Winamp Logo
Jukwaa la Michezo Cover
Jukwaa la Michezo Profile

Jukwaa la Michezo

Swahili, Sports, 1 season, 98 episodes, 1 day, 14 hours, 45 minutes
About
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episode Artwork

Tanzania na Kenya zafuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika U20 mwaka ujao

Tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya kufuzu AFCON U20 mwaka ujao, namna timu za Afrika zilicheza kwenye wiki ya kwanza ya Kombe la Dunia la kina dada wasiozidi miaka 17, timu ambazo tayari zimefuzu AFCON ya 2025 nchini Morocco na nafasi ya timu za Afrika Mashariki na Kati, AFCON ya ufukweni yaanza leo nchini Misri, droo ya klabu bingwa Afrika kwa kina dada, mashindano ya magari ya Rwanda Mountain Gorilla Rally, kutimuliwa kwa kocha Kavazovich klabuni Vipers na Ligi za ukanda na Ulaya
10/19/202424 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

AFCON U20: DRC yafuzu Kombe La Mataifa Ya Afrika ya mwaka ujao

Tuliyokuandalia ni pamoja na faniali za kufuzu mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20, uchambuzi wa vikosi vilivyotajwa na wakufunzi kuelekea raundi ya tatu ya kufuzu AFCON 2025, masaibu ya Samuel Eto'o na kocha wa Senegal Aliou Cisse kutemwa, kifo cha nyota wa basketboli Dikembe Mutombo pamoja na matokeo ya mechi za ligi ya mabingwa ulaya.
10/5/202424 minutes, 3 seconds
Episode Artwork

Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano ya juu zaidi ya baiskeli barani Afrika

Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa mechi ya Kombe la Super Cup Afrika, Kenya kuwa mwenyeji wa mashindano ya baiskeli Afrika kwa mara ya kwanza, matokeo ya riadha jijini New York, sura mpya za wanariadha watakaoshiriki Berlin Marathon hapo kesho, Ligi za ukanda kwenye soka, voliboli na basketboli lakini pia matokeo ya Kombe la Europa League raundi ya kwanza.
9/28/202424 minutes, 5 seconds
Episode Artwork

CHAN 2024 kuanza Februari 1-28 mwaka 2025 nchini Uganda, Kenya na Tanzania

Tuliyokuandalia ni pamoja na taarifa ya ziara ya rais wa CAF Patrice Motsepe nchini Kenya, awamu ya pili kufuzu hatua ya makundi mechi za klabu bingwa Afrika, timu za Kenya za soka na mchezo wa Kabaddi tayari kushiriki Kombe la Dunia, timu za taifa Afrika Mashariki zimepanda kwenye msimamo wa dunia wa FIFA, uchambuzi wa raundi ya kwanza mechi za UEFA na mchezo wa ndondi kati ya Anthony Joshua na Daniel Dubois leo usiku.
9/21/202424 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

Mwanariadha wa Uganda Rebecca Cheptegei azikwa kwa heshima kamili za kijeshi

Tuliyokuandalia hii leo ni mkusanyiko wa uchambuzi na matokeo ya mechi za kufuzu AFCON 2025, mechi za klabu bingwa Afrika kufuzu awamu ya makundi, washindi wa riadha za Diamond League, matokeo ya lLigi ya basketboli ya Afrika U18, droo ya AFCON U20 ukanda wa CECAFA, ligi za ukanda na ulaya pamoja na uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya msimu mpya utakaoanza wiki ijayo
9/14/202423 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

AFCON 2025: Safari ya kuelekea Morocco yaanza kwa mataifa ya Afrika

Tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo na uchambuzi wa mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2025, kifo cha mwanariadha wa Uganda nchini Kenya, matokeo ya Zurich Diamond League, matokeo ya U18 Afrobasket na Congo Cup, uchambuzi wa matokeo ya  mataifa ya Afrika kwenye Olimpiki ya walemavu jijini Paris, mechi za Ligi ya Mataifa ya Ulaya na tuzo za Ballon D'Or mwaka 2024
9/7/202424 minutes, 2 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya Tong IL Moo Do, Mombasa Open yafutiliwa mbali kutokana na ufadhili

Tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya kufuzu klabu bingwa kwa kina dada, uchambuzi wa vikosi vya timu za Afrika Mashariki na kati kuelekea mechi za kufuzu AFCON 2025, matokeo ya riadha ya Rome Diamond League na riadha za dunia U20, mashindano ya Tong IL Moo Do Mombasa Open kufutiliwa mbali, matokeo ya Olimpiki ya walemavu na uhamisho wa wachezaji ulaya.
8/31/202423 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya kimataifa, Mombasa Open Tong IL Moo Do 2024 yacheleweshwa kwa wiki

Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchambuzi wa mechi za kufuzu klabu bingwa Afrika, riadha za Diamond League, FIBA Afrobasket kwa kina dada, hatma ya mashindano ya Mombasa Open Tong IL Moo Do mwaka huu, unachostahili kujua kuhusu Olimpiki ya walemavu inayoanza wiki ijayo jijini Paris huku kiungo Ilkay Gundogan akirejea klabuni Man City.
8/24/202423 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Namna wanariadha wa Afrika walivyopokelewa kutoka Olimpiki ya Paris

Jumamosi hii tumezungumzia namna wanariadha wa Afrika walivyopokelewa na mataifa yao kutoka Olimpiki ya Paris, michuano ya klabu bingwa Afrika imeanza kusaka tiketi ya hatua ya makundi, uhamisho tata wa wachezaji wa soka nchini Kenya huku ligi za Afrika Mashariki na Ulaya zikianza kurejea, Mbappe ashinda taji la kwanza Real Madrid, Pochettino kuwa kocha wa Marekani
8/17/202424 minutes, 8 seconds
Episode Artwork

Paris Olimpiki: Tamirat Tola kutoka Ethiopia ndiye mshindi wa mbio za marathon

Tuliyokuandalia Jumamosi hii kutoka taasisi ya Alliance Francaise, ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya marathon, riadha na mashindano mengine ya Olimpiki ya Paris yaliyotukia wiki hii. Pia tunaangazia fainali kubwa zinazosubiriwa jioni ya leo na kesho asubuhi kwenye marathon ya kina dada lakini pia kifo cha aliyekuwa rais wa tano wa shirikisho la soka Afrika CAF, Issa Hayattou.
8/10/202419 minutes, 48 seconds
Episode Artwork

Jukwaa La Michezo: Fainali ya mita 100 kwa wanaume yasubiriwa, Olimpiki Paris

Tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo ya Olimpiki hapo jana raia wa St Lucia Julien Alfred akishindia taifa lake medali ya kwanza ya Olimpiki, Sudan Kusini yaaga mashindano ya basketboli kibingwa, uchambuzi wa wanariadha wa Afrika Mashariki wanaotarajiwa kushiriki nusu fainali na fainali kadhaa leo usiku na kesho, uchambuzi wa mechi za nusu fainali ya soka lakini pia kwenye mjadala tunazungumzia kashfa ya jinsia ya mabondia Angela Carini na Imane Khelif
8/4/202423 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Jukwaa La Michezo: Cheptegei aishindia Uganda medali ya kwanza Olimpiki ya Paris

Joshua Cheptegei ashinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 10,000 huku Malkia Strikers ikibanduliwa mashindanoni. Morocco na Misri zafuzu nusu fainali huku waafrika kwenye uogeleaji wakifanya vibaya. Pia tutakufahamisha matokeo ya judo, basketboli, kuendesha basikeli na jedwali la medali ambapo Uchina inazidi kuongoza jedwali hilo
8/3/202423 minutes, 43 seconds
Episode Artwork

Paris Olimpiki: Ufaransa yashinda dhahabu ya raga, Kenya ikimaliza nambari tisa

Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya Olimpiki na mjadala kuhusu wanariadha wanaotarajiwa kung'ara kwenye Olimpiki wiki ijayo riadha zitakapoanza pamoja na matokeo ya Toyota Cup Yanga ikiilaza Kaizer Chiefs huku George Russel akishinda mkondo wa Belgian GP kwenye mashindano ya langalanga.
7/28/202423 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Olimpiki ya Paris: Mambo muhimu ya kujua kuhusu mashindano ya mwaka huu

Tuliyokuandalia ni pamoja na mambo muhimu unahitaji kujua kuhusu Olimpiki  ya mwaka huu kabla ya kuanza, uchambuzi wa fainali ya CECAFA Kagame Cup kati ya APR ya Rwanda na Red Arrows ya Zambia, tetesi za uhamisho Afrika Mashariki n aUlaya pamoja na matokeo ya Tour de France ikielekea ukingoni huku kocha wa Uingereza Gareth Southgate akijiuzulu kuifunza timu ya taifa ya wanaume.
7/20/202417 minutes, 22 seconds
Episode Artwork

Timu ya Kenya yaanza kuwasili Miramas, Ufaransa tayari kwa Olimpiki

Tuliyokuandalia ni pamoja na droo ya hatua ya awali kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika msimu ujao, matokeo ya Monaco Diamond League, Team Kenya yaanza kuwasili Ufaransa tayari kwa Olimpiki, matokeo ya CECAFA Kagame Cup na tetes iza uhamisho pamoja na uchambuzi wa fainali ya EURO, Copa America na fainali za tenisi kwenye Wimbledon.
7/13/202423 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Shirikisho la soka barani Afrika CAF latangaza droo ya michuano ya kufuzu AFCON 2025

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya mwaka 2025, fainali ya Cosafa Cup, mipango ya Team Kenya kuelekea Olimpiki ya mwaka huu, uchambuzi wa mechi za robo fainali michuano ya Euro na Copa America, raia wa Eritrea Girmay Hailu Biniam ashinda hatua ya nane ya Tour de France wakati kocha wa Manchester  United Erik ten Hag aongeza mkataba wake. 
7/6/202423 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

CAF: Kenya Police FC yafuzu kushiriki Kombe la Shirikisho barani Afrika msimu ujao

Tumekuandalia mengi ikiwemo matokeo na uchambuzi wa mashindano ya COSAFA Cup inayoendelea nchini Afrika Kusini, Leopards voliboli ya ufukweni yafuzu Kombe la Dunia wakati Kinshasa yajiandaa kuandaa mechi za kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mchezo wa basketboli ya kutumia viti vya magurudumu, Kenya yateua kikosi kitakachoshiriki riadha za dunia U20 nchini Peru, tetesi za uhamisho katika vilabu vya Afrika Mashariki, Kenya Police yafuzu kombe la shirikisho barani Afrika msimu ujao. Tour de France yaanza leo nchini Italia kabla ya kurejea Ufaransa huku michuano ya EURO na Copa America ikiingia hatua za mtoano.
6/29/202423 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

CAF yatangaza tarehe mpya kwa michuano ya AFCON na WAFCON 2025

Tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo ya riadha za Afrika nchini Cameroon, matokeo ya tenisi ya Davis Cup nchini Angola, bondia wa DRC Christophe Mputu ashinda medali ya 70, watu 13 wapigwa marufuku nchini Uganda kwa visa vya upangaji mechi, Ons Jabeur na Aryna Sabalenka kukosa Olimpiki kuzingatia afya yao.
6/22/202423 minutes, 47 seconds
Episode Artwork

Kipyegon, Omanyala wafuzu Olimpiki ya Paris kwenye mchujo wa kitaifa

Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na mchujo wa kitaifa wa Kenya kuteua timu itakayowakilisha kwenye Olimpiki ya Paris mwaka huu, Kenya yakosa kupandishwa daraja kwenye tenisi mashindano ya Billie Jean King Cup, uwanja wa Amahoro nchini Rwanda umeidhinishwa na FIFA kuandaa mechi za kimataifa, Junior Starlets ipo guu moja kufuzu Kombe la Dunia, droo ya kufuzu AFCON 2025 kuandaliwa Julai na michuano ya EURO kuanza Ujerumani. 
6/15/202423 minutes, 43 seconds
Episode Artwork

French Open: Iga Swiatek ashinda ubingwa wake wa nne wa Roland Garros

Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchambuzi wa mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 (Afrika), Kenya kuandaa mashindano ya mchujo kutafuta timu itakayowakilisha katika Olimpîki ya Paris mwezi Julai huku wanamichezo 33 wakipigwa na marufuku kwa kutumia dawa za kusisimua misuli, matokeo ya Congo Cup, kocha Gamondi arefusha mkataba wake klabuni Yanga huku zikiwa zimesalia siku sita kabla ya mashindano ya EURO nchini Ujerumani, Iga Swiatek ashinda ubingwa wake wa nne wa French Open
6/8/202423 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

BAL2024: Petro de Luanda yaibuka na taji la Ligi ya Basketboli barani Afrika

Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa fainali ya Ligi ya Basketboli Afrika mwaka huu, matokeo ya Diamond League mkondo wa Oslo na mchujo wa raga duniani, uchambuzi wa vikosi vya Afrika Mashariki na Kati kuelekea mechi za kufuzu Kombe la Dunia la mwaka 2026, uchambuzi wa Fainali ya Klabu bingwa Ulaya (Dortmund dhidi ya Real Madrid) na matokeo ya French Open huku Ronaldo akitokwa na machozi baada ya kupoteza fainali ya Saudi Kings Cup
6/1/202423 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

DRC: Sebastian Desabre arefusha mkataba wake kama kocha wa timu ya taifa

Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa fainali ya Klabu bingwa Afrika, Tanzania waibuka na kombe la shule za upili afrika mchezo wa soka, fainali za ligi ya basketboli kuanza nchini Rwanda wakati makocha wa Kenya na Uganda wataja vikosi vyao kufuzu Kombe la Dunia na matokeo ya Ligi za ulaya.
5/25/202423 minutes, 46 seconds
Episode Artwork

CAF: Nani ataibuka na taji la Klabu bingwa barani Afrika 2024?

Tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa fainali ya Klabu Bingwa Afrika mwaka 2024, Zanzibar kuandaa fainali za mashindano ya shule za upili barani Afrika, Mkusanyiko wa michezo kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, Maniema yarejea kwenye mashindano ya vilabu barani Afrika, uchambuzi wa mbio za kuwania taji la Uingereza kati ya Man City na Arsenal, Ngolo Kante arejea kikosini mwa Ufaransa, Brazil yateuliwa kuandaa Kombe la Dunia la kina dada la mwaka 2027.
5/18/202424 minutes, 42 seconds
Episode Artwork

Diamond League: Mary Moraa na Beatrice Chebet waibuka washindi riadha za Doha DL

Tuliyokuandalia hii leo ni pamoja na matokeo ya riadha kwenye Doha Diamond League, AFCON UAE kuanza hapo kesho huko Dubai, michuano ya Congo Cup, uchambuzi wa mechi za Ligi ya Basketboli ya Afrika, Guinea yafuzu fainali za Olimpiki kwenye soka, mechi za kufuzu Kombe la Dunia la U17 kwa kina dada, Mbappe atangaza rasmi kuondoka PSG na uchambuzi wa fainali za mwaka huu za michuano ya bara Ulaya.
5/11/202423 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Uganda : Uwanja wa Namboole kuanza kutumika kwa mechi za kufuzu Kombe la dunia

Tuliyokuandalia ni pamoja na Uchambuzi wa orodha ya mwisho ya Kikosi cha Marathon cha Team Kenya kuelekea Olimpiki, watu watano nchini Kenya wapigwa marufuku ya muda kwa madai ya upangaji mechi. Nchini Uganda, Rais wa FUFA asema uwanja wa Naambole utakuwa tayari kuandaa mechi wa kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2026 na Ligi ya Basketboli barani Afrika mkondo wa Sahara umeanza leo.
5/4/202423 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

KipKeino Classic: Mmarekani Kenneth Bednarek ashinda mbio za mita 100

Tuliyokuandalia hii leo ni pamoja na matokeo ya riadha za KipKeino Classic, uchambuzi wa debi la Tanzania na Mashemeji nchini Kenya, mabondia 11 wa DRC wafuzu nusu fainali ya michuano ya African Boxing Cup, matokeo ya ligi ya basketboli Afrika mkondo wa Nile na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya
4/20/202423 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Olimpiki: Nigeria na Zambia zafuzu mashindano ya Olimpiki soka ya kina dada

Kwenye makala haya utasikiliza uchambuzi wa mechi za kufuzu soka ya kina dada Olimpiki na shirikisho la riadha duniani kuwa shirikisho la kwanza kutoa tuzo za fedha, maandalizi kuelekea riadha za KipKeino Classic, mkusanyiko wa michezo DRC, uchambuzi wa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati Tiger Woods na Novak Djokovic waweka historia kubwa duniani kwenye gofu na tenisi mtawalia.
4/13/202423 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

CAFCL:Simba na Yanga zabanduliwa michuano ya Klabu Bingwa Afrika

Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchambuzi wa hatua ya robo fainali mkondo wa pili michuano ya Klabu Bingwa Afrika, matokeo ya kufuzu soka Olimpiki ya kina dada, mwanasoka wa Afrika Kusini kuuawa, PSG Academy yatoa mafunzo kwa makocha nchini Rwanda, Kenya yatangaza orodha yake ya wanariadha wa mbio za Marathon kwenye Olimpiki ya mwaka huu, Ufaransa na Kenya kushirikiana kujenga viwanja nane nayo PSG ikiwa tayari kutoa pauni milioni 111 kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen
4/6/202423 minutes, 45 seconds
Episode Artwork

WRC Safari Rally Kenya : Mashindano ya mbio za magari yanaendelea nchini Kenya

Karibu katika makala jukwaa la michezo, leo hii tumekuandalia taarifa kadhaa kuanzia katika mashindano ya  mbio za magari Safari rally nchini kenya, michuano ya klabu bingwa barani afrika Al Ahly wakiishinda Simba goli moja sifuri kisha Tp Mazembe kupata sare dhidi ya Petro Atletico ya Angola na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Sierra Leone Lamin Bangura afariki akiwa na umri wa miaka 59 katika ajali ya basi.
3/30/202423 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya barani Afrika mwaka 2023 yakamilika nchini Ghana

Tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na Kenya kuongoza chati ya medali Afrika Mashariki katika mashindano ya Afrika, Shirikisho la soka Cameroon yaondoa kashfa ya udanganyifu wa miaka dhidi ya Nathan Doualla, mkurugenzi mwandalizi wa WRC Safari Rally Jim Kahumbura ajiuzulu, droo ya soka mashindano ya Olimpiki na Nottingham Forest kupokonywa alama nne kutofuata sheria wa fedha Uingereza.
3/23/202423 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

CAF CL: Tp Mazembe, Yanga na Simba wafahamu wapinzani wao wa robo fainali

Karibu katika makala ya jukwaa la michezo, leo tumekuandalia mengi tukianzia na droo ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani afrika, mashindano ya bara afrika pamoja na droo ya robo fainali katika mashindano ya klabu bingwa barani ulaya.
3/16/202423 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Ndondi : Anthony Joshua amshinda Francis Ngannou katika raundi ya pili

Karibu katika makala ya jukwaa la michezo leo tunaangazia kushindwa kwa mwana masumbwi Francis Ngannou na Anthony Joshua,kuanza kwa mashindano ya 13 ya bara Afrika nchini Ghana pamoja na Paris Saint Germain kufuzu katika robo fainali michuano ya klabu bingwa barani ulaya.
3/9/202424 minutes, 4 seconds
Episode Artwork

Kenya kujenga uwanja mpya kwa ajili ya michuano ya Afcon mwaka 2027

Karibu katika makala ya jukwaa la michezo leo tunaangazia kujengwa kwa uwanja mpya wa michezo nchini kenya, michuano ya klabu bingwa barani afrika pamoja na taifa la ufaransa kukamilisha ujenzi wa kijiji kitakachotumiwa na wanariadha katika michezo ya olimpiki.
3/2/202423 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya Tour du Rwanda mwaka 2024 yamekamilika hii leo jijini Kigali

Karibu katika makala jukwaa la michezo, leo hii tunaangazia kukamilika kwa mashindano ya kuendesha baiskeli ya Tour du Rwanda, mashindano ya mchezo ya gofu Magical kenya open pamoja na klabu ya Yanga na Tp Mazembe kufuzu katika hatua ya robo fainali katika michuano ya robo fainali katika michuano ya klabu bingwa barani afrika.
2/25/202422 minutes, 41 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya Tour du Rwanda kuanza hapo kesho katika mji wa Kigali

Karibu katika makala ya Jukwaa la michezo, leo tumekuandalia mengi ikiwemo kuanza kwa mashindano ya kuendesha baiskeli ya Tour du Rwanda, mazungumzo ya kipekee na waziri wa michezo nchini Tanzania Damas Ndumbaro pamoja na  kupigwa marufuku mechi nne kwa mchezaji wa timu ya taifa ya senegal Kreppin Diatta.
2/17/202424 minutes
Episode Artwork

AFCON 2024 : DRC kucheza dhidi ya Afrika Kusini katika nafasi ya tatu

Miongoni mwa taarifa kuu tutakazozianhazia ni pamoja na fainali ya kombe la mataifa ya bara afrika AFCON kuchezwa hapo kesho mwenyeji Ivory coast wakipambana na Nigeria. Mchezaji wa tenisi nambari moja barani afrika Ons Jabeur kushindwa katika mashindano ya Abu dhabi na fainali ya kombe la mataifa ya bara Asia kuchezwa leo.
2/10/202425 minutes, 1 second
Episode Artwork

AFCON 2024: DRC na Nigeria zatinga hatua ya nusu fainali

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na taifa la DR Congo pamoja na Nigeria kufuzu kwa hatua ya nusu fainali katika michuano ya  kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Dereva wa magari ya langalanga Lewis Hamilton kuhamia katika timu ya Ferrari kutoka Mercedes mwaka 2025.
2/3/202423 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

AFCON 2024: Michuano ya hatua ya 16 bora kuanza

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya hatua ya 16 kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Mashindano ya mchezo wa mikono bara Afrika yanayoendelea kule Misri na Aryna Sabalenka  kushinda mashindano ya Australian Open kwa upande wa wanawake.
1/27/202423 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Mataifa ya Afrika yaendelea kupambana kutafuta taji la AFCON

Tunaendelea kukuletea uchambuzi wa michuano ya soka kuwania ubingwa kwa mataifa ya Afrika, inayoendelea nchini Cote Dvoire. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania, pia zinapambana kuwania taji hilo. Ungana na wachambuzi wetu Jason Sagini, George Ajowi na Jason Sagini akiwa mjini San Pedro.
1/20/202423 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Michuano ya AFCON yaanza nchini Cote Dvoire, nani ataibuka mshindi ?

Michuano ya soka kuwania taji la mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON, inaanza leo nchini Cote Dvoire. Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya makubwa kurejea kwenye nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40. Kuna timu 24 zinazotafuta ubingwa wa taji hili, ikiwemo Taifa Stars ya Tanzania na Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Afrika Mashariki na Kati. Wachambuzi wetu Paul Nzioki, George Ajowi na Jason Sagini, akiwa  Abidjan, wnachambua.
1/13/202423 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

CAF yaongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa AFCON 2024

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa  Shirikisho la soka barani Afrika CAF kuongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa michuano ya AFCON, itakayoanza Januari 13 nchini Cote Dvoire,  Bondia wa DRC Martin Bakole aomba mchango wa fedha kushiriki mechi za mkanda wa WBA, matokeo ya Mapinduzi Cup na kombe la Amani visiwani Zanzibar na Brazil yamfuta kazi kocha Fernando Diniz.
1/6/202423 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Timu za Afrika zaanza kutangaza vikosi kuelekea AFCON 2024

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa vikosi vya mwisho vilivyotangazwa na mataifa kadhaa kuelekea AFCON ya mwaka 2023 itakayoanza Januari 13, 2024, raia wa Rwanda Clare Akamanzi ateuliwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa NBA Africa, Guy Bukasa atangazwa kocha mpya wa AS Kigali, rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach atangaza mikakati ya kujumuisha michezo ya kielektroniki e-sports kwenye Olimpiki na kocha Carlo Ancelotti atia saini mkataba mpya klabuni Real Madrid.
12/30/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Kenya yaibuka bingwa wa mashindano ya Tong Il Moo Do

Tuliyokuandalia ni pamoja na Kenya kuhifadhi taji lake la Tong Il Moo Do kwa mara ya 11, mkenya Angella Okutoyi ashinda dhahabu mbili kwenye tenisi ya kimataifa ya W25, uchambuzi wa matokeo ya mechi za Klabu bingwa Afrika wiki hii, Man City kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu bingwa Duniani kwa mara ya kwanza na Mahakama ya Ulaya kupinga uamuzi wa FIFA na UEFA kuzuia kuanzishwa kwa Ligi mpya ya Ulaya kuwa kinyume na sheria. 
12/23/202323 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya Kimataifa ya Tong-Il-Moo-Do yafanyika nchini Kenya

Kenya yaandaa makala ya 11 ya michuano ya kimataifa ya mchezo wa Tong-Il-Moo-Do jijini Mombasa. Uganda ndio washindi wa CECAFA katika mechi za kufuzu kwa michuano ya CAF ya Shule za Afrika. Al Ahly waishinda Al-Ittihad kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu Kisha Paris Saint - Germain yatinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.
12/16/202321 minutes, 1 second
Episode Artwork

Messi ashinda tuzo ya Ballon d'Or tena

Miongoni mwa yale tunayojadili ni pamoja na tuzo za wachezaji bora barani Afrika mwaka huu katika mchezo wa soka, timu ya taifa ya Uganda Cranes kupata kocha mpya, mechi za soka kufuzu michezo ya Olimpiki Paris 2024 miongoni mwa wanawake, Lionel Messi kushinda tuzo ya nane la Ballon d'Or, miongoni mwa mengine.
11/4/202323 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Uchaguzi wa viongozi wa mchezo wa Tennis barani Afrika

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Afrika kupata viongozi wapya wa Shirikisho la mchezo wa Tenisi, uchambuzi wa fainali ya kombe la dunia la raga, pigano la ndondi kati ya Tyson Fury na Francis Ngannou, mechi za kufuzu olimpiki ya mwaka kesho kwa kina dada, Ligi Kuu ya soka Afrika, debi la Manchester na El Clasico na mchezaji wa Newcastle Sandro Tonali kupigwa marufuku ya miezi kumi kwa kujihusisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu.
10/28/202323 minutes, 39 seconds
Episode Artwork

Raga: Afrika Kusini na New Zealand kuchuana fainali ya kombe la dunia

Tumekuandalia uchambuzi kuhusu fainali inayotarajiwa kati ya Afrika Kusini na New Zealand, kuwania taji la kombe la dunia katika mchezo wa raga lakini pia kuendelea kwa michuano mipya ya soka ya ligi ya Afrika.
10/22/202323 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

CAF yatangaza droo ya hatua ya makundi, michuano ya klabu bingwa na Shirikisho

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika, Gor Mahia yaibuka na ushindi kwenye debi la mashemeji, uchambuzi wa matokeo ya mechi za klabu bingwa ulaya, Kombe la Dunia la mwaka 2030 kuandaliwa kati ya mataifa sita na Pogba kupatikana ametumia dawa za kusisimua misuli katika kipimo cha pili.
10/7/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Afrika Mashariki kuwa wenyeji wa AFCON 2024

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Afrika Mashariki kuteuliwa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2027, hatua ya mwisho ya kufuzu Kombe la Mataifa ya wanawake mwaka 2024, raundi ya mwisho kufuzu hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa barani Afrika na Kombe la dunia la raga, linaloendelea nchini Ufaransa.
9/30/202323 minutes, 32 seconds
Episode Artwork

Mkenya Eliud Kipchoge ashinda tena taji la Berlin Marathon

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na mwanariadha kutoka Kenya, Eliud Kipchoge kushinda mashindano ya riadha ya Berlin Marathon kwa mara ya tano, Kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Rwanda, asimamishwa kazi ni  miongoni mwa mengine mengi yanayotokea viwanjani.
9/24/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Klabu za Afrika zachuana kunyakuwa taji la klabu bingwa

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na mahojiano kuhusu kongamano la kibiashara la soka barani Afrika, lililofanyika wiki hii jijini Nairobi. Misri waibuka washindi wa kombe la mataifa ya Afrika voliboli ya wanaume, APR ya Rwanda yashinda ubingwa wa ligi kuu ya basketboli, uchambuzi wa mechi za kufuzu klabu bingwa barani Afrika na kombe la dunia la raga. 
9/16/202323 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Kombe la dunia la mchezo wa raga, laanza nchini Ufaransa

Tuliyokuandalia ni pamoja na kuanza kwa  Kombe la Dunia katika  mchezo wa raga nchini Ufaransa, Tanzania kufuzu Kombe la mataifa ya Afrika mchezo wa soka mwaka 2023 na Rwanda yaondolewa  kwenye mashindano ya voliboli barani Afrika.
9/9/202323 minutes, 49 seconds
Episode Artwork

Matukio makubwa yaliyotokea duniani wiki hii

Tuliyokuandalia ni pamoja kifo cha mshindi wa kwanza tuzo la Ballon D'Or  la Afrika Selif Keita, ushirikiano wa Azam  na FKF kupeperusha ligi kuu ya Kenya, rais wa FERWAFA kujiuzulu, Uganda yashinda medali yao ya kwanza kwenye mashindano ya Pentathlon, mlinda lango Andre Onana arejea kwenye kikosi cha Cameroon na uchambuzi wa Droo ya michuano ya klabu bingwa Ulaya na siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji ulaya.
9/2/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Faith Kipyegon aweka historia mashindano ya riadha ya dunia 2023

Faith Kipyegon ameishindia Kenya medali mbili za dhahabu katika mbio za mitaa 1500 na 5000 katika mashindano ya riadha ya dunia, katika jiji la Budapest nchini Hungary. Tunajadli hili na mengine mengi yanayotokea viwanjani wiki hii.
8/27/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya riadha ya dunia yaanza nchini Hungary

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na kuanza kwa mashindano ya riadha ya dunia, jijini Budapest. Kocha wa mchezo wa soka nchini Uganda, Sam Timbe ameaga dunia. Mechi za kufuzu hatua ya makundi michuano ya CAF, LALIGA kuweka mipango ya vilabu vyake kuzuru Afrika Mashariki pamoja na Luciano Spalletti kutajwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Italia.
8/19/202323 minutes, 50 seconds
Episode Artwork

Msimu mpya wa ligi kuu ya soka barani Ulaya waanza

Tuliyokuandalia leo ni pamoja na kuanza kwa ligi kuu ya soka nchini Uingereza na mataifa kadhaa ya Ulaya,  uchambuzi wa Kombe la dunia la wanawake katika mchezo wa soka, fainali za ngao ya jamii  katika mchezo wa soka Afrika Mashariki na mashindano ya shule za Sekondari nchini Kenya na michuano ya kufuzu kushiriki taji la klabu bingwa barani Afrika kwa upande wa wanawake, miongoni mwa mengine.
8/12/202324 minutes
Episode Artwork

Kombe la dunia la Wanawake: Timu za Afrika zafika hatua ya 16 bora

Tuliyokuandalia Jumamosi hii, ni pamoja na uchambuzi wa timu za Afrika kwenye raundi ya mtoano Kombe la Dunia la wanawake katika mchezo wa soka. Kombe la dunia la netiboli kwa kina dada na mechi ya ngao ya jamii ya Uingereza kati ya Manchester  City na Arsenal. Pia matokeo ya mashindano ya La Francophonie inayokamilika Jumapili nchini DRC, miongoni mwa mengine. 
8/5/202323 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Michezo ya Francophonie yaanza jijini Kinshasa

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na kuanza kwa  mashindano ya La Francophonie nchini DRC, maandalizi kuelekea Olimpiki ya mwaka 2024? Uchambuzi wa mechi za Kombe la Dunia soka la kina dada droo ya klabu bingwa barani Afrika na michuano ya Kombe la Dunia mchezo wa netiboli.
7/29/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Vingegaard bingwa wa mashindano ya Tour de France mwaka 2023

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Jonas Vingegaard ndio bingwa wa mashindano ya kukimbiza baiskeli ya Tour de France ya mwaka 2023 , uchambuzi wa mechi za Kombe la Dunia la wanawake, mashindano ya  riadha Monaco Diamond League, tetesi za uhamisho barani Afrika na Ulaya pamoja na maandalizi ya mashindano ya La Francophonie nchini DRC.
7/22/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Tennis: Vondrousova amshinda Ons Jabeur kunyakua taji la Wimbeledon 2023

Miongoni mwa matukio hayo ni pamoja na uhamisho wa wachezaji wa klabu za soka kutoka nchi za Afrika Mashariki kuelekea kuanza kwa msimu mpya.Droo ya hatua ya makundi kwa mataifa ya Afrika kufuzu kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 katika mchezo wa soka nchini Marekani, Mexico na Canada.Katika mchezo wa Tennis, kuwania taji la Wimbeledon, Marketa Vondrousova ndio bingwa kwa upande wa wanawake….miongoni mwa mengine mengi
7/15/202323 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Morocco mabingwa wa taji la vijana wasiozidi miaka 23 Afrika

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na Morocco kushinda ubingwa wa kombe la Mataifa ya Afrika U23, timu ya soka ya wanawake ya Afrika Kusini Banyana Banyana yafanya  uamuzi wa kuelekea Newzealand kwa ajili ya michuano ya Kombe la dunia baada ya kusuluhisha mzozo wa malipo. 
7/9/202323 minutes, 37 seconds
Episode Artwork

Michuano ya soka kutafuta ubingwa vijana chini ya miaka 23 yashika kasi Morocco

Miongoni mwa yale  tuliyokuandalia ni pamoja na  klabu ya Kakamega Homeboyz kutoka Kenya, kufuzu kwenye michuano ya Shirikisho barani Afrika msimu ujao, mashindano ya Fatshi Cup kuanza leo nchini DRC, uchambuzi wa Kombe la Mataifa ya Afrika U23, matokeo ya michezo ya Ufukweni barani Afrika na riadha za Diamond League naye Mbappe aongoza wachezaji wa timu za ufaransa kukomesha vurugu kufuatia maandamano.
7/1/202323 minutes, 57 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya Safari Rally yaendelea kutifua vumbi nchini Kenya

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na mashindano ya Kimataifa ya kukimbiza magari nchini Kenya, Safari Rally, klabu ya soka ya Yanga nchini Tanzania, yampata kocha mpya na matukio yanayojiri viwanjani kote duniani.
6/24/202324 minutes, 40 seconds
Episode Artwork

Tennis: Morocco mabingwa wa taji la Billie Jean King

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia Jumamosi hii, ni pamja na Morocco yashinda  taji la tenisi Billie Jean King  barani Afrika , uchambuzi wa mechi za kufuzu Kombe la EURO na Kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao, kocha Nabi kuondoka Yanga na matokeo ya riadha Oslo Diamond League.
6/17/202323 minutes, 32 seconds
Episode Artwork

Faith Kipyegon avunja rekodi ya dunia kwenye mbio za Mita 5,000

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na Mkenya Faith Kipyegon kuvunja rekodi ya dunia katika  mbio za Mita 5,000 katika mashindano ya riadha ya Diamond League jijini Paris, Iga Swiatek ashinda tena taji la French Open kwenye mashindano ya Tennis na fainali ya klabu bingwa barani Ulaya, kati ya Manchester City na Inter Milan.
6/12/202323 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

Manchester City mabingwa wa taji la FA nchini Uingereza

Kocha wa klabu ya Manchester City nchini Uingereza, Pep Guardiola ameiongoza klabu yake kuishinda Manchester United mabao 2-1 katika fainali ya FA. Fainali ya pili ya shirikisho barani Afrika kati ya USM Algier na Yanga kutoka Tanzania, matukio ya riadha na Tennis ni miongoni mwa yale tuliyokuadalia kwenye Makala ya leo.
6/3/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Bayern Munich mabingwa wa ligi mara ya 11

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na maandalizi ya fainali ya kwanza kuwania taji la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga SC ya Tanzania na USM Alger, ya Algeria. Vituo vya kukuza soka nchini Rwanda, vinavyofadhiliwa na klabu ya Ufaransa ya Paris Saint-Germain na Bayern Munich yashinda taji lake ya 11 katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.
5/27/202323 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Dondoo ya taarifa za michezo, ikiwemo Senegal U-17 kuwa mabingwa wa Afrika.

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na ligi ya mpira wa vikapu barani Afrika kuanza leo nchini Rwanda, Yanga yatinga fainali ya kombe la shirikisho wakati Senegal watawazwa washindi wa kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17, CAF yatangaza mfumo mpya wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2026 na orodha ya mwisho ya wachezaji watakaowania tuzo la Marc-Vivien Foe yatangazwa na RFI/France 24.
5/20/202324 minutes
Episode Artwork

Omanyala awika mashindano ya riadha ya Kip Keino Classic jijini Nairobi

Mkenya Ferdinand Omanyala ameshinda mbio za Mita 100 katika mashindano ya riadha ya Kip Keino Classic yaliyofanyika jijini Nairobi, huku Mmarekani Sha'Carri Richardson naye akiibuka bingwa katika Mita 200 kwa upande wa wanawake.Tunachambua pia ligi ya soka nchini Rwanda,  kufukuzia ubingwa na mchuano wa watani wa jadi nchini Kenya, kati ya Gor Mahia na AFC Leopards.
5/13/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Wanariadha wajipima nguvu katika mashindano ya Diamond League

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo na uchambuzi mashindano ya riadha ya Diamond League, kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 17 na maendeleo ya ligi kuu za soka katika nchi za Afrika Mashariki na Kati.
5/6/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Simba SC yaondolewa kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na  kuanza kwa kombe la mataifa ya Afrika CHAN kwa vijana wasiozidi miaka 17, Simba kuondolewa kwenye mashindano ya CAF, Kenya yashinda Kombe la dunia katika mchezo wa wavu na uchambuzi wa mataifa ya  Kenya, Uganda na Tanzania kuomba kuwa wenyeji wa michuano ya AFCON 2027.
4/29/202323 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Mechi za robo fainali klabu bingwa Afrika zashika kasi

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja  na shirikisho la soka nchini Kenya FKF limeitaka bunge la Kenya kutunga  sheria dhidi ya wapangaji mechi, uchambuzi wa mechi za robo fainali mashindano ya vilabu bingwa barani Afrika, matokeo ya riadha wiki hii na tuzo ya RFI na France 24 kuhusu mchezaji wa zamani wa Cameroon Marc Vivien Foe.
4/22/202323 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Ligi kuu Tanzania bara: Nani ataibuka mshindi kati ya Simba na Yanga ?

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa mechi ya watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba kuwania taji la soka Tanzania bara, sakata la wachezaji Sadio Mane na Achraf Hakimi, CAF yampiga marufuku refarii wa Botswana na kocha wa Ethiopia ameacha kuifunza Ethiopia.
4/15/202323 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Droo ya robo fainali kuwania taji la klabu bingwa Afrika

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa hatua ya droo ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika. Shirikisho la mchezo wa Raga nchini Kenya limepata viongozi wapya na Mo Farah ashindwa kwenye mbio fupi nchini Gabon. 
4/8/202323 minutes, 56 seconds
Episode Artwork

Ripoti kuhusu hali ya wanamichezo wanaotumia dawa zilizozuiwa, yatolewa Kenya

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na Kenya kutoa ripoti ya kupambana na visa vya dawa zilizopigwa marufuku  za kusisimua misuli kwa wanamichezo na hali ya michuano ya soka, kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika na ile ya kufuzu kwa AFCON 2024.
4/1/202323 minutes, 24 seconds
Episode Artwork

Mataifa ya Afrika yaendelea kusaka nafasi ya kushiriki AFCON 2024

Jumamosi hii, miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na mwanamasombwi kutoka Tanzania, Karim Mandonga kupambana na mpinzani wake kutoka nchini Uganda jijini Nairobi, matokeo, matukio na uchambuzi wa mashindano ya kufuzu Kombe la mataifa ya Afrika mwaka huu na Kombe la EURO mwaka ujao huko barani Ulaya.
3/25/202323 minutes, 53 seconds
Episode Artwork

Gianni Infantino achaguliwa tena kuwa rais wa FIFA

Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na kongamano la Shirikisho la soka duniani  FIFA lililofanyika jijini Kigali nchini Rwanda, timu za taifa za Afrika Mashariki zajiandaa kwenye mechi za kimataifa na uchambuzi wa mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika na droo ya UEFA.
3/18/202323 minutes, 38 seconds
Episode Artwork

Watu watatu wakamatwa nchini Kenya kwa madai ya kupanga michuano ya soka

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na watu watatu, wawili raia wa kigeni, wakamatwa nchini Kenya  kwa tuhuma za upangaji mechi za ligi kuu ya soka nchini humo. Utasikia pia kuhusu fainali ya kombe la Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 na matokeo ya mashindano ya mchezo wa gofu ya Magical Kenya Open.
3/11/202323 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Tanzania yamteua  Adel Amrouche kuwa kocha mpya wa Taifa Stars

Miongoni mwa yale tuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) kumteua  Adel Amrouche raia wa Ubelgiji, kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya mchezo wa soka, michuano ya soka kuwania taji la Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 na madai ya  ubakaji dhidi ya Achraf Hakimi beki wa Morocco na PSG. 
3/4/202324 minutes
Episode Artwork

Mashindano ya Tour du Rwanda yaendelea kupamba moto

Raia wa Italia Manuele Tarozzi wa timu ya Green Project ameshinda mzunguko wa  7 wa mashindano ya kukimbiza  Baiskeli ya mwaka 2023  ya Tour du Rwanda. Mashindano hayo yatakamilika siku ya Jumapili. Tutakuletea pia matokeo na uchambuzi wa mechi za kuwania taji la klabu bingwa Afrika katika mchezo wa soka.
2/25/202323 minutes, 48 seconds
Episode Artwork

Mashindano ya Tour du Rwanda yawakutanisha magwiji wa kukimbiza baiskeli

Mashindano ya mwaka 2023 ya kukimbiza Baiskeli ya Tour du Rwanda, yanaanza siku ya Jumapili jijini Kigali, na kuwavutia magwiji wa mchezo huo  kama Chris Froome raia wa Kenya na Uingereza. Tutakuletea pia mashindano ya soka, kuwania taji la klabu bingwa Afrika.
2/18/202324 minutes
Episode Artwork

Klabu zaanza kuchuana kutafuta taji la klabu bingwa Afrika

Michuano ya hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, imeanza, lakini pia tutakuletea matukio mengine yanayotokea viwanjani kote  duniani.
2/11/202324 minutes
Episode Artwork

CHAN 2023: Nani atakuwa mbabe kati ya Algeria na Senegal ?

Fainali ya CHAN, kuwania ubingwa wa mchezo wa soka kwa wachezaji wanaocheza katika ligi za nyumbani barani Afrika, inachezwa baadaye siku ya Jumamosi kati ya wenyeji  Algeria na Senegal, tunachambua hili na mengine mengi.
2/4/202324 minutes
Episode Artwork

Aryna Sabalenka ashinda taji la Australian Open 2023

Aryna Sabalenka kutoka Belarus ndio mshindi wa taji la Australian Open katika mchezo wa Tennis, baada ya kumshinda Elena Rybakina kutoka Kazakhstan kwa seti, 6-4 ,3-6 na 6-4, katika fainali iliyochezwa siku ya Jumamosi katika mji wa pwani wa Melbourne. Tunachambua hili na mengine mengi.
1/28/202324 minutes
Episode Artwork

Michuano ya CHAN yaendelea kushika kasi nchini Algeria

Miongoni mwa yale tunayojadili ni pamoja na kuendelea kwa michuano ya soka kutafuta ubingwa wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka katika ligi za nyumbani CHAN, tuzo ya mwanamichezo bora nchini Kenya, SOYA na maandalizi ya mechi kati ya Arsenal na Manchester United nchini Uingereza.
1/21/202323 minutes, 43 seconds
Episode Artwork

Michuano ya CHAN yaanza nchini Algeria, Morocco yapata changamoto

Miongoni mwa yale tunayoangazia ni pamoja na michuano ya soka CHAN, kuwania taji la Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka nyumbani iliyoanza nchini Algeria. Pambano la masumbwi kati ya wanabondia kutoka Kenya na Tanzania, inayofanyika jijini Nairobi.
1/14/202323 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

Didier Deschamps kuendelea kuwa kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa

Didier Deschamps ametangaza kuwa ataendelea kuwa kocha wa timu ya taifa ya soka ya Ufaransa hadi michuano ijayo ya kombe la dunia mwaka 2026. Tunajadili hili na mengine mengi katika Makala ya leo ya Jukwaa la Michezo.
1/7/202323 minutes, 51 seconds
Episode Artwork

Matukio makubwa yaliyotokea viwanjani mwaka 2022

Haya ni makala ya mwisho ya Jukwaa la Michezo kwa  mwaka wa  2022. Tunakuletea kwa ufupi, matukio makubwa yaliyotokea viwanjani . Tunakutakia kila la heri  katika mwaka mpya wa 2023.Asante kwa kuwa shabiki wetu.
12/31/202223 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

André Onana atangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Cameroon

Miongoni mwa yale tunayoangazia ni pamoja na tangazo la kipa wa timu ya taifa ya Cameroon,  André Onana, kutangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa.
12/24/202223 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

JUKWA LA MICHEZO KUHUSU FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA QATAR

Kwenye Makala ya leo Jumapili 18 12 2022 tunaangazia fainali ya kombe la dunia kati ya Ufaransa dhidi ya Argentina. Sikiliza hapa iwapo ulikosa kwenye radio
12/18/202220 minutes, 23 seconds
Episode Artwork

Nani atashinda kombe la dunia, kati ya Ufaransa na Argentina ?

Mabingwa watetezi wa kombe la dunia, Ufaransa, watachuana na Argentina katika mchuano wa fainali kuwania taji la kombe la dunia, siku ya Jumapili, Desemba 18 2022. Je, nani atashinda ?
12/17/202223 minutes, 52 seconds
Episode Artwork

Kombe la dunia: Hatua ya robo fainali yapamba moto

Michuano ya hatua ya robo fainali, kuwania taji la dunia, katika mchezo wa soka, inaendelea nchini Qatar.Tunachambua nafasua ya Morocco dhidi ya Ureno na Ufaransa dhidi ya Uingereza. Croatia na Argentina tayari zimefuzu hatua ya nusu fainali.
12/10/202223 minutes, 54 seconds
Episode Artwork

Michuano ya kombe la dunia yafikia hatua ya 16 bora

Michuano ya kombe la dunia imefika katika hatua ya mwondoano, huku timu mbili za Afrika, Senegal na Morocco zikifanikiwa, kufika katika hatua hiyo.
12/3/202224 minutes, 21 seconds
Episode Artwork

Mataifa mbalimbali yaendelea kupambana kushinda kombe la dunia

Michuano ya soka, kuwania taji la dunia inaendelea kushika kasi nchini Qatar, huku mataifa ya Afrika yakianza vibaya. Hata hivyo, Senegal ilishinda mechi yake ya pili dhidi ya wenyeji Qatar.
11/26/202223 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Maandalizi ya kombe la dunia, yakamilika nchini Qatar

Macho na masikio sasa yanaelekezwa nchini Qatar, kuanzia siku ya Jumapili, kushuhudia kipute cha kombe la dunia katika mchezo wa soka. Tunachambua hili kwa kina.....
11/19/202223 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

Sadio Mane, ajumuishwa kwenye kikosi cha Senegal licha ya kuwa na jeraha

Makocha wameanza kutangaza vikosi vya mataifa 32, yatakayoshiriki kwenye michuano ya kombe la dunia, kuanzia Novemba 20 nchini Qatar. Mshambuliaji wa Senegal Sadio Mane, amejumuishwa katika kikosi cha mwisho, licha ya kuwa na jeraha. Tunachambua hili kwa kina na mengine mengi.
11/12/202223 minutes, 58 seconds
Episode Artwork

TP Mazembe yatupwa nje ya mashindano ya klabu bingwa Afrika

Klabu ya soka ya TP Mazembe kutoka DRC, imetupwa nje ya mashindano ya kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika. Somalia na Sudan Kusini, nazo zimefuzu katika michuano ya bara Afrika, mchezo wa soka kwa wachezaji wasiozidi miaka 17.
10/15/202223 minutes, 55 seconds
Episode Artwork

CAF klabu bingwa: Timu mbalimbali zasaka fursa za kufika hatua ya makundi

Klabu za soka barani Afrika, zinachuana katika michuano ya kufuzu katika hatua ya makundi kuwania taji la klabu bingwa na Shirikisho barani.Tunajadili hili na mengine mengi.
10/10/202223 minutes, 48 seconds