Tanzanian music, from Genesis to currently status told by Stake holders.
Mezani na LUCCI #22
Marehemu Cpwaa anatajwa kama mmoja wa wasanii wa kwanza kufanya muziki wa Crank (King of Bong fleva Crank) kupitia ngoma ya PWAA iliyotayarishwa na Lucci chini ya Mawingu Studio.
Hii inamaanisha kuwa Lucci ni mmoja wa waandaaji wa kwanza kwa muziki wa Bongo Fleva wenye mahadhi ya Crank.
Mbali na kutayarisha muziki vilevile Lucci anasimama kama msanii baada ya kushiriki kwenye nyimbo kadhaa mfano Kaka na Dada aliyoshirikishwa na Jokate ambae kwasasa ni Katibu Mkuu wa UWT kupitia chama cha CCM.
10/4/2024 • 1 hour, 55 minutes, 20 seconds
Mezani na DARK MASTER #21
Bado kiwanda cha Bongo Fleva kinaendelea kukumbuka mchango mkubwa wa vijana walioiwakilisha Dodoma mwanzoni mwa mwaka 2001 kupitia ngoma zao kadhaa ambazo zinachezwa na kusikilizwa mpaka hivi sasa.
Wanaitwa Chemba Squad, ambapo ndani yake majina kama Noorah aka Baba stylz, Dark Master, Albert Mangwea na Mez B wa area C yalitajwa kuunda kundi hilo.
Ngoma kama Ice Cream, Ghetto langu na Kama Vipi zinatajwa kama ngoma bora za muda wote kutoka kwa wakali hao ambapo hivi sasa wamebaki wawili tu (Noorah yupo zake Shy Town na Dark Master akiwa Dar es salaam) huku bahati mbaya Ngwea na Mez B wakiwa ni marehemu (RIP).
Leo tunakusogezea historia kamili na mengi usiyoyajua kuhusu Dark Master aka MwanaChemba.
9/20/2024 • 1 hour, 30 minutes, 4 seconds
Mezani na FEROOZ #20
Je Unamfahamu FERUZI MRISHO? Gwiji na moja wa waanzilishi na NUNDA mkuu wa DAZ NUNDAZ. Mwenyewe akitambulika zaidi kama Kamanda kabla Kamanda haijawa THE ANTHEM it is now. Leo tuko nae mezani akitusimulia safari yake yote ya mziki, toka anaandikiwa mashairi na dada yake Achane mpaka anatunga tungo matata kama Starehe, Kamanda, Nitafanya Nini, Jirushe, Elimu dunia N.K. Karibu Mezani.
8/2/2024 • 1 hour, 35 minutes, 55 seconds
Mezani na MARLON LINJE #19
Je, Unamfahamu producer ambaye, dare I say it, bila yeye labda kwaya au bendi yako maarufu usingeisikia kama ulivyoisikia? Producer ambaye amefanya zaidi ya 80% ya production ya mziki wote wa bendi na kwaya Tanzania kwa miaka 30. Marlon Linje, bonge la mshika dau, leo yupo nawe mezani, karibu.
7/12/2024 • 2 hours, 36 minutes, 48 seconds
Mezani na BONILUV #TheGodfather Part II
Sehemu ya pili na Kaka Boniphace Kilosa a.k.a #Boniluv. Kati ya wale magwiji wawili wanaotajwa sana, huyu ni Kaka yao na hatajwi sana pengine kwa makusudi ama bahati mbaya na hilo halijatuzuia kufanya naye mazungumzo na kumpatia maua yake. Boniluv ni Baba, Kaka, Rafiki na mwanafamilia. Ni mtu wa Muziki haswa. Ni mtu wa old school jams, akianza story za 80's hatumshiki!! Amefanya kazi na Ma-Pioneer wote wa muziki wa kizazi kipya. Amekuwepo kabla ya Bongo Fleva hivyo anastahili HESHIMA ya kuwa #TheGodFather wa muziki wa Bongofleva Ametupa heshima kubwa Sana na historia ya safari yake ya muziki na maisha tangu miaka hiyo mpaka leo. Jumuika nasi mezani, tusikilize PART II ya Poppaluv 😉 Karibu. #MezaniNaBoniluv #MezaHuru
Anchor - https://anchor.fm/meza-huru
Google podcast - https://podcasts.google.com/feed/aHR0...
Applepodcast - https://podcasts.apple.com/us/podcast/meza-huru/id1644168683
Spotify - https://open.spotify.com/show/6Ym3U2r...
Deezer - https://www.deezer.com/en/show/4499797
Amazon music - https://music.amazon.com/podcasts/bc2...
Boomplay - https://www.boomplay.com/podcasts/32087
Castbox - https://castbox.fm/podcasts/meza-huru...
YouTube - https://www.youtube.com/channel/UCutp...
Facebook - https://www.facebook.com/MEZA-HURU-10...
Twitter - https://twitter.com/MezaHuru