Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Hatua zilizopigwa katika kumuinua mtoto wa kike
Katika muendelezo wa makala kuhusu siku ya mtoto wa kike duniani, tunaangazia vyanzo vya visa vya unyanyasaji wa watoto wa kike na hatua zilizopigwa na mashirika mbalimbali katika kuifanya sauti ya mtoto wa kike kusikika.
24.10.2024 • 10 Protokoll, 15 Sekunden
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani
Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 11 Oktoba, ni fursa ya kuangazia changamoto zinazokabili watoto wa kike duniani na kukuza usawa wa kijinsia. Katika mwaka 2024, mada ilikuwa "Kutoa sauti kwa watoto wa kike: Fursa na Changamoto katika Utu wa Kike."Makala haya yataangazia kwa kina haki za mtoto wa kike na hatua zilizopigwa katika kusababisha mtoto wa kike kuskizwa na hata hatua zilizochukuliwa ili kuboresha elimu, afya, na usalama wa watoto wa kike, pamoja na jinsi jamii zinaweza kushiriki katika kuwasaidia kufikia ndoto zao.Aidha, itajadili umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wazazi katika kufanikisha malengo haya.
18.10.2024 • 9 Protokoll, 22 Sekunden
MAMILLIONI YA WATU HASA WATOTO BARANI AFRIKA HAWAJAPATA HAKI ZA CHAKULA
Chakula ni muhimu kwa maisha, kuishi, heshima, ustawi, na maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa watu binafsi, jamii, na mataifa. Sheria za kimataifa zinatambua haki ya kila mtu kupata chakula cha kutosha na haki ya kuwa huru kutokana na njaa. Haki hii ni ya msingi kwa utekelezaji wa haki zote za binadamu. Nchini Kenya, ni haki ya kikatiba, iliyoko katika Kifungu cha 43(1)(C) kinachosema: "Kila mtu ana haki ya kuwa huru kutokana na njaa na kuwa na chakula bora na cha kutosha .Lakini je, sheria hii inatambuliwa ? Je, watu wanaelewa haki yao ya chakula? Na hali ya usalama wa chakula nchini Kenya iko vipi leo?Katika kipindi cha leo ,cha jua haki zako , tunaangazia iwapo watu wanapata haki zao za kupata chakula na jinsi changamoto za kiuchumi na kimazingira zinavyoathiri upatikanaji wa chakula nchini Kenya
16.10.2024 • 9 Protokoll, 40 Sekunden
DRC : Wanawake wabakwa katika gereza la Makala nchini
Katika makala haya tunaangazia ripoti ya umoja wa mataifa kusema kwamba zaidi ya wanawake wafungwa ya 260 walibakwa katika jela ya Makala nchini DRC, mapema mwezi huu wakati wa jaribio la wafungwa kutoroka jela. Ripoti hiyo imebaini kwamba kati ya wafungwa 348 katika gereza hilo la Makala, wafungwa 268, walitendewa vitendo vya unyanyasaji wa kingono ikiwemo ubakaji, wanawake 17 kati ya waliobakwa wakiwa chini ya umri wa miaka 19.Ripoti hiyo aidha imeongeza kuwa wanawake hao walilazimika kutafuta mbinu za kuzuia magonjwa baada ya kutendewa vitendo hivyo vya kikatili.Awali serikali ya DRC ilikuwa imekiri kubakwa kwa wanawake hao ila haikotoa idadi ya wanawake waliobakwa.Kadhalika ripoti hiyo pia imesema wafungwa 129 waliojaribu kutoroka jela waliuawa kwa kupingwa risasi, katika gereza hilo la Makala ambao linastahili kutoa huduma kwa wafungwa 1500, ila lina zaidi ya wafungwa alfu 15.Rais Felix Tshisekedi aliagiza kufanyika kwa uchuguzi kuhusiana na jaribio hilo la wafungwa kutoka, na mikakati ya kupunguza idadi ya wafungwa katika gereza hilo la jiji Kinshasa.
19.9.2024 • 9 Protokoll, 30 Sekunden
Kenya : Watoto wateketea shuleni, je jukumu la nani kumlinda mtoto akiwa shuleni
Nchini Kenya zaidi serikali inaendesha uchunguzi wa chembechembe za DNA, za wanafunzi 21 wa shule ya msingi ya Endatasha baada yao kuteketea kiasi ya kutotambulika, kabla ya miili yao kutolewa kwa familia. Miili limewaacha wazazi kwenye njia panda wasijue la kufanya, wakati huu maswali yakiendelea kuulizwa je nani wakulaumiwa baada ya mkasa huo wa moto shuleni. Kufahamu mengi skiza makala haya.
16.9.2024 • 9 Protokoll, 43 Sekunden
Kenya: Vikundi vya kina mama vyajitokeza kupinga ukeketaji
Katika makala haya tunajikiti kuangazia uketetetaji ambapo wasichana wamekuwa ukiendelea kukeketewa nchini Kenya licha ya serikali kanzisha kampeni ya kuhamasisha umma kuhusu athari zinazotokana na ukeketaji huo. Jamii za Kenya, kupitia kwa kina mama na wasichana waliopitia ukeketaji kwa ushirikiano na mashirika ya kijamii wameanzisha vikundi vya kutetea haki za wasichana ili kuwalinda kutokana na ukeketaji huo. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
27.8.2024 • 10 Protokoll, 4 Sekunden
Kenya : Jamii za mipakani zataka serikali kuwapa vitambulisho
Jamii zinazoishi mikapani nchini Kenya kwa muda zimekuwa zikikosa huduma muhimu ya kupata vitambulisho kutoka na sababu ambazo wenyewe wanasema serikali inawabagua. Katika makala haya tunajikiti kuangazia masaibu ya jamii za mipakani nchini kenya kupata vitambulisho. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
24.8.2024 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Kenya : Mawikili watoa mafunzo ya sheria kwa vijana
Mawakili mjini Mombasa pwani ya Kenya wamenza kutoa mafunzo ya sheria kwa vijana waliokuwa wakiandamana kushinikiza mabadiliko. Mawakili hao ambao ni wanachama wa chama cha mawakili nchini LSK, wamesema hatua hiyo imechochewa na maandamano yaliokuwa ya vijana maarufu kama Gen-Z leo lengo lao kuu likiwa kuwawajibisha viongozi serikalini. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya
17.8.2024 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Tanzania : Human Right Watch lasema Tanzania inawahangaisha raia wa Ngorongoro
Katika makala haya saba yetu inalenga taifa la Tanzania eneo la Ngorongoro ambapo serikali imekuwa ikiwahamisha wenyeji eneo hilo, ili kuihifadhi eneo hilo kutokana na historia yake. Tuangazia repoti ya shirika la kimataifa la kutete haki za biandamu la Human Watch ambayo imetuhumu serikali ya Tanzania kwa kuwafurusha kwa nguvu mamia ya raia wa kimasaai kutoka eneo la Ngorongoro, maafisa wa wanyama pori wakidaiwa kuwahangaisha kwa kuwapiga wenyeji ili kuwafurusha kutoka katika ardhi za mababu zao.Karibu kwenye makala haya utaskia kutoka kwa wadau mbalimbali huku tukijadili ripoti hii ya Human Right Watch.
6.8.2024 • 10 Protokoll, 2 Sekunden
Kenya : Haki za wanawake pamoja na kina dada wanaojiuza
Katika makala haya tunajadili haki za kina dada pamoja na kina dada wanaojiuza. Nchini Kenya, kina dada wanaojiuza pia wanataka kutambuliwa.
3.8.2024 • 10 Protokoll
Kenya : Haki ya wanahabari kuteleza majukumu yao bila vikwazo
Juma hili tunaangazia haki za wanahabari kupeperusha habari zao bila kuingiliwa na vyombo vya usalama katika mataifa yao. Shaba yetu bila shaka inalenga taifa la Kenya, nchi ambayo wanahabari wamejeruhiwa wakati wakitekeleza majukumu yao, ya kuangazia maandamano ya vijana wa Gen Z, ambao wamekuwa wakishinikiza mabadiliko nchini Kenya. Kwa siku sasa kilio cha wanahabari nchini Kenya kimekuwa ni kutaka serikali kuheshimu haki zao kwa kuwaruhusu kutekeleza wajibu wao bila vikwazo.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
27.7.2024 • 9 Protokoll, 22 Sekunden
Kenya : Polisi wa Uingereza watuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu
Katika makala haya tunaangazia dhuluma zinazodaiwa kutekelezwa na wanajeshi wa Uingereza ambao wana kambi ya mazoezi nchini Kenya leo la Nanyuki. Wanajeshi hao wanadaiwa kuwabaka na kuwaua wanawake mbali na kuwacha vilipuzi katika maeneo ya mazoezi ambavyo baadaye hulipuka na kusababisha majiraha na maafa. Wanawake wambao wamekuwa na uhusiano wa kimapaenzi na wanjeshi wa uingreza eneo hilo la Nanyuki wamesumulia namna gani wamesalia na majiraha ya moyo kutokana na kuachwa na wapenzi wao wa kizungu ambao baada ya mazoezi yao, wao hurejea nchini mwao licha ya kuwazalisha.
16.7.2024 • 9 Protokoll, 29 Sekunden
Kenya : Wanaume wanapitia dhuluma za kijinsia kwenye ndoa, ila wamesalia kimya
Visa vya dhuluma dhidi ya wanawake vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara katika jamii mbalimbali barani Afrika na hata duniani,jambo ambalo limechangia sheria nyingi kuanzishwa kulinda wanawake,lakini hata hivyo dhuluma hizo zimeanza kuwakumba wanaume wengi kwa kunyanyaswa na kupingwa na wake wao. Katika makala haya tunaangazia dhuluma za kijinsia dhidi ya wanaume shaba yetu ikilenga taifa la Kenya, ambapo mwanahabari wetu Victor Moturi alitangamana na wanaume ambao wamehangaishwa na kudhulumiwa kwenye jamiii nchini Kenya hasa eneo la Magharibu. Kufahamu mengi skiza makala haya.
10.7.2024 • 9 Protokoll, 58 Sekunden
Sudan Kusini inakabiliwa na hali ya binadamu kutokana na wimbi kubwa la wakimbizi
Taifa la Sudan Kusini linashuhudia wimbi kubwa la wakimbizi wanaoendelea kukimbia vitra nchini Sudan, licha taifa hilo kuendelea kushuhudia changamoto nyingi tu ikiwemo ukosefu wa amani katika baadhi ya majimbo yake. katika makala haya tunazama kuangazia ripoti ya shirika la Care in South Sudan ambayo imechangia ripoti kuhusiana na hali ya binadamu nchini Sudan Kusini. Kufahamu mengi skiza makala haya.
6.7.2024 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Kenya : Haki ya raia kuandamana kufikisha ujumbe kwa serikali
Nchini Kenya vijana wamekuwa wakiandamana kulalamikia kile wataja mpango wa serikali kuongeza kodi kwa kutumia mswada wa fedha wa mwaka 2024. Idadi kubwa ya vijana hao wanapinga mswaada huo wanaosema utaongeza gharama ya maisha kipindi hiki wengi wao wakiwa tayari hawana ajira, makali ya gharama ya maisha nayo yakiendelea kulemaza shughuli zao za kila siku.Maandamano hayo yameandliwa na kundi la vijana linalojiita Gen Z, yaani kizazi cha vijana waliozaliwa kati ya mwaka 1995 hadi 2010.Vijana hawa wanadai serikali ya rais William ruto imeanza kuwa dhalimu kwa kuongeza ushuru kwa bidhaa muhimu kama vile soda za wanawake na vinengnevyo. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi
25.6.2024 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Amnesty International : Adabu ya kifo imeongeza zaidi duniani
Idadi ya watu waliopewa adabu ya kifo iliongezeka zaidi mwaka 2023, mataifa ya mashariki ya kati na nchini Somalia abadu hiyo ikiripotiwa kuwa ya juu zaidi. Kwa mjibu wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, katika ripoti yake ya kila mwaka, zaidi ya watu 1, 153 walipewa adabu ya kifo mwaka 2023 pekee, bila kujumuisha idadi kutoka nchini China, taifa ambalo linaripotiwa kuwa msiri katika kutoa taarifa kama hizi. Idadi hii ni asilimia 30 zaidi ikilinganishwa na mwaka 2022. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
18.6.2024 • 10 Protokoll, 2 Sekunden
Kenya : Haki za watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi wanataka kutambuliwa zaidi
Katika makala haya ni awamu ya pili tunaendelea na mazungumzo yetu na bwana meshaka Sisende raia wa Kenya anayeishi na ulemavu wa ngozi. Juma lililopita tuliangazia pakubwa changamoro wanazopitia raia hawa naoishi na ulemavu wa ngozi na hapa tunazidi kuangazia mananikio ya raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi.Miaka kadhaa iliopita mauwaji ya raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi yalikithiri sana nchini Tanzania, hatua iliochangia viongozi wa tabaka mbalimbali kusimama kidete kukemea mauwaji hayo mamlaka nazo zikiwakamata waliokuwa wakihusishwa na mauaji hayo kwa misingi ya kishirikiana. Ni hapo ndipo wasanii kama vile Herbert Naktare maarufu Nonini kutoka nchini Kenya aliachilia wimbo wake wa Colour Kwa Face, kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuwakumbatia watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
17.6.2024 • 9 Protokoll, 51 Sekunden
Haki za raia wanaoishi na ulemavu wa ngozi hapa Africa
Kila mwaka Juni 14 dunia huadimisha siku ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi sherehe zilizoanza kuadimisha tangu mwaka 2014, ili kuhamasisha jamii kwamba watau wanaoishi na ulemavu wa ngozi wao ni watu wa kawaida katika jamii. Katika makala haya Meshaka Sisende kutoka nchini Kenya anasimulia maisha ya kawaida ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya
12.6.2024 • 9 Protokoll, 40 Sekunden
Tume ya haki za binadamu nchini Uganda yatuhumiwa kuegemea upande wa serikali
Makala haya yanaangazia tendekazi wa tume za kutetea haki za biandamu za serikali zetu za Africa mashariki.Hii ni baada ya lalama kutoka kwa kiongozi wa upinznai nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine kwamba tume ya haki nchini Uganda imekuwa ikiegemea upande wa serikali katika kutekeleza majukumu yake. Robert Kyagulanyi,amelazimika kuondoa lalama zake mbele ya tume ya haki ya kutetea haki za biandamu nchini Uganda kutokana na madai inayosema tume hiyo imeshindwa kuyashughulikia.Wine alikuwa amewasilisha kesi yake mwaka 2018 akilalamikia hatua ya polisi nchini Uganda kukiuka haki zake kwa kumzuia kuandaa tamasha za muziki zaidi ya 20, mbali na polisi kuchukuwa nyombo vyake vya mziki, hili akidai lilimzuia kupata haki yake ya kupata mapato kutokana na mrengo wake wa kisiasa. Fahamu mengi kwa kuskiza makala haya.
31.5.2024 • 9 Protokoll, 38 Sekunden
Kenya : Unyanyapaa wanaopitia kina mama tasa kwa jamii
Katika makala haya tunaangazia haki za kina dada ambao hawajafanikiwa kupata watoto katika jamii zetu za kiafrica. Barani Afrika wanawake ambao hawana uwezo kupata watoto au wale huchukuwa muda mrefu kupata watoto , hupitia changamoto si haba ,na kukosa haki,kama vile kutotambuliwa na jamii,uridhi wa Mali na hata wengine kufukuzwa kwenye ndoa,hali hiyo ikichochewa na tamaduni ambazo zimekita mizizi. Kwa mjibu wa twakwimu za shirika la afya duniani WHO ni kwamba wanawake 15 kati ya 100 barani Afrika hawana uwezo wa kupata watoto, na kati ya wanawake 6 angalau mmoja huwa hawana uwezo wa kupata mtoto kidunia.Swala la kukosa kupata mtoto hushuhudiwa kati ya wanawake na wanaume, ila hapa barani africa kasumbuka mara nyingi huelekezewa kina mama, hili likisababisa dhiki, unynyapaa, ufukara miongoni mwa wanawake wengi wao sasa wakiathiriwa na afya ya akili na hata kisaikolojia.Licha ya tatizo hili kuwa na suluhu, wengi wamesalia kukosa imani kutokana kwani hawana pesa za kutafuta tatibu husika.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
21.5.2024 • 10 Protokoll, 3 Sekunden
DRC : Makundi ya waasi yatuhumiwa kwa ukatili wa kijinsia dhidi ya raia mbilimo
Nchini DRC ; familia ya jamii ya mbilikimo , ukipenda wambute kama wanavyo wanavyofahamika nchini DRC, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukiukaji wa haki za binadamu. Wanawake na wasichana kutoka jamii hii wengi ni waathiriwa wa vitendo vya ubakaji , vinavyo tekelezwa na wanaume kutoka makundi ya waasi mashariki mwa DRC, visa hivi vina tendwa na wanaume .Mwezi Aprili mwaka huu kule mkowani Ituri, watetezi wa haki za binadamu walichapisha ripoti ilioashiria namna wasichana na wanawake mbilikimo , wamebakwa na wanapiganaji wa makundi ya waasi.Hali hii imedaiwa kuchochewa na imani potofu kwamba , ukitenda tendo la ndoa na mwanamke au msichana mbilikimo, huwezi kufariki kwa risasi vitani wala kuambukizwa baadhi ya magonjwa .Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
18.5.2024 • 10 Protokoll
Je haki za mtoto wa kiume unazifahamu, na je unafikiri zimekiukwa?
Katika makala haya mtetezi wa haki za mtoto wa kiume Faith Maina Wanjiku, anasisitiza kwamba kampeini za kumpa uwezo mtoto wa kike ndizo zimechangia kudidimia kwa hadhi ya mtoto wa kiume. Wajiku Maina raia kutoka nchini Kenya, anasema katika jamii ya leo hakuna anayeshughulikia haki na majukumu ya mtoto wa kiume, hali ambayo imechangia kizazi kizembe cha mtoto wa kiume. Skiza makala haya kufahamu suluhu kwa baadhi ya changamoto za mtoto wa kiume.
9.5.2024 • 9 Protokoll, 54 Sekunden
Kenya : Polisi watuhumiwa kuwaua raia kiholela zaidi ya raia 118 wakiuawa mwaka 2023
Makala haya tunaangazia ripoti ya mashirika ya kiraia nchini kenya kuhusu vifo vya kiholela vinavyodaiwa kutekelezwa na polisi. Ripoti hiyo inakaria kwa mwaka uliopita wa 2023, polisi waliwaua zaidi ya raia 118, masharika hayo yakisema licha ya mauwaji hayo ya raia hakuna hatua ambazo zimechukuliwa na serikali waathibu wahusika.Hata hivyo masharika hayo yanasema idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na mwaka 2022 ambapo zaidi ya watu 130, wanadaiwa kuuawa na polisi nchini Kenya.Mauwaji haya ya raia kwa mjibu wa masharika haya yanayojumuisha, shirika la kimataifa la haki za binadamu, Amnesty International , tume ya haki za binadamu nchini Kenya , na masahrika mengine, ni kwamba yalitekelezwa wakati wa operesheni ya uhalifu. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
2.5.2024 • 9 Protokoll, 56 Sekunden
Kenya : Serikali yaanza kutoa miili ya waumini waliofariki baada ya kususia chakula ili wamuone Yesu
Unamkumbuka kiongozi wa wa dini Paul Mackenzi anayetuhumiwa kwa kushiwishi waumini wake kususia chakula hadi kufa, ili kukutana na yesu nchini Kenya. Baada ya takriban mwaka moja na mwezi mmoja wa serikali ya Kenya kufukua miili ya waumini waliofariki na kuzikwa katika msiku wa Shakahola na kuzifanyia uchuguzi wa vina saba yaani DNA, serikali sasa imeanza kutoa miili hiyo kwa familia za jamaa waliofariki.Serikali ya Kenya kupitia kwa mwanapatholijia wake mkuu daktari Johason Odour, imesema ilichukuwa muda mrefu kutoa miili kwa family zilizoathirika kutokana na kuharibika kupita kiasi.Soma piaWazee wauliwa pwani ya Kenya kwa tuhuma za kwamba ni wachawiKatika haya mwanahabari Diana Wanyonyi kutoka pwani ya Kenya alihudhuria mazishi ya baadhi ya waathiriwa wa mafunzo ya itikadi kali Paul Mackenzie na anasimulia hali ilivyokuwa
25.4.2024 • 9 Protokoll, 51 Sekunden
Haki ya watoto chotara shirika la African Futures Lab linataka Ubelgiji kuwatambua
Shirika lisilo la kiserikali la kutetea haki za binadamu la African Futures Lab, lenye makao yake jijini Brussels nchini Ubelgiji, lilizindua ripoti kushinikiza watoto chotara na mama zao kutoka nchini DRC, Rwanda na Burundi, kulipwa fidia, kutambuliwa kuwa raia wa Ubelgiji na kupata haki nyingine za msingi. Wakati wa ukoloni wa nchi ya Ubelgiji kwa nchi hizo za maziwa makuu, wakoloni, wanaume wazungu kutoka nchini Ubelgiji, waliwachukua kwa nguvu wanawake kutoka DRC, Rwanda na Burundi na kuwapeleka Ubelgiji na kuwazalisha, huku wengine wakifanyiwa hivyo wakiwa kwenye nchi zao.Makala haya yameandiliwa na Benson WakoliSoma piaHaki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)
17.4.2024 • 9 Protokoll, 9 Sekunden
Madaktari nchini Kenya wagoma kuishinikiza serikali kuzingatia haki zao
Muungano wa madaktari, wauza dawa na madakrati wa meno, KMPDU, ambao unawakilisha zaidi ya wanachama 7,000 uliitisha mgomo Machi 15, ili kudai mishahara iliyocheleweshwa, pamoja na kupewa ajira mara moja kwa madaktari wanafunzi.Mgomo ambao umesababisha hali ya sintofahamu kwa wagonjwa kwa takribani wiki tatu sasa.
16.4.2024 • 9 Protokoll, 29 Sekunden
DRC : Jamii ya mbilikimo yalilia serikali kuwapa nafasi kuhudumu serikalini
Nchini DRC , mara kwa mara jamii ya mbilikimo ama wambute kama wanavyo julikana katika taifa hilo, wamekuwa kilalamikia kile wanachodai kubaguliwa na raia kutoka jamii ya wabantu nchini DRC. Jamii hiyo imekuwa ikidai wameachwa nje kwenue nyadhifa kama vile viongozi wa nyumba 10 hadi cheo cha rais, wanadai hakuna raia kutoka jamii hiyo anashikilia wadhifa wowote serikali.Moja ya mashirika za haki za binadamu kwa jina " Greats lakes Human Right Programme" katika ripoti ya hivi karibuni , imesema kwamba sheria nzuri zipo za kuwalinda na kutetea haki za mbilikimo , ila utekelezaji wake ndio umekuwa changamoto.Mwandishi wetu wa Beni nchini DRC Eriksson Luhumbwe amezungumza na raia hao kutoka jamii ya mbilikimo na kutuandalia ripoti hii, skiza.
10.4.2024 • 10 Protokoll, 5 Sekunden
Haki za raia wa mataifa ya Afrika wanaofanya kazi katika mataifa ya ughaibuni.
Raia wa mataifa tofauti tofauti ya Afrika ikiwemo Kenya na Uganda huelekea katika mataifa ya kiarabu kutafta ajira Kila mwaka . Changamoto nyingi zikiripotiwa.Kwenye makala haya Florence amezungumza nao wakina dada wanaofanya kazi huko .
4.4.2024 • 10 Protokoll, 8 Sekunden
Kenya : Dhuluma za kijinsia na mrundiko wa kesi mahakamani
Katika makala haya tujahadili dhuluma za kijinsia swala ambalo limekuwa ni donda sugu kwenye familia zetu, na jamii kwa ujumla. Wakili Latifa Njoki na wakili Elizabeth Njambi wote kutoka nchini Kenya wanafafanua swala la mrundiko wa kesi mahakani zinazohusiana na dhuluma za kijinsia na suluhu.
19.3.2024 • 10 Protokoll, 7 Sekunden
DRC: Waasi wa CODECO wadaiwa kutekeleza mauwaji ya kikabila
Mashariki mwa DRC , vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vinazidi kushika kasi hasa mauwaji ya raia, vinavyoendelezwa na makundi ya waasi. Makundi haya ni yale ya ndani na ya kigeni kutoka mataifa jirani ya Uganda "ADF" Sudan kusini "Bororo" na Jamuhuri ya Afrika ya kati "LRA" . Wapiganaji Hao sasa hivi wame fikia hata kiwango cha kushambulia vituo vya afya na kuwazika raia wakiwa hai.Makala haya yamlika hali wilayani Djugu mkowani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC , ambapo zaidi ya raia 800 wameuawa kikatili na kundi lenye silaha la CODECO katika kipindi cha miaka 6 , kwa mujibu wa mashirika ya kirai mashariki mwa DRC .
15.3.2024 • 10 Protokoll, 7 Sekunden
Kenya: siku ya wanawake duniani nini Kipya?
Siku ya wanawake duniani huadimishwa kila kila tarehe nane ya mwezi machi, kuangazia mchango wa mwanamke katika jamii na pia changamoto zinazowakumba wanawake. Kauli mbiu ya maadimisho ya mwaka huu, nchini Kenya ni uwekeza kwa wanawake ili kufanikisha maendeleo kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
8.3.2024 • 9 Protokoll, 17 Sekunden
Kenya : Wasanii walilia haki yao
Muungano wa wanamziki nchini Kenya (MAAK), unamtaka mwenyekiti wa Shirika la Hakimiliki ya Muziki ya Kenya, Ezekiel Mutua kujiuzulu kutokana na kile wanadai amekuwa akipora peza za wamziki. Kupitia taarifa muungano huo, unasema Mutua amekuwa akijilimbikizia pesa za wasanii huku wahusika wakiendelea kusalia maskini. Ili kufahamu zaidi skiza makala haya.
2.3.2024 • 9 Protokoll, 59 Sekunden
Haki ya kutali Africa bila vikwazo
Ni vigumu kwa watu wachache kutumia usafiri wa beskeli hapa Africa lakini Yusufu raia wa Morocco kwake kutali Africa kwa kuendesha beskeli ni kama kazi. Benson Wakoli aliketi chini na Yusuf, kuthamini safarizake barani Africa na jinsi gani amekuwa akipokelewa na raia wa mataifa mengine.
21.2.2024 • 10 Protokoll, 11 Sekunden
Valentine : Haki ya wanaume na wanawake
Kila mwaka Feb 12 dunia huadimisha siku ya wapendanao, raia wengine wakionesha mapenzi kwa wachumba, pamoja na marafiki. Lakini nini maana ya valentine? kufahamu zaidi skiza makala haya.
17.2.2024 • 9 Protokoll, 56 Sekunden
Kenya : Viongozi wa dini wapinga ushoga
Kwenye haya tunajadili hatua viongozi wa dini nchini Kenya kulitaka bunge kuanza uchuguzi wa haraka kuhusiana na madai kwamba kuna njama ya makusudi kueneza sera za ushoga nchini Kenya. Viongozi hao wa dini wanadai kwamba kuna mpango wa ambao tayari umepangwa kupinga vita dhidi ya mashoga na wasagaji, na watu wanaodai kutetea haki za mashoga, hulka ambayo inaenda kinyume kabisa na maadili ya jamii za kiafrica. Kufahamu zaidi skiza makala haya.
9.2.2024 • 10 Protokoll
DRC : Je haki za raia zilikiukwa kipindi cha uchaguzi?
Katika makala haya tunapiga darubini kuangazia haki za raia wa DRC wakati wa kipindi cha kampeini za uchaguzi, na baada ya uchaguzi. Mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu Mapendo Kusudi alifanya mazungumzo kupitia njia ya simu na mwandishi wetu Benson Wakoli. Kufahamu zaidi skiza makala haya.
3.2.2024 • 10 Protokoll
Haki ya mtoto kupata elimu ( Fizi)
Katika haya tunaangazia haki ya watoto kupata elimu ambapo utaskia kwa wadau mbalimbali walioazisha kutuo cha elimu cha Fizi kinatoa elimu ya somo la kifaransa nchini Kenya kwa watoto wakimbizi kutoka nchini DRC , Rwanda na Burundi. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 2014 lengo likiwa kuwasaidia watoto wakimbikizi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ili kuendelea kujifunza na kuendeleza tamaduni ya lugha ya Kifaransa,hasa ikizingatiwa kwamba nchini Kenya raia wengi huzungumza kingereza na Kiswahili.
26.1.2024 • 10 Protokoll
Human watch yatahumu jamii ya kimataifa kwa kukosa kusadia Sudan
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch limetuhumu jamii ya kimataifa kwa kukosa kushughulikia vita vinavyoendelea nchini Sudan. Kwa mjibu wa ripoti ya kila mwaka ya shirika hilo, jamii ya kimataifa haijafanya juhudi za kutosha kushawishi pande hasimu nchini Sudan Kusitsha vita. Ili Kufahamu negi zaidi skiza makala haya.
21.1.2024 • 10 Protokoll
Hali ya haki za binadamu nchini Kenya na Tanzania
Visa vya raia kupotea na kisha kuonekana baada ya siku kadhaa nchini Kenya si vipya tena, hili likishuhudia mara kwa mara nchini Kenya, polisi wakituhumiwa kuhusika kwenye visa hivi lakini je tume ya haki za binadamu nchini Kenya inafahamu hili? na je nchini Tanzania hali ya hali za haki za binadamu ipo je?Maswali haya yanajibiwa ndani ya makala.
9.1.2024 • 9 Protokoll, 46 Sekunden
Mashirika ya misaada ya kibinadamu yakumbwa na uhaba wa fedha
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR, limeonya kuwa mashirika ya misaada yanakabiliwa na uhaba wa fedha, na kwamba yanahitaji dola milioni 400 kufikia mwisho wa mwaka huu. Katika kongamano la siku tatu kuhusu wakimbizi huko Geneva, Wiki iliyopita, Mkuu wa shirika hilo Filippo Grandi, alisema asilimia 75 ya wakimbizi wanaishi katika nchi maskini na zile zinazoendelea.Grandi ameiomba jamii ya kimataifa kutofumbia macho mamilioni ya waliokimbia makazi yao huko Ukraine, Sudan, Syria, Afghanistan, na vile vile DRC.Kuzungumzia haya na pia haki za wakimbizi kwa ujumla, Bi. Faith Kasina, msimamizi wa UNHCR ukanda wa Afrika mashariki alizungumza na George Ajowi.
19.12.2023 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Ipo siku watu wanaoishi na walemavu watapata nafasi sawa katika jamii
Tarehe 3 Disemba mwaka huu, dunia iliadhimisha Siku ya Kimataifa ya watu wanaoishi na ulemavu. Siku hii iliasisiwa mwaka 1992 na umoja wa mataifa. Nchini Kenya, siku hii ilifana sana huku sherehe ikiandaliwa katika maeneo mbalimbali. Katika eneo la Dagoreti, jijini Nairobi, tulikutana na Grace Wanjiku Maina ambaye alizaliwa na ulimavu lakini amejizatiti na kufanikiwa sana katika Jamii.Licha ya kuishi na Ulemavu Grace ni mshinda wa tuzo ya urembo ya kinadada wanaotumia vitu vya magurudumu, tuzo alioyoishinda 2017 na 2018, vile vile ni mwakilishi wa watu wanaoishi na ulemavu katika eneo la Dagoreti na pia mkurugenzi katika wakfu wa Sweet Aroma foundation, wakfu ambao unawatetea walemavu. Katika makala ya leo nimeanza kwa kumuuliza, nini kimebadilika tangu aliposhinda taji la urembo la miss Wheelchair miaka 6 iliyopita?
11.12.2023 • 10 Protokoll, 5 Sekunden
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu kushinikiza serikali kutekeleza maamuzi ya mahakama
Mtandao wa Taasisi za Kitaifa za Haki za Kibinadamu za Kiafrika (NHRI)kwa ushirikiano na Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu ya Kenya (KNCHR) pamoja na Taasisi ya Sheria ya Kibinadamu na Haki za Kibinadamu ya Raoul Wallenberg iliyo na makao yake makuu nchini Sweden iliandaa warsha ya kutathmini miradi kuhusu mafunzo ya Haki za Kibinadamu barani Afrika na ufuatiliaji wa jinsi ya Kutekeleza mapendekezo ya Maamuzi. Katika makala haya Petronila Mukaindo, naibu mkurugenzi wa KNCHR anatoa twasira kamili ya changamoto na hatua za kutetea haki za kibinadamu nchini kenya na katika mataifa mengine.Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
4.12.2023 • 10 Protokoll, 5 Sekunden
Siku 16 za mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake
Kila mwaka dunia hutumia siku 16 kuadhimisha mapambano ya kupinga ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto . Umoja wa mataifa huongoza kampeni hii na hufanyika kuanzia tarehe 25 Novemba na kumalizika tarehe 10 Desemba ya kila mwaka kwa ajili ya kupinga ukatili na kutetea haki za wanawake.Siku hiyo ilianza kuadhimishwa rasmi mwaka 1991 na tangu wakati huo zaidi ya asasi 6,000 kwa zaidi ya nchi 187 hushiriki katika maadhimisho haya. Nchini Kenya katika eneo la Kibra baadhi ya kinadada wamethibitisha kuwa visa vya dhulma bado vipo na kati ya wanawake 5 wawili wamedhulumiwa kisaikologia na hata kingono .Ili kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
1.12.2023 • 10 Protokoll, 3 Sekunden
Manufaa ya mitandao, mwandishi Paul Braine anasimulia
Ujio wa mitandao umekuja na masaibu mengi tu, licha ya manufaa mengi, katika makala haya Benson Wakoli anakamilisha mahojiano yake na mwandishi wa kitabu cha Parenting in Dijital Era, yaani uzazi kipindi hiki cha kidijiti, bwana Paul Braine kuhusu manufaa na hasara za mitandao. Ili kufahamu mengi skiza makala haya.
28.11.2023 • 9 Protokoll, 55 Sekunden
Haki ya watoto kipindi hiki cha kidigiti
Paul Braine mwandishi wa vitabu nchini Kenya, amechapisha kitabu kinachoangazia haki za watoto kulelewa kipindi hiki cha dijitali na jukumu la wazazi kuwalea watoto kipindi hiki. Benson Wakoli amezungumza naye kuangazia haki za kila pande yaani watoto na wazazi katika makala haya ya Jua Haki Zako. Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
7.11.2023 • 9 Protokoll, 48 Sekunden
Kenya : Serikali yaendesha bomoabomoa kwenye ardhi inayodai kuwa yake
Katika makala haya tunajadili hatua ya serikali nchini kenya kubomoa makaazi ya raia wanaodiwa kujenga nyumba zao kwenye ardhi ya serikali, ambayo inamilikiwa na kampuni ya simiti ya East African Portland cement. Kwa mjibu wa kampuni ya simiti ya East African Portland cement, raia waliojenga kwenye ardhi inayodai kuwa yake walikuwa wameonya dhidi ya kujenga kwenye ardhi hiyo.Ili kuelewa mengi zaidi skiza makala haya.
27.10.2023 • 9 Protokoll, 25 Sekunden
DRC : Haki za raia kuelekea uchaguzi mkuu
Nchini DRC raia wanajitarayarisha kushiriki uchaguzi mkuu mwezi disemba ambapo watapata fulsa kuwachagua wabunge pamoja na rais. Katika mantiki haya mwanaharakati ambaye sasa ni mwanasiasa Pascal Mpenda anafafanua ni vipi raia wa DRC wanapaswa kutumia haki yao ya kikatiba kuwachagua viongozi.Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
23.10.2023 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Sudan Kusini : Serikali inaminya uhuru wa kujieleza wa wanahabari
Kwenye makala ya juma hili tunaganzia ripoti ya bazara la haki za binadamu la umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini, ambayo iliangaizia kwa kina mathila yanayotekelezwa na serikali ya Sudan Kusini dhidi ya wanahabari, wanaharakati pamoja na wanasiasa wa upinzani. Umoja wa mataifa kupitia afiasi yake ya haki za biandamu nchini Sudan Kusini, imeeleza kustitishwa kwake namna waandishi wa habari wanavyonyanyaswa na vyombo vya usalama nchini Sudan Kusini, Lengo likiwa kuuzia taarifa zozote zinazopaka tope serikali, baadhi ya wanahabari wanaokiuka hili wakitishwa, kufungwa jela na hata baadhi kuuawa.Skiza makala haya kwa mengi zaidi.
10.10.2023 • 9 Protokoll, 58 Sekunden
Jamii zisizo na uraia zalilia serikali ya Kenya
Nchini Kenya serikali inalenga kuanza kutoa vitambulisho vya kidijiti ili kuimarisha huduma zake mbali na kuzuia wizi wa mitandao ambao umekuwa ukiteklezwa na wahalifu. Hata hivo mashariki mbalimbali yamejitokeza kupinga kuanza kwa shughuli hiyo hadi pale jamii mbalimbali ambazo zimekuwa zikishuhudia changamoto za kupata vitambulisho kutokana na kukosa uraia zikitaka serikali kushughulikia matatizo hayo kabla ya kuendelea na shughuli ya kuanza usajili.Jamii ni hizo ni pamoja raia kutoka nchini Rwanda, Wapemba, Wanubi na washona. Ili kufahamu mengi skiza makala haya.
3.10.2023 • 9 Protokoll, 28 Sekunden
Kenya : Mashirika ya kirai yaitaka serikali kuzingatia sheria
Nchini Kenya serikali inapanga kuzindua mpango wa kusajili wakenya upya ili kuwapa kitambushi cha kidijiti, ambacho serikali inasema kitasaidia kuimarisha huduma zake. Hata hivyo masharika ya kiraia nchini humo yamepinga mpango huo yakisema haujazingatia sheria kwani serikali haijatoa hakikisho kuhusu usalama wa data ya wakenya. kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
25.9.2023 • 9 Protokoll, 27 Sekunden
Mazingira yaathiri haki za watoto Africa
Wataalamu wa mazingira yameonya kuhusu athari kubwa inayotokana na maingira ambayo moja kwa moja inathiri watoto. Katika makala haya wanamazingira na watetezi wa haki za watoto wanajadili namna gani haki za watoto zinaweze lindwa kipindi hiki dunia inapotafuta mbinu ya kukabiliana na athari ya mabadiliko ya tabia nchi.
21.9.2023 • 9 Protokoll, 53 Sekunden
DRC : Visa vya ubakaji kambini Nyiragongo
Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka (MSF ) na wanawake wanaoishi kwenye kambi baada ya kutoroka makaazi yao katika vijiji vya mkowa Kivu Kaskazini mashariki mwa Congo DRC, wameeleza kuongezeka kwa visa vya ubakaji katika kambi ya Nyiragongo, wanawake hao wakitaka serikali ya DRC kuwashughulikia. Tangu mwezi Julai mwaka 2023 hadi sasa ni kwamba zaidi ya wanawake elfu moja wamedhulumiwa kingono eneo la Nyiragongo Mkoani Kivu kaskazini. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
18.9.2023 • 9 Protokoll, 43 Sekunden
Haki ya wanawake kutumia mitandao
Katika makala ya haya tunaangazia haki za wanawake kutumia mitandao na haki za wanawanawake kwa jumla, kwa mengi zaidi skiza makala
6.9.2023 • 9 Protokoll, 55 Sekunden
Changamoto za wachimba madini ya dhahabu nchini Kenya
Mchakato wa kupata madini ya dhahabu huwa ni ngumu sana. Wengi ambao wanajihusisha na kazi hii wanapitia changamoto nyingi ikiwemo kutotumia vifaa bora vya kujikinga, kazi nzito na hatimaye huenda hata kuangamia iwapo maporomoko ya ardhi yanapotokea.George Ajowi amezuru Kaunti ya Migori, Magharibi mwa nchi ya Kenya. Ameandaa ripoti ifuatayo.
17.8.2023 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Uhalifu wa kivita unafanyika Sudan : Amnesty International
Shirika la kimataifa la ketetea haki za binadamu Amnesty International katika repoti yake ya hivi punde limesema pande hasimu nchini Sudan, zinatekeleza uhalifu wa kivita na kutaka jamii ya kimataifa kuingilia kati kunusuru hali. Shirika hilo linasema raia wa taifa hilo wanapitia mithila makubwa mikoni mwa wapiganaji wa RSF na jeshi, kwa mengi zaidi skiza makala haya.
9.8.2023 • 10 Protokoll
Jamii za mipakani taabani kupata vitambulisho
Kinyume na jamii nyingine nchini Kenya kundelea kupata vitambulisho bila vikwazo, jamii zinazoishi mikapani nchini humo zinaendelea kupitia changamoto za kupata vitambulisho, wengi wakilazimika kufanyiwa ukaguzi kabla ya kupewa stakabadhi hiyo muhimu. Katika makala haya, utaskia kutoka kwa wahusika ambao wametia changamoto si hapa ili kupata vitamblulisho, mashirika ya kiraia kama vile Namati yakiingilia kati kuhakikisha wahusika wanapata haki.kwa mengi zaidi skiza makala haya.
31.7.2023 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Kenya: Polisi watumia nguvu kupita kiasi
Mashirika kadhaa ya kirai nchini yametuhumu polisi kwa kumia nguvu kupita kaisi kuwakabili wandamanaji wa upinzani wambao wamekuwa wakishiriki maandamano kutaka serikali kushughulikia kupanda kwa gharama ya maisha. Mashirika hayo yanatka polisi wanaohusika kutumia kuchukuliwa hatua za kisheria, wakati huu serikali ikiwatetea wahusika.
28.7.2023 • 9 Protokoll, 55 Sekunden
Je wanawake wanatetea haki zao?
Katika makala haya tunajadili dhana kuwa wanawake hawapo mstari wa mbele kupigania haki zao, ambapo utaskia kauli ya Allan Ngare kutoka Human Right Watch anayekanusha vikali dhana hiyo, pia utaskia kutoka kwa mratibu wa kina dada wanaotumia miili yao kupata riziki bi Felister Abdalla anayesema wakati umewadia jamii kuwakumbatia. kwa jumla hata hivyo wote wanakiri kuwa hatua zaidi zastahili kuchukuliwa ili kulinda haki za wanawake.
26.7.2023 • 10 Protokoll
Hali ya kibinadamu katika mataifa ya Kenya,Burundi na DRC
katika makala haya tunaangazia hali ya Kinadamu ilivyo katika mataifa ya Kenya, Burundi na DRC, hii ni baada ya masharika kadhaa ya kutetea haki za binadamu kungazia hali ilivyo katika mataifa hayo. Watafiti kutoka shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International wanatoa kauli zao kuhusu hali ya biandamu katika mataifa husika.skiza makala haya kwa mengi zaidi.
11.7.2023 • 9 Protokoll, 24 Sekunden
Haki ya kupata habari za kweli na kuaminika
Taasisi ya Bazara Media Lab nchini Kenya imezindua mpango unalenga kutambua habari za kzeli na uongo, tasisi hi ikisema wamechochewa kuja na mpango huo kutokana na kuongezeka kwa habari ghushi katika mitandao ya kijamii. Na licha ya taasisi kuwa na makao yake nchini Kenya, inalenga kupanua mabawa yake katika mataifa ya Africa Mashaki ili kuwasaidia wenye kuhumu mengi zaidi kuhusu habari za kweli na uongo.kwa Mengi zaidi skiza makala haya.
6.7.2023 • 10 Protokoll, 1 Sekunde
Watoto wanyanyaswa kigongo nchini DRC
Bunge la watoto wilayani Masisi Mashariki mwa DRC, linashutumu unyanyasaji unaofanyiwa watoto kwa kuhusishwa katika biashara ya ngono. Kulingana na mashairika ya kiraia na wanaharakati wa haki za binadamu huko Masisi, maelfu ya watoto wanatumiwa kiuchumi na wazazi wao ambao huwalazimisha kufanya kazi nao katika shughuli zao za vijijini na katika biashara ndogo ndogo za kingono .Kwa mujibu wa wanaharakati kwa haki za binadamu, hali linatokana na vita vya M23 na makundi mengine yenye silaha ambayo yanafanya eneo hili kukosa usalama. Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
5.7.2023 • 9 Protokoll, 50 Sekunden
DRC yatunga sheria kudhibiti kiwango cha mahari
Nchini DRC wabunge wametunga sheria kudhibiti kiwango cha mahari kinachostahili kutolewa, hii ni baada ya wanaume wingi kudaiwa kususia ndoa kutokana na kiwango cha juu cha mahari kinachoitishwa na familia ya wasichana. Je kuna haja ya kiwango cha mahari kuthibitiwa hasa ikizingatiwa jamii mbalimbali za kiafrica zina tamaduni zake?Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi
20.6.2023 • 9 Protokoll, 50 Sekunden
Matumizi ya nguvu kupitia kiasi na polisi wakati wa maandamano
Mashirika ya kutetea haki za binadamu Human Right Watch na Amnesty International, yametuhumu polisi nchini Kenya kwa matumizi ya nguvu kupita kiasi wakati wa kuwakabili wandamanaji wakati wa maandamano yaliokuwa yameitishwa na upinzani mwezi Machi. Katika ripoti yao mashirika hayo mawili, pia yametuhumu serikali ya Kenya kwa kukosa kuwachukulia hatua polisi wanaotuhumiwa kuhusika na visa vya ukiukaji wa haki za binadamu ikiwemo mauwaji ya raia 16.Ili kufahamu mengi zaidi sikiza makala haya.
16.6.2023 • 9 Protokoll, 44 Sekunden
Kenya :Watoto wanaoishi na ulemavu vijijini wakosa mahitaji ya kimsingi
Nchini Kenya Watoto walio na ulemavu nchini kenya hasa maeneo ya mashinani wanazidi kupitia changamoto si haba ukilinganisha na wenzao wa mijini.Hii ni kutokana na ufukara unaozidi kuongezeka mashinani.-Takwimu kutoka shirika la afya duniani zinaonyesha kuwa takriban watoto milioni 2.5 wanaishi na ulemavu nchini Kenya huku asilimia 72 ya watoto walemavu wanaishi mashinani na asilimia 27.4 wanaishi mijini.Mwandishi wetu, Victor Moturi, alitembelea kaunti ya Kisii na Nyamira Ni msimu wa mvua na katika shule hii spesheli ya Mwata iliyoko Kaunti ya Kisii nchini Kenya,wanafunzi wasiokuwa na uwezo wa kuongea wamekongamana darasani kupokea mafunzo;Japo wanafunzi hawa wamo darasani,wamekosa vifaa muhimu vya mafunzo pamoja na chakula,Diana Metobo mmoja wa mwanafunzi anasema wao wamekuwa wakipitia changamoto si haba..‘’’Tuna changamoto nyingi, tunakosa chakula, nguo, soksi, viatu, hatuna bweni zuri, maji hayapo. Nyumbani kwetu hatuna chakula na hata vitabu vya kusoma hakuna. Tunayo nyumba lakini ni ya zamani sana,’’Amesema Metobo. John Oigara ni mwanafunzi mwingine asiye na uwezo wa kuongea ,Oigara anadokeza kuwa,.yeye pamoja na wanafunzi wengine, hutegemea msaada kutoka kwa majirani pamoja na wahisani wengine ,ili kujiendeleza kimasomo vile vile kupata mahitaji mengine.‘’Wakati wageni walipokuja shuleni kwetu, walinunua chakula, blanketi, tangi la maji, sabuni, walituletea viatu, soksi na nguo.’’ Kilomita 40 kutoka mji wa kisii,shule ya msingi ya Riang’ombe DOK iliyoko Borabu ,kaunti ya Nyamira ni moja wapo ya shule zilizochaguliwa ili kutenga madarasa maalum kwa minajili ya watoto wanaoishi na ulemavu,lakini kulingana na mwalimu mkuu wa shule hii,George Onditi ,kwa muda sasa,wanafunzi hawajafika shuleni kwa sababu ya ukosefu wa waalimu pamoja na vifaa maalum vya masomo.‘’,,,,Watoto walikuwa wengi,takriban ishiriki lakini kwa sababu nimekosa mwalimu,wengine wamefichwa,wengine hawakuji shuleni,wengine wakiingia wakiona mwalimu wao hayuko basi wanarudi kwa sababu sisi hawatuoni kama waalimu wao.Serikali tafadhali wanisaidie ,watusaidie kama jamii tuweze kupata waalimu,tuweze kupata vifaa,ndiposa tuwashughulikie haa watoto hawa watoto ambao ni walemavu,’’ Amesema George Onditi ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Riang’ombe,,,,Kwa majina naitwa Stella Masaki,hili ni darasala la gredi 5,sasa wajua sisi hatujasomea taaluma hii,kwa hivyo tukiwachanganya hivi ,inatuchukuwa muda kuwafunza hawa badala ya kuwafunza wale ambao tumefunzwa jinsi ya kuwafundisha,kwa hivyo tunahitaji mwalimu ambaye atawashughulikia,wengine walichukuliwa na wazazi wao kwa sababu hatukuwa na uwezo wa kuwachunga,tukaona wale ambao wanaweza kuongea tukaona wabaki hapa tukae nao.Idadi ya wanafunzi walio na ulemavu wanaojiunga na shule vijijini ni chache mno ukilinganisha na wenzao wanaoishi mijini.Hali hii imesababishwa na gharama ya juu ya vifaa vinavyohitajika kuwapa watoto hao mafunzo,ukosefu wa madarasa maalumu,na ukosefu wa usafiri .Agasa Maroko ni mwalimu maalum katika shule ya msingi magombo,kaunti ya Nyamira..’’.mimi nashughulikia wanafunzi ambao wana shida ya kiakili na wako wanafunzi kumi na watatu lakini kwa kijiji hiki kuna wale amabao hawajaingia shuleni kwa sababu hawana vifaa vya kuwaleta shuleni kama vile viti vya magurudumu.Hapa shuleni kuna mwingine akiona wenzake wanacheza nje anatoka darasani bila kuitisha ruhusa ,sasa mimi kama mwalimu ,lazima nitafute mbinu zote ambazo zitafanya huyo mtoto aingie darasani,na hata hawa walimu wengine kwa vile wana mapenzi kwa hao watoto,pia huwa wananisaidia sana’’Amedokeza mwalimu Maroko Wengi wa wanafunzi wanaoishi na ulemavu katika kaunti za kisii na nyamira ,hufichwa na wazazi ,hatua ambayo huwanyima haki zao za kimsingi pamoja huduma maalumu.‘’kwa mfano unakuta shule zimejengwa ambazo watoto hawawezi pita kuingia darasani,vyoo vya kujisaidia hawawezi tumia na watoto wengine,sasa inabidi tunawafungia hawa watoto nyumbani,kama mimi ninaye mmoja aliyekuwa katika shule ya msingi ya Riang’ombe D.O.K,ikawa sasa hatangamani na watoto wengine kwa sababu ni mlemavu,na hawezi ingia darasani ,na lazima abebwe,hivyo ikabidi tumuweke nyumbani’’Amesema Shujaa Mathias Maina ambaye ni mzazi wa mtoto anayeishi na Ulemavu. Licha ya vizuizi hivi,Mashirika binafsi, kwa kushirikiana na utawala wa mitaa, wameanzisha mikakati na mipango ya kuongeza idadi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaohudhuria shule nchini Kenya.Kama anavyoeleza Anthony Nyabera kutoka shirika la Progressive Africa, Ushirikiano huo una lengo la kutoa msaada muhimu kwa watoto wenye mahitaji maalum, kama vile vifaa vya masomo, sare za shule, viti vya magurudumu, na maelekezo ya kihisia.,’’,Haswa tunawasaidia wale watoto walemavu,pia tunawasaidia wale wenye ni wagonjwa,pengine wanataka kuenda kliniki,tunawapeleka,kama Kijabe ,Kisii,na wakati mwengine madaktari wanawatembelea nyumbani,tulianza kuwafundisha watoto wale wako na shida ya uti wa mgongo,vile vile tukawalipia huduma ya NHIF na ndio huwa wanatumia kwa sasa,pia tunawasaidia na viti vya magurudumu ili viwasaidie kuenda shuleni,vile vile tunawapa vitanda maalum walio na shida za uti wa mgongo,wenye hawawezi kusimama au kutembea,pia kuna vile tunawasaidia’’Amedokeza NyaberaKupitia juhudi hizi, idadi kubwa ya watoto tayari wamenufaika. Zaidi ya watoto 3000 wamepokea msaada unaohitajika ili kuendelea na elimu yao, hivyo kuwawezesha kuafikia malengo ya elimu.Esther Nyaribari,ni mkurugenzi mkuu katika shirika la Touching souls initiative nchini Kenya‘’Mara ya kwanza tuligundua hawa watoto wako na changamoto za kupata chakula,na watoto hawawezi enda darasani na hawajakula,hivyo huwa tunatafuta wafadhili ambao husaidia hawa watoto kuwapa chakula kama vile mahindi maharagwe nakadhalika,halafu pia unapata watoto wamekuja shuleni wamevalia mavazi ya nyumbani,tunahakikisha tumewatafutia sare za shule angalau pia wafanane na wanafunzi wengine,pia kuna wale wanafunzi wenye umri mkubwa hasa wale walio na matatizo ya kiakili,pia hao tunawafikia manyumbani mwao na kuhakikisha maslahi yao yameshughulikiwa’’ Kulingana na takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani, inakadiriwa kuwa watoto milioni 2.5 wanaishi na ulemavu nchini Kenya. Katika idadi hii, takribani asilimia 72 wanaishi katika maeneo ya vijijini, wakati asilimia 27.4 wanapatikana mijini.Kwa mujibu wa Nyaribari, Takwimu hizi zinaonyesha hitaji la haraka la kushughulikia changamoto maalum zinazowakabili watoto wenye ulemavu katika maeneo ya vijijini.‘’Wito wangu kwa wazazi ni kuwa,wasifiche watoto na labda wasione wamepata watoto walemavu ni pigo wamepata,la hasha ,wawachukulie kama watoto wengine,wawatoe nje na wasiwafiche kwa sababu pia hao watoto wanahitaji masomo,wanahitaji matibabu na mambo mengine,kwa hivyo wawaweke wazi ndio sasa tuweze kuwasaidia kwa sababu wakiwaficha hatutaweza kujua kuna watoto wanahitaji msaada,’’Ameongeza NyaribariHuku idadi ya watoto wanaoishi na ulemavu ikizidi kuongezeka nchini Kenya,wazazi pamoja na mashirika ya kijamii ,wanaiomba serikali kuhakikisha uwepo wa vifaa vinavyohitajika kuwapa watoto hao masomo,kuongeza madarasa maalum vile vile kuajiri waalimu zaidi ili kupiga jeki masomo ya watoto wanaoishi na ulemavu.
13.6.2023 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Haki ya raia wa wafaarika kuabudu
Katika makala haya tunaangazia haki ya kuadubudu ambapo nchini Kenya uhuru huo umesbabisha vifo vya zaidi ya watu 200 kupoteza maisha yao kutokana na mafunzo potovu ya mchangaji Paul Mackenzi. Mackenzi anadaiwa kuwashawishi wafuasi wake kufunga, yaani kukaa bila kula chakula hadi kufa ili kuonana na Masi Yesu Kristo mwana wa Mungu.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
30.5.2023 • 9 Protokoll, 58 Sekunden
Mashoga na wasagaji wakimbizi walilia haki nchini Kenya
Shirika la kimataifa la kutetea haki za biandamu Amnesty International limechapisha ripoti kuhusu kudhulumiwa kwa haki za mashago na wasagaji nchini Kenya, ripoti hiyo hasa ikijikiita zaidi kwa wakimbizi na watafuta hifadhi katika kimbi kubwa ziadi nchini Kenya ya Kakuma;
Kambi ya kakuma ni nyumbani kwa zaidi ya watafuta hifadhi na wakimbizi 200,000 ikiwemo familia ya mashoga na wasagaji.
Ili kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
23.5.2023 • 10 Protokoll
Hali ya haki za binadamu nchini Tanzania
Shirika la kimataifa la kutetea haki za bindamu Amnesty Internatonal limeeleza wasiwasi wake kuhusu namna serikali ya Tanzania inavyotumia nguvu kupita kiasi kufurusha jamii ya Maasai ambayo inaishi eneo la Ngorongoro na Loliondo.
Amnesty linasema serikali ya Tanzania haikushauriana na jamii hiyo kabla ya kuanza zoezi la kuwaondoa wenyeji hao katika ardhi zao asilia.
Kwa mengi zaidi skiza makala haya.
15.5.2023 • 9 Protokoll, 51 Sekunden
Je haki za wanawake zinaheshimiwa
Kwa kipindi kirefu wanawake wametazamwa kama viungo daifu kwa jamii hadi baadhi ya jamii bado zina dhana kwamba hawana haki ya kumiliki ardhi, je haki hizi zinaweza kuheshimiwa?
Katika makala haya utaskia maswali yakiekelezwa kwa wanaharakati Sara Metei mtetezi wa haki za wanawake kumiliki ardhi kaunti ya Kajiado nchini Kenya, pamoja na Irene Maina kutoka Kituo cha haki cha Dandora.
11.5.2023 • 9 Protokoll, 58 Sekunden
Haki ya wanawake kumiliki ardhi
Katika jamii nyingi za kiafrica si rahisi wanawake kuruhusiwa kumiliki ardhi, ni swala wengi sasa wanaliona kama limepitwa na wakati.
Ni kutokana na hatua hiyo ndio maana wanaharakati kama vile Sarah Metei na Irene Maina wamejitokeza kupigania haki za wanawake kumiliki ardhi nchini Kenya.
Wanaharakati hawa wanasema wakati umewadia katiba za mataifa ya Africa kuruhusu wanawake kumiliki ardhi, kwa mengi zaidi skiza makala haya.
1.5.2023 • 9 Protokoll, 44 Sekunden
Haki ya watoto kupata elimu barani Africa
Changamoto za kupata elimu bora barani Africa zinazidi kuongezeka kadri watoto wanavyojiunga na shule, hili linatokana na ukosefu wa miundo bora pamoja na waalimu wa kutosha .
Hali hii imechangia watoto wengi kutojua kusoma na kuandika licha ya kuwa kwenye madarasa ya juu.
Mfano nchini ,utafiti uliofanywa na shirika la uweza waonyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi wa gredi ya nne nchini humo hawawezi kusoma masomo ya wale wa gredi ya tatu, ili kufahamu zaidi skiza makala haya.
10.4.2023 • 10 Protokoll
Mchango wa vijana kwa uchaguzi wa DRC
Taifa la DRC, linajianda kwa uchaguzi baadaye mwaka huu, lakini je vijana nchini humo wanafahamu mchango wao katika kufanikisha uchaguzi huo na kuhakikisha vijana wanapata haki yao ya kimsingi ya kuwachagua viongozi wanaofaa?
katika makala haya tunaangazi hilo kwa kina.
3.4.2023 • 9 Protokoll, 43 Sekunden
Mchango wa sanaa kupigania haki za binadamu
Mbali na wanaharakati kutumia sheria kuhakikisha maswala ya haki za binadamu zinaheshimiwa, wanaharakati pia wanatumia njia za Sanaa kama vile uingizaji, kuhakikisha kwamba ujumbe unawafikia wahusika.
Katika makala haya,wanaharakati Domic Mutemi na Irene Maina, wote walijibu maswali kutoka kwa hadhira katika ukumbi wa Alliance Française, jijini Nairobi katika makala haya ya Jua Haki zako.
1.4.2023 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Matumizi ya sanaa kupigania haki za binadamu Africa
Sanaa ni moja wapo ya nguzo muhimu katika kupigania haki za binadamu, katika makala haya mwanahabari wetu Benson Wakoli kwa undani anajadili na wanaharakati waagizaji Irene Kamau kutoka kituo cha haki cha Dandora, nchini Kenya pamoja na Domic Mutemi kutoka kituo cha haki cha Githurai.
Bi Irene na bwana Mutemi anasema kutokana na sanaa wamafikia mengi tu, katika kutetea haki za binadamu.
21.3.2023 • 9 Protokoll, 41 Sekunden
Hedhi pasua kichwa kwa wasichana na wanawake
Nchini Kenya, Seneta Gloria Orwoba, anaendeleza kampeini ya kuhakikisha watoto wakike wanapata visodo ( taolo za kike) kampeni ambayo imepata hisia mseto kutoka kwa wakenya.
Serikali ya Kenya, kwa muda imekuwa ikiahidi kuanza kutoa visodo bila malipo kwa wasichana wa shule lakini hili limebakia tu ahadi.
Katika makala haya Benson Wakoli, anajadili kwa kina na mwanaharati wa haki za wanawake bi Lucy Opondo, kufahamu ni vipi kampeini ya seneta Opondo itafaulu.
6.3.2023 • 10 Protokoll, 2 Sekunden
Mchango wa vyombo vya habari kutetea haki za watoto
Runinga pamoja na redio ni baadhi ya vyombo vya habari ambayo vimetanjwa kuchangia kuimarika kwa ukuwaji wa watoto, hata hivyo baadhi ya vyombo hivi vya habari vinatuhumiwa kwa kukiuka haki za watoto ambapo vinapeperusha vipindi vinavyoenda kinyume na maandili ya watoto.
Katika Makala haya Benson Wakoli, anazungumza na bi Ann Sato, mratibu wa vipindi katika taasisi ya kuzalisha vipindi vya watoto ya Akili Kids, kujadili kile wanachozingatia katika kuzalisha vipindi hivi, ambapo pia utapata nafasi ya kuskia kutoka kwa bwana Peter Martin afisa kutoka mamlaka ya mawasiliano nchini Kenya.
24.2.2023 • 9 Protokoll, 51 Sekunden
Serikali ya Uganda yasitisha huduma za afisi ya haki za bindamu ya umoja wa mataifa
Uamuzi wa Serikali ya Uganda wa kutoongeza kibali cha afisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu umewaacha wadau wengi wa masuala ya haki za binadamu na wanasiasa wa upinzani wakiwa wamekata tamaa na kutaka uamuzi huo ubadilishwe.
Hatua inatokana na kukamilika kwa leseni iliotolewa na serikali ya uganda kwa afisi hiyo kuendelea kuhudumu nchini Uganda.
Serikali ya Uganda inasisitiza kuwa si lazima kila taifa liwe na afisi za umoja wa mataifa zinazoshugulikia haki za binadamu na kwamba tume ya kitaifa ya Uganda inayoshughulikia haki za binadamu ina nguvu zaidi za kuendelea kutekeleza wajibu uliokuwa unatekeleza na afisi hiyo ya umoja wa mataifa.
Raia wengi wa Uganda hata hivyo wamelaini hatua hiyo ya serikali na kudai kuwa tume ya kutetea haki za biandamu nchini Uganda haina nguvu na kwamba mara nyingi huegemea upande wa serikali.
Kwa ufahamu zaidi skiza makala haya.
14.2.2023 • 9 Protokoll, 56 Sekunden
Biashara ya ngono pwani ya Kenya
Tatizo la biashara ya ngono pwani ya Kenya linazidi kuwa donda sugu, wadau wakiitaka serikali kuweka mikakati kuzuia kabisa biashara hiyo.
Skiza makala haya kwa ufahamu zaidi.
13.2.2023 • 9 Protokoll, 46 Sekunden
Human Right Watch - Serikali za Africa zinakandamiza wapinzani wao
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch, limesema bado serikali za Africa linawakandamiza wapinzani wao.
Skiza makala hay kwa mengi zaidi.
1.2.2023 • 9 Protokoll, 59 Sekunden
Viongozi wa Africa wanatazama haki za raia wao zikiukwa
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch, linatuhumu viongozi wa Africa kwa kuendelea kusalia kimya wakati makundi ya waasi yanazidi kukiuka haki za raia wasio kuwa na hatia.
Benson Wakoli amezungumza na Otsieno Namwaya mkurugezi wa Human Right Watch, Africa Mashariki.
27.1.2023 • 9 Protokoll, 57 Sekunden
Demokrasia Africa na uhusiano wake na haki za binadamu
Demokasia kwa kiasi kikubwa ihusishwa na haki za binadamu ndio kauli ya Prof Winnie Mitullah ambaye na mhadhiri wa chuo kikuu cha Nairobi na mwanachama wa shirika la Afrobarometer.
Skiza makala haya kwa mengi zaidi.
16.1.2023 • 9 Protokoll, 56 Sekunden
Dhuluma za kijinsia nchini DRC zimeripotiwa kuongezeka
Nchini DRC ukatili wa kijinsia bado ni changa moto, haya ni kutokana na ripoti ya wizara ya jamii mama na mtoto ya miaka miwili iliopita, katika makala haya tunaangazia hayo hiyo kwa kina, kwa mengi zaidi skiza makala haya.
14.11.2022 • 9 Protokoll, 32 Sekunden
Namna ya kuwekeza katika hali ya Kibinadamu na ustahimilivu
Katika makala haya tunaangazia ni vipi tunaweza kuhakikisha kuwa hali ya binadamu katika mataifa yetu inaweza kuimarishwa kwa kijumla na kwa kuharakisha na kuwekeza katika hali ya kibinadamu na ustahimilifu.
12.11.2022 • 9 Protokoll, 39 Sekunden
Haki za mtoto ambaye hajazaliwa
Raia wengi hapa Africa hawana Ufahamu kuhusiana na haki za watoto ambao bado hajazaliwa, katika makala ya leo tunajadili kuhusu haki za watoto ambao hawajazaliwa.
Skiza makala haya kwa mengi zaidi.
11.11.2022 • 9 Protokoll, 52 Sekunden
Kenya : Kazi ni Kazi kila mtu na riziki yake
Makala haya tunazidi kuangazia jukumu la kila mmoja wetu kuhakikisha anatafuta kipato kukimu familia yake, ambapo mwandishi wetu Benson Wakoli, anazidi kutangamana na vijana wanaopta riziki kwa kupunguza vioo vya majumba marefu nchini Kenya.
24.10.2022 • 9 Protokoll, 59 Sekunden
Kenya : Haki ya kutafuta riziki
Kila mtu ana jukumu la kuhakikisha anapata chochote ili kukidhi mahitaji yake mbali na kulisha familia yake.
katika makala haya nimekutana na vijana ambao wanatafuta riziki kupitia njia ambayo si ya kawaida kusafisha vioo vya majumba marefu jijini Nairobi ili kupata riziki, skiza makala usiskie mengi kuwahusu.
17.10.2022 • 9 Protokoll, 54 Sekunden
Haki za wanawake na watoto nchini DRC zaendelea kukandamizwa
Hali ya kibinadamu nchini DRC, inazidi kuzorota wanawake na watoto wakionekana ndio waathiriwa zaidi katika taifa hilo.
Katika makala haya mwanaharakati na wakili Placide Ntole anatoa ufafanuzi.
11.10.2022 • 9 Protokoll, 46 Sekunden
Wazee wauliwa pwani ya Kenya kwa tuhuma za kwamba ni wachawi
wazee katika pwani ya kenya wanaendelea kuishi kwa hofu kutokana na baadhi yao kuawa kwa misingi ya kwamba ni wachawi.
Katika makala haya mwandishi wetu Diana Wanyonyi anasimulia.
10.10.2022 • 9 Protokoll, 34 Sekunden
Haki za binadamu nchini Uganda ni tete
Mashariki mengi ya kutetea haki za binadamu nchini Uganda yanatuhumu utawala wa taifa hilo, kwa kuendelea kukandamiza haki za binadamu.
Katika makala haya mwanaharakati Hashim Awadi kutoka Uganda, anasimulia hali ya halk za binadamu nchini Uganda.
10.10.2022 • 9 Protokoll, 54 Sekunden
Mchango wa vijana katika haki za raia wa Afrika
Katika makala haya tunaangazia haki za raia wa Africa kwa jumla na mchango wa vijana katika kudumisha haki, ambapo utaskia kauli ya Ann Maua, mratibu wa vuguvugu la African Rising kanda ya Africa Mashariki.
21.9.2022 • 10 Protokoll
Kenya : Mimba za mapema miongoni mwa wasichana
Mimba za mapema zasalia changamoto miongoni mwa wasichana, mwandishi wetu Diana Wanyonyi kutoka Mombasa Kenya anaangazia tatizo hilo katika makala haya.
12.9.2022 • 9 Protokoll, 59 Sekunden
Kenya : Wasichana wakimbia dhuluma za kijinsia
Katika makala haya mwanahabari wetu wa Mombasa Diana Wanyonyi, anasimulia ni vipi dhuluma za kijinsia, ndoa za mapema na umaskini umelazimu baadhi ya wasichana kukimbia makwao.
8.9.2022 • 9 Protokoll, 53 Sekunden
Tamaduni zalemaza kina mama nchini Kenya
Tunaendelea kuangazia changamoto ambazo wanawake wanaendelea kupitia nchini Kenya kutokana na misimamamo mikali ya tamaduni zilizopitwa na wakati na pia taasubi ya kiume.
29.8.2022 • 9 Protokoll, 56 Sekunden
Kenya : Haki ya watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi
Raia nchini Kenya, wameandikisha historia kwa kumchagua Martin Wanyonyi raia anayeishi na ulemavu wa ngozi kuwa mbunge wa kwanza katika historia ya taifa hilo.
Skiza makala haya kwa mengi zaidi