa wa kupambana na TB wameeleza kuna hatua nyingi ambazo Kenya imepiga kuelekea mwaka wa 2030 ambapo mataifa yanatazamiwa yawe yameelekea kuushinda ugonjwa huo
3/28/2023 • 10 minutes, 22 seconds
Mapambano ya kumaliza kifua kifuu nchini Kenya kuelekea mwaka 2035
Kwa mujibu wa mpango kazi wa shirika la afya duniani,WHO,mataifa yanastahili kupunguza vifo vinavyosababishwa na TB kwa asilimia 90 na maambukizo mapya kwa asilimia 80.
Kila mwake tarehe 24 mwezi Machi ,dunia huungana kuadhimisha siku ya TB , kaulimbiu ya siku ya kifua kikuu duniani mwaka huu. ikiwa Ndiyo tunaweza kuwekeza zaidi kumaliza Kifua Kikuu nchini Kenya kufikia 2035 ikiwa tutashirikiana. Kukomesha Kifua Kikuu nchini Kenya si jukumu la Wizara ya Afya kupitia mpango wa kitaifa wa Kifua Kikuu pekee bali ni jukumu letu sote.
Aidha katika makala haya ,utaskia utambulisho kuhusu usafi wa kinywa naye daktari David Amenya.
3/21/2023 • 10 minutes, 12 seconds
Kongamano la afya kujadili uthabiti wa mifumo ya afya na athari za mabadiliko ya tabia nchi Afrika
Kuna haja ya Afrika kuwa na mifumo thabit ya afya ,kuweka rasli mali zake pamoja na kuwa ajenda moja kuhusu afya ,wakati huu athari hasi ya mabadiliko ya tabia nchi zinapoendelea kukabili ulimwengu
Viongozi wa mataifa ya Afrika pamoja na wadau kwenye sekta ya afya wamejadiliana jijini Kigali kwenye kongamano la AHAIC, kuhusu kutembea pamoja kuwa na ajenda inayofanana,mifumo inayostahimili majanga na jinsi ya kuoanisha swala la mabadiiko ya tabia nchi kwenye mifumo ya afya
3/14/2023 • 10 minutes, 14 seconds
Magonjwa yaliyotengwa ya Chikungunya na Homa ya Dengue bado changamoto
Magonjwa yaliyotengwa ingawaje hayajapewa kipau mbele bado ni changamoto kwa raia katika mataifa yanayoendelea
Katika makala haya ,tunakufahamisha kuhusu ugonjwa wa Chikungunya na Homa ya Dengue,inayosababishwa na mbu anayependa mahali pana joto.Katika maeneo haya aina ya mbu anayebeba virusi vinavyosababisha magonjwa haya mawili yenye dalili za kufanana ,huzalia katika maeneo yenye maji maji na huambukiza hata mchana.Daktari Hussein Gure Bilal anasimamia kitengo cha magonjwa yaliyotengwa katika kaunti ya Mombasa
3/8/2023 • 10 minutes, 4 seconds
Unene uliopitiliza na magonjwa yasiyoambukizwa
Shirika la afya duniani limeonya kuhusu kuongezeka kwa watu walio na uzito wa kupitiliza ,hali inayowaweka hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa
Shirikisho lilaloangazia unene ulimwenguni ,limesema zaidi ya nusu ya watu ulimwengu watakuwa na uzito wa juu au unene wa kupitiliza kufikia mwaka 2035 ikiwa hatua madhubuti kudhibiti hali hiyo hazitachukuliwa
Mataifa yanayoendelea na maskini barani Afrika na Asia yanatazamiwa kushuhidia hali hii.
Baadhi ya sababu zinazochangia hali hii ni ulaji na watu kushindwa kufanya mazoezi.Katika makala haya tunazungumza na watu wanaopambana kupunguza uzito,watalaam wa afya na pia wapishi kuelewa nini kinaweza kusaidia mtu kufanya chaguo zuri kuhusu chakula na mifumo ya maisha inayofanya mtu kuishi maisha yenye afya.
3/3/2023 • 9 minutes, 42 seconds
Wakaazi wa Mombasa washiriki matembezi ya masafa marefu kupambana na magonjwa yasiyoambukizwa
Shirika la afya duniani limeonya kuhusu ongezeko la magonjwa yasiyoambukizwa haswa katika mataifa yanayoendelea
Magonjwa yasiyoambukizwa ni changamoto kubwa kwa watu wengi kote ulimwenguni ,magonjwa haya yakichangiwa na maisha ya kisasa ambapo watu wengi hawazingatii vyakula vyenye lishe na mazoezi.Katika Makala haya tunakuletea namna moja ya kupambana na magonjwa haya ,mazoezi ya kutembea ambayo wakaazi wa Mombasa wamekumbatia.
2/21/2023 • 10 minutes, 19 seconds
Ongezeko la akina mama wanaochagua kujifungua kwa njia ya upasuaji nchini Kenya
Idadi ya Wanawake nchini Kenya wanaojifungua hospitalini imeongezeka ingawaje idadi kubwa pia wanachagua njia ya upasuaji
Licha ya gharama kubwa ya kujifungua kwa njia ya upasuaji,wanawake wengi nchini Kenya wanachagua njia hiyo na kupuzia hatari ambazo huwakumba wengi wanaotumia njia hiyo.
2/18/2023 • 9 minutes, 37 seconds
Vipimo vya DNA vinavyofanyika nyumbani
Utata kuhusu unasaba umekuwa ndiyo sababu ya watu wengi kutaka kufanya vipimo vya DNA ambavyo huwa ghali na kuhitaji umakini mkubwa.
Ugunduzi wa vifaa vya kupimia vipimo vya vinasaba au DNA nyumbani umeendelea kuibua mjadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maswala ya uhalisia wa vipimo hivyo na pia maadili ya kuzingatiwa katika vipimo hivyo.Daktari Yusuf Mahat anayehudumu katika hopsitali ya rufaa ya Nakura,nchini Kenya,anaeleza yote unayohitaji kufahamu kuhusu vipimo hivyo.
2/7/2023 • 10 minutes, 2 seconds
Kushamiri kwa kipindu pindu katika mataifa ya Afrika na juhudi kuikabili
Mataifa ya Afrika yameendelea kuripoti uwepo wa Kipindu Pindu nchi la Malawi ikiwa imeathirika zaidi.
Barani Afrika ,mlipuko wa ugonjwa Kipindu Pindu umeendelea kuripotiwa .Taifa la Malawi ilibidi kufunga shule na kuomba msaada kutoka mataifa mengine kuikabili. Nchini DRC ,maambukizo mapya pia yamezifdi kupanda na wahudumu wa afya wako mbioni kutoa chanjo kwa raia katika maeneo yenye idadi kubwa ya maambukizo mapya.
2/3/2023 • 10 minutes, 10 seconds
HAMASISHO KUHUSU SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI ( CERVICAL CANCER)
Saratani ya shingo ya kizazi ni mojawapo ya aina ya saratani inayoongoza katika idadi ya vifo dunia ikifuatiwa na saratani ya matiti.
Kwenye Makala ya wiki hii, mwandishi wetyu wa masuala ya afya Carol Korir, amezungumza na Dkt Yusuf Mahat, daktari nchini Kenya ilikufahamu zaidi kuhusu aina hii ya saratani.
1/24/2023 • 9 minutes, 50 seconds
Mzigo wa matumizi ya dawa za Kulevya nchini Kenya
Matumizi ya dawa za kulevya ,umeendelea kuwa mzigo katika mataifa mengi ,familia nyingi zikilazimika kuwapoteza jamaa zao ambao wangechangia ujenzi wa taifa
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani ,WHO ,kuna watu karibu milioni 40 ambao wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya na wanaohitaji msaada wa matibabu ya kitalaam kuwarejesha katika hali zao za kawaida.
Kwenye makala haya tumezungumza na raia,watu waliotumia dawa za kulevya ,walio wahi kuuza na watalaam kuhusu swala zima la dawa za kulevya. Je ina manufaa yoyote?
1/20/2023 • 9 minutes, 53 seconds
Mashirika ya kiraia yanavyopambana na unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya HIV Kenya
Unyanyapaa na ukosefu wa usawa kwenye mikakati ya kupambana na HIV ni baadhi ya sababu zinazorudisha nyuma mapambana kushinda UKIMWI
Katika mtaa wa Kibera ,jijini Nairobi Kenya ,mashirika ya kiraia yanawasaidia watu wanaoishi na virusi vya HIV kuishi maisha ya kawaida.Victor Moturi amezungumza na wakaazi wa Kibera wanaonufaika na mpango wa Mentor Mother
1/5/2023 • 9 minutes, 57 seconds
MSF inatumia teknolojia ya Antibiogo kupambana na usugu wa vimelea
Shirika la afya duniani WHO limeeleza wasi wasi kuhusu ongezeko la usugu wa vimelea.
Takwimu za WHO zinaeleza kuwa idadi ya kubwa ya dawa aina za antibiotics zinazotumika kwenye mataifa yanayoendelea,yanatumika vibaya na hii inatia wasi wasi ya kuongeza visa vya usugu wa vimelea vinavyosababisha magonjwa tofauti.
Shirika la madaktari wasio na mipaka,MSF limekuja na teknolojia mpya ya kukabili tatizo hili ,kutumia Antibiogo
12/26/2022 • 9 minutes, 20 seconds
WHO yasambaza chanjo ya Ebola Uganda ,utapiamlo ukiendelea kuwa Sugu Nigeria na nchi za Afrika
Shirika la afya duniania WHO limesambaza tayari dozi kadhaa za chanjo ya Ebola nchini Uganda. Na katika mataifa kadhaa ya Afrika yakiwemo Nigeria ,Kenya ,utapia mlo unaendelea kushuhudiwa.
Katika Makala haya ,tumeangazia shughuli ya kuchoma chanjo ya Ebola nchini Uganda. Vile vile hali ya baa la njaa nchini Nigeria na mataifa ya Pembe ya Afrika ,Afrika Mashariki ambapo hali hiyo imesababisha kuongezeka visa vya utapia mlo. Nchini Nigeria ,majimbo yanayokabiliwa na mashambulio ya makundi ya kijihadi ,yameathirika zaidi.
12/26/2022 • 10 minutes, 10 seconds
Waathiriwa wazungumzia unyanyapaa na ukosefu wa usawa
Shirika la umoja wa mataifa linaloratibu mikakati ya kupambana na Ukimwi ,UNAIDs limeonya kuhusu kutokuwa na usawa ulimwengu katika mapambano hayo
Watu ambao wameishi na virusi vya HIV na kuongoza kampeni za kupigana na ugonjwa wa UKIMWI wamehofu kuwa bado unyanyapaa na ukosefu wa usawa ni tishio kubwa. Maureen Murenga ni mwanaharakati kutoka Kenya na Meja Rubaramira Rubanga anatokea Uganda
12/9/2022 • 10 minutes, 16 seconds
Vyakula vya kiasili kama njia ya kukabili njaa
Watu wengi wanakabiliwa na njaa barani Afrika
Vyakula vya kiasili vimependekezwa kuwa njia mojawapo ya kupambana na njaa .Raia wanahimizwa kukuza na kukumbatia kando na vyakula walivyozoea kila siku.
12/5/2022 • 9 minutes, 25 seconds
Kuzalishwa kwa Vyakula vya GMO nchini Kenya,watalam wakinzana
Katika kujaribu kuimarisha usalama wa chakula nchini Kenya ,serikali iliondoa maarufuku ya uzalishaji na uagizaji wa vyakula vya GMO.
Serikali ya Kenya miezi michache ,iliyopita iliidhinisha kuzalishwa na kuagizwa kwa vyakula vinavyozalisha kwa njia ya kisayansi ,GMO ,kuliziba pengo la uhaba wa chakula.Watalaam ,wasayansi wamekuwa wakilumbana kuhusu usalama wa vyakula hivyo na mahakama ya Kenya kwa sasa imeharamisha amri hiyo ya serikali.
12/5/2022 • 10 minutes, 8 seconds
Uviko 19 ulivyoathiri mapambano dhidi ya Ukimwi DRC
Uwekezaji kwenye mapambano dhidi ya Uviko 19 umefanya serikali kuweka pembeni mikakati ya kupigana na Ukimwi
Katika maeneo kadhaa nchini DRC ,watalaam wameripoti ongezeko kubwa la maambukizo mapya ya virusi vya HIV na hata vifo tangu kuzuka kwa janga la Corona.
12/5/2022 • 9 minutes, 59 seconds
Dalili na utaratibu kuwasaidia wanaokabiliwa na matatizo ya afya ya akili
Katika makala hayo ,tunatambua namna unaweza kumsaidia mapema yeyote anayesumbuka na afya ya akili
Bara Afrika bado ina idadi kubwa ya watu wanaojitoa uhai au kusumbuliwa na matatizo ya akili. Ni muhimu basi kwa jamii kutambua baadhi ya viashiria vya mtu anayesumbuka na matatizo hayo na kuweza kumpa msaada mapema iwezekanavyo.
Mshauri nasaha Naomi Ngugi anatupa mwanga nini cha kuangalia kuweza kutambua mtu huenda ana matatizo hayo ya akili.
11/11/2022 • 10 minutes, 6 seconds
Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwenye Mataifa ya Kusini mwa Afrika
Nchi kadhaa barani Afrika na Asia zimeripoti mlipuko wa kipindupindu mwaka 2021 na 2022, ambapo nchini Kenya takwimu zilionyesha katika mwezi Oktoba, kaunti 6 katii ya 47 zilikuwa katika hatari.
11/9/2022 • 9 minutes, 51 seconds
Afya ya akili barani Afrika bado haizingatiwi
Kwenye makala haya ,tunazungumzia namna ya kujikinga na Ebola ,ugonjwa unaoendelea kuripotiwa nchini Uganda ,vile vile tunazungumzia afya ya akili ,wakati ulimwengu ukiwa umeadhimisha siku ya kimataifa ya afya ya akili ;jumatatu tarehe 10 mwezi wa Kumi.WHO ina was wasi idadi kubwa ya watu wanaojiua wanatokea Afrika
10/13/2022 • 9 minutes, 51 seconds
Hali ya Sekta ya Afya Afrika wakati wa magonjwa ya milipuko
Kwenye makala haya tunaangazia hali ya huduma za afya na hali ya wahudumu wa afya barani Afrika ,wakati huu ukanda huu ukiripoti kuongezeka kwa magonjwa ya milipuko.Shirika la afya duniani linasikitika kuwa wahudumu wa afya wanandelea kupoteza maisha wakati wanahudumia wagonjwa wakati wa magonjwa ya milipuko. Baada ya janga la Corona ,mataifa kadhaa ya Afrika yanashuhudia msambao wa ugonjwa wa Ebola
10/5/2022 • 10 minutes, 18 seconds
Mlipuko wa Ebola Sudan nchini Uganda
Tunazungumzia ugonjwa wa Ebola ambao unaendelea kuripotiwa nchini Uganda ukiwa ni mlipuko wa tano. Watu 24 wamepoteza maisha huku ugonjwa huu ukiendelea kusambaa. Aina hii ya Ebola Sudan japo haijaripotiwa kusababisha vifo vingi kwa haraka kama vile Ebola Zaire iliyokuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,bado haina chanjo.
Mataifa majirani kama vile Rwanda ,Tanzania na Kenya kutokana na hali hii zimeanza kuweka mikakati ya kukabiliana na hali ya dharura
9/29/2022 • 9 minutes, 24 seconds
Magari ya Tuk Tuk yanavyotumika Mombasa Kenya kuwaokoa akina mama
Idadi ya akina mama haswa waja wazito na watoto chini ya umri wa miaka mitatu wanaofariki ,bado iko juu barani Afrika.Hii ni kutokana na ukosefu wa huduma za afya au miundo mbinu ambazo wanawake wanaoweza kufikia kwa haraka.Jiji Mombasa ,Pwani ya Kenya wanaharakati wamekuja na mbinu ya Tuk Tuk ambazo zimekarabatiwa kuwa ambulensi kuwasaidia wanawake kufika hospitali kwa urahisi