Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Naibu rais wa Kenya Gachagua atimliwa, usalama wa mashariki ya DRC wajadiliwa Luanda
Kuondolewa madarakani kwa naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua na uteuzi wa profesa Kithure Kindiki, serikali ya Kinshasa yakaribisha makubaliano yaliyoafikiwa kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa DRC na Rwanda kuhusu suala kulitokomeza kundi la FDLR na Rwanda kusema iko tayari kuwaondoa wanajeshi kwenye ardhi ya Congo, maandamano ya upinzani kule Msumbiji baada ya uchaguzi mkuu, kuuawa kwa kiongozi wa Hamas Yahya Sunwar, uchaguzi mkuu wa Marekani na mengineyo.
10/19/2024 • 20 minutes, 16 seconds
Mchakato wa kuondolewa madarakani naibu rais wa Kenya, mazishi ya waliokufa Goma
Wabunge 281 walipiga kura ya ndio kumwondoa naibu wa Rais wa Kenya Rigathi Gachagua madarakani, mazishi ya watu waliokufamaji katika ajali ya Meli huko Goma DRC, ziara ya mkurugenzi wa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika, Dr Jean Kaseya, nchini Rwanda kutathmini mikakati ya kupambana na mlipuko wa MPOX pamoja na marburg, mafuriko makubwa nchini Mali, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon, mchakato wa uchaguzi mkuu kule Marekani. Ungana na Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi
10/12/2024 • 20 minutes, 17 seconds
Mswada wa kumwondoa naibu rais wa Kenya Kachagua, watu zaidi 78 wafamaji DRC
Makala imeangazia mchakato wa kumwondoa madarakani naibu wa rais wa Kenya Rigathi Gachagua, makumi ya watu wafamaji katika ajali ya boti huko Goma mashariki mwa DRC, hali nchini Rwanda na ugonjwa wa murburg, Uganda na Sudan, siasa za Nigeria na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na yale ya Hezbollah nchini Israeli na mambo mengine.
10/5/2024 • 20 minutes, 17 seconds
Lisu kuishitaki Tanzania kwa jaribio la kumuua, Kenya kupeleka polisi Haiti
Mwanasiasa wa upinzani kule Tanzania Tundu Lisu kuishitaki serikali na kampuni ya mawasiliano TIGO kwa jaribio la kumuua, rais wa Kenya William Ruto alisema polisi 2500 watapelekwa Haiti, wakati rais wa DRC Félix Tshisekedi atoa wito kwa jumuia ya kimataifa kuiwekea vikwazo Rwanda kwa kuivamia nchi yake na kushirikiana na waasi wa M23, hali nchini Sudan, siasa za Senegal na maeneo mengine ya Afrika magharibi, mashambulio ya jeshi la Israeli dhidi ya ngome za Hezbollah nchini Lebanon na mengineyo.
9/28/2024 • 20 minutes, 12 seconds
Rais wa Tanzania Samia Suluhu na wanadiplomasia, msamaha kwa mkuu wa polisi Kenya
Makala hii imeangazia kauli ya rais wa Tanzania kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao ilivyozua gumzo katika uga wa kimataifa, msamaha wa mahakama kwa afisa mkuu wa polisi Kenya, ziara ya mjumbe wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa anayehusika na masuala ya kibinadamu ulinzi wa amani Jean Pierre Lacroix huko DRC, UN kughadhabishwa na kuahirishwa uchaguzi wa sudan Kusini, jeshi Ia Israeli lashambulia Hezbollah kwa kulipua vifaa vyao vya mawasiliano na kwengineko duniani.
9/21/2024 • 20 minutes, 15 seconds
Uchunguzi wa miili ya wanafunzi waliokufa Kenya, hali ngumu ya wakimbizi DRC na mengineyo
Ni wiki iliyoshuhudia matukio mengi miongoni ni pamoja na serikali ya Kenya kuendelea na uchunguzi wa mkasa wa moto uliowauwa wanafunzi, maandamano ya maelfu ya wakimbizi kwenye mji wa Goma mashariki mwa DRC wakiomba serikali iwarejeshe makwao na kumaliza vita, kule Senegal rais Bassirou alilivunja Bunge la taifa, na mdahalo wa kwanza wa televisheni kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na makamu wa rais Kamala Harris wanaowania kiti cha urais katika uchaguzi wa Novemba na mengineyo.
9/14/2024 • 20 minutes, 14 seconds
Mkutano wa 9 China na Afrika, miili200 yazikwa DRC, wanafunzi 17 wateketea Kenya.
Makala hii imeangazia mkutano wa tisa kati ya China na Afrika huko Beijing, wafungwa zaidi ya 100 waliuawa katika gereza la makala nchini DRC, Kenya na mkasa wa moto ulivyowaua wanafunzi Kaunti ya Nyeri, uchaguzi kufanyika nchini Tunisia, na nchini Ufaransa Michel Barnier aliteuliwa kuwa waziri Mkuu, miezi miwili baada ya mvutano wa kisiasa nchini Ufaransa, na mambo mengine kwengineko duniani.
9/7/2024 • 20 minutes, 12 seconds
Kampeni ya Odinga kuwania uenyekiti tume ya AU, DRC yafungua kesi dhidi ya Rwanda
Uzinduzi wa kampeni ya aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga, anayegombea unyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, kongamano la 74 la WHO mjini Brazzaville, nchini Congo, DRC na Kampeni inayoitwa ICC Haki kwa DRC, hali ya usalama kuendelea kuzorota nchini Sudan, shambulio la kigaidi Burkina Faso laua zaidi ya watu 300, hali nchini Israeli, na mchakato wa uchaguzi wa Marekani mwezi Novemba
8/31/2024 • 20 minutes, 3 seconds
DRC yaathirika na M-Pox, Raila asema siasa za Kenya, basi! na mengineyo
Tumeangazia katika makala ya wiki hii ni pamoja na ugonjwa wa Mpox ulitangazwa kuwa dharura ya kimataifa, DRC ikiathirika zaidi, nchini Kenya Raila Odinga kutojihusisha tena na siasa, jeshi la Uganda lilivamia na kuharibu kambi ya kundi la waasi la LRA huko Sudan pande hasimu zasusia mkutano wa Geneva, nchini Marekani, makamu wa rais Kamala Harris akubali uteuzi wa chama chake cha Democratic kuwa mgombea wa nafasi ya urais, na mengineyo
8/24/2024 • 20 minutes, 12 seconds
Mpox yatangazwa janga la kimataifa la kiafya, mwanahabari wa Burundi Irangabiye aachiwa na mengineyo
Matukio ya dunia yaliyokithiri vichwa vya habari ni pamoja na virusi vya Mpox kutangazwa kuwa janga la dharura la kiafya huku bara la Afrika likiathiriwa zaidi, Burundi yamwachia mwanahabari aliyehukumiwa kifungo cha miaka 10, tutaangazia siasa za Tanzania baada ya wanasiasa wa upinzani kukamatwa baadaye wakaachiwa, lakini pia hatua za mazungumzo kule Geneva kuhusu amani nchini Sudan. Pia tutaangazia mgomo wa vyombo vya habari nchini Senegal kadhalika tutachambua wito wa Umoja wa Mataifa kutaka Afrika kupewa kiti cha kudumu katika baraza la usalama la umoja huoKule Gaza, kundi la Hamas limekataa masharti 'mpya' ya upatanishi na Israeli na mazungumzo ya kupata mkataba wa kusitisha vita hivyo, kurejelewa tena wiki hii jijini Cairo, Misri.
8/20/2024 • 20 minutes
Tshisekedi amshutumu mtangulizi wake Kabila, serikali mpya Kenya na mengineyo
Makala ya Juma hili imeangazia hukumu iliyotolewa dhidi ya kiongozi wa chama cha waasi wa M23/AFC mashariki mwa DRC Corneille Nangaa, Rais wa Kenya aapisha baraza jipya la mawaziri miongoni mwao wanasiasa wa upinzani, mapigano ya nchini Sudan, maandamano nchini Nigeria na uongozi mpya wa mpito nchini Bangladesh baada ya kutoroka kwa waziri mkuu pia tumengazia yaliyojiri kwengineko duniani.
8/10/2024 • 20 minutes, 14 seconds
Hamas yalaani mauaji ya kiongozi wake, mauaji ya kimbari DRC Genocost, na mengineyo
Makala hii imeangazia kuuawa kwa kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh nchini Iran, mazishi yake yalifanyika Doha, Urusi, mataifa ya Magharibi wabadilishana wafungwa, waziri mkuu wa DRC Judith Suminwa aongoza kumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya wakongo maarufu, Genocost, yaliyojiri nchini Kenya, na mgomo wa wafanyabiashara wa Uganda, hukumu dhidi ya dikteta wa zamani wa nchini Guinea na kwengineko duniani.
8/3/2024 • 20 minutes, 15 seconds
Michezo ya olimpiki yaanza Paris Ufaransa, Siasa za Kenya, DRC na kwengineko
Makala imeangazia hafla ya ufunguzi wa michezo ya Olimpiki ya Paris siku ya Ijumaa ya wiki hii, huku miundombinu ya treni za umeme ikishambuliwa, rais William Ruto atangaza baraza la mawaziri akiwajumuisha wanasiasa wanne wa upinzani, kesi dhidi ya kiongozi wa muungano wa waasi Corneille Nangaa jijini Kinshasa nchini DRC, Maandamano na kukamatwa kwa vijana kule Uganda, siasa za Afrika Magharibi, na Kaskazini,Joe Biden ajijiondoa katika ki nyang’anyiro cha uchauguzi huku Kamala Harris akiteuliwa kuwa mgombea wa chama cha Demokratic nchini Marekani.
7/27/2024 • 20 minutes, 6 seconds
Ruto ateua mawaziri wapya, Paul Kagame ashinda uchaguzi, usalama bado mashariki DRC
Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto ya kuwateua mawaziri wapya baada ya mashinikizo, nchi yake ikishuhudia maandamano ya vijana, Kukamatwa kwa mshukiwa wa mauaji ya watu ambao miili yao ilikutwa jalalani Kware jijini Nairobi akiri kuwaua wanawake 42, rais wa Rwanda Paul Kagame ashinda uchaguzi kwa kishindo, Waasi wa M23 na jeshi la congo FARDC wakubali kusimamisha vita baada ya Marekani kutangaza kuongeza muda wa siku 15 kuruhusu misaada ya kibinadamu...na mengineyo..kwengineko duniani ambako watu wamestushwa ulimwenguni kuhusu hitilafu iliyojitokeza kiteknolojia..-
7/20/2024 • 20 minutes, 12 seconds
Rais Ruto avunja baraza la mawaziri, uchaguzi huko Rwanda, usalama wazorota DRC
Makala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya rais wa Kenya William Ruto kulivunja baraza lake la mawaziri, huku inspekta mkuu wa polisi Japhet Koome akubali kujiuzulu, raia nchini Rwanda wajiandaa kushiriki uchaguzi mkuu wa rais na wabunge nchini Rwanda jumatatu ya julai 15, pia hali ya mapigan yashuhudiwa nchini DRC licha ya wito wa Marekani wa kusitishwa mapigano kwa sababu za kibinadamu.Hali iliyojiri kwenye nchi za Afrika magharibi na kaskazini, Ufaransa, na Marekani.
7/13/2024 • 20 minutes, 20 seconds
DRC: Wanajeshi wanaodaiwa kutoroka adui kwenye mapambano wahukumiwa
Miongoni mwa yale utakayosikia katika makala ya wiki hii ni pamoja na hatua ya Rais wa Kenya William Ruto kuzungumza na wapiga kura kwa njia ya mtandao wa X, wanajeshi waliotoroka adui DRC kuhukumiwa na vilevile mkutano wa nchi za Sahel zinazoongozwa na wanajeshi.
7/6/2024 • 20 minutes, 7 seconds
Ruto asema hatasaini mswada wa fedha 2024, M23 wauteka mji wa Kanyabayonga
Makala hii imeangazia maandamano nchini Kenya huku rais Ruto akisema hatasaini mswada wa fedha wa 2024 uliokuwa umeidhinishwa na wabunge walio wengi, waasi wa M23 huko DRC walifanikiwa kuuteka mji wa kimkakati wa Kanyabayonga wilayani Lubero mashariki mwa DRC, mgomo wa wafanyabiashara nchini Tanzania, na nini hatima yake, siasa za Afrika kusini lakini pia mdahalo kati ya rais wa zamani wa Marekani Donald Trump na Joe Biden kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, yaliyojiri nchini Ufaransa na kwengineko Duniani.
6/29/2024 • 20 minutes, 11 seconds
Maandamano nchini Kenya kupinga mswada wa fedha 2024, hali ya usalama DRC
Makala imeangazia hatua ya wabunge wa Kenya kuidhinisha mswada wa fedha wa 2024 kuingia katika hatua ya pili kabla ya kupitishwa licha ya maandamano makubwa nchini, ziara ya rais Felix Tshisekedi huko Lubumbashi, na kuendelea kwa mapigano kati ya FARDC na waasi wa M23, Uganda yawasamehe waasi wa zamani wa ADF, kuapishwa kwa rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa, hali huko Afrika Magharibi, na kwengineko duniani
6/22/2024 • 20 minutes, 14 seconds
Nchi za Afrika mashariki zawasilisha bajeti, serikali mpya DRC yazinduliwa
Tunayoangazia ni pamoja na kutangazwa kwa badgeti ya mwaka 2024/2024 kwenye nchi za jumuia ya Afrika mashariki, serikali ya mwanamke wa kwanza aliyeteuliwa kuwa waziri mkuu mpya huko DRC ilizinduliwa wiki hii, mauaji ya ADF huko Lubero mashariki mwa nchi hiyo, kifo cha makamu rais wa Malawi katika ajali ya ndege, lakini tutaangazia yaliyojiri Afrika Magharibi, kabla ya kuelekea kwengineko duniani
6/15/2024 • 20 minutes, 14 seconds
Mapigano Kanyabayonga DRC, katibu mkuu mpya wa EAC, na mengineyo
Makala hii imeangazia mkutano wa viongozi wa afrika huko Korea Kusini, hali ya wasiwasi kutanda kwenye mji wa Kanyabayonga, na mashirika kadhaa ya misaada kuanza kuhama, Burundi na kampeni ya kuvunja ndoa zisizorasmi, hotuba ya rais wa Uganda Yoweri M7, siasa za nchini Kenya, juhudi za kimataifa kuhusu amani ya Sudan, hali ya kisiasa Afrika kusini baada ya uchaguzi, hali ya usalama huko Gaza na siasa za Marekani
6/8/2024 • 20 minutes, 6 seconds
Serikali yatangazwa DRC, ndege aliyokodisha rais Ruto yazua gumzo na mengineyo
Tunayoangazia wiki hii ni pamoja na uteuzi wa baraza jipya la mawaziri huko DRC pia kuendelea mapigano eneo la mashariki mwa nchi hiyo, mchakato wa uchaguzi wa mwezi Julai nchini Rwanda, safari ya rais wa Kenya William Ruto huko Marekani na ndege aliyotumia ilivyozua gumzo, juhudi za kimataifa kuhusu amani ya Sudan, uchaguzi wa Afrika kusini, Hali ya Gaza na siasa za Marekani.
6/1/2024 • 20 minutes, 6 seconds
Marekani yataka Kenya kujiunga na NATO, mapigano mashariki yaendelea DRC
Makala imeangazia ziara ya rais wa Kenya William Ruto nchini Marekani, Uingereza na mpango wa kuwapeleka waomba hifadhi Rwanda, Jeshi la Congo FARDC laimarisha mapambano kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo, uchaguzi kule Afrika kusini, siasa za Chad baada ya kuapishwa kwa Mahamat Idriss Debi, siasa za Afrika Magharibi, hati ya kukamatwa kwa waziri mkuu wa Israeli B-Netanyahu, na viongozi wa Hamas pia mengineyo
5/25/2024 • 20 minutes, 13 seconds
Mazishi ya wakimbizi wa ndani 35 DRC, Uganda na Kenya zaimarisha mapatano yao
Baadhi ya mambo tunayoangazia ni mazishi ya watu 35 waliouawa baada ya bomu kulipuka katika kambi ya wakimbizi wa ndani eneo la Mugunga nje kidogo ya jiji la Goma, suala la Uingereza kuwahamisha wahamiaji huko Rwanda, ziara ya rais wa Uganda Yoweri Museveni nchini Kenya, siasa za Sudan na eneo la Afrika Magharibi, pia huko Ulaya na Marekani
5/18/2024 • 20 minutes, 9 seconds
Mazungumzo ya amani kuhusu Sudan Kusini yamerejelewa jijini Nairobi, Kenya
Katika makala ya wiki hii baadhi ya matukio ya ulimwengu tutakayoangazia ni mazungumzo ya kutafuta amani nchini Sudan Kusini ambayo yalianza Alhamisi jijini Nairobi, lakini pia madaktari nchini Kenya kusitisha mgomo wa siku 56, vilevile kule DRC, shirika la OCHA kusema kuongezeka kwa mapigano huko Kivu Kaskazini kumesababisha wimbi jipya la watu kuyahama makazi yao. Nchi ya Chad, ina rais mpya ambaye alikuwa kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby Itno, kadhalika tutaangazia hali kule Gaza na nchini Ukraine.
5/11/2024 • 19 minutes, 59 seconds
Athari za mvua katika ukanda wa Afrika Mashariki haswa nchini Kenya
Wiki hii baadhi ya mambo tunayoangazia ni athari za mvua katika ukanda wa Afrika Mashariki, pia mgogoro kule Sudan, lakini pia kauli ya Ufaransa kwa Rwanda kuacha kuunga mkono kundi la M23 kule DRC. Kadhalika tutaangazia uhuru wa vyombo vya habari kuminywa nchini Burkina Faso lakini pia kibali cha kukamatwa kwa rais wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
5/4/2024 • 20 minutes, 2 seconds
Tanzania yaadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika ,mafuriko yaripotiwa Kenya
Makala haya yanaangazia yaliyojiri nchini Kenya na Tanzania kufuatia mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 70 ,mgomo wa madaktari nchini Kenya, Tanzania kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, safari za wahamiaji walioko nchini Uingereza kuelekea nchini RwandaTutaangazia pia uchaguzi wa wabunge nchini Togo,usalama wa Burkina Faso , na Ulimweguni tutazidi kuangazia Mzozo unaondelea baina ya Israel na Hamas .
4/27/2024 • 19 minutes, 51 seconds
Mkuu wa majeshi ya Kenya Francis Ogolla aaga dunia, ziara ya wajumbe wa EU DRC
Makala hii inaangazia yaliyojiri nchini Kenya na kifo cha mkuu wa majeshi ya nchi hiyo KDF aliyepoteza maisha na maafdisa wengine tisa wa jeshi katika ajali ya helikopta Alhamisi Aprili 18, rais William Ruto alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa, mgomo wa wafanyabiashara huko Kampala Uganda, ziara ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa na EU huko Goma kutathmini hali ya kibinadamu kwa waliokimbia mapigano ya M23, Senegal, pia Togo kuhusu ziara ya ujumbe wa ECOWAS, lakini pia mashambulio kati ya Iran na Israel.
4/20/2024 • 20 minutes, 7 seconds
Miaka 30 ya mauaji ya kimbari Rwanda, UN yaondoa jeshi lake DRC na mengineyo duniani
Makala yameangazia mambo mengi ikiwemo maadhimisho ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi yanaendelea wiki hii, MONUSCO kuanza kuwaondoa wanajeshi wake eneo la mashariki mwa DRC, mgomo wa madaktari nchini Kenya, mwaka mmoja wa mzozo wa Sudani kutimia jumatatu ya aprili 15 na mengineyo duniani. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi
4/13/2024 • 20 minutes, 15 seconds
Maadhimisho ya miaka 30 mauaji ya kimbari nchini Rwanda, uteuzi wa waziri mkuu mpya DRC
Ni makala maalum, kuhusu kumbukumbu ya miaka 30 ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994, tunahoji mchakato wa maridhiano umefikia wapi miaka 30 baadaye..... hali iko vipi kwa sasa. na dunia imepata somo gani? Pia kuhusu mauaji hayo, tutarejelea kauli ya Rais Emanuel Macron iliyoonekana kuwa inalenga kutuliza hisia za waathiriwa.Huko DRC uteuzi wa Judith Tuluka Suminwa, mwanamke wa kwanza kuwa waziri mkuu. Mahakama nchini Uganda ilitoa uamuzi wake kuhusu sheria dhidi ya ushoga. Kabla ya kwenda Kenya, Sudani..pamoja na Senegal ambako Bassirou DF aliapishwa kuwa rais mpya, tutakwenda Israeli na maeneo mengine duniani.
4/6/2024 • 20 minutes, 18 seconds
Diomaye Faye kuapishwa jumanne kama rais wa Senegal, ziara ya rais wa DRC Mauretania
Rais mteule wa senegal akutana na rais anayemaliza muhula wake Macky Sall, chama kipya cha aliyekuwa rais wa Afrika kusini Jacob Zuma chazuwiwa kushiriki uchaguzi wa mwezi mei,kamati ya haki za kibinadamu ya umoja wa mataifa, yaitaka Uingereza kuachana na mpango wake wa kuwahamisha wahamiaji kwenda nchini Rwanda, na rais wa DRC Félix Tshisekedi ahitimisha ziara yake huko Mauretania, tutaangazia siasa za Kenya, Tanzania, yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani.
3/30/2024 • 20 minutes, 10 seconds
Rais Museveni amteua mwanae kuwa mkuu wa majeshi, kifo cha okende kilipangwa
Makala hii imeangazia hatua ya rais wa Uganda Yoweri Museveni ya kumteua mwanawe kuwa mkuu wa majeshi ya nchi hiyo, mazishi ya mwanasiasa Cherubin Okende, yaliyojiri nchini Rwanda, lakini pia Sudan huko ambako wiki hii Marekani ilisema kuwa ina matumaini mazungumzo ya kumaliza mzozo wa nchi hiyo yatarejea hivi karibuni baada ya mfungo wa Ramadan, uchaguzi wa urais huko Senegal jumapili ya Marchi 24 tumeangazia yaliyojiri huko Israeli na kwengineko duniani. Ungana nami Reuben Lukumbuka
3/23/2024 • 20 minutes, 7 seconds
Kagame akubali kukutana na Tshisekedi, upinzani Burundi wamfukuza rais wake chamani, Ousmane Sonko aachiwa kule Senegal...
Kwenye Makala ya wiki hii tunaangazia hatua ya Rais Kagame kukubali kukutana na mwenzake wa DRC Tshisekedi, pia tutaangalia alivyofukuzwa chamani kiongozi wa chama cha CNL nchini Burundi, Agathon Rwassa, lakini vilevile kilichojadiliwa katika mkutano kati ya marais wa Kenya, Tanzania na Uganda. Tutatupia jicho hali ya kibinadamu nchini Sudan, lakini pia siasa za Senegal baada ya kuachiwa kwa Ousmane Sonko, siku chache kabla ya uchaguzi wa Machi 24, kule Nigeria tutaangalia yanayojiri baada ya wanafunzi kutekwa na rais Tinubu kusema hawatatii agizo la watekaji la kutaka kulipwa ili kuwaachia wanafunzi hao.Pia hali kule Haiti baada ya waziri mkuu Ariel Henry kukubali kujiuzulu, Meli ya kwanza ya chakula cha msaada kutoka Cyprus kuwasili Gaza na pia siasa za Marekani baada ya rais Joe Biden na mtangulizi wake Donald Trump kushinda uteuzi katika vyama vyao.Niliyeshika usukani ni Jupiter Mayaka kwa niaba ya Ruben Lukumbuka ambaye yuko Pwani ya Kenya anakula upepo wa bahari. Kwa mengi zaidi bonyeza linki usikilize makala.
3/16/2024 • 19 minutes, 59 seconds
Mashirika ya misaada yatatizika kuhudumia wakimbizi DRC, Ufaransa yahalalisha uaviaji
Hali ya usalama kuendelea kuzorota mashariki mwa DRC baada ya waasi wa M23 kuteka miji kadhaa kama Nyanzale na maeneo jirani, wabunge nchini Uingereza kupinga mpango wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda, uchaguzi wa urais kufanyika marchi 24 nchini Senegal, mpya wa 32 wa jumuiya ya kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.
3/9/2024 • 20 minutes, 6 seconds
Kifo cha rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, hali ya usalama DRC na mengineyo
Yaliyojiri wiki hii ni pamoja na kifo cha rais wa zamani wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, na kauli za rais Felix Tshisekedi kuwa yuko tayari kwa mazungumzo na rais mwenza wa Rwanda Paul Kagame, ziara ya waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed nchini Tanzania na pia Kenya, maandamano ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kule Arusha, yaliyojiri nchini Rwanda, kwenye kanda ya Afrika magharibi lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.
3/2/2024 • 20 minutes, 11 seconds
Rais wa DRC F.Tshisekedi kudumisha amani na jirani zake, mazishi ya mwanariadha Kiptum
Makala hii imeangazia kuzorota kwa hali ya usalama pembezoni mwa mji wa Sake DRC,na kauli za rais Felix Tshisekedi mbele ya wanahabari wiki jijini Kinshasa, maandamano ya chama cha upinzani cha Chadema nchini Tanzania kule Mbeya, mazishi ya mwanariadha wa Kenya aliyekuwa anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za marathon Kelvin Kiptum, yaliyojiri nchini Rwanda, na pia kwenye kanda ya Afrika magharibi lakini pia hali ya Israeli na kwengineko duniani.
2/24/2024 • 20 minutes, 13 seconds
Mashambulio mjini Sake mashariki ya DRC, hali ya Kenya, kifo cha mpinzani wa Urusi
Wiki imejaa matukio ya kutamausha kwanza; wanajeshi wawili wa Afrika kusini waliuawa mashariki mwa DRC, kinara wa upinzani wa nchini Kenya Raila Odinga kuwania uwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, maandamano ya wapinzani nchini Tanzania, yaliyojiri Sudani, pia Senegal huko Afrika magharibi, kifo cha mpinzani huko Urusi Alexei Navalyn, shinikizo za kimataifa dhidi ya Israeli ikubali kusitisha vita dhidi ya Hamas,na mengineyo
2/17/2024 • 20 minutes, 10 seconds
Usalama waendelea kuzorota mashariki DRC,UN na hali ya Sudan
Hali ya wasiwasi iliyoshuhudiwa kwenye mji wa Goma, baada ya waasi wa M23 kuonekana kuukaribia mji huo huko mashariki mwa DRC,ziara ya rais wa Poland nchini Kenya na huko Rwanda, kuapishwa kwa rais mpya wa muda nchini Namibia baada ya kifo cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Hague GeinGhob, yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika magharibi pia uteuzi wa baraza jipya la mawaziri nchini Ufaransa, siasa za Marekani na kwengineko duniani
2/10/2024 • 20 minutes, 1 second
Watatu wafa katika mlipuko wa gas jijini Nairobi Kenya, M23 waendeleza mapigano DRC
Miongoni ni pamoja na watu watatu wafariki dunia katika mlipuko wa gesi jijini Nairobi nchini Kenya, kundi la waasi wa Uganda wa ADF waendeleza mauaji ya raia wa kawaida nchini DRC,lakini pia yaliyojiri kwenye kanda ya Afrika Mashariki, Afrika magharibi na Mgomo wa wakulima nchini Ufaransa, hali ya Israeli na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
2/3/2024 • 20 minutes, 7 seconds
Mvutano kati ya Kigali na Bujumbura, mauaji ya watu zaidi ya 10 Mwesso DRC
Yaliyojiri wiki hii inaangazia kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame kwamba ataitetea nchi yake kwa gharama yoyote ile, upinzani nchini Tanzania uliandamana kupinga mabadiliko ya sheria za uchaguzi, mauaji ya watu zaidi ya kumi mjini Mwesso mashariki mwa DRC, uchaguzi visiwani Komoro hali katika ukanda wa Afrika Magharibi lakini pia uchaguzi mdogo huko Marekani,
1/27/2024 • 20 minutes, 9 seconds
Kuapishwa kwa rais Felix Tshisekedi jumamosi, Rwana na UK njia panda bado
Makala hii imeangazia kuhusu kuapishwa rais wa DRC Félix Tshisekedi baada Mahakama ya katiba kuidhinisha ushindi wake katika uchaguzi wa desemba 20, viongozi wa nchi wananchama wa IGAD walikutana jijini Kampala huku wakitoa wito wa kusitishwa mapigano Sudan, waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak na mpango wa kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda.
1/20/2024 • 20 minutes, 14 seconds
Mahakama ya katiba yaidhisha ushindi wa Tshisekedi, Burundi yafunga mpaka na Rwanda
Mahakama ya katiba huko DRC iliidhinisha ushindi wa rais Félix Tshisekedi,rais wa Uganda Yoweri Museveni awatahadharisha waasi wa ADF, Waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak akabiliwa na wakati mgumu kuhusu suala la kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda, yaliyojiri katika ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia uteuzi wa Gabriel Attal kuwa waziri Mkuu wa kwanza kijana nchini Ufaransa, mashambulio ya jeshi la Israeli yawaathiri raia wa kawaida mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
1/13/2024 • 20 minutes, 9 seconds
Dunia yakaribisha mwaka mpya, mvutano kati ya rais Ruto na idara ya mahakama
Miongoni mwa habari kuu za wiki hii ni pamoja na dunia kuukaribisha mwaka mpya 2024, mvutano kati ya rais wa Kenya William Ruto na idara za mahakama, wapinzani wa DRC waendelea kuonesha kutofurahishwa na ushindi wa rais Felix Tshisekedi kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa desemba 20 mwaka uliopita, yaliyotangazwa na CENI, yaliyojiri katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia mashambulio mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
1/6/2024 • 20 minutes, 15 seconds
DRC: Rais Felix Tshisekedi ashinda uchaguzi kwa muhula wa pili
Baadhi ya habari ambazo tumeangazia ni matokeo ya uchaguzi nchini DRC ambapo Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi kwa muhula wa pili kwa asilimia 73.34, katika matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa na Ceni Jumapili jioni. Tutaangazia pia mashambulio ya ADF kule Uganda lakini pia mkutano wa ana kwa ana kati ya majenerali wanaopigana Sudan ambao haukufanikiwa, hali kule Nigeria kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika jimbo la Plateau, Urusi kufungua tena ubalozi wake nchini Burkina Faso na ulimwenguni tutazidi kuangazia hali ya vita vya Gaza
12/31/2023 • 20 minutes, 1 second
Raia DRC wasubiri matokeo ya uchaguzi, Rais Biden amsuta Netanyahu kulinda raia
Kwenye makala yaliyojiri wiki hii, tumeangazia uchaguzi kule DRC wakati huu shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea, kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki chaondoka rasmi nchini DRC, mapigano kule Sudan. Pia tumeangazia uhusiano wa kidiplomasia kati ya Ufaransa na Niger, pia siasa za Afrika Kusini na kwingineko ulimwenguni tumeangazia masaibu yanayomkabili Donald Trump lakini pia hali kule Gaza.
12/24/2023 • 20 minutes, 1 second
CENI uchaguzi utafanyika desemba 20 DRC, Uingereza kuhamishia wahamiaji Rwanda
Yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC CENI kusisitiza kuwa uchaguzi utafanyika desemba 20 kama ulivyopangwa; wakati huo huo aliyekuwa mwenyekiti wa CENI Corneille Nangaa alizindua chama kipya cha AFC Alliance Fleuve Congo, wabunge wa Uingereza walipiga kura kuunga mkono mpango wa kuwahamishia wahamiaji nchini Rwanda, siasa za Senegal, na huko Niger Mahakama ya ECOWAS yaamuru kuachiwa huru kiongozi aliepinduliwa nchini Niger Muhamed Bazoum, Jeshi la Israel laendeleza mashambulio mjini Gaza, na pia matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.
12/16/2023 • 20 minutes, 15 seconds
Rwanda na Uingereza zasaini mkataba kuhusu wahamiaji, jeshi la EAC laondoka DRC
Makala hii imeangazia hatua ya Rwanda na Uingereza kutiliana saini mkataba mpya kuhusu kuwahamisha wahamiaji kutoka Uingereza kupelekwa Rwanda, makumi ya watu wapoteza maisha katika mafuriko nchini Tanzania, kampeni za uchaguzi mkuu zashika kasi kuelekea desemba 20 huko DRC, Waasi wa M23 wazidisha Mapigano eneo la mashariki mwa DRC, hali ya siasa nchini Kenya, na mataifa mengine ya Afrika magharibi, lakini pia kongamano la Kimataifa kuhusu hali ya hewa waendelea Dubai kwenye Nchi ya Falme za kiarabu, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani...
12/9/2023 • 20 minutes, 15 seconds
Mkutano wa COP28, EU kuondoa waangalizi wake wa Uchaguzi huko DRC na mengineyo
Makala hii imeangazia mkutano wa kilele wa kimataifa kuhusu hali ya tabia nchi COP28 huko Dubai, kuachiwa kwa baadhi ya mateka waliokuwa wameshikilwia na Hamas huko Gaza, DRC ilisema muda wa Kuwepo kwa vikosi vya Jumuia ya EAC hautaongezwa baada ya desemba 08, Umoja wa Ulaya waamua kusitisha mpango wa kuwasambaza waangalizi wake wa uchaguzi nchini DRC, siasa za Kenya, Tanzania, na mengine yaliyojiri kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi na kwengineko duniani.
12/2/2023 • 20 minutes, 14 seconds
Rais George Weah akubali kushindwa kwenye duru ya pili ya uchaguzi
Matukio kadhaa wa kadhaa yamefanyika ulimwenguni kukiwemo George Weah kukubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi nchini Liberia kwa Joseph Boakai. Hii ina maana atakuwa miongoni mwa marais waliohudumu kwa muhula mmoja. Tutaangazia pia mafuriko yalivyoathiri nchi nyingi, Hali ya usalama na kisiasa nchini DRC, kadhalika Kenya kuidhinisha polisi kutumwa Haiti, tutaangazia uamuzi wa mahakama ya Uingereza kuhusu sera ya wahamiaji nchini Rwanda, kadhalika usalama Mali na chaguzi nchini Madagascar na hali halisi katika vita vinavyoendelea huko Gaza na pia tutaangazia mkutano kati ya Rais Joe Biden na Xi Jinping.
11/18/2023 • 20 minutes, 3 seconds
Burundi kuondoa wanajeshi wake DRC, Ufaransa na mkutano kuhusu Gaza
Makala ya Yaliyojiri wiki Hii, imeangazia hatua ya kikosi cha wanajeshi wa Burundi chini ya Jumuia ya Afrika Mashariki, EAC kujiondoa maeneo ya mashariki mwa DRC, mapigano kati ya jeshi la serikali ya DR Congo FARDC na waasi wa M23 mkowani Kivu kaskazini, hotuba ya rais wa Kenya wiki hii yazua hisia mseto, hali ya kibinadamu nchini Sudan yausikitisha Umoja wa mataifa, kongamano la Kimataifa kuhusu Gaza lafunguliwa nchini Ufaransa na mengine mengi duniani.
11/11/2023 • 20 minutes, 15 seconds
Zaiara ya mfalme wa tatu wa Uingereza, kukamatwa kwa muasi wa ADF Uganda
Makala ya wiki hii imeangazia matukio kadhaa yaliyojitokeza wiki hii kote ulimwenguni, miongoni ni pamoja na ziara ya mfalme Charles wa tatu wa Uingereza nchini Kenya, ambapo pia rais wa shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kule Tanzania, hali ya kisiasa na kiusalama nchini DRC, mkutano kuhusu utalii barani Afrika ulitamatika jijini Kigali, nchini Rwanda, na matukio mengine yaliyoshuhudiwa kwenye ukanda huu na kwengineko duniani.
11/4/2023 • 20 minutes, 18 seconds
Ziara ya rais E. Macron huko Israel, mapigano mashari mwa DRC, siasa za Kenya
Makala hii imeangazia ziara ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Israeli, maombi kutaka bunge liidhinishe mpango wa kutumwa kwa askari wake elfu 1 nchini Haiti, hali ya kisiasa na usalama huko DRC, nchini Sudan, lakini pia hali tete ya kiafya ya kinara wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani. Ungana na mwanahabari wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi
10/28/2023 • 20 minutes, 10 seconds
Mashambulio ya Gaza huko Israeli, siasa za DRC, Kenya na Burundi na mengineyo
Makala hii imeangazia ziara ya rais wa Marekani Joe Biden huko Israeli, kuuawa kwa watalii huko Uganda mpakani na DRC, siasa za Kenya na siku ya mashujaa iliyoadhimishwa oktoba 20, hali ya kisiasa na usalama huko DRC, Burundi na nchini Sudan lakini pia ziara ya rais wa Chad nchini Ufaransa, na matukio mengine mengi ya wiki hii duniani.
10/21/2023 • 20 minutes, 12 seconds
Mashambulio ya Hamas nchini Israel, siasa za DRC na ukanda wa Afrika mashariki
Miongoni mwa mengi yaliyoangaziwa katika makala ya juma hili ni pamoja na mashambulio yaliyofanywa na kundi la Hamas huko Israeli, siasa za Kenya, Uganda na Tanzania, kulegezwa kwa hali ya dharura iliyowekwa kwenye majimbo mawili ya Kivu kaskazini na Ituri huko DRC, hali ya Sudan na kuondoka kwa awamu ya kwanza ya wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger, na mengineyo duniani.
10/14/2023 • 20 minutes, 14 seconds
Mwanasiasa wa upinzani Uganda Bobi Wine akamatwa, mauaji ya Sondu Kenya
Makala ya wiki hii imeangazia baadhi ya habari kuu za dunia matukio makubwa kama vile kukamatwa na kuwekwa katika kizuizi cha nyumbani kwa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Bobi Wine, ziara ya rais wa Kenya William Ruto magharibi mwa Nchi na kuwasilishwa kwa faili za wanasiasa wanaogombea urais katika ofisi za Tume ya uchaguzi nchini DRC, CENI, siasa na hali ya ukanda wa Afrika magharibi na kaskazini na kwengineko duniani.
10/7/2023 • 20 minutes, 8 seconds
Kenya, Uganda na Tanzania kuandaa Afcon 2027, Tshisekedi asema uchaguzi utafanyika tu
Katika makala hii tumeangazia baadhi ya habari kuu za dunia za wiki hii na miongoni ni pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania ziliteuliwa na shirikisho la soka Afrika CAF kuwa wenyeji wa mashindano ya kombe la Afrika mwaka 2027, DRC na Rwanda ziligubika mkutano wa Baraza la Umoja wa mataifa, balozi wa Ufaransa nchini Niger Sylvain Itté aliongea kwa mara ya kwanza kuhusu namna alivyofurushwa Niamey, Siasa za Marekani Israeli na kwengineko duniani ni miongoni mwa mengi tumekuandalia
9/30/2023 • 20 minutes, 13 seconds
Mkutano wa 78 wa umoja wa mataifa, rais wa DRC aitaka Monusco kuondoka DRC
Makala hii imeangazia hotuba za viongozi wa Afrika katika baraza la Umoja wa mataifa huko Newyork Marekani,rais wa zamani wa jamhuri ya Afrika ya kati ahukumiwa kifungo cha maisha jela, Ecowass na hali ya nchini Niger, ziara ya Mfalme wa 3 wa Uingereza nchini Ufaransa lakini kiongozi wa Kanisa katoliki Papa Francis kule Marseilla Ufaransa, na mengine mengi.
9/23/2023 • 20 minutes, 11 seconds
Mafuriko nchini Libya tetemeko la ardhi nchini Morocco, na siasa za DRC
Makala hii inaangazia hali inavyoendelea huko Libya baada ya mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu idadi ya vifo kutokana na Tetemeko la ardhi huko Morocco yaendelea kuongezeka, aliyekuwa mshirika wa karibu wake rais wa DRC Félix Tshisekedi na naibu spika wa bunge Jean Marc Kabund ahukumiwa kifungo cha miaka 7, tutaangazia hali ya kisiasa na kijamii nchini Kenya, Tanzania lakini pia ziara ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong UN huko Urusi pamoja na mambo mengine.
9/16/2023 • 20 minutes, 18 seconds
Zaidi ya watu 600 wamefariki kutokana na tetemeko la ardhi nchini Morocco
Tetemeko kubwa la ardhi siku ya Ijumaa usiku limeitikisa nchi ya Morocco wakati huu zaidi ya watu 600 wakiafriki, kwa mujibu wa takwimu za wizara ya mambo ya ndani, idadi hii ikihofiwa kuendelea kuongezeka. Tetemeko hilo la ukubwa wa 6.8 lilipiga kilomita 72 kusini magharibi mwa eneo la watalii la Marrakesh, Utafiti wa Jiolojia wa Marekani umeripoti.Tetemeko pia ilisikika katika miji ya pwani ya Rabat, Casablanca na Essaouira.
9/9/2023 • 20 minutes, 1 second
Mapinduzi Gabon, moto Afrika Kusini, siasa na usalama DRC na masaibu ya Trump
Mambo ambayo yamegonga vichwa vya habari ni pamoja na mapinduzi ya Gabon na kiongozi kuteuliwa amabye anatarajiwa kuapishwa Jumatatu ya Septemba 4, pia tuaangalia mapinduzi katika nchi jirani ya Niger, vilevile kisa cha kusikitisha cha moto nchini Afrika Kusini uliogharimu maisha ya zaidi ya watu 70. Kadhalika tutaangalia kuteuliwa kwa rais wa DRC Felix Tschisekedi kupeperusha bendera ya cha UPDS katika uchaguzi wa Disemba na tunavuka Tanzania ambapo rais Samia Suluhu alifanya mabadiliko katika baraza lake na kusema kuwa hatua hiyo si adhabu.
9/2/2023 • 20 minutes
Matukio ya wiki hii, kifo cha kiongozi wa wagner, siasa za DRC, Kenya, na kwengineko
Makala ya Yaliyojiri wiki hii,imeangazia kuenea kwa taarifa ya kifo cha mtu anayedaiwa kuwa kiongozi wa kundi la mamluki wa Wagner Yevgeny Prigozhin, mkutano wa Brics huko Johannesburg Afrika kusini, siasa za Kenya, DRC, matukio ya kule Uganda, uchaguzi wa Gabon, pia hali inavyoendelea Niger na kwengineko duniani
8/26/2023 • 19 minutes, 58 seconds
Hali ya dharura mashariki ya DRC, siasa za Kenya, Niger na kwengineko
Tathmini juu ya hali ya dharura iliyotangazwa na rais wa DRC Felix Tshisekedi kwenye mikowa ya Kivu kaskazini na Ituri, Siasa za Kenya, kukamatwa kwa Dokta Slaa mwanasiasa mkongwe wa nchini Tanzania, Hali ya huko Sudan, Niger na kwengineko duniani. Kupata mengi zaidi, ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka
8/19/2023 • 20 minutes, 3 seconds
Taasisi za kimataifa zasikitikia mazingira anayozuiliwa Mohamed Bazoum
Tumekuandalia mengi tu ikiwemo mazungumzo kati ya serikali na upinzani yalioaanza kule nchini Kenya, siasa na maandalizi ya uchaguzi mkuu huko nchini DRC na mengine mengi tu.
8/12/2023 • 20 minutes, 2 seconds
Juhudi za kimataifa na za kikanda zaendelea kurejesha Bazoum Niger
Makala hii imeangazia juhudi za kikanda na za kimataifa kuendelea ili kulaani mapinduzi ya kijeshi nchini Niger na kutaka kurejeshwa kwa utawala wa kiraia, Umoja wa mataifa ulikaribisha hatua ya Kenya kukubali kuongoza kikosi cha ulinzi huko Haiti, Siasa za DRC kuelekea Uchaguzi wa desemba 20, Sudan na kwengineko duniani, kwa hayo na mengine mengi ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka
8/5/2023 • 20 minutes, 9 seconds
Mapinduzi ya kijeshi nchini Niger, mkutano wa Wakuu wa Afrika na Urusi
Makala hii imeangazia mkutano wa viongozi wa Afrika na Urusi huko St Petersburg, Urusi, mapinduzi ya Niger, mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kule Daresalaam nchini Tanzania, upinzani wa Kenya ulitangaza kusitisha maandamano, Siasa za DRC na ufunguzi wa michezo ya Francophonie, hali ya Sudan na matukio mengine duniani.
7/29/2023 • 20 minutes, 5 seconds
Maandamano ya upinzani nchini Kenya, DRC mauaji ya Okende yalipangwa asema Ambongo
Makala hii imeangazia kuhusu maandamano yaliyoitishwa na wapinzani nchini Kenya, ziara ya rais wa Hungary nchini Tanzania, lakini pia uchunguzi kuhusu mauaji ya Cherubin Okende, mwanasiasa mshirika wa karibu wake Moise Katumbi, aliyeuawa katika mazingira tatanishi katika mji mkuu wa Kinshasa, nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo lakini pia siasa za kikanda, na mambo mengine duniani..
7/22/2023 • 20 minutes, 11 seconds
Wapinzani nchini DRC watoa tamko kuhusu kifo cha Okende, maandamano nchini Kenya
Makala hii imeangazia ripoti mbali mbali za waandishi wetu lakini kubwa ni kuhusu mauaji ya kuvizia dhidi ya mwanasiasa wa upinzani na mshirika wa karibu wake Moise Katumbi kule DRC pamoja na kauli ya Upinzani nchini Kenya kuhusu maandamano kuendelea juma lijalo, kule Sudan mapigano bado yaendelea, ICC yasema inafuatilia visa vya uhalifu dhidi ya binadamu, nchini Senegeal, mpinzani Ousmane Sonko ateuliwa na chame chake kuwa mgombea wa urais, na mambo mengine mbali mbali
7/15/2023 • 20 minutes, 4 seconds
Polisi wa Kenya watawanya maandamano ya upinzani, M23 na ripoti ya EU DRC
Makala hii imeangazia maandamano yaliyofanyika jijini Nairobi na maeneo mengine nchini Kenya, siku ya Kiswahili duniani, lakini pia ripoti ya umoja wa Ulaya kuhusu vita ya M23 mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mapigano ya Sudan na matukio mengine kwengineko duniani ..Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi.
7/8/2023 • 20 minutes, 2 seconds
Waombahifadhi kutumwa Rwanda, kinyume cha sheria: Mahakama, miaka 63 uhuru wa DRC
Makala hii imeangazia hatua ya mahakama ya London Uingereza kuhusu waomba hifadhi kwamba ni kinyume cha sheria na kwamba Rwanda si salama huku Rwanda ikisema itakata rufaa wahamiaji walioko nchini humo. Maadhimisho ya miaka 63 ya uhuru wa DRC na mkutano wa Luanda Angola kuhusu amani ya mashariki ya Nchi hiyo, imeangazia pia yaliyojiri nchini Kenya, Uganda, Sudan an Ethiopia na kwengineko duniani.
7/1/2023 • 20 minutes, 4 seconds
Mkutano kuhusu madeni na mabadiliko ya tabianchi watamatika Paris Ufaransa, usalama DRC
Makala hii imeangazia mkutano wa kimataifa unaolenga kutafuta mwafaka kuhusu namna ya kubadili mfumo wa ufadhili wa kifedha na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwenye mataifa yote ya dunia. Shambulio liliotekelezwa na waasi wa Uganda ADF dhidi ya shule moja laua 42, na mkataba wa kibiashara kati ya Kenya na Umoja wau laya, mchakato wa uchaguzi nchini DRC na pia yaliyojiri kwenye mataifa mengine duniani..
6/24/2023 • 20 minutes, 20 seconds
Ziara ya marais wanne wa Afrika huko Urusi na Ukraine, mauaji ya wakimbizi 46 DRC
Makala hi imeangazia ziara ya ujumbe wa viongozi wa Afrika huko Ukraine na Urusi, Nchi za Jumuia ya Afrika mashariki wiki hii zilisoma Badgeti zao za mwaka wa 2023/2024, Ripoti ya Shirika ya kimataifa la haki za binadamu kuhusu kundi la waasi wa M23 mashariki mwa DRC mauaji ya katika kambi ya wakimbizi huko Ituri, tumeangazia pia yaliyojiri kule Khartoum Sudan, kwengineko Afrika na duniani
6/17/2023 • 20 minutes, 6 seconds
Wizara ya mambo ya ndani yasitisha shughuli za CNL Burundi, msako makazi ya Katumbi DRC
Hatua ya rais wa Rwanda Paul Kagame kufanya mabadiliko katika vyombo vya usalama na jeshi nchini mwake, viongozi wa COMESA wakutana jijini Lusaka nchini Zambia, msako mkali ulifanyika katika makazi ya Moise Katumbi na mshauri wake nchini DRC, tumeangazia yaliyojiri nchini Kenya, Uganda, na hali ya mapigano kule Sudan Khartoum, na pia Afrika magharibi na kwengineko duniani! Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza mengi zaidi
6/10/2023 • 20 minutes, 14 seconds
Kikosi cha EAC chaongezewa muda wa kuhudumu DRC, mapigano yaendelea Sudan
Makala hii imeangazia hatua ya viongozi wa Jumuia ya Afrika mashariki kukiongezea muda wa miezi sita kikosi cha Jumuia hiyo kuhudumu kwa ajili ya kupatikana kwa amani ya mashriki mwa DRC, nchi za magharibi na Marekani zasikitikia hatua ya Uganda kupinga Ushoga, ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Urusi Lavrov jijini Bujumbura Burundi, hali ya mapigano kule Sudan Khartoum, lakini pia yaliyojiri katika eneo la Afrika magharibi na mkutano wa Moldova na mapigano ya Ukraine. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza zaidi
6/3/2023 • 20 minutes, 12 seconds
Ziara ya rais wa DRC Félix Tshisekedi China, mradi wa umeme wa Uganda na Tanzania
Katika makala ya yaliyojiri wiki hii, tunaangazia habari kuu za dunia, matukio ya wiki hii ikiwa ni pamoja na ziara ya rais wa DRC Felix Tshisekedi huko China, Uganda na Tanzania zilizindua bwawa la pamoja la kuzalisha umeme wa megawati 16, katika mto Kagera eneo la Kikagati, miaka 60 tangu kuundwa kwa Umoja wa Afrika AU, hali ya mapigano kule Sudan Khartoum, lakini pia eneo la Afrika magharibi na mapigano ya Ukraine ni miongoni mwa mengi yaliyomo
5/27/2023 • 20 minutes, 8 seconds
Wafanyabiashara wa Kariakoo Tanzania wakutana na waziri mkuu, hali Sudan yatisha
Katika makala ya Yaliyojiri wiki Hii, tunaangazia baadhi ya habari kuu za dunia matukio ya wiki hii katika miongoni ikiwa ni pamoja na mgomo wa wafanyabiashara katika soko la kimataifa la Kariakoo jijini Daresalaam nchini Tanzania, DRC na Rwanda zilikubaliana kutengeneza mazingira kwa wakimbizi wa pande zote kurejea makwao, Hali ya kisiasa na nchini Sudan, lakini pia yaliyojiri katika eneo la Afrika magharibi na Mkutano wa G7 huko Japani ni miongoni mwa mengi utayasikia
5/20/2023 • 20 minutes, 14 seconds
SADC kupeleka wanajeshi DRC, miili 150 yafukuliwa nchini Kenya na mengineyo
Makala hii imeangazia kuhusu maafa yaliyosababishwa na mafuriko wilayani Kalehe DRC, pia hatua ya jumuia ya SADC kusaidia juhudi za upatikanaji wa amani ya mashariki mwa DRC, miili zaidi yafukuliwa nchini Kenya, hali ya nchini Sudan,pamoja na mambo mengine yaliyojiri katika eneo la Afrika magharibi na kwengineko duniani.
5/13/2023 • 20 minutes, 16 seconds
Mafuriko yasababisha maafa mengi nchini Rwanda na maeneo mengine ya Afrika
Makala hii imeangazia matukio mengi ya wiki hii lakini kubwa ni kuhusu maafa yaliyoripotiwa huko Rwanda na nchini DRC katika mafuriko yaliyosababisha maporomoko ya ardhi baada ya mvua kubwa kunyesha maeneo kadhaa, maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari tukiangazia kwa namna ya pekee mazingira ya wanahabari wa mashariki ya DRC hali nchini Sudan, yaliyojiri katika eneo la Afrika magharibi, kutawazwa kwa mfalme Charles wa 3 na mambo mengine kwengineko duniani.
5/6/2023 • 20 minutes, 15 seconds
Hali ya usalama nchini Sudan yaboreka, mkuu wa jeshi la EAC DRC forces arejea Nairobi
Makala imeangazia hali inavyoendelea nchini Sudan baada ya usitishwaji wa mapigano uliokubaliwa na pande zinazokinzana, ziara ya rais wa Rwanda Paul Kagame nchini Tanzania,hali ya usalama wa mashariki kule DRC, na tukio la moto kwenye gereza la Bukavu, mkoani Kivu kaskazini, nchini Kenya Kulifukuliwa miili kadhaa ya wakristo waliokufa wakifunga baada ya mchungaji wao kuwaaminisha kufunga hadi kufa ili waonane na YESU,Tumeangazia yaliyojiri pia katika eneo la afrika magharibi na kwengineko duniani,
4/29/2023 • 20 minutes, 14 seconds
Hali ya usalama yazidi kuzorota Sudan, sheria dhidi ya ushoga bungeni Uganda
Makala hii imeangazia mapigano na hali inavyoendelea nchini Sudan, na miito ya kusitishwa mapigano, muswada wa sheria unaopinga ushoga ulirejeshwa bungeni wiki hii, na kuanza kwa mazungumzo kati ya wajumbe wa muungano wa Upinzani wa Azimio nchini Kenya na wajumbe wa rais wa Kenya William Ruto nchini, tumeangazia yaliyojiri katika eneo la Afrika magharibi na kwengineko duniani
4/22/2023 • 20 minutes, 13 seconds
Watu 60 wauawa DRC, chanjo ya Malaria yaidhinishwa Ghana, nyaraka za siri za Marekani zavuja
Kwenye makala haya, tutakayoangazia wiki hii ni pamoja na upinzani nchini Kenya kusema utaendelea na maandamano huku wafanyakazi wa umma wakikosa kulipwa, tutaangazia usalama nchini DRC na uchaguzi unaotarajiwa mwishoni mwa mwaka huu. Chad na Ujerumani kuwafukuza mabalozi wake, kadhalika kuvuja kwa nyaraka za siri nchini Marekani na Korea kaskazini kutishia usalama wa kikanda.
Zaidi ya raia 60 wameuawa katika mashambulizi mapya ya vijiji vitano mkoani Ituri, waasi wa CODECO na makundi ya kikabila ya Zaire wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo. Kwa mengi zaidi, sikiliza makala haya.
4/15/2023 • 20 minutes, 1 second
Siasa za Kenya, DRC na Uganda zaungana dhidi ya ADF, miaka 29 baada ya mauaji ya Rwanda
Makala hii imeangazia mpango wa kufanyika mazungumzo kati ya upinzani na serikali nchini Kenya kusuasua, ziara ya rais wa Kenya William Ruto nchini Rwanda, wakuu wa majeshi ya DRC na Uganda wapongeza operesheni Shujaa huko Beni, raia wa Senegal, waliadhimisha miaka 63 tangu wapate uhuru wao kutoka kwa Ufaransa, kwengineko aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump, alifikishwa mahakamani jijini New York, ziara ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron nchini China kuishawishi Urusi kuachana na vita vya Ukraine, na mambo mengine.
4/8/2023 • 20 minutes, 3 seconds
Maandamano ya upinzani nchini Kenya yashika kasi, Uganda yatuma wanajeshi wake DRC
Kubwa katika makala hii ni kuhusu maandamano ya upinzani nchini Kenya, ziara ya makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris nchini Tanzania, wiki hii wanajeshi wa Uganda waliwasili kwenye mji wa Bunagana mashariki mwa DRC, lakini pia muswada wa sharia unaohusu uraia kwa mtu anayetakiwa kuwa kwenye wadhifa wa rais kuzua hisia mseto. Hukumu dhidi ya kiongozi wa upinzani nchini Senegal; Ziara ya mfalme Charles wa 3 wa Uingereza huko Ujerumani, na mambo mengine...
4/1/2023 • 20 minutes, 7 seconds
Rais Tshisekedi awateua Bemba na Kamerhe kuwa Mawaziri
Miongoni mwa yale utakayosikia, ni hatua ya rais wa DRC Felix Tshisekedi kumteua Jean Pierre Bemba kuwa Waziri mpya wa Ulinzi na Vital Kamerhe kuwa Waziri wa Uchumi, maandamano ya upinzani nchini Kenya na makabiliano ya waandamanaji na polisi nchini Ufaransa kupinga mageuzi ya mfumo wa pensheni.
3/25/2023 • 20 minutes, 12 seconds
Bunge la Angola laidhinisha kupelekwa kwa wanajeshi DRC, maandamano nchini Kenya
Miakala hii imeangazia hatua ya bunge la Angola kuidhinisha kutumwa kwa wanajeshi 500 wa nchi hiyo mashariki mwa DRC, hali ya wasiwasi nchini Kenya, kufuatia wito wamaandamano kupinga ugumu wa maisha kama ulivyoitishwa na kinara wa upinzani wa Azimio Raila Odinga, watu zaidi ya 300 wauawa na kuwaacha maelfu bila makaazi katika kimbunga Freddy kule Malawi, kesi ya mwanasiasa wa upinzani Ousmane sonko kule Senegal, mvutano kuhusu suala la mageuzi ya pensheni nchini Ufaransa, ni miongoni mwa mengi utakayoyasikia.
Ungana na mwandishi wetu Reuben Lukumbuka kupata mengi zaidi.
3/18/2023 • 20 minutes, 14 seconds
Rais wa Ufaransa E.Macron barani Afrika, usalama mashariki ya DRC, ushoga nchini Kenya
Ziara ya rais wa Ufaransa kwenye nchi nne za Afrika wiki hii, uchaguzi mkuu wa urais nchini Nigeria ambao ulimpa ushindi Bola Tinubu, msimamo wa serikali ya Kenya kuhusu ushoga, hali ya usalama wa mashariki ya DRC, lakini pia ziara ya rais wa Uganda Yoweri Museveni nchini Afrika kusini, pamoja na juhudi za kimataifa katika kuisaidia Ukraine, ni miongoni mwa mengi utakayoyasikia
3/4/2023 • 20 minutes, 13 seconds
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine watimiza Mwaka mmoja, M23 washika Mushaki-DRC
Sehemu kubwa ya makala hii itaangazia uvamizi wa Urusi kule Ukraine, mwaka mmoja ulitimia siku ya ijumaa ya ebruary 24 huku vita vikiendelea, wasi wasi kule Sake karibu na mji wa Goma kutokana na mapigano ya waasi wa M23 na jeshi la serikali ya DRC FARDC katika Vijiji kadhaa wilayani Masisi ; Siasa za Kenya, lakini pia ziara ya waziri wa Ufaransa Kenya na Tanzania, pamoja na mashambulio ya wanajihadi kule Burkina Faso
2/25/2023 • 20 minutes, 16 seconds
M23 walibaka na kuua Kishishe DRC yasema Amnesty international, Watu 41 elfu wafa Uturuki
Makala hii imeangazia kuanzishwa kwa zoezi la usajili wa wapigakura eneo la mashariki ya DRC, masuala ya uchaguzi wa mwaka uliopita nchini Kenya na wadukuzi kutoka Israeli, kuingilia mawasiliano binafsi ya washirika wawili wa rais William Ruto, mkutano wa viongozi wa Afrika huko Addis Ababa Ethiopia, na kufifia kwa matumaini ya kupatikana kwa watu zaidi waliokwama kwenye vifusi katika mitetemeko ya ardhi Uturuki na Syria, pamoja na mambo mengine.
2/18/2023 • 20 minutes, 19 seconds
Sintofahamu ya usalama wa Sake DRC, siasa za Kenya na tetemeko la uturuki
Makala hii imeangazia kwa sehemu kubwa hasara na maafa yaliyotokana na tetemeko la ardhi kule Syria na Uturuki, hali ya wasiwasi kwenye miji ya Sake na Goma, siasa za Kenya, Rwanda na kwengineko
2/11/2023 • 20 minutes, 4 seconds
Ziara ya papa Francis nchini DRC na Sudan Kusini, siasa za Kenya na mengineyo
Makala ya yaliyojiri wiki hii imeangazia kwa kina ziara ya kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis nchini DRC na pia huko Sudan kusini, mapigano yanayoendelea mashariki mwa nchi hiyo, lakini pia siasa za nchini nchini Kenya, Rwanda, na kwengineko duniani.
2/4/2023 • 20 minutes, 9 seconds
Waasi wa M23 wauteka mji wa Kitshanga, rais wa Kenya W.Ruto azuru Ufaransa
Makala hii imeangazia mvutano wa kidiplomasia kati ya Rwanda na DRC waendelea kushika kasi baada ya ndege ya jeshi la Congo kutunguliwa kutoka Rwanda, waasi wa M23 wiki hii walishika mji wa Kitshanga katika mkowa wa Kivu kaskazini, rais wa Kenya William Ruto atembelea Ufaransa, Balozi wa Ufaransa nchini Burkina Faso arejeshwa Paris na mapigano huko Ukraine
1/29/2023 • 20 minutes, 5 seconds
Ebola yatangaza kumalizika kwa maambukizi ya Ebola
Miongoni mwa yale tumekuandalia ni pamoja na mkutano wa waasi wa kundi la M23 na mpatanishi wa juluia ya Afrika mashariki, EAC rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, Uganda wiki hii ilisema hakuna tena Ebola nchini, mvutano kati ya DRC na Rwanda kuhusu wakimbizi, waasi wa Tigray waanza kuutekeleza mkataba wa amani, Ufaransa tayari kuimarisha uhusiano wake na Burkina faso na waziri mkuu wa Ufaransa aweka wazi msimamo wa serikali yake kuhusu umri wa kustaafu
1/14/2023 • 20 minutes, 16 seconds
Matukio ya wiki ya kwanza ya mwezi Januari 2023
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na Watu tisa, walipoteza maisha jijini Kampala Uganda wakati ulimwengu ulipokuwa ukiukaribisha mwaka mpya, waasi wa 23 huko mashariki ya DRC hatimaye wakubali kukabidhi kambi kubwa ya kijeshi ya Rumangabo kwa kikosi cha Jumuiya ya Afrika mashariki ijumaa ya January 06, Hatua ya rais wa Tanzania ya kuondoa marufuku ya mikutano ya vyama vya kisiasa kwenye nchi hiyo, miongoni mwa mengine mengi.
1/7/2023 • 20 minutes, 17 seconds
Matukio makubwa tuliyoyapa uzito mwaka 2022
Tunakuletea mkusanyiko wa matukio makubwa yaliyojiri mwaka 2022, inikiwa ni pamoja utovu wa usalama Mashariki mwa DRC, siasa za nchini Kenya, mzozo wa Ethiopia miongoni mwa matukio mengine makubwa yaliyotokea duniani.
12/31/2022 • 20 minutes, 15 seconds
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy azuru Marekani
Baadhi ya matukio makubwa wiki hii ni pamoja na kundi la waasi wa M 23 kuanza kujiondoa Mashariki mwa DRC, siku 100 za uongozi wa rais wa Kenya William Ruto pamoja na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kuzuru nchini Marekani.
12/24/2022 • 20 minutes, 11 seconds
Mkutano wa Marekani na viongozi wa Afrika
Mkutano wa viongozi wa nchi za Afrika na Marekani huko Washington, watu zaidi ya 100 wafariki dunia katika mafuriko makubwa kuwahi kushudiwa Jijini Kinshasa, DRC. Wananchi wa Kenya waliadhilisha miaka 59 ya uhuru kutoka kwa mkoloni wa Nchi hiyo Uingereza, ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa kwenye eneo la Afrika magharibi huko Rabat, hali ya mapigano kuendelea Kushuhudiwa huko Ukraine ambapo wakaazi wa maeneo mengi wamesalia bila ya umeme na maji.
12/17/2022 • 20 minutes, 15 seconds
Mwafaka wa amani ya DRC wapatikana jijini Nairobi, kiongozi wa Azimio aanza mikutano
Makala hii imeangazia vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya waasi wa DRC, na pia hatua ya makundi ya waasi wa mashariki mwa DRC kusaini mkataba wa kusitisha vita, kinara wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga aanza mikutano yake ya kisiasa, Uganda yapokea shehena ya kwanza ya chanjo za majaribio dhidi ya virusi Ebola, Ufaransa na Senegal zilitiliana saini kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, Marekani na Urusi zilibadilishana wafungwa..
12/10/2022 • 20 minutes, 18 seconds
Mazungumzo ya amani kuhusu Mashariki mwa DRC yafanyika Nairobi
Makala hii imeangazia mazungumzo ya kusaka amani ya mlashariki ya DRC yaendelea kufanyika jijini Nairobi chini ya Jumuia ya afrika mashariki, Uganda yasema, maambukizo ya virusi vya Ukimwi yadhibitiwa, kinara wa Upinzani nchini Kenya Raila Odinga wiki hii aliikosoa hatua ya bunge kuhusu makamishna wanne wa Tume ya Uchaguzi, Kesi ya mauaji ya septemba 28 nchini Guinea, ziara ya rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron nchini Marekani.
12/3/2022 • 20 minutes, 14 seconds
M23 wataka kukutana na Joao Laurenso, GMO yapingwa Kenya, wakaazi wa Ukraine gizani
Makala hii imeangazia kauli la kundi la waasi wa M23 kutaka kukutana na msuluhishi wa mgogoro kati ya DRC na Rwanda rais wa Angola Joao Laurenso, Uganda yasema, maambukizo ya virusi vya Ebola, yameanza kupungua, kinara wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga wiki hii aliikosoa serikali kwa kukubali kuagizwa kwa mahindi yaliyotengenezwa kwa vinasaba maarufu kama GMO, nchini Mali serikali ya mpito ilitangaza kusitisha shughuli za mashirika yote yanayofadhiliwa na Ufaransa, pamoja na matukio mengine.
11/26/2022 • 20 minutes, 8 seconds
Jeshi la DRC lapambana na waasi wa M23 Kivu Kaskazini
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia wiki hii ni pamoja mapambano kati ya waasi wa M 23 na wanajeshi wa serikali ya DRC katika jimbo la Kivu Kaskazini.
11/19/2022 • 20 minutes, 12 seconds
Kenya yatuma wanajeshi mashariki ya DRC, mkataba wa amani Ethiopia pia siasa za Israeli
Makala hii imeangazia hatua ya Kenya kuwatuma wanajeshi wake huko mashariki ya DRC baada ya waasi wa M23 kuyateka miji ya Rutshuru na Kiwanja huku juhudi za kidiplomasia kupatanisha nchi za DRC na Rwanda zikiendelea, pande hasimu nchini Ethiopia zafikia makubaliano ya amani, na uchaguzi wa wabunge nchini Israeili wampa ushindi waziri mkuu wa zamani Benjamin Netanyahu, pia utasikia mengi zaidi.....
11/5/2022 • 20 minutes, 19 seconds
Hali ya maambukizi ya Ebola nchini Uganda
Utasikia mengi miongoni ni pamoja na hali ya maambukizi ya Ebola nchini Uganda, DRC ina Mkuu mpya wa majeshi na vita vya Ukraine na Urusi vinavyoendelea.
10/15/2022 • 20 minutes, 18 seconds
Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari afikishwa Hague, Francois Hollande azuru mashariki ya DRC
Utasikia mengi miongoni ni pamoja na kusikilizwa kwa kesi dhidi ya mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Felicien Kabuga, ziara ya rais wa zamani wa Ufaransa Francois Hollande mashariki ya DRC na pia mapinduzi mapya ndani ya mapinduzi mengine ya kijeshi nchini Burkina Faso, kimbunga Ian chahathiri maeneo makubwa Marekani na Cuba. Ungana na mwandishi wetu Ruben Lukumbuka kusikiliza mengi zaidi.
10/1/2022 • 20 minutes, 4 seconds
William Ruto awa rais wa tano wa Kenya, Vital Kamerhe azuru mashariki ya DRC
Katika makala hii tumeangazia kuapishwa kwa William Samoei Ruto, na kuwa rais wa tano wa nchi hiyo; ziara ya aliyekuwa mkuu wa ofisi ya rais wa DRC Félix Tshisekedi, na kiongozi wa chama cha UNC Vital Kamerhe, mashariki mwa nchi hiyo, Cote d’Ivoire yaitaka Mali kuwaachilia huru wanajeshi wake wasiopungua 46, pia hali iliyoko Ukraine na siasa za Marekani, na mambo yanavyoendelea kwengineko duniani.